Daniel
Daniel 1
Daniel 1:1-2
Nebukadneza
Jina hili humrejelea Nebukadneza na wanajeshi wake, siyo yeye peke yake.
kuzuia mahitaji yake yote
"Kuwazuia watu wasipokee mahitaji"
Yehoyakimu mfalme wa Yuda
Hii inamrejelea Yehoyakimu na wanajeshi wake, siyo Yehoyakimu peke yake.
alimpatia
Yehoyakimu alimpa Nebukadneza
alivipeleka ...aliviweka
Ingawa Nebukadneza hakufanya vitu hivi peke yake, ni vizuri kwa msomaji kutumia umoja tu.
Alivipeleka
Kiwakilishi 'vi' kinarejelea vitu/vifaa vitakatifu vilivyochukuliwa kutoka Yerusalemu.
hazina ya mungu wake
Hiki kitendo kilikuwa na ibada kwa mungu wake
Daniel 1:3-5
mfalme akamwambia
inmrejelea Nebukadneza
Ashipenazi
Huyu alikuwa na afisa wake mkuu
kiungwana
hili ni tabaka la juu sana la kijamii
wasio na hila
Maneno haya mawili ya kukanusha kwa pamoja yametumika kutilia mkazo wazo chanya. "wenye mwonekano kamili"
wenye kujawa na ufahamu na weledi
Hii ni nahau. Hii ina maana ya kwamba walijua vitu vingi na waliweza kupanga na kutumia maelezo yale.
ikulu ya mfalme
Hii ni nyumba au jengo kubwa mahali ambapo mfalme aliishi
Alitakiwa kuwafundisha
"Ashipanezi alitakiwa kuwafundisha"
Mfalme aliwatengea kwa ajili yao
Maafisa wa mfalme walifanya hivyo kwa niaba ya mfalme.
chakula kizuri
Chakula maalumu, adimu na kizuri ambacho mfalme alikula.
Vijana hawa walitakiwa kufunzwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Ashipenazi alitakiwa kuwafunza vijana hawa"
kufunzwa
"kufundisha maarifa"
Daniel 1:6-7
miongoni mwao
Miongoni mwa vijana kutoka Israeli
Afisa mkuu
Inamrejelea Ashipenazi aliyekuwa afisa wa juu sana katika utawala wa Mfalme Nebukadneza.
Belteshaza...Shadraka...Meshaki...Abednego
Haya yote ni majina ya wanaume.
Daniel 1:8-10
Danieli alinuia katika akili yake
Hapa neno "akili" linamrejelea Danieli mwenyewe. "Danieli aliamua mwenyewe"
asingejitia ujanisi
"kujitia unajisi" ni kukifanya kitu fulani kuwa kichafu. Baadhi ya vyakula na vinywaji vya Kibabeli vingemfanya Danieli kuwa mchafu kutokana na sheria za Mungu.
chakula kizuri
Hii inarejelea chakula maalumu,adimu na kizuri ambacho mfalme alikula.
Kwa nini awaone ninyi mkiwa mnaonekana vibaya kuliko vijana wengine wa umri wenu?
Afisa allitumia swali hili ili kuelezea kile alichodhani kuwa kingetokea. Pia yaweza kuwa maelezo kama "Hataki kuwaoneni ninyi mkionekana kuwa wabaya zaidi ya vijana wengine wa umri wenu"
Mfalme aweza kukitwaa kichwa changu
Hii ni nahau "Mfalme aweza kukikata kichwa changu" au "Mfalme aweza kuniua"
Daniel 1:11-13
ulinganishe mwonekano wetu na mwonekano
Danieli alimwomba msimamizi kuangalia kama yeye na rafiki zake walionekana vibaya kuliko vijana wengine.
Daniel 1:14-16
aliwajaribu...mwonekano wao...ulikuwa...vyakula ..na vinywaji vyao
Viwakilishi hivi vyote vinawarejelea akina Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria.
wenye afya
Hii ina maana kwamba walikuwa wenye afya nzuri kutokana na kile walichokula.
Daniel 1:17-18
Mungu aliwapa uelewa na ufahamu
Hii inaweza kuongezwa ili kwamba nomino dhahania "Uelewa na ufahamu" zaweza kuelezwa kwa kutumia vitenzi "kujifunza na kufahamu" yaani "Mungu aliwapa uwezo wa kujifunza na kufahamu kwa uwazi"
maandiko yote na hekima
Haya ni maneno ya kutia chumvi kuonesha kwamba walikuwa na elimu na ufahamu mzuri
Daniel 1:19-21
Mfalme aliongea nao
Mfalme aliongea na vijana wanne (1:17)
miongoni mwa kundi lote hapo hapakuwa na wa kuwalinganisha na akina Danieli,Hanania, Mishaeli, na Azaria
Hii yaweza kuelezwa kwa kutumia muundo kubalifu. "Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria walimfurahisha sana zaidi ya mtu yoyote katika kundi"
"Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria
Haya ni majina ya wanaume.
mara kumi zaidi
hapa maneno "mara kumi" yanatia chumvi kumaanisha ubora wa hali.
kwanza wa Mfalme Koreshi
"mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi alitawala Babeli."
Daniel 2
Daniel 2:1-2
katika mwaka wa pili
"ndani ya mwaka wa pili"
alikuwa na ndoto
"Nebukadneza aliota ndoto"
akili yake ilisumbuka
Hapa neno "akili" linarejelea mawazo yake. "mawazo yake yalimsumbua"
na hakuweza kulala
Mawazo yake yaliyomsumbua yalimzuia asipate usingizi.
Ndipo mfalme alipowaita waganga
"kisha mfalme aliwaita waganga"
wafu
"watu waliokwisha kufa"
walikuja
"waliingia ndani ya ikulu"
walisimama mbele
"walisimama mbele ya "
Daniel 2:3-4
akili yangu ina mashaka
hapa neno "akili" linamrejelea mfalme mwenyewe.
mashaka
"kusumbuka"
Kiaramaiki
Hii ni lugha ambayo watu wa Babeli waliiongea.
" Mfalme, aishi milele!
Watu waliyasema maneno haya kuonesha heshima kwa mfalme. "Mfalme, tunatumaini utaishi milele"
sisi, watumishi wako
Watu walijiita wao wenyewe kuwa ni watumishi wa mfalme kuonesha heshima.
tutaifunua
Hapa kiwakilishi 'tu' kinarejelea watu/wanaume ambao mfalme alikuwa akiongea nao na hakimjumuishi mfalme.
Daniel 2:5-6
Jambo hili limeshamalizika
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Nimeamua cha kufanya juu ya jambo hili"
miili yenu itakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vichuguu vya uchafu
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Nitawaamuru wanajeshi wangu kukata miili yenu katika vipande na kuzifanya nyumba zenu kuwa vichuguu vya uchafu"
mtapokea zawadi kutoka kwangu
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Nitawapeni zawadi"
Daniel 2:7-9
Mfalme na atuambie
Watu wenye hekima walimweleza mfalme kwa nafsi ya tatu kama ishara ya heshima.
mmeona maamuzi yangu ni magumu kuhusu jambo hili
Maamuzi ambayo hayatabadilika yanasemwa kama ni kitu ambacho ni imara. "mmeona kwamba sitabadili maamuzi yangu juu ya hili"
kuna sentensi moja tu kwa ajili yenu
"kuna hukumu moja kwa ajili yenu"
uongo na maneno ya kudanganya
Maneno haya mawili kwa ukaribu yanamaanisha kitu kile kile na kutia mkazo kwamba huu ni "uongo uliokusudia kudanganya."
Daniel 2:10-11
mkuu na mwenye nguvu
Maneno haya mawili kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na kutia mkazo juu ya ukubwa wa nguvu za Mfalme.
hakuna yeyote awezaye kumwambia mfalme isipokuwa miungu
Maneno haya hameelezwa kwa kukanusha kwa ajili ya kutia mkazo. Yaweza pia kuelezwa kwa sentensi chanya. "Ni miungu tu yaweza kumwambia mfalme hili"
Daniel 2:12-13
kasirike na kughadhabika
Maneno haya kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na kutia mkazo juu ukali wa hasira yake.
wale wote katika Babeli
"watu wote katika Babeli"
Hivyo, amri ilitoka
Amri inaongelewa kama ni kitu chenye uhai na chenye uwezo wa kwenda nje. "Mfalme aliipitisha amri"
wale wote waliojulikana kwa hekima yao ni lazima wauawe
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Wanajeshi walitakiwa kuwaua watu wote waliojulikana kwa hekima zao"
ili kwamba wauawe
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "kwa lengo la kuwaua"
Daniel 2:14-16
busara na umakini
Maneno haya mawili kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na kutia mkazo juu ya ukubwa wa busara.
Arioki
Hili ni jina la kamanda wa mfalme.
walinzi
Hili ni kundi la watu ambao kazi yaoni kumlinda mfalme
ambaye alikuwa amekuja kuwaua
ambaye mfalme alikuwa amemtuma ili kuua"
Danieli aliingia ndani
Huenda Danieli alienda katika ikulu. "Danieli alienda katika ikulu"
akaomba ahadi ya muda wa kuonana na mfalme
"aliomba muda maalumu uliopangwa ili kukutana na mfalme"
Daniel 2:17-18
nyumba yake
Hii inarejelea nyumba ya Danieli
kile kilichotokea
"kuhusu amri ya mfalme"
Aliwasihi kutafuta rehema
"Aliwaomba waombe huruma"
ili kwamba yeye na wao wasije wakauawa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Ili kwamba mfalme asije akawaua"
Daniel 2:19-20
Usiku ule siri ilifunuliwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Usiku ule Mungu aliifunua siri"
siri
hii inarejelea ndoto ya mfalme na tafsiri yake.
"Litukuzwa jina la Mungu
Hapa"jina" linamrejelea Mungu mwenyewe. "Mungu atukuzwe"
Daniel 2:21-22
Maelezo ya jumla
Mistari hii pia ni sehemu ya sala ya Danieli.
anaondoa wafalme
"huyaondoa mamlaka ya kifalme ya kutawala"
kuweka wafalme katika viti vyao vya enzi
Kuwa katika kiti cha enzi ina maana ya kutawala ufalme. "huwafanya wafalme wapya kutawala juu ya falme zao."
naye anaishi pamoja na mwanga.
"Mwanga hutoka sehemu ambako Mungu aliko"
Daniel 2:23
Maelezo ya jumla
Mstari huu pia ni sehemu ya sala ya Danieli. Aliacha kumwongelea Mungu kwa nafsi ya tatu na alianza kutumia nafsi ya pili.
umeyafanya yawe wazi kwetu yale tuliyokuomba
"aliniambia marafiki zangu na nilikuomba utuambie."
umetujulisha mambo yamhusuyo mfalme
"alituambia kile ambacho mfalme alitaka kujua"
Daniel 2:24
Arioki
Hili ni jina la Kamanda wa Mfalme.
kila mtu aliyekuwa na hekima
"watu wenye hekima"
Daniel 2:25-26
Beliteshaza
Hili ni jina ambalo Wababeli walimpa Danieli.
Daniel 2:27-28
Siri ambayo mfalme ameiomba haiwezi kufunuliwa na watu wenye hekima, wala wale wenye kuongea na wafu, wala wachawi, na wala wataalamu wa nyota
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Wale wenye hekima, wale wenye kuongea na wafu, waganga na wanajimu hawawezi kufunua siri kuhusu kile mfalme alichokiomba"
Siri ambayo mfalme ameiomba
Kirai hiki knarejelea ndoto ya mfalme.
Daniel 2:29-30
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na Mfalme
yule afichuaye siri
Kirai hiki kinamrejelea Mungu. "Mungu ambaye hufunua siri"
siri hii haikufunuliwa kwangu
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu hakuifunua siri hii kwangu"
Siri hii imefunliwa kwangu ili kwamba wewe
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji.
Amefunua siri hii kwangu ili kwamba wewe
Kirai hiki kinatumia kiwakilishi "wewe" kumrejelea mtu katika akili.
Daniel 2:31-33
Maelezo ya jumla
Daniel anaendelea kuongea na mfalme
kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi
"kilikuwa cha dhahabu safi" au "ilikuwa dhahabu nzuri"
sehemu chuma na sehemu kwa udongo
"ilikuwa kwa sehemu chuma na sehemu nyingine udongo"
Daniel 2:34-35
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na mfalme.
jiwe lilikuwa limechongwa, ingawa si kwa mikono ya wanadamu, na lili...
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji kama yatagawanywa katika sehemu mbili. "mtu fulani alilikata jiwe kutoka mlimani, lakini si mtu aliyelikata jiwe. Jiwe..."
kama makapi yaliyo katika sakafu za kupuria kipindi cha kiangazi
kirai hiki kinalinganisha vipande vya sanamu na vitu vidogo vilivyo vyepesi na ambavyo vinaweza kupeperushwa mbali na upepo. "kama vipande vikavu vya nyasi vinavyopeperushwa na upepo"
hakuna alama inayoachwa
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo chanya. "viliondolewa kabisa"
kuijaza dunia yote
"kuenea dunia yote"
Daniel 2:36-38
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na mfalme
Na sasa tutamwambia mfalme
Hapa kiwakilishi "tu" kinamrejelea Danieli peke yake. Inawezekana ametumia muundo wa wingi katika unyenyekevu kuepuka kuchukua heshima kwa kujua maana ya ndoto ambayo Mungu ameifunua kwake.
mfalme wa wafalme
"mfalme wa muhimu sana" au "mfalme anayetawala juu ya wafalme wengine"
nguvu, uweza
Maneno haya kimsingi yanamaanisha kitu kile kile.
Amevitia mkononi mwako
Hapa neno "mkono'' linarejelea utawala. "amekupa utawala"
sehemu ambazo binadamu huishi
sehemu imetumika kuwakilisha watu ambao wanaishi hapo.
Amekupa wanyama wa mwituni na ndege wa angani katika mkono wako,
Hapa neno "mkono" linarejelea utawala. "Amekupa utawala juu ya wanyama wa mwituni na ndege wa angani"
ndege wa angani
hapa neno "angani" limetumika kumaanisha mbinguni.
Wewe u kichwa cha dhahabu cha sanamu
Katika ndoto ya mfalme kichwa cha sanamu kinamwakilisha mfalme. "Kichwa cha dhahabu kinakumaanisha wewe mfalme"
Daniel 2:39
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na mfalme
ufalme mwingine utainuka
Katika ndoto ya mfalme ilionekana kwamba ufalme wake ni wa dhahabu, hivyo ufalme mdogo utakuwa wa shaba. "ufalme mwingine ambao ni shaba utainuka"
hata ufalme wa tatu wa shaba
"bado ufalme wa tatu ambao ni wa shaba" au kisha bado kuna ufalme mwingine ambao unawakilishwa na shaba katika sehemu ya sanamu"
Daniel 2:40
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na mfalme
kutakuwa na ufalme wa nne
"kutakuwa na ufalme wa namba ya nne''
wenye nguvu kama chuma
Ufalme wa nne unaongelewa kuwa na nguvu kama chuma
Itaviharibu vitu hivi vyote na kuvisaga.
Lugha hii mfano inamaana ya kwamba ufalme wa nne utashinda na kuchukua nafasi ya falme zingine.
vitu hivi vyote
"falme zilizopita/zilizotangulia"
Daniel 2:41-43
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na mfalme
kama vile ulivyoona
Nebukadneza alione miguu iliyo na udongo na chuma. Hakuweza kuona mchakato wa utengenezaji wa miguu.
vilikuwa kwa sehemu vimetengenezwa kwa udongo na kwa sehemu vimefanywa kwa chuma,
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ilikuwa ya mchanganyiko wa udongo na chuma"
hawatakaa kwa pamoja
"hawatabaki wameshikamana"
Daniel 2:44-45
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na mfalme
katika siku za wafalme hao
Katika kifungu hiki maneno "wafalme hao" yanawarejelea watawala wa falme zinazooneshwa katika sehemu mbalimbali za sanamu
ambao hautaweza kuangushwa, wala kushindwa na watu wengine
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " kwamba hakuna hata mmoja ambaya ataangamizwa, na ya kwamba watu wengine hawatashinda."
jiwe lilichongwa kutoka katika mlima, lakini si kwa mikono ya wanadamu
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "mtu fulani alilikata jiwa kutoka mlimani, lakini si mtu aliyelikata"
kuaminika
aminifu na sahihi
Daniel 2:46-47
alianguka kifudifudi
Tendo hili linaonesha kwamba mfalme alikuwa anamheshimu Danieli. "lala chini huku kichwa kimeelekea chini."
sadaka zitolewe na manukato yatolewe kwake
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Watumishi wake walitoa sadaka na kutoa manukato kwa Danieli."
Hakika Mungu wako
"Ni kweli kwamba Mungu wako"
Mungu wa miungu, Bwana wa wafalme,
"mkuu kuliko miungu mingine, na mfalme juu ya wafalme wengine wote"
ambaye hufunua mafumbo
"yeye ambaye hufunua siri"
kufumbua mafumbo haya
"kufunua siri za ndoto yangu"
Daniel 2:48-49
Alimfanya kuwa mtawala
"Mfalme alimfanya Danieli kuwa mtawala"
Shadraka...Meshaki....Abeddinego
Haya yalikuwa ni majina ya Kibabeli waliyopewa vijana watatu wa Kiyahudi walikuwa wameletwa Babeli pamoja na Danieli.
Daniel 3
Daniel 3:1-2
urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa sita.
"urefu wa takribani mita 27 na upana upatao mita tatu"
uwanda wa Dura
Hii ni sehemu ndani ya ufalme wa Babeli.
magavana wote wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji
Haya ni madaraja ya mamlaka juu ya himaya ya ukubwa fulani.
wahazini
hawa ni maafisa walikuwa wanawajibika kwa mambo ya fedha
sanamu aliyokuwa ameiweka
hii inamhusu Mfalme Nebukadneza ambaye aliweka sanamu iliyojengwa kana kwamba alijijenga mwenyewe. "Sanamu ambayo Nebukadneza aliwaagiza watu wake kuiweka."
Daniel 3:3-5
magavana wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana
Angalia ulivyotafsiri katika 3:1
sanamu ambayo Nebukadneza aliyokuwa ameiweka
hii inamhusu Mfalme Nebukadneza ambaye aliweka sanamu iliyojengwa kana kwamba alijijenga mwenyewe. "Sanamu ambayo Nebukadneza aliwaagiza watu wake kuiweka."
mtangazaji
Huyu mtu ni mjumbe maalumu wa mfalme
mmeamriwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mfalme anawaagizeni ninyi"
zeze
Hivi ni vyombo vya muziki ambavyo ni sawa na vinubi. Muundo wake ni wa pembe tatu na vina nyuzi nne.
kuanguka na kuisujudia ninyi wenyewe
Haya ni matendo ya alama ya kuabudu.
Daniel 3:6-7
Na yeyote asiyeanguka na kuiabuda, kwa wakati huo huo atatupwa katika tanuru la moto
Sentensi hii yaweza kuandikwa kwa muundo tendaji. " Wanajeshi watamtupa katika tanuru liwakalo moto mtu yeyote ambaye hataanguka na kuabudu sanamu katika muda ule watakaposikia muziki."
kuanguka
Hili ni tendo linaloonesha alama ya kuabudu.
tunuru liwakalo moto
Hiki ni chumba kikubwa kilicho jazwa moto
watu wote, mataifa na lugha
Maneno haya yanajumuisha kundi kubwa la maafisa kutoka katika miko mbalimbali waliokuwapo hapo.
sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki,
Hivi ni vyombo vya muziki.
walianguka na kuisujudia wao wenyewe
Haya ni matendo yanayoonesha ibada.
sanamu ya dhahabu ambayo Nebukadneza mfalme alikuwa ameiweka.
Hii inaongelea juu ya Mfalme Nebukadneza kutoa agizo kwamba ijengwe sanamu kana kwamba aliijenga mwenyewe. "Sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza aliwaagizawatu wake waiweke."
Daniel 3:8-10
mfalme aishi milele
Hii ilikuwa na salamu ya kawaida kwa mfalme
auti ya pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari, na aina zote za muziki,
Angalia ulivyotafsiri orodha hii katika 3:3
kuanguka na kuisujudia sanamu ya dhahabu.
Haya ni matendo ya kuabudu.
Daniel 3:11-12
Mtu yeyote asiyeanguka na kuiabudu sharti atupwe katika tanuru linalowaka moto
Tungo hii yaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. "Wanajeshi watawatupa katika tanuru liwakalo moto mtu yeyote ambaye hatalala chini na kuabudu."
kuanguka chini
Hili ni tendo la ishara ya kuabudu
tanuru la moto
Hiki ni chumba kikubwa chenye moto mkali
masuala
"mambo" au "shughuli"
Shadraka, Meshaki, na Abednego
Haya yalikuwa ni majina ya Kibabeli ya vijana watau wa Kiyahudi ambao walikuwa ni marafiki wa Danieli.
hawakutii wewe
"hawakusikilizi wewe"
kuisujudia wenyewe
Hii ni ishara ya tendo la kuabudu
sanamu ya dhahabu ambayo umeiweka
Hii inazungumzia juu ya mfalme Nebukadneza kutoa amri ya kujengwa kwa sanamu kana kwamba yeye mwenyewe aliijenga. "Sanamu uliyowaagiza watu wako waijenge"
Daniel 3:13-14
alijawa na hasira na ghadhabu
Hasiria na ghadhabu ya mfalme Nebukadneza ilikuwa ni kubwa na ya kwamba inaongelewa kana kwamba ilikuwa imemjaa. Mahali hapa maneno "hasira na ghadhabu" yanamaanisha kitu kile kile na yametumika kuonesha mkao juu ya vile mfalme alivyokasirishwa.
Shadraka, Meshaki na Abednego
Haya ni majina ya Kibabeli ya marafiki watatu wa Kiyahudi wa Danieli.
Je mmejipanga katika akili zenu
hapa neno "akili" linarejelea juu ya kufanya maamuzi. Ni nahau yenye maana ya kuamua kwa dhati.
kuisujudia wenyewe
Hili ni tendo la ishara ya kuabudu.
sanamu ile ya dhahabu ambayo nimeiweka
Hii inazungumzia juu ya mfalme Nebukadneza kutoa amri ya kujengwa kwa sanamu kana kwamba yeye mwenyewe aliijenga. "Sanamu uliyowaagiza watu wako waijenge"
Daniel 3:15
sauti pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinumbi na zumari, aina zote za muziki
Hivi ni vyombo au ala za Muziki
kuanguka chini na kuisujudia wenyewe
Haya ni matendo yanayoashiria ibada.
mambo yote yatakuwa mazuri
"hapatakuwa na shida zaidi' au "mtakuwa huru kwenda"
sanamu ile ambayo nimeitengeneza,
Hii inazungumzia juu ya mfalme Nebukadneza kutoa amri ya kujengwa kwa sanamu kana kwamba yeye mwenyewe aliijenga. "Sanamu uliyowaagiza watu wako waijenge"
mtatupwa mara katika tanuru la moto
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "wanajeshi wangu
mtatupwa mara katika tanuru la moto
hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "wanajeshi wangu watawatupeni ninyi katika moto uwakao."
tanuru la moto
Hiki ni chumba kikubwa chenye moto
Ni mungu gani.... katika mikono yangu?"
Mfalme hatarajii jibu. Anawatisha vijana watatu. "Hakuna mungu awezaye kuwaokoeni katika nguvu zangu"
kutoka katika mikono yangu
Mahali hapa neno "mikono" lina maana ya nguvu, mamlaka ya kuhukumu.
Daniel 3:16-18
Nebukadneza, hatuhitaji
Katika sehemu hii watu watatu wanaongea na Mfalme bila kutumia wadhifa wake. Hii ni hali ya kuonesha dharau kwa mamlaka yao.
Kama sivyo, na ijulikane kwako, wewe mfalme,
"Lakini mfalme unapaswa kujua kwamba hata kama Mungu wetu hatatuokoa sisi"
sanamu ya dhahabu uliyoiweka.
Katika kirai hiki, kiwakilishi "u" hakimhusu mfalme kuiweka sanamu, bali mfalme aliamuru watu wake waisimamishe.
Daniel 3:19-20
Nebukadneza alijawa na ghadhabu
Mfalme alikuwa amekasirika kwa kiwango kwamba hasira yake inasemwa kana kwamba ilikuwa imemjaa.
Daniel 3:21-23
kilemba
Kilemba ni kipande cha nguo kinachovaliwa ili kufunika kichwa.
Kwasababu ya agizo la mfalme lilifuatwa
Maneno haya yweza kuandikwa kwa muundo tendaji. "Kwasababu watu walilifuata agizo la mfalme kwa usahihi."
Daniel 3:24-25
Je hatukutupa watu watatu wakiwa wamefungwa katika moto?
"Tuliwatupa watu watatu katika moto wakiwa wamefungwa, sawa?"
Mng'ao wa mtu wa nne ni kama
"Mtu wa nne anatao mng'ao mkali"
kama mwana wa miungu."
miungu iliaminika kuwa ilikuwa iking'aa sana kwa mwanga. "Mtu wa nne anang'aa sana kama ing'aavyo miungu."
Daniel 3:26-27
Magavana wa majimbo, magavana wengine
Haya ni madaraja ya mamlaka juu ya himaya tofauti tofauti.
nywele katika vichwa vyao hazikuungua
Muundo tendaji waweza kutumika kwa tungo hii."moto haukuweza kuunguza nywele vichwani mwao."
Kuungua
"kuchomeka"
mavazi yao yalikuwa hayajaharibiwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Moto haukuweza kuharibu mavazi yao."
na hawakuwa na harufu ya moto
"hawakunukia harufu ya moto"
Daniel 3:28
walipoikana amri yangu
Kutokutii amri ya mfalme kunasemwa kana kwamba kilikuwa kitendo dhahiri cha kutoka na kwenda mbali.
waliitoa miili yao
Kirai hiki kinawahusu watu watatu waliokuwa wamehialika kufa kwa kile wanachokiamini.
kusujudia
Kitendo hiki kina maana ya kulala katika nchi, uso ukiwa umeelekea chini, katika hali ya kuabudu.
isipokuwa Mungu wao
kwa mungu mwingine isipokuwa Mungu"
Daniel 3:29-30
watu wote, taifa au lugha ambayo itazungumza kitu chochote kinyume na Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego lazima wakatwe vipande, na ya kwamba nyumba zao lazima zifanywe kuwa vichuguu vya uchafu
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "watumishi wangu watawaharibu watu wowote, taifa, au lugha... na kuzifanya nyumba zao kuwa vichuguu vya uchafu."
itazungumza kitu chochote kinyume na Mungu
"kuongea maneno ambayo yamheshimu Mungu"
lazima wakatwe vipande
"kukatwa kwa miili yao katika vipande
hakuna mungu mwingine anayeweza kuokoa kama hivi
Muundo wa kubalifu waweza kutumika hapa. "Ni Mungu wao tu aweza kuwaokoa kama hivi"
Daniel 4
Daniel 4:1-3
Maelezo ya jumla
Katika surahii, Nebukadneza anasema kile ambacho Mungu alimfanyia. Katika mistari ya 1-18, Nebukadneza anaeleza ndoto yake kwa nafsi ya kwanza. Katikamistari ya 19-33 anageuka na kutumia nafsi ya tatu katika kuelezea hukuma ya Nebukadneza. Mistari ya 34-37 anabadilika tena na kutumia nafsi ya kwanza katika kuelezea jibu lake kwa Mungu.
Mfalme Nebukadneza aliituma
Kirai hiki kinamrejelea mjumbe wa mfalme kana kwamba ni mfalme mwenyewe. "Mfalme aliwatuma wajumbe wake pamoja"
watu wote, mataifa, na lugha
"watu wote wa kila taifa na lugha"
walioishi katika nchi
Wafalme mara nyingi hutia chumvi kuhusu upana wa ufalme wao ulivyokuwa. Nebukadneza alitawala juu ya sehemu kubwa ya dunia inayojulikana katika kipindi ambacho kitabu hiki kiliandikwa.
amani yenu na iongezeke
Hii ni salaamu ya kawaida.
ishara na maajabu
Maneno haya yana maana sawa na yanarejelea vitu vya kushangaza ambavyo Mungu alikuwa amevifanya.
Ni kwa namna gani Ishara zake ni kubwa, na ni kwa namna gani maajabu yake
Virai hivi viwili vina maana moja na vimetumika katika kutia mkazo juu ya ukubwa wa ishara na maajabu ya Mungu yalivyo.
Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizaz
Virai hivi vina maana moja na vimerudiwa ili kutia mkazo jinsi utawala wa Mungu ni wa milele.
Daniel 4:4-6
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 1-18 Nebukadneza anaelezea maono yake kutoka kwa Mungu kwa kutumia nafsi ya kwanza.
nilikuwa ninaishi kwa furaha katika nyumba yangu, na nilikuwa nikifurahia mafanikio
Virai hivi viwili viko sambamba na vinamaanisha kitu kile kile.
nyumba yangu ....ikulu yangu
Virai hivi kimsingi vina maana moja.
ndoto...taswira...maono...
Maneno haya yana maana moja tu kimsingi.
iliniogopesha....ilinitaabisha
Virai hivi viko sambasamba vina maana moja
watu wote wa Babeli walio na hekima
"wote wenye hekima katika Babeli"
Daniel 4:7-9
Maelezo ya jumla
katika mstari 1-18, Nebukadneza anaelezea maono yake kutoka kwa Mungu kwa kutumia nafsi ya kwanza.
huitwa Belteshaza
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambaye nilimwita Belteshaza."
Belteshaza
Hili ni jina ambalo Wababeli walimpa Danieli.
roho ya miungu watakatifu
Nebukadneza aliamini kwamba nguvu za Danieli zilitokana na miungu ya uongo ambayo Nebukadneza aliiabudu.
hakuna siri iliyo ngumu kwako
tungo hii yaweza kuelezwa kwa kauli ya kukubali. "wewe unafahamu maana ya kila siri"
Daniel 4:10-12
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 1-18, Nebukadneza anaeleza maono yakekutoka kwa Mungu katika nafsi ya kwanza.
niliyoyaona
mambo ambayo unayoyaona
urefu wake ulikuwa ni mkubwa sana
"ulikuwa ni mrefu sana"
Na sehemu ya juu yake ilifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote.
Hii ni lugha ya mfano ambayo inatia chumvi juuu ya jinsi mti ulivyokuwa mrefu na jinsi ambavyo mti ulikuwa unajulikana. "Inaonekana kwamba sehemu ya juu ya ti ilifika angani na ya kwamba kila mtu katika dunia aliweza kuuona."
matunda yake yalikuwa ni mengi
"kulikuwa na matunda mengi katika mti"
chakula kwa ajili ya wote
"kilikuwa chakula cha watu wote na wanyama"
Daniel 4:13-14
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 1-18, Nebukadneza anaeleza maono yake kutoka kwa Mungu katika nafsi ya kwanza.
niliona katika akili zangu
Hii inarejelea kitendo cha kuiona ndoto au maono.
Alipiga kelele na kusema
Inaweza kuwekwa wazi kwamba mjumbe mtakatifu alikuwa akiongea na mtu zaidi ya mmoja
Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege wapae mbali kutoka katika matawi yake.
"Wanyama watakimbia chini yake na ndege watapaa kutoka katika matawi yake."
Daniel 4:15-16
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 1-18, Nebukadneza anaeleza maono yake kutoka kwa Mungu katika nafsi ya kwanza
Maelezo ya jumla
Mjumbe mtakatifu katika maono anaendelea kupiga kelele kwa baadhi ya watu.
kisiki cha mizizi yake
Hii ni sehemy ya mti ambayo huuchwa ardhini baada ya mti kukatwa.
umande
huu ni unyevu nyevu juu ya nchi ambao unapatikana wakati wa asubuhi.
Akili yake na ibadilishwe kutoka... mpaka ipite miaka saba
Kwa kuwa mti unamwakilisha Nebukadneza, kwa hiyo viwakilishi vyote vimetumika katika kifungu hiki kumwongelea yeye.
Daniel 4:17-18
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 1-18, Nebukadneza anaeleza maono yake kutoka kwa Mungu katika nafsi ya kwanza
Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu
Kauli hii yaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Yeye aliye mtakatifu amefanya uamuzi."
mtakatifu
Kirai hiki huenda kinawarejelea Malaika. "Malaika watakatifu"
hao walio hai
"kila mtu aliye hai" au "kila mtu"
huwapa
"huwapa falme"
Belteshaza
Hili ni jina ambalo Wababeli walimpa Danieli.
anayeweza kunitafsiria
"wewe unaweza kuitafsiri ndoto"
roho ya miungu watakatifu
Nebukadneza aliamini kuwa nguvu za Danieli zilitoka kwa miungu ya uongo ambayo yey aliiabudu. Hii haina maana moja na "yey aliye mtakatifu" katika mstari wa 17.
Daniel 4:19
Maelezo ya jumla
katika mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu katitka kuelezea hukumu ya Nebukadneza.
Ndipo Danieli aliyeitwa pia Belteshaza
hii nayo yew Ambaye mimi nilimwita Belteshaza
Ufahamu wa Danieli juu ya maono ndiyo yalimwasha.
ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako.
ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako
Danieli anazungumza matakwa yake kwamba ndoto hii haimhusu mfalme, ingawa alijua kuwa ndoto ilimhusu mfalme.
Daniel 4:20-22
Maelezo ya jumla
Mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu kuelezea hukumu ya Nebukadneza
Maelezo ya jumla
Maneno mengi katika mistari hii inafanana kama katika 4:10
mengi
"mengi sana"
huu mti ni wewe, mfalme,
"mti huu unakuwakilisha wewe mfalme"
Ukuu wako umeongezeka na kufika mbinguni, na mamlaka yako yamefika hata miisho ya dunia.
Virai hivi viwili vina maana sawa
Ukuu wako umeongezeka
Kirai hiki kinatumia neno "kuongezeka" kama njia ya kuuzungumzia ukuu wa mfalme uliokua.
mbinguni... hata miisho ya dunia
Virai hivi viwili vinatia chumvi kwamba kila mtu kila mahali alijua namna ambavyo Nebukadneza alikuwa mkubwa.
Daniel 4:23
Maelezo ya jumla
Mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu kuelezea hukumu ya Nebukadneza
Maelezo ya jumla
Mistari hii inafanana sawa sawa kama 4:13 na 4:15
kisiki cha mizizi yake
Hii ni sehemu ya mti ambayo huachwa juu ya ardhi baada ya mti kukatwa.
katikati ya mche mororo katika shamba
"imezungukwa na miche nyororo ya shamba"
umande
"unyevu nyevu ulio katika nchi wakati wa asubuhi"
Daniel 4:24-25
Maelezo ya jumla
Mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu kuelezea hukumu ya Nebukadneza
Maelezo ya jumla
Maneno mengi katika mistari hii inafanana sawa sawa kama 4:15
ambalo limekufikia
"ambalo umelisikia"
Utafukuzwa utoke miongoni mwa watu,
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Watu watakufukuza utoke miongoni mwao."
Utafanywa uwe unakula majani
Hii yaweza pia kuelezwa kwa muundo tendaji. "utakula majani"
Daniel 4:26-27
Maelezo ya jumla
Mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu kuelezea hukumu ya Nebukadneza
mbingu inatawala
Mahali hapa neno "mbingu" linamrejelea Mungu ambaye anaishi mbinguni. "Mungu wa mbingu ni mtawala wa wote"
ushauri wangu na ukubalike kwako
Maneno haya yaweza kuelezeka kwa muundo tendaji. " tafadhali pokea ushauri wangu"
Geuka uache uovu wako
kukataa uovu kunasemwa kna kwamba ni kugeuka na kuuacha.
walioonewa
Nomina kivumishi hiki kinarejelea watu walioteswa
na itakuwa kwamba mafanikio yako yataongezwa
Muundo tendaji waweza kutumika. "Mungu aweza kuongeza mafanikio yako"
Daniel 4:28-30
Maelezo ya jumla
Mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu kuelezea hukumu ya Nebukadneza
Vitu hivi vyote...katika Babeli
Maelezo katika 4:38 yamepangwa upya ili kwamba maana yake ieleweke kwa urahisi.
miezi wa kumi na miwili
"miezi 12"
Je hii si Babeli kuu....kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?
Nebukadneza anauliza swali hili kwa kutia mkazo katika utukufu wake mwenyewe. Maneno haya yaweza kuelezwa kwa maelezo. "Hii ni Babeli kuu...kwa utukufu wa enzi yangu."
kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu
"kuwaonesha watu heshima yangu na ukuu wangu"
Daniel 4:31-32
Maelezo ya jumla
Mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu kuelezea hukumu ya Nebukadneza
Wakati maneno yakali katika midomo ya mfalme
Nahau hii ina maana kwamba wakati mfalme akiwa akiongea
sauti ilisikika kutoka mbinguni
"alisikia sauti kutoka mbinguni"
"Mfalme Nebukadneza.... umeondolewa kutoka kwako
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mfalme Nebukadneza, amri imetoka kinyume na wewe kuwa ufalme huu si miliki yako"
Utafukuziwa mbali kutoka miongoni mwa watu
Kauli hii yaweza kuelezeka kwa muundo tendaji. "Watu watakufukuza uende mbali nao"
mtu yeyote amtakaye
"Yeyote amchaguaye"
Daniel 4:33
Maelezo ya jumla
Mistari ya 19-33 inatumia nafsi ya tatu kuelezea hukumu ya Nebukadneza
Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla
Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Amri hii iliyo kinyume na Nebukadneza ilitokea ghafla"
Aliondolewa miongoni mwa watu
Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Watu walimfukuzia mbali mfalme atoke kwao"
makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege
"Makucha yake ya vidole yalionekana kama makucha ya ndege"
Daniel 4:34
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 34-37 Nebukadneza anaongelea katika nafsi ya kwanza katika kueleza jibu lake kwa Mungu.
katika mwisho wa siku
Hii inarejelea miaka saba katika 4:31
utimamu wa akili nilirudishiwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "utimamu wangu ulirudi kwangu"
nilimheshimu na kumtukuza
Maneno yote yanarejelea kitendo kile kile
Kwa kuwa utawala wake ni wa milele, na ufalme wake unadumu katoka katika vizazi vyote hadi vizazi vyote.
Virai vyote viwili vinamaanisha kimsingi kitu kile kile na vimetumika kwa kutia mkazo juu ya jinsi utawala wa Mungu usivyo na mwisho.
Daniel 4:35
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 34-37 Nebukadneza anaongelea katika nafsi ya kwanza katika kueleza jibu lake kwa Mungu.
Wenyeji wote wa duniani huhesabiwa na yeye kuwa bure
Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Huwahesabu wakaaji wote wa duniani kuwa si kitu"
Wenyeji wote wa duniani
"watu wote katika dunia"
jeshi la mbinguni
"jeshi la malaika huko mbinguni"
hufanya lolote limpendezalo
"lolote linalotimiza kusudi lake" au kila kitu anachotaka kufanya"
Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia
Itakuwa na msaada kuongeza maelezo ya ziada. "Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia kufanya kile alichoamua kufanya"
Hakuna hata mmoja awezaye kumwambia, "Mbona umefanya hivi?"
Hii yaweza kuelezeka kwa kutumia nukuru isiyo ya moja kwa moja. "Hakuna awezaye kumwuliza kile anachofanya"
Daniel 4:36-37
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 34-37 Nebukadneza anaongelea katika nafsi ya kwanza katika kueleza jibu lake kwa Mungu.
utimamu wa akili zangu uliponirudia
Mahali hapa utimamu unaongelewa kana kwamba ulikuwa na uwezo wa kurudi kwa nguvu zake.
utukufu wangu na fahari yangu ilinirudia
Mahali hapa utukufu wake na fahari kwa pamoja unaongelewa kana kwamba ulikuwa na uwezo wa kurudi kwa nguvu zake .
utukufu wangu na fahari yangu
Maneno haya yana maana sawa na yametumika kutilia mkazo juu ya ukubwa wa utukufu wake.
watu wenye heshima walitafuta msaada wangu
"Watu wangu wa heshima waliomba msaada wangu tena"
Nilirudishwa kwenye kiti changu cha enzi, na nilipewa ukuu zaidi
Mahali hapamaneno "kiti cha enzi" yanarejelea mamlaka yake ya kutawala. Pia muundo tendaji waweza kutumika. "Nilirudi kutawala ufalme wangu tena, na nilipata ukubwa zaidi."
ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu
Maneno haya matatu kimsingi yana maana moja na yametumika kutia mkazo juu ya jinsi alivyomsifu Mungu.
wanaotembea katika kiburi chao wenyewe.
Kitenzi "kutembea" kinamrejelea mtu anayetenda kwa kiburi.
Daniel 5
Daniel 5:1-2
Belshaza
Huyu ni mtoto wa kiume wa Nebukadneza ambaye alikuwa mfalme baada ya baba yake.
elfu moja
"kwa 1,000"
alikunywa divai mbele
"alikkunywa divai akiwa mbele za"
vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu
Hii yaweza kuandikwa kwa muundo tendaji. "vyombo vya dhahabu au fedha ambavyo waisraeli walikuwa wamevitengeneza"
vyombo
Hivi vilikuwa vikombe na vifaa vingine ambavyo vilikuwa vidogo kwa mtu kuvishikilia na kuvinywea.
Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua
Kirai hiki kinatumia jina Nebukadneza kurejelea jeshi la mfalme. "Jeshi la Nebukadneza baba yake walikuwa wamevichukua"
Daniel 5:3-4
vyombo ya dhahabu vilivyokuwa vimechukulia katika hekalu,
Muundo tendaji waweza kutumika. "vyombo vya dhahabu ambavyo jeshi la Nebukadneza walikuwa wamevichukua kutoka katika hekalu"
kutoka hekaluni, nyumba ya Mungu
Kirai "nyumba ya Mungu" kinatueleza kitu zaidi juu ya hekalu.
Daniel 5:5-6
Kwa wakati huo huo
"Mara baada ya kufanya hivyo" au "ghafla"
ukuta uliopigwa lipu
saruji au udongo uliosambazwa katika ukuta au darini ili kuleta ulaini katika sehemu ya juu baada ya kukauka
uso wa mfalme ulibadilika
Hii ilisababishwa na hofu yake
magoti yake yalikuwa yakigongana kwa pamoja
Haya yalikuwa ni matokeo ya hofu yake kubwa.
Daniel 5:7
wale waliojulikana kwa hekima katika Babeli
Hii inarejelea nyuma kwa wale watu wanaodai kusema na wafu, watu wenye hekima na wanajimu
Yeyote atakayeyaeleza maandishi haya na maana yake atavikwa nguo za zambarau na atavikwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake
Kauli hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Nitampa nguo za zambarau na shingo ya dhahabu kwa yeyote atakayeyaeleza maandishi yake na maana yake."
atavikwa nguo za zambarau
Nguo za dhahabu zilikuwa adimu na zilitunzwa maalumu kwa ajili maafisa wa kifalme.
mtawala wa tatu wa juu
"mtawala namba tatu"
Daniel 5:8-9
Belshaza
Hili lilikuwa ni jina la mtoto wa kiume wa Nebukadneza ambaye alikuwa mfalme baada yake.
mwonekano wa uso wake ulibadilika
Uso wa mfalme uliendelea kuonekana dhaifa na hafifu kuliko hata ulivyokuwa katika 5:5
walishangazwa
"kuchanganyikiwa"
Daniel 5:10
Malkia
Matoleo ya kisasa huelewa hili kuwa ni rejea kwa mama malkia, ambaye ni mama wa mfalme. Mama malkia alipewa heshima kubwa katika Babeli ya zamani.
Mfalme na aishi milele
Hii ilikuwa ni njia ya kawaida ya kumsalimia mfalme.
Usiuruhusu mwonekano wa uso wako ubadilike.
"Hakuna haja ya uso kubadilika na kuwa dhaifu"
Daniel 5:11-12
roho ya miungu watakatifu
Malkia aliamini kwamba nguvu za Danieli zilitoka kwa miungu ya uongo ambayo Nebukadneza aliiabudu.
Katika siku za baba yako
"Wakati ambao baba yako alikuwa akitawala"
mwanga na weledi na hekima ya miungu ilipatikana ndani yake
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "alikuwa na mwanga na ufahamu na hekima kama hekima ya miungu"
Mfalme Nebukadneza, baba yako mfalme
"Baba yako Mfalme Nebukadneza"
hizi ni sifa zilizopatikana kwa mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza.
Muundo tendaji waweza pia kutumika."huyu Danieli ambaye mfalme alimwita Belteshaza, alikuwa na sifa hizi zote."
kile kilichoandikwa
"kile kilichokuwa kimeandikwa ukatani"
Daniel 5:13-14
Ndipo Danieli alipoletwa mbele ya mfalme
Hii yaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. "Kisha walimleta Danieli mbele ya mfalme" au "wanajeshi walimleta Danieli mbele ya mfalme"
ambao baba yangu mfalme aliwaleta kutoka Yuda
Katika kirai hiki, neno "baba" limetumika kumaanisha wanajeshi wote.
roho ya miungu
Belshaza aliamini kuwa nguvu za Danieli zilitoka kwa miungu ya uongo ambayo Belshaza aliiabudu.
mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "una mwanga na ufahamu na hekima bora"
Daniel 5:15-16
Na sasa watu wanaojulikana ....wamekwisha kuletwa mbele yangu
Muundo tendaji waweza kutumika pia."sasa watu waliojulikana ....wamekuja mbele yangu"
kunijulisha
"kuniambia"
utavikwa nguo za zambarau na kuwa na kuvalishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji."Nitakupatia nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni"
utavikwa nguo za zambarau
Nguo za zambarau zilikuwa ni adimu na zilitunzwa kwa ajili ya maafisa wa kifalme.
mtawala wa tatu
"mtawala wa namba ya tatu"
Daniel 5:17-19
Zawadi yako na iwe kwa ajili yako
"Sihitaji zawadi zako"
watu wote, mataifa, na lugha
Kirai hiki kina neno "wote" ili kuwakilisha namba kubwa.
walimtetemekea na kumwogopa
Maneno haya kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na yametumika kwa ajili ya kutia mkazo juu ya ukubwa wa hofu.
Aliwauwa wale aliotaka wafe
Kirai hiki cha maneno hakina maana ya kwamba mfalme Nebukadneza hakuwauwa watu yeye mwenyewe, bali wale aliowaagiza.
Aliwainua wale aliowataka
"Aliwainua wale aliowataka kuwainua"
aliwashusha wale aliowataka.
"aliwashusha wale aliotaka kuwashusha"
Daniel 5:20-21
moyo ulipokuwa na kiburi
Mahali hapa neno "moyo" linamrejelea mfalme mwenyewe.
roho yake ilifanywa kuwa mgumu
Mahali neno "roho" linamaanisha mfalme mwenyewe. Kiburi chake kinasemwa kana kwamba kilikuwa kimefanywa kuwa kigumu.
kwa kiburi
"kwa kiburi na zaidi ya kujiamini
alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme
Mahali "kiti cha enzi" kina maana ya mamlaka yake ya kutawala. Hii pia yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Watu waliutwaa ufalme wake."
Aliondolewa katika ubinadamu
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. Watu walimfukuza atoke kati yao"
alikuwa na akili za mnyama,
Mahali hapa neno "akili" lina maana ya mawazo. "Alifikiri kama vile mnyama anavyofikiri"
umande
Ni unyevu nyevu ulio juu ya nchi ambao hupatikana nyakati za asubuhi.
yeyote amtakaye
"yeyote amchaguaye"
Daniel 5:22-24
Belshaza
Hili lilikuwa ni jina la mtoto wa kiume wa Nebukadneza ambaye alikuwa mfalme baada yake
haujaunyenyekeza moyo wako
Mahali hapa neno 'moyo' linamwakilisha Nebukadneza mwenyewe.
umwenyewe kinyume cha Bwana
Kitendo cha kuasi kinyume na Mungu kinasemwa kana kwamba ni kujiinua mtu mwenyewe.
kutoka katika nyumba yake
Kirai "nyumba yake" kinaeza kuelezwa kwa uwazi sna "kutoka kwa hekalu la mfalme."
njia zako zote"
"kila kitu uanchokifanya"
Mungu ambaye anaishikilia pumzi yako katika mkono wake
Mahali hapa neno 'pumzi" lina maana ya fedja ma memp "mkono" lina maana ya mamlaka au utawala.
maandishi haya yaliandikwa
Muundo tendaji waweza kutumika. "iliandika ajumbe huu"
Daniel 5:25-28
Haya ndiyo maandishi ambayo yaliandikwa
Kwa kutumia muundo tendaji twaweza kusema. " huu ni ujumbe ambao uliandikwa na mkono"
'Mene, Mene, Tekeli na Peresin.
Haya ni maneno ya Kiramaiki ambayo yalikuwa yameandikwa ukutani.
'Mene,' 'Mungu ameuhesabu
"mene' ina maana ya kuwa Mungu amehesabu"
Tekeli' 'umepimwa katika mizani
"Tekeli' ina maana ya wewe umepimwa"
Peresi' 'ufalme wako
"Peresi" ina maana ya ufalme wako
'umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua
kuhukumu na kuamua juu ya uthamani kwa mfalme katika kutawala unasemwa kana kwamba ni kumpima. Hii ina maana ya kwamba mfalme hafai kuongoza/kutawala.
'ufalme wako umegawanyika na wamepewa Wamedi na Waajemi.'"
Kwa kutumia muundo tendaji twaweza kusema. "Mungu ameugawa ufalme wako na amewapa Wamedi na Waajemi.
Daniel 5:29-31
Mkufu wa dhahabu walimvisha shingoni
Hii yaweza kuelelzwa kwa muundo tendaji. " Waliuweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake"
mtawala mwenye mamlaka ya nafasi ya tatu
"mtawala wa namba ya tatu"
aliuchukua ufalme
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "alikuwa mtawala wa ufalme"
alipokuwa na miaka ipatayo sitini na miwili.
"wakati alipokuwa takribani miaka 62"
Daniel 6
Daniel 6:1-3
Sentensi kiunganishi
Matukio katika sura hii yalitukia baada ya Waajemi kuwaangusha Wababeli na Dariuo Mmedi alianza kutawala juu ya Babeli.
Ilimpendeza Dario
"Mfalme Dario aliamua"
magavana wa majimbo 120
"Magavana wa majimbo wapatao mia na ishirini"
juu yao
Neno 'wao' linawarejelea magavana 120
ili kwamba mfalme asipate hasara.
"ili kwamba chochote kisiibiwe kutoka kwa mfalme"
alipambanuliwa juu
"alifaulu juu ya " au " alikuwa na uwezo kuliko"
likuwa na roho isiyo ya kawaida
Mahali hapa "roho" inamrejelea Danieli. Inamaanisha kuwa kile alichokuwa nacho kilikuwa si cha kawaida kwa watu. "alikuwa ni mtu wa kipekee"
isiyo kawaida
"ya kuvutia" au "bora"
kumweka juu ya
"kumpa mamlaka juu ya " au " kumweka kuwa masimamizi wa "
Daniel 6:4-5
Basi watawala wakuu wengine na magavana wa majimbo .... kwa ufalme
Watawala wengine walimwonea Danieli wivu. Hii yaweza kuwekwa dhahiri. "kisha watawala wengine na magavana wa majimbo walikuwa na wivu. Hivyo, wakatafuta makosa katika kazi za Danieli alizozifanya kwa ajili ya ufalme. "
Hakuna kosa au uzembe uliopatikana ndani yake
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Hawakuweza kupata makosa au uzembe katika kazi yake."
kumshitaki huyu Danieli
"kumlalamikia Danieli"
Daniel 6:6-7
walileta mpango mbele ya mfalme
"waliwasilisha mpango kwa mfalme"
Mfalme Dario, uishi milele!
Hii ilikuwa ni njia ya kawaida ya kumsalimia mfalme.
siku thelathini
"kwa siku 30"
mtu yeyote anayefanya dua
"yeyote atakayetoa ombi"
mtu huyo lazima atupwe katika tundu la simba
Maneno haya yaweza kuelezeka kwa muundo tendaji. "wanajeshi wako lazima wamtupe mtu huyo katika tundu la simba"
tundu la simba
Hii inarejelea chumba au shimo mahali ambapo simba walikuwa wametunzwa
Daniel 6:8-9
Sentensi kiunganishi
Katika mstari wa 8, watawala wanaendelea kuongea na mfalme
kama ilivyoelekezwa katika sheria
"kutokana na sheria"
haiweze ikabatilishwa
"haiwezi kusitishwa"
kuifanya amri kuwa sheria
"kulifanya agizo kuwa sheria"
Daniel 6:10-11
Danieli alipojua kuwa nyaraka imekwisha kusainiwa kuwa sheria
Ni muhimu katika habari hii kueleza wazi kwamba Daniel alijua juu ya sheria mpaya kabla hajamwomba Mungu.
madirisha yake katika chumba cha juu yalikuwa wazi kuelekea Yerusalemu
Haya ni maelezo ya muhimu ambayo yanaelezea jinsi maadui wa Danieli walijua kuwa Danieli alikuwa akiomba kwa Mungu wake.
kushukuru mbele ya Mungu wake,
"alitoa shukrani kwa Mungu wake"
hila
mpango wenye kusudi ovu
Daniel 6:12
Je .haukuweka amri ....simba?
Walimwuliza swali hili ili kumfanya mfalme ahakikishe kuwa alikuwa ametoa amri.
mtu yeyote akayefanya maombi
"ambaye afanyaye maombi"
tundu la simba
Hii inarejelea chumba au shimo mahali simba walikuwa wanatunzwa.
kama ilivyoelekezwa katika sheria
"kutokana na sheria"
Daniel 6:13-14
Mtu yule Danieli
Hii si njia ya heshima ya kumzungumzia Danieli. Walitumia maelezo haya kimakusudi ili kutompa Danieli heshima aliyostahili kama mtawala mkuu.
ambaye ni mmoja wa watu wa mateka kutoka Yuda,
"ambaye ni mhamiaji kutoka Yuda"
hakutii wewe
Hii ni nahau inayoonesha kuwa anakatalia Mfalme "Hakutii wewe"
, alitumia akili
Mahali hapa neno "akili"linarejelea fikra zake.
Alisumbuka sana
Hii inarejelea masumbuko ya kiakili badala ya masumbuko ya kimwili.
Daniel 6:15
hakuna amri....yaweza kubadilishwa
maelezo ya ziada yaweza kuongezwa hapa ili kusaidia ufahamu. "hakuna amri... yaweza kubadilishwa. Lazima wamtupe Danieli katika shimo la simba"
Daniel 6:16
walimleta ndani Danieli
"wanajeshi wake walienda na kumleta Danieli"
tundu la simba
Hii inarejelea chumba au shimo mahali simba walikuwa wanatunzwa.
Mungu wako..... na akuokoe
Mfalme anaelezea matakwa yake kwa ya Mungu kumwokoa Danieli.
akuokoe
"kukuokoa kutoka katika simba"
Daniel 6:17-18
tundu
Hii inarejelea chumba au shimo mahali simba walikuwa wanatunzwa.
mfalme alilitia muhuri wa pete yake mwenyewe na pamoja na muhuri wa wakuu wake.... kuhusiana na Danieli
Kazi ya pete yea muhuri yaweza kuelezewa kwa uwazi. Mfalme pamoja na wakuu wake walikandamiza pete katika chapa iliyotengenezwa kwa nta.
na usiku ule alikuwa na mfungo
Hili ni tendo linaloashiria kwamba mfalme alikuwa na wasiwasi kuhusu Danieli.
chochote kisiweze kubadilishwa kuhusiana na Danieli
"hakuna awezaye kumsaidia Danieli"
Hakuna starehe yoyote iliyoletwa mbele yake
maneno haya yaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. " Hapakuwa na mtu yeyote wa kumburudisha"
nao usingizi ulimkimbia
Usingizi unaongelewa kana kwamba unaweza kukimbia kutoka kwa mfalme. "hakulala kabisa usiku wote ule"
Daniel 6:19-20
tundu la simba
Hii inarejelea chumba au shimo mahali simba walikuwa wanatunzwa.
Daniel 6:21-22
Kwa kuwa sikuwa na hatia yoyote
Muundo tendaji waweza kutumika. " Anajua kuwa sijafanya chochote kibaya"
sijakufanyia jambo lolote la kukudhuru
"Sijakudhuru wewe kabisa"
Daniel 6:23
tundu la simba
Hii inarejelea chumba au shimo mahali simba walikuwa wanatunzwa
Hakuna dhara lolote lililoonekana kwake
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Hawakuona jeraha lolote kwa Danieli"
Daniel 6:24-25
tundu la simba
Hii inarejelea chumba au shimo mahali simba walikuwa wanatunzwa
Kabla hawajafika sakafuni
"kabla hawajafika chini katika tundu la simba"
kuvunjavunja mifupa yao vipande vipande
"kuvunja mifupa yao"
watu wote, mataifa na lugha
"watu wa mataifa yote na lugha"
katika dunia yote:
Mfalme Dario aliandika ujumbe huu kwa ufalme wake wote ulikuwa mkubwa. Hapa anatumia maneno "dunia yote" kutilia mkazo juu ya ukubwa wa ufalme wake ulivyokuwa, ingawa haukuwa kwa watu wote wa duniani"
Amani na iongezeke kwenu
Huu ni muundo wa salaamu iliyotumika kwa kumtakia mtu mema katika sehemu zote za maisha.
Daniel 6:26-27
Maelezo kiunganishi
Hii inaendelea kueleza ujumbe ambao Dario aliutuma kwa kila mtu katika ufalme wake.
watetemeka na kumcha
Maneno haya yana maana sawa na yanaweza kuunganishwa. "kutetemeka kwa hofu"
Mungu wa Danieli
"Mungu ambaye Danieli alimwabudu"
kwa kuwa ni Mungu aliye hai na huishi milele
Virai hivi viwili "Mungu aliye hai" na "aishiye milele" vinaelezea dhana moja, kwamba Mungu huishi milele.
ufalme wake ha....; utawala wake uta..
Virai hivi vyote viko sambasamba, na vinatia nguvu juuu ya jinsi ufalme wa Mungu hautakuwa na mwisho."
ufalme wake hauwezi kuharibiwa
Maneno haya yaweza kuelezwa katika muundo tendaji. " hakuna yeyote aweza kuuangusha ufalme wake" au "ufalme wake utadumu milele"
utawala wake utakuwepo hadi mwisho.
"atatawala milele"
amemhifadhi Danieli salama dhidi ya uwezo wa simba.
"hajawaruhusu simba wenye nguvu kumdhuru Danieli"
Daniel 6:28
atika utawala wa Dario na katika utawala wa Koreshi Mwajemi
Koreshi Mwajemi alikuwa mfalme aliyetawala baada ya Dario.
Daniel 7
Daniel 7:1-3
Maelezo ya jumla
Sura ya 7 na ya 8 haziko katika mpango wa mtiririko wa kawaida. Zilitokea wakati Belshaza alipokuwa akali ni mfalme, kabla ya utawala wa Dario na Koreshi walioongelewa katika sura ya 6.
Maelezo ya jumla
Katika maono ya Danieli, aliona wanyama waliokuwa ni ishara ya mambo mengine. Baadaye katika maono mtu fulani alifafanua maana ya ishara hizo.
Belshaza
Hili ni jina la mtoto wa kiume wa Nebukadneza, ambaye alikuwa mfalme baada yake.
ndoto na maono
Maneno haya "ndoto na maono" yote yanarejelea ndoto ile ile iliyoelezewa katika sura hii.
pepo nne za mbinguni
"pepo kutoka kila sehemu" au "pepo zenye nguvu kutoka sehemu zote nne za mwalekeo"
zinaitikisa
"piga piga" au "kusababisha mawimbi makubwa"
Daniel 7:4-5
Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba
Huyu ni mnyama wa ishar, na si mnyama halisi anayeishi.
mabawa yake yalikuwa yamepasuka na alikuwa ameinuliwa katika ardhi na alikuwa amesimama kwa miguu miwili kama mtu
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "mtu fulani alipasua mabawa yake na kumwinua kutoka chini na kumifanya asimame kwa miguu miwili kama binadamu."
Na alipewa akili za kibinadamu
Mahali hapa neno "akili" limetumika kumaanisha "fikra.' Muundo tendaji waweza kutumika. "Mtu fulani alimpa uwezo wa kufikiri kama mtu"
kulikuwa na mnyama wa pili, alikuwa kama dubu
Huyu hakuwa dubu halisi, bali ni mnyama wa ishara ambaye alifanana na dubu.
mbavu
Mifupa mikubwa ya kifuani iliyopinda ambayo imeungana na uti wa mgongo.
aliambiwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mtu fulani alimwambia"
Daniel 7:6-7
mnyama mwingine ambaye alionekana kama chui
Huyu hakuwa chui halisi, bali mnyama wa ishara ambaye alikuwa akifanana na chui.
mabawa manne ....vichwa vinne
Mabawa manne na vichwa vinne ni mifano/ishara, lakini maana zake haziko wazi.
alikuwa na vichwa vinne.
"mnyama alikuwa na vichwa vinne"
Alipewa mamlaka ya kutawala
Kauli hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mtu fulani alimpa mamlaka ya kutawala"
mnyama wa nne...alikuwa na pembe kumi
Huyu pia si mnyama halisi. Ni mnyama wa mfano.
kusaga saga katika miguuni
"kutembea juu yake na kuvunja vunja''
Daniel 7:8
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuyaelezea maono yake ya mnyama wa nne ambayo aliyoyaona katika 7:6
pembe
Watafsiri waweza kuandika tanbihi chini ya ukurasa. "Pembe" ni alama au ishara ya ngur
Mizizi ya pembe tatu kati ya pembe za mwanzo iling'olewa
Tungo hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Pembe ndogo ilichomoza kati ya pembe tatu za mwanzo."
mdomo ambao ulikuwa ukijivuna kwa mambo makubwa.
Mahali hapa kuna pembe ilikuwa inajivuna kwa kutumia mdomo wake. "pembe ilikuwa na mdomo na ulijivuna kuhusu kufanya mambo makubwa"
Daniel 7:9
Maelezo ya jumla
Vifungu vingi vya mistari 9-14 ni lugha ya picha ikiwa na mistari sambamba iliyo na maana sawa.
viti vya enzi vilikuwa vimewekwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " mtu fulani aliviweka viti vya enzi katika sehemu zake"
Mtu wa Siku za Kale
Hili jina la Mungu ambalo lina maana kwamba yeye ni wa milele.
alikaa sehemu yake...mavazi yake... nywele zake
"Kifungu hiki kinamwelezea Mungu akiwa amekaa, akiwa na mavazi na nywele kama mtu. Hii haina maana kwamba Mungu yuko hivyo, bali ni vile ambavyo Danieli alivyomwona Danieli katika maono.
alikaa sehemu yake
Hii ni lugha ya picha ikiwa na maana ya kwamba Mungu alikaa katika kiti chake cha enzi.
Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji
Mavazi yake yanalinganishwa na theruji kuonesha kwamba zilikuwa ni nyeupe sana. "nguo zake zilikuwa nyeupe sana"
ywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu
nywele za Mungu zilionekana kama sufu. maana zinazokkubalika ni 1) zilikuwa ni nyeupe sana 2) zilikuwa ni nzito na zilizopinda pinda.
sufu safi
"sufu nzuri" au "sufu zilizooh
Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto
Hii inafafanua juu ya kiti cha enzi cha Mungu na magurudumu yake kana kwamba yalikuwa yametenenezwa kwa moto. Maneo''miali ya moto' na 'kuwaka moto" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na inaweza kufasiriwa kwa namna ile ile.
magurudumu yake
Haiko wazi sana kwanini kiti cha enzi cha Mungu kinaelezwa kuwa na magurudumu. Viti vya enzi kikawaida huwa havina maguruduma, lakini kifungu kwa uwazi kinaelezea kwamba kiti hiki cha enzi kilikuwa na magurudumu.
Daniel 7:10
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuelezea maono yake juu ya jibu kutoka mbingu kwa mnyama wa nne ambaye alimwona katika 7:6
Maelezo ya jumla
Vifungu vingi vya mistari ya 9-14 ni lugha ya picha yenye mistari sambamba iliyo na maana sawa.
Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake
Kitendo cha moto kutoka kwa haraka mbele za Bwana kunasemwa kana kwamba ni maji yanatiririka.
mbele yake
Neno "yake" inamrejelea Mungu, Siku za Kale kutoka 7:9
mamilioni
Hii huenda inarejelea kundi kubwa kulilka hesabu ndogo. "Maelfu elfu" au "hesabu kubwa ya watu"
mia moja milioni
Hii huenda inarejelea kundi kubwa kulilka hesabu ndogo. "makumi elfu mara makumi elfu" au "watu wasio hesabika"
mahakama iliitishwa
Hiii ina maana kwamba Mungu, hakimu, alikuwa tayari kuchunguza ushahidi na kufanya hukumu yake.
vitabu vilifunguliwa
Hivi ni vitabu ambavyo vimejumuisha ushahidi utakaotumika katika mahakama. "vitabu vya ushahidi vilifunguliwa"
Daniel 7:11-12
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuelezea maono yake ya mahakama ya mbinguni katika kujibu mnyama wa nne aliyemwona katika 7:6
mnyama anauliwa...kwa ajili ya kuchomwa moto
Kauli hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "walimwua mnyama wa nne, wakaharibu mwili wake na wakampa mtu fulani ili auchome."
mnyama
Hii inamrejelea mnyama wa nne ambaye alikuwa na pembe kumi na pembe ile iliyojivuna.
Na kwa wale wanyama wanne waliosalia,
Inaweza kuwa wazi kusema, "wanyama wengine watatu"
mamlaka yao yalitwaliwa mbali,
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "hakimu aliyachukua mamlaka yao ya kutawala" au "mamlaka yao ya kutawala yalikoma'
maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " waliendelea kuishi kwa kipindi fulani cha muda" au "hakimu aliwaacha waishi kidogo"
Daniel 7:13-14
Maelezo ya jumla
Vifungu vingi vya mistari ya 9-14 ni lugha ya picha yenye mistari sambamba iliyo na maana sawa.
nilimwona mtu mmoja anakuja ... kama mwana wa mtu
Mtu ambaye Danieli alimwona hakuwa ni mtu wa kawaida, lakini alikuwa na mwonekano kama wa kibidamu. "Niliona usiku ule mtu fulani ambaye anafanana na na mwana wa mtu, yaani alikuwa na umbo la kibinadamu"
katika mawingu ya mbinguni
"pamoja na mawingu ya angani"
kwa Mzee wa Siku
Hii inamrejelea Mungu ambaye ni wa milele.
aliletwa mbele zake
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. 'walimleta huyu mwana wa mtu kwa Mzee wa Siku" au "alisimama mbele yake"
Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme
Maelezo haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " Yeye aliyeonekana kama mwana wa mtu alipokea mamlaka ya kutawala, utukufu, na nguvu za kifalme."
nguvu za kifalme
Hii inarejelea "mamlaka"
hayatapita,..... hautaangamizwa
Virai hivi viwili vina maana ile ile
ule ambao hautaangamizwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " kwamba hakuna hata mmoja atakayeangamiza"
Daniel 7:15-16
roho yangu ilihuzunishwa ndani yangu, na maono niliyoyaona katika akili zangu yalinisumbua.
Virai hivi viwili vinaelezea jinsi Danieli alivyokuwa akijisikia. Kirai cha pili kinatoa maelezo ya ziada juu ya kirai cha kwanza, kikieleza juu ya roho inayosumbuka.
roho yangu ilihuzunishwa ndani yangu
Mahali hapa maneno "roho yangu" inamrejelea Danieli mwenyewe. "Nilikuwa na huzuni ndani yangu"
mmoja wa hawa walikuwa wamesimama hapo
Huyu ni moja wa viumbe vya mbinguni aliyekuwa amesimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Maana zinazokubalika 1) hawa ni malaika, roho zinazomtumikia Mungu 2) hawa ni watu walikwisha kufa na sasa wako mbinguni.
anioneshe
"kuniambia mimi"
mambo haya
"mambo niliyokuwa nimeyaona"
Daniel 7:17-18
Hawa wanyama nne wakubwa
"Hawa ni wanyama wakubwa"
ni wafalme wanne
"inawakilisha wafalme wanne"
wafalme wanne ambao watatoa katika nchi
Hapa maneno "kutoka katika nchi" ina maana ya kuwa ni watu wa kawaida.
wataumiliki
"watatawala juu yake"
milele na milele
Haya mawazo ya kujirudia yanatia mkazo kwamba ufalme huu hautakuwa na mwisho.
Daniel 7:19-20
alikuwa wa kutisha
"wa kuogofya sana"
alisaga saga kwa miguu yake
"alitembea juu yake na kukanyaga"
pembe kumi katika kichwa chake
"pembe kumi juu ya kichwa cha mnyama wa nne"
iliyochomoza, na ambayo mbele yake pembe zingine tatu zilianguka chini
"ilikua na pembe takribani tatu zilianguka chini mbele yake" au "ilichomoza na kuhusu pembe tatu ambazo zilianguka chini kwa sababu yake."
ambayo mbele yake pembe zingine tatu zilianguka chini
Hapa neno "kuanguka chini" ni tafsida ambayo ina maana kwamba ziliteketezwa"
mdomo uliokuwa unajisifu
"mdomo wake wenye kujisifu" au "mdomo wa pembe mpya ambao unajisifu"
ambayo ilionekana kuwa ni kubwa kuliko zingine
pembe yenye macho na mdomo ilionekana kuwa kubwa kuliko pembe zingine
Daniel 7:21-22
pembe hii
"pembe hii ya nne" Hii inarejelea pembe ambayo imeelezewa katika 7:19
mpaka pale Mzee wa Siku alipokuja, na haki alipewa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji "mpaka Mzee wa Siku alipokuja na kuleta haki"
Mzee wa Siku
Hili ni jina la Mungu ambalo linatia mkazo kwamba Yeye ni wa milele.
watu watakatifu waliupokea ufalme
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " Mungu aliwapa watu wake watakatifu ufalme wake"
Daniel 7:23-24
Maelezo ya jumla
Vifungu vingi vya mistari ya 23-27 ni lugha ya picha.
Hiki ndicho mtu yule alichokisema
Huyu niNa kuhusu pembe kumi mtu ambaye Danieli alimkaribia katika 7:15
mtu yule alichokisema
mtu yule alijibu
Kwa habari ya mnyama wanne...Na kuhusu pembe kumi
"kuhusu mnyama wa nne...kuhusu pembe kumi"
Utaimeza ..... vipande vipande
Hii haina manna kwamba ufalme wa nne utaiharibu sayari, bali ni kwamba utashambulia, kushinda na kuharibu falme zingine zote za duniani.
kutoka katika ufalme huu, wafalme kumi watainuka
Watatawala mmoja baada ya mwingine. Hii yaweza kuwekwa wazi. "wafalme kumi watautwala ufalme wa nne, mmoja baada ya mwingine"
mwingine atainuka baada yao
Mfalme huyu si mmoja wa wale kumi. Ni vizuri kumrejelea kama mfalme wa kumi na moja.
Atakuwa wa tofauti na wale waliomtangulia,
"atakuwa tofauti na waflme wengine kumi"
atawashinda wale wafalme watatu
Atawashinda wafalme halisi watatu. inaeza kusaidia kueleza kuwa wale wafalme watatu wanawakilishwa ba pembe tatu zilizong'olewa.
Daniel 7:25-26
Maelezo ya jumla
Mtu ambaye Danieli alimwona katika maono anaendele kuongea na Danieli.
Maelezo ya jumla
vifungu vingi vya mistari ya 23-27 vinatumia lugha ya picha.
Atazungumza maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu sana
Hii ina maana kwamba mfalme mpya ajaye atamkataa wazi wazi na kusema maneno mabaya juu ya Yeye aliye juu sana.
Atajaribu.....katika mikono yake.
Kiwakilishi "a" na kimilikishi "yake" vinamrejelea mfalme mpaya, siyo Yeye aliye juu sana.
watu watakatifu
Watu wakatifu wa Mungu
kuzibadili sikukuu na sheria.
Maneno yote rana rejelea sheria za Musa. Sikukuu zilikuwa nia muhimu katika masuala ya kidini katika Israeli katika Agano lake.
Mambo haya atapewa mikononi mwake
hapa maneno "mkono wake" inarejelea utawala. Hii yaeza kuelezwa kwa muundo tendaji " Mfalme mpya atatawala sikukuu zote za dini na sheria.
mwaka mmoja, miaka miwili na nusu mwaka.
Hii ina maana ya "miaka mitatu na nusu" Hii si njia ya kawaida ambayo Waisraeli walitumia katika kuhesabu.
mahakama kitaitishwa
Hii ina maana kwamba hakiku atakuwa tayari kuchunguza ushahidi na kufanya hukumu yake.
watazichukua nguvu zake za kifalme
Wanachama katika mahakama watazitwaa nguvu zake za kifalme kutoka mfalme mpya.
nguvu za kifalme
Hii inarejelea "mamlaka"
aweza kuharibiwa na kuteketezwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "na kuharibu na kuangamiza mwishoni"
Daniel 7:27-28
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kuongea na mtu yule aliyemwona katka maono.
maelezo ya jumla
Vifungu vingi vya mistari ya 23-17 vinatumia lugha ya picha.
Ufalme na utawala....watapewa watu walio wa wat
Hii yaweza kuelezwa kwa muuundo tendaji. "Mungu atawapa watu...ufalme na utawala...
Ufalme na utawala
Maneno haya maweili yana maana ile ile na yanatia mkazo juu ya miundo yote ya mamlaka rasmi
ukubwa wa falme
Nomino dhahania "ukubwa" yaweza kutafsiriwa kwa kivumishi "kubwa"
chini ya mbingu yote
Nahau "chini ya mbingu yote" inarejelea falme juu ya nchi.
ufalme wake
"ufalme wa Mungu aliye juu"
ufalme wa milele
"ufalme ambao utadumi milele" au " ufalme ambao hautakoma"
Na huu ndio mwisho wa mambo
Hii ina maana kwamba Danieli amemaliza kuelezea maono yake.
mwonekano wa uso wangu ulibadilika
"uso wangu ulikuwa dhaifu/hafifu"
Daniel 8
Daniel 8:1-2
Maelezo ya jumla
Sura ya 7 na ya 8 haziko katika mtiririko maalumu. Zilitokea wakati Belshaza alipokuwa angali ni mfalme, kabla ya utawala wa Dario na Koreshi ambazo zimeongelewa katika sura ya 6.
Maelezo ya jumla
Katika maono ya Danieli, aliona wanyama waliokuwa ni ishara ya mambo mengine. Baadaye katika maono mtu fulani alimwelezea maana ya ishara hizo.
Katika mwaka wa tatu
"Ndani ya mwaka wa tatu"
niliona maono (baada ya maono ya awali yaliyonipata)
Haya ni maelezo ya nyuma ili kumkumbusha msomaji kwamba haya yalikuwa ni maono ya pili kwa Danieli.
Belshaza
Huyu ni mtoto wa kiume wa Nebukadneza ambaye alikuwa mfalme baada ya baba yake.
ngome
kulindwa na kuhifadhiwa
Shusha....Elamu...Mfereji wa Ulai
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Mfereji
Mfereji ni njia nyembamba ya maji iliyotengenezwa na mwanadamu.
Daniel 8:3-4
kondoo dume lenye mapembe mawili
kondoo dume lenye mapembe mawili ni kawaida kwa beberu kuwa na pembe mbili. ingawa, Mapembe haya yana maana yanayoiashiria.
lakini pembe ndefu .....ilirefuka na kuizidi nyingine.
"lakini pembe ndefu ilikua pole pole kuliko ile fupi, na pembe fupi ilikua na kuwa ndefu kuliko ile."
Niliona kondoo mme akiishambulia
"Nilimwona kondoo mme akiharakisha" au "nilimwona beberu akikimbia kwa haraka sana"
kumwokoa yeyote katika mkono wake
"Beberu huwa hazina mikono. Mahali hapa "mkono" unarejelea 'nguvu za kondoo"
Daniel 8:5-6
kuvuka katika uso wa dunia yote
Mahali hapa neno "uso" linarejelea sehemu ya juu ya nchi. Kirai "dunia yote" kinatia chumvi chenye maana kwamba alikuja kutoka mbali sana.
Mbuzi huyo alikuwa na pembe kubwa katikati ya macho yake
Mbuzi huwa na pembe mbili katika pande mbili za vichwa vyao. Sura hii lazima ielezeke kama "Mbuzi alikuwa na pembe moja kubwa katikati ya kichwa chake"
nilikuwa nimemwona kondoo dume amesimama katika ukingo wa mfereji
Kirai hiki kimechomekwa ili kuleta maelezo ya nyuma ili kuelezea mahali ambapo beberu alikuwa.
kwa hasira kali
"na alikuwa na hasira kali"
Daniel 8:7-8
akamkanyaga
Kukanyaga kitu fulani kwa kutembea juu yake.
kutoka katika nguvu zake
"kondoo kutoka kwa mbuzi kwasababu ya nguvu zake"
mbuzi alikua akawa mkubwa
"mbuzi alikuwa mkubwa na mwenye nguvu"
pembe kubwa ilivunjwa,
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Kitu fulani kiliivunja pembe kubwa"
kuelekea pepo nne za mbingu.
Mahali hapa "pepo nne za mbinguni" ni nahau inayorejelea pembe kuu nne (kaskazini, mashariki, magharibi na kusini) kutoka huko pepo huvuma.
Daniel 8:9-10
ilikuwa pembe kubwa
"lakini ilikuwa kubwa sana"
upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri
Hii huenda ina maana ya kwamba pembe imeelekea sehemu hizo. "na imeelekea upande wa kusini na kisha upande wa mashariki na kisha nchi nzuri ya Israeli"
ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita
Mahali hapa pembe amepewa sifa za mtu na anajihusisha katika vita.
Baadhi ya jeshi na nyota kadhaa zilitupwa chini duniani
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. Pembe ilitupa baadhi ya jeshi na baadhi ya nyota chini ya dunia.
zilikanyagwa.
mahali hapa "pembe" imepewa sifa za binadamu na amezikanyaga nyota na juu ya jeshi.
Daniel 8:11-12
Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama
Hapa pembe ya mbuzi inasemwa kana kwamba ilikuwa ni mtawala ambaye alifanyika mkuu.
Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye
Neno "ziliondolewa" lina maana ya alizizuia sadaka. Pembe inaongelewa kana kwamba alikuwa ni mtawala wa kibinadamu.
sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Ilitengeneza sehemu yake takatifu kuwa najisi"
Pembe itautupa ukweli chini ardhini
Hii ina maana kwamba pembe itakataa ukweli na utauwa. Pembe inasemwa kana kwamba alikuwa ni mtawala wa kibinadamu.
Daniel 8:13-14
mtakatifu mmoja
"malaika"
ukabidhiajia wa sehemu takatifu
"kutiisha sehemu takatifu"
jeshi la mbinguni kukanyagwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "pembe ilikanyaga juu ya jeshi la mbinguni"
jioni na asubuhi zipatazo 2,300
Mahali hapa maneno "jioni na asubuhi" yanarejelea kila kitu kilicho katikati yake, iliyo na maana ya siku kamili.
mahali patakatifu patawekwa sawa.
"hekalu litasafishwa na kuwekwa katika utaratibu tena. "
Daniel 8:15-17
mfereji wa Ulai
Mfereji ni shimo lililotengenezwa na watu kwa ajili ya kupitisha maji.
sauti ya mtu ikiita
Mahali mtu amerejelewa kwa sauti yake. "mtu alikuwa akiita kutoka mfereji wa Ulai"
nilisujudia hadi chini
Hili ni tendo la ibada ambalo katika hilo mtu fulani hulala wima juu ya nchi.
wakati wa mwisho
"siku za mwisho" au "mwisho wa dunia" Hii hairejelei mwisho wa muda kidogo, bali matendo ambayo yatatokea ghafla kabla ya mwisho.
Daniel 8:18-19
usiingizi mzito
Hii ni aina ya usingizi ambao mtu hulala fofo na hawezi kuamka kiurahisi.
kipindi cha ghadhabu
Hii inarejelea wakati ambapo Mungu atahukumu.
wakati wa mwisho uliopangwa
"wakati ambapo dunia itafikia mwisho"
Daniel 8:20-21
Maelezo ya jumla
Katika mistari hii, malaika anamwelezea Danieli maana ya kimfano ya vitu alivyoviona katika maono yake. Wanyama na pembe kiuhalisia zinawakilisha watawala wa kibinadamu na falme.
pembe mbili ni
"pembe mbili zinawakilisha"
wafalme wa Umedi na Uajemi
Maana zinazokubalika ni 1) hii inarejelea wafalme wa Umedi na Uajemi au 2) hiki ni kiwakilishi cha falme za Umedi na Uajemi.
mfalme wa Ugiriki
Maana zinazokubalika 1) hii inarejelea mfalme wa Ugiriki au 2) hiki ni kiwakilishi cha ufalme wa Ugiriki.
Pembe kubwa katikati ya macho yake
"Pembe kubwa katikati ya macho yake inawakilisha"
Daniel 8:22-23
Na kuhusu pembe iliyovunjika.... pembe zingine nne zilichipuka
"mahali ambapo pembe kubwa ilivunjikia, pembe zingine nne zilizuka"
Maelezo ya jumla
Katika mistari hii, malaika anamwelezea Danieli maana ya mifano ya vitu vile alivyoona katika maono yake. Pembe kiuhalisia zinawawakilisha watawala wa kibinadamu au falme.
falme nne zitakazoinuka kutoka katika taifa lake
Pembe nne zinawakilisha falme mpya nne. Hii yaweza kuwekwa wazi. " zinawakilisha falme nne ambazo ndani yake ufalme wa mfalme wa kwanza utagawanyika."
lakini hazitakuwa na nguvu kubwa
"lakini hazitakuwa na nguvu nyingi kama mfalme aliyewakilishwa na pembe ndefu"
Katika siku zijazo za falme hizo,
Kama falme zile zilipokaribia mwisho"
watakuwa wamefikia kikomo
"wamefikia ukamilifu wao"
uso katili
Hii ina maana kwamba mtu huyo anaonekana akiwa na ukatili au mkaidi aliyekataa kutii.
Daniel 8:24-25
Maelezo ya jumla
Katika mistari hii, malaika anamwelezea Danieli maana ya ishara ya vitu ambavyo aliviona katika maono yake. Wanyama na pembe zinawakilisha watawala wa kibinadamu au falme.
lakini si kwa nguvu zake mwenyewe
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo chanya. "lakini mtu fulani atampa nguvu zake"
Ataufanya udanganyifu usitawi
Hapa neno "udanganyifu" unaongelewa kana kwamba alikuwa ni mtu ambaye atafanikiwa. "kiwango cha uongo utaongezeka"
chini ya mkono wake
Hapa "mkono" unarejelea utawala wake. "chini ya utawala wake."
Mfalme wa wafalme
HIi inamrejelea Mungu
akini si kwa mkono wowote wa binadamu
Neno ''mkono'' lina maana ya nguvu/mtawala.
Daniel 8:26
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kumwagiza Danieli juu ya maono ambayo Danieli aliyaona.
uyafunge maono haya
Malaika anaongea juu ya maono kana kwamba lilikuwa ni gombo ambalo laweza kufungwa kwa chapa ya nta. Na hii humzui kila mtu asiweze kuona kile kilichomo mpaka pale chapa yake itakapovunjwa.
Daniel 8:27
nilichoka sana na nikalala nikiwa dhaifu kwa siku kadhaa
"alikuwa amechoka na alilala kitandani akiwa anaumwa kwa siku kadhaa"
nikaenda kufanya kazi za mfalme
"nilifanya kazi ambazo Mfalme alikuwa amenipangia"
nilikuwa nimetishwa sana na maono
"Nilikuwa nimeshangazwa na maono" au " nilichanganywa na maono"
Daniel 9
Daniel 9:1-2
Maelezo ya jumla
Sura ya 7 na ya 8 haziko katika mtririko wa moja kwa moja. Zilitokea wakati Belshaza alipokuwa akali ni mfalme. Sura ya 8 imeyarudia matukio ya utawala wa Dario ambaye alikuwa mfalme katika sura ya 6.
Alikuwa na Ahasuero ambaye alifanywa mfalme juu ya ufalme wa watu wa Babeli.
Haya ni maelezo ya nyuma kumhusu Ahasuero alikuwa ni nani.
ambaye alifanywa mfalme juu ya ufalme wa watu wa Babeli.
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambaye alikuwa mfalme juu ya Wababeli" au "ambaye aliwashinda Wababeli."
juu ya ufalme
"juu ya nchi"
kungekuwa na miaka sabini hadi mwisho wa kuachwa kwa Yerusalemu ungefika.
"tangu kipindi cha kuangushwa kwa Yerusalemu, itabaki katika hali ya ukiwa kwa miaka 70"
kuachwa
Hii ina maana ya kwamba hakuna ambaye angeweza kusaidia au kuijenga tena Yerusalemu katika kipindi kile.
Daniel 9:3-4
Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu
Hapa "uso" unawakilisha kusudi la Danieli. "Nililielekeza kusudi langu kwa Bwana Mungu"
kumtafuta yeye
Wale wanaotaka kumjua Yahweh na kumpendeza Yeye wanasemwa kana kwamba walikuwa wakimtafuta ili kumpata Yahweh.
kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu.
Hizi ni ishara za matendo ya toba na huzuni
niliungama dhambi zetu
"Nilikiri dhambi zetu"
hutunza maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wanaokupenda
"hufanya kile alichokisema angelikifanya katika agano lake na hutunza ahadi zake ili kuwapenda wale"
Daniel 9:5-6
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kumwomba Mungu juu ya watu wa Israeli.
Tumetenda dhambi na tumefanya yaliyo mabaya
Virai hivi viwili vinaelezea wazo moja katika njia mbili ili kutia mkazo.
Tumeenenda kwa uovu na tumeasi
Virai hivi viwili vinaelezea wazo moja katika njia mbili ili kutia mkazo.
amri na maagizo yako
Maneno haya "amri na maagizo" yana maana moja na yanarejelea sheria zote kwa ujumla.
Hatujawasikiliza watumishi wako
Mahali hapa "hatujawasikiliza" ina maana kwamba hawakuutii ujumbe wao.
kwa jina lako
Neno "jina" linarejea mamlaka ya Mungu. "kuzungumza kwa mamlaka"
watu wote wa nchi
Mahali hapa neno "nchi" linairejelea Israeli. "watu wa Israeli."
Daniel 9:7-8
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kumwomba Bwana kwa ajili ya watu wa Israeli.
Kwako Bwana, kuna uadilifu
Nomino dhahania "uadilifu" yaweza kuelezwa kwa kutumia kitenzi. "Bwana, wewe unatenda kwa uadilifu"
Hata hivyo, kwetu kuna aibu katika nyuso zetu, kwa..
Nomino dhania "aibu" yaweza kuelezwa kama kitenzi. "Lakini kwetu, tumeaibika kwa ajili ya hayo ambayo tumeyatenda"
kwetu sisi
neno "sis" linamjumuisha Danile na waisraeli, lakini halimjumuishi Mungu.
kuna aibu katika nyuso
Nahau hii ina maana ya aibu yao inaonekana kwa watu wote.
kwasababu ya udanganyifu mkubwa tulioufanya
"kwa kuwa tumekusaliti wewe " au "kwasababu tumekuwa si waaminifu kwako"
Daniel 9:9-11
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kumwomba Bwana kwa ajili ya watu wa Israeli.
Kwa Bwana Mungu wetu kuna huruma na msamaha
Kuwa na sifa hizi kunasemwa kana kwamba kumilikiwa na Bwana. "Bwana Mungu wetu ni mwenye huruma na msamaha."
Hatujaitii sauti ya Yahweh
Mahali "sauit'' inarejelea maagizo ambayo Yahweh aliyasema. "hatujatii kile ambacho Yahweh ametuambia kukifanya"
kugeukia upande,
Maneno "kugeukia upande" yana maana kwamba Israeli iliacha kuzitii sheria za Mungu.
vilivyoandikwa katika sheria ya Musa
Maneno haya yaweza kuandikwa kwa muundo tendaji. "ambavyo Musa aliyaandika katika sheria"
zimemwagwa juu yetu
Wingi wa laana na kiapo vinasemwa kana kwamba yalikuwa ni maji yamemwaga. "Umeleta juu yetu"
Daniel 9:12-14
Maelezo ya jumla
Danieli anaendelea kumwomba Bwana kwa ajili ya watu wa Israeli.
Kwa kuwa chini ya mbingu yote ...... na kile kilichofanyika huko Yerusalemu
Danieli anatia chumvi kuonesha huzuni yake kubwa juu ya Yerusalemu. Miji mingi imekwisha haribiwa kweli.
haijawahi kufanyika kitu chochote
"hakuna kilichofanyika"
kile kilichofanyika huko Yerusalemu
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Kile mlichokifanya katika Yerusalemu"
kama ilivyoandikwa kwenye sheria ya Musa
Muundo tendaji waweza kutumika. " Kama Musa alivyoandika katika sheria"
kugeuka na kuacha maovu yetu
Kuacha matendo mabaya kunasemwa kana kwamba ni kugeuka kutoka katika uovu. "kuacha matendo yetu mabaya"
Yahweh ameyaweka tayari maafa
"Yahweh amekwisha kuandaa majanga"
bado hatujaitii sauti yake.
mahali hapa "sauti" inarejelea mambo ambayo Yahweh alikuwa ameyaagiza. "hatujafanya yale uliyotuambia tuyafanye"
Daniel 9:15-16
mkono wenye nguvu
Mahali "mkono wenye nguvu" una maana ya "nguvu"
umejifanyia jina maarufu kwa ajli yako mwenyewe, hata siku hii ya leo
"umewafanya watu kujua jinsi ulivyo mkuu, kama vile ulivyo hata leo"
Lakini bado tumekutenda dhambi; tumefanya mambo ya hila
Vishazi hivi viwili kimsingi vinamaanisha kitu kimoja na vimetumika kwa pamioja kwa ajili ya kutia mkazo juu ya dhambi ilivyo mbaya.
tumekutenda dhambi; tumefanya mambo ya hila
Danieli na Waisraeli walitenda dhambi na kufanya mambo mabaya, lakini kiwakilishi "tu"hakimjumuishi Mungu.
hasira na ghadhabu yako
Maneno " hasira na ghadhabu" yana maana moja na yametumika hapa kwa ajili ya kutia mkazo juu ya hasira ya Mungu ni ya hatari inapotenda kazi"
Mlima wako mtakatifu
Mlima huu waweza kuwa mtakatifu kwasababu Hekalu la Mungu liko pale. "Mlima ambako hekalu lako takatifu liko"
dhambi zetu....baba zetu
Mahali hapa neno "zetu" linamrejelea Danieli na Israeli, lakini si kwa Mungu.
kitu cha kudharauliwa
"lengo la kutoheshimiwa"
Daniel 9:17-19
Basi sasa
Hii haina maana ya "wakati huu", bali ni njia ya kuonesha kwamba jambo jingine linalofuata katika maombi ya Danieli liko karibu kuanza.
mtumishi wako na maombi yake kwa ajili ya rehema;
Maneno "mtumishi wako" na "yake" yanamrejelea Danieli. Anajiongelea yeye mwenyewe katika nafsi ya tatu kama ishara ya heshima kwa Mungu.
maombi kwa ajili ya rehema
"dua kwa ya huruma"
ufanye uso wako ung'ae
Mwandishi anamwongelea Yahweh akitenda kwa neema kana kwamba Uso wa Yahweh uling'aa kwa mwanga.
sehemu yako takatifu
Inarejelea hekalu la Yerusalemu
fungua masikio yako na usikie
"kufungua masikio yako na kusikia" ni nahau yenye maana ya kusikia. Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kile kile na kukazia hamu ya Danieli kwa Mungu ili ayasikilize maombi yake.
unaoitwa kwa jina lako
Mahali hapa "jina'' linawakilisha umiliki. "ni mali yako"
usichelewe
Hii yaweza kuelezwa kwa sentensi chanya. "fanya haraka"
Daniel 9:20-21
watu wangu
"watu wa Israeli ambako mimi ninatokea"
Mlima mtakatifu wa Mungu
Mlima waweza kuwa mtakatifu kwasababu ya hekalu. "mlima ambako kuna hekalu takatifu la Mungu"
mtu Gabrieli
Huy ni Gabrieli yule yule ambaye alionekana katika umbo la Mwanadamu katika 8:15
katika ndoto hapo awali,
Hii yaweza kurejelea maono ya mwanzo ambayo Danieli aliyaona wakati alipokuwa macho.
alipaa kwa kasi kushuka kuja nilipo
"alipaa haraka akija nilipo"
wakati wa sadaka ya jioni
Watu wa Kiyahudi walitoa sadaka kila jioni kabla jua halijazama.
Daniel 9:22-23
utambuzi na ufahamu
Maneno "utambuzi na ufahamu" yanamaanisha kitu kile kile na yanatia mkazo kwamba Gabrieli atamsaidia Danieli kuuelewa ujumbe.
amri ilitolewa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu alitoa amri"
tafakari neno hili
Mahali hapa "neno" linarejelea ujumbe wote. "firikiria juu ya ujumbe huu"
ufunuo
Hii inarejea nyuma kwa unabii wa Yeremia katika 9:1
Daniel 9:24-25
Miaka sabini na saba zimeamriwa kwa ajili ya watu wako na mji wako mtakatifu
Mungu alitoa amri kwamba angefanya mambo kwa ajli ya watu na mji mtakatifu
Miaka sabini na saba...majuma saba na majuma sitini na mbili.
Hii si njia ya kawaida ya kuhesabu kwa Waisraeli. Kama itawezekana tafsiri kwa njia ambayo itatunza matumizi ya namba saba. "sabini mara miaka saba...saba mara miaka saba... sitini na mbila mara miaka saba"
watu wako na mji wako mtakatifu
Neno "wako" linamrejelea Danieli. Watu ni Waisraeli na mji mtakatifu ni Yerusalemu.
kukomesha hatia na kumaliza dhambi
Wazo limerudiwa ili kutia mkazo juu ya jinsi jambo hili litakavyotokea.
kutimiza maono
Hapa maneno 'kutimiza maono" ni nahau yenye maana ya kuhitimisha. "kukamilisha maono"
maono na unabii
Maneno haya katika muktadha huu yana maana moja. Yanatoa uhakika kwa Danieli kwamba maono ya Yeremia yalikuwa ni unabii kweli.
Ujue na kufahamu
Maneno haya yametumika kwa pamoja kuonesha na kuufanya umuhimu uwe wazi.
Mpakwa mafuta
Kutia mafuta ni tendo la ishara linaloonesha kwamba mtu fulani alichaguliwa. "Mtu yule ambaye Mungu anamtia mafuta"
kutakuwa na majuma saba na majuma sitini na mbili.
Haya yakiwekwa pamoja ni 69 kati ya 70 saba ilivyoongelewa ni 24.
Yerusalemu itajengwa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "watu wataijenga Yerusalemu"
handaki
ni shimo chini ya ardhi kuuzunguka mji au jengo, mara kwa mara huwa na maji ndani yake.
kwa nyakati za shida
"muda wa mateso makubwa"
Daniel 9:26
sitini na mbili saba
Hii si njia ya kawaida ya kuhesabu kwa Waisraeli. Kama inawezekana jaribu kuhifadhi matumizi ya namba saba.
mtiwa mafuta ataharibiwa na atakuwa hana kitu chochote
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "watu watamharibu mpakwa mafuta na hatakuwa na kitu"
mpakwa mafuta
kupaka mafuta ni tendo la ishara linaloonesha kwamba mtu fulani amechaguliwa.
kiongozi ajaye
Huyu ni mtawala wa kigeni, si "mpakwa mafuta"
Mwisho wake utatatokea kwa gharika,
Jeshi litauharibu mku na sehemu takatifu kama vila gharika linavyoharibu vitu.
Uharibifu umekwisha amriwa.
Kauli hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu amekwisha amuru kuuharibu mji na mahali patakatifu."
Daniel 9:27
Ata....ata...
Hii inamrejelea mtawala akayekuja ambaye atamharibu mpakwa mafuta.
miaka saba...Katikati ya miaka saba
Mahali neno "saba" limetumika kurejelea kipindi cha miaka saba.
atakomesha
"kuacha" au "kusimamisha"
dhabihu na sadaka
maneno haya kimsingi yanamaanisha kitu kile kile. Marudio yanaonesha kwamba mtawala ajayea atakomesha aina zote za sadaka.
mtu atakayeleta ukiwa
Mtu ambaye atateketeza kabisa"
Mwisho kamili na uharibifu umeamriwa kutokea kwa yeye aliyesababisha ukiwa.
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu ameamuru kwamba ataleta mwisho kamili na uharibifu"
Mwisho kamili na uharibifu
Maneno haya mawili yana maana moja. Yanatia mkazo juu ya uhalali na ukamilifu wa uharibifu.
yeye aliyesababisha ukiwa
"mtu ambaye ataleta uharibifu"
Daniel 10
Daniel 10:1
Katika mwaka wa tatu wa Koreshi mfalme
"mwaka wa 3 wa utawala wa Koreshi mfalme"
ujumbe ulifunuliwa kwa Danieli
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu aliufunua ujumbe kwa Danieli"
ufumbuzi
"ufahamu"
Daniel 10:2-3
Sikula chakula kizuri
Hakuna chakula cha gharama kubwa au chakula adimu
mpaka ukamilifu wa wiki tatu nzim
"hadi mwisho wa majuma matatu mazima"
Daniel 10:4-6
4Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza,
Huu ni mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiebrania. Siku ya ishirini na nne iko karibu na katikati ya mwezi wa Aprili matika kalenda ya Magharibi.
akiwa na mkanda kiunoni mwake
"na alikuwa amevaa mkanda"
Ufazi
Ufazi ni sehemu. sehemu yake haijulikanai.
Mwili wake ulikuwa kama kito
Mwlii wake uling'ara kwa mwanga wa bluu na njano kana kwamba ulikuwa umetengenezwa kwa kito.
kito
jiwe la thamani lenye rangi ya bluu au njano.
na sura yake ilikuwa kama radi
Sura yake iling'aa kama mwali wa radi unavyong'ara.
Macho yake yalikuwa kama miali ya tochi
Macho yake yalikuwa yanang'aa kwa mwanga kana kwamba yalikuwa miali ya tochi.
mikono yake na miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosafishwa
Mikono yake na miguu yake ilikuwa iking'aa kana kwamba ilikuwa imetengenezwa kwa shaba iliyosafishwa.
Sauti ya maneno yake ilikuwa kama sauti ya umati mkubwa wa watu
Sauti yake ilikuwa na nguvu sana kwamba ilikuwa ni kundi kubwa la watu wengi likiongea kwa sauti ya juu.
Daniel 10:7-9
Hivyo niliachwa peke yangu
"Hakuna yeyote aliyekuwa pamoja nami, na niliona"
mwonekano wangu wa kung'aa ulibadilika na kuwa mwonekano wa uharibifu
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "mwonekano wangu unaong'aa ulibadilika kuwa katika mwonekano ulioharibiwa"
mwonekano wangu wa kung'aa
Hii inaelezea juu ya uso wa mtu fulani ambaye ana afya nzuri.
Mwonekano ulioharibiwa
Uso mbaya, usio na afya na wa kikatili unasemwa kana kwamba ni jengo.
Nilisikia maneno yake
Hii ina maana kwamba mtu fulani alikuwa anazungumza katika maono. Hii yaweza kuwekwa wazi. "Nilisikia maneno ya mtu aliyekuwa anaongea"
nilianguka kifudifudi na kupata usingizi mzito
Danieli aliogopeshwa na kile alichokiona na ya kwamba huenda alilala chini ardhini, mahali ambapo alizimia.
Daniel 10:10-11
Mkono ulinigusa
Hii ni lugha ya picha inayowakilisha mtu, huenda ni mtu yule ambaye Danieli alimwona.
Danieli, mtu aliyetunzwa
Hii pia yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji."Danieli, wewe ambaye Mungu anakuhifadhi sana"
aliyetunzwa sana
anayethaminiwa na kupendwa sana
Daniel 10:12-13
ulipoiweka akili yako kutaka kufahamu
"ulihitaji kufahamu maono"
maneno yako yalisikiwa
Kauli hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu aliyasikia maneno yako"
Mwana wa mfalme
hii inarejelea roho ambayo ina mamlaka juu ya taifa la mtu.
mfalme wa Uajemi
Hii huenda inarejelea wafalme mbalimbali waliotawala mataifa mbalimbali katika dola ya Uajemi, na wale waliopaswa kumtii mfalme wa Uajemi.
Daniel 10:14-15
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli
niligeuza uso wangu na kuuelekeza chini
"Niliangalia chini ardhini" Danieli huenda alifanya hivi ili kuonesha unyenyekevu katika heshima kubwa, au kwasababu alikuwa ameogopa.
Daniel 10:16-17
Yeye aliyekuwa kama wana wa mtu
Kauli hii inamrejelea yeye ambaye alikuwa ameongea na Danieli. Ingawa, baadhi ya matoleo hutafsiri kwamba alikuwa anamrejelea mtu mwingine tofauti.
kama wana wa mtu
Maelezo haya yanawarejelea watu kwa ujumla
masumbuko
mateso makali ya kihisia
Mimi ni mtumishi wako. Je ninawezaje kuongea na Bwana wangu?
Danieli anauliza swali hili kumaanisha kwamba yeye hawezi kuongea na malaika kwasababu yeye halingani na malaika. Sentensi hizi zaweza kuunganishwa. "siwezi kukujibu wewe kwasababu mimi ni mtumishi wako"
hakuna pumzi iliyosalia ndani yangu."
Nahau hii inarejelea upumuaji. "Siwezi kupumua" au "ni vigumu sana kupumua"
Daniel 10:18-19
ule mwenye mwonekano wa mtu
"Yeye anayeonekana kama mtu"
Uwe mwenye nguvu, uwe na nguvu
Maneno "Uwe mwenye nguvu" yamerudiwa kwa ajili ya kutia mkazo.
mtu ulithaminiwa sana
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "wewe ambaye Mungu amekuthamini sana"
umenitia nguvu
Kauli hii pia yaweza kuandikwa kwa muundo tendaji."Nilikuwa mwenye nguvu"
Daniel 10:20-21
mkuu wa Uajemi
"mkuu" hurejelea roho ambayo inatawala na kulilinda taifa la watu. "mkuu wa roho ya uajemi"
Lakini nitakwambia
Hii ina maana kwamba Malaika atamwambia Danieli juu ya hili muda mfupi kabla hajaenda mbali.
kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Ukweli
Kauli hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "kile Kitabu cha Ukweli kinayasema" au "kile ambacho mtu fulani alikiandika katika Kitabu cha Ukweli.
yeyote anayejionesha kuwa na nguvu
"yeye anayejihakikisha kuwa na nguvu"
isipokuwa Mikaeli mkuu wenu
Kirai hiki chaweza kuelezeka kama sentensi inayojitegemea. "Mikaeli mkuu wako ni yeye pekee ambaye huyatenda haya"
Mikaeli mkuu wenu
Neno "wenu" liko katika wingi. Linamrejelea Danieli na watu wengine waliosalia wa Israeli.
Mkuu
Angalia jinsi ulivyotafsiri "mkuu" inapomrejelea Mikaeli katika 10:12.
Daniel 11
Daniel 11:1-2
Maelezo ya jumla
Katika Danieli 11:1 hadi 12:4, yeye aliyekuwa akiongea na Danieli katika sura ya 10 anamwambia kile kilichoandikwa katika kitabu cha ukweli. Hiki ni kama kile alichosema angekifanya katika 10:20.
Katika mwaka wa kwanza wa Dario
Dario alikuwa ni Mfalme wa Umedi. "Mwaka wa kwanza" hurejelea mwaka wa kwanza ambao alikuwa Mfalme.
Wafalme watatu watainuka katika Uajemi,
"Wafalme watatu watatawala juu ya Uajemi"
na mfalme wa nne atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote
"baada yao mfalme wa nne atakuja kutawala ambaye atakuwa na fedha nyingi kuliko watatu waliomtangulia"
nguvu
Maana zinazoweza kukubalika ni 1)mamlaka au 2) nguvu za kijeshi
atamwamsha kila mtu
"atamsababisha kila mtu atake kupigana"
Daniel 11:3-4
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
Mfalme wenye nguvu atainuka
Wazo la kusimama au kuinuka mara kwa mara limetumika kwa ajili ya mtu anayekuwa na nguvu.
ambaye atatawala ufalme mkubwa
Maana zinazokubalika ni 1)ukubwa wa ufalme huu utakuwa wa ajabu, au 2) kwamba mfalme angetawala ufalme wake kwa nguu kubwa.
falme wake utavunjika na utagawanyika
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ufalme wake utavunjika na kugawanyika" au "ufalme wake utavunjika katika vipande vipande"
pepo nne za mbinguni
Angalia jinsi ulivyofasiri 7:1
lakini hawatakuwa wazao wake mwenyewe,
Wazo la kutokugawanywa linamaanishwa hapa. "Lakini hautagawanywa kwa watoto wake mwenyewe"
falme wake utang'olewa kwa ajili ya wengine tofauti na wazawa wake
Ufalme unaongelewa kana kwamba ni mmea ambao mtu fulani anaweza kuuharibu kwa kuung'oa. Wazo hili laweza kuelezeka kwa muundo tendaji. "utawala mwingine utaung'oa na kuuharibu ufalme wake, na watu wengine ambao siyo watoto wake watautawala.
Daniel 11:5-6
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli
mmoja kati ya maamiri jeshi wake atakuwa mwenye nguvu kuliko yeye na atautawala ufalme wake kwa nguvu kubwa
Kamanda wa mfalme wa Kusini atakuwa Mfalme wa Kaskazini.
watafanya mwungano
Mfalme wa Kusini atafanya ushirika na Mfalme wa Kaskazini. Mwungano huu utakuwa wa makubaliano rasmi ambayo kila taifa lazima kuyafuata.
Binti wa mfalme wa Kusini atakuja kwa mfalme wa Kaskazini kuyathibitisha makubaliano yao.
Mfalme wa Kusini atampa binti yake mfalme wa kusini ili amwoe. Ndoa itathibitisha makubaliano kati ya wafalme hawa wawili.
nguvu za mkono wake.... mkono wake
Mahali hapa "mkono" unatumika kumaanisha nguvu.
Ataachwa
Hii inarejelea hila ya kuuliwa kwa binti na wale ambao wamefanya mwungano. Kirai hiki chaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " Watamwacha"
Daniel 11:7-9
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli
tawi kutoka katika mizizi
Familia inaongelea kana kwamba ni mti. Mizizi inawakilisha mababu, na matawi yanawakilisha wazawa.
mizizi yake
Neno "yake" inarejelea kwa binti wa mfalme wa Kusini katika 11:5
Atalishambulia jeshi
Kiwakilishi "a" kinarejelea uzao wake, na hapa pia inawakilisha jeshi lake.
Atapigana nao
Mahali hapa neno "nao" inawakilisha wanajeshi wa jeshi la adui.
lakini atajitoa
Kiambishi 'a' kinamrejelea mfalme wa Kaskazini.
Daniel 11:10
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli
Wana wake
"wana wa mfalme wa Kaskazini"
kuunganisha jeshi kubwa
"kukusanya watu wengi kwa pamoja ambao wanaweza kupigana katika vita"
litagharikisha kila kitu
Kitendo cha jeshi kubwa kuivamia na kuijaza nchi yote kitakuwa sawa na maji ya gharika.
Daniel 11:11-12
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
atainua jeshi kubwa
"atakusanya jeshi kubwa"
jeshi litatiwa katika mkono wake
Mahali hapa neno "mkono" linawakilisha utawala wa mfalme
Jeshi litachukuliwa
Hii yaweza kuandikwa kwa muundo tendaji. "Mfalme wa Kusini ataliteka jeshi la Kaskazini"
utainuliwa juu
Kuinuliwa juu kunawakilisha wazo wa kuwa na kiburi.
atawafanya makumi maelfu kuanguka
Mahali hapa kuanguka kunawakilisha kufa katika vita.
makumi maelfu
"Maelfu mengi"
Daniel 11:13
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
jeshi kubwa likiwa na vifaa vingi
Hii pia yaweza kuandikwa kwa muundo tendaji. "jeshi kubwa ambalo litakua na zana za kutosha"
Daniel 11:14
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
wengi watainuka kinyume na mfalme
Mahali hapa wazo la kuinuka linawakilisha uasi. "watu wengi wataasi kinyume na mfalme"
Wana wa vurugu
Maelezo haya yanasimama kwa ajili ya watu wenye vurugu
watajikwaa
Mahali hapa kitendo cha kujikwaa kinamaanisha kuanguka.
Daniel 11:15-16
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
Mfalme wa Kaskazini atakuja
Hapa "mfalme wa Kaskazini" anajumuisha na jeshi lake pia. "Jeshi la mfalmw wa Kaskazini litakuja"
kuizingira nchi kwa kuweka vilima
Hii inarejelea kitendo cha kurundika udongo ili wanajeshi waweza kuufikia urefu wa ukuta wa mji iili kuwashambulia. Wanajeshi na watumwa wataweka udongo kwenye vikapu na kuvibeba hadi mahali sahihi, na kuumwaga ili kuinua kilima cha udongo.
Mfalme wa Kaskazini atakuja, kuizingira nchi kwa kuweka vilima
"Mfalme wa Kaskazini" hapa inamaanisha wanajeshi katika jeshi la mfalme, ambao wangefanya kazi halisi ya kutengeneza vilima vya udongo.
ngome
Kuta na vitu vingine vilivyojengwa ili kulinda mji
Hawatakuwa na nguvu za kusimama
Mahali hapa kitendo cha kusimama kinawakilisha uwezo wa kupigana.
yeye ajaye ataenenda kwa kufuata tamaa zake kinyume chake
"Mfalme atakayevamia atafanya kili kitu anachokitaka kinyume na mfalme mwingine."
Atasimama
Mahali hapa kusimama kuna maana ya kutawala
nchi ya uzuri
Hii inarejelea nchi ya Israeli . angalia ulivyotafsiri katika 8:9
uharibifu utakuwa mkononi wake
Mahali hapa "uharibifu" unawakilisha nguvu ya kuharibu. Pia, nguvu ya kuharibu inasemwa kana kwamba kilikuwa ni kitu ambacho mtu anaweza kukishikilia katika mikono yake.
Daniel 11:17-19
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli
atauelekeza uso wake
"kuamua"
kuja kwa nguvu
Hii huenda inarejelea juu ya nguvu za kivita.
binti wa wanawake
Hii ni njia ya madaha ya kusema "mwanamke"
atakikomesha kiburi chake
"atamfanya mfalme wa Kaskazini asiwe na atakisababisha kiburi chake kiishekiburi"
atakisababisha kiburi chake kiishe
"atamsababisha mfalme wa Kusini ateseke kwasababu alikuwa na kiburi dhidi ya wengine"
atafuatilia
"Mfalme wa Kaskazini atazingatia"
hatapatikana
Hii ni njia ya kusema kuwa atakufa. Wazo hili laweza kuandikwa kwa muundo tendaji. "atatoweka" au "atakufa"
Daniel 11:20-22
mtu mwingine atainuka
Kuinuka katika nafasi ya mfalme inawakilisha kufanyika kuwa mfalme katika nafasiya mfalme aliyepita.
atamfanya mtoza ushuru apite
mtoza ushuru atapita katika nchi akiwalazimisha watu walipe kodi.
atakatiliwa mbali
Kiambishi 'a' kinamrejelea mfalme mpya. Kukatiliwa mbali ina maana ya kufa.
lakini si kwa hasira
Maana zinazokubalika 1) hakuna hata mmoja aliyekuwa na hasira na mfalme 2) tuko hilo na sababu ya kifo cha mfalme yalitunzwa kama siri.
mtu wa kudharauliwa ambaye watu hawatampa heshima ya nguvu ya kifalme
Watu watakataa kumheshimu kama mfalme kwasababu yeye si mzawa wa wafalme.
jeshi litafutiliwa mbali kama gharika
Kufutiliwa mbali kunawakilisha hali ya kuharibiwa. Hii pia yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji."jeshi lake litaangamiza kabisa jeshi kubwa kama gharika linavyoteketeza kila kitu katika njia yake"
Jeshi na kiongozi wa agano wataangamizwa wote kwa pamoja
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ataliangamiza jeshi na kiongozi wa agano"
kiongozi wa agano
Kirai hiki kinamrejelea mtu alijawa na nafasi muhimu ya kidin ambayo Mungu anaihitaji katika agano, ambaye ni kuhani mkuu (ambaye aliuawa katika mwama 171 KK)
Daniel 11:23-24
Tangu katika kipindi kile ambacho makubaliano yalifanywa pamoja naye
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "wakati viongozi wengine walipofanya mkataba wa amani pamoja naye"
Atagawanya mateka, nyara, na mali zake miongoni mwa wafuasi wake
"atagawa kwa wafuasi wake"
mateka, nyara, na mali
"vitu vya thamani ambaye yeye na jeshi lake walichkua kutoka kwa watu waliowashinda"
Daniel 11:25-27
Ataamsha nguvu zake na moyo wake
Nguvu na moyo (ni ujasiri) vinaongelewa kana kwamba walikuwa ni watu ambao mtu fulani angeweza kuwaamsha ili watendo tendo.
moyo
Mahali hapa unawakilisha ujasiri
atapigana vita
"atapigana kinyume chake"
jeshi kubwa
"pamoja na jeshi kubwa ambalo atalikusanya"
hataweza kusimama
Kutokusimama kunawakilisha hali ya kushindwa.
wanaokula chakula chake kizuri
Hii inarejelea washauri wa mfalme. Ilikuwa na kawaida kwa washauri waliominiwa na mfalme kula chakula pamoja naye.
jeshi lake litakatiliwa mbali kama gharika,
Mahali hapa kushindwa kabisa kwa jeshi kunasemwa kana kwamba lilikuwa ni gharika la maji ambalo hulifutilia mbali.
wengi wao watauawa
Hii inarejelea kufa katika vita.
wakiwa na mioyo yao imejawa na uovu kinyume na mwenzake
Mahali hapa neno "moyo" linawakilisha tamaa za mtu. Tamaa zinaongelewa kana kwamba kilikuwa ni kitu ambacho mtu anaweza kukiweka katika mkao fulani.
watakaa katika meza moja
Kukaa katika meza moja kuna maanisha kitendo cha kuongea pamoja na mtu mwingine.
haitakuwa na maana yoyote
"lakini mazungumzo yao hayatawasaidia"
Kwa kuwa mwisho utatokea katika kipindi ambacho kimeshapangwa
Hii inatuambia kwamba mkutano wao hautakuwa na mafanikio.
Daniel 11:28
moyo wake ukipinga vikali agano takatifu
Hii inarejelea tamaa ya mfalme ya kupinga agano la Mungu na waisraeli. Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Atafahamika kwa kupinga agano takatifu."
moyo
Hii inarejelea tamaa za mfalme
agano la takatifu
Mahali hapa "takatifu" inaelezea juu ya agano la Mungu na Israeli. Ina maana kwamba agano lazoma liheshimiwe na liheshimiwe kwasababu linatoka kwa Mungu mwenyewe.
ukipinga vikali agano takatifu
Hamu ya mfalme kutenda kinyume na agano takatifu inawakilisha hamu yake kuwazuia waisraeli waache kulitii agano takatifu.
atatenda
Hii ina maana kwamba mfalme atafanya matendo fulani katika Israeli.
Daniel 11:29-30
meli kutoka Kitimu zitamshambulia
Meli zinawakilisha jeshi likitoka katika meli hizo.
Kitimu
Hii inarejelea makazi katika kisiwa cha Kipro katika Bahari ya Meditraniani.
Atakuwa mwenye hasira
"atakasirika sana"
atawaonyesha mema wale
"atatenda kwa wema kwa wale" au "atawasaidia wale"
Daniel 11:31-32
Majeshi yake yatainuka
"Jeshi lake litatokea" au "jeshi lake litakuja" Neno "lake" linamrejelea mfalme wa Kaskazini.
sehemu takatifu katika ngome
"sehemu takatifu ambayo watu huitumia kama ngome"
Wataziondoa sadaka za kawaida
Kuondolewa kwa sadaka kunawakilisha kuwazuia watu wasitoe sadaka. "Watawazuia makuhani wasitoe sadaka za kawaida za kuteketezwa"
chukizo la uharibifu litakalosababisha ukiwa.
Hii inarejelea sanamu ambayo italifanya hekalu kuwa ukiwa, hii ina maana kwamba itamfanya Mungu aliache hekalu lake.
walioenenda kwa ouvu kinyume na agano
"waliliasi agano kwa kutenda uovu"
kuwatia uovu
"kuwashawishi watende dhambi"
wale wanaomjua Mungu wao
Mahali hapa neno "kujua" lina maana ya "kuwa mwaminifu,"
watakuwa jasiri na watachukua hatua.
"watakuwa imara na kuwapinga"
Daniel 11:33-35
watajikwaa
Mahali hapa " kujikwaa" inawakilisha kupatwa na majanga ya aina hii au nyingine, ikijumuisha na kifo chenyewe.
Upanga
Mahali hapa "upanga"unawakilisha mapigano na vita.
miali ya moto
Mahali hapa "miali" inawakilisha moto.
watatiwa mateka
"kufanywa kuwa mtumwa"
kunyang'anywa
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Maadui zao watawaibia mali zao"
watasaidiwa kwa msaada kidogo
Hii yaweza kuwekwa katika muundo tendaji. " watu wengine watampa msaada kidogo"
Watu wengi watajiunga nao wenyewe katika unafiki
Hii inarejelea watu wengine ambao watajifanya kuwasaidia watu wenye hekima, lakini si kwasababu wamekusudia kuwasaidia kweli.
watajiunga nao
Mahali hapa "watajiunga nao" ina maana ya "kuja na kuwasaidia"
ili kujisafisha kutokee kwao,
Neno "ili" lina maana kwamba "matokeo kwamba"
Baadhi ya watu wenye hekima watajikwaa
Mahali hapa " kujikwaa" inawakilisha kupatwa na majanga ya aina hii au nyingine, ikijumuisha na kifo chenyewe
kujisafisha kutokee kwao, na kujiosha, na kujitakasa
Matendo haya yanaelezwa hapa kana kwamba ilikuwa ni vitu. Ingawa, yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji au tendewa. "watasafishwa, kuoshwa na kutakaswa"
kujisafisha
Hii inarejelea kusafisha kito kwa kukiyeyusha katika moto. Wakati Mungu anawatengeneza watu wake ili wawe waaminifu kwake, kunasemwa kana kwamba walikuwa ni vito ambavyo mfanyakazi alikuwa akivifanya kuwa safi zaidi kwa kuviweka katika moto.
kujiosha,
Hii inarejelea kitendo cha kuwatengeneza watu, sehemu au vitu ili vifae kwa ajili ya Mungu kwa kuvitenga na dhambi au aina nyingine yoyote ya ubaya. Uovu unasemwa kana kwamba ni uchafu wa kawaida.
kujitakasa,
Hili wazo ni sawa na kujisafisha, lililojadiliwa awali. Kito kilichosafishwa chaweza kusemwa kwamba chaweza kutakaswa.
wakati wa mwisho.
"siku za mwisho" au " mwisho wa ulimwengu.
Kwa kuwa wakati ulioamriwa haujaja bado
Mahali hapa 'wakati ulioamriwa' ina maana kwamba Mungu amepanga muda. Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Yahweh amepanga muda kwa wakati ujao"
Daniel 11:36-37
Mfalme atafanya kutokana na matakwa yake
Mfalme atafanya chochote akitakacho"
Mfalme
Hii inamrejelea mfalme wa Kaskazini.
Atajiinua mwenyewe na kujifanya mkubwa
Kirai "Atajiinua mwenyewe" na "kujifanya kuwa mkubwa" vina maana sawa na vinaonesha kwamba mfalme atakuwa na kiburi.
Atajiinua mwenyewe
Mahali ina maana ya kuwa na kiburi.
kujifanya mkubwa
Hapa ina maana ya kujifanya kuwa mtu wa muhimu na mwenye nguvu.
atasema vitu vibaya
"vitu vya ajabu" au "vitu ya kusikitisha"
mpaka pale ghadhabu itakapokuwa imekamilika
Kirai hiki kinaonesha picha kwamba Mungu huhifadhi ghadhabu mpaka pale stoo yake itakapokuwa imejaa na kisha atakuwa tayari sawasawa na hasira hiyo.
Mungu wa miungu
Hii inamrejelea Mungu mmoja na wa kweli. "Mungu mkuu" au "Mungu pekee wa kweli"
mungu anayependwa na wanawake
Hii inaonekana kurejelea mungu wa kipagani aliyeitwa Tamuzi.
Daniel 11:38-39
mungu wa ngome
Huenda mfalme aliamini kwamba huyu mungu wa uongo angemsaidia kuzishambulia ngome za watu wengine na kuitunza ngome yake.
badala ya haya
Neno "haya" linarejelea miungu iliyotajwa
ataigawanya nchi kama thawabu
Maana zinazokubalika ni 1)"atawapa wafuasi wake nchi kama thawabu au 2) ataiuza nchi kwa wafuasi wake.
Daniel 11:40-41
wakati wa mwisho
"siku za mwisho" au " mwisho wa ulimwengu"
mfalme wa Kusini ...... Mfalme wa Kaskazini
Virai hivi vimesimama hapa kuwakilisha wafalme na majeshi yao.
atamshambulia
Hili ni shambulio la vurugu la jeshi linasemwa kana kwamba ni dhoruba imetokea.
kuwagharikisha
Kitendo cha jeshi kusambaa katika nchi kunasemwa kana kwamba ni gharika limetokea.
kupita katikati
jeshi hitazuiliwaa na chochote.
nchi ya uzuri,
Hii inarejelea nchi ya Israeli.
wataanguka
Mahali hapa kuanguka kuna maana ya kitendo cha kufa.
Lakini watu hawa watatoroka kutoka katika mkono wake
Mahali hapa "mkono" una maana ya nguvu. "Lakini watu hawa watatoroka kutoka katika nguvu zake"
Daniel 11:42-43
Maelezo ya jumla
Hii bado inamhusu mfalme wa Kaskazini.
Naye ataunyosha mkono katika nchi
Mahali hapa "mkono" unawakilisha nguvu na utawala.
Katika nchi
Hapa wazo ni kwamba nchi nyingi au nchi kadhaa
nchi ya Misri haitaokolewa
Hii yaweza kuwekwa katika muundo tendaji. ""Nchi ya Misri haitatoroka"
watu wa Libya na Ethiopia watakuwa chini katika nyayo za miguu yake
Hapa " nyayo za miguu" inawakilisha hali ya kujishusha/ utii. "watu wa Libya na Ethiopia watamtumikia"
watu wa Libya na Ethiopia
"watu waLIbya na Ethiopia" Libya ni nchi ya Magharibi mwa Misri, na Ethiopia ni nchi iliyo Kusini mwa Misri.
Daniel 11:44-45
Maelezo ya jumla
Hii bado inamhusu mfalme wa Kaskazini.
naye atatoka akiwa mwenye hasira nyingi
Nomino dhahania "hasira" yaweza kuelezwa kwa neno "ghadhabu" Yaweza kuelezwa wazi kwamba ataenda nje pamoja na jeshi lake.
atatoka
Hapa inawakilisha kitendo cha kuwashambulia maadui.
na kuwahifadhi kwa ajli ya uharibifu
"Kuwaharibu watu wengi"
hema ya makao yake
Hii inarejelea hema za starehe za mfalme ambazo aliishi ndani yake wakati alipokuwa pamoja na jeshi lake katika wakati wa vita.
milima ya uzuri wa utakatifu
Hii inarejelea mlima wa Yerusalemu mahali ambapo hekalu la Mungu lilikuwa.
Daniel 12
Daniel 12:1-2
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kumwagiza Danieli. Alianza katika 10:20
Mikaeli, jemedari mkuu
Mikaeli ni malaika mkuu. Mahali hapa pia amepewa jina jingine "jemedari mkuu"
watu wako wataokolewa
Mungu alifanya kitendo cha kuwaokoa watu. " Mungu ataokoa watu wako"
yeyote ambaye jina lake litapatikana katika kitabu
Mungu hufanya kazi ya kuandika katika kitabu. "wale ambao majina yao Mungu ameyaandika katika kitabu"
watu wako wataokolewa
Hii inarejelea tukio kubwa la kiroho ambapo watu wa Mungu watapewa maisha mapya, wote walio hai na walio kufa, na watu waovu watakatiliwa mbali katika hukumu ya milele.
Daniel 12:3-4
watang'ara kama mng'ao wa anga la juu,
Hii inawarejelea watu wa Mungu wakiwa wamejawa na utukufu wake kwahiyo watang'aa kama anga wakati juu likiwa linaangaza.
wale wenye kuwaelekeza wengine katika haki
Wale ambao huwasaidia wengine kuelewa kwamba wametengwa na Mungu wanasemwa kana kwamba walikuwa wanabadili mwelekeo walikuwa wakielekea. "ambaye huwafundisha wengine waishi katika haki"
watakuwa kama nyota milele na milele
Watu hawa watang'aa kama nyote. Hii ni tabia ya watu waliojawa na utukufu wa Mungu.
yafunge maneno haya; kihifadhi kitabu kikiwa kimetiwa chapa
Kuna mambo ambayo Danieli alikuwa ameoneshwa na kufunzwa na ya kwamba Danieli alikuwa ameambiwa kwamba asiyafunue katika kitabu hiki.
nyakati za mwisho
"siku za mwisho" au "mwisho wa ulimwengu"
Watu wengi watakimbia huku na kule, na maarifa yataongezeka.
Mambo haya yanaonekana kutokea wakati wa kufungwa kwa kitabu. Hii yaweza kuwekwa wazi. "Kabla ya kutokea haya, watu wengi watasafiri hapa na kule, wakijifunza mengi na mengi zaidi kuhusu vitu vingi"
Daniel 12:5-6
Maelezo ya jumla
Malaika amemaliza kuongea, na Danieli anaendelea kusema kile alichokiona baadaye katika maono yake tangu katika 10:4
kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama
"kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama"
Mmoja wao alimwambia mtu aliyevaa nguo za kitani,
Hii inamrejelea mtu aliyekuwa akiongea na Danieli, siyo mmoja wale watu waliokuwa wamesimama pembeni mwa mtu.
ukingo wa mto,
Maana zinazoweza kukubalika 1) malaika alikuwa juu ya mto au 2) malaika alikuwa mbali katika ukingo sambamba na mto.
Je itachukua muda gani mpaka mwisho wa matukio haya ya kushangaza?
"Matukio haya ya kushangaza yatadumu kwa muda gani?" Hii inarejelea mwanzo hadi mwisho wa matukio.
matukio haya ya kushangaza
Katika muda ule ambao malaika alikuwa akiongea na Danieli, hakuna hata tukio hata moja lilikuwa limetokea. Hii kwa uhalisia inarejelea matukio katika 12:1, na huenda yalijumuisha matukio yaliyo katika maono kutoka sura ya 11.
Daniel 12:7
mtu yule aliyevaa nguo za kitani
Hii yaweza kuelezwa katika muundo tendaji. " mtu aliyekuwa amevaa nguo za kitani"
mkondo wa mto
Maana zinazoweza kukubalika 1) malaika alikuwa juu ya mto au 2) malaika alikuwa mbali katika ukingo sambamba na mto.
yeye aishiye milele
"Mungu ambaye anaishi milele"
itakuwa kwa wakati, nyakati, na nusu wakati
Ni vizuri kuiacha katika utata kama ilivyoanza. Na kama utachagua sehemu ya kuanzia, miaka mitatu na nusu huenda itaanza pamoja na matukio ya 12:1.
wakati, nyakati, na nusu wakati
"miaka mitatu na nusu: Maneno "nyakati au wakati" kwa ujumla yanapaswa kufahamika kuwa yanarejelea miaka. Mwaka mmoja na miwili na nusu ni sawa na miaka mitatu na nusu.
mambo haya yote yatakuwa yamemalizika
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mambo haya yote yatatokea"
Mambo haya yote
Katika muda ule ambao malaika alikuwa akiongea na Danieli, hakuna hata tukio hata moja lilikuwa limetokea. Hii kwa uhalisia inarejelea matukio katika 12:1, na huenda yalijumuisha matukio yaliyo katika maono kutoka sura ya 11.
Daniel 12:8-9
Mambo haya yote
Katika muda ule ambao malaika alikuwa akiongea na Danieli, hakuna hata tukio hata moja lilikuwa limetokea. Hii kwa uhalisia inarejelea matukio katika 12:1, na huenda yalijumuisha matukio yaliyo katika maono kutoka sura ya 11.
maneno yamefungwa na kutiwa chapa
Maono ambayo Danieli alikuwa amepewa hayakupaswa kufafanuliwa kana kwamba kitabu kilikuwa kimefungwa na hakuna mtu yeyote awezaye kukifungua.
wakati wa mwisho.
"siku za mwisho: au "mwisho wa ulimwenguni"
Daniel 12:10-11
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
Watu wengi watakuwa wametakaswa, wameoshwa, na kusafishwa
Yahweh anafanya kazi ya kutakasa. Maneno haya matatu kimsingi yanamaanisha kitu kile kile.
kusafishwa
kusafishwa kwa kuondoa kila kitu kisichotakiwa sehemu ile.
lakini waovu wataenenda katika uovu
Watu waovu watateda yaliyo maovu au mambo ya dhambi.
Hakuna kati ya waovu atakayefahamu
Watu waovu hawawezi kufahamu mambo ya kiroho.
Lakini wenye hekima watafahamu
Hii inarejelea watu wale wenye hekima katika kumtii Yahweh watafahamu.
sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ...imeondolewa
Mfalme wa Kaskazini ndiye atakayekomesha sadaka katika hekalu.
chukizo la uharibifu liliosababisha ukiwa
Hii inarejelea sana ambayo italifanya hekalu liwe ukiwa, na hiyo ndiyo itamsababisha Mungu aliache hekalu katika hali ya ukiwa.
siku zipatazo 1,290
Mahali hapa "siku" inarejelea kipindi cha muda. Mara nyingine hueleweka kama siku, ingawa pia ina maana ya miaka.
Daniel 12:12-13
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
Ana heri mtu yule anayengojea
"amebarikiwa mtu ambaye anasubiri" au "ana heri yeyote anayengojea"
anayengojea
"kuvumilia" au "kubakia mwaminifu"
siku 1,335
Mahali hapa "siku" inarejelea kipindi cha muda. Mara nyingine hueleweka kama siku, ingawa pia ina maana ya miaka.
Unapaswa uondoke
"Danieli, lazima uende" Hii inamrejelea Danieli kuendelea kuishi na kumtumikia mfalme mpaka muda uliopangwa wa kifo chake.
utapumzika
Hii ni njia ya upole ya kusema kuwa "utakufa"
Utainuka
Hii inarejelea Ufufuo wa kwanza wa wafu wakati ambao watu wenye haki watafufuliwa.
ehemu uliyopewa
"sehemu ambayo Mungu amekupatia wewe"