Philemon
Philemon 1
Philemon 1:1-3
Paulo mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo ndugu yetu kwa Filemoni
Lugha yako inaweza kuwa na njia maalum kwa mwandishi kujieleza kwa barua. "Sisi, Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo, ndugu yetu, naandika hii barua kwa Filemoni."
mfungwa wa Kristo Yesu
"Mtu aliyefungwa kwa kufundisha kuhusu Yesu Kristo."
ndugu
Hapa hii inamaanisha mkristo mwenzake.
na mtendakazi mwenzetu
"Aliye, kama sisi, anakazi ya kueneza injili"
Afia dada yetu
Hii inamaanisha "Afia mkristo mwenzetu" au "Afia dada yetu kiroho"
Arkipo
Hili ni jina la mtu
Askari mwenzetu
Hapa ni "askari" ni fumbo inayomuelezea mtu anayepambana kwa kueneza injili. "Mwenzetu shujaa kiroho "au pia mpambanaji katika vita vya kiroho pamoja nasi."
neena iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo
"Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo awape neema na amani."Hii ni baraka. Neno "kwenu" ni kwa wengi na inarejea kwa watu wote waliosalimiwa na Paulo katika mstari wa 1 na 2.
Sentensi unganishi
Paulo amedhihirisha mara tatu kuwa yeye ni mwandishi wa barua hii. Timotheo alikuwa naye na aliandika maneno aliyoambiwa na Paulo. Paulo aliwasalimia waliokutana kusali katika nyumba ya Filemoni.
Maelezo ya jumla
Neno "mimi" linamaanisha Paulo. Filemoni ni mtu ambaye aliandikiwa barua hii. Sehemu zote zilizoandikwa "wewe" zinamuelezea Filemoni.
Maelezo ya jumla
Neno "yetu" inawajumuisha Paulo, Filemoni na waamini wa kanisa waliokuwa wakikutana kwenye nyumba ya Filemoni.
Baba yetu
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu.
Philemon 1:4-7
Maelezo ya jumla
Neno "sisi" ni wingi ikimaanisha Paulo, Timotheo na Filemoni.
Wewe
Hapo na zaidi katika barua hii, neno" wewe" inamtaja Filemoni.
Kuwa na ufanisi katika ujuzi wa kila jambo jema
Matokeo ya kujua kilicho chema
Katika Kristo
"Kwa sababu ya Kristo"
mioyo ya waumini imekuwa ikitulizwa nawe
"umewatia moyo waamini" au "umewasaidia waamini"
Ndugu
"marafiki" Paulo anamuita Filemoni rafiki maana wote ni waamini na anasisitiza urafiki wao.
Philemon 1:8-9
Ujasiri wote katika Kristo
Inawezekana inamaanisha "mamlaka kwa sababu ya Kristo" au " kutiwa moyo kwa sababu ya Kristo."
lakini kwa sababu ya upendo
Inawezekana inamaanisha ni 1} "kwa sababu 1 ninajua unawapenda watu wa Mungu,"2} "kwa sababu unanipenda mimi" au 3} "kwa sababu ninakupenda."
Sentensi unganishi.
Paulo anaanza kutoa sababu ya kuandika barua yake.
Philemon 1:10-13
mwanangu Onesmo
"kijana wangu Onesmo." Paulo analinganisha uhusiano wake wa karibu na Onesmo sawa na ule uhusiano walionao baba na mwanawe. Kiuhalisia Onesmo sio kijana wa Paulo, lakini alipata maisha ya kiroho wakati Paulo alipomfundisha kuhusu Yesu, na Paulo alimpenda. "Mwanangu mpendwa Onesmo" au "Onesmo mwanangu wa kiroho."
Onesmo
Hili ni jina la mtu
niliyemzaa
Jinsi Onesmo alivyokuwa kama kijana kwa Paulo alimfanya kuwa muwazi. Niliyemfanya mwanangu wa kiroho wakati nilipomfundisha kuhusu Kristo na kuzaliwa mara ya pili." "amekuwa mwanangu"
katika vifungo vyangu
"katika minyororo. "Wafungwa mara nyingi kwa minyororo. Paulo alikuwa kifungoni wakati akimfundisha Timotheo, na aliendelea kuwa kifungoni hata wakati alipoandika barua hii. Wakati akiwa kifungoni."
Namtuma yeye ... kwenu
Paulo pengine ameandika barua kabla ya kumtuma Onesmo.
mpendwa wa moyo wangu.
Hapa neno "moyo" ilitumika kwa mtu anayependwa sana. Paulo alisema hivi kuhusu Oesmo. "Ambaye nampenda daima."
hivyo anaweza kunisaidia badala yako
"kwamba, tangu wewe usipokuwepo hapa, yeye ananguvu kunisaidia. Inaweza kutafsiriwa pia kama ni sentensi tofauti: Yeye angenisaidia mimi badala yako."
Mimi nimefungwa minyororo
"wakati nilipokuwa nimefungwa" au "kwa sababu nipo kifungoni."
kwa ajili ya injili
kwa sababu ya kuhubiri injili
Maelezo ya jumla
Onesmo alikuwa mtumwa na Filemoni aliyemuibia kila kitu na kukimbia.
Philemon 1:14-16
Lakini sikutaka kufanya jambo lolote bila ridhaa yako
"Lakini sikutakutaka kumweka yeye hapa bila idhini yako" au "Lakini nilitaka awe pamoja nami kama wewe umekubali"
hivyo kila jambo zuri ulilofanya si kwa sababu nimekulazimisha
hivyo kila jambo jema utakalofanya, si kwa sababu nakulazimisha."
lakini kwa sababu ulitaka kufanya
"kwa sababu uliwa huru kuchagua kufanya jambo lililo jema"
labda kwa sababu mlitengwa naye
Hii yaweza kutafsiriwa hivi "Labda ni sababu ya Mungu kumpeleka Onesmo awe mbali nawe."
kwa wakati
"kwa muda huu"
bora zaidi ya mtumwa
"ana thamani zaidi ya mtumwa"
ndugu mpendwa
"ndugu mpendwa" au "ndugu wa thamani katika Kristo"
zaidi sana kwako
"anamaanisha zaidi sana kwako"
kibinadamu
uhusiano wa kibinadamu unaweza kuonekana wazi: "kwa sababu yeye ni mtumwa wenu" "kama mtu" au "uhusiano wa kibinadamu."
na katika Bwana
"na kama ndugu katika Bwana" au na kwa sababu yeye ni mali ya Bwana."
Philemon 1:17-20
kama unanichukulia kama mshiriki
"kama wewe unanidhania mimi mtenda kazi wa Kristo"
unidai mimi malipo
"malipo yatatoka kwangu" au "sema kwamba mimi ni mmoja wa unaowadai."
mimi Paulo ninaandika kwa mkono wangu
Paulo niliyeandika hivyo, kwamba Filemoni ujue kwamba ni maneno ya kweli; Paulo kweli angemlipa. "Mimi, Paulo, ninaandika hivi mwenyewe."
Sikutaka kukwambia
"Sikuhitaji kukukumbusha wewe" "wewe unajua"
unanidai maisha yako
"wewe unanidai maisha yako" Paulo anamwambia Filemoni asiseme kuwa anawadai Onesmo au Paulo maisha yake kwa sababu Paulo anamdai zaidi Filemoni. "Ninakudai zaidi maana nimeyaokoa maisha yako"
furahisha moyo wangu
Paulo alitaka Onesmo angefanya kwa uaminifu: furahisha moyo wangu kwa kumkubali Onesmo. "uufanye moyo wangu ufurahi" au "unifurahishe" au "unifariji."
Philemon 1:21-22
Ujasiri kuhusu utii wako
"Kwa sababu nina hakika kwamba utafanya kile nilichosema"
Na wakati mwingine
"Pia"
andaa chumba kwa ajili yangu
andaa chumba hapo kwako iwe tayari kwa ajili yangu. Paulo alimwambia Filemoni afanye hivyo.
nitakutembelea hivi karibuni
"Wale walioniweka gerezani wataniachia huru hivyo ntakuja kwako"
Sentensi unganishi
Paulo anamalizia barua yake kwa kuwabariki Filemoni na waamini wote waliokuwa wakikusanyika kusali katika nyumba ya Filemoni.
Maelezo ya jumla
Maneno "wewe, ninyi" yanawaelezea Filemoni na waamini waliokutana nyumbani.
Philemon 1:23-25
Epafra
Huyu alikuwa mwaminu na mfungwa pamoja na Paulo.
mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu
"ambaye yupo gerezani pamoja na mimi kwa sababu ya Yesu Kristo"
Marko, Aristarko, Dema, Luka, watendakazi wenzangu.
Marko, Aristarko, Dema, Luka, watendakazi wenzangu nawasalimu.
Marko ... Aristarko ... Dema ... Luka
Haya ni majina ya watu.
watendakazi wenzangu
"wafanyakazi wenzangu" au "wote wanaofanya kazi na mimi"
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho yako.
Neno "yako" inawaelezea Filemoni na wote waliokutana nyumbani. "roho yako" inawakilisha watu wenyewe. "Bwana wetu Yesu Kristo awe mwema kwenu"