John
John 1
John 1:1-3
Hapo mwanzo
Ina maanisha mwanzoni kabisa ya wakati kabla Mungu hajaumba mbingu na nchi.
Neno
Iina maanisha Yesu. Kama inawezekana litafsiri kama "Neno" Kama katika lugha yako "Neno" ni ngeli ya kike, inawe kufasiriwa kama "yule anayeitwa "Neno."
Vitu vyote viliumbwa kwa yeye
Hii inaweza kufasiriwa katika hali tendaji. "Mungu alivifanya vitu vyote kwa yeye."
pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichofanyika ambacho kilichofanyika.
Hii inaweza kufasiriwa katika hali tendaji. "Mungu hakufanya kila kitu chochote pasipo yeye" au " Mungu alifanya vitu vyote akiwa naye."
John 1:4-5
Ndani yake kulikuwa uzima
Hapa "uzima"ni mfano kwa kusababisha kila kitu kuishi. A: "Yeye anayeitwa Neno ndiye aliyesababisha kila kitu kuishi.
Uzima
hapa tumia neno la jumla kwa "uzima." Kama utatafasiri moja kwa moja unaweza kufasiri kama "uzima wa kiroho".
Uzima huo ulikuwa nuru ya wanadamu wote
"Nuru" ni mfano ambao ambao unamaanisha ufunuo wa Mungu.AT: aliifunua kweli kwetu kama vile nuru ifunuavyo kile kilichomo gizani.
NUru yang'ara gizani wala giza halikuliweza
Kama vile ambavyo giza lisivyoweza kuizima nuru, watu wabaya hawajaweza kumzuia yeye ambaye ni kama nuru katika kuifunua kweli ya Mung.
John 1:6-8
Kuishuhudia nuru
Hapa "Nuru" ni mfano kwa ajili ufunuo wa Mungu katika Yesu. AT: "onyesha jinsi ambavyo Yesu alivyo kama nuru halisi kutoka kwa Mungu."
John 1:9
Niru ya kweli
Hapa "nuru" ni mfano ambao unamwakilisha Yeus kama ufunuo wa kweli kutoka kwa Mungu.
hutia nuru
"hutoa nuru kwa"
John 1:10-11
Alikuwapo duniani, na kwa yeye ulimwengu ulipata kuwepo, lakini ulimwengu haukumjua
AT: "Lakini pamoja kwamba alikuwa ulimwenguni, na kwamba Mungu aliumba vitu vyote kwa yeye, bado watu hakumtambua."
alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea
AT: "Alikuja kwa wenzake , na wenzake hwakumpokea."
John 1:12-13
Amini juu ya
Hii ina maanisha Yesu kuwa Mwokozi na kuishi kwa jinsi ambayo inamtukuza.
Jina
Neno 'jina" ni neno ambalo linaelezea utamblisho wa "Yesu" na kila kitu kitu kuhusu yeye.
aliwapa uwezo
aliwapa mamlaka" au "aliwezesha kwa ajili yao"
Wana wa Mungu
Neno "watoto"ni mfano ambao unawakilisha uhusiano wetu na Mungu, ambao ni kama vile watoto na baba.
John 1:14-15
Neno
Huu ni mfano ambao unamaanisha kwa Yesu. Yeye ndiye aliye mfunua Mungu alivyo.
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa cha Mungu.
amejaa neema
AT: "ambaye mara zote hufanya kwa wema kwa ajili yetu katika njia mbazo hatustahili."
yeye ajaye baada yangu
Yohana anaongea kuhusu Yesu. Neno "anakuja baada yagu" linamaanisha kwamba huduma ya Yohana ilikuwa tayari imeanza na huduma ya Yesu itaanza baadaya, baada ya Yohana.
ni mkuu kuliko mimi
"ni mkuu zaidi yangu" au" ni muhimu zaidi"
kwa sababu amekuwapo kabla yangu
Kuwa mwangalifu usitafsiri kwamba Yesu ni wa muhimu zaidi kwa sababu ni mzee kuliko Yohana. Yesu ni mkuu zaidi ya Yohana kwa sababu yeye ni Mungu Mwana, ambaye amekuwepo na kutawala juu ya vitu vyote pamoja na Mungu.
John 1:16-18
utimilifu
Huli neno linamaanisha kwa neema ya Mungu ambayo haina mwisho.
kipawa cha bure baada ya kingine
"baraka baada ya baraka"
aliye mwanadamu pekee, ambaye ni Mungu
Hii inaweza kumaanisha1)aliye Mungu wa wa pekee" au" 2) yeye aliye Mwana wa pekee,"
aliye katika kifua cha Baba
Neno "kifua" ni mfano . Hii inamaanisha kuwa Yesu ndiye aliye karibu na Baba" ikimaanisha ushusino wa karibu.
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.
John 1:19-21
Wayahudi walitumwa kwake kutoka Yerusalemu
Hapa mwandishi anatumia mfano. Neno "Wayahudi" limetumika kwa kuwakilisha "Viongozi wa Kiyahudi." AT:" Viongozi wa Kiyahudi waliwatuma kwake kutoka Yerusalemu.
Yeye alisema wazi, wala hakukana
Neno la pili linaeleza maneno hasi ambayo neno la kwanza linachokisema katika mtazamo chanya. Hii inasisitiza kuwa Yohana alikuwa akisema kweil.AT: "Aliwambia ukweli bila woga".
U nani?
AT: "U nani ni kama sio Masihi"? au " Nini kinachoendelea?" au " Unafanya nini."
John 1:22-23
Kiunganishi cha sentesi:
Johana anaendela kuongea na makuhani na walawi.
wakamwambia
"makuhani na Walawi wakamwambia Yohana>"
sisi...sisi
Makuhani na Walawi, sio Yohana.
Akasema
"Yohana akasema"
Mimi ni sauti aliaye nyikani
Neno "sauti" ni mfano ambao unamwakilisha Yohana na ujumnbe wake. AT: Mimi ni kama mtu ongea kwa sauti mbapo hakuna mtu yeyote anaweza kunisikia.
Inyosheni njiai ya Bwana
Hapa neno "njia" limetumika kama mfanoAT: Jiandae mwenyewe kwa ajili ya ujio wa Bwana kama vile ambavyo watu waandaavyo barabara kwa ajili ya ujio wa mtu muhimu.
John 1:24-25
Basi kulikuwa na mtu ametumwa kutoka kwa Mafarisayo
Haya ni habari ya nyuma kuhusu watu waliomuuliza Yesu kutoka kwa Mafarisayo.
John 1:26-28
Maelezo kwa jumla:
mstari wa 28 unatwambia habari za nyuma kuhusu mwanzo wa hadithi.
Huyu ndiye ajaye baada yangu
AT: " Atawahubiri baada ya mimi kuondoka"
Mimi sisitahili "kufungua gidamu ya viatu vyake
kazi ya kufungua viatu vyake " ambayo ni kazi ya mtumwa au mja kazi ni fumbo. Johana nasema kuwa hasitahili kumfanyia Yesu kazi hata ile ya chini kabisa liyofanywa na watumwa.
John 1:29-31
Mwanakondoo wa Mungu
Huuu ni mfano ambao unawakilisha Utimilifu wa dhabihu kamilifu ya Mungu. Yesu anaitwa "Mwanakondoo wa Mungu" kwa sababu alikuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi za watu.
dunia
neno "dunia" ni neno ambalo linalojumuisha watu wote duniani.
ajaye nyuma yangu, ni mkuu, kwa maana amekuwapo kabala yangu
Tafsili hili kama ulitafsiri 1:14:1:15
John 1:32-34
shuka
"shuka chini"
kama njiwa
hili ni neno lenye lugha ya picha . "Roho " anashuka chini kama vile ambavyo njiwa ashukavyo kwa mtu.
mbinguni
Neno "mbingu" linamaanisha "anga."
Mwana wa Mungu
Baadhi ya nakala za kifungu hiki husema "Mwana wa Mungu": wengine husema " mchaguliwa wa Mungu."
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
John 1:35-36
Tena, siku iliyofuata
Hii ni siku nyingine. Ilikuwa ni siku ya pili Yohana alipomwona Yesu.
Mwanakondoo wa Mungu
Huu ni mfano ni mfano ambao unawakilisha dhabihu timilifu. Yesu ni Mwanakondoo wa Mungu kwa sababu alidhabihiwa kulipa dhambia za watu.
John 1:37-39
muda wa saa kumi
Neno linaonyesha wakati wa mchana, kabla ya giza, ambao usinge ruhusu kusafiri kwenda katika mji mwingine, yawezekana 10 za jioni.
John 1:40-42
Maelezo kwa Ujumla:
Mistari hii utupa maelezo kuhusu Andrea na jinsi alivyomleta ndugu yake Petro kwa Yesu. Hii ilitokea kabla hajaenda mahali ambapo Yesu alikuwa akikaa.
mwana wa Yohana
Huyu ni Yohana Mbatizaji. " Yohana lilikuwa jina la kawaida.
John 1:43-45
Basi Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mji wa Andrea na Petro
Hii ni habari ya nyuma kuhusu Filipo.
John 1:46-48
Nathanaeli akamwambia
"Nathaneli akamwambia Filipo."
Je jambo jema laweza kutoka Israeli?
Neno hili lijitokeza kama swali kuonyesha msisitizo.AT: "Hakuna kitu kizuri kinaweza kutoka Nazarti."
ambaye ndani yake hakuna udanganyifu
Hili linaweza kusema katika mtazamo chanya. AT: "mtumkweli aliyekamilika."
John 1:49-51
Rabbi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni mfalme wa Israeli!
Nathanaeli anasema Yesu ni "Mwana wa Mungu" kwa sababu Yesu amjua Nathanaeli pasipo kukutana naye awali.
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.
Kwa sababu nilikuambia.. je unaamini?
Hili jibu linaonekana katika jinsi ya swali kuonesha msisitizo. unaweza kuifasili kama sentesi. AT: "Unaamini kwa sababu nilisema, nilikuona chini ya mtini'!
Amini, amini
Tafsiri hili jinsi ambavyo lugha yako inavyosisitiza kuwa kile kinachofuata ni kweli.
John 2
John 2:1-2
Maelezo kwa Jumla:
Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini. Mstari huu unaonyesha habari ya nyuma juu ya habari inavyoanza.
Siku tatu baadaye
Wafaasili wengi husoma hili kama siku ya tatu baada ya Yesu kumwiita Filipo and Nathanaeli kuja kwake. Siku ya kwanza inaonekana katika Yohana 1:35 na siku ya pili ni 1:43
Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa harusini
Hii inaweza kutamkwa kama tendaji. AT: " Mtu alimwalika Yesu na wanafunzi wake katika arusi."
John 2:3-5
Mwanamke
Hii inaa mweelezea Mariamu. Kama ni neno lenye ukakasi katika lugha yako kwa mwana kumwiita mama mwanamke, tumia neno jingine.
hiyo inanihusu nini?
Hili linaonekana katika muundo wa swali ili kuonesha msisitizo . unaweza kukuifasili kama sentensi. AT: " hii haimaanishi kufanya nami" au " usiniambie nini cha kufanya."
Muda wangu bado haujatimia
Neno "muda" ni neno ambalo inawakilisha kuwa tukio maalumu kwa Yesu kuonesha kwamba yeye ni Masihi kwa miujiza.AT: "Sio muda mwafaka kwangu kufanya matengo makuu."
John 2:6-8
nzio mbili hadi tatu
"lita 80 hadi 120." nzio moja lilikuwa was
hadi juu
hii inamaanisha "juu sana' au "iliyojaa kabisa."
mhudumiaji mkuu
Hii ina maanisha mtu aliye na mamlaka juu ya chakula na kinywaji.
John 2:9-10
(lakini watumishi waliochota maji walifahamu)
hii ni habari ya nyuma.
kulewa
kutokuweza kuelewa pombe ghali na isiyo ghali kwa sababu ya kunywa kiasi kingi cha kileo.
John 2:11
Viunganishi vy maneno:
Hii si mwenendelezo wa hadithi kuu, badala yake inashamilisha hadithi.
Kana
Jina la sehemu
akifunua utukufu wake
Hapa "utukufu" ni neno linaonesha nguvu za Yesu.
John 2:12
akateremka
Hii inamaanisha kwamba walisafiri kutoka sehemu ya mwinuko kuelekea bondeni. Kana in kusini magaharibi ya Kaperanaumu na iko juu.
ndugu zake
Neno "ndugu"linajumisha kaka na dada. Kaka na dada wa Yesu walikuwa wadogo kuliko alivyokuwa.
John 2:13-14
Maneno ya jumla:
Yesu na wanafunzi wake wanapanda kwenda Yerusalemu kwenye hekalu.
juu hadi Yerusalemu
Hii inamaasha kuwa walisafiri kutoka kwenye mwinuko kwenda chini. Yerusalemu imejengwa juu ya kilima.
ndani ya hekalu
inamaanisha sehemu ya nje ya hekalu mahali ambapo wasio wayahudi waliruhusiwa kuabudu.
wale waliouza
watu waliweza kununua hekaluni na kuwadhabihu kwa ajili ya kumuheshimu Mungu.
wabadili fedha
Mamlaka ya Kiyahudi iliitaji watu ambao walihitaji kununua wanyama kwa ajili ya dhabihu kubadilisha pesa zao kutoka kwa wabadilishaji wa fedha.
John 2:15-16
Basi
Neno hili linaonyesha tukio lililotokea kwa sababu ya kile kilichotokea mwanzoni. Katika hali hii, Yesu aliwaona wabadili fedha wamekaa katika hekalu.
Acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu soko
Yesu, Mwana wa Mungu, anawafukuza wafanyabiashara kutoka mahali palipoandaliwa kwa ajili ya ibada ya Baba yake, Mungu Baba, kumuheshimu.
nyumba ya Baba yangu
Haya ni maneno ambayo Yesu aliyasema yakimaanisha hekalu.
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.
John 2:17-19
iliandikwa
Hii inaweza kusema katika muundo wa kutenda. Kuna mtu alikuwa ameandika."
nyumba yako
Neno hili linamaanisha, nyumba ya Mungu.
maliza
Neno hili "maliza" linaelekeza kwenye "moto." Upendo wa Yesu kwa ajili ya hekalu ni kama moto unaowaka ndani yake.
ishara
Hili ni tendo ambalo linalothibitisha kuwa ni jambo la kweli.
mambo haya
Haya yanamaanisha matendo ya Yesu aliyokuwa kinyume na wabadili fedha ndani ya hekalu.
Livunjenihili hekalu, na nitaliinua baada ya siku tatu
Yesu anamaanisha mwili wake kama hekalu kwamba atakufana kwamba atakuwa mzima tena baada ya siku tatu. Lakini, ni muhimu kutafasili haya maneno kuwa yameelezwa kuelezea kuvunja na kujenga jengo. Yesu hawaamuru wanafunzi wake kuvunja jengo la hekalu.
nitaliinua
Hii inamaanisha "kujenga" au 'kurudisha"
John 2:20-22
Yohana 2: 20- 22
Maelezo ya jumla: ilichukuwa miaka arobaini na sita...utaijenga kwa siku tatu? Miaka arobaini na sita... siku tatu aliamini/ waliamini hii sentesi
John 2:23-25
Basi alikuwa Yerusalemu
Neno basi linatutambulisha katika tukio jingine katika hadithi
wakaalimini jina lake
Hapa "jina" ni neno linalowakilisha utu wa Yesu. "aminini" au "kuamini katika yeye."
ishara za maajabu
Miujiza inaweza kuitwa "ishara" kwa sababu yanatumiwa kama ushahidi kwamba Mungu ni mwenye nguvu ambaye aliye na mamlaka kamili juu ya dunia.
John 3
John 3:1-2
Maneno kwa Ujumla:
Nikodemo anakuja kumwona Yesu.
sasa
Neno hili lintumika hapa kutambulisha sehemu nyingine ya hadithi na kumtambulisha Nikodemo.
mjumbe
sehemu ya kundi
Halimashauli ya Wayahudi
hHalimashauli ya Kiyahudi inaitwa "Sanihedrini." Hili lilikuwa ndilo baraza muhimu kwa mabaraza yote ya Kiyahudi.
twafahamu
hapa "sisi" linajumuisha, likimaanisha tu kwa Nikodemo na wanachama wengine wa halimashauli ya Kiyahudi.
John 3:3-4
Kiunganishi cha sentesi:
Yesu na Nikodemo wanaendelea kuongea.
Amini, amini
Tafsiri haya kama ulivyotafsiri 1:49; 1:51.
zaliwa mara ya pili
"kuzaliwa kutoka juu" au kuzaliwa na Mungu."
ufalme wa Mungu
Neno "ufalme" ni mfano kwa utawala wa Mungu." 'Sehemu ambayo Mungu anatawala."
Je mtu anaweza kuzaliwa awapo mzee?
Nikodemo alitumia swali hili kusisitiza kwamba hili lisingelitokea. "Ni kweli mtu hawezi kuzaliwa tena wakati akiwa mzee!"
Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili ili azaliwe, je anaweza kufanya hivyo?
Pia Nikodemo anatumia swali hili kusisitiza imani yake kuwa imani yake kuwa kuzaliwa mara ya pili ni jambo lisilowezekana." Ni kweli, hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili!"
mara ya pili
"tena"au "mara mbili"
tumbo
sehemu ya tumbo la mwanamke ambapo mtoto hukulia.
John 3:5-6
amezaliwa kwa maji na kwa roho
kuna maana mbili: 1)"kubatizwa ndani ya maji na katika Roho" au 2)"kuzaliwa kimwili na kiroho"
Amini, amini
unaweza kufasiri mane haya kama yalivyotumika katika tafsiri za hapo mwanzo.
ufalme wa Mungu
Neno "ufalme" ni fumbo kwa ajili ya utawala wa Mungu katika maisha ya mtu.
John 3:7-8
Kiunganishi cha Sentesi:
Yesu anaendelea kuongea na Yesu.
Ni lazima uzaliwe mara ya pili
"unapaswa kuzaliwa kutoka juu"
upepo huvuma popote upendako
Katika lugha ya mwanzo, maneno. upepo na Roho ni maneno sawa. Mwongeaji anamaanisha upepo kama ni mtu. "Roho Mtakatfu ni kama upepo ambao unavuma popote upendapo."
John 3:9-11
Mambo haya yanawezekanaje?
hili ni swali mbalaga ambalo linalosisitiza sentesi. "Hii hawezekani!" au" Hili haliwezi kutokea!"
Wewe ni mwalimu wa Israeli na hauyajui mambo haya?
Hili ni swali mbagala ambalo linaonyesha msisitizo. "weweni mwalimu wa Israeli , na ninashangaa kwamba haufahamu maneno haya!"
Amini, amini
Tafsiri kama ulivyotafsiri.
twazungumza
Yesu aliposema "sisi' hakuwa anamjumuisha Nikodemo.
John 3:12-13
Kiunganishi cha Maneno:
Yesu anamjibu Nikodemo
mtawezaje kuamini kama nitawaeleza mambo ya mbinguni?
katika sehemu "wewe" ni umoja.
mtawezaje kuamini kama nikiwambiamambo ya mbinguni
"Hautaamini kama nikiwambia mambo ya mbinguni."
mbinguni
hii inamaanisha mahali ambapo Mungu anaishi.
John 3:14-15
Kama vile Musa alivyomwinua juu yule nyoka jangwani
hili ni fumbo baadhi ya watu "watainua" Yesu kama Musa alivyoinuliwa nyoka wa shaba katika jangwa.
Vivyo hivyo Mwana wa Adamu ni lazima ainuliwe juu
Jangwani ni sehemu kavu lakini hapa anamaanisha mahali walipotembea Musa na Waisraeli.
katika jangwa
Jangwani ni sehemu kavu, sehemu ya jangwa, lakini hapa wanamaanisha mahali ambapo Musa na Waisraeli walizunguka."
John 3:16-18
Mungu aliupenda ulimwengu
Neno "dunia" hapa ni neno linalojumuisha kila kitu duniani.
alipenda
hii ni aina ya upendo ambao unatoka kwa Mungu na unatakia mema wengine, hata kama mtu hanufaiki. Mungu mwenyewe ni upendo na ndiye chanzo cha upendo wa kweli.
mwana wa pekee
"mmoja na Mwana wa pekee"
kwa sababu Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu, bali ulimwengu uokolewe kwa yeye
maneno mawili yanaweza kuwa yanamaanisha na yametajwa mara mbili ili kwamba kusisitiza kwanza katika mtazamo hasi na chanya. Baadhi ya lugha inaweza kuonyesha msisitizo kwa namna nyingine. Kusudu la Mungu kumtuma Mwanae ni kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.
ahukumiwi
anachiwa huru
hukumu
adhibu
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.
John 3:19-21
Kiunganishi cha Sentesi:
Yesu anamaliza kumjibu Nikodemo.
nuru imekuja ulimwenguni
Neno "nuru" ni fumbo kwa kweli ya Mungu iliyofunuliwa katika Yesu. Dunia ni neno linalojumisha vitu vyote vilivyomo duniani. Yeye ambaye ni kama nuru ameifunua kweli ya Mungu kwa watu."
watu wakalipenda giza
"giza" ni fumbo linalomaanisha mahali ambapo hawajapokea nuru" ya ufunuo wa Mungu katika Kristo.
ili kwamba matendo yake yasiwe dhahili
inaweza kutamkwa katika muundo wa kutenda. "ili kwamba nuru isioneshe mambo ayafanyayo" au " kwamba ili nuru isifunue matendo yao.
matendo yake yaonekane wazi
Hili linaweza kutamkwa katika muundo tenda. " Watu wanaweza matendo yake" au "kila mtu aweze kuona mambo ahafanyayo.
John 3:22-24
Baada ya haya
Hii inamaanisha baada ya Yesu kuongea na Nikodemo.
Aenoni
Neno hili linamaanisha "chemuchemi."
Salimu
kijiji au mji ulio karibu na Mto Yorodani.
kwa sababu mahali pale kulikuwa na maji mengi
"kwa sababu kilikuwa na chemuchemi nyingi katika sehemu ile."
walikuwa wakibatizwa
hili linaweza kusemwa kwa muundo wa kutenda. '" Yohana alikuwa akiwabatiza " au " alikuwa akiwabatiza."
John 3:25-26
kukatokea malalamiko baina ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi
"Tena wanafunzi wa Yohana na Myahudi wakaanza kubishana.
kutoelewana
kugombana kwa maneno
tazama, anabatiza
Katika sentesi hii "tazama" ni amri ikimaanisha tilia manani!" " Tazama! Anabatiza" au " Tazama! anabatiza."
John 3:27-28
Mtu hawezi kupokea kitu chochote isipokuwa
"Hakuna mtu aliye na nguvu isipokuwa"
amepewa kutoka mbinguni
Neno "mbinguni" likimaanisha Mungu. Hili linaweza kuchukuliwa katika muundo tenda. " Mungu amempa."
ninyi wenyewe
ninyi ni kwa wingi na inamaanisha watu wote ambao Yohana anazungumza nao.
nimetuma mbele zake
"Mungu amenituma kufika kabla yake."
John 3:29-30
Viunganishi vya maneno:
Yohana Mbatizaji anaendelea kuongea.
Yeye aliye naye bibi harusi ndiye bwana harusi
Hapa bwana na "bibi" "arusi" ni mfano. Yesu ni kama "bwana arusi" na Yohana ni kama rafiki wa bwana arus." "bwana huoa bibi
Hii, tena, furaha yangu imetimilizwa
'' Hivyo tena ninafurahia sana" au nina furahia zaidi."
furaha yangu
hili neno "yangu" lina maanisha Yohana Mbatizaji , ndiye anayeongea.
Ni lazima aongezeke
anamaanisha bwana arusi, Yesu, ambaye ataendelea kuwa wa muhimu.
John 3:31-33
Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote
Yohana anaongea kuhusu Yesu. "Yeye ajaye kutoka mbinguni ni wa muhimu zaidi yeyote.
Yeye aliye wa chini ni wa chini na huongea mambo ya chini
Yohana anajipinga mwenyewe dhidi ya Yesu. hamaanishi kuwa kwa kuwa alizaliwa duniani ni mwovu. Ana maanisha kuwa Yesu ni mkuu kuliko yeye kwa sababu Yesu alitoka mbinguni na Yohana alizaliwa hapa duniani. "Yeye aliyezaliwa hapa duniani ni kama mtu yeyote na na anaishi na anaongea kuhusu kilichotokea duniani."
hakuna mtu apokeaye ushuhuda wake
Yohana anaongea kwa kuonyesha neno katika hali ya kulikuza neno kwamba ni watu wachache walimwamini Yesu. "Watu wachache walimwamini."
Yeye apokeaye ushuhuda wake
Aliye ina maanisha mtu. " Mtu yeyote anayeamini kile ambacho Yesu alikisema."
amethibitisha
"kuthibitisha" au "inakubaliana"
John 3:34-36
Kiiunganishi cha Sentesi:
Yohana Mbatizaji anamaliza kuongea."
Kwa maana yeye ambaye Mungu amemtuma "
Huyu Yesu, ambaye Mungu amemtuma kumwakilisha."
kwa kuwa hatoi Roho kwa kipimo
" Kwa sababu yeye ndiye ambaye Mungu amempa nguvu zote za Roho wake."
Baba...Mwana
Hiki ni cheo kinachoelezea uhusiano wake kati ya Mungu na Yesu.
amepewa...katika mikono yake
Hii ina maanisha kuwekwa katika nguvu zake au kuotawala.
Yeye aaminiye
"Mtu aaminiye" au "mtu yeyote aaminiye."
ghadhabu ya Mungu inamkalia
Nomino dhaniwa "ghadhabu" linaweza kufasiriwa kama kitenzi "adhibu." "Mungu ataendelea kumwadhibu."
John 4
John 4:1-3
Maelezo kwa Ujumla:
Huu ni sehemu nyingine ya simulizi ambayo inamuhusu Yesu na mwanake Msamalia. Mstari huu unatoa habari ya mwanzoni kwa ajili ya sehemu ya simulizi
Basi Yesu alipofahamu
Neno "sasa" limetumika hapa kuonyesha kusimama kidogo katika simulizi kuu. Hapa Yohana anaanza kuelezea sehemu mpya ya simulizi.
Yesu mwenyewe hakuwa anabatiza
Nomino hii mwenyewe inongeza msisitizo kwmba sio kwamba Yesu mwenyewe alikuwa akibatiza, bali wanafunzi wake.
John 4:4-5
eneo la
"sehemu ya ardhi" au "kipande cha ardhi"
John 4:6-8
Nipe maji
Hili ni ombi la upole, na sio amri.
John 4:9-10
Kisha mwanamke Msamalia akamwambia
Neno "akamwambia" linamaanisha Yesu.
Inawekanaje wewe uliye Muyahudi unaomba maji ya kunywa?
Hili neno linaonekana katika muundo wa swali kuonesha mshangao wa mwanamke kwa Yesu kuomba maji. "Siamini kama wewe uliye Muyahudi unamwomba mwanamke Msamalia maji!"
hamchangamani na
"hamchangamani na."
maji ya uzima
Yesu anatumia mfano "maji ya uzima" kumaanisha Roho Mtakatifu ambaye anafanya kazi ya kumbadilisha mtu na kuleta maisha mapya.
John 4:11-12
wewe si mkuu, je wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo... mifugo?
hili neno linaonekana katika muundo wa swali na kuonesha msisitizo, "wewe sio mkuu kama zaidi ya baba yetu... naYakobo... mifugo?
baba yetu yakobo
"babu yetu Yakobo"
alikunya maji ya kisima hiki
alikunywa maji yaliyoka katika kisima
John 4:13-14
atapata kiu tena
"atahitaji kunywa maji tena.""
maji nimpayo yatakuwa chemchemi ndani yake
Neno "chemchemi" ni fumbo kwa maji yatiayo uzima. "maji nitakayompa yatakua kama chemchemi ya maji ndani yake."
uzima wa milele
hapa "uzima" lina maanisha "uzima wa kiroho" ambao ni Mungu pekee anayeweza kutoa.
John 4:15-16
Bwana
katika mkitadha huu, mwanamke Msamalia anamwita Yesu "Bwana" ambayo ni neno la upole au unyenyekevu.
teka maji
"pata maji" au "vuta maji kutoka ndani ya kisima" kwa kutumia chombo na kamba
John 4:17-18
Umenena vyema... Katika hili umenena vyema
Yesu anarudia kauli hii kusisitiza kuwa anafahamu kuwa mwanamke anaongea ukweli.
John 4:19-20
Bwana
Katika mkitadha huu mwanamke Msamalia anamwelezea Yesu kama "Bwana," ambalo ni neno la heshima na upole.
Naona ya kuwa unabii
"Naelewa kuwa unabii."
mababa
Mababu wa zamani
John 4:21-22
niamini
Kumwamini mtu ni kukubali kuwa alichokisema ni kweli.
Ninyi mwaabudu msichokijua. Twaabudu kile tukijuacho
Yesu alimaanisha kuwa Mungu amajifunua na amri zake kwa Wayahudi, sio kwa Wasamalia. Kupitia maadiko Wayahudi wanajua Mungu ni nani kuliko Wasamalia.
Mtamwabudu Baba...kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi
Wokovu wa milele kutoka dhambini unatoka kwa Mungu Baba, ambaye ni Yaweh, Mungu wa Wayahudi.
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.
Kwa sababu wokovu watoka kwa Wayahudi
Hii haimaanishi kuwa Wayahudi watawaokoa wengine kutoka dhambini. Ina maanisha kuwa Mungu amewachagua Wayahudi kama watu maalumu ambao watakaowambia watu wengine kuhusu wokovu wake. "kwa sababu watu wote watafahamu wakovu wa Mungu kwa sababu ya Wayahudi.
John 4:23-24
Kiunganishi cha Sentesi:
kuabudu ka
Ingawa, saa inakuja, na sasa ipo, ambapo waabudu wa kweli wata
"Ingawa, huu ni wakati sahihi kwa waabudu w kweli."
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.
kuabudu katika roho na kweli
"kumwabudu katika njia sahihi."
John 4:25-26
Ninafahamu kwamba Masihi...Kristo
Haya maneno mawili yana maanisha "mfalme aaliyeahidia na Mungu."
atatwambia kila kitu
Haya maneno "atawambia kila kitu" yanamaanisha mambo yote ambayo watu wanahitaji kujua. "atatwambia kila kitu tunachohitaji kufahamu."
John 4:27
Wakati huo wanafunzi wake wakarudi
"wakati Yesu alipokuwa akiyasema haya wanafunzi wake walirudi kutoka mjini."
nao walikuwa wakishangaa kwa nini alikuwa akiongea na mwanamke
lilikuwa ni jambo la nadra kwa Muyahudi kuongea na mwanamke asiye mfahamu.
John 4:28-30
Njoni mumwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda
Hii ni hali ya kusema jambo dogo kwa kulikuza. Mwanamke Msamalia anavutiwa na Yesu na kwamba anaamini kuwa Yesu anawelewa mambo yote. "Njooni mumwone mtu anaye fahamu mengi zaidi kunihusu, pamoja kwamba sijawahi kukutana naye!"
Yamkini akawa ndiye Kristo, inawezakana?
Mwanamke hana uhakika kuwa Yesu ni Kristo, kwa hiyo anauliza swali ambalo linahitaji jibu la '"hapana" lakini anauliza swali badala ya kuweka sentesi kwa sababu anataka watu wenyewe waamue wenyewe.
John 4:31-33
Wakati wa mchana
"Wakati mwananamke alipokuwa akienda mjini"
Wanafunzi walikuwa wakimuuliza
"wanafunzi walikuwa wakimwambia Yesu" au wanafunzi walikuwa wakimtia moyo"
Ninacho chakula ambacho hamkijui
Hapa Yesu haongelei "chakula" bali anawaandaa wanafunzi wake kwa ajili ya fundisho la kiroho.
Hakuna mtu ambaye amemlea kitu chochote
Wanafunzi wanafikiri kuwa anaongelea chakula cha kawaida.Wakaanza kuulizana wakitegemea mwitikio wa hapana. Hakika hakuna mtu aliye mletea chakula tulipokuwa mjini!"
John 4:34-36
chakula changu ni kufanya mapenzi yake aliyenituma na kutimiza kazi yake
"Chakula" hapa ni lugha ya picha inayowakilisha "kutii mapenzi ya Mugu." Kama vile ambavyo chakula kinavyo mtoshelea mwenye njaa, kutii mapenzi ya Mungu ndich kinachonitosheleza."
Je hamsemi
'Je hii sio miongoni mwa misemo yenu maarufu"
tazameni mashamba, kwa sababu yako tayari kwa mavuno
maneno haya mashamba na mazao yaliyo tayari yana lugha ya picha. Mashamba yanawakilisha watu wa mataifa. Na neno wako tayari linamaanisha utayari wa watu wa mataifu wa kupokea ujumbe wa Yesu kama vile mashamba yalivyo tayari kwa kuvunwa. "tazameni hawa watu wa mataifa!wako tayari kupokea ujumbe wangu, kama vile mazao katika mashamba yalivyo tayari kwa ajili ya kuvunwa."
Yeye avunaye anapokea posho na hukusanya matunda kwa uzima wa milele
Yesu anaonyesha kuwa kuna tuzo kwa wale "wanaofanya kazi katika mashamba" na kuwashirikisha ujumbe wake wengine. Na yule atakaye pokea ujumbe atapokea pia uzima wa milele ambao Mungu anawapa watu.
John 4:37-38
Kiunganishi cha Sentesi:
Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake.
Mmoja hupanda na mwingine huvuna
Maneno "kupanda" na kuvuna ni maneno ya lugha ya picha. Yeye anayepanda anashirikisha ujumbe wa Yesu. Yeye anayevuna anawasaidia watu kupokea ujumbe wa Yesu." Mtu mmoja hupanda mbegu, na mwingine huvuna mazao."
ninyi wenyewe mmeingia katika kazi zao
ninyi wenyewe hutia msisitizo kwa neno "wewe" tafsiri hili katika lugha yako katika namna ya kumsisitiza mtu.
John 4:39-40
muamini katika yeye
"Kuamini katika" maana yake ni "kuamini katika" huyo mtu. Hapa pia ina maanisha kuwa waliamini kuwa alikuwa Mwana wa Mungu.
ameniambia mambo yangu yote niliyofanya
hili ni hali ya kuelezea jambo dogo katika hali kulifanya jambo kuwa kubwa zaidi ya lilivyo. Mwanamke alivutiwa sana na Yesu na akahisi kuwa lazima akuwa anajua kila kitu kumuhusu yeye. "Ameniambia mambo mengi kuhusu maisha yangu."
John 4:41-42
neno lake
"Neno" hapa lina sisimama kwa kumaanisha ujumbe ambao Yesu alihubiri. "ujumbe wake"
ulimwengu
ulimwengu hapa unasimama kwa kumaanisha watu wote wanaoishi duniani. "Watu wote wanaoishi duniani."
John 4:43-45
Maelezo kwa Ujumla:
hii ni sehemu ya simulizi ambayo Yesu anatelemka kwenda Galilaya na anamponya kijana.Mstari 44 inatupa habari kuhusu kitu ambacho Yesu alikuwa amekisema mwanzoni.
Kwa kuwa Yesu mwenyewe alitangaza
yeye mwenyewe limeongezwa kwa kutia msisitizo kwamba Yesu alikuwa ametangaza" au alisema haya.. Unaweza kuliweka katika lugha kwa jinsi ya kutia msisitizo kwa mtu.
nabii hana heshima katika nchi yake
Watu haonyeshi heshima au kumuhesimu nabii wa nchi ya kwao" au "nabii haheshimiwi na watu wa jamii yake."
kwenye sikukuu
sikukuu hapa ni Pasaka.
John 4:46-47
Sasa
Neno hili linaonyesha ukomo wa masimulizi na kuhamia sehemu nyingine ya simulizi. kama katika lugha yako kuna jinsi ya kuweka hili unaweza kuweka.
afisa
mtu ambaye yuko katika huduma ya mfalme
yuko katika hali ya kufa
"kuwa katika hali kufa."
John 4:48-50
ninyi hamwezi kuamini hadi mwone ishara na maajabu
Msipo...hamwe kuamini" ni mashaka hasi. Katika lugha nyingine hili linatafsiriwa katika mtazamo chanya. "Mtaamini tu pale mtakapoona miujiza."
kuliamini neno
Hapa "neno" lina maanisha ujumbe ambao Yesu alioutoa. "amini ujumbe."
John 4:51-52
Wakati
hili neno limetumika kuonesha matukio mawili ambayo yanatokea kwa wakati mmoja. Afisa alipokuwa akienda nyumani, wafanya kazi wake wakimpokea njiani.
John 4:53-54
Kwa hiyo akaamini yeye na nyumba yake yote
yeye mwenyewe imetumika kusistiza neno "yeye" kama katika lugha yako una namna ya kusema unaweza kufikiri namna ya kutumia.
Ishara
Miujiza inaweza kuitwa "ishara" kwa sababu yametumika kama kiilelezo cha ushahidi kuwa Mungu ni mwenye nguvu zaidi na aliye na mamlaka juu ya dunia.
John 5
John 5:1-4
Maneno kwa Ujumla:
hili ni tukio linalofuata katika simulizi,ambalo Yesu anapanda kwenda Yerusalemu na anamponya mtu.Mistari hii inatoa mambo ya nyuma kuhusu mwanzoni mwa simulizi.
Baada ya hili
ina maanisha baada Yesu kumponya mwana wa afisa. ona namna ambavo unaweza kufasiri hili.
kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi
"Wayahudi walikuwa wakisherehekea sikukuu"
alipanda kwenda Yerusalemu
Yerusalemu iko juu ya kilima. Mabarabara ya Yerusalemu yalipanda juu na kutelemka katika vilima vidogo . Kama lugha yako ina neno tofauti kwa kupanda juu ya kilima kuliko kuliko kutembea katika tambarare unaweza kuitumia hapa.
dimbwi
hili lilikuwa ni shimo chini ambalo watu walijaza maji. Wakati mwingine walilizungushia kwa vigae na mawe.
Bethzatha
"Bethzatha" maana yake ni nyumba ya huruma.
matao
muundo ulioezekwa angalau pasipo kuwa ukuta mwingine katika jengo.
Idadi kubwa ya watu
"watu wengi"
John 5:5-6
Maelezo kwa Ujumla:
Mstari wa 5 unatambulisha mtu amelala pembeni mwa dimbwi la simulizi.
kulikuwa
"Kulikuwa kwenye dimbwi la Bethzatha"
amekuwa hawezi
"amepoza"
miaka thelathini na minane
miaka minane - miaka 38
akatambua
"alifahamu" au "alipata kuelewa"
akamwambia
"Y esu akamwambia yule mtu aliye poza"
John 5:7-8
Bwana, sina
hapa neno "Bwana" ni namna ya kumkabili mtu wa upole. "Bwana, hakuna mtu"
wakati maji yanapotibuliwa
Hii linaweza kufasiriwa katika muundo tendaji. "wakati malaika hutibua maji"
ndani ya dimbwi
hili lilikuwa ni shimo katika chini ambalo watu walijaza maji. wakati mwingine walilizungushia kwa vigae na mawe.
mwingine huenda mbele yangu
watu walishuka kwa hatua kadhaa kuingia ndani ya maji. "mtu mwingine mara zote huingia ndani ya maji kabla yangu.
Inuka
"simama!"
chukua kitanda chako na uende
"Chukua godor lako la kulalia, na utembee!"
John 5:9
mtu aliponywa
"mtu alikuwa na afya tena"
Sasa
Neno "sasa" limetumika hapa kwa ajili ya Yohana kutoa historia ya nyuma kwamba tukio hili linatukia siku ya Sabato.
John 5:10-11
Basi
hili neno linaonyesha tukio ambalo lilitokea kwa sababu ya kitu fulani kutokea. Katika hili Yesu alikuwa
Yeye aliye nifanya kuwa mzima
"Mtu aliye nifanya mzima."
John 5:12-13
Wakamuuliza
"Viongozi wa Kiyahudi wakamuuliza mtu aliyeponywa"
John 5:14-15
Yesu akampata
"Yesu alimpata mtu aliye mponya
Tazama
"Tazama" au "Sikiliza" au "Tilia manani kile ninachokueleza"
John 5:16-18
Basi
'Basi" linamwonesha Yohana anatoa kwa ufupi kuhusu tabia za viongozi wa Kiyahudi kwa Yesu.
kazi
Hii ina maanisha shughli au kitu chochote kinachofanywa kuwatumikia watu.
akijifanya yeye kuwa sawa na Mungu
"sema kwamba alikuwa sawa na Mungu"au kusema kwamba alikuwa na mamlaka makuu kama Mungu"
Baba yangu
Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu
John 5:19-20
Kiunganishi cha sentesi:
Yesu anaendelea kuongea na viongozi wa Wayahudi.
Amini, amini
Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri 1:49; 1:51
mtashangazwa
"mtashangazwa" au mtasitushwa"
chochote anachofanya Baba, Mwana anayafanya haya mambo pia. Kwa Baba anampenda Mwana
Yesu, kama Mwana wa Mungu, alifuata na kutii uongozi wa Baba yake chini ya nchi kwa sababu Yesu alijua Baba anampenda.
Mwana...Baba
Hivi ni vyeo muhimu ambavyo zinaelezea uhusiano kati ya Yesu na Mungu.
penda
aina hii ya upendo unatoka utokao kwa Mungu unajali mazuri ya wengine, hata kama haina faida yake. Mungu mwenyew ni upendo na chanzo cha upendo wa kweli.
John 5:21-23
Kama vile Baba afufuavyo wafu na kuwapa uzima...Mwana pia humpa uzima kwa yeyote apendaye
Neno "kwa" ni linganifu Mwan wa Mungu (Mungu Mwana) anatoa maisha kama Mungu Baba anavyotoa uzima.
Baba...Mwana
Hivi ni vyeo ambavyo vinaelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu.
uzima
ina maanisha "uzima wa kiroho."
Kwa kuwa Mwana Baba hamhukumu mtu yeyote, bali amempa Mwana uwezo wote wa kuhukumu.
Neno "kwa" linaonesha ulinganifu. Mwana wa Mungu ndiye anayehukumu kwa niaba ya Mungu Baba.
mheshimu Mwana kama ...Baba. Yeye amuheshimu Mwana hamheshimu Baba
Mungu Mwana ni lazima aheshimiwe na kuabudiwa kama vile ambavyo Mungu Baba. Kama tukishindwa kumuheshimu, pia tunashindwa kumuheshimu Mungu Baba.
John 5:24
Amini, amini
Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri
hatahukumiwa bali
"atahukumiwa kuwa hana hatia na"
John 5:25
Amini, amini
Tafsiri hii kama ulivyotafsiri mahali pengine pa "amini, amini."
wafu wataisikia sauti yangu,Mwana wa Mungu, na wao waisikiao watakuwa hai
Sauti ya Yesu , Mwana wa Mungu, itawafufua wafu kutoka makaburini.
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.
John 5:26-27
Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana ili awe na uzima ndani yake
Neno "kwa" linaonyesha ulinganifu. Mwana wa Mungu ana uzima sawa kama aliona nao Baba.
Baba...Mwana wa Adamu
Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea ushirika kati ya Mungu na Yesu.
uzima
hii ina maanisha uzima wa kiroho
Baba amempa Mwana Mwana uwezo kufanya hukumu
Mwana wa Mungu ana mamlaka ya Mungu Baba kuhukumu.
John 5:28-29
sikia sauti yake
"sikia sauti ya Mwana wa Adamu"
John 5:30-32
kutofanya chochote kutoka
Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri 5:19
mapenzi ya aliyenituma mimi
Neno "aliye" lina maanisha Mungu Baba
John 5:33-35
ushuhuda ninao pokea sio wa mwanadamu
"Sihitaji ushuhuda wa watu"
okolewa
Hii ina maanisha "kuokolewa" ni katika maana ya kiroho. Kama mtu amekwisha "akolewa" ina maanishakwambaMungu amekwisha msamehe na kumuokoa kutoka katika adhabu ya Jehanamu kwa ajili ya dhambi zake.
Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara
Yohana anonesha utakatifu wa Mungu kama vile ambavyo taa itoavyo mwanga.
John 5:36-38
kazi alizonipa Baba kuzitimiliza ...zinashuhudia...kuwa Baba amenituma
Mungu Baba amemtuma Mungu Mwana, Yesu, Mwana wa Mungu, duniani. Yesu anatimiza kile ambacho Baba amempa kufanya.
Baba
Cheo muhimu kwa Mungu
hamana neno lake...ndani yenu, kwa sababu hamumwamini yeye aliyemtuma
"Hamuamini katika yeye aliyetumwa. Hivi ndivyo ninavyofahamu kuwa hamna neno lake ndani yenu." Kumjua Mungu wa kwelikatika Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye Baba amemtuma. Maneno "Baba" na "Mwana" lazima yatafsiriwe katika utambulisho ambaye ni lazima tuamini.
likikaa ndani yenu
"kukaa pamoja nanyi
John 5:39-40
ndani yao mna uzima wa milele
"mtapata uzima wa milele kama mtasoma maandiko" au "maandiko yatakwambia namna mtakavyo pata uzima wa milele."
Ili mpate uzima
"uzima" hapa ina maanisha "uzima wa milele."
John 5:41-42
pokea
"pokea"
hamna upendo wa Mungu ndani yenu
Hii ina maanisha 1)"kweli kabisa hamumpendi Mungu" au 2)"kweli hamjapokea upendo wa Mungu."
John 5:43-44
katika jina la Baba yangu
Hapa neno "jina" lina maanisha mamlaka na nguvu za Baba.
Baba
Cheo muhimu kwa Mungu.
pokea
"pokea"
mtawezaje kuamini, ninyi ambao hupokea ...Mungu?
"Hakuna namna mnaweza kuamini kwa sababu mnapokea sifa... Mungu!"
amini
hii ina maanisha kuamini katika Yesu.
Nimekuja kwa jina la Baba yangu...kutoka kwa Mungu pekee
Yesu amekuja duniani kwa jina la Mungu Baba, Mungu pekee.
John 5:45-47
Yupo mwingine ambaye anawashitaki
Mungu alitoa sheria, ili kwamba mahitaji ya agano, kwa Israeli kupitia Musa. Hiki ndicho Wayahudi walimaanisha walipokuwa wakisema, "Musa alitupa sheria."Lakini kwa Waisraeliambao hawakutii sheria, Yesu alimaanisha kuwa Musa angewa shitakikwa kutokutii. Lakini "Musa" anasimama hapa kwa niaba ya sheria yenyewe.
matumaini yenu
"ujasiri wenu'
kama hamyaamini maandiko yake, mtawezaje kuamini maneno yangu?
"Hamuamini maandiko , hivyo hamtaamini maneno yangu!"
maneno yangu?
"Ninachosema?"
John 6
John 6:1-3
Maelezo ya Jumla:
Hii ni sehemu ya pili ya simulizi. Mkutano ulikuwa umemfuata Yesu juu ya mlima. Mistari hii inazungumzia mahali ambapo simulizi inaanzia.
Baada ya mambo haya
Neno " haya mambo" ina maanisha matukio katika. "wakati mwingine baadaye."
Yesu akaenda zake
"Yesu akaenda mahali" au "Yesu kasafiri"
John 6:4-6
Maelezo kwa UJumla:
kitendo katika simulizi kinaanza msitari wa 5.
(Pasaka, sikukuu ya Wayahudi ilikuwa karibu.)
Yohana kwa ufupi anaacha kuongea kuhusu matukio katika simulizi ili kwamba alete hisotia ya nyuma kuhusu lini tukio lilitokea.
(Basi Yesu alisema maneno haya ili kumjaribu Filipo, kwa sababu yeye mwenyewe alifahamu atakachokifanya.)
kwa ufupi Yohana anaacha kuongea kuhusu matukio katika simulizi ili kwamba afafanue kwa niniYesu alimuuliza Filipo mahali pa kunua mkate.
Kwa sababu yeye mwenyewe alifahamu
Neno "mwenyewe" hapa linaweka wazi kwamba neno "yeye" lina maanisha Yesu.Yesu alifahamu nini angefanya.
John 6:7-9
ya thamani ya dinari
" Mikate ambayo inagharimu mshahara wa siku mia mbili." Dinari ni wingi wa "dinari nyingi."
mikate ya shayili
mkate mdogo wa mvilingo uliotengenezwa kwa nafaka ya kawaida.
Hii itafaa nini kwa watu wengi?
hii"silesi chacheya mikate na samaki haitoshikulisha watu wengi."
John 6:10-12
kaa chini
au "kaa chini" tegemea na desturi yako
(Basi kulikuwa na nyasi nyingi katika sehemu ile.)
Hii ilikuwa ni sehemu nzuri kabisa kwa ajili ya watu kukaa.
watu... wanaume... watu
Mkutano
elfu tano kwa idadi
wakati mkutano pengine ulijumuisha wanawake na watoto.
akashukuru
Yesu aliomba kwa Mungu Baba na kumshukuru kwa ajili ya mkate na samaki.
aliwagawia
Yesu aliivunja mikate na samaki akawapitishia wanafunzi wake. Kisha wanafunzi wakawapitishia watu mikate na samaki.
John 6:13-15
Maelezo ya Jumla:
Yesu anajitoa katika mkutano. Hii ni sehemu ya mwisho ya simulizi kuhusuYesu kuwalisha mkutano juu ya mlima.
wakakusanyika
"Wanfunzi wakakusanya"
wakaacha
chakula ambacho hakuna mtu aliye amekila
ishara hii
Yesu anawalisha watu 5000kwa mikate mitani ya shairi na samaki wawili.
John 6:16-18
Kiunganishi cha Maneno:
ili ni tukio linalofuata katika simulizi;wanafunzi wa Yesu wanaenda ziwani.
(wakati giza lilikuwa limeingia, na Yesu alikuwa bado hajaenda kwa wanafunzi.)
Tumia lugha yako jinsi ya kuonesha hii ni habari ya nyuma ya habari.
John 6:19-21
wanafunzi wake wakuwa wamepiga makasia
kwa kawaida mitumbwi ilikuwa na watuwawili, au sita watu waliopiga makasia kwa pamoja. Mila yako inaweza ikawa na namna nyingine ya kusababisha mtumbwikukatisha katika maji mengi .
kama makasia ishirini na matanoau thelathini
tano au makasia sita "kama kilometa tano au sita." kasia ni kama makasia, mita 185.
John 6:22-23
bahari
Bahari ya Galilaya
(Ingawa, palikuwa... Bwana aliposhukuru)
tumia lugha yako kuonesha kuwa hii ni habari ya nyuma.
mitumbwi iliyokuja kutoka Tiberia
siku iliyofuata baada ya Yesu kuwalisha watu, baadhi ya mitumbwi kutoka Tiberia ilikuja na watu ili wamwone Yesu.Ingawa, Yesu na wanafunzi wake walikuwa wametoka usiku mmoja kabla.
John 6:24-25
Maelezo ya Jumla:
mkutano unaanza kumuuliza Yesu maswali
John 6:26-29
Amini, amini
tafsiri hili kama ulivyo tafsiri mengine kama haya maneno.
uzima wa milele ambao Mwana wa Adamu atawapa ninyi, Mungu Baba ametia muhuri juu yake
Baba amfanya uthibitisho wake kwa Yesu, Mwana wa Adamu na Mwanawa Mungu, kutoa uzima wa milele kwa wale wanao amini katika yeye. Baba na Mwana wamekwisha timiza msamaha wa milele na uzima.
Mwana wa Adamu, Mungu Baba
Hivi ni vyeo muhimu ambavyo zinaelezea uhusiano kati Mungu na Yesu.
ametia muhuri juu yake
"ametia muhuri" juu ya kitu maana yake kuweka alama juu yake kuonesha ina milikiwa na.Hii ina maana kuwa Mwana anatokana na Baba.
John 6:30-31
mababa
"mababa wa zamani"
mbingu
Ina maanisha sehemu ambayo Mungu huishi
John 6:32-34
Amini, amini
Tafsiri hili kama ulivyo tafsiri maneno kama haya.
Baba yangu ndiye awapaye mkate wa kweli kutoka mbinguni
Baba anatupa "mkate wa kweli" kutoka mbinguni, Mwanae Yesu. Pamoja Baba na Mwana pamoja na Roho Mtakatifu wanawapa watu maisha ya kimwili, kiroho na maisha ya milele.
Baba yangu
Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.
mkate wa kweli
Yesu anajilinganisha na mkate. Kama vile mkate uliyo muhimu kwa ajili ya maisha yetu ya mwili, Yesu ni wa muhimu kwa ajili ya maisha yetu ya kiroho.
uzima
hili lina maanisha uzima wa kiroho.
John 6:35-37
Mimi ni mkate wa uzima
Yesu anajifananisha na mkate. Kama vile mkate ulivyo muhimu kwa maisha yetu ya mwili, Yesu ni wa muhimu kwa maisha yetu ya kiroho.
aaminiye katika
Hii ina maanisha kuaminia kuwa Yesu ni Mwan wa Mungu, kumtegemea kama mwokozi, na kuishi katika namna ambayo ina mpendeza.
Wale wote anipaye Baba watakuja kwangu
Mungu Baba na Mungu Mwana ni washirika katwa milele kwa wale wanao mwamini Yesu, Mwana wa Mungu.
Baba
Cheo muhimu kwa Mungu.
Yeye ajaye kwangu sitamtupa kamwe nje
"Nitamtunza kila mmoja ambaye ajaye kwangu.
John 6:38-40
Kiunganishi cha Maneno:
Yesu anaendelea kuongea na mkutano
yeye aliyenituma
"Baba yangu, aliyenituma mimi"
nisimpoteze hata mmoja
"Niwatunze wote"
mapenzi ya Baba yangu...kila amtazamaye
Yesu anafafanua kwamba Mpango wa Baba unatoauzima wa milele kwa walew wanaoamini " Mwana,"Mwana wa Mungu, Yesu Kristo atakaye fufua na kutukuza miili ya wote wanao amini.
Mwana na kuamini katika yeye awe na uzima wa milele
Yesu anafafanua kwamba mpango wa Mung unaleta uzima wa milele kwa wale wote wanao mwanini "Mwana," Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye atakaye wafufua na kutukuza miili ya wale wanaoamini.
John 6:41-42
Kiunganishi cha Maneno:
Viongozi wa Wayahudi wanaingilia kati wakata Yesu anaongea na mkutano.
nung'unika
Kuongea katika hali ya kutokuwa na furaha
Mimi mkate wa uzima
Tafsiri hii kama ulivyotafsiri 6:35
John 6:43-45
kiunganishi cha maneno:
Yesu anaendela kuongea na mkutano na sasa anaongea na viongozi wa Wayahudi.
kuvuta
hii inaweza kufasiriwa 1) "kuvuta" 2)"kuvutia"
imeandikwa katika manabii
"Manabii waliandika"
Kila aliyekwisha sikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu
Wayahudi walifikiri Yesu alikuwa mwana wa Yusufu" lakini ni Mwana wa Mungu kwa sababu Baba yake ni Mungu Baba , sio Yusufu. Wale wote ambao kweli wanajifunza kwa Mungu Baba wanaamini katika Yesu, Mungu Mwana.
Baba
Cheo muhimu kwa Mungu.
John 6:46-47
kinganishi cha maneno
Yesu anaendelea kuongea na mkutano na viongozi wa Wayahudi.
Amini, amini
Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri maneno mengine ya namna hii.
hakuna mtua yeyote aliyemwona, isipokuwa yeye aliyetoka kwa Mungu
Ingawa hakuna mwadamu aishie katika dunia amemwona Mungu Baba, Yesu, Mwana wa Mungu, amemwona Baba.
Baba
Cheo muhimu kwa mungu.
yeye aaminiye ana uzima wa milele
"uzima wa milele" umeunganishwa katika Yesu, Mwana wa Mungu.
John 6:48-49
Mimi ni mkate wa uzima
Tafsiri hii kama ulivyotafsiri maneno yanayofanana na haya.
mababa
"mababa wa zamani"
kufa
hii ina maanisha kifo cha kimwili.
John 6:50-51
Huu ni mkate
tazama notisi 6:35
hakuna kufa
"ishi milele." hapa neno "kufa" lina maanisha kifo cha kiroho.
mkate wa uzima
Hii ina maanisha" mkate ambao una sababisha watu kuishi"
John 6:52-53
Kiunganishi cha maneno
Baadhi ya Wayahudi waliopo wanaanza kubishana wenyewe na Yesu anajibu kwa swali lao.
Amini, amini
tafsiri hili kama ulivyo tafsiri maneno mengine ya namma hii.
kula mwili wa Mwana Adamu na kunywa damu yake
Kumpokea Mwana wa Adamukwa imani ni sawa kupokea chakula na kinywaji.
John 6:54-56
Kiunganishi cha Sentesi:
Yesu anaendelea kuongea kwa wote wanao msikiliza.
chakula cha kweli... kinywaji cha kweli
Kumpokea Yesu kwa imani kunaleta uzima wa milele kama vile ambavyo chakula na kinywaji vinavyoawilisha mwili.
John 6:57-59
Baba mwenye uzima
Hii inaweza 1) "Baba atoaye uzima" au "Baba aishie," kama watu au wanyama wanavyoishi, kinyume cha "kifo"
Baba
hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.
Baba mwenye uzima alinituma...kwa sababu ya Baba...yeye anilaye...ata...ishi kwa sababu ya
Yesu alitumwa na Baba, na anaishi kama mwanadamu kwa sababu ya Mungu Baba. Kama Mungu Mwana alivyotumwa na Mungu Baba, Yesu ni chanzo cha uzima wa milele.
mababa
"mababa wa zamani"
Yesu aliyasema mambo haya ndani ya Sinagogi... huku Kaperanaumu
hii ni babari ya nyuma kuhusu wakati tukio hili lilipotukia.
John 6:60-61
ni nani awezaye kulipokea?
"hakuna mtu anaweza kulipokea." au "halipokeleki."
Je hili lina kukwaza?
"Nin shangazwa kwamba hili lina wakwaza!"
linakukwaza wewe
"linakusababisha kukata tamaa kwa imani yako"
John 6:62-63
Basi ni vipi kama mkimwona Mwana wa Adamu akishuka kutokakule aliokuwa kabla?
"Labda mtaamini ujumbe wangu kama mkiniona, yeye aliye kuja kutoka mbinguni, akishuka kule nilikokuwa kabla!"
faida
Hii ina maanisha kusababisha vitu vizuri kutokea.
maneno
"Ujumbe" Pengine maana: 1) maneno yake ndani au 2) kila kitu anachofundisha.
maneno niliyokuambia wewe
"Nilichowambia"
roho
Maana zinazo wezekana ni 1)Roho Mtakatifu au2) vitu vya kiroho.
ni roho, na ni uzimaa
maana dhaniwa 1)"karibia Roho na uzima wa milele" au "kutoka kwa Roho na inatoa uzima wa milele" au 3)" ni kuhusuvitu vya kiroho na uzima."
John 6:64-65
hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba
Mwana wa Mungu, amepewa na Baba. Mungu Baba na Mungu Mwana kwa pamoja ni njia katika wokovu msamaha wa milele. Yeyote atakaye kuamini ni lazima aje kwa Mungu kwa kupitia Baba na Mwana.
njoo kwangu
"nifuate mimi"
Baba
hiki ni cheo muhimu kwa Mungu
John 6:66-69
wanafunzi wake
"wanafunzi wake" hapa ina maanisha jumuisho ambao walimfuata Yesu.
kumi na wawili
Hili kundi maalumu ya wanaume 12 walio mfuata Yesu kwa huduma yake yote. Hii inaweza kufasiriwa "wafuasi kumi na wawili."
John 6:70-71
Je mimi sikuwachagua, ninyi kumi na wawili, na mmja wenu ni shetani?
"mwenyewe niliwachagua wote, lakini mmoja wenu ni mtumishi wa shetani."
John 7
John 7:1-2
Na baada ya mambo haya
"Na baada ya kumaliza kuongea pamoja na wanafunzi"
Safiri
"tembea"
John 7:3-4
ndugu
Hili linaelekeza kwa ndugu zake halisi, wana wa Mariamu na Yusufu.
Ulimwengu
"Watu wote" au "kila mmoja"
John 7:5-7
kaka zake
kaka zake wadogo
Wakati wangu bado haujafika
Yesu anamaanisha kuwa wakati muafaka bado haujafika kwa ajili ya huduma yake
John 7:8-9
Hawa
wingi
John 7:10-11
Naye vile vile alienda
Yerusalemu ilikuwa upande wa juu kutoka pale walipokuwa
Siyo kwa wazi bali kwa siri
Mafungu haya mawili yana maanisha jambo moja, iliyorudiwa kwa kuweka mkazo. Lugha zingine huweka mkazo kwa njia tofauti.
John 7:12-13
Hofu
Hili huchukuliwa katika hisia zisizokuwa za furaha wakati ambapo kuna utisho wa kuumizwa kwake au wengine.
John 7:14-16
Kwa jinsi gsni mtu huyu anajua mengi hivi?
"Haiwezekani akajua mengi juu ya maandiko."
Ni yeye aliyenituma
Neno "yeye" linamhusu Mungu Baba.
John 7:17-18
Lakini yeyete atafutaye utukufu wake aliyenituma, mtu huyo ni wa kweli na ndani yake hakuna kutokutenda haki.
"lakini ninafanya mambo ili kwamba wengine wapate kumheshimu yeye aliyenituma, nami ni yule asemaye kweli. Sidanganyi kamwe."
John 7:19-20
Musa hakuwapa ninyi sheria?
"Ni Musa aliyewapa ninyi sheria."
Kwa nini mnataka kuniua?
"Mnatafuta kuniua."
Una pepo
"Wewe ni kichaa."
Nani anataka kukuua?
"Hakuna yeyote anayetaka kukuua."
John 7:21-22
Kazi moja
"Muujiza mmoja" au "ishara moja"
(Siyo kwamba inatoka kwa Musa, lakini inatoka kwa mababa)
Hapa mwandishi anatoa maelezo ya nyongeza.
John 7:23-24
Kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima katika siku ya Sabato"
"Hamkupaswa kunikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima siku ya Sabato."
John 7:25-27
Siye huyu wanayemtafuta kumwua?
"Huyu ni Yesu wanayemtafuta kumwua."
John 7:28-29
Ninyi nyote mnanijua na mnajua ninakotoka
"Ninyi" iko katika wingi.
Ni kweli
"Ni shahidi wa kweli."
John 7:30-32
Kristo atakapokuja, atafanya ishara zaidi ya hizi anazofanya mtu huyu?
"Kristo atakapokuja hataweza kufanya ishara zaidi ya hizi ambazo mtu huyu amefanya."
Ishara
"Hii inamaanisha miujiza inayothibitisha kuwa yeye ni Kristo."
John 7:33-34
Yeye aliyenituma
Mungu Baba
John 7:35-36
Mtawanyiko
Wayahudi sehemu mbali mbali katika ulimwengu wa Wagiriki, nje ya Palestina.
John 7:37-38
Sasa
Neno "sasa" linatumika hapa kuonyesha mkato ndani ya mstari mkuu wa hadithi.
Siku kubwa
Ni "kubwa" kwa sababu ni ya mwisho, au muhimu zaidi siku ya sikukuu.
Ikiwa yeyote ana kiu
Hii inamaanisha hamu ya mambo ya Mungu, kama vile mwingine anavyoweza kuwa na hamu au "kiu" kwa maji.
Na aje kwangu anywe.
Neno "yeye" maana yake "yeyote." Neno "kunywa" hapa linawakilisha utimilifu wa kiroho katika Kristo.
Maandiko
Hapa "maandiko" linasimama kwa unabii wa Masihi kuhusiana na Kristo. Hii siyo nukuu ya moja kwa moja kutoka fungu lolote maalum la Agano la Kale.
kutiririka ito ya maji ya uzima
Kristo atatoa pumziko la "kiu" ya kiroho kwa watu katika kiwango kikubwa kwamba itatiririkia nje kumsaidia kila aliyepo kama
Maji ya uzima
Hii inamaanisha 1) "maji yatoayo uzima" au "maji yanayowafanya watu kuishi au 2) maji ya asili yatiririkayo kutoka kwenye chemchemi, iliyotofautishwa na maji yatokayo kisimani.
John 7:39
Lakini yeye
"Yeye" inamaanisha Yesu
John 7:40-42
Nini, Kristo anaweza kutokea Galilaya?
"Kristo hawezi kutoka Galilaya."
Maandiko hayasemi kwamba Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji alichokuwa Daudi?
"Maandiko yanafundisha kwamba Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa."
Maandiko hayajasema?
"Manabii waliandika katika maandiko."
John 7:43-44
Kukainuka mgawanyiko
Makutano hawakuweza kukubaliana juu ya nani au Yesu alikuwa nani.
Lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono juu yake
"Lakini hakuna aliyemkamata."
John 7:45-46
Maafisa
"Walinzi wa Hekalu"
Kwa nini nyinyi hamkumleta?
Hapa "nyinyi" inamaanisha walinzi wa hekalu.
John 7:47-49
Ndipo Mafarisayo walipowajibu
Hapa "wao" inamaanisha walinzi wa hekalu.
Kupotoshwa
Kudanganywa
Kuna yeyote kati ya watawala aliyemwamini, au yeyote kati ya Mafarisayo?
"Si watawala wala Mafarisayo waliomwamini."
Sheria
Hii ilirejea sheria ya Mafarisayo na si sheria ya Musa.
John 7:50-52
Sheria yetu humhukumu mtu
Nikodemo alimaanisha kuwa wale wanaoifuata sheria hawamhukumu mtu kabla ya kumhoji.
sheria yetu humhukumu mtu... sivyo?
"Sheria yetu ya Kiyahudi haituruhusu kumhukumu mtu
Na wewe pia unatokea Galilaya?
Inawezekana pia na wewe ni mmoja wa watu wa chini kutoka Galilaya
Hakuna Nabii anayetoka Galilaya
Hii pengine ilirejea katika imani kwamba Masihi hawezi kuzaliwa Galilaya
John 7:53
7:53- 8:11
8:11 Maelezo yaliyotangulia hayana mistari hii.
John 8
John 8:1-3
Watu wote
Watu wengi
Mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha uzinzi
Mwanamke ambaye walimkuta akizini
John 8:4-6
Sasa katika sheria
"Sasa" ni utangulizi wa kilichotangulia kuwa Yesu na Wayahudi wenye mamlaka walielewa
Watu kama hao
"Watu kama hao" au "watu wafanyao hayo"
Unasemaje kuhusu yeye?
Hii inaweza kutafsiriwa kama amri. "Kwa hiyo tuambie. Tufanyeje kuhusu yeye?"
Kumtega
"Kumtega." Hii inamaanisha kutumia swali la mtego.
Ili kwamba wapate jambo la kumshitaki kwalo
Nini watakachomshitaki nacho inaweza kufanywa wazi. "Ili kwamba wapate kumshitaki kwa kusema jambo baya" au ili kwamba wapate kumshitaki kwa kutoitii sheria ya Musa na sheria ya Warumi.
John 8:7-8
Wakati walipoendelea
Neno "walipo" linarejea kwa waandishi na Mafarisayo.
Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu
"Kama yeyote kati yenu hana dhambi" au Ikiwa mmoja kati yenu hajatenda dhambi kamwe"
Miongoni mwenu
Yesu alikuwa anaongea na waandishi na Mafarisayo, na pengine makutano ya watu pia.
Mwacheni
Mwacheni mtu huyo
Aliinama chini
Aliinama kufikia chini
John 8:9-11
Mmoja baada ya mwingine
Mmoja baada ya mwingine
Mwanamke, wako wapi washitaki wako?
Wakati Yesu alipomwita "mwanamke," hakumaanisaha kumdharau au kumfanya ajione mdogo. Ikiwa watu katika makundi yao ya lugha watafikiri kwamba alikuwa akifanya hivyo, hii itafsiriwe bila kutumia neno "mwanamke."
John 8:12-13
Mimi ni nuru ya ulimwengu
mimi ndiye nitoaye nuru kwa ulimwengu. Maana yake ni kwamba Yesu ameleta ujumbe wa kweli wa Mungu katika ulimwengu uwaokoao wanadamu kutoka giza la dhambi zao.
Ulimwengu
"Watu wa Ulimwengu"
Yeye anifuataye
"Kila mmoja anifuataye." Hii ni njia ya mafumbo isemayo "Kila mmoja atendaye yale ninayofundisha" au " kila mmoja anayenitii."
Uzima
Hii inamaanisha uzima wa kiroho
Unajishuhudia mwenyewe
"Unayasema mambo haya kwa ajili yako mwenyewe."
Ushuhuda wako siyo kweli
"ushuhuda wako siyo kweli" huwezo kuwa shahidi wa kujishuhudia mwenyewe au kile unachokisema juu yako hakiwezi kuwa kweli.
John 8:14-16
Ingawa najishuhudia mwenyewe
Hata ingawa nasema mambo haya juu yangu binafsi
Mwili
Kanuni za kibinadamu na sheria za watu
Simhukumu yeyote
Maana zuinazowezekana zaweza kuwa 1) Sijamhukumu yeyote bado au 2) Simhukumu yeyote sasa
ikiwa nitahukumu
Ikiwa nitahukumu watu. Maana inawezekana 1) Ninapowahukumu watu ( kwa wakati ujao) au 2) wakati wowote ninapowahukumu watu (sasa) au 3) ikiwa nitahukumu watu.
Hukumu yangu ni kweli
Maana inayowezekana 1) "Hukumu yangu itakuwa sahihi" au 2) Hukumu yangu ni sahihi
Siko peke yangu, lakini niko pamoja na Baba aliyenituma
Yesu, Mwana wa Mungu, anayo mamlaka kwa sababu ya uhusianomwake maalumu na Baba yake, aliyemtuma. Neno "Baba" na "Mwana" linaonyesha uhusiano wa watu wa Mungu kati yao.
Siko peke yangu
Siko peke yangu katika hukumu. "Siko peke yangu jinsi ninavyohukumu" au "sihukumu peke yangu."
Niko pamoja na Baba
"Baba pia anahukumu pamoja na mimi" au "Baba anahukumu kama nihukumuvyo mimi."
Baba
Hiki ni cheo maalumu kwa Mungu
Baba aliyenituma
Neno "aliyenituma" inazungumza jambo zaidi kuhusu Baba. "Baba, yeye pekee aliyenituma."
John 8:17-18
Ndiyo, na katika sheria yenu
Neno "Ndiyo" inaonyesha kwamba Yesu anaongeza kile alichosema kabla.
Imeandikwa
Musa aliandika
Ushuhuda wa watu wawilini kweli
"Ikiwa watu wawili watasema jambo lile lile, ndipo watu watakapojua ni kweli"
John 8:19-20
Hamnijui mimi wala Baba yangu, kama mngelinijua mimi, mngelimjua na Baba yangu vile vile."
Yesu anaonyesha kwamba kumjua yeye ni kumjua Baba pia. Wote Baba na Mwana ni Mungu mmoja, kwa hiyo kumjua mmoja ni kuwajua wote.
Baba yangu
Hiki nicheo muhimu kwa Mungu.
John 8:21-22
Kufa katika dhambi zenu
"Kufa wakati ukiwa mwenye dhambi." au "utakufa wakati ukiendelea kutenda dhambi." Hapa neno "Kufa" linaelezea kifo cha kiroho.
Hauwezi kuja
"Hauna uwezo wa kuja"
Je atajiua mwenyewe, yeye aliyesema
Hii yaweza kutafsiriwa kama maswali mawili yaliyotenganishwa. Atajiua mwenyewe? Hivyo ndiyo sababu anasema"
John 8:23-24
isipokuwa uamini kwamba MIMI NDIYE, utakufa
Ikiwa hautaamini
kwamba MIMI NDIYE
Kwamba mimi ni Mungu
John 8:25-27
Walisema
Neno hili linamaanisha viongozi wa Kiyahudi
Baba
Baba yake
John 8:28-30
Utakapoinuliwa juu
Utakapoinuliwa. Hili halijatokea bado.
Mwana wa Mtu.... Baba
Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano wa Yesu na Mungu.
MIMI NDIYE...BABA alinifundisha
kama Mungu Mwana, anavyomjua Mungu Baba tofauti na mwingine yeyote, na divyo ilivyo wakati wote
Kama Baba alivyonifundisha
katika njia ile ile kwamba Baba alinifundisha
Yeye aliyenituma
Neno linamaanisa Baba
Kama Yesu alivyosema
wakati Yesu alipokuwa akisema
John 8:31-33
baki katika neno langu
Tii kile nilichosema
kweli itakuweka huru
Ikiwa mtautii ukweli, Mungu atawaweka huru"
John 8:34-36
Amini, amini
Tafsiri hii kama ilivyofanyika Yoh. 1:49
Ni mtumwa wa dhambi
"Ni kama mtumwa wa dhambi." Hii inamaanisha kwamba dhambi ni kama bwana wa mwenye dhambi.
Katika nyumba
Nyumbani mwa
Ikiwa Mwana atawaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli
Kulingana na tamaduni zao, mwana mkubwa anaweza kumweka huru mtumwa katika nyumba yake.
Mwana
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
John 8:37-38
Neno langu
Mafundisho yangu
John 8:39-41
Baba
Mababa
Ibrahimu hakufanya hili
Ibrahimu kamwe hakujaribu kumwua yeyote aliyemwambia ukweli kutoka kwa Mungu
Hatukuzaliwa katika dhambi ya zinaa
Wote tulizaliwa kutoka ndoa sahihi
John 8:42-44
Pendo
Huu ni aina ya upendo unaotoka kwa Mungu na unaelekea katika mema ya wengine, hata kama haufaidiki chochote.
Kwa nini hamyaelewi maneno yangu?
Yesu anatumia swali hili hasa hasa kuwakemea viongozi wa Kiyahudi kwa kutomsikiliza yeye.
John 8:45-47
Nani kati yenu ananishuhudia kuwa ni mwenye dhambi?
Hakuna yeyote kati yenu anayeweza kunishuhudia kuwa mimi nina dhambi." Yesu aliuliza swali hili kuweka mkazo kuwa yeye hana dhambi.
Kwa nini haniamini
Hamna sababu ya kushindwa kuniamini" Yesu alitumia swali hili kuwakemea viongozi wa Kiyahudi kwa kutoamini kwao.
John 8:48-49
Wayahudi
Neno Wayahudi linatumika kuwakilisha viongozi wa Kiyahudi.
John 8:50-51
Kuyashika maneno yangu
Tii kile ninachosema
Kifo
Hii inamaanisha kifo cha kiroho
John 8:52-53
Baba
Mababa
John 8:54-56
Ni Baba yangu anayenitukuza
Hakuna mwanadamu amjuaye Mungu Baba kama Mungu Mwana, Yesu Mwana wa Mungu. Mungu Baba humtukuza Mwana kwa sababu wote Baba na Mwana ni Mungu wa milele.
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu
John 8:57-59
Haujafikisha bado umri wa miaka hamsini, na umeshamuona Ibrahimu?
Miaka yako ya umri ni chini ya hamsini. Usingelikuwa umemuona Ibrahimu."
Amini, amini
Tafsiri hii kama ulivyofanya katika Yoh. 1:49
John 9
John 9:1-2
Yesu alipopita karibu
hapa inamaanisha Yesu na wanafunzi wake
John 9:3-5
Sisi
Neno sisi linawahusisha wote Yesu na wanafunzi wake aliokuwa akiongea nao.
Mchana...Usiku
Yesu analinganisha wakati watu wanaweza kufanya kazi wakait wa mchana, wakati ambao kwa kawaida watu hutenda kazi, na wakati wa usiku watu hawawezi kufanya kazi ya Mungu.
Nuru ya Ulimwengu
Yule ambaye aonyeshaye kile kilicho cha kweli kama vile nuru ionyeshacho kilicho halisi.
John 9:6-7
alifanya udongo kwa kutumia mate
Yesu alitumia vidole kuchanganya udongo na mate.
aliosha
aliosha macho yake kwenye kisima
John 9:8-9
Huyu siye mtu....mwombaji?
Huyu mtu ni yule ... omba, siyo yeye? au "Huyu ni mtu... omba. Ndiyo ni yeye.
John 9:10-12
alipakwa... macho
Angalia jinsi ulivyotafsiriwa Yoh. 09:06
John 9:13-15
siku ya Sabato
Siku ya mapumziko kwa Wayahudi
John 9:16-18
Hawezi kutunza sabato
Hii inamaanisha kuwa hakutii sheria kuhusu Sabato.
Ishara
Miujiza pia yaweza kuitwa ishara kwa sababu imetumika kama viashirio au ushahidi kwamba Mungu ana uwezo wote aliye na mamlaka kamili juu ya ulimwengu.
John 9:19-21
Waliwauliza wazazi
hapa inamaanisha viongozi wa Wayahudi
yeye ni mtu mzima
yeye ni mwanaume au yeye si mtoto tena
John 9:22-23
Hofu
Hii inamaanisha hisia zisizokuwa mzuri anazokuwa nazo mtu kama kuna utisho au madhara kwake au kwa wengine
John 9:24-25
Walimwita mtu
Hapa, "Walimwita" walimaanisha Wayahudi.
Mtu huyu
Hili linarejea kwa Yesu
Mtu yule
Hili linarejea kwa mtu aliyekuwa kipofu
Awe ni mwenye dhambi, mimi sijui
Sijui kama ni mwenye dhambi au la
John 9:26-29
Sentensi unganishi:
Wayahudi wanaendelea kuongea na mtu aliyekuwa kipofu
Kwa nini mnataka kusikia tena?
Kauli hii ipo katika mfumo wa swali kuelezea kushangazwa kwa yule mtu aliyeponywa awaelezee tena kuhusu kilichotokea.
John 9:30-31
Hawasikilizi wenye dhambi...humsikiliza
"Hajibu maombi ya mwenye dhambi...Mungu hujibu maombi yake."
John 9:32-34
Haijasikiwa kamwe kwamba mtu amefungua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu
"Hakuna aliewahi kusikia mtu amefumbua macho"
Ikia mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingefanya chochote
"Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingefanya chochote, lakini ameniponya, kwa hiyo yamkini ametoka kwa Mungu."
ulizaliwa katika dhambi, na wewe sasa unataka kutufundisha sisi?
"Ulizaliwa kamili katika dhambi. Hauna sifa za kutufundisha.
John 9:35-38
Kuamini
Hii in maana ya kumwamini Yesu, kuamini kwamba, ni Mwana wa Mungu, kumtumaini yeye kama Mwokozi, na kuishi katika njia iletayo heshima kwake.
John 9:39-41
Ili kwamba wale wasioweza kuona wapate kuona na kwamba wale wanaoona wawe vipofu.
Ili kwamba wale wasioona kwa macho yao wapate kumtambua Mungu na ili kwamba wale ambao wanaona kwa macho yao wasimtambue Mungu.
John 10
John 10:1-2
Amini, amini
Itafsiriwe kama ilivyofanyika katika Yoh. 1:49
zizi la kondoo
Hili ni eneo lenye uzio sehemu ambayo mchungaji huwatunza kondoo wake.
Mwizi na mnyang'anyi
Hili ni tumizi la maneno mawili yanayofanana ili kuongeza mkazo
John 10:3-4
mlinzi wa geti
huyu ni mtu aliyeajiriwa kulinda getini wakati wa usiku
kondoo husikia sauti yake
kondoo husikia na kuelewa sauti yake
John 10:5-6
Hawakuelewa
Maana inayowezekana: 1) "Wanafunzi hawakuelewa" au 2) Makutano hawakuelewa." Unaweza pia kuiacha kama "hawakuelewa>"
John 10:7-8
Amini, amini
Tafsiri kama ulivyofanya katika Yoh. 1:49
Mimi ni mlango wa kondoo
"Mimi ni njia wanayoipitia kondoo kwenda zizini." Yesu anasema yeye ndiye anayeruhusu kuingia. Neno "kondoo" limetumika kumaanisha watu wa Mungu.
Wote waliokuja kabla yangu
Hili linarejea kwa walimu wengine waliofundisha kabla ya Yesu.
wezi na wanyang'anyi
Yesu anawaita "wezi na wanyang'anyi" kwa sababu mafiundisho yao yalikuwa ya uongo, na walikuwa wakkijaribu kuwaongoza watu wa Mungu wakati hawaujui ukweli.
John 10:9-10
Mimi ni mlango
Alimaanisha yeye mwenyewe kama "mlango," Yesu anaonyesha kwamba anatoa njia ya kweli kupata kile zizi la kondoo linawakilisha.
Malisho
Neno "malisho" linamaanisha eneo lenye nyasi mahali kondoo huenda kula.
Hawezi kuja isipokuwa
Hiki ni kinyume mara mbili. Katika lugha zingine ina uasilia zaidi kwa kutumia sentensi chanya.
Ili kwamba wawe na uzima
Neno "wawe" linamaanisha kondoo. "uzima" linamaanisha uzima wa milele.
John 10:11-13
Mimi ni mchungaji mwema
Mimi nafanana na mchungaji mwema
Huyatoa maisha yake
Kuweka kitu chini maana yake kuondoa uwezo wake. Ni lugha laini yenye kumaanisha kufa.
John 10:14-16
Mimi ni mchungaji mwema
Mini nafanana na mchungaji mwema
Baba ananijua mimi, nami namjua Baba
Mungu Mwana na Mungu Baba (na Mungu Roho Mtakatifu) wanafahamiana na wote ni nafsi ya Mungu.
Baba
Hiki ni cheo maalumu cha Mungu
Zizi
Kundi la kondoo linalomilikiwa na mchungaji. Neno hili linatokana na neno "Zizi" mahali ambapo kondoo hukaa.
Nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo
Hii ni njia ya upole ya Yesu kusema kwamba atakufa ilikuwalinda kondoo. "Ninakufa kwa ajili ya kondoo."
John 10:17-18
Anapenda
Aina hii ya upendo hutoka kwa Mungu, na unaelekezwa kwa ajiliya mema ya wengine, hata kama haimfaidii mtu binafsi. Aina hii ya upendo huwajali wengine, haijalishi wamefanya nini.
Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Nami nautoa uhai wangu
Mpango wa Mungu wa milele ulikuwa kwa Mungu Mwanakuutoa uhai wake ili kulipa kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Kifo cha Yesu Msalabani unafunua wenye nguvu wa Mwana kwa Baba na wa Baba kwa Mwana.
Baba
Hiki ni cheo maalumu cha Mungu.
Ninayatoa maisha yangu ili kwamba nipate kuyatwaa tena
Hii ni njia ya upole ya Yesu kusema atakufa na baadaye kuwa mzima tena. "Najiruhusu mwenyewe kufa ili kwamba ninaweza kujirudisha kuwa mzima tena.
John 10:19-21
Kwa nini mnamsikiliza?
"Msimsikilize"
Je pepo laweza kufumbua macho ya aliyekuwa kipofu?
"Pepo hawezi kumfanya kipofu apate kuona."
John 10:22-24
Sikukuu ya kuwekwa wakfu
Hii ni siku ya nane, mapumziko ya wakati wa baridi Wayahudi huitumia kukumbuka muujiza wa Mungu alipofanya mafuta kidogo kubaki katika taa mpaka walipopata mafuta mengine baada ya siku nane baadaye. Taa ilitumika kuweka wakfu hekalu la Kiyahudi kwa Mungu. kuweka wakfu kitu ni ahadi ya kukitumia tu kwa kusudi maalumu.
kibaraza
Huu ni muundo uliounganishwa na jengo, ina paa na inaweza kuwa na ukuta ama isiwe nao.
John 10:25-28
Katika jina la Baba yangu
Hii inamaanisha kuwa Yesu alifanya mambo haya kwa uwezo na mamlaka ya Baba yake. Yesu ni mkamilifu , mtakatifu Mwana w Mungumwenye uwezo wa milele kutoka kwa Baba ili kulipa kwa ajili ya dhambi zote milele na kuokoa na kuwasamehe wote waliomwamini.
Haya yanashuhudia kuhusu mimi
Miujiza yake ilithibitisha kuhusu yeye kama vile shahidi anavyoshuhudia mahakamani.
Siyo kondoo wangu
"Siyo wafuasi wangu" au "siyo wanafunzi wangu" au "siyo watu wangu"
John 10:29-31
Baba yangu...amewatoa kwangu...hakuna aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
Mungu Baba na Mungu Mwana kwa uwezo wao huwalinda waliookoka.
Baba yangu
Hiki ni cheo uhimu kwa Mungu
Mkono wa Baba
Neno "mkono" linatumika kumaanisha umiliki wa Mungu au madaraka na ulinzi wake.
Mimi na Baba yangu tu umoja
Yesu, Mungu Mwana,na Mungu Baba ni umoja. Wao ni nafsi za Mungu mmoja na wa kweli (pamoja na Roho). Wana umoja katika makusudi, uwezo, mamlaka, huruma na utakatifu. Wao ni Mungu.
John 10:32-33
Yesu aliwajibu, "Nimeshawaonyesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba
Kazi za Yesu zilifanyika katika uwezo wake kama Mwana wa Mungu, katika umoja na Mungu Baba. Kazi za Yesu ni kazi za Baba vile vile (na Roho Mtakatifu).
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu
Unajifanya kuwa Mungu
"Alidai kuwa yeye ni Mungu"
Tuna...kuponda mawe kwa...kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu
Yesu alidai kuwa yeye ni Mwana wa Mungu ilikuwa ni kufuru kwa Wayahudi kwa sababu walidhani kuwa Yesu alikuwa akidai kuwa yeye ni Mungu - na ndivyo alivyokuwa.
John 10:34-36
Ninyi ni miungu
Kwa kawaida neno "mungu" huonyesha "mungu wa uongo" vinginevyo iwe imeandikwa kwa herufi kubwa "M," imaanishayo kwa mmoja Mungu wa kweli. Lakini hapa, Yesu ananukuu maandiko mahali Mungu anawaita wafuasi wake "miungu" kwa sababu amewachagua kumwakilisha duniani.
Je haikuandikwa...miungu?
"Mnapaswa kujua tayari kuwa imeandikwa...miungu"
Maandiko hayawezi kuvunjwa
Maana inayowezekana ni 1) "hakuna atakayebadilisha maandiko." 2) "Maandiko yataendelea kuwa kweli."
'Unakufuru; kwa sababu nilisema, mimi ni Mwana wa Mungu
Wapinzani wa Yesu waliamini kuwa Yesu alikuwa anakufuru alipojiita "Mwana wa Mungu" kwa sababu kusema hivyo ilikuwa ni kudai kuwa sawa na Mungu.
Baba... Mwana wa Mungu
Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu
John 10:37-39
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu
Niaminini
Hapa neno "amini" maana yake ni kukubali au kutumaini kile ambacho mtu huyo amesema ni cha kweli.
Ziaminini kazi
Hapa "Zizminini" maana yake kutumaini kuwa kitu ni cha kweli na kutenda kwa njia hiyo inayoonyesha imani hiyo.
Baba yu ndani yangu na kwamba mimi ni ndani ya Baba
Mungu Baba yuko ndani ya Yesu, Mwana wa Mungu, kwa sababu Mungu Mwana yu ndani ya Baba. Kama nafsi za Mungu, Baba na Mwana wote ni Mungu mmoja wa milele, pamoja na Mungu Roho.
mkono wao
"ufahamu wao." Hii maana ya ke ni kuwa katika nafasi isiyo salama anapoweza kukamatwa.
John 10:40-42
Yohana kweli hakufanya ishara, lakini mambo yote ambayo Yohana alisema juu ya mtu huyu ni ya kweli.
Ni kweli kwamba Yohana hakufanya ishara, lakini aliongea ukweli juu ya huyu mtu, anayefanya ishara.
Ishara
Miujiza inayothibitisha kwamba kitu fulani ni cha kweli au kinachompa mwingine kuwa na kibali
John 11
John 11:1-2
Maelezo ya jumla:
Hii ni habari inayomhusu Lazaro. Mistari hii inamtambulisha yeye na kutoa historia fupi juu yake na dada yake Mariamu.
Ni Mariamu ndiye aliyempaka Bwana mafuta...nywele zake
Yohana pia anamtambulisha Mariamu, dada yake na Matha.
John 11:3-4
aliomba Yesu aje
"alitaka Yesu aje kwake"
upendo
Hapa "upendo" inamaanisha upendo wa ndugu, wa asili, upendo wa kibinadamu kati ya marafiki na ndugu.
Kifo
Hii inamaanisa kifo cha kimwili
badala yake kwa utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika hilo
Yesu kama Mwana wa Mungu, amepokea utukufu ule ule kama wa Mungu
Mwana wa Mungu
Hili ni jina muhimu kwa Yesu
John 11:5-7
Sasa Yesu alimpenda Martha na dada yake pamoja na Lazaro
Haya ni maneno ya utangulizi
John 11:8-9
Rabi, Wayahudi walikuwa sasa wanatafuta kukuponda mawe, na unarudi tena huko?
"Mwalimu, kwa hakika huhitaji kurudi huko! Wayahudi wanajaribu kukuponda mawe.!"
Je hakuna masaa kumi na mbili ya mchana?
"Unajua kwamba siku ina masaa kumi na mbili za mchana
John 11:10-11
Nuru haimo ndani yake
Maana halisi 1) "hawezi kuona" au 2) hawezi kuona"
Rafiki yetu Lazaro amelala
Lazaro amekufa lakini kwa ajili ya muda mfupi tu.
Lakini ninaenda ili kwamba nipate kumwamsha kutoka usingizini
Yesu anaufunua mpango wake wa kumfufua Lazaro.
John 11:12-14
Maelezo ya jumla
Katika mustari wa 13 kuna kituo katika mtiririko wa habari kama ambavyo Yohana unaongelea kuhusu wanafunzi wa Yesu kutokuelewa kile ambacho Yesu alimaanisha aliposema kuwa Lazaro amelala.
kama amelala
Wanafunzi walidhani kuwa Lazaro amepumzika tu na baadaye ataamka.
John 11:15-16
Sentensi unganishi:
Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake
kwa ajili yenu
kwa faida yenu
John 11:17-20
Maelezo ya jumla:
Kwa sasa Yesu yupo Bethania.
alimkuta Lazaro tayari alikuwa kaburini kwa muda wa siku nne
Unaweza kutafasiri hivi pia, "alijua kwamba watu walikuwa wamekwisha kumweka Lazaro kaburini kwa muda wa siku nne kabla ya yeye kufika"
kuhusiana na kaka yao
Lazaro alikuwa kaka yao mdogo
John 11:21-23
Kaka yangu asingalikufa
"Kaka yangu angeendelea kuwa mzima"
Fufuka tena
Maana yake kumfanya mtu aliyekufa kuishi tena
John 11:24-26
Ajapokufa
Hapa "kufa" inamaanisha kifo cha kimwili
Bado ataishi
Hapa "Ishi" linamaanisha uzima wa kiroho
Naye aishiye na kuniamini hatakufa kamwe
Na wote waniaminio mimi hawatatengwa kamwe milele kutoka kwa Mungu.
Hatakufa kamwe
Hapa "kufa" inamaanisha kifo cha kiroho
John 11:27-29
Ndiyo, Bwana, ninaamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye... ajaye katika ulimwengu.
Martha aliamini kwamba Yesu ni Bwana, Kristo (Masihi), Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo maalumu cha Yesu.
Mwalimu
Cheo hiki kinamhusu Yesu
John 11:30-32
Anguka chini ya miguu yake
Mariamu alilala chini au alipiga magoti katika miguu ya Yesu kuonyesha heshima
Kama ungelikuwa hapa, kaka yangu asingelikufa
Angalia hili ulivyotafsiri katika Yoh. 11:21
John 11:33-35
alisikitika sana moyoni mwake na roho yake iliumia
Yohana anatumia sentensi hizi mbili kuelezea uzito wa maumivu ya moyo ambayo Yesu aliyapata.
Mme mweka wapi
Hii ni njia nyingine ya kuuliza, "mmemzika wapi?"
Yesu akalia
Yesu alianza kulia
John 11:36-37
Mpendwa
Hili linamaanisha juu ya upendo wa ndugu au upendo wa kibinadamu kwa rafiki au mtu wa familia.
isingefaa huyu mtu, aliyefungua macho ya yule aliyekuwa kipofu, hakuweza kumfanya mtu huyu asife?
Aliweza kumponya mtu aliyekuwa kipofu, kwa hiyo angeweza pia kumponya mtu huyu ili kwamba asife." au "Hakuweza kumfanya mtu huyu asife, kwa hiyo tunajua kuwa hakumponya kweli mtu aliyezaliwa kipofu kama wanavyosema alifanya."
Kufungua macho
Kuponya macho
John 11:38-40
Je sikusema kwamba, ikiwa utaamini, utauona utukufu wa Mungu?
"Kumbuka kwamba nilikuambia, ikiwa utaniamini, utaona ni kwa jinsi gani Mungu ni Mkuu
mpaka muda huu mwili wake utakuwa umeoza
mpaka muda huu kutakuwa na harufu mbaya
John 11:41-42
Baba, ninakushukuru kwamba umenisikiliza
Yesu alikuwa akiomba moja kwa moja kwa Baba kama ushuhuda kwa waliokuwa pamoja naye
Baba
Hiki ni cheo maalumu kwa Mungu
John 11:43-44
Amefungwa mikono na miguu kwa nguo za kuzikia, na uso wake ulikuwa umefungwa kwa nguo.
Utamaduni wa kuzika kwa wakati huu ulikuwa wa kuufunga mwili wa marehemu kwa nguo ndefu za kitani
Yesu aliwaambia
Neno "wao" linamaanisha juu ya watu waliokuwa pale na kuona muujiza.
John 11:45-46
Maelezo ya jumla
Mistari hii inatuambia mambo yaliyotokea baada ya Lazaro kufufuliwa kutoka wafu.
John 11:47-48
Maelezo ya jumla
Hii ni sehemu ya pili ya simulizi. Kuhani mkuu pamoja na Mafarisayo wanakutana kwa ajili ya kikao cha baraza la Kiyahudi
Kisha makuhani wakuu
kisha viongozi kati ya makuhani
wote wataishi ndani yake
Viongozi wa Kiyahudi waliogopa kwamba watu wangemfanya Yesu kuwa mfalme wao.
John 11:49-50
Haujui chochote kabisa
"Hauelewi ni itu gani kinatendeka" au Haujui nini cha kufanya lakini mimi najua."
mtu mmoja kati yao
Hii ni njia ya kumtambulisha mhusika mpya katika simulizi.
John 11:51-53
kufa kwa ajili ya taifa
Neno "taifa" linatumika kuonyesha watu wa taifa la Israel.
Watoto wa Mungu
Hili linamaanisha watu wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu na ni watoto wake wa kiroho.
John 11:54-55
Maelezo ya jumla:
Yesu anaondoka Bethania na kwenda Efraimu.
tembea kwa uhuru mbele ya Wayahudi
Hapa anaongelea viongozi wa Kiyahudi.
nchi
hili ni eneo nje ya mji ambapo watu wachache wanaishi.
John 11:56-57
Walikuwa wakimtafuta Yesu
Neno "Walikuwa" linawazungumza Wayahudi waliosafiri kuja Yerusalemu.
Unafikiri nini? Kwamba hawezi kuja katika sikukuu?
Mzungumzaji hapa alikuwa akishangaa ikiwa Yesu atakuja katika sikukuu ingawa kulikuwa na hatari ya kukamatwa. Aliwauliza wengine waliomzunguka kuhusiana na mawazo yao. "Mnafikiri Yesu anaweza kuwa woga sana kuja katika sikukuu?"
Sasa wakuu wa makauhani
Haya ni maelezo ya nyuma ambayo yanaelezea kwa nini waabudu wa Kiyahudi walikuwa wakishangaa ikiwa Yesu atakuja katika sikukuu au la. Ikiwa lugha yako inayo njia ya kuweka alama ya maelekezo ya nyuma fanya hivyo.
John 12
John 12:1-3
Litra
Litra ni kipimo cha uzito - paundi ya Kirumi ni sawa na gramu 327.5
Manukato
Hiki ni kimiminika chenye harufu nzuri kilichotengezwa kwa mafuta ya miti na maua yanayonukia vizuri.
nardo
Haya ni manukato yaliyotengenezwa kutokana na maua yanayopatikana katika milima ya Nepali, China, na India.
nyumba yote ilijaa harufu ya manukato
"harufu nzuri ya manukato yake iliijaza nyumba"
John 12:4-6
yeye ambaye angemsaliti Yesu
"Yeye ambaye baadaye aliwasaidia maadui wa Yesu kumkamata"
Basi alisema hivi...chukua baadhi ya vilivyomo ndani kwa ajili yako
Yohana anaeleza kwanini Yuda aliuliza swali kuhusu maskini.
aliyasema haya, sio kwasababu aliwahurumia maskini, bali kwasababu alikuwa mwizi
"alisema hivi kwasababu alikuwa mwizi. Hakuwajali maskini"
John 12:7-8
mwache atunze alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu
Yesu anaeleza kuwa matendo ya yule mwanamke yanaweza kueleweka kama tazamio la kifo na maziko yake
maskini mtakuwa nao siku zote
Yesu anamaanisha kuwa mtakuwa na nafasi ya kuwasaidia maskini siku zote
lakini hamtakuwa na mimi siku zote
Kwa njia hii Yesu anasema kwamba atakufa
John 12:9-11
Basi
Neno hili limetumika hapa kuonesha kituo katika simulizi. Hapa Yohana anaelezea kundi jipya la watu katika simulizi.
kwasababu yake
Ukweli kwamba Lazaro alikuwa hai kulisababisha Wayahudi wengi wamwamini Yesu.
Walimwamini Yesu
Hii inamaanisha "walimwamini Yesu"; hivi, waliamini kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, kumwamini yeye kama Mwokozi, na kuishi kwa kumheshimu yeye.
John 12:12-13
Hosana
Hii inamaanisha "Mungu aokoe."
Mbarikiwa
Hii huelezea hamu ya kutaka Mungu afanye mambo mazuri kwa mtu huyo.
ajae kwa jina la Bwana
Kuja kwa jina la mtu fulani humaanisha kutumwa kwa mamlaka na nguvu zake, au kuja kama mwakilishi wake.
John 12:14-15
binti Sayuni
"Binti Sayuni" ni neno linalomaanisha Israeli, kama vile "wana wa Israeli" au "watu kutoka Yerusalemu."
kama ilivyoandikwa
Unaweza kutafasiri hivi, "kama ambavyo manabii waliandika katika maandiko."
John 12:16
wakati Yesu alitukuzwa
"wakati Mungu alimtukuza Yesu"
walikumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye
Yohana, mwandishi, anafafanua hapa ili kumpa msomaji taarifa za jinsi mitume walivyoelewa baadaye.
John 12:17-19
ishara hii
Hili ni tukio au tokeo linalodhihirisha kuwa jambo fulani ni la kweli; kwa hali hii, inathibitika kuwa Yesu ni Masihi.
tazama, ulimwengu umekwenda kwake
"inaonekana kuwa kila mtu anakuwa mwanafunzi wake"
ulimwengu
neno hili limaanisha watu wote duniani
John 12:20-22
kisha baadhi ya Wayunani
hii inatoa utambulisho wa wahusika wapya katika simulizi
kuabudu katika sherehe
Yohana anamaanisha kuwa Wayunani walikuwa wanaenda kumwabudu Mungu wakati wa Pasaka.
Bethsaida
huu ulikuwa mji katika jimbo la Galilaya
na kisha wakamwambia Yesu
Filipo na Andrea wakamwambia Yesu kuhusiana na Wayunani walioomba kukutana naye.
John 12:23-24
Maelezo ya jumla:
Yesu anaanza kuwajibu Filipo na Andrea.
Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa matunda mengi.
"Kuwa makini zaidi na mfano huu ninaowaambia. Uhai wangu ni kama mbegu iliyopandwa katika nchi na kufa. Kama isipopandwa, hubakia mbegu moja tu. Lakini ikipandwa, hubadilika na kukua kwa kuzaa mbegu nyingi zaidi."
John 12:25-26
Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimwengu huu atausalimisha hata uzima wa milele.
"Kwa jinsi iyo hiyo, yeyote apendaye mapenzi yake, huyaharibu maisha yake. Bali yeye asiyefuata mapenzi yake, kwasababu ya utii kwangu, ataishi na Mungu milele."
anapenda maisha yake...huchukia maisha yake
Hii inamaanisha uzima wa mwili.
John 12:27-29
Niseme nini? Baba, niokoe mimi na saa hii?
Hii ni lugha ya balagha. Japokuwa Yesu anatamani kuepuka mateso, bado anachagua kumtii Mungu na kuuawa.
Baba
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu
saa hii
Hii inamaanisha wakati Yesu atateswa na kufa msalabani.
ulitukuze jina lako
ufunue utukufu wako (Mungu) ili ujulikane
sauti ikaja kutoka mbinguni
Mungu aliongea kutoka mbinguni
John 12:30-31
Maelezo ya jumla
Yesu anaelezea sababu za sauti kutoka mbinguni
Sasa ni wakati wa hukumu ya ulimwengu
ulimwengu humaanisha watu wote walio duniani
sasa mtawala wa dunia hii atatupwa nje
mtawala wa dunia hii ni Shetani
John 12:32-33
Maelezo ya jumla:
Katika mstari wa 33 Yohana anaeleza historia ya maneno ya Yesu aliposema habari za kuinuliwa juu.
nitakapoinuliwa juu kutoka katika nchi
Hapa Yesu anamaanisha kusulubiwa kwake.
nitawavuta wote kwangu
Kwa kusulubiwa kwake, Yesu atafanya njia kwa ajili ya kila mmoja kumwamini yeye.
John 12:34-36
Mwana wa Mtu ni lazima atainuliwa juu
Neno "kuinuiwa juu" maana yake ni kusulubiwa.
Huyu mwana wa Mtu ni nani?
Maana yake ni, sifa za mwana wa mtu ni zipi?
John 12:37-38
Maelezo ya jumla:
Yohana anaanza kuongelea juu ya kutimizwa kwa unabii ambao nabii Isaya alitabiri.
ili kwamba neno la nabii Isaya litimizwe
kwa ajili ya kutimiza ujumbe wa nabii Isaya
mkono wa Bwana
Hii inamaanisha, uwezo wa Bwana wa kuokoa kwa nguvu.
John 12:39-40
ameifanya mioyo yao kuwa migumu
Huu ni msemo wenye maana kwamba Mungu amewafanya kuwa wasumbufu
mioyo yao kuelewa
Wayahudi waliamini kuwa moyo ndicho kiungo kinacholeta uelewa
John 12:41-43
ili kwamba wasifukuzwe katika Sinagogi
ili kwamba watu wasiwazuie kwenda kwenye Sinagogi
Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu
Walitaka watu wawasifie zaidi kuliko Mungu
John 12:44-45
Maelezo ya jumla
Huu ni wakati mwingine ambapo Yesu anaanza kuongea na makutano
Yesu alilia na kusema
Hii inamaanisha kuwa Yesu alipiga kelele na kusema
yeye anionaye mimi amemwona yule aliyenituma
"yeye" hapa inamaanisha "Mungu"
John 12:46-47
Sentensi unganishi:
Yesu anaendelea kuongea na makutano
Nimekuja kama nuru
Hii inamaana ya "Nikuja kuwaonesha iliyo kweli"
wasibaki gizani
"giza" hapa humaanisha kuishi katika ujinga wa kutokujua kweli ya Mungu.
John 12:48-50
katika siku ya mwisho
wakati ambapo Mungu atahukumu dhambi za watu
Nami najua ya kuwa amri yake ni uzima wa milele
Nami najua ya kuwa maneno aliyoniagiza mimi kusema ni maneno yaletayo uzima milele.
Baba
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu
John 13
John 13:1-2
Maelezo ya jumla
Kipindi hiki siyo cha Pasaka lakini tayari Yesu ameketi na wanafunzi wake mezani.
mpendwa
Hii ni aina ya upendo utokao kwa Mungu
Baba
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu
John 13:3-5
Sentensi unganishi
Mstari wa 3 unaendelea kutufahamisha mambo ambayo Yesu aliyajua.
alivitoa vitu vyote kwa mkono wake
Hapa 'Mkono" unamaanisha mamlaka
alitoka kwa Mungu na alikuwa anarejea kwa Mungu
Yesu alikuwa na Baba siku zote, na angerudi kwake baada ya kumaliza kazi yake hapa duniani.
John 13:6-9
Bwana, unataka kuniosha miguu yangu?
Swali la Petro linaonesha kwamba hayupo tayari kuosha miguu yake na Yesu.
Kama sitakuosha miguu, basi hauna shirika nami
Yesu anatumia maneno magumu kumshawishi Petro akubali kuoshwa miguu.
John 13:10-11
Sentensi unganishi
Yesu anaendelea kuongea na Simoni Petro
Maelezo ya jumla:
Yesu anatumia neno "ninyi" kumaanisha wanafunzi wake wote.
John 13:12-15
Je mwajua nimefanya nini kwenu?
Yesu anajaribu kusisitiza mafundisho yake kwa wanafunzi wake
Ninyi mnaniita mimi 'mwallimu' na 'Bwana'
Yesu anamaanisha kuwa wanafunzi wake wanamheshimu sana.
John 13:16-18
Sentensi unganishi:
Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake
mkubwa
wa muhimu zaidi
umebarikiwa
kubariki hapa kuna maana ya kusababisha vitu vizuri, vyenye faida kumpata mtu.
John 13:19-20
nawaambieni sasa kabla haijatokea
Ninawaambieni sasa yale yatakayotokea kabla hayajatokea
mpate kuamini kuwa MIMI NDIYE
mpate kuamini ya kuwa Mimi ndiye niliyesema kuwa Nipo
John 13:21-22
mwenye shida
nisiye na furaha
amini, amini
Tazama tafasiri katika 1:49
John 13:23-25
mmoja wa wanafunzi ambao Yesu alimpenda
Hii inamaanisha Yohana
kifua cha Yesu
kuweka kichwa kwenye kifua cha mwingine ilikuwa utamaduni mwingine wa Kiyunani uliomaanisha urafiki wa karibu
John 13:26-27
Iskarioti
Hii inamaanisha kuwa Yuda alitoka katika kijiji cha Keriothi
Shetani akamwingia
Hii inamaana kwamba Shetani alimteka na kumwongoza
John 13:28-30
kwamba awape maskini kitu
Unaweza kutafasiri hii kama, "Nenda na uwape maskini fedha"
aliondoka na kwenda haraka. Ilikuwa usiku
Yohana anamaanisha hapa kwamba Yuda angefanya uovu wake gizani wakati wa usiku
John 13:31-33
sasa mwana wa Mtu ametukuzwa na Mungu ametukuzwa ndani yake
Unaweza kutafasiri hii hivi, "Sasa watu wataona jinsi ambavyo mwana wa Mtu atapokea heshima na jinsi ambavyo Mungu atapokea heshimu kupitia yale anayoyafanya mwana wa Mtu."
watoto wadogo
Yesu anatumia neno watoto wadogo kumaanisha kwamba aliwapenda wanafunzi wake kama watoto wake.
kama nilivyosema kwa Wayahudi
Hii inamaanisha viongozi wa Kiyahudi
John 13:34-35
Sentensi unganishi:
Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake
upendo
Hii ni aina ya upendo utokao kwa Mungu wenye kuleta mema kwa wengine
kila mtu
Hii ni hali ya kutia chumvi katika usemi kwamba kwa kila mtu aonaye upendo wa wanafunzi wake.
John 13:36-38
kuweka chini uhai wangu
kuutoa uhai wangu au kufa
Je utautoa uhai wako kwa ajili yangu?
Hii ni hali ya kuweka mkazo katika sentensi kwamba "wewe unasema utautoa uhai wako kwa ajili yangu..."
John 14
John 14:1-3
Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko.
Huu ni msemo wenye maana kwamba , "acha kuogopa na kuwa na mashaka"
Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi...
Mungu Baba ametayarisha eneo mbinguni kwa kila mtu ambaye ni muumini, kuishi pamoja naye na Mwanawe milele.
Baba
Hiki ni cheo cha muhimu kwa ajili ya Mungu.
John 14:4-7
Je! Twawezaje kuijua njia?
"Je! Tunawezaje kujua namna ya kufika pale?"
njia
Hii inaweza kuwa 1)"njia kwa Mungu" au 2) "mtu yule awapelekaye watu kwa Mungu."
kweli
Hii inaweza kuwa 2) "mtu wa kweli" au 2) "mtu anayenena maneno ya kweli."
uzima
"mtu ambaye anaweza kuwafanya watu wawe hai."
Yesu alimwambia, "Mimi ni njia, kweli, na uzima; hakuna mmoja wenu huja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu
Yesu, Mwana wa Mungu, ni njia pekee kwenda kwa Mungu Baba.
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu.
John 14:8-9
Je! Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Philipo?
"Nimekuwa tayari pamoja nanyi wanafunzi kwa muda mrefu sana. Wewe, Philipo ungenijua mimi kwa wakati huu."
Jinsi gani unasema, 'Tuonyeshe Baba?
"hivyo wewe, Philipo, hakika usingekuwa unasema, 'Tuonyeshe Baba."
Bwana, tuonyeshe Baba...
Kumwona Mungu Mwana, Yesu, ni kumwona Mungu Baba.
John 14:10-11
Hamniamini mimi?
"Hakika mngeamini kuwa Baba yu ndani yangu."
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu.
Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa mamlaka yangu mwenyewe
"Ujumbe ninaowaambia hautokani na mawazo yangu mwenyewe."
Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yangu yu ndani yangu
Kumwamini Yesu, Mwana wa Mungu, ni kuwamini Mungu Baba. Nafsi za Mungu ziko kwa kila yeyote kwasababu kila nafsi ya Mungu na zote katika Mungu, kupitia nafsi hizo zi tofauti kutoka kila moja.
John 14:12-14
amini, amini
Hii ina maana ya kumwamini Yesu, ndiyo kwamba, Kuamini kwamba ni Mwana wa Mungu, kumtumaini yeye kama Mwokozi, na kuishi katika njia ambayo inamweshimu yeye.
Chochote mkiombacho katika jina langu, nitafanya
Hii ni hali ya kuonesha ukuu na uwezo wa Yesu
Baba...Mwana
Hivi na vyeo muhimu vikielezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu.
John 14:15-17
Mfariji
Neno linaelezea Roho Mtakatifu, "ambaye atakuja karibu kuwasaidia." Kuwafundisha wanafunzi
Roho wa Kweli
Roho Mtakatifu
ambaye ulimwengu hautampokea
Hapa neno "ulimwengu" linamaanisha watu wasioamini. Watu walio kinyume na Mungu.
John 14:18-20
Ulimwengu
Watu ambao hawajamwamini Mungu
mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba
Kuamini kwa kweli katika Kristo, Baba na Mwana huishi ndani ya muumini kupitia Roho.
Baba yangu
Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu
John 14:21-22
kupenda
Aina ya upendo huu huja kutoka kwa Mungu na unalenga kufanya mema kwa wengine, hata kama hautafaa kwa mhusika. Aina ya upendo huu hujari wengine, haijalishi wanafanya nini.
Yeyote anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu
Wakati mmoja anampenda Yesu, naye Baba ampenda mtu yule.
Baba yangu
Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu.
Yuda (Siyo Iskarioti)
Huyu ni Yuda mwingine si yule aliyemsulubisha Yesu.
John 14:23-24
Sentensi unganishi:
Yesu anamjibu Yuda (Siyo Iskarioti)
Baba yangu
Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu
Neno ambalo mwasikia silo langu bali la Baba ambaye kanituma.
Yesu anasema kwamba yale ayasemayo yatoka kwa Baba. Ujumbe wa Yesu pia ni ujumbe wa Baba kwasababu Baba na Mwana wanakubaliana kikamilifu siku zote
Neno
Hii inaweza pia kuwa ujumbe
John 14:25-27
Mfariji
Roho Mtakatifu
Ulimwengu
Neno linaelezea watu wa ulimwengu huu.
Katika jina langu
Neno hapa "Jina" linaelezea juu ya nguvu na mamlaka ya Yesu
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.
John 14:28-31
Mpendwa
Aina ya upendo huu kutoka kwa Mungu unalenga kuwatendea mema wengine, hata wakati usipomfaidia mwenyewe. Upendo wa aina hii unajali wengine, bila kujali wanafanya nini.
Baba ni mkuu kuliko mimi
Mungu Baba ni mkuu kuliko Yesu, aliyekuwa akipitia kudharauliwa kama mwanadamu, lakini umilele, kama nafsi ya Mungu, wote wako sawa
Baba
Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu
John 15
John 15:1-2
Sentensi unganishi
Simulizi inaendelea. Yesu anaketi mezani pamoja na wanafunzi wake
Mimi ni mzabibu wa kweli
Yesu anajilinganisha mwenyewe na mzabibu kwa kuwa yeye ni chanzo cha uzima.
Baba yangu ndiye mkulima
Hii inamaanisha "Mungu" ni kama mkulima
John 15:3-4
kaeni ndani yangu
endeleeni kukaa/kuungana na mimi, nami nitaendelea kukaa na ninyi.
mpaka mtakapokaa ndani yangu
Hii ni hali ya kundelea kumtegmea Yesu
Ninyi
Neno hili limetumika katika wingi
John 15:5-7
Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi
Mzabibu unamwakilisha Yesu. Matawi yanawakilisha wale wote wanaomwamini Yesu.
Yeye akaaye ndani yangu nami ndani yake
Yesu anajaribu kueleza kuwa wanafunzi wake wameunganisha na yeye kama yeye alivyounganishwa nao
huzaa sana
Hii inamwelezea muumini anayempendeza Mungu kwamba kama vile tawi lizaalo sana.
ombeni lolote mtakalo
Yesu anawaambia waumini kwamba ni lazima wamuombe Mungu ajibu maombi yao.
John 15:8-9
Baba yangu anatukuzwa katika hili
Unaweza kutafasiri hii kama, "Inawafanya watu wamuheshimu Baba yangu"
Baba yangu
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu
ya kwamba mzae matunda mengi
hapa matunda yametumika badala ya maisha yanayompendeza Mungu
ni wanafunzi wangu
dhihirisheni ya kuwa mu wanafunzi wangu
dumuni katika pendo langu
endeleeni kupokea upendo wangu
John 15:10-11
Ikiwa mtazishika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyozshika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.
Wanafunzi wanapomtii Yesu, wanaonesha upendo wao kwake.
Baba yangu
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu
ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu
Unaweza kutafsiri hii kama, "ili furaha yenu itimie."
John 15:12-13
Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu
Upendo wa aina hii unatoka kwa Mungu na unawafaidia wengine pasipo kujali matendo yao.
Uhai
uzima wa kimwili
John 15:14-15
Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo
Mnaonesha ya kuwa mu rafiki zangu ikiwa mtaendelea kufanya yae niliyowaagiza
nimewajulisha mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba
Nimewaambia kila kitu ambacho Baba yangu aliniambia.
Baba yangu
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu
John 15:16-17
Hamkunichagua mimi
Yesu anasema kuwa wanafunzi wake hawakuchagua wenyewe kuwa wanafunzi
nendeni mkazae matunda
hii inamaanisha kuishi maisha yanayompendeza Mungu
kwamba matunda yenu yapate kukaa
matokeo ya matendo yenu yadumu milele
lolote muombalo kwa Baba kwa jina langu, atawapeni
"jina langu" ni kiwakilishi cha mamlaka ya yesu.
Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake
Upendo wa aina hii unatoka kwa Mungu na unawafaidia wengine pasipo kujali matendo yao.
John 15:18-19
kama ulimwengu utawachukia....
Yesu anatumia neno Ulimwengu kumaanisha watu ambao hawamwamini Mungu
upendo
Hii inarejea upendo wa kibinadamu, wa undungu, rafiki au mtu wa familia
John 15:20-22
Kumbukeni neno ambalo niliwaambia
Hii ni sawa na kusema kumbukeni ujumbe niliowaambia
kwa ajili ya jina langu
kwa sababu ni watu wangu
John 15:23-25
Yeye anichukiaye mimi humchukia Baba yangu pia ..... wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu
Kumchukia Mungu mwana ni kumchukia Mungu Baba pia.
wangelikuwa hawana dhambi
wasingekuwa wamefanya dhambi
sheria
Hii inamaanisha Agano la Kale lote ambalo lilikuwa na maagizo yote ya Mungu kwa wanadamu
John 15:26-27
Mfariji
Hii inamaanisha Roho Mtakatifu
Roho wa Kweli
Roho ambaye atawaambia kweli yote
Ninyi pia mnashuhudia
Kushuhudia ni kuwaambia wengine habari za Yesu
Mwanzo
Hii inamaanisha siku za mwanzo za huduma ya Yesu.
John 16
John 16:1-2
Sentensi unganishi:
Yesu ameketi chakulani na wanafunzi wake na anaendelea kuwafundisha
hamtaanguka
Hii inamaanisha kuwa hamtaiacha imani ndani ya Yesu.
John 16:3-4
Watawatendea haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala mimi.
Baadhi ya waamini wanaweza kuuawa kwa sababu wasiomjua Mungu Baba pia hawamjui wala kumuelewa Mungu Mwana, Yesu Kristo.
Baba
Hiki ni cheo cha Muhimu cha Mungu.
Hapo mwanzo
Angalia ulivyotafsiri "tangu mwanzo" kwenye Yohana 15:26
John 16:5-7
Kama nisipoondoka, mfariji hatakuja
"Mfariji atakuja ikiwa nitaondoka"
Mfariji
Angalia jinsi ulivyotafsiri kwenye Yohana 14:25
John 16:8-11
Mfariji atauhukumu ulimwengu kutokana...haki...naenda kwa Baba
Yesu alipoondoka duniani na akarudi kwa Mungu Baba, kisha Mungu Roho akaanza kuwaonyesha watu wana dhambi na wanahitaji msamaha unaopatokana kwa Yesu pekee.
Ulimwengu
Inamaanisha watu wanaoishi duniani
kutokana na haki, kwa sababu naenda kwa Baba, na hamtaniona tena
"Atawaambia watu kwamba kwa sababu narudi kwa Baba, hamtaniona tena, mtajua kuwa ni mimi mwenye haki ya kweli"
Baba
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu.
Mkuu wa ulimwengu
Angalia jinsi ulivyotafsiri kwenye Yohana 12:30
John 16:12-14
Mambo ya kuwaambia
"ujumbe kwa ajili yenu"
Roho wa kweli
Hili ni jina la Roho Mtakatifu atakayewaambia watu kweli ya Mungu
atawaongoza katika kweli yote
kweli inamaanisha ukweli wa kiroho
John 16:15-16
Vitu vyote...alivyonavyo Baba ni vyangu...Roho atachukua mambo yangu
Mungu Baba, Mwana, na Roho wote wanamiliki ulimwengu. Kwa pamoja ni wamoja na ni Mungu pekee.
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.
Muda mfupi
"karibu" au "kabla ya muda mrefu"
John 16:17-18
Maelezo ya jumla:
Wanafunzi wanaulizana kuhusu alichosemaYesu
muda mfupi na hamtaniona tena
wanafunzi hawakuelewa kuwa yesu alikuwa anaongelea kifo chake msalabani
na kisha muda mfupi mtaniona
Hii inaweza kumaanisha kufufuka kwa Yesu, au kuja kwa Yesu mara ya pili
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu
John 16:19-21
Sentensi unganishi:
Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake
amini, amini nawaambia
tafsiri kwa kuonesha kuwa kifuatacho ni cha muhimu zaidi
lakini ulimwengu utashangilia
lakini watu wanaompinga Mungu watashangilia
John 16:22-24
Kama mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu
Baba na Mwana wanajibu maombi pamoja. Wanaomwamini Yesu wana msamaha wa milele wa dhambi na wanaweza kuomba kwa Baba kupitia kwa Mwana, na Baba atajibu.
Baba
Hiki ni cheo cha Muhimu cha Mungu.
Kwa jina langu
Baba atawapatia mahitaji yao kwa sababu ya mahusiano yao na Yesu. "kwa sababu ni wafuasi wangu" au "kwenye mamlaka yangu"
John 16:25
Kwa lugha isiyoeleweka
"kwa lugha ambayo ni ngumu kueleweka"
Nitawaambia waziwazi kuhusu Baba
Kibinadamu kujifunza kuhusu Mungu Baba kupitia Mwana wa Mungu, Yesu. Kumjua Mwana ni kumjua Baba.
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.
John 16:26-28
Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi
Mtu akimpenda Yesu, Mwana, pia anampenda baba, kwa sababu Baba na Mwana ni mmoja.
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.
Nilitoka kwa Baba... Naondoka ulimwenguni na ninaenda kwa Baba.
Baba alimtuma mwana msalabani awaokoe waamini toka kwenye dhambi na jehanamu, akafufuka toka kwa wafu, na akarudi Mbinguni.
Ulimwengu
"dunia." Ni mahali ambapo watu wanaishi.
John 16:29-31
Sentensi unganishi:
wanafunzi wanamjibu Yesu
Sasa mmeamini?
"Hatimaye sasa mmeiweka imani yenu kwangu!"
John 16:32-33
Sentensi unganishi:
Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake
nanyi mtatawanyika
"wengine watawatawanya"
Baba yu pamoja nami
Hili jina la muhimu la Mungu
ili kwama ndani yangu muwe na amani
amani ya ndani
nimeushinda ulimwengu
nimezishinda taabu na mateso ya duniani
John 17
John 17:1-2
Baba ...mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe
Yesu anamwomba baba yake, Mungu Baba amtukuze, mwana wa Mungu
Baba...Mwana
Hivi ni vyeo vya mhimu amabavyo huelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu
Mbingu
Hii inamaanisha sehemu ya juu
John 17:3-5
Na uzima wa milelel ndio huu...wakujue wewe Mungu wa kweli, na.. Yesu Kristo
Uzima wa milele ni kumjua Mungu wa kweli na wa pekee, Mungu Baba na Mungu Mwana na Mungu Roho.
Kwamba inawapasa wakujue wewe
Hii inamaanisha kumjua mungu kwa uzoefu na wala si juu ya Mungu
Ile kazi uliyonipa kuifanya
"Kazi"inamaanisha jumla ya huduma ya Yesu hapa Duniani.
Baba, nitukuze mimi...kwa niliokuwa nao nilipokuwa na wewe kabla dunia haijaumbwa
Yesu alikuwa na utukufu pamoja na Mungu Baba '"Kabla ulimwengu haujaumbwa" Kwa sababu Yesu ni Mungu Mwana. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ndio Mungu wa Kweli ambaye amekuwepo milele yote na ataendelea kuwepo milele ne milele.
Baba...Mwana
Hivi ni vyeo vinavyoonyesha uhusiano kati ya Mungu na Yesu.
John 17:6-8
Si wa Dunia
Hapa neno "Dunia" humanisha watu wa dunia. Hii inamaanisha Mungu amewatofautisha na wale wasioamini.
Wamelishika neno lako
Wameyatii mafundisho yako
John 17:9-11
Mimi siuombei ulimwengu
Hapa neno ulimwengu linamanisha watu waovu duniani au watu wasiomtii Mungu
Duniani
Hii inamaanisha hali ya kuwa duniani na kuwa mmoja wa wale wanaoishi humo.
Baba Mtakatifu, uwalinde... ii wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja
Yesu anamwomba Baba ili awalinde wale wanaoamini. Mungu Baba huwalinda wale wanaomwamini Mungu Mwana na kuwafanya wawe na umoja na Mungu katika utatu wake
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu
Uwalinde kwa jina lako ulilonipa mimi
Hapa neno "jina"linamaanisha ulinzi na usimamaizi wa Mungu. "Uwalinde na kwa ulinzi wa jina lako kama ulivyonilinda mimi" au "uwalinde kwa nguvu za jina lako ulilonipa mimi
John 17:12-14
Hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa mwana wa upotevu
"mtu pekee aliyepotea ni mwana wa upotevu"
mwana wa upotevu
"yule ambaye tokea awali uliamua kumwamngamiza"
ili kwamba maandiko yatimie
"Ili mambo yaliyoandikwa kwenye maandiko"
John 17:15-17
ulimwengu
watu wakaao duniani
uwalinde na yule mwovu
uwalinde didi a Shetani
uwaweke wakfu kwako katika kweli
wafanye kuwa watu wako kwa kuwafundisha kweli
Neno lako ndiyo kweli
ujumbe wako ni kweli au unachosema ni kweli
John 17:18-19
ulimwenguni
kwa kila mtu duniani kote
ili kwamba na wao wajitoe kwako kwa ile kweli
unaweza pia kutafsiri kuwa: "ili kwamba wajitoe kikamilifu kwako"
John 17:20-21
ili kwamba wote wawe na umoja...kama, vile wewe Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako...ili kwwamba wao pia wawezekuwa ndani yetu
Mungu Baba yumo ndani ya Mungu Mwana na mwanaYumo ndani ya Baba. Wla wamwaminioa Yesu, Mungu mwana huwa na umoja na Baba na mwana wamwaminipo.
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu
Dunia
Hii humanisha watu wa duniani
John 17:22-23
Utukufu ule ulionipa mimi nimewapa wao
nimewaheshimu wafuasi wangu kama ambavyo wewe umeniheshimu mimi
ili kwamba waweze kuwa na umoja
Unaweza kutafsiri kama: "ili uweze kuwaunganisha kama ambavyo umetuunganisha sisi"
kukamilishwa katika umoja
kuwa kitu kimoja
ili ulimwengu ujue
ulimwengu ni watu
John 17:24
Baba...ulinipenda mimi kabla y kuumbwa kwa isingi ya ulimwengu
Mungu Baba amempenda Mungu mwana. Kabla Mungu hajauumba ulimwengu, nafsi za Mungu hupendana, na zitaendelea kupendana milele yote.
Nilipo mimi
hii inamaanisha mbinguni
ili waweze kuona utukufu wangu
ili waweze kujua ukuu wangu
kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu
Hapa Yesu anamaanisha wakati wa kabla ya uumbaji
John 17:25-26
Ulimwengu haukukutambua, lakini mimi nakujua; na hawa wanajua kuwa ulinituma
"ulimwengu hauna uzoefu wa kukujua wewe kama ninavyokujua; na hawa wanajua kuwa wewe umenituma"
jina
Hili linamanisha Mungu.
lile pendo...ulilonipenda
Upendo wa jinsi hii hutoka kwa Mungu na hulenga mema ya wengine, hata kama hauna maslahi binafsi. Upendo wa jinsi hii huwajali wengine bila kujali wanachofanya
Mungu mwenye haki
Hiki ni cheo cha muhimucha Mungu
John 18
John 18:1-3
Bonde la Kidron
Hili ni bonde liliko Yerusalem ambalo hutenganisha Mlima wa hekalu na Mlima wa mizeituni
palipokuwaa na bustani
hili lilikuwa shamba la mizabibu
John 18:4-5
Maelezo ya jumla:
Yesu anaanza kuongea na askari, waheshimiwa, na Mafarisayo
Naye Yesu hali akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake
Yesu alijua mambo yote yaliyopaswa kumpata
John 18:6-7
Mimi
Hapa neno "yeye" halipo kwenye tafsiri ya asili lakini limefananishwa tu na "mimi ndiye"
kuanguka chini
watu walianguka chini kwa sababu ya nguvu za Yesu
Yesu Mnazareth
Yesu, mtu wa kutoka Nazareth
John 18:8-9
Mimi ndiye
Hapa neno "yeye" halipo kwenye tasfsiri ya asili lakini limehusishwa tu.
Haya yalikuwa hivyo ili lile neno linalosema
"Neno" linamaanisha maneno ambayo Yesu aliyaomba.
John 18:10-11
Markusi
Markusi ni mtumishi wa kiume wa Kuhani Mkuu
Ala
Huu ni mkoba wakisu au sime unauzuia kisu kisimkate mwenye nacho
Kikombe
Hii inamaanisha 1) Kiasi cha mateso ambayo Yesu alitakiwa kuyapokea 2) Gadhabu ya Mungu ambayo Yesu ilimlazimu kuivumilia ili kuwalkomboa watu wake.
Je nisikinywee kikombe ambacho Baba yangu amenipa?
Yesu anahoji hili swali kuonesha msisitizo kwamba lazima ateseke.
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.
John 18:12-14
Maelezo ya jumla:
Mstari wa 14 unatoa maelezo yanayomhusu Kayafa
Wayahudi
hii inamaanisha viongozi wa Wayahudi
Walimkamata Yesu na kumfunga
Askari walimfunga Yesu mikono ili asitoroke
John 18:15-16
mwanafunzi mwingine, na yule mwanafunzi
Huyu ni mtume Yohana, mwandishi wa wa hii injili
John 18:17-18
Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wa huyu mtu?
"Wewe ni mmoja wa wanafunzi wa huyu mtu"
John 18:19-21
Kuhani mkuu
Huyu alikuwa Kayafa
Nimeumbia waziwazi ulimwengu
Yesu aliifanya huduma yake katika uma wa watu
Hawa watu
Hawa ni wale watu waliomsikia Yesu akifundisha
John 18:22-24
Je, hivyo ndivo inavyokupas kumjibu kuhani mkuu?
'Hivyo sivyo inavyokupasa kumjibu Kuhani Mkuu"
uwe shahidi kwa ajili ya uovu
"niambie makosa yangu niliyoyasema"
kama nimejibu vyema kwa nini kunipiga?
"kama nimejibu kwa ukweli usinipige"
John 18:25-27
Maelezo ya jumla:
Hapa habari inarudi kumwelezea Petro.
Je, wewe ni mmoja wa wanafunzi wake?
Swali hili linatoa msisitizo wa ukweli wa jambo
Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?
hapa neno "naye" linamaanisha Yesu
Kisha Petro akamkana tena
Hii inamaanisha kuwa petro alimkana kwa kujua kuwa alikuwa na Yesu.
na papo kwa papo jogoo akawika
Ikumbukwe kuwa Yesu alimwambia Petro kuwa jogoo atawika kabla hajamkana
John 18:28-30
Maelezo ya jumla:
Askari na washitaki wa yesu wanamleta kwa Kayafa. Mstari wa 28 unaeleza sababu zilizowafanya wasiingie katika Praitorio.
Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.
Huyu mtu ni mtenda maovu, na ni lazima tumlete kwako ili aadhibiwe"
Kumleta
Hili neno "kumleta" linamaanisha kumkabidhi kwa adui
John 18:31-32
Maelezo ya jumla:
Kwenye mstari wa 32 mwandishi anaelezea jinsi ambavyo yesu alitabiri kifo chake
Wayahudi wakamwambia
Hawa ni viongozi wa Wayahudi aliompinga Yesu na kumkamata.
sheria haituruhusu sisi kumpa tu adhabu ya kifo
Kulingana na sheria ya Kirumi, Wayahudi wasingweza kumuua mtu.
John 18:33-35
Mimi siyo Myahudi, au sivyo?
Hapa Pilato anauliza swali kuelezea jinsi ambavyo hana haja na tamaduni za Kiyahudi
watu wako mwenyewe
Wayahudi wenzako
John 18:36-37
Ufalme wangu si wa ulimwengu huu
Sentesihii yaweza kumaanisha 1) "Ufalme wangu si sehemu ya dunia hii" au 2) "Si hitaji ruhusa ya dunia hii kuwa mtawala wao" au "Si kwa kutokana na ulimwengu huu kwamba nina mamalaka ya kuwa mfalme."
Ili kwamba nisitolewe kwa Wayahudi.
"wangewazuia viongozi wa Kiyahudi kunikamata"
Sauti yangu
"mambo ninayoyaongelea" au "mimi"
John 18:38-40
kweli ni nini?
"Hakuna awezaye kujua kitu kilicho cha kweli"
Wayahudi
hii inamaanisha viongozi wa Kiyahudi
siyo huyu, ufungulie Baraba
tafsri kuonesha kuwa hawakumtaka Baraba bali Yesu
Baraba alikuwa mnyang'anyi
Hapa Yohana anaeleza Baraba alikuwa mtu wa aina gani
John 19
John 19:1-3
Salaam, mfalme wa Wayahudi
Hii "Salaam" inayoambatana na mkono ulioinuliwa ilitumika kwa msalimia Kaisari pekee yake. Wakati asakari wakitumia kofia ya miiba na vazi la dhambarau kwa kumkejeli Yesu, hawakumtambua kwa hakika kuwa ni mfalme.
John 19:4-6
Mimi sioni hatia yoyote ndani yake
Hii ni sawa na kusema kuwa sioni sababu ya kumwadhibu
taji ya miiba...vazi la dhambarau
taji na vazi la dhambarau ni vitu vinavyovaliwa na wafalme tu.
John 19:7-9
inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu
Yesu alihukumiwa kufa kwa kifo cha kusulibiwa kwa sababu ya kudai kuwa yeye alikuwa "mwana wa Mungu"
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo cha muhimu cha Yesu
Wewe uatoka wapi?
"Unatoka wapi? Pilato alimuliza Yesu kwa ajili ya kujua utambulisho wake. utamaduni wako unaweza kuwa njia maalumu ya kutambua utamaduni wa mtu.
John 19:10-11
Je, wewe huongei na mimi?
Pilato anaonyesha kushangazwa na Yesu kwa kutokuitumia nafasi hiyo ya kujiteteta. "Nijibu"
Usingekuwa na nguvu kama usingepewa toka juu
"Una mamalaka kinyume changu kwa sababu tu umepewa"
aliyenitoa
Neno "kutoa" linamaanisha kumkabidhi Yesu kwa adui, kama vile Yuda alivyomtoa Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi
John 19:12-13
ajaifanyaye kuwa mfalme
"madai ya kuwa yeye ni mfalme"
akamleta Yesu nje
Hii inamaanisha kuwa aliwaagiza askari kumleta Yesu nje il ikumwonyesha kwa makutano.
akakaa
Watu wakubwa walikaa wakati watu wengine amabao si wskubwa walisimama.
Kwenye kiti cha hukumu
Hiki ni kiti maalumu ambacho watu mhimu walikaa wakati wa kufanya maamuzi ya kiofisi. Utamaduni wako unaweza kuwa na njia tofauti wautaratibu huu.
Fuvu la kichwa
Hili ni eneo maalumu ambalo watu maalumu ndio wsalioruhusiwa kupaingia, Utamaduni wako unaweza kuwa na maeneo maalumu kama hili.
Kihebrania
Hii ilikuwa lugha ambayo wahebrania waliongea
John 19:14-16
Sentensi unganishi:
Muda umepita na sasa ni saa la sita, wakati Pilato anawaagiza askari wamsulibishe Yesu.
saa la sita
kama muda wa mchana
Pilato akwaambia Wayahudi
Hapa inamaanisha Pilato aliwaambia viongozi wa Kiyahudi
Je, mimi nimsulibishe mfalme wenu?
Pilato anawauliza Wayahudi ikiwa wanataka askari wake wamsulibishe Yesu.
John 19:17-18
kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa
Unaweza kutafsiri kama: "kwenye eneo ambalo watu wanaliita fuvu la kichwa"
ambalo kwa Kiebrania huitwa "Golgotha"
Kiebrania ni lugha ya Waisraeli
pamoja naye wanaume wawili
Unaweza kutafsiri kama: "pia waliwasulibisha wahalifu wengine wawili kwenye misalaba yao"
John 19:19-20
Pilato pia aliandika alama na kuiweka juu ya msalaba
hapa inamaanisha mtu aliyeandika kwa niaba ya Pilato na kuiweka juu ya msalaba wa Yesu
Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETHH, MFALME WA WAYAHUDI
Unaweza pia kutafsiri hii kama: "hivyo yule mtu aliandika maneno haya: Yesu ya nazarethi, mfalme wa Wayahudi"
Kiyunani
Hii ni lugha ya serikali ya Kirumi
John 19:21-22
Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato
Wakuu wa makuhani walienda mpaka Ikulu kumshitaki Yesu juu ya maneno na miujiza yake.
Niliyoyaandika nimeandika
Pilato anamaanisha kuwa hawezi kubadilisha maneno katika kibao
John 19:23-24
Maelezo ya jumla:
Mwishoni mwa mstari wa 24 kuna tofauti kutoka habari kwa kuwa Yohana anaelezea jinsi tukio hili linatimiza maandiko.
kanzu
askari waliweka kando kanzu na hawakuigawa
wakapiga kura
hivi ndivyo askari walivyogawana mavazi ya Yesu.
John 19:25-27
Yule mwanafunzi aliyempenda
Huyu ni Yohana mwandishi wa injili hii
Mwanamke, mtazame, mwanao huyu hapa
"Mwanamke, tazama na ufifkiri juu huyu mtu kama angekuwa mwano"
Mama yako huyu hapa
"fikiri juu ya huyu mwanamke kama angekuwa mama yako"
John 19:28-30
Siki
Hiki ni kinywaji cha makomamanga kilchokuwa kimechachushwa kwa muda mrefu
wakaweka
"Hawa" nia walinzi wa Kirumi
Sifongo
Hi ni kiufito kilichokuwa na uwezo wa kunyonya kimiminika
Akaisalimu roho yake
Yesu aliito roho yake kwa Mungu na kuruhusu mwili wake kufa
John 19:31-33
Wayahudi
Hii inamaanisha viongozi wa Kiyahudi
siku ya maandalio
Huu ni muda uliokuwa kabla ya pasaka ambao ulitumika kuandaa chakula
kuvunja miguu yao na kuiondoa
Unaweza kutafsiri kama, "kuvunja miguu ya waliosulibiwa na kuiondoa miili yao kutoka kwenye misalaba yao"
aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.
Unaweza kutafsiri kama, "ambaye walimsulibisha karibu na Yesu"
John 19:34-35
Naye aliyeona hili
Sentesi hii inatoa mukhutadha wa habari. Mwandishi ambaye ni (Mtume Yohana) anawafahamisha wasomaji kuwa yeye alikuwepo na kwamba tukiamini alichoandika
John 19:36-37
Hapana mfupa wake utakaovunjwa
"Hakuna atayevunja hata mmoja ya mifupa yake"
John 19:38-39
Yusuph wa Arimathaya
Yusuph kutoka mji wa Arimathaya
kwa kuwaogopa wayahudi
"Kwa kuwahofia viongozi wa Kiyahudi"
Nikodemo
Huyu ndiye aliyeenda kwa Yesu wakati wa giza
manemane na udi
Haya ni manukato yaliyo kabla ya mazishitumika kuandaa maiti
Mia moja
Kipimo cha mia moja
Ratli
"Ratli moja" ni sawa na kipimo cha gramu 31
John 19:40-42
Sasa mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani....hakuna mtu alikuwa amezikwa humo
Hapa mwandishi Yohana anatoa maelezo kuhusu mahali ambapo kaburi lilikuwa
Kwa sababu ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi
Kulingana na sheria ya Kiyahudi, hakuna mtu aliyeruhusiwa kufanya kazi baada ya jua kuzama. Ilikuwa ni mwanzo wa Sabato na Pasaka
John 20
John 20:1-2
Siku ya kwanza ya Juma
Jumapili
Mwanfunzi ambaye Yesualimpenda
Sentesi hii inaonekana kuwa ni njia ambayo Yohana aliitumia kumwonyesha yeye katika kitibu chote. Neno "upendo" linamaanisha upendo wa ndugu au upendo wa rafiki au kwa mwanafamilia
Wamemchukua
Mtu amechukua
John 20:3-5
mwanafunzi mwingine
Yohana anatumia neno hili kwa kuonyesha unyenyekevu akimaanisha yeye mwenyewe badala ya kutumia jina lake.
Sanda za kitani
Hizi zilikuwa nguo za mazishi zilizotumika kuuzongazonga mwili wa Yesu.
John 20:6-7
Sanda za Kitani
Hizi ni nguo azazovalishwa mfu kabla ya kuzikwa
leso ilyokuwa kichwani mwake
Hiki ni kitambaa kidogo ambacho hutumika kwa kufutia jasho usoni amabcho pia kilitumika kufunika uso wake
John 20:8-10
mwanafunzi mwingine
Yohana anatumia neno hili kwa kuonesha unyenyekevu akimaanisha yeye mwenyewe pasipo kutaja jina lake.
aliona na kuamini
Alipoona kuwa kaburi lipo wazi, aliamini ya kuwa yesu alikuwa amefufuka kutoka wafu
bado hawakuyajua maandiko
hapa mwandishi anawaongelea wanafunzi ambao hawakujua bado maandiko yanayosema kuwa Yesu angefufuka tena.
John 20:11-13
aliwaona malaika wawili na nguo nyeupe
Malaika walikuwa wamevaa nguo nyeupe
wakamwambia
walimuuliza
Kwa sababu wamemchukua Bwana wangu
Kwa sababu wameuchukua mwili wa Bwana wangu
Nami sijui walikomweka
Nami sijui walipouweka mwili
John 20:14-15
Yesu alimwambia
Yesu alimuuliza
Bwana, kama ni wewe uliyemchukua yeye
neno "yeye" hapa linarejjea kwa yesu
niambiie ulikomweka
niambie ulipokiweka
nami nitamchukua
Maria Magdalena anataka kuchukua mwili wa Yesu na kuuzika tena.
John 20:16-18
Rabboni
Neno "Rabboni" linamanisha rabi au mwalimu katika Matamushi ya Kiaramaic ya Mariamu
ndugu
Yesu alitumia neno "ndugu" akimaanisha wanafunzi wake
nitapaa kwenda kwa baba amabye pia ni baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.
Yesu alifufuka toka wafu kisha akatabiri kupaa mbinguni, akirudi kwa Baba, Mungu Baba
Baba yangu na Baba yenu
Hivi ni vyeo muhimu vinavyofafanua uhusiano kati ya Yesu na Mungu, na kati ya waumini na Mungu.
John 20:19-20
Siku hiyo, siku ya kwanza ya juma
hii inamaanisha Jumapili
Amani iwe kwenu
hii ni salamu ya kawaida"
akawaonyesha mikono yake na ubavu wake
"aliwaonyesha vle vidondo mikononi mwake na ubavuni.
John 20:21-23
amani iwe nanyi
hii nisalamu ya kawaida
Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi...akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu"
Mungu Baba alimtuma Mungu Mwana anayewatuma waumini katika nguvu ya ya Mungu Roho.
Baba
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu
watasamehewa
"Mungu atawasamehe"
Watafungiwa
"Mungu hatawasamehe"
John 20:24-25
Pacha
Tazama tafsiri tok Yohana 11:15
yule mwanafunzi mwingine walimwambia baadaye
neno "yule" linamaanisha Thomaso
Kma staona alama za misumari sitamini
Nitaamini tu pale nitakapoona alama za misumari na ubavu wake
Mikononi mwake
Neno "mwake" linamaanisha Yesu
John 20:26-27
Wanafunzi wake walikuwa chumbani tena
Neno "wake" linamaanisha Yesu
Amani na iwe nanyi
Hii ni salamu ya kawaida
asiyeamini
bila imani
John 20:28-29
umeamini
"umeamini kuwa niko hai"
pasipokuona
"ambao ambao hawajaniona nikiwa hai
John 20:30-31
ishara
Hii inamanisha miujiza inayotumika kuonyesha ushahidi kuwa Mungu ana nguvu zote na ambaye ana mamalaka kamili juu ya ulimwen
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo muhimu cha Mungu
Uzima katika jina lake
"Munaweza kuwa na uzima katika jina lake"
uzima
hii inamaanisha maisha ya kiroho
John 21
John 21:1-3
Baada ya mambo haya
"Baadaye kitambo"
na Tomaso aitwaye Didimasi
unaweza kutafsiri pia kwa kusema, "na Tomaso tuliyemwita Didimasi"
Didimasi
Maana ya jina hili ni "mapacha"
John 21:4-6
vijana
hii ni hali ya kusema rafiki zangu
mtapata wachache
maana yake, "mtakamata samaki wachache kwenye nyavu zenu"
tupeni ndani
vuteni nyavu ndani
John 21:7-9
aliyempenda
Huu ni upendo unaotoka kwa Mungu ambao hutazama zaidi mema ya wengine, hata kama hauna maslahi binafsi. Upendo wa aina hii huwajali zaidi wengine bila kujali wanachokifanya
(maana hakuwa amelivaa vizuri)
Hii ni kwa mujibu wa mukhutadha
Kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni)
Hii ni kwa mujibu wa mukhutadha
yapata dhiraa miambili
"mita tisini"dhiraa ni ndogo kuliko nusu mita
John 21:10-11
Simoni Petro kisha akaenda juu
Hii inamaanisha kuwa Petro alirudi kwenye mtumbwi
na akatoa nyavu nchi kavu
na akatoa nyavu na kuziweka ufukweni
nyavu ilikuwa haijararuka
Unaweza kutafsiri hii kama, "nyavu hazikuharibika
John 21:12-14
kifungua kinywa
mlo wa asubuhi
mara ya tatu
unaweza kutafsiri hii kama muda nambari tatu.
John 21:15-16
je, unanaipenda...wanipenda mimi
Hapa "upendo" linamanisha aina ya upendo unaotoka kwa Mungu, amabao unaangalia mema ya wengine, hata pale ambapo hakuna maslahi binafsi
wewe wajua kuwa mimi na kupenda wewe
Petro anajibu, anatumia neno kwa "upendo" ambalo linonyesha upendo kwa ndugu au upendo wa urafiki au upendo wa kifamila.
Lisha wanakondoo wangu
"Lisha watu wangu ninaowajali"
Chunga kondoo wangu
"Wajali watu wangu ninaowajali"
John 21:17-18
Je, wanipenda mimi?
Mara hii Yesu anapouliza swali hili anatumia neno kwa "upendo" ambalo linamanisha upendo wa ndugu au upendo wa urafiki au upendo wa kifamila
Lisha kondoo wangu
"Uwajali watu wangu ninaowajali"
Kweli, kweli
itafsiriwe kama ilivyo kwenye Yohana 1:49, 1:51
John 21:19
Sasa
Yohana analitumia neno hili kuonyesha kuwa anatoa maelezo ya mukhutadha kabla hajaendelea na simulizi
John 21:20-21
alimpenda
Huu ni aina ya upendo amabao hutoka kwa Mungu ambao huangalia mema ya wengine hata kama hauna maslahi binafsi. Aina ya upendo huu huwajali wengine, bila kujali wanachokifanya
kwenye chakula cha jioni
Hii inakumbushia chakula cha mwisho ambacho Yesu alikula na wanfunzi wake
Petro alimwona
Hapa neno "yeye" linalemlenga "mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda"
John 21:22-23
nataka abaki
Hapa "yeye", "a...ki", linamanisha "mwanafuzi ambaye Yesu alimpenda" Tazama 21:20
Nitakapokuja
Inamaaninisha kur duniani kwa Yesu mara ya pili, atakapokuja kutoka mbinguni.
hilo linakuhusu nini?
"usijihusishe na jambo hilo"
ndugu
Yesu ana anatumia neno hili kwa wanafuzi wake kama nduguze.
John 21:24-25
Taarifa za jumla:
Huu ndio mwisho wa Injili ya Yohana. Hivyo mwandishi ambaye ni Yohona anatoa salamu za mwisho na kusema kidogo kuhusiana na yeye mwenyewe.
mwanafunzi
mwanafunzi wa Yohana
ambaye hushuhudia kuhusu mambo yaleyale
neno kushuhudia kama lilivyotumika hapa linamaanisha kuona kitu
sisi tunajua
"sisi" hapa inamaanisha wale wanaomwamini Yesu
kama kila kitu kingeandikwa
unaweza kutafsiri pia kwa kusema, "kama mtu angeandika kila kitu"
hata dunia pia isingeweza kutosha vitabu vyote
Yesu alifanya miujiza mingi kuliko ambavyo watu wangeweza kuandika kwenye vitabu