Philippians
Philippians 1
Philippians 1:1-2
Sentensi unganishi
Mwandishi anatoa salamu kwa watu wa kanisa la Filipi
Maelezo ya jumla
Kwa sababu Paulo anaandika baadaye katika barua akisema "mimi," linaleta maana kwamba Paulo ndiye mwandishi na kwamba Timotheo ndiye alikuwa pamoja naye. Na maneno yote ya "wewe" na "ninyi" katika barua hii yanaongelea wakristo wa kanisa la Filipi katika wingi wao. Na neno "yetu" pengine linamaanisha wakristo wote akiwemo Paulo, Timotheo na wakristo wa Filipi.
Paulo na Timotheo
kama lugha yako ina njia maalumu ya kutambulisha waandishi wa barua, itumie hapa.
Timotheo, watumishi wa Yesu
"Timotheo. Sisi ni watumishi wa Kristo Yesu"
Kwa wale walitengwa katika Kristo
"kwa waumini wote katika Kristo Yesu"
waangalizi na wahudumu
" wazee wa Kanisa"
Philippians 1:3-6
Ninawashukuru kwa ushirika wenu katika injili
Paulo anamshukuru Mungu kwamba wafilipi wnahubiri injili pia. "Ninamshukuru Mungu kwamba mnatangaza injili"
Ninaujasiri
Ninauhakika
Yeye aliyeanza
"Mungu aliyeanza"
Philippians 1:7-8
Ni haki kwangu
"ni sahihi kwangu" au "ni vizuri kwangu"
nimewaweka moyoni wangu
"ninawapenda sana"
mmekuwa washirika wenza wa neema
"mmefanyika washiriki wa neema pamoja nami" au "kushiriki katka neema pamoja"
Mungu ni shahidi wangu
"Mungu anajua" au "Mungu anafahamu"
katika undani wa huruma ya Kristo Yesu.
Kirai "katika undani wa huruma" inaweza kutafsiriwa pamoja na kitenzi "upendo." "na ninawapenda kama Yesu Kristo alivyotupenda mno sisi sote"
Philippians 1:9-11
sentensi unganishi
Paulo anawaombea wakristo wa Filipi na kuzungumzia juu ya furaha iliyo katika mateso kwa ajili ya Bwana.
Paulo anazungumzia upendo kana kwamba kulikuwa na upinzani watu wangeweza kupata zaidi. iongezeke"
Katika maarifa na ufahamu wote
Hapa "ufahamu" maana yake ni Mungu kuweza kuwa wazi. "kama ujifunzvyo na kufahamu zaidi kuhusu nini ambacho kinamtukuza Mungu"
"kwa jinsi "mnavyojifunza na kufahamu kwa uwazi mambo yanayompendeza Mungu. "
Thibitisha
Hii hurejea kupima vitu na kuchukua vile ambavyo ni vizuri. "pima na chunguza"
mambo yenye adili
"kile kinachompendeza Mungu zaidi"
muwe safi pasipokuwa na hatia
Maneno" safi" na " kutokuwa na hatia"kimsingi yanabeba maana ile ile. Paulo anayatumia kwa pamoja ili kukazia usafi wa rohoni. "hali ya kutokuwa na lawama"
Ninyi pia mtajazwa
Paulo anazungumzia waamini kana kwamba walikuwa chombo cha kuwekea kitu amabacho kinaweza kujazwa na matunda. "Ili pia kwamba Yesu Kristo awasababishe kumtii Mungu zaidi na zaidi"
mjazwe na tunda la haki itokayo
Matendo mazuri ya mwamini ambaye Mungu aliyaweka wazi vizuri humfurahisha Mungu kama ambavyo tunda kukua kwenye ni mtamu kwa wale walao. "kuweza kumfurahisha Mungu na watu wengine kwa njia unayoishi sasa kwamba Mungu alikusamehe dhambi zako"
kwa utukufu na sifa ya Mungu
Maana ziwezekanazo ni 1) "Ndipo watamsifu na kumpa Mungu heshima kubwa 2)n"Ndipo watu watamsifu Mungu na kumpa Mungu heshima kubwa kwa sababu ya mambo mazuri waonayo ufanayayo." Hizi tafsiri ya mmoja mmoja inaweza kufanya kuhitajike sentensi mpya.
Philippians 1:12-14
Maelezo ya Ujumla
Paulo anasema kwamba mambo mawili yametokea kwa sababu ya "maendeleo ya injili": watu wengi ndani na nje waligundua kwa nini yuko gerezani, na Wakristo wengine hawana hofu kuhubiri habari njema.
sasa nataka
hapa neno" sasa" limetumika kuonesha mwanzo mpya wa barua
ndugu
hapa linamaanisha wakristo wenzake, likijumuisha wanaume na wanawake, kwa kuwa wauimini wote katika Kristo ni viungo katika familia moja ya kiroho, pamoja na Mungu, baba yao wa mbinguni.
mambo yaliyotukia kwangu
Paulo anazungumzia muda alipokuwa gerezani. mateso niliyoyapata kwasababu nilikuwa nimewekwa gerezani kwa sababu ya kumhubiri Yesu.
yameifanya injili iendelee sana
"yamesababisha watu wengine kumwamini Yesu"
kifungo changu changu katika Kristo kimejulikana
"Minyororo katika Kristo" ni neno linalosimama badala ya kuwa gerezani kwa ajli ya Kristo. "Kumejulikana" ni mfano kwa "kujulika." "Ilijulikana kwamba nipo katika minyororo kwa ajili ya Kristo"
minyororo yangu katika Kristo imejulikana...walinzi...yeyote mwingine
Hii inaweza kuanza muundo wa utendaji. "walinzi wote wa ikulu na watu wengi katika Rumi wanajua kwamba nipo katika minyororo kwa ajili ya Kristo"
minyororo yangu katika Kristo
Hapa Paulo anatumia kihusishi "katika" kumaanisha "kwa ajili ya." "minyororo yangu kwa ajili ya Kristo" au "minyonyororo yangu kwasababu nafundisha watu kuhusu Kristo"
minyororo yangu
Hapa neno "minyororo" linasimama badala "kifungo. "kifungo changu"
ikulu
Hili ni kundi la maaskari waliosaidia kulinda utawala wa Rumi.
Philippians 1:15-17
kwa hakika, hata Baadhi yao humtangaza Kristo
"Baadhi ya watu huhubiri habari njema ya Yesu"
kwa wivu na ugomvi
"kwasababu hawapendi watu wanisikilize mimi na wanapenda kusababisha matatizo"
wengine kwa nia njema
"lakini watu wengine hufanya hivyo kwasababu ni wapole na wanapenda kunisaidia"
mwishoni mwa hotuba yake
"Wale ambao wanamtangaza Kristo kwa nia mbaya"
Nimewekwa hapa kwa ajili ya kuitetea injili
Hii inaweza kuanza kwa muundo tendaji. Maana zinazowezekana ni 1) "Mungu amenichagua kuitetea injili" au 2) "nipo gerezani kwa sababu naitetea injili."
kwa ajili ya kutetea injili
"kumhubiri kila mmoja kuwa uhabari za Yesu Kristo ni za kweli"
Bali wengine wamtangaza Kristo
"bali wengine" au "bali mwingine anamuhubiri Kristo nje kwa hila na vita
wakati nipo katika minyororo yangu
Hapa neno "minyororo" linasimama badala ya kifungo. "while nimimefungwa" au "wakati nimefungwa"
Philippians 1:18-19
ni nini hii?
Paulo anatumia hili swali kuwaambia vile asikiavyo kuhusus hali aliyoandika katika 1:15. maana zaweza kuwa "haijalishi" neno "nitafikiria kuhusu hii" ilieleweka kama sehemu ya swali. "nitajali kuhusu nini?" au "Hivi ndivyo ninavyofikiri kuhusu hii"
katika njia yoyote ile, katika kusudi baya au zuri, Kristo anahubiriwa
"kwa kuwa watu wanamhubiri Kristo, hakuna shida, kama wanafanya hivyo kwa makusudi mazuri au kwa makusudi mabaya"
ninafurahia jambo hilo
"Nina furaha kwasababu watu wanamhubiri Kristo"
nitafurahia
"Nitasherekea" au "nitashangilia"
hili litaleta kufunguliwa kwangu
"kwa sababu watu wanamuhubiri Kristo, Mungu atanitoa kifungoni/ gerezani"
katika kufunguliwa kwangu
maana halisi ya "kufunguliwa," ni nini Mungu atamfungua Paulo kutoka, haiko wazi. maana hizi zinawezekana 1) Paulo alikuwa anarejea kusaidiwa kutoka katika katika hali mbya au 2) Paulo alikuwa narejea wazi wazi kuwa huru mbali na kifungo.
kupitia maombi yenu na msaada wa Roho wa Kristo Yesu
"kwa sababu mnaomba na Roho wa Yesu Kristo inanisaidia"
Roho wa Yesu Kristo
"Roho Mtakatifu"
Philippians 1:20-21
matarajio yangu ya uhakika na kweli
"hapa maneno " matarajio ya hakika" na "matarajio ya Kweli" yanamaanisha kimsingi jambo lile lile tu. Paulo anayatumia kwa pamoja ili kutilia mkazo kuonesha matarjio ya dhati aliyonayo. "Ninashawishika kwa dhati"
kwa ujasiri wote, kama ambavyo siku zote na sasa, Kristo atainuliwa"
Hii ni sehemu ya matarajio na matumaini ya Paulo. "lakini natarajia na kutumaini kwamba katika ujasiri wote, sasa kama siku zote, Kristo atainuliwa"
"katika ujasiri wote, sasa na siku zote"
"nitakuwa na ujasiri mkubwa sasa, kama siku zote nilivokuwa na"
Kristo atainuliwa kwenye mwili wangu wangu
kifungu hiki cha neno "mwili wangu" ni neno linalosimama badala vile Paulo amefanya kwenye mwili wake. Hii inaweza kuanza muundo tendaji. Yawezekana maana zikawa 1) "Nitamtukuza Kristo kwa kile nifanyacho" 2) "watu watamsifu Kristo kwa sababu ya kile nifanyacho"
Ikiwa ni kwa uzima au kwa kifo
"kama nitaendelea kuishi au nikifa"
Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo na kufa ni faida"
"Kwa maana kama nikiendelea kuishi, nitaishi kumtukuza Kristo, na kama nikifa, hiyo itakuwa nzuri.
Philippians 1:22-24
kama kuishi katika mwili huleta tunda katika kazi yangu
Neno "tunda" hapa limetumika kurejelea matokeo mazuri ya kazi ya Paulo. " kama kuishi katika mwili kuna nipa fursa ya kuwatia moyo watu ili waamini katika Kristo."
inamaana kwamba matunda ya kazi yangu
Neno "tunda" hapa linarejea matokeo mazuri ya kazi ya Paulo. "inamaana kwamba nitaweza kufanya kazi na kazi yangu itazaa matokeo mazuri" au "maana nitakuwa na nafasi zaidi kuwatia moyo watu kumwamini Kristo"
Ninasukumwa katika vitu viwili
Paulo anazungumzia vile ilivo vigumu kwake kuchagua kati ya kuishi na kufa kama vitu vizito vnavyopingana, kama mawe au magogo, vilikuwa vikimsukuma kwenda kinyume katika wakati mmoja. Lugha yako inaweza kupendelea kupinga kuvuta kuliko kusukuma. "nipo ndani ya mvutano. Sijui kama naweza kuchagua kuishi au kufa"
Ninahamu ya kuuacha mwili na kuwa na Kristo
Paulo anatumia tafsida hapa kuonyesha kwamba haogopi kufa. "ningependa kufa kwa sababu nitaenda kuwa na Kristo"
Philippians 1:25-27
Kwa kuwa nina uhakika juu ya hili
"Kwa kuwa ninauhakika kwamba ni vizuri kwako kwamba ninaenedelea kuishi"
ninajua nitabaki
" Ninajua kuwa nitaendelea kuishi or ninajua kwamba nitabaki katika mwili, yaani sitakufa"
Ili kwamba kwa mimi
"Hivyo basi kwa sababu ya mimi" au "Kwa hiyo basi kwa sababu ya kile nifanyacho"
kwamba mmesimama imara katika roho mmoja...mkishindania imani ya injili kwa pamoja.
Haya mambo mawili vinashirikiana maana moja kusisitiza umuhimu wa umoja.
kushindana pamoja
"kufanya kazi kwa bidii pamoja"
imani ya injili
ina maana ya "kueneza imani ambayo imejengwa juu ya injili ya Kristo" au "kuamini na kuishi kulingana na habari njema inavyotufundisha"
Philippians 1:28-30
na msitishwe na kitu chochote
hili ni agizo kwa Wakristo wa Filipi kuwa wasiogope kitu chochote.
Hii ni kwao ni ishara ya uharibifu . Bali kwenu ni ishara ya wokovu, kutoka kwa Mungu
"Ujasiri wenu utawaonyesha kwamba Mungu atawaharibu. Pia itawaonyesha kwamba Mungu atawaokoa"
kwa maana mna ugomvi uleule kama mlivyoona na ule mnaosikia ninao hata sasa
Ndiyo maana mmekuwa na ugomvi ua ushindani uleule kama mlivyoona kwangu na kwa sasa mnasikia kuwa bado ninao.
Philippians 2
Philippians 2:1-2
Sentensi Unganishi
Paulo anawashauri waamini kuwa katika hali ya umoja na unyenyekevu na kuwakumbusha mfano wa Kristo.
Ikiwa
"Ninaamini ni kweli"
ikiwa kuna kutia moyo katika Kristo
"kwamba Kristo amewatia moyo"
ikiwa kuna faraja kutoka katika pendo lake
"ikiwa pendo lake limekupa faraja"
ikiwa kuna ushirika wa Roho
"ikiwa una ushirika pamoja na Roho"
ikiwa kuna rehema na huruma
"ikiwa mmezoea matendo mengi ya Mungu ya huruma na rehema"
fanya furaha yangu
Paulo hapa anazungumzia furaha kana kwamba kilikuwa kimiminika kinajazwa kwenye kibebeo. "Kumenisababisha kusifu mno"
Philippians 2:3-4
Msifanye kwa majivuno au majivuno
"Usijihudumie mwenyewe au kujiona ni bora kuliko wengine"
Kila mmoja asiangalie mahitaji yake mwenyewe, bali pia ajali mahitaji ya wengine
"usiangalia tu kile unachohitaji, bali nini wengine wanahitaji pia"
Philippians 2:5-8
Muwe na nia moja kama aliyokuwa nayo Kristo
"Kuwa na nia moja ambayo Kristo Yesu alikuwa nayo" au "fikirieni vile ambavyo Kristo Yesu alivyofanya"
hakujali kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho
hapa Paulo anazungumzia usawa na Mungu Baba kana kwamba kulikuwa na kitu ambacho Kristo angeweza kushikilia kwenye mikono yake.
alijishusha mwenyewe
Paulo anamzungumzia Kristo kana kwamba alikuwa kitu cha kubebea ili kusema kwamba Kristo alikataa kutenda katika nguvu ya uungu wake katika kipindi huduma yake duniani
Alijitokeza katika mfano wa mwanadamu. Alinyenyekea
"Maneno "alijitokeza...kama" ni lahaja ya "kuwa." "Kuwa mwanadamu, alinyenyekea"
kuwa mtumwa hadi kifo
Paulo hapa anazungumzia kifo katika njia ya umbo. Anayetafsiri naweza kuielewa aidha kama mfano wa eneo (Kristo alipitia kifo) au kama mfano wa mda (Kristo alitii hata mpaka wakati alipokufa).
kifo cha msalaba
"kufa kwenye msalaba"
Philippians 2:9-11
jina kuu lipitalo kila jina
Hapa "jina" linasimama badala ya cheo au heshima kuu. "cheo ambacho ni juu ya cheo kingine" au "heshima ambayo ipitayo heshima yeyote"
lipitalo kila jina
Jina ni muhimu zaidi, zaidi kusifiwa kuliko jina jingine lolote.
katika jina la Yesu
Yawezekuwa maana hii "wakati kila mmoja anaposikia jina Yesu"
kila goti lipigwe
Hapa "got" inarelea utu wote, na liiname chini ni mfano wa kuinama kwa kuabudu. "kila mtu atamwabudu Mungu"
juu ya ardhi
yamkini maana zikawa 1) sehemu ambayo watu waendayo wakati wafapo au 2) sehemu ambayo mapepo washipo.
kila ulimi
Hapa "ulimi" inarejea kwenye utu wote. "kila mtu" au kila "kiumbe"
kwa utukufu wa Mungu baba
Hapa neno "kwa" linaonyesha matokeo: "na matokeo ambayo watamsifu Mungu Baba"
Philippians 2:12-13
Sentensi Unganishi
Paulo anawatia moyo Wakristo wa Filipino na kuwaonyesha jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo mbele ya wengine na na kuwakumbusha mfano wake.
mpendwa wangu
"wapendwa wangu waamini"
katika uwepo wangu
"wakati nikiwa nanyi hapo"
katika kutokuwepo kwangu
"wakati pasipo uwepo wangu nanyi hapo"
wajibikieni wokovovu wenu
"kuendelea kumtii Mungu"
kwa hofu na kutetemeka
neno "hofu" na "kutetemeka" kimsingi inamaana moja. Paulo anayatumia kusisitiza utakatifu mbele za Mungu" "tetemeka na hofu" au "na utakatifu wa ndani"
wote kunia na kutenda
"Mungu hutenda kwa hiyo basi mtatamani kumtii na kwa hiyo basi mtamtii"
Philippians 2:14-16
manung'uniko na uaminifu
Paulo anaeleza wazo moja kutumia maneno ya hasi na chanya. "bila kosa kabisa"
watoto wa Mungu bila lawama
"watoto wa mungu bila kubadilika" au mtoto wa Mungu mkamilifu"
kung'aa kama mwanga
Hapa Paulo anawazungumzia waamini kana kwamba walikuwa mwanga waking'aa gizani, kuwasaidia wengine kutafuta njia ya kumheshimu Mungu. " ishi katika nija ya kumheshimu Mungu"
katika dunia
Hapa "dunia" inarejea kila kitu na tabia ambacho hakimwabudu Mungu
uasi na uovu
haya maneno mawili kimsingi ni kitu kimoja. Paulo anayatumia kusisitiza jinsi kizazi kilivyo kiovu. "kiuvo kabisa"
Shikeni sana neno la uzima
Paulo hapa anazungumzia neno la Mungu kanakwamba lilikuwa kitu ambacho kingeweza kushikika.
kutukuza
"kufurahia" au "kuna na furaha"
katika siku ya Kristo
hii inarejea wakati Yesu atakaporudi kuchukua himaya yake na kutawala dunia nzima. "wakati Yesu atakapokuaja"
sikupiga mbio bure wala sikutaabika
Msisitizo "kupiga mbio bure" na "kutaabika bure" hapa inamaanisha kitu kimoja. Paulo ameyatumia haya maneno yote kusisitiza vile alivyofanya kwa bidii kuwasaidia watu kumwamini Yesu. "sikufanya kazi kwa nguvu bila kitu"
mbio
mara chache maandiko yamezungumza kama mwenendo wa kila mmoja. kupiga mbio ni kuishi maisha yanayoshadidiana.
Philippians 2:17-18
Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabihu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote
Paulo anazungumzia kifo chake kana kwamba kilikuwa ni kifo cha kuteketeza mnyama ambayo mafuta yalimiminwa. Kile Paulo alimaanisha ni kwamba alikuwa tayari kufa kwa ajili ya Wafilipi kama hiyo ingewafanya wamheshimu Mungu. Pia, hii inaweza kuonyesha katika muundo kamili. "Lakini, hata kama Warumi waliamua kunibagua, nitafurahi katika kifo changu kama kifo changu kitafanya imani yenu na utii zaidi kwa kumheshimu Mungu"
vilevile ninyi pia mnafurahi pamoja nami
Maelezo haya mawili kwa pamoja ni alama ya hiyo furaha. " "ninataka mfurahi pamoja nami"
Philippians 2:19-21
Sentensi unganishi
Paulo anawaambia waumini wa Filipi kuhusu hili wazo la kumtuma Timotheo baada ya mda mfupi na watamtumia Epafradito kama mtu maalumu
Lakini natumaini katika Bwana Yesu
"Lakini, kama Bwana Yesu atapenda, natumaini"
Kwa kuwa sina mwingine aliye na mtazamo kama mimi
"Hakuna mwingine hapa awapendaye kama yeye awapendavyo"
Wengine wote ambao
Hapa memo "wengine" linarejea kwenye kundi la watu Paulo hawezi kusikia anaweza kuwaamini kuwatuma kwa Wafilipi. Pia Paulo anaeleza kuvunjwa moyo na kundi, ambao wangeweza kuondoka, lakini Paulo hawaamini kuhitimisha makusudi yao.
Philippians 2:22-24
kama mtoto anayemhudumia baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami
Paulo anamzungumzia Timotheo, ambaye alimtumikia Kristo pamoja na Paulo, kana alikuwa mtoto akimhudumia baba yake. Paulo anasisitiza mahusiano ya baba na mtoto alinayo pamoja na Timotheo katika kumtumikia Mungu.
katika injili
Hapa "injili" inasimama kama kazi ya kuwaambia watu kuhusu Yesu. "katika kuwaambia watu kuhusu injili"
Nina hakika katika Bwana kwamba mimi mwenyewe nitakuja hivi karibuni
"Ninauhakika, kama ni mapenzi ya Bwana, kwamba nitakuja hivi karibuni"
Philippians 2:25-27
Epafradito
Hili ni jina la mtu aliyetumwa na kanisa la Filipi kumhudumia Paulo gerezani.
mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu
Hapa Paulo anamzungumzia Epafradito kana kwamba alikuwa askari. Anamaanisha kwamba Epafradito amejifunza na kuamua kumtumikia Mungu, haijalishi ambavyo mambo makubwa yakayomsonga. "muumini mwenzangu ambaye anafanya kazi na kusumbuka pamoja nasi"
na mjumbe wenu kwa ajili ya mahitaji yangu
"na ambaye aletaye ujumbe wenu kwangu na anisaidiaye wakati ninapokuwa mhitaji"
alikuwa na hofu, na alitamani kuwa pamoja nanyi nyote
"alikuwa na hofu na alitaka kuwa nanyi nyote"
huzuni juu ya huzuni
sababu ya huzuni ingeweza kutengenezwa wazi. "huzuni ya kumpoteza kujumlisha na huzuni aliyokuwa nayo kuwa gerezani"
Philippians 2:28-30
nitaondolewa wasi wasi
"sintoogopa kama nilivyokuwa"
Mkaribisheni Epafradito
"mpokeeni Epafradito kwa furaha"
katika Bwana kwa furaha
"kama muumini mpendwa katika Bwana pamoja na furaha yote"
alikaribia kufa
hapa Paulo anzungumzia kifo kana kwamba kilikuwa ni sehemu ambayo angeweza kwenda.
kufanya kile ambacho hamkuweza kufanya katika kunihudumia
Paulo anzungumzia mahitaji yake kana walikuwa chombo cha kubebea kwamba Epafradito alijazwa vitu vizuri kwa ajili ya Paulo.
Philippians 3
Philippians 3:1-3
Sentensi unganishi
ili kuwaonya waumuni wake wapendwa kuhu Wayahudi ambao wangependa kupata kufwata sheria za zamani, Paulo anatoa ushuhuda wake kuhusu ambavyo alivyo watesa waamini.
Hatimaye, ndugu zangu
"Sasa kutembea pamoja, ndugu zangu"
ndugu
neno hili humaanisha Wakristo wenza, ikijumuisha wanaume na wanawake, kwa kuwa waumuni wote katika Kristo ni washiriki wa familia moja ya kiroho, ambayo Mungu ni baba wa mbinguni.
furahini katika Bwana
"kuweni na furaha kwa sababu ya yote Yesu aliyafanya"
usumbufu
kuudhi
haya mabo yatawapa usalama
Hapa "haya mambo" inarejea kwa mafundisho ya Paulo.
kujihadhari
"kuwa makini na" au "kujihadhari kwa"
mbwa...watenda kazi wabaya...pruni
Haya ni maneno matatu tofauti ya kueleza kundi moja la walimu wa uongo. Paulo anatumia maelezo imara kuonyesha hisia zake kuhusu hawa Wayahudi walimu.
Mbwa
Neno "mbwa" lilitumiwa na Wayahudi likimaanisha wale waliokuwa siyo Waisrael.Walitazamwa kama wachafu. Paulo anawalinganisha walimu wa uongo kama tusi. Kama kuna mnyama wingine katika utamaduni wenu anayefikiriwa kuwa mchafu, au anatumiwa kama mchafu, unaweza kutumia mnyama huyu badala yake.
wajikataaokatika miili yao
Paulo anabagua kuhusu kitendo cha tohara kuwatukana walimu wa uongo. Walimu wa uongo wanafundisha Mungu atamwokoa mtu aliyetahiriwa tu, ambaye amekatwa sehemu ya mbele ya ngozi.Hili tendo lilitakiwa lifanyike kwa sheria ya Musa kwa wanaume wote wa Israeli.
Kwa kuwa sisi
Paulo anatumia "sisi" kurejea yeye mwenyewe na waamini wa kweli katika Kristo, pamoja na waamini wa Wafilipi
tohara
Paulo anatumia kirai/kifungu cha maneno kurejea waamini katika Kristo ambao bado hawajatahiriwa katika mwili lakini wametahiriwa katika kiroho, maana yake ni kwamba wamempokea Roho Mtakatifu kupitia imani. "watu wa Mungu wa kweli"
hakuna ujasiri katika mwili
"msiamini kwamba kukata sehemu ya mwili pekee kunaweza kumpendeza Mungu"
Philippians 3:4-5
Hata hivyo.
"Bado" au "Hata hivyo"
Mimi mwenyewe ningeweza kujivunia mwili. Kama kungekuwa na mtu wa kuutumainia mwili huu, mimi ningeweza kufanya hivyo zaidi.
Hii hali ya kufikirika ambayo Paulo anasema kama ingekuwa inawezekana kuwa Mungu anaokoa watu kwa misingi wa yale waliyofanya, basi Mungu angekuwa kwa uhakika amemuokoa yeye: "Kama yeyote angeweza kuwa amefanya mambo ya kutosha kumpendeza, ingekuwa kuliko mtu yeyote"
Mimi mwenyewe
Paulo anatumia "mimi mwenyewe" kwa kusisitiza. "hakika mimi"
Nilitahiriwa
"Kuhani alinitahiri mimi"
Siku ya nane
"siku saba baada ya kuzaliwa kwangu"
Mwebrania wa Waebrania
"mtoto wa Mwebrania aliye na wazazi wa Kiebrania"
katika kutimiza sheria ni Farisayo
Kama Mfarisayo, "hakika nilijitoa katika sheria"
Philippians 3:6-7
Kwa juhudi zangu nililitesa Kanisa
Nilidhamiria kuwaumiza waumini wa Kikiristo
kwa kuitii haki ya sheria, sikuwa na lawama kisheria
"Nilitii sheria sheria yote kikamilifu"
mambo yote niliyaona kuwa faida kwangu
hapa Paulo anajea kwenye sifa alizozipata kwa kuwa Mfarisayo mwenye shauku.
Nayahesabu yote kama takataka
Paulo anamalizia kwamba matendo yake ya haki katika dini yalikuwa bure mbele Kristo.
Philippians 3:8-11
Kwa kweli
"Kwa uhakika"au Kweli kweli"
Nayahesabu
anaelezea na kuweka msisitizo tangu pale paulo alipo acha kuwa Falisayo na kuwa mfuasi na muumini wa Yesu Kristo
Nayahesabu mambo yote kuwa bure
Paulo anaeleza kuwa ni upuuzi kuweka matumaini katika mambo mengine pasipo Kristo Yesu
kwa sababu ya ubora wa kumjua Kristo Yesu Bwana wangu ni wathamani zaidi"
kwa sababu ya kumjua Kristo Yesu Bwana wangu
Kwa ajili yake nimeacha mambo yote
"Kwa sababu yake ninatarajia kutupa kila kitu mbali"
kuweka mbali
tumia neno lako unalifahamu kwa ajili ya usivyovihitaji milele.
Nayahesabu kama takataka
Paulo anazungumzia vitu ambavyo alivyokuwa anavitumainia lakini baadae anaviona kama takataka na kuvitupa kwenye jalala.
ili nimpate Kristo
"ili nimpate Kristo peke yake"
na niwe ndani yake
Kirai "kupata" ni lugha ambayo inasisitiza wazo la "kuwa" "na kuwa pamoja na Kristo"
Sina haki yangu binafsi kutoka kwenye sheria
"Sijaribu kumpendeza Mungu mimi mwenyewe kwa kutii sheria"
Nguvu ya ufufuo wake
"Ni kufahamu nguvu ya ile itupayo uzima"
ushirika katika mateso yake
ni ile hali ya kushiriki mateso yake
Na nimebadilishwa na Kristo katika mfano wa kifo chake
Neno "badilisha"lina maanisha kugeuza kitu katika hali nyingine kifo cha kimeleta matokeo katika uzima wa milel. Hivyo Paulo anataka kifo chake kifanane na kile cha Yesu,kwamba aweze kuupata uzima wa milele
angalau niweze kuwa na matumaini katika ufufuo wa wafu
Neno "angalau" Paulo hajui nini kinakwenda kutokea katika haya maisha, lakini chochote kitakachotokea, kitakuwa matokeo ya maisha milele. "hivyo basi, haijalishi nini kimetoke sasa, nitaendelea kuishi hata nitakapokufa"
Philippians 3:12-14
Sentensi unganishi
Paulo anawaagiza waumini wa Filipi kufuata mfano wake kwa sababu ya mbingu na miili mipya iniyowasubiria waamini. Anazungumza vile alivyofanya kwa juhudi ili kuwa kama Krsto, akijua kwamba Mungu atamruhusu aishi mbinguni milele.
Nimeishayapata
Hii inajumuisha katika kumfahamu Krist, kufahamu nguvu za ufufuo wake, mateso yake na kupata kile tunachostahili katika ufufuo na kifo chake Kristo Yesu
au kwamba nimekuwa mkamilifu
"Kwa hiyo mimi sio mkamilifu" au "hivyo mimi sijakomaa bado"
Bali najitahidi
"Bali ninajaribu"
Naweza kupata
"Ninaweza kuyapokea"
kile ninachoweza kukipata katika Krsto Yesu Bwana wetu
"Hii inaweza kuanza na muundo kamili. "kwa sababu ndio maana Yesu ameniita wake"
Ndugu
Tafsiri kutoka 1:12
Nimekwisha kupata mambo haya
"haya mambo yote bado mmiliki wake ni mimi"
Nasahau ya nyuma natazamia ya mbele
Kama mwanaraidha kwenye mstari hashulikii mambo ya kwenye mstari yeye anaangalia yaliyoko mbele yake. "Mimi sijali kile nilichofanya nyuma; mimi ninashughulikia kwa bidii niwezavyo kupata kilichoko mbele yangu"
Najitahidi kufikia lengo kusudi ili niweze kupata tuzo ya juu ya wito wa Mungu katika Kristo Yesu
Kama mwanariadha anakimbia kwenda mbele kwa ajili ya kuvuka mstari. Paulo anakimbia mbele katika kutumika na kuishi katika maisha ya kumtii Kristo.
juu ya wito
Paulo anazungumzia kuishi milele na Mungu kana kwamba Mungu alimwita Paulo na kumtuma.
Philippians 3:15-16
Sisi tulioukulia wokovu, tunapaswa kuwaza namna hii.
Paulo alitaka wakristo wenzake wawe na hamu ile ile kama yeye alivyo. Kuwa imara katika imani Kufikiri katika jambo moja.
Mungu pia atalifunua hilo kwenu
"Mungu pia atalifanya wazi kwako" au "Mungu atakuhakikishia unalijua"
Mungu atakifunua hilo kwenu
Mungu ataweza wazi hilo jambo au kitu hicho kwako/kwenu
Kwa vyovyote tulivyokwisha kuwa , na tuenende katika hali hiyo
Na tuendelee kuutii ukweli wa neno la Mungu ule ambao tumekwisha pata tayari.
Philippians 3:17-19
Niigeni mimi
"Fanya yale ninayofanya"au ishi kama ninavyoishi.
ndugu
neno hili humaanisha Wakristo wenza, ikijumuisha wanaume na wanawake, kwa kuwa waumini wote katika Kristo ni washiriki wa familia moja ya kiroho, ambayo Mungu ni baba wa mbinguni.
wale wanaotembea kwa mfano wetu
"wale wanaoishi kama ninavyoishi au wale tayari wanafanya yale niyafanyayo"
wengi wanaishi... kama maadui wa msalaba wa Kristo
Haya maneno ni wazo kuu la Paulo katika mstari huu.
Wengi wanatembea
"Wengi wanaishi"
wale ambao mara nyingi nimewaambieni , na sasa na nawaambia kwa machozi
Paulo anaingilia/anadakia wazo lake kuu kwenye haya maneno ambayo yanaeleza "nyingi."
Nimewaambia mara nyingi
"Nimewaambia mara nyingi"
ninawaambia kwa machozi
"ninawaambia kwa huzuni kubwa"
kama maadui wa msalaba wa Kristo
Hapa "msalaba wa Kristo" inarejea kwa mteso ya Kristo na kifo" Maadui ni wale wasemao wanamwamini Yesu lakini hawako tayari kuteseka au kufa kama Yesu alivyofanya.
Mwisho wao ni uharibifu
"Siku moja Mungu atawaharibu"
miungu wao ni tumbo
Hapa "tumbo" hurejea kwa matamanio ya furaha ionekanayo. Kuita miunga yao inamaana kwamba wanataka heshima ya kuonekana zaidi kulikuwa wanavyotakiwa kumtii Mungu. "wanatamani chakula na heshima nyingine zaidi kuliko kutamani kumtii Mungu"
kiburi chao kipo katika aibu yao
Hapa "aibu" inasimama badala ya matendo ambayo watu wangetakiwa kuonea aibu lakini hawafanyi hivyo. "wanajivunia vitu ambavyo vitawasababishia aibu"
Wakifikiria mambo ya kidunia
Hapa "kidunia" inarejea kila kitu ambacho kitoacho heshima ya kuonekana na hawamheshimu Mungu "Yate wafikiriavyo ni kile kiwapocho heshima wao kuliko kitakacho mpa heshima Mungu"
Philippians 3:20-21
Maelezo ya jumla:
Kwa matumizi ya Paulo ya "yetu" hapa, amejijumuisha yeye na waamini katika Filipi
Uraia wetu uko mbinguniau
"mji wa nyumbani kwetu ni mbinguni"au nyumbani kwetu halisi ni mbinguni.
Atabadilisha miili yetu
"atabadilisha miili hii minyonge,miili ya asili au tuliyonayo hapa duniani"
kuwa kama mwili wake wa utukufu
"katika miili ifananayo na mwili wake wa utukufu"
mwili, unaowezesha kuvidhibiti vitu vyote kweke
"atabadilisha miili yetu kwa ileile anayotumia kuvitawala vitu vyote"
Philippians 4
Philippians 4:1-3
Sentensi unganishi
Paulo anaendelea na baadhi ya maelekezo kwa waamini wa Filipi kuhusu umoja na kuwapa maelekezo kuwasaidia kuishi kwa ajili ya Bwana.
Maelezo ya Jumla
Wakati Paulo anaposema, "watenda kazi wa kweli pamoja," "neno wewe ni umoja. Paulo hasemi jina la mtu. Anamuita hivyo kuonyesha amefanya kazi na Paulo kueneza injili.
Kwa hiyo wapendwa wangu ambao nawatamani
"Waumini wenzangu, nawapenda na ninatamani sana kuwaona"
ndugu
hapa anamaanisha Wakrsto wenza, ikijumuisha wanaume na wanawake, kwa kuwa waumini wote katika Kristo ni washiriki wa familia moja ya kiroho, ambayo Mungu ni baba wa mbinguni.
Furaha na taji yangu
Paulo anatumia neno "Furaha"akimaanisha kuwa kanisa la Filipi nicho kisababishi cha furaha yake. Taji ilitengenezwa kwa majani na mtu aliivaa kichwani kwake kama ishara ya heshima baada ya ushindi alioupata kwenye mchezo. Neno "taji" linamanisha kuwa kanisa la Filipi lilimletea Paulo heshima kwa Mungu. AT:" Mnanipa furaha kwa sababu mmemwamini Yesu, na ninyi ni zawadi na taji
Kwa njia hii simameni imara katika Bwana, enyi rafiki wapendwa
"Kwa hiyo endeleeni kuishi kwa Bwwana katika namna ambayo nimewafundisha, enyi marafiki wapendwa"
Ninamsihi Audia, na ninamsihi Sintike
Hawa ni wanawake waumini waliomsaidia Paulo katika kanias la Filipi. Ninamsihi Audia, na ninamsihi Sintike
Muwe na nia ileile katika Bwana
"Sentensi hii ya "muwe na nia ileile" inamaanisha kuwa na tabia au mawazo yaleyale. "kukubaliana ninyi kwa ninyi kwa kuwa nyote mnamwamini Bwana yuleyule
pamoja nanyi pia
Hapa "wewe" inarejea kwa "mtenda kazi mpendwa" and kama umoja
mtenda kazi
hiki kifungu cha maneno kinatokana na kilimo, ambapo wanyama wawi wangweza kuunganishwa kwenye kongwa/ yoki. "mtenda kazi"
Pamoja na Kelement
Kelement alikuwa Muumin na mtenda kazi katika kanisa laFilipi
Ambao majina yao yamenandikwa kwenye kiabu cha uzima
"Ambao majina yao Mungu ameyaandika kwenye kitabu cha uzima"
Philippians 4:4-7
Muwe na furaha itokanayo na Bwana siku zote. Tena nasema muwe na furaha
Paulo anawaambia wakristo wa Filipi. Airudia amri ya kufurahi ili kuonyesha msisitizo wa umhimu wa kufurahia. "Furahini kwa sababu ya kile ambacho Bwana amefanya, tena nasema iweni na furaha"
Bwana amekaribia
Sentensi hii imetumika kulenga maana mbili ambazo ni: 1) Bwana Yesu Kristo yuko karibu na wakristo katika roho. 2) Siku ya Bwana Yesu kurudi duniani iko karibu
bali fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kuomba, kusali na kushukuru, mahitaji yenu yajulikane na Mungu
"mwambieni Mungu mahitaji yenu kwa kusali kushukuru"
Iliyo juu ya fahamu zote
"ile iliyozaidi ya uelewa wetu"
italinda mioyo na mawazo mawazo yenu
Hii inawakilisha amani ya Mungu kama askari alindaye hisia zetu na mawazo yetu kutoka kwenye hofu. "itakuwa kama askari na akilinda hisia zako na mawazo kutoka kwenye uoga kuhusu masumbuko ya haya maisha"
Philippians 4:8-9
Hatimaye
Hili ni hitimisho la sehemu hii ya waraka. Paulo sasa anaelekea kutoa muhtasari wa jinsi wakristo wanavyotakiwa kuishi pale wanapohitaji amani ya Mungu.
ndugu
Neno hili humaanisha Wakristo wenza, ikijumuisha wanaume na wanawake, kwa kuwa waumini wote katika Kristo ni washiriki wa familia moja ya kiroho, ambayo Mungu ni Baba wa mbinguni
kama kuna mambo ya upendo
"ni mambo yanayopendeza"
kama kuna mambo yenye taarifa njema
"haya ni mambo ambayo watu huyatamani" au "mambo ambayo watu huyaheshimu"
kama kuna mambo ya busara
"haya ni mambo ya busara na tabia njema"
na kama kuna mambo yanayohitaji sifa
"kama kuna kisababishi cha sifa"
yale miliyojifunza, mliyopokea, na kuniona nikifanya
'yale niliyowafundish na kuwaonyesha"
Philippians 4:10-13
Sentensi Unganishi:
Paulo anazungumzia kuhusu waamini wa Filipi wamekuwa wakimsaidia kifedha na kumalizia na salam na shukran.
kuridhika
"kutosheka" au "kufurahi"
katika mazingira yote
"haijalishi mazingira niliyo nayo"
Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa...kuwa na vingi
Paulo anajua jinsi ya kuishi maisha ya furaha aidha akiwa hana au akiwa navyo.
namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhitaji
Ki-msingi sentensi hizi mbili zinamaanisha kitu kile kile. Paulo huzitumia kusisitiza kuwa amejifunza kurithika katika mazingira ya namna yeyote ile.
Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na yeye anitiaye nguvu.
"Naweza kufanya mambo yote kwa sababu Kristo hunipa nguvu"
Philippians 4:14-17
katika dhiki zangu
"wakati ambapo mambo yanakuwa magumu"
mwanzo wa injili
Hii humanisha wakaati Paulo alipokuwa akisafiri kwenda maeneo mbalmbali kwa ajili ya kuwaambia watu habari za Yesu.
hakuna kanisa lililoniwezesha katika mambo yanayohusu utoaji na kupokea isipokuwa ninyi peke yenu.
"ninyi ndiyo kanaisa pekee lililonitumia pese au mlionisaidia"
nasema ili mpate matunda yaletayo faida kwenu
Paulo analinganisha zawadi za kanias na utajiri wa mtu ambao unaongezeka zaidi na zaidi. Paulo anawataka Wafilipi watoe matolea ili wapate baraka za kiroho. "Napenda kumuona Mungu akiwapeni baraka za rohoni zaidi na zaidi"
Philippians 4:18-20
Nimepokea vitu vyote, na sasa nimejazwa na vitu vingi
Paulo alipokea kila kitu ambacho Wafilipi walimtumia
Nimejazwa
Paulo anamaanisha kujazwa vitu ambavyo yeye mwenyewe.
Ni vitu vizuri vyenye kunukia mithili ya manukato, vyenye kukubalika abavyo vyote ni sadaka inayompendeza Mungu
manukato yenye kunukia, yenye kukubalika inayompendeza Mungu. Paulo anafananisha sadaka za kanisa la Filipi na zile za zilizokuwa zikitolewa kipindi cha Agano la Kale. Makuhani waliteketeza zile sadaka, ambazo zilikuwa zikinukia kwa Mungu. Paulo anasisitiza kwamba sadaka zina thamani kubwa kwa Mungu. "Ninawahakikishieni kuwa sadaka hizi zinampendeza Mungu"
atawajazeni mahitaji yenu
"atatoa kila hitaji mlilonalo"
kwa utajiri wa utukufu wake katika Yesu Kristo
"kutoka kwwenye utajiri wa utukkufu ambao huutoa kupitia Kristo Yesu"
Sasa kwa Mungu
Neno "sasa" limetumika kuonyesha mwisho wa maombi na hitimisho la waraka huu.
Philippians 4:21-23
Ndugu
anawazungumzia wale watu ambao penginenwalitumika pamoja au na Paulo.
ndugu
neno hili humaanaisha Wakristo wenza, ikijumuisha wanaume na wanawake, kwa kuwa waumini wote katika Kristo ni washiriki warithi wa familia moja ya kiroho, ambayo Mungu ni baba wa mbinguni.
kila muumini...waumini wote
Baadhi ya matoleo yametafsiri kutumia "mtu mtakatifu" na "watu watakatifu"
hususani wale wa familia Kaisari
Hii inazungumzia watumishi waliofanya kazi kwenye eneo la Kaisari.
pamoja na roho zenu
Paulo anazungumzia waumini kwa kutumia neno "roho," ambayo huwawezesha wanadamu kuhusiana na Mungu. "pamoja nanyi"