Kiswahili: Open Bible Stories

Updated ? hours ago # views See on DCS

Kiswahili: Open Bible Stories

1. Uumbaji

Frame 01-15

Mungu aliumba mwanamke na mwanaume kwa mfano wake. Akawabariki akasema, "zaeni watoto na wajukuu mkaijaze dunia." Mungu aliona kila kitu alichokifanya ni chema sana, na alifurahishwa sana na kila kitu. Hii ilitokea katika siku ya sita ya uumbaji wake.

Frame 01-12

Mungu alisema, "Si vyema mtu kuwa peke yake." Lakini hakuna hata mnyama mmoja aliyeweza kuwa msaidizi wa Adamu.

Frame 01-13

Ndipo Mungu alimletea Adamu usingizi mzito. Akatoa ubavu mmoja kwa Adamu na kutengeneza mwanamke na akamleta kwake.

Frame 01-06

Katika siku ya nne ya uumbaji, Mungu alisema na kuumba jua, mwezi na nyota. Mungu aliviumba ili kuleta mwanga duniani na kuonesha mchana na usiku, nyakati na miaka. Mungu aliona alichokiumba ni chema.

Frame 01-10

Mungu alichukua vumbi, akamfanya mtu, na akapulizia uhai ndani yake. Akamwita Adamu kwa jina lake. Akatengeneza bustani ya Edeni akamweka aishi humo, na aitunze.

Frame 01-04

Siku ya tatu, Mungu alisema na kutenganisha maji na nchi kavu. Nchi kavu akaiita "dunia," na maji akayaita "bahari." Mungu aliona kila kitu alichokiumba ya kuwa ni chema.

Frame 01-02

Ndipo Mungu akasema, "Na iwe mwanga." Na ikawa hivyo, Mungu aliona kuwa mwanga ni mzuri na akauita mchana, na akatenganisha kutoka giza, akauita usiku. Mungu aliumba mwanga siku ya kwanza ya uumbaji.

Frame 01-01

Hivi ndivyo mwanzo wa kila kitu ulivyotokea. Mungu aliumba ulimwengu na vitu vyote katika siku sita. Maana nchi ilikuwa giza na tupu, na hakuna kilichokuwa kimeumbwa. Lakini Roho ya Mungu ilikuwa juu ya maji.

Frame 01-07

Siku ya tano, Mungu alisema na kuumba vitu vyote viishivyo majini na ndege wote. Mungu aliona kuwa ni vyema, na akavibariki.

Frame 01-09

Ndipo Mungu akasema, "Na tumfanye mtu kwa mfano wetu kuwa kama sisi. Watakuwa na mamlaka juu ya dunia na wanyama wote."

Frame 01-14

Adamu alipomwona, alisema, "Angalau! Huyu ni kama mimi! Ataitwa 'mwanamke' maana ametoka kwa mwanaume." Kwa maana mwanaume atamwacha baba na mama yake watakuwa pamoja na mkewe.

Frame 01-03

Siku ya pili ya uumbaji, Mungu alisema na kuumba anga juu ya dunia. Aliumba anga kwa kutenganisha na maji ya juu kutoka maji ya chini.

Frame 01-11

Katikati ya bustani, Mungu alipanda miti miwili muhimu- mti wa uzima na wa ujuzi wa mema na mabaya. Mungu alimwambia Adamu anaweza kula aina zote za miti isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kama akila tunda la mti huu, atakufa.

Frame 01-16

Siku ya saba ilipofika, Mungu alikuwa amemaliza kazi yake.Hivyo Mungu alipumzika katika kila alichokifanya. Aliibariki siku ya saba akaifanya takatifu kwa sababu katika siku hii alipumzika. Hivyo ndivyo Mungu alivyoumba ulimwengu na kila kitu ndani yake.

Frame 01-08

Siku ya sita ya uumbaji, Mungu alisema, "Na iwe wanyama wa aina zote katika nchi." Na ilitokea kama Mungu alivyosema. Wengine walikuwa wa shambani, wengine wa kutambaa na wa porini. Na ilitokea kama yeye alivyotamka. Na Mungu aliona kwamba ilikuwa ni vyema.

Frame 01-05

Ndipo Mungu akasema, "Nchi izae aina zote za miti na mimea." Na ndivyo ilivyotokea. Mungu aliona kila kitu alichokiumba ni chema.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 1-2

2. Dhambi Inaingia Ulimwenguni

Frame 02-12

Kisha Mungu akasema, "Kwakuwa sasa wanadamu wamekuwa kama sisi kwa kujua mema na mabaya, wasiruhusiwe kula tunda la mti wa uzima wakaishi milele." Hivyo Mungu aliwafukuza Adamu na Eva kutoka katika bustani nzuri ya Edeni. Mungu akaweka Malaika wenye nguvu kwenye malango ya bustani ili kuzuia mtu yeyote asile matunda ya mti wa uzima.

Frame 02-06

Mara macho yao yakafunguliwa, na wakagundua kwamba walikuwa uchi. Wakajaribu kuficha miili yao kwa kushona majani ili kujifanyia nguo.

Frame 02-10

Mungu akamwambia mwanamke, "Nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa kwako. Hamu yako itakuwa juu ya mume wako, naye atakutawala."

Frame 02-04

Yule Nyoka akamjibu mwanamke, "Hiyo sio kweli! Hamwezi kufa. Mungu anajua kwamba pindi mtakapokula mtakuwa kama Mungu kwa kujua mema na mabaya kama ajuavyo."

Frame 02-02

Lakini kulikuwa na Nyoka mwerevu katika bustani. Alimuuliza mwanamke, "Je, ni kweli kwamba Mungu aliwaambia msile matunda ya mti wowote katika bustani?"

Frame 02-01

Adamu na mke wake waliishi kwa furaha katika bustani nzuri ambayo Mungu aliwaandalia. Hawa wawili hawakuvaa nguo, lakini hawakuona haya kwa sababu hakukuwa na dhambi duniani. Mara nyingi walitembea katika bustani na kuongea na Mungu.

Frame 02-07

Ndipo Adamu na mke wake wakasikia sauti ya Mungu akitembea katika bustani. Wote wakajificha. Mungu akamwita mwanaume, "Uko wapi?" Adamu akajibu, "Nimekusikia ukitembea katika bustani, nikaogopa kwa kuwa ni uchi, hivyo nikajificha."

Frame 02-09

Mungu akamwambia Nyoka, "Umelaaniwa! kwa tumbo lako utaenda na utakula mavumbi. Wewe na mwanamke mtakuwa maadui, watoto wake na watoto wako watakuwa maadui pia. Uzao wa mwanamke utakuponda kichwa, nawe utamgonga kisigino chake."

Frame 02-03

Mwanamke akajibu, "Mungu alisema twaweza kula matunda ya miti yote ya bustani isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya." Mungu alisema, "mukila au kugusa matunda ya mti huo, mtakufa."

Frame 02-11

Mungu akamwambia mwanaume, "Umemsikiliza mke wako na hukunitii mimi. Sasa ardhi imelaaniwa, na utafanya kazi kwa bidii ili upate chakula. Na kisha utakufa, na mwili wako utarudi katika uchafu." Mwanaume akamwita mke wake jina Eva, akimaanisha "Mtoa uhai," kwakuwa atafanyika mama wa watu wote. Na Mungu akawavalisha Adamu na Eva mavazi ya ngozi ya Wanyama.

Frame 02-08

Kisha Mungu akamuuliza, "Ni nani aliyekuambia kuwa u uchi? Je, umekula tunda nililokuambia usile?" Mwanaume akajibu, "wewe ulinipa huyu mwanamke, naye amenipa tunda." Ndipo Mungu akamuuliza mwanamke, "Umefanya nini?" Mwanamke akajibu, "Nyoka alinidanganya."

Frame 02-05

Mwanamke aliona kuwa matunda yalikuwa mazuri na yalionekana kuwa matamu. Pia alitaka kuwa na hekima, hivyo alichuma tunda akala. Kisha akampa mume wake aliyekuwa pamoja naye, naye pia akala.

Simulizi ya Biblia Kutoka: Mwanzo 3

3. Gharika

Frame 03-15

Mungu aliahidi, "hata laani tena ardhi kwa sababu ya maovu wayafanyayo wanadamu, au kuharibu dunia kwa mafuriko. Japokuwa watu ni wenye dhambi tangu utotoni mwao."

Frame 03-12

Nuhu alisubiri wiki moja zaidi akamtuma Njiwa kwa mara ya tatu. Wakati huu, Njiwa alipata mahali pa kutua na hakurudi kwa Nuhu. Maji yalikuwa yamekauka!

Frame 03-13

Miezi miwili baadaye, Mungu alisema na Nuhu, "wewe na familia yako na wanyama wote sasa mwaweza kutoka nje ya Safina. Mzae watoto na wajukuu muijaze nchi." Ndipo Nuhu na familia yake wakatoka nje.

Frame 03-06

Mungu akatuma kwa Nuhu wanyama na ndege wawili wawili dume na jike, waingie katika Safina ili waokolewe na gharika. Mungu alituma wanyama wengine saba madume na saba majike wa kila aina ya wanyama, watakao tumika kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Baada ya wote kuingia ndani ya Safina, Mungu mwenyewe akafunga mlango.

Frame 03-10

Baada ya siku arobaini zaidi, Nuhu alimtuma Kunguru kwenda kutazama kama maji yamekauka. Lakini Kunguru alipopaa hakupata mahali pa kutua, kwani maji yalikuwa bado yameijaza nchi.

Frame 03-04

Nuhu alimtii Mungu. Yeye pamoja na watoto wake watatu wa kiume waliijenga Safina kama Mungu alivyo waagiza. Na kwa vile Safina ilivyokuwa kubwa, ilichukua miaka mingi kukamilika. Vile vile Nuhu aliwapa watu angalizo juu ya mafuriko yajayo, akawasihi wamrudie Mungu, lakini hawakumwamini.

Frame 03-02

Lakini Nuhu alipata neema machoni pa Mungu. Kwa sababu alikuwa ni mwenye haki miongoni mwa waovu. Mungu alimjulisha Nuhu kuhusu mpango wake wa kutuma mafuriko kwa wanadamu. Akamwambia Nuhu atengeneze Safina.

Frame 03-01

Baada ya muda mrefu, watu wengi waliishi katika ulimwengu. Nao walikuwa waovu na wenye vurugu. Hali ilikuwa mbaya sana hata Mungu akaaamua kuwaaangamiza kwa mafuriko.

Frame 03-07

Mvua ikaanza kunyesha, na kunyesha, na kunyesha. Ilinyesha kwa siku arobaini usiku na mchana bila kukata! Maji yalizidi kuongezeka na kuijaza dunia yote. Kila kitu katika dunia kilifunikwa na maji, hadi milima mirefu zaidi ilifunikwa.

Frame 03-09

Baada ya mvua kukata, Safina ilielea kwenye maji kwa muda wa miezi mitano, na baadaye maji yalianza kupungua. Hatimae siku moja Safina ikatulia juu ya mlima, wakati huo maji yalikuwa bado yameenea duniani kote. Na miezi mitatu baadaye, vilele vya milima vilianza kuonekana.

Frame 03-14

Baada ya Nuhu kutoka nje ya Safina, Nuhu alimjengea Mungu madhabahu na akamtolea sadaka ya aina ya wanyama waliopaswa kutolewa sadaka. Mungu alifurahishwa na sadaka hiyo akambariki Nuhu pamoja na familia yake.

Frame 03-03

Mungu alimwambia Nuhu atengeneze Safina yenye urefu wa meta 140, upana wa meta 23, na urefu kwenda juu meta 13.5. Nuhu aliijenga Safina yenye ghorofa tatu, vyumba vingi, madirisha pamoja na paa kwa kutumia mbao. Nayo Safina ilikuwwa na uwezo wa kumtunza Nuhu, familia yake na kila aina ya wanyama kwa yale mafuriko.

Frame 03-11

Baadaye Nuhu alimtuma njiwa. Lakini Njiwa pia hakupata mahali pa nchi kavu, hivyo alirudi kwa Nuhu. Wiki moja baadaye Nuhu alituma tena Njiwa, Safari hii njiwa alirudi na tawi la mzabibu mdomoni mwake! Hii ilionyesha kuwa maji yameanza kukauka, na miti imeanza kukua tena.

Frame 03-16

Mungu akatengeneza upinde wa mvua kama ishara ya ahadi yake. Kila upinde wa mvua unapotokea angani, Mungu akumbuke ahadi yake vilevile watu wake wakumbuke ahadi ya Mungu.

Frame 03-08

Kila kitu kilichoishi katika aridhi kilikufa, isipokuwa watu na wanyama waliokuwa katika Safina ndiyo walio salia. Safina ilielea juu ya maji na vyote vilivyokuwa ndani ya safina havikuzama.

Frame 03-05

Pia Mungu alimwamuru Nuhu na familia yake, akusanye chakula cha kutosha kwa ajili yao na wanyama. Na kila kitu kilipo kamilika, Mungu akamwambia Nuhu na mke wake, watoto wake watatu wa kiume, na wake zao waingie ndani ya Safina. Jumla yao ilikuwa watu wanane.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 6-8

4. Agano la Mungu na Abrahamu

Frame 04-06

Abrahamu alipofika Kanaani, Mungu akamwambia, "Tazama nitakupa nchi hii yote unayoiona wewe na uzao wako kuwa urithi wako." Kisha Abrahamu akaishi katika nchi ile.

Frame 04-04

Miaka mamia baadaye Mungu aliongea na mtu aitwaye Abrahamu. 'Toka katika nchi yako na jamaa zako uende mpaka nchi nitakayokuonesha. Nitakubariki na kukufanya taifa kubwa nitalikuza jina lako. Nitawabariki wakubarikio, Nitawalaani wakulaanio. Na katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa ."

Frame 04-02

Walikuwa na majivuno na hawakujali kama Mungu alivyosema. Wakajenga mji wakaweka mnara mrefu uliokaribia kufika mbinguni. Mungu akaona watu hawa wakiendelea kufanya uovu pamoja, watafanya matendo ya dhambi zaidi.

Frame 04-01

Miaka mingi baada ya gharika, watu wakaongezeka sana juu ya nchi. Wakati huo wakiwa wanaongea lugha moja. Badala ya kuijaza nchi kama Mungu alivyoamuru, walikusanyika sehemu moja wakajenga mji.

Frame 04-07

Siku moja Abrahamu akakutana na Melkizedeki, kuhani mkuu wa Mungu aliye juu. Melkizedeki akambariki Abrahamu akasema, "Mungu Mkuu mmiliki wa mbingu na dunia ambariki Abrahamu.'' Abrahamu akamtolea Melkizedeki fungu la kumi toka katika mali alizonazo.

Frame 04-09

Mungu akaweka tena agano na Abrahamu. Agano ni patano kati ya wawili. Mungu akamwambia "Nitakupa mtoto wa kiume kutoka katika mwili wako. Nitawapa uzao wako nchi ya Kanaani." Lakini Abrahamu bado alikuwa hajapata mtoto.

Frame 04-03

Mungu akagawanya lugha zao zikatokea lugha nyingi. Wakatawanyika juu ya dunia yote. Na jina la ule mji ukaitwa Babeli kwa kuwa'' hawakuelewana."

Frame 04-08

Abrahamu na Sarai waliishi miaka mingi bila kupata mtoto. Mungu Akasema na Abrahamu na kumuahidi tena kuwa atampa mtoto wa kiume na uzao mwingi kama nyota za angani. Abrahamu akaamini ahadi ya Mungu. Mungu akamwita Abrahamu mwenye haki kwa kuwa aliamini ahadi yake.

Frame 04-05

Hivyo, Abrahamu akamtii Mungu. Akamchukua Sarai mkewe, na watumishi wake na mali zote alizokuwa nazo, akaenda mpaka nchi ile Mungu aliyomuonesha nchi ya Kanaani.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 11-15

5. Mtoto wa Ahadi

Frame 05-06

Isaka alipokuwa kijana, Mungu akaijaribu imani ya Ibrahimu na kumwambia, "Mchukue, Isaka kijana wako wa pekee, na umuue kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yangu. "Ibrahimu alimtii Mungu na kumwandaa kijana kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

Frame 05-10

Kisha Mungu akamwambia Ibrahimu. "Kwa sababu ulikuwa tayari kutoa kila kitu kwa ajili yangu hata kijana wako wa pekee, naahidi kukubariki wewe. Uzao wako utaongezeka zaidi kama nyota za angani. Kwa sababu umenitii mimi, familia zote ulimwenguni watabarikiwa kwa sababu ya familia yako ."

Frame 05-04

Mkeo Sarai, atapata mtoto wa kiume, atakuwa mtoto wa ahadi. Utamwita Isaka. Nitafanya Agano langu pamoja naye. Naye atakuwa taifa kubwa. Nitamfanya Ishmaeli kuwa Taifa kubwa pia. Lakini Agano langu litakuwa pamoja na Isaka. "Kisha Mungu akabadili jina la Abrahamu kuwa Ibrahimu, maana ya jina hilo ni "baba wa wengi." Mungu pia akabadili jina la Sarai kuwa Sara, maana yake "mtoto wa mfalme ."

Frame 05-02

Hivyo Abraham akamwoa Hajiri. Hajiri akapata mtoto wa kiume, Abrahamu akampa jina Ishmaeli. Lakini Sarai akamwonea wivu Hajiri. Alipotimiza umri wa miaka kumi na tatu, Mungu akaongea na Abrahamu.

Frame 05-01

Baada ya kuishi miaka kumi katika nchi ya Kaanani, Abraham na Sarai hawakuwa na mtoto. Sarai mke wa Abraham akamwambia," kwa kuwa Mungu hajanipa mtoto nami ni mzee sana siwezi kupata mtoto. Mchukue Hajiri mjakazi wangu umwoe ili anizalie mtoto."

Frame 05-07

Ibrahimu na Isaka walipokuwa wakitembea kuelekea eneo la kutoa sadaka, Isaka akauliza. "Baba, kuni kwa ajili ya sadaka tunazo, lakini kondoo yuko wapi?" Ibrahimu akajibu. "Mungu atajipatia kondoo kwa ajili ya sadaka, mtoto wangu."

Frame 05-09

Karibu naye, Ibrahimu akaona kondoo amejinasa kwenye kichaka. Mungu akampatia kondoo kuwa sadaka ya kuteketezwa badala ya Isaka. Ibrahimu kwa furaha akamtoa kondoo kuwa sadaka ya kutekezwa.

Frame 05-03

Mungu akasema, "Mimi ni Mungu mkuu. nitafanya agano pamoja nawe. "Kisha Abrahamu akasujudu. Pia Mungu akamwambia Abrahamu, "Utakuwa baba wa mataifa mengi. Nitakupatia wewe na uzao wako nchi ya kanaani kuwa miliki yao na nitakuwa Mungu wao milele. Nawe utawatairi wanaume wote wa familia yako."

Frame 05-08

Walipofika eneo la kutoa sadaka, Ibrahimu akamfunga kijana wake Isaka na kumlaza juu ya mazabahu. Alikuwa anajiandaa kumwua kijana wake Mungu akasema, "Acha! Usimdhuru kijana! Sasa natambua unaniogopa mimi kwa sababu hukumwacha kijana kwa ajili yangu."

Frame 05-05

Siku hiyo Abrahamu akawatairi wanaume wote wa nyumba yake. Baada ya mwaka mmoja, Ibrahimu alitimiza miaka 100 na Sara miaka 90, Sara akazaa na Ibrahimu mtoto wa kiume. Wakamwita jina lake Isaka kama Mungu alivyowaagiza.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 16 - 22

6. Mungu anamjalia Isaka

Frame 06-06

Mungu akamwambia Rebeka, " Mataifa mawili yatatokea kutokana na watoto wawili wa kiume walio tumboni mwako. Na kutakuwa na ushindani kati yao, na mtoto mkubwa atamtumikia mdogo."

Frame 06-04

Baada ya muda mrefu, Ibrahimu alifariki na ahadi zote alizokuwa ameahidiwa na Mungu katika agano zilihamishwa kwa Isaka, mwanae. Mungu alikuwa ameahidi kuwa Ibrahimu atakuwa na uzao mwingi usiohesabika, lakini Rebeka, mkewe Isaka, hakujaliwa kuwa na watoto.

Frame 06-02

Baada ya safari ndefu ya kwenda walikoishi ndugu zake na Ibrahimu, Mungu alimwongoza mtumishi wa Ibrahimu kwa Rebeka. Rebeka alikuwa ni mjukuu wa kaka yake na Ibrahimu.

Frame 06-01

Wakati Ibrahimu alipokuwa mzee sana, mtoto wake wa kiume, Isaka alikuwa amekuwa mtu mzima. Ibrahimu alimtuma mmoja wa watumishi wake kwenda katika nchi walioishi ndugu zake na Ibrahimu ili kumtafutia mke kwa ajili ya mtoto wake, Isaka.

Frame 06-07

Na siku ile walipozaliwa watoto wa Rebeka, mtoto mkubwa alitoka akiwa mwekundu na mwenye nywele nyingi katika mwili wake; walimwita jina lake, Esau. Mtoto mdogo alizaliwa huku akiwa amekishikilia kisigino cha Esau, naye walimwita jina lake, Yakobo.

Frame 06-03

Rebeka alikubali kuiacha familia yake na kwenda pamoja na yule mtumishi wa Ibrahimu hadi nyumbani kwa Isaka. Na mara baada ya kufika huko, Isaka alimuoa Rebeka.

Frame 06-05

Isaka alimwombea Rebeka. Mungu alimjibu na Rebeka akabeba mimba ya mapacha. Wale watoto wawili walikuwa wakishindana tumboni mwa Rebeka. Rebeka akamwuliza Mungu juu ya hicho kilichokuwa kikitokea tumboni mwake.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 24 :1-25:26

7. Mungu Anambariki Yakobo

Frame 07-06

Rebeka alisikia mpango wa Esau. Yeye na Isaka walimtorosha Yakobo aende mbali akaishi na ndugu zake.

Frame 07-10

Ila Esau alikuwa amemsamehe Yakobo, na walifurahi kuonana tena kila mmoja.Yakobo akaishi Kanaani kwa amani. Isaka akafa huko, Esau naYakobo wakamzika. Ahadi za agano, Mungu alizomhaidia Ibrahimu kumpata zikatoka kwa Isaka kwenda kwa Yakobo.

Frame 07-04

Yakobo alikuja kwa Isaka akasema, "mimi ni Esau. Nimekuja ili kwamba unibariki." Isaka aliposikia harufu na kuhisi nywele za mbuzi na kunusa nguo, alidhani ni Esau na akambariki.

Frame 07-02

Siku moja Esau alipotoka kuwinda, alikuwa na njaa sana, Esau alisema kwa Yakobo, "tafadhali naomba chakula ulichopika." Yakobo akajibu akamwambia, "kwanza nipe mimi haki yako ya mtoto mkubwa". Ndipo Esau akampa haki yake ya mtoto mkubwa."Hivyo Esau alimpa Yakobo chakula.

Frame 07-01

Wavulana walipokomaa, Yakobo alipenda kukaa nyumbani, ila Esau alipenda kuwinda. Rebeka alimpenda Yakobo, ila Isaka alimpenda Esau.

Frame 07-07

Yakobo akaishi na ndugu zake Rebeka kwa miaka mingi. Katika kipindi hicho alioa na akazaa watoto wa kiume kumi na wawili na wa kike mmoja. Mungu akamtajirisha sana.

Frame 07-09

Yakobo aliogopa sana kwa sababu alidhani Esau bado alitaka kumuua. Akatuma makundi ya mifugo kwa Esau kama zawadi. Watumwa waliopeleka mifugo wakasema kwa Esau, "Mtumwa wako Yakobo anakupa wewe mifugo hii. Anakuja hivi karibuni."

Frame 07-03

Isaka alitaka kumpa Esau baraka zake. Kabla ya kufanya hivyo, Rebeka na Yakobo wamdanganya kwa Yakobo kujifanya kuwa Esau. Isaka alikuwa mzee na hakuweza kuona. Yakobo alivaa nguo za Esau na ngozi za mbuzi mikononi na shingoni.

Frame 07-08

Baada ya kuishi nje ya Kanaani kwa miaka ishirini, Yakobo alirudi nyumbani na familia yake, watumwa wake, na mifugo yake yote.

Frame 07-05

Esau alimchukia Yakobo kwa kuwa Yakobo alikuwa ameiba haki yake ya kuwa mkubwa na baraka zake. Hivyo alipanga moyoni mwake kumuua baada ya baba yao kufariki.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 25:27 - 33:20

8. Mungu anamuokoa Yusufu na Familia yake.

Frame 08-15

Kama ambavyo Mwenyezi Mungu alikuwa amemuahidi Ibrahimu, maagano yote yakarithishwa kwa vizazi vyake yaani, Isaka, kisha Yakobo, na hatimaye watoto kumi na wawili wa Yakobo pamoja na uzao wao, ambao ndio wanaounda kabila kumi na mbili za Israeli.

Frame 08-12

Yusufu aliamua kufanya mahojiano nao akitaka kujua iwapo walikuwa wamebadilika kitabia, kisha akawaambia hivi: "msihofu ndugu zangu, mimi mnaeniona ndiye mdogo wenu Yusufu. Najua fika hamkuwa na nia njema na mimi mliponiuza kama mtumwa, lakini Mwenyezi Mungu aliitumia nia yenu mbaya kwa ajili ya kusudi jema." Nawakaribisha muwe huru kuja kuishi hapa Misri ili niwatunze ninyi na familia zenu.

Frame 08-13

Ndipo kaka zake Yusufu waliporudi nyumbani kwao, Kanaani, walimpasha habari baba yao kuwa Yusufu , mwanae mpendwa bado yuko hai; Yakobo baba yake na Yusufu alijawa na furaha isiyo kifani.

Frame 08-06

Yusufu alikuwa bado yumo gerezani hadi miaka miwili baadae, japo hakuwa na kosa lolote. Siku moja nyakati za usiku, Farao, mfalme wa Wamisri, aliota ndoto mbili zikamsumbua sana mawazoni mwake usiku ule. Miongoni mwa washauri wake wote na wenye hekima, hapakuwa na mtu yeyote mwenye uwezo wa kutoa maana ya ndoto hizo.

Frame 08-10

Hali ya ukame na njaa, ikazidi kuwaathiri watu wengi wa Misri yenyewe na hata nchi ya Kanaani alikoishi Yakobo baba yake na Yusufu pamoja na familia yake.

Frame 08-04

Na ndipo wale wafanyabiashara ya watumwa, wakamsafirisha Yusufu hadi nchi ya mbali sana iitwayo Misri. Nchi ya Misri ilikuwa maarufu na hodari kwa mambo mengi katika nchi za mwambao wa mto Naili.Yusufu akauzwa kama mtumwa katika nyumba ya afisa mmoja wa serikali ya misri aliyekuwa tajiri sana. Naye Yusufu akatumika kwa uaminifu sana katika nyumba ya bwana wake, na Mungu akambariki sana Yusufu.

Frame 08-02

Kwakuwa Yusufu alikuwa anapendwa sana na baba yake, na kwamba siku moja aliwahi kuota ndoto na akawasimulia kaka zake kwamba yeye atakuwa mtawala wao hapo baadae, kaka zake walimchukia. Hivyo, Yusufu alipofika kwa kaka zake, walimteka na wakamuuza kwa watu wenye kufanya biashara ya watumwa.

Frame 08-01

Baada ya miaka mingi kupita, Yakobo alipokuwa mzee sana, alimuagiza kijana wake aitwaye Yusufu, kuwatembelea kaka zake waliokuwa wakichunga mifugo ya baba yao.

Frame 08-07

Kwakuwa Mwenyezi Mungu alikuwa amemjalia Yusufu uwezo wa kipekee wa kutafsiri ndoto, Farao, mfalme wa Misri, aliamuru Yusufu aletwe kwake kutoka gerezani ili atoe maana halisi ya ndoto hiyo. Kwa kuongozwa na Mwenyezi Mungu, Yusufu akasimama mbele ya Farao kutafsiri ndoto zile akisema; "Wakati unakuja ambapo Mwenyezi Mungu ataruhusu pawepo na kipindi cha miaka saba ya mavuno mengi, itakayofuatiwa na miaka mingine saba ya ukame na njaa."

Frame 08-09

Basi Yusufu akawatangazia watu wote wa Misri kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha watakapovuna katika kipindi cha miaka saba ya mavuno mengi. Ilipowadia ile miaka saba mingine ya njaa, ndipo Yusufu akatumia sehemu ya akiba ya chakula kuwauzia watu ili kiwafae katika kile kipindi cha miaka saba ya njaa.

Frame 08-14

Katika kipindi hicho, Yakobo alikuwa amekwisha kuwa mzee sana. Lakini akalazimika kuhamia katika nchi ya Misri yeye na familia yake yote. Hivyo, Yakobo akaishi pamoja na familia yake katika nchi ya Misri na kabla hajafariki akawapa mibaraka wanae wote, kila mmoja na mbaraka wake.

Frame 08-03

Basi kaka zake na Yusufu walipotaka kurudi nyumbani, walikubaliana kwa hila kuzichanachana nguo za mdogo wao, Yusufu, kisha wakaziloweka kwenye damu ya mbuzi. Walipofika wakamuonyesha baba yao nguo hizo zenye damu, ili kumuaminisha kuwa kuna mnyama mkali wa porini amemrarua na kumuua Yusufu. Basi Yakobo aliposikia habari hiyo alimhuzunikia sana Yusufu.

Frame 08-11

Hivyo, Yakobo akawaagiza vijana wake wakubwa kwenda Misri kununua chakula. Walipokuwa wakingojea zamu yao ya kununua chakula, Yusufu aliwaona kaka zake na akawatambua, ila wao walikuwa wamemsahau Yusufu.

Frame 08-08

Yusufu akateuliwa kuwa mtu wa pili kwa mamlaka katika nchi yote ya Misri, kwa kuwa Farao, mfalme wa Misri, alifurahishwa na kuvutiwa sana na Yusufu.

Frame 08-05

Mke wa tajiri yake alimtaka Yusufu ili azini naye, lakini Yusufu alikataa ili asimkosee Mungu. Kisha baada ya hayo, yule mwanamke, mke wa tajiri, alikasirika sana, hata akamtuhumu Yusufu kwa kumsingizia ili Yusufu akamatwe na kufungwa gerezani. Hata hivyo, Yusufu aliendelea kuwa mwaminifu mbele za Mungu hata alipokuwa amefungwa gerezani, na Mwenyezi Mungu akambariki. Hata ilipotimia miaka miwili baadae, Yusufu alikuwa bado yumo gerezani, japo hakuwa na kosa lolote.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 37-50

9. Mungu Anamwita Musa

Frame 09-15

Musa hakutaka kwenda kwa Farao kwani aliogopa, kwa sababu alihofia kutoweza kuongea vizuri. Mungu alimruhusu Haruni nduguye amsaidie. Aliwaonya kuwa Farao atakuwa na moyo mgumu.

Frame 09-12

Siku moja Musa alikuwa akichunga kondoo wake, aliona kichaka kilichowaka moto bila kuteketea. Musa alisogea kuona vizuri, alipokaribia, Mungu alisikika akisema, "Musa vua viatu vyako. Ardhi uliyosimama juu yake ni takatifu".

Frame 09-13

Mungu alimwambia Musa," Nimeyaona mateso ya watu wangu. Ili kuwakomboa kutoka utumwani huko Misri, nitakutuma wewe kwa Farao ukawaondoe Waisraeli kutoka utumwani Misri. Nami nitawapa nchi ya Kanaani, niliyowaahidia Ibrahimu, Isaka na Yakobo."

Frame 09-06

Mtoto huyo alipokuwa hawezi kufichika tena, ili kumuokoa wazazi walimweka katika kikapu kieleacho na kukiweka katika majani kando ya mto Naili. Ili kujua kuwa ni jambo gani lingempata mtoto huko mtoni dada yake alikuwa akifanya uchunguzi.

Frame 09-10

Habari za mauaji zilipomfikia Farao, aliazimia kumuua Musa. Musa alitoroka kutoka Misri na kukimbilia nyikani ili kujiokoa na walinzi wa Farao.

Frame 09-04

Farao aliona kuwa Waisraeli walikuwa wanazaa watoto wengi, aliamuru watoto wa kiume wauawe kwa kutupwa katika mto Naili.

Frame 09-02

Mamia ya miaka mingi ilipita, wakazidi kuongezeka. Wamisri walimsahau Yusufu na kazi nzuri alizozifanya kwa Wamisri. Wamisri waliwaogopa Waisraeli kwa kuwa walikuwa wengi na Farao wa kipindi hicho aliwafanya kuwa watumwa kwa Wamisri.

Frame 09-01

Yusufu alipofariki, ndugu zake walidumu kuishi huko Misri. Wao pamoja na wazazi wao, kwa miaka mingi waliongezeka na walikuwa na watoto wengi. Kabila hilo waliitwa Waisraeli

Frame 09-07

Mtoto wa kike wa Farao aliona kikapu na alichungulia ndani yake. Alipoona mtoto, alimchukua awe wake na kumwajiri mwanamke wa Kiyahudi amtunze. Bila kutambua, mama huyo mlezi ndiye alikuwa mzazi wa mtoto huyo. Mtoto alipoacha kunyonya alikabidhiwa kwa binti Farao naye akamwita jina lake Musa.

Frame 09-09

Musa alimuua Mmisri na kuuzika mwili wake akidhani kwamba hakuna mtu ambaye angemwona. Kumbe mtu mmoja alimwona akifanya kitendo hicho.

Frame 09-14

Musa akauliza, watakapotaka kujua Ni nani aliyenituma kwao nisemeje? Mungu akasema, "MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Waambie AMBAE NIKO amenituma. Mimi ni YEHOVA Mungu wa baba zenu Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Jina langu ndilo hilo milele."

Frame 09-03

Waisraeli walitumikishwa na Wamisri kwa kazi ngumu kwa kujenga majumba na miji mikubwa. Ugumu wa kazi ulisababisha huzuni kimaisha. Bali baraka za Mungu ziliwazidishia watoto kwa wingi.

Frame 09-11

Musa alikuwa mchungaji wa kondoo huko nyikani mbali na nchi ya Misri. Alioa huko na kuzaa watoto wawili wa kiume.

Frame 09-08

Akiwa mtu mzima, siku moja Musa alimkuta Mmisri akimpiga mtumwa wa Kiisraeli. Na alijitahidi kumuokoa Mwisraeli mwenzake.

Frame 09-05

Mtoto wa kiume alizaliwa na mama mmoja wa Kiisraeli. Wazazi wa mtoto huyo walimficha kwa muda walioweza.

Simulizi ya Biblia katika: Kutoka 1-4

10. Mapigo Kumi

Frame 10-12

Ingawa kulitokea mapigo tisa Farao hakukubali kuwaruhusu Waisraeli kuondoka. Kwa kuwa Farao hangeweza kusikiliza Mungu alikusudia kuleta pigo la mwisho. Pigo hili lingemfanya Farao kubadilisha mawazo yake.

Frame 10-06

Mungu alileta pigo la ugonjwa kwa mifugo wa Wamisri kwamba mifugo iliugua na kufa. Hata hivyo Farao alikuwa kaidi kuweza kuwaruhusu Waisreli kuondoka.

Frame 10-10

Kwa sababu hiyo Mungu alituma nzige wengi sana walioharibu mazao yote yaliyosalia na mvua ya mawe katika nchi ya Misri

Frame 10-04

Mungu alileta vyura kuwasumbua Wamisri wote. Farao alimwomba Musa aombe ili vyura wasiendelee kuwepo. Lakini baada ya Musa kuomba na vyura kutoweka moyo wa Farao uliendelea kuwa mgumu asiwaruhusu Waisraeli kuondoka katika nchi ya Misri.

Frame 10-02

Farao aliendelea kuwakatalia Waisraeli wasiondoke, kwa sababu hiyo Mungu alileta mapigo kumi kwa Wamisri ya madhara makubwa sana. Kwa kufanya hivyo Mungu alionesha kuwa yeye anao uwezo mkubwa kuliko Farao na miungu yote ya Wamisri.

Frame 10-01

Watu wawili ambao ni Musa na Haruni walimwendea Farao na kumweleza kwamba, "Mungu wa Israeli anasema hivi, waruhusu watu wangu kuondoka katika nchi ya Misri." Farao hakukubali, alichofanya ni kuongeza uzito wa kazi kuliko hapo awali.

Frame 10-07

Ndipo Mungu akamwambia Musa kupeperusha majivu angani machoni pa Farao. Majivu hayo yalisababisha majipu yenye vidonda kwa Wamisri peke yake, Waisraeli hawakudhurika na majipu hayo. Mungu alimfanya Farao kuwa na moyo wa ukaidi na hivyo hakuweza kuwaruhusu Waisraeli kuondoka.

Frame 10-09

Farao hata hivyo, hakuacha kutenda dhambi na moyo wake ukaendelea kuwa wenye ukaidi kwa kutowaachia uhuru Waisraeli kuondoka.

Frame 10-03

Mungu aliyabadilisha maji ya mto Naili kuwa damu. Pamoja na pigo kama hilo Farao hakutoa ruhusa kwa Waisraeli kuondoka katika nchi ya Misri.

Frame 10-11

Ndipo Mungu alileta giza totoro katika nchi ya Misri lillosababisha Wamisri wabakie majumbani mwao, wasitoke kwa muda wa siku tatu. Lakini mahali Waisraeli walipokuwa hapakuwa na giza.

Frame 10-08

Baada ya janga la majipu, Mungu alileta mvua ya mawe iliyo haribu mazao na kuleta maafa kwa mtu yeyote aliyenyeshewa na mvua hiyo katika nchi ya Misri. Farao alionekana kujuta aliwaita Musa na Haruni na kusema, "nimefanya dhambi," sasa nitawaruhusu kuondoka. Musa alimwomba Mungu, mvua haikuendelea kunyesha.

Frame 10-05

Kwa sababu hiyo Mungu alileta pigo la chawa. Zaidi ya hapo Mungu alileta nzi, pigo ambalo lilimfanya Farao kuwaita Musa na Haruni kuwaambia kuwa kama janga hilo wataliondoa watapewa ruhusa ya kuondoka katika nchi ya Misri. Musa alimwomba Mungu kuondoa janga la nzi na Mungu akawaondoa nzi wote. Hata hivyo moyo wa Farao ulikuwa mgumu asiwaruhusu Waisraeli kuondoka.

Simulizi ya Biblia katika: Kutoka 5-10

11. Pasaka

Frame 11-06

Wamisri hawakuamini wala kutii maelekezo ya Mungu. Hivyo basi Mungu hakupita juu ya nyumba zao. Akawauwa wazaliwa wao wa kwanza wa kiume.

Frame 11-04

Waisraeli walitimiza yote waliyoagizwa na Mungu. Usiku wa manane Mungu alipita juu ya Wamisri wote na kuwaua wazaliwa wao wote wa kwanza wa kiume.

Frame 11-02

Mungu alifanya njia ya kuwaokoa wazaliwa wa kwanza wa kiume kwa yeyote atakayemwamini Yeye. Kila nyumba ya Israeli ilipaswa kuchagua mwanakondoo aliye mkamilifu na kumchinja.

Frame 11-01

Mungu alimuonya Farao ikiwa hatawaruhusu Waisraeli kuondoka, ya kuwa atawaua wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa watu wa Misri na wa wanyama. Baada ya kusikia hayo Farao aliendelea kutomwamini wala kumtii Mungu.

Frame 11-07

Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Wamisri alikufa, tangu mzaliwa wa kwanza wa aliyekuwa gerezani mpaka mzaliwa wa kiume wa kwanza wa Farao. Wengi walilia na kuomboleza kwa ajili ya huzuni kubwa iliyowapata.

Frame 11-03

Mungu aliwaelekeza Waisraeli kupaka damu ya Mwanakondoo kwenye milango yao, kuichoma nyama ya Mwanakondoo na kuila kwa haraka pamoja na mikate isiyowekewa amira. Vile vile Mungu aliwaambia mara baada ya kula wawe tayari kuondoka Misri.

Frame 11-08

Usiku ule ule, Farao aliwaita Musa na Haruni na kuwaambia, "wachukueni Waisraeli muondoke haraka." Hata Wamisri pia waliwasihi Waisraeli watoke haraka.

Frame 11-05

Nyumba zote za Waisraeli zilipakwa damu katika milango yake, hivyo Mungu alipita juu ya nyumba zao. Katika nyumba hizo wote waliokolewa. Walipona kwa sababu ya damu ya Mwanakondoo.

Simulizi ya Biblia: Kutoka 11:1-12:32

12. Kutoka

Frame 12-12

Waisraeli walipowaona Wamisri wamekufa, walimsifu Mungu na kuamini kuwa Musa alikuwa nabii wa Mungu.

Frame 12-13

Waisraeli walifurahi sana vile ambavyo Mungu alivyo waokoa kutoka katika kifo na utumwa! Sasa walikuwa huru kumtumikia Mungu. Waisrali waliimba nyimbo nyingi kusherehekea uhuru wao na kumsifu Mungu kwa kuwa amewaokoa kutoka majeshi ya Wamisri.

Frame 12-06

Kisha Mungu akaiweka ile nguzo ya wingu kati ya Waisraeli na Wamisri ili Wamisri wasiwaone Waisraeli.

Frame 12-10

Kwa hiyo Wamisri wakawafuata Waisraeli kwa kupitia njia ile ya Bahari. Mungu akawatia hofu Wamisri na magari yao yakakwama. Ndipo Wamisri wakaambizana, "tukimbie maana Mungu anawapigania Waisraeli!"

Frame 12-04

Kwa hiyo Farao alilituma jeshi lake ili wawafuate Waisraeli ili kusudi waendelee kuwa watumwa wao. Na Waisraeli walipotambua kuna majeshi ya Farao yanawafuata na ya kwamba mbele yao kuna Bahari ya Shamu, mioyo yao ilijaa hofu na wakaanza kulia, "kwa nini tumetoka Misri? Tutakufa!"

Frame 12-02

Mungu aliwaongoza Waisraeli kwa nguzo ya wingu iliyokuwa juu yao wakati wa mchana, ambayo wakati wa usiku ilibadilika na kuwa nguzo ya moto. Mungu alikuwa pamoja na Waisraeli na kuwaongoza. Walichopaswa kufanya ni kumfuata yeye pekee.

Frame 12-01

Waisraeli walifurahia sana kutoka katika nchi ya Misri. Hawakuwa watumwa tena. Walikuwa wakienda katika nchi ya ahadi! Wamisri waliwapa Waisraeli chochote walichohitaji, hata dhahabu na shaba na mali zingine za thamani. Waliondoka na watu wa mataifa mengine waliomwamini Mungu wa Israeli.

Frame 12-07

Mungu akamwambia Musa ainue mkono wake kuelekea kwenye Bahari na kuyagawanya maji. Ndipo Mungu akaleta upepo ulio sababisha kuyatenga maji ya Bahari upande wa kushoto na upande wa kulia na kukawa na njia kubwa katikati ya Bahari.

Frame 12-09

Kisha Mungu akaiondoa ile nguzo ya wingu aliyoiweka ili kwamba Wamisri, waliokuwa wakiwafuata washuhudie vile ambavyo Waisraeli walivyokuwa wakikimbia. Wamisri wakaamua kuwafuatilia.

Frame 12-14

Mungu aliwaamuru Waisraeli kuazimisha Pasaka kila mwaka kukumbuka jinsi Mungu alivyowapa ushindi dhidi ya Wamisri na kuwaokoa na utumwa. Walisherehekea kwa kuchinja mwanakondoo mkamilifu, na kumla pamoja na mikate isiyo na amira.

Frame 12-03

Baada ya kipindi kifupi Farao na washauri wake walibadili mawazo na kutaka Waisraeli wawe watumwa wao tena. Mungu aliushupaza moyo wa Farao ili kwamba watu wajue kuwa yeye ni Mungu mmoja wa kweli, na wajue kwamba yeye, Yawe, ni mwenye uwezo mkuu kuliko Farao na miungu yake.

Frame 12-11

Baada ya Waisraeli wote kuvuka na kufika upande wa pili wa bahari, Mungu akamwabia Musa nyosha mkono wako tena. Alipotii, maji yalirudi kwenye sehemu yake na kuwafunika Wamisri wote waliokuwa wakiwafuatilia. Jeshi lote la Wamisri wakafa maji.

Frame 12-08

Waisraeli walipita katika ile nchi kavu baharini wakiwa wamezungukwa na maji pande zote.

Frame 12-05

Musa akawambia Waisraeli, "msiogope, kwa sababu Mungu atawapigania na kuwaokoa dhidi ya majeshi ya Farao. Kisha Mungu akamwambia Musa, waambie Waisraeli wasonge mbele kuelekea Bahari ya Shamu.

Simulizi ya Biblia: Kutoka:12:33-15:21

13. Agano la Mungu na Israeli

Frame 13-15

Musa alitengeneza mbao mpya za mawe za amri kumi za Mungu sawa na zile za kwanza zilizovunjika. Kisha alipanda tena mlimani na kuomba kwamba awasamehe hao watu. Musa alishuka mlimani na hizo mbao mpya za mawe zilizoandikwa amri kumi za Mungu. Kisha Mungu aliwaongoza Waisraeli kutoka mlima Sinai kuelekea nchi ya ahadi.

Frame 13-12

Haruni alitengeneza sanamu ya dhahabu kwa sura ya ndama. Watu walianza kuiabudu sanamu ya dhahabu nyikani na kutoa dhabihu juu yake. Mungu aliwakasirikia Kwa sababu ya dhambi yao na kupanga kuwaangamiza. Bali Musa aliwaombea, na Mungu akasikiliza maombi yake na kutokuwaangamiza.

Frame 13-13

Musa aliposhuka mlimani na kuiona hiyo sanamu alikasirika sana akazivunja hizo mbao za mawe zilizoandikwa amri kumi za Mungu.

Frame 13-06

Waheshimu Baba yako na Mama yako, usiue, usizini, usiibe., usiseme uongo, usimtamani mke wa jirani yako, nyumba yake au chochote kilicho chini ya milki yake.

Frame 13-10

Watu walikubali kutii sheria ambazo Mungu aliwapa, kumwabudu Mungu pekee na kuwa watu wake maalumu. Lakini muda mfupi baada ya kuahidi kumtii Mungu, walimwasi vibaya sana.

Frame 13-04

Kisha Mungu aliwapa Agano akisema, "Mimi ni Yawe, Mungu wako aliyekuokoa kutoka utumwani Misri. Msiabudu miungu mingine."

Frame 13-02

Mungu akasema na Musa na wana wa Israeli, "kama mtanitii na kulishika agano langu mtakuwa miliki yangu ya thamani, Makuhani wa Kifalme na taifa takatifu."

Frame 13-01

Baada ya Mungu kuwaongoza wana wa Israeli kupita bahari nyekundu, aliwaongoza kupitia nyikani hadi mlima ulioitwa Sinai. Mlima huu ndio mlima Musa alikiona kichaka kilichokuwa kikiwaka moto. Watu waliweka mahema yao pembezoni mwa mlima.

Frame 13-07

Ndipo Mungu akaandika amri kumi katika mbao mbili za mawe akampa Musa. Vilevile Mungu alitoa sheria na amri nyingi na miongozo ya kufuata. Ikiwa watu watazitii sheria hizo, Mungu aliwaahidi kuwalinda na kuwabariki. Kama hawatamtii, Mungu angewaadhibu.

Frame 13-09

Kila ambaye hakuzitii sheria za Mungu, alipaswa kuleta mnyama kwenye madhabahu mbele ya hema ya kukutania kama dhabihu kwa Mungu. Kuhani alimchinja huyo mnyama na kumteketeza juu ya madhabahu. Damu ya mnyama huyo ilikuwa dhabihu ya kufunika dhambi za mtu na kuwa safi machoni pa Mungu. Mungu alimchagua Haruni ndugu yake na Musa na uzao wa Haruni kuwa Makuhani.

Frame 13-14

Musa aliisagasaga sanamu na kuwa unga na kuutupa huo unga katika maji na watu kunywa hayo maji . Mungu alituma pigo kwa watu na wengi wao walikufa.

Frame 13-03

Baada ya siku tatu, watu walipokuwa wamejiandaa kiroho, Mungu alishuka juu ya mlima Sinai kwa ngurumo na radi, moshi na sauti ya mvumo wa tarumbeta. Musa peke yake aliruhusiwa kupanda mlimani.

Frame 13-11

Kwa siku nyingi, Musa alikuwa juu ya mlima Sinai akizungumza na Mungu. Watu walichoka kumsubiri alipokawia kurudi. Kwa hiyo walimletea Haruni dhahabu na kumtaka awatengenezee sanamu kwa ajili yao!

Frame 13-08

Mungu aliwapa Waisraeli maelekezo ya kina ya namna hema alivyota liwe. liliitwa hema la kukutania, na lilikuwa na vyumba viwili vilivyogawanywa kwa pazia kubwa. Kuhani Mkuu peke yake aliruhusiwa kuingia kwenye chumba nyuma ya pazia. Kwa sababu Mungu aliishi humo.

Frame 13-05

"Usijifanyie sanamu ya kuchonga wala usiiabudu, kwa sababu mimi Yawe ni Mungu mwenye wivu. Msilitaje bure jina la Bwana Mungu. Ikumbukeni siku ya sabato na kuitakasa. Kwa maneno mengine, fanya kazi kwa siku sita na siku ya saba ni sabato ya kupumzika kunikumbuka mimi."

Simulizi ya Biblia: Kutoka 19-34

14. Kuzunguka Jangwani

Frame 14-15

Kisha Mungu alimwambia Musa kwenda juu ya kilele cha mlima ili aione nchi ya ahadi. Musa aliiona nchi ya ahadi lakini Mungu hakumruhusu kuiingia. Kisha Musa alikufa, na Waisraeli walimwombolezea kwa siku thelathini. Yoshua akawa kiongozi wao. Yoshua alikuwa kiongozi mzuri kwa sababu alimtegemea na kumtii Mungu.

Frame 14-12

Mungu kwa miujiza aliwapa maji kutoka katika mwamba. Lakini pamoja na hayo yote, Waisraeli walimlalamikia na kumnung'unikia Mungu. Hata hivyo, Mungu alikuwa mwaminifu kutunza ahadi zake kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

Frame 14-13

Wakati mwingine watu walipokuwa hawana maji yoyote, Mungu alimwambia Musa, "Uambie mwamba, na maji yatatoka humo." Lakini Musa hakumheshimu Mungu mbele ya watu wote kwa kuupiga mwamba mara mbili kwa fimbo badala ya kuuambia. Maji yalitoka katika mwamba kwa ajili ya kila mmoja kunywa , lakini Mungu alimkasirikia Musa na kusema, "Hutaingia katika nchi ya ahadi."

Frame 14-06

Hapo hapo, Kalebu na Yoshua, wapelelezi wengine wawili walisema, "Ni kweli kwamba watu wa Kanaani ni warefu na wenye nguvu lakini kwa hakika tunaweza kuwashinda! Mungu atatupigania!"

Frame 14-10

Mungu hakwenda nao katika vita hivi, kwa hiyo walishindwa vitani na wengi wao waliuawa. Kisha Waisraeli walirudi kutoka Kanaani nao wakazunguka jangwani kwa miaka arobaini.

Frame 14-04

Waisraeli walipofika mpakani mwa Kanaani, Musa alichagua wanaume kumi na wawili, mmoja kutoka kila kabila la Israeli. Aliwapa maelekezo ya kwenda kuipeleleza nchi kuona ilivyo. Walipaswa pia kuwachunguza wakanaani kuona kama ni wenye nguvu au dhaifu.

Frame 14-02

Mungu alikuwa amemwahidi Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwamba atawapa wazao wao nchi ya ahadi, lakini wakati huo kulikuwa na makundi ya watu wengi waliokuwa wakiishi humo. Walikuwa wakiitwa Wakanaani. Wakanaani hawakumwamini wala kumtii Mungu. Waliabudu miungu yao ya uongo na walifanya maovu mengi.

Frame 14-01

Mungu alipokwisha kuwaambia Waisraeli sheria ambazo alitaka wazitii kama sehemu ya Agano lake na wao, walitoka Mlima Sinai. Mungu alianza kuwaongoza kuelekea Nchi ya Ahadi iliyoitwa Kanaani. Nguzo ya wingu ilikwenda mbele yao ikiwangoza kwenda Kanaani na wao waliifuata.

Frame 14-07

Lakini watu hawakuwasikiliza Kalebu na Yoshua. Walimkasirikia Musa na Haruni na kusema, "Kwa nini umetuleta sehemu hii hatari? Tulipaswa kubaki Misri badala ya kuuawa vitani na wake zetu na watoto kufanywa watumwa." Watu walitaka kuchagua kiongozi mpya awarudishe Misri.

Frame 14-09

Mara watu waliposikia hivyo, walisikitika kwamba wametenda dhambi. Walichukua silaha zao na kwenda kuwavamia Wakanaani. Musa aliwaonya wasiende kwa sababu Mungu hakuwa pamoja nao, lakini wao hawakumsikiliza.

Frame 14-14

Baada ya Waisraeli kuzunguka jangwani kwa miaka arobaini, wale waliokuwa wamemwasi Mungu walikwishakufa. Kisha Mungu aliwaongoza watu hadi mpakani mwa nchi ya ahadi tena. Musa alikuwa mzee sana, hivyo Mungu alimchagua Yoshua kumsaidia kuongoza watu. Mungu pia alimwahidi Musa siku ile, kwamba atamtuma nabii mwingine kama Musa.

Frame 14-03

Mungu aliwaambia Waisraeli, "Lazima muwaangamize Wakanaani wote kabisa katika Nchi ya Ahadi. Msifanye amani nao wala msioane nao. Lazima muangamize kabisa miungu yao. Iwapo hamnitii mimi, mtaabudu miungu yao!"

Frame 14-11

Kwa kipindi cha miaka arobaini Waisraeli walizunguka jangwani, Mungu aliwapa mahitaji. Aliwapa mkate kutoka mbinguni, ulioitwa, "mana." Pia aliwatumia kware (ambao ni ndege wa umbo la kati) katika kambi zao ili wapate nyama ya kula. Kwa muda wote huo, Mungu alitunza nguo zao na viatu vyao visiharibike.

Frame 14-08

Mungu alikasirika sana na akaja kwenye hema la kukutania. Mungu akasema, "Kwa sababu mmeniasi mimi, watu wote mtazunguka jangwani. Isipokuwa Yoshua na Kalebu, kila mmoja aliye na miaka ishirini au zaidi atafia humo na kamwe hataingia katika nchi ya ahadi.

Frame 14-05

Wale wanaume kumi na wawili walisafiri ndani ya nchi ya Kanaani kwa muda wa siku arobaini na baadaye walirejea. Waliwaambia watu, "Nchi ina rutuba sana na ina mazao kwa wingi." Lakini wapelelezi kumi walisema, " Miji ni imara sana na watu wake ni wenye miraba minne." Kama tutapigana nao, watatushinda na kutuua."

Simulizi ya Biblia Kutoka: Waamuzi 16-17; Hesabu 10-14; 20; 27; Kumbukumbu la Torati 34

15. Nchi ya Ahadi

Frame 15-12

Baada ya vita hii, Mungu akatoa kwa kila kabila sehemu yake katika nchi ya ahadi. Tena Mungu akaipa Israeli amani kwenye mipaka yake yote.

Frame 15-13

Wakati Yoshua alipokua mzee, akawaita watu wote wa Israeli pamoja. Tena Yoshua akawakumbusha watu wajibu wao wa kutii agano ambalo Mungu aliliweka na Waisraeli Sinai. Watu wakamuhaidi kubaki kuwa waaminifu kwa Mungu na kuzifuata sheria zake.

Frame 15-06

Mungu akawamuru waisraeli kutokufanya makubaliano ya amani na makundi yoyote ya watu katika nchi ya Kaanani. Lakini kundi moja la wakaanani, lililoitwa Wagibeoni, walimdanganya Yoshua na wakasema wametoka mbali na nchi ya Kaanani. Wakamuuliza Yoshua kufanya makubaliano ya amani na wao. Yoshua na Waisraeli hawakumuuliza Mungu kuwa ni wapi Wagibeoni wametokea. Yoshua akafanya makubaliano ya amani nao.

Frame 15-10

Mungu pia akasababisha jua kukaa sehemu moja katika anga ili Israeli iwe na muda wa kutosha wa kumaliza na kuwashinda kabisa Waamori. Katika siku hii, Mungu akashinda ushindi mkuu kwa Israeli.

Frame 15-04

Na katika siku ya saba, Waisraeli wakauzunguka mji kwa mara saba zaidi. Wakati walipokua wakiuzunguka mji kwa mara ya mwisho, wanajeshi wakapiga kelele ilihali makuhani walipuliza tarumbeta zao.

Frame 15-02

Waisraeli walipaswa kuvuka mto Yordani walipotaka kwenda kwenye nchi ya ahadi. Mungu akamwambia Yoshua, " Makuhani waanze kwenda kwanza". Wakati makuhani walipoanza kupiga hatua kwenye mto Yordani, mkondo ukasimama kutiririsha maji na Waisraeli wakaweza kuvuka mto kwenye ardhi kavu na kwenda upande wa pili.

Frame 15-01

Hatimaye wana Israeli wanaingia Kaanani, nchi ya ahadi. Yoshua akatuma wapelelezi wawili Yeriko, mji wa wakaanani ambao ulikua ukilindwa kwa kuta zenye nguvu. Ndani ya mji kulikua na Rahabu, kahaba akiishi na ambaye aliwaficha wapelelezi, baadae akawasaidia kutoroka. Aliwaficha sababu alimwamini Mungu. Wapelelezi walihaidi kumlinda Rahabu na familia yake wakati Waisraeli watakapokuja kuangamiza Yeriko.

Frame 15-07

Waisraeli waliingiwa na hasira pale walipogundua wamedanganywa na Wagibeoni, lakini waliamua kutunza makubaliano ya amani nao kwa sababu ilikua ahadi mbele za Mungu. Lakina baadae mfalme mwingine wa kundi lingine la watu katika Kaanani, wa Waamori, aliposikia Wagibeoni wamefanya makubaliano ya amani na Waisraeli, wakaamua kuunganisha majeshi yao kuwa jeshi moja kubwa na kuwavamia Wagibeoni. Wagibeoni wakatuma ujumbe kwa Yoshua wakiomba msaada.

Frame 15-09

Mungu akaipigania Israeli katika siku hiyo. Akasababisha Waamori kuchanganyikiwa na akatuma mvua ya mawe makubwa toka mbinguni ambayo yaliwaua Waamori wengi.

Frame 15-03

Baada ya kuvuka mto Yordani, Mungu akamwambia Yoshua jinsi ya kuuvamia mji wenye nguvu wa Yeriko. Watu wakamtii Mungu. Kama ambavyo Mungu alivyowaambia, kwa wanajeshi na makuhani kuuzunguka mji wa Yeriko mara moja kwa siku sita.

Frame 15-11

Baada ya Mungu kuyashinda majeshi hayo, makundi mengine ya watu wa Wakaanani waliunganika pamoja kuishambulia Israeli. Yoshua na Waisraeli wakawavamia na kuwaangamiza.

Frame 15-08

Kwa hiyo Yoshua akalikusanya jeshi la Waisraeli na wakatembea usiku kucha kufika kwa Wagibeoni. Na asubuhi na mapema wakalishangaza jeshi la Waamori na kuwavamia.

Frame 15-05

Tena kuta za Yeriko zikaanguka chini! Waisraeli waliharibu kila kitu kilichokuepo ndani ya mji kama Mungu alivyoamuru. Walimwacha Rahabupeke yake na familia yake, ambaye alifanyika kua sehemu ya Waisraeli. Na watu wengine waliokua wakiishi katika nchi ya Kaanani waliposikia Waisraeli wameuharibu mji wa Yeriko, waliogopeshwa maana Waisraeli wangewavamia wao pia.

Simulizi ya Biblia kutoka: Yoshua 1-24

16. Wakombozi

Frame 16-15

Watu walitaka kumuweka Gidioni kuwa mfalme wao. Lakini Gidioni hakuwaruhusu kufanya hivyo, lakini akawaomba baadhi ya pete za dhahabu walizochukua kutoka kwa Wamidiani. Watu wakampatia Gidioni kiasi kikubwa cha dhahabu.

Frame 16-17

Tukio hili lilijirudia mara kwa mara: Waisraeli walipotenda dhambi, Mungu aliwaadhibu, walipotubu, na Mungu alituma mkombozi kwao. Yapata miaka mingi, Mungu alikuwa akituma wakombozi wa kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa maadui zao.

Frame 16-12

Baadaye Gidioni akarudi kwa wanajeshi wake na kuwapa pembe, vyungu na kurunzi. Wakazunguka kambi ambayo Wamidiani walikuwa wamelala. Maaskari 300 wa Gidioni walikuwa na kurunzi zilizokuwa zimefichwa ndani ya vyungu ili kwamba Wamidiani wasije wakaona mwanga wa hizo kurunzi.

Frame 16-13

Ndipo, wanajeshi wote wa Gidioni walipovunja vile vyungu kwa pamoja, ghafla pakatokea mwanga wa kurunzi. Wakatoa pembe zao na kupaza sauti, "Upanga kwa Yehova na kwa Gidioni!"

Frame 16-06

Baba yake Gidioni alikuwa na madhabahu aliyoweka wakifu kwa mungu. Mungu akamwambia Gidioni kuvunja madhabahu hiyo. Lakini Gidioni aliogopa watu, hivyo akasubiri hadi ilipofika wakati wa usiku. Kisha akaivunjavunja madhabahu vipande vipande. Akamjengea Mungu madhabahu mpya karibu na ilipokuwa madhabahu ya mungu na kumtolea Mungu sadaka juu yake.

Frame 16-10

Maaskari 32,000 wa Kiisraeli walikwenda kwa Gidioni, lakini Mungu akamwambia kuwa hao ni wengi mno. Ndipo Gidioni akawarudisha 22,000 waliokuwa na hofu ya kupigana. Mungu akamwambia Gidioni kuwa bado ana wanaume wengi sana. Hivyo Gidioni kuwarudisha wote nyumbani isipokuwa maaskari 300.

Frame 16-04

Wamidiani walichukua mazao yote ya Waisrael kwa miaka saba. Waisraeli wakaogopa sana; wakajificha mapangoni ili Wamidiani wasiwapate. Hatimaye, wakamuomba Mungu awaokoe.

Frame 16-02

Kwa sababu Waisraeli waliendelea kutomtii Mungu, aliwaadhibu kwa kuruhusu maadaui zao kuwashinda. Hawa maadui walichukua vitu kutoka kwa Waisraeli, wakaharibu mali zao na kuwaua wengi wao. Baada ya miaka mingi ya kutomtii Mungu na kuteswa na maadui, Waisraeli walitubu na kumuuomba Mungu awaokoe.

Frame 16-01

Baada ya Yoshua kufa, Waisraeli hawakumutii Mungu na hawakuwaondoa Wakanaani wala kuzitii amri za Mungu. Waisraeli walianza kuhabudu miungu ya Wakanaani badala ya Yehova, Mungu wa kweli. Waisraeli hawakuwa na mfalme, kwa hiyo kila mmoja alifanya alichofikiri ni sahihi.

Frame 16-07

Asubuhi yake watu waliona mtu fulani amevunja na kuharibu madhabahu, na wakakasirika sana. Wakaenda nyumbani kwa Gidioni kumua, lakini baba yake Gidioni akasema, "Kwa nini mnajaribu kumsaidia mungu wenu? Kama ni mungu, muacheni ajilinde mwenyewe!" Kwa sababu alisema hayo, watu hawakumuua Gidioni.

Frame 16-09

Kwa ishara ya kwanza, Gidioni alitandika ngozi ya kondoo juu ya ardhi na akamwambia Mungu kuwa umande wote ufikie juu ya hiyo ngozi tu na sio juu ya ardhi. Mungu akafanya kama alivyoomba. Usiku uliofuata, akaomba ardhi ilowane maji lakini ngozi ibaki kuwa kavu. Na Mungu akafanya kama alivyoomba pia. Ishara hizi mbili zilimhamasisha Gidioni kuwa Mungu atamtumia kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Wamidiani.

Frame 16-14

Mungu aliwachanaganya Wamidiani, kiasi kwamba walianza kupigana na kuuwana wao kwa wao. Mara ghafla, Waisraeli wengine waliitwa kutoka kwenye miji yao ili kuja kusaidia kufukuza Wamidiani. Wakawaua wengi wao na kuwafukuza waliobaki kutoka katika nchi ya Waisraeli. Wamidiani 120,000 waliuwawa siku hiyo. Mungu akaiokoa Israeli.

Frame 16-03

Baadaye Mungu alituma mkombozi aliyewaokoa kutoka kwa maadui zao na kuleta amani katika nchi. Lakini baadaye watu walimsahau Mungu na kuunza kuhabudu miungu yao tena. Kwa hiyo Mungu akaruhusu Wamidiani, kundi la watu maadui wakaribu, kuwashinda.

Frame 16-11

Usiku huo ndipo Mungu akamwambia Gidioni, " Shuka chini kwenye kambi ya Wamidiani na utakaposikia wanachoongea, usiogope." Kwa hiyo usiku huo, Gidioni akashuka chini kambini kwa Wamidiani na akasikia askari midiani akimwambia rafiki yake kuhusu ndoto aliyoota. Rafiki yake akamwambia, "Ndoto hii inamaanisha kwamba jeshi la Gidioni litashinda jeshi la Wamidiani!" Gidioni aliposikia hivyo akamwabudu Mungu.

Frame 16-16

Baadaye Gidioni akatumia hizo dhahabu kutengeneza vazi maalumu kama lililokuwa likivaliwa na kuhani mkuu. Lakini watu wakaanza kulihabudi kana kwamba lilikuwa mungu. Kwa hiyo Mungu akaiadhibu Israeli tena kwa sababubu ya kuhabudu miungu. Mungu akaruhusu maadui wawashinde. Hatimaye walimuomba Mungu awasaidie tena, na Mungu aliwatumia mkombozi mwingine.

Frame 16-18

Mwishowe, watu walimuomba Mungu awape mfalme kama mataifa mengine. Walitaka mfalme aliyekuwa mrefu na mwenye nguvu, na atakayeweza kuwaongoza vitani. Mungu hakupendezwa na ombi hilo, lakini akawapatia mfalme sawa na ombi lao.

Frame 16-08

Baadaye Wamidiani walikwenda tena kuiba kwa Waisraeli. Walikuwa wengi sana kiasi cha kutohesabika. Gidioni alikusanya Waisraeli pamoja ili kupigana nao. Gidioni akamuuliza Mungu ishara mbili zitakazompa uhakika kwamba Mungu atamtumia kuokoa Israeli.

Frame 16-05

Siku moja, mtu wa Israeli jina lake Gidioni alikuwa akipura ngano katika sehemu ya siri ili Wamidiani wasije wakaiba. Malaika wa Yehova alimtokea Gidioni na kusema "Usiogope, Mungu yuko pamoja na wewe. Nenda ukawaokoe Waisraeli kutoka kwa Wamidiani."

Simulizi ya Biblia kutoka: Waumuzi 1-3; 6-8

17. Agano la Mungu na Daudi

Frame 17-12

Mume wa Betisheba, aliyeitwa Uria, alikuwa askari hodari miongoni mwa askari wa Daudi. Daudi akamuita Uria arudi nyumabani kwake kutoka vitani na kumwambia aende kuwa na mke wake. Lakini Uria alikataa kurudi nyumbani wakati askari wenzake wakiwa bado vitani. Kwa hiyo Daudi akamtuma tena Uria arudi vitani na akamwambia mkuu wa jeshi kumuweka Uria mahali palipo na mapigano makali ili apate kuuwawa.

Frame 17-13

Baada ya Uria kuuwawa, Daudi akamwoa Betisheba. Baadaye akamzalia Daudi mtoto wa kiume. Mungu alikasirika sana kutokana na kitendo kile alichokifanya Daudi, kwa hiyo Mungu akamtuma nabii Nathani kumwambia Daudi jinsi gani dhambi yake ilikuwa mbaya. Daudi akatubu dhambi yake na Mungu akamsamehe. Katika maisha yake yaliyosalia, Daudi alimfuata na kumtii Mungu, hata katika nyakati ngumu.

Frame 17-06

Daudi alitaka kujenga hekalu ambalo watu wange mwabudu Mungu na kumtolea sadaka. Kwa takribani miaka 400, watu walikuwa wakimwabudu Mungu na kumtolea sadaka katika hema ya kukutania ambayo Musa aliijenga.

Frame 17-10

Siku moja, wakati maaskari wote wa Daudi walipokuwa vitani mbali na nyumbani, Daudi alitazama nje ya nyumba ya kifalme na akaona mwanamke mzuri akioga. jina lake aliitwa Betisheba.

Frame 17-04

Sauli aliona wivu kutokana na upendo wa watu kwa Daudi. Sauli alijaribu kumuua Daudi mara nyingi, kwa hiyo Daudi akajificha mbele ya Sauli. Siku moja, Sauli alikuwa akimtafuta Daudi ili apate kumuua. Sauli akaenda kwenye pango ambalo Daudi alikuwa amejificha lakini hakumuona. Kwa sasa Daudi alikuwa karibu sana na Sauli kiasi kwamba angeweza kumuua lakini hakufanya hivyo. Badala yake, alikata kipande cha nguo ya Sauli kumthibitishia kuwa hakuweza kumuua ili awe mfalme.

Frame 17-02

Mungu alimchagua kijana mwisraeli aliyeitwa Daudi kuwa mfalme baada ya Sauli. Daudi alikuwa mchungaji kutoka mji wa Bethelehemu. Mara kadhaa wakati Daudi akiwa anachunga kondoo wa baba yake, Daudi alikuwa ameua simba na dubu waliokuwa wameshambulia kondoo. Daudi alikuwa mtu mnyenyekevu na mwenyehaki aliye mtumaini na kumtii Mungu.

Frame 17-01

Sauli alikuwa mfalme wa kwanza wa Israel. Alikuwa mrefu na mzuri, kama watu walivyopenda. Sauli alikuwa mfalme mwema kwa miaka michache ya mwanzoni aliyotawala Israel. Lakini, baadaye alikuwa mfalme muovu ambaye hakumtii Mungu, Kwa hiyo Mungu alimchagua mtu mwingine ambaye angekuwa mfalme badala yake.

Frame 17-07

Lakini Mungu alimtuma nabii Nathani aende kwa Daudi na ujumbe huu, "Kwa kuwa wewe ni mtu wa vita, hautajenga hekalu hili kwa ajili yangu. Mtoto wako wa kiume ndiye atakaye lijenga. Lakini, wewe nitakubariki sana. Mmoja kati ya watu wa uzao wako atatawala kama mfalme juu ya watu wangu milele". Mtu pekee wa uzao wa Daudi ambaye angetawala milele alikuwa ni Masihi. Masihi alikuwa ni mteule wa Mungu ambaye angewaokoa watu wa dunia katika dhambi zao.

Frame 17-09

Daudi alitawala kwa haki na uaminifu kwa miaka mingi, na Mungu alimbariki. Hatahivyo, mwishoni mwa maisha yake alitenda dhambi mbaya kinyume na Mungu.

Frame 17-14

Lakini kama adhabu kwa dhambi ya Daudi, mtoto wake wa kiume alifariki. Kukawa pia na mapigano katika familia ya Daudi kwa maisha yake yaliyosalia, na nguvu ya Daudi ilizidi kufifia mno. Ingawa Daudi hakuwa mwaminifu kwa Mungu, Mungu alizidi kuwa mwaminifu katika ahadi zake. Baadaye Daudi na Betisheba walipata mtoto mwingine, na wakamuita Sulemani.

Frame 17-03

Daudi alikuwa askari na kiongozi mwenye nguvu. Wakati Daudi alipo kuwa kijana, alipigana na jitu aliyeitwa Goliati. Goliati alikuwa askari aliyefuzu, na mwenye nguvu, na alikuwa takribani na urefu wa mita tatu! Lakini Mungu alimsaidia Daudi kumuua Goliati na kuwaokoa Israeli. Baada ya hapo, Daudi aliwashinda maadui wengi wa Israeli na hii ndiyo sababu watu walimsifu Daudi.

Frame 17-11

Badala ya kutazama upande, Daudi akatuma mtu kwenda kumleta mwanamke huyu kwake. Akalala naye na baadaye akamrudisha nyumbani kwake. Muda mfupi baadae Betisheba akatuma ujumbe kwa Daudi akisema kwamba alikuwa na mimba.

Frame 17-08

Daudi aliposikia maneno haya, mara alimshukuru na kumtukuza Mungu kwa sababu amemwahidia Daudi heshima na baraka tele. Daudi hakujua ni wakati gani Mungu angefanya mambo haya. Lakini kama ilivyotokea, Waisrael wangekuwa wamesubiri kwa muda mrefu kabla ya Masihi kuja, takribani miaka 1000.

Frame 17-05

Mwishowe, Sauli aliuawa vitani na Daudi akawa mfalme wa Israeli. Alikuwa mfalme mwema na watu walimpenda. Mungu alimbariki Daudi na kumfanya kuwa mwenye mafanikio. Daudi alipigana vita nyingi na Mungu akamsaidia kuwashinda maadui wa Israel. Daudi akauhusuru mji wa Yerusalem na kuufanya makao makuu yake. Katika kipindi cha utawala wake, Israeli likawa taifa lenye nguvu na lenye utajiri.

Simulizi ya Biblia kutoka: 1Samwel 10; 15-19; 24; 31; 2Samuel 5; 7; 11-12

18. Ufalme Uliogawanyika

Frame 18-12

Wafalme wote , na watu wengi waliopo katika ufalme wa Israeli waliabudu sanamu. Baadhi ya vitu walivyoabudu ni pamoja na uzinzi na kutoa kafara ya watoto wao.

Frame 18-13

Wafalme wa Yuda ni wazaliwa wa Daudi, baadhi ya wafalme hao waliongoza kwa haki na kumuabudu Mungu, hata hivyo wengi wa wafalme wa Yuda walikuwa waovu na walarushwa, baadhi yao hutoa watoto wao kama kafara kwa miungu. Pia watu wengi wa ufalme wa Yuda walimuasi Mungu na kuabudu miungu mingine.

Frame 18-06

Mfalme Rehoboamu aliwajibu kwa upumbavu kuwa , msidhani ya kuwa baba yangu aliwapa ninyi kazi nguu , kwani mimi nitawafanya ninyi mfanye kazi ngumu zaidi kuliko alizowapa Baba yangu na kuwapatia ninyi adhabu zaidi kuliko yale ya Baba yangu.

Frame 18-10

Ufalme wa Yuda na Israeli wakawa maadui, na mara nyingi hupigana wao kwa wao

Frame 18-04

Mungu alimkasirikia Solomoni, na kukusudia kumuadhibu kwasababu ya kukosa uaminifu. Hivyo Mungu akaahidi kugawa Taifa la Israeli kuwa falme mbili baada ya kifo chake.

Frame 18-02

Katika mji wa Jerusalemu, Solomoni alijenga Hekalu ambayo Baba yake Daudi alikusudia kuujenga na hivyo kuandaa vifaa vya ujenzi. Watu walianza kumuabudu na kumtolea Mungu sadaka ndani ya Hekalu badala ya kwenye hema ya kukutania. Mungu alishuka na kukaa ndani ya hekalu na kuishi pamoja na watu wake.

Frame 18-01

Baada ya miaka mingi Daudi alifariki, na mwanae aitwaye Solomoni akatawala Israeli badala yake. Mungu alimuuliza Solomoni kitu muhumu amabcho angetaka apewe. Mungu alimpa Solomoni hekima nyingi kuliko watu wote kama alivyoomba. Naye alijifunza mambo mengi na kutawala kwa haki. Pia Mungu alimpa Solomoni utajiri mwingi.

Frame 18-07

Makabila kumi ya Taifa la Israeli yalimuasi mfalme Rehoboamu , na makabila mawili yaliendelea kuwa waaminifu kwake. Hayo makabila mawili yaliunda ufalme wa Yuda.

Frame 18-09

Jeroboamu alimuasi Mungu a kuwafanya watu kutenda dhambi. Alitengeneza sanamu mbili na kuwafanya watu kuiabudu badala ya kumuabudu Mungu wa kweli anayeabuduiwa katika Hekalu lililoko Yuda.

Frame 18-03

Lakini Solomoni aliwapenda wanawake wa mataifa mengine .Hakumtii Mungu kwa kuwaoa wanawake wengi. Aliwaoa karibu wake 1000. Hao wanawake waliolewa na Solomoni kutoka mataifa mengine walileta na kuaendelea kuabudu miungu yao . Hata Solomoni alipokuwa mzee, naye akaabudu hizo miungu.

Frame 18-11

Katika Ufalme mpya wa Israeli wafalme wote walikuwa waovu, na wafalme wengi waliuwawa na waisraeli waliotaka kuwa wafalme badala yao

Frame 18-08

Makabila yale kumi ya Israeli yaliyo muasi Rehoboamu, waliungana na kumchagua mtu aitwaye Jeroboamu kuwa mfalme wao. Wao walikaa kazikazini mwa nchi ya Israeli. Makabila hayo kumi yaliunda ufalme wa Israeli.

Frame 18-05

Baada ya Solomoni kufa, Rehoboamu mwanaye , akawa Mfalme. Rehoboamu alikuwa mfalme mpumbavu , watu wote wa Israeli walimridhia yeye kuwa mfalme wao. Watu walimjia na kumlalamikia kuwa Baba yake Solomoni aliwatesa kwa kazi ngumu na kuwatoza gharama kubwa ya kodi.

Simulizi ya Biblia kutoka: 1Wafalme 1-6; 11-12

19. Manabii

Frame 19-15

na mara ya kwanza Naaman alionekana kukasirika na kuona kama ni ujinga, badae alibadili mawazo yake na kuoga mara saba, na alipokwisha mailiza mara ya saba ngozi yake ilitakasika na ukoma ukaisha na Mungu akamponya.

Frame 19-17

watu wakaacha kumtii Mungu, wakawatesa na wakati mwingine wakawauwa manabii. mfano Jeremia aliekuwa nabii wa Mungu alichukuliwa na kuwekwa kwenye kisima kikavu na akadumbukizwa kwenye matope na kuachwa huko akafe. Ndipo Mfalme akamuhurumia Jeremia na kutuma watumishi wake wakamwokoe kabla hajafa.

Frame 19-12

Elia akaamuru manabii wote wa Baal wakamatwe na asitoweke hata mmoja. Watu wote wakawakamata manabii wa Baal na kuwapeleka mbali na kuwauwa.

Frame 19-13

Elia akamwambia Ahabu "rudi mjini maana kuna mvua kubwa inakuja" Ndipo anga likawa jeusi na mvua kubwaikaanza kunyesha. Hivyo ikajulikana kuwa Yawee ndie Mungu wa kweli na ukame ukaisha.

Frame 19-06

Ndipo taifa la Israel na manabii wa Baal 450 wote wakaja katika mlima wa kamel. Elia akasema" ni mpka lini akili zenu zitabadilika? kama Yawee ni Mungu na mumtumikie na kama Baal ni Mungu mumtumikie".

Frame 19-10

hivyo Elia akaomba akisema " Yawee Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, na ujioneshe leo kuwa wewe ni Mungu wa Isarael.Nijibu na watu wako wajue wewe ni Mungu wa kweli.

Frame 19-04

Ndipo nabii Elia akaenda katika nchi ya karibu huko akamkuta mwanamke mjane aliyekuwa na mtoto wake wa kiume hawakuwa na chakula kwa sababu ya ukosefu wa mvua na njaa kali, yule mama mjane akampokea Elia na kumkarimu, na yule mama mjane Mungu alimbariki yeye pamoja na mwanae hata kipindi chote cha njaa kali, hivyo mifuko ya unga na chupa zake za mafuta havikumuishia. Na Elia kaishii huko mda mrefu.

Frame 19-02

Na Elia alikuwa nabii katika taifa la Israel chini ya ufalme wa Mfalme Ahabu. Mfalme Ahabu ali asi na kuwalazimisha watu waabudu mungu wake asiye wa ukweli aitwaye Baal. Ndipo nabii Elia akamwambia Ahabu "hapatakuwa na mvua wala ukungu katika Israel mpka nitakaposema" na Mfalme Ahabu aligadhabika saana.

Frame 19-01

Katika historia ya wana wa Israel ,Mungu aliwatumia manabii wake. manabii walisikia ujumbe kutoka kwa Mungu na kuwambia watu wa Mungu neno lake.

Frame 19-07

Ndipo Elia akawambia manabii wa Baal wauwe ng'ombe kwa ajili ya sadaka, na musiwashe moto, na nitafanya vivyohivyo. Na Mungu atakaeachilia moto ndiye atakuwa Mungu wa kweri. na makuhani wa Baal wakaandaa sadaka lakini moto haukuwaka.

Frame 19-09

Ndipo Elia akaandaa sadaka kwa Mungu na akawaambia watu wote "mwageni maji, mapipa kumi na mbili, na juu ya sadaka wekeni nyama, kuni na madhabahu yote ikajaa maji na kulowana.

Frame 19-14

Baada ya Elia, Mungu akainua nabii mwingine aitwae Elisha, na Mungu akatenda miujiza kupitia Elisha pamoja na kuponya ukoma wa Naamani aliekuwa kamanda wa vita. Baada ya Naaman kumsikia nabii Elisha, akamwendea na kumuomba amponye ukoma wake. ndipo Elisha akamwambia Naaman nenda katika mto Jordani ni huko uoge mara saba.

Frame 19-03

Ndipo Mungu akamwambia Elia, " nenda katika jangwa na huko ukajifiche mbali na uso wa Mfalme Ahabu maana anataka kukuuwa, na alipokuwa huko ndege walimpelekea Mkate na nyama kwa ajili ya chakula asubuhi na jioni. Hata alipokuwa huko majeshi ya Ahabu yalimtafuta na yasimpate. Hivyo ukame ukazidi na mifereji kukauka

Frame 19-11

Na ndipo moto ukashuka toka juu na kuteketeza nyama, kuni miamba, uchafu na maji yote kwenye madhabahu. na watu wote walipokwisha kuona hivyo wakaanguka chini na kusema Yawee ni Mungu Yawee ni Mungu".

Frame 19-16

Mungu akatuma manabii wengi kuwafundisha watu wawe na huruma na ukarimu wao kwa wao, manabii wakawaonya watu wasiabudu sanamu manabii wakawaonya watu waache mabaya na kummuheshimu Mungu wa kweri. Manabii wakawambia watu wasipotii Mungu atawahukumu atawaadhibu.

Frame 19-18

Hivyo manabii wakaendelea kuwwambia watu habari njema japo watu waliwachukia,wakiwaonya kuwa Mungu atawaadhibu wasipotubu maana mwokozi atakuja.

Frame 19-08

Na hata manabii wa Baal wakaomba kwa mungu wao " tusikie Baal" wakapiga kelele kutwaa wakiomba na kujikata kwa visu lakini mungu wao asiwajibu.

Frame 19-05

Baada ya miaka mitatu na nusu, Mungu akasema na Elia" Nenda ukaonane na Mfalme Ahabu maana nitaleta mvua " na ndipo Mfalme Ahabu alipomuona Elia akasema " ewe mkorofi" Elia akajibu " wewe ndiye mkorofi, umemwacha Yawee, Mungu wa kweli na kumwabudu Baal,walete watu wote wa taifa la Israel katika mlima wa kamel"

Simulizi ya Biblia kutoka: Wafalme ya kwanza16-18; Wafalme ya pili 5; Yeremia 38

20. Kuchukuliwa Mateka na Kurudi

Frame 20-12

Ufalme wa Uajemi ulikua na nguvu lakini ulikua na huruma kwa watu waliowateka. Baada ya Koreshi kua Mfalme wa Uajemi alitoa amri kuwa Myahudi yeyote anaetaka kurudi Yuda anaweza kuondoka uajemi na kurudi Yuda. Aliwapa pesa kwa ajili ya kujenga upya hekalu. Baada ya miaka sabini ya kuwa mateka wayahudi wachache walirudi Yuda katika mji wa Yerusalemu.

Frame 20-13

Waliporudi Yerusalemu walijenga upya hekalu pamoja na ukuta wa mji. Japokua walikua wakitawaliwa na watu wengine lakini walipata nafasi ya kuishi kwenye nchi ya ahadi na kumwabudu Mungu hekaluni.

Frame 20-06

Takribani miaka 100 baada ya Waashuru kuharibu ufalme wa Israeli Mungu alimtuma Nebukadneza mfalme wa Babiloni kuvamia taifa la Yuda. Babiloni lilikua taifa ;enye nguvu. Mfalme wa Yuda akakubali kuwa mtumishi wa Nebukadneza na kulipwa pesa nyingi kila mwaka.

Frame 20-10

Japokua Mungu aliwaadhibu watu wake kwa dhambi zao kwa kuwafanya mateka lakini hakuwasahau watu wake na ahadi aliyowaahidi. Mungu aliendelea kuwaangalia na kuzungumza nao kupitia manabii. Aliwaahidi kua baada ya miaka sabini atawarudisha kwenye nchi ya ahadi.

Frame 20-04

Waashuru waliwaleta wageni ili waishi katika nchi ya Israel. Wageni hao walijenga miji iliyoharibiwa na kuoa waisrael waliobaki. Kizazi cha wana wa Israel waliooana wa wageni kiliitwa Wasamaria.

Frame 20-02

Ndipo Mungu aliadhibu falme zote kwa kuruhusu maadui zao kuwapiga. Ufame wa Ashuru ulikua ni ufalme wenye nguvu, taifa korofi likaharibu ufalme wa Israel. katika ufalme wa Israel Waashuru waliwaua watu wengi sana na kuwanyang'anya kila kitu cha thamani kisha kuchoma moto sehemu kubwa ya ardhi yao.

Frame 20-01

Ufalme wa Israel na ufalme wa Yuda walitenda dhambi mbele za Mungu. walivunja agano waliloweka na Mungu Sinai. Mungu aliwatuma Manabii wake kuwaonya ili watubu na kumuabudu yeye lakini walikataa.

Frame 20-07

Miaka michace baadae Mfalme wa Yuda akasi juu ya Babiloni. Ndipo wababiloni wakarudi na kuuteka ufalme wa Yuda. Waliuvamia mji wa Yerusalem wakaharibu hekalu na kuchukua vitu vyote vya thamani vilivyokuwemo katika mji.

Frame 20-09

Mfalme Nebukadneza pamoja na jeshi lake waliwapeleka watu wengi wa Yuda Babiloni, wakawaacha masikini ili wafanye kazi katika mashamba. Kipindi ambacho watu wa Mungu walilazimishwa kuondoka nchi ya ahadi kiliitwa kipindi cha Mateka.

Frame 20-03

Waashuru waliwakusanya viongozi wote, matajiri na watu wenye ujuzi kisha kuwapeleka Ashuru. Masikini ambao hawakuuawa ndio waliobaki Israeli.

Frame 20-11

Miaka sabini baadae mfalme wa Uajemi alimshinda Babiloni hivyo ufalme wa Uajemi ukachukua nafasi ya ufalme wa Babiloni. Waisrael wakaanza kuitwa wayahudi na wengi wao waliishi Babiloni. Wachache waliokua wazee waliikumbuka nchi ya Yuda.

Frame 20-08

Kwa sababu ya uasi Askari wa Mfalme Nebukadneza waliwaua watoto wote wa mfalme wa Yuda mbele ya macho yake kisha wakamharibu macho yake. Baada ya hayo wakamchukua mfalme na kumpeleka gerezani Babiloni ili afie huko.

Frame 20-05

Watu wa ufame wa Yuda waliona jinsi ambavyo Mungu alivyowaadhibu watu wa Israel kwa kutokumtii na kumwamini Mungu. lakini waliendelea kuiabudu miungu na akiwemo Mungu wa wakaanani. Mungu alituma manabii kuwaonya lakini hawakusikia.

Simulizi ya Biblia kutoka: 2Wafalme 17; 24-25; 2Mambo ya nyakati 36; Ezra 1-10; Nehemia 1-13

21. Mungu Anaahidi Ujio wa Masihi

Frame 21-15

Mungu aliwaonyesha mambo mengi kwa manabii kuhusu mwokozi, bali masihi hakuja kwa wakati wa manabii wengine na ni zaidi ya miaka, 400 baada ya nabii wa mwisho kupitta na wakati timilifu Mungu alimtuma masihi Duniani.

Frame 21-12

Manabii walisema ni jinsi gani mwokozi atakufa, Isaya alitabili yakwamba watu wata mtemea mate, kumdhihaki na kumpiga masihi, kumsulubisha watamchoma mkuki nae atakufa na maumivu makali ijapokuwa hakutenda lolote baya.

Frame 21-13

Manabii walisema yakwamba masihi alikuwa mkamilifu na hakuwa na dhambi, alikufa ili azichukue dhambi za watu, mateso yake yataleta amani kati ya Mungu na wanadamu kwa maana hiyo ndipo Mungu akamsuribisha masihi.

Frame 21-06

Manabii wa Mungu wanasema masihi nae atakuwa nabii, Kuhani na Mfalme. Maana nabii ni mtu anaesikia neno la Mungu na kulitangaza kwa watu nae aliyeahidiwa kutumwa na Mungu atakuwa ni nabii wa kweli.

Frame 21-10

Nabii Isaya alisemamasihi ataishi Galilaya, atawafariji waliopondeka moyo na kutangaza uhuru kwa waliofungwa, pia walitabili masihi ataponya wagonjwa, viziwi, vipofu na mabubu.

Frame 21-04

Mungu alimuahidi Mfalme Daudi yakwamba mmoja kati ya mzaliwa wa vizazi vyake atainuliwa nakuwa Mfalme wa watu wa Mungu milele, hii inamaanisha kwamba masihi atakuwa miongoni kizazi kutoka kwa Daudi.

Frame 21-02

Mungu alimuahidi Ibrahim kuwa kupitia yeye watu wote Duniani watabarikiwa, ahadi hii itatimia pale mwokozi atakapokuja, na watu katika makundi wa ulimwengu wataokoka kupitia ujio wa masihi.

Frame 21-01

Tangu mwanzo Mungu alipanga kumtuma masihi na ahadi ya kwanza ilikuwa kwa Adamu na Eva, Mungu akaahidi uzao kutoka kwa Eva kuwa atamponda Nyoka kichwa, Kwa maana aliyemdanganya Eva alikuwa Nyoka nae ni Shetani, ahadi hii inamaanisha mwokozi atakuja kumshinda Shetani.

Frame 21-07

Makuhani wa iziraeli walimtolea Mungu dhabihu kwa niaba ya watu kwa hukumu ya dhambi zao pia humuomba Mungu kwaajili ya watu, Mwokozi ni kuhani aliyejitoa kuwa dhabihu kamilifu kwa Mungu.

Frame 21-09

Manabii wa Mungu walitabili mengi kuhusu masihi, nabii Malaki alitabili ujio wa nabii mkubwa kabla wa Masihi kuja, nae nabii Isaya alitabili mwokozi kuzaliwa na bikila, nabii Maiko alisema masihi atazaliwa katika mji wa Betelehemu.

Frame 21-14

Manabii walinena yakwamba masihi atakufa na Mungu atamuinua kutoka kwa wafu, kutokana na kifo na kufufuka kwa masihi, Mungu amekamilisha mpango wake wa kuokoa na dhambi na kuanza agano jipya.

Frame 21-03

Mungu alimuahidi Musa yakwamba baada ya yeye kumaliza atamuinua Nabii mwingine kama yeye, na hii ni ahadi nyingine juu ya ujio wa Masihi kwa siku zijazo.

Frame 21-11

Nabii Isaya alitabili juu ya kujchukiwa masihi atachukiwa bila sababu na kukataliwa, manabii wengine walinena yakwamba watakao kumuua masihi watagawa nguo zake na msaliti atakuwa mtu wa kalibu yake, nae nabii Zakaria akanena yakwamba sarafu therasini za fedha zitatumika kumlipa awezekumsaliti masihi.

Frame 21-08

Mfalme ni mtu anaetawala falme na kutoa hukumu kwa watu, mwokozi atakuwa Mfalme mkamilifu na kuweza kumiliki nafasi ya Daudi ili atawale na kutoa hukumu ya haki.

Frame 21-05

KUpitia Nabii Nehemia Mungu aliahidi kuweka maagano mapya, lakini hayatafanana na maagano aliyoweka kwa Wayahudi kwa iziraeli, kwenye maagano mapya Mungu ataandika sheria zake ndani ya miyoyo ya watu ili waweze kumjua kumjua Mungu nao watakuwa watu wake, na Mungu kuwasamehe dhambi zao, masihi kuanza maagano mapya.

Simuliza ya Biblia Kutoka: Mwanzo 3:15; 12:1-3; Kumbukumbu la Torati 18:15; 2Samweli 7; Yeremia 31; Isaya 59:16; Danieli 7; Malaki 4:5; Isaya 7:14; Mika 5:2; Isaya 9:1-7; 35:3-5; 61; 53; Zaburi 22:18; 35:19; 69:4; 41:9; Zakaria 11:12-13; Isaya 50:6; Zaburi 16:10-11

22. Kuzaliwa kwa Yohana

Frame 22-06

Baada ya malaika kuongea na Maria, Maria akaenda kumtembelea Elizabeti. Baada ya Elizabeti kusikia salaamu ya Maria mtoto aliekuwepo tumboni kwake aliruka. Na wote wawili walishangilia kwa furaha mambo mazuri waliotendewa. Baada ya Maria kumtembelea Elizabeti kwa miezi mitatu. Maria alirudi nyumbani kwake.

Frame 22-04

Elizabeti alipokuwa na mimba ya miezi sita, malaika yule yule alimtokea ndugu yake Elizabeti aliyeitwa Maria.Alikuwa ni bikira na alikuwa amechumbiwa aolewe na kijana aitwae Yusufu. Malaika akamwambia "Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume. Utamuita jina lake Yesu. Atakuwa ni mtoto wa Mungu aliye juu na atatawala milele."

Frame 22-02

Malaika akamwambia Zakaria "tazama mke wako atapata mtoto wa kiume, nawe utamuita jina lake Yohana. Nae atajazwa Roho Mtakatifu na atawaandaa watu kwaajili ya Kristo!". Zakaria akamjibu "Mimi na mke wangu tu wazee sana kuweza kupata watoto. Nitajuaje kama haya yatatokea?"

Frame 22-01

Hapo zamani Mungu alikua akiongea na watu wake kwa kupitia Malaika na Manabii. Ilipita miaka 400 Mungu alikua hajazungumza na watu wake. Ghafla Malaika alikuja na ujumbe kutoka kwa Mungu kwenda kwa kuhani mzee aitwae Zakaria. Zakaria na mke wake Elizabeti walikua ni watu wa Mungu lakini Elizabeti alikuwa hajapata mtoto yeyote.

Frame 22-07

Baada ya Elizabeti kujifungua mtoto wake wa kiume, Zakaria na Elizabeti walimuita huyo mtoto Yohana, kama malaika alivyoamuru. Kisha Mungu alifungua kinywa cha Zakaria na akaweza kusema tena. Zakaria alisema "Asifiwe Mungu kwa kuwa amewakumbuka watu wake! Nawe mwanangu utaitwa nabii wa Mungu aliye juu utakae waambia watu jinsi ya kupokea msamaha wa dhambi zao.

Frame 22-03

Malaika akamjibu Zakaria akasema " tazama nilitumwa na Mungu kukuletea habari hizi njema. Kwakua umeshindwa kuniamini hutaweza kuongea mpaka pale mtoto atakapozaliwa" Hapohapo Zakaria hakuweza kuongea. Ndipo malaika alimuacha Zakaria. Baada ya hapo Zakaria alirudi nyumbani na mke wake akapata mimba.

Frame 22-05

Maria akajibu "Inawezekanaje jambo hili kutokea ingali mimi ni bikira?" Malaika akamwambia "Roho wa Bwana atakuja kwako na nguvu za Mungu zitakuwa juu yako na kukufunika kama kivuli. Kwa sababu hiyo mtoto atakuwa mtakatifu, mwana wa Mungu". Maria akaamini na kukubali alichoambiwa na malaika.

Simulizi ya Biblia kutoka: Luka 1

23. Kuzaliwa kwa Yesu

Frame 23-06

Usiku ule ule walikuwepo wachungaji wa maeneo jirani wakilinda mifugo yao. Ghafla waliona malaika akin'gaa mbele yao wakatekewa; Malaika akasema, "msiwe na wasiwasi ninazo habari nzuri. Kristo Bwana amezaliwa Bethlehem!"

Frame 23-10

Na wataalamu hawa walipomuona Yesu na mama yake, wakainama na kumwabudu. Ndipo walimpa Yesu zawadi za gharama kubwa. Wakarudi kwao mashariki.

Frame 23-04

wakati Mariamu alipokaribia kuzaa, ni kipindi kile utawala wa Rumi ulielekeza kila mtu ahesabiwe katika jamii anayotokea. Hapa inabidi sasa Yusufu na Mariamu wasafiri safari ndefu waelekee Bethlehemu tokea Nazareti kwa sababu ndiyo mji wao kwa asali yaani mji wa Daudi.

Frame 23-02

Ndipo Malaika akamtahadharisha Yusufu kwamba asimwache Mariamu kwasababu mimba hiyo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu hivyo asiwe na wasiwasi. Mtoto atakayezaliwa ni wa kiume ataitwa jina lake Yesu (yaani Yehova huokoa), kwa kuwa atawaokoa watu waondoke dhambini.

Frame 23-01

Mariamu alikuwa amechumbiwa na mtu mwadilifu aitwaye Yusufu. Yusufu kwasababu ya uhaki hakutaka Mariamu apate aibu kwaajili ya ujauzito ambao haukumhusu hivyo akaanza kutafuta njia akwepe kwa siri. Malaika akamtokea Yusufu katika ndoto.

Frame 23-07

Akaongeza; "nendeni kwa mtoto, mtamuona amefungwa nguo akiwa amelazwa kwenye lishio la mifugo." Mawinguni walionekana Malaika, wakitukuza na kuimba Utukufu uko mbinguni kwa Mungu na amani duniani kwa wapendwa."

Frame 23-09

Badaye wenye ujuzi tokea mashariki ya mbali wakiongozwa na nyota walifika Bethlehemu na hapo wakatambua ile nyota ilimaanisha Mfalme wa Wayahudi. Hivyo wakasafiri safari ndefu na wakaipata nyumba alimokuwa Yesu akiwa pamoja na wazazi wake.

Frame 23-03

Yusufu aliamua kumchukua Mariamu kuwa mkewe; lakini, hawakukaribiana mpaka pale Mariamu atakapomzaa mwana.

Frame 23-08

Wachungaji walifika mahali pale alipokuwa Yesu kama maelekezo ya malaika yalivyokuwa wakiwa wamejawa furaha. Baada ya hapo wakarudi ilipokuwa mifugo yao; wakimtukuza Mungu kwa yale waliyosikia na kuyaona.

Frame 23-05

Baada ya kufika Bethlehemu hapakuwa na mahali ya kujihifadhi. Nafasi waliyopata ni pale mifugo ilihifadhiwa, ndipo mtoto alipozaliwa na mama yake alimlaza kwenye lishio la ng'ombe kwa kuwa hakuna kitanda; jina lake aliitwa Yesu.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 1; Luka 2

24. Yohana Anambatiza Yesu

Frame 24-06

Siku iliyofuata Yesu alikuja ili abatizwe na Yohana .Wakati alipomwona Yohana alisema,'angalia huyu ni mwanakondoo wa Mungu atakayechukua dhambi ya ulimwengu.

Frame 24-04

Yohana akawaambia viongozi wa dini" enyi nyoka wenye sumu! tubuni na kubadilisha tabia zenu.Kila mti usiozaa matunda mema hukatwa na kutupwa motoni. Yohana alitimiza kile kilichosemwa na manabii "angalia namtuma mjumbe wangu mbele yenu ambaye atawandalia njia zenu."

Frame 24-02

Watu wengi walimfuata Yohana nyikani kumsikiliza.Aliwahubiri akisema,"tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia"

Frame 24-01

Yohana mwana wa Zakaria na Elizabeth alikuwa na akawa nabii .Aliishi nyikani akila asali ya porini, nzige ,na kuvaa nguo zilizotengenezwa na manyoya ya ngamia.

Frame 24-07

Yohana akamwambia Yesu mimi sistahili kukubatiza wewe ila wewe unastahili kunibatiza mimi.Lakini Yesu akasema "ni lazima kunibatiza mimi kwa sababu ni kitu sahihi kwa hiyo Yohana akambatizaYesu pamoja na kwamba Yesu hakuwahi kutenda dhambi.

Frame 24-09

Mungu akamwambia Yohana," Roho wa Mungu atakuja juu ya mtu ambaye umembatiza .Na mtu huyo ni mwana wa Mungu ,"Kuna Mungu mmoja tu.Lakini wakati Yohana alipokuwa akimbatiza Yesu alisikia Baba Mungu akisema na akamuona Mungu mwana ,ambaye ni Yesu ,na akamwona Roho Mtakatifu.

Frame 24-03

Wakati watu waliposikia ujumbe wa Yohana wengi walitubu dhambi zao na kubatizwa .Viongozi wengi wa dini walikuja kubatizwa na Yohana lakini hawakutubu wala kuungama dhambi zao .

Frame 24-08

Wakati Yesu alipotoka majini baada ya kubatizwa Roho wa Mungu alitokea katika umbo la njiwa alishuka akatulia juu yake.Wakati huo sauti ya Mungu ikaongea kutoka mbinguni na kusema "Wewe ni mwanangu ambaye ninakupenda na ninayependezwa naye ".

Frame 24-05

Baadhi ya Wayahudi wakamwuuliza Yohana kama yeye ni Kristo ,Yohana akajibu mimi siyo Kristo lakini kuna mmoja ajaye baada yangu ambaye ni mkuu sanakwani sistahili kufungua kamba ya viatu vyake .

Simulizi ya Biblia kutoka: Matayo 3; Marko1:9-11; Luka 3:1-23

25. Shetani Anamjaribu Yesu

Frame 25-06

Kisha Shetani alimwonyesha Yesu falme zote za ulimwengu na fahari zake zote na akasema; "Nitakupa hivi vyote iwapo utanisujudia na kuniabudu mimi".

Frame 25-04

Kisha Shetani alimchukua Yesu mpaka juu ya mnara wa hekalu na kumwambia; "Kama wewe ni Mwana wa Mungu jirushe mwenyewe chini, kwa vile imeandikwa, Mungu atakuagizia malaika wake wakuchukue ili usijigonge mguu wako katika jiwe".

Frame 25-02

Shetani alimjaribu Yesu akisema; "Kama wewe ni mwana wa Mungu yaamuru mawe haya yawe mikate upate kula".

Frame 25-01

Mara tu Yesu alipokwisha kubatizwa, Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu nyikani, huko alifunga siku arobaini mchana na usiku. kisha Shetani alifika kumjaribu Yesu ili atende dhambi.

Frame 25-07

Yesu akajibu; ondoka kwangu Shetani! Katika neno la Mungu ameagiza, "Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia Yeye peke yake".

Frame 25-03

Yesu akajibu; "Imeandikwa katika neno la Mungu, watu hawahitaji mkate pekee ili wapate kuishi, bali wanahitaji kila neno linalosemwa na Mungu".

Frame 25-08

Yesu hakujitia chini ya majaribu ya Shetani, hivyo Shetani aliondoka akamwacha. kisha malaika walikuja na kumhudumia Yesu.

Frame 25-05

Lakini Yesu alimjibu Shetani kwa kunukuu Maandiko akisema; " Katika neno la Mungu, anaagiza watu wake, usimjaribu Bwana Mungu wako".

Simulizi ya Biblia Kutoka: Mathayo 4:1-11; Marko 1:12-13; Luka 4:1-13

26. Yesu Anaanza Huduma yake.

Frame 26-06

Yesu akaendelea kusema "Kipindi cha nabii Elisha kulikuwa na watu wengi katika Israeli wenye magonjwa ya Ngozi. lakini Elisha hakumponya hata mmoja wao. lakini aliponya ugonjwa wa ngozi wa Naamani pekee aliyekuwa kamanda wa maadui wa Israel. watu waliokuwa wanamsikiliza Yesu walikuwa ni wayahudi. Kwa hiyo walipomsikia anasema hayo wakawa na hasira juu yake.

Frame 26-10

Tena Yesu akachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume. Mitume walizunguka na Yesu tena walijifunza kutoka kwake.

Frame 26-04

Tena Yesu akaa chini "Kila mmoja akamsogelea na kumtazama. walijua aya aliyoisoma inamhusu masia. Yesu akasema "Maneno niliyosoma mbele yenu yanatokea sasa. watu wote wakashangaa. huyu si mwana wa Yusufu"? Walisema.

Frame 26-02

Yesu akaenda mji wa Nazareti alikokuwa akiishi wakati wa utoto wake. Siku ya sabato, alienda sehemu ya kuabudia. wakamkabidhi chuo cha nabii isaya ili aweze kusoma. Yesu akakifungua chuo na kusoma sehemu yake mbele za watu.

Frame 26-01

Baada ya kushinda majaribu ya Ibilisi Yesu alirudi kwa nguvu za Roho mtakatifu katika mkoa wa Galilaya. Yesu alienda sehemu moja baada ya nyigine akifundisha. Kila mmoja alisema vyema juu yake.

Frame 26-07

Watu wa Nazareti wakamvuta Yesu mbali na mahali pa kuabudia na kumtupa nje ili wamwue. Lakini Yesu akaondoka Mbele yao na akauacha mji wa Nazaleti.

Frame 26-09

Watu wengi waliokuwa na mapepo ndani yao waliletwa kwa Yesu. Kwa amri ya Yesu aliwaamuru wawatoke watu hao, na waliendelea kupiga kelele "Wewe ni mwana wa Mungu!" Umati wa watu walishangaa na walimwabudu Mungu.

Frame 26-03

Yesu kasema "Bwana amenipa Roho wake ili kwamba nitangaze habari njema kwa maskini, uhuru kwa wafungwa, vipofu kuona, kutolewa waliodhurumiwa. huu ni mwaka wa Bwana uliokubalika.

Frame 26-08

Tena Yesu alienda mpaka mkoa wa Galilaya na mkutano mkubwa wakaja kwake. wakawealeta watu wengi waliokuwa wagonjwa, au walemavu, kama wasioona, kutembea, kusikia au kuongea, na Yesu akawaponya.

Frame 26-05

Tena Yesu akasema "Ni kweli kwamba hakuna nabii anayekubalika katika mji wa kwao. Wakati wa nabii Eliya, kulikuwa na wajane katika Israeli. lakini mvua iliposimama bila kunyesha kwa miaka mitatu na nusu, Mungu hakumtuma Eliya kumsaidia mwanamke mjane kutoka Israel, badala yake alikuwa ni mjane kutoka taifa tofauti"

Simulizi ya Biblia kutoka: Matahayo 4:12-25; Marko 1:14-15; 35-39; 3:13-21; Luka 4:14-30, 38-44

27. Simulizi ya Msamaria Mwema

Frame 27-06

"Muda mfupi baada ya tukio hilo Kuhani wa Kiyahudi alikuwa akisafiri na kupitia katika barabara hii ambayo Myahudi yule alikuwa amepigwa na kuachwa pale. Alipomuona alipita upande mwingine wa barabara mbali na alipokuwepo mtu huyo na kuendelea na safari yake wala asimjali na kumsaidia mtu yule."

Frame 27-10

"Siku iliyofuata Msamaria huyu alihitaji kuendelea na safari yake na hivyo alimkabidhi yule muangalizi wa nyumba ya wageni na kumwambia " Mhudumie Myahudi huyu aliyepigwa na wezi. Akampa fedha yule muangalizi na kumwambia, kama utatumia fedha zaidi katika kumhudumia Myahudi huyu basi nikirudi kutoka safari yangu nitakuja nilipe kiasi kilichoongezeka."

Frame 27-04

Yesu alimjibu huyu Mwalimu wa mambo ya sheria ya Kiyahudi kwa kumpa simulizi. " Kulikuwa na Myahudi mmoja aliyekuwa anasafiri kwa barabara kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko.

Frame 27-02

Mwalimu wa mambo ya sheria ya Kiyahudi alimjibu Yesu na kusema, sheria ya Mungu inasema "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na pia inasema "Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Yesu akamwambia "uko sahihi. Fanya hivyo na utaurithi uzima wa milele."

Frame 27-01

Siku moja Mwalimu wa mambo ya sheria ya Kiyahudi alimwendea Yesu na kumuuliza kwa kumjaribu akisema,"Mwalimu nifanyeje ili ni urithi uzima wa milele?" Yesu akamjibu " sheria ya Mungu imeandikwaje?"

Frame 27-07

"Baada ya muda mfupi Mlawi (Walawi walikuwa kabila la Wayahudi ambao lilikuwa linawasadia makuhani katika huduma hekaluni) naye alipita barabara hiyohiyo na alipomuona mtu yule aliyekuwa amepigwa na kuumizwa na wezi alipita upande mwingine wa barabara na kuendelea na safari yake bila kumjali."

Frame 27-09

"Msamaria baada ya hapo alimchukua huyo Myahudi na kumpandisha kwenye Punda wake na kumpeleka kwenye nyumba ya wageni iliyokuwa karibu na barabara na kumuhudumia zaidi."

Frame 27-03

Lakini huyu Mwalimu wa mambo ya sheria ya Kiyahudi akitaka kujionyesha kwamba yeye ni mwenye haki, alimuuliza Yesu; "Jirani yangu ni nani?"

Frame 27-11

Baada ya hadithi hiyo, Yesu alimuuliza yule Mwalimu wa mambo ya sheria ya Kiyahudi, kwamba "Unafikiri katika watu hao watatu, ni nani aliyekuwa jirani yake yule Myahudi aliyepigwa na wezi?" Yule Mwalimu wa mambo ya sheria ya Kiyahudi alijibu na kumwambia Yesu "ni yule aliyemuonea huruma". Yesu akamwambia "Wewe nawe nenda kafanye vivyo hivyo."

Frame 27-08

"Mtu mwingine aliyepita barabara hiyo alikuwa ni Msamaria (Wasamaria walikuwa wa uzao wa Wayahudi na ni watu waliooa na kuolewa na watu wa mataifa mengine. Wasamaria walikuwa wanachukiana sana na Wayahudi). Huyo Msamaria alipomuona Myahudi yule aliyekuwa amepigwa na kuumizwa sana na wezi, alimuonea sana huruma. Alimchukua na kuyahudumia majeraha yake na kumfunga pandeji."

Frame 27-05

"Wakati Myahudi huyu alipokuwa akisafiri kikundi cha wezi kilimvamia na kumwibia kila kitu na kumpiga sana karibu ya kufa. Walipokuwa wamempiga sana karibu ya kufa, walimwacha hapo barabarani na kuondoka zao."

Simulizi ya Biblia kutoka: Luka 10:25-37

28. Kijana Tajiri Kiongozi

Frame 28-06

Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Ni vigumu sana kwa watu matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu! Ndiyo, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu

Frame 28-10

Yesu akajibu, "Kila mmoja aliyeacha nyumba, kaka, dada yake, baba, mama, watoto, au mali kwa ajili yangu atapokea mara 100 zaidi na pia atapokea uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wengi walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."

Frame 28-04

Yesu akajibu, kama unataka kuwa mkamilifu, nenda ukauze kila kitu ulichonacho na utoe pesa kwa maskini, na utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.

Frame 28-02

"Ni mambo gani nahitaji kutii?" Aliuliza. Yesu akajibu, "usiuwe. Usizini. Usiibe. Usidanganye. Mheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.

Frame 28-01

Siku moja, kiongozi kijana tajiri alimwendea Yesu na kumuuliza, "mwalimu mwema nifanye kitu gani cha lazima ili niwe na uzima wa milele?" Yesu akamwambia, "kwanini unaniita mwema?" Kuna mmoja tu aliye mwema naye ni Mungu. Lakini ukitaka kuwa na uzima wa milele, tii sheria za Mungu.

Frame 28-07

Wanafunzi waliposikia alichosema Yesu, walishikwa na mshangao na kusema, "Ni nani basi anaweza kuokolewa?"

Frame 28-09

Petro akamwambia Yesu, "Tumeacha kila kitu na kukufuata wewe. Je, tutapata thawabu gani?"

Frame 28-03

Lakini kijana akasema, "Nimezitii sheria hizo zote tangu nikiwa kijana. Je, nahitaji kufanya nini bado ili niishi milele? Yesu alimwangalia na akampenda.

Frame 28-08

Yesu akawatazama wanafunzi na kusema, "Kwa watu mambo haya hayawezekani, lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana".

Frame 28-05

Yule kijana aliposikia alichokisema Yesu, alihuzunika sana, kwa sababu alikuwa tajiri sana na hakutaka kutoa vitu vyote alivyomiliki. Akageuka na akaenda mbali na Yesu.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 19:16-30; Marko 10:17-31; Luka 18:18-30

29. Simulizi ya Mtumishi Asiye na Huruma.

Frame 29-06

"Yule mtumishi mwenzake alianguka na kupiga magoti na kumwambia, 'Tafadhali nivumilie, nitakulipa kiasi chote unachonidai.' Ila, yule mtumishi alimtupa mtumishi mwenzake ndani ya gereza hadi atakapo lipa deni lake."

Frame 29-04

"Yule mtumishi alianguka na kupiga magoti mbele ya mfalme na kusema, ' naomba nivumilie, na nitalipa deni loote unalonidai.' Mfalme alimuonea huruma yule mtumishi, ndipo akafuta deni lake lote na kumuacha aende zake."

Frame 29-02

Yesu akasema, " Ufalme wa Mungu unafananishwa na mfalme alie taka kukusanya madeni yake kutoka kwa watumishi wake. Mmoja wa watumishi wake alikua anadaiwa deni kubwa lenye thamani ya mshahara wa miaka 200,000."

Frame 29-01

Siku moja, Petro alimuuliza Yesu "Bwana, ni mara ngapi inanipasa kumsamehe ndugu yangu akinikosea? Hadi mara saba?" Yesu akasema, "Sio mara saba, bali sabini mara saba!" Kwa hili, Yesu alimaanisha inatupasa kusamehe kila wakati. Yesu akawaambia habari hii.

Frame 29-07

"Baadhi ya watumishi wengine walioona kilicho tokea walifadhaika sana. Wakaenda kwa mfalme na kumuambia kila kitu."

Frame 29-09

Ndipo Yesu akasema " Hivi ndivyo baba yangu wa mbinguni atakavyo fanya kwa kila mmoja wenu kama hamtawasamehe ndugu zenu kutoka moyoni".

Frame 29-03

"Kwakua yule mtuishi hakuweza kulipa deni, mfalme alisema, 'muuzeni huyu mtu na familia yake kama watumwa ili kulipa deni lake."

Frame 29-08

"Mfalme alimwita yule mtumishi nakumuambia, 'Ewe mtumishi muovu! Nilikusamehe deni lako kwasababu ulinisihi. Ungefanya vivyo hivyo.' Mfalme alikasirika sana na kumtupa yule mtumishi muovu gerezani mpaka atakapo lipa deni lake lote."

Frame 29-05

"Ila baada ya mtumishi kutoka kwa mfalme, alimpata mtumishi mwenzake aliekua akimdai deni lenye thamani ya mshahara wa miezi minne. Alimkamata yule mtumishi mwenzake na kusema, ' Nilipe hela ninayo kudai!"'

Simulizi ya Biblia kutoka: Matayo18:21-35

30. Yesu Anawalisha Watu Elfu Tano

Frame 30-06

Yesu akawaambia wanafunzi wa waambie watu kwenye umati wakae chini kwenye nyasi kwa makundi ya watu 50

Frame 30-04

na ilipokuwa jion wanafunzi walimwambia Yesu, tumechelewa na hakuna mji karibu, basi uwaage watu ili waweza kwenda kujitafutia kitu wale.

Frame 30-02

Lakini walikuwako watu wengi waliomuona Yesu na wanafunzi wakaondoka kwenye mashua, Watu walipita pembezoni mwa ziwa kuelekea upande wa pili mbele yao, hivyo Yesu na wanafunzi wake walipowasili, tayari kundi kubwa la watu walikuwako huko wakiwasubili.

Frame 30-01

Yesu aliwatuma mitume kuwahubiri na kuwafundisha watu vijiji tofauti, nao waliporudi kwa Yesu, waka mueleza kile walicho fanya, Yesu akawaalika kwenda faragha ng'ambo ya mto kwa mapunziko, nao wakapanda mashua kuelekea ng'ambo ya mto.

Frame 30-07

Na Yesu akachukua vile vipande vitano vya mikate na samaki wawili, akatazama mbinguni akamshukuru Mungu kwa Chakula.

Frame 30-09

Baada ya hapo wanafunzi walikusanya mabaki ya chakula, navyo vilikuwa vikapu kumi na mbili, nacho chakula chote kilitokana na Mikate mitano na Samaki wawili.

Frame 30-03

Umati ulikuwa zaidi ya wanaume 5000 bila kuhesabu wanawake na watoto, Yesu aliona mkutano mkubwa mbele yake nao walikuwa kama kondoo waliokosa mchungaji, kwa hiyo akawafundisha na kuwaponya watu miongoni mwao ambavyo walikuwa wagonjwa.

Frame 30-08

Kisha Yesu akaigawa mikate na samaki vipande, akawapatia vile vipande wanafunzi wawagawie watu. Wanafunzi wakaendelea kupita nje na chakura, wala hakikuisha, watu wote wakala na kutosheka.

Frame 30-05

Yesu akawaambia wanafunzi, "mnaweza kuwapatia chochote wale!" wakamjibu ni vipi tunaweza kufanya hivyo? sisi tuna vipande vitano vya mkate na samaki wawili

Simulizi ya Biblia kutoka: Matayo14:13-21; Marko 6:31-44; Luka 9:10-17; Yohana 6:5-15

31. Yesu Atembea Juu ya Maji

Frame 31-06

Hivyo, Petro akatoka kwenye mtumbwi na kuanza kutembea kwenda kwa Yesu juu ya uso wa maji. Lakini baada ya kwenda mwendo mfupi, aliyaondoa macho yake kwa Yesu na kuanza kutazama mawimbi na kuhisi nguvu ya upepo.

Frame 31-04

Wanafunzi walijawa na hofu kuu walipomwona Yesu, sababu walidhani walikuwa wakiona roho. Yesu hali akijua kuwa wanafunzi wake wameogopa, alipaza sauti kwao kusema, "Msiogope. Ni mimi!

Frame 31-02

Wakati huo huo, wanafunzi walikuwa wakipiga kasia kwa mtumbi wao, lakini wakati wa usiku wa manane walikuwa pekee yao katikati ya ziwa. Walikuwa wakipiga kasia kwa shida kwa sababu upepo ulikuwa ukivuma kinyume chao.

Frame 31-01

Kisha Yesu aliwaambia wanafunzi wapande kwenye mtumbwi na wasafiri hadi ng'ambo ya ziwa wakati alipokuwa akiyaaga makutano. Baada ya Yesu kuyaaga makutano kwenda zao, alipanda mlimani ili aombe huko. Yesu alibaki huko pekee yake, na aliomba mpaka usiku wa manane.

Frame 31-07

Kisha Petro akashikwa na woga na kuanza kuzama ndami ya maji. Akapaza sauti kwake, "Bwana, niokoe!" Yesu alimwendea na kumnyakua. Kisha akamwambia Petro, "Wewe mwenye imani haba, kwa nini umeona shaka?"

Frame 31-03

Kisha Yesu alimaliza kuomba na akaenda kwa wanafunzi. Alitembea juu ya maji akivuka ziwa mbele ya mtumbwi wao!

Frame 31-08

Wakati Yesu na Petro walipopanda ndani ya mtumbwi, mara upepo ulikoma kuvuma na maji yakatulia. Wanafunzi wakashangaa. Wakamwabudu Yesu wakisema, "Hakika, wewe ni Mwana wa Mungu".

Frame 31-05

Kisha Petro akamwambia Yesu, "Bwana, kama ni wewe niruhusu nije kwako juu ya maji". Yesu akamwambia Petro "Njoo!"

Simulizi ya Biblia Kutoka: Mathayo 14:22-33; Marko 6:45-52; Yohana 6:16-21.

32. Yesu Amponya Mwanamume Aliyepagawa - pepo na Mwanamke Mgojwa

Frame 32-15

na ndipo Yesu akagundua yakuwa nguvu zimemuishia, hivyo akageuka nyuma na kuuliza " je ni nani aliye nigusa", wanafunzi wakamjibu " kuna kundi kubwa la watu limekuzunguka na wakikugusa je ni kwa nini umeuliza "ni nani aliyenigusa"

Frame 32-12

ndipo mtu yule akaondoka na kumweleza kila mtu yale yote Yesu aliyomtendea. Na kila mtu aliye sikia simulizi hizi alishangaa na kusitaajabishwa.

Frame 32-13

ndipo Yesu akarudi upande mwingine wa ziwa, na lipofika lilikuwako kundi kubwa la watu waliokusanyika wakimzunguka. na hapo alikuwapo mwanamke aliegua na kutokwa damu miaka kumi na miwili. Alilipa pesa yake yote kwa waganga ili wamponye lakini hali ilizidi kuwa ngumu.

Frame 32-06

mtu huyo mwenye pepo akalia kwa sauti " unataka nini kwangu Yesu, mwana wa Mungu aliyetukuzwa juu? tafadhali usinitese" ndipo Yesu akaliuliza lile pepo " je unaitwa nani"? akajibu " jina langu ni legioni" na kwa sababu tupo wengi ( " legioni" kikundi cha wanajeshi maelfu katika vikosi vya rumi).

Frame 32-10

watu waliogopa na wakamuomba Yesu aondoke, ndipo Yesu akapanda ndani ya mashua na akijiandaa kwa ajili ya kuondoka. na mtu yule aliekuwa na mapepo akamusihi Yesu aondoke pamoja naye.

Frame 32-04

Mtu huyo aliishi maeneo ya makaburi na mtu huyu alitetemeka mchana na usiku kwa sababu hakuvaa nguo zozote na mwili wake alijikata kwa mawe.

Frame 32-02

Na walipofika upande wa pili wa ziwa, na alikuwako mtu mwenye mapepo alimkimbilia Yesu.

Frame 32-01

Siku moja Yesu na wanafunzi wake walipanda mashua kuelekea mjini, ambako waliishi watu wa Gerasini.

Frame 32-07

Yale mapepo yakamwomba Yesu " tafadhali usituondoe katika mji huu", na hapo palikuwa na kundi la nguruwe karibu na kilima, yale mapepo yakamwomba Yesu " tuamuru twende kwenye nguruwe hao" na Yesu akajibu "nendeni".

Frame 32-09

Na watu wale waliokuwa wakiwaangalia wale nguruwe walipoona hayo yakitokea, walikimbia na kuelekea mjini na huko wakamwambia kila mmoja yakuwa wamemkuta Yesu na aliyokuwa akitenda. Na watu wa mjini wakaenda na kumwona yule mtu aliekuwa na mapepo. Alikuwa amekaa kwa utulivu,amevaa nguo na alikuwa anaonekana kama mtu wa kawaida.

Frame 32-14

Alisikia ya kuwa Yesu aliponya watu wengi na akafikiri" hakika kama nitagusa vazi la Yesu na mimi nitapona pia". hivyo akaja karibu na Yesu akamgusa vazi lake. na baada ya kumgusa tu, alipona na hakutokwa damu kwake kukaisha.

Frame 32-03

Mtu huyu alikuwa mwenye nguvu na hapukuwa na mtu yeyote wa kumdhibiti. watu walimfunga kamba mikonom na miguuni mwake lakini bado aliweza kuzikata.

Frame 32-11

Yesu akajibu " hapana, ondoka uende nyumbani na uwaeleze marafiki na familia yako kuhusu yote alivyokutendea Mungu na alivyokufanyia huruma yake kwako.

Frame 32-16

kisha yule mwanamke akaanguka magotini pa Yesu akitetemeka na kuogopa, akamwambia yale yote aliyo yatenda na alivyopokea uponyaji. Yesu akamwambia " enenda kwa amani, imani yako imekuponya.

Frame 32-08

yale mapepo yakamtoka yule mtu na kuwaingia wale nguruwe, Na wale nguruwe wakakimbilia huko chini bondeni kwenye ziwa........ na palikuwako na nguruwe 2000 kundini.

Frame 32-05

Mtu huyo alipokuja kwa Yesu, alianguka mbele ya magoti yake. Na Yesu akaliaamuru lile pepo "limtoke mtu huyo".

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 8:28-34; 9:20-22; Marko 5:1-20; 5;24b-34; Luka 8:26-39; 8:42b-48.

33. Simulizi ya Mkulima

Frame 33-06

Hadithi iliwachanganya watu. Naye Yesu akawafafanulia akasema, "mbegu ni neno la Mungu. Mbegu zilizoanguka kwenye njia, ni yule mtu anaye lisikia neno la Mungu, lakini halielewi. Shetani huja na kulichukua neno kwa mtu huyo."

Frame 33-04

"Mbegu zingine zilianguka kwenye miiba, nazo zikamea lakini zikasongwa na miiba. Kwa hiyo mbengu hizo hazikuweza kuzaa matunda."

Frame 33-02

Yesu aliwasimulia hadithi," Mpanzi alikwenda kupanda mbegu shambani, alipokuwa akimwaga mbegu kwa kutumia mikono yake. Mbegu zingine ziliangukia kwenye njia, ndege wakazila zote."

Frame 33-01

Siku moja, Yesu alikuwa akifundisha makutano wengi katika pwani ya ziwa. Na watu wengi walimfuata wapate kumsikiliza. Yesu aliingia ndani ya mashua mahali pa juu apate nafasi nzuri ya kuzungumza nao. Yesu alikaa kwenye mashua akawafundisha watu.

Frame 33-07

"ile ardhi ya udongo wa mawe, ni yule mtu anayelisikia neno na kulipokea kwa furaha. Lakini yajapotokea mateso na majaribu, hushindwa kustahimili na huanguka dhambini."

Frame 33-09

"ule udongo mzuri ni yule mtu anaye lisikia neno la Mungu na kuliaminii hivyo huzaa matunda.

Frame 33-03

"Mbegu zingine zilianguka kwenye ardhi yenye mawe, nazo zikachipuka haraka. Lakini jua lilipowaka zote zika ungua, kwa sababu mizizi haikuweza kustawi vizuri katika ule udongo mchache, hivyo miche ile ikafa."

Frame 33-08

"Ardhi yenye miiba, ni yule mtu anayelisikia neno la Mungu, lakini kwa kadri siku zinavyoendelea, utajiri, anasa za maisha humtenga na upendo wa Mungu. Matokeo yake, lile neno la Mungu alilolisikia halizai matunda."

Frame 33-05

"Mbegu zingine ziliangukia penye udongo mzuri. Mbengu hizo ziliweza kustawi na kuzaa 30, 60 na 100 zaidi kadri ya wingi wake katika kupandwa. Aliye na masikio, na asikie."

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 13:1-8, 18-23; Marko 4:1-8, 13-20; Luka 8:4-15

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine

Frame 34-06

Tena Yesu akawaambia simulizi ya baadhi ya watu ambao wameweka tumaini katika matendo yao mema na kudharau watu wengine .Akasema. "Watu wawili walikwenda hekaluni kusali .Mmoja alikuwa mtoza ushuru na mwingine kiongozi wa dini."

Frame 34-10

"Kisha Yesu akasema, "Lakini nawaambieni ukweli, Mungu alisikia maombi ya mtoza ushuru na kumtangaza kuwa mwenye haki. Lakini hakuyapenda maombi ya kiongozi wa dini. Mungu humshusha kila ajikwezae na humpandisha kila ajinyenyekezaye,"

Frame 34-04

"Ufalme wa Mungu pia unafanana kama hazina ambayo mtu ameificha shambani.Mtu mwingine akaikuta hazina hiyo na kuifukia tena. Alijawa na furaha kiasi kwamba akaenda kuuza kila kitu alichonacho na akatumia fedha hiyo kununua shamba hilo."

Frame 34-02

"Lakini wakati punje ya haradali inapokuwa, inakuwa kubwa kuliko mimea yote bustanini, inakuwa na ukubwa wa kutosha hata ndege huja na kutua kwenye matawi yake,"

Frame 34-01

Yesu aliwaambia masilimuzi mengi kuhusu ufalme wa Mungu .Kwa mfano,alisema,"Ufalme wa Mungu ni kama punje ya haradali ambayo mtu aliipanda shambani mwake.Unajua kwamba punje ya haradali ni ndogo kuliko punje zote."

Frame 34-07

"Kiongozi wa dini aliomba hivi. 'Asante, Mungu kwamba mimi siyo mwenye dhambi kama watu wengine - mfano wanyanganyi, wasio haki, wazinzi, au hata kama huyu mtoza ushuru'".

Frame 34-09

"Lakini mtoza ushuru alisimama mbali na kiongozi wa dini hata hakuelekeza uso wake mbinguni. Badala yake alijipiga ngumi kifua chake na akaomba, "Mungu, tafadhali unirehemu mimi kwa sababu ni mwenye dhambi."

Frame 34-03

Yesu akawaambia simulizi nyingine ,"Ufalme wa Mungu ni kama amira aliyoichanganya mwanamke kwenye baadhi ya donge la mkate na mpaka kusambaa kwenye donge lote."

Frame 34-08

"Kwa mfano, nafunga mara mbili kwa wiki na kukutolea moja ya kumi ya pesa zote na mali zote nizipatazo."

Frame 34-05

"Ufalme wa Mungu pia ni kama lulu kamili ya thamani kubwa .Mfanyabiashara wa lulu alipoipata, aliuza vitu vyote alivyokuwanavyo na kutumia fedha hiyo kununua hiyo lulu.

Simuliziya Biblia kutoka: Mathayo 13:31-33; 44-46; Marko 4:30-32,; Luka 13:18-21; 18:9-14

35. Habari za Baba mwenye Huruma

Frame 35-12

"Kijana mkubwa akamuambia Baba yake, mimi nimefanya kazi kwa uaminifu miaka yote , nimekutii kwa wakati wote, na hujawahi hata kunipa mbuzi mdogo wa kumchinja ili kusheherekea na rafiki zangu, ila alipokuja huyo kijana wako aliyetapanya na kutumia mali zako vibaya ulimchinjia ndama aliyenona."

Frame 35-13

Baba yake akamjibu kuwa, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni cha kwako. Imetupasa kusherehekea kwa kuwa, Mdogo wako alikuwa amekufa na sasa yu hai, alikuwa amepotea na sasa amepatikana.

Frame 35-06

Mwishowe, yule kijana mdogo akajiambia moyoni, ninafanya nini hapa? Watumishi nyumbani mwa Baba yangu wanakula vizuri wakati mimi nakufa na njaa hapa. Nitakwenda na kumuomba Baba anifanye mmoja wa watumishi wake.

Frame 35-10

Watu wakaanza kusherehekea, na kabla mda mwingi haujapita, kaka yake mkubwa akarudi toka shambani. Alipofika nyumbani alisikia sauti ya muziki na watu wakicheza , akashangaa juu ya kilichokuwa kinaendelea.

Frame 35-04

Baada ya muda mfupi, yule kijana mdogo alikusanya uridhi wake wote , kisha akaenda nchi ya mbali na kuanza kutapanya fedha zake kwa njia ya anasa.

Frame 35-02

Viongozi wa dini waliokuwepo pale walimshutumu Yesu, kwa vile walimuona akiongea na wale wenye dhambi kama rafiki zake. Yesu akawaambia hadidhi hii.

Frame 35-01

Siku moja, Yesu alikuwa akiwafundisha watoza ushuru wengi na watu wenye dhambi waliokusanyika kumsikiliza.

Frame 35-07

Hivyo, kijana mdogo akaanza safari ya kurudi nyumbani, akiwa bado mbali na nyumbani, Baba yake alimuona na kumuonea huruma kisha akamkimbilia na kumkumbatia na kumbusu mtoto wake.

Frame 35-09

Lakini Baba yake akamwambia mmoja wa Watumishi wake, harakisha kachukue nguo nzuri na kumvisha mwanangu, mvisheni pete kwenye kidole chake, mvalisheni viatu miguuni mwake. Kisha mchinjeni ndama aliyenona ili tule na kusheherekea, kwasababu mwanangua alikuwa amekufa na sasa yu hai, alikuwa amepotea na sasa kapatikana.

Frame 35-03

"Kulikuwa na mtu mwenye watoto wawili wa kiume, Mdogo alimuambia Baba yake, Baba nipe sehemu ya uridhi wangu! Baba yake akagawa mali zake kwa watoto wake wawilii.

Frame 35-11

Baada ya kutambua kuwa watu wanasheherekea kwasababu ya kurudi kwa mdogo wake, alikasirika sana na kukataa kuingia nyumbani. Baba yake alikuja kumbembeleza na kumsihi aingie nyumbani ili washerehekee pamoja lakini alikataa.

Frame 35-08

Kijana mdogo akasema, "Baba, nimemtenda Mungu dhambi na wewe pia, sistahili kuitwa mwanao tena."

Frame 35-05

Baada ya muda, njaa kali ikatokea katika nchi alikokwenda huyo kijana mdogo, akawa hana fedha ya kununulia chakula. Akatafuta kazi aliyoweza kufanya ambayo ni kulisha nguruwe. Hali yake ya maisha ikawa mbaya kiasi kwamba alitamani kula chakula kile cha nguruwe.

Simulizi ya Biblia kutoka: Luka 15:11-32

37. Kubadilika Sura

Frame 36-06

Ndipo Yesu akawagusa na kuwaambia "Msiogope inukeni". walipotazama pembeni ni Yesu pekee ndiye aliyebaki pale.

Frame 36-04

Wakati Musa na Eliya wanaongea na Yesu, Petro akamwambia Yesu, "Ni vizuri sisi kuwa hapa, hivyo naomba tutengeneze nyumba tatu moja ya kwako, nyingine ya Eliya na nyingine ya Musa". Lakini Petro hakujua alinenalo.

Frame 36-02

Yesu akiwa anaomba uso wake ulibadilika na kung'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga, yalikua meupe sana zaidi awezavyo mtu duniani kuyafanya yang'ae.

Frame 36-01

Siku moja, Yesu aliwachukua wanafunzi wake watatu Yakobo, Petro na Yohana. ( Mwanafunzi aitwae Yohana sio yule aliyembatiza Yesu.) Walipanda juu ya mlima mrefu kuomba pekeyao.

Frame 36-07

Yesu pamoja na wanafunzi wake watatu wakashuka kutoka mlimani. Yesu akawaambia "Msimwambie mtu yeyote yale yaliyotokea, siku chache baadae nitakufa kisha nitakua hai tena. Baada ya hapo mtawaambia watu."

Frame 36-03

Ndipo Musa na nabii Eliya wakawatokea. Watu hawa waliishi duniani miaka mingi kabla. Waliongea na Yesu juu ya kifo chake ambacho kitatokea Yerusalemu siku chache baadae.

Frame 36-05

Wakati Petro anaongea wingu jeupe lilishuka na kuwazunguka na sauti ikatoka katika lile wingu ikisema " Huyu ni Mwanagu nimpendaye. Ninayependezwa naye msikilizeni yeye".Wale wanafunzi watatu waliogopa na kuanguka chini.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 17: 1-9; Marko 9:2-8; Luka 9:28-36

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu

Frame 37-06

Maria alipofika. Alianguka miguuni pa Yesu akasema, "Bwana, kama wewe tu ungekuwepo kaka yangu asingekufa." Yesu akawauliza, "Mmemuweka wapi Lazaro?" Walimjibu " Kaburini, njoo uone." Yesu alilia.

Frame 37-10

Ndipo Lazaro alitoka nje! Alikuwa bado amefungwa sanda, Yesu akawaambia, "Msaidieni kuondoa sanda na mwacheni huru!." Wayahudi wengi walimwamini Yesu kwa sababu ya muujiza huu.

Frame 37-04

Yesu alipofika katika mji wa Lazaro, Lazaro alikuwa tayari amekufa kwa siku nne. Martha alikwenda kumwona Yesu akasema, "Bwana, kama ungekuwa hapa, kaka yangu asingekufa . Lakini ninaamini kuwa Mungu atakupa chochote umwombacho."

Frame 37-02

Baada ya siku mbili, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, ''Twendeni tena Uyahudi." "Lakini mwalimu. " Wanafunzi wake walisema, "Muda mfupi tu uliopita watu walitaka kukuua!" Yesu alisema "Rafiki yetu Lazaro amelala usingizi na ni lazima nimwamshe."

Frame 37-01

Siku moja, Yesu alipata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa sana. Lazaro na dada zake wawili- Martha na Maria walikuwa marafiki wa karibu wa Yesu. Yesu alipopata habari hizi alisema, "Huu si ugonjwa wa kifo, bali ni ugonjwa wa kumtukuza Mungu." Yesu aliwapenda marafiki zake, lakini alisubiri hadi siku mbili.

Frame 37-07

Kaburi lilikuwa pango limefunikwa na jiwe. Yesu alipofika kaburini aliwaambia, "Liondoeni jiwe." Lakini Martha alisema, "Amekuwa kaburini sasa siku nne, ananuka!"

Frame 37-09

Basi Yesu alitazama juu mbinguni akasema, "Baba, asante kwa kuwa unanisikia. Tena najua wewe hunisikia siku zote. Lakini nimesema haya kwa ajili ya watu hawa waliosimama hapa, kwa kuwa wataamini kuwa ulinituma." Kisha Yesu akapaza sauti, "Lazaro, njoo nje."

Frame 37-03

Wanafunzi wa Yesu walijibu, "Bwana, kama Lazaro amelala, basi atapata nafuu." Yesu aliwaambia wazi, "Lazaro amekufa, nafurahi kuwa sikuwepo ili mpate kuniamini."

Frame 37-11

Lakini viongozi wa dini ya kiyahudi waliona wivu, ndipo wakakusanyika pamoja kupanga watakavyoweza kumuua Yesu na Lazaro.

Frame 37-08

Yesu alijibu, "Je, sikusema kuwa kama ukiniamini utaona utukufu wa Mungu?" Ndipo wakaliondoa jiwe.

Frame 37-05

Yesu akajibu akasema, "Mimi ni Ufufuo na Uzima, yeyote aniaminiye ataishi, hata kama akifa. Kila aniaminiye hatakufa. Unaamini hivyo?" Martha akajibu, "Ndiyo Bwana ninaamini kuwa wewe ni Masihi, Mwanawa Mungu."

Simulizi ya Biblia kutoka: Yohana 11:1-46

38. Yesu Anasalitiwa

Frame 38-15

Wakati askari walipomkamata Yesu, Petro akatoa upanga wake na kumkata sikio mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu. Yesu akasema, "Weka upanga mbali! Ninaweza kumwambia Mungu Baba alete jeshi la malaika kunitetea. Lakini lazima nimtii Baba yangu." Kisha Yesu akamponya mtu aliyekatwa sikio.Baada ya Yesu kukamatwa, wanafunzi wote wakakimbia.

Frame 38-12

Yesu aliomba mara tatu, "Baba yangu, kama inawezekana, tafadhali nisinywe kikombe hiki cha mateso. Lakini kama hakuna njia nyingine ya kuwasamehe watu dhambi zao, basi mapenzi yako yatimizwe." Yesu alihuzunika na jasho lake likawa kama matone ya damu. Mungu akatuma malaika akamtia nguvu.

Frame 38-13

Kila mara anapomaliza kuomba, Yesu aliwarudia wanafunzi wake, lakini walikuwa wamelala. alipowarudia mara ya tatu, Yesu akasema, ''Amkeni! msaliti wangu amefika.''

Frame 38-06

Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, ''Mmoja wenu atanisaliti." Wanafunzi walishituka, na wakauliza nani atafanya jambo kama hili. Yesu akasema, '"Nitakayempa kipande cha mkate huu ndiye msaliti.'' Kisha akampa Yuda mkate.

Frame 38-10

Kisha Petro akamwambia Yesu, "Hata kama itanilazimu kufa, sitakukana.'' Wanafunzi wengine nao wakasema vile vile.

Frame 38-04

Huko Yerusalem, Yesu alisherehekea Pasaka pamoja na wanafunzi wake. Wakati wa chakula cha Pasaka, Yesu alichukua mkate na kuuvunja. Na kusema ''Chukueni na kuleni. Huu ni mwili wangu, uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi." Kwa jinsi hii, Yesu alimaanisha kuwa mwili wake utatolewa sadaka kwa ajili yao.

Frame 38-02

Mmoja wa wanafunzi wa Yesu aliitwa Yuda. Yuda alikuwa mtunza mfuko wa fedha wa mitume, lakini alikuwa mpenda fedha na mara nyingi aliiba fedha kutoka mfuko huo. Baada ya Yesu na wanafunzi wake kufika Yerusalemu, Yuda alikwenda kwa viongozi wa Kiyahudi na kumsaliti kwa kupewa fedha. Alijua kwamba viongozi wa Kiyahudi walikataa kwamba Yesu ni Masihi na walikuwa wanapanga kumuua.

Frame 38-01

Kila mwaka wayahudi walisherehekea sikukuu ya Pasaka. Hii ilikuwa sherehe ya kukumbuka jinsi Mungu alivyowatoa mababu zao toka utumwani Misri karne nyingi zilizopita. Yapata miaka mitatu baada ya Yesu kuanza kuhubiri na kufundisha hadharani, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa alitaka kusherehekea Pasaka huko Yerusalem pamoja nao, na kwamba angeuawa huko.

Frame 38-07

Baada ya Yuda kupokea mkate, akaingiwa na Shetani. Yuda akaondoka na kwenda kuwasaidia viongozi wa Kiyahudi kumkamata Yesu. Wakati huo ilikuwa usiku.

Frame 38-09

Petro akajibu, ''Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha!" Kisha Yesu akamwambia Petro, "Shetani anawataka ninyi nyote, lakini nimekuombea, Petro, ya kwamba imani yako haitaisha. Hata hivyo usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu kana kwamba hukunijua.''

Frame 38-14

Yuda akaja pamoja na viongozi wa Kiyahudi, askari,na umati mkubwa. Wakiwa na mapanga na marungu. Yuda akamjia Yesu akamwambia, ''Salaam, mwalimu,'' na kumbusu. Hii ilikuwa ishara kwa viongozi wa Kiyahudi ili wajue watakayemkamata. Kisha Yesu akasema, ''Yuda , unanisaliti kwa kunibusu?"

Frame 38-03

Viongozi wa Wayahudi, wakiongozwa na Kuhani mkuu, wakamlipa Yuda vipande thelathini vya fedha ili amsaliti Yesu. Hii ilitokea kama manabii walivyotabiri. Yuda akakubali, akachukua fedha, na kuondoka. Akaanza kutafuta nafasi ya kuwasaidia kumkamata Yesu.

Frame 38-11

Kisha Yesu akaenda na wanafunzi wake sehemu inayoitwa Gethsemane. Yesu aliwaambia wanafunzi wake ombeni ili msiingie majaribuni. Kisha Yesu akaenda kuomba peke yake.

Frame 38-08

Baada ya chakula, Yesu na wanafunzi wake wakaenda mlima wa Mizeituni. Yesu akasema, "Wote mtaniacha usiku huu. Imeandikwa, 'Nitamshambulia mchungaji na kondoo wote watatawanyika.'''

Frame 38-05

Kisha Yesu akachukua kikombe na kusema, "Kunyweni. Hii ni damu ya Agano Jipya iliyotolewa kwa ondoleo la dhambi. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi kila mnapokunywa.''

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 26:14-56; Marko 14:10-50; Luka 22:1-53; Yohana 12:6; 18:1-11

39. Yesu Anashitakiwa.

Frame 39-12

Pilato akaogopa kwamba makutano wataanza kuleta Ghasia, kwa hiyo aliwaruhusu askari wake kumsulubisha Yesu. Askari wa Kirumi wakampiga Yesu huku wakimpa vazi la kifalme na kofia iliyotengenezwa na miiba wakamvika. pia wakamdhihaki kwa kusema "Mtazame mfalme wa wayahudi"

Frame 39-06

Na Petro alikuwa inje ya nyumba akisubiri. Mtumishi mmoja msichana akamwona na akamwambia "Na wewe pia ulikuwa na Yesu!" Petro akakana. baadaye binti mwingine akasema kitu hichohicho. Na petro akakataa tena. hatimaye watu wakasema "Tunajua wewe ulikuwa pamoja naye maana ninyi nyote ni wenyeji wa Galilaya.

Frame 39-10

Yesu akamjibu "Wewe ndiye umesema hivyo, lakini ufalme wangu si ufalme wa dunia hii, kama ingekuwa hivyo watumishi wangu wangepigana kwa ajili yangu. Nimekuja ulimwenuni ili kuusema ukweli kuhusu Mungu. na kila mmoja anayependa huu ukweli hunisikiliza. Pilato akasema "Ukweli ni nini?"

Frame 39-04

Yesu akamjibu, "Mimi ndiye, utaniona nimekaa na Mungu na pia nikishuka kutoka mbinguni" Kuhani mkuu akararua mavazi yake kwa hasira na akasema kwa sauti kuu kwa viongozi wa kidini wengine "Hatuhitaji mashahidi zaidi ya hawa! Mmesikia toka kwake mwenyewe, akisema yeye ni mwana wa Mungu. Hukumu yenu ni ipi?"

Frame 39-02

Ndani ya Nyumba viongozi wa kiyahudi wakamshitaki Yesu. Wakaleta mashahidi wengi wa uongo walioshuhudia uongo dhidi ya Yake. vile vile hata maelezo yao yalitofautiana kila mmoja alisema tofauti. kwa hiyo viongozi wa kiyahudi hawakukubaliana kama alikuwa na hatia yeyote. Yesu hakusema chochote.

Frame 39-01

Ilikuwa usiku wa manane wakati huo. Askari wakampeleka kwenye nyumba ya kuhani mkuu ili kumhoji. Petro akawafuata kwa mbali nyuma yao. Wakati Yesu anachukuliwa kwenye nyumba, Petro alikuwa nje peke yake akiota moto.

Frame 39-07

tena Petro akaapa, akisema, "Mungu wangu na anilaani kama mimi namjua mtu huyu!" Mara ghafla Jogoo akawika na Yesu akageuka kumwangalia Petro.

Frame 39-09

Asubuhi na mapema, viongozi wa kiyahudi wakamleta Yesu kwa Pilato liwali wa Kirumi. wakitumaini kuwa Pilato atamhukumu Yesu kama mtu mwenye hatia na wakamwambia auawe. Pilato akamuuliza Yesu "Wewe ni mfalme wa wayahudi?"

Frame 39-03

Hatimaye kuhani mkuu akamwangalia Yesu na kusema "Tuambie wewe ni Masihi mwana wa Mungu aliye hai?"

Frame 39-11

Baada ya kuongea na Yesu Pilato alitoka nje katika umati wa Watu na kusema "Nimeona hakuna hatia juu ya mtu huyu" lakini viongozi wa kiyahudi na makutano wote wakapiga kelele "Msulubishe" pilato akajibu "Hana hatia" lakini waliendelea kupiga kelele tena kwa nguvu. na Pilato akasema kwa mara ya tatu "Hana hatia yeyote"

Frame 39-08

Petro akaondoka na akilia kwa huzuni kubwa. Wakati huo huo, Yuda, mwenye kumsaliti Yesu, akaona kwamba viongozi wa kiyahudi wamemweka Yesu hatiani. Yuda akapatwa na huzuni kubwa sana na akaondoka mahali pale akaenda kujiua mwenyewe.

Frame 39-05

Viongozi wa kiyahudi wote wakamjibu kuhani mkuu kuwa "Anastahili kufa" baadaye wakamfunika macho Yesu, wakamtemea mate, wakampiga, na kumdhihaki.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 26:57 - 27:26; Marko14:53-15:15; Luka 22:54-23:23; Yohana 18:12-19:16

40. Yesu Anasulubiwa

Frame 40-06

Ndipo katika eneo hilo kukawa giza nene, ingawa ilikuwa mchana. Mchana huo kukawa giza kwa saa tatu.

Frame 40-04

Yesu alisulibiwa katikati ya wanyang'anyi wawili; mmojawapo alimdhihaki Yesu, lakini mwingine alisema, "Humwogopi Mungu!? Sisi tunahatia, lakini huyu hana hatia" Ndipo yeye akamwabia Yesu "Tafadhali unikumbuke katika ufalme wako" Yesu akamjibu, leo, utakuwa nami Paradiso."

Frame 40-02

Askari walimpeleka Yesu eneo liitwalo "fuvu la kichwa" wakaipigilia miguu na mikono yake msalabani. Lakini Yesu akasema, "Baba wasamehe, kwa sababu hawajui wanalotenda." Pilato akaagiza waandike kwamba, "Mfalme wa Wayahudi" ikiwa ni ishara; na waweke msalabani, juu ya kichwa cha Yesu.

Frame 40-01

Baada ya askari kumdhihaki Yesu, walimpeleka kumsulibisha. walimlazimisha aubebe msalaba ambao ungetumika kumuua.

Frame 40-07

Yesu akalia, "Baba imekwisha naweka mikononi mwako roho yangu." Ndipo akainama akajitoa mwenyewe roho yake. Alipokufa lilitokea tetemeko la ardhi na pazia la hekaluni lililowatenga watu na Mungu lilipasuka vipande viwili, tokea juu hadi chini.

Frame 40-09

Na ndipo Yusufu na Nikodemo viongozi wa Wayahudi walioamini Yesu kuwa ni Masihi wakauomba mwili wa Yesu na kuufunga kwenye sanda na kupeleka kwenye kaburi lililochongwa tayari mwambani na wakasogeza jiwe kubwa kulifunga kaburi.

Frame 40-03

Askari walipigia kura mavazi yake. Na kitendo hiki kinatimiza unabii usemao kwamba, " wakagawana nguo zangu na kucheza kamali."

Frame 40-08

Kifo chake Yesu kinafungua njia ili watu waje kwa Mungu. Askari aliyemlinda Yesu alipoona mambo haya yote yanatokea alisema, "Hakika mtu huyu hakuwa na hatia, alikuwa Mwana wa Mungu."

Frame 40-05

Viongozi wa wayahudi na baadhi ya wengine katika umati walimdhihaki Yesu. Wakisema, "kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka msalabani, jiokoe mwenyewe, ndipo tutakuamini."

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 27:27-61; Marko 15:16-47; Luka 23:26-56; Yohana 19: 17-42

41. Mungu Anamfufua Yesu kutoka katika Wafu

Frame 41-06

Malaika akawaambia wale wanawake, "Nendeni na mkawaambie wanafunzi, 'Kwamba Yesu amefufuka kutoka katika wafu na atawatangulia kwenda Galilaya."

Frame 41-04

Ghafla, kulikuwa na tetemeko kubwa. Malaika ambaye mng'ao wake ulikuwa kama mng'ao wa mwanga wa radi alitokea kutoka mbinguni. Aliliviringisha mbali lile jiwe lilokuwa limeufunika mlango wa kaburi na kulikalia. Askari waliokuwa wanalilinda kaburi waliogopa sana na kuanguka chini na kuwa kama watu waliokufa.

Frame 41-02

Pilato alisema, "Chukueni baadhi ya askari na muhakikishe kaburi limelindwa ipasavyo." Hivyo wakaweka muhuri kwenye jiwe katika mlango wa kuingilia kaburini na kuweka maaskari ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu yeyote ambaye angeuiba mwili.

Frame 41-01

Baada ya askari kuwa wamemsulubisha Yesu, viongozi wa Kiyahudi wasioamini walimwambia Pilato, "Yule Muongo, Yesu, alisema angefufuka baada ya siku tatu. Mtu mmoja lazima alilinde kaburi ili kujihakikishia kwamba wanafunzi wake hawatauiba mwili wake na kusema amefufuka kutoka katika wafu."

Frame 41-07

Wanawake walijawa na hofu na furaha kuu. Wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi habari njema.

Frame 41-03

Siku iliyofuata baada ya Yesu kuzikwa ilikuwa ni Sabato, na wayahudi hawakuruhusiwa kwenda kaburini siku hiyo. Hivyo asubuhi na mapema baada ya Sabato, wanawake wengi walijiandaa kwenda kwenye kaburi la Yesu kuupaka mwili wa Yesu marashi ya maziko.

Frame 41-08

Wale wanawake walipokuwa wanaenda kuwaambia wanafunzi wake habari njema, Yesu aliwatokea wale wanawake, nao wakamuabudu. Yesu akasema, "Msiogope. Nendeni mkawaambie wanafunzi wangu waende Galilaya.Wataniona huko."

Frame 41-05

Wale wanawake walipofika kaburini, malaika aliwaambia. "Msiogope. Yesu hayupo hapa. Amefufuka kutoka katika wafu, kama alivyosema kwamba atafufuka! Angalieni kaburini na muone." Wale wanawake wakaangalia mle kaburini na kupaona mahali mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa. Mwili wake haukuwepo pale!

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 27:62-28:15; Marko 16:1-11; Luka 24:1-12; Yohana 20:1-18

42. Yesu Anarudi Mbinguni

Frame 42-06

Wakati wanafunzi wanaendelea kuongea, Yesu alijitokeza katikati yao kwenye kile chumba na kusema, "Amani iwe kwenu!" Wanafunzi walidhani kuwa ni mzimu, lakini Yesu akawaambia, "Mbona mnaogopa na kuwa na mashaka? Angalieni mikono yangu na miguu. Mizimu haina mwili kama mimi." Kuwahakikishia kuwa Yeye si mzimu, aliwaomba chakula. Walimpa kipande cha samaki kilichopikwa, naye akala.

Frame 42-10

Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, mkiwafundisha kuyatii yote niliyowaamuru. Kumbukeni kuwa nitakuwa pamoja nanyi siku zote."

Frame 42-04

Hawa wanaume wawili walimkaribisha Yesu akae nao, naye akafanya hivyo. Walipokuwa tayari kula chakula cha jioni, Yesu alichukua kipande cha mkate, alimshukuru Mungu kwa mkate huo, akaumega. Ghafla, wakamtambua kuwa ni Yesu. Lakini wakati huo huo, Yesu akatoweka eneo hilo.

Frame 42-02

Yesu aliwakaribia na akaanza kutembea nao, lakini hawakumtambua. Aliwauliza juu ya mazungumzo yao, nao wakamueleza maajabu yote yaliyo tokea kumuhusu Yesu kwa siku chache zilizopita. Kwani walidhani wanaongea na mgeni asiyejua habari zilizotokea katika Yerusalemu.

Frame 42-01

Siku ile Yesu alipofufuka, wanafunzi wake wawili walikuwa wanaenda mji jirani. Wakiendelea kutembea, walizungumza habari zilizotokea kumuhusu Yesu. Walitumaini kuwa alikuwa Masihi, lakini aliuawa. Wanawake waliwaambia yu hai anaishi tena. Nao hawakujua cha kuamini.

Frame 42-07

Yesu alisema, "Niliwaambia kila kitu kilicho andikwa katika neno la Mungu kunihusu mimi ni lazima kitimie." Ndipo alipofungua akili zao ili waweze kulielewa neno la Mungu. Akasema, "Iliandikwa muda mrefu uliopita yakuwa Masihi atateswa, atakufa na kufufuka kwa wafu siku ya tatu."

Frame 42-09

Ndani ya siku arobaini zilizofuata, Yesu aliwatokea wanafunzi wake mara kwa mara. Wakati mwingine aliwatokea watu zaidi ya 500 kwa wakati mmoja! aliwadhibitishia wanafunzi wake kwa njia nyingi kuwa Yeye yu hai, na aliwafundisha kuhusu ufalme wa Mungu.

Frame 42-03

Ndipo Yesu akawaelezea jinsi neno la Mungu linavyo sema kumuhusu Masihi. Aliwakumbusha manabii walivyosema, kwamba Masihi atateswa na kuuawa, na atafufuka tena siku ya tatu. Nao walipofika katika mji waliokuwa wamepanga kufikia hawa wanaume wawili, ilikuwa imekaribia jioni.

Frame 42-11

Siku arobaini baada ya Yesu kufufuka kwa wafu, aliwaambia wanafunzi wake, "Kaeni Yerusalemu mpaka hapo Baba yangu atakapo wapa nguvu, pale Roho Mtakatifu atakapowajilia ninyi. Kisha Yesu akaenda mbinguni, nayo mawingu yakamfunika akatoweka kwao. Yesu alikaa mkono wa kuume wa Mungu kutawala vitu vyote.

Frame 42-08

"Iliandikwa pia katika maandiko kwamba wanafunzi, wangu watatangaza kwa kila mtu katika makundi, kwamba lazima watubu ili wapate msamaha wa dhambi zao. Nao watafanya hivyo kuanzia Yerusalem, nao wataenda kwa watu wote mahali pote. Ninyi ni mashahidi wa mambo haya."

Frame 42-05

Hawa wanaume wawili waka ambiana, "Yule alikuwa ni Yesu! Ndiyo maana mioyo yetu ilikuwa inaungua wakati akielezea neno la Mungu kwetu." Punde, walirudi Yerusalemu. Nao walipofika, waliwaambia wanafunzi, "Yesu yu hai! tumemuona."

Simulizi ya Biblia kutoka: Matayo 28:16-20; Marko 16:12-20; Luka 24:13-53; Yohana 20:19-23; Matendo ya Mitume 1:1-11

43. Kanisa Linaanza

Frame 43-12

Yapata Watu 3,000 wakaamini alichokisema Petro wakawa wanafunzi wa Yesu. Nao wakabatizwa wakawa washirika wa kanisa la Yerusalemu.

Frame 43-13

Wanafunzi waliendelea kusikiliza mafundisho ya mitume, walikaa pamoja na kula pamoja na kuomba pamoja. Walifurahi wakamsifu Mungu kwa pamoja na walishirikishana kila kitu walichokuwa nacho kwa pamoja. Kila mtu alikuwa na mtizamo mzuri juu yao. kila siku watu wengi waliendelea kuamini.

Frame 43-06

"Wanaume wa Israeli Yesu alikuwa mwanadamu alitenda miujiza na maajabu mengi kwa uwezo wa Mungu, nanyi mnajua na kuona lakini mlimsulubisha."

Frame 43-10

Watu waliomsikiliza Petro walivutwa kwa undani na mafundisho aliyosema. Wakamwuliza Petro na wanafunzi. Je mnataka tufanye nini?

Frame 43-04

Watu wa Yerusalemu waliposikia kelele, kusanyiko la watu walikuja kushuhudia kilichotokea. Watu waliposikia waumini wakitangaza matendo ya ajabu ya kazi za Mungu, walishangaa sana kwa kuwa walisikia maneno hayo kwa lugha zao za asili.

Frame 43-02

Kila mwaka baada ya siku 50 za Pasaka, Wayahudi walisheherekea siku muhimu ya Pentekosti. Pentekosti ni kipindi ambacho wayahudi walisheherekea mavuno ya ngano, Wayahudi walikwenda Yerusalemu wakitokea ulimwenguni kote kusheherekea kwa pamoja Pentekosti. Mwaka huu kipindi cha Pentekosti kilikuwa baada ya wiki moja Yesu aliporudi mbinguni.

Frame 43-01

Baada ya Yesu kurudi mbinguni, wanafunzi wake walibaki Yerusalem kama alivyowaagiza kufanya. Waumini wake walikuwa na utaratibu wa kukusanyika na kuomba pamoja.

Frame 43-07

Ingawa Yesu alikufa, Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na hii inatimiza unabii unaosema "Hutamwacha mtakatifu wako kuoza kaburini" Nasi tu mashahidi wa mambo hayo kuwa ukweli kwamba Mungu alimfufua Yesu.

Frame 43-09

"Mlimsulubisha mtu huyu Yesu. Lakini mfahamu kwa uhakika Mungu amesababisha Yesukufanyika kuwa Bwana na Masihi."

Frame 43-03

Wakati waumini wakiwa pamoja, ghafla nyumba ilijawa na sauti kama upepo mkali. Kisha kitu kama mwali wa moto kikaonekana juu ya vichwa vya waumini wote. Wote walijazwa na Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha nyingine.

Frame 43-11

Petro akawajibu, "kila mtu anapaswa atubu na kubatizwa kwa Jina la Yesu Kristo na Mungu atawasamehe dhambi zenu. Kisha atawapa kipawa cha Roho Mtakatifu."

Frame 43-08

"Yesu anatukuzwa kwenye mkono wa kuume wa Mungu baba, na Yesu amemtuma Roho Mtakatiifu kama alivyoahidi kuwa angefanya. Roho Mtakatifu anasababisha mambo mnayoyaona na kuyasikia.

Frame 43-05

Baadhi ya watu wakawashutumu wanafunzi kuwa wamelewa, lakini Petro akasimama akawaambia, nisikilizeni, hawa watu hawajalewa, bali unatimizwa unabii uliotolewa na Yoeli ambao Mungu alisema "Siku za mwisho nitamdhihirisha Roho"

Simulizi ya Biblia Kutoka: Matendo ya Mitume 2

44. Petro na Yohana Wamponya Ombaomba

Frame 44-06

Viongozi wengi wa Hekalu walisikitishwa sana na yale maneno ya Petro na Yohana. Kwa hiyo wakawakamata na kuwaweka gerezani. Pamoja na hayo, bado watu wengi walimwamini Yesu kwa ujumbe wa Petro, na idadi ya wanaume waliomwamini Yesu siku hiyo walikuwa 5,000.

Frame 44-04

Watu wengi wakakusanyika kwa haraka ili kumwona yule kiwete aliyeponywa. Petro akawaambia, "Kwa nini mnashangazwa na uponyaji ambao mtu huyu ameupata? Uponyaji huu haujafanyika kwa sababu ya wema na nguvu zetu. Bali ni kwa nguvu na imani itokayo kwa Yesu Kristo."

Frame 44-02

Petro akamtazama yule kiwete na kumwambia, "Sina fedha za kukupa. Japo nitakupa kile nilichonacho. Kwa jina la Yesu Kristo, simama na utembee!"

Frame 44-01

Siku moja, Petro na Yohana walikuwa wakihudhuria Hekaluni. Na walipokaribia kwenye lango la hekalu, walimwona kiwete aliyeketi langoni na kuomba fedha.

Frame 44-07

Siku iliyofuata, viongozi wa hekalu waliwaleta Petro na Yohana kwa kuhani mkuu na mbele ya viongozi wa kidini na kuwauliza, "Ni kwa nguzu gani mlimponya huyu kiwete?"

Frame 44-09

Wale viongozi wa dini walipowatazama na kuwasikiliza Petro na Yohana na ujasiri wa hotuba yao, na kuowaona kuwa walikuwa watu wa kawaida na wasio na elimu, walishitushwa. Walikumbuka kuwa walikuwa pamoja na Yesu Kristo. Baada ya kuwatisha waliwaruhusu waende zao.

Frame 44-03

Mara tu, Mungu akamponya yule kiwete akaamka na akaanza kutembea na kurukaruka hapa na pale na kumsifu Mungu. Watu wote waliokuwa kwenye ua wa Hekalu walishikwa na mshangao mkubwa.

Frame 44-08

Petro akawajibu, " Mtu huyu asimamaye mbele yenu, aliponywa kwa nguzu za Yesu. Ambaye nyinyi mlimsulubisha, lakini Mungu alimfufua katika wafu. Hamkumkubali, ila hakuna njia jingine duniani inayoweza kuokoa isipokuwa kwa nguvu za Yesu Kristo!"

Frame 44-05

"Ninyi ndio mliomshawishi Mtawala kutoka Rumi kumuua Yesu. Mlimuua mwanzilishi wa uzima, lakini Mungu alimfufua katika wafu. Ingawa hamkujua kile mlichokuwa mkikifanya, Mungu alitumia matendo yenu maovu kwa kutimiza unabii wa kwamba Masihi atateswa na kufa. Kwa hiyo mnapaswa kutubuna kurudi kwa Mungu ili msamehewe dhambi zenu."

Simulizi ya Biblia Kutoka: Matendo ya Mitume 3:1-4:22

45. Stephano na Filipo

Frame 45-12

Kwa hiyo walienda kwenye maji, na Filipo akambatiza yule mtu wa Etheopia. Baada ya kutoka majini, ghafla Roho Mtakatifu alimwondoa Filipo na kumpeleka mahali pengine kuendelea kuwaambia watu habari za Yesu.

Frame 45-13

Yule mtu wa Ethiopia aliendelea na safari yake kwenda nyumbani akimfurahia za Mungu kuwa amemjua Kristo.

Frame 45-06

Kijana mmoja aitwaye Sauli alikubaliana na watu waliomwua Stephano na akalinda nguo zao walipokuwa wanamponda mawe. Tangu siku hiyo, watu wa Yerusalemu wakaanza kuwatesa wafuasi wa Yesu, hivyo waamini wakakimbia kwenda sehemu zingine. Licha ya hayo, walihubiri habari za Yesu popote walipoenda.

Frame 45-10

Filipo alimuelezea Muethiopia kuwa Isaya aliiandika juu ya Yesu. Vile vile Filipo alitumia maandiko mengine kumuelezea habari njema za Yesu.

Frame 45-04

Viongozi wa kidini ya kiyahudi waliposikia hayo, walikasirika, wakaziba masikio yao na kupaza sauti kubwa. Walimburuta Stephano kwa nguvu na kumpeleka nje ya mji na kumponda kwa mawe ili kumwua.

Frame 45-02

Siku moja wakati Stephano anafundisha habari za Yesu, baadhi ya Wayahudi wasiomwamini Yesu walianza kubishana na Stephano. Walikasirika sana na kusema uongo kinyume cha Stephano kwa viongozi wa kidini. Wakasema, "Tumemsikia akisema vibaya juu ya Musa na Mungu!" Hivyo viongozi wa kidini walimkamata Stephano na kumpeleka kwa Kuhani Mkuu na viongozi wengine wa kiyahudi mahali ambapo mashahidi wengine zaidi walishuhudia uongo juu ya Stephano.

Frame 45-01

Mmoja wa viongozi wa Kanisa la kwanza aliyeitwa Stephano. Alikuwa na tabia nzuri, mwenye kujawa na Roho Mtakatifu na hekima. Stephano alifanya miujiza mingi na kutumia ushawishi mkubwa illi watu wapate kumwamini Yesu.

Frame 45-07

Mwanafunzi wa Yesu jina lake Filipo, alikuwa mmoja wa waumini waliokimbia kutoka Yerusalemu wakati wa mateso. Alienda Samaria alipohubiri habari za Yesu na watu wengi wakaokolewa. Ndipo siku moja malaika kutoka kwa Bwana akamwambia Filipo kwenda katika njia fulani jangwani. Alipokuwa akitembea barabarani, Filipo alimuona afisa mashuhuri kutoka nchi ya Ethiopia akiwa amepanda gari lake. Roho Mtakatifi alimwambia aende kukutana na kuzungumza na mtu huyo.

Frame 45-09

Filipo alimwuliza huyo mtu wa Ethiopia, "Unaelewa kile unachokisoma?" Yule mtu akajibu, "Hapana. Siwezi kuelewa isipokuwa awepo mtu wa kunielezea. Tafadhali njoo ukae pamoja nami. Isaya aliandika kuhusu yeye au juu ya mtu mwingine?"

Frame 45-03

Kuhani Mkuu akamwuliza Stephano, "Maneno hayo ni ya kweli?" Stephano aliwajibu kwa kuwakumbusha mambo mengi makuu ambayo Mungu ameyafanya kutoka Ibrahimu hata wakati wa Yesu, jinsi ambavyo watu wa Mungu waliendelea kutomtii Mungu. Ndipo aliposema, "Enyi watu wagumu na waasi kila mara mnamkataa Roho Mtakatifu, kama wazazi wenu walivyomkataa Mungu na kuwaua manabii wake. Na nyinyi mmefanya jambo baya zaidi kuliko wao! Mmemwua Masihi."

Frame 45-11

Filipo na yule mtu wa Ethiopia walipokuwa wanasafiri, walifika kwenye maji. Muethiopia akasema, "Tazama! Kuna maji hapa! Je naweza kubatizwa?" Akamwambia dereva wake kusimamisha gari.

Frame 45-08

Filipo alipolikaribia gari, alimsikia mu-Ethiopia akisoma kile ambacho nabii Isaya aliandika. Huyo mtu alisoma, "Walimwongoza kama mwanakondoo na kumwua, kama mwanakondoo, alikaa kimya bila kusema neno. Walimtendea vibaya na hata hawakumheshimu. Walitoa uhai wake na kumwua."

Frame 45-05

Stephano alipokaribia kufa, alilia kwa sauti, "Ee Yesu, pokea roho yangu." Ndipo alipopiga magoti na kusema tena, "Bwana, usiwahesabie dhambi hii." Baadaye akafa.

Simulizi ya Biblia kutoka: Matendo ya Mitume 6:8-8:5; 8:26-40

46. Paulo Anakuwa Mkristo

Frame 46-06

Mara hiyo, Sauli alianza kuhubiri Wayahudi katika Dameski akisema, "Yesu ni Mwana wa Mungu". Wayahudi walishangaa kuona mtu aliyekuwa akijitahidi kuwaangamiza wakristo amegeuka kuwa mfuasi wa Yesu! Sauli alibainisha kuwa Yesu ndiye Masihi.

Frame 46-10

Hapo Antiokia, siku moja wakristo walipo kuwa katika maombi ya kufunga, Roho Mtakatifu aliwaambia nitengeeni Sauli na Barinaba wafanye kazi niliyo waitia. Hivyo kanisa liliwaombea na kuwawekea mikono, kisha wakawatuma waende maeneo mengine mengi kuhubiri habari njema za Yesu. Barinaba na Sauli walifundisha makundi ya watu wa matifa mbalimbali, watu wengi wakamwamini Yesu.

Frame 46-04

Huko Dameski alikuwapo mwanafunzi wa Yesu aliyeitwa Anania. Mungu alimwagiza, "Nenda katika nyumba ambamo anaishi Sauli. Weka mikono juu yake ili apate kuona tena." Bali Anania akajibu, "Bwana nimesikia jinsi mtu huyu anavyowaudhi wafuasi wa wako. "Mungu akamwambia, Nenda! Nimemchagua alitangaze Jina langu kwa Wayahudi na kwa watu kutoka Mataifa mengine. Naye atateseka sana kwa ajili ya jina langu."

Frame 46-02

Sauli alipokuwa akienda Damesiki, nuru kuu kutoka mbinguni ilimwangaza pande zote na akaanguka chini. Sauli alisikia mtu akisema, "Sauli! Sauli! Kwa nini unaniudhi?" Sauli alimuuliza" Wewe ni nani Bwana?" Jibu la Yesu lilikuwa, "Mimi ni Yesu unayeniudhi."

Frame 46-01

Kijana Sauli ndiye alitunza nguo za wanaume waliomuua Stefano. Yeye hakuwa mfuasi wa Yesu. Kazi yake ilikuwa kuwatesa wakristo. Alizungukia kila kaya mjini Yerusalemu akiwakamata watu wa jinsia zote waliomwamini Yesu na kuwaweka gerezani. Mkuu wa makuhani alimpa kibali kwenda Dameski kuwakamata wafuasi wa Yesu na kuwaleta Yerusalemu.

Frame 46-07

Siku nyingi baadaye, Wayahudi walipanga kumuua Sauli. Waliwatuma watu kumfuatilia katika malango ya miji kwa lengo la kumwangamiza. Lakini Sauli aligundua mpango huo, na rafiki zake walimsaidia kutoroka. Usiku mmoja aliteremshwa akiwa ndani ya kikapu ukutani, akishatoroka kutoka Dameski aliendelea tu kuhubiri habari za Yesu.

Frame 46-09

Baadhi ya waumini waliokimbia mateso huko Yerusalemu na kwenda mbali huko Antiokia, walizidi kuhubiri kuhusu Yesu. Wenyeji wengi wa Antiokia hawakuwa Wayahudi, hicho ndicho kipindi ambacho watu wa mataifa kwa mara ya kwanza waliipokea imani. Barinaba na Sauli walikwenda huko kuwafundisha hao waumini wachanga zaidi kuhusu Yesu na kulikomaza kanisa. Kwa mara ya kwanza wafuasi wa Yesu waliitwa Wakristo hapo Antiokia.

Frame 46-03

Sauli alipoamuka, hakuweza kuona. Waliokuwa pamoja naye ilibidi wampeleke Dameski. Alikaa siku tatu bila kula wala kunywa.

Frame 46-08

Sauli alitembelea Yerusalemu, lakini wanafunzi wa Yesu walimhofu. Kisha muumuni aliyeitwa Barinaba alimpeleka kwa mitume kuwaeleza jinsi alivyo hubiri kwa ujasiri habari njema huko Dameski. Taarifa hiyo ilisababisha mitume wamkubali Sauli.

Frame 46-05

Ndipo Anania alikaenda kwa Sauli, akamwekea mikono, akasema, "Yesu uliyekutana naye njiani wakati unakuja hapa, amenituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe na Roho Mtakatifu". Mara akaweza kuona tena. Kisha Anania akambatiza, akala chakula na nguvu zake zikamrudia.

Simulizi ya Biblia Kutoka: Matendo ya Mitume 8:3; 9:1-31; 11:19-26;13:1-3

47. Paulo na Sila wakiwa Filipi

Frame 47-12

Mlinzi wa wafungwa na kila mtu katika nyumba yake walimwamini Yesu na kubatizwa. Mlinzi wa wafungwa aliwahudumia chakula Paulo na Sila na walifurahi pamoja.

Frame 47-13

Siku iliyofuata, Paulo na Sila waliachiliwa huru kutoka gerezani na waliambiwa kuondoka Filipi na viongozi wa mji. Paulo na Sila walipata nafasi kumtembelea Lidia na wapendwa wengine na ndipo walipoondoka katika mji. Injili ya Yesu iliendelea kuenea na Kanisa liliendelea kukua.

Frame 47-06

Watumikishaji wa msichana walipotambua kuwa bila ya pepo mtumwa wao alikuwa hawezi kuwatabiria watu, walikasirika. Kwa kuwa hangewaingizia kipato cha fedha tena, kwa kulipwa wao ili afanye utabiri kwa watu.

Frame 47-10

Askari mlinzi wa wa wafungwa aliamuka, alijawa na hofu kubwa sana baada ya kuona milango ya gereza iko wazi, akifikiri kuwa, wafungwa wote watakuwa wametoroka, alikusudia kujiangamiza. (Alijua serikali ya Kirumi ingemhukumu kifo endapo aliwaachia wafungwa kutoroka). Lakini Paulo alipaza sauti kumkataza "Acha kujiangamiza, sisi sote hatujatoroka.

Frame 47-04

Msichana mtumwa alikuwa akipaza sauti kila alipowaona wakitembea, na kusema, "Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye hai." Wanawaelezeeni njia ya kupata wokovu! Alifanya hivyo bila ya kuchoka kiasi cha kumkera Paulo.

Frame 47-02

Mungu alimwongoza Lidia kuupokea ujumbe wa Yesu, yeye, wakiwemo watu wa nyumbani mwake, wote walibatizwa. Paulo na Sila walikaa kwake na watu wake, aliwakaribisha nyumbani.

Frame 47-01

Sauli alianza kujiita Paulo, kwa jina lake la Kirumi, alipofanya safari katika ufalme wote wa madola ya Kirumi. Paulo na mtu wake wa Karibu aitwaye Sila walienda kuhubiri habari njema kuhusu Yesu katika mji wa Filipi. Walienda nje ya mji, kando ya mto mahali ambapo watu walikutana kusali. Walipokuwa hapo walionana na mwanamke mfanya biashara aliyeitwa Lidia. Alimpenda na alimcha Mungu.

Frame 47-07

Kwa sababu hiyo Paulo na Sila walipelekwa kwenye vyombo vya dola vya serikali ya Kirumi na Watumikishaji wa msichana mtumwa, watu hawa waliwapiga na kuwatia gerezani.

Frame 47-09

Kushtukia, kulitokea tetemeko kubwa lililosababisha milango ya gereza na pingu za minyororo ya wafungwa kufunguka na kuanguka kutoka mikononi.

Frame 47-14

Miji mingi ilifikiwa na Paulo pamoja na viongozi wengine wakristo waliosafiri kwenda katika miji hiyo wakihubiri na kufundisha habari njema za Yesu. Zaidi ya hapo waliandika barua nyingi za kuwatia moyo wakristo makanisani. Baadhi ya barua hizi ni sehemu ya vitabu vya Biblia.

Frame 47-03

Kulikuwa na mahali ambapo watu walikuwa wakikutana na kusali. Hapo ndipo mahali Paulo na Sila mara nyingi walikutana na watu. Walipokuwa akienda mahali pale kila siku, mwanamke mmoja mwenye umri mdogo kabisa, akiwa mtumwa, na mwenye pepo, aliwafuata. Alikuwa akiwatabiria watu kwa kuongozwa na pepo, kutokana na uwezo kama huo aliwafaidisha waliomtumikisha, kwa kuwapatia fedha nyingi kwa kazi yake ya utambuzi.

Frame 47-11

Mlinzi wa wafungwa alienda kwa Paulo na Sila akitetemeka na kuwauliza, "Nifanye nini nipate kusalimika?" Paulo alimjibu, "mwamini Yesu, Bwana, wewe na watu wa nyumbani mwako mtapata wokovu. Hivyo mlinzi wa wafungwa aliwakaribisha Paulo na Sila nyumbani kwake na kuwaosha majeraha yao. Kila mtu katika nyumba yake alipata kuhubiriwa na Paulo habari njema za Yesu.

Frame 47-08

Paulo na Sila waliwekwa katika chumba cha ndani kabisa sehemu mojawapo ya gereza, kwa usalama wasitoroke na hata kufungwa miguu yao. Usiku wa manane walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu.

Frame 47-05

Hatimaye siku moja msichana mtumwa alipoanza kupaza sauti, Paulo aligeuka kwake na kumkemea pepo aliyekuwa ndani yake, akisema, "kwa jina la Yesu toka," palepale pepo alimwacha.

Simulizi ya Biblia kutoka: Matendo ya Mitume 16:11-40

48. Yesu ndiye Masihi aliyeahidiwa:

Frame 48-12

Japokuwa Musa pia alikuwa ni nabii mkubwa aliyetangaza neno la Mungu, Yesu ndiye nabii mkuu zaidi ya manabii wote.Kila jambo alilolifanya na kulisema Yesu lilikuwa ni tendo na neno la Mungu kwakuwa yeye ni Mungu. Ndio maana wakati mwingine Yesu anaitwa neno la Mungu.

Frame 48-13

Mungu alimuahidi mfalme Daudi kuwa mmoja ya wazaliwa wake atawatawala watu wa Mungu milele. Kwakuwa Yesu ni mwana wa Mungu na Masihi , yeye ndiye yule mzaliwa wa uzao wa Daudi atakayetawala milele.

Frame 48-06

Katika kipindi cha mamia ya miaka, makuhani wakadumu katika kutoa sadaka za kuteketezwa, wakidhihirisha aina ya adhabu iliyowapasa kupewa kwa ajili ya dhambi zao. Hata hivyo, sadaka hizo hazikuweza kabisa kuwaondolea dhambi zao. Hivyo, Yesu ndiye kuhani mkuu asiyelingana na makuhani wengine. Yeye alijitoa nafsi yake mwenyewe ili awe sadaka ya pekee ya kuteketezwa kwa ajili ya kuziondoa dhambi za watu wote duniani. Yesu ndiye kuhani mkuu wa kweli maana alibeba adhabu ya dhambi iliyotendwa na watu wote.

Frame 48-10

Yesu hakuwa na kosa wala dhambi yoyote na aliuawa katika kipindi cha maazimisho ya pasaka. Hakika Yesu ndiye mwanakondoo wetu wa pasaka. kwa yeyote anaemwamini Yesu, damu yake Yesu hulipia dhambi za mtu huyo na adhabu ya Mungu humruka mtu huyo.

Frame 48-04

kupitia mpango huo, Mwenyezi Mungu aliahidi kuwa mmoja wa wazaliwa katika uzao wa Eva atakiponda kichwa cha shetani, na shetani atakigonga kisigino chake. Maneno haya yana maana kwamba, shetani atamuua Masihi, lakini Mwenyezi Mungu atamfufua tena, na kisha huyo Masihi atazishinda nguvu za shetani milele. Baada ya miaka mingi kupita, Mwenyezi Mungu akaudhihirishia ulimwengu kuwa Yesu ndiye Masihi.

Frame 48-02

Katika bustani ya Edeni, Shetani alijitokeza kama nyoka. Akazungumza na Eva kwa lengo la kumdanganya. Kwa njia hiyo, Adam na Eva wakawa wamemtenda Mungu dhambi, na leo watu wote duniani tunaweza kuugua na kufa kama matokeo ya dhambi.

Frame 48-01

Mwenyezi Mungu alipoumba ulimwengu, vitu vyote vilikuwa sawa pasipo dosari yoyote. Hapakuwa na dhambi, wala magonjwa, wala kifo duniani. Adam na Mkewe, Eva, walipendana sana na walimpenda Mungu pia. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyokusudia ulimwengu uwe.

Frame 48-07

Ndipo Mwenyezi Mungu akazungumza na Ibrahimu akamwambia, "Kupitia wewe Ibrahimu, watu wa kila kabila duniani wamebarikiwa." Naye Yesu alitokana na uzao wa Ibrahimu, na watu wa kila namna wanabarikiwa kupitia Ibrahimu. Hivyo, kila anayemwamini Yesu ameokolewa kutoka katika dhambi, na anafanyika kuwa uzao wa Ibrahimu kwa jinsi ya kiroho.

Frame 48-09

Hata Mwenyezi Mungu alipoamuru mapigo saba katika nchi ya Misri, aliagiza kila familia ya kiisraeli kuchinja mwana kondoo asiye na kasoro na kisha kunyunyiza damu ya kondoo juu na chini ya miimo ya milango yao. Na ndipo Mwenyezi Mungu alipoiona damu katika miimo ya milango yao, aliziruka nyumba zile na hakuwauwa watoto wao wa kiume wa kwanza .Tendo hilo linajulikana kama pasaka.

Frame 48-14

Daudi alikuwa mfalme wa Israeli, lakini Yesu ni mfalme wa ulimwengu wote. Atarudi tena kuutawala ufalme wake kwa haki na amani milele.

Frame 48-03

Jambo jingine la hatari zaidi likajitokeza kama matokeo ya dhambi ya Adam na Eva. Uhusiano wao na Mungu ukaharibika na toka wakati huo, kila mwanadamu anazaliwa akiwa na asili ya dhambi, akiwa hana mahusiano mazuri na Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu akawa na mpango wa kurejesha uhusiano ulioharibiwa na dhambi baina ya mwanadamu na Mungu.

Frame 48-11

Ni kweli kuwa Mwenyezi Mungu alifanya agano na watu wake, taifa la Israel. Bali sasa Mwenyezi Mungu anafanya agano lililo wazi kwa kila mtu. Kwa sababu ya agano hili jipya, watu wote wa kila mahali, wanaweza kuwa sehemu ya watu wa Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo.

Frame 48-08

Mwenyezi Mungu alipomwagiza Ibrahimu kumtoa mwanae, Isaka, kama sadaka ya kuteketezwa na akatii, Bwana Mungu akampatia Ibrahimu mwana kondoo achinjwe na kutolewa sadaka badala ya mwanae, Isaka.Hii inatufundisha kuwa sisi sote tunastahili kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini Mwenyezi Mungu amemtoa Yesu, mwanakondoo wa Mungu ili atolewe kama sadaka na kisha kufa badala yetu.

Frame 48-05

Katika siku zile Mwenyezi Mungu alipouangamiza ulimwengu kwa mafuriko, aliandaa chombo cha kuwaokoa na gharika hilo watu wote waliokuwa wanamwamini. Kwa sababu ya dhambi, ni kwa namna iyo hiyo, watu wote duniani wanastahili kuangamizwa. Lakini ashukuriwe Muwenyezi Mungu aliyemtoa Yesu kumuokoa kila mtu anayemwamini.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 1-3, 6, 14, 22; Kutoka 12, 20; 2Samueli 7; Waebrania 3:1-6, 4:14-5:10, 7:1-8:13, 9:11-10:18; Ufunuo 21

49. Agano Jipya la Mungu

Frame 49-15

Ikiwa unaamini katika Yesu na nini amefanya kwa ajili yako, wewe ni mkristo! Mungu amekutoa kwenye ufalme wa giza wa Shetani na amekuweka kwenye ufalme wa nuru wa Mungu. Mungu amechukua ukale wako, amechukua njia zako za kufanya dhambi na amekupa upya, njia ya ufanyaji haki kwa mambo.

Frame 49-17

Ikiwa ni rafiki wa Mungu na mtumishi wa Yesu, Bwana, unatakiwa kutii kile Yesu alichokufundisha wewe. Hata kama, umkristo, unaweza jaribiwa kutenda dhambi. Lakini Mungu ni mwaminifu na anasema ikiwa utakiri dhambi zako, atakusamehe. Atakupa nguvu ya kupambana dhidi ya dhambi.

Frame 49-12

Matendo mema hayawezi kukuokoa. Hivyo hakuna chochote unachoweza kufanya kwa ajili ya mahusiano yako na Mungu. Yesu pekee awezae kuosha dhambi zako. Unapaswa kumuamini Yesu kuwa ni mwana wa Mungu, alikufa msalabani badala yako, na Mungu alimfufua tena na kumpa uhai.

Frame 49-13

Mungu atamuokoa kila mtu amwaminiye Yesu na kumpokea kama Bwana wake. Lakini hatamuokoa mtu yeyote asiyemuamini yeye. Haijalishi wewe ni tajiri au maskini, mwanaume au mwanamke, mzee au kijana au mahali unapoishi. Mungu anakupenda wewe na anataka umuamini Yesu ili aweze kuwa na mahusiano ya karibu na wewe.

Frame 49-06

Yesu alifundisha kua baadhi ya watu watampokea na kuokolewa, lakini wengine hawataokolewa. Akasema baadhi ya watu ni kama udongo mzuri. Wamepokea habari njema ya Yesu na wameokolewa. Lakini watu wengine ni udongo mgumu wa njiani, ambapo mbegu ya neno la Mungu haiwezi kuingia na kutengeneza mavuno yoyote. Watu hawa wamekataa ujumbe kumuhusu Yesu na hawataingia katika ufalme wake.

Frame 49-10

Kwa sababu ya dhambi yako, una hatia na unastahili kufa. Mungu anapaswa kuwa na hasira nawe, lakini alimwaga hasira yake kwa Yesu badala yetu. Wakati Yesu alipokufa msalabani, alipokea hukumu yako.

Frame 49-04

Pia alifundisha uhitaji wa kumpenda Mungu kuliko vitu vyote, pamoja na mali zako.

Frame 49-02

Yesu alifanya miujiza mingi kuthibitisha yeye ni Mungu. Alitembea katika maji, alizuia mawimbi, aliponya watu wengi, akatoa mapepo, akafufua wafu kua hai na akabadilisha vipande vya mikate mitano na samaki wawili kuwa chakula cha kutosha kwa watu 5000.

Frame 49-01

Malaika akamwambia bikira alieitwa Mariamu kuwa atazaa mtoto atakaekua mwana wa Mungu. Sasa wakati alipoendelea kuwa bikira, Roho Mtakatifu akamfunika na akapata ujauzito. Nae akazaa mtoto mwanamume na kumwita jina lake Yesu. Kwa hiyo Yesu ni Mungu na binadamu.

Frame 49-07

Yesu alifundisha kuwa Mungu anawapenda wenye dhambi sana. Anataka kuwasamehe wenye dhambi na kuwafanya kuwa watoto wake.

Frame 49-09

Lakini Mungu alimpenda kila mtu sana katika ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminiye Yesu hatahukumiwa kwa dhambi zake, lakini ataishi na Mungu milele.

Frame 49-14

Yesu anakualika umuamini yeye na uweze kubatizwa. Je unaamini Yesu ni Masiya, mwana wa pekee wa Mungu? Je unaamini wewe ni mwenye dhambi na unastahili Mungu akuhukumu? Je unaamini Yesu alikufa msalabani kuondoa mbali dhambi zako?

Frame 49-03

Pia Yesu alikua mwalimu mkuu, alizungumza kwa mamlaka kwa sababu alikua mwana wa Mungu. Alifundisha watu kua inahitajika kupenda watu wengine kama unavyojipenda mwenyewe.

Frame 49-11

Yesu hakuwai kufanya dhambi, lakini alikubali kuadhibiwa na kufa akiwa sadaka kamilifu kuondoa dhambi zako na dhambi za kila mtu katika ulimwengu. Kwa sababu Yesu alijitoa dhabihu mwenyewe. Mungu anaweza kusamehe dhambi yoyote, hata dhambi zenye kutisha.

Frame 49-16

Ikiwa ni mkristo, Mungu ameshakusamehe dhambi zako kwa sababu ya kile alichofanya Yesu kwa ajili yako. Sasa, angalia Mungu anakuona kuwa rafiki wa karibu badala ya adui.

Frame 49-18

Mungu anasema uombe, usome neno lake, umuabudu yeye na wakristo wengine, na kuwaambia wengine nini amefanya ndani yako. Mambo yote haya yanatusaidia kuwa na uwezo mpana wa ushirikiano na Mungu.

Frame 49-08

Yesu alituambia kuwa Mungu anachukia dhambi. Wakati Adamu na Hawa walivyofanya dhambi, iliharibu uzao wao wote. Na matokeo yake kila mtu duniani ana dhambi na ametenganishwa na Mungu. Na hata sasa, kila mtu amekua adui wa Mungu.

Frame 49-05

Yesu alisema ufalme wa Mungu ni wa thamani kuliko kitu chochote duniani. Kitu cha msingi ni kila mtu kuwemo kwenye Ufalme wa Mungu. Kuingia kwenye Ufalme wa Mungu, ni lazima uweze kuokolewa kutoka kwenye dhambi zako.

Simulizi ya Biblia kutoka: Warumi 3:21-26; 5:1-11; Yohana 3:16; Marko 16:16; Wakolosai 1:13-14; 2Wakorintho 5:17-21; 1Yohana 1:5-10

50. Yesu Anarudi

Frame 50-15

Wakati Yesu akirudi, atamwangamiza kabisa Shetani na ufalme wake. Atamtupa Shetani Jehanamu ambapo atachomwa milele, pamoja na kila mmoja aliyechagua kumfuata yeye badala ya kumtii Mungu.

Frame 50-17

Yesu na watu wake wataishi katika nchi mpya, na atatawala milele juu ya kila kitu kilichopo. Atafuta kila chozi na hapatakuwa tena na mateso, huzuni, kilio, uovu, maumivu, au kifo. Yesu atatawala katika ufalme wake kwa haki na amani, na atakuwa na watu wake milele.

Frame 50-12

Kisha wakristo watakaosalia hai watanyakuliwa juu katika mawingu na kuungana pamoja na wakristo waliofufuka kutoka wafu. Wote watakuwa pamoja na Yesu huko. Baada ya hapo, Yesu atakaa na watu wake katika amani timilifu na umoja wa milele.

Frame 50-13

Yesu aliahidi kuwapa taji kwa kila mtu amwaminiye yeye. Watakaa na kutawala pamoja na Mungu katika amani timilifu ya milele.

Frame 50-06

"Wakati mimea ilipoota, watumishi wa bwana walisema, 'Bwana, ulipanda mbegu njema katika shamba lile, Je, kwanini kuna magugu ndani yake?' Bwana akajibu, 'Lazima adui ameyapanda.'"

Frame 50-10

Wakati wa mwisho wa dunia, malaika watawakusanya pamoja watu wote walio wa milki ya Ibilisi na kuwatupa katika moto, mahali watakapolia na kusaga meno katika mateso ya kutisha. Kisha wenye haki watang'aa kama jua katika ufalme wa Mungu Baba yao."

Frame 50-04

Pia Yesu alisema, "Mtumwa si mkuu juu ya bwana wake. Kama ilivyo mamlaka ya dunia hii inavyonichukia mimi, watawatesa na kuwaua kwa sababu yangu. Ingawaje katika dunia hii mtateswa, iweni na ujasiri kwa sababu nimemshinda Shetani, ambaye anatawala dunia hii. Ikiwa mtabaki waaminifu kwangu hadi mwisho, kisha Mungu atawaokoa!"

Frame 50-02

Wakati tunamsubiri Yesu kurudi, Mungu anataka tuishi maisha ya utakatifu na ya kumweshimu. Tena anatutaka tuwaambie wengine habari za ufalme wake. Wakati Yesu alipokuwa akiishi duniani alisema, "Wanafunzi wangu wataihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu kwa watu wote ulimwenguni na ndipo mwisho utawadia."

Frame 50-01

Kwa zaidi ya miaka 2,000, zaidi na zaidi watu ulimwenguni kote wamekuwa wakisikia habari njema kuhusu Yesu Masihi. Kanisa limekuwa likikua. Yesu aliahidi angerudi mwisho wa dunia. Ingawa bado hajarudi, ataitimiza ahadi yake.

Frame 50-07

"Watumishi wakamjibu bwana wao, 'Je, tunaweza kuyang'oa magugu?' Bwana akasema, 'Hapana. Mkifanya hivyo, mtang'oa na ngano pamoja. Subirini hadi mavuno kisha mkusanye magugu katika matita na kuyateketeza kwa moto, bali muilete ngano gharani mwangu.'"

Frame 50-09

"Magugu yanawakilisha watu wa milki ya mwovu. Adui aliyepanda magugu anamwakilisha Ibilisi. Mavuno yanawakilisha mwisho wa dunia, na wavunaji wanawakilisha Malaika wa Mungu."

Frame 50-14

Lakini Mungu atamhukumu kila mmoja ambaye hakumwamini Yesu. Atawatupa wote jehanamu, mahali watakapolia na kusaga meno katika mateso ya milele. Moto usioweza kuzimika utaendelea kuwaunguza, na funza hawatakoma kuwatafuna.

Frame 50-03

Makundi ya watu wengi bado hawajasikia habari za Yesu. Kabla hajarudi mbinguni, Yesu aliwaambia wakristo kuitangaza habari njema kwa watu ambao kamwe hawajasikia. Alisema, "Enendeni na kufanya wanafunzi kwa watu wa makundi yote!" na "Mashamba yamekomaa kwa mavuno!"

Frame 50-11

Pia Yesu aliwaambia kwamba angerudi duniani kabla ya mwisho wa dunia. Atarudi kwa namna ilie ile alivyoondoka, kwa hali hiyo, atakuwa na mwili na atakuja na mawingu katika anga. Wakati Yesu akirudi, kila mkristo aliye kufa atafufuka kutoka wafu na kukutana naye mawinguni.

Frame 50-16

Kwa sababu Adamu na Eva walimwasi Mungu na kuleta dhambi humu ulimwenguni, Mungu aliilaani na kukusudia kuiangamiza. Lakini kuna siku Mungu ataumba mbingu mpya na nchi mpya itakayokuwa kamilifu.

Frame 50-08

Wanafunzi hawakufahamu maana ya simulizi, hivyo walimwomba Yesu awafafanulie. Yesu alisema, "Mtu aliyepanda mbegu njema anawakilisha Masihi. Na shamba linawakilisha ulimwengu. Mbegu njema inawakilisha watu wa ufalme wa Mungu.'"

Frame 50-05

Yesu aliwaambia wanafunzi wake simlizi juu ya namna itakavyotokea kwa watu wakati dunia itakapokwisha. Alisema, "Mtu alipanda mbegu njema katika shamba lake. Wakati alipokuwa amelala, adui yake alikuja na kupanda mbegu za magugu sambamba na ngano na kisha akaenda zake."

Simulizi ya Biblia Kutoka: Mathayo 24:14; 28:18; Yohana 15:20; 16:33; Ufunuo 2:10; Mathayo 13:24-30, 36-42; 1Wathesolanike 4:13-5:11; Yakobo 1:12; Mathayo 22:13; Ufunuo 20:10, 21:1-22:21

Simulizi Wazi za Biblia

__

Simulizi Wazi za Biblia

__