3 John
3 John 1
3 John 1:1-4
Sentensi unganishi
Yohana anatuma salaam kwa Gayo
Maelezo ya jumla
Hii ni barua mtu binafsi Yohana anaituma kwa Gayo. Maneno yote ya kiwakilishi cha majina yanamtaja Gayo katika umoja.
Mzee
Ni kiwakilishi cha Yohana, mtume na mwanafunzi wa Yesu. Yeye mwenyewe anajiwakilisha kama "mzee" pengine kwa sababu ya umri wake au kwasababu ya uongozi wake wa kanisa. Jina la mwandishi linaweza kufupishwa: Mimi, Yohana mzee, ninaye andika.
Gayo
Huyu ni mshirika mwamini ambaye Yohana anamwandikia barua hii.
Ambaye ninayempenda katika kweli
"Ambaye ninampenda kweli"
Unaweza kufanikiwa katika mambo yote na kuwa na afya
"Unaweza kufanya mambo yote vizuri na kuwa na afya"
Kama na roho yako ifanikiwavyo
"Kama vile unavyoendelea vizuri kiroho"
Ndugu
"washirika waumini"
dhihirisha ushuhuda wa kweli yako, kuwa unatembea katika kweli
"aniambia kuwa unaishi kulingana na ukweli wa Mungu"
Wanangu
Yohana anazungumzia wale aliowafundisha kumwamini Yesu kama vile watoto wake. Hii inauelezea upendo wake na nia yake kwa ajili yao. Inaweza pia kuwa yeye mwenyewe aliwaongoza kumjua Bwana. "Watoto wangu wa kiroho"
3 John 1:5-8
Sentensi unganishi
Kusudi la Yohana la kuandika barua hii ilikuwa kumhimiza Gayo kuwa makini katika njia aliyoianza ya kufundisha Biblia; kisha anazungumzia habari za watu wawili, mmoja mwovu na mwingine mwema.
Maelezo ya Jumla
Hapa neno "sisi" linamtambulisha Yohana na wale waliokuwa pamoja naye na yawezekana linawaunganisha waumini wote.
Mpendwa
Hapa inatumika kama neno la utambulisho kwa wafuasi waumini.
Unaenenda kwa uaminifu
"Unatenda kwa uaminifu kwa Mungu" au "Umekuwa mtii kwa Mungu"
unapowahudumia ndugu na wageni
"Kuhudumia ndugu waumini na wale usiowajua"
ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa.
"Wageni, ambao wamewaambia waumini katika kanisa jinsi mnavyowapenda"
Unafanya vizuri kuwasafirisha
"Kwa unyenyekevu ninawaomba mpate kuwasafirisha
Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda
Hapa Jina linamaanisha Yesu. Walienda kuwaambia watu wengine kuhusu Yesu.
bila kuchukua kitu chochote
Bila kupokea zawadi au misaada
wa Mataifa
Hapa watu "wa mataifa" Haimaanishi kuwa ni watu wasio Wayahudi. Inamaanisha watu wasio na tumaini kwa Yesu.
ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli
"Ili kwamba tutashirikiana nao kuutangaza ukweli wa Mungu kwa watu"
3 John 1:9-10
Maelezo ya jumla
Neno "sisi" linamwelezea Yohana na wele waliokuwa pamoja naye bila kumjumuisha Gayo.
kusanyiko
Hapa anamtaja Gayo na kundi la waumini wanaokutana pamoja kumwabudu Mungu.
Diotrofe
Alikuwa hapo awali mmoja wa kundi la waumini waliokuwa wakikusanyika
anayependa kuwa wa kwanza miongoni mwao
"Aliyependa kuonekana kuwa wa muhimu sana miongoni mwao" au "ambaye alipenda kujifanya kama vile ni kiongozi wao"
jinsi anavyosema maneno mabaya dhidi yetu
"Jinsi anavyonena mambo mabaya kutuhusu sisi na hakika siyo ya kweli"
yeye mwenyewe
Neno "yeye mwenyewe" linamwelezea Diotrofe aliyekuwa akifanya mambo hayo.
hawapokei ndugu
hataki kuwapokea ndugu waumini"
Hata huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao
"Anawazuia wale wanaotaka kuwakaribisha waumini"
na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko.
"Anawalazimisha kutoka kwenye kusanyiko"
3 John 1:11-12
Maelezo ya jumla
Hapa neno "sisi" linaelezea kuhusu Yohana na wale waliokuwa pamoja naye bila kumjumuisha Gayo.
Mpendwa
Hapa inatumika kama neno la utambulisho kwa wafuasi waumini.
usiige kilicho kibaya
"Usifuatishe mambo maovu ambayo watu wanayatenda"
bali iga kilicho chema
"Fuatisha mambo mema ambayo watu wanayatenda"
ni wa Mungu
"Yanatokana na Mungu"
hajamwona Mungu
eye si mali ya Mungu" au "Hajamwamini Mungu"
Demetrio ameshuhudiwa na wote
Wote ambao wanamfahamu Demetrio wanamshuhudia" au "Kila mwumini anayemjua Demetrio ananema mema kumhusu yeye"
Demetrio
Huyu yawezekana kuwa ni mtu ambaye Yohana anamtaka Gayo na kusanyiko lote kumkaribisha wakati wa ziara yake.
na kweli yenyewe
"Kweli yenyewe pekee inanena ukweli juu yake, kwamba ni mtu mwema"
sisi pia ni mashahidi
"Sisi pia tunanena mema yahusuyo Demetrio"
3 John 1:13-15
Maelezo ya jumla
Huu ni mwisho wa barua ya Yohana kwa Gayo. Anampatia mambo ya hitimisho na kuifunga kwa salaamu.
lakini sipendi kukuandikia kwa kalamu na wino
Yohana hana utashi wa kuwaandikia mambo mengine yote. Hasemi kwamba kwamba angewaandikia mambo fulani zaidi ya kalamu na wino.
ana kwa ana
"Kwa pamoja" au "kwa mmoja mmoja"
Amani iwe pamoja nawe
"Mungu aweza kukupa amani"
Marafiki wanakusalimu
"Marafiki hapa wanakusalimu
marafiki
"Rafiki zako" au "Waumini wenzako"