Kiswahili: translationWords

Updated ? hours ago # views See on DCS

Names

Abiathari

Ufafanuzi

Abiathari alikuwa kuhani mkuu wa taifa la Israeli wakati wa mfalme Daudi. Mfalme Sauli alipowaua manabii, alitoroka na kwenda kwa Daudi nyikani. Abiathari na kuhani mkuu mwingine aitwaye Zadoki walimhudumia Daudi kwa uaminifu katika kipindi chote cha utawala wake. Baada ya kifo cha Daudi, Abiathari alijaribu kumsaidia Adoniya kuwa mfalme badala ya Sulemani. Kwa sababu hii mfalme Sulemani alimuondoa Abiathari kutoka kwenye ukuhani.


## Abimeleki ### Ufafanuzi Abimeleki alikuwa mfalme wa Wafilisti huko Gera katika kipindi ambacho Abrahamu na Isaka wanaishi katika nchi ya Kaanani. Abrahamu alimdanganya Abimeleki kwa kumwambia kuwa Sara alikuwa dada yake badala ya mke wake. Abrahamu na Abimeleki walikubaliana kuhusu umiliki wa visima vilivyopo Belisheba. Miaka mingi baadaye Isaka naye akamdanganya Abimeleki na watu wengine wa Gera kwa kumwambia kuwa Rebeka alikuwa dada yake na sio mke wake. Mfalme Abimeleki alimkemea Abrahamu na Isaka kwa kumdanganya. Mtu mwingine aliyeitwa Abimeleki alikuwa mtoto wa Gidioni na kaka wa Yoramu.
## Abinieri ### Ufafanuzi Abinieri alikuwa binamu wa mfalme Sauli katika agano la Kale. Abinieri alikuwa mkuu wa majeshi ya Sauli na alimtambulisha kijana Daudi kwa Sauli baada ya Daudi kumuua Goliati. Baada ya kifo cha Sauli Abinieri alichaguliwa na mtoto wa Sauli Ishibosheti kuwa mfalme wa Israeli wakati Daudi akiteuliwa kuwa mfalme katika Yuda. Baadaye Abinieri aliuawa kikatili na mkuu wa majeshi ya Daudi, Yoabu.
## Abiya ### Ufafanuzi Abiya lilikuwa jina la Mfalme wa Yuda aliyetawala tangu 915-913 BC. Alikuwa mtoto wa mfalme Rehoboamu. Walikuwepo watu wengine walioitwa Abiya katika agano la kale. Watoto wa Samweli Abiya na Yoeli walikuwa viongozi wa wana wa Israeli huko Belisheba. Kwa kuwa Abiya na kaka yake hawakuwa waaminifu watu walimuomba Samweli ateue mfalme mwingine wa kuwaongoza. Abiya mwingine ni yule aliyekuwa kwenye hekalu la kinabii wakati wa mfalme Daudi. Abiya lilikuwa jina la mtoto wa mfalme Yeroboamu. Abiya pia lilikuwa jina la kuhani mkuu aliyerudi na Zerubabeli Yerusalemu toka utumwani Babiloni.
## Abiya ### Ufafanuzi Abiya ni jina la watu mbalimbali katika agano la kale. Wafuatao ni watu hao: * Abiya lilikuwa jina la nabii katika kipindi cha Sauli. * Abiya alikuwa katibu katika kipindi cha utawala wa Sulemani. * Abiya lilikuwa jina la nabii toka Shilo aliyetabiri kuwa ufalme wa Israeli utagawanyika mara mbili. * Baba wa mfalme Baasha wa Israeli aliitwa Abiya.
## Abrahamu, Abramu ### Ufafanuzi Abramu alikuwa Mkalidayo toka mji wa Urialiyechaguliwa na Mungu kuwa baba wa Waisraeli. Mungu alibadilisha jina lake na kuwa "Abrahamu." * Jina "Abramu" lina maana ya "baba aliyeinuliwa." * "Abrahamu" lina maana ya "baba wa wengi." * Mungu alimuahidi Abrahamu kuwa atakuwa na uzao mwingi, na atakuwa taifa kubwa. * Abrahamu alimuaminina kumtii Mungu. Mungu alimuongoza Abrahamu toka Kaldayo mpaka nchi ya Kaanani. * Alipokuwa akiishi katika nchi ya Kaanani, walipokuwa wazee sana Abrahamu na mke wake Sara walipata mtoto, Isaka.
## Abusalomu ### Ufafanuzi Abusalomu alikuwa mtoto wa tatu wa mfalme Daudi. Alijulikana kwa utanashati wake pamoja na hasira kali. * Tamari Dada yake na Abusalomu alipobakwa na kaka yake Amnoni, Abusalomu alipanga mpango wa kumuua Amnoni. * Baada ya kumuua Amnoni, Abusalomu alikwenda mpaka mji ya Geshuri (mahali alipotokea Mika mama yake) na kuishi kule miaka mitatu. Kisha mfalme Daudi akaagiza arudi Yerusalemu, lakini hakumruhusu Abusalomu akaribie kwenye uwepo wake kwa miaka miwili. * Abusalomu aliwafanya baadhi ya watu kuwa kinyume na mfalme Daudi na kuwaongoza katika uasi dhidi ya mfalme. * Jeshi la Daudi lilipigana na Abusalomu na kumuua. Daudi alikuwa na huzuni sana yalipotokea haya.
## Adamu ### Ufafanuzi Adamu alikuwa binadamu wa kwanza aliyeumbwa na Mungu. Yeye na mke wake Hawa walitengenezwa kwa mfano wa Mungu. * Mungu alimtengeneza Adamu toka kwenye mavumbi na kumpulizia pumzi ya uhai. * Jina la Adamu linafanana naneno la Kiebrania linalomaanisha "udongo mwekundu" * Jina "Adamu" ni sawa na neno kwenye Agano la kale linalomaanisha "mwanadamu" au binadamu." * Watu wote ni uzao wa Adamu na Hawa. * Adamu na Hawa walimuasi Mungu. Mungu alijitenga nao hivyo dhambi na mauti vikaingia duniani.
## Adoniya. ### Ufafanuzi Adoniya alikuwa mtoto wa nne wa mfalme Daudi. * Adoniya alijaribu kutaka kuwa mfalme wa Israeli baada ya kifo cha kaka yake Abusalomu na Amnoni. * Kwa kuwa Mungu aliahidi ufalme kwa mtoto wa Daudi Sulemani, hivyo mpango wa Adoniya ulipinduliwa na Sulemani akapewa ufalme.
## Ahabu ### Ufafanuzi Ahabu alikuwa mfalme muovu sana katika ufalme wa Kaskazini mwa Israeli toka 875-854 BC. * Mfalme Ahabu aliwashawishi watu wa Israeli kuabudu miungu. * Nabii Eliya alimkabidi Ahabu na kumwambiakuwa kutakuwa na ukame mkubwa kwa miaka mitatu na nusu kwa dhambi ambazo Ahabu alisababisha wana wa Israeli wafanye. Ahabu na mkewe walifanya mambo mengi maovu ikiwemu kutumia nguvu zao kuwaua watu wasio na hatia.
## Ahazi ### Ufafanuzi Ahazi alikuwa mfalme muovu aliyetawala ufalme wa Yuda toka 732-716 BC. Hii ilikuwa yapata miaka 140 kabla ya wakati ambao wana wa Israeli na Yuda walichukuliwa mateka Babiloni. * Alipokuwa akitawala Yuda, Ahazi alikuwa na madhabahu ya kuabudu miungu ya Asiria, iliyosababisha watu kumuacha Mungu wa kweli, Yahweh. * Mfalme ahazi alikuwa na miaka 20 alipoanza kutawala Yuda, na alitawala miaka 16.
## Ahazia ### Ufafanuzi Lilikuwa jina la wafalme wawili: mmoja alitawala Israeli mwingine alitawala ufalme wa Yuda. * Ahazia mfalme wa Yuda alikuwa mtoto wa mfalme Yehoramu. alitawala mwaka mmoja (841BC) kisha akauawa na Yehu. Mtoto mdogo wa Ahazia Yoashi akachukua nafasi yake kama mfalme. * Ahazia mfalme wa Israeli alikuwa mtoto wa Ahabu. Alitawala miaka miwili 850-849 BC. Alikufa kutokana na majeraha yaliyomtesa alipoanguka toka kwenye ikulu yake na kaka yake Yoramu akawa mfalme.
## Ahusuero ### Ufafanuzi Ahusuero alikuwa mfalme aliyetawala ufalme wa Perusia kwa miaka ishirini. * Hiki ni kipindi ambacho Wayahudi waliokuwepo Babiloni kweye mateka, iliyokuja chini ya utawala wa Perusia. * Jina lingine la mfalme huyu aliitwa Ahasuero. * Baada ya kumfukuza malkia wake kwa hasira kubwa, mfalme Ahusuero alimchagua mwanamke wa Kiyahudi Esta kuwa mke wake na malkia.
## Ai ### Ufafanuzi Katika agano la kale, Ai lilikuwa jina la mji wa Kaanani uliopo kusini mwa Betheli na takribani kilometa 8 kaskazini mashariki mwa Yeriko. * Baada ya kuishinda Yeriko, Yoshua anawaongoza Waisraeli kuiteka Ai. Lakini walishindwa kwa sababu Mungu hakupendezwa nao. * Muisraeli aitwaye Akani aliiba nyara toka Yeriko na Mungu akaamuru kuwa yeye na familia yake wauawe. Kisha Mungu akawasaidia Waisraeli kuishinda Ai.
## Akila ### Ufafanuzi Alikuwa Mkristo wa kiyahudi aliyeishi Ponto. * akila na Prisila waliishi Rumi, Italia kwa mda lakini ,tawala wa Rumi aliwafukuza kwa nguvu Wayahudi waondoke Rumi. * Baada ya hayo Akila na Prisila walisafiri kwenda Korintho na kukutana na Paulo. * walifanya kazi ya kutengeneza mahema na Paulo pamoja na kumsaidia kazi za kimisionari. * Akila na Prisila waliwafundisha waamini ukweli kuhusu Yesu, mmoja wa waamini hao alikuwa mwalimu aliyeitwa Apolo.
## Amaleki, Mwamaleki ### Ufafanuzi Waamaleki ni wafugaji walioishi Kusini mwa Kaanani, toka jangwa na Negevu mpaka nchi za uarabuni. Watu hawa walikuwa uzao wa Ameleki, mjukuu wa Esau. * Waamaleki walikuwa maadui wakubwa wa Israeli toka kipindi ambacho Waisraeli walienda kuishi Kaanani. * Mara nyingine Amaleki hutumika kuelezea Waamaleki wote. * Katika vita moja dhidi ya Waamaleki, Musa alikuwa akinyanyua mikono yake juu Waisraeli walishinda na alipochoka na kushusha mikono yake chini Waisraeli walishindwa. Hivyo Haruni na Huri walimsaidia Musa kuishikilia mikono yake juu mpaka jeshi la Israeli lilipowashinda Waamaleki. * Wafalme wote Sauli na Daudi waliyaongoza majeshi dhidi ya Waamaleki. * Baada ya ushindi juu ya Waamaleki Sauli hakumtii Mungu kwa kuchukua baadhi ya nyara na kutokumuua mfalme wa Waamaleki kama Mungu alivyomuamuru.
## Amazia ### Ufafanuzi Amazia alikuwa mfalme ya Yuda baada ya baba yake mfalme Yuashi kuuawa. * Mfalme Amazia alitawala Yuda kwa miaka ishirini na tisa toka 796-767 BC. * Alikuwa mfalme mzuri, lakini hakuharibu mahali ambapo miungu iliabudiwa. * Amazia aliwahukumu kifo wote waliohusika na kumuua baba yake. * Aliwashinda waasi wa Edomu na kuwarejesha chini ya ufalme ya Yuda. * Alimtaka Mfalme Yoashi wa Israeli wapigane katika vita lakini alishindwa. Sehemu ya ukuta wa Yerusalemu ulivunjwa shaba na vyombo vya dhahabu vya hekali vikaibiwa. * Miaka michache baadaye mfalme Amazia alimuacha Yahweh na baadhi ya watu katika Yerusalemu wakakusanyika pamoja na kumuua.
## Amnoni ### Ufafanuzi Amnoni alikuwa mtoto mdogo wa mfalme Daudi na mke wake Ahinoamu. * Amnoni alimbaka dada yake Tamari ambaye alikuwa dada yake na Abusalomu. * Kwa sababu hii Abusalomu akapanga kumuua Amnoni.
## Amoni, Waamoni wanaume, Waamoni wanawake. ### Ufafanuzi "Waamoni" lilikuwa kundi la watu walioishi Kaanani. Walikuwa uzao wa Benyamini, aliyekuwa mtoto wa Lutu. * Waamoni wanawake walitafsiriwa moja kwa moja kuelezea kuwa walikuwa wanawake. * Wakati fulani Waamoni walimlipa nabii Balamu ili awalaani Waisraeli, lakini Mungu hakuliruhusu hilo.
## Amosi ### Ufafanuzi Amosi alikuwa Nabii wa Kiisraeli aliyeishi kipindi cha mfalme Uzia wa Yuda. * Kabla ya kuwa nabii, Amosi alikuwa mchungaji na mkulima wa mtini aliyeishi katika ufalme wa Yuda. * Amosi alitoa unabii dhidi ya kaskazini mwa ufalme wa Israeli kwa namna ambavyo wanadhulumu watu haki zao.
## Amozi ### Ufafanuzi Amozi alikuwa baba wa nabii Isaya. * Ametajwa mara moja tuu kwenye Biblia Isaya akiwa anatambulishwa kama "mtoto wa Amozi. * Jina hili ni tofauti na jina la nabii Amosi na linapaswa kutamkwa tofauti.
## Anasi ### Ufafanuzi Anasi alikuwa kuhani mkuu wa Kiyahudi kwa miaka 20 toka AD 6-AD 15. Kisha akaondolewa kwenye ukuhani mkuu na serikali ya Kirumi japokuwa aliendelea kuwa kiongozi mwenye ushawishi kati ya Wayahudi. * Anasi alikuwa baba mkwe wa Kaefa, kuhani mkuu katika kipindi cha Yesu. * Baada ya kuhani mkuu kustaafu, aliendelea kutumia cheo hicho na kufanya baadhi ya majukumu, hivyo Anasi bado aliendelea kuitwa kuhani mkuu katika kipindi cha ukuhani wa Kaefa na wengine. * Katika kesi yake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kwa mara ya kwanza Yesu alipelekwa kwa Anasi kwa ajili ya kuhojiwa maswali.
## Andrea ### Ufafanuzi Andrea alikuwa mmoja kati ya wanafunzi kumi na wawili aliowachangua Yesu kuwa karibu naye ambao baadaye waliitwa Mitume. * Kaka yake na Andrea aliitwa Simoni Petro. Wote walikuwa wavuvi. * Petro na Andrea walikuwa wakivua katika bahari ya Galilaya ambapo Yesu aliwaita kuwa wanafunzi wake. * Kabla Petro na Andrea hawajakutana na Yesu walikuwa wanafunzi wa Yohana Mbatizaji.
## Antiokia ### Ufafanuzi Antiokia ni jina la miji miwili katika agano jipya. Mji wa kwanza ulikuwa Siria karibu na bahari ya Mediterania na mji mwingine ulikuwa Rumi katika jimbo la Pisidia. * Kanisa la Antiokia huko Siria ilikuwa ni sehemu ya kwanza ambayo waliomwamini Yesu waliitwa Wakristo. Kanisa pia lilitoa wamishenari wakaenda kuwafikia mataifa. * Viongozi wa kanisa Yerusalemu alituma barua kwa waamini wa kanisa la Antiokia Siria kuwajulisha kuwa wao kuwa Wakristo sio lazima washike sheria za Kiyahudi. * Paulo, Barnaba na Yohana Marko walisafiri mpaka Antiokia ya Pisidia kuwashirikisha injili. Baadhi ya Wayahudi walikuja kuleta vurugu na kutaka kumuua Paulo. Lakini watu wengi Wayahudi na watu wa mataifa walisikiliza mafundisho na kumwamini Yesu.
## Apolo ### Ufafanuzi Apolo alikuwa Myahudi toka katika nchi ya Misri aliyekuwa na uwezo wa kipekee wa kufundisha kuhusu Yesu. * Apolo alikuwa msomiwa maandiko ya Kiebrania na alikuwa mzungumzaji mzuri. * Alipewa maelekezo na Wakristo wawili kule Efeso, Akila na Prisila. * Paulo alisisitiza kuwa yeye na Apolo pamoja na wainjilisti wengine na waalimu, walifanya kazi kwa lengo moja la kuwasaidia watu kumwamini Yesu.
## Araba ### Ufafanuzi Katika agano la kale "Araba" imetumika kuelezea jangwa kubwa au maeneo tambarare yanayojumuisha bonde jirani na mto Yordani hadi kusini kwenye ncha ya kaskazini mwa bahari ya shamu. * Waisraeli walisafiri kupitia jangwa toka Misri kwenda Kaanani. * "Bahari ya Araba" inaweza kutafsiriwa kama "bahari iliyopo kwenye mji wa jangwa la Araba" au "bahari ya chunvi" au "bahari iliyokufa." Araba pia yaweza kuwa sehemu yoyote yenye jangwa.
## Arami, Waarami ### Ufafanuzi "Arami" ni jina la watu wawili katika agano la kale. Pia lilikuwa jina la mji uliopo kaskazini mashariki mwa Kaanani, ambayo kwa sasa ni Siria. * Watu wanaoishi Arami wanajulikana kama Waarami wanaozungumza Kiarami. Yesu na Wayahudi wengine pia walizungumza Kiarami. * Moja ya watoto wa Shemu aliitwa Arami. Mtu mwingine aliyeitwa Arami alikuwa binamu yake na Rebeka. * Arami baadaye ikaja kujulikana kwa jina la Kigiriki kama Siria. * "Padani Arami" ina maanisha "Tambarare ya Arami" na ilikuwa kaskazini mwa Arami. * Baadhi ya ndugu wa Abrahamu walioishi Harani ambayo ilikuwepo Padani Arami. * Katika agano la kale neno Arami na Padani Arami linamaanisha sehemu moja. * Neno "Arami Naharaimu" ina maana ya "Arami ya mito miwili" Mji huu ulikuwepo Kaskazini mwa Mesopitamia na mashariki mwa Padani Arami.
## Ararati ### Ufafanuzi Kwenye Biblia "Ararati" ni jina la mahali, ufalme na milima mbalimbali. * "Nchi ya Ararati" ipo kaskazini mashariki mwa Uturuki. * Ararati hujulikana zaidi kama mlima ambao safina ya Nuhu ilitua baada ya maji ya mafuriko kupungua. * Kwa sasa mlima unaoitwa "Mlima Ararati" unadhaniwa kuwa ni ule uliopo katika "Milima Ararati" ya kwenye Biblia.
## Artashasta ### Ufafanuzi Artashasta alikuwa mfalme aliyetawala ngome ya Peru toka 464-424 BC. * Katika utawala wa Artashasta Waisraeli toka Yuda walikuwa mateka huko Babiloni, ambayo ilikuwa chini ya usimamizi wa Peru kwa wakati ule. * Artashasta alimruhusu Ezra kuhani na Wayahudi wengine kuondoka Babiloni na kurudi Yerusalemu kuwafundisha Waisraeli sheria za Mungu. * Baadaye Artashasta alimruhusu Nehemia kurudi Yerusalemu ili awaongoze Wayahudi katika kujenga ukuta uliozunguka mji. * Kwa kuwa Babiloni ilikuwa chini ya utawala wa Peru wakati mwingine Artashasta aliitwa mfalme wa Babiloni.
## Asa ### Ufafanuzi Asa alikuwa mfalme aliyetawana ufalme wa Yuda kwa miaka arobaini. toka 913-873 BC. * Mfalme Asa alikuwa mfalme mzuri aliyeondoa sanamu nyingi za miungu na kusababisha Waisraeli waanze kumuabudu tena Yahweh. * Yahweh alimpa mfalme Asa mafanikio ya utajiri dhidi ya mataifa mengine. * Baadae katika utawala wake Asa aliacha kumuamini Yahweh na akaugua ugonjwa ambao ulipelekea kifo chake.
## Asafu ### Ufafanuzi Asafu alikuwa kuhani wa Kilawi na mtaalamu wa muziki aliyetunga mziki wa Zaburi ya mfalme Daudi. Pia aliandika zaburi yake mwenyewe. * Asafu alichaguliwa na mfalme Daudi kuwa moja ya wanamuziki watatu waliokuwa wakitengeneza nyimbo za kuabudu hekaluni. Baadhi ya nyimbo hizi zilikuwa unabii. * Asafu aliwafundisha watoto wake na wakabeba majukumu ya kutumia vyombo vya muziki na kutoa unabii hekaluni. * Baadhi ya vyombo vya mziki vilivyokuwepo ni kinanda, kinubi, tarumbeta na matoazi. * Zaburi ya 50, 73-83 inasemekana zimetoka kwa Asafu. Na pia inawezekana baadhi ya zaburi hizi zimeandikwa na wanafamilia wake.
## Ashdodi, Azoto ### Ufafanuzi Ashdodi ulikuwa ni moja kati ya miji mitano muhimu kwa Wafilisti. Mji huu ulikuwa kusinimagharibi mwa Kanani karibu na bahari ya Mediterranean, kkati ya miji ya Gaza na Jopa. * Hekalu la Wafilisti lililokuwa mungu wa uongo dagoni lilikuwa Ashdodi. * Mungu aliwaadhibu watu wa Ashdodi wakati Wafilisti walipoiba sanduku la agano na kuliweka katika hekalu la kipangani huko Ashdodi. * Jina la kigiriki la huu mji lilikuwa Azoto. Ulikuwa moja kati ya miji ambayo mwinjilisti Philipo alihubiri injili.
## Ashera, sanamu ya ashera, Ashtorethi ### Ufafanuzi Ashera lilikuwa jina la mungu wa kike aliyeabuniwa na Wakaanani kipindi cha agano la kale. Ashtorethi ni jina lingine la Ashera. * Sanamu ya Ashera ni kinyago kilichochongwa kwa mbao au mti uliochongwa kwa ajili ya kumwakilisha mungu wa kike. * Sanamu za Ashera zilikuwa zinawekwa karibu na madhabahu za mungu Baali, aliyekuwa anadhaniwa kuwa mume wa Ashera. Watu wengine walikuwa wanamuabudu Baali kama mungu wa jua na Ashera kama mungu wa mwezi. * Mungu aliwaamuru Waisraeli wahaaribu vinyago vyote vilivyochongwa vya Ashera. * Baadhi ya Waisraeli kama Gideoni, mfalme Asia na mfalme Yosia walimtii Mungu na kuwaongoza watu kuharibu sanamu hizo. * Lakini viongozi wengine wa Israeli kama mfalme Solomoni, Mfalme Manase na mfalme Ahabu hawakuziharibu sanamu za Ashera na waliwashawishi watu waziabudu.
## Asheri ### Ufafanuzi Asheri alikuwa mtoto wa nane wa Yakobo. Uzao wake unaunda moja ya makabila kumi na mbili ya Israeli ambalo pia linaitwa Asheri. * Mama yake na Asheri aliitwa Zilpa, mtumwa wa Lea. * Maana ya jina lake ni "furaha" au "baraka." * Asheri pia lilikuwa jina la ngome ambayo kabila la Asheri walipewa baada ya Waisraeli kuingia nchi ya ahadi.
## Ashikelo ### Ufafanuzi Katika Biblia, Ashikelo ni mji wa wafilisti ulioko pwani Bahari ya Mediterania. Bado ipo mpaka leo Israeli. * Ashikelo ulikuwa mji wa muhimu sana wa Wafilisti pamoja na Ashdodi, Ekironi, Gati na Gaza. * Waisraeli hawakuiteka kabisa Ashikelo japokuwa ufalme wa Yuda ulisambaa nchi nzima. * Ashikelo iliendelea kukaliwa na Wafilisti kwa miaka mia.
## Ashuru, Waashuru, Dola ya Waashuru ### Ufafanuzi Ashuru lilikuwa taifa lenye nguvu kipindi ambacho wana wa Israeli walikuwa wakiishi Kaanani. Ngome ya waashuru ilikuwa ni kundi la mataifa waliotawaliwa na mfalme wa Ashuru. * Taifa la Ashuru lilikuwa sehemu ambayo kwa sasa ni nchi ya Iraq. * Mwaka 722 BC Waashuru waliuteka ufalme wa Israeli na kuwalazimisha Waisraeli wengi kwenda Ashuru. * Waisraeli waliobaki waliwaoa wageni walioletwa na Waashuru toka Samaria. Kizazi cha watu hao waliotokana na mwingiliano huo wa kuoana waliitwa Wasamaria.
## Asia ### Ufafanuzi Katika Biblia Asia ni jina la jimbo la utawala wa Kirumi. Ilikuwa magharibi mwa nchi inayoitwa Uturuki kwa sasa. * Paulo alisafiri mpaka Asia kueneza injili katika miji mbalimbali huko. Baadhi ya miji hiyo ni Efeso na Kolose. * Ili kuondoa utata wa kuchanganya na Asia ya sasa, ni vizuri kuitafsiri Asia hii kama "mkoa wa zamani wa Kirumi ulioitwa Asia" au "mkoa wa Asia." * Makanisa yote yanayotazamwa katika Ufunuo yalikuwa katika mkoa wa Kirumi uitwao Asia.
## Athalia. ### Ufafanuzi Athalia alikuwa mke mbaya wa Yehoramu mfalme wa Yuda. Alikuwa mjukuu wa mfalme muovu wa Israeli, mfalme Omri. * Ahazia mtoto wa Athalia alikuwa mfalme baada ya kifo cha Yehoramu. * Ahazia alipokufa, Athalia alipanga kuwauwa ndugu waliosalia wa familia ya mfalme. * Lakini mjukuu mdogo wa Athalia Yoashi alifichwa na shangazi yake hivyo hakuuawa. Baadaye alikuwa mfalme wa Yuda.
## Ayubu ### Ufafanuzi Ayubu alikuwa mtu anayeelezwa katika Biblia kama mtu asiye na hatia na mwenye haki mbele ya Mungu. Anajulikana zaidi kwa kutunza imani yake katika Mungu katika nyakati za mateso makali. Ayubu aliishi katika nchi ya Usi iliyokuwa sehemu ndani ya nchi ya Kanaani, inawezekana katika maeneo ya Edomu. Inafikiriwa kuwa aliishi wakati wa Esau na Yakobo kwa sababu mmoja wa marafiki wa Ayubu alikuwa "Mtemani," ambalo lilikuwa jina la kundi lililoitwa baada ya mjukuu wa Esau. Kitabu cha Agano la Kale cha Ayubu kinaelezea jinsi Ayubu na wengine walivyoitikia mateso yake. Pia inatoa mtazamo wa Mungu kama muumbaji mwenye enzi na mtawala wa ulimwengu. Baada ya maafa hayo yote, hatimaye Mungu alimponya Ayubu na kumpa watoto wengine na utajiri. Kitabu cha Ayubu kinasema kuwa alikuwa mzee sana alipokufa.
## Azaria ### Ufafanuzi Azaria ni jina la watu kadhaa kwenye agano jipya. * Aharia wa kwanza alijulikana sana kwa jina lake la Kibabiloni kama Abedinego. Alikuwa mmoja kati ya Waisraeli wengi toka Yuda waliokamatwa na jeshi la Nebukadneza na kupelekwa kuishi Babiloni. * Mfalme Uzia wa Yuda pia alijulikana kama Azaria. * Azaria mwingine alikuwa kuhani mkuu katika agano la kale. * Katika kipindi cha nabii Yeremia, Azaria aliwataka Waisraeli wasimtii Mungu kwa kuondoka kwenye nchi yao.
## Baali ### Ufafanuzi "Baali" maana yake "bwana" lilikuwa jina la mungu wa kwanza wa uongo aliyekuwa akiabudiwa na Wakanaani. * Pia kulikuwa na miungu mingine ya uongo yenye jina "Baali, kama vile "Baali wa Peori." Wakati mwingine miungu hii kwa pamoja inarejerewa kama "Mabaali." * Baadhi ya watu walikuwa na majina yenye jina "Baali" ndani yake. * Ibada ya Baali ilihusisha matendo maovu kama vile kutoa watoto kama sadaka na ukahaba. * Kwa nyakati tofauti katika historia, Waisraeli pia walijiingiza katika ibada ya Baali, kwa kufuata mfano wa mataifa ya kipagani yaliyowazunguka. * Wakati wa utawala wa Mfalme Ahabu, Eliya nabii wa Mungu aliweka jaribio la kuwathibitishia watu kwamba Baali si mungu wa kweli na kwamba Yahwe pekee ndiye aliyekuwa Mungu wa kweli. Matokeo yake, manabii wa Baali waliangamizwa na watu wakaanza kumwabudu Yahwe tena.
## Baasha ### Ufafanuzi Baasha alikuwa miongoni mwa wafalme waovu wa Israeli,waliowashawishi Waisraeli kuabudu vinyago. * Baasha alikuwa mfalme wa tatu wa Israeli na alimiliki kwa miaka ishirini na minne, wakati Asa akiwa mfalme wa Yuda. * Alikuwa jemedari wa jeshi aliyejifanya mfalme baada ya kumwua mfalme Nadabu, mtangulizi wake. * Kulikuwa na mapigano mengi wakati wa utawala wa Baasha kati ya ufalme wa Israeli na Yuda, hasa na Asa mfalme wa Yuda. * Dhambi nyingi alizozitenda Baasha hatimaye zilimfanya Mungu kumwondoa katika nafasi yake kwa kifo.
## Babeli ### Ufafanuzi Babeli ulikuwa mji mkuu katika eneo lililoitwa Shinari kusini mwa Mesopotamia. Shinari ulikuja baadaye kuitwa Babiloni. * Mji wa Babeli ulianzishwa na Nimrodi, mjukuu wa Hamu, aliyemiliki eneo la Shinari. * Watu wa Shinari hatimaye wakawa na kiburi kwa kuamua kujenga mnara mrefu wa kuweza kufika mbinguni. Baada ulijulikana kama "Mnara wa Babeli." * Kwa kuwa kwa kujenga mnara watu walikataa kutawanyika kama Mungu alivyokuwa ameagiza, yeye alichanganya lugha zao ili wasielewane. Hii iliwalazimisha kuondoka na kwenda kuishi maeneo mbalimbali ya dunia. * Kiini cha maana ya neno "Babeli" ni "machafuko," likitokana na wakati Mungu alipochanganya lugha ya watu.
## Bahari ya Chumvi, Bahari iliyo Kufa ### Ufafanuzi Bahari ya Chumvi( inayo itwa pia Bahari iliyo Kufa) ilikuwa kati ya kusini mwa Israeli upande wa magharibi na Moabu upande wa mashariki. * Mto Yordani una shuka kusini kwenye Bahari ya Chumvi. * Kwasababu ni ndogo kuliko bahari nyingine, hii yaweza itwa "Ziwa la Chumvi." * Hii bahari ina idadi kubwa ya madini (au "chumvi) inayo maanisha kwamba hakuna kinacho weza kuishi ndani ya maji yake. Hapo ndipo jina "Bahari iliyo Kufa" limetoka. * Kati Agano la Kale, hii bahari inaitwa pia "Bahari ya Araba" na "Bahari ya Negevi" kwasababu ya maeneo yake karibu na pande za Araba na Negevi.
## Bahari ya Galilaya, Bahari ya Shinerethi, Ziwa la Genezareti, Bahari ya Tiberia ### Ufafanuzi "Bahari ya Galilaya" ni jina la ziwa mashariki mwa Israeli. Katika Agano la Kale liliitwa "Bahari ya Shinerethi." * Maji ya hii bahari yana shuka kusini kupitia Mto Yordani kwenda Bahari ya Chumvi. * Kapernaumu, Bethsaida, Genezareti, na Tiberia zilikuwa baadhi ya miji ambayo ilikuwa upande wa Bahari ya Galilaya kipindi cha Agano Jipya. * Matukio mengi ya maisha ya Yesu yalitokea karibu na Bahari ya Galilaya. * Bahari ya Galilaya ili tajwa pia kama "Bahari ya Tiberia" na "Ziwa la Genezareti."
## Bahari ya shamu ### Ufafanuzi Bahari ya shamu ni jina la la bahari iliyokuwa Misri na Uarabbuni. Sasa inaitwa bahari ya Shamu. * Bahari ya shamu ni ndefu na nyembamba. Ni kubwa zaidi ya ziwa au mto lakini ndogo kuliko bahari. * Waisraeli walivuka bahari ya shamu walipotoka Misri. Mungu aliwafanyia muujiza na kusababisha maji kugawanyika na watu wakapita. * Nchi ya Kanaani ilikuwa kaskazini mwa bahari hii.
## bahari, Bahari Kuu, bahari ya magharibi, Bahari ya Medeterenia ### Ufafanuzi Katika Biblia, "Bahari Kuu" au " bahari ya magharibi" inaelezea ile ambayo sasa ujulikana "Bahari ya Medeterenia," ambayo ilikuwa ni eneo la maji lilokulikana na watu wa Biblia. * Bahari ya Medeterenia ina pakana: Israeli (mashariki), Ulaya (kaskazini na magharibi), na Africa (kusini) * Bahari ilikuwa muhimu kipindi cha kale kwa ajili ya biashara na kusafiri maana ili pakana na nchi zingine. Miji na makundi ya watu yaliyo pwani ya hii bahari yalifanikiwa sana kwasababu ya urahisi wa kupata bidha nchi zingine kwa meli.
## Balaamu ### Ufafanuzi Balaamu alikuwa nabii wa kipagani aliyeajiriwa na Mfalme Balaki kuwalaani Israeli walipokuwa wamepiga kambi katika Mto Yordan kaskazini mwa Moabu, wakijiandaa kuingia nchi ya Kanaani. * Balaamu alikuwa akitoka katika mji wa Pethori, ulikuwa katika eneo karibu na Mto Frati, umbali wa maili 400 kutoka katika nchi ya Moabu. * Balaki, mfalme wa Wamidiani, alitishwa na nguvu na idadi ya Waisraeli, hivyo akamwajiri Balaamu kuwalaani. * Kadiri Balaamu alivyosafiri kuwaelekea Israeli, malaika wa Mungu alisimama katika njia yake hivyo punda wa Balaamu alipomwona alisimama. Mungu akampa punda uweza wa kuongea na Balaamu. * Mungu hakumuruhusu Balaamu kuwalaani Israeli badala yake alimwagiza kuwabariki. * Baadaye, Balaamu bado alilete uovu juu ya Israeli alipowafuta kuabudu mungu wa Baar- peori.
## Baraba ### Ufafanuzi Baraba alikuwa mfungwa huko Yerusalemu wakati Yesu anakamatwa. * Baraba alikuwa mwalifu aliyekuwa ametenda makosa ya kuuwa na uasi dhidi ya serikali ya Kirumi. * Pontio Pilato alipotoa msamaha wa kumfungua kati ya Baraba au Yesu, watu walimchagua Baraba. * Hivyo Pilato alimwacha huru Baraba, lakini akamhukumu Yesu auawe.
## Barnaba ### Ufafanuzi Barnaba ni miongoni mwa wakristo wa mwanzo aliyeishi wakati wa mitume. * Barnaba alikuwa wa kabila ya Lawi na alikuwa mwenyeji wa kisiwa cha Mileto. * Wakati Sauli (Paulo) anakuwa mkristo, Barnaba aliwasihi waamini wangine kumpokea kama mwamini mwenzao. * Barnaba na Paulo walisafiri kwa pamoja katika miji mbalimbali ili kuhubiri injili. * Jina lake lilikuwa Yusufu, lakini aliitwa "Barnaba," jina linalomaanisha "mwana wa faraja."
## Baruku ### Ufafanuzi Baruku ni jina la watu kadhaa katika Agano la Kale. * Baruku wa kwanza (mwana wa Zabeli) alifanya kazi ya Nehemia kujenga upya kuta za Yerusalemu. * Lakini pia katika nyakati za Nehemia, Baruku mwingine (mwana wa Kol-Hoze) alikuwa miongoni mwa viongozi walioishi Yerusalemu baada ya kuta zake kujengwa. * Baruku mwingine (mwana wa Neria) alikuwa mhudumu wa nabii Yeremia, kwa kumsaidia kazi mbalimbali kama vile kuandika jumbe Mungu alizompa Yeremia na kisha kuwasomea watu.
## Bashani ### Ufafanuzi Bashani lilikuwa ni enea mashariki mwa Bahari ya Galilaya. Ilihusisha eneo ambalo kwa sasa ni sehemu ya Syria na milima ya Golani. * Mji wa makimbilio katika Agano la Kale ulioitwa "Golani" ulikuwa katika eneo la Bashani. * Bashani lilikuwa eneo lenye rutuba sana likijulikana kwa miti yake ya mitende na malisho ya wanyama. * Mwanzo 14 inataarifu kuwa Bashani ilikuwa eneo la vita kati ya wafalme kadhaa na mataifa yao. * Wakati Waisraeli wakitangatanga jangwani baada ya kutoka Misri, walichukua sehemu ya eneo la Bashani. * Miaka kadhaa baadaye, mfalme Sulemani alipokea mahitaji kutoka katika eneo hilo.
## Batholomayo ### Ufafanuzi Batholomayo alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu. * Batholomayo alitumwa pamoja na wale mitume wengini kuhubiri injili na kufanya miujiza kwa jina la Yesu. * Alikuwa miongoni mwa wale waliomwona Yesu akienda mbinguni. * Majuma kadhaa baada ya hayo, alikuwa pamoja na mitume wengine huko Yerusalemu siku ya Pentekoste wakati Roho Mtakatifu alipowashukia.
## Bathsheba ### Ufafanuzi Bathsheba alikuwa mke wa Uria, askari katika jeshi la Daudi. Baada ya kifo cha Uria, akawa mke wa Daudi, na mama wa Sulemani. * Daudi alizini na Bethsheba akiwa mke wa Uria. * Bathsheba alipokuwa mjamzito kwa Daudi, Daudi alisababisha Uria kuuawa vitani. * Kisha Daudi alimwoa Bethsheba na akazaa mwana. * Mungu alimwadhibu Daudi kwa dhambi yake kwa kufanya mtoto afe siku chache baada ya kuzaliwa. * Baadaye, Bethsheba alizaa mwana mwingine, Sulemani, aliyekuja kuwa mfalme baada ya Daudi.
## Beelzebuli ### Ufafanuzi Beelzebuli ni jina lingine kwa Shetani, au mwasi. Wakati mwingine linaandikwa "Beelzebubu." * Jina hili kwa kawaida linamaanisha "bwana wa nzi" kumaanisha, mtawala wa mapepe." Lakini ni vizuri zaidi kutafasiri neno karibu na herufi zake za asili kuliko kutafasiri maana. * Ingeweza pia kutafasiriwa kama "Beelzebubu mwovu" kuweka wazi anayetajwa. * Jina hili linahusiana na jina la Baal-Zebubu mungu wa Ekroni.
## Beersheba ### Ufafanuzi Katika nyakati za Agano la Kale, Beersheba ulikuwa mji uliokuwa umbali wa maili 45 kusini magharibi mwa Yerusalemu katika eneo la jangwa ambalo kwa sasa linaitwa Negevu. * Jangwa lililouzunguka Beersheba lilikuwa ni eneo la nyika ambapo Hajiri na Ishmaeli walipotelea baada ya Ibrahimu kuwafukuza kutoka katika hema zake. * Jina la mji linamaanisha "kisima cha nadhiri." Ulipewa jina hili Ibrahimu walipoapa kwa kiapo kutokuwaadhibu watu wa Mfalme Abimeleki kwa kukatalia mojawapo ya visima vya Ibrahimu.
## Benaya ### Ufafanuzi Benaya lilikuwa jina la watu kadhaa katika Agano la Kale. * Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa miongoni mwa mashujaa wa Daudi. Alikuwa shujaa mwenye ujuzi na aliwekwa kuwa mlinzi wa Daudi. * Sulemani alipotawazwa kuwa mfalme, Benaya alimsaidia kuwaaribu adui zake, hatimaye akawa jemedari wa jeshi la Israeli. * Watu wengine wenye jina Benaya katika Agano la Kale ni pamoja na Walawi watatu: kuhani, mwimbaji, na mwana wa Asafu.
## Benjamini ### Ufafanuzi Benjamini alikuwa mwana wa mwisho wa Yakobo aliyezaliwa na Raheli mkewe. Jina lake linamaanisha mwana wa "mkono wangu wa kulia." * Yeye na Yusufu, nduguye mkubwa walikuwa wana pekee wa Raheli, aliyekufa baada ya kuzaliwa kwa Benjamini. * Wana wa Benjamini walikuwa mojawapo ya makabila ya Israeli. * Mfalme Sauli alikuwa akitokea katika kabila la Benjamini. * Mtume Paulo pia alikuwa wa kutoka katika kabila la Benjamini.
## Berea (Beroya) ### Ufafanuzi Katika nyakati za Agano Jipya, Berea(Beroya) ulikuwa mji wa Kigriki wenye mafanikio kusini mashariki mwa Masedonia, umbali wa kilometa 80 kusini mwa Thesalonike. * Paulo walikimbilia katika mji wa Berea baada ya Wakristo wenzao kuwasaidi kutoroka kutoka kwa Wayahudu kadhaa waliowasababishia shida huko Thesalonike. * Watu waliokuwa wakiishi Berea walipomsikia Paulo akihubiri, waliyachunguza maandiko kuthibitisha ikiwa alichokuwa akiwambia kilikuwa kweli.
## Beth Shemeshi ### Ufafanuzi Beth Shemeshi lilikuwa jina la mji wa Kikanaani kama kilometa 30 magharibi ya Yerusalemu. * Waisraeli waliuteka mji wa Beth Shemeshi wakati wa uongozi wa Yoshua. * Beth Shemeshi ulikuwa mji uliokuwa umetengwa kama sehemu ya makuhani Walawi kuishi. * Wafilisiti walipokuwa wakilirudisha Yerusalemu sanduku la agano walilokuwa wameliteka, Beth Shemeshi ni mji wa kwanza waliposimama pamoja nalo.
## Betheli ### Ufafanuzi Betheli ulikuwa mji uliokuwa kaskazini mwa Yerusalemu katika nchi ya Kanaani. Hapo mwanzo uliitwa "Luzu." * Baada ya kupokea ahadi za Mungu kwa mara ya kwanza, Ibrahimu alimjengea Mungu madhabahu karibu na Betheli. Jina lake wakati huo halikuwa Betheli, lakini kwa kawaida ulirejerea kama "Betheli" uliokuwa unatambuliwa sana. * Wakati akikimbia kutoka kwa Esau nduguye, Yakobo alikaa usiku kucha karibu na mji huu na akalala pale nje juu ya ardhi. Alipokuwa amelala, aliota ndoto malaika wakipanda na kushuka mbinguni juu ya ngazi. * Mji huu haukuwa na jina hilo mpaka Yakobo alipouita hivyo. Kwa kuwa wazi zaidi, baadhi ya tafasiri zaweza kuiita Luzu "(baadaye ukaitwa Betheli)" katika kifungu kuhusu Ibrahimu, vilevile wakati Yakobo anafika pale kwa mara ya kwanza (kabla hajabadili jina lake). * Betheli imetajwa mara kwa mara katika Agano la Kale na ilikuwa sehemu ambapo matukio mengi mhimu yalitokea.
## Bethlehemu ### Ufafanuzi Bethlehemu ulikuwa mji mdogo katika nchi ya Israeli, karibu na mji wa Yerusalemu. Ulijulikana pia kama "Efratha," ambalo pengine ndilo jina lake la awali. * Bethlehemu umekuwa ukiitwa mji wa "Daudi," kwa kuwa Daudi alizaliwa pale. * Nabii Mika alitabiri kuwa Masiya angekuja kutokea katika "Bethlehemu ya Efratha." * Ili kutimiza unabii huo, Yesu alizaliwa Bethlehemu, miaka mingi baadaye. * Jina "Bethlehemu" maana yake ni "nyumba ya mikate" au "nyumba ya chakula."
## Bethueli ### Ufafanuzi Bethueli alikuwa mwana wa Nahori ndiguye Ibrahimu. * Bethueli alikuwa baba wa Rebeka na Labani. * Pia kulikuwa na mji uliokuwa ikiitwa Bethueli, ambao yawezekana ulikuwa kusini mwa Yuda, siyo mbali kutoka mji wa Beersheba.
## Boazi ### Ufafanuzi Boazi alikuwa mwisraeli aliyekuwa amemwoa Ruthi, babu wa mfalme Daudi, na babu wa Yesu Kristo. * Boazi aliishi nyakati za Waamzi katika Israeli. * Alikuwa ndugu wa Naomi mwanamke wa Kiisraeli aliyekuwa amerudi kutoka Moabu baada ya mmewe na wanawe kufariki. * Boazi "alimkomboa" Ruthi mkwewe Naomi, kwa kumwoa Ruthi na kumpa hatima njema, mme na watoto. * Yeye ni taswira ya jinsi Yesu alivyotuokoa na kutukomboa kutoka dhambini.
## Bonde la Kidroni ### Ufafanuzi Bonde la Kidroni ni bonde refu nje kidogo ya mji wa Yerusalemu, katikati ya ukuta wa mashariki na mlima wa Mizeituni. Bonde lina kina zaidi ya mita 1,000 na urefu karibu wa kilomita 32. Wakati mfalme Daudi alipokuwaakimtoroka mwanaye Absalomu, alipita bonde la Kidroni kufika mlima wa Mizeituni. Mfalme Yosia na mfalme Asa wa Yuda waliamuru kwamba sehemu zilizoinuka na madhabahu za miungu wa uongo zivunjwe na kuchomwa; majivu yalitupwa bonde la Kidroni. Wakati wa utawala wa mfalme Hezekia, bonde la Kidroni ndipo makuhani walipotupa kila kitu kisicho kisafi walichokitoa kwenye hekalu. Malkia muovu Athalia aliuliwa katika bonde kwa sababu ya maovu aliyoyafanya.
## Dameski ### Ufafanuzi Dameski ni mji mkuu wa nchi ya Shamu. Bado upo sehemu ile ile kama ulipokuwa kipindi cha Biblia. Dameski ni moja ya miji kongwe, inayoendelea kukaliwa kwa uendelevu duniani. Katika kipindi cha Abrahamu, Shamu ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Aramu (ulio mahali ambapo sasa ni Shamu). Katika Agano la Kale lote, kuna marejeo mengi ya miingiliano kati ya wakazi wa Dameski na watu wa Israeli. Baadhi ya unabii wa Kibiblia zinatabiri uharibifu wa Dameski. Unabii huu unaweza kuwa umekamilika pale ambapo Shamu iliangamiza mji ule katika wakati wa Agano la Kale, au kunaweza kuwa na muda wa baadaye, utakaokuwa na uharibifu kamili wa mji huu. Katika Agano Jipya, Mfarisayo Sauli (aliyejulikana baadaye kama Paulo) alikuwa njiani kukamata Wakristo katika mji wa Dameski ambapo Yesu alimkabili na kumfanya awe muumini.
## Dani ### Ufafanuzi Dani alikuwa mwana wa tano wa Yakobo na alikuwa mmoja wa makabila kumi na mawili ya Israeli. Eneo lililokaliwa na kabila la Dani sehemu ya kaskazini ya Kaanani pia lilipatiwa jina hili. Katika kipindi cha Abrahamu, kulikuwa na mji ulioitwa Dani uliokuwa magharibi mwa Yerusalemu. Miaka ya baadaye, katika kipindi ambapo taifa la Israeli lilipoingia katika nchi ya ahadi, mji tofauti ulioitwa Dani ulikuwa kama maili 60 kaskazini mwa Yerusalemu. Msemo "Wadani" una maana ya vizazi vya Dani, ambao pia ni wanajumuiya wa ukoo wake.
## Danieli ### Ufafanuzi Danieli alikuwa nabii wa Kiisraeli ambaye alikuwa kijana mdogo aliyechukuliwa mateka na mfalme wa Babeli Nebukadreza mnamo wa 600 KK. Huu ulikuwa wakati ambapo Waisraeli wengine wengi kutoka Yuda walishikwa mateka huko Babeli kwa miaka 70. Danieli alipewa jina la Kibabeli la Belteshaza. Danieli alikuwa kijana aliyeheshimika na mwenye haki aliyemtii Mungu. Mungu alimwezesha Danieli kutafsiri ndoto kadhaa au maono kwa wafalme wa Babeli. Kwa sababu ya uwezo huu na kwa sababu ya hulka yake ya heshima, Danieli alipewa nafasi ya juu ya uongozi katika ufalme wa Kibabeli. Miaka mingi baadaye, maadui wa Danieli walimdanganya mfalme wa Babeli Dario kutunga sheria inayokataza kumwabudu mtu yeyote isipokuwa mfalme. Danieli aliendelea kuomba kwa Mungu, kwa hiyo alikamatwa na kutupwa katika tundu la simba. Lakini Mungu alimkomboa na hakudhuriwa kabisa.
## Dario ### Ufafanuzi Dario lilikuwa jina la wafalme kadhaa wa Uajemi. Inawezekana "Dario" ilikuwa ni cheo na siyo jina. "Dario, Mmedi" alikuwa mfalme aliyedanganywa kumfanya nabii Danieli kutupwa katika tundu la simba kama adhabu ya kumwabudu Mungu. "Dario Muajemi" alisaidia kurahisisha ujenzi tena wa hekalu Yerusalemu katika kipindi cha Ezra na Nehemia.
## Daudi ### Ufafanuzi Daudi alikuwa mfalme wa pili wa Israeli na alimpenda na kumtumikia Mungu. Alikuwa mwandishi mkuu wa kitabu cha Zaburi. Daudi alipokuwa mvulana mdogo akichunga kondoo wa familia yake, Mungu alimchagua kuwa mfalme afuataye wa Israeli. Daudi alikuwa mpiganaji hodari na aliongoza jeshi la Israeli katika vita dhidi ya maadui zake. Kumshinda kwake Goliati na Wafilisti kunajulikana sana. Mfalme Sauli alijaribu kumuua Daudi, lakini Mungu alimlinda, na kumfanya awe mfalme baada ya kifo cha Sauli. Daudi alitenda dhambi mbaya sana, lakini alitubu na Mungu alimsamehe. Yesu, Masihi, anaitwa "Mwana wa Daudi" kwa sababu ni uzao wa Mfalme Daudi.
## Delila ### Ufafanuzi Delila alikuwa mwanamke wa Kifilisti aliyependwa na Samsoni, lakini hakuwa mke wake. Delila alipenda pesa zaidi ya alivyompenda Samsoni. Wafilisti walimhonga Delila kumdanganya Samsoni amwambie jinsi awezavyo kufanywa mnyonge. Nguvu yake ilipotoweka, Wafilisti walimkamata.
## Edeni, bustani ya Edeni ### Ufafanuzi Katika kipindi cha zamani, Edeni ilikuwa eneo ambalo lilikuwa na bustani ambapo Mungu aliweka mwanamume na mwanamke wa kwanza kuishi. Bustani ambayo Adamu na Hawa waliishi ilikuwa sehemu tu ambayo waliishi. Sehemu husika ya eneo la Edeni halina uhakika, lakini Mito ya Hidekeli na Frati zilitiririka katikati yake. Neno "Edeni" hutokana na neno la Kiebrania lenye maana ya "kufurahishwa sana na".
## Edomu, Muedomu, Idumaya ### Ufafanuzi Edomu ilikuwa jina lingine la Esau. Eneo ambalo aliishi pia kukajulikana kama "Edomu" na baadaye, "Idumaya". "Waedomu" walikuwa vizazi vyake. Eneo la Edomu lilibadilisha maeneo baada ya muda. Ulikuwa zaidi kusini ya Israeli na baadaye kupanuka katika kusini mwa Yuda. Katika wakati wa Agano Jipya, Edomu ilifunika nusu ya kusini ya mkoa wa Yuda. Wagiriki waliita "Idumaya" Jina "Edomu" ina maana ya "nyekundu" ambayo inaweza kumaanisha ukweli kwamba Esau alifunikwa na nywele nyekundu alipozaliwa. Au inaweza kumaanisha mchuzi mwekundu ambao Esau aliuza kwa haki yake ya mzawa wa kwanza. Katika Agano la Kale, nchi ya Edomu mara kwa mara hutajwa kama adui wa Israeli. Kitabu kizima cha Obadia kinahusu uharibifu wa Edomu. Manabii wengine wa Agano la Kale pia walizungumza tabiri hasi dhidi ya Edomu.
## Efeso ### Ufafanuzi Efeso ulikuwa mji wa zamani wa Kigiriki katika fukwe ya magharibi ya pale ambapo siku ya sasa ni Uturuki. Katika kipindi cha Wakristo wa kwanza, Efeso ilikuwa mji mkuu wa Asia, ambao ulikuwa mkoa mdogo wa Kirumi katika kipindi hicho. Kwa sababu ya eneo lake, mji huu ulikuwa kitovu muhimu sana katika biashara na safari. Hekalu la kipagani linalojulikana kwa kuabudu mungu wa Artemi (Diana) ilikuwa Efeso. Paulo aliishi na kufanya kazi Efeso kwa zaidi ya miaka miwili na baadaye kumteua Timotheo kuwaongoza waumini mapya kule. Kitanu cha Waefeso katika Agano Jipya ni barua ambayo Paulo aliandika kwa waumini wa Efeso.
## Efraimu ### Ufafanuzi Efraimu alikuwa mwana wa pili wa Yusufu. Vizazi vyake, Waefraimu, waliunda moja ya kabila kumi na mbili za Israeli. Kabila la Efraimu lilikuwa moja la makabila kumi ambayo yalikuwa katika sehemu ya kaskazini ya Israeli. Mara nyingine jina la Efraimu linatumika katika Biblia kumaanisha ufalme wote wa kaskazini wa Israeli. Efraimu ilikuwa eneo lenye milima na miinuko mingi sana, kutokana na kumbukumbu zenye "nchi yenye milima Efraimu" au "milima ya Efraimu".
## Efrata, Mwefrathi ### Ufafanuzi Efrata ilikuwa jina la mji na eneo katika sehemu ya kaskazini ya Israeli. Mji wa Efrata baadaye uliitwa "Bethehemu" au "Efrata-Bethlehemu". Efrata ilikuwa jina la mmoja wa wana wa Kalebu. Mji wa Efrata yawezekana uliitwa baada yake. Mtu ambaye alikuwa ametoka mji wa Efrata alikuwa akijulikana kama "Mwefrathi". Boazi, babu mkuu wa Daudi, alikuwa Mwefrathi.
## Ekroni ### Ufafanuzi Ekroni ni mji mkuu wa Wafilisti, uliopo maili tisa barani kutoka bahari ya Mediteraniani. Hekalu la mungu wa uongo Baal-zebubu ilikuwa Ekroni. Pale Wafilisti walipokamata sanduku la agano, walilichukua hadi Ashdodi, kisha kuhamisha hadi Gathi na Ekroni kwa sababu Mungu aliendelea kusababisha watu kuugua na kufa katika kila mji sanduku lilipokuwa likipelekwa. Hatimaye Wafilisti walirudisha sanduku Israeli. Pale mfalme Ahazia alipoanguka kutoka kwenye paa ya nyumba yake na kujiumiza, alifanya dhambi kwa kujaribu kutafuta kutoka kwa mungu wa uongo Baal-zebubu wa Ekroni kama angekufa au la kutokana na majeraha yake. Kwa sababu ya dhambi hii, Yahwe alisema ya kuwa angekufa.
## Elamu ### Ufafanuzi Elamu alikuwa mwana wa Shemu na mjukuu wa Nuhu. Vizazi vya Elamu vilikuwa vinaitwa "Waelami" na waliishi katika eneo lililoitwa "Elamu". Eneo la Elamu lilikuwa kusini mashariki mwa Mto Hidekeli, ambayo sasa ni Irani magharibi.
## Eleazari ### Ufafanuzi Eleazari lilikuwa jina la wanamume kadhaa katika Biblia. Eleazari alikuwa mwana wa tatu wa kaka yake Musa Haruni. Baada ya Haruni kufa, Eleazari akawa kuhani mkuu Israeli. Eleazari lilikuwa pia jina la mmoja wa "wanamume hodari" wa Daudi. Eleazari mwingine alikuwa mmoja wa uzao wa Yesu.
## Eliakimu ### Ufafanuzi Eliakimu lilikuwa jina la wanamume wawili katika Agano la Kale. Mwanamume mmoja aliyeitwa Eliakimu alikuwa msimamizi wa kasri chini ya Mfalme Hezekia. Mwanamume mwingine aliyeitwa Eliakimu alikuwa mwana wa Mfalme Yosia. Alifanywa mfalme wa Yuda na farao wa Misri, Necho. Necho alibadili jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu.
## Elisabeti ### Ufafanuzi Elisabeti alikuwa mama wa Yohana Mbatizaji. Jina la mume wake lilikuwa Zakaria. Zakaria na Elisabeti hawakuwahi kuweza kupata watoto, lakini katika uzee wao, Mungu alimuahidi Zakaria ya kwamba Elisabeti angezaa mtoto wa kiume. Mungu alitunza ahadi yake, na punde Zakaria na Elisabeti wakaweza kupata mimba, naye akazaa mtoto wa kiume. Walimuita mtoto yule Yohana. Elisabeti pia alikuwa jamaa kwa Mariamu, mama wa Yesu.
## Elisha ### Ufafanuzi Elisha alikuwa nabii katika Israeli wakati wa tawala za wafalme wa Israeli: Ahanu, Ahazia, Yehoramu, Yehu, Yehoahazi, na Yehoashi. Mungu alimwambia nabii Eliya kumpaka mafuta Elisha kama nabii. Eliya alipochukuliwa kwenda mbinguni katika kibandawazi cha moto, Elisha akawa nabii wa Mungu kwa wafalme wa Israeli. Elisha alifanya miujiza mingi, ikiwemo kuponya mwanamume kutoka Shamu aliyekuwa na ukoma na kufufua kutoka kwa wafu mtoto wa mwanamke kutoka Shunemu.
## Eliya ### Ufafanuzi Eliya alikuwa mmoja wa manabii muhimu sana wa Yahwe. Eliya alitabiri katika wakati wa tawala za wafalme kadhaa wa Israeli au Yuda, akiwemo Mfalme Ahabu. Mungu alifanya miujiza mingi kupitia Eliya, ikiwemo kumfufua mvulana mfu kurudi katika uhai. Eliya alimkaripia Mfalme Ahabu kwa kuabudu mungu wa uongo Baali. Aliwapa changamoto manabii wa Baali katika mtihani ambao ulithibitisha ya kwamba Yahwe ni Mungu mmoja wa kweli. Katika mwisho wa maisha ya Eliya, Mungu alimchukua kimuujiza juu mbinguni angali bado yu hai. Miaka mia moja baadaye, Eliya, pamoja na Musa, walijitokeza na Yesu juu ya mlima na waliongea pamoja juu ya kurudi, kuteseka na kufa kwa Yesu Yerusalemu.
## Engedi ### Ufafanuzi Engedi ni jina la mji katika nyika ya Yuda kusini mashariki mwa Yerusalemu. Engedi ilikuwa mahali mwa ukingo wa magharibi wa Bahari ya Chumvi. Sehemu ya jina lake, "chemichemi" ina maana ya chemichemi ya maji ambayo inatiririka chini kutoka kwenye mji hadi baharini. Engedi ilijulikana kwa kuwa na mashamba ya mizabibu mizuri na ardhi yenye rutuba nyingine, yawezekana kutokana na mwendelezo wa umwagiliaji kutoka kwa chemichemi ya maji. Kulikuwa na ngome katika Engedi ambayo Daudi alitoroka kule alipokuwa akifukuzwa na Mfalme Sauli.
## Esau ### Ufafanuzi Esau alikuwa mmoja wa mapacha wana wa Isaka na Rebeka. Alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa. Pacha ndugu yake alikuwa Yakobo. Esau aliuza haki yake ya mzawa wa kwanza kwa kaka yake Yakobo kwa kubadilishana na bakuri la chakula. Kwa kuwa Esau alizaliwa kwanza, baba yake Isaka alitakuwa kumpatia baraka maalumu. Lakini Yakobo alimdanganya Isaka kumpatia hiyo baraka badala yake. Mara ya kwanza Esau alikuwa na hasira sana hadi alitaka kumuua Yakobo, lakini baadaye alimsamehe. Esau alikuwa na watoto wengi na wajukuu, na vizazi hivi viliunda kuni kubwa la watu walioishi katika nchi ya Kaanani.
## Esta ### Ufafanuzi Esta alikuwa mwanamke wa Kiyahudi ambaye alikuwa malkia wa ufalme wa Ashuri katika kipindi cha mateka ya Babeli kwa Wayahudi. Kitabu cha Esta kinaelezea simulizi ya jinsi Esta alivyokuwa mke wa mfalme wa Waashuri Ahasuero na jinsi Mungu alivyomtumia kukomboa watu wake. Esta alikuwa yatima ambaye alikuzwa na binamu yake mkubwa, Mordekai. Kutii kwake kwa baba yake wa kambo kulimsaidia kuwa mtiifu kwa Mungu. Esta alimtii Mungu na kuweka maisha yake hatarini ili kuwakomboa watu wake, Wayahudi. Simulizi ya Esta inaelezea utawala wa Mungu wa enzi juu ya matukio na historia, haswa jinsi anavyolinda watu wake na kutumika kupitia wale wanaomtii.
## Ethiopia, Mtu wa Ethiopia ### Ufafanuzi Ethiopia ni nchi katika Afrika iliyo kusini mwa Misri mpakana mwa Mto wa Naili magharibi na katika Bahari ya Shamu mashariki. Mtu kutoka Ethiopia na "mtu wa Ethiopia". Ethiopia ya zamani ilikuwa kusini mwa Misri na ilijumuisha nchi ambayo kwa sasa ni sehemu ya baadhi ya nchi za Afrika, kama Sudani, Ethiopia ya sasa, Somalia, Kenya, Uganda, Afrika ya Kati na Chadi. Katika Biblia, Ethiopia mara nyingine huitwa "Kushi" au "Nubia". Nchi za Ethiopia ('Kushi') na Misri mara nyingine hutajwa pamoja katika Biblia, labda kwa sababu zilikuwa karibu na nyenzake na watu wake yawezekana walikuwa na mababu wa kufanana. Mungu alimtuma Filipo mwinjilisti katika jangwa ambapo alisambaza habari njema kuhusu Yesu na towashi wa Ethiopia.
## Ezekieli ### Ufafanuzi Ezekieli alikuwa nabii wa Mungu wakati wa kipindi cha uhamisho ambapo Wayahudi wengi walipelekwa Babeli. Ezekieli alikuwa kuhani aliyeishi katika ufalme wa Yuda ambapo yeye na Wayahudi wengine wengi walikamatwa na jeshi la Babeli. Kwa zaidi ya miaka ishirini, yeye na mke wake waliishi Babeli karibu na mto, na Wayahudi walikuja pale kumsikiliza akizungumza ujumbe kutoka kwa Mungu. Miongoni mwa wafalme wengine, Ezekieli alitabiri juu ya uharibifu na ujenzi wa Yerusalemu na hekalu. Pia alitabiri kuhusu ufalme wa baadaye wa Masihi.
## Ezra ### Ufafanuzi Ezra alikuwa kuhani wa Israeli na mtaalamu wa sheria ya Kiyahudi ambaye aliweka kumbukumbu ya historia ya kurudi kwa Waisraeli Yerusalemu kutoka Babeli ambapo Israeli alikuwa mateka kwa miaka 70. Ezra aliweka kumbukumbu ya sehemu hii ya historia ya Israeli katika kitabu cha kibiblia cha Ezra. Inawezekana aliandika kitabu cha Nehemia, kwa maana vitabu hivi viwili asili yake ilikuwa kitabu kimoja. Ezra aliporudi Yerusalemu aliimarisha Sheria, kwa maana Waisraeli waliacha kutii Ssheria za Sabato na walioana na wanawake ambao walitenda dini za kipagani. Ezra pia alisaidia kujenga hekalu ambalo liliharibiwa na Wababeli walipoteka Yerusalemu. Kuna wanamume wengine wawili wanaoitwa Ezra waliotajwa katika Agano la Kale.
## Farao, mfalme wa Misri. ### Ufafanuzi Hapo nyakati za kale wafalme waliotawala nchi ya Misri waliitwa Mafarao. * Kwa pamoja zaidi ya wafalme 300 walitawala Misri kwa miaka zaidi ya 2,000. * Wafalme hawa wa Misri walikuwa na nguvu na utajiri. * Baadhi ya Mafarao hawa wametajwa kwenye Biblia. * Mara nyingi cheo hiki kimetajwa kama jina na sio cheo.
## Filipi ### Ufafanuzi Filipi ulikuwa mji muhimu na koloni la Rumi lililokuwa Makedonia kaskazini mwa Ugiriki ya kale. * Paulo na Sila walisafiri kuhubiri kuhusu Yesu kwa watu wa huko. * Wakiwa Filipi Paulo na Sila walikamatwa, lakini Mungu aliwaweka huru kwa muujiza. * Katika agano jipya kitabu cha Wafilipi ni barua ya mtume Paulo aliyowaandikia Wakristo katika kanisa la Filipi. * Kumbuka kuwa huu ni mji tofauti na Kaisaria Failipi ambayo ilikuwa kaskazini mashariki mwa Israeli karibu na mlima Hermoni.
## Filipo, mtume ### Ufafanuzi Mtume Filipo alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu alikuwa anatoka mji wa Bethsaida. * Filipo alimleta Nathanaeli kumwona Yesu, * Yesu alimuuliza Filipo namna ya kuwapa chakula kundi la watu zaidi ya 5,000. * Katika chakula cha mwisho cha pasaka ambacho Yesu alikula na wanafunzi wake alizungumza nao kuhusu Mungu baba yake. Filipo aliuliza swali awaoneshe baba. * Lugha zingine huwa zinaandika herufi tofauti ili kutofautisha jina la Filipo na Filipo wengine kama Mwinjilisti Filipo ili kuondoa utata.
## Filipo, mwinjilisti ### Ufafanuzi Katika kanisa la kwanza huko Yerusalemu Filipo alikuwa mmoja wa viongozi saba waliochaguliwa ili kuwajali masikini, Wakristo wenye uhitaji hasa wajane. * Mungu alimtumia Filipo kushirikisha Injili kwa watu katika miji mingi tofauti huko Yudea na Galilaya akiwepo mtu wa Ethiopia aliyekutana naye katika njia za jangwa la Gaza toka Yerusalemu. * Miaka mingine baadaye Filipo aliishi Kaisaria ambapo Paulo na wafuasi wake waliishi katika nyumba yake walipokuwa wakirudi Yerusalemu. * Wanafunzi wengi wa Biblia wanafikiri kwamba mwinjilisti Filipo hakuwa yule mtume wa Yesu aliyeitwa jina hilo.
## Finehasi ### Ufafanuzi Finehasi ni jina la watu wawili katika agano la kale. * Mmoja wa wajukuu wa Haruni alikuwa kuhani aliyeitwa finehasi aliyepinga kwa nguvu kuabudu miungu ya uongo. * Finehasi aliwaokoa Waisraeli toka kwenye pigo ambalo bwana alilituma ili kuwaadhibu kwa kuwaoa wanawake wa Midiani na kuabudu miungu yao ya uongo. * Katika matukio mbali mbali Finehasi alikwenda na jeshi la Israeli kuwapiga Wamidiani. * Finehasi mwingine aliyetajwa kwenye agano la kale alikuwa mmoja wa wana waovu wa kuhani Eli katika kipindi cha nabii Samweli. * Finehasi na kaka yake Hofini waliuawa kipindi ambacho Wafilisti walivamia Israeli na kuiba sanduku la agano.
## Finisia ### Ufafanuzi Nyakati za kale Finisia lilikuwa taifa lenye utajiri lililokuwa Kanaani karibu na pwani ya barari ya Mediteraniani, kaskazini mwa Israeli. * Finisia ilijumuisha sehemu ya nchi iliyokuwa magharibi mwa mji ambao kwa sasa ni Lebanoni. * Katika agano jipya Mji kuu wa Finisia ulikuwa Tire. Mji mwingine wa Muhimu ulikuwa Sidoni. * Wafinisia alijulikana sana kwa ustadi wao wa kutendeneza mbao kwa kutumia mwerezi, pia walijulikana kwa uwezo wao wa kusafiri na kufanya biashara baharini. Walikuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza Boti. * Moja ya alfabeti za mwanzoni kabisa ziliundwa na Wafinisia. Alfabeti zao zilitumika sana kwa sababu ya mwingiliano mkubwa waliokuwa nao na makundi ya watu kupitia biashara.
## Gabrieli ### Ufafanuzi Gabrieli ni jina la mmoja wa malaika wa Mungu. Anatajwa kwa majina kadhaa, kote katika Agano la kale na Jipya. Mungu alimtuma Gabrieli kumwambia nabii Danieli maana ya maono aliyoyaona. Muda mwingine, Danieli alipokuwa akiomba, malaika Gabrieli alipaa kwake na kutabiri kuhusu kile kitakachotokea hapo baadaye. Danieli alimfafanua kama "mwanamume". Katika Agano Jipya inaandikwa ya kwamba Gabrieli alitokana na Zakaria kutabiri ya kwamba mke wake mzee Elizabeti angepata mwana wa kiume, Yohana. Miezi sita baada ya hapo, Gabrieli alitumwa kwa Mariamu kumwambia ya kwamba Mungu angemuwezesha kwa miujiza kupata mimba ya mtoto amabye angekuwa "Mwana wa Mungu". Gabrieli alimwambia Mariamu kumuita mwanawe "Yesu" .
## Gadi ### Ufafanuzi Gadi ni jina la mmoja wa wana wa Yakobo, yaani, Israeli. Familia ya Gadi ilikuja kuwa moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Mwanamume mwingine katika Biblia aitwaye Gadi alikuwa nabii, ambaye alimkabili Mfalme Daudi kwa dhambi ya kufanya sensa ya watu wa Israeli. Miji ya Baalgadi na Migdalgadi kila moja wapo ni maneno mawili katika maandishi asili na mara nyigine huandikwa " Baali gadi" na "Migdali Gadi".
## Galatia ### Ufafanuzi Katika kipindi cha Agano Jipya, Galataia ulikuwa mkoa mkubwa wa Kirumi ulioko sehemu ya kati ya mahali ambapo sasa ni nchi ya Uturuki. Sehemu ya Galatia ilikuwa mpaka na Bahari Nyeusi upande wa Kaskazini. Ilikuwa mpakani na mikoa ya Asia, Bithinia, Kapadocia, Selisia na Pamfilia. Mtume Paulo aliandika barua kwa Wakristo walioishi katika mkoa wa Galatia. Barua hii ni kitabu cha Agano Jipya cha "Wagalatia". Sababu moja ambayo Paulo aliandika barua yake kwa Wagalatia ilikuwa kusisitiza tena injili ya wokovu kwa neema, na sio kazi. Wakristo Wayunani wa Galatia walifundishwa na Wakristo wa Kiyahudi kule ya kwamba ilikuwa lazima kwa waumini kukaa na baadhi ya sheria za Kiyahudi.
## Galilaya, Mgalilaya ### Ufafanuzi Galilaya ni eneo la kaskazini ya Israeli, kaskazini ya Samaria. "Mgalilaya" alikuwa mtu ambaye aliishi Galilaya. Galilaya, Samaria, na Yudea ilikuwa miji mitatu ya msingi ya Israeli wakati wa Agano Jipya. Galilaya imepakana upande wa mashariki na ziwa kubwa liitwalo "Ziwa la Galilaya". Yesu alikua na kuishi katika mji wa Nazareti Galilaya. Miujiza mingi na mafundisho ya Yesu yalifanyika katika eneo la Galilaya.
## Gathi ### Ufafanuzi Gathi ilikuwa moja ya miji mikubwa mitano ya Wafilisti. Ilikuwa kaskazini mwa Ekroni na mashariki ya Ashdodi na Ashkeloni. Hodari wa Kifilisti Goliati alitoka katika mji wa Gathi. Katika wakati wa Samueli, Wafilisti waliiba sanduku la agano kutoka Israeli na kulipeleka katika hekalu lao la kipagani kule Ashdodi. Baadaye likahamishwa kwenda Gathi na baadaye Ekroni. Lakini Mungu aliwaadhibu watu wa miji hiyo na maradhi, kwa hiyo walilirudisha Israeli tena. Daudi alipokuwa akitoroka kutoka kwa Mfalme Sauli, alielekea Gathi na kuishi kule kwa muda pamoja na wake zake wawili na wanamume mia sita waliokuwa wafuasi wake waaminifu.
## Gaza ### Ufafanuzi Wakati wa Biblia, Gaza ulikuwa mji tajiri wa Kifilisti uliokuwa pwani mwa Bahari ya Mediteranea, kama kilomita 38 kusini ya Ashdodi. Ilikuwa moja ya miji mitano mikuu ya Filisti. Kwa sababu ya mahali ilipo, Gaza ilikuwa bandari muhimu ambapo masuala ya kibiashara yalifanyika kati ya makundi ya watu wengi tofauti na mataifa. Leo, mji wa Gaza bado ni bandari muhimu katika kanda ya Gaza, ambayo ni eneo la nchi iliyoko katika pwani ya Bahari ya Mediteranea iliyopakana na Israeli upande wa kaskazini na mashariki, na kusini mwa Misri. Gaza ilikuwa mji ambao Wafilisti walimchukua Samsoni baada ya kumkamata. Filipo mwinjilisti alikuwa akitembea katika barabara ya jangwa kuelekea Gaza alipokutana na towashi wa Ethiopia.
## Gerari ### Ufafanuzi Gerari ni mji na sehemu katika nchi ya Kaanani, iliyopo kusini magharibi mwa Hebroni na kaskazini magharibi mwa Beersheba. Mfalme Abimeleki alikuwa mtawala wa Gerari pale Abrahamu na Sara walipokuwa pale. Wafilisti walitawala eneo la Gerari wakati wa kipindi Waisraeli waliishi Kaanani.
## Geshuri ### Ufafanuzi Katika kipindi cha Mfalme Daudi, Geshuri ilikuwa ufalme mdogo uliokuwa upande wa mashariki wa Ziwa la Galilaya, kati ya nchi za Israeli na Aramu. Mfalme Daudi alimuoa Maaka, binti wa mfalme wa Geshuri na akamzalia mwana wa kiume, Absalomu. Baada ya kumuua ndugu yake Amnoni, Absalomu alikimbilia kaskazini mashariki mwa Yerusalemu hadi Geshuri, umbali wa kama maili 88. Alikaa kule miaka mitatu.
## Gethsemane ### Ufafanuzi Gethsemane ilikuwa bustani ya mizeituni mashariki mwa Yerusalemu mbali ya bonde la Kidroni karibu na Mlima wa Mizeutuni. Bustani ya Gethsemane ilikuwa sehemu ambapo Yesu na wafuasi wake walienda kuwa wenyewe na kupumzika, mbali na mikusanyiko. Ilikuwa Gethsemane ambapo Yesu aliomba kwa huzuni kubwa, kabla ya kukamatwa pale na viongozi wa Kiyahudi.
## Gibea ### Ufafanuzi Gibea ni jina la mji ambao ulikuwa kaskazini mwa Yerusalemu na kusini ya Betheli. Gibea ilikuwa eneo la kabila la Benyamini. Ilikuwa eneo la vita kubwa kati ya Wabenyamini na Israeli.
## Gibeoni. Wagibeoni ### Ufafanuzi Gibeoni ilikuwa mji ambao ulikuwa kama kilomita 13 kaskazini magharibi mwa Yerusalemu. Watu walioishi Gibeoni walikuwa Wagibeoni. Wagibeoni waliposikia jinsi Waisraeli wameangamiza miji ya Yeriko na Ai, waliogopa. Kwa hiyo Wagibeoni walikuja kwa viongozi wa Israeli Gilgali na kuvunga kuwa watu kutoka nchi ya mbali. Viongozi wa Israeli walidanganywa na kufanya makubaliano na Wagibeoni ya kwamba watawalinda na kutowaangamiza.
## Gideoni ### Ufafanuzi Gideoni alikuwa mwanamume wa Kiisraeli ambaye aliinuliwa na Mungu kuwakomboa Waisraeli kutoka kwa adui zao. Katika kipindi ambacho Gideoni aliishi, kundi la watu lijulikanalo kama Midiani waliendelea kuwashambulia Waisraeli na kuangamiza mazao yao. Ingawa Gideoni aliogopa, Mungu alimtumia kuwaongoza Waisraeli kupigana dhidi ya Midiani na kuwashinda. Gideoni pia alimtii Mungu kwa kuangusha madhabahu chini ya miungu wa uongo wa Baali na Ashera. Hakuwaongoza tu watu katika kuwashinda adui zao lakini pia aliwatia moyo kutii na kumwabudu Yahwe, Mungu mmoja wa ukweli.
## Gileadi ### Ufafanuzi Gileadi ni jina na eneo la milima mashariki mwa mto Yordani, ambapo kabila la Waisraeli la Gadi, Rubeni na Manase waliishi. Eneo hili pia lilijulikana kama "nchi ya mlima wa Gileadi" au "Mlima Gileadi". "Gileadi" ilikuwa jina la wanamume kadhaa katika Agano la Kale. Mmoja wa wanamume hawa alikuwa mjukuu wa Manase. Gileadi mwingine alikuwa baba wa Yefta.
## Gilgali ### Ufafanuzi Msemo Gilgali ulikuwa mji kaskazini mwa Yeriko na ilikuwa sehemu ya kwanza ambayo Waisraeli waliweka kambi baada ya kuvuka mto Yordani kuingia Kaanani. Kula Gilgali, Yoshua aliweka mawe kumi na mawili kutoka mto uliokauka wa Mto Yordani ambao walimaliza kuuvuka. Gilgali ulikuwa mji ambao Eliya na Elisha walishi walipovuka Yordani pale Eliya alipochukuliwa kwenda mbinguni. Kulikuwa na sehemu zingine pia zijulikanazo kama "Gilgali" katika Agano la Kale. Neno "gilgali" lina maana ya "mduara wa mawe" labda kumaanisha sehemu ambapo dhabahu ya mduara ilijengwa. Katika Agano la Kale, jina hili mara nyingi hujitokeza kama "gilgali". Hii inaweza kuonyesha ya kwamba haikuwa mahali bayana lakini ilikuwa ufafanuzi wa ain fulani ya sehemu.
## Giriki ### Ufafanuzi Katika kipindi cha Agano Jipya, Giriki ilikuwa mkoa katika Ufalme wa Kirumi. Kama nchi ya siku ya sasa ya Giriki, ilikuwa katika peninsula ambayo ilikuwa mpakani na Bahari ya Mediteranea, Bahari ya Aegea, na Bahari ya Ionia. Mtume Paulo alizuru miji kadhaa ya Giriki, na kuimarisha makanisa katika miji ya Korintho, Thesalonike, na Filipi na labda mingine. Watu ambao hutoka Giriki wanaitwa "Wagiriki" na lugha yao ni "Kigiriki". Watu kutoka mikoa mingine ya Kirumi pia walizungumza Kigiriki, ikiwemo Wayahudi wengine. Mara nyingine msemo "Giriki" hutumika kumaanisha Mataifa.
## Golgotha ### Ufafanuzi Msemo "Golgotha" ni jina la mahali ambapo Yesu alisulubiwa. Inatokana na neno la Kiaramea ambalo lina maana ya "Fuvu la kichwa" au "Mahali pa fuvu la kichwa". Golgotha ilikuwa mahali nje ya kuta za mji wa Yerusalemu, eneo la karibu. Labda ilikuwa mahali ya mteremko wa Mlima wa Mizeituni. Katika tafsiri za Kiingereza za zamani za Biblia, Golgotha inatafsiriwa kama "Kalivari" ambayo inatokana na neno la Kilatini kwa ajili ya "fuvu la kichwa". Tafsiri nyingi za Biblia hutumia neno ambalo huonekana au kusikika kama "Golgotha" kwa maana maana yake tayari imefafanuliwa katika maandisha ya Biblia.
## Goliati ### Ufafanuzi Goliati alikuwa mwanajeshi mrefu sana, na mkubwa sana katika jeshi la Wafilisti ambaye aliuwawa na Daudi. Goliati alikuwa kati ya mita mbili au tatu kwa urefu. Mara nyingi huchukuliwa kama jitu kwa sababu ya umbo lake kubwa. Ingawa Goliati alikuwa na silaha bora zaidi na mkubwa kuliko Daudi, Mungu alimpa Daudi nguvu na uwezo wa kumshinda Goliati. Waisraeli walitangazwa washindi juu ya Wafilisti kama matokea ya ushindi wa Daudi juu ya Goliati.
## Gomora ### Ufafanuzi Gomora ilikuwa mji katika bonde lenye rutuba, karibu na Sodoma ambapo mpwa wa Abrahamu Lutu alichagua kuishi. Mahali haswa pa Gomora na Sodoma hapajulikani, lakina kuna viashiria ya kwamba inaweza kuwa mahali moja kwa moja kusini mwa Bahari ya Chumvi, karibu na Bonde la Sidimu. Kulikuwa na wafalme wengi vitani katika eneo ambapo Sodoma na Gomora na ilikuwepo. Familia ya Lutu ilipokamtwa katika ugomvi kati ya Sodoma na miji mingine, Abrahamu na wanamume wake waliwakomboa. Sio muda baada ya hapo, Sodoma na Gomora ziliteketezwa na Mungu kwa sababu ya uovu wa watu walioishi pale.
## Gosheni ### Ufafanuzi Gosheni ni jina la eneo la nchi yenye rutuba ambalo lilikuwa mahali katika Mto Naili katika sehemu ya kusini ya Misri. Yusufi alipokuwa mtawala wa Misri, baba yake na ndugu na familia zao walikuja kuishi Gosheni kutoroka njaa Kaanani. Wao na uzao wao waliishi vzuri Gosheni kwa zaidi ya miaka 400, lakini walilazimishwa katika utumwa na farao wa Kimisri. Hatimaye Mungu alimtuma Musa kuwasaidia watu wa Israeli kuondoka nchi ya Gosheni na kutoroka utumwa.
## Habakuki ### Ufafanuzi Habakuki alikuwa ni nabii wa Agano la Kale aliyeishi kipindi cha Mfalme Yehoyakimu alipokuwa akiitawala Yuda. Pia, nabii Yeremia alikuwa bado yuko hai katika kipindi hicho. Nabii huyu aliandika kitabu cha Habakuki mnamo mwaka 600 KK, katika kipindi ambacho Wababeli walikuwa wameuhusuru mji wa Yerusalem na kuchukua watu wengi wa Yuda na kuwapeleka matekani. Yahweh alimpa Habakuki unabii kuhusu Wakaldayo (Wababeli) ambao wangekuja na kuwateka watu wa Yuda. Moja kati ya misemo maarufu na iliyojulikana sana ya nabii Habakuki ni "Mwenye haki ataishi kwa imani."
## Habili ### Ufafanuzi Habili alikuwa mtoto wa Adamu na Hawa. Alikuwa ndogo wake na Kaini. Habili alikuwa mfugaji. Habili alitoa sadaka ya baadhi ya mifugo yake kwa Mungu. Mungu alipendezwa na sadaka ya Habili. Mtoto wa kwanza wa Adamu na Hawa, Kaini alimuua Habili.
## Hagai ### Ufafanuzi Hagai alikuwa ni nabii wa Yuda katika kipindi ambacho Wayahudi walikuwa wamerudi kutoka matekani huko Babeli. Hagai alitabiri katika kipindi ambacho watu wa Israeli walikuwa chini ya utawala wa liwali Zerubabeli. katika kipindi hiki pia, nabii Zekaria alikuwa akitabiri yaani Hagai na Zekaria walifanya kazi katika kipindi kimoja. Hagai na Zekaria waliwasihi sana Wayahudi ili walijenge Hekalu ambalo lilikuwa limebomolewa na Wababeli chini ya mfalme Nebukadreza.
## Hajiri ### Ufafanuzi Hajiri alikuwa ni mwanamke wa Kimisri alikuwa mtumwa wa Sara. Sara alimtoa Hajiri kwa Ibrahimu ili aweze kuzaa naye, baada ya kuona kuwa yeye (Sara) hana uwezo wa kuzaa . Hajiri alipata mimba na akamzalia Ibrahim mwana, Ishmaeli. Mungu aliiangalia taabu ya Hajiri katika jangwa na akaahidi kuubariki uzao wa Hajiri.
## Hamathi, Lebo Hamathi, Wahamathi ### Ufafanuzi Hamathi ulikuwa ni mji muhimu sana kasikazini mwa Kanaani. Wahamathi walikuwa ni uzao wa mtoto wa Nuhu, Kanaani. Jina 'Lebo Hamathi' huenda linarejelea mlima ulikuwa karibu na mji wa Hamathi. Baadhi ya tafsiri hufasiri 'Lebo Hamathi' kama "Mlango wa Hamathi" Mfalme Daudi alimshinda mfalme Tou wa Hamathi, ushindi ambao uliwafanya kuwa katika makubaliano na mahusiano mazuri. Hamathi ulikuwa ni mji wa bohari au ghala la mfalme Sulemani, mahali ambapo alitunza hazina yake. Ni katika nchi hii ya Hamathi ambapo mfalme Zedekia aliuawa na mfalme Nebukadreza, pia ni mahali ambapo mfalme Yehoyazi alikamatwa na Farao wa Misri. Neno 'Wahamathi' laweza kutafsiriwa kama ' watu wa Hamathi'
## Hamori ### Ufafanuzi Hamori alikuwa mkanaani aliyeishi katika mji wa Shekemu katika kipindi ambacho Yakobo na familia yake walikuwa wakiishi karibu na Sukothi. Alikuwa ni Mhivi. Yakobo alinunu eneo la maziko kutoka kwa wana wa Hamori. Wakali wakiwa huko mwana mmoja wa Hamori, Shekemu alimbaka binti wa Yakobo aliyeitwa Dina. Kaka zake na Dina walilipiza kisasi kwa familia ya Hamori na kuwaua watu wote katika mji wa shekemu.
## Hamu ### Ufafanuzi Hamu ni mtoto wa pili kati ya wana watatu wa Nuhu. katika gharika kuu la kidunia ambalo liliigharikisha dunia yote, Hamu na ndugu zake pamoja na wake zao walikuwa pamoja na baba yao, Nuhu katika safina. Baada ya gharika, kulikuwa na tukio la Hamu kutomweshimu baba yake, Nuhu. Na matokeo yake, Nuhu alimlaani mtoto wa Hamu alilyeitwa Kanaani pamoja na uzao wake wote, ambao baadaye walijulikana kama Wakanaani.
## Hana ### Ufafanuzi Hana alikuwa ni mama wa nabii Samwel. Alikuwa ni mmoja kati ya wake waili wa Elikana. Hana alikuwa tasa, alikuwa hawezi kuzaa mtoto. Hiki kilikuwa ni kilio kikubwa sana kwa Hana. Hana alimwomba Mungu kwa bidii sana hekaluni ili apate mtoto. Hana alimwahidi Mungu kumtoa mtoto huyu ili amtumikie Mungu. Mungu alimpa haja yake na mtoto Samweli alipokuwa na umri wa kutosha, alimleta ili atumike hekaluni hekaluni. Mungu alimpa Hana watoto wengine baada ya hayo.
## Hanania ### Ufafanuzi Jina Hanania limetumika katika Agano la Kale kurejelea watu mbalimbali. Hanania mmoja alikuwa ni mwisraeli aliyechukuliwa matekani huko Babeli ambaye Jina lake lilibadilishwa na kuwa 'Shadraka.' kutoka na tabia na uwezo wake, alipewa nafasi nzuri maana alikuwa mtumwa wa kifalme. Hanania (Shadraka) na vijana wengine wawili wa Kiisraeli walitupwa katika tanuru la mot kwasababu walikataa kumwabudu wa mfalme wa Babeli. Mungu alionesha uwezo wake kwa kuwalinda ili wasije wakadhurika. Hanania mwingine alikuwa ni mzao wa ukoo wa Mfalme Sulemani. Kulikuwa na Hanania mwingine tofauti aliyekuwa nabii wa uongo katika kipindi cha nabii Yeremia. Mtu mmoja aliyeitwa Hanania alikuwa ni kuhani aliyesaidia kuongoza sherehe katika kipindi cha Nehemia.
## Harani ### Ufafanuzi Harani alikuwa kaka mdogo wa Ibrahimu na baba yake na Lutu. harani pia lilikuwa ni jina la mji ambao Ibrahimu na familia yake waliishi kwa muda mfupi walipokuwa njiani kutoka Uru kwenda nchi ya Kanaani. Mtu mwingine tofauti aliyeitwa Harani alikuwa ni mtoto wa Kalebu. Mtu wa tatu katika Biblia aliyeitwa Harani alikuwa ni wa uzao wa Lawi.
## Haruni ### Ufafanuzi Haruni alikuwa kaka yake na Musa. Mungu alimchagua Haruni kuwa kuhani mkuu wa kwanza wa watu wa Israeli. Haruni alimsaidia Musa kuzungumza na Farao kuhusu kuwaachia huru wana wa Israeli. Wakati wana wa Israeli wanasafiri jangwani, Haruni alitenda dhambi kwa kutengeneza sanamu ili watu waiabudu. Pia Mungu alimchagua Haruni na uzao wake kuwa makuhani.
## Hawa ### Ufafanuzi Hili lilikuwa jina la mwanamke wa kwanza. Jina lake linamaanisha "uhai" au "kuishi". Mungu alimuumba Hawa kutoka kwa ubavu ambao aliuchukua kutoka kwa Adamu. Hawa aliumbwa kuwa "msaidizi" wa Adamu. Alikuja kando ya Adamu kumsaidia katika kazi ambayo Mungu aliwapa kufanya. Hawa alijaribiwa na Shetani (kwa mfano wa nyoka) na alikuwa wa kwanza kufanya dhambi kwa kula tunda ambalo Mungu aliwaambia kutokula.
## Hebroni ### Ufafanuzi Hebroni ulikuwa ni mji uliokuwa katika milima mirefu na ya miamba kama maili 20 hivi kusini mwa Yerusalemu. Mji huu ulijengwa mnamo mwaka 2000 KK katika kipindi cha Abramu. Mji huu ulitajwa mara nyingi katika mtiririko wa matukio mbalimbali katika Agano la Kale. Mji wa Hebroni ulikuwa na wajibu na nafasi ya muhimu sana katika maisha ya Mfalme Daudi. Wana kadhaa wa Mfalme Daudi kama vile Absalomu walizaliwa huko. Mji huu uliharibiwa na Warumi mnamo mwaka 70 BK.
## Henoko ### Ufafanuzi Henoko ni jina la wanamume wawili katika Agano la Kale. Mwanamume mmoja aliyeitwa Henoko alitokana kwa Sethi. Alikuwa babu mkuu wa Nuhu. Henoko huyu alikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu na alipokuwa na miaka 365, Mungu alimchukua kwenda mbinguni bila ya kufa. Mwanamume tofauti aliyeitwa Henoko alikuwa mwana wa Kaini.
## Herode Antipa ### Ufafanuzi Katika kipindi kirefu cha maisha ya Yesu, Herode Antipa alikuwa ni mtawala wa Dola ya Kirumi iliyojumuisha jimbo la Galilaya. Antipa mara nyingine alitajwa kama 'Mfalme" kama alivyokuwa baba yake, Herode Mkuu, ingawa hakuwa mfalme kweli. Herode Antipa alitawala robo au moja ya nne ya Dola ya Kirumi na hivyo aliitwa Herode 'Tetraki' yaani mkuu wa mkoa. Antipa ni 'Herode' aliye Yohamuru Yohana mbatizaji auawe kwa kukatwa kichwa. Alikuwa ni Herode Antipa pia aliyemwuuliza Yesu maswali kabla ya kusulubiwa kwake. Maherode wengine katika Agano Jipya walikuwa ni mtoto wa Antipa (Agripa) na mjukuu ( Agripa wa pili) aliyetawala kipindi cha mitume.
## Herode Mkuu ### Ufafanuzi Herode mkuu alikuwa akitawala Uyahudi
## Herodia ### Ufafanuzi Herodia alikuwa ni mke wa Herode Antipa huko Uyahudi kipindi cha Yohana Mbatizaji. Herodia alikuwa mke halali wa kaka yake na Antipa, aliyeitwa Philipo, lakini baadaye aliolewa na Herodi Antipa kinyume na sheria. Yohana mbatizaji aliwakemea Herode na Herodia kwa sababu ya ndoa yao haramu. Na kwasababu hiyo, Yohana alifungwa gerezani na baadaye aliuawa kwa kukatwa kichwa.
## Hezekia ### Ufafanuzi Hezekia alikuwa ni mfalme wa 13 wa ufalme wa Yuda. Alikuwa ni mfalme aliyemtumaini Mungu na kumtii. Tofauti na baba yake, Ahazi aliyekuwa mfalme mwovu, Mfalme Hezekia alikuwa ni mfalme mzuri aliyeharibu maeneo yote ya ibada ya miungu katika Yuda. Wakati Hezekia alipougua na alipokuwa karibu kufa, alimwomba Mungu sana ili alinde na kuhifadhi maisha yake. Mungu alimponya na alimruhusu kuishi miaka 15 zaidi. Mungu alifanya muujiza kwa Hezekia kwa kurudisha muda nyuma. Mungu alijibu maombi ya Hezekia kwa kuwaokoa watu wake kutoka mikononi mwa Mfalme Senakaribu wa Siria, aliyekuwa akiwashambulia.
## Hilikia ### Ufafanuzi Hilikia lilikuwa ni jina la kuhani mkuu katika kipindi cha utawala wa mfalme Yosia. Hilikia alipata kitabu cha sheria, katika kipindi ambacho hekalu lilifanyiwa matengenezo na akamuru kitabu hicho kipelekwe kwa mfalme Yosia. Baada ya kusomewa kitabu cha sheria, Yosia alihuzunika na aliwafanya watu wa Israeli kumwabudu Yahweh tena na kutii sheria zake. Mtu mwingine aliyeitwa Hilikia alikuwa ni mwana wa Eliyakimu na alifanya kazi ikulu kipindi cha utawala wa mfalme Hezekia.
## Horebu ### Ufafanuzi Mlima Horebu ni jina jingine la mlima Sinai, mahali ambapo Mungu alimpa Musa vipande vya mawe vya amri kumi za Mungu. Mlima Horebu huitwa Mlima wa Mungu Musa aliiona kichaka kilichokuwa kinawaka moto wakati akichunga kondoo katika mlima Horebu. Katika mlima Horebu, Mungu alifunua agano lake kwa Waisraeli kwa kuwapa vipande vya mawe vilivyo na Amri juu yake. Ni mahali ambapo Mungu alimwambia Musa kuupiga mwamba ili maji yatoke kwa ajili ya waisraeli katika kipindi walichokuwa wanazunguka jangwani. Sehemu maalumu ulipo mlima huu haijulikani, huenda ni sehemu ya kusini ambayo kwa sasa inajulikana kama 'Penisula ya Sinai Inawezekana kuwa Horebu lilikuwa ni jina kamili la mlima na kwamba Mlima Sinai ina maana ya milima ya Sinai kwa kurejelea ukweli kwamba Mlima Horebu ulikuwa katika jangwa la Sinai.
## Hosea ### Ufafanuzi Hosea alikuwa ni nabii wa Israeli aliyeishi na kutabiri mnamo mwaka 750 KK. Huduma yake Hosea ilidumu kwa miaka mingi katika vipindi vya wafalme kadhaa, kama vile Yeroboam, Zekaria, Yotham, Ahazi, Hoshea, Uzia na Hezekia. Hosea aliambiwa na Mungu kuoa kahaba aliyeitwa Gomeri . Ingawa alikuwa mwanamke aliyekuwa si mwaminifu, Hosea aliambiwa aendelee kumpenda. Hii ilikuwa picha inayoonyesha Upendo wa Mungu kwa ajli ya watu wake, Israeli waliokuwa si waaminifu. Hosea alitabiri kinyume na watu wa Israeli kwasababu ya dhambi zao, akiwaonya kugeuka na kuacha kuabudu miungu.
## Hoshea ### Ufafanuzi Hoshea lilikuwa ni jina la Mfalme wa Israeli na baadhi ya watu wengine katika Biblia. Hoshea mwana wa Ala, alikuwa ni Mfalme wa Israeli kwa miaka tisa katika kipindi ambacho Ahazi na Hezekia walikuwa wafalme wa Yuda. Yoshua mwana wa Nuni aliitwa Hoshea hapo awali. Musa alilibadilisha jina lake na kuwa Yoshua kabla ya kumtuma pamoja na wale wanaume kumi na mmoja kuipeleleza nchi ya Wakanaani. Baada ya kufa kwa Musa, Joshua aliwaongoza watu wa Israeli kuimiliki nchi ya Kanaani. Mtu mwingine aliyeitwa Hoshea alikuwa ni mwana wa Azazia na alikuwa ni mmoja wa viongozi wa Waefraimu.
## Ikonio ### Ufafanuzi Ikonio ulikuwa mji sehemu ya kusini kati ya nchi ambayo sasa ni Uturuki. Katika safari ya kwanza ya kimisionari ya Paulo, yeye na Barnaba walienda Ikonio baada ya Wayahudi kuwalazimisha kuondoka katika mji wa Antiokia. Kisha wayahudi wasioamini na Wayunani ndani ya Ikonio walipanga pia kumponda mawe Paulo na watumishi wenzeka, lakini walitoroka katika mji wa karibu wa Listra. Baada ya watu kutoka Antiokia na Ikonia kuja Listra na kuwachochea watu kumponda mawe Paulo.
## Isaka ### Ufafanuzi Isaka alikuwa mwana pekee wa Abrahamu na Sara. Mungu aliwaahidi kuwapa mwana wa kiume ingiwa walikuwa wazee sana. Jina "Isaka" linamaanisha "kicheko." Mungu alipomuambia Abrahamu kuwa Sara atazaa mwana wa kiume, Abrahamu alicheka kwa sababu wote walikuwa wazee sana. Baada ya muda, Sara pia alicheka aliposikia taarifa hii. Lakini Mungu alitimiza ahadi yake na Isaka alizaliwa kwa Abrahamu na sara katika uzee wao. Mungu alimuambia Abrahamu kuwa agano alilofanya na Abrahamu itakuwa pia ya Isaka na vizazi vyake milele. Wakati Isaka alikuwa kijana, Mungu aliijaribu imani ya Abrahamu kwa kumuamuru kumtoa isaka kama sadaka. Mwana wa Isaka, Yakobo, alikuwa na wana kumi na mbili ambao uzao wao baadaye ukawa makabila kumi na mbili ya taifa la Israeli.
## Isakari ### Ufafanuzi Isakari alikuwa mwana wa tano wa Yakobo. Mama yake alikuwa Lea. Kabila la Isakari lilikuwa moja ya makabila kumi na mbili ya Israeli. Nchi ya Isakari ilikuwa jirani na Naftali, Zabuloni, Manase, na Gadi. Ilikuwa chini ya bahari la Galilaya.
## Isaya ### Ufafanuzi Isaya alikuwa nabii wa Mungu aliyetabiri wakati wa utawala wa wafalme wanne wa Yuda: Uzia, Yothamu, Ahazi, na Hezekia. Aliishi Yerusalemu wakati Waashuri walipokuwa wakivamia mji, wakati wa utawala wa Hezekia. Kitabu cha Agano la Kale cha Isaya ni moja ya vitabu vikuu vya Biblia. Isaya aliandika unabii mwingi ulitokea wakati wa uhai wake. Isaya anajulikana zaidi kwa unabii alioandika kumhusu Masihi uliotimia miaka 700 baadaye wakati Yesu alipoishi duniani. Yesu na wanafunzi wake walinukuu utabiri wa Isaya kuwafundisha watu kuhusu Masihi.
## Ishmaeli ### Ufafanuzi Ishmaeli alikuwa mwana wa Abrahamu na mtumwa wa Kimisri Hagai. Kuna wana kadhaa pia katika Agano la Kale wanaoitwa Ishmaeli. Jina "Ishmaeli" linamaanisha, "Mungu husikia." Mungu aliahidi kumbariki mwana wa Abrahamu, Ishmaeli, lakini hakuwa mwana ambaye Mungu aliye ahidi kuweka agano lake naye. Mungu alimlinda Hagai na Ishmaeli walipotumwa jangwani. Wakati Ishmaeli alipokuwa akiishi katika jangwa la Parani, alimuoa mwanamke wa Misri. Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa afisa wa jeshi kutoka Yuda aliyeongoza kundi la wanaume kumua gavana aliyeteuliwa na mfalme wa Kibabeli, Nebukadreza. Pia kuna wanaume wengine wanne walioitwa Ishmaeli katika Agano la Kale.
## Kadeshi, Kadesh-Barnea, Meriba Kadeshi ### Ufafanuzi Majina Kadeshi, Kadesh-Barnea, na Meriba Kadeshi yote yanazungumzia mji muhimu katika historia ya Israeli ambao ulikuwa sehemu ya kusini ya Israeli, karibu na eneo la Edomu. Mji wa Kadeshi palikuwa oasisi, mahali palipokuwa na maji na udongo wenye virutubisho katikati ya jangwa liitwalo Sini. Musa alituma wapelelezi kumi na mbili katika nchi ya Kanaani kutoka Kadesh-Barnea. Israeli pia waliweka kambi Kadeshi wakati wakizunguka-zunguka jangwani. Kadesh-Barnea ndipo Miriamu alipofia. Ilikuwa Kadesh-Barnea ambapo Musa hakumtii Mungu na kuupiga mwamba kupata maji kwa ajili ya Waisraeli, badala ya kuzungumza nayo kama Mungu alivyomuagiza. Jina "Kadeshi" linatoka katika neno la Kihebrania lenye maana ya "takatifu" au "kuwekwa tofauti."
## Kaini ### Ufafanuzi Kaini na mdogo wake Abeli walikuwa atoto wakwanza wa Adam na Hawa wametajwa katika Biblia. * Kaini alikuwa mkulima ambaye alizalisha mazao ya chakula wakati Abeli alikuwa mfuga Kondoo. * Kaini alimuua kaka yake Abeli kwa sababu ya wivu, kwa sababu Mungu aliipokea sadaka ya kuteketeza ya Abeli. * Kama adhabu, Mungu alimpeleka mbali na Edeni na kumwambia kwamba aridhi hatatoa mazao kwa ajili yake. * Mungu aliweka alama kwenye paji la uso la Kaini kama ishara kwamba Mungu atamlinda ili asiuawe na watu wengine wakati akizurura.
## Kaisari ### Ufafanuzi Neno "Kaisari" lilikuwa jina au jina la heshima lililotumika kwa watawala wengi wa Dola ya Rumi. Katika Biblia, hili neno linahusisha kwa tawala tatu tofauti tofauti. * Mtawala wa kwanza wa Rumi alikuwa anaitwa Kaisari alikuwa "Kaisaria Agustino," ambaye alitawala katika kipindi ambacho Yesu alizaliwa. * Kama miaka thelathini baadaye, katika kipindi wakati Yohana Mbatizaji alipokuwa akihubiri, Tiberia Kaisari alikuwa mtawala wa dola ya Rumi. * Tibaria Kaisari Alikuwa bado anatawala Rumi wakati Yesu alipowaambia watu kumlipa Kaisari kile alichokuwa anastahili na kumpa Mungu alichokuwa anastahili. * Wakati Paulo alipokata rufaa kwa Kaisari, hii ilimhusu mtawala mkuu wa Rumi, Neru, ambaye pia alikuwa na cheo "Kaisari" * Wakati "Kaisari" linatumika lenyewe kama cheo, pia linaweza kutafsiriwa kama: "Dola" au "Utawala wa Rumi." Katika majina kama Kaisari Agustino au Tiberia Kaisari, "Kaisari" inaweza kutamkwa karibia na vile lugha ya taifa inavolitamka.
## Kaisaria, Kaisaria Filipi ### Ufafanuzi Kaisaria ulikuwa mji wa muhimu katika pwani ya Bahari ya Meditrania, kama 39 kilomita kusini mwa Mlima Karmeli Kaisaria Filipi ulikuwa mji unaoonyesha kusinimagharibi sehemu ya Israeli, karibu na Mlima Herimoni. * Hii miji iliitwa kwa ajili ya Makaisari ambao walitawala Dola ya Rumi. * Pwani ya Kaisaria ilikuja ikawa mji mkuu wa Rumi mkoa wa Yudea karibia na mda wa kuzaliwa kwa Yesu. * Mtume Petro alihubiri kwa mara ya kwanza kwa Wayunani katika Kaisaria. * Paulo alianza safari yake kutoka Kaisaria kwenda Tarso na pia alipitia huu mji mara mbili katika safari zake za kimisionari. * Yesu pamoja na wanafunzi wake walisafiri hadi mkoa kuzunguka Kaisaria Filipi. katika Siria. Miji yote iliitwa baada ya Herodi Filipi.
## Kalebu ### Ufafanuzi Kalebu alikuwa mmoja wa wapelelezi wa Israeli ambao walitumwa na Munsa kuipeleleza nchi ya Kanaani. * Yeye na Yoshua waliwaambia watu wamwamini Mungu ili awasaidie wawashinde Wakanaani. * Yoshua na Kalebu walikuwa watu pekee katika uzao wao waliokubaliwa kuingia katika nchi ya ahadi ya Kanaani. * Kalebu aliomba kuwa nchi ya Hebroni apewe yeye na familia yake. Alijua kuwa Mungu atamsaidia kuwashinda watu wanaoishi huko.
## Kana ### Ufafanuzi Kana kilikuwa kijiji au mji katika Galilaya, maili tisa kaskazini mwa Nazareti. * Kana palikuwa nyumbani kwa Nathanaeli mmoja wa wale kumi na mbili. * Yesu alihudhuria sherehe ya harusi huko Kana na akafanya muujiza huko wa kugeuza maji kuwa divai. * Baadaye Yesu alirudi tena Kana na akakutana na viongozi toka Kapernaumu waliomuomba amponye mtoto wao.
## Kanaani, Mkanaani ### Ufafanuzi Kanaani alikuwa mtoto wa Hamu, ambaye alikuwa moja ya watoto wa Nuhu. Wakanaani walikuwa vizazi vya Kanaani. * Neno "Kanaani" au "nchi ya Kanaani" pia limerejelewa kwenye eneo la nchi kati ya Mto Yordani na Bahari ya Meditrenia. Iliendelea kusini mpaka kwenye mpaka wa Misri na kaskazini ya mpaka wa Siria. * Hii nchi ilikuwa makazi kwa Wakanani, na makundi ya watu wengine wengi. * Mungu aliahidi kumpa Ibrahim na uzo wake nchi ya Kanaani, Waisraeli.
## Kapranaumu ### Ufafanuzi Kapranaumu kilikuwa kijiji cha uvuvi katika kusini magaharibi ya pwani ya Bahari ya Galilaya. * Yesu aliishi Kaperanaumu wakati alipokuwa akifundisha Kalilaya. * Baadhi ya wanafunzi wake walitokea Kaperanaumu. * Yesu pia alifanya miujiza mingi katika mji huu, pamoja na kumfufua binti aliyekuwa amekufa. * Kapranaumu ilikuwa moja ya miji mitatu ambayo Yesu aliwaonya hadharani kwa sababu watu wao walimkataa na hawakuamini ujumbe wake. Aliwaonya kwamba Mungu angewaadhibu kwa kutokuamini kwao.
## Karmeli, Mlima Karmeli ### Ufafanuzi Mlima Karmeli ni mlima uliokuwa pwani mwa bahari ya Mediteraniani kaskazini mwa nchi tambarare ya Sharon. Urefu wake ni mita 546. * Pia kulikuwa na mji ulioitwa Karmeli uliokuwepo Yuda kusini mwa bahari ya chunvi. * Tajiri aliyemilikia ardhi Nabali na mke wake Abigaili waliishi karibu na mji wa Karmeli ambapo Daudi na watu wake walimsaidia Kulinda manyoya ya kondoo. * Katika mlia Karmeli Eliya alishindana na manabii wa Baali ili kuthibitisha kuwa Bwana ni Mungu wa kweli pekee. * Kuliweka hili sawa huu haukuwa mlima mmoja. Mlima Karmeli waweza kutafsiriwa kama "mlima katika safu ya milima ya Karmeli."
## Kedari ### Ufafanuzi Kedari lilikuwa jina la mwana wa pili wa Ishmaeli. Lilikuwa pia jina la mji muhimu ambalo linawezekana kuwa liliitwa baada ya huyo mwanamme Mji wa Kaderi inapatikana katika eneo la kaskazini la Arabia karibu na mpaka wa kusini ya Filisti. Katika nyakati za Biblia, palikuwa panajulikana kwa ukuu na uzuri wake. Wazawa wa Kaderi waliunda kundi kubwa la watu linaloitwa "Kaderi." Usemi "hema za Kedari nyeusi" inamaanisha hema za nywele nyeusi za mbuzi ambamo watu wa Kaderi waliishi. Watu hawa walifuga kondoo na mbuzi. Pia walitumia ngamia kwa kusarifishia vitu. Katika Biblia, usemi "utukufu wa Kedari" inamaanisha ukuu wa mji na watu wake.
## Kedeshi ### Ufafanuzi Kedeshi ulikuwa mji wa Kanaani uliochukuliwa na Waisraeli walipoingia Kanaani. Mji huu ulikuwa sehemu ya kaskazini mwa Israeli, katika kipande walichopewa kabila la Naftali. Kedeshi ulikuwa moja ya miji iliyochaguliwa kwa ajili ya makuhani wa Kilawi kuishi, kwa sababu hawakuwa na ardhi yao wenyewe. Ilitengwa pia kama "mji wa ukimbizi."
## Kefa ### Ufafanuzi Kefa alikuwa kuhani wa Israeli katika kipindi cha Yohana Mbatizaji na Yesu. * Kefa alicheza nafasi kubwa katika kujaribu kumlaani Yesu. * Kuhani mkuu Anasi na Kefa walijaribu kuwajaribu Petro na Yohana wakati walipokuwa wamekamatwa baada ya kumponya kiwete. * Kefa ndiye aliyesema kwamba ilikuwa vyema mtu mmoja afe kwa ajili ya taifa kuliko kwa taifa zima kuangamia. Mungu alimfanya kusema hii kama unabii unaohusu ambavyo Yesu angeweza kufa kuokoa watu wake.
## Kilikia ### Ufafanuzi Kilikia ni mkoa mdogo wa Rumi uliokuwa kusini mashariki mwa nchi ya Uturuki. * Mtume Paulo alikuwa mwananchi wa mji wa Tarso uliokuwa Kilikia. * Paulo alikaa miaka saba Kilikia baada ya kukutana na Yesu njiani Damaskas. * Baadhi ya Wayahudi toka Kilikia walikuwa wale waliomfuata Stefano na kuwashawishi watu wampige kwa mawe mpaka kufa.
## Kipro ### Ufafanuzi Kipro ni kisiwa katika bahari ya Mediteraniani karibu kilometa 64 kusini mwa nchi ya sasa ya Uturuki. * Barnaba alikuwa anatokea Kipro hivyo inawezekana binamu yake Johana Marko alitokea huko pia. * Paulo na Barnaba walihubiri kwa pamoja katika kisiwa cha Kipro katika mwanzo wa safari yao ya Kimisionari. Yohana Marko alikuja baadaye kuwasaidia katika safari zao. * Baadae Barnaba na Marko walitembelea tena Kipro. Katika agano la kale Kipro imetajwa kama eneo lenye utajiri wa miti ya Miteashuri.
## Kolosai, Wakolosai ### Ufafanuzi Katika agano jipya Kolosai ulikuwa mji katika Rumi nchi ambayo sasa ni kusini mangharibi mwa uturuki. Wakolosai ni watu walioishi Kolosai. * Ilikuwa kama maili 100 toka bahari ya mediteraniani, Kolosai ilikuwa njia kuu ya biashara kati ya mji wa Efeso na mto Efrata. * Alipokuwa gerezani Rumi Paulo aliandika barua kwa Wakolosai ili kusahihisha mafundisho ya uongo kati ya waamini waliokuwa Kolosai. * Alipokuwa akiandika barua Paulo hakutembelea kanisa katika Kolosai lakini alisikia habari za waamini toka kwa mtumishi mwenzake Epafra. * Epafra alikuwa mfanyakazi wa Kikristo aliyeanzisha kanisa Kolosai. * Kitabu cha Filemoni ni barua ya Paulo kwa waliokuwa wakimiliki watumwa huko Kolosai.
## Kora ### Ufafanuzi Kora lilikuwa jina la wanaume watatu katika Agano la Kale. Mmoja wa wana wa Esau aliitwa Kora. Alikuwa kiongozi katika jamii yake. Kora pia alikuwa mzawa wa Lawi na kwa hiyo alitumika katika maskani kama kuhani. Alikuwa na wivu juu ya Musa na Haruni na kuongoza kundi la watu kuwapinga. Mwanamme wa tatu aliyeitwa Kora aliorodheshwa kama uzao wa Yuda.
## Koreshi ### Ufafanuzi Koreshi alikuwa mfalme wa Uajemi aliyetengeneza himaya ya Uajemi katika mwaka wa 550 Kabla ya Kristo kwa njia ya kutawala Kijeshi. Katika historia alijulikana kama Koreshi mkuu. * Mfalme Koreshi aliishinda Babeli na kusababisha kuachiwa kwa Waisraeli waliokuwa mateka huko. * Koreshi alijulikana kwa tabia yake ya tabia yake ya uvumilivu kwa watu wa taifa alilolishinda. Ukarimu wake kwa Wayahudi ukapelekea kujengwa upya kwa hekalu ya Yerusalemu baada ya kipindi cha mateka. * Koreshi alitawala katika kipindi cha Danieli, Ezra na Nehemia.
## Korintho, Wakorintho ### Ufafanuzi Korintho ulikuwa mji katika nchi ya Ugiriki maili 50 mangharibi mwa Athene. Wakorintho walikuwa watu walioishi Korintho. * Korintho ilikuwa moja kati ya sehemu ya makanisa ya kwanza. * Vitabu vya agano jipya kitabu cha kwanza cha Wakorintho na kitabu cha pili cha Wakorintho ni barua zilizoandikwa na Paulo kwa wakristo walioishi Korintho. * Paulo alikutana na waamini Akila na Prisila alipokuwa Korintho. * Viongozi wengine wa mwanzo wa Korintho waliokuwa na mahusiano na Korintho ni Timotheo, Tito, Apolo na Sila.
## Kornelio ### Ufafanuzi Kornerio alikuwa mtu wa Mataifa, asiye Myahudi afisa wa jeshi la Rumi. * Aliomba mara kwa mara kwa Mungu na alikuwa akiwasaidia masikini. * Kornelio na familia yake waliposikia kuwa mtume Petro anafafanua injili walikuja kuwa wanaomwamini Yesu. * Watu wa nyumba ya Kornelio walikuwa watu wa kwanza wasio Wayahudi kumwamini Yesu. * Hii iliwaonesha wafuasi wa Yesu kuwa alikuja kuwaokoa watu wote wakiwemo na wamataifa.
## Krene ### Ufafanuzi Krene ulikuwa mji wa Kigiriki kaskazini mwa pwani ya Afrika kwa upande wa bahari ya Mediteraniani, moja kwa moja kusini mwa kisiwa cha Krene. * Katika agano jipya Wayahudi na Wakristo waliishi Krene. * Krene yaweza kuwa maarudu sana kwenye Biblia kama mji wa mtu aliyeitwa Simoni aliyebeba msalaba wa Yesu.
## Krete, Mkrete ### Ufafanuzi Krete ni kisiwa kilichokuwepo kusini mwa fukwe ya Ugiriki. Mkrene ni mtu aliyeishi katika kisiwa hicho. * Mtume Paulo alisafiri katika kisiwa cha Krene akiwa katika safari zake za Kimishenari. * Paulo alimuacha mfanyakazi mwenzake Toto huko Krene ili kuwafundisha Wakristo na kuwasaidia kuchagua viongozi huko.
## Kushi ### Ufafanuzi Kushi lilikuwa jina la mtoto mkubwa na Nuhu, Hamu. Pia alikuwa babu wa Nimrodi. Kaka zake wawili waliitwa Misri na Kanaani. * Katika agano la kale Kushi lilikuwa jina la mkoa mkubwa katika nchi ya kusini kwa Israeli. * Mkoa wa zamani wa Kushi ulikuwa ardhi ya nchi iliyokuwa na sehemu za nchi kama Sudani, Misri, Ethiopia na Saudi Arabia. * Mtu mwingine aliyeitwa Kushi ametajwa katika Zaburi. Alikuwa Mbenyamini.
## Labani ### Ufafanuzi Katika Agano la Kale, Labani alikuwa mjomba na baba mkwe wa Yakobo. Yakobo aliishi na nyumba ya Labani Padan-aramu na kuchunga kondoo na mbuzi wake kama sharti la ndoa kwa binti wa Labani. Pendeleo la Yakobo kwa mabinti wa Labani lilikuwa Raheli kuwa mke wake. Labani alimdanganya Yakobo na kumfanya kumuoa binti yake mkubwa Lea kabla ya kumpa Raheli kama mke wa pili.
## Lameki ### Ufafanuzi Lameki lilikuwa jina la wanaume wawili waliotajwa katika kitabu cha Mwanzo. Lameki wa kwanza aliyetajwa alikuwa uzao wa Kaini. Alijivunia kwa wake zake wawili kuwa alimuua mtu kwa kumuumiza. Lameki wa pili alikuwa uzao wa Sethi. Alikuwa pia baba wa Nuhu.
## Lazaro ### Ufafanuzi Lazaro na dada zake, Mariamu na Martha, walikuwa marafika wa karibu wa Yesu. Mara nyingi alikaa nao katika nyumba yao Bethania. Lazaro anajulikana zaidi kwa kufufuliwa na Yesu kutoka wafu baada ya kuzikwa kaburini kwa siku kadhaa. Viongozi wa Kiyahudi walikasirika na kuwa na wivu kuwa Yesu alifanya muijiza huu na wakatafuta njia ya kumua Yesu na Lazaro. Yesu pia alitoa fumbo kuhusu maskini ombaomba na mtu tajiri ambapo ombaomba aliitwa "Lazaro."
## Lea ### Ufafanuzi Lea alikuwa mmoja wa wake wa Yakobo. Alikuwa mama wa wana kumi wa Yakobo ambao uzao wao ni miongoni wa makabila kumi na mbili ya Israeli. Baba wa Lea alikuwa Labani, aliyekuwa kaka wa mama yake Yakobo, Rebeka. Yakobo hakumpenda Lea kama alivyompenda mke wake mwingine Raheli, lakini Mungu alimbariki kwa wingi Lea kwa kumpa watoto wengi. Mmoja wa wana wa Lea, Yuda, alikuwa babu wa mfalme Daudi na Yesu.
## Lebanoni ### Ufafanuzi Labanoni ni sehemu nzuri yenye milima iliyopo mwambao wa Bahari Kuu, kaskazini mwa Israeli. Katika nyakati za Biblia, eneo hili lilikuwa limejaa misonobari, kama seda na mvinje. Mfalme Sulemani alituma wafanyakazi Lebanoni kuvuna miti ya seda kwa ajili ya kujengea hekalu la Mungu. Lebanoni ya zamani waliishi watu wa Fonikia ambao walikuwa wajenzi wenye ujuzi wa meli zilizotumika kwa viwanda vya biashara vizuri. Miji ya Tiro na Sidoni ilikuwa Lebanoni. Ilikuwa katika miji hii ambamo rangi ya zambarau ilitumika kwanza.
## Lewiathani ### Ufafanuzi Neno "Lewiathani" linamaanisha mnyama mkubwa sana aliyekuwepo zamani katika maandishi ya kwanza ya Agano la Kale, katika vitabu vya Ayubu, Zaburi na Isaya. Lewiathani anaelezwa kuwa kama joka, mwenye nguvu na mkali na mwenye uwezo wa kufanya maji yaliyomzunguka "kuchemka." Maelezo yake yanakaribiana na yale ya wanyama wakubwa sana waliokuwepo zamani. Nabii Isaya anaelezea Lewiathani kama "joka wa kutereza". Ayubu anaandika kama mtu mwenye ujuzi mzuri wa Lewiathani, kwa hiyo inawezekana kuwa huyu mnyama alikuwepo wakati wa uhai wake.
## Listra ### Ufafanuzi Listra ni jina mji katika Asia ndogo ambao Paulo alitembelea katika moja ya safari zake za kimisionari. Ilikuwa katika eneo la Likaonia ambapo sasa ni nchi ya Uturuki ya leo. Paulo na wenzake walitoroka kwenda Derbe na Listra walipotishwa na Wayahudi Ikonio. Akiwa Listra, Paulo alikutana na Timotheo aliyekuwa mwinjilisti mwenzake na mpandaji wa makanisa. Baada ya Paulo kumponya kilema Listra, watu walijaribu kuwaabudu Paulo na Barnaba kama miungu, lakini mitume waliwakemea na kuwazuia kufanya hivyo.
## Luka ### Ufafanuzi Luka alikuwa mwandishi wa vitabu viwili vya Agano Jipya: injili ya Luka na kitabu cha Matendo ya Mitume. Katika barua yake kwa Wakolosai,Paulo alimtaja Luka kama daktari. Paulo anamtaja Luka kwenye barua zake mbili. Inadhaniwa kuwa Luka alikuwa Mgiriki na Myunani kabla hajamjua Kristo. Katika injili yake, Luka anajumuisha matukio yanayoonesha upendo wa Yesu kwa watu wote, Wayahudi na Wayunani. Luka alifuatana na Paulo katika safari mbili za kimisionari na kumsaidia na kazi zake, Katika maandiko kadhaa ya awali ya kanisa, inasemekana kuwa Luka alizaliwa katika mji wa Antiokia ndani ya Shamu.
## Lutu ### Ufafanuzi Lutu lilikuwa jina la mpwa wa Abrahamu. Alikuwa mwana wa ndugu yake Abrahamu, Harani. Lutu alisafiri na Abrahamu kwenda nchi ya Kanaani na kuishi katika mji wa Sodoma Lutu alikuwa babu wa Wamoabi na Waamoni. Wafalme maadui walipovamia Sodoma na kumteka Lutu, Abrahamu alikuja na mamia kadha ya wanaume kumuokoa Lutu na kurudisha mali zake. Watu walioishi katika mji wa Sodoma walikuwa watu waovu sana kwa hiyo Mungu aliuangamiza mji huo. Lakini kwanza alimwambia Lutu na familia ya kuuondoka mji ili watoroke.
## Maaka ### Ufafanuzi Maaka alikuwa mmoja wa wana wa kaka yake Ibrahimu Nahori. Watu wengine katika Agano la kale walikuwa na jina hili. * Mji wa Maaka au Bethi Maaka ulikuwa upande wa mbali wa kaskazini mwa Israeli, eneo lililo tawaliwa na kabila la Naftali. * Ulikuwa mji muhimu na ulishambuliwa na maadui mara kadhaa. * Maaka lilikuwa jina la baadhi ya wanawake, akiwepo mama yake na mwana wa Daudi Absalomu. * Mfalme Asa alimuondoa bibi yake Maaka kutoka kuwa malikia kwasababu alipenda kuabudu Ashera.
## Makedonia ### Ufafanuzi Katika Agano jipya, eneo lililo upande wa kaskazini wa Ugiriki. * Miji Muhimu ilikuwa Berea, Filipi, na Thesalonika. * Katika maono, Mungu alimwambia Paulo kuhubiri injili kwa watu wa Makedonia. * Paulo na wafanya kazi wake walienda Makedonia na kuwa fundisha watu kuhusu Yesu na kuwasaidia kukua kiimani. * Katika Biblia kuna barua ambazo Paulo aliandika kwa waaminin wa Makedonia katika miji ya Filipi na Thesalonike.
## Malaki ### Ufafanuzi Malaki alikuwa mmoja wa manabii wa Mungu kwa ufalme wa Yuda. Aliishi katika ya miaka 500 kabla Kristo kuwa ulimwenguni. * Malaki alitabiri kipindi ambacho hekalu la Israeli lilikuwa likijengwa baada ya kurudi kutoka matekani ya Babiloni. * Ezra na Nehemia waliishi kipindi kimoja na Malaki. * Kitabu cha Malaki ni kitabu cha mwisho cha Agano la Kale. * Kama manabii wa Agano la Kale, Malaki alisisitiza watu kutubu dhambi zao na kumrudia kumuabudu Yahweh.
## Manase ### Ufafanuzi Hawa walikuw wanaume watano kwa jina Manase katika Agano la Kale: * Manase lilikuwa jina la mzaliwa wa kwanza wa Yusufu. * Manase na mdogo wake Efraimu walichukuliwa na baba Yusufu, Yakobo walipe nafasi ya kuwa miongoni mwa makabila kumi na mbili ya Israeli. * Uzao wa Manase uliunda kabila moja la Israeli. * Kabila la Manase lilikuwa mara nyingi la itwa "kabila nusu la Manase" kwasababu nusu tu ya kabila ili ishi Kanani, kwa upande wa magharibi wa Mto Yordani. Sehemu nyingine ili ishi upande wa mashariki wa Yordani. * Mmoja wa wafalme wa Yuda aliitwa pia Manase. * Mfalme Manase alikuwa muovu aliye toa dhabihu za watoto wake kama sadaka za kuteketeza kwa miungu ya uongo. * Mungu alimuadhibu Mfalme Manase kwa kuruhusu akamatwe na jeshi la adui. Manase alimgeukia Mungu na kuharibu madhabahu sanamu zilipo kuwa zikiabudiwa. * Wanaume wawili waliyo itwa Manase waliishi kipindi cha Ezra. Hawa wanaume walitakiwa kuwapa talaka wake zao wa kipagani, waliyo washawishi kuabudu miungu ya uongo. * Manase mwingine alikuwa babu wa Wadani waliyo kuwa makuhani wa miungu ya uongo.
## Mariamu (dada wa Martha) ### Ufafanuzi Mariamu alikuwa mwanamke kutoka Bethania aliye mfuata Yesu. * Mariamu alikuwa na dada jina la Martha na kaka jina Lazaro aliye mfuata Yesu. * Siku moja Yesu alisema kwamba Mariamu alichagua kilicho bora alipo chagua kumsikiliza akifundisha kuliko kuwa na wasiwasi kuhusu kuandaa chakula kama Mariamu alivyo kuwa. * Yesu alimleta kaka yake Lazaro na kumpa uzima. * Baada ya hapo, Yesu alipo kuwa anakula nyumbani kwa mtu Bethania, Mariamu alimmiminia mafuta ya gharama miguuni ili kumuabudu. * Yesu alimsifu kwa kufanya hili na kusema anaanda mwili wake kwa kuzikwa.
## Mariamu Magdalena ### Ufafanuzi Mariamu Magdalena alikuwa miongoni mwa wanawake waliyo muamini Yesu na kumfuata katika huduma yake. Alijulikana kama kama Yesu aliye mponya kutoka kwa mapepo saba waliyo mtawala. * Mariamu Magdalena na wanawake wengine walimsaidia Yesu na mitume kwa kutoa kwa. * Pia anatajwa kama mmoja wa wanawake waliyo muona Yesu alipoo fufuka.
## Mariamu, mama yake Yesu ### Ufafanuzi Mariamu alikuwa mwanamke mdogo aliye ishi katika mji wa Nazarethi aliye poswa kuolewa na Yusufu. Mungu alimchagua Mariamu kuwa mama wa Yesu Mesia, Mwana wa Mungu. * Roho Mtakatifu kimiujiza alisababisha Mariamu kuwa na mimba wakati akiwa bikra * Malaika alimwambia Mariamu kuwa mtoto atakaye zaliwa ni Mwana wa Mungu na kuwa amwite Yesu. * Mariamu alimpenda Mungu na akamsifu kwa kuwa na neema kwake. * Yusufu alimuoa Mariamu , lakini alibaki bikra mpaka mtoto kuzaliwa. * Mariamu alidhani kwa undani kuhusu vitu vya ajabu wachungaji na mamajusi alivyo visema kuhusu Yesu. * Mariamu na Yusufu walimchukuwa mtoto Yesu kuwekwa wakfu hekaluni. Baadae wakamchukuwa Misri kutoroka njama ya Farao kuuwa watoto. Hatimae wakarudi Nazarethi.
## Martha ### Ufafanuzi Martha alikuwa mwanamke kutoka Bethania alimfuta Yesu. * Martha alikuwa na dada aliye itwa Mariamu na kaka jina la Lazaro, aliye mfuata Yesu. * Wakati mmoja Yesu alikwenda watembelea nyumbani, Martha alisumbuliwa na maandalizi ya chakula wakati dada yake Mariamu kaketi na kumsikiliza Yesu akifundisha * Lazaro alipo kufa, Martha alimwambia Yesu kuwa ana amini Yesu ni Kristo, mwana wa Mungu.
## Mathayo, Lawi ### Ufafanuzi Mathayo alikuwa mmoja wa wanaume kumi na mbili Yesu aliyo wachagua kuwa mitume wake. Alijulikana kama pia kama Lawi, mwana wa Alfayo. * Lawi (Mathayo) alikuwa mtoza ushuru kutoka Kapernaumu kabla kukutana na Yesu. * Mathayo aliandika injili iliyo beba jina lake. * Kuna wanaume wengine kadhaa waitwao Lawi kwenye Bibli.
## Mede, Media ### Ufafanuzi Media ulikuwa mji wa zamani uliyo kuwa mashariki mwa Asiria na Babilonia, na kaskazini mwa Elamu na Persia. Watu waliyo ishi katika utawala wa Media walitwa "Wamede." * Utawala wa Media ulikuwa maeneo yote ya Uturuki, Irani, Syria, Iraq na Afghanistani. * Wamede walikuwa karibu na Waajemi na tawala hizi mbili ziliungana kuwashinda Wababilonia. * Babilonia ilivamiwa na Darius Mmede kipindi cha nabii Danieli kuishi huko.
## Melkizedeki ### Ufafanuzi Kipindi cha Abramu akiishi, Melkizedeki alikuwa mfalme wa mji wa Salemu (baadae, "Yerusalelmu") * Jina la Melkizedeki lina maana ya, "mfalme wa haki" na cheo chake "mfalme wa Salemu" ina maana ya, "mfalme wa amani" * Pia aliitwa "kuhani wa Mungu wa Juu Sana" * Melkizedeki anatajwa katika Biblia alipo mtumikia Abramu kwa mkate na mvinyo baada ya Abramu kumuokoa binamu yake Lutu kutoka kwa wafalme wenye nguvu. Abramu alimpa Melkizedeki moja ya kumi ya mali alizo chukuwa kwenye pambano. * Katika Agano la Kale, Melkizedeki anaelezwa kama mtu asiye na baba na mama. Aliitwa kuhani na mfalme atakaye tawala milele.
## Memfisi ### Ufafanuzi Memfisi ilikuwa mji mkuu wa Misri wa zamani, pembeni mwa Mto Nile. * Memfisi ili kuwa upande wa chini mwa Misri, kusini mwa Mto Nile, ambapo udogo ulikuwa wenye rotuba na mazao mengi. * Ardhi yake ya rotuba na eneo lake muhimu katika ya Misri ya Juu na ya Chini ili sababisha Memfisi kuwa mji mkuu wa biashara.
## Mesheki ### Ufafanuzi Mesheki ni jina la wanaume wawili katika Agano la Kale. * Mesheki mmoja alikuwa mwana wa Yafeti. * Mwingine alikuwa mjukuu wa Shemu. * Mesheki pia lilikuwa jina la eneo la nchi, ambalo labda lilipewa jina baada ya hawa wanaume. * Eneo la Mesheki liliweza kuwa upande wa kule ambapo sasa ni nchi ya Uturuki.
## Mesopotamia, Aramu Naharaimu ### Ufafanuzi Mesopotamia ni sehemu ya nchi katika ya Tigrisi na Mto Frati. Sasa ipo katika nchi inayo julikana kama Iraqi. * Katika Agano la Kale, hili eneo liliitwa "Aramu Naharaimu." * Neno "Mesopotamia" lina maana "katika ya mito." Maneno "Aramu Naharaimu" yana maana "Aramu ya mito miwili" * Ibrahimu aliishi katika miji ya Mesopotamia Uri na Harani kabla ya kuamia nchi ya Kanani. * Babiloni ilikuwa mji mwingine muhimu katika Mesopotamia. * Eneo linalo itwa "Kaldea" ili kuwa sehemu ya Mesopotamia.
## Mgirgashi ### Ufafanuzi Wagirgashi walikuwa kundi la watu wanaoishi karibu na Bahari ya Galilaya katika nchi ya Kaanani. Walikuwa uzao wa mwana wa Hamu Kaanani na kwa hiyo walikuwa moja wa kundi la watu wengi ambao pia walijulikana kama "Wakaanani". Mungu aliahidi Waisraeli ya kwamba angewasaidia kuwashinda Wagirgashi na makundi mengine ya Wakaanani. Kama watu wote wa Kaanani, Wagirgashi waliabudu miungu ya uongo na kufanya mambo maouvu kama sehemu ya ibaaa hiyo.
## Mgiriki, Kigiriki ### Ufafanuzi Msemo "Mgiriki" una maana ya lugha inayozungumzwa katika nchi ya Giriki. Giriki pia ilizungumziwa kote katika Ufalme wa Kirumi. Msemo "Kigiriki" una maana ya "kuzungumza Kigiriki". Kwa kuwa watu wasiokuwa Wayahudi katika Ufalme wa Kirumi walizungumza Kigiriki, Watu wa mataifa mara kwa mara humaanisha "Wagiriki" katika Agano Jipya, haswa inapolinganishwa na Wayahudi. Msemo "Wayahudi wa Kigiriki" walikuwa wakimaanisha Wayahudi ambao walizungumza Kigiriki kulinganisha na "Wayahudi wa Kiebrania" ambao walizungumza Kiebrania pekee, au labda Kiaramea. Njia zingine za kutafsiri "Kigiriki" zinaweza kujumuisha "kuzungumza Kigiriki" au "Kigiriki cha kitamaduni" au "Kigiriki". Pale inapomaanisha wasio Wayahudi, "Giriki" inaweza kutafsiriwa kama "watu wa mataifa"
## Mhiti ### Ufafanuzi Wahiti walikuwa ni uzao wa Hamu kupitia kwa mtoto wake Kanaani. Walifanyika kuwa dola kubwa katika eneo ambalo kwa sasa linaitwa Uturuki na Kaskazini mwa Palestina. Ibrahimu alinunua sehemu ya ardhi kutoka kwa Efroni, Mhiti ili aweze kumzika Sara katika pango huko. Hatimaye, Ibrahimu na wazao wake kadhaa walizikwa katika pango hilo pia. Wazazi wa Esau walihuzunika sana baada ya Esau kuoa wanawake Wahiti. Mmoja kati ya watu wa Daudi aliyekuwa na nguvu aliitwa Uria Mhiti. Miongoni mwa wanawake aliowaoa Sulemani walikuwa ni Wahiti. Wanawake hawa wa kigeni waliugeuza moyo wa Sulemani kutoka kwa Mungu kwasababu ya miungu waliyoiabudu. Wahiti walikuwa mara zote ni hofu kwa waisraeli, kimwili na kiroho pia.
## Mhivi ### Ufafanuzi Wahivi walikuwa ni moja kati ya makundi saba ya watu walioishi katika nchi ya Kanaani. Kama ilivyokuwa kwa makundi yote, Wahivi walikuwa ni uzao wa Kanaani, aliyekuwa ni mjukuu wa Nuhu. Shekemu mhivi alimbaka Dina, binti wa Yakobo na kaka zake na Dina walilipiza kisasi kwa kuwauwa Wahivi wengi. Katika kipindi ambacho Yoshua aliwaongoza waisraeli kuiteka nchi ya Kanaani, Waisraeli walidanganywa na kufunga mkataba na Wahivi badala ya kuwaangamiza.
## Midiani, Wamidiani ### Ufafanuzi Midiani alikuwa mwana wa Ibrahimu na mkewe Ketura. Pia ni jina la kundi la watu na eneo upande wa kaskazini mwa Jangwa la Kiarabu sehemu ya kusini mwa nchi ya Kanani. Kundi la watu liliitwa "Wamidiani." * Musa alipo ondoka Misri, alienda eneo la Midiani alipo kutana na binti wa Yethro na kuwasaidia kunyeshwa maji mifugo yao. Baadae Musa alimuoa mmoja wa binti wa Yethro. * Yusufu alichukuliwa Misri na kundi la wanfanya biashara ya watumwa Wamidiani. * Miaka mingi baadae Wamidiani alishambulia na kuvamia Waisraeli katika nchi ya Kanani. Gidioni aliongoza Waisraeli katika ushindi wao. * Waarabu wengi wa leo ni wa kabila la uzao wa hili kundi.
## Mika ### Ufafanuzi Mika alikuwa nabii wa Yuda katika ya miaka 700 kabla ya Yesu, wakati nabii Isaya alipo kuwa ana hudumu Yuda. Mwanaume mwingine aliye itwa Mika aliishi kipindi cha waamuzi. * Kitabu cha Mika ni karibu na mwisho wa Agano la Kale. * Mika alitabiri uharibifu wa Samaria kwa Waasiria. * Mika aliwakemea watu wa Yuda kwa kuto mtii Mungu na kuwaonya kuwa maadui wao watawashambulia. * Unabii unaisha na ujumbe wa matumaini kwa Mungu, aliye mwaminifu na kuokoa watu wake. * Katika kitabu cha waamuzi, adithi ya mtu aitwaye Mika anaye ishi Efraimu aliye tengeneza sanamu kwa fedha ya simuliwa. Kijana wa kikuhani aliye kuja kuishi naye akiiba sanamu huyo na vitu vingine, na kuondoka na kundi la Wadani. Hatimaye Wadani na kuhani huyo wakaishi mji wa Laishi na wakaweka sanamu huyo huyo wa kumuabudu.
## Mikaeli ### Ufafanuzi Mikaeli ni mkuu wa malaika wa tiiifu na watakatifu. Yeye ni malaika pekee anaye tajwa kama "malaika mkuu" wa Mungu. * Neno "malaika mkuu" lina maana "malaika kiongozi." * Mikaeli ni shujaa anaye pigana dhidi maadui wa Mungu na kulinda watu wa Mungu. * Aliongoza Waisraeli kupigana dhidi ya jeshi la Wajemii. Katika siku za mwisho ataongoza jeshi la Israeli katika pambano la mwisho dhidi ya majeshi maovu, kama alivyo tabiri Danieli. * Pia kuna baadhi ya wanaume katika Biblia wenye jina Mikaeli. Baadhi ya wanaume wana tajwa kama "wana wa Mikaeli"
## Miriamu ### Ufafanuzi Alipo kuwa mdogo, Miriamu aliongozwa na mama yake kumlinda mdogo wake Musa aliye kuwa katika kikapu miongoni mwa Mto Nile. * Miriamu aliwaongoza Waisraeli katika kucheza kwa furaha na shukurani baada ya kutoroka kwa Wamisri kwa kuvuka Bahari ya Shamu. * Miaka mingi baadae Waisraeli walipo kuwa wana tanga jangwani, Miriamu na Aruni walianza kunena vibaya kuhusu Musa kwasababu alimuoa mwanamke wa Kikushi. * Kwasababu ya uasi wake wakuongea viabya dhidi ya Musa, Mungu alimsababishi ukoma. Lakini baadae Mungu alimponya Musa alipo muombea.
## Misri, Mmisri ### Ufafanuzi Misri ni nchi katika sehemu ya kaskazini ya Afrika, kusini mashariki mwa nchi ya Kaanani. Mmisri ni mtu ambaye anatoka katika nchi ya Misri. Katika miaka ya zamani, Misri ilikuwa nchi yenye nguvu na utajiri. Misri ya zamani iligawanyika katika sehemu mbili, Misri ya Chini (sehemu ya kaskazini ambapo mto hutiririka chini kuelekea baharini) na Misri ya Juu (sehemu ya kusini). Katika Agano la Kale, sehemu hizi zinajulikana kama "Misri" na "Pathrosi" katika lugha ya maandishi asili. Wakati mwingine ambapo kuna chakula kichache Kaanani, wakuu wa koo walisafiri kwenda Misri kununua chakula kwa ajili ya familia zao. Kwa miaka mia moja hivi, Waisraeli walikuwa watumwa Misri. Yusufu na Mariamu walishuka chini Misri na mtoto mdogo Yesu kutoroka kwa Herode Mkuu.
## Mizpa ### Ufafanuzi Mizpa ni jina la baadhi ya miji inayo tajwa katika Agano la Kale. Ina maana, "mnara wa doria" * Daudi alipo kuwa anakimbizwa na Sauli, aliwaacha wazazi wake Mizpa, chini ya ulinzi wa mfalme Moabu. * Mji moja unaoitwa Mizpa ulikuwa mpakani katika ya falme za Yuda na Israeli. Ilikuwa sehemu kubwa ya kijeshi.
## Mji wa Babeli ### Ufafanuzi Mji wa Babeli ulikuwa makao makuu wa jimbo la Babeli ya kale, ambao pia ulikuwa sehemu ya Himaya ya Babeli. * Babeli ulikuwa kandokando ya Mto Frati, katika eneo ambalo mnara wa Bebeli ulikuwa umejengwa mamia ya miaka iliyokuwa imepeita. * Wakati mwingine jina "Babeli" linarejerea Himaya yote ya Babeli. Kwa mfano, "mfalme wa Babeli alitawala himaya yote ya Babeli, siyo mji tu. * Watu wa Babeli walikuwa wenye nguvu walioishambuli Yuda na kuwapeleka watu katika uhamisho huko Babeli kwa miaka 70. * Sehemu yake iliitwa "Ukalidayo" na watu walioishi pale waliitwa "Wakalidayo." Matokeo yake neno "Ukalidayo mara kwa mara lilitumika kurejerea Babeli. * Katika Agano Jipya, neno "Babeli" wakati mwingine linatumika kama sitiari kurejerea maeneo, watu, na vitu vya kufikirika viusianishwavyo na ibada ya sanamu na tabia nyingine za dhambi. * Kirai "Babeli Mkuu" au "Babeli mji mkuu" kisitiari inarejerea kwa mji au taifa kubwa, tajiri, na lenye dhambi, kama ulivyokuwa mji wa kale wa Babeli.
## Mji wa Bethani ### Ufafanuzi Mji wa Bethani ulikuwa katika bonde la mteremko wa Mlima wa Mizeituni, kama maili mbili mashariki ya Yerusalemu, * Bethani ulikuwa karibu na njia iliyokwenda kati ya Yerusalemu na Yeriko. * Yesu alitembelea Bethani mara kwa mara walipokuwa wakiishi Lazaro, Matha na Mariamu, rafiki zake wa karibu. * Bethani unajulikana maalumu kama sehemu Yesu alipomfufua Lazaro kutoka kwa wafu.
## Mji wa Daudi ### Ufafanuzi Mji wa Daudi ni jina la Yerusalemu na Bethlehemu. * Yerusalemu ni mahali ambapo Daudi aliishi alipotawala Israeli. * Bethlehemu ni mahali ambapo Daudi alizaliwa.
## Mlawi, Lawi ### Ufafanuzi Lawi alikuwa mmoja wa wana kumi na mbili wa Yakobo, au Israeli. Neno "Mlawi" inamaanisha mtu aliyemmoja wa kabila la Israeli ambalo babu yao alikuwa Lawi. Walawi walihusika na kulitunza hekalu na kuendesha taratibu za kidini, zikiwemo kutoa sadaka na maombi. Makuhani wote wa Kiyahudi walikuwa Walawi, wazawa wa Lawi na sehemu ya kabila la Lawi. (Ingawa Walawi wote hakuwa makuhani.) Makuhani wa Kilawi walitengwa na kuwekwa wakfu kwa kazi maalum ya kumtumikia Mungu hekaluni. Wanaume wengine wawili wenye jina "Lawi" walikuwa mababu wa Yesu na majina yao yako kwenye ukoo katika injili ya Luka. Mwanafuzi wa Yesu, Mathayo, pia aliitwa Lawi.
## Mlima Hermoni ### Ufafanuzi Mlima Hermoni ni jina la mlima mrefu wa Israeli chini ya Lebanoni. * Upo kaskazini mwa Bahari ya Galilaya, kaskazini mwa mpaka wa Israeli na Syria. * Majina mengine yaliyo pewa Mlima Hermoni na watu wengine ni "Mlima Sirioni" * Mlima Hermoni una vilele vitatu. Kikubwa ni karibu mita 2,800 kwenda juu.
## Mlima wa Mizeituni ### Ufafanuzi Mlima wa Mizeituni ni mlima au kilima kikubwa karibu na mashariki mwa mji wa Yerusalemu. Una mita787 kwenda juu. * Katika Agano la Kale, huu mlima unatajwa kama "mlima mashariki mwa Yerusalemu." * Nakala za Agano Jipya zataja maeneo ambayo Yesu na wanafunzi wake walienda Mlima wa Mizeituni kuomba na kupumzika. * Yesu alikamatwa Bustani ya Gethsemane, uliyo upande wa Mlima wa Mizeituni.
## Moabu, Mmoabu ### Ufafanuzi Moabu alikuwa mwana wa kwanza wa binti wa Lutu. Pia likawa jina la nchi ambapo yeye na familia yake waliishi. Neno "Moabu" la husu mtu wa uzao wa Moabu au anaishi katika nchi ya Moabu. * Nchi ya Moabu ilikuwa mashariki mwa Bahari ya chumvi. * Moabu ilikuwa kusini mashariki kutoka mji wa Bethelehemu ambapo Naomi na familia yake waliishi. * Watu wa Bethelehemu wallimuita Ruthi "Mwanamke Mmoabu" kwasababu alikuwa mwanamke wa nchi ya Moabu.
## Modekai ### Ufafanuzi Modekai alikuwa mwanaume wa Kiyahudi katika nchi ya Jemi. Alikuwa mlinzi wa binamu wake Esta, ambaye baadae alikuwa mke wa mfalme wa Kijemi, Ahasuerusi * Wakati akifanya kazi hikulu, Modekai alisikia watu wakipanga njama kumuua mfalme Ahasuerusi. Alitoa taarifa na maisha ya mfalme yakapona. * Wakati mwengine, Modekai aligundua mbinu ya kuua Wayahudi wote katika ufalme wa Kijemi. Alimshauri Esta kumuomba mfalme kuokoa watu wake.
## Moleki, Moloki ### Ufafanuzi Moleki lilkuwa jina la miungu wa uongo ambao Wakanani waliabudu. * Watu waliyo abudu Moleki alitoa dhabihu watoto wao kwake kwa moto. * Waisraeli wengine pia waliabudu Moleki badala ya Mungu wa kweli, Yahweh. Walifuata matendo maovu ya waabudu Moleki, pamoja na kutoa dhabihu watoto wao
## Mperizi ### Ufafanuzi Waperizi walikuwa watu wa kundi fulani katika nchi ya Kanaani. Ni machache yamezungumzwa juu ya kundi hili. * Waperizi wanatajwa sana katika agano la kale kitabu cha Waamuzi ambapo ilirekodiwa kuwa Waperizi walioana na Wisraeli na kuwashawishi kuabudu miungu ya uongo. * Ukoo wa Perezi ulioitwa "waperezi" lilikuwa kundi tofauti na Waperizi.
## Mshaeli ### Ufafanuzi Mishaeli ni jina la wanaume wa tatu katika Agano la Kale. * Mwanaume mmoja anaye itwa Mishaeli alikuwa binamu wa Aruni. Wana wawili wa Aruni walipo uliwa na Mungu baada ya kufukiza uvumba kwa namna ambayo haikumpendeza Mungu, Mishaeli na kaka yake walipewa jukumu la kubeba maiti nje ya kambi ya Waisraeli. * Mwanaume mwingne aitwaye Mishaeli alisimama kando ya Ezra alipo soma hadharani sheria aliyo ikuta.
## Mto Frati ### Ufafanuzi Frati ni jina la moja ya mito minne ambayo ilitiririka katika bustani ya Edeni. Ni mto ambao umetajwa sana katika Biblia. Mto wa sasa unaitwa Frati na upo eneo la Mashariki ya Kati na ni mrefu zaidi na mto muhimu zaidi Asia. Pamoja na Mto Hidekeli, Frati inapakana na eneo la nchi inayojulikana kama Mesopotamia. Mji wa zamani wa Uri ambapo Abrahamu alitoka ulikuwa mdomo wa Mto Frati. Mto huu ulikuwa moja ya mipaka ya nchi ambayo Mungu aliahidi kumpa Abrahamu (Mwanzo 15:18). Wakati mwingine Mto Frati hujulikana kama "ule Mto"
## Mto Nili, Mto wa Misri ### Ufafanuzi Nili ni mto mrefu na mpana katika kaskazini mashariki mwa Africa. Unajulikana kama mto rasmi wa Misri. * Mto Nili unapita kaskazini kupita Misri na kwenda Bahari ya Medetarenia. * Mimea ina kua kwenye nchi ya rotuba pande zote mbili za Mto Nili. * Wamisri wengi wanaishi karibu na Mto Nili maan ni muhimu kwa maji na mazao ya chakula. * Waisraeli waliishi nchi ya Gosheni iliyo kuwa na rotuba kwababu ilikuwa upande wa Mto Nile
## Mto Yordani, Yordani ### Ufafanuzi Mto Yordani ni mto unaotiririka toka kaskazini hadi kusini, na inaunda mpaka wa mashariki wa nchi iliyokuwa inaitwa Kanaani. Leo, mto Yordani unatenganisha Israeli magharibi kutoka Yordani mashariki. Mto Yordani unatiririka katikati ya Bahari ya Galilaya na kuishia katika Bahari iliyo Kufa. Wakati Yoshua anawaongoza Waisraeli kuelekea Kanaani, ilibidi wavuke mto Yordani. Kwa sababu palikuwa parefu sana, Mungu alisimamisha maji kutembea kwa miujiza ili watu wavuke. Mara nyingi Biblia katika Biblia Mto Yordani unajulikana ka "Yordani."
## mtu wa Mungu ### Ufafanuzi Msemo "mtu wa Mungu" ni heshima ya kutaja nabii wa Yahweh. Pia utumika kuhusu malaika wa Yahweh. * Unapo taja nabii, hii yaweza pia tafsiriwa kama " mtu aliye wa Mungu" au "mwanaume Mungu aliye mchagua" au "mwanaume anaye mtumikia Mungu"
## Musa ### Ufafanuzi Musa alikuwa nabii na kiongozi wa watu wa Israeli kwa miaka 40. * Musa alipo kuwa mtoto, wazazi wa Musa walimueka kwenye kikapu Mto Nile kumficha na Farao wa Misri. Dada wa Miriamu alimwangalia hapo. Maisha ya Musa yalinusurika binti wa Farao alipo mkuta na kumchukuwa kama mwanae. * Mungu alimchagau Musa kuwa toa Waisraeli utumwani Misri na kuwaongoza Nchi ya Ahadi. * Baada ya Waisraeli kutoka Misri na walipo kuwa jangwani wakitanga, Mungu alipa Musa mawe mawili ya mbao yenye Amri Kumi. * Mwisho wa maisha yake, Musa aliona Nchi ya Ahadi, lakini hakuishi sababu hakumtii Mungu.
## Muumbaji ### Ufafanuzi Kwa ujmla, "muumbaji" ni mtu anaye tengeneza au kufanya vitu. * Katika Biblia, neno "Muumbaji" mara nyingine linatumika kama jina au cheo cha Yahweh, kwasababu ameumba kila kitu. * Mara kwa mara hili neno lina ambatana na "wake" au "wangu" au "wako"
## Mwamori ### Ufafanuzi Waamori walikuwa watu wenye nguvu sana ambao ni uzao wa mjukuu wa Nuhu Kanani. * Jina lao lilikuwa na maana ya "aliye juu" ambalo lilimaanisha miji ya milima ambapo walikuwa wakiishi au kwa sababu walijulikana kuwa ni watu warefu kwa kimo. * Waamori waliishi katika majimbo yote yaliyokuwa kandokando ya mto Yordani. Mji wa Ai ulikaliwa na Waamori. * Mungu alisema "dhambi za waamori" akiwa anajumuisha waliabudu miungu ya uongo na walitenda dhambi. * Yoshua aliwaongoza Waisraeli kuwaangamiza Waamori kama ambavyo Mungu alimuamuru afanye.
## Myebusi, Yebusi ### Ufafanuzi Wayebusi walikuwa kundi la watu walioishi nchi ya Kanaani. Walikuwa uzao wa mwana wa Hamu, Kanaani. Wayebusi waliishi katika mji wa Yebusi, ambalo jina lake lilibadilishwa baadaye kuwa Yerusalemu mfalme Daudi alipoutawala. Melkizedeki, mfalme wa Salemu, inawezekana alikuwa Myebusi kwa asili.
## Naamani ### Ufafanuzi Katika Agano la Kale, Naamani alikuwa mkuu wa jeshi wa mfalme Aramu. * Naamani alikuwa na ungonjwa mbaya wa ngozi uitwao ukoma usiyo tibika. * Myahudi mtumwa katika nyumba ya Naamani alimwambia aende kwa nabii Elisha apone. * Elisha alimwambia Naamani ajisafishe mara saba katika Mto Yordani. Naamani alipo tii, Mungu akamponya ugonjwa wake. * Baada ya matokeo, Naamani alikuja kuamini kuwa Mungu ndiye wa kweli, Yahweh. * Wanaume wengine wawili waliitwa Naamani walikuwa uzao wa mjukuu wa Yakobo Benjamini.
## Naftali ### Ufafanuzi Naftali alikuwa mwana wa sita wa Yakobo. Uzao wake uliunda kabila la Naftali, ambalo lilikuwa moja ya kabila la Israeli. * Wakati mwingine jina Nafatali linatumika kueleza nchi kabila lipo ishi. * Nchi ya Naftali ilikuwa upande wa kaskazini mwa Israeli, karibu na kabila la Dani na Asheri. Pia lilikuwa mpaka wa magharibi wa Bahari ya Chinerethi. * Hili ni kabila lilotajwa katika Agano la Kale na Jipya katika Biblia.
## Nahori ### Ufafanuzi Nahori lilikuwa jina la ndugu wawili wa Ibrahimu: babu yake na kaka. * Kaka yake Ibrahimu Nahori alikuwa babu wa mke wa Isaka Rebeka. * Maneno "mji wa Nahori" ulimaanisha, "mji uliyo itwa Nahori" au "mji ambao Nahori aliishi" au " Mji wa Nahori"
## Nahumu ### Ufafanuzi Nahumu alikuwa nabii aliye ubiri kipindi ambacho mfalme mouvu Manase alitawala Yuda. * Nahumu alitoka mji wa Elkoshi, maili 20 kutoka Yerusalemu. * Agano la Kale kitabu cha Nahumu kimeandika unabii wake kuhusu uharibifu wa mji wa Ninewi.
## Nathani ### Ufafanuzi Nathani alikuwa nabii mwaminifu wa Mungu aliye ishi kipindi cha Daudi akiwa mfalme wa Israeli. * Mungu alimtuma Nathani kumuona Daudi alipo tenda dhambi dhidi ya Uria. * Nathani alimkemea Daudi, japo kuwa Daudi alikuwa mfalme. * Daudi alitubu dhambi yake baada ya Nathani kumfuata.
## Nazarethi, Nazarini ### Ufafanuzi Nazarethi ni mji katika mji wa Galilaya kusini mwa Israeli. Ilikuwa kama kilomita 100 kaskazini mwa Yerusalemu, iliyo chukuwa kam siku tatu hadi tano kufika kwa miguu. * Yusufu na Maria walitoka Nazarethi, na hapo ndipo walipo mlelea Yesu. * Ndio maana Yesu alijulikana kama "Mnazarini" * Wayahudi wengi wanao ishi Nazarethi hawaku muheshimu Yesu na mafundisho yake, kwasababu alikulia miongoni mwao na wakadhani alikuwa mtu tu wa kawaida. * Wakati Yesu alipo kuwa anafundisha sinagogi la Nazarethi, Wayahudi walijaribu kumuua kwasababu alidai kuwa Mesia na akawakemea kwa kumkataa.
## Nebukadneza ### Ufafanuzi Nebukadneza alikuwa mfalme wa Utawala wa Babiloni ambaye jeshi lake kuu liliwashinda makundi ya watu na mataifa. * Chini ya uongozi wa Nebukadneza, jeshi la Wababiloni walishambulia na kuishinda Yuda, na kuchukuwa watu wa Yuda kwenda Babiloni. Hii ndio "Mateka ya Babiloni" kwa miaka 70. * Mmoja wa mateka, Danieli, alitafsiri ndoto ambazo Nebukadneza alikuwa nazo. * Waisraeli wengine wa tatu, Hanania, Meshaeli, na Azaria, walitupwa katika tanuru kali walipo kataa kuinama kwa sanamu kubwa Nebukadneza alilo tengeneza. * Mfalme Nebukadneza alikuwa na kiburi na kuabudu miungu ya uongo. Alipo shinda Yuda, aliiba dhahabu nyingi na fedha kutoka hekaluni Yerusalemu. * Kwasababu Nebukadneza alikuwa na kiburi na kukataa kugeuka pembeni asiabudu miungu ya uongo, Yahweh alimsababisha kuwa na uwitaji kwa miaka saba, akiishi kama mnyama. Baada ya miaka saba Mungu alimrejesha Nebukadneza alipo jinyenyekesha na kumuabudu Mungu wa kweli, Yahweh.
## Negevi ### Ufafanuzi Negevi ni jangwa kusini mwa Israeli, kusini magharibi wa Bahari ya Chumvi. * Neno halisi lina maana "Kusini." * Ina wezekana kuwa hili eneo la kusini sio eneo la leo la Jangwa la Negevi. * Ibrahimu alipo ishi nchi ya Kadeshi, alikuwa Negevi au kusini. * Isaka alikuwa anaishi Negevi Rebeka alipo safiri kukutana naye na kuwa mke wake. * Makabila ya Yuda na Simeoni yaliishi Kusini mwa eneo.
## Nehemia ### Ufafanuzi Nehemia alikuwa Muisraeli aliye ishi Babiloni wakati watu wa Israeli na Yuda walip chukuliwa mateka na Wababiloni. * Alipo kuwa mbeba kikombe wa mfalme wa Jemi, Artaxerxesi, Nehemia aliomba ruhusu kwa mfalme kurudi Yerusalemu. * Nehemia waliwaongoza Waisraeli kujenga kuta za Yerusalemu iliyo haribiwa na Wababiloni. * Kwa miaka kumi na mbili Nehemia alikuwa mkuu wa Yerusalemu kabla ya kurudi kwa nyumba ya mfalme. * Kitabu cha Agano la Kale cha Nehemia kinaeleza habari ya Nehemian kazi yake kwa kujenga kuta na kuongoza watu wa Yerusalemu.
## Ninawi, Mninwai ### Ufafanuzi Ninawi ilikuwa mji mkuu wa Asyria. Mninawi alikuwa mtu aliye ishi Ninawi. * Mungu alimtuma nabii Yona kuwaonya Waninawi kugeuka kutoka njia zao mbaya. Watu walitubu na Mungu hakuwa haribu. * Waasyria baadae waliacha kumtumikia Mungu. Walishinda ufalme wa Israeli na kubeba watu kwenda Ninawi.
## Nuhu ### Ufafanuzi Nuhu alikuwa mwanaume aliye ishi miaka 4,000 iliyo pita, kipindi ambacho Mungu alipotuma garika duniani kuharibu watu waovu. Mungu alimwambia Nuhu ajenge meli kubwa ambayo yeye na familia yake waliweza kuishi wakati mafuriko yalipo funika dunia. * Nuhu alikuwa mwenye haki aliye mtii Mungu kwa kila kitu. * Wakati Mungu alipo mwambia Nuhu kujenga meli kubwa, Nuhu alijenga kama Mungu alivyo mweleza. * Ndani ya hiyo meli, Nuhu na familia yake walihifadhiwa salama na baadae watoto wao na wajukuu wao walijaza dunia na watu tena. * Kila mtu aliye zaliwa kipindi cha garika ni mzao wa Nuhu.
## Nyumba ya Daudi. ### Ufafanuzi Maelezo 'nyumba ya Daudi' yanarejelea familia au uzao wa Mfalme Daudi. Neno 'nyumba ya Daudi' laweza kutafsiriwa kama '' uzao wa Daudi'' au ''familia ya Daudi." Yesu ni sehemu ya nyumba ya Daudi kwasababu alikuwa ni uzao wa Daudi. Wakati mwingine neno 'nyumba ya Daudi' hurejelea watu wa familia ya Daudi wale ambao wakali hai. Mara nyingine laweza kuwajumuisha wazao wa Daudi hata wale waliokwisha kufa.
## Obadia ### Ufafanuzi Obadia alikuwa nabii wa Agano la Kale aliye tabiri dhidi ya watu wa Edomu, waliyo kuwa wazao wa Esau. Pia palikuwa na wanaume wengine waliyo itwa Obadia katika Agano la Kale. * Kitabu cha Obadia ni kifupi katika Agano la Kale na kinaeleza unabii Obadia aliyo upokea kupitia maono kutoka kwa Mungu. * Sio wazi sana lini Obadia aliishi na kutabiri. Inawezekana kipindi cha utawala wa Yehoramu, Ahazia, Yoashi, na Athalia, mfalme wa Yuda. Nabii Danieli, Ezekieli, na Yeremia walikuwa wakitabiri kipindi hichi. * Obadia pia ina wezekana aliishi kipindi cha mwisho cha muda huu, wakati wa utawala wa Mfalme Zedekia na mateka ya Babiloni. * Wanaume wengine wa wenye jina Obadia ni mzao wa Sauli, Mgadi aliye kuwa mmoja wa wanaume wa Daudi; mtumishi wa hikulu wa Mfalme Ahabu; afisa wa Mfalme Yehoshafati; Mlawi aliye kuwa mlinzi wa lango kipindi cha Nehemia. * Ina weza kuwa mwandishi wa kitabu cha Obadia alikuwa mmoja wapo.
## Omri ### Ufafanuzi Omri alikuwa mkuu wajeshi aliye kuwa mfalme wa sita wa Israeli. * Mfalme Omri alitawala miaka 12 katika mji wa Tirza. * Kama wafalme wote wa Israeli kabla yake, Omri alikuwa muovu aliye ongoza watu wa Israeli kuabudu sanamu. * Omri pia alikuwa baba wa mfalme Ahabu.
## Padan-aramu ### Ufafanuzi Padan-aramu lilikuwa jina la mji ambao familia ya Abrahamu waliishi kabla ya kuhamia kwenye nchi ya Kanaani. Inamaanisha "uwazi wa Aramu." * Abrahamu alipoondoka Harani kule Padan-aramu akasafiri kwenda nchi ya Kanaani watu wengi wa familia yake walibaki Harani. * Miaka mingi baadae mtumishi wa Abrahamu alikwenda Padan-aramu kutafuta mke kwa ajili ya Isaka miongoni mwa ndugu zake na akampata Rebeka, mjukuu wa Bethueli. * Pia mtoto wa Isaka na Rebeka Yakobo alisafiri mpaka Padan-aramu na kuoa mabinti wawili wa kaka yake na Rebeka, Labani aliyekuwa akiishi Harani. Aramu, Padan-aramu na Aramu-Nahariamu zilikuwa sehemu za mji mmoja ambao kwa sasa ni zipo katika nchi ya Syria.
## Parani ### Ufafanuzi Parani ni jangwa lililopo mashariki mwa Misri na kusini mwa nchi ya Kanaani. Pia kulikuwa na mlima Parani ambalo yaweza kuwa jina lingine la mlima Sinai. * Mtumwa Hagari na mtoto wake walikwenda kuishi katika jangwa la Parani baada ya Sara kumuamuru Abrahamu amfukuze. * Musa alipowaongoza Waisraeli kutoka Misri walipitia jangwa la Parani. * Ilikuwa toka Kadesh-barnea kupitia jangwa la Parani ambalo Musa aliwatuma wapelelezi kumi na mbili kupeleleza nchi ya Kanaani na kuleta ripoti. * Jangwa la Sini lilikuwa kaskazini mwa Parani.
## Paulo, Sauli ### Ufafanuzi Paulo alikuwa kiongozo wa kanisa la kwanza aliyetumwa na Mungu kupeleka habari njema kwa makundi mengi ya watu. * Paulo alikuwa Myahudi aliyezaliwa Rumi kwenye mji wa Tarso hivyo alikuwa raia wa Rumi. * Paulo kwa jina la Kiyahudi aliitwa Sauli. * Sauli alikuwa kiongozi wa dini ya Kiyahudi na aliwafunga Wayahudi waliokuwa Wakristo kwa sababu alifikiri kuwa hawakumuheshimu Mungu kwa kumwamini Yesu. * Yesu alijidhihirisha mwenyewe kwa Sauli kwa kutumia mwanga unaopofua na kumwambia aache kuwatesa Wakristo. * Sauli alimwamini Yesu na akaanza kuwahubiria Wayahudi wenzake kuhusu Yesu. * Baadaye Mungu akamtuma Sauli kwenda kuwahubiria wasio Wayahudi kuhusu Yesu na kuanzisha makanisa katika miji na vijiji mbalimbali. Wakati huu sasa akaanza kuitwa Paulo. * Paulo pia aliandika barua ili kuwatia moyo Wakristo katika makanisa kwenye miji hiyo. Barua hizi zipo katika agano jipya.
## Peori, Mlima Peori, Baali Peori ### Ufafanuzi Peori na Mlima Peori ni mlima uliokuwepo kaskazini mwa bahari ya chunvi katika mji wa Moabu. * Beth Peori lilikuwa jina la mji uliokuwepo karibu na mlima ule. Hapa ni mahali ambapo Musa alikufa baada ya Mungu kumuonesha nchi ya ahadi. * "Baali Peori" alikuwa mungu wa uongo wa Wamoabu walioabudiwa katika mlima Peori. Waisraeli pia walianda kuabudu sanamu hii na Mungu akawaadhibu kwa hili.
## Petro, Simoni Petro, Kefa ### Ufafanuzi Petro alikuwa mmoja wa mitume wa Yesu. Alikuwa kiongozi wa muhimu katika kanisa la kwanza. * Kabla Yesu hajamuita kuwa mwanafunzi wake aliitwa Simoni. * Baadae Yesu akamuita Kefa yenye maana ya "jiwe" au "mwamba." Jina Petro pia linamaana ya "jiwe" au "mwamba" kwa lugha ya Kigiriki. * Mungu alifanya kazi kupitia Petro kwa kuwaponya watu na kuhubiri habari njema kuhusu Yesu. * Vitabu viwili vya agano jipya ni barua ambazo Petro aliandika kuwatia moyo na kuwafundisha waamini wenzake.
## Pilato ### Ufafanuzi Pilato alikuwa kiongozi wa serikali ya Rumi katika Yudea aliyumuhukumu Yesu kifo. * Kwa sababu Pilato alikuwa gavana alikuwa na mamlaka ya kuamua hukumu ya kifo kwa watu wenye hatia. * Viongozi wa dini ya Kiyahudi walimtaka Pilato amsulubishe Yesu hivyo wakadanganya na kusema Yesu alikuwa mhalifu. * Pilato aligundua kuwa Yesu hakuwa na makosa lakini aliwaogopa makutano na akataka kuwaridhisha hivyo akawaamuru askari wake wamsulubishe Yesu.
## Ponto ### Ufafanuzi Ponto ulikuwa mkoa wa Rumi katika kipindi cha himaya ya Rumi na kanisa la kwanza. ilikuwa karibu na kusini mwa pwani ya Bahari nyeusi na kaskazini ambapo sasa ni nchi ya Uturuki. * Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Matendo ya mitume watu toka mkoa wa Ponto walikuwa Yerusalemu wakati ambao Roho mtakatifu alikuja kwa mitume siku ya Pentekoste. * Akula aliyeamini alitokea Ponto. * Wakati Petro anawaandikia Wakristo waliotawanyika katika miji mbali mbali Ponto ilikuwa mmoja wa miji iliyotajwa.
## Potifa ### Ufafanuzi Potifa alikuwa kiongozi wamuhimu sana kwa Farao wa Misri katika kipindi ambacho Yusufu aliuzwa utumwani kwa Waishmaili. * Potifa alimchukua Yusufu kwa Waishamaili na akamteua kuwa msimamizi wa nyumba yake. * Yusufu aliposingiziwa kwa kutenda kosa Potifa alimuweka Yusufu gerezani.
## Prisila ### Ufafanuzi Prisila na Akula mume wake walikuwa Wakristo wa Kiyahudi waliofanya kazi na mtume Paulo katika kazi yake ya kimishenari. * Prisila na Akula waliondoka Rumi kwa sababu mtawala aliwalazimisha Wakristo kuondoka. * Paulo alikutana na Akula na Prisila Korintho. Walikuwa watengeneza mahema na Paulo akaungana nao katika kazi hiyo. * Pauli alipoondoka Korintho kwenda Syria Prisila na Akula walikwenda pamoja naye. * Toka Syria watatu hao wakaenda Efeso. Paulo alipoondoka Efeso Prisila na Akula walibaki na kuendelea kuhubiri injili.
## Rabai ### Ufafanuzi Rabai ulikuwa mji wa muhimu sana kwa watu wa Waamoni. * Katika vita dhidi ya Waamoni Waisraeli walivamia Rabai. * Mfalme Daudi wa Israeli aliiteka Rabai kama mateka yake ya mwisho. * Katika nyakati za sasa mji wa Amman Yordani ni sehemu ambayo Rabai ilikuwepo.
## Rahabu ### Ufafanuzi Rahabu alikuwa mwanamke aliyeishi Yeriko Waisraeli walipovamia mji. Alikuwa kahaba. * Rahabu aliwaficha Waisraeli wawili waliokuja kupeleleza Yeriko kabla ya Waisraeli kuvamia. Aliwasaidia wapelelezi kurudi kwenye kambi ya Israeli. * Rahabu akamwamini Bwana. * Yeye na familia yake hawakudhuriwa Yeriko ilipoharibiwa na wakaenda kuishi Israeli.
## Raheli ### Ufafanuzi Raheli alikuwa mmoja wa wake wa Yakobo. Yeye na dada yake Lea walikuwa watoto wa mjomba wake Yakobo. * Raheli alikuwa mama yake na Yusufu na Benyamini ambao uzao wake ukaja kuwa moja ya kabila la Israeli. * Kwa miaka mingi Raheli hakuweza kupata mtoto. Mungu alimuwezesha kumzaa Yusufu. * Miaka mingine baadae alimzaa Benyamini, Raheli alikufa na Yakobo alimzika karibu na Bethelehemu.
## Rama ### Ufafanuzi Rama ulikuwa mji wa zamani wa Israeli uliokuwa kilometa 8 toka Yerusalemu. Ulikuwa mji ambao Benyamini aliishi. * Rama ni mahali ambapo Raheli alimzaa Benyamini. * Waisraeli walipochukuliwa mateka Babeli Waliletwa kwanza Rama kabla ya kwenda Babeli. * Rama ilikuwa nyumbani kwa mama na baba yake Samweli.
## Ramothi ### Ufafanuzi Ramothi ulikuwa mji wa muhimu sana katika milima ya Gileadi karibu na mto Yordani. Pia iliitwa Romothi Gileadi. * Ramothi ni milki ya Israeli kabila la Gadi na ulikuwa mji wa makimbilio. * Mfalme Ahabu wa Israeli na mfalme Yohoshafati wa Yuda walipanga vita dhidi ya mfalme Aramu wa Ramothi. Ahabu aliuawa vitani. * Baadae mfalme Ahazia na mfalme Yoramu walijaribu kuchukua mjiwa Ramothi toka kwa mfalme Aramu. * Ramothi Gileadi ni mahali ambapo Yehu aliteuliwa kuwa mfalme juu ya Israeli.
## Rebeka ### Ufafanuzi Rebeka alikuwa mjukuu wa kaka yake na Abrahamu yaani Nuhu. * Mungu alimchagua Rebeka kuwa mke wa mtoto wa Abrahamu, Isaka. * Rebeka alitoka mjia wa Aramu alipokuwa akiishi na kwenda na mtumishi wa Abrahamu katika mji wa Negevu ambapo Isaka aliishi. * Kwa muda mrefu Rebeka hakuwa na mtoto lakini baadaye Mungu akambariki na mapacha Esau na Yakobo.
## Rehoboamu ### Ufafanuzi Rehoboamu alikuwa mmoja wa wana wa mfalme Sulemani na alikuja kuwa mfalme baada ya Sulemani kufa. * Katika mwanzo wa utawala wake Rehoboamu alikuwa mkali sana kwa watu wake hivyo makabila kumi ya Israeli waliasi dhidi yake na kuunda ufalme wa Israeli huko Kaskazini. * Rehoboamu aliendelea kuwa mfalme wa ufalme wa Kusini wa Yuda ambapo kulikuwa na makabila mawili Yuda na Benyamini. * Rehoboamu alikuwa kiongozi mbaya asiyemtii Mungu na kuabudu miungu ya uongo.
## Rimoni ### Ufafanuzi Rimoni ni jina la mtu na jina la mahali lililotajwa sehemu katika Biblia. Pia lilikuwa jina la mungu wa uongo. * Mtu aliyeitwa Rimoni alikuwa mbenyamini toka mji ya Zebuloni. Mtoto wa mtu huyu alimuua Ishboshethi mwana kilema wa Yonathani. * Rimoni ulikuwa mji uliokuwa Kusini mwa Yuda katika mkoa uliotawaliwa na kabila la Benyamini. * Mwamba wa Rimoni palikuwa mahali pa usalama ambapo Wabenyamini walikimbilia wakitoroka kuuawa vitani. * Rimoni Perezi ni mji usiojulikana ulipokuwa katika jangwa la Yuda. * Naamani jemedari wa Shamu aliongea katika hekalu la mungu wa uongo Rimoni ambapo watu wa Shamu waliabudu.
## Rubeni ### Ufafanuzi Rubeni alikuwa mtoto wa kwanza wa Yakobo. Mama yake alikuwa Lea. * Kaka zake walipopanga kumuua mdogo wao Yusufu, Rubeni aliyaokoa maisha ya Yusufu kwa kuwaambia wamtupe katika shimo. * Robeni alikuja baadae kumuokoa Yusufu lakini kaka zake wengine walikuwa wameshamuuza kama mtumwa kwa wafanyabiashara waliokuwa wakipita. * Uzao wa Rubeni ulikuja kuwa moja ya makabila ya Israeli.
## Rumi ### Ufafanuzi Katika agano jipya mji wa Rumi ulikuwa mji muhimu wa himaya ya Warumi. Sasa ni mji kuu wa Itali. * Himaya ya Warumi ilitawala miji yote kuzunguka bahari ya Mediteraniani pamoja na Israeli. * Rumi ni neno linaloelezea chochote kinachozungumzia miji iliyotawaliwa na serikali ya Rumi. * Mtume Paulo alipelekwa mji wa Rumi kama mfungwa kwa sababu alihubiri habari njema kuhusu Yesu. Kitabu cha Warumi ni barua ya Paulo kwa Wakristo waliokuwa Rumi.
## Ruthu ### Ufafanuzi Ruthu alikuwa mwanamke Mmoabu aliyeolewa na Muisraeli aliyeamia Moabu na familia yake wakati ambao waamuzi wanaongoza Israeli. * Mume wa Ruthu alikufa na baada ya hayo aliondoka Moabu akasafiri na mama mkwe wake Naomi aliyerejea mjini kwao Bethelehemu iliyoko Israeli. * Ruthu alikuwa mwaminifu kwa Naomi na alifanya kazi kwa bidii ili kumpatia chakula Naomi. * Ruthu alijitoa kumtumikia Mungu wa kweli wa Israeli. * Ruthu aliolewa na Muisraeli aliyeitwa Boazi na akazaa mtoto mwanaume aliyekuja kuwa babu yake na mfalme Daudi na uzao wa Yesu Kristo.
## Sadoki ### Ufafanuzi Sadoki lilikuwa ni jina la kuhani mkuu aliyekuwa mtu mhimu katika Israeli wakati wa utawala wa Mfalme Daudi. * Wakati Absalomu aliasi dhidi ya Mfalme Daudi, Sadoki alimsaidia Daudi na alisaidia kwa kulirudisha Yerusalemu sanduku la agano. * Miaka kadhaa baadaye, alihusika katika sherehe ya kumtia mafuta Sulemani mwana wa Daudi kuwa mfalme. * Watu wawili tofauti wenye jina Sadoki walihusika katika kujenga kuta za Yerusalemu nyakati za Nehemia. * Sadoki pia lilikuwa ni jina la babu yake Mfalme Yothamu.
## Sakothi ### Ufafanuzi Sakothi ni jina la miji miwili ya Agano la Kale. Neno, "sakothi" lina maana ya "hifadhi." * Mji wa kwanza uliyo itwa Sakothi ulikuwa mashariki mwa Mto Yordani. * Yakobo alibaki Sakothi na familia yake na mifugo, akijenga mahifadhi yao hapo. * Miaka mia na zaidi baadae, Gideoni na wanaume wake waliyo choka alisimama Sakothi walipo kuwa wakiwakimbiza Wamidiani, lakini watu huko walikataa kuwapa chakula chochote. * Sakothi ya pili ipo kaskazini mwa mpaka wa Misri na ilikuwa sehemu moja Waisraeli walisimama walipo vuka Bahari ya Shamu walipo kuwa wanatoroka utumwa Misri.
## Samaria, Msamaria ### Ufafanuzi Samaria ilikuwa jina la mji na maeneo yake jirani kaskazini mwa Israeli. Eneo hili lilikuwa katikati ya Milima ya Sharoni magharibi na Mto Yordani mashariki. * Katika Agano la Kale, Samaria ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa kaskazini wa Israeli. Baadae eneo lililo kuwa jirani liliitwa Samaria. * Wakati Waassiria walipo chukuwa ufalme wa kaskazini wa Israeli, waliteka mji wa Samaria na kuwa lazimisha Waisraeli wa kaskazini kuondoka eneo hilo na kuwa hamisha maeneo tofauti katika miji ya Assiria. * Waassiria pia walileta wageni wengi katika eneo la Samaria kuwaweka katika maeneo Waisraeli waliyo ondolewa. * Baadhi ya Waisraeli waliyo baki eneo hilo walioa wageni waliyo hamia, na wazao wao waliitwa Wasamaria. * Wayahudi waliwadharau Wasamaria kwasababu walikuwa nusu Wayahudi na kwasababu mababu zao waliabudu miungu ya wapagani. * Katika kipindi cha Agano Jipya, eneo la Samaria lilipakana na Galilaya upande wa kaskazini na eneo la Yudea upande wa kusini.
## Samsoni ### Ufafanuzi Samsoni alikuwa mmoja wa waamuzi, au mkombozi, wa Israeli. Alitoka kabila la Dani. * Mungu alimpa Samsoni uwezo mkubwa wa kibanadamu aliyo tumia kupigana na maadui wa Israeli, Wafilisti. * Samsoni aliwekwa chini ya kiapo kutonyoa nywele na kutokunywa mvinyo au kinywaji chochote kilicho chachwa. Kadri alivyo shika hichi kiapo, Mungu aliendelea kumpa uwezo. * Hatimaye alivunja kiapo chake na kuruhusu nywele zake kunyolewa, ambao ili ruhusu Wafilisti kumkamata. * Wakati Samsoni alipo kuwa matekani, Mungu alimruhusu kupata tena uwezo wake na kumpa nafasi ya kuharibu hekalu la mungu wa uongo Dagoni, pamoja na Wafilisti wengi.
## Samweli ### Ufafanuzi Samweli alikuwa nabii na muamuzi wa mwisho wa Israeli. Alimpaka mafuta Sauli na Daudi kama wafalme juu ya Israeli. * Samweli alizaliwa kwa Elikana na Hanna katika mji wa Rama. * Hanna alikuwa tasa, hivyo aliomba kwa shauku kwamba Mungu ampe mtoto. Samweli alikuwa jibu la hilo ombi. * Samweli alivyo kuwa mvulana mdogo, Hanna alimtuma kumsaidia Eli kuhani katika hekalu kutimiza ahadi yake kwa Mungu. * Mungu alimuinua Samweli kuwa nabii mkuu wake.
## Sara, Sarai ### Ufafanuzi Sara alikuwa mke wa Ibrahimu. * Jina lake awali lilikuwa "Sarai," lakini Mungu akalibadilisha kuwa "Sara" * Sara alimza mwana Mungu alilye muahidi kumpa yeye na Ibrahimu.
## Sauli (A K) ### Ufafanuzi Sauli alikuwa mwanaume wa Kiisraeli ambaye Mungu alimchagua kuwa mfalme wa kwanza wa Israeli. * Sauli alikuwa mrefu na mtanashati, na mwanajeshi mwenye nguvu. Alikuwa aina ya mwanaume Waisraeli walitaka awe mfalme wao. * Japo kuwa alimtumikia Mungu mwanzoni, Sauli baadae alikuwa na kiburi na hakumtii Mung. Matokeo yake, Mungu alimteua Daudi kuchukuwa nafasi ya mfalme na kumruhusu Sauli kuuawa katika pambano. * Katika Agano Jipya, kulikuwa na Myahudi aliye itwa Sauli ambaye pia alijulikana kama Paulo na akawa mtume wa Yesu Kristo.
## Sedekia ### Ufafanuzi Sedekia, mwana wa Yosia, alikuwa mfalme wa mwisho wa Yuda (597- 587 KK). Lakini pia kuna watu kadhaa katika Agano la Kale wenye jina Sedekia. * Mfalme Nebukadneza alimtawaza Sedekia kuwa mfalme wa Yuda baada ya kumteka Mfalme Yehoyakini na kwenda naye huko Babeli. Baadaye Sedekia aliasi jambo lililomfanya Nebukadneza kumkamata na kuuangamiza Yerusalemu. * Sedekia, mwana wa Kenaana, alikuwa nabii wa uongo wakati wa Mfalme Ahabu wa Israeli. * Mtu aliyeitwa Sedekia alikuwa mmojawapo wa wale waliosaini mkataba kwa Bwana nyakati za Nehemia.
## Senakeribu ### Ufafanuzi Senakeribu alikuwa mfalme mkubwa wa Assiria aliye sababisha Ninawi kuwa tajiri, na mji wa muhimu. * Mfalme Senakeribu anajulikana kwa vita vyake dhidi ya Babiloni na ufalme wa Yuda. * Alikuwa mfalme mwenye kiburi na kumdhihaki Yahweh. * Senakeribu alishambulia Yerusalemu kipindi cha Mfalme Hezekia. * Yahweh alisababisha jeshi la Senakeribu kuharibiwa. * Vitabu vya Agano la Kale vya Wafalme na Nyakati vina adisia baadhi ya matukio ya Senakeribu na utawala wake.
## Sethi ### Ufafanuzi Katika kitabu cha Mwanzo, Sethi alikuwa mwana wa tatu wa Adamu na Hawa. * Hawa alisema kwamba Sethi alipewa kwake kwa sehemu ya mwanae Abeli, aliye uawa na kaka yake Kaini. * Nuhu alikuwa mzao wa Sethi, hivyo kila mtu aliye ishi tangu kipindi cha gharika ni mzao wa Sethi. * Sethi na familia yake walikuwa watu wa kwanza "kuliita jina la Bwana."
## Sharoni, Milima ya Sharoni ### Ufafanuzi Sharoni lilikuwa jina la ardhi ya rotuba pembeni ya Bahari ya Mediterenia, kusini mwa Mlima Karmeli. Unajulikana pia kama "Mlima wa Sharoni." * Miji kadhaa iliyo tajwa kwenye Biblia ilikuwa karibu na Mlima wa Sharoni, pamoja na Jopa, Lidia, na Kaesarea. * Hii yaweza tafsiriwa kama "mlima unao itwa Sharoni" au "Mlima Sharoni." * Watu waliyo ishi maeneo haya ya Sharoni waliitwa "Washaroni."
## Sheba ### Ufafanuzi Wakati wa zamani, Sheba ulikuwa mji wa zamani wa kisasa au eneo la nchi lililo kuwa karibu na kusini mwa Arabia. * Nchi ya Sheba au eneo lilikuwa karibu na nchi inayo julikana sasa kama Yemeni au Ethiopia. * Wakazi wake walikuwa wazao wa Hamu. * Malikia wa Sheba alienda mtembelea Mfalme Sulemani alipo sikia umaarufu wa utajiri wake na hekima. * Pia kuna baadhi ya wanaume wanao itwa "Sheba" waliyo tajwa kwenye kizazi cha Agano la Kale. Yawezekana jina la eneo lilitokana na mmoja wa hawa watu. * Mji wa Beersheba umefupishwa kwa Sheba mara moja katika Agano la Kale.
## Shekemi ### Ufafanuzi Shekemi ni mji uliyopo maili 40 kaskazini mwa Yerusalemu. Shekemi ni jina pia la mwanaume katika Agano la Kale. * Mji wa Shekemi ndipo Yakobo alipo ishi baada ya kupatana na kaka yake Esau. * Yakobo alinunua ardhi kutoka kwa wana wa Hamori na Wahivi huko Shekemi, ambao baadae wakawa makaburi ya familia yake na sehemu wana wa Yakobo walipo zikwa. * Mwana wa Hamori Shekemi alimbaka binti wa Yakobo Dina, ambao ilileta wana wa Yakobo kuuwa wanaume wote wa mji wa Shekemi.
## Shemu ### Ufafanuzi Shemu alikuwa mmoja wa wana wa Nuhu aliye enda nae kwenye safina kipindi cha gharika ya ulimwengu inayo elezwa katika kitabu cha Mwanzo. * Shemu alikuwa babu wa Ibrahimu na wazao wake. * Wazao wa Shemu wanajulikana kama "Wasemi" wanao zungumza lugha za "Kisemi" kama vile Kiebrania na Kiarabu. * Biblia ina kumbukumbu ya maisha ya Shemu kuwa takribani miaka 600.
## Shilo ### Ufafanuzi Shilo ulikuwa mji wa ukuta wa Kikanani uliyo shindwa na Waisraeli chini ya uongozi wa Yoshua. * Mji wa Shilo ulikuwa magharibi mwa Mto Yordani na kaskazini mashariki mwa mji wa Betheli. * Kipindi Yoshua alipo waongoza Israeli, mji wa Shilo ulikuwa sehemu ya kukutana watu wa Israeli. * Makabila kumi na mbili ya Israeli yalikutana pamoja Shilo kusikia Yoshua akiwaambia kiasi gani cha nchi ya Kanani ilipangiwa kila mmoja.
## Shimei ### Ufafanuzi Shimei ni jina la wanaume kadhaa wa Agano la Kale. * Shimei mwana wa Gera, alikuwa Mbenjamini aliye mlaani Mfalme Daudi na kutupa mawe kwake alipo kuwa akikimbia Yerusalemu kutoroka asiuliwe na mwanaye Absalomu. * Pia kulikuwa na makuhani wa Kilawi katika Agano la Kale waliyo itwa Shimei.
## Shinari ### Ufafanuzi Shinari ina maana ya "nchi ya mito miwili" na lilikuwa jina la mlima au eneo kusini mwa Mesopotamia. * Shinari baadae ilijulikana kama "Kaldea" na baadae, "Babilonia." * Watu wa kale waliyo ishi mji wa Babeli katika Mlima wa Shinari walijenga mnara mrefu kujaribu kujifanya wakuu. * Vizazi baadae, mababa wa Kiyahudi Ibrahimu aliishi katika mji wa Uri katika hili eneo, ambalo liliitwa "Kaldeo."
## Sidoni, Wasidoni ### Ufafanuzi Sidoni alikuwa mwana wa kwanza wa Kanani. Pia kuna mji wa Kikanani unao itwa Sidoni, labda uliitwa baada ya mwana wa Kanani. * Mji wa Sidoni ulikuwa upanda wa kaskazini mgharibi pwani ya Bahari ya Mediterenia eneo lililo sasa Lebanoni. * "Wasidoni" wa kundi la Foenisi waliyo ishi Sidoni na maeneo yanayo zunguka. * Katika Biblia, Sidoni ipo karibu na mji wa Tairi, na miji yote miwili ilijulikana kwa utajiri na uhuni wa tabia za watu wao.
## Sila, Silivanu ### Ufafanuzi Sila alikuwa kiongozi miongoni mwa waamini wa Yerusalemu. * Wazee wa kanisa la Yerusalemu alichagua Sila na Paulo na Barnaba kuleta barua kwa mji wa Antioki. * Sila baadae alisafiria na Paulo kwenye miji mingine kufundisha watu kuhusu Yesu. * Paulo na Sila waliwekwa gerezani katika mji wa Filipi. Waliimba nyimbo kwa Mungu wakati walipo kuwa huko na Mungu akawafungua kutoka gerezani. Askari wa gereza akawa Mkristo sababu ya ushuhuda wao.
## Simeoni ### Ufafanuzi Katika Biblia, kuna wanaume kadhaa wenye jina Simeoni. * Katika Agano la Kale, mwana wa pili wa Yakobo (Israeli) na Leah aliitwa Simeoni. Wazao wake walikuwa moja ya makabila kumi na mbili ya Israeli. * Kabila la Simeoni lilitawala eneo la kusini katika nchi ya ahadi ya Kanani, eneo lilio kuwa sehemu ya urithi wa Yuda. * Wakati Yusufu na Mariamu walipo mleta mtoto Yesu kwenye hekalu Yerusalemu kumtoa kwa Mungu, mzee mmoja jina lake Simeoni alimsifu Mungu kwa kumruhusu kumuona Mesiya.
## Simoni ### Ufafanuzi Simoni alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu. * Simoni anatajwa mara tatu katika orodha ya wanafunzi wa Yesu, lakini machache yana julikana kuhusu yeye. * Simoni alikuwa mmoja wa wale Kumi na Moja waliyo kutana kuomba pamoja Yerusalemu baada ya Yesu kurudi mbinguni.
## Sinai, Mlima Sinai ### Ufafanuzi Mlima Sinai ni jina la mlima uliyo upande wa kusini wa unao julikana kama Sinai Peninsula kwa sasa. Pia ulijulikana kama "Mlima wa Horebu." * Mlima Sinai ni sehemu kubwa ya jangwa la mawe. * Waisraeli walikuja Mlima Sinai walipo kuwa wanasafiri kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi. * Mungu alimpa Musa amri kumi Mlima Sinai.
## Soari ### Ufafanuzi Soari ulikuwa mji mdogo Alipokimbilia Lutu wakati Mungu alipoiaribu Sodoma na Gomora. * Hapo mwanzo ilikuwa inajulikana kama "Bela" lakini baadaye yake uliitwa "Soari" wakati Lutu alipomwomba Mungu kuuifadhi mji huu "mdogo". * Soari unaaminiwa kuwa ulikuwa katika tambarare za Mto Yordani au katika mpaka wa kusini wa Bahari ya Chumvi.
## Sodoma ### Ufafanuzi Sodoma ulikuwa mji kusini mwa kanani ambapo mpwa wa Ibrahimu Lutu aliishi na mke na watoto wake. * Nchi ya eneo linalo zunguka Sodoma ulinyeshewa vizuri na kurotubishwa, hapo ndipo Lutu alichagua kuishi alipo hamia Kanani. * Sehemu maalumu ya huu mji haujulikana kwasababu Sodoma na mji wa jirani wa Gomora ili haribiwa kabisa na Mungu kama adhabu kwa matendo maovu waliyo kuwa wanafanya.
## Stefano ### Ufafanuzi Stefano anajulikana kama Mkristo wa kwanza kuuawa, sababu ya imani yake kwa Yesu. Maisha yake na kifo yameandikwa kwenye kitabu cha Matendo. * Stefano alichaguliwa na Kanisa la awali la Yerusalemu kutumikia Wakristo kama shemasi kuwapa chakula wajane na wengine Wakristo wenye maitaji. * Baadhi ya Wayahudi walimshtumu kwa uongo Stefano kuzungumza dhidi ya Mungu na dhidi ya sheria ya Musa. * Stefano kwa ujasiri alisema ukweli kuhusu Yesu Mesiya, kwa kuanza na historia ya matendo ya Mungu kwa Waisraeli. * Viongozi wa Wayahudi walikasirika na kumuua Stefano kwa kumpiga mawe hadi kufa nje ya mji. * Kifo chake kilishuhudiwa na Sauli wa Tarso, baade kuwa mtume Paulo. * Stefano anajulikana pia kwa maneno yake ya mwisho kabla ya kufa: Bwana, tafadhali usihesabu dhambi hii dhidi yao," iliyo onyesha upendo aliyo kuwa nao kwa wengine.
## Sulemani ### Ufafanuzi Sulemani alikuwa mmoja wa wana wa Mfalme Daudi. Mama yake alikuwa ni Bathsheba. * Sulemani alipo kuwa mfalme, Mungu alimwambia aulize chochote alicho taka. Hivyo Sulemani aliomba hekima kutawala watu wake kwa haki na kweli. Mungu alifurahishwa na Sulemani na kumpa hekima na utajiri. * Sulemani ni al maarufu kwa kuwa na hekalu zuri Yerusalemu. * Japo kuwa Sulemani alitawala kwa hekima mwanzoni mwa utawala wake, baadae alioa kijinga wanawake wengi wa kigeni na kuanza kuabudu miungu yao. * Kwasababu ya kutokuwa mwaminifu, baada ya kifo chake Mungu aligawanya Waisraeli kwenye falme mbili: Israeli na Yuda. Hizi falme mara nyingi zilipigana.
## Syria ### Ufafanuzi Syria ni nchi iliyopo kaskazini mashariki ya Israeli. Wakati wa kipindi cha Agano Jipya, ilikuwa mkoa chini ya utawala wa Serikali ya Kirumi. * Katika Agano la Kale, Wasyria walikuwa jeshi kubwa la maadui wa Israeli. * Naamani alikuwa kiongozi mkuu wa jsehi la Syria aliye ponywa ukoma na nabii Elisha. * Wakazi wengi wa Syria ni wazao wa Aramu, aliye mzao wa mwana wa Nuhu Shemu. * Damasko, mji mkuu wa Syria, unatajwa mara nyingi kwenye Biblia. * Sauli alienda mji wa Damasko kwa mpango wa kutesa Wakristo, lakini Yesu alimzuia
## Tairi, Watairi ### Ufafanuzi Tairi ulikuwa mji wa zamani wa Kanani eneo la pwani mwa Bahari ya Mediterenia, katika eneo ambalo sasa ni sehemu nchi ya Lebanoni. Watu wake waliitwa "Watairi." * Sehemu ya mji pia ulikuwa katika kisiwa kwenye bahari, karibu na kilomita moja na pwani. * Kwasababu ya eneo na thamani ya mali halisi kama miti mierezi, Tairi ulikuwa na biashara iliyo fanikiwa ya masoko na ilikuwa tajiri sana. * Mfalme Hiramu wa Tairi alituma mbao kutoka mti wa mierezi na wa jenzi wa ujuzi wa kujenga jumba ya Mfalme Daudi. * Miaka mingi baadae, Hiramu pia alimpa Mfalme Sulemani mbao na wajenzi wa ujuzi wa kutengeneza hekalu. Sulemani alimlipa kiasi kikubwa cha ngano na mafuta ya mzaituni.
## Tamari ### Ufafanuzi Tamari ni jina la wanawake kadhaa katika Agano la Kale. Ni jina la miji ya maeno kadhaa katika Agano la Kale. * Tamari alikuwa mke wa mtoto wa Yuda. Alimzaa Perezi aliye kuwa babu wa Yesu Kristo. * Mmoja wa mabinti wa Mfalme Daudi pia aliitwa Tamari; alikuwa dada wa Absalomu. Kaka yake wa kambo Amnoni alimbaka na kutelekeza. * Absalomu pia alikuwa na binti aitwaye Tamari. * Mji unao itwa "Hazezoni Tamari" ni mji sawa na mji wa Engedi magharibi mwa pwani ya Bahari ya Chumvi.
## Tarishishi ### Ufafanuzi Tarishishi lilikuwa jina la wanaume wawili wa Agano la Kale. Lilikuwa jina la mji. * Mmoja wa wajukuu wa Yafeti aliitwa Tarishishi. * Tarishishi pia lilikuwa ni jina la mmoja wa wanaume wenye hekima wa mfalme Ahashuerusi. * Mjia wa Tarishishi ulikuwa wa kitajiri wa bandari, ambao mali zake zilibeba bidha za kuuza au kubadilisha. * Huu mji ulishirikiana na Tairi na wazo lake wakuwa mji wa Foenisia lilikuwa mbali na Israeli, yamkini kusini ya pwani ya Spain * Nabii wa Agano la kale Yona alipanda meli iliyo kuwa yaelekea Tarishishi badala ya kutii amri ya Mungu kwenda kuubiri Ninawi.
## Tarso ### Ufafanuzi Tarso ulikuwa mji uliyo fanikiwa katika mko wa Kirumi wa Silisia, ambao sasa ni Uturuki ya kati. * Tarso ulikuwa kando ya mto mkubwa na karibu na Bahari ya Mediterenia, uliyo ufanya njia muhimu ya biashara. * Wakati mmoja katika historia, ulikuwa mji mkuu wa Silisia. * Katika Agano Jipya, Tarso ulikuwa maarufu kwa kuwa mji wa nyumbani wa Paulo Mtume.
## Tera ### Ufafanuzi Tera alikuwa mzao wa mwana wa Nuhu, Shemu. Alikuwa mwana wa Abramu, Nahori na Harani. * Tera aliondoka nyumbani Uri ilikuweza kwenda kwenye nchi ya Kanani na mwanae Abramu, mtoto wa mjomba yake Lutu, na mke wa Abramu Sarai. * Alipo kuwa njiani kwenda Kanani, Tera na familia yake waliishi miaka mingi mji wa Harani Mesopotamia. Tera alikufa Harani na miaka 205.
## Thesalonike, Wathesalonike ### Ufafanuzi Katika kipindi cha Agano Jipya, Thesalonika ulikuwa mji mkuu wa Makedonia katika utawala wa zamani wa Rumi. Watu waliyo ishi kwenye mji waliitwa "Wathesalonike." * Mji wa Thesalonike ulikuwa muhimu kwa bandari na pia ulikuwa karibu na barabara iliyo unganisha na Rumi mashariki mwa serikali ya Rumi. * Paulo, na sila na Timotheo, walitembelea Thesalonike katika safari yake ya pili ya kimisheni na matokeo yake, kanisa lilijengwa. Baadae, Paulo alitembelea mji huu kwenye safari yake ya pili ya umisheni. * Paulo aliandika barua mbili kwa Wakristo wa Thesalonike.
## Thomaso ### Ufafanuzi Thomaso alikuwa mmoja wa wanaume kumi na mbili Yesu aliye wachagua kuwa wanafunzi na baadae, mitume. Alijulikana kama "Didimasi" yenye maana ya "pacha." * Mwisho wa maisha ya Yesu, aliwaambia wanafunzi wake anaenda kuwa na Baba na ata andaa sehemu ya wao kuwa naye. Thomaso alimuuliza Yesu jinsi gani watajua njia ya kufika huko wakati hawakujua wapi anaenda. * Baada ya Yesu kufa na kufufuka, Thomaso alisema hataamini kwamba Yesu yu hai tena mpaka atakapo ona na kugusa makovu ya Yesu.
## Tikiko ### Ufafanuzi Tikiko alikuwa mmoja wa watumishi wa Paulo wa injili. * Tikiko alienda na Paulo kati ya moja ya safari ya kimisheni ya Paulo huko Asia. * Paulo alimueleza kama "mpendwa" na "mwaminifu." * Tikiko alibeba barua za Paulo kwenda Efeso na Kolosai
## Timotheo ### Ufafanuzi Timotheo alikuwa jina mdogo kutoka Lystra aliye kuwa mwaamini katika Kristo kutokana na huduma ya Paulo mjini kwake. Baadae alijiunga na Paulo kwenye safari kadhaa za misheni na kusaidia chunga waamini wapya. * Baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki, lakini bibi yake na mama walikuwa Wayahudi na waamini wa Kristo. * Wazee na Paulo walimchagua Timotheo kwenye huduma kwa kumuekea mikono na kumuombea. * Vitabu viwili kwenye Agano Jipya (1Timotheo na 2Timotheo) ni barua zilizo andikwa na Paulo, akitoa muongozo kwa Timotheo kama kiongozi mdogo wa kanisa.
## Tirza ### Ufafanuzi Tirza ulikuwa mji muhimu wa Kanani uliyo chukuliwa na Waisraeli. Lilikuwa jina la binti wa Gileadi, mzao wa Manase. * Mji Tirza ulikuwa eneo lenye wakazi wa kabila la Manase. Inadhaniwa kuwa mji ulikuwa maili 10 kaskazini mwa mji wa Shekemi. * Miaka baadae, Tirza ukawa mji mkuu wa ufalme wa kaskazini wa Israeli kwa muda mfupi, kipindi cha wafalme wa nne wa Israeli. * Tirza pia lilikuwa jina la mjukuu mmoja wa Manase aliye omba apewa kiasi cha ardhi, maana hawakuwa na kaka wa kurithi kama ilivyo kuwa kawaida.
## Tito ### Ufafanuzi Tito alikuwa Mpagani alikuja kuwa mwamini kupitia huduma ya Paulo mtume. Alifunzwa na Paulo kuwa kiongozi mwanzo wa makanisa. * Barua kwa Tito na Paulo ni moja ya vitabu vya Agano Jipya. * Katika hii barua Paulo ana muelekeza Titp kuteua viongozi wa kanisa katika kisiwa cha Krete. * Katika barua zake zingine kwa Wakristo, Paulo anamtaja Tito kama mtu aliye mtia moyo na kumletea furaha
## Troa ### Ufafanuzi Mji wa Troa ulikuwa bandari kaskazini magharibi mwa pwani ya eneo la Rumi huko Asia. * Paulo alitembelea Troas mara tatu kipindi cha safari zake maeneo tofauti kuhubiri injili. * Siku moja huko Troa Paulo alihubiri muda mrefu hadi usiku na kijana mmoja Eutiko alianguka chini kwasababu ya usingizi kwa kumsikiliza. Maana alikuwa ameketi katika dirisha lillio wazi, Eutiko alianguka chini sana na kufa. Kwa nguvu za Mungu, Paulo alimleta kijana huyu uzimani. * Paulo alipo kuwa Rumi, alimuomba Timotheo kuleta vitabu vyake na koti, aliyo acha Troa.
## Tubali ### Ufafanuzi Kuna wanaume kadhaa kwenye Agano la Kale waliyo kuwa na majina "Tubali." * Mwanaume mmoja aliye itwa Tubali alikuwa mmoja wa wana wa Yafeti. * Mwanaume aliye itwa "Tubali Kaini" alikuwa mwana wa Lameki na mzaliwa wa Kaini. * Tubali pia ni jina la kundi la watu linalo tajwa na nabii Isaya na Ezekieli.
## Uajemi, Waajemi ### Ufafanuzi Uajeni ni nchi ambayo ilikuja kuwa ngome kubwa iliyoundwa na mfalme Cyrus mwaka 550 kabla ya Kristo. Nchi ya uajemi ilikuwa kusini mashariki mwa Babeli na Ashuru ambayo kwa sasa ni Irani. * Watu wa Uajemi waliitwa Waajemi. * Mfalme Cyrus alisema kuwa Wayahudi wapo huru toka mateka huko Babeli na akawaruhusu kurudi nyumbani na hekalu la Yerusalemu likajengwa kwa pesa zilizotoka katika ngome ya Uajemi. * Mfalme Artashasta alikuwa kiongozi wa ngome ya Uajemi wakati ambao Ezra na Nehemia walirudi Yerusalemu na kujenga tena ukuta wa Yerusalemu. * Esta akawa malkia wa ngome ya Uajemi alipoolewa na mfalme Ahusuero.
## Uarabuni, mwarabu ### Ufafanuzi Uarabuni ni sehemu kubwa sana duniani yenye kilomita za mraba 3,000,000. Inapatikana kusini mashariki mwa Israeli na imepakana na bahari ya shamu, bahari ya Arabia na ghuba ya uajemi. * Mwarabu ni mtu anayeishi uarabuni. * Watu wa kwanza kuishi uarabuni walikuwa wajukuu wa Shemu. Mwingine ni mtoto wa Abrahamu Ishmaeli na kizazi chake pamoja na kizazi cha Esau. * Jangwa ambalo Waisraeli walizunguka miaka 40 lilikuwa Uarabuni. * Baada ya kumwamini Yesu mtume Paulo aliishi miaka michache katika jangwa la Arabia. * Katika barua yake kwa Wakristo wa Galatia, Paulo anataja mlima Sinai uliopo Uarabuni.
## ufalme wa Israeli ### Ufafanuzi Usemi "ufalme wa Israeli" unamaanisha sehemu ya kaskazini mwa taifa la Israeli wakati makabila kumi na mbili ya Israeli yalipogawanyika katika falme mbili baada ya Sulemani kufa. Ufalme wa Israeli wa kaskazini ulikuwa na makabila kumi na ufalme wa Yuda ulikuwa na makabila mawili. Mji mkuu wa ufalme wa Israeli ulikuwa Samaria. Ilikuwa kama kilomita 50 kutoka Yerusalemu, mji mkuu wa Yuda. Wafalme wote wa ufalme wa Israeli walikuwa waovu. Waliwashawishi watu kutumikia sanamu na miungu ya uongo. Mungu aliwatuma Waashuri kuvamia taifa la Israeli. Waisraeli wengi walikamatwa na kupelekwa kuishi Ashuru. Waashuri waliwaleta wageni kuishi miongoni mwa watu waliobaki wa Israeli. wageni hawa waliowana na Waisraeli, na uzao wao ukawa watu wa Samaria.
## Ufilisti ### Ufafanuzi Ufilisti ni jina la mji mkubwa katika nchi ya Kanaani iliyopo pwani mwa Bahari ya Mediteraniani. * Mji huu ulikuwa kando ya pwani yenye rutuba toka Yopa kaskazini kwenda Gaza kusini. Ilikuwa Kilometa 64 urefu na upana Kilometa 16. * Ufilisti ilikaliwa na "Wafilisti" kundi la watu lenye nguvu ambao mara nyingi walikuwa maadui wa Waisraeli.
## Ukaldayo, Wakaldayo ### Ufafanuzi Ukaldayo ulikuwa mkoa wa kusini mwa Mesopotamia au Babeli. Watu walioishi katika mkoa huo waliitwa Wakaldayo. * Katika mji wa Uri alipotoka Abrahamu ulikuwepo Ukaldayo. Hutajwa kama "Uri ya Ukaldayo. * Mfalme Nebukadreza alikuwa mmoja wa Wakaldayo waliokuwa wafalme katika Bebeli. * Baada ya miaka mingi katika mwaka wa 600 Kabla ya Kristo Ukaldayo ilikuja kuwa na maana ya Babeli. * Katika kitabu cha Danieli "Wakaldayo" walikuwa ni kundi fulani maalumu la watu waliokuwa na elimu kubwa na wataalamu wa nyota.
## Uri ### Ufafanuzi Uri ulikuwa mji muhimu pembeni mwa Mto Frati katika mji wa zamani wa Kalidea, ambao ulikuwa sehemu ya Mesopotamia. Hili eneo lilikuwa ambapo sasa ni Iraqi. * Ibrahimu alitoka mji wa Uri na ndipo huko Mungu alimuita kuondoka kwenda nchi ya Kanani. * Harani, kaka wa Ibrahimu na baba wa Lutu, alikufa Uri. Hii inawezana ikawa sababu Lutu aliondoka Uri na Ibrahimu.
## Uria ### Ufafanuzi Uria alikuwa mwanaume mwenye haki na mmoja wanajeshi hodari wa Mfalme Daudi. Utajwa kama "Uria Mhiti" * Uria alikuwa na mke mzuri sana aliye itwa Bathisheba. * Daudi alifanya uasherati na mke wa Uria, na akashikwa mimba na mtoto wa Daudi. * Kufunika hii dhambi, Daudi alisababisha Uria kufa kwenye pambano. Kisha Daudi akamuoa Bathisheba. * Mwanaume mwingine aliye itwa Uria alikuwa kuhani wakati wa Mfalme Ahazi.
## Uzia, Azaria ### Ufafanuzi Uzia alikuwa mfalme wa Yuda akiwa ni umri wa miaka 16 na akatawala miaka 52, ambao ulikuwa utawala mrefu. Uzia alijulikana kama "Azaria." * Mfalme Uzia alijulikana kwa mpangilio na ujuzi wa kijeshi. Alikuwa na maghorofa yaliyo jengwa kulinda mji na silaha maalumu za vita zilizo undwa na kuwekwa juu yake kubeba mishale na mawe makubwa. * Kadri Uzia alivyo mtumikia Bwana, alifanikiwa. Mwisho utawala wake, walakini, alipatwa na kiburi na hakumtii Bwana kwa kuchoma uvumba kwenye hekalu, ambaye kuhani tu ndiye aliruhusiwa kufanya hivyo. * Kwasababu ya dhambi hii, Uzia aliumwa na ukoma na alibidi aishi mbali na watu hadi mwisho wa utawala wake.
## Vashti ### Ufafanuzi Katika agano la kale kwenye kitabu cha Esta, Vashti alikuwa mke wa Ahasuero mfalme wa Uajemi. * Mfalme Ahasuero alimfukuza malkia Vashti baada ya kukataa kutii amri zake yake ya kwenda kwenye chakula cha jioni na kuonesha uzuri wake kwa wageni. * Matokeo yake mfalme alikwenda kutafuta malkia mpya na Esta akachaguliwa kuwa mke mpya wa Mfalme.
## Wafilisti ### Ufafanuzi Wafilisti walikuwa kundi la watu waliokaa katika mji wa Ufilisti kando ya bahari ya Mediteraniani. Jina lao linamaana ya "watu wa baharini" * Kulikuwa na miji mikuu mitano ya Wafilisti: Ashodi, Ashkelon, Ekroni, Gathi, na Gaza. * Mji wa Ashodi ulikuwa kaskazini mwa Ufilisti na mji wa Gaza ulikuwa kusini. * Wafilisti walijulikana kwa miaka mingi walikuwa katika vita na Waisraeli. * Mwamuzi Samsoni alikuwa shujaa aliyejulikana sana dhidi ya Wafilisti aliyetumia nguvu zake toka kwa Mungu. * Mfalme Daudi alionfoza vita dhidi ya Wafilisti ikiwemo kipindi alipokuwa kijana alipomshinda shujaa wa Wafilisti Goliati.
## Wakerethi ### Ufafanuzi Wakerethi walikuwa kundi la watu ambao walikuwa kama sehemu ya Wafilisti. Pia imeandikwa kama "Wakerethi." * "Wakerethi na Waperisi" walikuwa kundi maalumu la maaskari kutoka jeshi la mfalme Daudi. ambao walikuwa wametengwa kwa ajili yake kama walizi. * Benaya, mwana wa Yehoyada, mdau wa msimamizi wa watu wa Daudi, alikuw akiongozi wa Waperithi na Waperesi. * Waperethi walibaki na Daudi wakati alipokuwa anakimbia Yerusalimu kwa sababu ya kuchukizwa na Absalomo.
## Yafa ### Ufafanuzi Katika nyakati za Biblia, mji wa Yafa ulikuwa mji muhimu wa kibiashara uliopo Bahari ya Kati, kusini mwa uwanda wa Sharoni. Eneo la zamani la Yafa ndio mji wa leo wa Yafa, ambayo sasa ni sehemu ya Tel Aviv. Katika Agano la Kale, Yafa ndio mji ambao Yona alipanda boti kwenda Tarshishi. Katika Agano Jipya, mwanamke wa Kikristo aitwaye Tabitha alifia Yafa na Petro alimfufua.
## Yafethi ### Ufafanuzi Yafethi alikuwa mmoja wa wana watatu wa Nuhu. Wakati wa mafuriko wa ulimwengu wote uliofunika dunia yote, Yafethi na ndugu zake wawili walikuwa na Nuhu katika safina, pamoja na wake zao. Wana wa Nuhu kawaida huorodheshwa hivi, "Shemu, Hamu, na Yafethi." Hii inaashiria kuwa Yafethi alikuwa mdogo kati ya hao ndugu.
## Yakobo (mwana wa Alfayo) ### Ufafanuzi Yakobo, mwana wa Alfayo, alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu. Jina lake linatolewa katika orodha ya wanafunzi wa Yesu katika injili za Mathayo, Marko, na Luka. Ametajwa pia katika kitabu cha Matendo ya Mitume kama mmoja wa kumi na moja ambao walikuwa pamoja wakiomba Yerusalemu baada ya Yesu kurudi juu mbinguni.
## Yakobo (mwana wa Zebedayo) ### Ufafanuzi Yakobo, mwana wa Zebedayo, alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili. Alikuwa na ndugu yake mdogo aliyeitwa Yohana ambaye pia alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu. Yakobo na ndugu yake Yohana walifanya kazi kwa kuvua samaki na baba yao Zebedayo. Yakobo na Yohana waliitwa jina la utani "wana wa ngurumo," labda kwa sabau walikuwa wepesi kukasirika. Petro, Yakobo, na Yohana walikuwa wanafunzi wa karibu zaidi na Yesu na walikuwa naye kwa matukio ya ajabu kama vile Yesu alipokuwa juu ya mlima na Eliya na Musa na Yesu alipomfanya msichana aliyekufa kurudia uhai wake. Huyu ni Yakobo tofauti na yule aliyeandika kitabu katika Biblia. Lugha zingine zinalazimika kuandika majina yao tofauti ili kuweka wazi kuwa walikuwa watu wawili tofauti.
## Yakobo (ndugu wa Yesu) ### Ufafanuzi Yakobo alikuwa mwana wa Mariamu na Yusufu. Alikuwa mmoja wapo wa wadogo zake Yesu. Ndugu zake wengine Yesu walikuwa ni, Yusufu, Yuda na Simoni Wakati wa uhai wa Yesu, Yakobo na ndugu zake hawakuamini kuwa Yesu ndiye Masihi. Baadaye, baada ya Yesu kufufuka katika wafu, Yakobo alimuamini na kuwa kiongozi katika kanisa la Yerusalemu. Kitabu cha Agano Jipya cha Yakobo ni barau ambayo Yakobo aliwaandikia Wakristo waliokimbilia nchi zingine kutoroka mateso.
## Yakobo, Israeli ### Ufafanuzi Yakobo alikuwa pacha mdogo aliyekuwa mwana wa Isaka na Rebeka. Jina la Yakobo linamaanisha "anakamata kisigino" ambao ni usemi unaomaanisha, "hudanganya." Wakati yakobo alipozaliwa, alikuwa akishilia kisigino cha pacha wake Esau. Miaka mingi baadaye, Mungu alibalisha jina la Yakobo kuwa "Israeli," inayomaanisha, "anashindana na Mungu." Yakobo alikuwa mjanja na muongo. Alipata njia ya kupata baraka za mwana wa kwanza na kurithi haki kutoka kwa kaka yake, Esau. Esau alikasirika na kupanga kumuua, kwa hiyo Yakobo akaondoka nchini mwake. Lakini baada ya miaka Yakobo alirudi na wake zake na watoto katika nchi ya Kanaani ambamo Esau alikuwa akiishi, na familia zao ziliishi kwa amani zikiwa jirani. Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili. Uzao wao ukawa makabila kumi na mbili ya Israeli. Mwanaume tofauti aitwaye Yakobo ameorodheshwa kama baba wa Yusufu katika ukoo wa Mathayo.
## Yeftha ### Ufafanuzi Yeftha alikuwa mpiganaji kutoka Gileadi aliyetumika kama mhukumu juu ya Israeli. Katika Wahebrania 11:32, Yeftha anasifiwa kama kiongozi muhimu aliyewatoa watu wake kutoka kwa maadui zake. Aliwaokoa Waisraeli kutoka kwa wamoabi na kuwaongoza watu wake kuwashinda Waefraimu. Hata hivyo, Yeftha alifanya kiapo cha kipumbavu na haraka kwa Mungu kilichosababisha yeye kumtoa sadaka binti yake.
## Yehoramu, Yoramu ### Ufafanuzi Yehoramu lilikuwa jina la wafalme wawili tofauti katika Agano la Kale. Wafalme wote hao wawili walijulikana kama "Yoramu." Mfalme mmoja Yehoramu alitawala ufalme wa Yuda kwa miaka minane. Alikuwa mwana wa Mfalme Yehoshafati. Huyu ndiye mfalme anayejulikna zaidi kama Yoramu. Mfalme Yehoramu mwingine alitawala ufalme wa Israeli kwa miaka kumi na mbili. Alikuwa mwana wa Mfalme Ahabu. Mfalme Yehoramu wa Yuda alitawala wakati wa manabii Yeremia, Danieli, Obadia, na Ezekieli wakitabiri katika ufalme wa Yuda. Yehoramu pia alitawala kwa muda kiasi wakati baba yake Yehoshafati alipokuwa akitawala Yuda. Tafsiri zingine zinaweza kuchagua kutumia jina "Yehoramu" pale ambapo huyu mfalme wa Israeli anatajwa na "Yoramu" kwa mfalme wa Yuda. Njia nyingine ya kumtambua vizuri kila mmoja ni kuongeza jina la baba yake.
## Yehoshafati ### Ufafanuzi Yehoshafati ni jina la angalua watu wawili katika Agano la Kale. Mtu anayejulikana vizuri zaidi kwa hili jina ni Mfalme Yehoshafati ambaye alikuwa mfalme wa nne kutawala ufalme wa Yuda. Alirejesha amani kati ya Yuda na Israeli, na kuangamiza madhabahu ya miungu wa uongo. Yehoshafati mwingine alikuwa "mtunza kumbukumbu" wa Daudi na Sulemani. Kazi yake ilikuwa pamoja na kuandika nyaraka kwa ajili ya mfalme kusaini na kurekodi historia ya matukio muhumi yaliyotokea katika ufalme.
## Yehoyada ### Ufafanuzi Yehoyada alikuwa kuhani aliyemsaidia kumficha na kumlinda mwana wa mfalme Ahazia, Yoashi hadi alipofikisha umri wa kuweza kutangazwa kuwa mfalme. Yehoyada alimpangia mamia ya walinzi kumlinda Yoashi alipokuwa mdogo wakati akitangazwa kuwa mfalmena watu hekaluni. Yehoyada aliwaongoza watu kuondoa madhabahu yote ya mungu wa uongo Baali. Maisha yake yote yaliyosalia, kuhani Yehoyada alimshauri mfalme Yoashi kwa kumsaidia kumtii Mungu na kuwatawala watu kwa hekima. Mwanamme mwingine aliyeitwa Yehoyada alikuwa baba wa Benaya.
## Yehoyakimu ### Ufafanuzi Yehoyakimu alikuwa mfalme aliyetawala ufalme wa Yuda. Yehoyakimu alikuwa mfalme alipokuwa na miaka 18. Alitawala miezi mitatu tu na baada ya hapo alikamatwa na jeshi la Babeli na kupelekwa Babeli. Wakati wa utawala wake mfupi, Yehoyakimu alifanya uovu kama babu yake mfalme Manase na baba yake Mfalme Yehoyakimu alivyofanya.
## Yehoyakimu ### Ufafanuzi Yehoyakimu alikuwa mfalme muovu aliyetawala ufalme wa Yuda, kuanzia mwaka 608 K.K. Alikuwa mwana wa mfalme Yosia. jina lake mwanzoni lilikuwa Eliakimu. Farao wa Misri Neko alibadili jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu na kumfanya kuwa mfalme wa Yuda. Neko alimlazimisha Yehoyakimu kulipa kodi ya juu kwa Misri. Yuda ilipovamiwa baadaye na mfalme Nebukadreza, Yehoyakimu alikuwa miongoni mwao wale walikamatwa na kupelekwa Babeli. Yehoyakimu alikuwa mfalme mwovu aliyeingoza Yuda mbali na Yahwe. Nabii Yeremia alitabiri dhidi yake.
## Yehu ### Ufafanuzi Yehu lilikuwa jina la wanaume wawili katika Agano la Kale. Yehu mwana wa Hanani alikuwa nabii wakati wa utawala wa Mfalme Ahabu na Mfalme Yehoshafati wa Yuda. Yehu mwana (uzao) wa Yehoshafati alikuwa jemedari katika jeshi la Israeli ambaye alitiwa mafuta kuwa mfalme kwa amri ya nabii Elisha. Yehu aliua vitu viwili viovu: Mfalme Yoramu wa Israeli na Mfalme Ahazia wa Yuda. Mfalme Yehu pia aliwaua ndugu wote wa mfalme wa zamani Ahabu, na akafanya yule malkia muovu Yezebeli auwawe. Yehu aliaangamiza sehemu zote za kumuabudia Baali ndani ya Samaria na kuwaua manabii wote wa Baali. Mfalme Yehu alimtumikia Mungu mmoja wa kweli, Yahwe, na alikuwa mfalme juu ya Israeli kwa miaka ishiri na nane.
## Yeremia ### Ufafanuzi Yeremia alikuwa nabii wa Mungu katika ufalme wa yuda. Kitabu cha Agano la Kale cha Yeremia kina unabii wake. Kama manabii wengi, Yeremia mara nyingi ilimbidi kuwaonya watu wa Israeli kuwa Mungu atawaadabisha kwa dhambi zao. Yeremia alitabiri kuwa Wababeli wataiteka Yerusalemu, jambo lililowafanya baadhi ya watu wa Yuda kukasirika. Kwa hiyo walimuweka katika kisima kilichokauka na kumuacha humo kufa. Lakini mfalme wa Yuda aliwaamuru watumishi wake kumuokoa Yeremia kutoka katika kisima. Yeremia aliandika kuwa alitamani macho yake yawe "chemchemi ya machozi," kuonesha masikitiko yake makali kuhusu uasi na mateso ya watu wake.
## Yeriko ### Ufafanuzi Yeriko ulikuwa mji wenye nguvu katika nchi ya Kanaani. Ulikuwa magharabi mwa mto wa Yordani na kaskazini mwa Bahari ya Chumvi. Kama Wakanaani wote, watu wa Yeriko waliabudu miungu ya uongo. Yeriko ulikuwa mji wa kwanza katika nchi ya Kanaani ambao Mungu aliwaambia Waisraeli kuuteka. Wakati Yoshua alipowaongoza Waisraeli dhidi ya Yeriko, Mungu alifanya muujiza mkubwa kuwasaidia kuushinda huo mji.
## Yeroboamu ### Ufafanuzi Yeroboamu mwana wa Nebati alikuwa mfalme wa kwanza wa ufalme wa kaskazini wa Israeli kati ya 900-910 K.K. Yeroboamu mwingine, mwana wa mfalme Yoashi, alitawala juu ya Israeli karibu miaka 120 baadaye. Yahwe alimpa Yeroboamu mwana wa Nebati utabiri kwamba atakuwa mfalme baada ya Sulemani na kwamba atayatawala makabila kumi ya Israeli. Sulemani alipokufa, makabila kumi ya kaskazini mwa Israeli yalimkaidi mwana wa Sulemani, Rehoboamu na badala yake walimfanya Yeroboamu kuwa mfalme wao, wakimuacha Rehoboamu kama mfalme wa makabila mawili tu ya kusini, Yuda na Benyamini. Yeroboamu alikuwa mfalme muovu aliyewaongoza watu kutomuabudu Yahwe na badala yake aliweka sanamu kwa ajili yao kuabudu. Waflame wengine wote wa Israeli walifuata mfano wa Yeroboamu na walikuwa wafalme waovu kama yeye alivyokuwa. Karibu miaka 120 baadaye, mfalme mwingine Yeroboamu alianza kutawala ufalme wa kaskazini mwa Israeli. Yeroboamu huyu alikuwa mwana wa Yoashi na alikuwa muovu kama wafalme wengine wote waliopita wa Israeli walivyokuwa. Licha ya haya yote, Mungu alikuwa na huruma juu ya Israeli na kumsaidia huyu mfalme Yeroboamu kuongeza ardhi na kuimarisha mipaka ya eneo lao.
## Yerusalemu ### Ufafanuzi Yerusalemu mwanzoni ulikuwa mji wa zamani wa Kikanaani ambao baadaye ulikuwa mji muhimu zaidi katika Israeli. Inapatikana karibu kilomita 34 magharibi mwa Bahari ya Chumvi na kaskazini mwa Bethlehemu. Bado ni mji mkuu wa Israeli ya leo. Jina "Yerusalemu" imetajwa kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Yoshua. Majina mengine ya mji huu katika Agano la Kale ni pamoja na "Salemu", "mji wa Yebusi," na "Sayuni." "Yerusalemu" na "Salemu" zote zina msingi wa "amani" katika maana. Yerusalemu mwanzoni ilikuwa ngome ya Yebusi iitwayo "Sayuni" amabyo mfalme Daudi aliikamata na kuifanya kuwa mji wake mkuu. Mwana wa Daudi Sulemani alijenga hekalu la kwanza Yerusalemu, katika mlima Moria, ambao ulikuwa mlima ambao Abrahamu alimtoa Isaka kama sadaka kwa Mungu. Hekalu lilirudiwa kujengwa hapo baada ya kutetezwa na Wababeli. Kwa sababu hekalu lilikuwa Yerusalemu, sherehe kuu za Kiyahudi ziliadhimishwa huko. Watu kawaida husema kwenda "juu" Yerusalemu kwa sababu palikuwa mlimani.
## Yese ### Ufafanuzi Yese Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi, na mjukuu wa Ruthu na Boazi. * Yese alikuwa kutoka kabila la Yuda. * Alikuwa "Muefrathi," inayomaanisha alikuwa kutoka mji wa Efrathi (Bethlehemu). * Nabii Isaya alitabiri kuhusu "tawi" ambalo litatoka katika "mzizi wa Yese" na kuzaa matunda. Hii inamaanisha Yesu aliyekuwa uzao wa Yese.
## Yethro, Reueli ### Ufafanuzi Majina "Yethro" na "Reueli" yote yanamaanisha baba wa mke wa Musa, Sipora. Kulikuwa kuna watu wawili wengine wenye jina "Reueli" katika Agano la Kale. Wakati Musa alipokuwa mchungaji katika nchi ya Medani, alimuoa binti wa mwanamme wa Medani aitwaye Reueli. Baadaye Reueli anajulikana kama "Yethro, kuhani wa Medani." Inawezekana kuwa "Reueli" lilikua jina la ukoo. Mungu alipozungumza na Musa kutoka kichaka cha moto, Musa alikuwa akichunga kondoo wa Yethro. Muda mwingine baadaye, baada ya Mungu kuwaokoa Waisraeli kutoka Misri, Yethro alikuja kwa Waisraeli jangwani na kumpa Musa ushauri mzuri kuhusu kuhukumu mambo ya watu. Alimuamini Mungu aliposikia miujiza yote Mungu aliyoifanya kwa watu Waisraeli ndani ya Misri. Mmoja wa wana wa Esau alitwa Reueli. Mwanamme mwingine Reueli anatajwa katika uzao wa Waisraeli aliyerudi kutishi Yuda baada ya kutekwa kwa Babeli kuisha.
## Yezebeli ### Ufafanuzi Yezebeli alikuwa mke muovu wa mfalme Ahabu wa Israeli. Yezebeli alimshawishi Ahabu na Israeli nzima kuabudu sanamu. Pia aliua manabii wengi wa Mungu. Yezebeli alisababisha mtu asiye na hatia aitwaye Nabothi kuuwawa ili Ahabu aibe shamba la mizabibu la Nabothi. Yezebeli hatimaye aliuwawa kutokana na maovu yote aliyotenda. Eliya alitabiri jinsi atakavyokufa na ikatokea hivyo hivyo kama alivyotabiri.
## Yezreeli ### Ufafanuzi Yezreeli lilikuwa jina la mji muhimu Israeli katika eneo la kabila la Isakari, lililokuwa kusini magharibi mwa Bahari ya Chumvi. Mji wa Yezreeli ni moja ya alama za magharibi za uwanda wa Megido, ambayo pia unaitwa "Bonde la Yezreeli." Wafalme kadhaa wa Israeli walikuwa na majumba yao ya utawala katika mji wa Yezreeli. Bustani la mizabibu la Nabothi ilikuwa karibu na nyumba ya mfalme Ahabu ndani ya Yezreeli. Nabii Eliya alitabiri dhidi ya Ahabu huko. Mke muovu wa Ahabu, Yezebeli, aliuwawa Yezreeli. Matukio mengine ya muhimu yalitokea katika mji huu, yakiwemo mapigano kadhaa.
## Yoabu ### Ufafanuzi Yoabu alikuwa kiongozi muhimu wa jeshi kwa mfalme Daudi katika utawala wake wote. Kabla Daudi hajawa mfalme, Yoabu tayari alikuwa mmoja wa wafuasi wake waminifu. Baadaye, wakati wa utawala wa Daudi kama mfalme wa Israeli, Yoabu alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la mfalme Daudi. Yoabu alikuwa pia mpwa wa mfalme Daudi kwa kuwa mama yake alikuwa mmoja wa madada zake Daudi. Wakati mwana wa Daudi, Absalomu, alipomsaliti kwa kujaribu kuuchukua ufalme, Yoabu alimuua Absalomu ili kumlinda mfalme. Yoabu alikuwa mpambanaji mwenye hima na aliua watu wengi waliokuwa maadui wa Israeli.
## Yoashi ### Ufafanuzi Yoashi lilikuwa jina la watu kadhaa katika Agano la Kale. Yoashi mmoja alikuwa baba wa mkombozi mmoja wa Israeli, Gideoni. Mwanamme mwingine aliyeitwa Yoashi alikuwa uzao wa mwana wa mwisho wa Yakobo, Benyamini. Yoashi anayejulikanai vizuri zaidi alikuwa mfalme wa Yuda akiwa na umri wa miaka saba. Alikuwa mwana wa Ahazia, mfalme wa Yuda aliyeuwawa. Yoashi alipokuwa mtoto mdogo, shangazi yake alimuokoa kuuliwa kwa kumficha hadi alipokuwa na umri wa kutosha kufanywa mfalme. Mfalme Yoashi alikuwa mfalme mzuri ambaye mwanzoni alimtii Mungu. Ila hakutoa sehemu zilizo inuka na Waisreali wakaanza tena kuabudu sanamu. Mfalme Yoashi alitawala Yuda wakati wa baadhi ya miaka mfalme Yehoashi alipotawala Israeli. Walikuwa wafalme wawili tofauti.
## Yoeli ### Ufafanuzi Yoeli ni jina la nabii ambaye inawezekana aliishi wakati wa utawala wa mfalme Yoashi wa Yuda. Kuna watu wengine pia katika Agano la Kale wenye jina Yoeli. Kitabu cha Yoeli ni moja ya vitabu vifupi vya kinabii katika sehemu ya mwisho ya Agano la Kale. Maelezo pekee tuliyonayo kumhusu nabii Yoeli ni kwamba jina la baba yake ni Pethueli. Katika mahubiri yake ya Pentekoste, mtume Paulo alinukuu kutoka kitabu cha Yoeli.
## Yohana (Mbatizaji) ### Ufafanuzi Yohana alikwa mwana wa Zekaria na Elisabeti. Kwa kuwa "Yohana" lilikuwa jina lililozoeleka, mara nyingi huitwa "Yohana Mbatizaji" ili kumtofautisha na watu wengine waitwao Yohana, kama mtume Yohana. Yohana alikuwa nabii ambaye Mungu alimtuma kuwaanda watu kumuamini na kumfuata Masihi. Yohana aliwaambia watu kutubu dhambi zao, kumgeukia Mungu, na kuacha kutenda dhambi, ili wawe tayari kumpokea Masihi. Yohana alibatiza watu wengi katika maji kama ishara ya kwamba wanatubu dhambi zao na kuziacha. Yohana aliitwa "Yohana Mbatizaji" kwa sababu alibatiza watu wengi. Hakikisha kuwa watu wataelewa kuwa "Mbatizaji" haiimaanishi kanisa kwa hili jina. Inaweza kulazimu kusema, "Yohana aliyebatiza".
## Yohana (mtume) ### Ufafanuzi Yohana alikuwa mmoja wa mitume kumi na mbili na rafiki wa karibu wa Yesu. Yohana na ndugu yake Yakobo walikuwa wana wa mvuvi wa samaki aitwaye Zebedayo. Katika injili aliyoandika kuhusu maisha ya Yesu, Yohana alijieleza kama "mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda." Hii inaonehsa kuwa Yohana alikuwa rafiki wa karibu wa Yesu. Mtume Yohana aliandika vitabu vitano katika Agano Jipya: injili ya Yohana, Ufuno wa Yesu Kristo, na barua tatu zilionadikwa kwa waumini wengine. Noti kuwa mtume Yohana alikuwa mtu tofauti na Yohana mbatizaji.
## Yohana Marko ### Ufafanuzi Yohana Marko, pia akijulikana kama "Marko," alikuwa mmoja wa wanaume waliosafiri na Paulo katika safari zake za kimisionari. Inawezekana kuwa yeye ndiye mwandishi wa Injili ya Marko. Yohana Marko alifuatana na binamu ya Barnaba na Paulo katika safiri yao ya kwanza ya kimisonari. Wakati Paulo alipowekwa gerezani Yerusalemu, waumini walikuwakimuombea katika nyumba ya mama yake Yohana Marko. Marko hakuwa mmoja wa mitume wa awali, lakini alifundishwa na Paulo na Petro na alifanya nao kazi katika huduma.
## Yona ### Ufafanuzi Yona alikuwa nabii wa Kihebrania katika Agano la Kale. Kitabu cha Yona kinaelezea hadithi ya wakati Mungu alipomtuma Yona kuhubiri kwa watu wa Ninawi. Yona alikataa kwenda Ninawi na badala yake akapanda katika meli iliyokuwa inaelekea mji mwingine. Mungu alisababisha dhoruba kali kuilemea meli. Watu waliukuwa wakidafiri katika meli walipogundua kuwa Yona hakuwaanamtii Mungu, walimtupa katika bahari na dhoruba ikakoma. Yona alimezwa na samaki mkubwa na akawa tumboni mwake kwa siku tatu, mchana na usiku. Baada ya hayo, Yona alienda Ninawi na kuwahubiri watu wa huko, na wakaziacha dhambi zao.
## Yonathani ### Ufafanuzi Yonathani ni jina la angalau wanaume kumi katika Agano la Kale. Jina linamaanisha "Yahwe ametoa." Rafiki wa karibu wa Daudi , Yonathani, ndiye anayejulikna zaidi katika Biblia kwa hili jina. Yonathani alikuwa mwana kwanza wa mfalme Sauli. Yonathani wengine waliotajwa katika Agano la Kale ni pamoja na: uzao wa Musa, mpwa wa mfalme Daudi, makuhani kadhaa, akiwemo mwana wa Abiathari; na mwandishi wa Agano la Kale ambaye nyumba yake ilitumika kumfunga nabii Yeremia.
## Yoramu ### Ufafanuzi Yoramu mwana wa Ahabu alikuwa mfalme Israeli. Wakati mwingine anajulikana kama "Yehoramu." Mfalme Yoramu wa Israeli alitawala wakati mmoja kama Yehoramu wa Yuda. Yoramu alikuwa mfalme muovu aliyeabudu miungu ya uongo na kusababisha watu wa Israeli kutenda dhambi. Mfalme Yoramu wa Israeli pia alitawala wakati wa nabii Eliya na Obadia. Mwanamme mwingine aitwaye Yoramu alikua mwana wa mfalme wa Hamathi wakati Daudi ni mfalme.
## Yoshua ### Ufafanuzi Kuna Waisraeli kadhaa kwenye Biblia waitwao Yoshua. Anayejulikana zaidi ni Yoshua mwana wa Nuni aliyekuwa msaidizi wa Musa na baadaye kuwa kiongozi muhimu wa watu wa Mungu. Yoshua alikuwa mmoja wa wapelelezi kumi na mbili amabo Musa aliwatuma tafiti nchi ya ahadi. Pamoja na Kalebu, Yoshua aliwasihi watu wa Israeli watu kutii amri ya Mungu kuingia nchi ya ahadi na kuwashinda Wakanaani. Miaka mingi baadaye, baada ya Musa kufa, Mungu alimchagua Yoshua kuwaongoza watu Waisraeli kwenda nchi ya ahadi. Katika mapambano ya kwanza na maarufu zaidi dhidi ya Wakanaani, Yoshua aliwaongoza Waisraeli kuuangamiza mji wa Yeriko. Kitabu cha Agano la Kale cha Yoshua kinaelezea jinsi Yoshua alivyowaongoza Waisraeli katika kuichukua mamlaka nchi ya ahadi na jinsi alivyopanga sehemu tofauti za nchi kwa kila kabila la Israeli kuishi. Yoshua mwana wa Yosadaki anatajwa katika vitabu vya Hagai na Zekaria; alikuwa kuhani mkuu aliyesaidia kujenga tena kuta za Yerusalemu. Kuna wanaume kadhaa wengine waitwao Yoshua waliotajwa katika koo na sehemu zingine katika Biblia.
## Yosia ### Ufafanuzi Yosia alikuwa mfalme mcha Mungu aliyetawala juu ya ufalme wa Yuda kwa miaka thelathini na moja. Aliwaongoza watu wa Yuda kutubu na kumuabudu Yahwe. Baada ya baba yake mfalme Amoni kuuwawa, Yosia akawa mfalme juu ya Yuda akiwa na miaka minane. Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, mfalme Yosia alimuamuru kuhani mkuu Hilkia kulijenga tena hekalu la Mungu. Wakati hili likifanyika, vitabu vya Sheria vilipatikana. Vitabu vya Sheria viliposomwa kwa Yosia, alisikitishwa na jinsi watu wake walivyokuwa hawamtii Mungu. Aliamuru kwamba sehemu zote za kuabudia sanamu ziteketezwe na makuhani wa miungu wa uongo wauwawe. Pia aliwaamuru watu kuanza kuadhimisha sherehe ya Pasaka tena.
## Yothamu ### Ufafanuzi Katika Agano la Kale kuna wanaume watatu wenye jina Yothamu. Mwanaume mmoja aitwaye Yothamu alikuwa mwana wa mwisho wa Gideoni. Yothamu alisaidia kumshinda kaka yake mkubwa Abimeleki, ambaye aliwauwa ndugu zake wengine wote. Mwanamme mwingine aitwaye Yothamu alikuwa mfalme juu ya Yuda kwa miaka kumi na sita baada ya kifo cha baba yake Uzia (Azaria). Kama baba yake, Yothamu alimtii Mungu na likuwa mfalme mzuri. Lakini hakuondoa sehemu za kuabudia sanamu na hii ilisababisha watu wa Yuda baadaye kumgeuka Mungu tena.
## Yuda ### Ufafanuzi Yuda alikuwa mmoja wa wana wakubwa wa Yakobo. Mama yake alikuwa Lea. Uzao wake uliitwa "kabila la Yuda." Alikuwa ni Yuda aliyewaambia ndugu zake kumuuza mdogo wao Yusufu kama mtumwa badala ya kumuuacha afe katika shimo. Mfalme Daudi na wafalme wote baada yake walikuwa uzao wa Yuda. Yesu pia alikuwa uzao wa Yuda. Utawala wa Sulemani ulipoisha na taifa la Israeli kugawanyika, ufalme wa Yuda ulikuwa wa sehemu ya kusini mwa nchi. Katika kitabu cha Agano Jipya cha Ufunuo, Yesu anaitwa "Simba wa Yuda." Maneno "Yahudi" na mji wa "Yuda" yametoka katika jina "Yuda."
## Yuda ### Ufafanuzi Neno "Yuda" linamaanisha sehemu katika nchi ya Israeli ya zamani. Wakati mwingine linatumika katika maana finyu na wakati mwingine katika maana pana. Wakati mwingine"Yuda" inatumika katika maana finyu kumaanisha jimbo lililo sehemu ya kusini ya Israeli ya zamani magharibi tu mwa Bahari iliyo Kufa. Wakati mwingine "Yuda" inamaana pana na inamaanisha majimbo yote ya Israeli ya zamani, ikiwemo Galilaya, Samaria, Perea, Edomu na Yuda. Maana pana ya Yuda (mfano. Luka 1:5) inaweza kutafsiriwa kama "nchi ya Yuda" na katika maana finyu (mfano Luka 1:39) inaweza kutafsiriwa kama "jimbo la Yuda" kwa sababu hii ndio sehemu ya nchi ya Israeli ya zamani ambapo kabila la Yuda ya lilikuwepo.
## Yuda Iskariote ### Ufafanuzi Yuda Iskariote alikuwa mmoja wa mitume wa Yesu. Alikuwa ndiye aliyemsaliti Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi. Jina "Iskariote" inaweza kumaanisha "kutoka Keriothi", labada kuashiria kuwa Yuda alikulia katika huo mji. Yuda Iskariote alitunza fedha ya mitume na mara kwa mara aliiba kutumia kwa ajili yake. Yuda alimsaliti Yesu kwa kuwaambia viongozi wa dini mahali alipo Yesu ili wamkamate. Baada ya viongozi wa dini kumhukumu Yesu kifo, Yuda alijuta kuwa alimsaliti Yesu kwa hiyo akarudisha fedha ya usaliti kwa viongozi wa Kiyahudi na kisha kujiua. Mtume mwingine pia aliitwa Yuda na alikuwa mmoja wandugu wa Yesu. Kuna wanaume wengi waitwao Yuda katika Biblia, kama vile ndugu yake Yesu na mtume mwingine.
## Yuda mwana wa Yakobo ### Ufafanuzi Yuda mwana wa Yakobo alikuwa mmoja wa mitume kumi na mbili wa Yesu. Huyu hakuwa Yuda Iskariote. Mara nyingi katika Biblia, wanaume wenye majina ya kufanana hutofautishwa kwa kutaja walikuwa wana wa nani. Hapa Yuda anatajwa kama "mwana wa Yakobo." Mwanamme mwingine aitwaye Yuda alikuwa ndugu yake Yesu. Kitabu cha Agano Jipya cha"Yuda" kinawezekana kuwa kimeandikwa na ndugu yake Yesu Yuda, kwa kuwa anajitambulisha kama "ndugu yake Yakobo." Yakobo alikuwa ndugu mwingine wa Yesu. Inawezekana kuwa kitabu cha Yuda kiliandikwa na mwanafunzi wa yesu, Yuda mwana wa Yakobo.
## Yuda, ufalme wa Yuda ### Ufafanuzi Kabila la Yuda lilikuwa kubwa zaidi kati ya makabila kumi na mbili ya Israeli. Ufalme wa Yuda uliundwa na makanila ya Yuda na Benyamini. Baada ya mfalme Sulemani kufa, taifa la Israeli liligawanyika katika falme mbili: Israeli na Yuda. Ufalme wa Yuda ulikuwa ufalme wa kusini, uliokuwa magharabi mwa Bahari ya Chumvi. Mji mkuu wa ufalme wa Yuda ulikuwa Yerusalemu. Wafalme wanane wa Yuda walimtii Yahwe na kuwaongoza watu kumwabudu yeye. Wafalme wengine wa Yuda walikuwa waovu na kuwaongoza watu kuabudu sanamu. Zaidi ya miaka 120 baada ya Ashuru kuishinda Israeli (ufalme wa kaskazini), Yuda ilitekwa na taifa la Babeli. Wababeli waliangamiza mji na hekalu, na kuwachukua watu wengi wa Yuda kwenda Babeli kama watekwa.
## Yusufu (Agano Jipya) ### Ufafanuzi Yusufu alikuwa baba wa duniani wa Yesu na kumkuza kama mwanaye. Alikuwa mtu mwenye haki aliyefanya kazi kama seremala. Yusufu alikuwa amemchumbia binti wa Kiyahudi aitwaye Mariamu, ambaye Mungu alimchagua kuwa mama wa Yesu Masihi. Malaika alimuambia Yusufu kwamba Roho Mtakatifu alimsababisha Mariamu kuwa na mimba, na kwamba mtoto wa Mariamu alikuwa ni mwana wa Mungu. Baada ya Yesu kuzaliwa, malaika alimuonya Yusufu kumpeleka mtoto na Mariamu Misri ili kumtoroka Herode. Yusufu na familia yake waliishi katika mji wa Nazareti ya Galilaya alipojipatia kipato kwa kufanya kazi ya useremala.
## Yusufu (Agano la Kale) ### Ufafanuzi Yusufu alikuwa mwana wa kumi na moja wa Yakobo na mwana wa kwanza wa mama yake Raheli. Yusufu alikuwa mwana kipenzi wa baba yake. Ndugu zake walimuonea wivu na wakamuuza katika utumwa. Wakati akiwa Misri, alisingiziwa na kuwekwa gerezani. Licha ya mateso yake, Yusufu alibaki mwaminifu kwa Mungu. Mungu alimuweka katika nafasi ya pili ya madaraka katika Misri na kumtumia kuwaokoa watu katika kipindi ambapo kulikuwa na chakula kidogo. Watu wa Misri, pamoja na watu wake, waliepusha na njaa.
## Zabuloni ### Ufafanuzi Zabuloni alikuwa mwana wa mwisho wa Yakobo na Lea na ni jina la mojawapo wa makabila kumi na mbili ya Israeli * Waisraeli wa kabila la Zabuloni walikuwa wamepewa nchi magharibi ya Bahari ya Chumvi. * Wakati mwingine jina "Zabuloni" limetumika pia kurejerea nchi hii ambayo kabila hili la Waisraeli liliishi.
## Zakaria ### Ufafanuzi Zakaria alikuwa nabii aliyetabiri wakati wa utawala wa Mfalme Dario I wa Uajemi. Kitabu cha Zakari katika Agano la Kale kina unabii wake, ambacho kinawasihi mateka waliorudi kulijenga tena hekalu. * Nabii Zakaria aliishi wakati mmoja na Ezra, Nehemia, Zerubabeli na Hagai. Alitajwa na Yesu kama nabii wa mwisho kati ya wale waliouawa katika nyakati za Agano la Kale. * Mtu mwingine mwenye jina la Zakaria alikuwa bawabu katika hekalu wakati wa Daudi. * Mmoja wa wana wa Mfalme Yehoshafati aliyeitwa Zakaria aliuliwa na Yehoramu nduguye. * Zakaria alikuwa kuhani aliyeuawa kwa kupigwa mawe na watu wa Israeli alipowakemea kwa ibada yao ya sanamu. * Mfalme Zakaria alikuwa mwana wa Yeroboamu na alimiliki juu ya Israeli kwa miezi sita tu kable ya kuuawa.
## Zakaria (Agano Jipya) ### Ufafanuzi Katika Agano Jipya, Zakaria alikuwa kuhani wa kiyahudi aliyekuja kumzaa Yohana Mbatizaji. * Zakari alimpenda Mungu na kumtii. * Zakari na Elsabethi mkewe waliomba miaka mingi kwa uaminifu ili wapate mtoto lakini hawakupata. Lakini Mungu alijibu maombi yao wakiwa wazee, kwa kuwapa mtoto. * Zakaria alitabiri kuwa Yohana mwanawe angekuwa nabii ambaye angetangaza na kuandaa njia ya Masiya.
## Zakayo ### Ufafanuzi Zakayo alikuwa mtoza ushuru katika mji wa Yeriko aliyepanda katika mti ili aweze kumwona Yesu aliyekuwa amezungukwa na kundi kubwa la watu. * Zakayo alibadilishwa kabisa alipomwamini Yesu. * Alitubu dhambi yake ya kuwaibia watu na kuahidi kuwapa masikini nusu ya mali yake. * Aliahidi pia kwamba angewarudishia mara nne watu aliokuwa amewatoza zaidi.
## Zebedayo ### Ufafanuzi Zebedayo alikuwa mvuvi kutoka Galilaya anayejulikana kwa sababu ya wanawe, Yakobo na Yohana, waliokuwa wanafunzi wa Yesu. Hawa wamekuwa wakitajwa katika Agano Jipya kama "wana wa Zebedayo." * Wana wa Zebedayo walikuwa wavuvi pia na walifanya naye kazi ya kuvua samaki. * Yakobo na Yohana waliacha kazi yao ya kuvua na Zebedayo baba yao na wakamfuata Yesu.
## Zefania ### Ufafanuzi Zefania, mwana wa Kushu, alikuwa nabii aliyeishi Yerusalemu na kutabiri wakati wa utawala wa Mfalme Yosia. Aliishi wakati mmoja na Yeremia. * Aliwakemea watu wa Yuda kwa kuabudu miungu ya uongo. Unabii wake umeandikwa katika kitabu cha Zefania katika Agano la Kale. * Kulikuwa na watu kadhaa katika Agano la Kale wenye jina Zefania, wengi wao wakiwa makuhani.
## Zerubabeli ### Ufafanuzi Zerubabeli lilikuwa jina la Waisraeli wawili katika Agano la Kale. * Mmoja wao alikuwa mzao wa Yehoyakimu na Sedakia. * Zerubabeli mwingine, mwana wa Shealitieli, alikuwa kiongozi wa kabila la Yuda wakati wa Ezra na Nehemia, Koreshi mfalme wa Uajemi alipowaacha huru Waisraeli kutoka katika utumwa wao huko Babeli. * Zerubabeli na Yoshua kuhani mkuu walikuwa miongoni mwa waliohusika kujenga upya hekalu na madhabahu ya Mungu.