Swahili: Open Bible Stories

Updated ? hours ago # views See on DCS

1. Uumbaji

OBS Image

Hivi ndivyo mwanzo wa kila kitu ulivyotokea. Mungu aliumba ulimwengu na vitu vyote katika siku sita. Maana nchi ilikuwa giza na tupu, na hakuna kilichokuwa kimeumbwa. Lakini Roho ya Mungu ilikuwa juu ya maji.

OBS Image

Ndipo Mungu akasema, "Na iwe mwanga." Na ikawa hivyo, Mungu aliona kuwa mwanga ni mzuri na akauita mchana, na akatenganisha kutoka giza, akauita usiku. Mungu aliumba mwanga siku ya kwanza ya uumbaji.

OBS Image

Siku ya pili ya uumbaji, Mungu alisema na kuumba anga juu ya dunia. Aliumba anga kwa kutenganisha na maji ya juu kutoka maji ya chini.

OBS Image

Siku ya tatu, Mungu alisema na kutenganisha maji na nchi kavu. Nchi kavu akaiita "dunia," na maji akayaita "bahari." Mungu aliona kila kitu alichokiumba ya kuwa ni chema.

OBS Image

Ndipo Mungu akasema, "Nchi izae aina zote za miti na mimea." Na ndivyo ilivyotokea. Mungu aliona kila kitu alichokiumba ni chema.

OBS Image

Katika siku ya nne ya uumbaji, Mungu alisema na kuumba jua, mwezi na nyota. Mungu aliviumba ili kuleta mwanga duniani na kuonesha mchana na usiku, nyakati na miaka. Mungu aliona alichokiumba ni chema.

OBS Image

Siku ya tano, Mungu alisema na kuumba vitu vyote viishivyo majini na ndege wote. Mungu aliona kuwa ni vyema, na akavibariki.

OBS Image

Siku ya sita ya uumbaji, Mungu alisema, "Na iwe wanyama wa aina zote katika nchi." Na ilitokea kama Mungu alivyosema. Wengine walikuwa wa shambani, wengine wa kutambaa na wa porini. Na ilitokea kama yeye alivyotamka. Na Mungu aliona kwamba ilikuwa ni vyema.

OBS Image

Ndipo Mungu akasema, "Na tumfanye mtu kwa mfano wetu kuwa kama sisi. Watakuwa na mamlaka juu ya dunia na wanyama wote."

OBS Image

Mungu alichukua vumbi, akamfanya mtu, na akapulizia uhai ndani yake. Akamwita Adamu kwa jina lake. Akatengeneza bustani ya Edeni akamweka aishi humo, na aitunze.

OBS Image

Katikati ya bustani, Mungu alipanda miti miwili muhimu- mti wa uzima na wa ujuzi wa mema na mabaya. Mungu alimwambia Adamu anaweza kula aina zote za miti isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kama akila tunda la mti huu, atakufa.

OBS Image

Mungu alisema, "Si vyema mtu kuwa peke yake." Lakini hakuna hata mnyama mmoja aliyeweza kuwa msaidizi wa Adamu.

OBS Image

Ndipo Mungu alimletea Adamu usingizi mzito. Akatoa ubavu mmoja kwa Adamu na kutengeneza mwanamke na akamleta kwake.

OBS Image

Adamu alipomwona, alisema, "Angalau! Huyu ni kama mimi! Ataitwa 'mwanamke' maana ametoka kwa mwanaume." Kwa maana mwanaume atamwacha baba na mama yake watakuwa pamoja na mkewe.

OBS Image

Mungu aliumba mwanamke na mwanaume kwa mfano wake. Akawabariki akasema, "zaeni watoto na wajukuu mkaijaze dunia." Mungu aliona kila kitu alichokifanya ni chema sana, na alifurahishwa sana na kila kitu. Hii ilitokea katika siku ya sita ya uumbaji wake.

OBS Image

Siku ya saba ilipofika, Mungu alikuwa amemaliza kazi yake.Hivyo Mungu alipumzika katika kila alichokifanya. Aliibariki siku ya saba akaifanya takatifu kwa sababu katika siku hii alipumzika. Hivyo ndivyo Mungu alivyoumba ulimwengu na kila kitu ndani yake.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mwanzo 1-2