Kiswahili: translationWords

Updated ? hours ago # views See on DCS

Other

Adui

Ufafanuzi

"Adui" ni mtu au kundi lililo kinyume na mtu au kitu fulani.

  • Adui ni mtu ambaye anajaribu kukupinga au kukudhuru.
  • Taifa linaweza kuitwa adui linapopigana na taifa jingine.
  • Kwenye Biblia Ibilisi ni adui.

## agano jipya ### Ufafanuzi Neno "agano jipya" la husu kujitolea au makubaliano Mungu aliyo fanya na watu wake kupitia dhabihu ya Mwanae, Yesu. * "agano jipya" la Mungu linaelezwa sehemu ya Biblia itwayo "Agano Jipya" * Hili agano jipya ni kinyume na lile la "kale" au "zamani" ambalo Mungu alifanya na Waisraeli katika Agano la Kale. * Agano jipya ni bora kuliko la kale kwasababu lina husu dhabihu ya Yesu, lilo patanisha dhambi za watu milele. * Mungu ana andika agano jipya ndani ya mioyo ya waamini wa Yesu. Hii ina sababisha wao kutii Mungu na kuishi maisha matakatifu. * Agano jipya litatimia siku za mwisho ambapo Mungu ataweka utawala wake duniani.
## agizo ### Ufafanuzi Agizo ni sharti au sheria ya hadhara inayo toa amri au maelekezo ya watu kufuata. Hili neno lina maana sawa na "kisimika" * Wakati mwingine agizo ni pokeo lilo imarishwa kwa miaka ya kulifanyia zoezi. * Katika Biblia, agizo lilikuwa kitu ambacho Mungu aliamuru Waisraeli kufanya. Wakati mwingine aliwaamuru kufanya milele.
## Ahadi ### Ufafanuzi "Ahadi" hii ni ya kuweka matumaini ya kufanya kitu au kutoa kitu. * Katika agano la kale viongozi wa Israeli waliweka ahadi ya kuwa waaminifu kwa mfalme Daudi. * Kitu kitakachotolewa kama ahadi kitarudishwa kwa mmiliki wake muda ambao ahadi hiyo itatimizwa. * Ahadi pia yaweza kutafsiriwa kama "kufanya rasmi" au "kuahidi kwa nguvu." * Pia ahadi yaweza kuwa kifaa kinachotolewa kama ahadi kwamba deni litalipwa.
## aibisha, ya kuaibisha ### Ufafanuzi Msemo wa "aibisha" una maana ya kufanya kitu ambacho si cha heshima kwa mtu. Hii inaweza pia kumsababishia mtu huyo aibu au fedheha. Msemo "ya kuaibisha" inaelezea tendo ambalo ni la aibu au litasababisha mtu kupungukiwa na sifa. Mara nyingine "kuabisha" inatumika kumaanisha vyombo ambavyo havina kazi kwa jambo lolote muhimu. Watoto wanaamuriwa kuwaheshimu na kuwatii wazazi wao. Pale ambapo watoto hawatii, wanakuwa hawaheshimu wazazi wao. Wanawafanya wazazi wao kwa njia ambayo haiwapi heshima kwao. Waisraeli walipunguza sifa kwa Yahwe walipoabudu miungu ya uongo na kutenda mwenendo muovu. Wayahudi hawakumheshimu Yesu kwa kusema ya kwamba alikuwa amepagawa na pepo. Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutoheshimu" au "kutenda bila heshima. Nomino ya "kutoheshimu" inaweza kutafsiriwa kama "kutoheshimu" au "kupotea kwa sifa". Kutegemea na muktadha, "ya kuaibisha" inaweza kutafsiriwa kama "siyo na heshima" au "ya aibu" au "haifai" au "haina thamani".
## aibu, fedhehesha ### Ufafanuzi Msemo "aibu" una maana ya kupotea kwa utukufu na heshima. Mtu anapofanya jambo la dhambi, inaweza kumsababisha awe katika hali ya aibu au kupoteza heshima. Msemo "fedhehesha" unatumika kuelezea tendo la dhambi au mtu aliyeifanya.. Mara nyingine mtu anayefanya mambo mema anatendewa kwa njia ambayo inamsababishia mtu fedheha au aibu. Kwa mfano, Yesu alipouwawa msalabani, hii ilikuwa njia ya fedheha kufa. Yesu hakufanya jambo lolote baya kustahili fedheha hii. Njia za kutafsiri "fedheha" zinaweza kujumuisha "aibu" au "kutokuwa na heshima. Njia za kutafsiri "fedhehesha" zinaweza kujumuisha "aibu" au kutokuwa na heshima.
## aina ### Ufafanuzi Neno "aina" linamaanisha makundi ya vitu vilivyoungana kwa kugawana tabia. Katika Biblia, usemi huu unatumika bayana kumaanisha aina tofauti za mimea na wanyama ambao Mungu alivyotengeza alipoumba ulimwengu. Mara nyingi kuna tofauti nyingi za spishi katika kila "aina." Kwa mfano, farasi, punda milia, na punda zote ni sehemu ya "aina" moja lakini ni spishi tofauti. Kitu kikuu kinachotofautisha kila "aina" kama kundi tofauti ni kwamba kila mmoja wa hilo kundi anaweza kuzaa zaidi wa "aina" hiyo. Viumbe wa aina tofauti hawawezi kufanya hivyo pamoja.
## Amani ### Ufafanuzi Amani ni kitendo cha kutokuwa na migogoro au hofu. Mtu mwenye amani anahisi shwari na ana uhakika wa kuwa salama. * Amani pia inaweza kuelezewa kama kipindi ambacho kundi la watu au nchi hawapo katika vita na watu wengine. Watu hawa wanasemwa kuwa na "mahusiano ya amani. * "Kutengeneza amani" na watu au kundi la watu linamaanisha kuchukua hatua ya kusababisha ugonvi uishe. * "mtengeneza amani" ni mtu anayefanya kitu au kusema kitu ili kuwashawishi watu waishi kwa amani na watu wengine. * Kuwa na amani na watu wengine inamaanisha kuwa katika hali ya kutogombana na watu hao. * Uhusiano mzuri kati ya Mungu na wanadamu hutokea pale ambapo Mungu aliwaokoa watu toka kwenye dhambi zao. Hii inaitwa kuwa na amani na Mungu. * Salamu "neema na amani" ilitumiwa na mitume katika barua zao kwa waamini aka baraka. * Amani pia inaweza kuonesha kuwa katika mahusiano mazuri na watu wengine au na Mungu.
## amri ### Ufafanuzi Amri ni tamko au sheria ambayo inatolewa kwa umma kwa watu wote. Sheria za Mungu pia zinajulikana kama makataa, maagizo au amri. Kama sheria na amri, makataa lazima yanapaswa kufuatwa. Mfano wa makataa ya mtawala wa kibinadamu ulikuwa ni tangazo la Kaisari Augusto ya kwamba kila mmoja aliyeishi katika milki ya Roma alipaswa kurudi nyumbani kwake ili ahesabiwe katika sensa. Kutoa amri juu ya jambo ina maana ya kutoa amri ambayo ilikuwa lazima kuitii. Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kuamuru" au "kuamrisha" au "kutaka rasmi" au "kuweka sheria kwa umma". Jambo linalofanywa kuwa "amri" kufanyika ina maana ya kwamba "lazima ifanyike" au "imeamuliwa na haitabadilishwa" au "kutamkwa kwa uhakika ya kuwa itafanyika"
## amri ### Ufafanuzi Amri ni sheria maalumu iliyo andikwa inayo toa muongozo watu kuishi. * Neno "amri" ni swa na "agizo" au "tamko" au "sheria." * Mfalme Daudi alisema alifurahia amri za Yahweh. * Neno "amri" la weza tafsiriwa "amri maalumu" au "tamko maalum."
## Amri kumi ### Ufafanuzi "Amri Kumi" zilikuwa amri ambazo Mungu alimpa Musa Mlima Sinai wakati Waisraeli waliishi jangwani wakiwa njiani kwenda nchi ya Kanani. Mungu aliandika hizi amri kwenye mawe makubwa mawili. * Mungu aliwapa Waisraeli amri nyingi za kutii, lakini Amri Kumi zilikuwa maalumu kuwasaidia Waisraeli kumpenda na kumuabudu Mungu na kupenda watu wengine. * Hizi amri pia zilikuwa sehemu ya agano la Mungu na watu wake. Kwa kumtii Mungu na aliyo waamuru kufanya, watu wa Israeli walionyesha kuwa wana mpenda Mungu na kuwa ni wao. * Amri kwenye mawe zilihifadhiwa katika Agano lililo kuwa pa takatifu zaidi mwa maskani na baadae, hekalu.
## Angalia, Mlinzi ### Ufafanuzi "Angalia" inamaanisha kuwa kutazama kitu kwa ukaribu na kwa makini. "Mlinzi" ni mtu ambaye kazi yake ni kuulinda mji kwa kuangalia kwa makini vyote vinavyomzunguka kama kuna hatari yoyote kwa watu wa mji ule. * Amri ya "angalia maisha yako na mafundisho kwa makini" inamaanisha kuwa ishi kwa makini na usiamini mafundisho ya uongo. * "Angalia" ni onyo la kuwa makini ili kukwepa hatari au ushawishi wa hatari. * "Angalia" inamaana ya kuwa makini dhidi ya dhambi na uovu. * Neno lingine la mlinzi ni mlindaji.
## angika au nyonga ### Ufafanuzi Neno hili nyonga au angika lina maana ya ninginiza au tundika kitu au mtu. kifo cha kunyongwa au kujinyonga hufanyika kwa kutumia kamba ambayo mtu humfungwa shingoni na kumning'niza kwa kitu kilicho juu kama vile mti. Yuda alijiua mwenyewe kwa kujinyonga. Kifo cha Yesu kwa kuangikwa kwenye msalaba wa mbao kilifanyika kwa utofauti: askari walimtundika Yesu kwa kumpigilia misumali miguuni na mikononi katika msalaba. kuangika au kunyonga mtu mara zote ni njia ya kumwua mtu kwa kumnyonga kwa kutumia kamba inayofungwa shingoni mwa mtu.
## Asali, sega la asali ### Ufafanuzi Asali ni kimiminika kitamu kinachotengenezwa na nyuki kutokana na maua. Sega ni fremu ya nta ambayo nyuki hutumia kutunzia asali. Asali inaweza kuwa na rangi ya njano au kikahawia kutegemea na aina. Asali yaweza kupatikana mstuni hasa katika mashimo ya miti au mahali popote ambapo nyuki zaweza kuweka makao. Watu pia hutunza asali katika mizinga ili kuzalisha asali za kula au kuuza, lakini huenda asali inayotajwa kwenye Biblia ni asali ya msituni. Biblia inawataja watu watatu walioishi kwa kula asali, watu hawa ni Yonathani, Samsoni na Yohana Mbatizaji. Neno hili 'asali' hutumika pia kimfano kumaanisha kitu kitamu au kitu cha kustarehesha. Mfano, Maneno na sheria za Mungu husemwa kuwa ni tamu sana kuliko asali. Wakati mwingine maneno ya mtu yanaweza kusemwa kuwa ni matamu kama asali, lakini matokeo yake huwa ni udanganyifu na kuwaumiza watu wengine.
## asiye amini, kuto amini ### Ufafanuzi Neno "kuto amini" la eleza kuto kuwa na imani ya kitu au mtu. * Katika Biblia, "kuto amini" kwa eleza kuto mwamini au kuto mtegemea Yesu kama mwokozi mmoja. * Mtu asiye mwamini Yesu anaitwa "asiye amini."
## Balozi, mwakilishi ### Ufafanuzi Balozi ni mtu aliyechaguliwa rasmi kuwakilisha nchi yake katika mataifa ya kigeni. Mara nyingine hutafsiriwa kama mwakilishi. * Balozi au mwakilishi huwapa watu ujumbe aliopewa na mtu au serikali iliyomtuma. * "Mwakilishi" ni yule aliyepewa mamlaka ya kufanya au kuzungumza kwa niaba ya yule anayemwakilisha. * Mtume Paulo anawafundisha Wakristo kuwa ni mabalozi wa Kristo au wawakilishi kwa kuwa wanamwakilisha Kristo duniani na kuwafundisha wengine ujumbe huu.
## barua, waraka ### Ufafanuzi Barua ni ujumbe wa kuandikwa unaotumwa kwa mtu au kundi la watu ambaokwaida wako mbali kutoka kwa mwandishi. Waraka ni barua maalum, mara nyingi huandikwa kwa njia rasmi, kwa kusudi maalum, kama kufundisha. Katika nyakati za Agano Jipya, waraka na aina zingine za barua ziliandikwa kwenye kartasi zilizotengenezwa kwa ngozi ya wanyama au kwenye karatasi za mafunjo ilitengenezwa kutoka kwenye ufumwele wa mimea. Nyaraka za Agano Jipya kutoka kwa Paulo, Yohana, Yakobo, Yuda na Petro ni barua za maelekezo walizoandika kuwatia moyo, kuwasihi, na kuwafundishia Wakristo wa kwanza katika miji tofauti katika ufalme wa Rumi. Njia za kutafsiri hili neno ni pamoja na, "ujumbe wa kuandikwa" au " maneno yalioandikwa" au "maandishi."
## Bibi harusi ### Ufafanuzi Bibi harusi ni mwanamke ambaye katika sherehe ya harusi anaolewa kwa mmewe, ambaye ni bwana harusi. * Neno "bibi harusi" linatumika kama sitiari kwa wanaomwanini Yesu, Kanisa. * Kwa sitiari Yesu anaitwa "bwana harusi" kwa ajili ya Kanisa.
## Bikira ### Ufafanuzi Bikira ni mwanamke ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya ngono. * Nabii Isaya alisema kuwa Masihi atazaliwa na bikira. * Mariamu alikuwa Bikira alipokuwa na mimba ya Yesu. Yesu hakuwa na baba wa kibinadamu. * Lugha nyingine zaweza kuwa na neno zuri badala ya neno bikira.
## Bure, ubatili ### Ufafanuzi Neno "bure" linaelezea kitu ambacho hakina maana au hakifai. Vitu vilivyo bure ni vitu tupu au vitu visivyo na maana. * Ubatili ni kitu ambacho hakifai au kipo tupu. Pia yaweza kuwa na maana ya kiburi au madaha. * Katika agano la kale sanamu zilielezewa kama vitu vya bure visivyoweza kuokoa au kukomboa. Havina kazi wala maana. * Kama kitu kilifanywa pasipo na maana hata matokeo yake sio mazuri. * Kuamini katika kitu kilicho tupu na maana ni kuamini katika kitu kisicho cha kweli na kinachokupa matumaini ya uongo.
## Busara ### Ufafanuzi Neno "busara" humuelezea mtu anayefikiri kwa makini kuhusu matendo yake na kufanya maamuzi ya hekima. * Busara ni uwezo wa kufanya maamuzi ya hekuma kuhusu mambo ya kimwili kama matumizi mauri ya pesa au mali. * Japokuwa busara ya hekuma vina maana sawa lakini hekima ni kwa ujumla zaidi na imelenga hasa mambo ya kiroho.
## Busu ### Ufafanuzi Busu ni tendo ambalo mtu mmoja anaweka mdomo wake juu ya mdomo wa mwingine au uso. Msemo huu unaweza pia kutumika kitamathali. Tamaduni zingine hubusiana kwenye shavu kama ishara ya salamu au kuaga. Busu linaweza kupitisha ujumbe wa upendo mkubwa kati ya watu wawili, kama mme na mke. Usemi "kumbusu mtu kwaheri" inamaanisha kumuagamtu kwa busu. Wakati mwingine neno "busu" linatumika kumaanisha "kusema kwaheri kwa." Wakati Elisha aliposema kwa Eliya, "Niache niende kumbusu baba na mama yangu," alitaka kuwaaga wazazi wake kabla yakuwaacha na kumfuata Eliya.
## Bwana ### Ufafanuzi Neno "Bwana" linamaanisha mtu anayemiliki na mwenye mamlaka juu ya watu wengine. Inapokuwa na herufi kubwa, ni jina linalomaanisha Mungu. (Noti hata hivyo inapotumika kama njia ya kumtambua mtu mwanzo mwa sentesi inaweza kuwa na herufi kubwa na kuwa na maana ya "mkuu.") Katika Agano la Kale, msemo huu pia unatumika maneno kama, "Bwana Mungu Mkuu" au "Bwana Yahwe" au "Yahwe Bwana wetu." Katika Agano Jipya, mitume walitumia neno hili katika misemo kama, "Bwana Yesu" na "Bwana Yesu Kristo," illiyoonyesha kuwa Yesu ni Mungu. Neno "Bwana" katika Agano Jipya pia linatumika peke yake kama njia ya moja kwa moja ya kumtambua Mungu, hasa katika nukuu za kutoka Agano la Kale. Kwa mfano, maandishi ya Agano la Kale ya, "Amebarikiwa ajaye kwa jina la Yahwe" na Agano Jipya lina, "Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana." Katika ULB na UDB, jina "Bwana" linatumika tu kutafsiri maneno halisi ya Kihebrania na Kigriki yanayomaanisha "Bwana." Halitumiki kama tafsiri ya jina la Mungu (Yahwe), kama inavyofanywa na tafsiri zingine.
## Bwana harusi ### Ufafanuzi Bwana harusi ni mtu anayemwoa bibi arusi katika sherehe ya harusi. * Katika utamaduni wa Kiyahudi nyakati za Biblia, sherehe iliwekwa siku ambayo bwana arusi alikuja kumchukua bibi harusi wake. * Katika Biblia, kwa kutumia tamathari ya semi, Yesu anaitwa "Bwana harusi" atakayetuijia siku moja "Bibi harusi wake," kanisa. * Yesu aliwafananisha thenashara na rafiki za Bwana harusi wanaosherehekea bwana harusi anapokuwa pamoja nao, lakini wanahuzunika anapoondoka.
## chafu ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "chafu" utumika kama fumbo kueleza vitu ambavyo Mungu alitangaza sio sahihi kwa watu wake kugusa,kula, au kutoa dhabihu. * Mungu aliwapa Waisraeli maelekezo kuhusu mnyama yupi alikuwa "msafi" na yupi alikuwa "mchafu." Wanyama wachafu hawakuruhusiwa kutumika kula au kutolea dhabihu. * Watu wenye aina fulani ya ugonjwa wa ngozi walisemekana kuwa "wachafu" mpaka walipo ponywa. * Waisraeli kama walipo shika kitu "kichafu" wao wenyewe walihesabika kuwa wachafu kwa kipindi cha muda fulani. * Kutii amri za Mungu kuhusu kutogusa au kula vitu vichafu kuliwatenga Waisraeli kwa huduma ya Mungu. * Hii hali ya uchafu wa mwili na mila ilikuwa ishara ya uchafu wa kijamii. * Maana nyingine ya fumbo, "roho chafu" ina eleza pepo.
## chemchem, kisima ### Ufafanuzi Msemo wa "chemchem" na "kisima" mara kwa mara una maana ya kiasi kikubwa cha maji ambacho kinatiririka kiasili kutoka kwenye ardhi. Maneno haya yanatumika kitamathali katika Biblia kumaanisha baraka inayotiririka kutoka kwa Mungu au kumaanisha kitu ambacho kinasafisha au kutakasa. Katika muda wa sasa, chemchem mara nyingi ni chombo kilichoundwa na mtu ambacho kina maji yakitiririka kutoka kwake, kama vile chemchem ya maji ya kunywa. Hakikisha ya kwamba tafsiri ya msemo huu una maana ya chanzo cha asili ya maji yanayotiririka. Fananisha tafsiri ya msemo huu na jinsi msemo "mafuriko" unavyotafsiriwa.
## chinja, chinjwa ### Ufafanuzi Neno "chinja" lina maana ya kuua mtu au mnyama. Mara nyingi ina maana ya kuua kwa vita au vurugu. * Neno "ua" la weza pia tumika kutafsiri hili neno. * Maneno "waliyo chinjwa" ya weza pia tumika kutafsiri "watu waliyo chinjwa" au "watu waliyo uawa."
## Chochea ### Ufafanuzi Neno "kuchochea" linamaanisha kumsababisha mtu apate hisia hasi. * Kumchochea mtu kwenye hasira inamaanisha kufanya kitu kitakachosababisha mtu huyo apate hasira. Hii inaweza kutafsiriwa kama "kumsababishia mtu apate hasira." * Unapokutana na maneno kama "usimchochee " maneno haya yaweza kutafsiriwa kama "usimsababishie hasira."
## chui ### Ufafanuzi Chui ni mnyama pori mkubwa kama paka, mwenye rangi ya kahawa na madoa meusi. Chui ni aina ya mnyama anayeshika wanyama wengine na kuwala. Katika Biblia, ughafla wa maafa unalinganishwa na chui anaye shambulia mawindo yake ghafla. Nabii Danieli na mtume Yohana wanazungumzia maono ambayo waliona mnyama aliyefanana na chui.
## chukiza, chukia ### Ufafanuzi Msemo "chukiza" unaelezea jambo ambalo linapaswa kutopendwa na kukataliwa. "Kuchukia" kitu ina maan ya kutokipenda kabisa. Mara nyingi Biblia huzungumzia kuhusu kuchukia uovu. Hii ina maana kuchukia uovu na kuukataa. Mungu alitumia neno "chukiza" kuelezea matendo maovu ya wale waliomwabudu miungu ya uongo. Waisraeli waliamriwa "kuchukia" matendo ya dhambi, na kinyume na maadili ambayo baadhi ya makundi ya watu majirani waliyafanya. Mungu aliyataja matendo yote ya uasherati kuwa "chukizo". Uaguzi, uchawi, na sadaka za mtoto yote yalikuwa "chukizo" kwa Mungu. Msemo "chukizo" unaweza kutafsiriwa kama "uovu mbaya" au "inayochukiza" au "inayostahili kukataliwa". Inapotumika na kiumbe takatifu "chukizo kwa" waovu, hii inaweza kutafsiriwa kama "kuchukuliwa kutotamanika kwa" au "kutokuwa na ladha" au "kukataliwa na" Mungu aliwaambia Waisraeli "kuchukia" aina kadhaa ya wanyama ambao Mungu alitamka kuwa "wachafu" na kutofaa kwa chakula. Hii inaweza kutafsiriwa kama "kuchukia kwa uzito" au "kukataa" au "kuchukua kama kutokubalika".
## dada ### Ufafanuzi Dada ni mtu wa jinsi ya kike anaye shiriki wastani wa mzazi mmoja na mtu mwingine. * Katika Agano Jipya, "dada" linatumika kimafumbo kumuelezea mwanamke aliye mwamini katika Yesu Kristo. * Wakati mwingine neno, "kaka na dada" linatumika kueleza waamini wote katika Kristo, wanaume na wanawake. * Katika cha Agano la kale cha, Nyimbo iliyo Bora, "dada" ina maana ya mpenzi.
## desturi ### Ufafanuzi Neno "desturi" la eleza tamaduni na mapokeo yaliyo tunzwa kwa muda na yanayo pokelewa na vizazi vijavyo. * Mara nyingi katika Biblia neno "desturi" la eleza mafundisho na mapokea watu waliyo fanya, sio amri za Mungu. Misemo "desturi za wanadamu" au "desturi za binadamu" inaeleza vizuri hii maana. * Maneno kama "desturi za wazee" au "desturi za baba zangu" ya maanisha tamaduni za Wayahudi na mapokeo viongozi wa kiyahudi kwa muda mrefu waliyo ongeza katika sheria ya Mungu kwa Waisraeli kupitia Musa. Ingawaje hizi desturi hazikutoka kwa Mungu, watu walidhani wana paswa kutii kuwa wenye haki. * Mtume Paulo pia utumia "desturi" katika maana tofauti kueleza mafundisho kuhusu mapokeo ya Kikristo yaliyo toka kwa Mungu na yeye na mitume wengine walifundisha waamini wapya.
## dhabihu, sadaka ### Ufafanuzi Katika Biblia, maneno "dhabihu" na "sadaka" ya husu zawadi maalumu anazopewa Mungu kama kitendo cha kumuabudu. Watu pia walitoa sadaka kwa miungu ya uongo. * Neno "sadaka" la husu chochote kinacho tolewa au kupewa. Neno "dhabihu" la husu kitu kinacho tolewa au kufanywa kwa gharama kubwa kwa mtoaji. * Sadaka kwa Mungu zilikuwa vitu maalumu alizo waamuru Waisraeli kutoa ili kuonyesha upendo na utii kwake. * Maneno ya sadaka tofauti, kama "sadaka ya kuteketeza" na "sadaka ya amani," ili hashiria aina gani ya sadaka ilitolewa. * Dhabihu kwa Mungu kulihusisha kuua mnyama. * Dhabihu peke yake ya Yesu, Mwana mkamilifu, asiye na dhambi, wa Mungu, anaweza kutakasa watu na dhambi. Mnyama hakuweza kufanya hivyo. * Mfano wa msemo "jitoeni kama dhabihu hai" ina maana, "ishi maisha yako kwa kumtii Mungu, kuacha kila kitu ili kuweza kumtumikia.
## dhahabu ### Ufafanuzi Dhahabu ni chuma cha manjano, cha ubora wa juu sana kinachotumika kutengeneza vito na vyombo vya dini. Ilikuwa chuma ya thamani zaidi katika kipindi cha zamani. Katika kipindi cha Biblia, aina nyingi tofauti ya vyombo vilitengezwa kwa dhahabu ngumu au kufunikwa na safu nyembamba ya dhahabu. Vyombo hivi vilijumuisha heleni na vito vingine, sanamu, madhabahu, na vyombo vingine vilivyotumika katika tabenakulo au hekalu, kama vile sanduku la agano. Katika Agano la Kale, dhahabu ilitumika kama njia ya kubadilishana katika kununua na kuuza. Ilipimwa juu ya mizani kupata thamani yake. Baadaye, dhahabu na vyuma vingine kama vile fedha vilitumika kutengeneza sarafu kutumiwa kununua na kuuza. Pale inapomaanisha kitu ambacho sio dhahabu ngumu, lakini ina safu nyembamba tu ya dhahabu, msemo "ya dhahabu" au "kufunikwa kwa dhahabu" inaweza kutumika. Mara nyingi chombo kinaelezewa kama "rangi ya dhahabu" ambayo ina maana ina rangi ya njano ya dhahabu, lakini haijatengenezwa kwa dhahabu.
## dhalimu, kwa dhalimu, udhalimu ### Ufafanuzi Maneno "dhalimu" na "kwa dhalimu" yanaeleza kutendea watu pasipo haki, na mara nyingi, namna ya kudhuru. * "Udhalimu" ni kitu kibaya kinacho fanywa kwa mtu asiye stahili. Inaeleza kufanyia watu pasipo haki. * Udhalimu pia una maana kuwa watu wengine wana tendewa vibaya wakati wengine wanatendewa vizuri. * Mtu anaye tenda kwa namna dhalimu ana kuwa na "upendeleo" au "ubaguzi" kwasababu hawatendei watu sawa.
## Dharau, kudharauliwa ### Ufafanuzi Dharau ni kitendo cha kutokuheshimu kinachooneshwa kwa mtu au kitu. Kitu kisichoheshimiwa kinaitwa kilichodharauliwa. * Mtu au tabia ambayo inaonesha kutokumuheshimu Mungu inaitwa kudharau. * Kushikilia katika dharau inamaanisha kumuona mtu kama asiye na thamani au kumuhukumu mtu kwa kumuona hana thamani. * Mfalme Daudi alipotenda dhambi ya uzingi na kuua Mungu alimwambia kuwa Daudi ameonesha "dharau" kwa Mungu. Hii inamaanisha kuwa amemdharau Mungu kwa kufanya hivyo.
## Dhifa ### Ufafanuzi Dhifa ni sherehe maalumu ya mlo ambayo kwa kawaida inahusisha aina tofauti ya vyakula. * Katika nyakati za kale, wafalme mara kwa mara waliandaa dhifa kuwaburudisha viongozi wa kisiasa na wageni wengine mhimu. * Hii yaweza pia kutafasiriwa kama, "mlo maalumu" au "sherehe mhimu" au "mlo wa mchanganyiko"
## dhihaki ### Ufafanuzi Neno kudhihaki ni kumtania mtu, kwa namna mbaya. * Kudhihaki mara kadha kuna husisha muingiza maneno ya watu au matendo kwa kusudi kuwaaibisha au kuonyesha kuchukizwa nao. * Wanajeshi wa Kirumi walidhihaki Yesu walipo mvalisha joho na kujifanya kumheshimu kama mfalme. * Kikundi cha vijana walimdhihaki Elisha walipo muita jina, wakimtania kichwa chake cha upara.
## dhiki ### Ufafanuzi Neno "dhiki" la husu kipindi cha ugumu, mateso, na msongo wa mawazo. * Agano Jipya lina sema kwamba Wakristo watavumilia kipindi cha mateso na dhiki tofauti kwasababu watu wengi ulimwenguni wana fahamu mafundisho ya Yesu. * Biblia inatumia neno "Dhiki kuu" kueleza kipindi cha Muda kabla ya Yesu kurudi mara ya pili amabapo gadhabu ya Mungu itamwaga duniani kwa miaka kadhaa. * Neno "dhiki" la weza tafsiriwa kama, "kipindi cha mateso sana" au "hali ngumu"
## Divai, kiriba, divai mpya ### Ufafanuzi Katika nyakati za Biblia "divai" ni kinywaji kilichotengenezwa na maji ya matunda yanayoitwa zabibu. Divai ilihifadhiwa kwenye viriba ambayo ni vyombo vilivyotengenezwa kwa ngozi ya wanyama. * Divai mpya ni maji ya zabibu ambayo hayajatolewa bado kwenye zabibu. * Kutengeneza divai zabibu hupondwa kwenye shinikizo na maji ya zabibu hutoka ndani yake. Maji haya huchachushwa na kuleo hutoka ndani yake. * Katika nyakati za Biblia divai kilikuwa kinywaji cha kawaida kikiambatana na mlo. Haikuwa na kilevi sana kama divai za wakati huu. * Kabla divai haijawekwa kwa ajili ya kutumika ilichanganywa na maji. * Viriba vilivyochakaa vilikuwa vimepasuka na kuruhusu divai kuvuja. Lakini viriba vupya havikuvuja na vilihifadhi divai vizuri.
## Dubu ### Ufafanuzi Dubu ni mnyama mkali mkubwa mwenye miguu minne na ana manyoa meusi, meno na makucha makali. Dubu walikuwa wamezoeleka katika Israeli nyakati za Biblia. * Wanyama hawa wanaishi misituni na katika maeneo ya milimani; wanakula samaki, wadudu, na mimea. * Katika Agano la Kale, dubu hutumika kama alama ya nguvu. * Wakati akichucha kondoo, Daudi kama mchungaji alipambana na dubu na kumshinda. * Dubu wawili walitoka msituni na kulishambulia kundi la vijana waliomdhihaki nabii Elisha.
## dunia, kidunia ### Ufafanuzi Msemo "dunia" una maana ya dunia ambayo wanadamu wanaishi, pamoja na kila aina ya viumbe hai. "Dunia" pia inaweza kumaanisha ardhi au udongo ambayo hufunika nchi. Msemo huu mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha watu wanaoishi juu ya dunia. Misemo, "acha dunia iwe na furaha" na "Atahukumu dunia" ni mifano ya matumizi ya tamathali ya msemo huu. Msemo "kidunia" mara kwa mara humaanisha vitu vya kimwili kinyume na vitu vya kiroho. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo huu unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao lugha ya taifa hutumia kumaanisha sayari ya dunia ambayo tunaishi. Kulingana na muktadha, "dunia" pia inaweza kutafsiriwa kama, "ulimwengu" au "ardhi" au "udongo". Unapotumika kitamathali, "dunia" inaweza kutafsiriwa kama, "watu wa dunia" au "watu wanaoishi juu ya dunia" au "kila kitu juu ya dunia". Njia za kutafsiri "kidunia" zinaweza kujumuisha, "kimwili" au "vitu vya dunia hii" au "vinavyoonekana".
## elekeza, maelekezo ### Ufafanuzi Usemi "elekeza" na "maelekezo" yanamaanisha kutoka uongozo bayana ya nini cha kufanya. "Kutoa maelekezo" inamaanisha kumuambia mtu bayana kitu anachotakiwa kufanya. Yesu alipowapa wanafunzi wake mikate na samaki kuwapa watu, aliwapa maelekezo bayana ya jinsi ya kuifanya. Kulingana na mazingira, neno "elekeza" inaweza kutafsiriwa kama "kumuambia" au "kuongoza" au "kufundisha" au "kutoa maelekezo kwa." Neno "maelekezo" inaweza kutafsiriwa kama "uongozo" au"ufafanuzi" au "kitu alichokuambia kufanya." Mungu akikupa maelekezo, huu usemi wakati mwingine unatafsiriwa kama "kuamuru" au "kuamrisha."
## erevu ### Ufafanuzi Neno "erevu" la elezea mtu enye akili na mahiri, hususani katika mambo ya utendaji. * Mara kadhaa "erevu" lina maana hasi kwa sehemu tangu linatumika kuonyesha ubinafsi. * Mtu erevu mara nyingi anaji tazama yeye, sio wengine.
## fagia ### Ufafanuzi Neno "fagia" mara nyingi ueleza maana pana, ya kuondoa kwa haraka uchafu kwa kutumia ufagio. * Neno "fagia" linatumika kifumbo kueleza jinsi jeshi linavyo shambulia kwa wepesi, umakini. * Kwa mfano, Isaya alitabiri kuwa wa Assiria wata "fagia" Ufalme wa Yuda. Hii ina maana wa haribu Yuda na kukamata watu wake. * Neno "fagia" lina weza kuleza maji yanayo tiririka ya navyo sukuma vitu na kuondoa.
## fahamu, ufahamu ### Ufafanuzi Neno "fahamu" lina maana ya kusikia ua kupokea taarifa na kuelewa ina maana gani. * Neno "ufahamu" lina weza eleza "maarifa" au "hekima" au kutambua jinsi ya kufanya kitu. * Kumfahamu mtu inaweza maanisha kujua jinsi huyo mtu ana jihisije. * Wakati wakutembea kwenye njia ya Emao, Yesu alisababisha kufahamu maana ya maandiko kuhusu Mesiya. * Kulingana na muktadha, neno "fahamu" la weza tafsiriwa kama "jua" au "amini" au "elewa" au "jua nini kitu kinavyo maanisha." * Mara nyingi neno "ufahamu" la weza tafsiriwa kama "maarifa" au "hekima" au "upeo."
## Faida ### Ufafanuzi Kwa ujumla "faida" ni kitendo cha kupata kitu kizuri kwa kufanya jambo fulani au kitu fulani kizuri ambacho mtu anakipata. Kitu kina faida kwa mtu ikiwa kinaleta mambo mazuri au kinasaidia kuleta mambo mazuri kwa watu wengine. * Mara nyingi faida inamaanisha pesa inayopatikana baada ya kufanya biashara. Biashara ina faida ikiwa inaongeza pesa zaidi ya zilizotumika. * Matendo yana faida ikiwa yanasababisha mambo mazuri kwa watu. * 2 Timotheo 3:16 maandiko yanazungumza kuwa kuna faida ya kumsahihisha mtu au kumfundisha mtu katika haki. Hii inamaanisha kuwa mafundisho ya Biblia yana faida na yanasaidia kufundisha watu kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu.
## familia ### Ufafanuzi Msemo "familia" una maana ya kundi la watu ambao wana uhusiano wa damu na mara nyingi hujumuisha baba, mama, na watoto wao. Mara kwa mara pia hujumuisha ndugu wengine kama babu na bibi, wajukuu, wajomba na shangazi. Familia ya Kiebrania ilikuwa jamii ya kidini inayopitisha utamaduni kupitia ibaada na maagizo. Mara kwa mara baba alikuwa mwenye mamlaka ya familia. Familia pia inaweza kujumuisha watumishi, masuria, na hata wageni. Baadhi ya lugha zina neno pana kama vile "ukoo" au "nyumba" ambayo litafaa zaidi kwa muktadha ambapo zaidi ya wazazi na watoto wanatajwa. Msemo "familia" pia unatumika kumaanisha watu ambao wana uhusiano wa kiroho, watu kama hawa ambao ni sehemu ya familia ya Mungu kwa sababu wanmwamini Yesu.
## Faraja, mfariji ### Ufafanuzi Faraja ni kumsaidia mtu anayeteseka kimwili au kihisia. * Mtu anayefariji anaitwa mfariji. * Katika agano la kale faraja imetumika kuelezea namna ambavyo Mungu anavyowajali na kuwapenda watu wake na kuwasaidia wanapoteseka. * Katika agano jipya inasema kuwa Mungu atawafariji watu wake kwa kupitia roho mtakatifu. Wale waliopokea faraja wanauwezo wa kutoa faraja kwa wanaoteseka. * "Mfariji wa Israeli" ni Masihi aliyekuja kuwaokoa watu wake. * Yesu anamuelezea roho mtakatifu kama mfariji anayewasaidia wanaomwamini Yesu.
## Farasi ### Ufafanuzi Farasi ni mnyama mkubwa mwenye miguu minne ambaye katika kipindi cha Biblia alitumiak katika kufanya kazi za shambani na katika usafirishaji. Baadhi ya farasi walitumika katika kuvuta gari, na wengine walipandwa na mpanda farasi binafsi. Farasi walivalishwa hatamu katika vichwa vyao ili waweze kuongozwa Katika Biblia, farasi walihesabiwa kama mali ya thamani, na kipimo cha utajiri, hasa hasa kwa ajili ya matumizi yake katika vita. Wanyama walikuwa wanafanana na farasi ni punda.
## fedha ### Ufafanuzi Fedha ya ng'aa, ni ya chuma ya kijivu inayo tumika kufanya sarafu, mikufu, vyombo, na mapambo. * Vyombo ni pamoja na vikombe vya fedha na mabakuli, miongoni mwa vitu vingine vinavyo tumika kupikia, kulia, au kutumikia. * Fedha na dhahabu vilitumika kujenga maskani na hekalu. * Kipindi cha Biblia, sarafu za fedha na fedha nzito zilizo itwa shekeli zilitumika. * Kaka yake Yusufu alimuuza kama mtumwa kwa shekeli ishirini za fedha. * Yuda alilipwa sarafu thelathini za fedha kumsaliti Yesu.
## fedhehesha. fedheha ### Ufafanuzi Neno 'fedhehesha' lina maana ya kumfanya mtu aaibike au adhalilike. Hii ni kwasababu mara kwa mara hufanyika hadharani. Tendo la kumwaibisha mtu huitwa " fedheha." KIpindi ambacho Mungu humshusha mtu, humaanisha kwamba Mungu humfanya mtu apate mambo mabaya ili kumsaidia mtu aachane na kiburi. Hii ni tofauti na kumdhalilisha mtu, maana fedheha ni kitendo ambacho hufanywa ili kumuumiza mtu. Kumfedhehesha mtu yaweza kutafsiriwa kama 'kumwaibisha' au kumdhalilisha mtu. kuna njia nyingi za kutafsiri neno 'fedheha' kwa kutegemea na Muktadha. Maneno kama 'udhalilishaji' na aibu,''
## filimbi, zumari ### Ufafanuzi Katika kipindi cha Biblia, zumari ilikuwa vyombo vya muziki iliyotengenezwa kwa mfupa au mbao na mashimo inayoruhusu sauti kutoka nje. Filimbi ilikuwa aina ya zumari. Zumari nyingi ilikuwa na matete yaliyotengenezwa kutoka kwa nyasi nene ambayo hutikisika pale hewa inapopulizwa kwake. Zumari bila matete mara kwa mara ilijulikana kama "filimbi". Mfugaji alicheza filimbi kutuliza mifugo yao ya kondoo. Zumari na filimbi ilitumika kucheza muziki wa huzuni na furaha.
## Fimbo ### Ufafanuzi Fimbo hiki ni kifaa chembamba kama fimbo kinachotumika kwa njia mbali mbali. * Fimbo ya mbao inatumiwa na mchungaji kuwalinda kondoo dhidi ya wanyama wengine. Pia kwa ajili ya kumrejesho katika kundi kondoo anayetangatanga. * Katika Zaburi ya 23 mfalme Daudi anatumia maneno fimbo na gongo kuelezea mwongozo wa Mungu na nidhamu kwa watu wake. * Fimbo ya mchungaji pia ilitumika kuhesabia mifugo. * Pia fimbo ya chuma inaelezea adhabu ya Mungu kwa watu wanaomuasi na kufanya mambo maovu. * Hapo kale fimbo za kupimia zilizotengenezwa kwa chuma au mbao zilitumika kupimia urefu wa majengo. * Katika Biblia fimbo ya chuma inaelezea kifaa cha kumfundishia adabu mtoto.
## fimbo ya kifalme ### Ufafanuzi Neno "fimbo ya kifalme" ina husu gongo zuri linalo shikiliwa na mtawala, kama mfalme. * Fimbo hizi zilikuwa tawi la mbao lenye mapindo ya mapambo. Baadae fimbo za kifalme zilitengenezwa kwa vyuma vya dhahabu. * Fimbo ya kifalme ilikuwa alama ya ufalme na mamlaka iliyo hashiria heshima na ukuu wa mfalme. * Katika Agano la Kale, Mungu anaelezwa kuwa na fimbo ya haki. Hii ina husu Mungu kutawala kama mfalme wa watu wake. * Unabii wa Agano la Kale kuhusu Mesiya unamueleza kuwa kama mfano wa fimbo ambayo itakuja kutoka Israeli kutawala mataifa yote. * Hii yaweza tafsiriwa kama, "gongo la utawala" au "gongo la mfalme."
## fundisha, kufundisha, mwalimu, fundishwa ### Ufafanuzi Haya maneno "fundisha" na "kufundisha" yanaeleza kuambia watu wengine taarifa wasiyo ijua kabla. Mara nyingi maelezo utolewa rasmi au kwa utaratibu. * "mwalimu" ni mtu anaye fundisha. Kitenzi kilicho pita cha "fundisha" ni "fundishwa." * Yesu alipo kuwa ana fundisha, alikuwa anaeleza vitu kuhusu Mungu na ufalme wake. * Wanafunzi wa Yesu walimuita "Mwalimu" kama heshima ya mtu aliye wafundisha kuhusu Mungu. * Taarifa inayo fundishwa yaweza onyeshwa au kuelezwa. * Neno "mafundisho" inaeleza baadhi ya mafunzo kutoka kwa Mungu kuhusu yeye pamoja na maelekezo ya jinsi ya kuishi. * Maneno "kile ulicho fundishwa" yaweza tafsiriwa kama, "kile watu walicho kufundisha" au "Mungu alicho kufundisha," kulingana na muktadha.
## funga ### Ufafanuzi Msemo "kufunga" una maana ya kuacha kula chakula kwa kipindi fulani, kama vile siku moja au zaidi. Mara nyingi inajumulisha kutokunywa. Kufunga kunaweza kusaidia watu kumlenga Mungu na kuomba bila kutolewa mawazo kwa kuandaa chakula na kula. Yesu aliwalaani viongozi wa dini wa Kiyahudi kwa kufunga kwa sababu ambazo sio sahihi. Walifunga ili kwamba wengine wafikiri kuwa wao ni watakatifu. Mara nyingi watu walifunga kwa sababu walikuwa na huzuni sana au majonzi juu ya jambo. Kitenzi cha "kufunga" kinaweza kutafsiriwa kama "kujizuia kula" au "kutokula". Nomino ya "funga" inaweza kutafsiriwa kama "muda wa kutokula" au "muda wa kujizuia na chakula"
## funga ### Ufafanuzi Msemo "funga" una maana ya kufunga kitu kuzunguka kitu kingine. Mara kwa mara humaanisha kutumia mkanda kuzunguka kiuno kuweka kanzu au gwanda mahali pake. Msemo wa kibliblia unaojulikana, "funga kiuno" una maana ya kuchomekea chini ya vazi ndani ya mkanda kuruhusu mtu kusogea kwa uhuru zaidi, mara nyingi kufanya kazi. Msemo una maana ya kujiweka tayari kufanya kazi au kujiandaa kufanya kitu kigumu. Msemo "funga kiuno" unaweza kutafsiriwa kutumia msemo katika lugha husika yenye maana moja. Au inaweza kutafsiriwa bila tamathali kama "jiandae kwa ajili ya tukio" au "jiandae" Msemo "kufngwa na" inaweza kutafsiriwa kama "kuzungushwa na" au "kufungwa na".
## Furaha ### Ufafanuzi "Furaha" ni jambo ambalo linamfurahisha mtu sana na kuleta furaha kubwa. "Kufurahishwa" na jambo ina maana ya "kuwa na furaha" au "kufurahia juu ya" kitu. Pale ambapo kitu kinakubalika sana au kupendeza kinasemekana kama "furahisha". Kama furaha ya mtu ipo katika kitu ina maana ya kwamba anakifurahia sana. Msemo wa, "furaha yangu ipo katika sheria ya Yahwe" inaweza kutafsiriwa kama, "sheria ya Yahwe inanipa furaha kubwa" au "Ninapenda kutii sheria za Yahwe" au "Nina furaha kutii amri za Yahwe". Misemo "kufurahia" na "kuwa na furaha katika" inaweza kutafsiriwa kama "sifurahishwi kabisa na" au "sina furaha juu ya". Msemo "kufurahishwa mwenyewe na" ina maana, "anafurahia kufanya" kitu au "ana furaha sana juu ya" kitu au mtu. Msemo "hufurahia" una maana ya vitu ambavyo mtu hufurahia. Hii inaweza kutafsiriwa kama "starehe" au "vitu vinavyoleta furaha". Msemo kama wa, "Ninafurahi kufanya mapenzi yako" unaweza kutafsiriwa kama, "Ninafurahi kufanya mapenzi yako" au "Nina furaha sana ninapokutii".
## furaha, mwenye furaha ### Ufafanuzi Furaha ni hisia ya kupendezwa au kuridhika inayotoka kwa Mungu. Maana inayokaribiana, "mwenye furaha" inaelezea mtu anayejisikia vizuri sana na mwenye furaha nyingi. Mtu anasikia furaha anapokua anahisi kuwa anachopitia ni chema sana. Mungu ndiye anayegawa furaha ya kweli kwa watu. Kuwa na furaha hakutegemei hali nzuri. Mungu anaweza kuwapa watu furaha hata kama vitu vigumu kabisa vinatokea katika maisha yao. Sehemu zingine zinaelezwa kama za furaha, kama nyumba na miji. Hii inamaanisha kuwa watu waiishio humo ni wenye furaha.
## furahia sana, mwenye furaha ### Ufafanuzi Msemo "furahia sana" na "mwenye furaha" una maana ya kuwa na shangwe sana kwa sababu ya mafanikio au baraka maalumu. "Kufurahia sana" kunajumuisha hisia za kushangilia jambo zuri. Mtu anaweza kufurahia sana ndani ya wema wa Mungu. Msemo "mwenye furaha" unaweza kujumuisha kuwa na kiburi ndani ya hisia za furaha juu ya mafanikio au utajiri. Msemo "furaha sana" unaweza kutafsiriwa kama "kushangilia kwa furaha" au "kusifu na furaha kubwa". Kulingana na muktadha, msemo "mwenye furaha" unaweza kutafsiriwa kama "kusifu kwa kishindo" au "kushangilia na sifaf binafsi" au "kiburi"
## fuvu ### Ufafanuzi Neno "fuvu" la eleza kichwa cha mifupa kisicho na nyama cha mtu au mnyama
## Gari ### Ufafanuzi Zamani za kale magari yalikuwa mepesi, yenye matairi mawili yalioendeshwa na farasi. * Watu walikaa au kusimama katika magari, waliyatumia katika vita au safari. * Katika vita jeshi lenye magari lilikuwa na faida ya kuwa na kasi na uwezo juu ya jeshi ambalo halikuwa na magari. * Katika nyakati za Wamisri na Rumi walijulikana sana kwa kutumia farasi na magari.
## gavana, kutawala, mtawala, serikali ### Ufafanuzi "Gavana" ni mtu anayetawala mkoa, eneo au mahali. Neno "kutawala" lina maana ya koungoza au kusimamia watu. Msemo "mtawala" ilikuwa jina mahususi kwa gavana aliyetawala juu ya mkoa wa Kirumi. Katika kipindi cha Biblia, magavana waliteuliwa na mfalme au mfalme mkuu na walikuwa chini ya mamlaka yake. "Serikali" inaundwa na viongozi wote ambao wanatawala nchi au ufalme fulani. Watawala hawa hutengeza sheria ambazo huongoza tabia ya wanachi il kwamba kuwepo na amani, ulinzi, na mafanikio kwa watu wato wa taifa hilo.
## Gereza, mfungwa , jela ### Ufafanuzi Gereza nisehemu ambayo wahalifu huwekwa kama adhabu kwa uhalifu waliofanya. Mfungwa ni mtu anayewekwa gerezani. * Mtu anaweza kuwekwa gerezani akiwa anasubiria hukumu ya kesi. * Neno "kufungwa" inamaanisha "kuwekwa gerezani" au "kuwekwa kifungoni." * Manabii wengi na watumishi wengine wa Mungu waliwekwa gerezani japokuwa hawakufanya jambo lolote baya.
## geuka, geuka kando, geuka nyuma ### Ufafanuzi "Kugeuka" kuna maana ya kubadili mwelekeo wa mwili au kusababisha kitu kingine kubadilisha muelekeo. * Neno "geuka" pia la weza "kugeuka nyuma" kuangalia nyuma au kuelekea mwelekeo mwingine. * "Kugeuka nyuma" au "geuka mbali" kuna maana ya "kurudi nyuma" au "kwenda mbali" au "kusababisha kwenda mbali." * "Kugeuka mbali na" ina weza maanisha "kusimama" kutofanya kitu au kumkataa mtu. * "kugeuka kuelekea" mtu ina maana ya kumuangalia huyo mtu. * "Kugeuka na kuondoka" au "kugeuza mgongo wake kwa kuondoka" ina maana ya "kwenda mbali." * "Kugeuka na kurudia" ina maana ya "kuanza kufanya kitu tena." * "Kugeuka mbali kutoka" ina maana ya "kuacha kufanya kitu."
## Ghadhabu ### Ufafanuzi Ghadhabu ni hasira iliyopitiliza isiyoweza kuzuilika. Mtu anapokuwa na ghadhabu inamaana mtu anaonesha hasira yenye uharibifu. * Ghadhabu inatokea pale ambapo hasira inashindwa kuzuiliwa. * Unapotawaliwa na adhabu waweza kufanya au kutenda jambo lenye kuharibu. * Mataifa yenye hasira ni watu wasiomtii Mungu na kuasi dhidi yake. * Kujazwa na gahadhabu ni kuwa na hasira iliyopitiliza.
## Giza ### Ufafanuzi Msemo "giza" una maana ya kutokuwepo kwa nuru. Kuna maana kadhaa za kitamathali za msemo huu: Kama sitiari, "giza" ina maana ya "uchafu" au "uovu" au "upofu wa kiroho". Pia ina maana ya jambo lolote linalohusu dhambi au uharibifu wa maadili. Msemo, "mamlaka ya giza" una maana ya kila kilicho kiovu na kinachotawaliwa na Shetani. Msemo "giza" unaweza pia kutumika kama sitiari ya kifo. Watu wasiomjua Mungu wanasemekana kuwa "wanaishi gizani", ambayo ina maana hawaelewi au hawatenda haki. Mungu ni nuru (utakatifu) na giza (uovu) haliwezi kushinda nuru hiyo. Mahali pa adhabu kwa wale wanaomkataa Mungu mara nyingi hujulikana kama "giza la nje". Mapendekezo ya Tafsiri Ni bora kutafsiri msemo huu kihalisia, kwa neno la lugha ya mradi ambalo lina maanisha kutokuwepo kwa nuru. Huu unaweza kuwa msemo wenye maana ya giza la chumba ambalo halina mwanga au wakati wa siku ambapo hakuna mwanga. Kwa matumizi ya kitamathali, ni muhimu kuweka picha ya giza kwa kutofautisha na mwanga, kama njia ya kuelezea uovu na udanganyifu kulinganisha na wema na ukweli. Kutegemea na muktadha, njia zingine za kutafsiri hili zaweza kuwa, "giza la usiku"
## gongo ### Ufafanuzi Ngo ni fimbo ndefu ya mbao, utumika kama fimbo ya kutembelea. * Yakabo alipokuwa mzee, alitumia bakora kumsaidia kutembea. * Mungu aligeuza gongo la Musa kuwa nyoka kuonyesha nguvu yake kwa Farao. * Wachungaji pia walitumia gongo kusaidia kuongoza kondoo zao, au kuokoa kondoo walipo anguka au kupotea. * Gongo la mchungaji lilikuwa na kishikio mwisho, kilicho kuwa tofauti na bakora ya mchungaji, lililo kuwa wima na lilitumika kuua wanyama waliyo jaribu kushambulia kondoo.
## gumia ### Ufafanuzi Msemo "gumia" una maana ya kutoa sauti ya chini, nzito ambayo inasababishwa na mateso ya kihisia au kimwili. Mara kwa mara gumia hutengenezwa bila maneno. Mtu anaweza kugumia kwa sababu ya kuhisi majonzi. Kugumia inaweza kusababishwa kwa kujisikia vibaya, mzigo wa kundamiza. Njia zingine za kutafsiri "gumia" zinaweza kujumuisha "kutoa sauti ya chini ya maumivu" au "kulia kwa kulalamika". Kama nomino, hii inaweza kutafsiriwa kama "kilio cha chini cha mateso" au "mnung'uniko wa chini wa maumivu"
## hakimu ### Ufafanuzi Hakimu ni mtu anayeamua nini kiko sawa au la ukiwepo ugomvi kati ya watu, mara nyingi katika mambo yanayofungamana na sheria. Katika Biblia, Mungu mara nyingi anatajwa kama hakimu kwa sababu yeye ndiye hakimu aliye kamili anayefanya maamuzi ya mwisho kuhusu nini kiko sawa au kisicho sawa. Baada ya watu wa Israeli kuingia nchi ya Kanaani na kabla hawajawa na wafalme wa kuwatawala, Mungu aliwapa viongozi waitwao "waamuzi" kuwaongoza nyakati za shida. Mara nyingi waamuzi hao walikuwa viongozi wa kijeshi waliowaokoa Waisraeli kwa kuwaangamiza maadui zao. Neno "hakimu" linaweza pia kuitwa "muamuzi" au "kiongozi" au "mkombozi" au "gavana," kutegemea na mazingira.
## halali, ipasavyo, kinyume na sheria ### Ufafanuzi Msemo "halali" unamaanisha kitu kinachoruhusiwa kufanywa kulingana na sheria au mahitaji mengine. Kinyume cha hiki ni "kinyume na sheria" inyomaanisha "sio halali." Katika Biblia, kama kitu kinasemwa kuwa "halali" inamaanisha inaruhusiwa na sheria ya kimaadili ya Mungu, au kwa sheria ya Musa au sheria zingine za Kiyahudi. Kitu ambacho "sio halali" "hakiruhusiwi" na sheria hizo. Kufanya kitu "ipasavyo" inamaanisha kuifanya "sawa" au "katika njia sahihi." Mambo mengi Wayahudi waliyoona ni halali au sio halali hayakuwa kwenye makubaliano na sheria za Mungu kuhusu kuwapenda wengine. Kulinga na mazingira, njia za kuafsiri "halali" ni pamoja na, "kuruhusu" au "kulingana na sheria ya Mungu" au "kufuatana na sheria zetu" au "sawa" au inafaa." Msemo "Je ni halali" inaweza pia kutafsiriwa kama "Je, sheria zetu zinaruhusu" au "Hilo ni jambo ambalo sheria zetu zinaruhusu?"
## hali ya chini, kuwa chini ### Ufafanuzi Misemo "wa hali ya chini" na "kuwa chini" inamaanisha kuwa maskini auna hadhi ya chini. Usemi huu pia unaweza kuwa na maana ya kuwa mnyenyekevu. Yesu alijinyenyekesha hadi nafasi ya chini ya kuwa binadamu na kuwatumikia wengine. Kuzaliwa kwake kulikuwa kwa hali ya chini kwa sababu alizaliwa mahali ambapo wanyama walitunzwa; sio katika nyumba ya kifalme. Kuwa na mtazamo wa chini ni kinyume na kuwa na majivuno. Njia za kutafsiri "hali ya chini" ni pamoja na , "unyenyekevu" au "hadhi ya chini" au "kutokua muhimu." Msemo "kuwa chini" unaweza pia kutafsiriwa kama "unyenyekevu" au "umuhimu mdogo."
## Halmashauri ### Ufafanuzi Halmashauri ni kundi la watu wanaokutana kujadili, kutoa ushauri na kufanya maamuzi juu ya masuala ya muhimu. * Halmashauri huratibiwa kwa namna maalumu kwa ajili ya lengo fulani kwa mfano kufanya maamuzi juu ya masuala ya kisheria. * "Halmashauri ya kiyahudi" katika Yerusalemu inayojulikana kama "Baraza" lilikuwa na wajumbe 70 wakiwemo viongozi wa kiyahudi, kuhani mkuu, waandishi, mafarisayo na masadukayo waliokusanyika mara kwa mara kuamua mambo ya sheria za Kiyahudi. Halmashauri hii ya viongozi wa dini iliyomuweka Yesu kwenye mashtaka na kuamua auawe. * Pia kulikuwa na halmashauri ndogo za Kiyahudi katika miji mingine. * Mtume Paulo alipelekwa mbele ya halmashauri ya Rumi alipokamatwa akihubiri injili.
## Hamira, Chachu ### Ufafanuzi "Chachu" ni neno la jumla la kitu kinachosababisha unga wa mkate kuumuka. "Hamira" ni aina ya chachu. * Katika kafsiri nyingine za Kiingereza neno chachu linatafsiriwa kama "hamira" ambayo hufanya unga wa mkate kujaa kabla ya kuoka. * Katika nyakati za agano la kale chachu ilitengenezwa kwa kuruhusu unga kukaa kwa mda. * Waisraeli walipotoroka Misri hawakuwa na muda wa kusubiria unga wa mkate ujae hivyo walitengeneza mkate usiokuwa na chachu na kuondoka nao. Kwa kumbukumbu hii kila mwaka Wayahudi hufanya sherehe kusherehekea sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu. * Pia chachu au hamira imetumika kwenye Biblia kama lugha ya picha kuelezea namna ambavyo dhambi inasambaa katika maisha ya watu au namna ambavyo dhambi inaweza kumchochea mtu mwingine. * Pia inaweza kuwa na maana ya mafundisho ya uongo ambayo husaambaa kwa watu wengi. * Pia chachu inaweza kutumika kwa namna hasi ikielezea namna ambavyo ushawishi wa ufalme wa Mungu unasambaa toka kwa mtu kwenda kwa mtu.
## Hasira ### Ufafanuzi "Kukasirika" au "kupata hasira" ina maana ya kutofurahishwa au kuhangaishwa juu ya jambo fulani au mtu fulani. * Watu wanapokasirika ni dhambi na ubinafsi lakini wakati mwingine kuna hasira ya haki dhidi ya udhalimu au mateso. * Hasira ya Mungu inaelezea namna ambavyo hapendezwi na dhambi. * "kuwatia hasira" maana yake ni "kuwasababisha wakasirike"
## hati ### Ufafanuzi Zamani za kale, hati ilikuwa aina ya kitabu kilicho tengenezwa kwa karatasi ndefu ya mafunjo au ngozi. * Baada ya kuandika kwenye hati au kusoma, watu waliviringisha kwa kutumia ufito kwenye miisho. * Hati zilitumika kwa ajili ya nyaraka na maandiko. * Wakati wingine hati zilizo tolewa na mjumbe zilifungwa kwa nta. Hii inazuia mtu ye yote kufungua hati na kuandika. * Hati zilizo kuwa na maandiko ya Kiebrania zilisomwa kwa sauti katika masinagogi.
## haya, aibu ### Ufafanuzi Neno "haya" la husu hali ya maumivu ya kuumizwa kihisia kwa kuaibishwa kwasababu ya kitu cha fedheha ambacho yeye au mtu mwingine amefanya. * Neno "kuona haya" la eleza jinsi mtu anavyo jisikia wakati amefanya kitu cha aibu. * Maneno "acha aibike" yana maana ya kushinda watu au kuweka wazi dhambi zao ili wajione haya. * Nabii Isaya alisema kwamba wao wanao fanya na kuabudu sanamu wataaibishwa. * Mungu anaweza leta aibu kwa mtu asiye tubu, kwa kudhihirisha dhambi na kusababisha kuaibika.
## hema ### Ufafanuzi Hema ni hifadhi linalo hama lililo tengenezwa na uzi uliyo zungushiwa kwenye nguzo pamoja. * Mahema yanaweza kuwa madogo, yenye kiasi cha nafasi cha watu kulala humo, au yanaweza kuwa makubwa, yenye nafasi ya familia nzima kulala, kupika, na kuishi. * Kwa watu wengi, mahema yanatumika kama sehemu ya kudumu ya kuishi. Kwa mfano, wakati wa muda mwingi familia ya Ibrahimu iliishi katika nchi ya Kanani, waliishi katika mahema makubwa yaliyo tengenezwa na nywele za mbuzi. * Waisraeli pia waliishi katika mahema kipindi cha miaka yao arobaini wakizunguka jangwa la Sinai. * Jengo la maskani lilikuwa aina ya hema kubwa, yenye kuta nene zilizo tengenezwa na vitambaa. * Wakati mtume Paulo alipo safiri miji tofauti kueneza injili, alifanya mahema kupata pesa kujikimu. * Wakati mwingine neno "hema" linaweza tumika kifumbo kueleza wapi watu wanaishi.
## hema la kukutania ### Ufafanuzi Neno "hema la kukutania" la husu hema ambalo lilikuwa la muda mfupi Mungu alipo kutana na Musa kabla ya maskani kujengwa. * Hema la kukutania lilikuwa nje ya kambi ya Waisraeli. * Wakati Musa alipoenda kwenye hema ya kukutania kukutana na Mungu, nguzo ya wingu ilisimama katika mwingilio wa hema kama ishara ya uwepo wa Mungu hapo. * Baada ya Waisraeli kujenga maskani, hema ya muda mfupi haiku hitajika tena na neno "hema la kukutania" lilitumika kueleza maskani.
## Heshima ### Ufafanuzi Heshima ni hisia za kumuheshimu mtu au kitu kwa hali ya juu. * Hisia za heshima zinaweza kuonekana kwa vitendo vinavyompa heshima mtu anayepokea. * Hofu ya Mungu ni heshima ya ndani inayojionesha yenyewe katika utii wa amri za Mungu.
## hudumu, huduma ### Ufafanuzi Neno "hudumu" lina maana kufanya vitu kusaidia watu wengine. Linaweza pia maanisha "kuabudu." * Katika muktadha wa mwanamke anatumikia wageni wake, hili neno lina maana "kujali" au "kutoa chakula" au "kutoa chakula kwa ajili." * Wakati Yesu alipo waambia wanafunzi kuhudumia watu na samaki, lina weza tafsiriwa kama "kusambaza" au "toa kwa ajili ya" au "kumpa yeye" * Neno "huduma" lina husu tendo la kuhudumu. Linaweza pia tumika kumanisha "mkutano" wa Wakristo wanapo mtumikia Mungu kwa pamoja. * Neno "hudumu" laweza tafsiriwa kama, "muhudumia" au "kumfanyia kazi" au "kujali" au "kutii," kulingana na muktadha. * "Kumtumikia Mungu" yaweza tafsiriwa kama "kumuabudu na kumtii Mungu" au "kufanya kazi Mungu aliyo amuru." * "Kutumikia meza" ina maana ya kuleta chakula kwa watu waliyo keti mezani. * Watu wanao fundisha wengine kuhusu Mungu anaelezwa kuwa ni wanamtumikia Mungu na wale wanao wafundisha. * Mtume Paulo aliandika kwa wa Kristo wa Korintho jinsi walivyo "hudumia" Agano la Kale. Hii ina maana ya kutii sheria ya Musa. * Sasa wana "hudumia" agano jipya, ambalo ni, kwasababu ya dhabihu ya Yesu msalabani, waamini katika Yesu wanawezeshwa na Roho Mtakatifu kumpendeza Mungu na kuishi maisha matakatifu.
## huru, uhuru ### Ufafanuzi Msemo "huru" au "uhuru" una maana ya kutokuwa katika utumwa au aina yoyote ya kifungo. Msemo "kumweka mtu huru" au "kumweka huru mtu" ina maana ya kutoa njia kwa mtu ili asiwe katika utumwa au kifungo. Katika Biblia, misemo hii mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha jinsi gani muamini katika Yesu hayupo chini ya nguvu ya dhambi. Kuwa "huru" au "uhuru" inaweza kumaanisha kutohitajika kutii Sheria ya Musa, lakini badala yake kuwa huru kuishi kwa mafunzo na uongozi wa Roho Mtakatifu. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "huru" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kutofungwa" au "kutokuwa katika utumwa" au "kutokuwa katika kifungo". Msemo "ukuru" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana, "hali ya kuwa huru" au "hali ya kutokuwa mtumwa" au "kutofungwa". Msemo "kuweka huru" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kuwa huru" au "kukomboa mtu kutoka utumwani" au "kumwachia kutoka kifungoni". Mtu ambaye "amewekwa huru" atakauwa "ameachiliwa" au "kutolewa kutoka" katika kifungo au utumwa.
## iga, mwigaji ### Ufafanuzi Maneno "iga" na "mwigaji" yanamaanisha kumuiga mtu mwingine na kuigiza sawa na mtu huyu afanyavyo. Wakristo wanafundishwa kumuiga Yesu Kristo kwa kumtii Mungu na kuwapenda wengine, kama Yesu alivyofanya. Mtume Paulo aliliambia kanisa la awali kumuiga yeye, kama yeye alivyomuiga Yesu.
## Ikulu ### Ufafanuzi Neno "ikulu" linamaanisha jengo au nyumba ambayo mfalme aliishi pamoja na familia yake na watumishi wake. * Kuhani mkuu pia aliishi katika ikulu kama ilivyotajwa katika agano jipya. * Ikulu ilikuwa imepambwa sana kwa usanifu na vifaa vizuri. * Majengo na vifaa vya ikulu vilitengenezwa kwa mawe na mbao na mara nyingi vilikuwa vinashikiliwa na mbao za thamani, dhahabu na ndovu. * Watu wengi pia walikuwa wakiishi na kufanya kazi katika ikulu ambayo ilijumuisha majengo kadhaa na uwanja.
## Imeandikwa ### Ufafanuzi maneno haya "Kama ilivyoandikwa" au "kilichoandikwa" yametokea mara nyingi katika agano jipya na yameelezea amri au unabii ulioandikwa katika maandiko ya Kiebrania. * Pia "kama ilivyoandikwa"m inamaanisha maneno yaliyoandikwa katika sheria ya Musa. * Mara nyingine ni nukuu toka kwa moja wa manabii walioandika katika agano la kale. * Yaweza kutafsiriwa kama "kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa" au "kama manabii walivyoandika zamani."
## inua, inuka ### Ufafanuzi Inua, inua juu inamaana ya kuinua kitu juu au kukuweka juu. * Kuinua juu ni kusababisha kitu kionekane. Pia yaweza kuwa kumteua mtu afanye kitu fulani. * "Inua" ina maan ya pekee katika "kuinuka toka kwenye kifo" ikiwa inamaanisha kusababisha mtu aliyekufa aishi tena. * Mara nyingine "kuinua juu" inamaana ya "kupandisha" kitu au mtu. * Mtu anapoinuka kwenda mahali fulani inamaana kuwa amenyanyuka na kwenda. * Yesu alitabiri kuwa atainuka toka kwa wafu . Baada ya siku tatu malaika akasema "ameinuka"
## jamaa wa karibu ### Ufafanuzi Usemi "jamaa wa karibu" unamaanisha ndugu wa damu wa mtu. Mara nyingi neno hili hutumika zaidi kumaanisha ndugu wa kiume. Usemi huu unaweza kumaanisha ndugu wa karibu, kama vile mzazi au kaka, au kwa ndugu wa mbali zaidi, kama vile shangazi, mjomba au binamu. Katika Israeli ya zamani, kama mwanamme akifa, ndugu yake wa karibu wa kiume alitarajiwa kumuoa mjane wake, kutunza mali zake, na kusaidia kulibeba jina la familia yake. Ndugu huyu alikuwa anaitwa "jamaa mkombozi." Usemi unaweza pia kutafsiriwa kama, "ndugu" au "mwana familia."
## jangwa, njika ### Ufafanuzi jangwa, au nyika, ni sehemu iliyokauka, isiyokuwa na mazao ambayo mimea na miti michache inaweza kuota pale. Jangwa ni eneo la ardhi lenye tabia ya nchi ya ukavu na mimea na wanyama wachache. Kwa sababu ya mazingira magumu, watu wachache sana wanaweza kuishi katika jangwa, kwa hiyo pia inajulikana kama "nyika". "Nyika" inaleta maana ya sehemu iliyojitenga, ya kipekee mbali na watu. Neno hili pia linaweza kutafsiriwa kama "sehemu ya jangwa" au "sehemu iliyojitenga" au "sehemu isiyokaliwa".
## jasiri, ujasiri, ushujaa ### Ufafanuzi Maneno yote haya yanamaanisha kuwa na ujasiri na ushujaa kwa kuongea ukweli kuhusu jambo halali hata kama ni vigumu na hatari. * Mtu "jasiri" haogopi kusema jambo jema na la haki, ikiwa ni pamoja na kuwatetea watu wanaonyanyaswa. Hii yaweza kufasiriwa kama "ujasiri" au "bila hofu". * Katika Agano Jipya, wanafunzi waliendelea kuhubiri kwa "ujasiri" kuhusu Kristo hadharani, bila kujari hatari ya kufungwa au kuuawa. Hii inatafasiriwa kama "ujasiri" au "ushujaa" au "kwa ujasiri." * "Ujasiri" wa wanafunzi hawa wa mwanzo katika kuhubiri habari njema ya kifo kiokoacho cha Kristo msalabani kilisababisha injili kuenea katika Israeli yote na nchi za jirani na hatimaye, katika dunia yote. "Ujasiri" waweza pia kutafasiriwa kama "ushujaa."
## jikwaa ### Ufafanuzi Neno "jikwaa" lina maana ya "karibu kuanguka" wakati wakutembea au kukimbia. Kujikwaa juu ya kitu. * Kifumbo, "kujikwaa" yaweza maanisha "kufanya dhambi" au "kuyumba" katika kuamini. * Hili neno laweza elezea kuyumba au kuonyesha udhahifu wakati wa pambano au kipindi cha mateso au adhabu.
## jirani ### Ufafanuzi Neno "jirani" mara kwa mara la mueleza mtu anaye ishi karibu. Pia yaweza kueleza kwa ujumla mtu anaye ishi katika jamii moja au kundi la watu. * "Jirani" ni mtu atakaye lindwa na kutendewa vizuri kwasababu anaishi kwenye jamii moja. * Katika Agano Jipya mfano wa Msamaria Mwema, Yesu alitumia "jirani" kifumbo, akitanua maana yake kumaanisha wanadamu wote, ata mtu anaye onekana kama adui.
## jitu ### Ufafanuzi Jitu mara nyingi ilimaanisha mtu ambaye alikuwa na ukubwa usio wa kawaida wa urefu na nguvu. Goliati, mwanajeshi wa Kifilisti aliyepigana na Daudi, aliitwa Daudi kwa sababu alikuwa mrefu sana, mkubwa, na mtu mwenye nguvu. Wapelelezi wa Israeli waliotafiti nchi ya Kaanani walisema ya kwamba watu wanaoishi pale walikuwa kama majitu.
## jiwe la kujikwaa ### Ufafanuzi Neno "jiwe la kijikwaa" la eleza kitu cha kimwili kinacho msababisha mtu kijikwaa na kuanguka. * Katika Agano Jipya, hili neno lilieleza fimbo au kitu kingine kilicho mtega mnyama aliye kanyaga. * Kifumbo jiwe la kijikwaa ni kitu chochote kinacho sababisha mtu kushindwa kimwili au kiroho. * Mara nyingi ni dhambi ambayo ni jiwe la kujikwaa kwa mtu. * Wakati mwingine Mungu anaweka jiwe la kujikwaa njiani kwa mtu anaye hasi dhidi yake.
## joho ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "joho" uleza vazi lililo valiwa chini ya ngozi, chini nguo nyingine. * Joho lilifika juu hadi chini kwenye kiuno au magoti na lilivaliwa na mkanda. Majoho yaliyo valiwa na watu matajiri yalikuwa na mikono mirefu na kufika hadi kwenye miguu. * Majoho yalitengenezwa na ngozi, manyoa vitambaa, sufi, au kitani, na yalivaliwa na wanaume na wanawake. * Joho lilivaliwa kawaida chini ya nguo ya ndani, kama toga au vazi la nje. Katika kipindi cha joto joho halikuvaliwa na nguo ya njee.
## juma ### Ufafanuzi Neno "juma" kwa kawaida lamaanisha kipindi cha kuishia siku saba. * Katika mfumo wa mahesabu ya Kiyahudi, juma huanza wakati wa jua kuzama Jumamosi na kuishia wakati wa jua kuzama Jumamosi inayofuata. * Katika Biblia, neno "juma" wakati mwingine linatumika kitamathari kurejerea kundi la uniti saba za wakati, kama vile miaka saba. * "Sikukuu ya majiuma" ni sherehe ya mavuno inayofanyika majuma saba baada ya Pasaka. Inajulikana kama Pentecoste.
## juu, juu sana ### Ufafanuzi Maneno " juu" na " juu sana" ni misemo inayo maanisha, "mbinguni." * Maana ingine ya msemo "juu sana" yaweza kuwa, "mwenye heshima sana" * Huu msemo waweza tumika kihalisia, kama katika msemo, "kwenye mti wa juu sana" unao maanisha "kwenye mti mrefu zaidi" * Msemo, "juu" waweza maanisha kuwa juu katika mbingu, kama kiota cha ndege kilicho juu. Katika Muktadha huo yaweza tafsiriwa, "juu katika mbingu" au "juu ya mti mrefu." * Neno "juu" pia la eleza sehemu iliyo inuka au ya umuhimu wa mtu au kitu. * Msemo "kutoka juu" yaweza tafsiriwa kama "kutoka mbinguni."
## kabila ### Ufafanuzi Kabila ni kundi la watu waliyo toka kwa babu mmoja. * Watu kutoka kabila moja mara nyingi walishiriki lugha moja na tamaduni. * Katika Agano la Kale, Mungu aligawanya watu wa Israeli katika makabila kumi na mbili. Kila kabila lilitoka kwa mwana au mjukuu wa Yakobo. * Kabila ni dogo kuliko taifa, lakini kubwa kuliko ukoo.
## kaburi ### Ufafanuzi Neno "kaburi" ni sehemu watu wanapo weka mwili wa mtu aliye kufa. * Wayahudi wakati mwingine walitumia mapango ya asili na makaburi, na wakati mwingine walichimba mapango katika miamba ya vilima. * Wakati wa Agano Jipya, ilikuwa ni kawaida kuviringisha, jiwe kubwa mbele ya uwazi wa kaburi ilikufunga. * Neno "kaburi" utumika kwa mfano wa kumaanisha hali ya kufa au sehemu nafsi za watu waliyo kufa zipo.
## Kahaba ### Ufafanuzi "Kahaba" ni mtu anayefanya vitendo vya uzinzi kwa sababu ya pesa au ibada za kidini. Mara nyingi kahaba huwa mwanamke ila kuna wanaume pia. * Katika Biblia "kahaba" imetumika kama lugha ya picha kumaanisha kitendo cha kuabudu miungu ya uongo au kufanya uganga. * Ukahaba ni kitendo cha kufanya kama kahaba. Hii imetumika kwenye Biblia kuelezea mtu anayeabudu sanamu. * Katika mahekalu ya wapagani hutumia makahaba kama sehemu ya ibada zao.
## kama, mfano ### Ufafanuzi Misemo "kama" na "mfano" inamaanisha kitu kuwa sawa au kufanana na kitu kingine. Neno "kama" pia inatumika katika mithali zinazoitwa "mfanano" ambapo kitu kinalinganishwa na kitu kingine, kawaida huonyesha tabia zinazolingana. Kwa mfano, "nguo zake zinang'aa kama jua" na "sauti ilivuma kama ngurumo." "Kuwa kama" au "kusikika kama" au "kuonekana kama" kitu au mtu inamaana kuwa na sifa zinazofanana na kitu anacholinganishwa nacho au mtu anayelingishwa naye. Watu waliumbwa katika "mfano" wa Mungu. Inamaanisha wana sifa au tabia ambazo ni "kama" au "zizafanana" na sifa ambazo Mungu anazo, kama uwezo wakufikiri, kuhisi na kuwasiliana. Kuwa na "mfano" wa kitu au mtu inamaana kuwa na tabia zinazofanana na hicho kitu au mtu.
## Kamanda, amri ### Ufafanuzi Kamanda ni kiongozi wa jeshimwenye jukumu la kuongoza kundi fulani la askari. * Kuamuru jeshi inamaanisha kuongoza jeshi na kuwa msimamizi kwa kila kitu. * Kamanda anaweza kuwa kiongozi kwa kundi dogo au kubwa kama watu elfu moja. * Neno hili pia linamuelezea Yesu kama kamanda wa jeshi la malaika. * Kamanda pia yaweza kutafsiriwa kama "kiongozi" au "afisa." * Kuamuru jeshi yaweza kutafsiriwa kama "kuongoza" au "kusimamia."
## kamata ### Ufafanuzi Neno "kamata" la maanisha kuchukuwa au kumteka mtu au kitu kwa nguvu. Inaweza maanisha ya kumzidi nguvu au kumtawala mtu. * Wakati mji ulipo chukuliwa kwa nguvu za kijeshi, wanajeshi walikamata mali za thamani za watu waliyo wa shinda. * Linapo tumika kifumbo, mtu anaeza elezwa kuwa "kakamatwa na hofu." Hii ya maanisha kuwa mtu "alichukuliwa kwa hofu" ghafla. Inaweza tafsiriwa kama, "ghafla alikuwa muoga sana." * Katika muktadha wa maumivu ya kujifungua yanayo "mkamata" mwanamke, maana ni kwamba maumivu ni ya ghafla na yazidi nguvu. * Hili neno la weza tafsiriwa kama, "chukuwa mamlaka juu ya" au "ghafla chukuwa."
## Kamili ### Ufafanuzi Katika Biblia neno kamili linamaana ya kukua katika maisha yetu ya Kikristo. Kukifanya kitu kuwa kamili ni kitendo cha kukifanyia kazi mpaka kikamilike bila dosari. * Kuwa kamili au kukua inamaanisha kuwa Mkristo ni mtii hatendi dhambi. * Katika kitabu cha Yakobo kinaeleza kuwa kupita katika majaribu kutetengeneza ukamilifu na kukua kwa waamini. * Wakristo wakijifunza Biblia na kutii watakuwa wakamilifu zaidi kiroho na kukua kwa sababu watafanana sana na Yesu kwa tabia zao.
## kanuni ### Ufafanuzi Neno "kanuni" lina maana ya "kufundisha". Mara nyingi lina maana ya mafunzo ya dini. Katika muktadha wa mafunzo ya Kikristo, "kanuni" ina maana ya mafundisho yote kuhusu Mungu - Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu - ikijumlisha silika yake yote na kila kitu alichofanya. Pia ina maana ya kila kitu Mungu anafundisha Wakristo juu ya namna ya kuishi maisha matakatifu ambayo yanaleta utukufu kwake. Neno "kanuni" mara nyingnie linatumika kumaanisha mafunzo ya dini ya kidunia ya uongo ambayo hutoka kwa wanadamu. Muktadha hufanya maana wazi. Msemo huu pia unaweza kutafsiriwa kama "mafunzo".
## kanyaga ### Ufafanuzi "Kanyaga" ina maana ya kukanyaga kitu na kukisaga kwa mguu. Neno pia utumika kimfano katika Biblia kumaanisha "haribu" au "shinda" au "aibisha." * Mfano wa "kukanyaga" utakuwa kama watu wakikimbia katika shamba la nyasi na kusigina nyasi na miguu yao. * Zama za kale, mvinyo mara nyingine ulifanywa kwa kukanyaga mizabibu kuondoa juisi ndani yake. * Wakati mwingine neno "kanyaga" lina maana ya umbo likimaanisha luadhibu kwa kuaibisha. * Neno "kanyaga" linatumika kiumbo kueleza jinsi Yahweh atavyo wadhibu watu wake Israeli kwa kiburi chao na uhasi.
## kanzu au vazi ### Ufafanuzi Kanzu ni vazi la mikono mirefu ambalo laweza kuvaliwa na mwanamke au mwanaume. Inafanana na koti. * Kanzu zipo wazi mbele na hufungwa kwa mkanda. * Kanzu yaweza kuwa fupi au ndefu. * Kanzu za zambarau zilivaliwa na wafalme kama ishara ua ufalme, utajiri na ufahari.
## karamu ### Ufafanuzi Msemo "karamu" una maana ya tukio ambapo kundi la watu hula chakula kingi sana pamoja, mara nyingi kwa kusudi ya kusherehekea kitu. Tendo "kula karamu" lina maana ya kula kiasi kikubwa cha chakula au kushiriki katika kula karamu pamoja. Mara nyingi kuna aina maalumu za chakula ambavyo huliwa katika karamu maalumu. Sherehe za kidini ambazo Mungu aliamuru Wayahudi kusherehekea mara kwa mara zilijumuisha kuwa na karamu ya pamoja. Kwa sababu hii sherehe hizo mara nyingi zilijulikana kama "karamu". Katika kipindi cha Biblia, wafalme na watu wengine matajiri na wenye nguvu walifanya karamu kuwafurahisha familia zao au marafiki. Katika simulizi kuhusu mwana mpotevu, baba yake alikuwa na karamu iliyoandaliwa kusherehekea ujio wa mwanawe. Karamu mara zingine hudumu siku kadhaa au zaidi. Msemo "kusherehekea" unaweza kutafsiriwa kama "kula kwa wingi mno" au "kusherehekea kwa kula chakula kingi" au "kula chakula kingi maalumu". Kulingana na muktadha, "karamu" inaweza kutafsiriwa kama "kusherehekea pamoja kwa chakula kingi" au "mlo wenye chakula kingi" au "mlo wa sherehe"
## kashfa, mtoa kashfa ### Ufafanuzi Kukashifu ina maana ya kusema kitu hasi, cha kudhalilisha kwa mtu mwingine. * Kashfa yaweza kuwa kweli au taarifa ya kuongo ya kusingizia, lakini lengo ni kusababisha wengine kumfikiria vibaya mtu anaye kashifiwa.
## kaya/famlia ### Ufafanuzi Istilahi 'kaya' hurejelea watu wote wanaoishi pamoja katika nyumba, ikijumuisha wana familia pamoja na watumishi walio nao. Mtu anaposimamia kaya, hujumuisha kuwaelekeza watumishi pamoja na kuangalia na kulinda mali. Wakati mwingine neno ' kaya' laweza kutumika kimfano kumaanisha ''ukoo wa mtu, hasa hasa wazao wake''
## kazi, mfanyakazi ### Ufafanuzi Neno "kazi" linamaanisha kufanya kazi ngumu ya aina yoyote. Kwa ujumla, kazi ni shughuli inayotumia nguvu, mara nyingi inaashiria kuwa shughuli ni ngumu. Mfanyakazi ni mtu afanyae aina yoyote ya kazi.
## kereza meno, saga meno ### Ufafanuzi Kukereza au kusaga meno ina maana ya kukaza meno na kuyakwangua kwenda na kurudi dhidi yao. Hii mara kwa mara huonyesha maumivu na hasira kubwa mno. Biblia inatuambia ya kwamba kusaga meno ni jambo moja ambalo wale walio jehanamu watafanya katika dhiki yao kuu. Msemo huu pia unaweza kutafsiriwa kama "kukwangua meno dhidi yao" au "kama haipo wazi nini tendo hili linamaanisha "kusaga meno kwa maumivu" au "kusaga meno katika uchungu".
## kiapo, kuapa, ### Ufafanuzi Katika Biblia, kiapo ni ahadi rasmi ya kufanya kitu. Mtu anaye kiapo anapswa kutimiza hiyo ahadi. Kiapo kinahusu kuwa mwaminifu na wa kweli. * Mara nyingi katika mahakama ya sheria, shahidi anatoa kiapo kuahidi kwamba chochote anachosema kitakuwa kweli na hakika. * Katika Biblia, neno "apa" lina maana ya kiapo. * Neno "kuapa" lina maana ya kutumia jina la kitu au mtu kama chanzo au nguvu ambayo kiapo kinatolewa. * Wakati mwengine haya maneno yanatumika pamoja kama, "apa kiapo" * Ibrahimu na Abimeleki waliapa kiapo walipo wafanya agano pamoja kuhusu matumizi ya kisima. * Ibrahimu alimwambia mtumishi wake aape kuwa atampatia Isaka mke kutoka miongoni mwa ndugu wa Ibrahimu. * Mungu pia alifanya kiapo ambacho alitoa ahadi kwa watu wake.
## kiasi ### Ufafanuzi Kiasi ni uwezo wa kutawala tabia ya mtu ili kuepusha kutenda dhambi. * Ina husu tabia njema, kuepuka mawazo mabaya, lugha, na matendo. * Kiasi ni tunda au tabia ambalo Roho Mtakatifu anawapa Wakristo. * Mtu anaye tumia kiasi anaweza jizuia kutofanya kitu kibaya anacho weza fanya. Mungu ndiye anaye mpa mtu uwezo wa kuwa na kiasi.
## Kiburi ### Ufafanuzi Kiburi maana yake ni kujivuna. * Mtu mwenye kiburi mara nyingi hujivuna juu yake mwenyewe. * Kuwa na kiburi pia inajumuisha kuona kuwa watu wengine sio muhimu kama wewe. * Watu wasiomuheshimu Mungu au wanaompinga Mungu wana viburi maana hawatambui uwepo wa Mungu na nguvu zake.
## Kiburi ### Ufafanuzi Neno 'Kiburi' lina maana ya kuwa mwenye kujisifu, kujigamba au kujiona. Inarejelea mtu ambaye hujiona mwenyewe kuwa ni wa juu sana kuliko wengine. Mara nyingi neno hili humzungumzia majivuno ya mtu ambaye huendelea kufanya dhambi kinyume na Mungu. Mara kwa mara mtu mwenye kiburi hujivuna na kujiinua yeye mwenyewe Mtu mwenye kiburi ni mpambavu, hana hekima. Neno 'kiburi' laweza kutafsiriwa kama 'majivuno' ' majigambo' 'kujiinua' au kujiona. Maneno "macho ya kiburi'' ni Lugha ya picha ambayo yaweza kutafsiriwa kama "kuangalia kwa kiburi'' au " kuwaangalia wengine kama watu wasio na umuhimu'' au ''mtu mwenye kiburi anayewadharau wengine kwa kuwaona kuwa wako chini.''
## Kiburi ### Ufafanuzi Kiburi ni hali ya mtu kujifikiria mwenyewe na kudhani kuwa yeye ni bora kuliko wengine. * Mtu mwenye kiburi huwa hakubali makosa yake. Sio mnyenyekevu. * Kiburi kinaweza kusababisha usimtii Mungu katika njia nyingine. * Pia kiburi kinaweza kuelezwa katika mtazamo chanya kwa mfano "kujivunia" kwa kitu ambacho mtu fulani amefanikiwa au "kujivunia" watoto wako. * Mtu anaweza kujivunia kwa alichokifanya bila kuwa na kiburi juu ya hilo.
## Kichwa ### Ufafanuzi Katika Biblia neno 'kichwa' lilmetumika kama tamathali ya semi likiwa lina maana nyingi: Mara nyingi neno hili limetumika kurejelea hali ya kuwa na mamlaka juu ya watu , kwa mfano, "mmenifanya kichwa cha mataifa" Sentensi hiyo yaweza kutafsiriwa kuwa "mmenifanya kuwa mtawala" au "mmenipa mamlaka juu ya..." Yesu anaitwa 'kichwa cha kanisa.' Kama ambavyo kichwa cha mtu huongoza viungo vingine vya mwili, hivyo na Yesu huongoza na huelekeza viungo vingine vya mwili wake, yaani kanisa. Agano la Jipya linatufundisha kuwa mme ni "kichwa'' au mwenye mamlaka kwa mkewe. Amepewa wajibu wa kumwongoza na kumwelekeza mkewe na familia. Maneno yanayosema "wembe hautagusa kich chake" maana yake ni kwamba" hatakata au hatanyoa nywele zake. Neno 'kichwa' laweza pia kurejelea mwanzo au asili ya kitu fulani, mfano 'kichwa cha mtaa" Maneno kama "kichwa cha nafaka" hurejelea sehemu ya juu ya ngano au mche wa shayiri ambao una mbegu ndani yake. Mfano mwingine wa 'kichwa' ni pale unapotumika kuwakilisha mtu mzima. Mfano, 'kichwa cheupe' humrejelea mtu mzee au tunaposema ' kicha cha Yusufu, tunamaanisha Yusufu mwenyewe. Msemo unaosema 'acha damu yao iwe juu ya kichwa chake' humaanisha kuwa mtu yule anawajibika kwa vifo vyao na atapokea adhabu/hukumu yake. Mapendekezo ya tafsiri Neno 'kichwa' laweza kutafsiriwa kama 'mamlaka' au 'mtu anayeongoza na kuelekeza' au 'mtu anayewajibika kwa..' kwa kutegemea na muktadha wenyewe. Maneno kama ' kichwa cha' hurejelea mtu mwenyewe mzima, na hivyo maneno hayo yaweza kutafsiriwa kwa kutumia jina la mtu husika. kwa mfano ''kichwa cha Yusufu'' ina maana ya 'Yusufu' Maelezo kama ' itakuwa juu ya kichwa chake' yanaweza kutafsiriwa kama " itakuwa juu yake'' au 'ataadhibiw'a kwa ajili ya' au 'atawajibika kwa ajili ya... Kwa kutegemea na muktadha wenyewe, maana zingine za neno kichwa zaweza kuwa "mwanzo' au "asili'' au ''chanzo'' au "mtawala" au ''juu ya''
## kifo, kufa, mfu ### Ufafanuzi Msemo huu unatumika kumaanisha vyote kifo cha kimwili na kiroho. Kimwili, ina maana ya mwili wa kihalisia wa mtu kukoma kuishi. Kiroho, ina maana ya wenye dhambi kutengwa na Mungu mtakatifu kwa sababu ya dhambi yao. Mapendekezo ya Tafsiri Kutafsiri msemo huu, ni vyema kutumia neno la kila siku au usemi ambao una maana ya kifo katika lugha husika. Katika baadhi ya lugha, "kufa" inaweza kuelezwa kama "kutokuishi". Msemo "kufa" unaweza kutafsiriwa kama "kutokuwa hai" au "kutokuwa na uhai wowote" au "kutokuishi". Lugha nyingi zinatumia msemo wa tamathali kuelezea kifo, kama "kuondoka" kwa Kiingereza. Ila katika Biblia ni bora kutumia msemo wa moja kwa moja kwa ajili ya kifo ambao unatumika kila siku katika lugha. Katika Biblia, uhai na kifo wa kimwili mara kwa mara hulinganishwa na uhai na kifo cha kiroho. Ni muhimu katika tafsiri kutumia neno moja au msemo kwa ajili kifo cha kimwili na kifo cha kiroho. Katika baadhi ya lugha inaweza kuwa wazi zaidi kusema, "kifo cha kiroho" ambapo muktadha unahitaji maana hiyo. Watafsiri wengine wanaweza kuhisi ni bora kusema, "kifo cha kimwili" katika muktadha ambapo unalinganishwa na kifo cha kiroho. Msemo wa "wafu" ni kivumishi chenye maana ya watu waliokufa. Baadhi ya lugha zitatafsiri hili kama, "watu waliokufa" au "watu ambao wamekufa"
## kifuko cha kifuani ### Ufafanuzi Neno "dirii" ni kipande cha silaha kinachofunika kifua kumlinda askari wakati wa vita. Neno "kifuko cha kifuani" linamaanisha kipande maalumu cha nguo ambacho kuhani mkuu wa Kiisraeli alivaa katika sehemu yake ya mbele kifuani. * "Dirii" iliyotumiwa na askari ilitengenezwa kwa miti, chuma au ngozi ya mnyama. Ilikuwa imetengenezwa kuzuia mishale, mikuke, na upanga katika kuchoma kifua cha askari. * "Kifuniko" kilichovaliwa na kuhani mkuu kilikuwa kimetengenezwa kwa nguo na kilikuwa kitu kilichounganiswa nacho. Kuhani alikivaa alipokuwa katika majukumu yake ya kumtumikia Mungu hekaluni. * Njia nyingine ya kutafasiri "dirii" ni pamoja na, "kifaa cha chuma cha kufunika kifua" au delaya ya kulinda kifua." * Neno "kifuniko" litafasiriwe kwa neno limaanishalo, vazi la kikuhani lifunikalo kifua" au "kipande cha vazi la kikuhani" au "kipande cha mbele cha vazi la kuhani."
## kikapu ### Ufafanuzi Neno "kikapu" linamaanisha chombo kilichotengenezwa kwa kusukwa. * Nyakati za Biblia, vikapu pengine vilitengenezwa kwa mimea, kama vile kutoka katika matawi ya miti au magome. * Kikapu kiliweza kuwekewa vitu vya kuzuia maji ili kiweze kuelea. * Musa alipokuwa mtoto, mama yake alitengeneza kikapu kisichopenyeza maji kwa kumweka humo na kukieleza katika mafunjo katika Mto Nile. * Neno lililotafasiriwa kama "kikapu" katika habari hiyo ni sawa na neno "safina" kurejerea mtumbwi alioutengeneza Musa. Maana ya kawaida ya matumizi yake katika mazingira mawili hayo yaweza kuwa' "chombo kieleacho."
## Kimbia ### Ufafanuzi Kukimbia ni kitendo cha kutembea haraka kwa miguu, haraka zaidi ya kutembea. Pia kukimbia yaweza kuwa na maana zifuatazo. * "Kukimbia ili kushinda taji" - hii inamaanisha kuwa kufanya mapenzi ya Mungu kama kukimbia mbio ili ushinde. * "Kukimbia ili kufanya uliyoamriwa" hii inamaana ya kwamba kutii haraka amri za Mungu. * "Kukimbilia miungu mingine"- Hii inamaanisha kwenda kuabudu miungu mingine. * "Kukimbilia kwako ili unifiche" - hii inamaanisha kuwa kukimbilia haraka kwa Mungu ili kupata usalama unapokutana na mambo magumu.
## Kimbilio, malazi ### Ufafanuzi "Kimbilio" ni sehemu au hali ya usalama na ulinzi. "Malazi" ni sehemu yenye muundo wa kimwili ambayo inakulinda kutokana na hali ya hewa au hatari. * Katika Biblia Mungu anaelezwa kama kimbilio ambapo watu wake huwa salama na kupata ulinzi kwake. * "Mji wa makimbilio" katika agano la kale ni miji ambayo mtu akiua kwa bahati mbaya hukimbilia huko kwa ajili ya usalama toka kwa watu wanaotaka kumvamia na kulipa kisasi. * Malazi ni sehemu inayojengwa kama jengo ambalo laweza kutoa ulinzi kwa watu au wanyama. * Mara nyinginge malazi humaanisha usalama. Lutu aliposema wageni wake wapo chini ya malazi ya paa lake alikuwa na maana kuwa walikuwa salama kwa sababu walikuwa kwenye nyumba yake.
## kinanda, kinubi ### Ufafanuzi Kinanda na kinubi ni vyombo vidogo vya muziki vyenye nyuzi zilizotumika na Waisraeli kumuabudu Mungu. Kinanda kinafanana sana na gita la siku hizi, lina sanduku ya mbao na shingo ndefu ambapo nyuzi zimefungwa. Kucheza kinanda au kinubi, nyuzi flani zinashikiliwa na mkono mmoja wakati nyuzi zingine zinapigwa na mkono mwingine. Kinanda na kinubi zote zinachezwa kwa kupigwa au kuvutwa nyuzi. Idadi ya nyuzi ilitofautiana, lakini Agano la Kale lilitaja bayana vyombo vyenye nyuzi kumi.
## kinara cha taa. ### Ufafanuzi Katika Biblia, usemi "kinara cha taa" kwa ujumla inamaanisha umbo ambapo taa inawekwa ili kutoa mwanga kwa chumba. Kinara cha taa cha kawaida kilibeba taa moja na kilitengenezwa kwa udongo, mbao au chuma (kama shaba, fedha, au dhahabu.) Katika hekalu la Yerusalemu kulikuwa na kinara cha taa maalumu cha dhahabu kilichokuwa na matawi saba kwa kushikilia taa saba.
## kinubi ### Ufafanuzi Kinubi ni chombo au kifaa cha muziki mara nyingi huwa na muundo ulio na uwazi mkubwa na nyuzi za wima. Katika Biblia, mbao za msonobari zilitumika kutengenezea vinubi pamoja na vyombo vingnei vya muziki. Vinubi mara kwa mara vilishikiliwa mikononi na kupigwa wakati mtu akiwa anatembea. Sehemu nyingi katika Biblia, vinubi vilikuwa vikitumika katika kumsifu na kumwabudu Mungu. Daudi aliandika Zaburi kadhaa ambazo zilikuwa zimepangwa kwa muziki wa kinubi. Daudi pia alicheza kinubi kwa mfalme Sauli ili kutuliza na kuburudisha roho ya mfalme iliyotaabika.
## kinyume cha sheria ### Ufafanuzi Maneno "kinyume cha sheria" na "sio kisheria" yanatumika kueleza matendo yanayo vunja sheria. * Katika Agano Jipya, neno "kinyume cha sheria" sio tu la tumika kueleza kuvunja amri ya Mungu, bali pia kuvunja sheria za Kiyahudi. * Baada ya miaka, Wayahudi waliongeza kwenye sheria Mungu alizowapa. Viongozi wa Kiyahudi waliita kitu "kinyume cha sheria" kama hakikuendana na sheria zao wao. * Yesu na wanafunzi wake walipo kuwa wana nyofoa nafaka siku ya Sabato, Mafarisayo waliwashtaki kufanya "kinyume cha sheria" kwasababu ilikuwa ina vunja sheria za Wayahudi za kutofanya kazi hiyo siku. * Wakati Petro alipo sema kula chakula najisi ni "kinyume cha sheria" kwake, alimaanisha kama angekula vyakula angekuwa na vunja sheria Munug alizo wapa Waisraeli kuhusu kuto kula baadhi ya vyakula.
## kinywaji kikali ### Ufafanuzi Neno "kinywaji kikali" ina eleza vinywaji vilivyo zindikwa na vina vilevi. * Vinywaji vya vilevi utengenezwa na nafaka au matunda na vimepitia njia ya kuzindikwa. * Aina ya "kinywaji kikali" ni mvinyo wa mzabibu, mvinyo wa mtende, bia. Katika Biblia, mvinyo wa mzabibu ndio unao tumika sana. * Makuhani na mtu ye yote walio chukuwa kiapo maalumu kama "kiapo cha Naziri" hawaku ruhusiwa kunywa kilevi.
## Kisasi ### Ufafanuzi "Kisasi" ni kitendo cha kumuadhibu mtu kama malipo ya yale mabaya aliyoyatenda. * Mara nyingi lengo la kisasi ni kuona kuwa haki inatendeka au kurekebisha kosa. * Kwa binadamu kulipa kisasi inajumuisha kumuadhibu mtu aliyefanya makosa. * Mungu akilipa kisasi anafanya kwa haki kwa sababu anahukumu watenda dhambi na waasi.
## Kisima,birika ### Ufafanuzi Kisima na birika ni vyanzo viwili tofauti vya maji katika nyakati za Biblia. * Kisima ni shimo refu linalochimbwa ardhini ili maji ya chini yamiminike juu yake. * Birika ni shimo refu lililopo kwenye mwamba linalotumika kushikilia tangi kwa ajili ya kukusanya maji. * Maranyingi birika huchimbwa kwenye mwamba na kukandikwa na plasta ili kuyahifadhi maji ndani. * Birika maranyingi huwekwa maeneo ya uani kwenye nyumba za watu ili kuvuna maji ya mvua yanayotiririka juu ya paa. * Visima vilichimbwa sehemu ambayo ilikuwa rahisi kwa familia au jamii kufika. * Kwa sababu maji yalikuwa muhimu kwa watu na wanyama mara nyingine haki ya kutumia maji ilileta ugonvi. * Kisima na birika vilifunikwa na jiwe kubwa ili kuzuia chochote kisianguke juu yake. * Mara nyingine birika lililokauka lilitumika kama gereza kwa mfano Yusufu na Yeremia walifungwa kwenye birika.
## Kitabu cha uzima ### Ufafanuzi Neno "Kitabu cha uzima" linatumika kumaanisha Mungu alipoandika majina ya watu aliowakomboa na kuwapa uzima wa milele. * Kitabu cha ufunuo kinarejerea kitabu hiki kama "Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo." Ingeweza kutafasiriwa kama "kitabu cha Yesu cha uzima, Mwanakondoo wa Mungu." Sadaka ya Yesu msalabani ililipa adhabu ya dhambi za watu ili waweze kuwa na uzima wa milele kwa njia ya kumwamini. * Neno kwa "kitabu" laweza pia kumaanisha, "gombo" au "andiko" "kitabu cha sheria." Inaweza kuwa na maana halisia au ya kimafumbo.
## kiti cha enzi ### Ufafanuzi Kiti cha enzi ni kiti ambacho mfalme ana keti kuamua mambo muhimu na kusikiliza maombi ya watu wake. * Kiti cha enzi ni ishara ya mamlaka na nguvu ambayo mfalme anayo. * Neno "kiti cha enzi" utumika mara nyingi kifumbo kumueleza mfalme, utawala wake, au nguvu yake. * Katika Biblia, Mungu anaonyeshwa kama mfalme anaye keti katika kiti chake cha enzi. Yesu anaelezwa akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba kwenye kiti chake cha enzi.
## Kiumbe ### Ufafanuzi Kiumbe ni kila kitu kilicho hai ambacho Mungu alikiumba, binadamu na wanyama. * Nabii Ezekieli anaelezea kuona "viumbe hai" katika maono ya utukufu wa Mungu. Hakujua ni nini hivyo akaviita hivyo. * Tambua kuwa neno kiumbe ina maana tofauti na kwa kuwa inajumuisha kila kitu ambacho Mungu amekiumba vilivyo hai na visivyo hai. Kiumbe ni vitu vilivyo hai peke yake.
## Kivuli ### Ufafanuzi Neno "kivuli" lina maana ya giza linalo sababishwa na kitu kinacho ziba mwanga. Pia lina maana kadhaa ya mafumbo. * "Kivuli cha mauti" ina maana kwamba kifo kipo karibu, kama vile kivuli kinavyo hashiria uwepo kitu. * Mara nyingi katika Biblia, maisha ya mwanadamu yana linganishwa na kivuli, ambacho hakidumu muda mrefu sana na hakina kiini. * Wakati mwingine, "kivuli" lina tumika kama neno lingine la "giza." * Biblia inaongea kuhusu kujificha au kulindwa ndani ya kivuli cha mabawa ya Mungu au mikono. Hii ni picha ya kulindwa na kufichwa kutoka kwenye hatari.
## kizazi ### Ufafanuzi Msemo "kizazi" una maana ya kundi la watu ambao wote wamezaliwa katika kipindi cha kufanana. Kizazi pia kinaweza kumaanisha kipindi cha muda. Katika kipindi cha Biblia, kizazi kilichukuliwa kuwa kama miaka 40. Wazazi na watoto waoo wanatoka katika vizazi viwili tofauti. Katika Biblia, msemo "kizazi" pia hutumika kitamathali kumaanisha kwa ujumla watu ambao huwa na tabia za kufanana. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo " kizazi hiki" au "watu wa kizazi hiki" unaweza kutafsiriwa kama "watu wanaoishi sasa" au "nyie watu". "Kizazi hiki kiovu" inaweza kutafsiriwa kama "watu hawa waovu wanaoishi sasa". Msemo "kutoka kizazi hadi kizazi" au "kutoka kizazi kimoja hadi kingine" inaweza kutafsiriwa kama "watu wanaoishi sasa, pamoja na watoto na wajukuu wao" au "watu katika kipini chote" au "watu wa kipindi hili na vipindi vya baadaye" au "watu wote na uzao wao". "Kizazi kinachokuja kitamtumikia; watawaambia kizazi kifuatacho juu ya Yahwe" inaweza kutafsiriwa kama "Watu wengi hapo baadaye watamtumikia Yahwe na kuwaambia watoto na wajukuu wao juu yangu".
## kizingiti ### Ufafanuzi Neno "kizingiti" la eleza sehemu ya chini ya mlango au sehemu jengo ambayo ipo ndani ya mlango. * Wakati mwingine kizingiti ni kijiti cha ambao ambcho lazima kikanyagwe ilikuingia chumbani au kwenye jengo. * Lango pamoja na uwazi wa hema la weza kuwa na kizingiti.
## Komamanga ### Ufafanuzi Komamanga ni aina ya tunda nene lenye ngozi ngumu lililojaa mbegu nyingi ndani zilizozungukwa na chakula chenye rangi nyekundu. * Komamanga mara nyingi huota katika nchi zenye joto, ukame kama Miisri na Israeli. * Bwana aliwaahidi wa Israeli kuwa Kanaani ni chi yenye maji ya kutosha na ardhi yenye rutuba iliyo na vyakula vya kutosha ikiwemo makomamanga. * Ujenzi wa hekalu la Sulemani lilikuwa na mapambo yaliyo katika muundo wa komamanga.
## komboa, mkombozi, ukombozi ### Ufafanuzi "Kukomboa" mtu ina maana ya kumukokoa mtu huyo. Msmo "mkombozi" una maana ya mtu ambaye hukomboa au kuweka huru watu kutoka utumwani, mateso au hatari zingine. Msemo "ukombozi" una maana ya kile kinachotokea pale mtu anapookoa au kuweka watu huru kutoka utumwani, matesoni, au hatari zingine. Katika Agano la Kale, Mungu aliwaweka wakombozi kuwalinda Waisraeli kwa kuwaongoza katika vita dhidi ya makundi ya watu wengine waliokuja kuwashambulia. Wakombozi hawa pia walijulikana kama "waamuzi" na kitabu cha Agano la Kale cha Waamuzi kimeweka kumbukumbu ya kipindi katika historia ambapo waamuzi hawa walikuwa wakitawala Israeli. Mungu pia anaitwa "mkombozi". Kote katika historia ya Israeli, aliwakomboa au kuwaokoa watu wake kutoka kwa maadui zao. Msemo "kutoa kwa" ina maana tofauti kabisa ya kumtoa mtu kwa adui, kama pale Yuda alipomtoa Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi. Mapendekezo ya Tafsiri Katika muktadha wa kusaidia watu kutoroka kutoka kwa adui zao, msemo "komboa" unaweza kutafsiriwa kama "okoa" au "kuweka huru" au "nusuru". Pale inapomaanisha kukabidhi mtu kwa adui, "kukabidhi" inaweza kutafsiriwa kama "kusaliti" au "kumpatia" au "kutoa kwa". Neno "mkombozi" linaweza kutafsiriwa kama, "mkombozi" au "mweka huru". Pale ambapo msemo "mkombozi" una maana ya waamuzi waliongoza Israeli, inaweza pia kutafsiriwa kama "bosi au "mwamuzi" au "kiongozi"
## kondoo, kondoo dume, kondoo jike ### Ufafanuzi "kondoo" ni mnyama wa saizi ya kati wa miguu minne mwenye manyoya mwili mzima. * Waisraeli mara kadhaa walitumia kondoo kwa dhabihu, hususani dume na kondoo mdogo. * Watu ula nyama ya kondoo na kutumia manyoya yake kufanya nguo na vitu vingine. * Kondoo ni wa piole, dhahifu, na waoga. Wanashawishika haraka kupotea. Wanaitaji mchungaji kuwaongoza, kuwalinda, na kuwapa chakula, maji, na hifadhi. * Katika Biblia, watu wanalinganishwa na kondoo waliyo na Mungu kama mchungaji wao.
## Kosa, mateso, kuumiza ### Ufafanuzi "kumkosea" mtu inamaanisha kumfanyia mtu isivyo haki na kwa udanganyifu. * Mateso ni kumtendea mtu vibaya na kumsabaishia maumivu ya kimwili au kihisia. * Kuumiza ni neno la jumla lenye maana ya kusababisha maumivu kwa mtu. Yawza kuwa kumsababishia majeraha ya kimwili. * Inategemea na mukhtadha maneno haya yanaweza kuwa na maana ya "kumtendea mtu kosa" au "kutomtendea haki" au "kusababisha maumivu" au "kujeruhi."
## kuachwa, kuacha ### Ufafanuzi Msemo wa "kuachwa" na "kuacha" ina maana ya kuangamiza sehemu isiyokuwa na watu ili kwamba isiwe ya makazi. Inapomaanisha mtu, msemo "kuachwa" inaelezea hali ya uharibifu, upweke, au majonzi. Msemo "kuacha" ni hali ya kuachwa. Iwapo shamba ambapo mimea inaota linaachwa, ina maana kitu kimeaangamiza mimea, kama wadudu au uvamizi wa jeshi. "Eneo lilioachwa" lina maana ya eneo ya ardhi ambapo watu wachache wanaishi kwa sababu kuna mazao machache au mimea mingine inayoota pale. "Ardhi iliyoachwa" au "nyika" mara kwa mara ilitengwa kwa watu waliotengwa na jamii (kama wakoma) na wanyama wa hatari. Kama mji "unatengwa" ina maana ya kwamba majengo yake na mali vimeharibiwa au kuibiwa, na watu wake wameuwawa au kukamtwa. Mji unakuwa "tupu" na "kuharibika". Hii ni sawa na maana ya "teketeza" au "teketezwa", lakini kwa msisitizo zaidi kwa utupu. Kutegemea muktadha, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "kuharibiwa" au "kuangamizwa" au "kuwekwa kama takataka" au "mpweke/iliyotengwa" au "kutelekezwa"
## Kuadhibu, adhabu ### Ufafanuzi "Kuadhibu" inamaana ya kusababisha mtu ateseke baada ya kufanya makosa. Adhabu ni matokeo hasi anayopewa mtu baada ya kufanya jambo baya. * Adhabu hutumika kumfanya mtu aache dhambi. * Mungu aliwaadhibu Waisraeli walipomuasi hasa walipoabudu miungu ya uongo, Mungu aliruhsu adui zao kuwavamia na kuwateka. * Mungu ni wa haki hivyo huadhibu wenye dhambi. Kila binadamu ametenda dhambi na anastahili adhabu. * Yesu aliadhibiwa kwa ajili ya makosa ya kila mtu. Alipokea adhabu ya kila mtu japokuwa yeye hakuwa na kosa lolote. * Maneno kama "bila kuadhibiwa" au "kuacha kuadhibiwa" yanamaana kuamua kutokuadhibu watu kwa matendo yao maovu. Mungu mara nyingine anawaacha wenye dhambi bila kuwaadhibu akisubiria watubu.
## kubeba ### Ufafanuzi Neno "kubeba" linamaanisha "kubeba" kitu fulani. Lakini pia kuna kuna matumizi ya tamathari mbalimbali ya neno hili. * Unapoongelea mwanamke atakayebeba mtoto, inamaanisha, "kuzaa" mtoto. * "kubeba mzigo" inamaanisha "kupitia magumu." Magumu haya yaweza kuwa ya kimwili au ya kihisia. * Matumizi yake yaliyozoeleka katika Biblia ni "kuzaa matunda" inayomaanisha, " "kuzalisha matunda" au "kuwa na matunda." * Kifungu "kubeba ushahidi" inamaanisha "kushuhudia" au "kutoa taarifa ya kile ulichokiona au kukipitia." * Taarifa ya "mwana hatabeba uovu wa mzazi" inamaanisha "hatawajibika kwa ajili ya" au "hataadhibiwa kwa ajili ya "dhambi za baba yake". * Kwa ujumla, neno laweza kutafasiriwa kama, "kubeba" au "kuwajibika kwa" au "kuzaa" au "kuwa na" au "kustaimili," kutegemeana na mazingira.
## kuchinja ### Ufafanuzi Neno "kuchinja" Maneno waliyo chinjwa ya weza pia tumika kutafsiri watu waliyo chinjwa au watu waliyo uawa. Pia la weza tumika kumaanisha mkua mnyama kwa kusudi la kumla. * Wakati Ibrahimu alipo pokea wageni watu katika hema yake jagwani, aliamuru watumishi wake kuua na kupika ndama kwa ajili ya wageni wake. * Nabii Ezekieli alitabiri kwamba Mungu atatuma malaika kuchinja wote wasio fuata neno lake. * 1 Samweli ya eleza kuchinjwa kwa Waisraeli 30,000 waliyo uliwa na adui zao. Kwasababu ya kutomtii Mungu. * "silaha za kuchinja" yaweza tafsiriwa kama "silaha za kuua."
## kudanganya, udanganyifu, hila, mdanganyifu ### Ufafanuzi Msemo wa"kudanganya" una maana ya kumfanya mtu aamini jambo ambalo sio la kweli. Tendo la kumdanganya mtu linajulikana kama "udanganyifu". Msemo mwingine, "udanganyifu" pia una maana ya tendo la kumfanya mtu aamini jambo ambalo sio kweli. Mtu anayefanya wengine kuamini jambo la uongo ni "mdanganyifu". Kwa mfano, Shetani anaitwa "mdanganyifu". Roho chafu anazoziongoza pia zinajulikana kama wadanganyifu. Mtu, tendo, au ujumbe ambao sio wa kweli unaweza kuelezwa kama "udanganyifu". Misemo ya "udanganyifu" na "hila" zina maana moja, lakini kuna tofauti kadhaa ndogo jinsi zinavyotumika. Misemo inayojieleza ya "udanganyifu" na "hila" ina maana moja na hutumika katika muktadha moja. Mapendekezo ya Tafsiri Njia zingine za kutafsiri "kudanganya" zinaweza kujumuisha "uongo" au "kusababisha kuwa na na imani potofu" au "kusababisha mtu afikiri jambo sio la kweli". Msemo "kudanganywa" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kufikiri jambo ni la uongo" au "alidanganywa" au "alifanyiwa hila" au "alipumbazwa" au "alipotoshwa". "Mdanganyifu" inaweza kutafsiriwa kama, "mwongo" au "mtu mpotoshaji" au "mtu anayedanganya". Kulingana na muktadha, msemo wa "udanganyifu" au "hila" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo unaomaanisha "uongo" au "kudanganya" au "upotoshaji" au "kutokuwa na uaminifu". Msemo "kudanganya" au "udanganyifu" unaweza kutafsiriwa kwa "uongo" au "upotoshaji" au "kudanganya" kumuelezea mtu anayezungumza au kutenda kwa njia ambayo inasababisha watu wengine kuamini mambo ambayo sio ya kweli.
## Kufanikiwa, mafanikio ### Ufafanuzi "Kufanikiwa" ni kitendo cha kuishi vizuri na kuwa na mafanikio kimwili na kiroho. Nchi inayofanikiwa inamaanisha wana utajiri na wanakila kitu wanachohitaji. * Mafanikio ni kufanikiwa kwa kuwa na pesa na mali. * Katika Biblia "mafanikio" yanajumuisha afya njema au kubarikiwa kuwa na watoto. * Mji wenye mafanikio ni mji wenye watu wengi, uzalishaji mzuri wa chakula na biashara inayozalisha pesa nyingi. * Biblia inafundisha kuwa mtu atafanikiwa kiroho pale atakapotii mafundisho ya Mungu. Pia tapata baraka ya furaha na amani. Mungu hawabariki tuu watu kwa kuwapa mali bali huwabariki pia kiroho. * Mafanikio pia yaweza kutafsiriwa kama "utajiri" au "matunda ya kiroho."
## Kufanya, nia, kujituma ### Ufafanuzi Kufanya au kujituma ni kitendo cha kufanya maamuzi au kuahidi kufanya jambo fulani. * Mtu anayeahidi kufanya jambo ni mtu mwenye nia ya kufanya jambo hilo. * Kumpa mtu afanye jambo fulani inmaanisha kumkabidhi mtu shughuli fulani ya kufanya * Kufanya pia yaweza kuwa na maana ya kufanya dhambi au kufanya uzinzi au kufanya uuaji. * Kujituma yaweza kutafsiriwa kama "kazi iliyotolewa" au "ahadi iliyotolewa."
## kufanywa haki ### Ufafanuzi Usemi "kufanywa haki" inamaanisha kumfanya mtu mwenye hatia kuwa mwenye haki. Mungu pekee ndiye awezaye kuwafanya watu kuwa na haki. Mungu anapowafanya haki watu, huwasamehe dhambi zao na kuwafanya kana kwamba hawana dhambi. Huwafanya haki watenda dhambi wanaotubu na kumuamini Yesu kuwaokoa kutoka dhambi zao. "kufanywa haki" inamaanisha kile Mungu anachofanya anaposamehe dhambi za mtu na kutamka kuwa mtu huyo ni mwenye haki machoni pake.
## kufinyanga ### Ufafanuzi Kufinyanga ni kutengeneza mbao, chuma, au udogo ilikutimia kuunda umbo kutokana na dhahabu, fedha, au vitu vingine vinavyo weza kumika kwa kufinyangwa. * Vituvya ufinyazi vilitumika kutengeneza mikufu, vyombo, na vitu vya kulia. * Katika Biblia, vitu vya ufinyazi vinatumika mara nyingi kwa kutengeneza sanamu. * Chuma zilipaswa kuchomwa ili kwamba viweze kufinyangwa.
## Kufurani ### Ufafanuzi Kufurahi inamaana ya kuwa na furaha. * Neno hili limetumika kuelezea hali ya kuwa na furaha sana juu ya mambo mazuri aliyoyafanya Mungu. * Hii inaweza kutafsiriwa kama "kuwa na furaha sana." * Mariamu aliposema kuwa "nafsi yangu inafurahi ndani ya Mungu mwokozi wangu" alimaanisha kuwa "Mungu mwokozi wangu amenifanya kuwa na furaha" au " ninasikia furaha kwa sababu ya kitu ambacho Mungu mwokozi wangu amefanya kwangu."
## kufuru ### Ufafanuzi Neno la "kufuru" lina maana ya kuharibu au kuchafua sehemu takatifu au kitu katika namna ambayo haikubaliki kutumika katika kuabudu. Mara kwa mara kukufuru kitu inahusisha kuonyesha okosefu mkubwa wa keshima kwake. Kwa mfano, wafalme wa kipagani walikufuru vyombo maalumu kutoka hekalu la Mungu kwa kuvitumia kwa ajili ya sherehe katika kasri zao. Mifupa kutoka watu waliokufa ilitumika na maadui kukufuru madhabahu katika hekalu la Mungu. Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama, "kusababisha kutokuwa mtakatifu" au "kumvunjia heshima kwa kufanya asiwe mtakatifu" au "kukufuru kwa kuvunja heshima" au "kusababisha kutokuwa msafi".
## kufuta ### Ufafanuzi Maneno "kufuta" au "kuondoa" ni vifungu vinavyomaanisha kuondoa kabisa au kuangamisa kitu au mtu. * Vifungu hivi vyaweza kutumika katika maana chanya, kama ambavyo Mungu "hufuta" dhambi kwa kusamehe na kuchagua kutokukumbuka tena. * Lakini pia yaweza kutumika katika maana mbaya, kama ambavyo Mungu "hufuta" au "kuondoa" kundi la watu, kuwaharibu kwa sababu ya dhambi. * Biblia inazungumzia juu ya jina la mtu "kufutwa" au "kuondolewa" katika kitabu cha Mungu, kumaanisha mtu hatapokea uzima wa milele. ### Maone ya Kutafasiri * Kwa kutegemea mazingira, vifungu hivi vyaweza kutafasiriwa kama "kuondoa" au "kutoa" au " kuharibu kabisa" au "kuondoa kabisa." * Kwa kurejerea kufuta jina la mtu katika Kitabu cha Uzima, yaweza kutafasiriwa kama "kuondoa kutoka" au "iliyofutwa."
## Kugawa, kupewa ### Ufafanuzi Kugawa au kupewa ni kitendo cha kumteua mtu kwa ajili ya kufanya kazi maalumu. * Nabii Samweli aliambiwa kuwa mfalme Sauli atateua vijana wazuri wa Israeli kwa ajili ya kulihudumia jeshi. * Musa aliwapa kila kabila la Israeli sehemu ya ardhi ya Kaanani ili waishi. * Katika sheria ya agano la kale, baadhi ya makabila walipewa kazi ya kuwahudumia makuhani, waimbaji na wajenzi. * Neno kugawa li naweza kutafsiriwa kama "kuchagua" au "kupewa kazi."
## kuhamisha, Uhamisho ### Ufafanuzi Msemo "kuhamisha" una maana ya watu waliolazimishwa kuishi mahali mbali na nchi yao ya nyumbani. Watu mara kwa mara hutumwa uhamishoni kwa ajili ya adhabu au sababu za kisiasa. Watu walioshindwa wanaweza kupelekwa uhamishoni katika nchi ya jeshi iliyowashinda ili kuwafanyia kazi. "Uhamisho wa Babeli" (au "Uhamisho") ni kipindi katika historia ya Biblia ambapo raia wengi wa Kiyahudi wa eneo la Yuda walichukuliwa kutoka nyumbani mwao na kulazimishwa kuishi Babeli. Ilidumu miaka 70. Msemo "waliohamishwa" una maana ya watu ambao wanaishi katika uhamisho, mbali na nchi yao ya nyumbani. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo wa "kuhamisha" unaweza kutafsiriwa kama "kufukuza" au "kulazimisha kutoka nje" au "kuondoa". Msemo "Uhamisho" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana "muda ambao walifukuzwa" au "muda wa kufukuzwa" au "muda wa kulazimishwa kutokuwepo" au "kuondolewa". Njia za kutafsiri "waliofukuzwa" zinaweza kujumuisha, "watu waliofukuzwa" au "watu ambao waliondolewa" au "watu walifukuzwa kwenda Babeli"
## Kuhani mkuu ### Ufafanuzi Kuhani mkuu alikuwa kiongozi wa muhimu sana katika dini ya kiyahudi wakati ambao Yesu aliishi duniani. * Makuhani mkuu walikuwa na wajibu kwa kila kitu kilichohitajika katika ibada ya kuabudu hekaluni. Pia walikuwa wanasimamia pesa zilizotolewa hekaluni. * Kilikuwa ni cheo cha juu na chenye nguvu kuliko cha kuhani. Kunahi wa juu ndiye aliyekuwa na mamlaka. * Makuhani wakuu baadhi yao walikuwa maadui wa Yesu na waliwashawishi sana viongozi wa Kirumi wamkamate Yesu na wamuue.
## Kuharibu ### Ufafanuzi Kuharibu kitu ni hali ya kuangamiza, kukiteketeza au kukifanya kisiwe na maana tena. * Nabii Zefania anazungumza juu ya siku ya ghadhabu ya Mungu kama "siku ya kuharibu" ambapo ulimwengu utahukumiwa na kuadhibiwa. * Katika kitabu cha Mithali kinasema kuharibu na kuteketeza kunawasubiri wale wasio na Mungu. * Kutegemeana na mukhtadha kuharibu yaweza kutafsiriwa kama "kuangamiza" au "kufanya isifae" au "kuvunja" au "uharibifu."
## Kuhitimu, waliohitimu ### Ufafanuzi Neno "kuhitimu" ni kitendo cha kupata haki ya kupokea faida fulani au kujulikana kwa kuwa na ujuzi fulani. * Mtu aliyehitimu kwa ajili ya kazi fulani ana ujuzi na amefundishwa kwa ajili ya kazi hiyo. * Katika barua ya mtume Paulo kwa kanisa la Korintho aliandika kuwa Mungu baba amewafanya waamini kuhitimu katika kushiriki kwenye ufalme wa mwanga. * Mwamini hawezi kupata haki ya kuwa sehemu ya ufalme wa Mungu. Bali anahitimu kwa sababu Mungu amemkomboa yeye kwa damu ya Kristo.
## Kuhubiri ### Ufafanuzi Kuzungumza na kundi la watu kuwafundisha kuhusu Mungu na kuwasihi wamtii Mungu. * Mara nyingi kuhubiri hufanywa na mtu mmoja kwa kundi kubwa la watu. Mara nyingi huzungumzwa na sio kuandikwa. * "kuhubiri" na "kufundisha" ni sawa japo haifanani sana. * "Kuhubiri" ni kitendo cha kutanganza hadharani ukweli wa kiroho na kuwasihi wasikilizaji watekeleze. "Kufundisha" ni kitendo cha kusisitiza maelekezo yanayotolewa kwa watu au kuwafundisha kitu cha kufanya. * Neno "kuhubiri" mara nyingi kunaambatana na neno "injili."
## Kuinama chini ### Ufafanuzi ## Kuinama maana yake kujikunja kwa unyenyekevu kuonesha heshima kwa mtu. "Kuinama chini" inamaanisha kupiga magoti chini sana, kwa kawaida uso na mikono ikielekea ardhini. * Viashiria vingine ni pamoja na "kupiga goti" na "kuinamisha kichwa"( maana yake ni kuinamisha kichwa mbele kwa heshima ya unyenyekevu au katika huzuni). * Kuinama chini pia kwaweza kuwa ishara ya mfadhaiko au maombolezo. Mtu "anayeinamishwa chini" amewekwa katika kiwango cha chini sana cha unyenyekevu. * Kwa kawaida mtu atainama mbele ya mtu mwenye heshima ya juu kuliko yake au mwenye umuhimu mkubwa, kama wafalme na viongozi wengine. * Kuinama mbele ya Mungu ni ishara ya kumwabudu. * Katika Biblia, watu walimwinamia Yesu walipotambua kutokana na miujiza yake na mafundisho yake kwamba alikuwa ametoka kwa Mungu. * Biblia inasema kwamba Yesu atakaporudi, kila mtu atapiga goti kumwabudu. ### Maoni ya Kutafasiri * Kwa kutegemea na mazingira, neno hili laweza kutafasiriwa kwa neno au kifungu kinachomaanisha, "kuinamia" au "kuinamisha kichwa" au "piga goti". * Neno "inama chini" laweza kutafasiriwa kama "Piga magoti" au "jinyenyekesha". * Baadhi ya lugha zitakuwa na njia zaidi ya moja ya kutafasiri neno hili, kutegemea na mazingira.
## kujiamini, ujasiri ### Ufafanuzi Kujiamini ni kuwa na uhakika kuwa jambo fulani ni la kweli au litatokea. * Katika Biblia neno "tumaini" linamaana ya kusubiri kwa kutegemea jambo fulani litakalotokea. Hii pia imetafsiriwa kama kujiamini hasa inapokuwa na maana ya kuwa na uhakika wa kupokea ambacho Mungu alikiahidi kwa wanaomwamini Yesu. * Kujiamini inamaana ya uhakika ambao wanaomwamini Yesu wanao kuwa siku moja watakuwa na Mungu mbinguni. * "kuwa na ujasiri kwa Mungu" inamaana kuwa kutegemea kupokea yale ambayo Mungu ameahidi. * Kuwa na ujasiri inamaanisha kuwa kuamini katika ahadi za Mungu na kujua kuwa Mungu ataafanya kama alivyosema.
## Kujivuna ### Ufafanuzi Kujikweza ni kitendo cha mtu kujivuna au kuwa na majivuno. * Mtu anayejivuna ana tabia ya kujiona bora kuliko wengine. * Paulo anazungumza kuwa kufahamu mambo mengi au kujua mambo ya dini kunaweza kusababisha mtu akajivuna. * Pia inaweza kutafsiriwa kama "kujivunia" au "kuwabeza wengine" au "kujiona bora kuliko wengine."
## Kujua kabla ### Ufafanuzi Msemo "kujua kabla" unatokana na maana ya kujua jambo kabla halijatokea. Mungu hazuiliwi na muda. Anajua kila kitu ambacho hutokea kipindi cha nyuma, sasa na baadaye. Neno hili mara kwa mara hutumika katika muktadha ya Mungu kujua tayari nani ataokolewa kupitia kumpokea Yesu Kristo. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "kujua kabla" unaweza kutafsiriwa kama "kujua kabla" au "kujua kabla ya wakati" au "kujua kabla ya" au "kujua tayari".
## kujua, ufahamu, kufanya kujulikana ### Ufafanuzi "Kujua" inamaanisha kuelewa kitu au kuwa na ufahamu wa jambo. Usemi "kufanya kujulikana" ni usemi unaomaanisha kutoa taarifa. Neno "ufahamu" linamaanisha taarifa ambazo watu wanajua. Inaweza kuwa kujua vitu katika dunia ya kimwili na kiroho. "Kujua kuhusu" Mungu inamaanisha kuelewa mambo kumhusu kwa sababu ya yale aliyotufunulia. "Kumjua" Mungu inamaanisha kuwa na uhusiano naye. Hii inamaanisha pia kuwajua watu wake. Kujua mapenzi ya Mungu inamaanisha kuwa na ufahamu wa yale aliyetoagiza, au kuelewa ni nini anataka mtu afanye. "Kujua Sheria" inamaanisha kuwa na ufahamu wa yale Mungu aliyoagiza au kuelewa yale Mungu aliyoagiza katika sheria alizompa Musa. Wakati mwingine "ufahamu" unatumika kama neno lingine la "hekima," linalojumuisha kuishi katika njia inayompendeza Mungu. "Ufahamu wa Mungu" wakati mwingine unatumika kama njia nyingine ya kusema hofu ya Yahwe.
## kukandamiza, ukandamizaji, mkandamizaji ### Ufafanuzi Meneo, "kukandamiza," "ukandamizaji," "mkandamizaji" ya husu kumtendea mtu kwa ukali. "mkandamizaji" ni mtu anaye kandamiza watu. * Neno "ukandamizaji" haswa la husu hali watu wa nguvu kubwa wanapo tendea vibaya au kufanya watumwa watu waliyo chini ya nguvu au utawala wao. * Neno "kukandamizwa" la eleza watu wanao tendewa vibaya. * Mara nyingi mataifa ya maadui na viongozi wao walikuwa wakandamizaji kwa watu wa Israeli.
## Kukataa ### Ufafanuzi "Kukataa" kitu au mtu inamaana kuacha kumkubali mtu au kitu. * Neno kukataa pia laweza kuwa na maana ya kuacha kuamini kwenye kitu fulani. * Kumkataa Mungu inamaana kutomtii Yeye. * Waisraeli walipomkataa kiongozi wao Munsa inamaana kuwa walikuwa wanaasi dhidi ya mamlaka yake. Hawakutaka kumtii. * Waisraeli walionesha kuwa walimkataa Mungu walipoabudu miungu ya uongo/
## Kukatwa ### Ufafanuzi Kukatwa ni kitendo cha kuondolewa, kufukuzwa au kutengwa toka kwenye kundi. Pia inaweza kuwa na maana ya kuuawa kama tendo la hukumu kwa ajili ya dhambi. * Katika agano la kale kutotii amri za Mungu hupelekea kukatwa au kutengwa na watu wa Mungu na uwepo wake. * Mungu pia alisema atawakata au kuwaharibu mataifa ambayo sio Waisraeli kwa sababu hawakumwabudu au kumtii yeye na walikuwa maadui wa Israeli. * Pia kukata inaweza kutumika kuonesha Mungu akisababisha mtu kuacha kutiririsha maji.
## Kukemea ### Ufafanuzi Kukemea ni kitendo cha kumrekebisha mtu ili kumsaidia mtu yule kuacha dhambi. * Katika agano jipya linawaamuru Wakristo wawakemee waamini wengine wanapoacha kumtii Mungu. * Katika kitabu cha Mithali kinaelekeza wazazi kuwakemea watoto wao wanapoacha kuwa watii. * Kukemea ni kumzuia mtu aliyetenda dhambi asirudie tena kutenda dhambi. * Kukemea pia kunaweza kutafsiriwa kama marekebisho.
## kukesha ### Ufafanuzi Katika nyakati za Biblia, "kukesha" ulikuwa wakati wa usiku ambao katika huo mlinzi au mwangalizi wa mji alikuwa kazini akiangalia hatari yoyote kutoka kwa maadui. * Katika Agano la Kale, Waisraeli walikuwa na zamu tatu zikiitwa "mwanzo"( machweo hadi saa 4:00 usiku), "katikati" (saa 4:00 usiku hadi saa 8:00 usiku), na "asubuhi" (saa 8:00 hadi mawio). * Katika Agano Jipya, Wayahudi walifuata mfumo wa Kirumi na walikuwa na zamu nne, zikiitwa "ya kwanza" (machweo hadi saa 3 usiku) "pili" (3 usiku hadi saa 6 usiku), "tatu" (6 usiku hadi 9 usiku), na ya "nne" (saa 9 hadi mawio). * Hizi pia zaweza kutafasiriwa kwa vifungu vya jumla kama vile "jioni" au "katikati ya usiku" au "alfajiri," kutegemea na zamu inayotajwa.
## Kula ### Ufafanuzi Kula ni kitendo cha kutumia kitu fulani. Pia ina maana nyingine. * Katika Biblia kutumia inamaana ya kuharibu vitu au watu. * Moto unaelezewa kula vitu ikiwa na maana ya kuharibu kwa kuviteketeza kwa moto. * Mungu anajielezea kama moto ulao akiwa na maana ya kuelezea hasira yake dhidi ya dhambi. Hasira yake inasababisha adhabu kali kwa watenda dhambi wasiotubu. * Kula chakula ni kitendo cha kuchukua na kula chakula au kinywaji. * "kuila nchi" inamaana ya "kuiharibu nchi."
## kulala na, kuwa na mahusiano na, fanya mapenzi ### Ufafanuzi Katika Biblia, haya maneno ni tafsida yanayo eleza kufanya ngono. * "kulala na" mtu ni namna maarufu ya kueleza kuwa na mahusiano ya kimapenzi. * Katika Agano la Kale, "Wimbo wa Sulemani," tafsiri ya ULB inatumia "kufanya mapenzi" kutafsiri neno "mapenzi," ambalo katika muktadha la eleza mahusiano ya kingono. Hii ina husiano na msemo, "kufanya mapenzi na."
## kulewa, mlevi ### Ufafanuzi Msemo "kulewa" ina maana ya kuleweshwa kutokana na kunywa kileo. "Mlevi" ni mtu ambaye hulewa mara kwa mara. Mtu wa aina hii anajulikana kama "mlevi". Biblia inawaambia waumini kutolewa na vilevi, lakini kutawaliwa na Roho Mtakatifu wa Mungu. Biblia inafundisha ya kwamba ulevi sio busara na inamshawishi mtu kutenda dhambi kwa njia zingine. Njia zingine za kutafsiri "kulewa" zinaweza kujumuisha "levya" au "kulewa" au "kupata kilevi kingi sana" au "kushiba kwa kinywaji chachu"
## kumbukumbu, sadaka ya kumbukumbu ### Ufafanuzi Neno "kumbukumbu" la husu tendo au kitu kinacho msababisha mtu au kitu kukumbukwa. * Hili neno linatumika kama kitenzi kueleza kitu kitakacho wakumbusha kuhusu kitu, kama katika "sadaka ya kumbukumbu," au "mawe ya kumbukumbu" * Katika Agano la Kale sadaka ya kumbukumbu ilitolewa ili Waisraeli wakumbuke ni Mungu alicho wafanyia. * Mungu aliwaambia makuhani wa Kiisraeli kuvaa mavazi maalumu yaliyo kuwa na mawe. Haya mawe yalikuwa na majina ya makabila kumi na mbili ya Israeli yaliyo andikwa juu yake. Hii ilikuwa kuwa kumbusha kuwa uwaminifu wa Mungu kwao. * Katika Agano Jipya, Mungu alimueshimu mtu mwenye jina Kornelio kwasababu ya matendo yake mema kwa maskini. Haya matendo yalisemwa kuwa "kumbukumbu" mbele za Mungu.
## Kumiliki, Miliki ### Ufafanuzi "Kumiliki" au "miliki" ni kitendo cha kuwa na kitu fulani. Pia inaweza kuwa na maana ya kuwa na mamlaka juu ya kitu fulani au kumiliki eneo la ardhi. * Katika agano la kale neno hili limetumika kama kumiliki ardhi katika eneo. * Bwana alipowaamuru Waisraeli wamiliki nchi ya Kanaani inamaanisha kuwa walitakiwa kwenda kwenye nchi ile na kukaa huko. Hii inajumuisha kuwashinda watu wa Kanaani waliokuwa wakiishi huko. * Bwana aliwaambia Waisraeli kwamba amewapa nchi ya Kanaani kama milki yao. Hii inaweza kutafsiriwa kama "sehemu sahihi ya kuishi."
## Kumuachia ### Ufafanuzi Neno "kumuachia" lina maana ya kukiri wazu kuwa mtu fulani hana hatia kwa kosa fulani au tabia fulani alikuwa ameshitakiwa. * Neno hili wakati mwingine kwenye Biblia hutumika kuzungumzia juu ya kusamehewa dhambi. * Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutangaza hana hatia"
## kumwaga damu ### Ufafanuzi Neno "kumwaga damu" linamaanisha kifo cha mwanadamu kwa sababu ya mauaji, vita, au sababu nyingine ya kikatiri. * Neno hili "kumwaga damu," kwa kawaida linamaanisha wakati damu inapotoka katika jeraha katika mwili wa mtu. * Neno "kumwaga damu" linatumika mara kwa mara kurejerea mauaji ya watu yaliyoenea. * Lakini pia linatumika kama kumbukumbu ya jumla kwa dhambi ya kuuwa. ### Maoni ya Kutafasiri * "Kumwaga damu" kwaweza kutafasiriwa kama, "mauaji ya watu" au "watu wengi waliouawa". * "Kupitia umwagaji wa damu" yaweza pia kutafasiriwa kama, "kwa kuuwa watu." * "Kumwaga damu ya wasio na hatia" yaweza kutafasiriwa kama "kuuwa watu wasio na hatia". * "Kumwaga damu kunafuata kumwaga damu" kwaweza kutafasiriwa kama, "wanaendelea kuuwa watu" au "kuuawa kwa watu kunaendelea" au "wameua watu wengi na wanaendelea kufanya hivyo" au "watu wanaendelea kuuwa wengine." * Matumizi mengine ya tamathari, "kumwaga damu kutakufuata" kwaweza kutafasiriwa kama "watu wako wataendelea kushuudia mauaji" au "watu wako wataendelea kuuawa" au "watu wako wataendelea kuwa katika vita na mataifa mengine na watu wataendelea kufa.
## Kundi la watu, watu ### Ufafanuzi "Watu" au "kundi la watu" linamaana ya makundi ya watu wenye lugha moja na utamaduni mmoja. Pia yaweza kuwa na maana ya watu waliokusanyika sehemu fulani au kwa ajili ya tukio fulani. * Mungu alipotenga "watu" kwa ajili yake inamaanisha aliwachagua watu wawe wake na wamtumikie yeye. * Katika nyakati za Biblia kundi la watu mara nyingi lilikuwa na mababu na waliishi pamoja katika nchi fulani au eneo fulani la nchi. * Inategemea na lengo katika kifungu fulani "watu wako" inaweza kuwa na maana ya "kundi lako la watu" au "famila yako" au "ndugu zako" * Neno "Watu" mara nyingi hutumika kuelezea watu wa makundi yote duniani.
## kundi, mifugo ### Ufafanuzi Katika Biblia "kundi" ina maana ya kundi la kondoo na mbuzi na "mifugo" ina maana ya kikundi cha ng'ombe, maksai, au nguruwe. Lugha tofauti zinaweza kuwa na njia tofauti za kutaja makundi ya wanyama au ndege. Kwa mfano, katika Kiingereza msemo "kundi" unaweza pia kutumika kwa ajili ya kondoo au mbuzi, lakini katika maandishi ya Biblia haitumiki kwa njia hii. Msemo "kundi" katika Kiingereza pia hutumika kwa ajili ya kundi la ndege, lakini unaweza kutumika kwa ajili ya nguruwe, maksai au ng'ombe. Fikiria ni misemo gani inatumika katika lugha yako kumaanisha makundi tofauti ya wanyama. Kwa mistari ambayo ina maana ya "makundi au mifugo" inaweza kuwa bora kuongeza "ya kondoo" au "ya ng'ombe" kwa mfano, kama lugha haina maneno tofauti kumaanisha aina tofauti za makundi ya wanyama.
## kuomba ### Ufafanuzi Neno "kuomba" lamaanisha kumwomba mtu kitu fulani kwa umuhimu. Mara kwa mara inamaanisha kuomba pesa, lakini pia limetumika kuonesha kuombeleza jambo fulani. * Mara kwa mara watu wanaomba wakati wanapoitaji jambo fulani kwa uzito, lakini wasijue kwamba kuna mtu atawapa waombacho. * "Mwombaji" ni mtu ambaye mara kwa mara hukaa au kusimama katika maeneo ya wazi kuomba pesa kwa watu. * Kwa kutegemea mazingira, neno hili lingetafsiriwa kama "kusihi" "omba kwa uzito" "kudai pesa" au "kuomba pesa mara kwa mara."
## kuomboleza ### Ufafanuzi "Kuomboleza" kwa husu huzuni ya ndani, mara nyingi wakati wa kifo cha mtu. * Katika tamaduni nyingi, kuomboleza kuna kuna husisha matendo ya njee yanayo onyesha uzuni. * Waisraeli na watu wengine zama za kale walionyesha kwa kilio kikubwa. Pia walivaa nguo za magunia na majivu. * Waombolezaji wakuajiriwa, wanawake sana sana, walilia kwa sauti kutoka kipindi cha kifo hadi mwili kuzikwa kaburini. * Kipindi cha kuomboleza kilikuwa siku saba, lakini ziliweza kwenda hadi siku thelathini (kama Musa na Aruni) au siku sabini (kama za Yakobo)
## kupiku ### Ufafanuzi Neno "kupiku" ina maana ya kupata uweza juu ya mtu au kitu. Mara nyingi ina maana ya kufikia kitu na kukipita baada ya kukufukuzia. * Wakati majeshi "yakipiku" adui, ina maana wamemshinda adui vitani. * Mnyama mwindaji anapo piku windo lake, ina maana kuwa imemkimbiza na kumkamata adui yake. * Kama laana "ikipiku" mtu, ina maana kuwa chochote kilicho semwa kwenye laana hiyo kitatokea. * Kama baraka zita wapiku watu, ina maana kuwa hao watu watapata hizo baraka. * Kulingana na muktadha, "kupiku" ya weza tafsiriwa kama "kushinda" au "kuchukuwa" au "kufikia" * Linapo tumika kama onyo kuwa giza au adhabu lita pikuwa watu kwasababu ya dhambi zao, ina maana kuwa hao watu watapata vitu vibaya kama wasipo tubu.
## Kupokea ### Ufafanuzi Kupokea ni kupata au kukubali kitu unachopewa au kuletewa. * "Kupokea" pia yaweza kumaanisha kuteseka au kupitia jambo fulani kama "alipokea adhabu kwa alichokifanya." * Pia kuna namna ya pekee ya kumpokea mtu. Kwa mfano kumpokea mgeni inamaanisha kumkaribisha na kumfanyia jambo la heshima ili kujenga mahusiano naye. * "Kupokea zawadi ya roho mtakatifu" inamaanisha tumepewa roho mtakatifu na kumkaribisha afanye kazi kwenye maisha yetu. * Kumpokea Yesu inamaana kukubali wokovu wa Yesu kwa njia ya Yesu Kristo. * Yule kipofu alipopokea uponyaji inamaana kuwa Mungu alimponya na kumuwezesha kuona tena.
## Kupotea, akipotea, kupotoshwa ### Ufafanuzi Kupotea ina maana ya kutomtii Mungu. Watu wanaopotoshwa wamewaruhusu watu wengine kuwasababisha wasimtii Mungu. * Kupotea inatuppa picha sahihi ya kuacha njia nzuri au sehemu salama na kwenda njia mbaya au sehemu yenye hatari. * Kondoo wanaoacha malisho wanayopewa na mchungaji wao Mungu anawafananisha wa watu waliomuacha yeye.
## kupumua, pumzi ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "kupumua" na "pumzi" yanatumika mara kwa mara kitamathari kumaanisha kutoa uhai au kuwa na uhai. * Biblia inafundisha kwamba Mungu "alimpulizia" Adamu pumzi ya uhai. Ikawa Adamu akawa kiumbe hai. * Wakati Yesu alipowapulizia wanafunzi na kuwaambia "pokeeni Roho," pengine kiualisia alipulizia hewa kwao kumaanisha "Roho Mtakatifu kuja kwao. * Wakati mwingine neno "kupumua" na "kupumua nje" yanamaanisha kuongea. * Kifungu cha kitamathali "pumzi ya Mungu" au "pumzi ya Yahwe" mara kwa mara inarejerea gadhabu ya Mungu ikimiminwa kwa uasi au mataifa yasiyomcha Mungu. Inaonesha nguvu yake. ### Maoni ya Kutafasiri * Kifungu "alipumua mara ya mwisho" inamaanisha kusema "alikufa." Inaweza pia ikatafasiriwa kama, "alichukua pumzi yake ya mwisho" au "aliacha kupumua na akafa" au "alivuta pumzi mara ya mwisho." * Kuelezea Maandiko kama "Pumze ya Mungu" inamaanisha Mungu alisema au aliyatia nguvu maneno ya Maandiko ambayo baadaye wanadamu waliandika. Pengine inafaa zaidi, ikiwa inawezekana, kutafasiri "enye kupuliziwa na Mungu" kwa kawaida kwa kuwa ni vigumu kuwasilisha maana yake halisi. * Ikiwa tafasiri ya moja kwa moja ya "enye pumzi ya Mungu" haikubaliki, njia nyingine yaweza kutumika, "kuongozwa na Mungu" au "kuandikwa na Mungu" au "kusemwa na Mungu." Yaweza pia kusemwa kwamba "Mungu alipuliza neno la Maandiko." * Kifungu "kuweka pumzi ndani" au kupulizia uhai ndani ya" au "kutoa uhai kwa" yaweza kutafisiriwa kama, "kusababisha kupumua" au "kufufua" au "kuwawezesha kuishi na kupumua" au "kumpa uzima." * Ikiwa inawezekana, ni vema kutafasiri "pumzi ya Mungu" kwa neno halisi litumikalo kwa "pumzi" katika lugha. Ikiwa Mungu hasemwi kuwa na "pumzi" hii itafasiriwe kama "nguvu ya Mungu" au "sauti ya Mungu." * Kifungu "shika pumzi yangu" au "pata uzima wangu" itafasiriwe kama, "tulia ili upumua taratibu" au "acha kukimbia ili upumue kawaida. * Kifungu "ni pumzi tu" chamaanisha "inaishia kitambo kidogo". * Vilevile kifungu "mtu ni pumzi moja" chamaanisha "watu huishi muda mfupi sana" au "maisha ya wanadamu ni mafupi sana, kama pumzi moja" au "kwa kulinganisha na Mungu, maisha ya mtu yaonekana mafupi sana kama inavyochukua kuvuta pumzi mara moja."
## kura, kupiga kura ### Ufafanuzi "Kura" ni kitu kilichowekwa alama kinachochaguliwa miongoni mwa vitu vya kufanana kama naamna ya kuamua jambo. "Kupiga kura" inamaanisha kurusha vitu vilivyo wekwa alama kwenye sakafu au ardhi yoyote. Mara nyingi kura yalikuwa mawe madogo yenye alama au vipande vidogo vilivyovunjika vya udongo. Tamaduni zingine zinafanya "bahati nasibu" au "kuvuta" kura kwa kutumia majani makavu. Mtu anayashikilia majani makavu ili asiwepo wakuona yana urefu gani. Kila mtu anavuta jani na yule atakayepata jani kavu refu zaidi (au fupi) ndiye atakayekuwa amechaguliwa. Zoezi la kupiga kura lilitumika na Waisraeli kujua ni nini Mungu aliwataka wafanye. Kama nyakati za Zekaria na Elisabeti, ilitumika pia kuchagua ni kuhani yupi atatenda jukumu bayana hekaluni katika muda maalumu. Askari walio msulubisha Yesu walipiga kura kuamua ni nani atakaa na joho la Yesu. Usemi "kupiga kura" inawezakutafsiriwa kama "kufanya bahati nasibu" au "kurusha kura". Kulinga na mazingira, neno "kura" inaweza pia kutafsiriwa kama "jiwe lenye alama" au "kipande cha udongo" au "kijiti" au "kipande cha jani." Kama maamuzi yakifanyika "kwa kura" hii inaweza kutafsiriwa kama "kufanya bahati nasibu (au kurusha) ya kura."
## kusaliti ### Ufafanuzi Neno "kusaliti" lamaanisha tendo la kumdanganya na kumdhuru mwingine. "Msaliti" ni mtu amsalitiye rafiki yake mwenye kumwamini. * Yuda alikuwa "msaliti" kwa sababu aliwaeleza viongozi wa Kiyahudi jinsi ya kumkamata Yesu. * Tendo la Yesu kuwalitiwa na Yuda ulikuwa uovu kwa sababu alikuwa mwanafunzi wake aliyepokea pesa kama malipo juu ya habari aliyowapa ya kumkamata Yesu kwa kifo kisicho cha haki. ### Maoni ya Tafasiri * Kwa kutegemea mazingira, neno "kusaliti" laweza kutafasiriwa kama "kudanganya na kusababisha madhara" au "kumsaidia adui" au "kufanya uhaini." * Neno "msaliti" laweza kutafasiriwa kama "mtu asalitiye" au "mfanya biashara mbili" au "msaliti."
## kusanya, kukusanya ### Ufafanuzi Msemo "kusanya" una maana ya kupita katika shamba au shamba la matunda kuokota nafaka yoyote au tunda ambao wavunaji wameacha nyuma. Mungu aliwaambia Waisraeli kuruhusu wajane, watu maskini, na wageni kukusanya mabaki ya nafaka ili kwamba wapate chakula kwa ajili yao. Mara nyingine mmiliki wa shamba angeruhusu wakusanyaji kwenda moja kwa moja nyuma ya wavunaji kukusanya, ambayo iliwawezesha wao kukusanya nafaka zaidi. Mfano wa wazi ni jinsi hii ilivyofanya kazi katika simulizi ya Ruhtu, ambaye aliruhusiwa kwa ukarimu kukusanya miongoni mwa wavunaji katika mashamba ya ndugu wa Boazi.
## Kushangaa, kushangaza ### Ufafanuzi "Kushangaa" ni hali ya mshangao na heshima kubwa inayokuja baada ya kuona jambo kubwa limefanyika na lenye nguvu. * "kushangaza" ni hali ya mtu au kitu kusababisha hali ya kushangaa. * Maono ya utukufu wa Mungu aliyoyaona nabii Ezekieli yalikuwa ya kushangaza. * Katika kuonesha hisia za kibinadamu pale ambapobinadamu anatambua kuwa Mungu anashangaza mara nyingi huogopa, husujudu au kupiga magoti, hufunika uso wake na kutetemeka.
## Kushangaa, mshangao ### Ufafanuzi Maneno haya yote yanamaana ya kushangazwa kwa sababu ya jambo fulani lisilo la kawaida ambalo limetokea. * Baadhi ya maneno haya yanatafsiriwa kwa Kigiriki yakiwa na maana ya "akapigwa kwa mshangao." Hii inaelezea ni kwa namna gani mtu amejisikia baada ya kushanganwa na jambo fulani. * Mara nyingi tukio linalosababisha mshangao ni muujiza ambao Mungu pekee ndo mwenye uwezo wa kufanya. * Maana nyingine ya maneno haya hujumuisha hisia za kuchanganyikiwa kwa sababu jambo lililotokea halikutegemewa kabisa. * Kwa ujumla maneno haya hutumika kwa mtazamo chanya kwamba watu wana furaha juu ya jambo fulani lililotokea.
## Kusifu ### Ufafanuzi Kumsifu mtu ni kuonesha pongezi au heshima kwa mtu yule. * Watu wanamsifu Mungu kwa namna alivyo mkuu na kwa sababu ya mambo ya ajabu anayoyafanya kama muumbaji na mwokozi wa dunia. * Kumsifu Mungu kunajumuisha kumshukuru kwa aliyoyafanya. * Muziki na kuimba hutumiwa kama njia ya kumsifu Mungu. * Kumsifu Mungu ni sehemu ya kumwabudu. * Neno "kusifu" yaweza kutafsiriwa kama "kusema mazuri" au "kusifia kwa maneno."
## Kusihi, ng'ang'ania ### Ufafanuzi "Kusihi" inamaana ya kumuomba mtu afanye jambo fulani. Ng'ang'ania ni ombi la haraka. * Kusihi ni kitendo cha mtu kuwa katika hali ya uhitaji mkubwa na anahitaji msaada. * Watu wanaweza wakamsihi Mungu kwa haraka awahurumie au kumuomba awapatie kitu fulani kwa ajili yao au kwa ajili ya watu wengine. * Njia nyingine za kutafsiri neno hili yaweza kuwa "kuomba."
## kusimika ### Ufafanuzi Kusimika kuna maana ya kuteuwa mtu kwa kazi maalumu au jukumu. Pia ina maana ya kufanya uamuzi au tamko. * Neno "kusimika" mara nyingi umaanisha kuteuwa mtu kuwa kuhani, mtumushi, au rabi. * Kwa mfano, Mungu aliwasimika Aruni na uzao wake kuwa makuhani. * Lina weza kuanzisha au kuimarisha kitu, kama sherehe ya dini au agano.
## Kusujudu ### Ufafanuzi Kusujudu ni kitendo cha kuinamisha uso chini kwenye ardhi. * "Kusujudu" mbele ya mtu kuna maana ya kuinama mbele ya huyo mtu. * Kitendo cha kusujudu ni kitendo cha kuonesha hofu kwa sababu muujiza fulani umetokea. Pia inaonesha heshima kwa mtu anayesujudiwa. * Kusujudu pia ni njia moja wapo ya kumwabudu Mungu. Watu wengi walifanya hivi kwa Yesu kama kumshukuru na kumwabudu baada ya kufanya muujuza fulani au kuonesha heshima kwa mafundisho yake mazuri.
## Kusukuma ### Ufafanuzi Hiki ni kitendo cha kuhamisha kitu kimwili kwa kutumia nguvu. Kuna maana mbali mbali za neno hili * "Kusukuma mbali" inamaana ya "kukataa" au "kukataa kusaidia." * "Kusukumachini" inamaana ya "kunyanyasa" au "kutesa." Pia yaweza kuwa namaana ya kusukuma kitu kwenda chini. * "Kusukuma mbele" inamaana ya kuvumilia au kuendelea kufanya jambo.
## Kutangaza, tangazo ### Ufafanuzi Kutanganza ni kitendo cha kutoa tamko hadharani. * Katika Biblia kutangaza nikutamka hadharani jambo ambalo Mungu ameliamuru au kuwaambia wengine juu ya Mungu na namna alivyo mkuu. * Katika agano jipya mitume walitangaza habari njema kuhusu Yesu kwa watu wengi katika miji mingi na mikoa. * Pia kutamka yaweza kutumiwa kama amri anayotolewa na wafalme kwa kupinga uovu katika jamii. * Neno "tangazo" pia laweza kutafsiriwa kama "kuhubiri hadharani."
## Kutawala ### Ufafanuzi Neno "kutawala" linamaana ya kuongoza kama mfalme juu ya watu wa nchi fulani au ufalme. Utawala wa kifalme ni wakati ambao mfalme alitawala. * Kutawala pia kunamuelezea Mungu anayetawala kama mfalme wa ulimwengu mzima. * Mungu aliwaruhusu wafalme wa kibinadamu kutawala juu ya Israeli walipomkataa yeye kama mfalme. * Yesu atakaporudi atatawala kama mfalme juu ya ulimwengu wote na Wakristo watatawala pamoja naye. * Hii pia yaweza kutafsiriwa kama "kutawala kama mfalme" au "kuongoza kama mfalme."
## Kutoboa ### Ufafanuzi "Kutoboa" ni kitendo cha kuchoma kitu kwa kutumia kitu chenye ncha. Pia hutumika kuelezea tendo la kusababisha maumivu makali ya kihisia kwa mtu. * Askari walimtoboa Yesu ubavuni alipokuwa msalabani. * Katika nyakati za Biblia mtumwa aliyeachiwa huru alitobolewa sikio kama ishara kuwa alichaguliwa kuendelea kufanya kazi kwa Bwana wake. * Simeoni anazungumza kwa lugha ya picha kumwambia maria kuwa upanga utatoboa moyo wake akimaanisha kuwa atapitia maumivu makali kwa kitakachotokea kwa Yesu mtoto wake.
## Kutupwa nje, kutupa nje ### Ufafanuzi "kutupwa nje" mtu au "kutupa nje" kitu inamaanisha kulazimisha kitu au mtu kuondoka. * Neno "kutupa" inamaanisha "kurusha." Kutupa nyavu inamaanisha kurusha nyavu. * Kumtupa mtu nje yaweza kuwa na maana ya kumkataa mtu na kumuondoa.
## Kuvika ### Ufafanuzi Kujivika na kitu ni kutafuta kuwa na tabia fulani. * Katika hali ya kawaida ya kuvaa inaonekana nje ya mwili wako na watu wote pia unapojivika tabia fulani nzuri watu wengine huona. "Kujivika wema" ina maana ya kuacha tabia zako zioneshe wema ambao utaonekana kwa kila mtu. * Kujivika nguvu toka juu ni kuwa na nguvu utakayopewa. * Pia neno hili linaweza kuwa na maana hasi kama "kujivika aibu" au "kujivika hofu."
## Kuvuna, mvunaji ### Ufafanuzi Kuvuna inamana ya kuvuna mazao kama nafaka. Mvunaji ni mtu anayevuna mazao. * Mara nyingi mvunaji huvuna mavuno kwa mkono kwa kung'oa mmea au kukata kwa kifaa chenye ncha kali. * Kuvuna mavuno pia hutumika kama lugha ya picha ikiwaelezea watu habari njema kuhusu Yesu na kuwaleta katika familia ya Mungu. * Pia huelezea matokeo anayoyapata mtu kutokana na matendo yake. "mtu atavuna alichokipanda.
## Kuwa "tasa" maana yake ni kutoweza kuzaa. ### Ufafanuzi Ardhi au nchi ambayo ni tasa haiwezi kuotesha mmea wowote. Mwanamke tasa ni yule asiyeweza kuzaa mto. Maoni ya Tafasiri Neno "tasa" linapotumika kurejerea nchi, lingeweza kutafasiriwa kama "isiyozaa" "isiyozalisha" au "isiyo na mimiea." Linapotumika kumtaja mwanamke mgumba, liliweza kutafasiriwa kama "asiye na mtoto" au "asiyeweza kuzaa watoto" au "asiyeweza kutunga mtoto."
## Kuwatesa, mateso ### Ufafanuzi "Kuwatesa" au "mateso" ni kitendo endelevu cha kumfanyia mtu au kundi la watu kitu katika namna mbaya ya kuwasababishia madhara. * Mateso yanaweza kuwa dhidi ya mtu mmoja au watu wengi na mara nyingi huhusisha mashambulizi ya kuendelea. * Waisraeli waliteswa na makundi mbalimbali ya watu waliowavamia, wakawakamata na kuwaibia vitu vyao. * Mara nyingi watu huwatesa watu wengine wenye dini tofauti na wao au wanyinge. * Dini ya Kiyahudi walimtesa Yesu kwa sababu hawakupenda alichokuwa akifundisha. * Baada ya Yesu kurudi mbinguni viongozi wa kidini wa Kiyahudi na serikali ya Rumi iliwatesa wafuasi wake. * "Mateso" pia yanaweza kutafsiriwa kama "manyanyaso."
## kuza ### Ufafanuzi Neno "kuza" lina maana ya kufanya kitu au mtu mkubwa au kuvuta umakini kwa ukuu wa mtu. * Linapo tumika kwenye Biblia, "kuza" mara nyingi la husu kutukuza mfalme au Mungu mwenyewe. * Mtu anapo jikuza yeye, ina maana ana jisifu na kujaribu kujifanya wa muhimu zaidi kuliko wengine.
## kuzidisha ### Ufafanuzi neno "kuzidisha" lina maana ya kuongezeka kiidadi. Pia yaweza kusababisha kitu kuongezeka kwa kiasi, kama vile kuzidisha maumivu. * Mungu aliwaambia wanyama na binadamu "kuongezeka" na kujaza dunia. * Yesu alifanya mkate na samaki kuongezeka ili kulisha watu 5000. Kiasi cha chakula kiliendelea kuongezeka kiasi kwamba kulikuwa na chakula zaidi kumlisha kila mtu. * Kulingana na muktadha, hili neno la weza tafsiriwa kama"ongeza" * Neno "kuongeza maumivu yako sana" ya weza tafsiriwa kama "maumivu yako kuwa makali sana" * "Kuzidisha farasi" ina maana ya "kuongeza farasi zaidi kwa tamaa"
## kuzika, zika ### Ufafanuzi ## Neno "zika" kwa kawaida linamaanisha kuweka kaburini mwili wa mtu aliyekufa. Neno "kuzika" ni kitendo cha kuzika kitu au linaweza kutumika kueleza sehemu itumikayo kuzikia. * Mara kwa mara watu uzika maiti kwa kuweka katika kaburi ardhini na kufukia kwa udongo * Wakati mwingine mwili huwekwa katika kitu chenye muundo wa boksi, kama vile jeneza kabla ya kuzika. * Nyakati za Biblia, mara kwa mara wafu walizikwa katika pango au eneo linalofanana na hilo. Baada ya Yesu kufa, mwili wake ulifunikwa kwa sanda na kuwekwa katika kaburi mwambani lililowekwa mhuri mkubwa. * Maneno "makaburini" au "chumba cha kuzikia" au "sehemu ya kuzikia" au "pango la kuzikia" yote kwa ujumla yanamaanisha mahali wafu wanapozikwa. * Vitu vingine pia vyaweza kuzikwa, kwa mfano Akani alifukia fedha na vitu vingine alivyokuwa ameviiba huko Yeriko. * Kirai "alifunika uso wake" kwa kawaida humaanisha, "kufunika uso kwa kutumia mikono." * Wakati mwingine neno "ficha" laweza kumaanisha "fukia" kama Akani alivyoficha ardhini vitu alivyokuwa ameviiba kutoka Yeriko. Hii inamaanisha alivifukia ardhini.
## Kuzima ### Ufafanuzi "Kuzima" inamaana kutoa au kusimamisha kitu ambacho kinatakiwa kikamilike. * Neno hili linatumika kwenye mukhtadha wa kuzima kiu na inamaana ya kusababisha kiu isimame kwa kunywa kitu. * Pia yaweza kutumika kama kutoa nje ya moto. * Kiu na moto vyote huzimwa na maji. * Paulo anatumia neno kuzima akiwa anamaanisha kuwa waamini "wasimzimishe Roho mtakatifu." Hii inamaana kuwa wasiwazuie watu kumruhuru Roho mtakatifu kuzalisha matunda yake na zawadi ndani yao. Kumzimisha Roho mtakatifu inamaana kumzuia Roho mtakatifu asidhihirishe nguvu zake na kufanya kazi ndani ya watu.
## kwato, ### Ufafanuzi Hizi ni sehemu ngumu za chini katika miguu ya wanyama kama vile ngamia, ng'ombe, farasi, punda, nguruwe, kondoo, mbuzi n.k Kwato za wanyama humlinda mnyama anapokuwa anatembea Baadhi ya wanyama wana kwato zilizogawanyika katika sehemu mbili, na wanyama wengine wana kwato ambazo hazijagawanyika.
## la kumi, zaka ### Ufafanuzi Maneno "la kumi" na "zaka" yanaeleza "asilimia ya kumi" au "moja-kati-ya -sehemu- ya-kumi" ya pesa, mazao, mifugo, au mali za mtu anazo mpa Mungu. * Katika Agano la Kale, Mungu aliwaelekeza Waisraeli kueka kando asilimia kumi ya mali zao kutoa kama sadaka ya shukurani kwake. * Hii sadaka ilitumika kufadhili kabila la Walawi wa Israeli waliyo tumikia Waisraeli kama makuhani na watunzi wa maskani na baadae, hekalu. * Katika Agano Jipya, Mungu haitaji asilimia kumi, lakini na waelekeza waamini kutoa kwa furaha na kwa hiari kusaidia watu wenye mahitaji na kufadhili huduma ya Kikristo.
## lala, kulala, aliye lala ### Ufafanuzi Haya maneno yana maana ya kimafumbo kuhusu kifo. * "lala" au "kulala" yaweza kuwa umbo linalo maanisha "kufa" * Msemo "aliye lala" yaeleza kipindi mtu anapo anza kulala, au kimfano, wakati mtu anapo kufa." * "kulala na mababu"
## lango, nguzo ya lango ### Ufafanuzi "Lango" ni kizuizi chenye bawaba katika njia ya kufikia ya uzio au ukuta ambao huzunguka nyumba au mji. "Nguzo ya lango" ina maana ya nguzo ya chuma au mbao ambayo inaweza kusogezwa katika sehemu kufunga lango. Lango la mji linaweza kufunguliwa kuruhusu watu, wanyama, na mizigo kusafiri ndani na nje ya mji. Kulinda mji, kuta zake na malango ilikuwa nene na imara. Malango yalifungwa na kukazwa na nguzo ya chuma au mbao kuzuia wanajeshi wa maadui kuingia mji. Lango la mji mara kwa mara ilikuwa kiini cha habari na katikati ya jamii ya kijiji. Pia ilikuwa mahali ambapo mihamala ya kibiashara hufanyika na hukumu kufanyika, kwa sababu kuta za mji zilikuwa na unene wa kutosha kuwa na njia ambayo ilitoa kivuli cha baridi kutoka kwa jua kali. Raia walifurahia kukaa chini ya kivui na kufanya biashara zao na pia kuhumu masuala ya kisheria. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, njia zingine za kutafsiri "lango" inaweza kuwa "mlango" au "uwazi wa ukuta" au "kizuizi" au "njia ya kuingia". Msemo "nguzo za lango" unaweza kutafsiriwa kama "komeo za lango" au "mihimili ya mbao ya kufunga lango" au "chuma cha kufunga lango"
## Laumu ### Ufafanuzi Kumlaumi mtu ni kumkosoa au kukataa matendo au tabia za mtu. Kulaumu ni maoni hasi kuhusu mtu. * Kusema kwamba mtu huyu "hana lawama" inamaanisha kuwa anaishi kwa namna ya kuheshimu njia za Mungu hivuo kuna kidogo au hamna kabisa kitu ambacho kitasababisha akosolewe. * Laumu pia yaweza kutafsiriwa kama "aibu" au "kulaumiwa."
## Lia, kupiga kelele ### Ufafanuzi Lia au piga kelele inamaana ya kusema kitu kwa nguvu au ghafla. Kupiga kelele kwa maumivu au hasira. * Kupiga kelele inamaanisha kuita kwa nguvu kwa lengo la kuomba msaada. * "Nakulilia wewe" inaweza kutafsiriwa kama "nakuita unisaidie" au "ninakuomba msaada."
## lsio huru, kuwa chini ya, chini ya ### Ufafanuzi Neno "sio huru" la eleza kuwa chini ya mamlaka ya mtu. Maneno "kuwa chini ya" ni amri inayo maanisha "tii" au "nyenyekea mamlaka ya." * Msemo "chini ya" ya eleza kusababisha watu kuwa chini ya mamlaka ya kiongozi au mtawala. * "Kumueka mtu chini ya kitu" ina maana kusababisha huyo mtu kupitia kitu hasi, kama adhabu.
## maangamizi ### Ufafanuzi Msemo "maangamizi" una maana ya hukumu ya shutuma ambayo haina uwezekano wa rufaa au utorokaji. Taifa la Israeli lilipochukuliwa mateka Babeli, nabii Ezekieli alisema, "maangamizi yamekuja juu yao". Kutegemea na muktadha, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "maafa" au "adhabu" au "uharibifu usio na matumaini".
## Madhabahu ya kufukizia. ### Ufafanuzi Madhabahu ya kufukizia ilikuwa sehemu ya samani ambayo kuhani aliitumia kuchoma uvumba kama sadaka kwa Mungu. Ilikuwa inaitwa madhabahu ya dhahabu. * Madhabahu ya kufukizia ilitengenezwa kwa mbao, pembeni na juu yake ilifunikwa kwa dhahabu. Ilikuwa kama nusu mita kwa urefuna nusu mita upana. * Kila siku asubuhi na jioni kuhani alifukiza uvumba. * Hii inaweza kutafsiriwa kama "madhabahu ya kuchoma uvumba" au "madhabahu ya dhahabu" au "madhabahu ya kufukizia" au "meza ya kufukizia."
## mafuriko ### Ufafanuzi Msemo "mafuriko" ina maana ya kiasi kikubwa cha maji ambacho kinafunika juu ya nchi. Msemo huu pia hutumika kitamathali kumaanisha kiasi kikubwa cha kitu, haswa kitu ambacho hutokea ghafla. Katika kipindi cha Nuhu, watu walikuwa waovu hadi Mungu akasababisha mafuriko duniani kote kuwa juu ya uso wote wa dunia, hata kufunika juu za milima. Kila mtu ambaye hakuwa katika mtumbwi pamoja na Nuhu alizama. Mafuriko yote mengine hufunika eneo dogo la nchi. Msemo huu pia unaweza kuwa tendo kama, "nchi ilifurika na maji ya mto". Mapendekezo ya Tafsiri Njia za kutafsiri maana halisi ya "mafuriko" inaweza kujumuisha, "maji yanayomwagikia" au "kiasi kikubwa cha maji" Mlinganisho wa kitamathali, "kama mafuriko" unaweza kukaa na msemo halisi, au msemo mbadala unaweza kutumika ambao una maana ya kitu ambacho kina hali ya kutiririka kwake, kama vile mto. Kwa msemo "kama mafuriko ya maji" pale ambapo maji yametajwa tayari, neno "mafuriko" linaweza kutafsiriwa kama "kiasi kikubwa sana" au "yanayomwagikia". Msemo huu unaweza kutumika kama sitiari kama, "usiruhusu mafuriko kunizoa juu yangu", ambayo ina maana ya "usiruhusu maafa haya makubwa kutokea kwangu" au "usiniache niteketezwe kwa maafa" au "usiache hasira yako initeketeze".
## mafuta ### Ufafanuzi Mafuta ni maji mazito yanayo chukuliwa kutoka kwenye mimea au matunda. Katika Biblia, mafuta yalito kwenye mizeituni. * Mafuta ya mizeituni utumika kupika, kupaka, kutoa dhabihu, taa, na dawa. * Zama za kale, mafuta ya mizeituni yalikuwa na gharama na kuwa na mafuta ni kipimo cha utajiri.
## Maji ### Ufafanuzi Pamoja na maana yake ya kawaida maji yaweza kuwelezea vyanzo vya maji kama vile bahari, mto au ziwa. * Pia maji yanaweza kuelezea majanga makubwa, majaribu na mateso. Kwa mfano Mungu ameahidi kuwa tukipita katika maji mengi atakuwa pamoja nasi. * Maji mengi inasisitiza ni kwa namna gani mambo yalivyo magumu. * Kunywesha wanyama inamaanisha kuwapatia maji. Katika nyakati za Biblia ilijumuisha kuchota maji na ndoo na kuyamimina kwenye chombo kwa ajili ya wanyama kunywa. * Katika agano jipya Mungu anaelezwa kama maji yaliyo hai kwa watu wake. Hii inamaanisha kuwa yeye ndo chanzo cha nguvu na raha. * Katika agano jipya Yesu anatumia neno maji yaliyo hai kuelezea kazi za roho mtakatifu ndani ya mtu katika kumgeuza na kumpa maisha mapya.
## majivu, vumbi ### Ufafanuzi Majivu ni vumbi la kijivu linalobaki baada ya kuni kuungua. Hutumika pia kama lugha ya picha kuonesha kitu kisicho na thamani. * Kwenye Biblia mara nyingine neno "vumbi" linatumika kuzungumzia majivu. pia inaweza kuwa uchafu unaotoka katika ardhi kavu. * "Majivu mengi" ni sawa na kusema "rundo la majivu." * Zamani kukaa kwenye majivu ilikuwa ishara ya kuomboleza. * Wakati wa kuomboleza, ilikuwa ni tamaduni kuvaa mavazi ya magunia, kukaa kwenye majivu nakujipaka majivu kwenye kichwa.
## Majuto ### Ufafanuzi "majuto" maana yake ni maumivu makali au dhiki. * Majuto yanaweza kuwa ya kimwili au maumivu ya kihisia. * Mara nyingi watu wenye majuto huonesha hata kwenye nyuso na tabia zao. * Mfano mtu mwenye maumivu makali au majuto anaweza kusaga meno yake au kulia kwa sauti. * Neno "majuto" linaweza kutafsiriwa pia kama "dhiki ya kihisia" au "maumivu ya ndani.
## Makabila kumi na mbili ya Israeli ### Ufafanuzi Makabila kumi na mbili inamaanisha watoto kumi na mbili wa Yakobo na uzao wao. Yakobo alikuwa mjukuu wa Abrahamu. Baadae Mungu alibadili jina lake na kumuita Israeli. Haya ndio majina ya makabila ya Israeli; Rubeni, Simoni, Lawi, Yuda, Naftali, Gadi, Asheri, Isakari, Zabuloni, Yusufu na Benjamini. Kizazi cha Lawi hakikurithi nchi ya Kaanani kwa sababu lilikuwa kabila la Kikuhani waliotengwa kumtumikia Mungu na watu wake. Yusufu alipokea urithi wa ardhi mara mbili ambapo aliwapatia watoto wake wawili Efraimu na Manase. Kuna mahali pengine kwenye Biblia orodha ya makabila kumi na mbili yamenukuliwa tofauti. Sehemu nyingine Lawi, Yusufu na Dani hawakuwekwa kwenye orodha na sehem nyingine watoto wawili wa Yusufu Efraimu na Manase wamewekwa kwenye orodha.
## makapi ### Ufafanuzi Makapi ni ganda kavu linalolinda mbegu ya nafaka. Makapi sio mazuri kwa chakula hivyo watu hutenganisha na mbegu na kuyatupa. * Makapi hutenganishwa na mbegu kwa kupeta nafaka juu ya hewa. Upepo hupeperusha makapi na mbegu huanguka chini. Hii huitwa kupeta. * Katika Biblia Neno hili hutumika kuelezea watu waovu na uovu, au vitu visovyofaa.
## Makerubi, Kerubi ### Ufafanuzi Kerubi ni umoja na makerubi ni wingi. Hivi ni viumbe vya pekee vya mbinguni alivyoviumba Mungu. Biblia inawaelezea makerubi kuwa wana mabawa na moto. * Makerubi wanadhihirisha utukufu na nguvu za Mungu na pia ni walinzi wa vitu vitakatifu. * Baada ya Adamu na Eva kutenda dhambi Mungu aliweka makerubi wenye upanga wa moto katika upande wa mashariki mwa bustani ya Edeni ili mtu yeyote asiweze kuupata mti wa uzima. * Mungu aliwaamuru Waisraeli kuchonga makerubi wawili wanaoangaliana mabawa yao yakiwa yamegusana kwenye mfuniko wa upatanisho wa sanduku la agano. * Pia aliwaambia wafume picha za makerubi katika mapazia ya maskani. * Katika vifungu vingine viumbe hawa wameelezewa kuwa na nyuso nne, ya mtu, simba, ng'ombe na malaika. * Makerubi wakati mwingine wanadhaniwa kuwa ni malaika japokuwa Biblia haijaeleza hivyo.
## Malkia ### Ufafanuzi Malkia ni kiongozi mwanamke wa nchi fulani au mke wa mfalme. * Esta alikuja kuwa Malkia wa himaya ya Uajemi alipoolewa na mfalme Ahusuero. * Malkia Yezebeli alikuwa mke muovu wa mfalme Ahabu. * Malkia wa Sheba alikuwa kiongozi maarufu aliyeenda kumtembelea mfalme Sulemani.
## Mambo ya nyakati ### Ufafanuzi Mambo ya nyakati ni kumbukumbu zilizoandikwa kwa kipindi fulani cha wakati. * Katika agano la kale kuna vitabu viwili "Kitabu cha kwanza cha mambo ya nyakati" na "kitabu cha pili cha mambo ya nyakati." * Kitabu cha mambo ya nyakati Kimerekodi sehemu ya simulizi ya wana wa Israeli mwanzoni imeorodhesha majina ya watu kwa kila kizazi kuanzia Adamu. * "Kitabu cha kwanza cha mambo ya nyakati" kimerekodi mwisho wa maisha ya Sauli na matukio ya utawala wa mfalme Daudi. * "kitabu cha pili cha mambo ya nyakati" Kimerekodi utawala wa mfalme Sulemani na baadhi ya wafalme pamoja na kujenga hekalu na kutenganisha ufalme wa kaskazini wa Israeli na ufalme wa kusini wa Israeli. * Mwishoni mwa 2 Mambo ya nyakati kinaelezea mwanzo wa mateka ya babeli.
## Maono ### Ufafanuzi Maono ni kitu ambacho mtu anakiona. Mara nyingi kitu hiki huwa sio cha kawaida au huwa chenye nguvu ambapo Mungu humuonesha mtu kwa lengo la kumpa ujumbe. * Mtu huona maono akiwa macho na maranyingine huona maono kwenye ndoto akiwa amelala. * Mungu hutuma maono ili kuwaambia watu jambo fulani la muhimu. Kwa mfano Patro aliona maono akiambiwa kuwa Mungu anamtaka awakaribishe Mataifa.
## mateka, kifungo ### Ufafanuzi Neno "mateka" au "kifungo" ni kitendo cha kukamata watu na kuwalazimisha waishi mahali ambapo hawataki kuishi kama kwenye nchi ya kigeni. * Waisraeli toka ufalme wa Yuda walichukuliwa mateka katika ufalme wa Babiloni kwa miaka 70. * Mateka mara nyingi hufanya kazi za watu au za taifa lililowateka. * Danieli na Nehemia walikuwa mateka wa Israeli waliofanya kazi kwa mfalme wa Babeli. * "kuchukua mateka" inamaana ya kumkamata mtu. * "kukuchukua mateka" inaweza kutafsiriwa kama "kukulazimisha kuishi kama mateka" au "kukupeleka kwenye nchi nyingine kama mfungwa." * Mtume paulo anawaambia Wakristo "kuchukua mateka" kila wazo na kufanya imtii Kristo. * Pia anazungumzia ni kwa namna gani watu wanaweza kuchukuliwa mateka kwa dhambi ikiwa na maana ya kutawaliwa na dhambi.
## Mateso ### Ufafanuzi Mateso ni kitendo cha kumsababishia mtu mateso. Mateso ni ugonjwa, huzuni ya kihisia au majanga mengine yatokanayo na mateso. * Mungu aliwapa mateso watu wake kupitia magonjwa na tabu zingine ili kuwasababisha watubu dhambi zao na wamrudie yeye. * Mungu alisababisha mateso au mapigo kwa wana wa Israeli kwa sababu mfalme wao alikataa kumtii Mungu.
## Matete ### Ufafanuzi Matete ni mimea nyenye mabua marefu yanayoota katika maji. * Matete katika mto Nile ambapo Musa alifichwa kama mtoto paliitwa kwenye nyasi. Zilikuwa ndefu zilizomea kwenye mto wa maji. * Matete haya yalitumiwa na Wamisri kutengeneza karatasi, vikapu na boti. * Matete haya ni laini na rahisi kupinda zinapopulizwa na upepo.
## maumivu makali ### Ufafanuzi Neno "maumivu makali" yaeleza kutesa sana. Kumtesa mtu ina maana ya kusababisha mtu kuteseka, mara nyingi kwa namna mbaya. * Wakati mwingine neno "maumivu makali" yaeleza maumivu na kuteseka. * Kuteseka pia kuna maana ya kiroho na maumivu ya hisia kama yale ya Ayubu. * Kwa maelezo ya kitabu cha Ufunuo, watu wasiyo amini katika Yesu kama mwokozi watapitia maumivu makali ya milele katika ziwa la moto.
## mavi, mbolea ### Ufafanuzi Msemo "mavi" una maana ya takataka ya binadamu au mnyama, na pia kinaitwa kinyesi. Unapotumika kama kirutubisho cha kurutubisha udongo, inajulikana kama "mbolea" Misemo hii pia inaweza kutumika kitamathali kumaanisha kitu ambacho hakina thamani au sio muhimu. Kinyesi kilichokaushwa cha mnyama mara kwa mara hutumika kama kichochea. Msemo "kuwa kama kinyesi katika uso wa dunia" unaweza kutafsiriwa kama "kusambazwa kama kinyesi kisicho na maana juu ya nchi". "Malango ya Kinyesi" katika Ukuta wa Kusini wa Yerusalemu yawezekana ulikuwa mlango ambapo takataka zote zilichukuliwa nje ya mji.
## mavuno/kuvuna ### Ufafanuzi Neno 'mavuno' hurejelea mkusanyiko wa matunda, mazao au mboga zilizoiva au kukomaa kutoka katika mimea iliyokuwa imepanda na kustawishwa. Muda wa mavuno mara kwa mara hutokea mwishoni mwa msimu wa kilimo. Waisraeli walikuwa na 'sherehe za mavuno' au 'sherehe ya ukusanyaji' ili kusherehekea uvunaji wa mazao ya chakula. Mungu aliwaagiza kutoa mazao ya kwanza ya mazao haya kama sadaka kwake. Katika lugha ya picha, neno mavuno laweza kutumika kutumika kurejelea watu wanaomwamini Yesu au kueleza juu ya ukuaji wa kiroho wa mtu. Wazo la mavuno ya mazao ya kiroho hukubaliana na huendana na mfano wa picha wa matunda kama picha ya mwenendo na tabia nzuri. Mapendekezo ya tafsiri Ni vizuri kutafsiri neno hili pamoja na neno ambalo hutumika mara kwa mara katika lugha husika kurejelea uvunaji wa mazao. Tukio la uvunaji laweza kutafsiriwa kama 'kipindi cha ukusanyaji' au ' kipindi cha ukusanyaji wa mazao' au ' kipindi cha kuchuma matunda' Kitenzi 'kuvuna' chaweza kutafsiriwa kama ' kukusanya' au 'kuchuma' or 'kuweka pamoja.'
## mawaa ### Ufafanuzi Neno "mawaa" humaanisha kasoro juu ya mtu au mnyama. Yaweza pia kumaanisha upungufu wa kiroho kwa mtu. * Kwa baadhi ya sadaka, Mungu aliwaagiza Waisraeli watoe mnyama asiye na kasoro au kosa. * Hii ni taswira ya jinsi Yesu Kristo alivyokuwa sadaka kamilifu, bila dhambi yoyote. * Waamini katika Kristo wamesafishwa kutokana na dhambi zao kwa damu yake na wanahesabiwa hawana makosa. * Njia ya kutafasiri neno hili laweza kujumuisha, "kasoro" au "upungufu" au "dhambi," kwa kutegemea mazingira.
## Mawaidha ### Ufafanuzi Neno "mawaidha" linamaana ya kuonya au kumshauri mtu. * Mara nyingi "mawaidha" huwa na maana ya kumshauri mtu asifanye jambo fulani. * Katika mwili wa Kristo, waamini wanafundishwa kupeana mawaidha wao kwa wao ili kuepuka dhambi na kuishi maisha matakatifu. * Neno mawaidha linaweza kutafsiriwa kama "kumhimiza mtu asitende dhambi."
## Mawindo, kwa mawindo ya ### Ufafanuzi "Mawindo" ni kitu kinachowindwa hasa mnyama anayetumika kwa ajili ya chakula. * Katika lugha ya picha mawindo anaweza kuwa mtu anayefanyiwa ukatili au kunyanyaswa na mtu mwenye nguvu. * Mawindo ya watu ni kitendo cha kuwanyanyasa watu au kuwaibia vitu walivyonavyo. * Pia mawindo yanaweza kutafsiriwa kama "mnyama anayewindwa"
## mazao ya kwanza ### Ufafanuzi Msemo "mazao ya kwanza" ina maana ya sehemu ya matunda ya kwanza ya mazao na mimea ambayo yalivunwa katika kila majira ya mavuno. Waisraeli walitoa mazao haya ya kwanza kwa Mungu kama sadaka ya toleo. Msemo huu unatumika kitamathali katika Biblia kumaanisha mzaliwa wa kiume wa kwanza kuwa mazao ya kwanza ya familia. Yaani, kwa sababu alikuwa mwana wa kiume wa kwanza kuzaliwa katika familia, yeye ndiye aliyekuwa akibeba jina na heshima ya familia. Kwa sababu Yesu alifufuka kutoka kwa wafu, anaitwa "mzawa wa kwanza" wa waumini wake wote ambao wamekufa lakini ambao hapo baadaye watafufuka. Waumini katika Yesu pia wanaitwa "wazawa wa kwanza" wa uumbaji wote, kuonyesha faida maalumu na nafasi ya wale ambao Yesu amewakomboa na kuwaita kuwa watu wake. Mapendekezo ya Tafsiri Matumizi halisi ya msemo huu yanaweza kutafsiriwa kama "sehemu ya kwanza"
## mbawala, paa, paa dume, paa mdogo ### Ufafanuzi Mbawala ni mnyama mkubwa, mwenye madaha, na miguu minne ambaye anaishi katika msitu au milimani. Mnyama wa kiume ana pembe kubwa kichwani mwake. Msemo wa "paa" una maana ya mbawala wa kike na "paa mdogo" ni jina la mtoto wa paa. Msemo wa "paa" una maana ya paa wa kiume. "Paa dume" ni dume wa aina ya "mbawala". Mbawala wana miguu myembamba na yenye nguvu inayowasaidia kuruka juu na kukimbia kwa kasi. Nyayo zao ina kwato iliyogawanyika ambayo huwasaidia kutembea au kupanda kwa urahisi kwenye mandhari ya kila aina.
## mbegu, manii ### Ufafanuzi Mbegu ni sehemu ya mmea unao oteshwa kwenye ardhi kuzalisha aina moja zaidi ya mmea huo. Pia ina maana kadha ya mafumbo. * Neno "mbegu" linatumika kwa fumbo na tafsida kuelezea seli ndogo ndani ya mwanaume au mwanamke zinazo jumuika kusababisha mtoto kukua ndani ya mwanamke, hii ina itwa manii. * Pamoja na hii, "mbegu" inatumika kueleza uzao wa mtu. * Neno hili lina maana ya wingi, likieleza zaidi ya mbegu moja au zaidi ya mzao mmoja. * Katika mfano wa mkulima akipanda mbegu, Yesu alifananisha mbegu na Neno la Mungu lililo pandwa katika mioyo ya watu ilikuweza kuzalisha matunda mazuri ya kiroho. * Mtume Paulo pia anatumia neno "mbegu" kumaanisha Neno la Mungu.
## mbuzi, mwanakibuzi ### Ufafanuzi Mbuzi ni mnyama wa ukubwa wa kati, mwenye miguu minne ambaye analingana na kondoo na hukuzwa kimsingi kwa ajili ya maziwa yake na nyama. Mtoto wa mbuzi huitwa "mwanakibuzi". Kama kondoo, mbuzi walikuwa wanyama muhimu wa sadaka, haswa wakati wa Pasaka. Ingawa mbuzi na kondoo wanaweza kufanana, kuna namna ambavyo wako tofauti. Mbuzi wanya manyoya ya kukwaruza; kondoo wana sufu. Mkia wa mbuzi husimama juu; mkia wa kondoo huning'inia chini. Kondoo mara kwa mara hupenda kukaa katika kundi lake, lakini mbuzi wanajitegemea zaidi na kutembea mbali na kundi lao. Katika kipindi cha Biblia, mbuzi walikuwa chanzo kikuu cha maziwa Israeli. Ngozi ya mbuzi ilitumika kwa ajili ya kufunika mahema na kutengeza mifuko ya kubeba divai. Pote katika Agano la Kale na Jipya, mbuzi alitumika kama ishara ya ukosefu wa utakatifu wa watu, labda kwa sababu ya mazoea yao ya kutangatanga mbali na yule aliyekuwa akiwatunza. Waisraeli pia walitumia mbuzi kama mfano wa mtu mwenye dhambi. Mbuzi mmoja anapotolewa sadaka, kuhani huweka mikono yake juu ya mbuzi wa pili aliye hai na kumwachilia jangwani kama alama ya mnyama kubeba dhambi ya watu.
## mbwa mwitu ### Ufafanuzi Mbwa mwitu ni mnyama mkali, anayekula nyama na anafanana na mbwa. * Mbwa mwitu mara nyingi huwinda kwa makundi na hunyemelea mawindo yao kwa werevu. * Katika Biblia "mbwa mwitu" imetumika kuelezea walimu wa uongo au manabii wa uongo wanaoharibu waamini wanaofananishwa na kondoo. Mafundisho ya uongo yanasababisha watu waamini uongo na kuwaletea madhara kwao. * Mfanano huu unaonesha kuwa kondoo ni rahisi sana kuvamiwa na kuliwa na mbwa mwitu kwa sababu hawana nguvu na hawawezi kujitetea.
## mchungaji, kuchunga ### Ufafanuzi Mchungaji ni mtu anaye linda kondoo. Kitenzi "kuchunga" ina maana ya kulinda kondoo na kuwapa chakula na maji. * Wachungaji wanachunga kondoo, kuwa ongoza sehemu yenye chakula kizuri na maji. Wachungaji pia wana chunga kondoo wasipotee na kuwalinda na wanyama hatari. * Hili neno linatumika kifumbo kwenye Biblia kueleza kutunza maitaji ya kiroho ya watu. Hii ni pamoja na kuwa fundisha nini Mungu alicho waambia kwenye Biblia na kuwa ongoza kwenye njia ya kuishi. * Katika Agano la Kale, Mungu amewaita "wachungaji" wa watu wake kwasababu ana watunza na maitaji yao yote na kuwalinda. Pia uwaongoza na kuwa elekeza. * Musa alikuwa mchungaji wa Waisraeli alipo waongoza kiroho katika kumuabudu Yahweh na kuwa ongoza kimwili katika safari yao kwenye nchi ya Kanani. * Katika Agano Jipya, Yesu anajitaja "mchungaji mwema." Mtume Paulo pia anamtaja kama "mchungaji mkuu" juu ya Kanisa.
## meneja, wakili ### Ufafanuzi Neno "meneja" au "wakili" katika Biblia ya husu mtumishi aliye kabidhiwa jukumu la kutunza mali na biashara. * Wakili alipewa majukumu mengi, yaliyo jumuisha kusimamia kazi za watumishi. * Neno "meneja" ni la kisasa zaidi kwa neno wakili. Maneno yote ya husu mtu aneye simamia kazi za mtu mwingine.
## Methali ### Ufafanuzi Methali ni sentensi fupi zinazoelezea hekima au kweli. * Methali zina nguvu kwa sababu ni rahisi kukumbukwa na kurudiwa. * Mara nyingi methali hujumuisha mifano ya maisha ya kila siku. * Mithali nyingine zipo wazi na nyingine ni ngumu kuzielewa. * Mfalme Sulemani alifahamika kwa hekima zake na aliandika mithali 1,000. * Yesu pia alitumia mithali au mifano katika mafundisho yake.
## meza ### Ufafanuzi Msemo wa "meza" una maana ya kula au kutumia kwa hali ya fujo. Kutumia neno hili kwa hisi ya tamathali, Paulo anatahadharisha waumini kutojimeza wao kwa wao, akimaanisha kutojishambulia au kuangamizana wao kwa wao kwa maneno au matendo (Wagalitia 5:15). Pia katika hisi ya tamathali, msemo "kumeza" mara kwa mara hutumika kwa maana ya "kuangamiza kabisa" kama kuzungumzia juu ya mataifa kumeza mengine au moto kumeza majengo na watu. Msemo huu pia unaweza kutafsiriwa kama "kumeza kabisa" au "kuangamiza kabisa".
## mfalme ### Ufafanuzi Neno "mfalme" linamaanisha mwanamme ambaye ni mtawala mkuu wa mji, jimbo, au nchi. Mfalme kawaida huchaguliwa kutawala kwa sababu ya uhsiano wake kifamilia na wafalme wa nyuma. Mfalme anapokufa, kawaida mwana wake mkubwa ndiye anayekuwa mfalme mpya. Katika nyakati za zamani, mfalme alikuwa na mamlaka yote juu ya watu katika ufalme wake. Neno "mfalme" halitumiki sana kwa mtu asiye mfalme wa kweli, kama "mfalme Herode" katika Agano Jipya. Katika Biblia, Mungu anajulikana kama mfalme anaye tawala juu ya watu wake. "Ufalme wa Mungu" unamaanisha utawala wa Mungu juu ya watu wake. Yesu aliitwa "Mfalme wa Wayahudi," "mfalme wa Israeli," na "mfalme wa wafalme." Yesu atakaporudi, atatawala kama mfalme wa dunia. Neno hili linaweza kutafsiriwa kama, "mkuu" au "kiongozi kamili" au "mtawala mwenye nguvu." Usemi "mfalme wa wafalme" unaweza kutasiriwa kama "mfalme anayetawala juu ya wafalme wengine wote" au "kiongozi mkuu aliye na mamlaka juu ya viongozi wengine wote."
## mgeni, ugeni, mgeni ### Ufafanuzi Msemo, "mgeni" una maana ya mtu anayeishi katika nchi ambayo sio yake. Katika Agano la Kale, msemo huu haswa humaanisha mtu yeyote ambaye alikuja kutoka kwa kundi tofauti la watu na watu ambao anaishi miongoni mwao. Mgeni pia ni mtu ambaye lugha yake na utamaduni ni tofauti na ya kwako. Kwa mfano, Naomi na familia yake alipohama kwenda Moabu, walikuwa wageni kule. Naomi na mkwe wake Ruthu walipohamia Israeli baadaye, Ruthu aliitwa "mgeni" kule kwa saba hakuwa wa Israeli kiasili. Mtume Paulo aliwaambia Waefeso ya kuwa kabla hawajamjua Kristo, walikuwa "wageni" kwa agano la Mungu. Mara nyingi, "mgeni" hutafsiriwa kama "mgeni" mtu ambaye hajulikani au hajazoeleka.
## mhenga, baba, mababu ### Ufafanuzi Inapotumika kihalisia, msemo "baba" una maana ya mzazi wa kiume wa mtu. Kuna baadhi ya matumizi ya tamathali ya msemo huu. Misemo "baba" na "babu" hutumika kumaanisha mababu wa mtu fulani au kundi la watu. Hii inaweza kutafsiriwa kama "babu" au "baba wa zamani". Msemo "baba wa" unaweza kumaanisha kitamathali mtu ambaye ni kiongozi wa kundi la watu wanaohusika au wenye chanzo na kitu. Kwa mfano, katika Mwanzo 4, "baba wa wale wote waishio katika mahema" inaweza kumaanisha "kiongozi wa kwanza wa ukoo wa watu wa kwanza ambao waliishi katika mahema". Mtume Paulo alijiita kitamathali "baba" wa wale ambao aliwasaidia kuwa Wakristo kupitia kutangaza injili pamoja nao. Mapendekezo ya Tafsiri Unapozungumza juu ya baba na mtoto wake halisi, msemo huu unatakiwa kutafsiriwa kutumia neno la kawaida kumaanisha baba katika lugha hiyo. "Mungu Baba" inatakiwa kutafsiriwa kutumia neno la kawaida la "baba". Unapomaanisha mababu, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "babu" au "baba wa zamani". Paulo anapomaanisha mwenyewe kitamathali kuwa baba wa waumini katika Kristo, hii inaweza kutafsiriwa kama "baba wa kiroho" au "baba katika Kristo". Mara nyingine neno "baba" linaweza kutafsiriwa kama "kiongozi wa ukoo". Msemo "baba wa uongo wote" unaweza kutafsiriwa kama "chanzo cha uongo wote" au "yule ambaye uongo wote hutokana".
## mifugo ### Ufafanuzi Neno "mfugo" linamaanisha wanyama wanaotunzwa kwa ajili ya chakula na mazao mengine ya maana. Aina zingine za mifugo wanafundishwa kuwa wanyama wa kazi. Aina wa mifugo ni pamoja na kondoo, ng'ombe, mbuzi, farasi, na punda. Katika nyakati za Biblia, utajiri kwa sehemu ulipimwa kwa idadi ya mifudo aliyonayo mtu. Mifugo inatumika kwa kuzalisha vitu kama sufu, maziwa, jibini, vifaa vya ujenzi, na nguo. Hii inaweza pia kutafsiriwa kama "wanyama wa shambani."
## milele ### Ufafanuzi Katika Biblia, msemo "milele" una maana ya muda usiofika mwisho. Mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha, "muda mrefu sana". Msemo "milele na milele" unasisitiza ya kwamba jambo litakuwepo milele. Msemo "milele na milele" ni njia ya kuelezea maisha ya milele yakoje. Pia una wazo la muda ambao hauishi. Mungu alisema ya kwamba ufalme wa Daudi utakuwepo "milele". Hii inamaanisha ukweli ya kwamba uzao wa Daudi Yesu atatawala kama mfalme milele. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "mara zote" au "kutokuwa na mwisho". Msemo, "utadumu milele" unaweza kutafsiriwa kama "kuwepo mara zote" au "hautakoma" au "utaendelea mara zote". Msemo wa kishindo, "milele na milele" unaweza kutafsiriwa kama "kwa mara zote na zote" au "kutomalizika" au "ambayo haifiki mwisho". Ufalme wa Daudi kudumu milele unaweza kutafsiriwa kama, "uzao wa Daudi atatawala milele" au "uzao wangu ataendelea kutawala".
## Mimi, Yahwe ### Ufafanuzi Mara nyingi katika Agano la Kale, wakati Mungu akijizungumzia, hutumia jina lake badala ya nomino kiwakilishi. Kwa mfano, badala ya kusema, "Niheshimu mimi," husema "Mheshimu Yahwe." Kuiweka wazi kuwa ni Mungu anayejizungumzia, ULB kawaida hutafsiri hii kwa kuongezea nomino kiwakilishi kama, "Niheshimu mimi, Yahwe" au "Mimi, Yahwe ninasema." Kwa kuongeza nomino kiwakilishi "mimi", ULB inaashiria kwa msomaji kuwa Mungu ndiye anayezungumza.
## Mizabibu ### Ufafanuzi Mizabibu ni bustani kubwa ambayo zabibu zinakua na kulimwa. * Mizabibu mara nyingi huwa na ukuta ili kulinda matunda dhidi ya wezi na wanyama. * Mungu anawafananisha wana wa Israeli na Mizabibu isiyozaa matunda. * Mizabibu inaweza kutafsiriwa kama "bustani ya zabibui" au "zao la zabibu".
## Mji mtakatifu ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno mji mtakatifu hurejelea mji wa Yerusalemu. Neno hili hurejelea mji wa zamani Yerusalemu pamoja na Yerusalemu mpya ya mbinguni mahali ambapo Mungu ataishi na kutawala miongoni mwa watu wake. Neno hili laweza kutafsiriwa kwa kuunganisha maneno 'takatifu' na 'mji' tafsiri ambayo imetumika katika tafsiri zote.
## mjumbe ### Ufafanuzi Neno, "mjumbe" la husu mtu anaye pewa ujumbe kuwa ambia wengine. * Katika zama za kale, mjumbe alitumwa katika mapambano kuwaambia watu waliyo mjini kinacho endelea. * Malaika ni aina ya mjumbe maalumu ambaye Mungu anamtuma kuwapa watu ujumbe. * Yohana Mbatizaji aliitwa mjumbe aliye kuja kabla ya Yesu kutangaza ujio wa Mesia na kuandaa watu kumpokea. * Mitume wa Yesu walikuwa wajumbe wake wa kwenda kushirikisha watu habari njema za ufalme wa Mungu.
## Mkate ### Ufafanuzi Mkate ni chakula kitengenezwacho kutokana na unga uliochanganywa na maji na matuta ili kutengeneza donge. Kisha donge linatengenezwa katika hali ya vipande na kuokwa. * Neno "boflo" linapotokea peke yake, linamaanisha, "kipande cha mkate." * Donge la mkate kwa kawaida linatengenezwa kwa kiti kinachofanya liumuke, kama vile amira. * Lakini pia mkate waweza kutengenezwa bila amira hivyo hauwezi kuumuka. Katika Biblia huu unaitwa "mkate usiotiwa chachu" na ulitumiwa na Wayahudi wakati wa mlo wa Pasaka. * Kwa vile mkate ulikuwa chakula kikuu kwa watu wengi katika nyakati za Biblia, hivyo neno hili linatumika katika Biblia pia kurejerea chakula kwa ujumla. * Neno "mkate wa wonyesho" linataja vipande kumi na mbili vya mkate vilivyokuwa vikiwekwa katika meza ya dhahabu katika hema ya kukutania au hekaluni kama sadaka kwa Mungu. Mikate hii inawakilisha makabila kumi na mbili ya Israeli na ililiwa na makuhani tu. Hii inatafasiri kama "mkate uoneshao kwamba Mungu aliishi kati yao." * Neno la kitamathari, "mkate kutoka mbinguni" linarejerea chakula maalumu cheupe kilichoitwa 'mana" alichokitoa Mungu kwa Waisraeli walipokuwa wakitangatanga jangwani. * Yesu alijiita "mkate ulioshuka kutoka mbinguni" na "mkate wa uzima." * Wakati Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wanaila Pasaka kabla ya kifo chake, alilinganisha, mkate usiotiwa chachu wa Pasaka na mwili wake ambao ungejeruhiwa na kufishwa msalabani. * Mara nyingi neno "mkate" laweza kutafasiriwa kwa ujumla kama "chakula."
## Mkoa, wilaya ### Ufafanuzi Mkoa ni sehemu ya nchi au himaya. * Kwa mfano katika zama za Himaya ya Uajemi iligawanyika katika mikoa kama Uajemi, Syria na Misri. * Katika nyakati za agano jipya himaya ya Roma iligawanyika katika mikoa kama Makedonia, Asia, Yudea, Samaria, Galatia, Galilaya. * Kila mkoa ulikuwa na mamlaka yake inayoongoza ambao walikuwa chini ya mfalme au kiongozi wa himaya. Viongozi hawa waliitwa magavana wa mikoa.
## mkono, mkono wa kuume, ### Ufafanuzi Neno 'mkono' limetumika katika Biblia kama lugha ya picha kwa njia mbalimbali Kuweka kitu katika mikono ya mtu fulani inamaana ya kukabidhi kitu hicho. Neno 'mkono' limetumika kurejelea uweza au nguvu ya Mungu na matendo yake. kwa mfano, Mungu anaposema "je si mkono wangu uliyoyafanya haya?" Neno "kabidhi" hurejelea maana ya kuweka kitu katika mkono au utawala wa mtu fulani. Kuweka mikono juu ya mtu fulani mara nyingi huambatana na utoaji wa baraka kwa mtu huyo. Pia kitendo cha 'kuweka mikono" juu ya mtu kinamaanisha kumweka mtu huyo wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu au kwa ajili ya kumwombea mtu huyo uponyaji. Baadhi ya lugha za picha za neno mkono ni: Kunyosha mkono juu ya mtu maana yake ni kumdhuru. ''kumwokoa kutoka katika mkono wa..." ni kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine. matumizi mengine ya mkono ni kama: "kunyosha mkono" ina maana ya 'kudhuru' au kuumiza" "kumwokoa mtu mikononi mwa" ina maana ya kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine. "kuwa karibu na mkono " kuwa 'karibu' "kuwa mkono wa kuume" humaanisha kuwa 'nafasi'' au ''sehemu ya'' au "upande wa kulia" Maelezo yanayosema "kwa mkono wa'' au ''kupitia mkono'' ina maana kuwa kitendo kimefanya na mtu huyo. kwa mfano, "kwa mkono wa Bwana'' ina maana kuwa Bwana ndiye amefanya tendo hilo. Wakati Paulo anasema " imeandikwa kwa mkono wangu" ina maana kuwa sehemu hii ya barua iliandikwa kwa mkono wake kabisa, badala tu kusema na mtu mwingine akayaandika. Mapendekezo ya tafsiri. Maelezo haya na tamathali hizi za semi zaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha zingine za picha ambazo zina maana sawa. Au maana inaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha ya moja kwa moja.
## mkuki ### Ufafanuzi Mkuki ni silaha ndefu ya mbao yenye ncha kali ya chuma mwishoni inayo tupwa umbali mrefu. * Mikuki ilitumika mara nyingi kwenye vita kipindi cha Biblia. Wakati mwingine utumika ata sasa katika malumbano katika ya makundi ya watu. * Mkuki ulitumika na mwanajeshi wa Kirumi kutoboa ubavu wa Yesu alipo kuwa ameni'ng'nia msalabani. * Wakati mwingine watu wanatupa mikuki kudaka samaki au mawindo mingine kula.
## Mkutano, kukusanyika ### Ufafanuzi Mkutano ni kundi la watu wanaokusanyika pamoja kujadili matatizo, kupeana ushauri na kufanya maamuzi. * Mkutano ni kundi la watu wanaokusanyika pamoja kwa mda mfupi kwa ajili ya jambo maalumu au tukio maalumu. * Katika agano la kale kulikuwa na mkutano maalumu ulioitwa mkutano takatifu ambapo wana wa Israeli walikusanyika kumuabudu Yahweh. * Mara nyingine mkutano ina maanisha Waisraeli kwa ujumla kama kundi. * Katika agano jipya viongozi wa Kiyahudi 70 katika miji mikuu kama Yerusalemu walikusanyika ili kutatua masuala ya kisheria na kutatua migogoro kati ya watu. Mkutano huo ulikuwa unajulikana kama Baraza.
## Mkuu ### Ufafanuzi "Mkuu" ni kiongozi wa muhimu na mwenye nguvu sana katika kundi fulani. * Kwa mfano "mkuu wa muziki," "kuhani mkuu," mkusanyaji mkuu wa kodi," na "kiongozi mkuu." * Pia inaweza kutumiwa kwa kiongozi wa familia fulani, katika Mwanzo 36 kulikuwa na watu walioitwa wakuu wa koo zao. * Inapotumika kama nomino neno hili laweza kutafsiriwa kama "kuongoza" au "mtawala wa kikuhani."
## Mkuu, Binti wa Mfalme ### Ufafanuzi Mkuu ni mtoto wa kiume wa mfalme. Binti wa mfalme ni mtoto wa kike wa mfalme. * "mkuu" imetumika mara nyingi kumuelezea kiongozi, mtawala au mtu mwenye nguvu. * Kwa sababu ya utajiri wa Abrahamu alielezewa kama mkuu kwa Wahiti aliokuwa akiishi kati yao. * Katika kitabu cha Danieli neno "mkuu" limetumika kuelezea roho chafu zilizokuwa zinatawala maeneo kama "wakuu wa uajemu" na "wakuu wa ugiriki." * Katika kitabu cha Danieli pia malaika mkuu Mikaeli anazungumwa kama Mkuu. * Pia katika Biblia Shetani anazungumzwa kama "mkuu wa ulimwengu huu." * Yesu anaitwa "Mkuu wa amani." * Katika Matendo ya mitume 2:26 Yesu anafananishwa na "Bwana na Kristo" Pia katika matendo ya mitume 5:31 anafananishwa kama "Mkuu na mwokozi" kuonesha maana kati ya "Bwana" na "Mkuu."
## mkuyu ### Ufafanuzi Mkuyu ni mrefu, mti wa kivuli wenye shina kubwa na lenye matawi mapana. * Mkuyu ina mbao ngumu iliyo tumika kutengeneza meli na kutengeneza majembe, na fimbo za kutembelea wazee. * Shina la badhi ya mikuyu inaweza kuwa na mita 6. * Miti ya mikuyu ilikuwa ni mfano wa maisha marefu na ilikuwa na maana zingine za kiroho. Katika Biblia, ilihusishwa na maeneo matakatifu.
## Mnara ### Ufafanuzi Mnara ni jengo refu kwa umbo ambalo hujengwa kwa ajili ya walinzi kuangalia kama kuna hatari yoyote. Minara hii mara nyingi ilijengwa kwa kutumia mawe. * Wamiliki wa ardhi maranyingi walijenga minara ili waweze kulinda mazao yao yasiibiwe. * Minara pia ilijumuisha vyumba ambavyo walinzi au familia ziliishi ili ziweze kulinda mazao mchana na usiku. * Minara ya jiji ilikuwa mirefu sana kuliko minara ya mji ili walinzi waweze kuona adui yeyote anayekuja kwenye jiji. * Neno "mnara" linatumika kama ishara ya ulinzi toka kwa adui.
## mnyama ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "mnyama" ni njia nyingine ya kusema "mnyama". * Mnyama wa porini ni aina ya mnyama anayeishi huru msituni au kondeni na hayawai kufundishwa na watu. * Mnyama wa kufugwa anaishi na watu na anatunzwa kwa mboga au kufanya kazi, kama vile kulima shamba. Mara kwa mara neno "mifugo" linatumika kurejerea aina hii ya wanyama. * Kitabu cha Danieli katika Agano la Kale na kitabu cha Ufunuo katika Agano Jipya vinaeleza maono yenye wanyama wanaowakilisha nguvu au mamlaka ya uovu inayompinga Mungu. * Baadhi ya wanyama hawa wanaelezwa wakiwa na tabia tofauti, kama vile vichwa kadhaa na pembe nyingi. Mara kwa mara wanakuwa na nguvu na mamlaka, kuonesha kwamba waweza kuwakilisha nchi, taifa au mamlaka nyingine ya kisiasa. * Njia ya kutafasiri hii yaweza kuhusisha, "kiumbe" au "kitu kilichoumbwa" au "mnyama" au "mnyama wa porini," kutegemea mazingira.
## Mnyweshaji ### Ufafanuzi Katika agano jipya "mnyweshaji" alikuwa mtumsihi wa mfalme aliyepewa kazi ya kupeleka kwa mfalme kikombe cha mvinyo, huonja mvinyo na kuhakikisha haujawekewa sumu. * Pia maana ya kawaida ya mnyweshaji ni mtu anayeleta kikombe. * Mnyweshaji alijulikana kwa kuwa mwaminifu kwa mfalme. * Kwa sababu ya nafasi yake ua uaminifu mnyweshaji alikuwa na nafasi kubwa ya ushawishi kwa maamuzi anayotoa kiongozi. * nehemia alikuwa mnyweshaji wa mfalme Artashasts wa Uajemi wakati ambao Waisraeli walikuwa mateka Babeli.
## moto ### Ufafanuzi Moto ni joto, mwanga na miale ambayo hutokana pale kitu kinapochomwa. Kuchoma mbao kwa moto hugeuza mbao kuwa majivu. Msemo "moto" pia hutumika kitamathali, mara kwa mara kumaanisha hukumu au utakaso. Hukumu ya mwisho ya wasioamini ipo katika moto wa jehanamu. Moto hutumika kusafisha dhahabu na vyuma vingine. Katika Biblia, hatua hii hutumika kuelezea jinsi Mungu husafisha watu kupitia mambo magumu ambayo hutokea katika maisha yao. Msemo "kuwabatiza kwa moto" unaweza kutafsiriwa kama "kukusababisha upitie mateso ili kwamba yakusafishe"
## mpagao ### Ufafanuzi Mpagao ni hali ya fikra ambayo mtu yupo macho lakini hatambui yanayo mzunguka kwasababu anaona na kupitia vitu tofauti. * Katika Agano Jipya, hili neno linaeleza hali ya kimuujiza ya fikra amabyo Petro na Paulo walikuwa nayo Mungu alipo zungumza nao kwenye maono. * Katika kila hali, Petro na Paulo walikuwa katika maombi walipo patwa na mpagao. * Mungu ndiye aliye sababisha wawe katika mpagao. * Neno "mpagao" ni neno tofauti na "maono" au "ndoto" na itafsiriwe tofauti. * Msemo "kuanguka katika mpagao" ina maana "kuwa katika hali ya usingizi ghafla" wakati bado macho.
## Mpanda farasi ### Ufafanuzi katika nyakati za Biblia, istilahi, ' mpanda farasi walikuwa ni wanaume ambao waliendesha farasi katika vita. Mashujaa walioendesha gari la kukokotwa na farasi waliitwa wapanda farasi, ingawa jina hili hurejelea watu ambao kiuhalisia huongoza farasi. Waisraeli waliamini kuwa kwa kutumia farasi katika vita ilitia mkazo katika nguvu zao kuliko kumtegemea Yahweh, hivyo hawakutumia wapanda farasi sana.. Neno hili laweza kutafsiriwa kama ' waendesha farasi
## Mpatanishi ### Ufafanuzi Mpatanishi ni mtu anaye saidia watu wawili au zaidi kusuluhisha malumbano yao au ugomvi baina yao. Ana wasaidia na kuwapatanisha. * Kwasababu watu wametenda dhambi, ni maadui wa Mungu wanoa stahili gadhabu yake na adhabu. Kwasababu dhambi, mahusino katika ya Mungu na watu wake umevunjwa. * Yesu ni mpatanishi katika ya Mungu Baba na watu wake, akirejesha uhusiano uliyo vunjika kupitia kifo chake kama malipo ya dhambi zao.
## mpenzi ### Ufafanuzi Neno "mpenzi" linamaanisha "mtu anayependa." Kawaida hii inamaanisha watu walio katika mahusiano ya kimapenzi. Neno "mpenzi" linapotumika katika Biblia, kawaida lina maana ya mtu aliye na uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hajamuoa au kuolewa naye. Huu uhusiano mbaya wa kimapenzi hutumika kwenye Biblia kumaanisha kutokutii kwa Israeli katika kuabudu sanamu, Kwa hiyo neno "wapenzi" pia hutumika kimafumbo kumaanisha sanamu ambazo watu wa Israeli waliabudu. Katika mazingira haya, neno hili linaweza kutafsiriwa kuwa, "wenzi waovu" au "wenzi katika kuzini" au "sanamu." "Mpenzi" wa fedha ni mtu anayeweka msisitizo mkubwa sana kupata fedha na kuwa tajiri. Katika kitabu cha Agano la Kale cha Wimbo ulio Bora, neno "mpenzi" linatumika kwa njia nzuri.
## Mpiga mishale ### Ufafanuzi Mpiga mishale ni mtu mwenye ujuzi wa kutumia upinde na mshale kama silaha. * Kwenye Biblia mpiga mishale mara nyingi ni askari anayetumia upinde na mshale kupigana vitani. * Wapiga mishale walikuwa watu wa muhimu sana katika Jeshi la Siria.
## Mrithi ### Ufafanuzi Mrithi ni mtu ambaye kisheria hupoke mali au pesa za mtu aliyekufa. Katika nyakati za Biblia, mrithi mkuu alikuwa ni mtoto wa kwanza ambaye alipokea sehemu kubwa ya mali au pesa za baba yake. Biblia hutumia neno mrithi kama lugha ya picha kumaanisha Wakristo wanapopokea baraka za kiroho kutoka kwa Mungu, baba yao wa kiroho. Kama watoto wa Mungu, Wakristo ni warithi pamoja na Yesu Kristo. Hii inaweza kutafsiriwa kama "warithi wenza.'
## Msamaha ### Ufafanuzi "Msamaha" ni kusamehe au kutokumhukumu mtu kwa sababu ya dhambi zake. * Neno hili pia linaweza kuwa na maana ya kutokuamua kumhukumu mtu kwa sababu ana makosa. * Kwenye mahakama, hakimu anaweza kumsamehe mtu anayekutwa na hatia katika kosa. * Japokuwa sisi tuna hatia ya dhambi Yesu alitusamehe toka kwenye hukumu kwa kufa msalabani.
## mshiriki ### Ufafanuzi Neno "mshiriki" la husu sehemu moja ya mwili au kundi. * Agano Jipya la elezea Wakristo kama "washiriki" wa Mwili wa Kristo. * Yesu Kristo ni "kichwa" wa mwili na waamini moja moja wanatumika kama washiriki wa mwili. Roho Mtakatifu anampa kila mshiriki wa mwili nafasi maalumu kusaidia mwili wote kufanya kazi vizuri. * Watu wanao shiriki katika makundi kama Baraza la Wayahudi na Mafarisayo pia wanaitwa "washiriki" wa haya makundi.
## Mshita ### Ufafanuzi Mshita ni mti uliopatikana katika nchi ya Kaanani katika nyakati za zamani. * Mbao za Mshita ni ngumu na zinazodumu, hutumika kutengenezea vifaa kwa ajili ya ujenzi. * Ni vigumu sana kwa mbao hii kuharibika, ni nene sana na aihifandhi maji, ina namna ya asili ya kujitunza ili isiharibiwe na wadudu. * Kwenye Biblia mbao za Mshita zilitumika kujengea hema na sanduku la agano.
## msimamizi ### Ufafanuzi Neno "msimamizi" la husu mtu aliye mwangalizi wa kazi na maendeleo ya watu wengine. * Katika Agano la Kale, msimamizi alikuwa na kazi ya kuhakikisha wafanya kazi chini yake walifanya kazi yao vizuri. * Katika Agano Jipya, hili neno la tumika kueleza viongozi wa kanisa la kwanza la Kristo. Kazi yao ilikuwa ilikuwa kushughulikia waamini wanapokea mafundisho sahihi ya Biblia. * Paulo anataja msimamizi kama kuwa mchungaji anaye jali waamini katika kanisa, waliyo "kundi" lake" * Msimamizi, kama mchungaji, anaangalia kondoo wake. Analinda na kutunza waamini kutoka mafundisho ya uongo na mambo mengine maovu. * Katika Agano Jipya, maneno "msimamizi," "mzee," na "mchungaji" ni namna tofauti za kutaja viongozi wale wale wa kiroho.
## msingi, kuanzishwa ### Ufafanuzi Kitenzi cha "kuanzishwa" ina maana ya kujengwa juu ya au kutokana na kitu. Msingi ni sehemu ya chini ambapo kitu kunajengwa. Msingi wa nyumba or jengo lazima uwe na nguvu na kutegemewa ili kuimarisha umbo lote. Msemo "msingi" unawvza kumaanisha mwanzo wa jambo au muda ambao kitu kiliumbwa. Kwa kitenzi cha kitamathali, waumini katika Kristo wanalinganishwa na jengo ambalo limejengwa juu ya mafunzo ya mitume na manabii, na Kristo mwenyewe kuwa jiwe la pembeni la jengo. "Jiwe la msingi" lilikuwa jiwe ambalo lililazwa kama sehemu ya msingi. Mawe haya yalijaribiwa kuhakikisha yalikuwa na nguvu ya kutosha kuimarisha jengo kamili. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "kabla ya msingi wa dunia" inaweza kutafsiriwa kama "kabla ya uumbaji wa ulimwengu" au "kabla ya muda ambapo dunia ilianza kuwepo". Msemo "kujengwa juu ya" inaweza kutafsiriwa kama "kujengwa kwa imara juu ya" au "kujengwa kwa imara kwa". Kulingana na muktadha, "msingi" inaweza kutafsiriwa kama "msingi imara" au "uimara wa kudumu" au "mwanzo" au "uumbaji"
## msonobari ### Ufafanuzi Msemo "msonobari" una maana ya aina ya mti ambao hubaki kijani mwaka wote na una pia zenye mbegu kwa ndani. Miti wa msonobari pia humaanisha mti wa "kijani" daima. Katika nyakati za zamani, mbao za msonobari zilitumika kutengenezea vyombo vya muziki na kwa ujenzi wa maumbo kama vile mitumbwi, nyumba, na hekalu. Baadhi ya mifano ya msonobari iliyotajwa katika Biblia ni msonobari, seda, mvinje na mreteni.
## Mtamba/Mfarika wa ng'ombe ### Ufafanuzi Neno Mtamba' lina maana ya ng'ombe jike mkubwa ambaye hajazaa bado.
## Mtawala, watawala, tawala ### Ufafanuzi "Mtawala" ni mtu mwenye mamlaka juu ya watu wengine kama vile kiongozi wa dini, ufalme au nchi. * Katika agano la kale Mfalme alitambulika kama Mtawala. Sentensi zingine zimesema "walimchagua yeye kuwa mtawala juu ya Israeli." * Mungu anazungumzwa kama mtawala mkuu anayetawala juu ya watawala wote. * Katika agano jipya kiongozi wa sinagogo aliitwa mtawala. * Aina nyingine ya mtawala katika agano jipya mi "gavana." * Kutegemeana na mukhtadha mtawala inaweza kutafsiriwa kama kiongozi au mtu mwenye mamlaka.
## mtego ### Ufafanuzi Neno mtego lina maana ya kifaa kinacho tumika kudaka wanyama na kuwazuia wasitoroke. Katika Biblia, hili neno linatumika kifumbo kueleza kuhusu jinsi dhambi na jaribu ni mitego inayo wanasa watu na kuwadhuru. * "mtego" una kamba au waya unao vuta kwa ghafla pindi mnyama anapo ingia ndani yake, na kutega miguu yake. * Mara nyingi mtego unafichwa ili kwamba mawindo yake ya naswe ghafla. * Maneno "tega mtego" ina maana kuanda mtego tayari kunasa kitu. * "kuanguka kwenye mtego" ina eleza kuanguka kwenye shimo refu lililo chimbwa na kufichwa kuweza kumdaka mnyama.
## mtenda uovu ### Ufafanuzi Msemo "mtenda uovu" ni kumbukumbu ya jumla kwa watu ambao hufanya mambo ya dhambi na maovu. Inaweza pia kuwa neno la jumla la watu ambao hawamtii Mungu. Msemo huu unaweza kutafsiriwa kwa kutumia neno kwa ajili ya "uovu" au "ubaya" na neno kwa ajili ya "kufanya" au "kutengeneza" au "kusababisha" kitu.
## Mtende ### Ufafanuzi "mtende" ni mti mrefu wenye matawi marefu, rahisi na yanayosambaa kutoka juu. * Mti wa mtende kwenye Biblia umeelezewa kuwa ni mti unaotoa matunda yanayoitwa "tende." Majani yake yako kama manyoya. * Miti ya mitende huota sehemu zilizo na joto na majani yake hubaki kuwa ya kujani mwaka mzima. * Yesu alipoingia Yerusalemu akiwa juu ya punda, watu walitandika chini majani ya mitende mbele yake. * Majani ya mitende yanaonesha ishara ya amani na kusherehekea ushindi.
## Mteserusi ### Ufafanuzi Neno Mteserusi ni jina la aina ya mti ambao ulipatikana kwa wingi katika maeneo ambapo waliishi watu nyakati za Kibiblia.
## mtini ### Ufafanuzi Tini ni tunda dogo, laini, tamu ambalo huota juu ya miti. Linapoiva, tunda hili linaweza kuwa na rangi nyingi, ikiwemo kahawia, njano na zambarau. Mitini inaweza kuota kuwa urefu wa mita 6 na matawi yao makubwa hutoa kivuli kizuri. Tunda hili lina urefu wa sentimita 3-5. Adamu na Hawa walitumia majani ya mtini kutengeneza mavazi kwa ajili yao baada ya kutenda dhambi. Mitini inaweza kuliwa mibichi, ikiwa imepikwa, au kukaushwa. Watu pia walikata katika vipande vidogo vidogo na kuzikandamiza kuwa keki kuliwa baadaye. Katika kipindi cha Biblia, mitini ilikuwa muhimu kama chanzo cha chakula na kipato. Uwepo wa mitini inayozaa mara kwa mara hutajwa katika Biblia kama ishara ya mafanikio. Mara kadhaa Yesu alitumia mitini kama mfano wa kufundisha wanafunzi wake kweli za kiroho.
## mtumishi, mtumwa, utumwa ### Ufafanuzi Neno "mtumishi" la weza pia maanisha "mtumwa" na kumueleza mtu anaye mfanyia mtu mwingine kazi, iwe kwa uwamuzi au kwa lazima. Muktadha wa maneno yaliyo zunguka yanaweka dhahiri kuwa kama mtumishi au mtumwa ndiye anaye tajwa. * Katika nyakati za Biblia, kulikuwa na tofauti ndogo katika ya mtumishi na mtumwa kuliko ilivyo leo. Wote watumishi na watumwa walikuwa sehemu muhimu ya nyumba ya bwana wao na wengi walichukuliwa kama ndugu wa familia. * Mtumwa ni aina ya mtumishi ambaye ni mali ya mtu anaye mfanyia kazi. Mtu anaye nunua mtumwa anaitwa "mmiliki" au "bwana." Mabwana wengine wanawatendea watumwa wao kwa ukatili sana, wakati wengine wana watendea vizuri. * Zamani za kale, watu wengine kwa hiari walikuwa watumwa kwa mtu aliye wadai ilikulipa deni lao. * Katika Biblia, maneno "mimi ni mtumishi wako" yalitumika kama alama ya heshima na huduma kwa mtu wa ngazi ya juu, kama mfalme. Haimanishi kwamba mtu anaye zungumza alikuwa mtumishi halisi. * Katika Agano la Kale, manabii wa Mungu na watu wengine waliyo muabudu Mungu mara nyingi waliitwa "watumishi." * Wakristo pia wanaitwa "watumwa wa haki," ambayo ni mfano unao linganisha uwaminifu wa kumtii Mungu kama mtu anavyo mtii bwana wake.
## muamuzi, waamuzi ### Ufafanuzi Muamuzi ni afisa aliye teuliwa anaye kuwa kama hakimu anaye amua mambo ya sheria. * Katika Biblia, muamuzi alitatua ugomvi baina ya watu. * Kulingana na muktadha, namna ya kutafsiri hili neno ya weza kuwa, "hakimu anaye amua" au "afisa wa sheria" au "kiongozi wa mji"
## muda ### Ufafanuzi Katika Biblia neno "muda" utumika sana kama fumbo kueleza wakati maalumu au kipindi cha muda fulani matukio yametokea. Lina maana sawa na "umri" au "wakati." * Danieli na Ufunuo unaeleza "muda" wa kipindi kigumu au dhiki itakayo kuja duniani. * Katika maneno "muda, mida, na nusu muda" neno "muda" lina maana ya "mwaka." Haya manano yanaeleza kipindi cha nusu mwaka wakati wa dhiki kuu mwisho wa muda huu uliyopo. * Maneno kama "wakati wa pili" au "mara nyingi" ueleza idadi ya marudio kitu kilicho tokea. * Kulingana na muktadha, neno "muda" uweza tafsiriwa kama, "majira" au "kipindi cha muda"
## muhuri, kutia muhuri ### Ufafanuzi Kutia muhuri kitu ina maana ya kufunga kwa kitu ambacho inafanya ngumu kufungua pasipo kuvunja muhuri. * Mara nyingi muhuri unatiwa alama ya kuonyesha mmiliki. * Nta iliyo yayushwa ilitumika kueka muhuri barua au nyaraka zilizo itaji kulindwa. Nta ilipo pata baridi na kuwa ngumu, barua haikuweza kufunguliwa pasipo kuvunja nta ya muhuri. * Kama muhuri uliweka katika jiwe mbele ya kaburi la Yesu kuweza kuzuia ye yote asisogeze jiwe. * Paulo kwa fumbo ana mtaja Roho Mtakatifu kama "muhuri" kuonyesha kuwa wokovu wetu ni wa salama.
## Mvua ya mawe ### Ufafanuzi Mvua ya mawe ni vipande vidogo vidogo au vikubwa vya maji yaliyoganda ambayo hushuka kutoka mawinguni. Mawe ya Mvua hushuka kutoka mawinguni katika umbo la kama mpira au vipande vya barafu. Mawe haya ya mvua mara nyingi huwa ni madogo madogo, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa makubwa yenye upana wa sentimita 20 hivi na uzito wa kilogramu moja hivi. Kitabu cha Ufunuo katika Agano la Jipya kinazungumzia juu ya mawe ya mvua makubwa yenye uzito wa kilogramu 50 hivi ambayo Mungu atayashusha juu ya dunia ili kuhukumu watu waovu katika siku za mwisho.
## mwaka linapotumika ### Ufafanuzi Neno "mwaka linapotumika, kwa hali ya kawaida katika Biblia linamaanisha kipindi cha muda wa siku 354. Hii ni kulingana na kalenda inayotumia mfumo wa mwezi unaochukua kuizunguka dunia. * Mwaka katika siku hizi unakamilisha siku 365 kwa kugawanywa katika miezi 12, kutegemea siku ambazo dunia inatumia kulizunguka jua. * Katika mifumo yote miwili mwaka una miezi 12. Lakini wakati mwingine ziada ya mwezi wa 13 unaongezwa katika mwaka unaotumia kalenda ya mwezi kwa kuzingatia kuwa kalenda ya mwezi ina siku 11 pungufu ya ule wa jua. Hii inasaidia kuzilinganisha kalenda zote mbili. * Katika Biblia, neno "mwaka" pia limetumika kwa tamathari kuonesha muda wa jumla tukio maalumu linapotokea. Mfano wake ni "mwaka wa Yahwe" au "katika mwaka wa kianganzi" au "mwaka wa Bwana uliokubarika." Katika mazingira haya, "mwaka" waweza kutafasiriwa kama "wakati" au "majira" au "kipindi cha wakati".
## mwalimu,Mwalimu ### Ufafanuzi Mwalimu ni mtu anaye toa taarifa mpya. Waalimu wanasaidiana kupata na kutumia maarifa na ujuzi. * Katika Biblia, neno "mwalimu" linatumika kwa namna maalumu kumueleza mtu anaye fundisha kuhusu Mungu. Haimuelezi mwalimu wa shule. * Watu wanao jifunza kutoka kwa mwalimu wanaitwa "wanafunzi." * Katika baadhi ya fasiri za Biblia, hili jina limewekwa herufi kubwa ("Mwalimu") wakati linapo tumika kama jina la Yesu.
## mwamini ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "mwamini" larejerea mtu anayeamini na kumtegemea Yesu Kristo kama Mwokozi. * Neno "mwamini" kwa maana halisi linamaanisha "mtu anayeamini." * Neno "Mkristo" lilikuja hatimaye kuwa jina la waamini kwa sababu linaonesha kwamba wanamwamini Kristo na kutii mafundisho yake. ### Maoni ya Kutafasiri. * Baadhi ya tafasiri zaweza kupendelea kusema, "mwamini wa Yesu" au "anayemwamini Kristo." * Neno hili pia laweza kufasiriwa kwa neno au kirai kinachomaanisha, "mtu anaye mwamini Yesu" au "mtu anayemfahamu Yesu na kuishi kwa ajili yake." * Njia nyingine ya kutafasiri "mwamini" laweza kuwa, "mfuasi wa Yesu" au "Mtu anayemjua na kumtii Yesu." * Neno "mwamini" ni neno la jumla kwa kila anayemwamini Kristo, wakati "mfuasi" na "mtume" yalitumika maalumu kwa watu waliomfahamu Yesu alipokuwa hai. Ni vema kutafasiri maneno haya kwa njia tofauti, ili kuyatofautisha.
## Mwananchi ### Ufafanuzi Mwananchi ni mtu anayeishi katika mji fulani au nchi au ufalme. Ni mtu ambaye anajulikana ni mkazi wa kisheria wa eneo hilo. * Inategemea na mukhtadha hii inaweza kutafsiriwa pia kama "mwenyeji." * Mwanamchi anaweza kuishi katika mkoa ambao ni sehemu ya ufalme mkubwa unaoongozwa na mfalme au kiongozi. Kwa mfano Paulo alikuwa mwananchi wa Rumi iliyokuwa na mikoa mingi. Paulo aliishi katika moja ya mikoa hiyo. * Kwa tafsiri nyingine wanaomwamini Yesu wanaitwa Wananchi wa Mbinguni kwa maana ya kuwa wataishi huko siku moja.
## Mwangamizi ### Ufafanuzi Msemo wa "mwangamizi" una maana ya, "mtu anayeangamiza". Msemo huu unatumika mara kwa mara katika Agano la Kale kama mrejesho wa jumla ya mtu yeyote anayeangamiza watu wengine, kama vile jeshi vamizi. Mungu alipotuma malaika kuua wana wote wa kiume wa kwanza Misri, malaika huyo alijulikana kama, "mwangamizi wa wana wa kwanza". Hii inaweza kutafsiriwa kama, "yule (au malaika) ambaye alwaua wana wa kiume wa kwanza". Katika kitabu cha Ufunuo kuhusu nyakati za mwisho, Shetani au roho nyingine chafu inajulikana kama, "Mwangamizi". Yeye ni "yule anayeangamiza" kwa sababu kusudi lake ni kuangamiza na kuharibu kila kitu alichoumba Mungu.
## mwenzi ### Ufafanuzi Mwenzi ni mtu anayekwenda na mtu mwingine au mwenye ushirika na mtu mwingine kwa mfano urafiki au ndoa. * Mwenzi hupitia katika jambo analipitia mwenzake kama kula pamoja na kutiana moyo. * Inategemea na mukhtadha neno hili laweza kutafsiriwa kama "rafiki" au "msafiri mwenzako" au "mtu anayekutia moyo."
## mwerezi ### Ufafanuzi "Mwerezi" ni mberoshi mkubwa ambao una rangi nyekundu. Kama miberoshi mingine ina umbo la sonobari na majani kama sindano. * Katika agano la kale mti wa mwerezi umetajwa ukihusishwa na labanoni ambapo ilikua kwa wingi. * Mbao ya mwerezi ilitumika kujenga hekalu la Yerusalemu. * Pia ilitumika katika sadaka ya kutakaswa na dhabihu.
## mwezi ### Ufafanuzi Neno "mwezi" linataja kipindi cha kuishia karibia majuma manne. Idadi ya majuma katika kila mwezi yalitofautiana kulingana na matumizi ya kalenda iliyotumika kwamba ilikumia jua au mwezi. * Katika kalenda ya mwezi, urefu wa mwezi unategemea kiwango cha muda mwezi unaotumia kuizunguka dunia, kama siku 29. Katika utaratibu huu kuna miezi 12 au 13 katika mwaka. Pamoja na mwaka kuwa na miezi 12 au 13, mwezi wa kwanza unaitwa kwa jina lilelile hata kama ni majira tofauti. * "Mwezi mpya," kuanza kwa awamu ya mwezi pamoja na nuru yake, unaashiria kuanza kwa kila mwezi katika kalenda ya mwezi. * Majina yote ya miezi yaliyotajwa katika Biblia yanatumia kalenda ya mwezi kwa kuwa ndio mfumo uliokuwa unatumiwa na Waisraeli. Wayahudu wa sasa bado wanatumia mfumo huu katika shughuri na makusudi ya kidini. * Kalenda ya siku hizi inayotumia jua imejengwa juu ya muda unaoichukua dunia kulizunguka jua (kama siku 365). Katika mfumo huu, mwaka kwa kawaida umegawanywa katika miezi 12, mwezi ukichukua kati ya siku 28-31.
## mwezi mpya ### Ufafanuzi Neno "mwezi mpya" katika Biblia ya husu mwezi unapo onekana mdogo, wa mwanga wa fedha. Huu ni mwanzo wa mwezi unapo hama na kuzunguka dunia. * Zama za kale, mwezi mpya ulitumika kuweka alama ya mwanzo wa nyakati. * Waisraeli walisherehekea mwezi mpya uliyo adhimishwa kwa kupuliza pembe la kondoo. * Biblia pia yataja hichi kipindi kama "mwanzo wa mwezi"
## mwiba, mbaruti ### Ufafanuzi Vicha vya miba na mbaruti ni majani matawi yaliyo chongoka au maua. Haya majani haya zalishi matunda au chochote kinacho tumika. * "Mwiba" ni mgumu, umechongoka katika tawi au jani. "Kichaka cha mwiba" ni aina ya mti mdogo mwenye miba mingi kwenye matawi yake. * "Mbaruti" ni mmea wenye majani yalichongoka. Mara nyingi majani yake ni ya zambarau. * Mwiba na mbaruti uota haraka na uweza shababisha mimea ya karibu kutostawi. Hii ni sura ya jinsi dhambi ina mzuia mtu kutozalisha matunda mazuri ya kiroho. * Taji lililo tengenzwa na matawi ya miba liliwekwa kwenye kichwa cha Yesu kabla ya kusulubiwa.
## mwizi, wezi, jambazi ### Ufafanuzi Haya maneno "mwizi" na "wezi" yanaeleza kwa jumla watu wanao iba pesa au mali kwa wengine. Neno "jambazi" mara nyingi la eleza mwizi anaye dhuru kimwili au kutishia watu anao waibia. * Yesu alitoa mfano kuhusu mwanaume mmoja Msamaria aliye msaidia mtu aliye shambuliwa na majambazi. Majambazi walimpiga na kumjeruhi kabla ya kuiba pesa na nguo zake. * Wezi na majambazi wanakuja ghafla kuiba, watu wasipo tarajia. Mara kadhaa wanatumia giza kuficha wanacho fanya. * Kwa fumbo, Agano Jipya la eleza Shetani kama mwizi anaye kuja kuiba, kuua, na kuharibu. Hii ina maana kuwa Shetani mpango wake ni kujaribu kushawishi watu wa Mungu kutomtii, kuiba vitu vizuri Mungu alivyo panga kwao.
## mwokovu ### Ufafanuzi Neno "mwokovu" la husu kuwa umeokolewa au kukombolewa kutoka kwenye uovu au hatari. * Katika Biblia, "mwokovu" wa husu ukombozi wakiroho na wa milele unao tolewa na Mungu kwa hao wanao tubu dhambi zao na kumuamini Yesu. * Biblia pia yazungumzia kuhusu Mungu kuokoa au kukomboa watu wake kutoka kwa maadui zao wa mwili.
## Mzabibu ### Ufafanuzi Mzabibu ni mmea unaopandwa na kukua kwa kutambaa ardhini au kwa kusimamisghwa juu ya mtu au kitu kingine. Katika Biblia neno mzabibu ni tunda pekee lililizalisha zabibu na kutoa mvinyo. * Matawi ya zabibu yanashikiliwa na shina kuu ambalo huyapa maji na virutubisho vingine ili iweze kukua. * Yesu alijiita mzabibu na akawaita watu wake matawi. Kwa mukhtadha huu mzabibu waweza kutafsiriwa kama shina la mzabibu.
## mzaliwa ### Ufafanuzi Neno "mzaliwa" ni fahirisi ya jumla kwa wazao wa kibaiolojia ya watu au wanyama. * Mara nyingi katika Biblia, "mzaliwa" ina maana moja na "watoto" au "wazao"\ * Neno "mbegu" wakati mwingine utumika kifumbo kumaanisha mzaliwa.
## mzawa wa kwanza ### Ufafanuzi Msemo "mzawa wa kwanza" una maana ya uzao wa watu au wanyama ambao huzaliwa kwanza, kabla ya wazawa wengine kuzaliwa. Mara kwa mara mzawa wa kwanza Katika Biblia, "mzawa wa kwanza" humaanisha mzaliwa wa kiume ambaye anazaliwa. Katika kipindi cha Biblia, mzawa wa kwanza wa kiume alipewa nafasi ya kujulikana na mara mbili ya urithi wa familia yake ya wana wengine. Mara nyingi ilikuwa mzawa wa kwanza wa kiume wa mnyama ambaye alitolewa sadaka kwa Mungu. Dhana hii inaweza kutumika kitamathali. Kwa mfano, taifa la Israeli linaitwa mzaliwa wa kwanza wa Mungu kwa sababu Mungu aliwapa faida maalumu kuliko mataifa mengine. Yesu, Mwana wa Mungu anaitwa mzawa wa kwanza wa Mungu kwa sababu ya umuhimu wake na mamlaka juu ya kila mtu. Mapendekezo ya Tafsiri Pale ambapo "mzaliwa wa kwanza" inajitokeza katika maandishi pekee, inaweza kutafsiriwa kama "mzawa wa kiume wa kwanza" kwa maana ndiyo kile kinachokusudiwa.
## mzeituni ### Ufafanuzi Mzeituni ni mdogo, tunda la mviringo kutoka mti wa mzeituni, ambayo uota maeneo yanayo zunguka Bahari ya Mediterenia. * Miti ya mizeituni ni ya majani makubwa yenye maua meupe. Uota vizuri sehemu za joto na kustahimili maji kidogo. * Matunda ya mzeituni ni ya kijani kwa rangi, ubadilika meusi yanapo komaa. Mzeituni utumika kula na kukamua mafuta. * Mafuta ya mzeituni yalitumika kupika, kuwasha taa, na sherehe za kidini. * Katika Biblia, miti ya mizeituni na matawi utumika kifumbo kumaanisha watu.
## mzigo ### Ufafanuzi Mzigo ni kitu kizito. Kwa uhalisia inamaanisha uzito wa kitu ambacho mnyama wa kazi angeweza kubeba. Neno "mzigo" pia linamaana kadhaa za kimafumbo: * Mzigo waweza kumaanisha kazi ngumu au wajibu wa mhimu ambao mtu anapaswa kuufanya. Anaswemwa "kuuchukua" au "kuubeba" "mzigo mzito." * Kiongozi katili aweza kuweka mizigo mizito kwa watu anaowaongoza, mfano kwa kuwalazimisha kulipa kiwango kikubwa cha ushuru. * Mtu asiyependa kuwa mzigo kwa mtu mwingine hapendi kumsababishia mtu huyo shida yoyote. * Hatia ya dhambi za mtu ni mzigo kwake. * "Mzigo wa Bwana" ni tamathari ya usemi kumaanisha "ujumbe kutoka kwa Mungu" ambao nabii anapaswa kuutoa kwa watu wa Mungu. * Neno "mzigo" laweza kufasiriwa kuwa "wajibu" au "jukumu" au "mzigo mzito" au"ujumbe," kutegemeana na mazingira.
## nabii wa uongo ### Ufafanuzi Nabii wa uongo ni mtu ambaye hudai kimakosa ya kwamba ujumbe wake unatoka kwa Mungu. Tabiri za manabii wa uongo mara kwa mara hazitimiliki. Yaani, haziji kuwa kweli. Manabii wa uongo hufundisha ujumbe ambao kwa juu juu au kwa ukamili hupingana na kile ambacho Biblia husema. Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "mtu ambaye hudai kwa uongo ya kuwa ni msemaji wa Mungu" au "mtu ambaye hudai kimakosa kuzungumza maneno ya Mungu". Agano Jipya hufundisha ya kwamba kipindi cha mwisho kutakuwa na manabii wengi wa uongo ambao watajaribu kudanganya watu kufikiri ya kwamba wanatoka kwa Mungu.
## nafaka ### Ufafanuzi Msemo "nafaka" mara nyingi ulimaanisha mbegu ya mmea wa chakula kama vile ngano, shayiri, mahindi, mtama, au mchele. Inaweza pia kumaanisha mmea wote. Katika Biblia, nafaka kuu ambayo inazungumziwa ni ngano na shayiri. Vichwa vya nafaka ni sehemu ya mmea ambao hushikilia nafaka. Kumbuka ya kwamba baadhi ya tafsiri za zamani za Biblia hutumia neno "mahindi" kumaanisha nafaka kwa ujumla. Hata hivyo katika lugha ya Kiingereza ya sasa, "mahindi" humaanisha aina moja ya nafaka tu.
## Najisi ### Ufafanuzi Kukinajisi kitu inamaana ya kufanya jambo kwa namna ya unajisi au kutokukiheshimu kitu ambacho ni kitakatifu. * Mtu ambaye ni najisi ni mtu ambaye anafanya mambo ambayo sio matakatifu na hamuheshimu Mungu. * Mungu aliwaambia Waisraeli kwamba wamejinajisi wenyewe kwa sanamu akiwa ana maana ya kwamba wamejichafua kwa dhambi hiyo. Pia hawakumuheshimu Mungu.
## najisi, kunajisiwa ### Ufafanuzi Msemo wa "najisi" na "kunajisiwa" ina maana ya kuchafuliwa au uchafu. Kitu kinaweza kunajisiwa kihalisia, kimaadili au kwa kaida za dini. Mungu aliwaonya Waisraeli wasijinajisi kwa kula au kugusa vitu ambavyo vimewekwa wakfu kuwa "chafu" au "kiovu". Baadhi ya vitu kama maiti na magonjwa ya kuambukiza vilitamkwa na Mungu kuwa vichafu na vinaweza kunajisi mtu iwapo atavigusa. Mungu aliwaamuru Waisraeli kuacha uasherati. Hivi vingewatia unajisi na kuwafanya kutokubalika kwa Mungu. Pia kulikuwa na aina kadhaa ya hatua za kimwili ambazo zilimnajisi mtu kwa muda mfupi hadi atakapokuwa safi kwa kaida za dini tena. Katika Agano Jipya, Yesu alifundisha ya kwamba mawazo ya dhambi na matendo ndiyo haswa yanayomnajisi mtu. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo wa "najisi" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kuwa chafu" au "kusababisha kuwa muovu" au "kusababisha kutokubalika kwa kaida za dini". "Kunajisiwa" kunaweza kutafsiriwa kama "kuwa mchafu" au "kusababisha kutokubalika kimaadili"
## ndara ### Ufafanuzi Ndara ni kiatu chenye soli bapa kilicho shika mguu na kamba iliyo zunguka mguu au kisigino. Ndara zinavaliwa na wanaume na wanawake. * Ndara wakati mwingine ilitumika kuthibitisha muhamala halali, kama kuuza mali kwa mtu mmoja kutoa ndara na kumpatia mwingine. * Kuondoa kiatu cha mtu au ndara ilikuwa ishara ya heshima, hususani katika uwepo wa Mungu. * Yohana alisema hakustahili kufungua kamba za ndara za Yesu, ambayo ingekuwa kazi ya mtumishi wa chini au mtumwa.
## ndoto ### Ufafanuzi Ndoto ni kitu ambacho watu huna au kupitia akilini mwao wanapokuwa wamelala. Ndoto mara kwa mara huonekana kama zinatokea kihalisia, lakini haziko hivyo. Mara nyingine Mungu husababisha watu kuota juu ya kitu ili waweze kujifunza kutoka na hicho kitu. Pia anaweza kuzungumza moja kwa moja na watu ndani ya ndoto zao. Katika Biblia, Mungu alitoa ndoto maalumu kwa baadhi ya watu kuwapa ujumbe, mara nyingi kuhusu jambo ambalo lingetoke hapo baadaye. Ndoto ni tofauti na maono. Ndoto hutokea wakati mtu amelala, lakini maono mara kwa mara hutokea wakati mtu yupo macho.
## Neno ### Ufafanuzi Neno ni kitu ambacho mtu husema. * Kwa mfano wakati ambao malaika alimwambia Zakaria "hauamini maneno yangu," alikuwa na maana ya kuwa "huamini nilichokisema." * Neno humaanisha ujumbe mzima na sio neno moja. * Kwenye Biblia neno ni kilakitu alichosema Mungu au kuamuru, "neno la Mungu" au "neno la kweli." * Matumizi ya pekee ya neno ni wakati Yesu anapoitwa "neno."
## Neno la kweli ### Ufafanuzi "Neno la kweli" ni njia nyingine ya kuelezea neno la Mungu au mafundisho yake. * Neno la kweli la Mungu ni pamoja na kilakitu ambacho Mungu anafundisha watu wake kuhusu yeye, uumbaji wake na mipango yake ya ukumbozi kupitia Yesu. * Neno la kweli linasisitiza kuwa anachotuambia Mungu ni kweli na hakika.
## ng'ombe ### Ufafanuzi "ng'ombe" lina husu aina ya mifugo waliyo fundishwa kulima mazao. * Katika Biblia, ng'ombe wana hashiriwa kama wanyama waliyo fungwa na nira kuvuta gari au kulima. * Ng'ombe wakifanya kazi pamoja chini ya nira ilikuwa kawaida ya tukio katika Biblia hadi kwamba msemo "kuwa chini ya nira" ilikuwa umbo la kazi ngumu. * Ng'ombe dume, hajatahiriwa walakufunidshwa kuwa mnyama wa kazi.
## Ng'ombe, fahali, ndama, mifugo ### Ufafanuzi Mifugo ni kundi kubwa la wanyama wenye miguu minne wanaokula majani na hufugwa kwa ajili ya maziwa na nyama. * Ng'ombe dume huitwa fahali na ng'ombe mdogo huitwa ndama. * Mara nyingine ng'ombe hutumika kuwakilisha aina zote za mifugo. * Katika tamaduni zingine ng'ombe hubadilishwa na bidhaa katika biashara. Mara nyingine hutumika kama zawadi itolewayo kwa wazazi wa binti na mwanaume anayetaka kumuoa. * Katika Biblia Wayahudi walitumia mifugo kwa ajili ya dhabihu hasa ng'ombe mwekundu. * Ng'ombe mwekundu ni ng'ombe ambaye hajazaa bado. * Pia kuna ng'ombe dume ambaye hutumika katika shughuli za kilimo.
## Ngamia ### Ufafanuzi Ni mnyama mkubwa mwenye miguu minne na mwenye nundu moja au mbili mgongoni.
## Ngano ### Ufafanuzi Ngano ni aina ya nafaka ambayo watu huzalisha kwa ajili ya chakula. Biblia inapotaja ngano au mbegu inazungumza juu ya nafaka ya ngano au mbegu. * Mbegu za ngano au nafaka huota juu ya mmea wa ngano. * Baada ya kuvuna ngano, nafaka hutenganishwa na shina la mmea kwa kupura. Shina ala ngano pia huitwa mabua na mara nyingine huwekwa chini kwa ajili ya wanyama kulalia. * Watu husaga ngano kwenye sakafu na hutumia kutengenezea mkate.
## ngao ### Ufafanuzi Ngao ni chombo kinacho shikiliwa na mwanajeshi katika pambano kuweza kujilinda hasiumizwe na silaha za maadui. * Ngao zilikuwa za mviringo na zilitengenezwa na vifaa kama vile ngozi, mbao, au chuma ngumu na nene kuweza kuzuia upanga au mshale kutoboa. * Kwa kutumia hili neno kama mfano, Biblia inamtaja Mungu kama ngao ya ulinzi kwa watu wake. * Paulo Pia anaeleza "ngao ya imani," ambayo ni umbo linalo onyesha kuwa kuishi kwa kumuamini Yesu, na kumtii Mungu, kutawalinda waamini kutokana na mashambulio ya kiroho ya Shetani.
## ngome, kimbilio ### Ufafanuzi Maneno "ngome" na "kimbilio" yote ueleza maeneo yaliyo lindwa dhidi ya shambulio na maadui wanajeshi. * Mara kadhaa, ngome na kimbilio ni sehemu zilizo tengenezwa na kuta kijihami. Zaweza pia kuwa sehemu zilizo inuka kama milimani. * Watu uimarisha ngome kwa kujenga kuta nene au majengo mengine yanayo fanya vigumu kwa adui kuingia. * "Ngome" au "kimbilio" yaweza tafsiriwa kama "sehemu iliyo lindwa" * Hili neno pia utumika kifumbo kumanisha Mungu ni ngome au kimbilio kwa wao wanao muamini.
## ngumu, ugumu, fanya - gumu ### Ufafanuzi Neno 'ngumu' lina maana nyingi sana kutegemea na muktadha. Mara nyingi hueleza kuwa kitu fulani ni kigumu, kuvumilia au kutotoa/kutozaa. Maelezo kama "moyo mgumu" au " kichwa kigumu" inarejelea watu wakaidi wasiotubu. Maneno haya yanaongelea watu wanaoendelea kumwasi Mungu. Lugha ya picha ya maneno 'ugumu wa moyo" na "ugumu wa mioyo yao' yana maana pia ya kuwa na kiburi na uasi. Kama moyo wa Mtu umefanywa 'kuwa mgumu' hii ina maana kuwa mtu huyo anakataa kumtii na kubaki kuwa mkaidi asiyetaka kutubu. Neno moyo likitumika kama kielezi " kwa moyo" likimaanisha kufanya kazi kwa nguvu na kwa juhudi ili kufanya kitu vizuri. Mapendekezo ya tafsiri Neno ' -gumu"laweza kufasiriwa kama 'ukaidi' au "ugumu' au 'changamoto' kwa kutegemea na muktadha. Maneno kama 'ugumu' au 'ugumu wa moyo'' .yanaweza kutafsiriwa kama " ukaidi' au kudumu katika uasi' au 'mtazamo wa uasi' au ' uasi' au hali ya kutotubu. "Usiufanye moyo wako kuwa mgumu" inaweza kufasiriwa kama "usikate kutubu '' au "usiendelee kuasi kwa ukaidi." Maneno kama "kuwatesa watu kwa kazi ngumu" yaweza kutafsiriwa kama "lazimisha watu kufanya kazi ngumu kwa kiwango cha kuwatesa au kusababisha mateso kwa watu kwa kuwalazimsha kufanya kazi ngumu. "kazi ngumu" neno hili huhusishwa zaidi na kazi ngumu au ugumu anaokutana nao mwanamke katika kipindi cha kujifungua mtoto.
## nguo ya gunia ### Ufafanuzi Nguo ya gunia ilikuwa ya kukwaruza, nguo iliyo tengenezwa kwa nywele ya mbuzi au nywele ya ngamia. * Nguo zilizo tengenezwa kwa gunia ili kuwa sio nzuri mwilini kwa mtu aliyo vaa. Ilivaliwa kwa ajili ya kuonyesha kilio, uzuni, au toa ya unyenyekevu. * Maneno "nguo ya magunia na majivu" ilikuwa ni msemo uliyo zoeleka ukihashiria namna ya kitamaduni ya uzuni na toba.
## Nguruwe ### Ufafanuzi Mguruwe ni mnyama mwenye mihuu minne anayefugwa kwa ajili ya nyama. Nyama yake inaitwa nyama ya nguruwe. * Mungu aliwaambia Waisraeli wasile nguruwe na kuiona kuwa ni najisi. Mpaka leo Wayahudi wanaona nguruwe kuwa ni najisi na hafai kuliwa. * Nguruwe wanafugwa kwenye mashamba na kuuzwa kwa watu wengine kwa ajili ya nyama.
## nguva ### Ufafanuzi Neno "nguva" ni mnyama mkubwa wa baharini anaye kula nyasi na mimea mingine katika sakafu ya bahari. * Nguva ni wa kijivu mwenye ngozi nene. Anatembea kwenye maji kwa kutumia kikono. * Ngozi za nguva zilitumika na watu wa Biblia kwa kutengeneza mahema. Hizi ngozi za wanyama zilitumika kwa vifuniko vya maskani.
## nguzo ya mlango ### Ufafanuzi "Nguzo ya mlango" ni mhimili ulio wima katika pande zote za mlango, ambao unategemeza kiunzi cha mlango cha juu. Kabla tu Mungu hajawasaidia Waisraeli kutoroka kutoka Misri, aliwaelekeza kuua mwanakondoo na kuweka damu yake juu ya nguzo za milango. Katika Agano la Kale, mtumwa aliyetamani kumtumikia bwana wake maisha yake yote aliweka sikio lake juu ya nguzo ya mlango wa nyumba ya bwana wake na msumari kupigiliwa katika sikio lake katika nguzo ya mlango. Hii inaweza kutafsiriwa kama "nguzo ya mbao iliyo katika kila upande wa mlango" au "pande za viunzi vya mlango" au "nguzo za mbao zilizo pande za mlango".
## nguzo, safu ### Ufafanuzi "Nguzo" ni nguzo kubwa zilizosimama wima zinazotumika kushikilia paa au sehemu nyingine ya jengo. Jina lingine la nguzo ni safu. * Katika nyakati za Biblia Nguzo zilitumika kushikilia majengo ambayo mara nyingi yalichongwa toka kwenye kipande cha jiwe. * Samsoni katika agano la kale alipokamatwa na Wafilisti aliharibu hekalu lao la kipagani kwa kuzisukuma nguzo zilizoshikilia na kusababisha hekalu kuanguka. * Nguzo pia inaweza kuwa jiwe kubwa lililowelwa kama alama ya kaburi au alama ya sehemu ambayo tukio la muhimu lilifanyika. * Pia nguzo yaweza kuwa sanamu iliyotengenezwa kwa ajili ya kuabudu miungu ya uongo. * Nguzo pia yaweza kuwa kitu kilichotengenezwa kama nguzo mfano "nguzo ya moto" iliyowaongoza Waisraeli usiku katika jangwa au "nguzo ya chunvi" ambayo mke wa Lutu alikuja kuwa hivyo baada ya kuangalia nyuma.
## nia ### Ufafanuzi Neno "nia" la husu sehemu ya mtu inayo fikiri na kufanya maamuzi. * Nia ya kila mtu ni jumla ya mawazo na fikra yake. * Kuwa na "nia ya Kristo" ina maana kufikiri na kutenda kama Yesu Kristo alivyo waza na kufanya. Ina maana kuwa mtiifu kwa Mungu Baba, kutii mafundisho ya Kristo, kuwezeshwa kufanya hivi kupitia nguvu ya Roho mtakatifu. * "Kubadilisha nia yake" ina maana mtu alifanya uwamuzi tofauti au alikuwa na maoni tofauti na yale alikuwa nayo.
## Nira ### Ufafanuzi Nira ni kipande cha mbao au chuma kinachowekwa kwa wanyama wawili au zaidi ili kuwaunganisha kwa ajili ya lengo la kuvuta plau au gari. * Pia nira imetumika kuelezea kitu kilichowaunganisha watu kwa ajili ya lengo la kufanya kazi pamoja kwa mfano kumtumikia Yesu. * Paulo anatumia neno "mjoli" kumaanisha mtu anayemtumikia Yesu kama alivyo. * Neno "nira" pia linaweza kutumika kama mzigo mzito ambao mtu anaubeba kwa mfano anayetumikishwa utumwani au kwenye mateso. * Namna nyingine ya kutafsiri neno hili waweza kutumia neno "mzigo mzito".
## njaa ### Ufafanuzi Msemo "njaa" una maana ya upungufu mkubwa sana wa chakula katika nchi au eneo lote, mara nyingi kutokana na kutokuwa na mvua ya kutosha. Mazao ya chakula yanawvza kushindwa kutokana na sababu za asili kama vile ukosefu wa mvua, magonjwa ya mazao, au wadudu. Upungufu wa chakula pia unaweza kusababishwa na watu, kama vile adui kuangamiza mazao. Katika Biblia, Mungu mara nyingi huleta njaa kama njia ya kuadhibu mataifa wanapotenda dhambi dhidi yake. Katika Amosi 8:11 msemo "njaa" unatumika kitamathali kumaanisha kipindi ambapo Mungu aliadhibu watu wake kwa kutozungumza nao. Hii naweza kutafsiriwa kwa neno moja kwa ajili ya "njaa" kwa lugha yako, au kwa msemo kama wa "upungufu mkubwa".
## njiwa, ninga ### Ufafanuzi Njiwa na ninga ni aina mbili ya ndege wadogo wa kijivu na kahawia ambao wanafanana. Njiwa mara nyingi hufikiriwa kuwa na rangi iliyo nyepesi, karibu na nyeupe. Baadhi ya lugha zina majina mawili tofauti kwa ajili yao, wakati wengine wanatumia jina moja kwa wote wawili. Njiwa na ninga walitumiwa katika sadaka kwa Mungu, hasa kwa watu ambao hawakuweza kununua wanyama wakubwa. Njiwa mara nyingine huashiria usafi, sio na hatia, au amani. Kama njiwa au ninga hawajulikani katika lugha ambayo tafsiri inafanywa, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "ndege mdogo, wa kijivu na kahawia anayeitwa njiwa". Kama njiwa na ninga wote wanawekwa katika mstari mmoja, ni vyema kutumia maneno mawili tofauti kwa ndege hawa, ikiwezekana.
## nuru ### Ufafanuzi Kuna matumizi kadhaa ya kimafumbo ya neno "nuru" katika Biblia. Mara nyingi inatumika kama sitiari ya haki, utakatifu, na ukweli. Yesu alisema, "Mimi ni nuru ya ulimwengu" kumaanisha kuwa analeta ujumbe wa kweli wa Mungu duniani na kuwaokoa watu kutoka kwenye giza la dhambi zao. Wakristo wanaamriwa "kutembea nuruni," ambayo inamaanisha wanatakiwa kuishi jinsi Mungu anavyotaka waishi na kuacha kutenda maovu. Mtume Paulo alisema kuwa "Mungu ni nuru," na hakuna giza ndani yake. Nuru na giza ni tofauti kabisa. Giza ni ukosefu wa nuru. Yesu alisema kuwa yeye "ni nuru ya ulimwengu" na kwamba wafuasi wake wanapaswa kung'aa kama nuru duniani, kwa kuishi kwa naamna inayoonesha ukubwa wa Mungu. "Kutembea nuruni" inaonesha kuishi njia inayompendeza Mungu, kufanya yaliyo mema na sawa. Kutembea gizani inaonesha kuishi kwa kuasi dhidi ya Mungu, kufanya mambo maovu.
## nyakuliwa, nyakuliwa pamoja ### Ufafanuzi Neno "nyakua" mara nyingi linamrejea Mungu akimchukua mtu juu mbinguni ghafula, katika njia ya muujiza. * Tafsiri ya "nyakua pamoja" inaonyesha kuja kwa mwingine baada kumfikia kwa haraka. Neno hili ni kitu kile kile na "pita." * Mtume Paulo alizungumzia kuhusu hali ya "nyakuliwa" pamoja kuonana naye mawinguni. * Paulo alisema kwamba wakati Kristo atakaporudi, Wakristo wata "nyakuliwa" pamoja kuonana naye hewani. * Maana ya fumbo, "dhambi zangu zimechukuliwa na mimi" inaweza kutafsiriwa kama, "Ninapokea matokeo ya dhambi zangu" au "kwa sababu ya dhambi zangu ninasumbuku" au "dhambi zangu zinanifanya nisumbuke"
## nyenyekea, kwa unyenyekevu ### Ufafanuzi Neno "nyenyekea" mara nyingi umanisha kumueka mtu chini * Biblia uwaambia waamini wa Yesu kunyenyekea kwa Mungu na mamlaka nyingine katika maisha yao. * Maelekezo "kunyenyekea ninyi kwa ninyi" ina maana ya kukubali marekebisho na kuangalia mahitaji ya wengine.
## nyoka ### Ufafanuzi Neno "nyoka" la husu
## Nyumba ### Ufafanuzi Istilahi 'nyumba' hutumika kama tamathali ya semi (mfano) katika Biblia. Mara nyingine hutumika kumaanisha 'kaya' kurejelea watu wanaoishi pamoja katika nyumba. Mara zote neno 'nyumba' humaanisha wazao au watoto au ndugu wengine. Mfano, nyumba ya Daudi huwa na maana ya uzao wa Daudi. Maneno kama 'nyumba ya Mungu' au 'nyumba ya Yahweh' huwa na maana ya hekalu au hema la kukutania au sehemu Mungu alipo. Katika Waebrania 3, "Nyumba ya Mungu" ni sitiari ikimaanisha Watu wa Mungu. Kifungu cha maneno ' nyumba ya Israeli" kwa ujumla huwa na maana ya taifa laote la Israeli au hasa hasa kwa makabila ya ufalme wa Kasikazini wa Israeli. Mapendekezo ya tafsiri kwa kutegemeana na muktadha, neno, nyumba linaweza kuwa na maana ya 'kaya' ' watu, familia, uzao, hekalu au sehemu ya kukaa.'' "Nyumba ya Daudi' in maana ya ''ukoo wa Daudi, familia ya Daudi au uzao wa Daudi. "Nyumba ya Israeli' ina maana ya watu wa Israeli au wazao wa Israeli au waisraeli. 'Nyumba ya Yahweh' ina maana ya hekalu au sehemu ya kumwabudia Mungu.
## nyumba ya ghala ### Ufafanuzi "nyumba ya ghala" ni jengo kubwa linalo tumika kuhifadhi chakula au vitu vingine, mara nyingi kwa muda mrefu. * Katika Biblia "nyumba ya ghala" ilitumika kuhifadhi nafaka na vyakula vingine kutumika baadae palipo kuwa na uaba wa chakula kwasababu ya ukame. * Nyumba za ghala la hekalu lilikuwa na hifadhi ya vitu vingi, kama dhahabu na fedha, vilivyo tolewa kwa Yahweh. Vingine vilitumika kukarabati hekalu.
## nzige ### Ufafanuzi Neno "nzige" linamaanisha aina kubwa ya panzi anayepaa ambaye wakati mwingine hupaa katika makundi makubwa ambayo huleta madhara makubwa, wakila mboga zote njiani. Nzige na panzi wengine ni wakubwa, wenye mabawa yaliyo wima na miguu ya nyuma mirefu inayowapa uwezo wa kuruka mbali. Katika Agano la Kale, makundi ya nzige yanazungumziwa kimafumbo kama alama au picha ya uharibifu mkubwa utakaokuja kama matokeo ya kutokutii kwa Israeli. Mungu alituma nzige kama moja ya mapigo kumi dhidi ya Wamisri. Agano Jipya linasema kuwa nzige walikuwa chanzo kikubwa cha chakula cha Yohana mbatizaji alipokuwa akiishi jangwani.
## Onyo ### Ufafanuzi Onyo ni kitu ambacho kinawatahadharisha watu juu ya jambo fulani ambalo linaweza kuwadhuru. "kuonywa" ni kuambiwa juu ya jambo fulani la hatari. * Mfalme Yehoshafati alionywa aliposikia Wamoabu wanapanga kuvamia ufalme wa Yuda. * Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasiwe na wasiwasi watakaposikia juu ya majanga yatakayotokea siku za mwisho. * "kutoa onyo" inamaanisha kutoa tahadhari. Zamani mtu aliweza kupaza sauti za kutoa onyo kwa kupiga kelele ya kitu kama kengele.
## Pagani ### Ufafanuzi Katika nyakati za Biblia neno "pagani" lilitumika kuwaelezea watu ambao waliabudu miungu ya uongo badala ya Bwana. * Kilakitu kilichokuwa kinahusiana na watu hawa kama madhabahu walizokuwa wanaabudia, ibada walizokuwa wakifanya na imani zao zote zilikuwa zikiitwa "pagani" * Mfumo wa imani wa kipagani ulijumuisha kuabudu miungu ya uongo na kuabudu asili * Baadhi ya dini za kipagani zilijumuisha ibada za uzinzi na mauaji ya watu kama sehemu ya kuabudu kwao.
## panda, mpandaji, mmea ### Ufafanuzi "kupanda" ina maana kuweka mbegu kwenye ardhi ilikuweza kuotesha mimea. "Mpandaji" ni mtu anaye mpanda au kupanda mbegu. * Njia ya kupanda au kuotesha kwa tafautiana, lakini mbinu moja ni kuchukuwa mkono uliyo jaa mbegu na kusambaza kwenye ardhi. * Mbinu nyingine ya kuotesha ni kufanya mashimo katika udogo na kuweka mbegu katika kila shimo. * Neno "panda" laweza tumika kimfano kama vile, "mtu atavuna alicho panda."
## Pazia ### Ufafanuzi Katika Biblia pazia ni kitu kinene, chenye nyenzo nzito kinachotumika kutengenezea maskani na hekalu. * Maskani ilitengemezwa kwa matabaka manne ya pazia kwa juu na pembeni. Mapazia haya yanayofunika yalitengenezwa kwa nguo au ngozi za wanyama. * Mapazia ya nguo yalitumika pia kutengeneza ukuta uliozunguka ua la maskani. * Yote maskani na jengo la hekalu, pazia zito lilikuwa kati ya patakatifu na patakatifu pa patakatifu. Ni pazia hili lililopasuka kwa miujiza Yesu alipokufa.
## Pembe, Mapembe ### Ufafanuzi Mapembe ni sehemu za juu katika kichwa cha mnyama zilizo ngumu, za kudumu na zilizochongoka. Wanyama wa aina nyingi huwa na mapembe, wanyama kama ng'ombe, kondoo, mbuzi, swala n.k. Pembe la kondoo dume lilitumika kutengeneza chombo cha muziki kilichoitwa 'sofari' ambacho kilipulizwa katika matukio maalumu ya sikukuu za kidini. Mungu aliwaambia waisraeli kutengeneza pembe nzuri katika kila kona ya madhabahu ya uvumba. Neno pembe wakati mwingine lilitumika kurejelea chupa iliyokuwa imetengenezwa kwa muundo kama pembe na ilitumika kwa ajili ya kutunza maji au mafuta. Chupa hii ilitumika katika kuwatia mafuta wafalme kama vile Samweli alivyofanya kwa Daudi. Neno hili inabidi litafsiriwe kwa neno tofauti na tarumbeta. Neno hili 'lpembe' hutumika pia kama lugha ya picha kumaanisha ' nguvu, uwezo, na mamlaka
## pepeta, chekecha ### Ufafanuzi "Pepeta" na "chekecha" ni kutenganisha ngano na makapi. Katika Biblia maneno yote mawili yametumika yakimaanisha kutenganisha au kuwagawa watu. * Kupepeta inamaana ya kutenganisha ngano na makapi kwa kupepeta juu ya hewa na kuruhusu upepo kupeperusha makapi. * Kuchekecha ni kutingisha ngano iliyopepetwa kwenye ungo ili kutoa makapi yaliyobaki kama mawe. * Katika agano la kale kupepeta na kuchekecha imetumika kuelezea ugumu unaotenganisha watu wenye haki na wasio haki. * Yesu pia anatumia neno kuchekecha kumwambia Simoni Petro ni kwa namna gani yeye na wanafunzi wengine watajaribiwa imani yao.
## Pigo ### Ufafanuzi Mapigo ni matukio yanayosababisha mateso au kifo kwa idadi kubwa ya watu. Mara nyingi pigo laweza kuwa magonjwa yanayosambaa kwa haraka na kusababisha watu wengi kufa kabla ya kuweza kudhibitiwa. * Mapigo mengi yana sababu zake lakini mengine yanatumwa na Mungu ili kuwaadhibu wenye dhambi. * Nyakati za Musa Mungu alituma mapigo kumi juu ya Wamisri ili kumfanya Farao awaache Waisraeli waondoke Misri. Mapigo haya yalikuwa maji kugeuka kuwa damu, magonjwa, wadudu kuharibu mazao, siku tatu za giza na vifo vya watoto wa kwanza. * Hii yaweza kutafsiriwa kama "majanga makubwa" au "ugonjwa unaoenea" kutegemea na muktadha.
## Plau ### Ufafanuzi "Plau" hiki i kifaa cha shambani kinachotumika kuvunjavunja udongo na kuandaa shamba kwa ajili ya kupanda. * Plau ina makali, na meno ya jembe yanayochimba kwenye udongo. Mara nyingi huwa na mpini ambao mkulima hutumia kuiongoza plau. * Katika nyakati za Biblia plau zilisukumwa na jozi ya ng'ombe au mnyama mwingine wa kazi. * Plau nyingi zimetengenezwa na mbao ngumu isipokuwa sehemu ya mcha ambayo hutengenezwa na chuma.
## Ponya, tibu ### Ufafanuzi Maneno 'ponya' na 'tibu' yote mawili yana maana ya kumfanya mtu aliye mgonjwa, aliyejeruhika na asiyejiweza (mlemavu) kuwa na afya nzuri tena. Mtu aliyeponya au kutibiwa amekuwa amefanywa mzima na mwenye afya nzuri tena. Uponyaji waweza kutokea tu kiuasilia bila kutumia kitu chochote, hii ni kwasababu Mungu alitupa miili yenye uwezo wa kupona na kurudia hali yake ya kawaida hata kama ina vidonda au magonjwa ya aina mbalimbali. Aina hii ya uponyaji hutokea polepole. Hata hivyo hali zingine kama kuwa upofu au ulemavu, na magonjwa mengine kama ukoma hayawezi kupona menyewe tu. Wakati watu wenye magonjwa kama haya wanapoponywa huwa ni muujiza ambao hautokei mara kwa mara. Kwa mfano, Yesu aliponya watu wengi walikuwa vipofu, vilema na wagonjwa na wakapona hapo hapo. Mitume pia waliponya watu kwa miujiza, kwa mfano Petro alimfanya mlevu aweze kutembea mara hiyo.
## pukuta, pukuchua ### Ufafanuzi Maneno "pukuta" na "pukuchua" yanaeleza sehemu ya kwanza ya gawanya nafaka ya ngano kutoka kwenye mmea wa ngano. * Kupukuta mmea wa ngano una legeza nafaka kutoka kwenye ganda lake. Baada ya hapo nafaka ina "pepetwa" kugawanya kabisa nafaka kutoka kwenye majani yote yasio itajika, ikiacha sehemu ya nafaka inayo lika. * Wakati wa Biblia, "eneo la kupukuta" lilikuwa sakafu au sehemu iliyo shindiliwa udongo, ikiweka ugumu, kwenye sakafu kusagia nafaka. * "Gari la kupukuta" wakati mwingine lilitumika kusaga nafaka na kusaidia kugawanya kutoka kwenye jani lake.
## Pumzika ### Ufafanuzi Pumzika inamaana ya kuacha kufanya kazi kwa nia ya kupumzika na kupata nguvu. * Kitu kikiwa kimepumzika ina maana kuwa kimesimama au kukaa mahali. * Meli iliyopumzika mahali imesimama na kutia nanga. * Mtu au mnyama anapopumzika yaweza kuwa amekaa au amelala kwa ajili ya kustarehe. * Mungu aliwaamuru Waisraeli wapumzike siku ya saba ya wiki. Siku hii ya kutokufanya kazi iliitwa Sabato.
## punda, nyumbu ### Ufafanuzi Punda ni mnyama wa kazi mwenye miguu minne, anayefanana na farasi, lakini mdogo kidogo na mwenye masikio marefu zaidi. Nyumbu ni uzao tasa atokanaye na punda dume na farasi jike. Nyumbu ni wanyama wenye nguvu sana na kwa hiyo ni wanyama wa kazi wenye thamani sana. Punda na nyumbu wote wanatumika kubeba mizigo na watu wanaposafiri. Katika kipindi cha Biblia, wafalme huendesha punda katika wakati wa amani, kuliko farasi, ambaye alitumika katika kipindi cha vita. Yesu aliendesha kuingia Yerusalemu juu ya punda mdogo wiki moja kabla hajasulubiwa kule.
## Ripoti ### Ufafanuzi Ripoti inamaana kuwaambia watu kuhusu kitu kilichotokea kutoa habari juu ya tukio hilo. Ripoti yaweza kutamkwa au kuandikwa. * "Ripoti" yaweza kutafsiriwa kama "kusema" au "kuelezea kwa kina." * Sentensi inayosema "usiripoti hili kwa mtu yeyote" inamaana kuwa "usiseme jambo hili kwa mtu yeyote."
## Rudi ### Ufafanuzi Neno "rudi" linamaanisha kurudi au kurudisha kitu. * "Kurudia" ni kitendo cha kuanza kufanya kitu tena. * Waisraeli walipoirudia miungu yao walianza kuiabudu tena. * Waliporudi kwa Bwana, walitubu na walimwabudu Mungu tena. * Kurudisha ardhi au vitu vilivyochukuliwa au kupokelewa toka kwa mtu inamaana ya kurudisha mali ile kwa mwenye mali. * "Kurudi" yaweza kutafsiriwa kama "kurudi nyuma" au "kurudisha"
## rushwa ### Ufafanuzi Neno "rushwa" inamaanisha kumpa mtu kitu cha thamani, kama pesa, kumshawishi afanye jambo bila uaminifu. * Askari waliolilinda kaburi wazi la Yesu walipewa rushwa ya pesa wakasema uongo juu ya kilichotokea. * Wakati mwingine maofisa wa serikali wanapewa rushwa ili wasilione kosa au kupiga kura kwa njia nyingine. * Biblia inazuia kutoa au kupokea rushwa. * Neno, "rushwa" laweza kutafasiriwa kama "malipo yasiyo harali" au "malipo ya uongo" au "thamani ya kuvunja sheria". * "Kufanya ongo" kwaweza kutafasiriwa kwa neno au kifungu kinachomaanisha, "kulipa ili kushawishi (mtu)" au "kulipa ili upendeleo usio halari ufanyike" au "kulipa kwa ajili ya upendeleo."
## Rushwa ### Ufafanuzi Rushwa ni hali ambayo watu wameharibika,hawana maadili na sio waaminifu. * Rusha inamaana ya kuharibika kimaadili. * Mtu ambaye ni fisadi ameacha kabisa kweli na kufanya mambo yasiyofaa na yaliyoharibika. * Pia kuna kitendo cha kumfanya mtu awe fisadi kwa kumchochea asiwe mwaminifu na afanye mambo yasiyo na maadili.
## saa ### Ufafanuzi Neno "saa" linatumika mara kwa mara katika Biblia kuonesha muda wa siku jambo fulani lilipotendeka. Pia linatumia tamathari kumaanisha "wakati" au "kitambo" * Wayahudi walihesabu masaa ya kutwa kuanzia mawio ya jua (kama saa 12:00 asubuhi). Kwa mfano, "saa tisa" alasiri. * Masaa ya usiku yalihesabiwa kuanzia machweo (kama saa 12: 00 jioni). Kwa mfano, "saa tatu ya usiku" kumaanisha karibia saa tisa za usiku" katika mfumo wetu wa siku hizi. * Kwa kuwa kumbukumbu za muda katika Biblia hazitalingana kamili na mfumu wa siku hizi, vifungu kama vile "karibia saa tisa" au "kama saa sita kamili" yaweza kutumika. * Baadhi ya tafasiri zaweza kuonesha vifungu kama vile "wakati wa jioni" au "wakati wa asubuhi" au "wakati wa mchana" kuweka wazi ni muda upi wa siku unaozungumzwa. * Kirai, "wakati uo" chaweza kutafasiriwa kama "katika wakati ule" au "katika kitambo hicho". * Kwa kumtaja Yesu, kifungu "wakati wake umefika" yaweza kutafasiriwa kama, "muda wake wa kufanya" au "muda uliowekwa kwa ajili yake ulikuwa umefika."
## Saa ### Ufafanuzi Pamoja na kutumika kuonesha wakati au muda gani jambo lilitokea, neno 'saa' hutumika kwa namna nyingi kimfano kama tamathali za semi. Wakati mwingine 'saa' hutumika kuonesha muda maalumu uliopangwa, kwa mfano 'saa ya maombi.' Wakati maandiko yanaposema kuwa saa imefika kwa Yesu kuteswa na kuuawa, ilikuwa na maana ya muda maalumu uliowekwa ambao MUngu alikuwa ameukusudia muda mrefu uliopita kuwa ungetokea. Neno 'saa' laweza kutumika pia kumaanisha 'kitambo' au 'wakati huo' Kifungu kinapozungumzia " saa kuchelwa" in maana kwamba ' ilichelewa katika siku wakati juu lingelikuwa linazama upesi' Mapendekezo ya tafsiri Neno 'saa' linapotumika kimfano laweza kuwa na maana ya 'muda' kitambo' au 'wakati ulioteuliwa.' Virai kama "katika saa ile" au ''saa ile ile'' vyaweza kutafsiriwa kama "kitambo kile'' au ''muda ule'' au mara'' au '' ghafla'' au ''hapo hapo'' Maelezo kuwa '' saa ilichelewa'' yana maana ya '' ilichelewa katika siku''
## Sadaka ### Ufafanuzi "Sadaka" yaweza kuwa ppesa, chakula au chochote ambacho masikini anaweza kupewa kama msaada. * Mara nyingi kutoa sadaka ilionekana kuwa jambo ambalo dini zao ziliwataka wafanye hivyo ili kuwa na haki. * Yesu alisema kutoa sadaka hakupaswi kuwa wazi wazi ili watu wengine wakuone. * Neno hili laweza kuafsiriwa kama "pesa" au "zawadi kwa masikini" au "kuwasaidia masikini."
## Sadaka ya amani. ### Ufafanuzi Sadaka ya amani ilikuwa moja ya sadaka ambayo Mungu aliwaamuru Waisraeli watoe. Mara nyingine iliitwa sadaka ya shukrani au sadaka ya ushirika. * Sadaka hii inajumuisha kutoa mnyama asiye na kasoro na kuinyunyuzia damu ya myama katika madhabahi na kuteketeza mafuta ya mnyama pamoja na vipande vya mnyama vilivyobaki kwa kutenganisha. * Katika sadaka hii iliambatana na mkate wenye chachu na usiotiwa chachu ambayo iliteketezwa juu ya sadaka. * Kuhani na mtoa sadaka waliruhusiwa kula chakula kilichotolewa kama sadaka. * Sadaka hii ilionesha ushirika wa Mungu na watu wake.
## sadaka ya dhambi ### Ufafanuzi "sadaka ya dhambi" ilikuwa moja ya dhabihu ambazo Mungu aliamuru Waisraeli kutoa. * Hii sadaka ilihusisha kumtoa dhabihu ng'ombe dume, kuchoma damu yake na mafuta kwenye madhabahu, na kuchukuwa mwili wa huyo mnyama na kuuchoma kwenye ardhi nje ya kambi ya Waisraeli. * Uchomwaji mzima wa huyu mnyama unaonyesha jinsi Mungu alivyo mtakatifu na jinsi dhambi ilivyo mbaya. * Biblia inafundisha ilikuweze kuwa na utakaso wa dhambi, damu alazima imwagwe kulipa gharama ya dhambi iliyo tendwa. * Dhabihu za wanyama hazikuweza kuleta daima msamaha wa dhambi.
## sadaka ya hatia ### Ufafanuzi Sadaka ya hatia ilikuwa sadaka ambayo Mungu alihitaji kwa Waisraeli kufanya kama walifanya jambo kwa bahati mbaya kibaya kama vile kutomheshimu Mungu au kuharibu mali ya mtu mwingine. Sadaka hii ilihusisha kutoa mnyama na kulipa faini, kwa pesa ya fedha au dhahabu. Kwa kuongeza, mtu mwenye kosa alikuwa na wajibu wa kulipa kwa uharibifu wowote ambao ulifanyika.
## sadaka ya kinywaji ### Ufafanuzi Sadaka ya kinywaji kilikuwa sadaka kwa Mungu amabyo ilihusisha kumwaga divai juu ya madhabahu. Mara kwa mara ilitolewa pamoja na sadaka ya kuteketeza na sadaka ya mazao. Paulo anamaanisha maisha yake kama kumwagwa nje kama sadaka cha kinywaji. Hii ina maana ya kwamba aliwekwa wakfu kabisa kumtumikia Mungu na kuwaambia watu juu ya Yesu, hata kama alijua angeteseka na labda kuuwawa kwa sababu ya hiyo. Kifo cha Yesu juu ya msalaba kilikuwa sadaka ya kinywaji ya mwisho, na damu yake ilimwagwa juu ya msalaba kwa ajili ya dhambi zetu. Mapendekezo ya Tafsiri Njia nyingine ya kutafsiri msemo huu unaweza kuwa, "saaka ya divai ya mizabibu". Paulo anaposema anakuwa "anamwagwa kama sadaka" hii inaweza kutafsiriwa kama, "nimejikabidhi kufundisha ujumbe wa Mungu kwa watu, kama sadaka ya divai inavyomwagwa kabisa juu ya madhabahu".
## sadaka ya kujitolea ### Ufafanuzi Sadaka ya kujitolea ilikuwa aina ya sadaka kwa Mungu ambayo haikuhitajika kwa Sheria ya Musa. Ilikuwa ni uchaguzi binafsi wa mtu kutoa sadaka hii. Kama sadaka ya kujitolea ilikuwa mnyama wa kutolewa sadaka, mnyama aliruhusiwa kuwa na kasoro chache kwa kuwa ilikuwa sadaka ya kujitolea. Waisraeli walikula wanyama waliotolewa sadaka kama sehemu ya sherehe ya karamu. Pale ambapo sadaka ya kujitolea inaweza kutolewa, hii ilikuwa sababu ya kufurahia kwa Israeli kwa kuwa ilionyesha ya kwamba mavuno yalikuwa mazuri ili kwamba watu wawe na chakula kingi. Kitabu cha Ezra kinaelezea aina tofauti ya sadaka ya kujitolea ambayo ililetwa kwa kujenga tena hekalu. Sadaka hii ilijumuisha pesa ya dhahabu na fedha, pamoja na mabakuri na vyombo vingine vilivyoundwa kwa dhahabu na fedha.
## Sadaka ya kuteketezwa ### Ufafanuzi "Sadaka ya kuteketezwa" ilikuwa ni aina ya sadaka iliyotolewa kwa Mungu kwa njia ya moto juu ya madhabahu. Ilitolewa ili kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu. Hii pia ilikuwa ikiitwa "toleo kwa njia ya moto." * Wanyama waliotolewa kwa njia hii kwa kawaida walikuwa kondoo na mbuzi, lakini ng'ombe na ndege pia walikuwa wakitolewa. * Nyama yote ya mnyama iliteketezwa kwa njia hii, isipokuwa ngozi. Ngozi alipewa kuhani. * Mungu aliwaagiza Wayahudi kutoa sadaka ya kuteketezwa mara mbili kwa siku.
## sadaka ya mlo ### Ufafanuzi "Sadaka ya mlo" ilikuwa dhabihu ya Mungu katika umbo la nafaka au mkate uliyo tengenezwa kwa unga. * Neno "mlo" la husu nafaka iliyo sagwa kuwa unga * Unga ulichanganywa na maji au mafuta kufanya mkate. Wakati mwingine mafuta yalisabazwa juu ya mkate. * Aina hii ya sadaka kawaida iliwekwa pamoja na sadaka ya kuteketeza
## sadaka ya nafaka ### Ufafanuzi Sadaka ya nafaka ilikuwa zawadi ya unga wa ngano au shayiri iliyotolewa kwa Mungu, mara nyingi baada ya sadaka ya kuteketeza. Nafaka iliyotumika kwa ajili ya sadaka ya nafaka ilitakiwa kuwa safi kutoka ardhini. Mara nyingi ilipikwa kabla ya kutolewa, lakini muda mwingine iliachwa bila kupikwa. Mafuta na chumvi yaliongezwa kwa unga wa nafaka, lakini hamira au asali haikuruhusiwa. Sehemu ya sadaka ya nafaka ilichomwa na sehemu yake kuliwa na makuhani.
## sadaka ya ushirika ### Ufafanuzi Katika Agano la Kale, "sadaka ya ushirika" ilikuwa aina ya sadaka ambayo ilitolewa kwa sababu tofauti, kama vile kutoa shukrani kwa Mungu na kutimiza kiapo. Sadaka hii ilihitaji sadaka ya mnyama, ambaye alikuwa wa kiume au kike. Hii ilikuwa tofauti na sadaka ya kuteketeza ambayo ilihitaji mnyama wa jinsia ya kiume. Baada ya kutoa sehemu ya sadaka kwa Mungu, mtu aliyeleta sadaka ya ushirika aligawana nyama na makuhani na Waisraeli wengine. Kulikuwa na mlo unaohusishwa na sadaka hii ambayo hujumuisha mkate usiotiwa chachu. Hii mara zingine unaitwa "sadaka ya amani"
## salfa ### Ufafanuzi Salfa ni kitu chenye rangi ya njano kinacho kuwa kimiminiko kinacho waka moto kinapo chomwa. * Salfa ina harufu kali kama mayai viza. * Katika Biblia, salfa ilikuwa yachomwa ni hishara ya hukumu ya Mungu watu wa hasi. * Wakati wa Lutu, Mungu alinyesha moto na salfa kwenye miji miovu ya Sodoma na Gomora.
## sanamu, waabudu sanamu ### Ufafanuzi Sanamu ni kitu ambacho watu hutengeza ili waiabudu. Kitu kinaitwa "kuabudu sanamu" kama kinahusisha kutoa heshima kwa kitu tofauti na Mungu wa kweli. Watu hutengeneza sanamu kuwakilisha miungu ya uongo wanayo abudu. Miungu hii ya uongo haiko hai; hakuna Mungu tofauti na Yahwe. Wakati mwingine mapepo hufanya kazi kupitia sanamu kuifanya ionekane kama vile ina nguvu, licha ya kuwa haina. Sanamu kawaida huundwa kwa vitu vya dhamani kama dhahabu, fedha, shaba, au mbao ya dhamani. "Ufalme unaoabudu sanamu" inamaanisha "ufalme wa watu wanaoabudu sanamu" au "ufalme wa watu wanaoabudu vitu vya duniani." Neno "umbo la waabudu sanamu" ni neno lingine kwa ajili ya "sanamu ya kuchonga" au "sanamu."
## Sauti ### Ufafanuzi Sauti hutumika kumaanisha kuongea au kuwasiliana kitu au jambo. * Mungu hutumia sauti yake japokuwa hana sauti kama ya mwanadamu. * Neno hili laweza kutumika kumaanisha mtu, kwa mfano kwenye sentensi "sauti ilisikika jangwani ikisema, tengenezeni njia ya Bwana." Hii inaweza kutafsiriwa kuwa "Mtu alisikika akisema huko jangwani...." * "Kusikia sauti ya mtu" inaweza kutafsiriwa kama "kusikia mtu akizungumza." * Wakati mwingine "sauti" inaweza kutumika kwa vitu ambavyo haviwezi kuzungumza. Mfano mfalme Dauti katika zaburi anasema "Sauti" ya mbinguni inatangaza matendo makuu ya Mungu. Hii inaweza kutafsiriwa kama "mapambo yao yanaonesha wazi ukuu wa Mungu ulivyo."
## Sehemu za juu ### Ufafanuzi Maneno 'sehemu za juu' yanarejelea madhabahu na maeneo matakatifu yaliyokuwa yakitumika katika kuabudu miungu. Mara zote maeneo haya yalikuwa sehemu za juu kama vile milimani au sehemu za vilima. Wafalme wengi wa Israeli walitenda dhambi kinyume na Mungu kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya miungu katika sehemu hizi za juu. Hii iliwafanya watu kujishughulisha kwa undani katika ibada ya miungu. Wakati mfalme aliyemcha Mungu, alipoanza kutawala juu ya Yuda au Israeli, mara kwa mara waliweza kuonda sehemu hizi za juu na madhabahu ili kuzuia ibada za hizi miungu. Hata hivyo, baadhi ya wafalme wazuri hawakuwa makini sana na hawakuziondoa sehemu hizi za juu, na matokeo yake taifa lote la Israeli liliendelea kuabudu miungu. Mapendekezo ya tafsiri Namna nyingine ya kutafsiri maneno haya twaweza kusema, " maeneo/sehemu iliyoinuliwa kwa ajili ya ibada ya miungu' au 'kilele cha mlima cha ibada ya miungu.' Hakikisha kuwa maneno unayoyatumia yawe na maana ya madhabahu ya miungu na siyo tu maeneo ya juu zilipo madhabahu hizo.
## sela ### Ufafanuzi Neno "sela" ni la Kiebrania lililopo sana katika kitabu cha Zaburi. Lina maana kadhaa. * Lina weza maanisha "kituo na sifa," litakalo wakaribisha wasomaji kufikiria kwa makini kuhusu kile kilicho zungumzwa. * Kwasababu Zaburi nyingi ziliandikwa kama nyimbo, ina fahamika kwamba "sela" yaweza kuwa neno la kimziki kuelekeza muimbaji kueka kituo katika uimbaji wake kuruhusu vyombo vya mziki kucheza au kufariji wasikilizaji kufikiria kuhusu maneno ya nyimbo.
## sensa ### Ufafanuzi Neno "sensa" lilitumika kuhesabu kawaida hesabu ya watu katika taifa au ufalme. * Agano la Kale limetunza idadi kwa mda tofauti tofauti wakati Mungu alipowaagiza kwamba wanaume wa Israeli wahesabiwe, kama vile wakati walipoondoka Misri kwa mara ya kwanza na baadaye tena kabla ya kuingia Kanaani. * Mara nyingi lengo la sensa lilikuwa kwa ajili kujua ni watu wangapi watatakiwa kulipa kodi. * Kwa mfano, mara moja katika Kutoka wanaume wa Waisraeli walihesabiwa ili kwamba kila mmoja angeweza kulipa nusu shekeli kwa ajili ya kutunza hekalu. * Wakati Yesu alipokuwa mtoto, serikali ya Rumi ilifanya sensa kuwahesabu watu wote walioishi katika ufalme wao, kuwataka walipe ushuru.
## shaba ### Ufafanuzi Neno "shaba" linamaanisha aina ya madini yatengenezwayo kwa kuyeyusha kwa pamoja metali, shaba nyekundu na bati. Ina rangi nyeusi inayoelekea njano, nyekundu kiasi. * Shaba huzuia kutu na kipitisho kizuri cha joto * Hapo kale, shaba ilitumika kutengeneza dhana, silaha, madhabahu, vyungu, silaha za askari na vitu vingine. * Vifaa vingi vya kujengea hema la kukutania na hekalu vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba. * Kwa kawaida vinyago vya miungu ya uongo vilitengenezwa kwa madini ya shaba. * Dhana za shaba zilitengenezwa baada ya kuyeyusha madini ya shaba na kisha kuyamimina katika chombo cha kutengenezea. Mchakato huu uliitwa "kutupa."
## shahidi wa uongo, shahidi aliyepotoka, ushuhuda wa uongo, taarifa ya uongo ### Ufafanuzi Misemo ya "shahidi wa uongo" na "shahidi aliyepotoka" ina maana ya mtu anayesema vitu vya uongo juu ya mtu au tukio, mara kwa mara katika mahala rasmi kama mahakamani. "Ushuhuda wa uongo" au "taarifa ya uongo" ni uongo halisia ambao unaambiwa. "kutoa ushahidi wa uongo" ina maana ya kudanganya au kutoa taarifa ya uongo kuhusu jambo. Biblia hutoa habari kadhaa ambapo mashahidi wa uongo waliajiriwa kudanganya kuhusu mtu ili kumfanya mtu huyo kuadhibiwa au kuuwawa. Mapendekezo ya Tafsiri "Kuwa shahidi wa uongo" au "kutoa ushahidi wa uongo" unaweza kutafsiriwa kama "kushuhudia uongo" au "kutoa taarifa ya uongo juu ya mtu" au "kuzungumza uongo dhidi ya mtu" au "uongo". Pale ambapo "shahidi wa uongo" ina maana ya mtu, inaweza kutafsiriwa kama "mtu anayedanganya" au "mtu anayeshuhudia uongo" au "mtu anayesema mambo ambayo siyo ya kweli".
## shahidi, Shahidi ### Ufafanuzi Shahidi ni mtu ambaye amepata uzoefu binafsi wa kitu kilichotokea. Maranyingi shahidi ni mtu anayetoa ushahidi wa jambo analijua kuwa ni kweli. Shahidi pia aneweza kuwa mtu aliyekuwepo pale na kuona kilichotokea. * Kushuhudia kitu ni kuona kikitokea. * Katika kesi shahidi hutoa ushahidi. * Shahidi anatazamiwa kusema ukweli wa kile kilichotokea na sio uongo. * Shahidi atakayesema uongo juu ya kilichotokea ushahidi wake unaitwa "ushahidi wauongo."
## shayiri ### Ufafanuzi Neno "shayiri" limamaanisha aina ya nafaka iliyokuwa ikitumika kutengeneza mkate. * Mche wa shayiri una bua refu lenye suke juu yake ambamo ndani yake punje au nafaka inakua. * Shayiri hustawi wakati wa joto hivyo kwa kawaida inavunwa wakati wa kiangazi. * Wakati shayiri inapopurwa, mbegu ya kuliwa inatenganishwa na makapi. * Nafaka ya shayiri inasagwa na kuwa unga, ambao hatimaye unachanganywa na maji na mafuta ili kutengeneza mkate.
## sheria, kanuni ### Ufafanuzi "Sheria" ni amri ambayo kawaida huandikwa chini na kushurutishwa na mtu aliye madarakani. "Kanuni" ni uongozo kwa ajili ya kufanya maamuzi na tabia. Zote "sheria" na "kanuni" zinaweza kumaanisha amri au imani inayoongoza tabia ya mtu. Maana hii ya "sheria" ni tofauti kwa maana ya kutoka "sheria ya Musa" ambapo inamaanisha amri na maelekezo ambayo Mungu aliwapa Waisraeli. Wakati sheria ya ujumla inapotajwa,"sheria" inaweza kutafsiriwa kama "kanuni" au "amri ya jumla."
## Shimo ### Ufafanuzi Shimo ni sehemu yenye kina kwenda chini iliyochimbwa kwenye ardhi. * Watu hichimba shimo kwa lengo la kuweka mtego wa wanyama au kutafuta maji. * Shimo pia linaweza kutumika kama sehemu ya muda ya kumuweka mfungwa. * Mara nyingine shimo linazungumzwa kama jehanamu. * Neno shimo pia hutumika kama lugha ya pivha kuonesha "shimo la uharibifu" ambayo huelezea kutekwa katika hali mbaya au kujiingiza katika dhambi na matendo ya uharibifu.
## Shimo lisilo na mwisho ### Ufafanuzi "Shimo lisilo na mwisho" ni shimo kubwa, lenye kina kirefu au pengo lisilo na mwisho. * Kwenye Bilblia "shimo lisilo na mwisho" ni sehemu ya adhabu. * Kwa mfano, Yesu alipokuwa anawaamuru pepo wachafu wamtoke yule mtu, walimuomba asiwapeleke kwenye shimo lisilo na mwisho. * Pia "shimo lisilo na mwisho" linaweza kutafsiriwa kama "kuzimu"
## shingo ngumu, kiburi ### Ufafanuzi Neno "shingo ngumu" ni msemo katika Biblia unao tumika kueleza watu wasio mtii Mungu na wanao kataa kutubu. Wana kiburi na hawata tii mamlaka ya Mungu. * Sambamba, neno "kiburi" umaanisha kukataa kubadili nia au matendo ata unapo shawishiwa kufanya hivyo. Watu wenye kiburi hawata sikiliza ushauri mzuri au maonyo watu wengine wanao wapa. * Agano la Kale liliwaeleza Waisraeli kama wenye "shingo ngumu" kwasababu hawakusikiliza jumbe nyingi kutoka kwa manabii wa Mungu waliyo wasii watubu na kumgeukia Yahweh. * Kama shingo ni "ngumu" ina maana haipindi kirahisi.
## Shinikizo la divai ### Ufafanuzi Katika nyakati za Biblia shinikizo la divai ni vyombo vikubwa au sehemu ya wazi ambapo maji ya zabibu yalitengenezwa na kufanywa kuwa divai. * Katika Israeli shinikizo la divai lilikuwa beseni kubwa lililochimbwa kwenye mwamba. Na watu walikanyaga zabibu kwa miguu yao ili wapate maji ya zabibu. * Shinikizo la divai lilikuwa na hatua mbili, zabizu zilizokanyagwa kwenye hatua ya juu ili maji ya zabibu yatiririke chini kwenye hatua ya chini ambapo hukusanywa. * Pia shinikizo la divai limetumika kuonesha picha ya hasira ya Mungu atakayoimimina juu ya watu waovu.
## Shoka ### Ufafanuzi Shoka ni kifaa kinachotumika kukatia miti au mbao. * Mara nyingi shoka huwa na mpini wa mbao. * Kama kwenye jamii yako kuna kifaa kinafanana na shoka ni vizuri kutumia jina la kifaa hicho kutafsiri "shoka." * Namna nyingine ya kutafsiri neno hili ni "kifaa cha kukatia mti au mbao."
## Shtaki, Mashtaka, Mshtaki ### Ufafanuzi Neno "shtaki au Mashtaka" linamaanisha kumlaumu mtu kwa kufanya jambo baya. Mtu anayeshitaki wengine anaitwa "mshtaki." * Mashtaka ya uongo ni pale ambapo makosa dhidi ya mtu fulani si ya kweli, ni kama vile Yesu alipopewa mashtaka ya uongo na viongozi wa Kiyahudi. * Katika agano jipya kwenye kitabu cha Ufunuo, shetani anaitwa "mshtaki."
## shtakio ### Ufafanuzi Neno "shtakiwa" la eleza hali ambayo mtu au kitu kina "jaribiwa." * Shtakio lina weza kuwa mahakamani ambapo ushahidi unatolewa kuthibitisha kama mtu hana hatia au ana kosa. * Neno "shtakio" lina weza maanisha hali ngumu mtu anayo pitia Mungu anapo jaribu imani zao. Maneno mengine ni "jaribu." * Watu wengi katika Biblia walijaribiwa kuona kama wataendelea kumuamini Mungu na kumtii. Walipitia mashtaka yaliyo husisha kupigwa, kufungwa, au kuuawa kwasababu ya imani yao.
## Shujaa, askari ### Ufafanuzi Shujaa na askari ni mtu anayepigana kwenye jeshi. Lakini pia kuna tofauti kadhaa. * Shujaa maranyingi ni neno la jumla kumaanisha mtu aliyebarikiwa na mwenye ujasiri vitani. * Yaweh anazungumzwa kama shujaa. * Askari ni mtu ambaye anatoka kwenye jeshi fulani au anayepigana katika vita fulani. * Askari wa Kirumi huko Yerusalemu walikuwa wakifuata amri na kufanya majukumu yao kama vile kuwalinda wafungwa. Walimlinda Yesu kabla ya kumsulubisha na wengine waliambiwa walilinde kaburi lake.
## si mcha Mungu, siye na Mungu ### Ufafanuzi Meneno "si mcha Mungu" na "siye na Mungu" ina eleza watu waliyo hasi dhidi ya Mungu. Kuishi kwa uovu, pasipo na wazo la Mungu uitwa "siye mcha Mungu" au "pasipo na Mungu." * Maana ya haya maneno yana fanana. Walakini, "siye na Mungu" na "pasipo na Mungu" ya weza eleza hali ambayo watu au mataifa hawamtambui Mungu au utawala wake kwao. * Mungu anatangaza hukumu na ghadhabu watu hasi, kwa wote waliyo mkataa na njia zake.
## si takatifu ### Ufafanuzi Neno "si takatifu" lina maana "kuto kuwa takatifu." Inaelezea mtu au kitu kisicho mtii Mungu. * Hili neno linatumika kueleza mtu asiye muheshimu Mungu kwa kuhasi dhidi yake. * Kitu kinacho itwa "si takatifu" kinaweza elezwa kama kuwa kawaida, upunjufu, chafu. Sio cha Mungu.
## si wa haki, ### Ufafanuzi Neno "si wa haki" ina maana ya wenye dhambi asiye na maadili. * Haya maneno yana maana ya kuishi kwa namna inayo kosea mfundisho ya Mungu na amri. * Watu ambao si wa haki hawana maadili katika fikra zao na matendo. * Wakati mwingine "asiye wa haki" ueleza watu wasiyo mwamini Yesu.
## sifa, mashuhuri ### Ufafanuzi Sifa ni kitendo cha kujulikana na kuwa na sifa. * Mtu mashuhuri ni mtu anayejulikana na anayenyenyekewa. * "Sifa" mara nyngi huwa nzuri na inayojulikana kwa mda mrefu. * Mji wenye sifa mara nyingi hujulikana kwa utajiri wake na mali.
## siku ### Ufafanuzi Neno "siku" kwa kawaida lamaanisha kipindi cha masaa 24 kuanzia kuzama kwa jua. Linatumika pia kitamathari. * Kwa Waisraeli na Wayahudi, siku ilianza wakati wa jua kuzama na kuishia wakati wa kuzama kwa jua siku iliyofuata. * Wakati mwingine neno "siku" latumika kitamathari kurejerea wakati mrefu, kama vile "siku ya Yahwe" au "siku za mwisho." * Baadhi ya lugha hutumia taarifa nyingine kutafasiri matumizi ya tamathari hili au zitatafasiri "siku" bila tamathari. * Tafasiri nyingine za "siku" zaweza kuhusisha, "wakati" au "majira" au "tukio" kutegemea na mazingira.
## sikukuu ### Ufafanuzi Kwa ujumla, sikukuu ni sherehe iliyofanyika na jamii ya watu. Neno kwa ajili ya "sikukuu" katika Agano la Kale lina maana ya "muda ulioteuliwa". Sikukuu zinazosherehekewa na Waisraeli zilikuwa nyakati maalumu zilizoteuliwa au nyakati ambazo Mungu aliwaamuru wao kuzifuata. Katika baadhi ya tafasiri za Kiingereza, neno "sikukuu" linatumika badala ya karamu kwa sababu sherehe zilijumuisha mlo mkubwa wa pamoja. Kulikuwa na karamu kadhaa ambazo Waisraeli walisherehekea kila mwaka: Pasaka Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu Mavuno ya Kwanza Sikukuu ya Wiki (Pentakuki) Sikukuu ya Tarumbeta Sikukuu ya Kulipia Kosa Sikukuu ya Vibanda Kusudi la sikukuu hizi ilikuwa kumshukuru Mungu na kukumbuka mambo ya ajabu aliyofanya kuwaokoa, kuwalinda na kuwapa watu wake.
## Silaha ### Ufafanuzi Silaha ni kifaa anachokitumia askari kupigana akiwa vitani na kujilinda dhidi ya maadui. Pia inaweza kutumika kama lugha ya picha ikimaanisha silaha za kiroho. * Baadhi ya silaha za askari ni kofia ya chuma, ngao, mguu, vifuniko vya miguu na upanga. * Kama lugha ya picha Paulo anafananisha silaha za kimwili na silaha za kiroho ambazo Mungu anawapa wamwaminio ili waweze kupigana vita vya kiroho. - * Silaha za kiroho ambazo Mungu amewapa watu wake ni ukweli, haki, injili ya amani, wokovu na roho mtakatifu.
## simba ### Ufafanuzi Simba ni mnyama mkubwa wa porini anayefanana na paka, mwenye meno yenye nguvu na makucha ya kuulia na kurarua mawindo yake. Simba wana miili yenye nguvu na kasi kubwa ya kushika mawindo yao. Manyoya yao ni mafupi na yana rangi ya mchanganyiko wa kahawa na dhahabu. Simba dume wana manyoya ya shingoni yanayozunguka vichwa vyao. Simba huua wanyama wengine ili kuwala na pia wanaweza kuwa hatari kwa binadamu. Mfalme Daudi alipokuwa mvulana, aliua simba waliojaribu kuvamia kondoo wake aliokuwa akiwachunga. Samsoni pia aliua simba kwa mikono yake.
## sio aminifu, kosa uaminifu ### Ufafanuzi Neno "sio aminifu"la eleza watu wasio fanya kile Mungu alicho amuru wafanye. Hali au ktitendo cha kuwa sio aminifu ni "kuso uaminifu." * Watu wa Israeli waliitwa "sio aminifu" walipo anza abudu sanamu na walipo kosa mtii Mungu kwa namna nyingine. * Katika ndoa, mtu anafanya uasherati ni "sio aminifu" kwa mpenzi wake. * Mungu alitumia neno "kosa aminifu" kueleza tabia hasi ya Israeli. Hawakumtii wala kumheshimu Mungu.
## sio leta faida ### Ufafanuzi Neno "sio leta faida" ina maana ya kuto kuwa na manufaa. * Ina maana ya kuto pata faida ya chochote au kuto msaidia mtu kupata kitu. * Kitu ambacho sio leta faida hakina maana ya kufanya kwasasabu hakitoi manufaa.
## siotahiriwa, kutotahiriwa ### Ufafanuzi Maneno "siotahiriwa" na "kutotahiriwa" ueleza mwanaume ambaye hajatahiriwa kimwili. Haya maneno utumika pia kifumbo. * Misri lilikuwa taifa lililo taka tohara. Hivyo Mungu anapo ongelea Misri kushindwa na wale "siotahiriwa," anasema watu Wamisri wanao wadharau kwa kutotahiriwa. * Biblia ina eleza watu wasio tahiriwa "mioyo siotahiriwa" au ambaye "hajatahiriwa moyoni." Hii ni njia ya fumbo ya kusema kuwa hawa watu sio wa Mungu, na hawa mtii.
## siri, ukweli uliyo fichika ### Ufafanuzi Katika Biblia, neno "siri" la husu kitu kisicho julikana au kigumu kuelewa ambacho Mungu sasa anaelezea. * Katika Agano Jipya linaeleza kuwa Kristo alikuwa siri ambayo haikujulikana awali. * Katika ya vitu maalumu vinavyo julikana kama siri ni kwamba Wayahudi na Wamataifa watakuwa sawa ndani ya Kristo.
## stuli ya mguu ### Ufafanuzi Msemo "stuli ya mguu" una maana ya chombo ambacho mtu huweka miguu yake kwa juu, mara nyingi kupumzisha anapokuwa ameketi. Msemo huu pia una maana za tamathali kwa kujishusha na hadhi ya chini. Watu katika kipindi cha Biblia walichukulia miguu kuwa sehemu yenye heshima ya chini kabisa ya mwili. Kwa hiyo "stuli ya mguu" ilikuwa heshima ya chini zaidi kwa sababu miguu ilipumzishwa juu yake. Mungu anaposema "Nitawafanya adui zangu stuli ya mguu kwa ajili ya miguu yangu" anatamka nguvu, utawala na ushindi juu ya watu ambao wanaasi dhidi yake. Watashushwa na kushindwa hadi hatua ya kujishusha kwa mapenzi ya Mungu. "Kuabudu katika stuli ya mguu ya Mungu" ina maana ya kuinama chini katika kuabudu mbele yake anapokuwa amekaa juu ya kiti chake cha enzi. Hii tena inatoa unyenyekevu na kujishusha kwa Mungu. Daudi anamaanisha hekalu kama "stuli ya mguu" ya Mungu. Hii inaweza kumaanisha mamlaka yake ya hakika juu ya watu wake. Hii inaweza pia kumpiga picha Mungu Mfalme juu ya kiti chake cha enzi, na miguu yake ikupumzika juu ya stuli ya mguu, ambayo inawakilisha kila kilcho chini yake.
## Suria ### Ufafanuzi Suria ni mwanamke ambaye ni mke wa pili wa mwanaume ambaye tayari ana mke. Suria mara nyingi sio mke halali wa mwanaume huyo. * Katika agano la kale masuria walikuwa wanawake watumwa. * Suria anaweza kupatikana kwa kununuliwa, kwa kushinda vita au kwa njia ya kulipa deni. * Kwa mfalme kuwa na masuria wengi ilikuwa alama ya mamlaka. * Katika agano jipya inafundisha kuwa kuwa na masuria ni kinyume na mapenzi ya Mungu.
## taa ### Ufafanuzi Neno "taa" kawaida inamaanisha kitu kinachotoa mwanga. Taa zilizotumika nyakati za Biblia kawaida zilikuwa taa za mafuta. Aina ya taa iliyotumika katika Biblia ni chombo na sehemu ya kuwekea mafuta, yanayotoa mwanga inapowashwa. Kawaida taa za mafuta zilitengenezwa kwa chombo cha kawaida cha udongo kilichojaa mafuta ya mzeituni, na utambi ukiwekwa kwenye mafuta ili uwake. Kwa baadhi ya taa, chombo lilikuwa na umbo la yai, na sehemu moja ikiwa imefinywa karibu kuushikilia utambi. Taa ya mafuta iliweza kubebwa au kuwekwa katika kinara ili mwanga wake ujaze chumba au nyumba. Katika maandiko, taa zinatumika kwa njia kadhaa kimithali kama ishara ya mwanaga na uhai.
## taabu, mataabiko, taabika ### Ufafanuzi Neno "taabu" ina eleza hali ya maisha ambayo ni ngumu na kusumbua. "Kutaabika" ina maanisha kusikia vibaya au kusongwa na mawazo ya jambo. * Taabu zina weka kuwa kimwili, kihisia, au vitu vya kiroho vinavyo muumiza mtu. * Katika Biblia, mara nyingi taabu ni kipindi cha majaribu Mungu anayo tumia kusaidia waamini kukua na kukomaa kiimani. * Agano la Kale lina tumia "taabu" kama hukumu iliyo kuja kwa makundi ya watu waliyo kuwa waasi na wamemkataa Mungu. * Tendo "kutaabisha" mtu lina maana ya "kusumbua" mtu au kusababisha mawazo.
## tafakari ### Ufafanuzi Neno "tafakari" lina maana ya kutumia muda kufiria jambo kwa umakini na undani. * Hili neno mara nyingi lina tumika kwenye Biblia kuhusu kuwaza Mungu na mafundisho. * Zaburi 1 inasema mtu anaye tafakari sheria ya Bwana "usiku na mchana" atabarikiwa sana.
## tafsiri, ufafanuzi ### Ufafanuzi Neno "tafsiri" na "ufafanuzi" inamaanisha kuelewa na kufafanua maana ya jambo ambalo haloki wazi. Mara nyingi Biblia inatumia misemo hii katika kueleza maana za ndoto na maono. Wakati mfalme wa Babeli alipopata ndoto za kuchanganya, Mungu alimsaidia Danieli kuzitafsiri na kufafanua maana zake. "Tafsiri" ya ndoto ni "ufafanuzi" wa maana ya ndoto. Katika Agano la Kale, wakati mwingine Mungu hutumia ndoto kuwafunulia watu kitakachotokea siku za usoni. Kwa hiyo ufafanuzi wa hizo ndoto zilikuwa ni utabiri. Neno "tafsiri" inaweza pia kumaanisha kuelewa maana ya vitu vingine, kama kuelewa hali ya hewa itakuaje kutokana na ubaridi au joto lililopo, upepo uliopo, na anga ilivyo. Njia za kutafsiri neno "tafsiri" ni pamoja na , "kuelewa maana ya" au "kufafanua" au "kutoa maana ya." Usemi "tafsiri" inaweza kutafsiriwa kama "maelezo" au "maana."
## tafuta ### Ufafanuzi Neno "tafuta" la maanisha kutafuta kitu au mtu. Inaweza kuwa na maana ya "jaribu kwa bidii" au "tia juhudi" kufanya kitu. * "tafuta" au "kuangalia" fursa ina maana ya "kujaribu kutafuta muda" kufanya kitu muhimu * "kumtafuta Yahweh" ina maana ya "kutumia muda na uweza kupata kumjua Yahweh na kujifunza kumtii." * "kutafuta ulinzi" ina maana ya "kujaribu kumpata mtu au sehemu itakayo kulinda na hatari." * "kutafuta haki" ina maana ya "kufanya juhudi kuona kwamba watu wana tendewa sawa." * "kutafuta ukweli" ina maana ya "kufanya juhudi kujua nini ni ukweli." * "kutafuta upendeleo" ina maana ya "kujaribu kupata upendeleo" au "kufanya vitu kumsababisha mtu akusaidie."
## tai ### Ufafanuzi Tai ni ndege mbua mkubwa sana, mwenye nguvu ambaye hula wanyama wadogo kama vile samaki, panya, nyoka na kuku. Biblia hulinganisha kasi na nguvu ya jeshi kwa jinsi tai hupaa chini kukamata nyama yake kwa kasi na ghafla. Isaya anasema ya kwamba wale wanaomtumaini Bwana watapaa juu kama tai afanyavyo. Hii ni lugha ya tamathali inayotumika kuelezea uhuru na nguvu ambao unakuja kutokana na kumuamini na kumtii Mungu. Katika kitabu cha Danieli, urefu wa nywele za Mfalme Nebukadreza zililinganishwa na urefu wa manyoya ya tai, ambayo yanaweza kuwa zaidi ya sentimita 50.
## Taifa ### Ufafanuzi Taifa ni kundi kubwa la watu wanao tawaliwa na serikali. Watu wa taifa mara nyingi wa mababu sawa na ni wajamii moja. * Neno "taifa" mara nyingi lina maana ya utamaduni ulifahamika vizuri na kuwa na mipaka ya eneo. * Katika Biblia, "taifa" la weza kuwa nchi (kama Misri au Ethiopia) lakini wakatik mwingine ni kwa ujumla na uhusu kundi la watu, sana inapotumika katika wingi. * Taifa katika Biblia ni Waisraeli, Wafilisti, Waasyria, Wababiloni, Wakanani, Warumi, Wayunani. * Wakati mwingine neno "taifa" linatumika kifumbo kutaja mababu wa kundi la watu, kama Rebeka alivyo ambiwa na Mungu kuwa mtoto wake tumboni alikuwa ni "mataifa" watakao pigana wenywe.
## Taji, kuvalisha taji ### Ufafanuzi Taji ni pambo la mviringo linalovaliwa kichwani kwa kiongozi wa juu kama mfalme na malkia. Kuvika taji ni kuweka taji juu ya kichwa cha mtu. Au yaweza kuwa na maana ya "kuheshimu." * Mataji hutengenezwa kwa dhahabu au fedha pia hupambwa kwa zumaridi au rubi. * Taji ni alama ya nguvu na utajiri wa mfalme. * Taji lililotengenezwa kwa miba ambalo askari wa Rumi walimvalisha Yesu kichwani lilikuwa kwa ajili ya kumdhihaki. * Zamani za kale mshindi wa mashindano ya riadha alizawadiwa taji iliyotengenezwa kwa majani ya mzeituni. Mtume Paulo aliitaja taji hii katika barua yake ya pili kwa Timotheo. * Kuvisha taji pia inaweza kuwa na maana ya kumuheshimu mtu. Tunamuheshimu Mungu kwa kumtii yeye na kumsifu yeye. Hii ni kama kuweka taji kichwa ni mwake na kumtambua kama mfalme. * Taji pia inaweza kuwa na maana ya "zawadi" au "heshima" au "ujira."
## takatifu ### Ufafanuzi Neno "takatifu" la elezea kitu kinacho husu kumuabudu Mungu au wapagani wanao abudu miungu ya uongo. * Katika Agano la Kale, mara nyingi neno "takatifu" la tumika kueleza nguzo za mawe na vitu vingine vinavyo tumika katika kuabudu miungu ya uongo. Hii yaweza tafsiriwa kama kama "kidini" * "nyimbo Takatifu" au "miziki takatifu" ya husu mziki unao imbwa au kuchezwa kwa utukufu wa Mungu. Hii yaweza tafsiriwa kama "mziki wa kumuabudu Yaheweh" au "nyimbo zinazo muabudu Yahweh." * Msemo "majukumu takatifu" ya husu "majukumu ya kidini" au "mila" ambazo kuhani ana tenda kuongoza watu katika kumuabudu Mungu. Yaweza pia husu mila zinazo tendwa na kuhani mpagani kumuabudu mungu wa uongo.
## takdiri, majaliwa, jaliwa ### Ufafanuzi Msemo wa "takdiri" una maana ya kile kitakachotokea kwa watu hapo baadaye. Kama mtu ana "takdiri" ya jambo, ina maana ya kwamba kile mtu huyo atafanya hapo baadaye kimepangwa na Mungu. Mungu anapopanga taifa kupatwa na ghadhabu, hii ina maana ya kwamba ameamua au kuchagua kuwaadhibu taifa hilo kwa sababu ya dhambi yao. Yuda alikuwa na "takdiri" ya kuangamizwa, ina maana ya kwamba Mungu aliamua ya kwamba Yuda angeangamizwa kwa sababu ya kuasi kwake. Kila mtu ana takdiri ya mwisho, ya milele, moja wapo mbinguni au jehanamu. Pale mwandishi wa Mhubiri anaposema ya kwamba kila mtu takdiri yake inafanana, anamaanisha ya kwamba kila mtu hatma yake atakufa. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "kupangwa kwa ghadhabu" unaweza pia kutafsiriwa kama "kuamua ya kwamba utaadhibiwa" au "kuamuliwa ya kwamba utapitia ghadhabu yangu". Msemo wa kitamathali, "wana takdiri ya upanga" inaweza kutafsiriwa kama, "Mungu ameamua ya kwamba wataangamizwa na adui zake ambao watawaua kwa upanga" au "Mungu ameamua ya kwamba adui wao watawaua kwa upanga". Msemo, "una takdiri ya" inaweza kutafsiriwa kutumia msemo kama, "Mungu ameamua ya kwamba utakuwa" Kutegemea na muktadha, "takdiri" inaweza kutafsiriwa kama "hitimisho la mwisho" au "kitakachotokea mwishoni" au "kile alichoamua Mungu kitatokea"
## Talaka ### Ufafanuzi Talaka ni tendo la kisheria la kusitisha ndoa. Msemo "kutengana" ina maana ya kutengana rasmi na kihalali kutoka kwa mwenzi wa mtu ili kusitisha ndoa. Maana halisi ya neno "kutengana" ni "kufukuza" au "kuachana rasmi kutoka kwa". Lugha zingine zinaweza kuwa na misemo ya kufanana yenye maana ya talaka. "cheti cha talaka" kinaweza kutafsiriwa kama, "karatasi inayosema ya kwamba ndoa imefika mwisho".
## tamaa ### Ufafanuzi Tamaa ni hamu kubwa sana, mara nyingi katika mazingira ya kutaka kitu kiouvu au kisicho na maadili mema. Katika Biblia, "tamaa" mara nyingi inamaanisha hamu ya kimwili kwa mtu mwingine tofauti na mme au mke wake. Wakati mwingine neno hili linatumika kimafumbo kumaanisha kuabudu sanamu. Kulingana na mazingira, "tamaa" inaweza kutafsiriwa kama "hamu mbaya" au "hamu kali" au "hamu mbaya ya kimwili" au "hamu kubwa isiyo ya kimaadili mema" au "kuwa na hamu kubwa ya kutenda dhambi." Msemo "kutamani kitu" inaweza pia kutafsiriwa kama "kuwa na hamu vibaya" au " kuwaza kinyume na maadili kuhusu" au "kuwa na hamu mbaya kimaadili."
## Tambua ### Ufafanuzi Neno "tambua" lina maana ya kutambua kwa usahihi kitu fulani au mtu. * Kumtambua Mungu pia inajumuisha kutenda kwa namna ambayo itaonesha kuwa anayoyasema ni kweli. * Watu wanaomtambua Mungu huonesha kwa kumtii Mungu ambayo huleta utukufu kwa jina lake. * Kutambua kitu ina maana ya kuamini kuwa ni kweli, kwa maneno na matendo yanayothibitisha hayo.
## tambua, tambuzi ### Ufafanuzi Msemo "tambua" una maana ya kuweza kuelewa jambo, haswa kuweza kujua kama jambo ni sahihi au baya. Msemo wa "tambuzi" una maana ya kuelewa na kuamua kwa hekima kuhusu jambo fulani. Ina maana kuwa na hekima na maamuzi mazuri. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, "tambua" inaweza pia kutafsiriwa kama "kuelewa" au "kujua tofauti kati ya" au "kutofautisha mema na mabaya" au "kuhukumu sahihi kuhusu" au "kuelewa mema kwa mabaya". "Tambuzi" inaweza kutafsiriwa kama, "uelewa" au "uwezo wa kuchambua mema na mabaya"
## tamka, tamko ### Ufafanuzi Msemo wa "tamka" au "tamko" una maana ya kutoa kauli maalumu kwa umma, mara nyingi kusisitiza jambo. "Tamko" halisisitizi umuhimu tu wa kile kinachotamkwa, lakini inavuta nadhari kwa yule anayetoa tamko hilo. Kwa mfano, katika Agano la Kale, ujumbe kutoka kwa Mungu mara nyingi hutanguliwa na "tamko la Yahwe" au "hivi ndivyo Yahwe asemavyo". Msemo huu unasisitiza ya kwamba ni Yahwe mwenyewe anayesema hivi. Ukweli ya kwamba ujumbe unatoka kwa Yahwe unaonyesha jinsi ujumbe ulivyo na umuhimu. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, "tamka" inaweza pia kutafsiriwa kama "tangaza" au "eneza wazi" au "sema kwa nguvu" au "tamka kwa kishindo". Msemo "tamko" unaweza kutafsiriwa kama, "kauli" au "tangazo". Msemo, "hili ni tamko la Yahwe" linaweza kutafsiriwa kama, "hivi ndivyo Yahwe anavyotamka" au "hivi ndivyo Yahwe anavyosema".
## tanuu ### Ufafanuzi Tanuu ilikuwa joko kubwa sana liyotumika kuchemsha vyombo katika halijoto la juu. Katika kipindi cha nyuma, tanuu nyingi zilitumika kuyeyusha vyuma kutengeneza vyombo kama vile vyungu vya kupikia, mapambo ya vito, silaha, na sanamu. Tanuu zilitumika pia kutengeneza vyungu vya udongo. Mara nyingine tanuu hujulikana kitamathali kufafanua ya kwamba kitu ni cha moto sana.
## Tapanya, nyika ### Ufafanuzi Kutapanya kitu ni kukitupa au kutokukitumia kwa hekima. Nchi ambayo ni nyika ni nchi au mji ulioharibiwa ili kitu chochote kisiishi ndani yake tena. * "Kuchakaa" inamaana ya kuwa na ugonjwa au kuharibiwa. Mtu aliyechakaa maranyingi anakuwa mwembamba kutokana na ugonjwa au kukosa chakula. * Neno lingine linalomaanisha nyika nin jangwa. Lakini nyika pia inamaanisha kuwa watu waliishi hapo na nchi ilikuwa na miti na mimea inayotoa chakula.
## tarumbeta ### Ufafanuzi Neno "tarumbeta" la eleza chombo cha kutoa mziki au kuita watu pamoka kwa mkutano au kikao. * Tarumbeta lilitumika na chuma, kombe, au pembe la mnyama. * Matarumbeta yalipigwa kuita watu kuja pamoja kwa pambano, na kukusanyika kwa Waisraeli. * Kitabu cha Ufunuo kinaeleza tukio la mwisho wa nyakati ambapo malaika walipenga matarumbeta kuhashiria kumwagwa kwa ghadhabu ya Mungu duniani.
## tawanya, mtawanyiko ### Ufafanuzi Msemo "tawanya" na "mtawanyiko" ina maana ya kutawanya watu au vitu katika pande nyingi tofauti. Katika Agano la Kale, Mungu anazungumza kuhusu "kutawanya" watu, kusababisha wao wajitenge na kuishi katika maeneo tofauti kati yao. Alifanya hivi kuwaadhibu kwa dhambi yao. Huenda kutawanyika ingeweza kuwasaidia kutubu na kuanza kumwabudu Mungu tena. Msemo "mtawanyiko" unatumika katika Agano Jipya kumaanisha Wakristo ambao walitakiwa kuacha nyumba zao na kuhamia katika mahali tofauti nyingi kutoroka mateso. Msemo "tawanyiko" unaweza kutafsiriwa kama "waumini katika maeneo mengi tofauti" au "watu waliohama kuishi katika mataifa tofauti". Msemo "tawanya" unaweza kutafsiriwa kama "kutuma mbali katika maeneo mengi tofauti" au "kusambaza ng'ambo" au "kusababisha kuhamisha mbali kuishi katika nchi tofauti"
## teketeza, uharibifu ### Ufafanuzi Msemo wa "kuteketezwa" au "uharibifu" ina maana ya kufanya mali ya mtu au ardhi kuharibika au kuangamizwa. Pia mara kwa mara hujumuisha kuangamiza au kukamata watu waishio katika ardhi hiyo. Hii ina maana ya maangamizi kamili na makali sana. Kwa mfano, mji wa Sodoma uliteketezwa na Mungu kama adhabu kwa dhambi za watu walioishi pale. Msemo "uharibifu" unaweza kujumuisha kusababisha majonzi ya hisia yatokanayo na hiyo adhabu au uharibifu. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "teketeza" unaweza kutafsiriwa kama "kuangamiza kabisa" au "kuharibu kabisa". Kulingana na muktadha, "uharibifu" inaweza kutafsiriwa kama "maangamizi kamili" au "uharibifu kamili" au "majonzi ya juu sana" au "balaa".
## Tembea ### Ufafanuzi Neno "tembea" mara nyingi hutumika ikiwa na maana ya "ishi." * "Enoko alitembea na Mungu" inamaanisha kuwa "Enoko aliishi kwa kuwa na mahusiano ya ukaribu sana na Mungu." * "Kutembea kwa roho" inamaanisha kuongozwa na Roho Mtakatifu ili kufanya mambo yanayomtukuza na kumpa heshima Mungu. * Mungu anaposema atatembea kati ya watu wake inamaana kuwa anaishi kati yao au anahusiana nao kwa karibu. * "Kutembea kinyume" inamaanisha kuwa kuishi au kufanya kinyume na mtu au kitu fulani.
## teseka, kuteseka ### Ufafanuzi Maneno "teseka" na "kuteseka" yanaeleza kupitia kitu kisicho pendeza, kama ugonjwa, maumivu, au magumu. * Watu wanapo teswa au kuumwa, wana teseka. * Wakati mwingine watu wana teseka kwasababu ya vitu vibaya walivyo fanya; wakati mwingine kwasababu ya dhambi na magonjwa duniani. * Kuteseka kunaweza kuwa kimwili, kama maumivi au ugonjwa. Inaweza pia kuwa hisia kama hofu, kusononeka, au upweke.
## tetemeka ### Ufafanuzi Neno "tetemeka" lina maana ya kutikisika kwa hofu au msongamano wa mawazo. * Hili utumika kifumbo kumaanisha "kuogopa sana" * Wakati mwingine neno "tetemeka" la eleza ardhi kutikisika kwasababu ya kelele kubwa. * Biblia ina sema katika uwepo wa Bwana dunia itatetemeka. Hii inaweza maanisha kwamba watu wa dunia watatikisika kwa hofu ya Mungu au dunia yenyewe itatikisika.
## Thamani ### Ufafanuzi "Thamani" ni watu au kitu kinachoonekana kuwa kina ubora. * Neno "mawe ya thamani" ni miamba na madini yenye dangi na yenye thamani inayofanya yawe mazuri na yenye kufaa. * Mfano wa mawe ya thamani ni kama dhahabu, rubi na zamaradi. * Dhahabu na fedha huitwa madini ya thamani. * Bwana alisema kuwa watu wake ni wa thamani kwenye macho yake (Isaya 43:4) * Petro aliandika kuwa Mataifa ni wa thamani mbele za Macho ya Mungu (1Petro 3:4)
## theluji ### Ufafanuzi Neno "theluji" ya husu chembe nyeupe za maji yaliyo ganda yanayo anguka kutoka mawinguni sehemu ambazo hali ya hewa ni ya baridi. * Theluji ya anguka sehemu ya muinuko Israeli, lakini inaweza isibaki muda wote kwenye ardhi kabla ya kuyayuka. Vilele vya mlima mara nyingi ubakiwa na theluji kwa muda mrefu. Mfano mmoja wa Biblia ni ule wa Mlima Lebanoni. * Kitu ambacho ni cheupe mara nyingi kinalinganishwa na rangi ya theluji, kama vazi au nywele za Yesu zinavyo elezewa "nyeupe kama theluji." * Weupe wa theluji pia una ashiria kuwa safi.
## thibitisha, uthibitisho ### Ufafanuzi Thibitisha au uthibitisho ni kuwa na hakika kuwa jambo fulani ni la kweli au kuaminika. * Katika agano la kale Mungu anawaambia watu wake kuwa atalithibitisha agano lake kwao. Hii inamaana kuwa anasema kuwa atatunza ahadi aliyoiweka katika lile agano. * Mfalme anathibitishwa hii inamaana ya kuwa maamuzi ya yeye kuwa mfalme yamekubalika na watu. * Kuthibitisha alichokiandika mtu inamaana ya kuwa kilichoandikwa ni kweli. * Uthibitisho wa agano maana yake ni kuwafundisha watu kuhusu habari njema za Yesu kwa namna ambavyo inaonesha kuwa ni kweli. * Kutoa kiapo kama uthibitisho inamanisha kuapa kuwa jambo fulani ni la kweli au la kuaminika
## tia moyo, kutia moyo ### Ufafanuzi Msemo "tia moyo" na "kutia moyo" ina maana ya kusema na kufanya mambo kusababisha mtu kuwa na faraja, matumaini, kujiamini na ujasiri. Msemo wa kufanana ni "shawishi", ambao una maana ya kumsihi mtu kukataa tendo ambalo ni baya na badala yake kufanya mambo ambayo ni mazuri na sahihi. Mtume Paulo na waandishi wengine wa Agano Jipya walifundisha Wakristo wajitie moyo wao kwa wao kupendana na kutumikiana. Mapendekezo ya Tafsiri Kulingana na muktadha, njia za kutafsiri "tia moyo" zinaweza kujumuisha, "kusihi" au "kufariji" au "kusema vitu vya upole" au "kusaidia na kuimarisha". Msemo, "toa maneno ya faraja" una maana ya "kusema mambo ambayo yatasababisha watu wengine kujisikia kupendwa, kukubalika, na kuwezeshwa".
## tia utumwani, katika kifungo ### Ufafanuzi "Kutia utumwani" mtu ina maana ya kumlazimisha mtu huyo kumtumikia bwana au nchi tawala. "Kutiwa utumwani" au "kuwa kifungoni" ina maana ya kuwa chini ya utawala wa kitu au mtu. Mtu ambaye yupo katika utumwa au kifungoni anatakiwa kutumikia wengine bila malipo; hayupo huru kufanya anavyotaka. "kutia utumwani" pia ina maana ya kuchukua uhuru wa mtu. Neno lingine la "kifungoni" ni "utumwa". Kwa njia ya tamathali, wanadamu ni "wafungwa" wa dhambi hadi Yesu awaweke huru kutoka katika utwala na nguvu yake. Mtu anapompokea maisha mapya ndani ya Yesu, anasitisha kuwa mtumwa wa dhambi na anakuwa mtumwa wa utakatifu. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "tia utumwani mwa" au "kuwa kifungoni mwa" unaweza kutafsiriwa kama "kulazimishwa kuwa mtumwa wa" au "kulazimishwa kumtumikia" au "kuwa chini ya utawala wa".
## tii, mtiifu, utiifu ### Ufafanuzi Neno "tii" lina maana ya kufanya unachopaswa au kuamriwa. Neno "mtiifu" la eleza tabia ya mtu anaye tii. Wakati mwengine amri ni kuhusu kutofanya kitu, "usiibe" * Mara kwa mara "tii" lina tumika katika muktadha wa kutii amri au sheria ya mtu mwenye mamlaka. * Kwa mfano, watu wanatii sheria zinazo tengenezwa na viongozi wa nchi, ufalme, au taasisi ingine. * Watoto wanatii wazazi wao, watumwa wanatii bwana zao, watu na mtii Mungu, na rahia wanatii sheria ya nchi. * Wakati mtu katika mamlaka anapo amuru watu wasifanye kitu, wanatii kwa kutofanya. * Neno "utiifu" la weza tafsiriwa kama, "kufanya kilicho amriwa" au "kufuata utaratibu" * Neno "utiifu" la weza tafsiriwa kama, "kufanya kilicho amriwa" au "kufuata utaratibu"
## totii, mkaidi, kutotii ### Ufafanuzi Msemo wa "totii" una maana ya kutotii kile mtu mwenye mamlaka ameamuru au kuagiza. Mtu anayefanya hivi anakuwa "mkaidi". Mtu anayefanya jambo aliloambiwa kutofanya anakuwa hatii. Kutotii pia ina maana ya kukataa kufanya jambo ambalo liliamriwa. Msemo "mkaidi" pia hutumika kuelezea silika ya mtu ambaye kimazoea hatii au huasi. Ina maana ya kwamba ni wenye dhambi au waovu. Msemo "ukaidi" una maana "tendo la kutotii" au "tabia ambayo ni kinyume na kile Mungu anataka". "Mtu kaidi" anaweza kutafsiriwa kwa "watu wanaondelea kutii" au "watu ambao hawafanyi kile Mungu anaamuru"
## tukuza ### Ufafanuzi Msemo "tukuza" ina maana ya kuonyesha au kunena jinsi gani kitu au mtu ni mkubwa au muhimu. Ina maana ya "kutoa utukufu". Watu wanaweza kumtukuza Mungu kwa kunena juu ya mambo mazuri aliyoyafanya. Wanaweza kumtukuza Mungu kwa kuishi kwa njia ambayo inampa heshima na kuonyesha jinsi alivyo mkuu na wa ajabu. Biblia inaposema ya kwamba Mungu hujitukuza mwenyewe, ina maana anajifunua kwa watu ukubwa wake wa ajabu, mara kwa mara kupitia miujiza. Mungu Baba atamtukuza Mungu Mwana kwa kudhihirisha kwa watu ukamilifu wa Mwana, ufaharu na ukuu. Kila mtu anayemwamini Kristo atatukuzwa na yeye. Wanapofufuliwa katika uzima, watabadilishwa kuakisi utukufu wake na kuonyesha neema yake kwa uumbaji wote. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "kutoa utukufu kwa" au "kuleta utukufu kwa" au "kusababisha kuonekana kubwa". Msemo "mtukuza Mungu" unaweza kutafsiriwa kama "kumsifu Mungu" au "kuzungumza juu ya ukuu wa Mungu" au "kuonyesha jinsi Mungu alivyo mkuu" au "kumheshimu Mungu"
## tuma, kutuma nje, kutumwa ### Ufafanuzi "Kutuma" ni kusababisha mtu au kitu kwenda sehemu. "Kutuma nje" mtu ni kumwambia huyu mtu kwenda na kufanya japo au shughuli. * Mara nyingi mtu anaye "tumwa nje" amechaguliwa kufanya kazi maalumu. * Maneno kama "tuma mvua" au "tuma janga" ina maana "kusababisha ...kuja." Aina hii ya msemo utumika kumuelezea Mungu akisababisha vitu kutokea. * Neno "tuma" pia la tumika katika msemo "tuma neno" au "tuma ujumbe" inayo maanisha kumpa mtu ujumbe ampe mtu mwingine. * "Kumtuma" mtu "na" inaweza maanisha "kumpa" hicho kitu "kwa" mtu mwingine. * Yesu mara nyingi utumia maneno "yeye aliye nituma" kumuelezea Mungu Baba aliye "mtu" duniani kuokoa watu.
## Tumbo la uzazi ### Ufafanuzi Tumbo la uzazi ni mahali ambapo mtoto hukua ndani ya mama yake. * Hili ni neno la zamani lililotumika kupunguza ukali wa neno. * Neno la kisasa ni kizazi. * Lunga nyingine hutumia neno tumbo.
## tunda, kuzaa ### Ufafanuzi Msemo "tunda" lina maana ya sehemu ya mmea ambao inaweza kuliwa. Kitu ambacho "kinazaa" kina matunda mengi. Misemo hii pia hutumika kitamathali katika Biblia. Biblia mara kwa mara hutumia "tunda" kumaanisha matendo na mawazo ya mtu. Kama vile tunda juu ya mti linavyoonyesha ni aina gani ya mti, vile vile maneno na matendo ya mtu hudhihirisha silika yake ikoje. Mtu anaweza kuzaa matunda ya kiroho mazuri au mabaya, lakini msemo "kuzaa" mara kwa mara una maana chanya ya kuzaa matunda mema. Msemo "kuzaa" pia hutumika kitamathali kumaanisha "mafanikio". Hii mara kwa mara humaanisha kuwa na watoto na uzao mwingi, pamoja na kuwa na chakula kingi na utajiri mwingine. Kwa ujumla, msemo "tunda la" una maana ya kitu chochote ambacho hutoka kwa au ambacho huzalishwa na kitu kingine. Kwa mfano, "tunda la hekima" lina maana ya mambo mazuri ambayo hutokana na kuwa na hekima. Msemo "tunda la roho" una maana kijumla ya kila kitu ambacho nchi huzaa kwa ajili ya watu kula. Hii inajumlisha sio matunda pekee kama mizabibu au tende, lakini pia mboga, karanga na nafaka. Msemo wa tamathali "tunda la Roho" una maana ya sifa nzuri ambazo Roho Mtakatifu hutoa katika maisha ya watu ambao humtii yeye. Msemo "tunda la tumbo" una maana ya "kile ambacho tumbo huzaa" yaani, watotot.
## Tunga mimba ### Ufafanuzi Kutunga mimba ni kitendo cha kuwa na mimba ya mtoto. Pia inaweza kutumika kwa wanyama wanapokuwa na mimba. * "Kupata mtoto" inaweza kutafsiriwa kama "kupata mimba." * "kutunga mimba" inaweza kutafsiriwa kama "mwanzo wa mimba" au "wakati wa kuwa na mimba." * Neno hili pia laweza kuwa na maana ya kuumba kitu au kufikiria kitu kama wazo au mipango. * Pia neno hili limetumika kama "dhambi ikitunga mimba" ikiwa na maana ya "dhambi inapofikiriwa" au "mwanzo wa dhambi" au "dhambi inapoanza."
## ua, mahakama ### Ufafanuzi "Ua" ni eneo ambalo liko wazi juu na limezungukwa na ukuta. Neno "mahakama" linamaanisha sehemu ambayo hakimu huamua mambo ya sheria na jinai. * Maskani ilizungukwa na ua ambalo lilikuwa na ukuta uliotengenezwa kwa mapazia mazito. * Jengo la hekalu lilikuwa na ua tatu za ndani moja kwa ajili ya kuhani, nyingine ya wanaume wa Kiyahudi, nyingine ya wanawake wa Kiyahudi. * Ua za ndani zilitenganishwa kwa ukuta wa mawe uliowatenganisha na ua wa nje ambapo Mataifa waliruhusiwa kuabudu. * Ua wa nyumba ilikuwa sehemu ya wazi katikati ya nyumba. * Mahakama ya mfalme ni sehemu ambayo ilikuwa ikulu ambapo Mfalme aliitumia kutoa hukumu.
## uadilifu ### Ufafanuzi Neno "uadilifu" inamaanisha kuwa mwaminifu, na mwenye msimamo mkali wa maadili na tabia. Kuwa na uadilifu ni kuchagua kutenda kilicho kweli na sawa hata wakati hakuna mwingine anayetazama. Baadhi ya watu katika Biblia, kama Yusufu na Danieli, walionesha uadilifu walipokataa kufanya uovu na kuchagua kumtii Mungu. Kitabu cha Mithali kinasema kuwa ni bora kuwa maskini na kuwa na uadilifu kuliko kuwa tajiri na mfisadi na muongo.
## uaguzi, mwaguzi, kutabiri, mtabiri ### Ufafanuzi Msemo "uaguzi" na "kutabiri" ina maana ya tendo la kujaribu kupata taarifa kutoka kwa roho katika ulimwengu wa rohoni. Mtu anayefanya hivi mara nyingine hujulikana kama "mwaguzi" au "mtabiri". Katika kipindi cha Agano la Kale, Mungu aliamuru Waisraeli kutofanya uaguzi au utabiri. Mungu hakuruhusu watu wake kutafuta taarifa kutoka kwake kutumia Urimu na Thumimu, ambayo yalikuwa mawe aliyoyatenga kutumika na makuhani wa juu kwa kusudi hilo. Lakini hakuruhusu watu wake kutafuta taarifa kupitia msaada wa roho chafu. Waaguzi wa kipagani walitumia taratibu tofauti za kujaribu kutafuta taarifa kutoka kwenye ulimwengu wa roho. Mara zingine walichunguza sehemu za ndani za mnyama aliyekufa au kurusha mifupa ya wanyama juu ya ardhi, wakitafuta violezo ambavyo vingeweza fasiri ujumbe kutoka kwa miungu yao ya uongo. Katika Agano Jipya, Yesu na mitume pia walikataa uaguzi, uchawi, ulozi na mazingaombwe. Matendo haya yote yalihusisha matumizi ya nguvu kutoka roho chafu na yanalaaniwa na Mungu.
## Ubaguzi ### Ufafanuzi "Kuonesha ubaguzi" ni kitendo cha kuamua kuwaonesha watu umuhimu zaidi ya watu wengine. * Hii ni sawa na kuonesha upendeleo ambayo ni kuwafanyia watu wengine vizuri zaidi ya watu wengine. * Ubaguzi au Upendeleo unaoneshwa kwa watu kwa sababu wana mali au wanajulikana sana kuliko watu wengine. * Biblia inawaelekeza watu wake wasioneshe ubaguzi wala upendeleo lwa watu matajiri au wenye cheo. * Barua kwa Warumi Paulo anafundisha kuwa Mungu atawahukumu watu bila ubaguzi. * Kitabu cha Yakobo kinatufundisha kuwa ni makosa kuwapendelea watu kwa sababu ni matajiri.
## ubani ### Ufafanuzi Ubani ni harufu nzuri ya kiungo kutoka kwenye mti wa utomvu. Inatumika kutengeneza manukato na udi. Katika kipindi cha Biblia, ubani ilikuwa kiungo muhimu kilichotumika kuandaa maiti kwa maziko. Kiungo hiki kilikuwa cha thamani kwa sifa zake za uponyaji na kutuliza. Wanaume wasomi walipokuja kutoka nchi ya mashariki kumwona mtoto Yesu Bethlehemu, ubani ilikuwa moja ya zawadi tatu walizoleta kwake.
## Uchawi, mchawi ### Ufafanuzi Neno "uchawi" lina husu zoezi la kutumia nguvu hisio ya kawaida ambayo haitoki kwa Mungu. "Mchawi" ni mtu anaye tumia uchawi. * Katika Misri, Mungu alipo fanya vitu vya maajabu kupitia Musa, wachawi wa Kimisri wa Farao aliweza kufanya baadhi ya vitu hivyo, lakini nguvu haikuwa ya Mungu. * Uchawi mara nyingi wa husu kupiga rambli au kurudia maneno kuweza kufanya kitu cha ajabu kutokea. * Mungu ana amuru watu wake wasifanye vitu hivi vya kichawi.
## uchawi, mchawi, uganga ### Ufafanuzi "Uchawi" au "uganga" umaanisha kutumia mazinga umbwe, inayo maanisha kufanya vitu venye nguvu kupitia msaada wa roho chafu. "Mchawi" ni mtu ni mtu anaye fanya hivi vitu venye nguvu vya kimazinga umbwe. * Matumizi ya mazinga umbwe na uchawi yaweza usisha vitu vyenye faida (kama kumponya mtu) na vitu kudhuru (kama kumlaani mtu). Lakini aina zote za uchawi si sawa, kwasababu utumia nguvu za roho chafu. * Katika Biblia, Mungu anasema kuwa matumizi ya uchawi ni uovu kama dhambi zote mbaya. * Maneno "uchawi" na "uganga" yaweza tafsiriwa kama, "roho chafu za nguvu"
## uchungu wa kuzaa ### Ufafanuzi Mwanamke aliye katika "uchungu" anapitia uchungu unaofatiwa na kujifungua mtoto wake. Huu unaitwa "uchungu wa kuzaa." Katika barua yake kwa Wagalatia, mtume Paulo alitumia neno hili kama mithali kuelezea jitihada yake kubwa ya kuwasaidia waumini wenzake kuwa kama Yesu zaidi na zaidi. Mfano wa uchungu wa kuzaa unatumika katika Biblia kuelezea jinsi maafa ya siku za mwisho yatakavyotokea kwa kasi na nguvu.
## udaku ### Ufafanuzi Msemo "udaku" una maana ya watu kuzungumza juu ya masuala binafsi ya mtu mwingine, mara nyingi katika hali ya hasi na isiyo na faida. Mara nyingi kile kinachozungumzwa hakijathibitishwa kuwa kweli. Biblia inasema ya kwamba kusambaza taarifa hasi kuhusu mtu ni kosa. Udaku na kashfa ni mifano ya aina hii ya kauli hasi. Udaku ni wa madhara kwa mtu anayezungumzwa kwa sababu mara nyingi humuumiza uhusiano wa mtu na watu wengine.
## ufalme ### Ufafanuzi Ufalme ni kundi la watu linalotawalwana mfalme. Linamaanisha pia dola au sehemu za kisiasa ambalo mfalme au kiongozi mwingine ana madaraka na mamlaka. Ufalme unaweza kuwa na ukubwa wowote kijiografia. Mfalme anaweza kutawala taifa au nchi au mji mmoja tu. Neno "ufalme" linaweza pia kumaanisha utawala wa kiroho au madaraka, kama usemi "ufalme wa Mungu." Mungu ni mtawala wa viumbe vyote, lakini usemi "ufalme wa Mungu" kwa mahsusi linamaanisha utawala juu ya watu waliomwamini Yesu na walionyenyekea kwa utawala wake. Biblia pia inazungumzia kuhusu Shetani kuwa na "ufalme" anao tawala kwa muda juu ya vitu vingi duniani. Ufalme wake ni uovu na unajulikana kama wa "giza."
## Ufalme ### Ufafanuzi Neno ufalme linawaelezea watu au vitu ambavyo vinahusiana na mfalme au malkia. * Mfano wa vitu vinavyoweza kuitwa vya kifalme ni kama mavazi ya mfalme, nyumba ya kifalme au taji. * Mfalme na malkia huwa wanaishi katika nyumba ya kifalme. * Mfalme huvaa mavazi maalumu yaitwayo "nguo ya kifalme." Mara nyingi nguo hii huwa na rangi ya zambarau ambayo ilikuwa hadimu na ya bei ghali. * Katika agano jipya Yesu aliitwa kuhani wa kifalme.
## ugomvi ### Ufafanuzi Neno "ugomvi" la eleza malumbano ya kimwili au kihisia kati ya watu. * Mtu anaye sababisha ugomvi anafanya vitu vinavyo sababisha kutoelewana. * Ugomvi wakati mwingine una hashiria kuwa hisia kali zinahusishwa, kama hasira au uchungu.
## Uhalifu, mhalifu ### Ufafanuzi Uhalifu ni dhambi inayohusisha kuvunja sheria za nchi. Mhalifu ni mtu anayefanya uhalifu. * Aina ya uhalifu ni kama kumuua mtu au kuiba mali ya mtu. * Mhalifu hukamatwa na kuwekwa mateka kama mfungwa. * Katika Biblia wahalifu wengine huwa wakimbizi, wakitoka sehemu moja hadi nyingine wakiwakimbia watu wanaotaka kuwadhuru kwa kulipa kisasi kwa uhalifu waliofanya.
## uhalifu, uasi ### Ufafanuzi Neno "uhalifu" linamuelezea mtu ambaye hatii sheria na maagizo. Wakati nchi au kundi la watu wako katika hali ya "uasi" inamaanisha kuna kutokutii na upotevu wa maadili kulikoenea. Mtu muasi ni mtu aliyekaidi na hatii amri za Mungu. Mtu Paulo aliandika kuwa katika siku za mwisho kutakuwa na "mwanamme wa uasi," au "yule mhalifu" atakaye shawishiwa na Shetani kufanya mambo maovu.
## ujasiri, jasiri ### Ufafanuzi Ujasiri ni kitendo cha kukabiliana au kufanya jambo gumu au la hatari. * Jasiri ni mtu anayefanya jambo la jema hatakama anahisi kuogopa au anakatishwa tamaa. * Mtu anaonesha ujasiri anapokutana na maumivu ya mwili au hisia na kukabiliana nayo. * "kuchukua ujasiri" ni "kutoogopa" au "kuwa na uhakika kuwa mambo yatakuwa sawa." * Joshua alipokuwa anajiandaa kwenda kwenye nchi hatari ya Kanaani Munsa alimwambia awe mwenye nguvu na jasiri. * Ujasiri inaweza kutafsiriwa kama "kutoogopa" au "imara." * Kuongea kwa ujasiri inaweza kutafsiriwa kama "kuongea bila kuogopa"
## ukoma, mkoma ### Ufafanuzi Neno "ukoma" linatumika katika Biblia kumaanisha aina kadhaaza magonjwa ya ngozi. "Mkoma" ni mtu mwenye ukoma. Neno "ukoma" pia linaweza kutumika kuelezea mtu au sehemu ya mwili iliyoadhirika na ukoma. Aina flani za ukoma zinasababisha ngozi kupoteza rangi na mabaka meupe, kama Miriamu na Naamani walivyokuwa na ukoma. Katika nyakati za sasa, ukoma mara nyingi husababisha mikono, miguu, na sehemu zingine za mwili kuharibika. Kulingana na maelekezo ambayo Mungu aliwapa Waisraeli, mtu akiwa na ukoma, alionekana "mchafu" na ilimbidi kukaa mbali na watu wengine ili asiwaambukize na ugonjwa. Mkoma kawaida angasema "mchafu" ili wengine waonywe wasije karibu yake. Yesu aliponya wakoma wengi, pamoja na aina zingine za magonjwa.
## Ukoo ### Ufafanuzi Ukoo ni kundi la wana familia wanaotokana na mababu. * Katika agano la kale Waisraeli walihesabiwa kutokana na koo zao au makundi ya familia. * Koo zilipewa majina kutokana na babu aliyejulikana sana. * Mtu mmoja mmoja mara nyingine huitwa kwa jina la ukoo wake. Kwa mfano baba mkwe wa Musa mara nyingine aliitwa kwa jina la ukoo wake Reueli. * Ukoo waweza kutafsiriwa kama "kundi la familia" au "ndugu."
## ulimi ### Ufafanuzi Kuna maana kadhaa katika Biblia ya "ulimi." * Katika Biblia, maana iliyo zoeleka ni "lugha" au "hotuba." * Wakati mwingine "ulimi" unaweza maanisha lugha inayo zungumzwa na baadhi ya makundi ya watu. * Wakati mwingine ina maana ya lugha ya kimuujiza ambayo Roho Mtakatifu anawapa waamini wa Kristo kama "karama za Roho" * Msemo "ndimi" za moto uleza "miyale" ya moto. * Katika maneno "ulimi wangu wafurahia," neno "ulimi" waeleza mtu wote. * Msemo "ulimi wa uongo" waeleza sauti ya mtu au hotuba.
## ulizia ### Ufafanuzi Usemi "ulizia" inamaana kumuomba mtu taarifa. Usemi wa "kuulizia kwa"mara nyingi unatumika kumaanisha kumuomba Mungu hekima au msaada. Agano la kale limetunza kumbukumbu ya mifano kadhaa ambapo watu walimuuliza Mungu. Neno pia linaweza kutumika kwa mfalme au afisa wa serikalini kufanya utafiti katika kumbukumbu za maandishi rasmi. Kulingana na mazingira, "ulizia" inaweza kutafsiriwa kama "kuomba" au "kuomba taarifa." Usemi "kumuuliza Yahwe" inaewza kutafsiriwa kama "kumuomba Yahwe uongozo" au "kumuuliza Yahwe nini cha kufanya." "Kuulizia juu ya" kitu inaweza kutafsiriwa ka "kuuliza maswali kuhusu" au "kuulizia taarifa kuhusu." Yahwe anaposema, "Sitaulizwa na wewe" hii inaweza kutafsiriwa kama, "Sita kuruhusu wewe uniombe taarifa" au "hautaruhusiwa kutafuta msaada kutoka kwangu."
## Umba, Uumbaji, Muumbaji ### Ufafanuzi Kuumba ni kutengeneza kitu au kusababisha kitu kitokee. Kitu kinachoumbwa kinaitwa uumbaji. Mungu anaitwa muumbaji kwa sabau alisababisha vitu vyote vya dunia vikatokea. * Neno hili linapotumika kumuelezea Mungu alipoumba dunia inaonesha kuwa aliiumba bila kutumia kitu. * Wanadamu wanapoumba vitu wanaviumba kwa kutumia vitu ambavyo vipo tayari. * Maranyingine uumbaji inatumika kuelezea vitu vya dhahania kama "kuumba amani au kuumba moyo safi kwa mtu." * Neno Uumbaji inaelezea mwanzo wa ulimwengu ambapo Mungu kwanza aliumba kila kitu
## umbo, sanamu ya kuchonga, umbo la kuchonga, umbo la chuma ### Ufafanuzi Maneno haya yote yanatumika kumaanisha sanamu ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuabudu miungu ya uongo. Katika mazingira ya kuabudu sanamu, neno "sanamu" ni njia fupi ya kusema "sanamu ya kuchonga." "Sanamu ya kuchonga" au "umbo la kuchonga" ni kitu cha mbao kilichofanywa kuonekana kama mnyama, mtu, au kitu. "Umbo la chuma" ni kitu au sanamu iliyoundwa kwa kuyeyusha chuma na kuimwaga katika umbo tupu ambalo lina umbo la kitu, mnyama, au mtu. Vitu hivi vya mbao na chuma vilitumika katika kuabudu miungu ya uongo. Neno "umbo" wakati wa kuzungumzia sanamu inamaanisha kati ya sanamu ya mbao au ya chuma.
## Umri ### Ufafanuzi "Umri" ni idadi ya miaka aishiyo mwanadamu. pia hutumika kuonesha nyakati kwa ujumla. * Maneno mengine yanayotumika kuelezea wakati ni kipindi au msimu. * Yesu anarejea "nyakati hizi" kama wakati wa sasa ambapo dhambi, uovu na kutokutii kumeijaza dunia. * Kutakuwa na nyakati zijazo ambapo haki itatawala mbinguni na duniani pote.
## unyofu ### Ufafanuzi Neno "unyofu" ueleza kutenda kwa namna inayo fuata sheria za Mungu.] * Maana ya hili neno ni pamoja kusimama wima na kuangalia mbele. * Mtu aliye "mnyofu" ni mtu anaye tii maagizo ya Mungu na hafanyi vitu vilivyo nje ya mapenzi yake. * Maneno kama "uadilifu" na "haki" yana maana moja na wakati mwingine utumika sambamba kama "audilifu na haki."
## uongo, ukaidi, kuipotosha ### Ufafanuzi Neno "kilichopotoka" linatumika kumuelezea mtu au tendo fulani ambalo linapotosha kimaadili. Neno "ukaidi" linamaana ya tabia ya kikaidi". Kupotosha kitu inamaana ya kugeuza jambo toka kwenye usahihi wake au uzuri wake. * Mtu au kitu ambacho kimepotoka kimegeuzwa toka kwenye kilicho kizuri au sahihi. * Katika Biblia Waisraeli walifanya kwa ukaidi walipomkosea Mungu. Walifanya hivi kwa kuabudu miungu ya uongo. * Tendo lolote lililo kinyume na tabia za Mungu linaelezewa kama lililopotoka. * "Hotuba iliyopotoka" inaweza kutafsiriwa kama "kuzungumza kwa namna mbaya. * "Matendo ya ukaidi" inaweza kutafsiriwa kama "kutenda matendo mabaya" au "kufanya mambo kinyume na amri za Mungu."
## upanga ### Ufafanuzi Upanga ni silaha ya chuma nyembamba inayo tumika kukata au kuchoma. Ina mshikio na nch ndefu.
## upinde ### Ufafanuzi Aina hii ya silaha ambayo inajumuisha mishale ya kurusha kutoka katika upinde. Katika nyakati za Biblia ilitumika kupigana na maadui na kuwindia. * Upinde unatengenezwa kwa mti, mfupa au chuma au vitu vingine vigumu, kama vile jino la dubu. Imepinda na kufungwa kwa kamba. * Mshale ni kitu chembamba chenye ncha kali, upande mmojawapo. Nyakati za kale, mshale ulitengenezwa kwa kutumia vitu mbalimbali kama vile mtu, mfupa, jiwe, au chuma. * Pinde na mishale kwa kawaida inatumiwa na wawindaji au maaskari. * Neno "mshale" wakati mwingine linatumika kitamathari katika Biblia kurejerea shambulio la adui au hukumu ya ki- Mungu.
## upole ### Ufafanuzi Neno "upole" la elezea mtu aliye mtaratibu, mnyenyekevu, na aliye tayari kuteseka dhuluma. Upole ni uwezo wa kuwa mtaratibu ata kama ukali au nguvu inaonekana ni sahihi. * Upole una endana na unyenyekevu. * Hili neno la weza tafsiriwa kama "utaratibu". * Neno "upole" la weza tafsiriwa kama "utaratibu" au "unyenyekevu."
## ushauri, mshauri ### Ufafanuzi Ushauri inamaana ya kumsaidia mtu kuamua kwa busara juu ya jambo fulani. Mshauri mwenye busara ni mtu anayetoa ushauri ambao utamsaidia mtu kuamua kwa usahihi. * Wafalme wana washauri maalumu wanaowasaidia kuamua mambo ya muhimu juu ya watu wanaowaongoza. * Mara nyingine ushauri unaotolewa waweza ukawa mbaya. Mshauri mbaya anaweza kumshauri mfalme kufanya maamuzi ya kuwadhuru watu. * Inategemea na mukhtadha ushauri yaweza kutafsiriwa kama "kusaidia kuamua." au "onyo" au "mwongozo."
## ushuru ### Ufafanuzi Ushuru ni pesa au bidha watu wanazo lipa kwa serikali iliyo na mamlaka juu yao. * Kiasi cha pesa kinacho lipwa kwa ushuru mara nyingi kina thamani ya bidha au kiasi ambacho mtu ana utajiri. * Kama ushuru zisipo lipwa, serikali inaweza chukuwa hatua za kisheria dhidi ya mtu kupata pesa zinazo daiwa. * Yusufu na Maria walisafiri Bethilehemu kuhesabiwa katika takwimu kwa lengo la kumtoza ushuru kila mtu anaye ishi katika Serikali ya Kirumi. * Pia kulikuwa na "ushuru wa hekalu" ambao ulikuwa ni pesa watu waliyo weka katika sanduku la sadaka. Baadhi ya hizi pesa zilitumika kushughulikia jengo la hekalu. * "Mtoza ushuru" ni mtu anaye fanya kazi serikalini kupokea pesa watu wanao takiwa kuwalipa.
## ushuru ### Ufafanuzi Neno "ushuru" la husu zawadi kutoka kwa mtawala mmoja kwenda kwa mwingine, kwa kusudi la ulinzi na mausiano mema kati ya mataifa yao. * Ushuru unaweza kuwa malipo ambayo mtawala au serikali ina itaji kutoka kwa watu, kama kodi. * Katika Biblia, wafalme wasafiri au watawala walilipa ushuru kwa mfalme wa eneo waliyo kuwa wanasafiri kupita kuhakikisha watalindwa na kuwa salama. * Mara nyingi ushuru una jumuisha vitu vingine kuacha pesa, kama vya kula, manukato, nguo za bei, na vitu vya gharama kama dhahabu.
## uso ### Ufafanuzi Neno "uso" lina maana ya sehemu ya mbele ya kichwa cha mtu. Msemo huu pia una maana kadhaa za tamathali. Msemo wa "uso wako" mara kwa mara ni njia ya tamathali ya kusema "wewe". Vivyo hivyo, msemo "uso wangu" mara kwa mara una maana ya "Mimi". Katika hali ya kimwili, "kumkabili" mtu au kitu ina maana ya kutazama upande wa huyo mtu au kitu. "Kukabiliana" ina maana ya "kutazamana" Kuwa "uso kwa uso" ina maana ya kwamba watu wawili wanatazamana katika umbali wa karibu. Yesu "alipoweka uso wake kuelekea Yerusalemu" ina maana ya kwamba aliamua kwa dhati kwenda. "Kuweka uso dhidi ya" watu au mji ina maana kuamua kwa nguvu: kutoimarisha tena, au kumkataa mtu au mji huo. Msemo "uso wa nchi" una maana ya sehemu ya juu ya dunia na mara kwa mara ni kumbukumbu ya jumla ya dunia nzima. Kwa mfano, "njaa inayofunika uso wa dunia" ina maana ya njaa inayosambaa ambayo hugusa watu wengi wanaoishi juu ya nchi. Msemo wa tamathali, "usifiche uso wako kwa watu wako" una maana "usiwakatae watu wako" au "usiwaache watu wako" au "usiache kuwatunza watu wako". Mapendekezo ya Tafsiri Ikiwezekana, ni bora kubaki na msemo au kutumia msemo katika lugha hii ambayo ina maana ya kufanana. Msemo "kukabili" unaweza kutafsiriwa kama "kugeuka upande wa" au "kutazama moja kwa moja" au "kuangalia uso wa". Msemo "uso kwa uso" unaweza kutafsiriwa kama "karibu kabisa" au "mbele ya" au "katika uwepo wa". Kulingana na muktadha, msemo "mbele ya uso wake" unaweza kutafsiriwa kama "kabla yake" au "mbele yake" au "katika uwepo wake". Msemo "weka uso wake kuelekea" unaweza kutafsiriwa kama "kuanza kusafiri kuelekea" au "aliamua akilini mwake kuondoka". Msemo "kuficha uso wake kutoka kwa" unaweza kutafsiriwa kama "kugeuka kutoka kwa" au "kuacha kusaidia au kulinda" au "kukataa". "Kuweka uso wake dhidi ya" mji au watu inaweza kutafsiri kama "kutazama kwa hasira na kushutumu" au "kukataa kukubali" au "kuamua kukataa" au "kulaumu na kukataa" au "kutoa kuhukumu". Msemo "tamka mbele ya uso wao" inaweza kutafsiriwa kama "sema kwao moja kwa moja". Msemo " katika uso wa nchi" inaweza kutafsiriwa kama "katika nchi yote" au "juu ya dunia nzima" au "kuishi katika dunia".
## Utaji ### Ufafanuzi Utaji ni kipande cha nguo kinachotumika kufunikia kichwa au uso ili usionekane. * Musa alifunika uso wake na utaji baada ya kuwa katika uwepo wa Bwana ili mwanga wa uso wake usionekane kwa watu. * Katika Biblia mwanamke hutumia utaji kujifunika kichwa chake au uso wake mbele za watu au katika uwepo wa wanaume. * Kitenzi "kufunika" inamaana ya kufunika kwa utaji. * Katika tafsiri zingine za Kiingereza Utaji inatumika kuelezea pazia kubwa lililitumika kufunikia mlango wa kuingilia patakatifu pa patakatifu.
## Utawala, mtawala ### Ufafanuzi Maneno "utawala" au "mtawala" yana maana ya kusimamia na kuongoza watu wa nchi ili kuwasaidia wafanye sawasawa na inavyotakiwa. * Danieli pamoja na vijana wengine watatu wa Kiyahudi walichaguliwa kuwa watawala au viongozi wa serikali katika eneo fulani la Babiloni. * Kwenye agano jipya neno "utawala" limetumika kumuelezea mtu aliye na karama za roho mtakatifu. * Mtu aliye na karama ya rohoni ya utawala ana uwezo wa kuongoza watu na kuwasimamia katika usimamizi wa majengo na mali nyingine.
## utukufu ### Ufafanuzi Neno "utukufu" la eleza uzuri wa ajabu na umaridadi ambao una ambatana na utajiri na muonekano wa kuvutia. * Mara nyingi utukufu utumika kufafanua utajiri ambao mfalme anao, au jinsi anavyo katika nguo zake nzurui na za gharama. * Neno "utukufu" lina weza pia kutumikakueleza uzuri wa miti, milima, na vitu vingine Mungu alivyo umba. * Badhi ya miji inasemwa kuwa na utukufu, ikielezea mali asili zao, majengo makubwa na barabara, na utajiri wa watu, pamoja na nguo za gharama, dhahabu na fedha.
## uvumba ### Ufafanuzi Neno "uvumba" linamaanisha mchanganyiko wa vikolezo vyenye manukato mazuri vinavyochomwa kutoa moshi wenye harufu nzuri. Mungu aliwaambia Waisraeli kuchoma uvumba kama sadaka kwake. Huu uvumba ulitakiwa kutengenezwa kwa kuchanganya kiwango sawa cha vikolezo maalumu vitano kama Mungu alivyoagiza. Huu ulikuwa uvumba mtakatifu, kwa hiyo hawakutakiwa kuutumia kwa kitu kingine chochote. "Madhabahu ya kufukuzia uvumba" ilikuwa madhabahu maalumu ya kuchomea uvumba. Uvumba ulitolewa angalau mara nne kwa siku, kwa kila saa ya maombi. Ilitolewa pia kila wakati sadaka ya kuteketeza ilipotolewa. Kuchomwa kwa uvumba kunaashiria maombi na kuabudu vinaponyanyuka juu kwa Mungu kutoka kwa watu wake. Njia zingine za kutafsiri "uvumba" zinaweza kuwa, "vikolezo vya manukato mazuri" au "mimea yenye harufu nzuri."
## Uvumilivu ### Ufafanuzi Uvumilivu ni kitendo cha kupita katika wakati mgumu na kuwa na subira. * Mtu akiwa na uvumilivu kwa mtu fulani inamaana kuwa anampenda yule mtu na atamsamehe kosa lolote ambalo mtu yule atafanya. * Biblia inawafundisha watu wa Mungu kuwa wavumilivu wanapopitia magumu na kuwavumilia watu pia. * Kwa sababu ya rehema zake Mungu anawavumilia watu wake japokuwa ni wenye dhambi wanaostahili adhabu.
## uwezo ### Ufafanuzi Neno "uwezo" la husu kuwa na nguvu nyingi. * Mara nyingi neno "uwezo" ni neno lingine la "uweza." Tunapo zungumza kuhusu Mungu, la weza manisha "nguvu." * Maneno, "wanaume wa uwezo" mara nyingi ya husu wanaume wenye ujasiri na washindi kwenye pambano. Kundi la Daudi la wanaume waaminifu waliyo mlinda na kumtetea mara nyingi walitwa "wanaume wa uwezo." * Mungu pia anatajwa kama "mwenye uwezo." * Maneno "matendo ya uwezo" mara kwa mara ya husu vitu vya ajabu Mungu anavyo fanya, sana sana miujiza.
## uwezo ### Ufafanuzi Neno "uwezo" la husu hali ya kuwa na nguvu kimwili, kihisia, au kiroho. * "Uwezo" yaweza elezea kuweza kusimama dhidi ya aina ya nguvu. * Mtu ana uwezo wa nia kama anaweza kutoanguka kwenye jaribu. * Mwandishi mmoja wa Zaburi anamuita Yahweh uwezo wake, inayo maanisha Mungu ana msaidia kuwa na nguvu.
## Uyahudi, dini ya Kiyahudi ### Ufafanuzi Neno "Uyahudi" inamaanisha dini inayofuatwa na Wayahudi. Inajulikana piakama "dini ya Kiyahudi." Katika Agano la Kale, neno "dini ya Kiyahudi" inatumika wakati katika Agano Jipya neno "Uyahudi" ndio linatumika. Uyahudi inajumuisha sheria zote za na maelekezo ya Agano la Kale ambayo Mungu aliwapa Wasiraeli kutii. Inajumuisha pia desturi na tamaduni zilizoongezwa katika dini ya Kiyahudi kadri muda ulivyoenda. Wakati wakutafsiri, usemi "dini ya Kiyahudi" au "dini ya Wayahudi" zinaweza kutumika katika Agano la Kale au Jipya. Lakini, neno "Uyahudi" linapaswa kutumika tu kwenye Agano Jipya, kwa sababu neno hilo halikuwepo kabla ya wakati huo
## uzao, kutokana na ### Ufafanuzi "Uzao" ni mtu ambaye ni ndugu wa damu moja kwa moja wa mtu mwingine nyuma kabisa katika historia. Kwa mfano, Abrahamu alikuwa uzao wa Nuhu. Uzao wa mtu ni watoto wake, wajukuu, na watukuu, na kuendelea. Vizazi vya Yakobo vilikuwa makabila kumi na mawili ya Israeli. msemo "kutokana na" ni njia nyingine ya kusema "uzao wa" kama vile "Abrahamu alitokana na Nuhu". Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutokana na uzao wa"
## viongozi wa Kiyahudi, mamlaka ya Kiyahudi, viongozi wa dini ### Ufafanuzi Usemi "viongozi wa Kiyahudi" au "mamlaka ya Kiyahudi" inamaanisha viongozi wa dini kama makuhani na walimu wa sheria za Mungu. Walikuwa na mamlaka yakufanya maamuzi ya mambo yasiyo yakidini pia. * Viongozi wa Kiyahudi walikuwa ndio makuhani wakuu, waandishi (walimu wa sheria za Mungu). * Makundi mawili makuu ya viongozi wa Kiyahudi walikuwa Mafarisayo na Masadukayo. * Viongozi sabini wa Kiyahudi walikutana pamoja katika Baraza la Wayahudi Yerusalemu kufanya maamuzi kuhusiana na mambo ya sheria. * Viongozi wengi wa Kiyahudi walikuwa na majivuno na walidhani ni watakatifu. Walimuonea wivu Yesu na walitaka kumdhuru. Walidai kumjua Mungu ila hawakumtii. * Mara nyingi usemi "Wayahudi" inamaanisha viongozi wa Kiyahudi, hasa katika mazingira walipokuwa na hasira na Yesu na walipojaribu kumtega au kumdhuru. * Maneno haya yanaweza pia kutafsiriwa kama "viongozi wa Kiyahudi" au "watu waliotawala juu watu wa Kiyahudi" au "Viongozi wa dini wa Kiyahudi."
## viuno ### Ufafanuzi Neno "viuno" kinamaanisha sehemu ya mwili ya mnyama au mtu aliyo katikati ya mbavu za chini na mifupa ya nyonga, pia ikijulikana kama tumbo la chini. Msemo "kaza viuno" unamaanisha kujiandaa kufanya kazi ngumu. Inatokea katika utamaduni wa kuchomekea sehemu ya chini ya joho kwenye mkanda kiunoni ili kusogea kwa urahisi. Neno "viuno" mara nyingi linatumika katika Biblia kumaanisha sehemu ya chini ya mnyama iliyotolewa sadaka. Katika Biblia, msemo "viuno" mara nyingi humaanisha sehemu za siri za mwanamme kimafumbo na kitasifida kama chanzo cha uzao wake. Msemo "atatoka katika viuno vyako" unaweza pia kutafsiriwa kama, "atakuwa uzao wako" au "atazaliwa kutokana na mbegu yako" au "Mungu atasababisha kutoka kwako." Inapozungumzia sehemu ya mwili, hii inaweza pia kutafsiriwa kama "tumbo" au "nyonga" au "kiuno," kulingana na mazingira.
## vumilia, uvumilivu ### Ufafanuzi Msemo "vumilia" una maana ya kudumu muda mrefu au kustahamili jambo gumu kwa uvumilivu. Pia ina maana ya kusimama imara wakati wa mitihani kuwepo, bila kukata tamaa. Msemo "uvumilivu" unaweza kumaanisha "subira", "ustahamilivu katika majaribu" au "kustahamili pale unapoteswa". Faraja kwa Wakristo "kuvumilia mpaka mwisho" ni kuwaambia wamtii Yesu, hata kama hili litasababisha wao kuteseka. "Kuvumilia mateso" pia inaweza kumaanisha "kupitia mateso". Mapendekezo ya Tafsiri Njia za kutafsiri msemo "vumilia" zinaweza kujumuisha "stahamili" au "kuendelea kuamini" au "kuendelea kufanya kile Mungu anachotaka ufanye" au "simama imara". Katika baadhi ya muktadha, "kuvumilia" kunaweza kutafsiriwa kama, "kupitia jaribu" au "kupitia". Kwa maana ya kudumu muda mrefu, msemo "vumilia" unaweza kutafsiriwa kama "kudumu" au "kuendelea". Msemo, "hatavumilia" unaweza kutafsiriwa kama, "hatadumu" au "hataendele kuishi". Njia za kutafsiri "uvumilivu" unaweza kujumuisha "ustahamilivu" au "kuendelea kuamini" au "kubaki mwaminifu".
## Vumilia, uvumilivu ### Ufafanuzi "vumilia" au "uvumilivu" ni kitendo cha kuendelea kufanya kitu fulani hatakama ni ngumu sana kufanya au itachukua mda mrefu. * Kuvumilia pia inamaana ya kuendelea kufanya kama Kristo alivyofanya japokuwa alipita katika majaribu magumu alivumilia. * Mtu kama ni "mvumilivu" inamaana ana uwezo wa kuendelea kufanya anachopaswa kufanya hatakama kuna maumivu ay ugumu. * Kuendelea kuamini anachofundisha Mungu kunahitaji uvumilivu hasa unapokutana na mafundisho ya uongo.
## Waasi, uasi. ### Ufafanuzi Uasi ni kukataa kuitumikia mamlaka ya mtu fulani. Waasi ni watu wasiotii na kufanya mambo maovu. Mtu huyu anaitwa muasi. * Mtu anaasi pale anapofanya jambo ambalo mamlaka iliyo juu yake imemkataza asifanye. * Pia mtu anaweza kuasi akikataa kufanya analoamriwa afanye na mamlaka yake. * Mara nyingine watu wanaasi juu ya serikali yao au kiongozi anayewaongoza. * Uasi inamaana ya kukataa kutii au kuvunja sheria.
## waheshima, heshima ### Ufafanuzi Neno "heshima" la husu kitu ambacho ni bora na chenye ubora. "mtu wa heshima" ni mtu aliye wa siasa au wa jamii ya juu. * Mtu waheshima alikuwa ni afisa wa jimbo, mtumishi wa karibu wa mfalme. * Neno "heshima" la weza tafsiriwa kwa, "afisa wa mfalme" au "afisa wa serikali" au "mtu wa uzao wa heshima"
## wanaume wasomi, mamajusi ### Ufafanuzi Katika akaunti ya Mathayo ya kuzaliwa kwa Yesu, hawa wanaume "wasomi" au "wenye elimu" walikuwa "wanaume wenye hekima" walioleta zawadi kwa Yesu Bethlehemu muda baada ya kuzaliwa huko. Inawezekana walikuwa "mamajusi," ambao ni watu wanaofuatilia nyota. Wanaume hawa walisafiri mbali kutoka nchi ya mbali kaskazini mwa Israeli. Haijulikani haswa ni wapi walipotokea na walikuwa kina nani. Lakini ni dhahiri walikuwa wasomi waliozisoma nyota. Wanaweza kuwa wazawa wa wanaume wenye hekima waliowatumikia wafalme wa Babeli wakati wa Danieli na waliofundishwa mambo mengi,ikiwemo kuzisoma nyota na kufafanua ndoto. Kiutamaduni inasemekana kuwa walikuwa wanaume watatu wenye hekima au wanaume wasomi kwa sababu ya zawadi tatu walizoleta kwa Yesu. Lakini, Biblia haisemi walikuwa wangapi.
## watoza ushuru ### Ufafanuzi "Mtoza ushuru" alikuwa mfanya kazi wa serikali ambaye kazi yake ilikuwa kupokea pesa watu waliyo paswa kulipa serikali ushuru. * Wakati wa Yesu na mitume, serikali ya Rumi
## watu wenye busara ### Ufafanuzi Kwenye Biblia watu wenye busara ni watu wanaomtumikia Mungu na kutenda kwa busara na sio wapumbavu. Pia ni neno lililotumika kuwalelezea watu wenye ufahamu wa kipekee na uwezo wanaotumika kama sehemu katika mahakama ya mfalme. * Maranyingine watu wenye busara huelezewa kwa kumumia maneno kama "watu wenye uelewa au watu wanaotenda kwa busara na haki kwa sababu wanamtii Mungu. * Watu wenye busara waliomtumikia Farao na wafalme wengine walikuwa wasomi wa nyota ambao walitafuta maana ya nyota ilivyokaa angani. * Pia watu wenye busara walitegemewa kutafsiri maana ya ndoto. Mfano mfalme Nebukadreza aliwataka watu wenye busara wamuelezee ndoto yake na kumwambia maana yake lakini hakuna aliyeweza kufanya hivyo isipokuwa Danieli aliyepokea ufahamu toka kwa Mungu. * Mara nyingine watu wenye busara hufanya miujiza kupitia roho chafu. * Katika agano jipya Yesu aliitwa mwanaume wenye busara.
## wavuvi ### Ufafanuzi Wavuvi ni wanamume ambao hukamata samaki kutoka majini kama njia ya kupata pesa. Katika Agano Jipya, wavuvi walitumia mitego mikubwa kukamata samaki. Msemo "wavuvi" ni jina lingine la mvuvi. Petro na mitume wengine walifanya kazi kabla ya kuitwa na Yesu. Kwa kuwa nchi ya Israeli ilikuwa karibu na maji, Biblia ina kumbukumbu nyingi ya samaki na wavuvi. Msemo huu unaweza kutafsiriwa na msemo kama "wanamume wanaokamata samaki" au "wanamume wanaopata pesa kwa kukamata samaki"
## Wazee ### Ufafanuzi Wazee ni wanamume wa kiroho waliokomaa ambao wana majukumu ya kiroho na uongozi wa utendaji miongoni mwa watu wa Mungu. Msemo "mzee" umetokana na kweli ya kwamba wazee asili yao walikuwa wanamume wa umri mkubwa ambao, kwa sababu ya umri wao na uzoefu, walikuwa na hekima kubwa. Katika Agano la Kale, wazee walisaidia kuongoza Waisraeli katika masuala ya haki ya jamii na Sheria ya Musa. Katika Agano Jipya, wazee wa Kiyahudi waliendelea kuwa viongozi katika jamii zao na pia walikuwa waamuzi kwa watu. Katika makanisa ya mwanzo ya Wakristo, wazee wa Kikristo walitoa uongozi wa kiroho kwa mikusanyiko ya jamii ya waumini. Wazee katika makanisa haya walijumuisha wanamume vijana ambao walikomaa kiroho. Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "wanamume wazee" au "wanamume waliokomaa kiroho wanaoongoza kanisa".
## Wazee wa ukoo ### Ufafanuzi Katika agano la kale "wazee wa ukoo" ni mababa wa Wayahudi hasa Abrahamu, Isaka na Yakobo. * Pia inaweza kuwaelezea wana kumi na mbili wa Yakobo ambao ni wazee wa koo 12 za kabila la Israeli. * Wazee wa ukoo ni sawa na mababu lakini mara nyingi inawaelezea hasa mababu wanaojulikana ambao ni viongozi wa kundi fulani la watu.
## weka wakfu, kuwekwa wakfu kwa ### Ufafanuzi Kuweka wakfu ni kuweka kando kitu kwa ajili ya kusudi maalumu au shughuli. Daudi aliweka wakfu dhahabu na fedha zake kwa Bwana. Mara kwa mara, neno "kujitolea" lina maana ya tukio rasmi au sherehe ya kuweka kando kitu kwa ajili ya kusudi maalumu. Kuweka wakfu kwa madhabahu ilijumuisha kutoa sadaka kwa Mungu. Nehemia aliwaongoza Waisraeli katika kuweka wakfu kwa kuta za Yerusalemu zilizotengenezwa kwa ahadi mpya ya kumtumikia Yahwe pekee kwa vyombo vya muziki na kuimba. Msemo wa "kuweka wakfu" unaweza kutafsiriwa kama "kutenga kusudi maalumu" au "kabidhi kitu kutumika kwa kazi maalumu" au "kabidhi mtu kutenda tendo maalumu".
## wivu, tamani ### Ufafanuzi Msemo "wivu" una maana ya kuwa na wivu kwa mtu kwa sababu ya kile ambacho mtu huyo anamiliki au kwa sababu ya sifa za kutamanisha za mtu huyo. Msemo "tamani" una maana ya kumuonea wivu mtu hadi hatua ya kutamani kwa nguvu kuwa na kitu ambacho mtu huyo anacho. Kwa kawaida wivu ni hisia ya hasi ya kuchukia kwa sababu ya mafanikio, bahati nzuri, au mali za mtu mwingine. Kutamani ni hamu kali ya kutaka mali ya mtu mwingine, au hata mke au mume wa mtu mwingine.
## woga, kutishwa ### Ufafanuzi Istilahi ' hofu' hurejelea hisia kali za woga or kitisho. Mtu aliye na hofu huwa ameogopa. woga ni hali kali na kubwa zaidi ya hofu, zaidi ya hofu ya kawaida. Mara kwa mara mtu anapokuwa ametishwa huwa ameshitushwa na ameshangazwa sana.
## woga, kuogopesha ### Ufafanuzi Neno "woga" uelezea hisia ya hofu kuu. "Kuogopesha" mtu ina maana ya kusababisha huyo mtu kujisikia wasi wasi sana. * "Woga" ni kitu au mtu anaye sababisha hofu kubwa. * Hizi oga zinaweza elezwa kama "kuogopesha." Hili neno la weza tafsiriwa kama, "kisababisha hofu" au "kizalisha woga" * Hukumu ya Mungu wakati mmoja itasababisha woga kwa wasio tubu waliyo kataa neema yake.
## yayuka, yayushwa ### Ufafanuzi Neno "yayusha" la husu kitu kuwa maji kinapo pashwa. Pia utumika kimfano. * Namna tofauti za vyuma vinapashwa hadi kuyayuka na kumiminwa katika vifaa ilikutengeneza vitu kama silaha au sanamu. * Kama mshuma unavyo waka, kasha lake lina yayuka na kutiririka. Enzi za kale, maandishi yalitiwa muhuri kwa kumimina kiasi kidogo cha kasha lililo yakuka kwenye miisho yake. * Matumizi ya mfano wa "yayuka" ina maana yakuwa nyepesi na dhaifu. * Msemo, "mioyo yao itayayuka" ina maana watakuwa dhaifu sana kwasababu ya hofu. * Msemo, "mioyo yao itayayuka na kuondoka" ina maana watalazimishwa kuondoka au wataonyeshwa kuwa dhaifu na kuondoka kwa kushindwa.
## Zabibu ### Ufafanuzi Mzabibu ni tunda dogo, la duara, laini ambalo huota katika vishada vya mizabibu. Juisi ya mizabibu hutumika kutengeneza divai. Kuna aina tofauti ya rangi ya mizabibu, kama vile kijani iliyoiva, zambarau au nyekundu. Mizabibu binafsi inaweza kuwa na ukubwa kama sentimita moja au tatu. Watu huotesha mizabibu katika bustani inayoitwa mashamba ya mizabibu. Hii huwa mistari mirefu ya zabibu. Mizabibu ilikuwa chakula muhimu sana wakati wa Biblia na kuwa na mashamba ya zabibu ilikuwa ishara ya utajiri. Ili kukaa na mizabibu isioze, watu mara kwa mara waliikausha. Mizabibu ya kukaushwa iliitwa "zabibu kavu" na ilitumika kutengeneza keki za zabibu kavu. Yesu alitoa fumbo juu ya shamba la zabibu kuwafundisha wanafunzi wake juu ya ufalme wa Mungu.
## Zambarau ### Ufafanuzi Hii ni rangi ambayo ni mchanganyiko kati ya rangu ya bluu na nyekundu. * Hapo kale rangi ya zambarau ilikuwa hadimu na ya thamani sana ilitumika kama vazi kwa wafalme na viongozi wakuu. * Kwa sababu ilikuwa ya gharama na ilichukua muda kutengeneza vazi la rangi ya zambarau ilikuwa alama ya utajiri na ufalme. * Pia zambarau ilikuwa rangi iliyotumika kwenye mapazia ya hekalu na nguo zilizovaliwa na makuhani. * Askari wa Rumi walimvalisha Yesu vazi la zambarau kabla hawajamsulubisha ili kumdhihaki kwa kuwa alisema yeye ni mfalme wa Wayahudi. * Lidia toka katika mji wa Filipi alikuwa mwanamke aliyejipatia kipato kwa kuuza nguo za zambarau.
## Zawadi ### Ufafanuzi Zawadi ni kitu anachopokea mtu kwa sababu amefanya jambo fulani liwe baya au zuri. Kumpa mtu zawadi ni kumpa mtu kitu anachostahili. * Zawadi yaweza kuwa kitu kizuri ambacho mtu hupokea kwa sababu amefanya vizuri au amemtii Mungu. * Maranyingine zawadi yaweza kuwa vitu hasi vinavyotokana na tabia mbaya. Haya ni matokeo hasi anayopata mtu baada ya kufanya matendo ya dhambi.
## zinaa ### Ufafanuzi Msemo "zinaa" una maana ya tendo la ngono ambalo hufanyika nje ya mahusiano ya ndoa ya mwanamume na mwanamke. Hii ni kinyume na mpango wa Mungu. Msemo huu unaweza kumaanisha tendo lolote la kingono ambalo ni kinyume na mapenzi ya Mungu, ikiwemo matendo ya usenge na ponografia. Aina moja ya zinaa ni uzinzi, ambayo ni tendo la ngono haswa kati ya mtu aliyeoa na mtu ambaye sio mke au mume wake. Aina nyingine ya zinaa ni "ukahaba" ambayo uhusisha kulipwa kufanya ngono na mtu. Msemo huu pia hutumika kitamathali kumaanisha ukosefu wa uaminifu wa Israeli kwa Mungu walipoabudu miungu ya uongo. Mapendekezo ya Tafsiri Msemo "zinaa" unaweza kutafsiriwa kama "uzinzi" ikiwa maana sahihi ya msemo inaeleweka. Njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "matendo mabaya ya ngono" au "ngono nje ya ndoa". Msemo huu unaweza kutafsiriwa katika njia nyingine kutoka kwa neno "uzinzi". Tafsiri ya matumizi ya tamathali ya msemo huu unatakiwa kukaa na maana halisi ikiwezekana kwa kuwa kuna ulinganisho wa kufanana katika Biblia kati ya kutokuwa mwaminifu kwa Mungu na kutokuwa mwaminifu katika mahusiano ya kimapenzi.
## zingira, kuzingira ### Ufafanuzi Neno "kuzingira" la husu pale jeshi shambulizi linapo zunguka mji na kuusababisha usiweze kupokea maitaji na maji. "Kuzingira" mji ina maana kusababisha mji kuwa chini ya kuzungukwa. * Wakati Babiloni ilipo kuja kushambulia Israeli, walitumia mbinu ya kuzingira Yerusalemu kudhohofisha watu kwenye mji. * Mara nyingi wakati wa kuzingira, mapande ya mchanga yana undwa taratibu kuwezesha jeshi shambulizi kuvuka kuta za mji na kuvamia mji.