Kiswahili: translationWords

Updated ? hours ago # views See on DCS

Key Terms

Abudu

Ufafanuzi

"Kuabudu" ni kuheshimu, kusifu na kumtii mtu hasa Mungu.

  • Neno hili lina maana ya kawaida ya kuinama kumnyenyekea mtu.
  • Tunamwabudu Mungu tunapo muheshimu, kumsifu na kumtii yeye.
  • Waisraeli walimwabudu Mungu kwa kutoa sadaka ya wanyama kwenye madhabahu.
  • Watu wengine wanaabudu miungu ya uongo.

## Adili, uadilifu ### Ufafanuzi Adili au uadilifu ni wema wa Mungu, haki, uaminifu na upendo. Kwa sababu Mungu ni wa adili hukemea dhambi. * Maneno haya pia hutumika kumuelezea mtu anayemtii Mungu na mwenye maadili mema. Kwa sababu wote wametenda dhambi Mungu pekee ndiye mwenye adili. * Mfano wa watu waliokuwa waadilifu kwenye Biblia walikuwa Nuhu, Ayubu, Abrahamu, Zakaria na Elizabeti. * Watu wakimwamini Mungu awaokoe, Mungu anawasafisha na kuwafanya kuwa waadilifu katika uadilifu wa Yesu.
## Agano ### Ufafanuzi Agano ni makubaliano kati ya pande mbili kuwa upande mmoja au zote unapaswa kutekeleza. * Makubaliano haya yanaweza kuwa ya mmoja mmoja, kati ya makundi ya watu au kati ya Mungu na watu. * Watu wanapoweka agano kati yao wanaahidi kufanya jambpo fulani ambalo wanapaswa wafanye. * Mfano wa maagano ya wanadamu ni maagano ya ndoa, makubaliano ya biashara na mikataba kati ya nchi. * Katika Biblia Mungu ameweka maagano mbalimbali na watu wake. * Katika baadhi ya maagano Mungu aliahidi kutekeleza bila masharti yoyote. Kwa mfano Mungu alipoweka agano na mwanadamu kuwa hataiangamiza duinia kwa mafuriko. * Katika maagano mengine Mungu ameahidi kutekeleza kama watu watamtii yeye.
## Ahadi ### Ufafanuzi Ahadi ni hali ya kuahidi kufanya jambo fulani. Mtu anapokuahidi kitu inamaana yupo tayari kufanya jambo hilo. * Biblia imeandika ahadi nyingi ambazo Mungu aliahidi watu wake. * Ahadi ni sehemu muhimu ya makubaliano kama maagano. * Ahadi mara nyingi huambatana na kiapo cha kuthibitisha kuwa itafanyika.
## Aliye Juu ### Ufafanuzi Neno "Aliye Juu" ni cheo cha Mungu. kina husu ukuu wake au mamlaka. * Maana ya hili neno ni sawa na "Ukuu" * Neno "juu" katika hichi cheo halihusu urefu wa kimwili au umbali. Lina husu ukuu.
## Aliyechaguliwa, chagua, watu waliochaguliwa, Aliyechaguliwa, Mteule ### Ufafanuzi Msemo, "wateule" una maana ya "waliochaguliwa" au "watu waliochaguliwa" na una maana ya wale ambao Mungu amewateua au chagua kuwa watu wake. "Aliyechaguliwa" au "Aliyechaguliwa na Mungu" ni jina ambalo lina maana ya Yesu, ambaye ni Masihi aliyechaguliwa. Msemo "chagua" una maana ya kuchagua kitu au mtu au kuamua jambo. Mara kwa mara hutumika kumaanisha Mungu kuteua watu wawe wake na wamtumikie. "Kuchaguliwa" ina maana ya "kuchaguliwa" au "kuteuliwa" kuwa au kufanya jambo. Mungu alichagua watu kuwa wasafi, kutengwa kando na yeye kwa kusudi la kuzaa matunda mema ya kiroho. Hiyo ni sababu kwa nini wanaitwa "wateule" au "waliochaguliwa". Msemo "aliyechaguliwa" hutumika mara nyingine katika Biblia kumaanisha baadhi ya watu kama Musa na Mfalme Daudi ambao Mungu aliwateua kama viongozi wa watu wake. Pia inatumika kumaanisha taifa la Israeli kama watu waliochaguliwa na Mungu. Msemo "wateule" ni msemo wa zamani ambao humaanisha "waliochaguliwa" au "watu waliochaguliwa". Msemo huu katika lugha asili ni wingi inapomaanisha waumini wa Kristo. Katika tafsiri za Biblia ya Kingereza za zamani, msemo "mteule" unatumika pote katika Agano la Kale na Jipya kutafsiri neno kwa ajili ya "waliochaguliwa". Tafsiri zaidi za kisasa hutumia "mteule" katika Agano Jipya pekee, kumaanisha watu ambao wameokolewa na Mungu kupitia imani kwa Yesu. Kwingineko katika Biblia, wanatafsiri neno hili kwa uwazi zaidi kama "waliochaguliwa". Mapendekezo ya Tafsiri Ni bora kutafsiri "mteule" kwa neno au msemo ambao una maana ya "waliochaguliwa" au "watu waliochaguliwa". Hizi zinaweza kutafsiriwa kama "watu ambao Mungu amechagua" au "wale ambao Mungu ameteua kuwa watu wake". Msemo, "ambao wamechaguliwa" unaweza kutafsiriwa kama "ambao wameteuliwa" au "ambao waliteuliwa" au "ambao Mungu amewachagua". "Ninakuchagua" inaweza kutafsiriwa kama, "ninakuteua" au "ninakuchagua". Kwa kulinganisha na Yesu, "Aliyeteuliwa" inaweza pia kutafsiriwa kama, "Aliyechaguliwa na Mungu" au "Masihi aliyeteuliwa mahsusi na Mungu" au "Yule ambaye Mungu alimteua"
## Amina, kweli ### Ufafanuzi Neno "Amina" hutumika kusisitiza au kuweka mkazo jambo ambalo mtu amesema. Mara nyingi hutumika mwisho wa sala. Mara nyingine hutafsiriwa kama "kweli." * Ikitumika mwisho wa sala, "amina" inaonesha kukubaliana na maombi au kuelezea shauku ya kutimizwa kwa maombi yale. * Katika mafundisho yake, Yesu alitumia neno "Amina" kusisitiza ukweli wa alichokisema. Mara nyinyi aliunganisha kwa kutumia " nawaambia ninyi" katika kutambulisha mafundisho mengine ambayo yaliendana na mafundisho yaliyopita. * Maana nyingine ya "kweli" yaweza kutafsiriwa kama "hakika" na pia hutumika kusisitiza jambo ambalo msemaji analisema.
## amri, kuamuru ### Ufafanuzi Kuamuru ni kutoa amri kwa mtu afanye jambo fulani. Amri ni jambo ambalo mtu ameamriwa afanye. * Japokuwa maneno haya yana maana inayofanana amri mara nyingi ni inamaanisha amri za Mungu ambazo ni "amri kumi." * Amri yaweza kuwa nzuri chanya kama "waheshimu wazazi wako" au hasi kama "usiibe." * Kuwa na amri inamaanisha "kuamuru" kitu au mtu.
## Batiza, ubatizo ### Ufafanuzi Katika Agano Jipya, maneno "batiza" na "ubatizo" kwa kawaida utaratibu wa kuoshwa kwa Mkiristo kwa kutumia maji kuonesha kwamba ameoshwa kutoka katika dhambi na ameungana na Kristo. * Mbali na ubatizo wa maji, Biblia inazungumzia "kubatizwa kwa Roho Mtakatifu" na "kubatizwa kwa moto." * Neno "ubatizo" katika Biblia limetumika pia kuonesha hali ya kupitia matiso makubwa. ### Maono ya Kutafasiri * Wakristo wanamaoni tofauti jinsi mtu anavyopaswa kubatizwa kwa maji. Pengine inafaa zaidi kutafasiri neno hili kwa njia ya jumla inayoruhusu njia mbalimbali ya kutumia maji. * Kwa kutegemea mazingira, neno "batiza" laweza kutafasiriwa kama "kutakasa," "kumimina juu, "kuzamisha"
## baya, ovu, uovu ### Ufafanuzi Msemo "baya" na "uovu" yote ina maana ya chochote ambacho kinapingana na tabia takatifu na mapenzi ya Mungu. Wakati "ubaya" unaweza kuelezea tabia ya mtu, "ovu" unaweza kumaanisha zaidi ya tabia ya mtu. Hata hivyo, misemo yote inafanana maana. Msemo "uovu" una maana ya hali ambayo watu hufanya maovu. Matokeo ya uovu yanaonywesha kwa uwazi kwa jinsi watu wanavyotenda vibaya wengine kwa kuwaua, kuiba, kusengenya au kuwa katili na kutokuwa mwema. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, misemo "uovu" na "ovu" inaweza kutafsiriwa kama "ubaya" au "dhambi" au "kinyume na maadili". Njia zingine za kutafsiri hii zinaweza kujumuisha "isiyo nzuri" au "sio takatifu" au "sio adilifu". Hakikisha maneno au misemo ambayo inatumika kutafsiri misemo hii kutosha muktadha ambayo ni kawaida katika lugha husika.
## Bila mawaa ### Ufafanuzi Neno "bila mawaa" kwa kawaida linamaanisha "bila lawama". Linatumika kumtaja mtu anayemtii Mungu kwa moyo wake wote, lakini haimaanisha kwamba hana dhambi. * Ibrahimu na Nuhu walihesabiwa kutokuwa na lawama mbele za Mungu. * Mtu mwenye heshima ya kuwa "bila lawama" anaenenda kwa namna inayomweshimu Mungu. * Kwa mjibu wa msitari mmoja, mtu asiye na lawama ni "yule anayemcha Mungu na kujiepusha na uovu." ### Maoni ya Ufasiri * Hii pia yaweza kutafasiriwa kama, "asiye na kasoro katika mwenendo wake" au "mwenye kumtii Mungu kikamilifu" au "kujiepusha na dhambi" au "kujilinda na uovu.
## Binti Sayuni ### Ufafanuzi "Binti Sayuni" ni njia ya kitamathali inayomaanisha watu wa Israeli. Inatumika haswa katika unabii. Katika Agano la Kale, "Sayuni" hutumika sana kama jina jingine la mji wa Yerusalemu. "Sayuni" na "Yerusalemu" zote zina maana ya Israeli. Msemo "Binti" ni msemo wa ubembelezi au mapenzi. Ni sitiari ya uvumilivu na utunzaji ambao Mungu anao kwa watu wake. Mapendekezo ya Tafsiri Njia za kutafsiri hili yaweza kuwa, "binti yangu wa Israeli, kutoka Sayuni" au "watu kutoka Sayuni, ambao ni kama binti kwangu" au "Sayuni, watu wangu wapendwa Israeli". Ni vyema kubaki na msemo "Sayuni" katika usemi huu kwa maana unatumika mara nyingi katika Biblia. Maandishi yanaweza kuwekwa katika tafsiri kuelezea maana yake ya kitamathali na matumizi ya kinabii. Ni bora kukaa na msemo "Binti" katika tafsiri ya usemi huu, ikiwa inaeleweka kwa sahihi.
## Busara, hekima ### Ufafanuzi Busara inamuelezea mtu anayeelewa jambo la haki na mambo ya maadili na akayafanya. Hekima ni uelewa na kutenda yaliyo sahihi na maadili ya haki. * Kuwa na busara inajumuisha uwezo wa kufanya maamuzi mazuri hasa kuchagua kufanya yanayompendeza Mungu. * Katika Biblia "busara za dunia" inamaanisha kitu ambacho watu wa dunia wanafikiri ni burasa lakini ni upuuzi. * Watu huwa na busara wanapomsikiliza Mungu na kunyeyekea kutii mapenzi yake. * Mtu mwenye busara ataonesha matunda ya roho mtakatifu kwenye maisha yake kama furaha, upendo na uvumilivu.
## Bwana wa Majeshi, Mungu wa majeshi, Majeshi ### Ufafanuzi Bwana wa majeshi ay Mungu wa majeshi ni vyeo vinavyoelezea mamlaka ya Mungu juu ya malaika maelfu wanaomtii yeye. * Majeshi linaelezea idadi kubwa ya vitu kama vile jeshi au idadi kubwa ya nyota. Pia yaweza kuwa na maana ya viumbe vyote vya kiroho ikiwemo roho wachafu. * Majeshi ya mbinguni ni nyota zote, sayari na vitu vingine vilivyoko mbinguni. * Katika agano jipya Bwana wa majeshi inamaanisha "Yaweh wa majeshi" lakini haiwezi kutafsiriwa hivyo kwa sababu neno la Kiebrania Yaweh halijatumika kwenye agano jipya.
## Bwana Yahwe, Yahwe Mungu ### Ufafanuzi Katika Agano la Kale, "Bwana Yahwe" inatumika mara kwa mara kumaanisha Mungu mmoja wa kweli. Neno "Bwana" ni cheo cha Mungu na "Yahwe" ni jina la Mungu mwenyewe. "Yahwe" mara nyingi huunganishwa na neno "Mungu" kuunda "Yahwe Mungu."
## bwana, mkuu ### Ufafanuzi Neno "bwana" linamaanisha mtu anayemiliki na mwenye mamlaka juu ya watu wengine. Neno hili wakati mwingine linatafsiriwa kama "mkuu" wakati wakumuita Yesu au wakati wakumaanisha mtu anayemiliki watumwa.
## chakula cha Bwana ### Ufafanuzi Msemo "Chakula cha Bwana" unatumika na mtume Paulo kumaanisha mlo wa Pasaka ambao Yesu alikula na wanafunzi wake usiku alipokamatwa na viongozi wa Kiyahudi. Katika mlo huu, Yesu aliuvunja mkate wa Pasaka katika vipande na kuuita mwili wake ambao punde utapigwa na kuuliwa pia. Aliita kikombe cha divai damu yake, ambayo itamwagwa hapo punde atakapokufa kama sadaka ya dhambi. Yesu aliamuru kila mara wafuasi wake wanapokula mlo huu pamoja, wanapaswa kukumbuka kifo chake na ufufuo. Katika barua yake kwa Wakorintho, mtume Paulo aliendeleza kuimarisha zaidi chakula cha Bwana kama zoezi la mara kwa mara la waumini wa Yesu. Makanisa siku hizi husema "ushirika" kumaanisha chakula cha Bwana. Usemi "Meza ya Bwana" hutumika wakati mwingine.
## Chukizo, mbaya ### Ufafanuzi Neno "chukizo" hutumika kuelezea jambo linalosababisha karahaau chuki iliyokithiri. Wamisri waliwaona Waebrania kama "chukizo." Hii ina maana kuwa Wamisri waliwachukia Waebrania na hawakutaka kushirikiana nao au kuwa karibu nao. Vitu ambavyo Biblia imeviona kama "Chukizo kwa Yahweh" ni; uongo, kujivuna, kafara za binadamu, kuua na dhambi za zinaa kama uzinzi na matendo ya zinaa kinyume na maumbile. Katika kuwafundisha wanafunzi wake kuhusu siku za mwisho, Yesu anarejea unabii wa nabii Danieli kuhusu "chukizo la uharibifu" kwamba itakuwa kama uasi dhidi ya Mungu, Kuchafua sehemu yake ya kuabudia.
## damu ### Ufafanuzi Neno "damu" linamaanisha kimiminika chekundu kinachotoka katika ngozi ya mtu panapokuwa na jeraha au kidonda. Damu inaleta viini lishe vya uhai katika mwili wote wa mtu. * Damu inaashiria uhai na inapomwagwa, inaashiria kifo. * Watu walipotoa sadaka kwa Mungu, walimwua mnyama na kumimina damu yake juu ya madhabahu. Hii inaashiria kutolewa kwa uhai wa mnyama kulipa dhambi za watu. * Kupitia kifo chake msalabani, Damu ya Yesu hutakasa watu kutokana na dhambi zao na kulipa kwa ajili ya adhabu wanayostahili kwa ajili ya dhambi zao. * Kifungu "mwili na damu" kinarejerea wanadamu. * Kifungu "mwili wake na damu yake" inarejerea kwa watu wanaohusiana kibaolojia. ### Maoni ya Kutafasiri * Neno hili litumika kwa kulingana na neno lifaalo katika lugha lengwa. * Kielezi "mwili na damu" chaweza kutafasiriwa kama "watu" au "wanadamu". * Kwa kutegemea mazingira, kifungu "mwili wangu na damu yangu mwenyewe" yaweza kutafasiriwa kama "familia yangu" au "ndugu zangu" au "watu wangu." * Ikiwa kuna kionyeshi katika lugha lengwa kinachotumika kwa maana hii, kifungu hicho kitumike kutafasiri "mwili na damu"
## dhambi,yenye dhambi, mwenye dhambi, kufanya dhambi ### Ufafanuzi Neno "dhambi" la husu matendo, mawazo, na maneno yaliyo kinyume dhidi ya mapenzi ya Mungu na Sheria. Dhambi yaweza maanisha kutofanya kitu Mungu alicho tuambia tufanye. * Dhambi ya jumuisha chochote tunacho fanya kisicho mtii au mpendeza Mungu, ata vitu watu wasivyo vijua. * Mawazo na matendo yanayo kosea mapenzi ya Mungu yanaitwa "yenye dhambi" * Kwasababu Adamu alitenda dhambi, wanadamu wote wanazaliwa na hasili ya dhambi inayo watawala. * "mwenye dhambi" ni mtu anaye tenda dhambi, hivyo kila mwanadamu ni mwenye dhambi. * Wakati mwingine neno "mwenye dhambi" lilitumika na watu wa dini kama Mafarisayo kueleza watu wasio shika sheria.
## Dhamira ### Ufafanuzi Dhamira ni sehemu ya fikra za mwanadamu ambazo Mungu anamfanya atambue kuwa anafanya dhambi. * Mungu amewapa watu dhamira ili awasaidie wafahamu tofauti kati ya mema na mabaya. * Mtu anayemtii Mungu ana dhamira safi. * Mtu akiwa na dhamira safi inamaana kuwa hafichi dhambi yoyote. * Mtu anayedharau dhamira yake na hajisikii kuhukumiwa anapofanya dhambi inamaana kuwa dhamira yake haishituki kwa mabaya.
## Dunia, kidunia ### Ufafanuzi Dunia ni sehemu ya ulimwengu ambapo watu wanaishi ndani yake. Kidunia inaelezea maadili na tabia mbaya za watu wanaoishi kwenye hii dunia. * Dunia inajumuisha mbingu, nchi na vyote vilivyopo ndani yake. * Katika sehemu nyingi "dunia" inamanisha watu wa duniani. * Mara nyingine inaelezea kuwa watu waovu wa duniani au watu wasiomtii Mungu. * Mitumi waliotumia "dunia" walielezea tabia za ubinafsi za watu wanaoishi kwenye dunia hii. * Watu au vitu wenye tabia hizi waliitwa wa kidunia.
## fadhila, yenye kufaa, upendeleo ### Ufafanuzi Msemo "fadhila" una maana ya kufanya jambo kumnufaisha mtu ambaye anachukuliwa ki chanya. Kitu ambacho "kinafaa" ni chanya, kinakubalika, au kina manufaa. Msemo "upendeleo" ina maana ya kutenda kwa upendeleo kwa baadhi ya watu lakini sio wengine kuonyeshwa kwa watu ambao ni matajiri au wanafikiriwa. Yesu alikua "kwa fadhila za" Mungu na wanadamu. Hii ina maana walimkubali silika na tabia yake . Msemo "kupata fadhila" ina maana ya kwamba mtu anakubalika na mtu mwingine. Mfalme anapoonyesha upendeleo kwa mtu, mara nyingi humaanisha anakubali maombi ya huyo mtu na kumpatia. Mapendekezo ya Tafsiri Njia zingine za kutafsiri msemo "fadhila" zinawvza kujumuisha "baraka" au "faida". "Mwaka wa baraka wa Yahwe" unaweza kutafsiriwa kama "mwaka
## Farisayo. ### Ufafanuzi Mafarisayo walikuwa watu wa muhimu sana, kundi la watu lenye nguvula dini ya Kiyahudi katika nyakati za Yesu. * Wengi wao walikuwa katika daraja la kati la wafanyabiashara na wengine walikuwa makuhani. * Katika viongozi wote wa Kiyahudi Mafarisayo walikuwa wakitii kwa nguvu sheria ya Musa na sheria nyingine za Kiyahudi na tamaduni. * Walikuwa makini sana katika kuwatenga Wayahudi toka kwenye ushawishi wa Mataifa yanayowazunguka. Neno "Farisayo" linatokana na neno "kutenganisha" * Mafarisayo wanaamini kuna maisha baada ya kifo pia wanaamini kuwepo kwa malaika na viumbe wengine wa kiroho. * Mafarisayo na Masadukayo walimpinga Yesu na kanisa la kwanza.
## Fidia ### Ufafanuzi Fidia ni kiasi cha pesa au malipo mengine yanayohitajika kwa ajili ya kumuachia mtu aliyefungwa. * "Kutoa fidia" ni kufanya malipo au kutoa kitu ili kumkomboa mtu aliyepo kifungoni au utumwani. * Yesu alikubali kuuawa kama fidia ya kuwaweka huru wenye dhambi toka kwenye utumwa wa dhambi. Hiki kitendo cha Mungu kuwanunua watu wake ki kitendo cha ukombozi.
## funga ### Ufafanuzi Neno "funga" linamaanisha kukaza kitu kwa usalama. Kitu kilichofungwa au kuunganishwa pamoja kinaitwa "muungano". Neno "kufunga" ni sehemu ya neno hili katika wakati uliopita. * "Kufungwa" inamaanisha kufunga au kuzonga katika kitu kingine. * Katika hali ya tamathari, mtu anaweza "kufungwa" katika nadhiri, kumaanisha "analazimika kutimiza" alichokiahidi. * Neno "vifungo" linamaanisha chochote kinachofunga, "weka pamoja, au kumweka mtu gerezani. Kwa kawaida inamaanisha vifungo vya kimwili, pingu au kamba zinazomfanya mtu asiwe huru kuondoka alipo. * Katika nyakati za Biblia, vifungo kama vile kamba au minyororo ilitumika kumfunga mfungwa katika ukuta au chini ya jiwe la gereza. * Neno "funga" laweza pia kutumika kuzungumzia kufunga kidonda kwa kitambaa ili kukisaidia kupona. * Mfu aweza "kuzongwa" kwa sanda katika maandalio ya mazishi. * Neno "kifungo" hutumika kitamathari kurejerea kitu fulani, kama vile dhambi, inayomwongoza au kumfanya mtumwa. * Kifungu chaweza kuwa uhusiano wa karibu kati ya watu ambao wanasaidiana kihisia, kiroho na kimwili. Hii inatumika katika kifungo cha ndoa. * Kwa mfano, mwanamke na mwanamme "wamefunwa" au "kuunganishwa. Ni kifungo ambacho Mungu hapendi kivunjike. ### Maoni ya Tafasiri Neno "funga" laweza pia kutafasiriwa kama "kaza" au "zungushia"
## ghadhabu, hasira ### Ufafanuzi Ghadabu ni hasira kali ambayo mara nyingine hudumu kwa mda mrefu. Hii maranyingi huelezea hukumu ya Mungu ya haki na adhabu ya watu walioasi dhidi yake. * Katika Biblia "ghadhabu" ni hasira ya Mungu juu ya wao wanaomtenda dhambi. * Ghadhabu ya Mungu ni hukumu na adhabu ya dhambi. * Ghadhabu ya Mungu ni adhabu ya haki kwa wale wasiotubu dhambi zao.
## habari njema, injili ### Ufafanuzi Msemo "injili" una maana ya "habari njema" na una maana ya ujumbe au tangazo ambalo linawaambia watu jambo ambalo lina manufaa kwako na kuwapa furaha. Katika Biblia, msemo huu humaanisha ujumbe kuhusu wokovu wa Mungu kwa watu kupitia sadaka ya Yesu msalabani. Katika Biblia nyingi za Kiingereza, "habari njema" mara nyingi hutafsiriwa kama "injili" na pia hutumika katika misemo kama vile "injili ya Yesu Kristo" au "injili ya Mungu" na "injili ya ufalme". Mapendekezo ya Tafsiri Njia tofauti za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "jumbe mzuri" au "tangazo zuri" au "ujumbe wa Mungu wa wokovu" au "mambo mazuri Mungu anayofundisha kuhusu Yesu". Kulingana na muktadha, njia za kutafsiri msemo "habari njema ya" inaweza kujumuisha "ujumbe/havbari njema" au "ujumbe mzuri kutoka" au "mambo mazuri Mungu husema juu ya" au "kile Mungu anasema kuhusu jinsi anavyookoa watu".
## Haki ya uzaliwa ### Ufafanuzi ## Neno "haki ya uzaliwa" inamaanisha heshima katika Biblia, jina la familia, na mali iliyokuwa ikitolewa kwa mzaliwa wa kwanza katika familia. * Haki ya mzaliwa wa kwanza ilijumuisha mara mbili katika urithi wa baba. * Mwana wa kwanza wa mfalme kwa kawaida alipewa haki ya uzaliwa ya kurithi baada ya kifo cha baba yake. * Esau aliuza haki ya uzaliwa kwa Yakobo mdogo wake, kwa sababu hii, Yakobo alirithi baraka ya mzaliwa wa kwanza badala ya Esau. * Haki ya kuzaliwa pia ilihusisha kuhesabiwa kwa vizazi vya familia kupitia mzaliwa wa kwanza. ### Maoni ya Kutafasiri. * Njia iwezekanayo kutafasiri "haki ya kuzaliwa" ni pamoja na "haki na utajiri wa mzaliwa wa kwanza" au "heshima ya familia" au "faida na urithi wa mzaliwa wa kwanza."
## haki, adilifu ### Ufafanuzi Maneno haya yanamaanisha kuwatendea watu vyema kulingana na sheria za Mungu. Sheria za binadamu zinazo onesha kiwango cha Mungu cha tabia sawa kwa watu wengine. Kuwa wa "haki" ni kutenda ya haki na mema kwa mtu mwingine. Pia inaashiria uaminifu na msimamo kufanya kilicho adilifu machoni pa Mungu. Kutenda kwa "haki" inamaanisha kuwatendea watu kwa njia iliyo sawa, nzuri na ya kufaa kulingana na sheria za Mungu. Kupokea "haki" inamaanisha kutendewa vyema chini ya sheria, aidha kulindwa kwa sheria au kuadhibiwa kwa kuvunja sheria. Wakati mwingine neno "haki" lina maana pana ya "utakatifu"au "kufuata sheria za Mungu."
## hatia, mwenye hatia ### Ufafanuzi Msemo "hatia" una maana ya ukweli wa kufanya dhambi au kutenda kosa. Kuwa na "hatia" ina maana ya kuwa umefanya kitu kiouvu kimaadili, yaani, kutomtii Mungu. Kinyume cha "mwenye hatia" ni "asiye na hatia". Mapendekezo ya Tafsiri Baadhi ya lugha zinaweza kutafsiri "hatia" kama "uzito wa dhambi" au "hesabu ya dhambi". Njia za kutafsiri "kuwa na hatia" inaweza kujumuisha neno au msemo ambayo ina maana ya "kuwa katika kosa" au "kuwa umefanya jambo ovu kimaadili" au "kuwa umefanya dhambi".
## hekalu ### Ufafanuzi Hekalu lilikuwa ni jengo lililo zungukwa na kuta za nyuani ambapo Waisraeli walikuja kuombaa na kutoa dhabihu kwa Mungu. Lilikuwa Mlima Moria katika mji wa Yerusalemu. * Mara nyingi neno "hekalu" lina husu jengo zima, pamoja na nyuani iliyo zunguka jengo lote. Wakati mwingine lina husu tu jengo. * Jengo la hekalu lilikuwa na vyumba viwili, Pa Takatifu na Pa Takatifu pa Pa Takatifu. * Mungu alitaja hekalu kama sehemu yake ya kuishi. * Wakati wa utawala wa Mfalme Sulemani alijenga Hekalu, ambalo lilikuwa sehemu ya kudumu ya kuabudu Yerusalemu. * Katika Agano Jipya, neno "hakalu la Roho Mtakatifu" linatumika kuelezea waamini wa Yeu, kwasababu ya Roho Mtakatifu kuishi ndani yao.
## heshima, kuheshimu ### Ufafanuzi Istilahi 'heshima' na 'kuheshimu' hurejelea kitendo cha kumpa mtu heshima au kumstahi mtu. Heshima mara kwa mara hutolewa kwa mtu mwenye hadhi ya juu na umuhimu wa juu kama vile mfalme au Mungu. Mungu pia huwaagiza Wakristo wote kuwaheshimu watu wengine, lakini si kutafuta heshima zao wenyewe. Watoto wameagizwa kuwatii wazazi wao na kuwatii. Maneno kama 'heshima' na 'utukufu' ni maneno yanayoenda kwa pamoja hasa yanapomrejelea Yesu. Heshima kwa Mungu inajumuisha kumshukuru na kumsifu Mungu, na kuonesha heshima kwa kumtii Mungu na kuishi katika njia inayoonesha kuwa Mungu ni Mkuu. Mapendekezo Njia nyingine za kutafsiri neno 'heshima' linajumuisha 'staha' Neno 'kuheshimu' laweza kutafsiriwa kama 'kuonesha heshima maalumu kwa au kuonesha mtu thamani ya juu.
## hukumu ### Ufafanuzi Neno "hukumu" mara nyingi humaanisha kufanya maamuzi kama jambo liko sawa kimaadili au kama haliko sawa. "Hukumu ya Mungu" mara nyingi humaanisha uamuzi wake kulaani kitu au mtu muovu. Hukumu ya Mungu mara nyingi huhusisha kuwaadhibu watu kwa dhambi zao. Neno "hukumu" inaweza pia kumaanisha "kulaani." Mungu anawaagiza watu wake kutowahukumu wengine kwa naamna hii. Maana nyingine ni "uamuzi kati ya" au "kuhukumu kati ya", yaani kuchagua ni mtu gani yuko sahihi katika ugomvi kati yao. Katika mazingira mengine, "hukumu" za Mungu ni yale aliyeamua ni mema na yenye haki. Zinafanana na amri, sheria na maagizo yake. "Hukumu" inaweza kumaanisha uwezo wa busara wa kufanya maamuzi. Mtu anayekosa "hukumu" hana hekima kufanya maamuzi ya busara.
## Huruma ### Ufafanuzi Huruma ni hisia za kujali wengine hasa wanaoteseka. Pia huruma ni kujali wengine na kuwasaidia. * Huruma pia inajumuisha kuwajali wenye uhitaji na kuchukua hatua ya kuwasaidia. * Biblia inasema Mungu ni wa huruma, ana upendo na rehema tele. * Katika barua ya Paulo kwa Wakolosai anawaambia "wajivike huruma." Anawaagiza wawajali watu na wawasaidie wenye uhitaji.
## imani ### Ufafanuzi Kwa ujumla, msemo "imani" una maana ya imani, au matumaini ndani ya mtu au jambo. "Kuwa na imani" na mtu ni kuamini ya kwamba kile anachosema na kufanya ni kweli na kuaminika. "Kuwa na imani na Yesu" ina maana ya kuamini mafundisho yote ya Mungu kuhusu Yesu. Ina maana haswa ya kwamba watu wanamuamini Yesu na sadaka yake kuwasafisha kutoka kwa dhambi zao na kuwakomboa kutoka na adhabu wanayostahili kwa sababu ya dhambi yao. Imani ya kweli kwa Yesu itamsababisha mtu kuzaa matunda mazuri ya kiroho au tabia kwa sababu ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani yake. Mara kwa mara "imani" kwa ujumla ina maana ya mafundisho yote kuhusu Yesu, yaani kama msemo, "ukweli wa imani". Katika muktadha kama wa "tunza imani" au "telekeza imani", msemo "imani" una maana ya hali ya kuamini mafundisho yote kuhusu Yesu. Mapendekezo ya Tafsiri Katika baadhi ya muktadha, "imani" inaweza kutafsiriwa kama "imani" au "hatia" au "kujiamini" au "kuamini". Kwa baadhi ya lugha misemo hii inaweza kutafsiriwa kutumia aina za kitenzi cha "imani".
## imani, aminifu, ### Ufafanuzi Neno "imani" la eleza kuamini kwamba kitu au mtu ni wa kweli au tegemeo. Mtu "mwaminifu" na weza kuwa tegemevu kufanya kitu na kusema kilicho sawa na kweli. * Imani ni ina maana ya karibu na imani ya Mungu. Kama tuna mwamini mtu, tuna imani kwamba mtu huyo atafanya alicho ahidi. * Kuwa na imani kwa mtu pia ina maana ya kumtegemea huyo mtu. * Kumuamini Yesu ina maana ya kukubali kuwa yeye ni Mungu na kwamba alikufa kwenye msalaba kulipa dhambi zetu, na kumtegemea kutuokoa. * "msemo aminifu" ni kitu kilicho semwa na kinaweza hesabiwa kuwa kweli.
## ingia bila ruhusa ### Ufafanuzi "Ingia bila ruhusa" ina maana ya kuvunja sheria au kukosea haki za mtu mwingine. * Ingia bila ruhusa ni kosa la kijamii au la kisheria au dhambi iliyo tendwa dhidi ya mwingine. * Huu msemo una maana ya "dhambi," haswa kwa kumkosea Mungu. * Dhambi zote ni kosa kwa Mungu
## ishara, kithibitisho, ukumbusho ### Ufafanuzi Ishara ni kitu, tukio, au kitendo kinacho wasilisha maana maalumu. * Ishara zinaweza kuwa kumbusho cha kitu kilicho ahaidiwa. * Upinde wa mvua Mungu aliyo uumba kwenye anga ulikuwa ni ishara ya kuwa kumbusha watu kwamba hataharibu maisha ya watu kwa gharika. * Mungu aliamuru Waisraeli kutairi wana wao kama ishara ya agano lake kwao. * Ishara zinaweza dhihirisha au kuelekeza kwa kitu. * Malaika aliwambia wachungaji ishara itakayo wasaidia wao mtoto yupi Bethilehemu ndiye mzaliwa Mesiya mpaya. * Yuda alimbusu Yesu kama ishara kwa viongozi wa kidini kwamba Yesu ndiye wamkamate. * Ishara yaweza thibitisha kwamba kitu ni kweli. * Miujiza iliyo fanywa na manabii na mitume ilikuwa ishara iliyo thibitisha walikuwa wanazungumza ujumbe wa Mungu. * Miujiza Yesu aliyo tenda ilikuwa ishara kuwa yeye ndiye Mesiya.
## Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli ### Ufafanuzi Neno "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Linamaanisha, "anashindana na Mungu." Uzao wa Yakobo walijulikana kama "watu wa Israeli," "taifa la Israeli" au "Waisraeli." Mungu aliunda agano lake na watu wa Israeli. Walikuwa watu wake aliowachagua. Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mbili. Mara baada ya mfalme Sulemani kufa, Israeli iligawanyika katika falme mbili: ufalme wa kusini, uliitwa "Yuda" na ufalme wa kaskazini, uliitwa "Israeli."
## Jehanamu, ziwa la moto ### Ufafanuzi Jehanamu ni sehemu ya mwisho iliyo na maumivu na mateso yasiyokoma, mahali ambapo Mungu atamhukumu kila mmoja anayemwasi Yeye na kuukataa mpango wake wa kuwaokoa kupitia kwa sadaka ya Yesu. Pia inarejelewa kama 'ziwa la moto. Jehanamu au Kuzimu kunatajwa kama sehemu ya moto na mateso makali. Shetani na roho chafu zinazomfuata zitatupwa katika Jehanamu kwa ajli ya hukumu ya milele. Watu wasioamini sadaka ya Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao, na wasiomtumaini Yeye, watahukumiwa Jehanamu milele Mapendekezo ya tafsiri Maneno haya yanapaswa kutafsiriwa tofauti tofuauti kwasababu yanatokea tofauti katika muktadaha tofauti. Katika baadhi ya lugha haziwezi kutumia neno 'ziwa' kwa sababu kwao ziwa ni 'maji' Neno Jehanamu laweza kutafsiriwa kama 'sehemu ya mateso au sehemu yenye giza na maumivu' Maneno 'ziwa la moto' yanaweza pia kutafsiriwa kama 'bahari ya moto' au 'moto mkubwa.'
## Jemadari ### Ufafanuzi Jemadari ni afisa wa jeshi la Rumi aliyekuwa na kundi la askari 100 juni ya amri yake. * Hii pia inaweza kutafsiriwa kama "kiongozi wa watu mia" au "kiongozi wa jeshi." * Jemadari mmoja wa Rumi alikwenda kwa Yesu akamwomba amponye mtumishi wake. * Jemadari aliyekuwa akihusika kumsulubisha Yesu alishangazwa kwa namna ambavyo Yesu alikufa. * Mungu alimtuma jemadari kwa Petro ili Petro amuelezee habari njema juu ya Yesu.
## jina ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "jina" linatumika kwa mifano kadhaa. * Katika muktadha kadhaa, "jina" la weza eleza tabia ya mtu, kama, "tujifanyie jina letu" * Neno "jina" pia laweza husu kumbukumbu ya kitu. Kwa mfano, "katilia majina ya sanamu" ina maana kuharibu hizo sanamu ili zisikumbukwe au kuabudiwa. * Kuzungumza "katika jina la Mungu" ina maana ya kuongea kwa nguvu zake na mamlaka, au kama mwakilishi. * "Jina" la mtu laweza husu mtu wote, kama "hakuna jina lingine chini ya jua ambalo twapaswa kuokolewa."
## Jiwe la pembeni ### Ufafanuzi "Jiwe la pembeni" ni jiwe kubwa mabalo limekatwa na kuwekwa katika kona ya msingi wa jengo. * Mawe yote ya jengo hupimwa na kuwekwa kutokana na jiwe la pembeni. * Ni la muhimu sana kwa uwezo na ustahimili wa jengo zima. * Katika agano jipya kusanyiko la waamini linafananishwa na jengo ambalo Yesu Kristo ndiye jiwe la pembeni. * Katika namna hiyo hiyo ambayo jiwe la pembeni linashikilia na kuweka msingi wa jengo zima hivyo Yesu Kristo ni jiwe la pembeni ambalo waamini wanajitegemeza kwake.
## jiwe, kupiga jiwe ### Ufafanuzi Jiwe ni mwamba mdogo. Neno "kupiga jiwe" la husu kurusha mawe na majabali makubwa kwa mtu kuweza kumuua. * Wakati wa Kale, kupiga mawe ilikuwa namna iliyo zoeleka ya kuua watu kama adhabu kwa makosa waliyo fanya. * Mungu aliamuru viongozi wa Israeli kupiga mawe watu kwa dhambi kadhaa, kama uasherati. * Agano Jipya ina eleza wakati Yesu alipo samehe mwanamke aliya kamatwa katika uasherati na kuzuia watu kumtupia mawe.
## Kanisa ### Ufafanuzi Katika agano jipya kanisa ni kundi la watu wanaomwamini Yesu wanaokutana na kuomba pamoja na kusikiliza mafundisho ya Mungu. * Yaweza kuwa na maana ya watu walioitwa kukutana pamoja kwa ajili ya jambo la muhimu. * Neno hili linapotumika linamaanisha waamini wote popote ni mwili wa Kristo, Baadhi ya Biblia zimeandika kwa kuanza na herufi kubwa ("Kanisa") Kutofautisha na kanisa la kawaida. * Mara nyingine waamini wa mji fulani hukutana katika nyumba ya mtu. Makanisa haya yalipewa majina ya miji mfano "Kanisa la Efeso." * Katika Biblia kanisa halimaanishi jengo.
## katika Kristo, katika Yesu, katika Bwana, katika yeye ### Ufafanuzi Usemi "katika Kristo" na maneno ya kukaribiana yanamaanisha hali ya kuwa na uhusiano na Yesu Kristo kwa imani katika yeye. Maneno mengine ya kukaribiana ni pamoja na, "katika Kristo Yesu, katika Yesu Kristo, katika Bwana Yesu, katika Bwana Yesu Kristo." Maana zinazowezekana kwa ajili ya maneno "katika Kristo" yanaweza kuwa pamoja na, "kwa sababu wewe ni wa Kristo" au "katika uhusiano ulionao na Kristo" au "kutokana na imani yako katika Kristo." Maneno haya ya kukaribiana yote yana maana sawa ya kuwa katika hali ya kumuamini Yesu na kuwa mwanafuzi wake. Noti: Wakati mwingine neno "katika" lina paswa kuwa na kitenzi. Kwa mfano, "gawana katika Kristo" inamaana "kugawana katika" faida zinazokuja kwa kumjua kristo. "Kusifu katika" Kristo inamaana kuwa na furaha na kutoa sifa kwa Mungu ambavyo Yesu alivyo na alichofanya. "Kuamini katika" Kristo inamaanisha kumuamini yeye kama Mwokozi na kumjua.
## kazi, vitendo, matendo ### Ufafanuzi Katika Biblia maneno kazi, vitendo, matendo ni vitu ambavyo Mungu au watu hufanya. * Neno kazi linamaana ya kufanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia watu wengine. * Kazi ya Mungu na kazi ya mikono yake ni kazi zote anazzozifanya ikiwemo kuumba dunia, kuokoa wenye dhambi, kuwapatia mahitaji wale aliowaumba. Matendo ni miujiza ya Mungu kama "matendo makuu." * Matendo anayofanya mwanadamu yaweza kuwa mazuri au mabaya. * Roho mtakatifu anatatia nguvu waamini kufanya kazi njema ambazo huitwa "matunda mema." * Watu hawaokolewi kwa kazi zao nzuri bali kwa imani yao kwa Yesu.
## Kiapo ### Ufafanuzi Kiapo ni ahadi ambayo mtu anaiweka kwa Mungu. Mtu anaahidi kufanya jambo fulani kwa ajili ya kumuheshimu Mungu na kuonesha ibada kwake. * Baada ya mtu kufanya kiapo anapaswa atekeleze kiapo kile. * Biblia inatufundisha kuwa mtu anaweza kuhukumiwa na Mungu asipitimiza kiapo chake. * Mara nyingine mtu anaweza kumuomba Mungu amlinde au amfanyie jambo fulani na akaweka kiapo kwa Mungu. Lakini Mungu hatakiwi kutimiza ombo la mtu aliloomba katika kiapo.
## kicho, uchaji ### Ufafanuzi ## Maneno "kicho" na "uchaji" yanamaanisha kujitoa kwa nguvu zote kumuunga mkono mtu au wazo. * Kicho inahusisha tamaa kubwa na matendo yanayoimiza jambo jema. Mara kwa mara inatumika kumwelezea mtu ambaye kwa uaminifu anamtii Mungu na kuwafundisha wengine kufanya hivyo pia. * Uchaji unahusisha kuweka bidii kubwa katika kufanya jambo na kuendelea katika bidii hiyo. * "Kicho cha Bwana" au "kicho cha Yahwe" yarejerea matendo ya Mungu yenye nguvu na endelevu katika kuwabariki watu wake au kuona haki ikitendeka. ### Maoni ya Ufasiri * Kuwa "mchaji" yaweza pia kufasiriwa, "kuwa na bidii kubwa" au kufanya jitihada "zaidi." * Neno "kicho" laweza pia kufasiriwa kama "uchaji wa ndani" au "maamuzi ya kina" au "hamu ya haki." * Kirai, "kicho cha nyumba yako" yaweza kufasiriwa, "kuliheshimu sana hekalu lako" au "tamaa ya kuitunza nyumba yako."
## Kipatanisho ### Ufafanuzi "Kipatanisho" ni sadaka inayotolewa ili kutimiza haki ya Mungu au kutuliza hasira yake. * Sadaka ya damu ya Yesu ni upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. * Kifo cha Yesu msalabani kimetuliza hasira ya MUNGU dhidi ya dhambi. Hii imetengeneza njia ya Mungu kuwaangalia wanadamu na kuwahurumia na kuwapatia uzima wa milele.
## Kristo, Masihi ### Ufafanuzi Masihi na Kristo inamaana ya mpakwa mafuta na inamuelezea Yesu mwana wa Mungu. * Masihi na Kristo vimetumika katika agano jipya kumuelezea mwana wa Mungu ambaye Mungu baba alimpaka mafuta kutawala kama mfalme juu ya watu wake na kuwaokoa toka kwenye dhambi. * Katika agano la kale manabii waliandika unabii juu ya Masihi miaka mia kabla ya kuja kwake duniani. * Neno mpakwa mafuta limetumika katika agano la kale kumuelezea Masihi atakayekuja. * Yesu alitimiza unabii huo na alifanya miujiza mingi iliyothibitisha kuwa yeye ni Masihi, unabii uliobaki utatimia atakaporudi. * Neno Kristo hutumika kama jina "Kristo Yesu."
## Kuamini, kuamini katika ### Ufafanuzi ## Neno "kuamini" na "kuamini katika" yanahusiana kwa karibu, lakini yana maana tofauti: ### Maoni ya Kutafasiri * "Kuamini" laweza kutafasiriwa kama "kujua kuwa ni kweli" au "Jua kuwa sawa." * "Kuwa na imani" laweza kufasiriwa kama "kuamini kikamilifu" au "kuamini na Kutii" au "kutegemea kwa ukamilifu na kufuata."
## Kuasili ### Ufafanuzi Neno "kuasili" ni hatua za kisheria za mtoto kuwa na wazazi fulani ambao sio wazazi wake wa kumzaa. * Biblia imetumia "kuasili" kuelezea namna ambavyo Mungu alivyosababisha watu kuwa sehemu ya familia yake, kuwafanya watu wawe watoto wake wa kiroho. * Watoto walioasiliwa pamoja na waamini ni warithi pamoja na Yesu Kristo wakiwa na haki zote kama wana wa Mungu.
## Kubariki ### Ufafanuzi "kubariki" mtu au kitu maana yake ni kusababisha mema na mambo ya manufaa kufanyika kwa mtu au kitu kinachobarikiwa. * Kumbariki mtu pia inamaanisha kuonesha nia chanya na vitu vyenye manufaa kumpata mtu huyo. * Katika nyakati za Biblia, kwa kawaida baba alitamka baraka maalumu kwa wanawe. * Watu "wanapombariki" Mungu au kuonesha hamu ya kuwa Mungu abarikiwe, inamaanisha wanamwinua. * Neno "baraka" wakati mwingine linatumika kwa kukitakasa chakula kabla hakijaliwa, au kwa kumshukuru na kumsifu Mungu kwa ajili ya chakula. //kutokana na maoni hapa chini: Ni mhimu kutoa maana, lengo, au kuzingatia matumizi ya mzizi wa neno "bariki" ambalo kimsingi linapendekea kustawi au kuwa na wingi wa vitu au utajiri. Kwa kuzingatia wingi wa mafundisho ya kimaandiko juu ya upendo wa Mungu, rehema na neema ambayo siyo ya kale tu bali hata sasa. Kwa kuzingatia uangalizi, ulinzi, na uwepo wa Roho wa Mungu. Na kwa ajili yetu kumbariki Mungu, kwa kutoa shukurani, kuthamini, na kuelewa kama tunavyojifunza na kumfuata(kumtii)// ### Maoni ya Kutafasiri * "Kubariki" kwaweza kutafasiriwa kama "kuandaa kwa wingi" au "kuwa mwema ." * "Mungu ameleta baraka kuu" ifasiriwe kama "Mungu ametoa mambo mengi mema kwa" au "Mungu ametoa kwa wingi kwa ajiri" au "Mungu amesababisha Mambo mema kutokea kwa". * "Amebarikiwa" ifasiriwe kama "atanufaika sana" au "atapitia mambo mema" au "Mungu atamfanya kustawi". * "Amebarikiwa mtu yule" yaweza kutafasiriwa kama "Ni vema kiasi gani kwa mtu ambaye". * Vioneshi kama vile, "abarikiwe Bwana" yaweza kutafasiriwa kama, "na asifiwe Bwana" au "Bwana asifiwe" au "Ninamtukuza Bwana". * Katika mazingira ya kubariki chakula, hii yaweza kutafasiriwa kama, "alimshukuru Mungu kwa ajili ya chakula" au "alimshukuru Mungu kwa kuwapa chakula" au "alikitakasa chakula kwa kumsifu Mungu.
## Kuchaguliwa tangu asili ### Ufafanuzi Kuchaguliwa tangu asili nikitendo cha kuamua au kupanga kabla ya jambo hilo kutokea. * Neno hili linamuelezea Mungu aliwachagua watu kupokea uzima wa milele. * Mara nyingine neno "kuteuliwa" hutumika likuwa na maana ya kuamua kabla.
## kuhani mkuu ### Ufafanuzi Neno 'kuhani mkuu' hurejelea kuhani maalumu aliyekuwa ameteuliwa kutumika kwa mwaka mmoja kama kiongozi wa makuhani wote wa Wayahudi. Kuhani mkuu alikuwa na majukuu mahususi. Alikuwa ni mtu pekee aliyeruhusiwa kuingia mahali patakatifu sana katika hekalu ili kutoa sadaka maalumu mara moja kwa mwaka. Waisraeli walikuwa na makuhani wengi sana, lakini walikuwa na kuhani mkuu mmoja kwa muda fulani. Kipindi alichokamatwa Yesu, Kayafa alikuwa kuhani mkuu. Anasi, Baba mkwe wa Kayafa anatajwa mara kadhaa kwasababu alikuwa kuhani mkuu hapo awali, huenda alikuwa bado na mamlaka na nguvu fulani juu ya watu. Mapendekezo ya tafsiri 'Kuhani mkuu" tunaweza kutafsiri kama "kuhani wa daraja la juu"
## Kuhani, ukuhani ### Ufafanuzi Katika Biblia Kuhani alikuwa mtu aliyechaguliwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu kwa niaba ya watu wa Mungu. Ukuhani lilikuwa jina au masharti ya kuwa kuhani. * Katika agano la kale Mungu alimchagua Haruni na uzao wake kuwa makuhani wa Israeli. * Ukuhani ilikuwa haki na majukumu yaliyorithishwa toka kwa baba kwenda kwa mtoto katika kabila ka Lawi. * Makuhani wa Israeli walikuwa na jukumu la kutoa sadaka za watu kwa Mungu pamoja na kazi nyingine katika hekalu. * Makuhani pia walitoa maombi kwa Mungu kawa niaba ya watu wake na kufanya kazi nyingine za kidini. * Makuhani walitangaza baraka kwa watu na kuwafundisha sheria za Mungu. * Katika wakati wa Yesu kulikuwa na ngazi mbalimbali za makuhani kama Makuhani Wakuu na Kuhani mkuu. * Yesu ni kuhani wetu mkuu anayetuombea mbele za Mungu. Alijitoa mwenyewe kama sadaka kwa dhambi zetu. * Katika agano jipya hata anayemwamini Mungu ni kuhani ambaye anaweza kwenda moja kwa moja kwa Mungu kwa njia ya maombi kujiombea mwenyewe na kuombea watu wengine. * Hapo kale kulikuwa pia na makuhani wa kipagani walioleta sadaka kwa miungu ya uongo kama Baali.
## Kuhukumu, hukumu ### Ufafanuzi "Kuhukumu" au "hukumu" ni kitendo cha kumpa mtu kumhukumu mtu baada ya kufanya jambo baya. * Maranyingine kuhukumu inamaanaisha kumshitaki mtu au kumhukumu vibaya mtu. * Hukumu ni kitendo cha kuhukumu au kumshitaki mtu.
## kujaribu, jaribu ### Ufafanuzi Kumjaribu mtu ni kufanya huyo mtu kufanya kitu kibaya. * Jaribu ni kitu kinacho sababisha mtu kutaka kufanya kitu kibaya. * Watu wanajaribiwa kwa dhambi zao na kwa watu wengine. * Shetani pia anajaribu watu kutomtii Mungu na kufanya dhambi dhidi ya Mungu na kwa kufanya vitu vibaya. * Shetani alimjaribu Yesu na kumtaka afanye kitu kibaya, lakini Yesu alizuia majaribu yote ya Shetani na hakutenda dhambi.
## kujazwa kwa Roho ### Ufafanuzi Msemo "kujazwa kwa Roho" ni msemo wa kitamathali ambao una maana ya Roho Mtakatifu kumwezesha kufanya mapenzi ya Mungu. Msemo "kujazwa na" ni msemo ambao hutumika mara kwa mara kumaanisha "kutawalwa na". Watu "wanajazwa na Roho" wanapofuata uongozi wa Roho Mtakatifu na kumtegemea kabisa kuwasaidia kufanya kile Mungu anachotaka. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "kuwezeshwa na Roho Mtakatifu" au "kutawaliwa na Roho Mtakatifu". Lakini haitakiwi kuonekana kana kwamba Roho Mtakatifu analazimisha mtu kufanya kitu. Sentensi kama "alijazwa na Roho" inaweza kutafsiriwa kama "alikuwa akiishi kikamilifu kwa nguvu ya Roho" au "Roho Mtakatifu alikuwa akimuongoza kikamilifu". Msemo huu ni sawa kwa maana na msemo "kuishi kwa Roho" lakini "kujazwa na Roho" inasisitiza ukamilifu ambao mtu huruhusu Roho Mtakatifu kuwa na utawala au ushawishi juu ya maisha yake. Kwa hiyo misemo hii miwili inatakiwa kutafsiriwa tofauti, ikiwezekana.
## Kujivuna ### Ufafanuzi Neno "kujivuna" humaaanisha kuongea kwa kiburi kuhusu mtu au kitu. Mara kwa mara inamaanisha kujivuna mwenyewe. * Mtu "mwenye majivuno" anajiongelea kwa njia ya kiburi. * Mungu aliwakemea Waisraeli kwa "kujivunia" sanamu zao. Kwa ujinga waliabudu miungu badala ya Mungu wa kweli. * Biblia inazungumzia pia watu wajivunao utajiri wao, nguvu, mashamba yenye rutuba, na sharia zao. Hii inamaanisha kwamba walijivunia vitu hivi hata awakumtambua Mungu awapaye vitu hivyo. * Mungu aliwaamru badala yake "wajivune" kwa sababu wanamfahamu yeye. * Mtume Paulo, pia alizungumzia kuhusu kujivuna katika Bwana, kumaanisha kufurahi na kumshukuru Mungu kwa yote aliyowafanyia. ### Maoni ya Tafasiri * Njia nyingine ya kutafasiri "majivuno" inahusisha "kuongea kwa kiburi" au kuwa na kiburi." * Neno "enye kujivuna" yaweza kutafasiriwa kwa kifungu kimaanishacho, "mwenye kujazwa na maneno ya kiburi" au "enye kiburi" au "kuongea kwa kiburi kuhusu mwenyewe." * Katika mazingira ya kujivuna katika au kuhusu Mungu, yaweza kufasiriwa kama "kujivunia" au "kujisifu katika" au kuwa na furaha kuhusu" au "kumshukuru Mungu kwa ajili ya". * Baadhi ya lugha zina maneno mawili kwa ajili ya "kiburi": moja ni hasi lenye maana mbaya, na lingine lenye maana nzuri, lenye maana ya kujivunia kazi , familia, au nchi.
## Kukiri ### Ufafanuzi Kukiri inamaana ya kukubali kuwa jambo fulani ni la kweli. Kukiri ni kauli ya kuwa kitu fulani ni kweli. * Kukiri pia yaweza kuwa na maana ya kusema ukweli kuhusu Mungu. Pia yaweza kuonesha kukubali kuwa sisi ni wenye dhambi. * Biblia inasema watu wakikiri dhambi zao kwa Mungu atawasamehe. * Mtume Yakobo aliandika kwenye barua yake kuwa waamini wakikiri dhambi zao wao wenyewe inawaletea uponyaji wa kiroho. * Mtume Paulo aliwaandikia Wafilipi kuwa siku moja kila mtu atakiri kuwa Yesu ni Bwana. * Paulo pia anasema watu wakikiri kuwa Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Mungu alimfufua toka kwa wafu wataokolewa.
## kukomboa, ukombozi, mkombozi ### Ufafanuzi "Kukomboa" au "ukombozi" ni kununua kitu kilichokuwa kinamilikiwa hapo mwanzo au kilichochukuliwa mateka. "Mkombozi" ni mtu anayekikomboa kitu au mtu. * Mungu alitoa sheria kwa Waisraeli kuhusu kukomboa watu wau vitu. * Kwa mfano mtu anaweza kumkomboa mtu aliyekuwa utumwani kwa kumlipia kiasi ambacho mtumwa yule atakuwa huru. * Kama ardhi ya mtu imeuzwa, ndugu wa yule mtu anaweza kuikomboa au kuinunua tena ardhi ile ili ibaki kwenye familia. * Tendo hili linaonesha namna ambavyo Mungu aliwakomboa watu wake toka kwenye utumwa wa dhambi. Yesu alipokufa msalabani alilipia dhambi za watu nakukomboa watu wote wanaoamini ukombozi wake. Watu waliokombolewa na Mungu wapo huru toka kwenye dhambi na adhabu.
## Kumkufuru ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "kufuru" inamaanisha kuzungumza kwa njia ambayo inaonesha dharau kubwa kwa Mungu au watu. "Kumkufuru" mtu ni kuongea kinyume cha mtu huyo ili watu wafikiri vibaya juu ya mtu huyo. * Mara nyingi, kumkufuru Mungu humaanisha kumtukana kwa kusema mambo ambayo siyo kweli kuhusu yeye au kwa kuenenda kwa njia isiyo na maadili hata kumvunjia heshima. * Ni kufuru kwa mwanadamu kudai kuwa Mungu au kudai kwamba kuna Mungu mwingine zaidi ya Mungu wa kweli. * Baadhi ya matoleo mengine yanatafasiri neno hili kama "kumtukana" linaporejerea kuwakufuru watu. ### Maoni ya Tafasiri * "Kukufuru" kwaweza kutafasiriwa kama, "kusema vibaya dhidi ya" au "kumdharau Mungu" au "kumtukana". * Jinsi ya kutafasiri "kufuru" ni pamoja na. "kusema vibaya kuhusu wengine" au "kutukana" au "kusambaza tetesi za uongo."
## Kumtia mafuta ### Ufafanuzi "Kumtia mafuta" ina maana ya kupaka au kummiminia mafuta mtu au kitu. Mara nyingine mafuta haya huchanganywa na viungo ambavyo huleta ladha au harufu ya manukato. Pia hutumika kama lugha ya picha kuonesha namna ambavyo Roho Mtakatifu anawachagua watu na kuwatia nguvu. * Katika agano la kale makuhani, wafalme na manabii walipakwa mafuta ili kuwatenga kwa ajili ya kazi maalumu ya kumtumikia Mungu. * Vitu kama madhabahu na hema vilipakwa mafuta kuonesha kuwa vilitakiwa kutumika kwa ajili ya kumuabudu Mungu na kumtukuza yeye. * Katika agano jipya mara mbili Yesu anapakwa mafuta ya manukato na mwanamke kama tendo la kumuabudu. Sehemu moja Yesu alionesha kuwa kwa kufanya hivyo yule mwanamke alikuwa akimuandaa kwa ajili ya maziko yake. * Baada ya Yesu kufan rafiki zake waliuandaa mwwili wa Yesu kwa ajili ya maziko kwa kuupaka mafuta na manukato. * Neno "Masihi" au "Kristo" lina maana ya mpakwa mafuta.
## Kuomba, maombi ### Ufafanuzi "Maombi" au "kuomba" ni kitendo cha kuongea na Mungu. Neno hili pia laweza kutumika kama kitendo cha watu kujaribu kuongea na miungu ya uongo. * Mtu anaweza kuomba taratibu, kuzungumza na Mungu katika mawazo au kuomba kwa nguvu kuzungunza na Mungu kwa sauti. Mra nyingine maombi huandikwa mfano kama Daudi alipoandika maombi yake katika kitabu cha Zaburi. * Mambi yanaweza kujumuisha kumuomba Mungu rehema, msaada kwa tatizo fulani au hekima ya kufanya maamuzi. * Mara nyingine watu humuomba Mungu awaponye wagonjwa au wanaohitaji msaada wake. * Pia watu hushukuru na kumsifu Mungu katika maombi. * Maombi yanajumuisha kukiri dhambi zetu na kumuomba Mungu atusamehe. * Kuongea na Mungu huitwa kunong'onezana naye roho zetu zikiwa na mazungumzo na roho yake na kufurahia uwepo wake. * Hii inaweza kutafsiriwa kama kuzungumza na Mungu au kuwasiliana na Mungu.
## Kupatanisha, maridhiano ### Ufafanuzi Kupatanisha na maridhiano ni kutengeneza amani kati ya watu waliokuwa maadui. * Katika Biblia neno hili linamuelezea Mungu kuwapatanisha watu na yeye mwenyewe kwa kumtoa mwana wake Yesu Kristo. * Kwa sababu ya dhambi watu wote ni adui wa Mungu. Lakini kwa sababu ya upendo wake Mungu anatoa njia ya watu kupatanishwa naye kupitia Yesu. * Kwa kuamini kujitoa kwa Yesu kama malipo ya dhambi zao watu wanaweza kusamehewa na kuwa na amani na Mungu.
## Kupotea, kuharibika ### Ufafanuzi "Kupotea" inamaanisha kufa au kuharibiwa maranyingi huwa ni baada ya mapigano au majanga. Katika Biblia inamaana zaidi ya kuhukumiwa milele jehanamu. * Watu waliopotea ni wale wanaoenda jehanamu kwa sababu walikataa kumwamini Yesu kwa ajili ya wokovu wao. * Yohana 3:16 inatufundisha "kupotea" ni kutokuishi milele mbinguni.
## Kurejesha, marejesho ### Ufafanuzi Kurejesha au marejesho ni kusababisha kitu kirudi katika uhalisia wake au katika hali nzuri. * Mwili wa mgonjwa unaporejeshwa inamaana kuwa unaponywa. * Mahusiana yaliyovunjika yakirejeshwa inakuwa kitendo cha kurudiana. Mungu huwarejesha wenye dhambi na kuwarudisha kwake. * Watu wakirejeshwa kwenye nchi zao inamaana "wanarudishwa" kwenye nchi hizo.
## kutenga ### Ufafanuzi Neno "kutenga" lina maana ya kutengwa kutoka kwenye kitu kutimiza aina ya kusudi. * Waisraeli walitengwa kwa huduma ya Mungu. * Roho Mtakatifu aliamuru Wakristo wa Antioki kumtenga Paulo na Barnabas kwa kazi Mungu aliyo taka wafanye. * Muamini aliye "tengwa" kwa kazi ya Mungu "ametolewa kutimiza" kazi ya Mungu. * Maana moja ya neno "takatifu" ni kutenga kama kuwa wa Mungu na kutengwa na dhambi za dunia.
## Kuteua, Kuteuliwa ### Ufafanuzi "Kuteua au kuteuliwa" linamaana ya kumchagua mtu ili aikamilishe kazi fulani. * Kuteuliwa pia inaweza kuwa kuchaguliwa ili kupokea kitu fulani. kuteuliwa kwenye uzima wa milele hii inamaanisha walichaguliwa kupokea uzima wa milele. * Neno "wakati ulioteuliwa" ina maana ya wakati ambao Mungu amepanga kufanya jambo fulani. * Neno "kuteua" pia laweza kuwa na maana ya kuamuru, kumpa mtu kazi fulani ya kufanya.
## kutokuwa na imani, upotofu wa imani ### Ufafanuzi Msemo "kutokuwa na imani" una maana ya kutokuwa na imani au kutoamini. Neno hili linatumika kuelezea watu ambao hawamuamini Mungu, ambayo inaonekana kwa njia ya chafu wanayofanya. Nabii Yeremia alimshtaki Israeli kwa kutokuwa na imani na kutomtii Mungu. Waliabudi sanamu na kufuata tamaduni zinginge ambazo si za kiungu za kundi la watu ambao hawakumwabudu au kumtii Mungu. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, msemo "kutokuwa na imani" unaweza kutafsiriwa kama "upotofu wa uaminifu" au "kutoamini" au "kutomtii Mungu". Msemo "upotofu wa imani" unaweza kutafsiriwa kama "ukosefu wa imani" au "uasi dhidi ya Mungu"
## Kutubu, toba ### Ufafanuzi Kutubu na toba ni hali ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu. * "Kutubu" ni hali ya kubadili nia ya mtu. * Katika Biblia "kutubu" inamaanisha kuacha dhambi, namna ya kufikiri kibinadamu na kutenda na kumrudia Mungu na njia zake na matendo yake. * Watu wanapotubu kabisa dhambi zao, Mungu anawasamehe na kuwasaidia kuanza kumtii.
## Kuwa na mapepo ### Ufafanuzi Mtu ambaye ana mapepo ana pepo au roho chafu ambalo humuongoza kile afanyacho au kufikiri. Mara kwa mara mtu mwenye pepo hujiumiza mwenyewe au watu wengine kwa sababu peopo husababisha afanye hivyo. Yesu aliponya watu waliokuwa na mapepo kwa kuwaamuru mapeopo kuwatoka . Hii mara kwa mara hujulikana kama "kutoa" mapepo. Mapendekezo ya Tafsiri Njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha, "kutawaliwa na pepo" au "kutawaliwa na roho mchafu" au "kuwa na roho mchafu aishiye ndani".
## Kuzaliwa upya, kuzaliwa na Mungu, kuzaliwa kwa roho ### Ufafanuzi Neno "kuzaliwa upya" lilitumiwa mara ya kwanza na Yesu kuelezea maana ya Mungu kumbadilisha mtu kutoka kuwa mfu kiroho na kuwa hai kiroho. Neno "kuzaliwa na Mungu" na "kuzaliwa kwa roho" pia hurejerea hali ya mtu kupewa uzima mpya kiroho. * Watu wote wanazaliwa wafu kiroho na wanapewa "kuzaliwa upya" wanapomwamini Yesu Kristo kama mwokozi wao. * Katika wakati wa kuzaliwa upya kiroho, Roho wa Mungu uanza kuishi ndani ya muumini mpya na kumtia nguvu ili azae matunda mema ya kiroho katika maisha yake. * Ni kazi ya Mungu kumfanya mtu kuzaliwa upya na kuwa mwana wake. ### Maoni ya Tafasiri * Njia nyingine ya kutafasiri "kuzaliwa tena" inahusisha, "kuzaliwa upya" au "kuzaliwa kiroho." * Ni vizuri kutafasiri neno hili katika maana ya kawaida na kutumia neno la kawaida katika lugha litumikalo kwa kuzaliwa. * Neno "uzao mpya" laweza kutafasiriwa kama "kuzaliwa kiroho." * Kirai "liyezaliwa na Mungu" laweza kutafasiriwa kama "kufanywa na Mungu kuwa na uzima mpya kama mtoto aliyezaliwa upya au "kupewa uzima mpya na Mungu." * Kwa njia ileile, "amewezeshwa na Roho Mtakatifu kuwa mtoto wa Mungu" au "kufanywa na Roho kuwa na uzima mpya kama mtoto mchanga."
## kuzimu ### Ufafanuzi katika Biblia kuna maneno mawili yametumika, neno la Kiebrania 'sheol' na neno la Kigriki 'hades.' Maneno haya yametumika katika Biblia kumaanisha kifo na sehemu ambako roho za watu waliokufa huenda. katika Kiebrania neno 'sheol' limetumika katika Agano la Kale kurejelea sehemu ya watu waliokufa au sehemu ya kifo. katika agano jipya, neno la Kigriki 'hades" limetumika kumaanisha sehemu ya roho za watu waliomwasi Mungu. Roho hizi hurejelewa kama zinaenda "chini." Wakati mwingine linaweza kutofautishwa na 'kwenda juu' mbinguni mahali ambako roho za watu za watu wanaomwamini Yesu zinaishi. Mapendekezo ya tafsiri Katika Agano la Kale neno "sheol" linaweza kutafsiriwa kama " sehemu ya wafu" au "sehemu kwa ajli ya roho za wafu" Baadhi ya tafsiri hufasiri neno hili kama "shimo" au "kifo" kwa kutegemea na muktadha. Neno "hades" limetumika sana katika Agano Jipya ambalo laweza kutafsiriwa kama "sehemu kwa ajili ya roho za wafu za watu wasioamini" au " sehemu ya mateso na adhabu ya kwa roho za wafu wasioamini." Baadhi ya tafsiri hutunza neno ''sheol" au ''Hades'' kwa kutumia herufi ambazo zinakubaliana katika mfumo wa sauti wa lugha husika. kwa kiswahili twaweza kusema 'sheoli" na 'hadesi'
## kweli, ukweli, kuwa kweli ### Ufafanuzi Maneno "kweli" na "ukweli" yana eleza mambo ambyo ni halisi, matukio yaliyo tukia, na maneno yaliyo semwa. * Vitu vya kweli ni halisi, thabiti, uhakika, sawasawa, halali. * Ukweli ni ufahamu, uamini, uhalisia, au maneno yaliyo kweli. * Msemo kuwa "kuwa kweli" au "kuja kuwa kweli" ni msemo unao maanisha kuwa unabii ulitokea hakika kama iliyo tabirika kuwa itakuwa. * Ukweli una jumuisha maelezo ya kutenda kwa namna iliyo tegemevu na aminifu. * Yesu alidhihirisha ukweli wa Mungu katika maneno aliyo zungumza. * Neno la Mungu ni kweli. Lina eleza vitu vilivyo tokea na kufundisha yaliyo kweli kuhusu Mungu na kuhusu kila kitu alicho fanya.
## Laana, kulaaniwa ### Ufafanuzi Laana ni kusababisha mambo mabaya yatokee kwa mtu au kitu kilicholaaniwa. * Laana yaweza kuwa kauli ya kusababisha madhara yatokee kwa mtu au vitu. * Kumlaani mtu ni kutamani mabaya yatokee kwake. * Pia inaweza kuwa adhabu au mambo mabaya ambayo mtu amesababisha yatokee kwa mtu.
## liwali ### Ufafanuzi Neno "liwali" la eleza afisa wa serikali aliye tawala sehemu ya Serikali ya Rumi. Kila liwali alikuwa chini ya mamlaka ya mfalme mkuu wa Kirumi. * Cheo "liwali" lina maana "mmoja wa watawala wa nne waliyo ungana." * Kwa kuanza na Mfalme Mkuu Diokletia, kulikuwa na migawanyiko minne ya Serikali ya Kirumi na kila liwali alitawala mmoja. * Ufalme wa Herode "Mkuu", aliye kuwa mfalme wa kipindi cha kuzaliwa kwa Yesu. * Kila mgawanyiko ulikuwa na moja au zaidi ya "mikoa" midogo, kama Galilaya au Samaria. * "Herode liwali" anatajwa mara kadhaa katika Agano Jipya. Pia ujulikana kama "Herode Antipasi."
## Mabaki ### Ufafanuzi Mabaki ni watu au vitu vilivyosalia toka kwenye kundi kubwa. * Mabaki mara nyingi huwa watu walioishi baada ya maisha yao kuwa mashakani au waliobaki kuwa waaminifu kwa mungu wakati wakipitia mateso. * Isaya anazungumzia kundi la Wayahudi kama mabaki ya waliosalia baada ya mashambulizi toka kwa watu wa nje na kurudi katika nchi ya Kanaani. * Paulo anazungumza kuhusu kuwa "mabaki" ya watu waliochaguliwa na Mungu kupokea rehema yake. * Neno "Mabaki" inaonesha kuwa kuwa watu wengine ambao hawakuwa waaminifu na hawakusalia au hawakuchaguliwa.
## Madhabahu ### Ufafanuzi Madhabahu ilikuwa sehemu yenye muundo ulioinuka ambao wana wa Israeli walichoma wanyama na mazao kama sadaka kwa Mungu. * Katika nyakati za Biblia madhabahu rahisi zilikuwa zinatengenezwa kwa kilima chenye udongo au mawe makubwa yaliyopangwa na kupafanya pawe imara. * Madhabahu nyingine zilitengenezwa kwa mbao pamoja na dhahabu na shaba. * Watu wengine walioishi karibu na Israeli walitengeneza pia madhabahu na kutoa sadaka kwa miungu yao.
## mahali takatifu ### Ufafanuzi Neno "mahali takatifu" ya husu sehemu ambayo Mungu amefanya takatifu. Inaweza maanisha eneo linalo toa ulinzi na usalama. * Katika Agano la Kale, neno "mahali takatifu" mara nyingi lilitumika kueleza maskani au hekalu ambapo "patakatifu" na "patakatifu pa patakafitu" kulikuwepo. * Mungu alitaja mahali takatifu kama sehemu aliyo ishi miongoni mwa watu wake, Waisraeli. * Pia alijiita "mahali takatifu" au sehemu salama watu wake wanaweza pata ulinzi.
## maisha, uhai, kuishi, kuwa hai ### Ufafanuzi Maneno haya yote yanamaanisha kuwa hai kimwili, sio kufa. Yanatumika pia kimafumbo kumaanisha kuwa hai kiroho. Yanayofuata yanaelezea nini kinamaanishwa na "maisha ya kimwili" na "maisha ya kiroho." Kulingana na mazingira, "maisha" inaweza kuetafsiriwa kama "kuwepo" au "mtu" au "roho" au "kuwa" au "kupitia." Neno "uhai" inaweza kutafsiriwa kama "kuishi" au "kukaa" au "kuwepo." Msemo "mwisho wa maisha yake" inaweza kutafsiriwa kama, "alipoacha kuishi." Msemo "alinusuru maisha yao" unaweza kutafisiri kama, "aliwaruhusu waishi" au "hakuwaua." Msemo "walihatarisha maisha yao" unaweza kutafsiriwa kama, "walijiweka hatarini" au "walifanya kitu ambacho kingiweza kuwaua." Bibilia inapozungumzia kuwa hai kiroho, "maisha" yanaweza kutafsiriwa kama "maisha ya kiroho" au "maisha ya milele," kulingana na mazingira. Wazo la "maisha ya kiroho" linaweza pia kutafsiriwa kama, "Mungu kutufanya kuwa hai katika roho zetu" au "maisha mapya kwa Roho wa Mungu" au "kufanywa hai ndani yetu." Kulingana na mazingira, msemo "toa maisha" unaweza kutafsiriwa kama, "kusababisha kuishi" au "kutoa uzima wa milele" au "kusababisha kuishi milele."
## Malaika, Malaika mkuu ### Ufafanuzi Malaika ni kiumbe chenye roho na chenye nguvu kilichoumbwa na Mungu. Malaika wanamtumikia Mungu kwa kufanya yale wanayoagizwa kuyafanya na Mungu. Malaika mkuu ni malaika anayewaongoza malaika wengine. * Malaika maana yake ni mjumbe. * Malaika mkuu maana yake ni mjumbe mkuu. Malaika pekee kwenye Biblia anayesemwa kama malaika mkuu ni Mikaeli. * Katika Biblia malaika wanafikisha ujumbe kwa watu toka kwa Mungu. Ujimbe huu ni pamoja na maelekezo juu ya nini Mungu anataka watu wafanye. * Malaika pia waliwaambia watu mambo yajayo. * Malaika wana mamlaka ya Mungu katika kumuwakilisha na wakati mwingine kwenye Biblia wamezungumza kama vile Mungu anazungumza. * Njia nyingine ambazo Malaika wanamtumikia Mungu nu kwa kuwalinda na kuwapa watu nguvu. * Malaika wa Yahweh ina maana mbili 1) "malaika wanaomwakilisha Yahweh" au "wajumbe wanaomtumikia Yahweh." 2) Yaweza kuwa na maana ya Yahweh mwenyewe aliyeonekana kama malaika alipoongea na mtu.
## Mamlaka ### Ufafanuzi Mamlaka ni nguvu ya kushawishi na kutawala ambayo mtu anakuwa nayo juu ya mtu mwingine. * Wafalme na viongozi wengine wanamamlaka juu ya watu wanaowaongoza. * Mamlaka pia yaweza kuwa watu, serikali au taasisi fulani yenye nguvu juu ya wengine. * Mabwana wana mamlaka juu ya watumwa wao. Wazazi wana mamlaka juu ya watoto wao. * Serikali ina mamlaka juu ya kuweka sheria zitakazowaongoza wananchi wake.
## manemane ### Ufafanuzi Manemane ni mafuta au manukato yanayo tengenezwa kwa majani ya manemane yanayo ota Africa na Asia. * Manemane utumika kutengeneza uvumba, marashi, na dawa, na kuanda miili kwa maazishi. * Manemane ni baadhi ya wasomi waliyo mpa Yesu alipo zaliwa. * Yesu alipewa mvinyo iliyo changanywa na manemane ili kupunguza maumivu alipo sulubiwa.
## manna ### Ufafanuzi Manna ili kuwa nyeupe, aina ya chakula cha unga ambacho Mungu alikitoa kwa ajili ya Waisraeli kula kipindi cha miaka 40 waliyo ishi nyikani baada ya kutoka Misri. * Manna ilikuwa kama theluji iliyo tokea kila asubui katika ardhi chini ya umande. Ladha yake ilikuwa tamu, kama asali. * Waisraeli walikusanya theluji za manna kila siku kasoro Sabato. * Katika siku kabla ya Sabato, Mungu aliwambia Waisraeli kukusanya mara mbili kiasi cha manna ili wasikusanye siku yao ya mapumziko. * Neno "manna" lina maana ya "nini hiki?" * Katika Biblia, manna pia ya tajwa kama "mkate kutoka mbinguni"
## Mapenzi ya Mungu ### Ufafanuzi Mapenzi ya Mungu ni kitu anachotamani Mungu au mipango. * Mungu atafananisha mahusiano yake na watu na namna anavyotaka watu waitikie kwake. * Pia mapenzi ya Mungu ni mipango yake kwa alivyoviumba. * Mapenzi ya Mungu pia yanaweza kutafsiriwa kama "Kusudi la Mungu" au "Linalompendeza Mungu."
## maskani ### Ufafanuzi Maskani ilikuwa hema muhimu Waisraeli walimuabudu Mungu kipindi cha miaka 40 walipo zunguka jangwani. * Mungu aliwapa Waisraeli maelekezo ya kujenga hema kubwa, iliyo kuwa na vyumba viwili na ilizungukwa na ua ya ndani. * Kila mara Waisraeli walipo enda sehemu tofauti jangwani kuishi, makuhani alitengua maskani na kuibeba kwenye kambi yao ifauatayo. * Maskani ilijengwa na mbao iliyo kuwa na mapazia na vitambaa, nywele za mbuzi, na ngozi za wanyama. * Sehemu mbili za maskani zilikuwa Pa Takatifu (ambapo madhabahu ya kufukiza uvumba ilikuwa) na Pa Takatifu Pa Patakatifu (ambapo sanduku la agano lilihifadhiwa.) * Uani ya maskani ilikuwa na madhabahu ya kuteketeza dhabihu za wanyama na beseni maalumu la kusafishia kimila.
## Mataifa ### Ufafanuzi Msemo "mataifa" una maana ya mtu yeyote ambaye sio Myahudi. Watu wa mataifa ni watu ambao sio uzao wa Yakobo. Katika Biblia, msemo "kutotahiriwa" pia hutumika kitamathali kumaanisha watu wa Mataifa kwa sababu wengi wao hawakutahiri watoto wao wa kiume kama Waisraeli walivyofanya. Kwa sababu Mungu aliwachagua Wayahudi kuwa watu maalumu, walifikiria juu ya watu wa mataifa kama watu wa nje ambao wasingeweza kuwa watu wa Mungu. Wayahudi pia waliitwa "Waisraeli" au "Waebrania" katika vipindi tofauti vya historia. Waliwajua wengine wote kama "watu wa Mataifa". Watu wa mataifa pia inaweza kutafsiriwa kama "asiye Myahudi" au "asiye Muisraeli" (Agano la Kale). Kitamaduni, Wayahudi hawakula na watu wa mataifa au kujihusishanao, ambapo mara ya kwanza ilisababisha matatizo miongoni mwa kanisa la kwanza.
## Matumaini ### Ufafanuzi Neno 'matumaini' hurejelea matarajio na hamu kubwa juu ya kitu fulani kitokee. Lakini pia inaweza kumaanisha kutokuwa na uhakika kwamba kitu fulani kitatokea. Katika Biblia, neno matumaini lina maana ya matarajio. mfano, matumaini yangu yako katika Bwana. Ina maana ya kuwa na matarajio ya kupokea kile ambacho Mungu amewaahidi watu wake. Wakati mwingine neno 'matumaini' laweza kutafsiriwa kama 'uhakika' au hali ya kujiamini. Hasa katika Agano Jipya neno uhakika hutumika zaidi kuonesha matumaini waliyo nayo watu waliomwamini Yesu juu ya kupokea ahadi walizoahidiwa na Mungu. Mapendekezo ya tafsiri katika mazingira tofauti, neno ' tumaini' lina maana ya ' kutaka ' au kutamani' au kutarajia. Maneno kama ' hakuna cha kutumaini' yana maana ya ' hakuna cha kutegemea. Maneno kama 'mtegemee Mungu' yana maana ya 'mtumaini Mungu.
## mbingu, anga, mbinguni ### Ufafanuzi Neno linalotafsiriwa kama "mbingu" hurejelea mahali anapoishi Mungu. Neno hilo hilo laweza kumaanisha " anga" kwa kutegemea na muktadha. Neno 'mbingu' hurejelea kila kitu tunachokiona juu mawinguni kama vile jua, mwezi, na nyota. Inaweza pia kujumuisha vitu vingine vya anga la mbali kama vile sayari, vitu ambavyo hatuwezi kuviona tukiwa hapa duniani. Neno "anga' hurejelea anga la bluu lililo juu ya dunia ambalo lina mawingu na hewa tunayopumua. Mara kwa mara, jua na mwezi husemwa kuwa ziko 'juu angani. Neno 'mbingu' laweza kumaanisha 'anga' au sehemu ambako Mungu anaishi' hii hutegemea na muktadha mbalimbali. Wakati neno 'mbingu' linapotumika kama tamathali ya semi, humrejelea Mungu mwenyewe. Kwa mfano, Mathayo anapoandika juu ya 'ufalme wa mbinguni' anarejelea ufalme wa Mungu. Mapendekezo ya tafsiri Wakati neno 'mbingu' linapotumika kimfano laweza kutafsiriwa kama 'Mungu" Maneno 'mbingu' au " vitu vya kimbingu' yaweza kutafsiriwa kama 'jua, mwezi na nyota. Kirai "nyota za mbinguni" chaweza kutafsiriwa kama " nyota za angani."
## Mchungaji ### Ufafanuzi Mchungaji inatumika kama cheo cha mtu ambaye ni kiongozi wa kiroho wa kundi fulani la waamini. * Katika toleo la Biblia kwa Kingereza neno "mchungaji" limeonekana mara moja katika kitabu cha Waefeso. * Katika lugha zingine neno mchungaji ni sawa sawa na neno mchungaji wa kundi fulani la wanyama. * Yesu pia anafananishwa na mchungaji mwema.
## Mfalme wa Wayahudi ### Ufafanuzi Usemi, "Mfalme wa Wayahudi" ni jina linalomaanisha Yesu, Masihi. Mara ya kwanza Biblia inaandika hili jina wakati linapotumika na wanaume wenye hekima waliosafiri kwenda Bethlehemu wakimtafuta mtoto aliye "Mfalme wa Wayahudi." Malaika alimfunulia Mariamu kuwa mwanaye, mzawa wa mfalme Daudi, atakuwa mfalme ambaye ufalme wake utadumu milele. Kabla Yesu hajasulibishwa, askari Wakirumi walimdhihaki Yesu kwa kumuita "Mfalme wa Wayahudi." JIna hili liliandikwa pia katika kipande cha mbao na kupigwa msumari juu ya msalaba wa Yesu. Yesu kweli ni Mfalme wa Wayahudi na mfalme wa viumbe vyote.
## Mfano ### Ufafanuzi "Mfano" ni simulizi fupi au somo fulani linalotumika kuelezea au kufundisha ukweli wa maadili. * Yesu alitumia mifano akiwafundisha wanafunzi wake. Japokuwa pia aliwaambia mifano makutano ya watu, mara nyingi hakuielezea mifano. * Mfano ulitumika kuonesha ukweli kwa wanafunzi wake wakati akificha ukweli huo kwa watu kama Mafarisayo ambao hawakumwamini Yesu. * Nabii Nathani alimwambia Daudi mfano wa kumuonesha mfalme dhambi zake. * Simulizi ya msamaria mwema ni moja ya mfano. Mfano wa Yesu wa viriba vipya na vya zamani ni moja ya mfano kama somo kwa wanafunzi wake ili kuwasaidia kuelewa mafundisho ya Yesu.
## mfano wa Mungu, mfano ### Ufafanuzi Neno "mfano" inamaanisha kitu kinachofanana na kitu kingine au ni kama tabia ya mtu au asili yake. Neno "mfano wa Mungu" inatumika katika njia tofauti, kulingana na mazingira. Katika mwanzo wa nyakati, Mungu aliwaumba binadamu "katika mfano wake", ambayo ni "kwa kumfanana." Hii inamaanisha kuwa binadamu wana sifa fulani zinazoonesha mfano wa Mungu, kama uwezo wa kusikia hisia, uwezo wa kufikiri na kuwasiliana, na roho inayoishi milele. Biblia inafundisha kwamba Yesu, Mwana wa Mungu, ni "mfano wa Mungu," kwamba yeye ni Mungu mwenyewe. Tofauti na binadamu, Yesu hakuumbwa. Kutoka milele yote. Mungu Mwana ana sifa zote za Mungu kwa sababu ana asili sawa na ya Mungu Baba.
## mfuasi ### Ufafanuzi Msemo wa "mfuasi" una maana ya mtu anayetumia muda mwingi na mwalimu, akijifunza kutoka kwa tabia na mafunzo ya mwalimu huyo. Watu waliomfuata Yesu, wakimsikiliza mafundisho yake na kuyatii, walijulikana kama "wanafunzi" wake. Yohana Mbatizaji pia alikuwa na wanafunzi. Katika kipindi cha huduma ya Yesu, kulikuwa na wanafunzi wengi waliomfuata na kusikiliza mafunzo yake. Yesu alichagua watume kumi na wawili wawe wafuasi wake wa karibu; wanamume hawa wakaja kujulikana kama "mitume" wake. Watume kumi na wawili waliendelea kujulikana kama "wanafunzi" wake au "wale kumi na wawili". Kabla tu ya Yesu kwenda juu mbinguni, aliwaamuru wanafunzi wake kuwafundisha watu wengine juu ya kuwa wafuasi wa Yesu pia. Yeyote anayemwamini Yesu na kumtii mafunzo yake anaitwa mfuasi wa Yesu. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "mwanafunzi" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo wenye maana ya "mfuasi" au "mwanafunzi". Hakikisha ya kwamba tafsiri ya msemo huu haimaanishi mwanafunzi anayejifunza darasani. Tafsiri ya msemo huu unatakiwa kuwa tofauti na tafsiri ya "mtume".
## Mfuniko wa upatanisho ### Ufafanuzi Mfuniko wa upatanisho ulikuwa mfuniko wa dhahabu uliotumika kufunika juu ya sanduku la agano. * Mfuniko wa agano ulikuwa na sentimeta 115 urefu na 70 upana. * Juu ya mfuniko wa upatanisho kulikuwa na Makerubi wawili wa dhahabu wakiwa wameshika na mabawa yao. * Yahweh alisema atakutana na Waisraeli juu ya mfuniko wa upatanisho chini ya mbawa za makerubi. Kuhani mkuu pekee ndiye aluyeruhusiwa kufanya hivyo na kuwawakilisha watu. * Mara nyingine Mfuniko wa upatanisho ulijulikana kama kiti cha rehema kwa sababu Mungu alishuka na kuonesha rehema zake kwa watu wenye dhambi na kuwasamehe.
## milele ### Ufafanuzi Msemo huu "milele" una maana ya kitu ambacho kitaendelea kuwepo au kutadumu daima. Msemo "milele" una maana ya hali ya kutokuwa na mwanzo au mwisho. Pia inaweza kumaanisha maisha ambayo hayana mwisho. Baada ya maisha haya ya sasa ya duniani, binadamu wataishi milele aidha mbinguni na Mungu au jehanamu kutengana na Mungu. Misemo "maisha ya milele" inatumika katika Agano Jipya kumaanisha kuishi milele pamoja na Mungu mbinguni. Msemo "milele na milele" ina wazo la muda ambao hauna mwisho na huelezea nini milele au maisha ya milele yakoje. Mapendekezo ya Tafsiri Njia zingine za kutafsiri "milele" zinaweza kujumuisha "kutokuwa na mwisho" au "kuendelea siku zote". Msemo "maisha ya milele" unaweza kutafsiriwa kama "maisha ambayo hayana mwisho" au "maisha ambayo yanaendelea bila kikomo" au "kufufua miili yetu kuishi milele". Kulingana na muktadha, njia tofauti za kutafsiri "milele" zinaweza kujumuisha "kuwepo nje ya muda" au "maisha yasiyo na mwisho" au "maisha mbinguni". Pia fikiria namna neno hili linatafsiriwa katika Biblia katika lugha ya taifa.
## mkate usiyotiwa chachu ### Ufafanuzi Neno "mkate usiyotiwa chachu" una lina maana mkate unatengenezwa pasipo hamira. Aina huu wa mkate ni bapa kwasababu hauna hamira kuufanya uumuke. * Mungu alipo wachia Waisraeli kutoka utumwani Misri, aliwaambia wakimbie Misri haraka pasipo kusubiri mkate wao uumuke. Hivyo walikula mkate usiyotiwa chachu na vyakula vyao. Tangu hapo mkate usiyotiwa chachu unatumika kwenye Pasaka zao za mwaka kuwa kumbusha hicho kipindi. * Maana chachu wakati mwingine utumika kama picha ya dhambi, "mkate usiyotiwa chachu" una wakilisha ondoleo la dhambi kwenye maisha ya mtu ilikuweza ishi namna inayo mpendeza Mungu.
## Mkono wa kulia. ### Ufafanuzi Mkono wa kulia humaanisha mahali pa heshima au nguvu ya mkono wa kiume wa mtawala au mtu wa muhimu. * Mkono wa kulia ulitumika kama alama ya nguvu na mamlaka. * Biblia inaeleza Yesu amekaa mkono wa kulia wa Mungu Baba kama kichwa cha kanisa na mwenye nguvu ya kutawala viumbe vyote. * Mkono wa kulia wa mtu ulitumika kuonesha heshima ya pekee unapowekwa kichwani mwa mtu akipewa baraka. (Kama Yakobo alivyombariki Mtoto wa Efraimu, Yusufu)
## Mkristo ### Ufafanuzi Baada ya Yesu kurudi mbinguni watu wakaanza kuitwa Wakristo ikiwa na maana ya wafuasi wa Kristo. * Ilikuwa katika mji wa Antiokia ambapo wafuasi wa Yesu waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza. * Mkristo ni mtu anayeamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na anayeamini kuwa Yesu anaweza kumuokoa toka kwenye dhambi. * Katika wakati wa sasa Mkristo ni mtu anayetambulishwa na dini ya Kikristo lakini sio mfuasi wa Yesu kabisa. Hii sio maana ya Mkristo ki Biblia. * Kwa sabau Mkristo kwenye Biblia inamaanisha mtu anayemwamini Yesu kabisa Mkristo pia anaitwa mwamini.
## Mnafiki, unafiki ### Ufafanuzi Neno 'mnafiki' humrejelea mtu ambaye hufanya mambo ili aonekane mwema, ingawa kwa siri hufanya mambo maovu. Neno 'unafiki' hurejelea tabia ambayo huwahadaa watu kwa kufikiri kuwa mtu huyo ni mwenye haki. Wanafiki wanapenda kuonekana wakiwa wanafanya mambo mazuri, hivyo watu hufikiri kuwa ni watu wazuri. Mara kwa mara watu wanafiki huwakosoa watu wengine kwa kufanya mambo yale yale ya dhambi ambayo wao wenyewe huyafanya. Yesu aliwaita Mafarisayo kuwa ni wanafiki kwasababu walifanya matendo ya kidini kama vile kuvaa aina fulani ya nguo na kula chakula fulani, lakini hawakuwa wema na wenye haki kwa watu. Mtu mnafiki huweka wazi makosa ya watu wengine, lakini yeye mwenyewe hakubali makosa yake. Mapendekezo ya tafsiri Baadhi ya lugha huwa na maneno kama "sura mbili" ambayo hutumika kumrejelea mnafiki au matendo ya mnafiki. Namna nyingine ya kutafsiri neno mnafiki ni "mdanganyifu, mtu anayejifanya, mwongo,"
## Mnaziri, Naziri ### Ufafanuzi Neno "Mnaziri" ni mtu aliye toa kiapo cha "Naziri." Sana wanaume wana toa hichi kiapo, pia wanawake waliweza kutoa. * Mtu aliye toa kiapo cha Naziri alikubali kuto kula chakula au kunywa kinywaji cha mizabibu kwa siku, wiki, au miezi ili kutimiza kiapo. Pia kipindi hicho hakukata nywele na hakukaribia maiti. * Baada ya muda kupita na kutimiza kiapo, Mnaziri alienda kwa kuhani na kutoa sadaka. Hii ilikuwa ni kukata na kuchoma nywele zake. Pia vizuizi vyote viliondolewa. * Samsoni ni maarufu katika Agano la Kale aliye kuwa chini ya kiapo cha Naziri. * Malaika aliye tangaza kuzaliwa kwa Yohana mbatizaji alimwambia Zekaria mwanae hatakunywa kinywaji kikali, iliyo ashiria kuwa Yohana alikuwa chini ya kiapo cha Naziri. * Mtume Paulo pia kwa wakati moja alichukuwa hichi kiapop, kulingana na kurasa moja katika Matendo.
## Moyo ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno 'moyo' limetumika mara nyingi kimfano kurejelea mawazo ya mtu, hisia, tamaa au utashi. Kuwa na 'moyo mgumu' ni msemo wa kawaida wenye maana ya mtu anayemwasi Mungu kwa ukaidi. Msemo "kwa moyo wote'' au '' kwa moyo wangu wote'' una maana ya kufanya kitu kwa kujitoa kikamilifu na kwa uhiari. Msemo mwingine '' weka moyoni" una maana kuchukulia kitu kwa umakini na kukitumia katika maisha. Maneno " kuvunjika moyo'' humwelezea mtu ambaye ana huzuni. Wamekuwa wameumizwa kihisia za ndani Mapendekezo ya tafsiri Baadhi ya lugha hutumia sehemu tofauti za mwili kama vile 'tumbo' au 'ini' kurejelea mawazo haya. Lugha zingine zaweza kutumia neno moja kuelezea dhana hizi na neno jingine kueleza dhana zingine. kama 'moyo' au sehemu nyingine ya mwili haina maana hii, lugha zingine zaweza kuhitaji kutumia maneno ya moja kwa moja kama vile 'fikra' au 'hisia' au 'tamaa.' Kwa kutegemeana na muktadha, maneno "kwa moyo wangu wote" yaweza kutafsiriwa kama "kwa nguvu zangu zote" au "kwa kujitoa kimamilfu" Maneno kama "weka moyoni" yaweza kutafsiriwa kama 'shughulikia kwa umakini' au fikiria kwa uangalifu" "kuvunjika moyo" ina maana ya kuwa 'mwenye huzuni' au 'kujisikia kuumizwa kwa ndani"
## mpendwa ### Ufafanuzi Neno "mpendwa" ni kifungu cha kitabia kinachomweleza mtu anayependa na mwingine. * Neno "aliyependwa" kwa kawaida limanaanisha "kupendwa" au "anayependwa". * Mungu anamtaja Yesu kama "Mwanawe mpedwa". * Katika barua zao kwa makanisa ya Kikristo, mitume mara kwa mara waliwataja waumini wenzao kama "wapendwa." ### Maoni ya Ufasiri * Neno hili pia laweza kufasiriwa kama "mpendwa" au "apendwaye" au "anayependwa sana" au "mpenzi." * Katika mazingira ya kuzungumzia rafiki wa karibu, yaweza kutafasiriwa kama "rafiki yangu mpenzi" au "rafiki yangu wa karibu." Katika Kiingereza ni kawaida tu kusema, "rafiki yangu mpenzi, Paulo" au Paulo, ambaye ni rafiki yangu mpenzi." Lugha nyingine zaweza kuwa na njia nyingine ya kueleza hali hii. * Angalia kwamba neno "mpendwa" linatokana na neno la upendo wa Mungu, ambao hauna masharti, ubinafsi, na wa kujitoa.
## Mpinga Kristo ### Ufafanuzi "Mpinga Kristo" linamaanisha mtu au mafundisho ambayo ni kinyume na Yesu Kristo na kazi zake. Wapo wapinga Kristo wengi sana duniani. * Mtume Yohana anaandika kwamba mtu anaweza kuwa mpinga Kristo pale anapowapotosha watu kwa kuwaambia kuwa Yesu sio Masihi na kukataa kuwa Yesu ni Mungu. * Biblia pia inatufundisha kuwa kuna roho ya mpinga Kristo duniani ambayo inapinga kazi za Mungu. * Kitabu cha ufunuo kinaeleza kuwa kutakuwa na mtu atakayeitwa "mpinga Kristo" atakayejidhihirisha siku za mwisho. mtu huyu atajaribu kuwaangamiza watu wa Mungu Yesu atamshinda.
## mpumbavu, upumbavu, upuuzi ### Ufafanuzi Msemo "mpumbavu" una maana ya mtu ambaye mara kwa mara hutengeneza uchaguzi mbaya, haswa kuchagua kutokutii. Msemo "upumbavu" unaelezea mtu au tabia ambayo siyo ya hekima. Katika Biblia, msemo "mpumbavu" mara kwa mara una maana ya mtu ambaye haamini au kumtii Mungu. Mara nyingi hii hutofautishwa na mtu mwenye hekima, ambaye humwamini Mungu na kumtii. Katika Zaburi, Daudi anaelezea mtu mpumbavu kama mtu ambaye hamwamini Mungu, ambaye hupuuza ushahidi wote wa Mungu na uumbaji wake. Kitabu cha Agano la Kale cha Mithali pia hutoa maelezo mengi ya mpumbavu ni nani, mtu mpumbavu yukoje. Msemo "upuuzi" una maana ya tendo ambao sio la hekima kwa sababu ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Mara nyingi "upuuzi" pia hujumuisha maana ya kitu ambacho ni cha kudharaulika au hatari. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "mpumbavu" unaweza kutafsiriwa kama "mtu mpumbavu" au "mtu asiye na hekima" au "mtu asiyejitambua" au "mtu asiyemcha Mungu" Njia za kutafsiri "mpumbavu" zinawvza kujumuisha "upungufu wa uelewa" au "kutokuwa na hekima" au "kutojitambua".
## Msalaba ### Ufafanuzi Katika Biblia msalaba ni mbao iliyosimama wima inayochimbiwa kwenye ardhi na yenye mbao nyingine inayopita kwa mlalo na inayoshikizwa karibu na juu. * Katika wanyati wa utawala wa Rumi serikali ya Rumi ilimhukumu mhalifu kwa kumgongelea msalabani na kumuacha afe hapo. * Yesu alihukumuwa bila kosa na walimuua msalabani.
## mtakatifu ### Ufafanuzi Neno "mtakatifu'' ni jina ambalo katika Biblia mara zote humrejelea Mungu. Katika Agano la kale, jina hili mara kwa mara lilitokea katika kirai ''mtakatifu wa Israeli" Katika Agano Jipya, jina mtakatifu lilitumika kumrejelea Yesu Mara nyingine katika Biblia, neno mtakatifu hutumika kumrejelea malaika.
## mtukufu ### Ufafanuzi Neno "mtukufu" la husu ukubwa na utukufu, mara nying katika sifa za mfalme. * Katika Biblia, "mtukufu" mara nyingi la husu ukuu wa Mungu, ambaye ndiye mtawala wa ulimwengu. * "mtukufu" ni namna ya kumwita mfalme katika mazungumzo.
## Mtume, utume ### Ufafanuzi Mitume walikuwa watu waliotumwa na Yesu kuhubiri kuhusu ufalme wa Mungu. Utume ni nafasi au mamlaka ya wale waliochaguliwa kuwa mitume. * "Mtume" maana yake ni mtu aliyetumwa kwa ajili ya lengo maalumu. Mtume ana mamlaka sawa na ya yule aliyemtuma. * Kwa nguvu za Mungu, Mitume waliweza kuhubiri injili na kuponya watu na kuwatoa watu mapepo.
## muhudumu, huduma ### Ufafanuzi Katika Biblia, maneno "muhudumu" na "huduma" ya husu kutumikia wengine kwa mafundisho kuhusu Mungu na kujali mahitaji yao ya kiroho. Neno "muhudumu" pia laweza eleza mtu anaye tumikia watu kwa namna hii. * Katika Agano la Kale, makuhani "walitumika" kwa Mungu ndani ya hekalu kwa kutoa sadaka za dhabihu kwake. * "Huduma" zao pia ilihusisha kuhudumia hekalu na kutoa maombi kwa Mungu kwa niaba ya watu. * Katika Agano Jipya, "muhudumu" wa injili alikuwa mtu aliye fundisha watu wengine ujumbe wa wokovu kupitia imani ya Yesu. Wakati mwingine muhudumu anatwa "mtumishi" * Kazi ya kuhudumu kwa watu yaweza maanisha kuwatumikia kiroho kwa kuwa fundisha kuhusu Mungu.
## Mungu ### Ufafanuzi Katika Biblia, msemo "Mungu" una maana ya kiumbe wa milele ambaye aliumba ulimwengu bila chochote. Mungu alikuwepo kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Jina binafsi la Mungu ni "Yahwe". Mungu mara zote alikuwepo; alikuwepo kabla ya kitu chochote kuwepo, na ataendelea kuwepo milele. Yeye ni Mungu mmoja wa kweli na ana mamlaka juu ya kila kitu ulimwenguni. Mungu ana haki timilifu, hekima isiyo na mwisho, mtakatifu, bila dhambi, wa haki, wa rehema, na upendo. Ni Mungu wa kutunza agano, ambaye hutimiza ahadi zake daima. Watu waliumvwa kumwabudu Mungu na ni yeye pekee wanaopaswa kumwabudu. Mungu alifunua jina lake kama "Yahwe" ambayo ina maana ya "yeye ni" au "Mimi ni" au "Yule anayekuwepo daima". Biblia pia hufundisha kuhusu "miungu" wa uongo ambao ni sanamu wasioishi ambao watu huabudu kwa makosa.
## Mungu Baba, Baba wa mbinguni, Baba ### Ufafanuzi Misemo, "Mungu Baba" na "Baba wa mbinguni" ina maana ya Yahwe, Mungu mmoja wa kweli. Msemo huu hujitokeza kama "Baba" haswa pale Yesu anamaan ya yeye. Mungu alikuwepo kama Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Kila mmoja ni Mungu kamili, na bado wote ni Mungu mmoja. Hii ni siri ambayo binadamu wa kawaia hawezi kuelewa kikamilifu. Mungu Baba alimtuma Mungu Mwana (Yesu) duniani na yeye humtuma Roho Mtakatifu kwa watu wake. Yeyote anayemwamini Mungu Mwana anakuwa mtoto wa Mungu Baba, na Mungu Roho Mtakatifu huja kuishi ndani ya mtu huyo. Hii ni siri nyingine ambayo binadamu hawawezi kuelewa kikamilifu. Mapendekezo ya Tafsiri Katika msemo "Mungu Baba" ni bora kutafsiri "Baba" na neno sawa ambalo lugha hutumia kikawaida kumaanisha baba wa kimwili. Msemo "Baba wa mbinguni" unaweza kutafsiriwa na "Baba anayeishi mbinguni" au "Baba Mungu ambaye anaishi mbinguni" au "Mungu Baba kutoka mbinguni". Kawaida "Baba" inaandikwa kwa herufi kubwa, kuonyesha ya kwamba hii inamaanisha Mungu.
## mungu wa uongo, mungu mgeni, mungu, mungu wa kike ### Ufafanuzi Mungu wa uongo ni kitu ambacho watu huabudu badala ya Mungu mmoja wa ukweli. Msemo "mungu wa kike" una maana haswa kwa mungu wa uongo wa kike. Miungu hawa wa uongo hawapo. Yahwe ni Mumngu wa pekee. Watu mara kwa mara hutengeneza vitu kuwa sanamu ili kuabudu kama ishara ya miungu yao ya uongo. Katika Biblia, watu wa Mungu mara kwa mara waligeuka kutoka kumtii yeye ili kuabudu miungu ya uongo. Mapepo mara kwa mara hudanganya watu kuamini ya kwamba miungu ya uongo na sanamu wanazoabudu ina nguvu. Baali, Dagoni, na Moleki walikuwa miungu watatu wa uongo ambao waliabudiwa na watu katika kipindi cha Biblia. Ashera na Artemi (Diana) walikuwa miungu wa kike wawili ambao watu wa zamani waliwaabudu. Mapendekezo ya Tafsiri Kunaweza kuwa tayari na neno kwa ajili ya "mungu" au "mungu wa uongo" katika lugha yako. Msemo "sanamu" unaweza kutumika kumaanisha miungu wa uongo. Katika Kiingereza, herufi ndogo ya "m" inatumika kumaanisha miungu wa uongo, na herufi kubwa ya "M" hutumika kwa ajili ya Mungu wa ukweli. Lugha zingine pia hufanya hivi. Njia nyingine inakuwa kutumia neno tofauti kabisa kumaanisha miungu wa uongo. Baadhi ya lugha zinaweza kuongeza neno kuelezea kama mungu wa uongo ni wa kiume au wa kike.
## muujiza, ajabu, ishara ### Ufafanuzi "Muujiza" ni kitu kinacho shangaza ambacho hakiwezekani pasipo Mungu kusababisha kitokee. * Mifano ya miujiza Yesu aliyo fanya ni kutuliza dhoruba na kumponya kipofu. * Miujiza wakati mwingine inaitwa "maajabu" kwasababu ina sababisha watu kujawa na mshangao au kustaajabika. * Neno "ajabu" pia laweza kwa ujumla kueleza nguvu za Mungu, kama alivyo umba mbingu na nchi. * Miujiza pia ya weza itwa "ishara" kwasababu inatumika kama kiashiria au ushaidi kwamba Mungu ni mwenye nguvu kamilifu juu ya ulimwengu. * Miujiza mingine ilikuwa matendo ya urejesho wa Mungu, kama vile alipo waokoa Waisraeli kutoka utumwani Misri na alipo mlinda Danieli kuto umizwa na simba. * Maajabu mengine yalikuwa matendo ya hukumu ya Mungu, kama alivyo tuma garika ulimwenguni kote kipindi cha Nuhu na alipo leta mapigo katika nchi ya Misri kipindi cha Musa. * Miujiza mingi ya Mungu ilikuwa uponyaji wa mwili wa wagonjwa au kuleta wafu kuwa hai.
## mwaminifu, uaminifu ### Ufafanuzi Kuwa "mwaminifu" kwa Mungu ina maana kuwa na desturi ya kuishi kulingana na mafunzo ya Mungu. Ina maana ya kuwa mwaminifu kwake na kumuamini. Hali ya kuwa mwaminifu ni "uaminifu". Mtu ambaye ni mwaminifu anaweza kuaminiwa kuweza kushika ahadi zake na kutimiza majukumu yake daima kwa watu wengine. Mtu mwaminifu huvumilia katika kutenda kazi, hata pale ambapo ni ndefu au ngumu. Uaminifu kwa Mungu ni matendo ya daima ya kutenda ambacho Mungu anatutaka kufanya. Mapendekezo ya Tafsiri Katika muktadha nyingi, "mwaminifu" inaweza kutafsiriwa kama "uaminifu" au "kujitolea" au "kutegemea". Katika muktadha zingine, "mwaminifu" inaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kuendelea kuamini" au "kuvumilia katika kuamini na kumtii Mungu". Njia ambazo "uaminifu" inaweza kutafsiriwa inaweza kumaanisha "kuvumilia katika kuamini" au "uaminifu" au "kuamini na kumtii Mungu".
## Mwana wa Adamu, mwana wa adamu ### Ufafanuzi Jina, "Mwana wa Adamu" lilitumika na Yesu akijieleza. Mara nyingi alitumia hili jina badala ya kusema "mimi." * Katika Biblia, mwana wa adamu" ina weza kuwa ya kumueleza mtu au kumtaja mtu. Yaweza pia maanisha "binadamu." * Katika Agano la Kale la kitabu cha Ezekieli, Mungu mara nyingi anamtaja Ezekieli kama "mwana wa adamu." Kwa mfano anasema, "Wewe, mwana wa adamu, utabiri." * Nabii Danieli aliona maono ya "mwana wa adamu" akija na mawingu, ambayo ni mfano wa kuja kwa Mesiya. * Yesu pia alisema Mwana wa Adamu atarudi siku moja na mawingu.
## Mwana wa Mungu, Mwana ### Ufafanuzi Neno "Mwana wa Mungu la husu Yesu, Neno la Mungu aliye kuja duniani kama binadamu. Anajulikana kama "Mwana." * Mwana wa Mungu ana tabia moja na Mungu Baba, na ni Mungu timilifu. * Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu yote ni maana moja. * Tofauti na wana wa binadamu, Mwana wa Mungu alikuwepo siku zote. * Mwanzo, Mwana wa Mungu alikuwepo katika uumbaji wa ulimwengu, pamoja na Baba na Roho Mtakatifu. * Kwasababu Yesu ni Mwana wa Mungu, na penda na kumtii Baba yake, na Baba yake anampenda.
## mwana, mwana wa ### Ufafanuzi Neno "mwana" la husu mvulana au mwanaume na wazazi wake. La weza eleza mzao wa kiume wa mwanaume au mwana aliye pangwa. * "Mwana" ni linatumika sana kifumbo katika Biblia kueleza mzao wa kiume, kama mjukuu au kitukuu. * Neno "mwana" pia la weza kama rasmi ya kumtaja mvulana au mwanaume aliye mdogo. * Wakati mwingine "wana wa Mungu" lina tumika katika Agano Jipya kueleza waamini wa Yesu. * Mungu anamuita Israeli "mwana wake wa kwanza." Hii yaeleza Mungu kuchagua taifa la Israeli kuwa watu wake maalumu. Ni kupitia wao kuwa ujumbe wa Mungu wa wokovu ulikuja, kwa matokeo kwamba wengi wamekuwa wana wake wa kiroho. * Maneno "mwana wa" mara nyingi ina maana ya kimafumbo, "kuwa na tabia ya." * Maneno "mwana wa" pia linatumika kueleza baba wa mtu. Hili neno linatumika katika vizazi na sehemu nyingine.
## mwanakondoo, Mwanakondoo wa Mungu ### Ufafanuzi Neno "mwanakondoo" linamaanisha kondoo mchanga. Kondoo ni wanyama wenye miguu minne na wana nywele nene ya sufu, waliotumika kwa sadaka kwa Mungu. Yesu anaitwa "Mwanakondoo wa Mungu" kwa sababu alitolewa kulipia dhambi za watu. Wanyama hawa huongozwa nje ya mstari kirahisi na wanahitaji ulinzi. Mungu anawafananisha binadamu na kondoo. Mungu anawaagiza watu wake kutoa sadaka kimwili kama kondoo na wanakondoo kamili kwake. Yesu anaitwa "Mwanakondoo wa Mungu" aliyetolewa sadaka kwa ajili ya dhambi za watu. Alikuwa sadaka kamili, bila kasoro kwa sababu alikuwa hata dhambi kabisa.
## mwandishi, mtaalamu katika sheria ya Kiyahudi ### Ufafanuzi Waandishi walikuwa wasimamizi waliyo wajibika katika kuandika au kunakili nyaraka muhimu za serikali au za kidini kwa mkono. Jina lingine la mwandishi wa Kiyahudi ni "mtaalamu katika sheria ya Kiyahudi." * Waandishi waliwajibika kunakili na kutunza vitabu vya Agano la Kale. * Pia walinakili, hifadhi, na kutafsiri maoni ya kidini na maelezo katika sheria ya Mungu. * Wakati mwingine, waandishi walikuwa wasimamizi muhimu wa serikali. * Waandishi muhimu katika Biblia walikuwa Baruku na Ezra. * Katika Agano Jipya, neno "waandishi" lina tafsiriwa pia kama "waalimu wa sheria" * Katika Agano Jipya, waandishi walikuwa sehemu ya makundi ya kidini yaliyo itwa "Mafarisayo" na makundi haya mawili mara nyingi utajwa pamoja.
## Mwenyezi ### Ufafanuzi "Mwenyezi" linamaanisha "nguvu yote. Kwenye Biblia inamaanisha Mungu. Cheo "mwenyezi" linamuelezea Mungu na kudhihirisha kuwa ana nguvu zote na mamlaka kwa kila kitu. * Pia linatumika kumuelezea Mungu kwa cheo chake "Mwenyezi Mungu" au Mungu Mwenyezi" au "Bwana Mwenyezi" au "Bwana Mungu Mwenyezi"
## mwili ### Ufafanuzi Neno "mwili" kwa kawaida linamaanisha mwili wa binadamu au mnyama. Nene hili hutumika pia kitamathari kurejerea kitu au jumla ya kundi lenye wajumbe. * Mara kwa mara neno "mwili" linarejerea mtu au mnyama aliyekufa. Wakati mwingine linarejerewa kama "mfu" au "maiti." * Yesu alipoongea na wanafunzi wake katika mlo wake wa mwisho wa Pasaka. "Huu(mkate) ni mwili wangu," alikuwa anamaanisha mwili wake ambao uawa ili kulipa dhambi zao. * Katika Biblia, Wakristo kama kundi wanatajwa kama "mwili wa Kristo." * Kama mwili ulivyo na viungo vingi, "mwili wa Kristo" unawaumini wengi. * Kila muumini mmoja mmoja ana kazi maalumu katika mwili wa Kristo kuliwezesha kundi lote kufanya kazi pamoja ili kumtumikia Mungu na kumpa utukufu. * Yesu anatajwa kama "kichwa" (kiongozi) wa "mwili" wa waumini. Kama ambavyo kichwa cha mtu kinavyouambia mwili cha kufanya, hivyo Yesu ndiye anayewaongoza Wakristo kama wajumbe wa "mwili" wake. ### Maoni ya Tafasiri * Njia nzuri ya kutafasiri neno hili lingekuwa ni neno ambalo linatumika sana kuonesha mwili katika lugha lengwa. Hakikisha kwamba neno linalotumika halileti chukizo. * Linaporejerea jumla ya waumini, kwa baadhi ya lugha yaweza kawaida kusema, "mwili wa kiroho wa Kristo." * Yesu anaposema, "Huu ni mwili wangu" ni vizuri kutafasiri hii kihalisia, na maelezo kama yanatakiwa. * Baadhi ya lugha zaweza kuwa na neno tofauti la kutaja mfu, kama vile "maiti" kwa mtu au "mzoga" kwa mnyama. Hakikisha neno litumikalo kutafasiri linaleta maana na linakubariwa katika mazingira yale.
## mwili ### Ufafanuzi Katika Biblia, msemo "mwili" una maana ya tishu laini ya mwili wa mwanadamu au mnyama. Biblia pia hutumia msemo "mwili" kitamathali kumaanisha wanadamu wote au viumbe wote. Katika Agano Jipya, msemo "mwili" unatumika kumaanisha asili ya dhambi ya wanadamu. Hii hutumika mara kwa mara kinyume na asili yao ya kiroho. Msemo, "mwili na damu yake" ina maana ya mtu ambaye anahusiana kibiolojia na mtu mwingine, kama vile mzazi, ndugu, mtoto au mjukuu. Msemo "mwili na damu" pia unaweza kumaanisha mababu au vizazi vya mtu. Msemo "mwili mmoja" una maana ya muungano wa kimwili wa mwanamume na mwanamke katika ndoa. Mapendekezo ya Tafsiri Katika muktadha wa mwili wa mnyama, "mwili" unaweza kutafsiriwa kama "mwili" au "ngozi" au "nyama". Inapotumika kumaanisha viumbe wote hai, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "viumbe hai" au "kila kitu chenye uhai". Inapomaanisha kwa jumla watu wote, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "watu" au "binadamu" au "kila mtu anayeishi". Msemo "mwili na damu" unaweza kutafsiriwa kama "jamaa" au "familia" au "ndugu wa karibu" au "ukoo wa familia". Kunaweza kuwa na muktadha ambapo inaweza kutafsiriwa kama "mababu" au "vizazi". Baadhi ya lugha zinaweza kuwa na msemo ambao unafanana na "mwili na damu". Msemo "kuwa mwili mmoja" unaweza kutafsiriwa kama "kuungana kimapenzi" au "kuwa kama mwili mmoja" au "kuwa kama mtu mmoja kimwili na roho". Tafsiri ya msemo huu unaweza kuangaliwa kuhakikisha inakubalika katika lugha na utamaduni wako.
## mwinjilisti ### Ufafanuzi "mwinjilisti" ni mtu ambaye huwaambia watu wengine habari njema juu ya Yesu Kristo. Maana halisi ya "mwinjilisti" ni "mtu ambaye anahubiri habari njema". Yesu aliwatuma mitume wake kusambaza habari njema kuhusu namna ya kuwa sehemu ya ufalme wa Mungu kupitia kumuamini Yesu na sadaka yake kwa ajili ya dhambi. Wakristo wote wanashawishiwa kutangaza hii habari njema. Baadhi ya Wakristo wanapatiwa karama maalumu kuwaambia kwa ufasaha watu wengine injili. Watu hawa wanasemwa kuwa na karama ya uinjilisti na wanaitwa "wainjilisti". Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "mwinjilisti" unaweza kutafsiriwa kama, " mtu anayehubiri habari njema" au "mwalimu wa habari njema" au "mtu ambaye anatangaza habari njema"
## Mwokozi ### Ufafanuzi Neno "Mwokozi" lina husu mtu anaye okoa au komboa wengine na hatari. Pia yaweza maanisha mtu anaye wapa wengine uwezo au waitaji yao. * Katika Agano la Kale, Mungu anatajwa kama Mwokozi wa Waisraeli kwasababu mara nyingi aliwaokoa na maadui zao, akawapa uwezo, na kuwapa maitaji yao. * Katika Agano Jipya, "Mwokozi" linatumika kama elezo au cheo cha Yesu Kristo kwasababu anaokoa watu kutoadhibiwa milele kwa dhambi zao. Pia ana waokoa na kutawaliwa na dhambi zao.
## Myahudi, Yahudi, Wayahudi ### Ufafanuzi Wayahudi ni watu ambao ni uzao wa mjukuu wa Abrahamu, Yakobo. Neno "Yahudi" linatoka katika neno "Yuda" Watu walianza kuwaita Waisraeli "Wayahudi" baada ya kurudi Yuda kutoka katika uhamisho kutoka Babeli. Yesu Masihi alikuwa Myahudi. Isipokuwa, viongozi wa dini wa Kiyahudi walitaka kwamba auliwe. Mara nyingi msemo "Wayahudi" inamaanisha viongozi wa Wayahudi, sio watu wote Wayahudi. Kwa mazingira hayo, tafsiri zingine huongeza "viongozi wa" kuiweka wazi.
## Nabii, unabii, mwonaji, nabii mwanamke. ### Ufafanuzi "Nabii ni mtu anayesema ujumbe wa Mungu kwa watu. Mwanamke anayefanya hivi anaitwa "nabii mwanamke." * Mara nyingi manabii waliwaonya watu kuacha dhambi zao na kumtii Mungu. * Unabii ni ujumbe unaozungumzwa na nabii. * Ujumbe wa unabii mara nyingi ulikuwa unahusu mambo yatakayotokea hapo baadae. * Unabii mwingi wa agano la kale umeshatimia. * Katika Biblia mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na manabii mara nyingine vinajulikana kama "manabii." * Kwa mfano maneno "sheria na manabii" ni namna ya kuelezea maandiko ya kiebrania ambayo yanajulikana kama "agano la kale" * Jina la zamani la nabii lilikuwa "mwonaji" au "mtu anayeona." * Mara nyingine "mwonaji" inamana ya nabii wa uongo au mtu anayefanya uganga.
## nafsi ### Ufafanuzi Nafsi ni sehemu ya ndani, isiyo onekana ya mtu. Ya husu sehemu isiyo ya kimwili ya mtu. * Maneno "nafsi" na "roho" yanaweza kuwa mitazamo miwili tofauti, au inaweza kuwa maneno mawili yanayo eleza mtazamo mmoja. * Mtu anapo kufa, nafsi yake ya acha mwili. * Neno "nafsi" wakati mwingine utumika kimafumbo kueleza mtu kamilifu. Kwa mfano, "nafsi inayo fanya dhambi" ina maana, "mtu anaye fanya dhambi" na "nafsi yangu imechoka," ina maana "nimechoka"
## naivera ### Ufafanuzi Naivera ilikuwa vazi kama aproni iliyovaliwa na makuhani wa Kiisraeli. Ilikuwa na sehemu mbili, mbele na nyuma, amnazo ziliunganishwa pamoja mabegani na kufungwa kuzunguka kiuno na mkanda wa kitambaa. Aina moja ya naivera ilitengenezwa na sufi ya kawaida na ilivaliwa na makuhani wa kawaida. Naivera iliyovaliwa na kuhani mkuu ilishonwa maalumu kwa kitani cha dhahabu, bluu, zambarau, na chekundu. Deraya ya kifua ya kuhani mkuu iliunganishwa na sehemu ya mbele ya naivera. Nyuma ya deraya ya kifuani kulitunzwa Urimu na Thumimu, ambaya yalikuwa mawe yaliyotumiwa kumuuliza Mungu mapenzi yake yalikuwa yapi katika baadhi ya masuala. Mwamuzi Gideoni kwa upumbavu alitengeneza naivera kwa dhahabu na ikawa kitu ambacho Waisraeli waliabudu kama sanamu.
## Nchi ya ahadi ### Ufafanuzi "Nchi ya ahadi" imaonekana tuu katika simulizi za Biblis. Ni namna ya kuelezea nchi ya Kanaani ambayo Mungu aliahidi kumpa Abrahamu na uzao wake. * Abramu alipokuwa akiishi katika nchi ya Uru Mungu aliwamuri kwenda kuishi katika nchi ya Kanaani. Yeye na uzao wake, Waisraeli waliishi huko kwa miaka mingi. * Wakata njaa kuu iliposababisha uhaba wa chakula Waisraeli wakahamiaMisri. * Miaka mia nne baadae Mungu akawaokoa Israeli kutoka utumwani Misri na kuwarudisha katika nchi yao ya Kanaani nchi ambayo aliahidi atawapa.
## ndugu ### Ufafanuzi Neno "ndugu" kwa kawaida linamaanisha ndugu wa kiume ambaye wanaunganishwa angalau na mzazi mmoja. * Katika Agano la Kale, neno "ndugu" lilitumika kama neno la taarifa ya jumla kwa ndugu, kama vile watu wa kabila moja, ukoo, au kikundi. * Katika Agano Jipya, mitume kwa kawaida walitumia "ndugu" kuwalejerea Wakristo wenzao, wakiwemo wa kike na wa kiume, kwa kuwa waumini wote katika Kristo ni washirika wa familia moja ya kiroho, wakiwa na Mungu kuwa Baba yao wa mbinguni. * Mara chache katika Agano Jipya, mitume kutumia neno "dada" wanaporejerea hasa kwa Mkristo mwenza aliyekuwa mwanamke, au katika kusisitiza kwamba wote wanaume na wanawake wanajumuishwa. Kwa mfano, Yakobo alisisitiza kwamba anazungumzia waumini wote anaporejerea "ndugu au dada aliye na mahitaji ya chakula au nguo." ### Maoni ya Kutafasiri * Ni vema zaidi kutafasiri neno hili kwa neno halisi litumikalo katika lugha lengwa kurejerea kwa ndugu wa kibayolojia, isipokuwa neno hili linatoa maana potofu. * Katika Agano la Kale hasa, neno"ndugu" linapotumika kwa ujumla sana kurejerea watu wa familia moja, ukoo, au kikundi, maana pendekezwa ni pamoja na "ndugu" au "wanaukoo" au "Waisraeli wenzao." * Katika mazingira ya kurejerea kwa washiriki wenzao katika Kristo, neno hili liliweza kutafasiriwa kama, "ngugu katika Kristo" au "ndugu wa kiroho." * Ikiwa wote, wanaume na wanawake wametajwa na "ndugu" lingetoa maana potofu, hivyo neno la jumla zaidi la kindugu lingetumika ili kuwahusishawa wote wanaume na wanawake. * Njia nyingine ya kutafasiri neno hili ili kuwahusisha waumini wote wa kiume na wa kike lingekuwa, "waumini wenzao" au "Wakristo wa kike na wa kiume." * Hakikisha unaangalia mazingira kuamua kwamba ni wanaume pekee wametajwa, au kwamba wote wamehusishwa.
## neema, mwenye neema ### Ufafanuzi Neno "neema" lina maana ya msaada au baraka ambayo hutolewa kwa mtu ambaye hajastahili. Msemo "mwenye neema" inamwelezea mtu ambaye huonyesha neema kwa wengine. Neema ya Mungu kwa wanadamu wenye dhambi ni zawadi ambayo inatolewa bure. Dhana ya neema pia ina maana ya kuwa na huruma na kusamehe mtu ambaye amefanya kosa au mambo ya kuumiza. Msemo "kupata neema" ni msemo ambao una maan aya kupokea msaada na rehema kutoka kwa Mungu. Mara nyngi inajumuisha maana ya kwamba Mughu anafurahishwa na mtu na kumsaidia.
## Neno la Mungu, Neno la Yaweh, Neno la Bwana, maandiko ### Ufafanuzi Katika Biblia neno la Mungu ni kitu chochote ambacho Mungu anawaambia wanadamu. Hii ni pamoja na lililoandikwa au kutamkwa. Yesu pia anaitwa "neno la Mungu. * "Maandiko" ni maandishi . Imetumika tuu katika agano jipya na imeelezea maandiko ya Kiebrania au agano la kale. Maandishi haya yalikuwa ujumbe toka kwa Mungu aliowaambia watu kuandika ili miaka ya baadae watu waweze kuyasoma. * Neno la Yaweh au neno la Bwana ni ujumbe toka kwa Mungu aliopewa nabii au mtu mwingine katika Biblia. * Mara nyingine neno hili hutokea kama "neno" au "neno langu" au "neno la Mungu. * Katika agano jipya Yesu anaitwa "neno" na "neno la Mungu." Cheo hiki kinamaanisha kuwa Yesu alidhihiridha Mungu ni nani kwa sababu yeye ni Mungu.
## Nguvu ### Ufafanuzi "Nguvu" ni uwezo wa kufanya jambo au kusababisha mambo yatokee mara nyingi hutumia nguvu. Pia nguvu yaweza kumaanisha watu au roho zenye uwezo wa kusababisha mambo yatokee. * "Nguvu ya Mungu ni uweza wa Mungu kufanya jambo hasa ambalo ni ngumu kufanywa na mwanadamu. * Mungu ana nguvu juu ya vyote alivyoviumba. * Mungu huwapa watu wake nguvuza kufanya anayoyataka ili kwamba wakiponya watu au kufanya miujiza wafanye kwa nguvu za Mungu. * Kwa sababuYesu na Roho mtakatifu ni Mungu wana hizi nguvu.
## nidhamu, nidhamu binafsi ### Ufafanuzi Msemo wa "nidhamu" una maana ya kufundisha watu kutii maelekezo kadhaa ya tabia za maadili. Wazazi huwafundisha watoto wao kwa kutoa maelekezo ya kimaadili na mwelekeo kwa ajili yao na kuwafundisha kutii. Vivyohivyo, Mungu huadhibu watoto wake kuwasaidia kuzaa matunda mazuri ya kiroho katika maisha yao, kama vile furaha, upendo, na uvumilivu. Nidhamu inashirikisha maelekezo yahusuyo jinsi ya kuishi namna ya kumpendeza Mungu, na pia adhabu kwa tabia ambayo ipo kinyume na mapenzi ya Mungu. Nidhamu binafsi ni njia ya kutumia kanuni za kimaadili na kiroho kwa maisha ya mtu mwenyewe. Mapendekezo ya Tafsiri Kutegemea na muktadha, "nidhamu" inaweza kutafsiriwa kama, "fundisha na kuelekeza" au "ongoza kimaadili" au "adhibu kwa kutenda mabaya". Nomino ya "nidhamu" inaweza kutafsiriwa kama "mafunzo ya maadili" au "adhabu" au "marekebisho ya maadili" au "mwongozo na maelekezo ya kimaadili".
## nyenyekea, unyenyekevu ### Ufafanuzi Neno 'nyenyekea' humwelezea mtu ambaye hufikirii kuwa ni bora kuliko watu wengine. Ni mtu asiye na kiburi au majivuno. Unyenyekevu ni sifa au hali ya kuwa mnyenyekevu. Kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu ina maana ya kujua udhaifu na hali ya kutokamilika, huku ukilinganisha na ukuu , hekima na ukamilifu wa Mungu. Mtu anapojinyenyekesha, hujiweka katika daraja la chini. 'Unyenyekevu' ni hali ya kujali mahitaji ya watu wengi kuliko mahitaji yako binafsi. Kirai 'uwe mnyenyekevu' kinaweza kutafsiriwa kama ' ''usiwe mwenye kiburi/majivuno.'' "Nyenyekea mbele za Mungu'' ina maana ya " wasilisha utashi wako kwa Mungu, kwa kuutambua ukuu wake.
## Nyumba ya Mungu, Nyumba ya Yahweh ### Ufafanuzi Katika Biblia, vifungu vya maneno "nyumba ya Mungu'' na "nyumba ya Yahweh'' hurejelea sehemu ambapo Mungu huabudiwa'' au 'sehemu ya kumwabudia Mungu.' Neno hili piakimahususi laweza kurejelea 'hema la kukutania au hekalu' Wakati mwingine neno 'nyumba ya Mungu' humaanisha ''watu wa Mungu" Mapendekezo ya tafsiri Wakati neno la nyumba ya Mungu linaporejelea sehemu ya kuabudia ina maana ya 'nyumba au sehemu ya kumwabudia Mungu.
## okoa, salama ### Ufafanuzi Neno "okoa" la husu kumzuia mtu kutopitia kitu kibaya au cha hatari. Kuwa "salama" ya maanisha kulindwa na hatari au majanga. * Kwa hali ya kawaida, watu wanaweza okolewa au kombolewa kutoka kwenye hatari, au kifo. * Katika hali ya kiroho, kama mtu ameokolewa ina maana kupitia kifo cha Yesu msalabani, Mungu amemsamehe na kumkomboa kutoadhibiwa jehanamu kwa dhambi zake. * Watu wanaweza okoa au kukomboa watu na hatari, lakini Mungu tu anaweza okoa watu kutoadhibiwa milele kwa dhambi zao.
## ombea, sala ya kuombea ### Ufafanuzi Msemo "ombea" na "sala ya kuombea" inamaanisha kufanya maombi kwa mtu kwa niaba ya mtu mwingine. Katika Biblia hii kawaida humaanisha kuwaombea watu wengine. Usemi "kuomba kwa ajili ya" na "kuombea" inamaanisha kufanya maombi kwa Mungu kwa faida ya watu wengine. Biblia inafundisha kuwa Roho Mtakatifu hutuombea, kwamba, humsihi Mungu kwa ajili yetu. Mtu huombea watu wengine kwa mtu mwenye mamlaka.
## omboleza, maombolezo ### Ufafanuzi usemi "omboleza" na "maombolezo" yanamaanisha hisia kali ya kulia, majonzi au huzuni. Wakati mwingine hii ni pamoja na kujuta kwa kina kwa ajili ya dhambi, au huruma kwa watu waliopitia maafa. Maombolezo yanaweza kujumuisha kulia, kutoa machozi au kulia kwa sauti.
## Onesha, ufunuo ### Ufafanuzi Kuonesha ni kusababisha kitu fulani kujulikana. Ufunuo ni kitu kilichojulikana. * Katika Biblia "kuonesha" limetumika kuelezea namna ambayo Mungu alijionesha mwenyewe kwa watu. * Mungu alijionesha mwenyewe kupitia kila kitu alichokiumba na kwa kupitia mawasiliano na watu kwa kuzungumzwa na kuandika ujumbe. * Mungu alijionesha mwenyewe kupitia ndoto na maono. * Paulo aliposema kwamba amepokea injili kwa "ufunuo toka kwa Yesu Kristo" anamaanisha kuwa Yesu mwenyewe alimuelezea injili. * Katika agano jipya kitabu cha "ufunuo" kinahusu namna ambayo Mungu anaonesha matukio yatakayotokea siku za mwisho. Aliyaonesha haya kwa mtume Yohana kupitia maono.
## Pasaka ### Ufafanuzi "Pasaka " ni jina la sherehe ya kidini ambayo Wayahudi walisherehekea kila mwaka kukumbuka mi kwa namna gani Mungu aliwaokoa mababu zao Waisraeli toka utumwani Misri. * Jina la sikukuu hii lilitokana na namna ambayo Mungu "alizipita" nyumba za Waisraeli na hakuwaua watoto wake pale alipowaua wazaliwa wa kwanza wa Misri. * Sikukuu ya pasaka inajumuisha chakula maalumu yaani kondoo mzuri waliomuua na kumpika, pia mkate usio na amira. Vyakula hivi vinawakumbusha chakula walichokula Waisraeli usiku ule kabla ya kuondoka Mirsi. * Mungu aliwaambia Waisraeli wale chakula hiki kila mwaka kama kumbukumbu na kusherehekea namna ambavyo Mungu "alizipita" nyumba zao na namna alivyowaweka huru toka utumwa nchini Misri.
## Pentekoste au sikukuu za majuma ### Ufafanuzi Sikukuu za majuma ilikuwa ni sikukuu ya Kiyahudi iliyofanyika siku hamsini kabla ya Pasaka. Baadae ilikuja kuitwa Pentekoste. * Sikukuu za majuma ilikuwa wiki sabini (siku hamsini) baada ya sherehe ya matunda ya kwanza. Katika agano jipya sikukuu hii iliitwa "pantekoste." * Sikukuu za majuma zilikuwa maalumu kwa ajili ya kusherehekea mwanzo wa mavuno ya nafaka. Pia ilikuwa muda wa kumkumbuka siku ambayo Mungu aliwapa sheria Waisraeli katika vibao vya mawe alivyopewa Musa. * Katika agano jipya siku ya Pentekoste imeelezewa moja kwa moja kwa sababu ilikuwa siku ambayo waliomwamii wa Yesu walipokea roho mtakatifu kwa njia mpya.
## pepo mbaya, roho ovu, roho chafu ### Ufafanuzi Misemo hii yote ina maana ya mapepo, ambayo ni viumbe vya roho vinavyopingana na mapenzi ya Mungu. Mungu aliwaumba malaika kumtumikia. Shetani alipomwasi Mungu, baadhi ya malaika pia waliasi na kutupwa kutoka mbinguni. Inaaminika ya kwamba mapepo na roho mbaya ndio hawa "mailak walioanguka". Mara kwa mara haya mapepo yanajulikana kama "roho chafu". Msemo "chafu" una maana ya "isiyo safi" au "uovu" au "isiyo takatifu". Kwa sababu mapepo humtumikia shetani, wanafanya mambo maovu. Mara kwa mara wanaishi ndani ya watu na kuwaendesha. Mapepo wana nguvu kuliko wanadamu, lakini hawana nguvu kama ya Mungu. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo wa "pepo" unaweza kutafsiriwa kama "roho mchafu". Msemo wa "roho mchafu" unaweza kutafsiriwa kama "roho chafu" au "roho iliyoharibika" au "roho mchafu". Hakikisha ya kwamba neno au msemo unaotumika kutafsiri msemo huu ni tofauti na msemo unaotumika kumaanisha shetani. Pia fikiria jinsi msemo wa "pepo" unaweza kutafsiriwa katika lugha ya kawaida au ya taifa.
## Rabi, Raboni ### Ufafanuzi Rabi ina maana ya bwana wangu au mwalimu wangu. * Kilikuwa cheo cha heshima kilichotumiwa kumuelezea mtu aliyekuwa kiongozi wa dini ya Kiyahudi hasi aliyefundisha sheria za Mungu. * Yohana mbatizaji na Yesu mara nyingine waliitwa Rabi na wanafunzi wao.
## rehema ### Ufafanuzi Neno "rehema" lina husu kusaidia mtu waliyo na shida, hususani wanapo kuwa chini au hali ngumu. * Neno "rehema" linaweza maanisha maana yakuto adhibu watu kitu walicho kosea. * Mtu mwenye nguvu kama mfalme anaelezwa kama mwenye "rehema" anapo tendea watu wema badala ya kuwaua. * Kuwa mwenye Rehema ina maana ya kusamehe mtu aliye kukosea. * Tuna onyesha rehema tunapo saidia watu mwenye shida kubwa. * Mungu ni wa rehema kwetu, na anataka tuwe na rehema kwa wengine.
## rithi, urithi, mrithi ### Ufafanuzi Maneno "rithi" na "urithi" zinamaanisha kupokea kitu cha dhamani kutoka kwa mzazi au mtu mwingine kwa sababu ya uhusiano maalumu na huyo mtu. "Mrithi" ni mtu ambaye anapokea urithi. Urithi wa halisia ambao unapokelewa unaweza kuwa fedha, ardhi, au aina zingine za mali. Urithi wa kiroho ni vyote ambavyo Mungu huwapa watu wanaomuamini Yesu, zikiwemo baraka za maisha ya sasa pamoja na maisha ya milele pamoja naye. Biblia pia inawaiita watu wa Mungu urithi wake, kinachomaanisha kuwa ni wake, ni mali yake ya dhamani. Mungu alimuahidi Abrahamu na uzao wake kuwa watarithi nchi ya Kanaani, kwamba itakuwa yao milele. Kuna maana ya kitamathali na kiroho ya jinsi watu walio wa Mungu wanasemwa "kurithi nchi." Hii inamaanisha kuwa watafanikiwa na kubarikiwa na Mungu kwa mambo ya kimwili na kiroho. Katika Agano Jipya, Mungu anaahidi kuwa wale wanaomuamini Yesu "watarithi wokovu" na "kurithi uzima wa milele." Pia inaelezwa kama, "kurithi ufalme wa Mungu." Huu ni urithi wa milele unaodumu milele. Kuna maana zingine za kitamathali za haya maneno: Biblia inasema kuwa watu wenye hekima "watarithi utukufu" na watakatifu "watarithi vitu vizuri." "Kurithi ahadi" inamaanisha kupokea vitu vizuri ambavyo Mungu ameahidi kuwapa watu wake. Msemo huu pia unatumika kwa njia ya uhasi kumaanisha watu wapumbavu au wasiotii ambao "wanarithi upepo" au "kurithi upumbavu." Hii inamaanisha wanapokea matokeo ya matendo yao ya dhambi, ikiwemo adhabu na maisha yasiyo na maana.
## Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho wa Bwana. ### Ufafanuzi Maneno haya yote humrejelea Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu. Mungu mmoja na wa kweli aishiye milele katika nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu mara zingine hutajwa kama 'Roho' na 'Roho ya Yahweh' au 'Roho wa ukweli' Roho Mtakatifu ni mtakatifu kwa sababu yeye ni Mungu. Yeye yuko kamili na mwadilifu katika kila jambo alifanyalo. Roho Mtakatifu alishiriki kikamilifu katika uumbaji wa ulimwengu pamoja na Baba na Mwana. Wakati Mwana wa Mungu, Yesu aliporudi mbinguni, Mungu alimtuma Roho Mtakatifu kwa watu ili awaongoze, kuwafundisha, kuwafariji na kuwawezesha kufunya mapenzi ya Mungu. Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu na pia anawaongoza wale wanaomwamini Yesu. Mapendekezo ya tafsiri Neno hili laweza kutafsiriwa tu kwa kutumia maneno yenye kumaanisha 'roho' na 'mtakatifu' Lakini maneno mengine ambayo yaweza kutumika ni kama 'Roho Safi' au 'Roho aliye Mtakatifu' au 'Mungu Roho.'
## roho, kiroho ### Ufafanuzi Neno "roho" la eleza sehemu isiyo ya kimwili ya watu isiyo onekana. Mtu anapo kufa, roho yake inaacha mwili wake. "Roho" inaweza eleza tabia au hali ya kihisia ya mtu. * Neno "roho" la eleza kiumbe kisicho kuwa na mwili, hususani roho chafu. * Roho ya mtu ni sehemu yake inayo weza mjua Mungu na kumuamini. * Kwa ujumla, neno "kiroho" la eleza chochote kisicho katika dunia ya mwili. * Katika Biblia, sana ueleza chochote kinacho muhusu Mungu, sana Roho Mtakatifu. * Mungu ni roho na ameumba roho za viumbe wengine wasiyo na miili. * Malaika ni roho, pamoja na hao waliyo hasi dhidi ya Mungu na kuwa roho chafu. * Neno "roho ya" la weza maanisha "kuwa na tabia za," kama vile, "roho ya hekima" au "katika roho ya Eliya." * Mifano ya "roho" kama tabia au hisia itahusisha "roho ya hofu" au "roho ya wivu"
## Sabato ### Ufafanuzi Neno "Sabato" la husu siku ya saba ya wiki, ambayo Mungu aliwaamuru Waisraeli waitenge kama siku ya kupumzika na kutofanya kazi. * Baada ya Mungu kumaliza kuumba dunia kwa siku sita, alipumzika siku ya saba. Kwa namna hiyo hiyo, Mungu aliwaamuru Waisraeli kutenga siku ya saba kama siku maalumu ya kupumzika na kumuabudu. * Amri "kutakasa Sabato" ni moja ya amri kumi Mungu alizo andika katika jiwe alilo mpa Musa kwa ajili ya Waisraeli. * Kwa kufuata kanuni ya Wayahudi ya kuhesabu siku, Sabato ya anza Ijumaa jua linapo zama na kudumu hadi Juma Mosi jua linapo zama. * Wakati mwingine katika Biblia Sabato yaitwa "siku ya Sabato" kuliko tu Sabato.
## Sadukayo ### Ufafanuzi Masadukayo walikuwa kikundi cha makuhani wa Kiyahudi kipindi cha Yesu Kristo waliyo unga mkono utawala wa Warumi na ambao hawakuamini ufufuo. * Masadukayo wengi walikuwa matajiri, Wayahudi wa daraja la juu waliyo shika vyeo vikubwa kama vile chifu kuhani na kuhani mkuu. * Majukumu ya Masadukayo yali husisha kutunza hekalu na kazi za kikuhani kama kutoa dhabihu. * Masadukayo na Mafarisayo walishawishi viongozi wa Kirumi kumsulubisha Yesu. * Yesu alizungumza kuhusu haya makundi mawili ya kidini kwasababu ya ubinafsi na unafiki wao.
## Safi, kusafisha ### Ufafanuzi Neno "safi" inamaana ya kawaida ya kutokuwa na uchafu au doa. Katika Biblia hutumika kuwa na maana ya "takatifu" au "kuwa huru na dhambi." * Kusafisha ni hatua ya kufanya kitu kiwe kisafi. Inaweza kutafsiriwa kama "kuosha" au "kutakasa." * Katika agano la kale Mungu aliwaambia Waisraeli ni wanyama gani waliokuwa safi na ambao hawakuwa safi. Wanyama wasafi tuu ndio walioruhusiwa kutumika kwa ajili ya chakula na dhabihu. * Mtu aliyekuwa na ugonjwa fulani wa ngozi hakuwa safi mpaka ngozi yake itakapopona. * Mara nyingine safi inaweza kutafsiriwa kama kuwa na usafi wa maadili.
## safi, kusafisha ### Ufafanuzi Kuwa "safi" inamaana kutokuwa na mapungufu au kutochanganya kitu ndani ya kitu ambacho hakitakiwi kuchanganywa. Kukisafisha kitu ni kitendo cha kukisafisha na kuondoa chochote kinachoweza kuchafua. * Kwa kutumia sheria za agano la kale "kusafisha" ni kitendo cha kuondoa uchafu kiibada kwenye kitu au mtu kinachoweza kumfanya asiwe msafi kama magonjwa, kutokwa damu au kujifungua. * Katika agano jipya pia kuna sheria zinazowaambia watu namna ya kujisafisha toka kwenye dhambi hasa kwa kutoa sadaka ya wanyama. Hii ilikuwa ya muda tuu na sadaka hii ilirudiwa mara kwa mara. * Katika agano jipya kusafishwa ni kitendo cha kusafishwa toka kwenye dhambi. * Njia pekee ya watu kusafishwa kabisa toka kwenye dhambi ni kwa kutubu dhambi zao na kupokea msamaha wa Mungu kwa kumwamini Yesu.
## samehe, kusamehe ### Ufafanuzi Kumsamehe mtu ina maana ya kutokaa na kinyongo dhidi ya mtu ambaye alifanya jambo la kuumiza. "Kusamehe" ni tendo la kumsamehe mtu. Kumsamehe mtu mara nyingi humaanisha kutomuadhibu mtu huyo kwa jambo ambalo amekosa. Msemo huu unaweza kutumika kitamathali kumaanisha, "katisha" kama msemo "kusamehe deni". Watu wanapokiri dhambi zao, Mungu huwasamehe kutokana na sadaka ya kifo cha Yesu msalabani. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusamehe wengine kama jinsi alivyowasamehe wao. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, "samehe" inaweza kutafsiriwa kama "omba radhi" au "katisha" au "achilia" au "kutoshikilia dhidi ya"
## Sanduku ### Ufafanuzi Maana ya kawaida ya "sanduku" ni sanduku la mbao la mstatili lililotengenezwa kwa ajili ya kushikilia au kulinda kitu fulani. Sanduku laweza kuwa kubwa au dogo kutokana na matumizi yake. * Kiingereza cha Biblia "Sanduku" limetumika kwa mara ya kwanza kuonesha kitu kikubwa, mashua ya mbao ya mstatili ambayo Nuhu aliitengeneza ili kuepuka mafuriko. Sanduku lilikuwa na gorofa chini, paa na kuta. * Njia za kutafsiri neno hili ni kusema "mashua kubwa" au "jahazi" au "meli ya mizigo." * Kwa Kiebrania neno ambalo linaweza kutumika kuelezea hii meli kubwa ni neno lile lile lililoumika kuelezea kikapu au sanduku lililotumika kumuweka Musa katika mto Nile ili kumficha. * Katika kuchagua neno la kutafsiri "sanduku" ni muhimu kujua ukubwa na limetumika kwa kazi gani.
## Sanduku la agano, Sanduku la Yahweh. ### Ufafanuzi Sanduku la agano ni sanduku la mbao maalumu lililofunikwa na dhahabu na lenye vibao viwili vya mawe vyenye amri kumi. Pia lina fimbo ya Haruni na mana. * Neno "Sanduku" lina maana ya "chombo." * Lengo la sanduku hili ni kuwakumbusha Wana wa Israeli agano lao na Mungu. * Sanduku la agano liliwekwa sehemu takatifu sana. * Uwepo wa Mungu ulikuwepo juu ya sanduku la agano mahali pa juu katika hema, ambapo aliongea na Musa kwa niaba ya Waisraeli. * Kipindi ambacho sanduku la agano lilikuwepo patakatifu pa patakatifu, kuhani mkuu pakeyake ndiye aliyeruhusiwa kulisogelea sanduku mara moja kwa mwaka.
## Sayuni, Mlima Sayuni ### Ufafanuzi Hapo awali, neno "Sayuni" au "Mlima Sayuni" lilimaanisha ngome ambayo Mfalme Daudi aliiteka kutoka kwa Wayebusi. Majina haya yakawa njia nyingine ya kuitaja Yerusalemu. * Mlima Sayuni na Mlima Moria ilikuwa milima miwili mji wa Yerusalemu ulipojengwa juu yake. Baadaye, "Sayuni" na "Mlima Sayuni" ikawa ikitumika kama maneno ya jumla kuitaja milima yote na mji wa Yerusalemu. Wakati mwingine pia yalitumika kutaja hekalu lililokuwako Yerualemu. (Tazama: [aina hii ya maana] (https://git.door43.org/Door43/en-ta-translate-vol2/src/master/content/figs_metonymy.md)) * Daudi aliita Sayuni, au Yerusalemu, kama "Mji wa Daudi." Hii ni tofauti na mji wa alikozaliwa Daudi, Bethlehemu, ambao pia uliitwa Mji wa Daudi. * Neno "Sayuni" limetumika katika njia nyingine za tamathali za semi, kuitaja Israeli au Ufalme wa kiroho wa Mungu au katika mji mpya wa Yerusalemu atakaouanzisha Mungu.
## Sehemu takatifu, sehemu takatifu sana (patakatifu pa patakatifu) ### Ufafanuzi Katika Biblia, maneno kama 'sehemu takatifu' na ' sehemu takatifu sana' yanarejelea sehemu mbili za hema la kukutania au jengo la hekalu. 'Sehemu takatifu' ni chumba cha kwanza kilicho na madhabahu ya uvumba na meza iliyo na 'mkate wa uwepo' juu yake. 'Sehemu takatifu sana' (patakatifu pa patakatifu) kilikuwa ni chumba cha pili cha ndani sana kilicho na sanduku la agano. Kulikuwa na pazia kubwa na pana lililotenganisha kati ya chumba cha nje na chumba cha ndani. Kuhani mkuu ndiye pekee aliyeruhusiwa kuingia sehemu takatifu sana yaani Patakatifu pa patakatifu. Wakati mwingine 'sehemu takatifu' hurejelea jengo na sehemu za nje za hekalu au hema la kukutania. Pia neno hili laweza kumaanisha eneo lolote lililotengwa kwa ajili ya Mungu. Mapendekezo ya tafsiri Maneno 'sehemu takatifu' yanaweza kutafsiriwa kama "chumba kilichotengwa kwa ajili ya Mungu'' au '' chumba maalumu kwa ajili ya kukutana na Mungu'' au chumba kilichotunzwa kwa ajli ya Mungu. ''sehemu takatifu'' yaweza kujumuisha sehemu iliyotakaswa' au hekaluni.
## shawishi, ushawishi ### Ufafanuzi Msemo "shawishi" una maana ya kumsihi mtu kwa nguvu na kumbembeleza mtu kufanya kilicho sahihi. Aini hii ya kusihi inaitwa "kushawishi". Kusudi la kushawishi ni kusihi watu wengine kuepukana na dhambi na kufuata mapenzi ya Mungu. Agano Jipya hufundisha Wakristo kujishawishi baina yao kwa upendo, sio kwa ukali au ghafula. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, "kushawishi" pia inaweza kutafsiriwa kama "kubembeleza kwa nguvu" au "kusihi" au "kushauri". Hakikisha tafsiri ya msemo huu hainyoeshi ya kuwa anayeshawishi ana hasira. Msemo unatakiwa kuonyesha nguvu na uzito, lakini usionyeshe kauli ya ukali. Katika muktadha nyingi, msemo "shawishi" unatakiwa kutafsiriwa tofauti na "kutia moyo" ambayo ina maana ya kutia msukumo, aminisha, au kufariji mtu. Mara kwa mara msemo huu pia unatafsiriwa tofauti na "onya" ambayo ina maana ya kuonya au kusahisha mtu kwa tabia yake mbaya.
## shemasi ### Ufafanuzi Shemasi ni mtu ambaye anatumika katika kanisa lake, akiwasaidia waumini kwa mahitaji ya kiutendaji, kama vile chakula au pesa. Neno "shemasi" limechukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye neno la Kigiriki lenye maana ya "mtumishi" au "mchungaji". Tangu kipindi cha Wakristo wa awali, kuwa shemasi ilikuwa ni nafasi na huduma iliyobainishwa katika mwili wa Kanisa. Kwa mfano, katika Agano Jipya, mashemasi walikuwa wanahakikisha ya kuwa kila pesa au chakula ambacho waumini hutoa zingegawanywa sawa sawa kwa wajane miongoni mwao. Msemo wa "shemasi" pia unaweza kutafsiriwa kama, "mchungaji wa kanisa" au "mfanyakazi wa kanisani" au "mtumishi wa kanisani", au msemo mwingine ambo unaonyesha ya kwamba mtu huyu amewekwa mahususi kufanya kazi maalumu ambayo ina manufaa kwa jamii yake ya Kikristo.
## sheria, sheria ya Musa, sheria ya Mungu, sheria ya Yahwe ### Ufafanuzi Misemo hii yote inamaanisha amri na maelekezo ambayo Mungu alimpa Musa kwa ajili ya Waisraeli kutii. Misemo "sheria" na "sheria ya Mungu" zinatumika pia kwa ujumla kumaanisha kila kitu Mungu anachotaka watu wake kutii. Kulingana na mazingira, "sheria" inaweza kumaanisha: Amri kumi ambazo Mungu aliandika katika jiwe kwa ajili ya Waisraeli. sheria zote alizopewa Musa vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale. Agano lote la Kale (pia inajulikana kama "maandiko" katika Agano Jipya). maelekezo yote ya Mungu na mapenzi yake. Usemi "sheria na manabii" inatumika katika Agano Jipya kumaanisha maandiko ya Kihebrania (au "Agano la Kale").
## Shetani, ibilisi, yule muovu ### Ufafanuzi Ibilisi ni roho hai Mungu aliyo umba, lakini aliasi dhidi ya Mungu na kuwa adui wa Mungu. Ibilisi anaitwa "Shetani" na "yule muovu." * Ibilisi ana
## siku ya Bwana, siku ya Yahwe ### Ufafanuzi Msemo wa Agano la Kale wa "siku ya Yahwe" unatumika kumaanisha kipindi/vipindi maalumu ambapo Mungu angewaadhibu watu kwa dhambi zao. Msemo wa Agano Jipya wa "siku ya Bwana" huwa una maana ya siku au kipindi ambapo Bwana Yesu atarudi kuwahukumu watu katika wakati wa mwisho. Huu wakati wa mwisho, wa baadaye wa hukumu na ufufuo, pia hujulikana kama "siku ya mwisho". Kipindi hiki kitaanza pale ambapo Bwana Yesu atakaporudi kuhukumu wenye dhambi na kuunda mamlaka yake ya kudumu. Neno "siku" katika misemo hii inaweza kumaanisha siku haswa au inaweza kumaanisha "kipindi" au "wakati maalumu" ambao ni mrefu zaidi ya siku moja. Mara nyingine adhabu huwa ina maana ya "kumwagwa kwa ghadhabu ya Mungu" juu ya wale wasioamini. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, njia zingine za kutafsiri "siku ya Yahwe" zinaweza kujumuisha, "kipindi cha Yahwe" au "kipindi ambapo Yahwe atawaadhibu adui zake" au "kipindi cha hasira ya Yahwe". Njia zingine za kutafsiri "siku ya Bwana" zinaweza kujumuisha "kipindi cha hukumu ya Bwana" au "kipindi ambacho Bwana Yesu atarudi kuhukumu watu".
## siku ya hukumu ### Ufafanuzi Usemi "siku ya hukumu" inamaanisha siku ya usoni ambapo Mungu atamhukumu kila mtu. Mungu amemfanya Mwanaye, Yesu Kristo, kuhukumu watu wote. Katika siku ya hukumu, Kristo atawahukumu watu kulingana na asili yake ya haki.
## siku ya mwisho, siku za mwisho ### Ufafanuzi Usemi wa "siku za mwisho" inamaanisha kwa ujumla kipindi cha mwisho wa muda wa sasa. Muda huu utakuwa muda usiojulikana. "Siku za mwisho" ni wakati wa hukumu kwa wale waliomgeuka Mungu.
## sinagogi ### Ufafanuzi Sinagogi ni jengo la watu wa Kiyahudi wanapo kutania pamoja kumuabudu Mungu. * Tangu zama za kale, huduma za sinagogi zimekuwa na maombi, kusoma maandiko, na kufundisha kuhusu maandiko. * Wayahudi walianza jenga masinagogi kama sehemu za kuomba na kumuabudu Mungu katika miji yao, kwasababu wengi waliishi mbali na hekalu lililo Yerusalemu. * Yesu alifundisha katika masinagogi na kuponya watu. * Neno "sinagogi" linaweza tumika kifumbo kueleza kundi la watu waliyo kusanyika hapo.
## sio na hatia ### Ufafanuzi Usemi "sio na hatia" unamaanisha kutokuwa na hatia la uhalifu au makosa mengine. Inaweza pia kumaanisha kwa ujumla watu ambayo hawahusiki na matendo maovu. Mtu anayetuhumiwa kwa kufanya kitu kibaya hana hatia kama hataambatanishwa na hilo kosa. Wakati mwingine usemi "sio na hatia" unatumika kumaanisha watu ambao hawajafanya kosa kustahili ubaya wanaoupata, kama jeshi la adui kushambulia "watu wasio na hatia."
## stahili, yenye thamani ya, wasiofaa, isiyo na maana ### Ufafanuzi "Stahili" linaelezea mtu au kitu kinachofaa kupewa heshima. "Kustahilisha" inamaana ya kuwa na thamani au muhimu. "isiyo na maana" inamaanisha isiyo na thamani. * Kustahili inamaana ya kuwa na thamani au kuwa na umuhimu. * Kutofaa imanaana ya kutostahili kuwa na nafasi maalumu. * Kuhisi kutothaminiwani kuhisi huna umuhimu zaidi ya mtu mwingine. * Maneno "wasiofaa" na "isiyo na thamani" yanaendana japokuwa yana maana tofauti. "Kutofaa" inamaana ya kutostahili heshima au kujulikana. "kutokuwa na maana" ni kutokuwa na thamani au lengo."
## Sulubisha ### Ufafanuzi Sulubisha inamaana ya kumuhukumu mtu kwa kumuweka msalabani na kumuacha ateseke mpaka afe. * Mtu huyo anaweza kufungwa msalabani au kugongewa misumari. Watu wanaosulubishwa hufa kwa kupoteza damu nyingi. * Huko Rumi walitumia sana njia hii kuwaadhibu watu na kuwaua wahalifu au watu walioasi dhidi ya serikali. * Viongozi wa Kiyahudi walimuomba gavana wa Rumi kuwaamuru askari wake wamsulubishe Yesu. Askari walimweka Yesu msalabani. aliteseka masaa siti kisha akafa.
## tahini, pima ### Ufafanuzi Neno "tahini" yaeleza hali ngumu au inayo umiza yenye kudhihirisha uweza na udhahifu wa mtu. * Mungu pima watu, lakini hawa jaribu. Shetani, vinginevyo ana jaribu watu kufanya dhambi. * Wakati mwingine Mungu anatumia tahini kuweka wazi dhambi za watu. Kipimo kina msaidia mtu kutogeukia dhambi na kwenda kwa karibu na Mungu. * Dhahabu na vyuma vinapimwa kwenye moto kugundua usafi na uimara wake. Hii ni picha ya jinsi Mungu anavyo tumia mazingira magumu kujaribu watu.
## takasa, utakaso ### Ufafanuzi Kutakasa ni kutenga kando au kufanya takatifu. Utakaso ni hatua ya kufanya takatifu. * Katika Agano la Kale, baadhi ya watu na vitu vilitakaswa, au kutengwa kando, kwa hudumu ya Mungu. * Agano Jipya lina fundisha kuwa Mungu anatakasa watu wanao mwamini Yesu. Hiyo ni kwamba, anawafanya watakatifu na kuwatenga kumtumikia. * Waamini katika Yesu wanaamriwa kujitakasa kwa Mungu, kuwa watakatifu katika kila kitu wanacho fanya.
## takatifu ### Ufafanuzi Msemo "takatifu" una maana ya kitu chochote kinachomhusu Mungu. Baadhi ya njia ambazo msemo huu unatumika ni, "mamlaka takatifu", "hukumu takatifu", "asili takatifu", "nguvu takatifu", na "utukufu mtakatifu". Katika sehemu moja ndani ya Biblia, msemo "takatifu" unatumika kuelezea jambo juu ya uungu wa uongo. Mapendekezo ya Tafsiri Njia za kutafsiri msemo wa "takatifu" zinaweza kujumuisha "ya Mungu" au "kutoka kwa Mungu" au "fungamana na Mungu" au "huonyesha ni ya Mungu". Kwa mfano, "mamlaka takatifu" inaweza kutafsiriwa kama "mamlaka ya Mungu" au "mamlaka ambayo yanatoka kwa Mungu". Msemo wa "utukutufu takatifu" unaweza kutafsiriwa kama "utukufu wa Mungu" au "utukufu ambao Mungu ame" au "utukufu unatoka kwa Mungu". Baadhi ya tafsiri zinapendelea kutumia neno tofauti wanapofafanua jambo ambalo linafungamana na mungu wa uongo.
## takatifu, utakatifu ### Ufafanuzi Maneno 'takatifu' na 'utakatifu' hurejelea tabia ya Mungu ambayo imetengwa na kutofautishwa na kila kitu ambacho ni chenye dhambi na kisicho kamili. Mungu pekee ndiye mtakatifu kweli. Hufawafanya watu na vitu kuwa vitakatifu. Mtu aliye mtakatifu ni mali ya Mungu na ametengwa maalumu kwa kusudi la kumtumika Mungu na kumpa utukufu Yeye. Na kitu ambacho Mungu amekitangaza kuwa ni kitakatifu ni kile ambacho Mungu amekitenga kwa ajili ya utukufu wake na matumizi yake, kwa mfano madhabahu ambayo makusudi yake ni kumtolea Mungu sadaka. Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu, hakuna mtu awezaye kumkaribia Mungu isipokuwa awe ameruhusiwa na Yeye kufanya hivyo, hii ni kwasababu wao ni watu tu, wenye dhambi na wasiokamili. katika Agano la Kale, Mungu alitenga makuhani kama watakatifu kwa huduma maalumu kwake. Walitakiwa kutakaswa kwa sherehe maalumu ili waweze kumkaribia Mungu. Mungu pia aliweza kutenga sehemu na vitu maalumu kuwa vitakatifu vilivyo mali yake au kupitia kwa vitu hivyo aweze kujifunua mwenyewe, vitu hivi ni kama hekalu. Mapendekezo ya tafsiri Njia za kutafsiri neno 'takatifu' zinaweza kuwa ' kutengwa kwa ajili ya Mungu,' au "kuwa mali ya Mungu" au "hali ya kutokuwa na dhambi" au "kuwa safi." kufanya kitu/kuwa kuwa mtakatifu ina maana ya "kutakasa'' au ''kutenga''
## telekeza, kutelekezwa, totoka ### Ufafanuzi Msemo "telekeza" ina maana ya kuacha mtu au kuacha kitu. Mtu ambaye "ametelekezwa" amekuwa ameachwa au kutorokwa na mtu mwingine. Pale watu "wanapomtelekeza" Mungu, ina maana wanakuwa bila uaminifu kwake kwa kutomtii yeye. Mungu "anapotelekeza" watu, ina maana ameacha kuwasaidia na kuruhu wapitia mateso ili kwamba kuwafanya wamgeukie na kumrudia yeye. Msemo huu unaweza kumaanisha kutelekeza vitu, kama vile kuacha, au kutomfuata mafundisho ya Mungu. Msemo "kutelekezwa" unaweza kutumika katika kisarufi cha nyuma kama vile "amekutelekeza" au kumaanisha mtu ambaye "ametelekezwa". Mapendekezo ya Tafsiri Njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "kuacha" au "kutojali" au "kuachana" au "kuondoka mbali na" au "kuacha nyuma" kulinga na muktadha. "Kutelekeza" sheria ya Mungu inaweza kutafsiriwa "kutotii sheria ya Mungu". Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutenga" au "kukata tamaa juu ya" au "kuacha kutii" mafunzo au sheria zake. Msemo "kutelekezwa" unaweza kutafsiriwa kama "kuachwa" au "kutengwa". Lugha ya mradi inaweza kupata kwa uwazi zaidi kutumia maneno tofauti kutafsiri msemo huu, kulingana na maandishi yanaongelea juu ya kutelekeza kitu au mtu.
## timiza ### Ufafanuzi Msemo "timiza" una maana ya kukamilisha au fanikisha jambo ambalo lilitarajiwa. Pale ambapo unabii unatimizwa, ina maana ya kwamba Mungu alisababisha itokee kile kilichotabiriwa katika unabii. Kama mtu anatimiza ahadi au kiapo, ina maana ya kwamba anafanya kile alichoahidi kufanya. Kutimiza jukumu ina maana kufanya kazi ambayo ulipangiwa au unapaswa kufanya. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, "timiza" unaweza kutafsiriwa kama "fanikisha" au "kamilisha" au "kusababisha kutokea" au "kutii" au "kutenda". Msemo "imetimizwa" inaweza kutafsiriwa kama "imekuwa kweli" au "imetokea". Njia za kutafsiri "timiza" kama vile "timiza huduma yako" inaweza kujumuisha, "maliza" au "fanya" au "mazoezi" au "tumikia watu wengine kama vile Mungu amekuita kufanya"
## Tohara ### Ufafanuzi Tohara ni kitendo cha kukata govi la mwanaume au mtoto wa kiume. Sherehe ya tohara hufanyika pamoja na tendo hili. * Mungu alimuamuru Abrahamu awatahiri wanaume wote katika familia yake na watumishi wake kama ishara ya agano lao na Mungu. * Mungu aliamuru uzao wa Abrahamu waendelee kufanya hivi kwa kila mtoto wa kiume katika nyumba hiyo. * "Kutahiri moyo" ni mitendo cha kuondoa uovu wa mtu. * Kwa namna ya kiroho "aliyetahiriwa" ni mtu ambaye ametakaswa na Mungu toka kwenye dhambi kupitia damu ya Yesu. * "Wasiotairiwa" ni watu ambao hawajatahiriwa kimwili. Pia yaweza kuwa na maana ya ambao hawajatahiriwa kiroho wasiokuwa na mahusiano na Mungu.
## towashi ### Ufafanuzi Mara kwa mara, "towashi" ina maana ya mwanamume ambaye amehanithishwa. Msemo baadaye ukawa msemo wa jumla kumaanisha afisa yeyote wa serikali, hata wale ambao hawana ulemavu huu. Yesu alisema ya kwamba baadhi ya towashi walizaliwa vile, yawezekana kwa sababu ya uharibifu ya viuongo vya siri au kwa sababu ya kutokuwa kutekeleza jukumu la kuingiliana. Wengine huchagua kuishi kama towashi kwa maisha ya mseja. Katika nyakati za kale, matowashi mara nyingi walikuwa watumishi wa wafalme ambao waliwekwa kama walinzi katika maeneo ya wanawake. Baadhi ya matowashi walikuwa maafisa muhimu wa serikali, kama vile towashi wa Ethiopia ambaye alikutana na mtume Filipo katika jangwa.
## tukuza, kutukuza ### Ufafanuzi Kutukuza ni kusifu kwa juu sana na kumheshimu mtu. Inaweza kumaanisha kumweka mtu katika nafasi ya juu. Katika Biblia, msemo "tukuza" unatumika sana kwa ajili ya kumtukuza Mungu. Mtu anapojitukuza mwenyewe, ina maana anawaza juu yake mwenyewe kwa hali ya kujiinua au namna ya kiburi. Mapendekezo ya Tafsiri Njia za kutafsiri "tukuza" zinaweza kujumuisha "kusifu kwa juu" au "kuheshimu sana" au "sifu sana" au "kuzungumza kwa juu sana" Katika baadhi ya muktadha, inaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kuweka nafasi ya juu zaidi" au "kutoa heshima zaidi" au "kuzungumza kuhusu kwa kiburi". "Usijitukuze mwenyewe" inaweza kutafsiriwa kama "Usijiwazie kuwa juu sana" au "Usijidai juu yako mwenyewe". "Wale wanaojiinua wenyewe" inaweza kutafsiriwa kama "Wale ambao hufikiri kwa kiburi kuhusu wao wenyewe" au "Wale wanaojidai juu yao wenyewe"
## Uaminifu wa agano, fadhili, upendo wa kudumu ### Ufafanuzi Maneno haya hutumika kuelezea Mungu alivyijitoa kikamilivu kutimiza ahadi alizoweka kwa watu wake. * Mungu amewaahidi Waisraeli kwa kutumia Agano. * Uaminifu wa agano wa Bwana ni kitendo cha yeye kushika ahadi alizowaahidi watu wake. * Uaminifu wa Mungu unajionesha kwa rehema zake kwa watu wake. * Uaminifu ni neno lingine linaloelezea kujitoa kufanya au kusema kilichoahidiwa na kitakachomfaidisha mtu mwingine.
## ufalme wa Mungu, ufalme wa mbinguni ### Ufafanuzi Usemi wa "ufalme wa Mungu" na "ufalme wa mbinguni" zote zinamaanisha utawala wa Mungu na madaraka yake juu ya watu wake na viumbe vyote. Wayahudi mara nyingi hutumia neno "mbingu" kumaanisha Mungu, ili kuepuka kutaja jina lake moja kwa moja. Katika kitabu cha Agano Jipya alichoandika Mathayo, aliuita ufalme wa Mungu kama "ufalme wa mbinguni," inawezekana kwa sababu alikuwa akiwaandikia zaidi Wayahudi. Ufalme wa Mungu unamaanisha Mungu kuwatawala watu kiroho pamoja na kuwatawala katika dunia ya kimwili. Manabii wa Agano la Kale walisema kuwa Mungu atamtuma Masihi kutawala kwa haki. Yesu, mwana wa Mungu, ndiye Masihi atakaye tawala juu ya watu wa Mungu milele.
## Ufufuo ### Ufafanuzi Ufufuo ni kitendo cha kuwa hai tena baada ya kufa. * Kumfufua mtu inamaana kumrudisha mtu katika hali ya kuwa hai tena. Mungu pekee ndio mwenye nguvu ya kufanya hivi. * Neno "ufufuo" mara nyingi humwelezea Yesu aliyekuwa hai tena baada ya kufa. * Yesu aliposema "yeye ni ufufuo na uzima" alimaanisha kuwa yeye ni chanzo cha ufufuo na ndiye husababisha watu wawe hai tena.
## uovu ### Ufafanuzi Neno "uovu" ni neno ambalo liko karibu kwa maana na neno "dhambi," lakini inaweza kumaanisha zaidi matendo ya ufahamu mabaya au uovu mkubwa. Neno "uovu" ina maana halisi ya kupindisha au kupotosha (sheria). Inamaanisha udhalimu mkubwa. Uovu unaweza kuelezwa kama matendo ya kudhuru ya makusudi dhidi ya watu wengine. Maana zingine za uovu ni pamoja na "ukaidi" na "kunyima," ambayo yote ni maneno yanayoeleza hali za dhambi mbaya.
## Upatanisho, kulipia ### Ufafanuzi "Upatanisho au kulipia" inaonesha ni jinsi gani Mungu alitoa sadaka ili kulipia dhambi za watu. * Katika agano la kale Mungu aliruhusu upatanisho wa muda ufanyike kwa ajili ya utakaso wa dhambi za wana wa Israeli, ambapo ilitolewa sadaka ya damu iliyohusisha kuchinjwa kwa mnyama. * Katika agano jipya kifo cha Kristo msalabani ni upatanisho wa pekee na wa kudumu kwa ondoleo la dhambi. * Yesu alipokufa alichukua adhabu ya watu waliostahili adhabu ile kwa sababu ya dhambi.
## upendo ### Ufafanuzi Kumpenda mtu mwingine ni kumjali huyo mtu na kufanya vitu vitakavyo msaidia. Kuna maana tofauti za "upendo" ambazo lugha zingine zinawezakueleza kwa kutumia maneno tofauti: 1. Aina ya upendo utokao kwa Mungu unalenga kwa ajili ya mema ya wengine, hata kama hayamnufaishi mtu anayependa. Aina hii ya upendo inawajali watu bila kujali wanachokifanya. Mungu mwenyewe ni upendo na ndiye chanzo cha upendo wa kweli. Yesu alionesha aina hii ya upendo kwa kujitolea maisha yake kama sadak ili kutuokoa kutoka kwenye dhambi na mauti. Aliwafundisha pia wafuasi wake kuwapenda wengine kwa kujitolea. Watu wanapowapenda wengine na aina hii ya upendo, inahusisha matendo yanayoonesha kuwa mtu anafikiria yale yatakomsaidia mtu mwingine kufanikiwa. Aina hii ya upendo inahusisha zaidi kusamehe wengine. Katika ULB, neno "upendo" linamaanisha aina hiiya upendo wa kujitoa, isipokuwa noti ya tafsiri iashirie maana tofauti. 1. Neno jingine katika Agano Jipya linamaanisha upendo wa kindugu au upendo kwa ajili ya rafiki au mwana familia. Neno hili linamaanisha upendo wa asili wa binadamu kati ya marafiki na ndugu. Inawezekana kutumika katika mazingira kama, "Wanapenda kukaa kwenye viti muhimu katika sherehe." Hii inamaanisha "wanatamani sana" kufanya hivyo. 1. Neno "upendo" linaweza pia kumaanisha upendo wa kimapenzi kati ya mwanamme na mwanamke. 1. Katika hali ya kimithali, "Yakobo nimempenda, lakini Esau nimemchukia", neno "mpenda" linamaanisha Mungu kumchagua Yakobo kuwa katika mahusiano ya maagano na yeye. Hii inaweza pia kutafsiriwa kama "kuchaguliwa." Ingawa Esau alibarikiwa pia na Mungu, hakupewa heshima ya kuwa katika maagano. Neno "kuchukia" linatumika kimithali hapa kumaanisha "kukataliwa" au "kutokuchaguliwa."
## ushirika ### Ufafanuzi Kwa ujumla, msemo "ushirika" ina maana ya muingiliano wa kirafiki kati ya wanajumuiya wa kundi la watu ambao huwa na upendeleo na mambo ya kufanana. Katika Biblia, msemo "ushirika" mara kwa mara humaanisha umoja wa waumini katika Kristo. Ushirika wa Kikristo na uhusiano ambao waumini wanao baina yao kupitia uhusiano wao na Kristo na Roho Mtakatifu. Wakristo wa awali walionyesha ushirika wao kwa kusikiliza mafundisho ya Neno la Mungu na kuomba pamoja, katika kugawa vitu vyao, na kula milo pamoja. Wakristo pia wana ushirika na Mungu kupitia imani ndani ya Yesu na kifo chake cha kujitolea cha msalabani ambacho kilitoa mpaka kati ya Mungu na watu. Mapendekezo ya Tafsiri Njia za kutafsiri "ushirika" zinaweza kujumuisha "kugawana pamoja" au "uhusiano" au "umoja" au "jamii ya Kikristo"
## ushuhuda, shuhudia ### Ufafanuzi Maneno, "ushuhuda" na "shuhudia" yanaeleza kutamka tamko kuhusu kitu ambacho mtu anajua kuwa ni kweli. * Mara nyingi mtu anaye "shuhudia" kuhusu kitu alicho nacho amepitia moja kwa moja. * Shahidi anaye toa "ushahidi wa uongo" hasemi ukweli kuhusu kilicho tokea. * Wakati mwingine neno "ushuhuda" wa husu unabii ambao nabii amesema. * Katika Agano la Kale, hili neno linatumika mara kadhaa kueleza jinsi wafuasi wa Yesu wana shuhudia kuhusu matukio ya maisha ya Yesu, kifo, na ufufuo.
## utauwa, utauwa ### Ufafanuzi Msemo "utauwa" unatumika kumwelezea mtu ambaye hufanya matendo kwa njia ambayo humheshimu Mungu na kuonyesha jinsi Mungu alivyo. "Utauwa" ni sifa ya tabia ya kumheshimu Mungu kwa kufanya mapenzi yake. Mtu ambaye ana tabia ya kiutauwa ataonyesha matunda ya Roho Mtakatifu, kama vile upendo, furaha, amani, uvumilivu, upole na kiasi. Sifa ya utauwa inaonyesha ya kwamba mtu ana Roho Mtakatifu na anamtii. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "watauwa" unaweza kutafsiriwa kama "watu wenye utauwa" au "watu ambao wanamtii Mungu"
## utawala ### Ufafanuzi Msemo wa "utawala" una maana ya nguvu, madaraka, au mamlaka juu ya watu, wanyama, au nchi. Yesu Kristo anasemekana kuwa na utawala juu ya nchi yote, kama nabii, kuhani na mfalme. Utawala wa Shetani umeshashindwa milele na kifo cha Yesu Kristo juu ya msalaba. Katika uumbaji, Mungu alisema ya kwamba mtu anatakiwa kuwa na utawala juu ya samaki, ndege, na viumbe wote juu ya nchi. Mapendekezo ya Tafsiri Kutegemea na muktadha, njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "mamlaka" au "nguvu" au "madaraka". Msemo "kuwa na utawala juu ya" unaweza kutafsiriwa kama "tawala juu ya" au "simamia".
## utukufu, fahari ### Ufafanuzi Kwa ujumla, msemo "utukufu" una maana ya heshima, fahari, na ukuu wa hali ya juu sana. Kitu chochote ambacho kina utukufu kinasemekana kuwa na "fahari". Mara nyingi, "utukufu" ina maana ya kitu chenye thamani kubwa na umuhimu. Katika muktadha zingine inawasilisha ufahari, mwanga, au hukumu. Kwa mfano, msemo "utukufu wa wafugaji" una maana ya malisho yaliyostawi sana ambapo kondoo wao walikuwa na nyasi nyingi za kula. Utukufu haswa hutumika kumfafanua Mungu, ambay ana ufahari zaidi ya yeyote au chochote katika ulimwengu. Kila kitu katika tabia yake huonyesha utukufu na ufahari wake. Msemo "kutukuzwa na" una maana ya kujidai juu ya au kujivunia na kitu.
## Uzinzi, zinaa, mzinifu, mzinzi ### Ufafanuzi Neno "uzinzi" hii ni dhambi ambayo inahusisha mwanandoa ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye sio mwenza wake. * "Mzinifu" ni mtu yeyote anayefanya uzinzi. * Mara nyingine mzinzi hutumika kuonesha kuwa ni mwanamke ndiye anayefanya uzinzi. * Uzinzi huvunja ahadi ambayo mke na mume wamewekeana katika agano la ndoa. * Mungu aliwaamuru Wana wa Israeli wasizini. * Pia "zinaa" hutumika kama lugha ya picha kuwaelezea wana wa Israeli namna ambavyo hawakuwa waaminifu kwa Mungu, hasa walipokuwa wakiabudu miungu mingine.
## vuka mpaka, kosa ### Ufafanuzi Maneno "vuka mpaka" na "kosa" ina eleza kuvunja amri, sheria. * Kifumbo, "vunja mpaka" yaweza elezwa kama "vuka mstari," yani, kwenda zaidi ya kiwango, kilicho wekwa kwa wema wa huyo mtu na wengine. * Maneno "vuka mpaka," "dhambi" "kosa," yote ina maana ya kutenda dhidi ya mapenzi ya Mungu na kutotii amri zake.
## Waebrania ### Ufafanuzi 'Waebrania' walikuwa ni watu wa uzao wa Ibrahimu kupitia kwa Isaka na Yakobo. Ibrahimu ni mtu wa kwanza kuitwa 'mwebrania' katika Biblia. Neno 'kiebrania' linarejelea pia lugha ambayo waebrania wanaongea. Agano la kale liliandikwa kwa lugha ya Kiebrania. Katika sehemu mbalimbali za Biblia, Waebrania waliitwa 'Wayahudi,' au 'Waisraeli' Ni vizuri kutunza maneno yote matatu katika muktadha wake, kwa kuwa majina yote matatu yanazungumzia kundi moja la watu.
## Wakfu ### Ufafanuzi Kuweka wakfu ni kutenga kitu fulani au watu ili wamtumikie Mungu. Kitu au vitu vinavyowekwa wakfu ni vitakatifu na vinatengwa kwa ajili ya Mungu. * Maana yaneno hili ni sawa na "kutakasa" lakini maana ya zaidi ni kumtenga mtu kwa ajili ya kumtumikia Mungu. * Vitu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya Mungu ni pamoja na wanyama, madhabahu ya kuteketezea dhabihu na maskani. * Watu waliowekwa wakfu kwa Mungu ni pamoja na makuhani, wana wa Israeli na watoto wa kwanza wa kiume .
## wale kumi na mbili, wale kumi na moja ### Ufafanuzi Neno "wale kumi na mbili" la husu wanaume kumi na mbili Yesu aliyo wachagua kuwa wanafunzi wake wa karibu. Baada ya Yuda kujiua, waliitwa "wale kumi na moja." * Yesu alikuwa na wanafunzi wengi, lakini jina "wale kumi na mbili" liliwa tofautisha waliyo mfuata kipindi chote cha miaka mitatu ya huduma. * Majina ya hawa kumi na mbili yameorodheshwa katika Mathayo 10, Marko 3, na Luka 6. * Wakati mwingine baada ya Yesu kurudi mbinguni, "wale kumi na moja" walimchagua wanafunzi jina lake Mathiasi kuchukuwa nafasi ya Yuda. Kisha wakaitwa "wale kumi na mbili" tena.
## wana wa Mungu ### Ufafanuzi Jina, "wana wa Mungu" ni msemo wa mfano wenye maana kadhaa. * Katika Agano Jipya, maneno "wana wa Mungu" ya husu waamini katika Yesu na mara nyingi utafsiriwa kama "watoto wa Mungu" maana ina jumuisha wakiume na wakike. * Haya matumizi ya jina la zungumzia mahusiano na Mungu ambayo ni kama mahusiano kati ya mwana na baba. * Katika Mwanzo 6, baadhi ya watu wanatafsiri "wana wa Mungu" kama malaika waliyo hasi, yani, roho chafu au mapepo. Wengine wanadhani inaweza maanisha viongozi wenye nguvu wa kisiasa au wazao wa Sethi. * Katika Agano la Kale, neno "wana wa Mungu" la husu waamini wote wa Yesu na mara nyingi utafsiriwa kama "watoto wa Mungu." * Jina, "Mwana wa Mungu" ni neno tofauti, linalo mtaja Yesu, ambaye ni Mwana wa Mungu
## watakatifu ### Ufafanuzi Neno "watakatifu" lina maana ya halisi ya "waliyo wasafi" na kueleza waamini wa Yesu. * Baadae katika historia ya Biblia, mtu aliye julikana kwa kazi yake njema alipewa cheo "mtakatifu," lakini sivyo jinsi hili neno lilitumika katika Agano Jipya. * Waamini katika Yesu ni watakatifu au waliyo wasafi, sio kwasababu kwa walicho fanya, lakini bali kupitia imani katika kazi ya kuokoa ya Yesu Kristo. Yeye ndiye anao wafanya kuwa wasafi.
## Watoto, mtoto ### Ufafanuzi Katika Biblia mtoto limetumika kwa namna ya jumla kuelezea mtu ambaye ni mdogo kwa umri. Watoto ni wingi wa neno mtoto. * Katika Biblia wanafunzi na wafuasi mara nyingine waliitwa watoto. * Watoto pia hutumika kuelezea uzao wa mtu. * Watoto wa mara nyingine hutumika kuelezea kitu fulani. kwa mfano * Watoto wa nuruni. * Watoto watii * Watoto wa muovu * Neno hili pia linaweza kumaanisha watu ambao ni watoto wa kiroho. Kwa mfano "Watoto wa Mungu" ni watu wa Mungu wenye imani kwa Yesu.
## Watu wa Mungu, watu wangu ### Ufafanuzi "Watu wa Mungu" ni watu ambao Mungu aliwaita toka duniami ili wawe na mahusiano ya kipekee naye. * Mungu anaposema "watu wangu" anazungumza juu ya watu aliowachagua na wenye uhusiano naye. * Watu wa Mungu wanachaguliwa na yeye na wanatengwa na ulimwengu ili kuishi maisha yanayompendeza yeye. Pia anawaita watoto wake. * Katika agano la kale "watu wa Mungu" ni taifa la Israeli ambao walichaguliwa na Mungu na kutengwa toka kwenye mataifa mengine ya ulimwengu ili wamtumikie na kumtii yeye. * Katika agano jipya "Watu wa Mungu" ni watu wote wanaomwamini Yesu na wanaitwa kanisa. Hii inajumuisha Wayahudi na Mataifa.
## wema, uzuri ### Ufafanuzi Neno "uzuri" una maana nyingi kutegemea na muktadha. Lugha nyingi hutumia maneno tofauti kutafsiri maana hizi tofauti. Kwa ujumla, kitu ni kizuri kama kinalingana na tabia ya Mungu, kusudi na mapenzi. Kitu ambacho ni "kizuri" kinaweza kufurahisha, bora, msaada, kinachofaa, chenye manufaa, au sahihi kimaadili. Ardhi ambayo ni "nzuri" inaweza kuitwa "yenye rutuba" au "yenye kuzaa". Zao "zuri" linaweza kuwa zao "la wingi". Mtu anaweza kuwa "mzuri" katika kile afanyacho kama ana ujuzi katika kazi yao, yaani "mkulima mzuri". Katika Biblia, maana ya jumla ya "nzuri" mara nyingi hutofautishwa na "uovu". Msemo "wema" mara nyingi humaanisha kuwa mzuri kimaadili kwa kutoa mambo mazuri na yenye manufaa. Inaweza kumaanisha utimilifu wake wa kimaadili.
## wito, kuita, ita ### Ufafanuzi wito, kuita ni kitendo cha kusema kitu kwa nguvu kwa mtu ambaye hayuko karibu. Pia kuna maana mbali mbali kama * Kuita mtu inamaana ya kupiga kelele au kuongea kwa sauti na mtu aliye mbali. Pia yaweza kuwa na maana ya kuomba msaada hasa kwa Mungu. * "wito" katika Biblia mara nyingi huwa na maana ya "kumwita" au "kuamuru aje" au "kumuomba aje." * Mungu huwaita watu kwake na kuwa watu wake. Huu ni wito wao. * Neno "kuitwa" limetumika kwenye Biblia kumaanisha kuwa Mungu aliwachagua au kuwateua watu kuwa watoto wake, watumishi wake na wasemaji wa ujumbe wa ukombozi kupitia Yesu. * Pia neno hili hutumika kwenye mukhtadha wa kumuita mju jina. Kwa mfano "Anaitwa Yohana," au "Jina lake ni Yohana." * "Nimekuita kwa jina lako" inamaana kuwa Mungu anafahamu jina la mtu na amemchagua yeye.
## wivu ### Ufafanuzi Neno "wivu" inaashiria hamu kubwa ya kulinda usafi wa uhusiano. Inaweza pia kumaanisha hamu kubwa ya kumili kitu au mtu. Msemo huu mara nyingi unatumika kuelezea hisia ya hasira ambayo mtu anayo juu ya mwenzi wake ambaye amekuwa sio mwaminifu katika ndoa yao. Inapotumika katika Biblia, neno hili huwa humaanisha hamu kubwa ya Mungu kwa watu wake kubaki watakatifu na kutochafuliwa na dhambi. Mungu ana "wivu" kwa ajili ya jina lake, kwamba litunzwe kwa utukufu na heshima. Maana nyingine ya wivu inahusisha kuwa na hasira kwa kuwa mtu mwingine ana mafanikio au ana umaarufu zaidi. Hii ina maana ya kukaribiana na neno "husuda."
## woe ### Ufafanuzi Ole ni hisia za dhiki kubwa. Pia inatupa onyo kuwa mtu fulani atapata shida kubwa. * Neno "ole wa" inafuatiwa na onyo kwa watu kuwa watapata mateso kama adhabu ya dhambi zao. * Sehemu mbalimbali katika Biblia neno "ole" limerudiwa ili kusisitiza hukumu mbaya inayokuja. * Mtu anaposema "ole wangu mimi" inaelezea huzuni ya mateso anayopitia.
## woga, hofu, hofu ya Yahwe ### Ufafanuzi Msemo "woga" au "hofu" ina maana ya hisia zisizo nzuri mtu huwa nazo ambapo kuna tishio la kudhuriwa kwake au kwa wengine. Msemo "hofu" unaweza kumaanisha heshima kubwa na hofu mtu huwa nayo kwa mamlaka. Msemo "hofu ya Yahwe" na misemo ya kufanana "hofu ya Mungu" an "hofu ya Bwana" ina maana ya kumheshimu sana Mungu na konyesha heshima kwa kumtii yeye. Hofu hii inahamasishwa kwa kujua ya kwamba Mungu ni mtakatifu na anachukia dhambi. Biblia inafundisha ya kwamba mtu anayemwogopa Yahwe atakuwa na hekima. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, "kuwa na hofu" kunaweza kutafsiriwa kama "kuogopa" au "kuheshimu sana" au "kuhofu" au " kuwa na hofu ya" Msemo "woga" inaweza kutafsiriwa kama "kuogopa". Sentensi, "Hofu ya Mungu ilianguka juu yao wote" inaweza kutafsiriwa kama, "Ghafla wote wakapatwa na hofu kuu na heshima kwa Mungu" au "Mara ghafla wote wakahisi kushangazwa sana na kumhofu Mungu sana" au "Wakati huo huo, wote wakapatwa na hofu ya Mungu"
## Yaweh ### Ufafanuzi Yaweh ni jina la Mungu alilolithihirisha alipozungumza na Musa katika kichaka kinachowaka moto. * Jina Yaweh linatokana na neno lenye maana ya "kuwepo." * Maana nyingine ya Yaweh ni "Niko" au "anayesababisha kuwepo." * Jina hili linadhihirisha kuwa Mungu alikuwepo na ataendelea kuishi daima. Pia inamaanisha kuwa yupo sasa. * Tafsiri nyingi za Biblia zimetumia neno "BWANA" kuwakilisha Yaweh. Biblia za kisasa zimeandika BWANA kwa herufi kubwa kuonesha heshima kwa jina la Mungu na kutofautisha na Bwana ambayo ilitumika katika maneno ya Kiebrania.
## Yesu, Yesu Kristo, Kristo Yesu ### Ufafanuzi Yesu ni mwana wa Mungu. Jina "Yesu" linamaanisha, "Yahwe anaokoa." Neno "Kristo" ni jina linalomaanisha "mtiwa mafuta" na ni jina jingine la Masihi. Majina mawili mara nyingi yanaunganishwa kama "Yesu Kristo" au "Kristo Yesu." Majina haya yanasisitiza kuwa mwana wa Mungu ndiye Masihi aliyekuja kuwaokoa watu kutoadhibiwa milele kwa dhambi zao. Katika njia za kimiujiza, Roho Mtakatifu alisababisha mwana wa milele wa Mungu kuzaliwa kama binadamu. Wazazi wake wa duniani waliambiwa na malaika kumuita "Yesu" kwa sababu alikusudiwa kuwaokoa watu kutoka katika dhambi zao. Yesu alifanya miujiza mingi iliyoonesha kuwa yeye ni Mungu na ni Kristo, au Masihi.
## Zaburi ### Ufafanuzi Zaburi ni nyimbo takatifu ambazo zipo kwenye mfumo wa ushairi zilizoandikwa ili ziimbwe. * Katika agano la kale kitabu cha Zaburi kina mkusanyiko wa nyimbo hizo zilizoandikwa na mfalme Daudi na Waisraeli wengine kama Musa, Sulemani na Asafu. * Zaburi zilitumiwa na taifa la Israeli katika kumwabudu Mungu. * Zaburi zilitumika kuelezea furaha, imani na heshima pamoja na maumivu na maombolezo. * Katika agano jipya Yesu aliwaelekeza waimbe Zaburi kwa Mungu kama njia ya kumwabudu yeye.
## zawadi ### Ufafanuzi Msemo "zawadi" una maana ya kitu chochote ambacho hupewa au kutolvwa kwa mtu. Zawadi inatolewa bila matarajio ya kurudishiwa kitu chochote. Pesa, chakula, mavazi, au vitu vingine zitolewazo kwa watu maskini zinaitwa "zawadi". Katika Biblia, sadaka itolewayo kwa Mungu pia hujulikana kama zawadi. Zawadi ya wokovu ni kitu ambacho Mungu anatupatia kupitia imani kwa Yesu. Katika Agano Jipya, msemo "zawadi" pia hutumika kumaanisha uwezo maalumu wa kiroho ambao Mungu hutoa kwa Wakristo wote kutumikia watu wengine. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo wa jumla wa "zawadi" unaweza kutafsiriwa na neno au msemo ambao una maana ya "kitu ambacho kinatolewa". Katika muktadha wa mtu kuwa na zawadi au uwezo maalumu ambao unatoka kwa Mungu, msemo "zawadi kutoka kwa Roho" unaweza kutafsiriwa kama "uwezo wa kiroho" au "uwezo maalumu kutoka kwa Roho Mtakatifu" au "kipaji maalumu cha kiroho ambacho Mungu ametoa"