James
James 1
James 1:1-3
Sentensi unganishi
Baada ya salam zake za ufunguzi, Yakobo anawaambia waamini kwamba kusudi la majaribu ni kupima imani.
Yakobo, mtumishi wa Mungu na Bwana Yesu Kristo.
Neno "Niko" linamaanisha " Mimi, Yakobo ni mtumishi wa Mungu na Bwna Yesu Kristo"
Yakobo
Yakobo alikuwa ndugu yake na Yesu.
Kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika.
Hii inaelezea eidha wayahudi wote wa Kikiristo waishio nje ya Israeli au Wakristo wote waishio popote duniani.
Makabila kumi na mbili.
Neno "makabila "kumi na mbili" yanamaanisha watu wote wa Israeli kwa kuwa waligawanywa katika makabila "kumi na mbili". Kwenye mistari hii makabila kumi na mbili yanamaanisha Wayahudi wote wa Kikristo au Wakristo wote duniani. Hapa neno "kumi na mbili" hutumika kama jina na namba "kumi na mbili" inapaswa kuandikwa kama neno sio kama namba.
Kutawanyika
Neno "kutawanyika" kunamaanisha Wayahudi wote waliotawanyika kwenye nchi nyingine mbali na nyumbani kwao Israeli. Kenye mistari hii "kutawanyika" linamaanisha Wakristo wa kiyahudi waishio nje ya Israeli au Wakristo wote waliopo popote duniani.
Salam
Salam ya kawaida kama "habari" au "siku njema".
Furahini ndugu zangu, mpatapo matatizo.
"Waamini wenzangu, yaone matatizo yote uliyonayo kama mambo ya kukufanya ushangilie"
Jaribu la imani yenu inatengeneza uvumilivu.
Maneno "jaribu", "imani yenu", na "kuvumilia" ni maneno yanayosimama kuonyesha matendo. Mungu hutujaribu ili kujua ni kwa namna gani tunamwamini yeye na kumtii. Waamini ("ninyi") mwamini yeye na mvumilie mateso. "Mnapokutana na magumu Mungu anagundua ni kwa kiasi gani unamwamini. Na matokeo yake unakuwa na uwezo wa kushinda majaribu magumu zaidi.
James 1:4-5
Tuache uvumilivu ukamilishe kazi yake.
Hapa uvumilivu imezungumzwa kama vile mtu yupo kazini. "Jifunze kuvumilia magumu yote"
Kukua kabisa
Kuwa na uwezo wa kumwamini Kristo na kumtii yeye katika hali zote.
Usipungukiwe chochote
Hii inaweza kuwa sentensi chanya "kuwa na uwezo kumtii Mungu kwa kila jambo"
Muombe Mungu, yeye atoaye
"Muombe Mungu. Ni yeye atoaye"
Ukarimu na "bila kukemea
Hii inaweza kuzungumziwa kwa mtazamo chanya "ukarimu au furaha"
Atawapa
"Mungu atawapa" au "Mungu atajibu maombi yenu"
James 1:6-8
Kwa imani, bila mashaka yoyote
Hii inaweza kuzungumziwa kwa mtazamo chanya. "Kwa uhakika zaidi kuwa Mungu atajibu"
Kwa yeyote mwenye mashaka ni kama mawimbi ya bahari yanavyoendeshwa na upepo na kuchafuka kwa bahari
Yeyote mwenye mashaka kuwa Mungu atamsaidia ni kama maji ndani ya bahari au maziwa makubwa yanayopita katika uelekeo tofauti.
Ana nia mbili
Nia. Neno "nia mbili" linamaanisha mawazo ya mtu pale anaposhindwa kufanya maamuzi. "Anashindwa kuamua amfuate Yesu as la"
Hana msimamo kwenye njia zake zote
Hapa anazungumziwa mtu amabye hawezi kukaa kwenye njia moja badala yake anaenda njia moja baada ya nyingine.
James 1:9-11
Ndugu masikini
"mwamini asiye na pesa nyingi"
Kujivuna kwa cheo chake cha juu
Mtu ambaye Mungu anembariki anazungumza kama vile amesimama mahali pa juu sana.
Lakini tajiri
"lakini mtu aliye na pesa nyingi." Maana nyingine ni 1) huyu mtu tajiri ni mwamini, au 2) huyu mtu tajiri si mwamini.
Wa cheo cha chini
Mwamini tajiri anapaswa kufurahi kwamba Mungu ameyaruhusu mateso. "anapaswa kuwa na furaha kwamba Mungu amempa nafsi hiyo"
Atapita kama ua la porini kwenye majani
Matajiri wanafananishwa na maua ya porini ambayo yanakuwa hai kwa mda mfupi.
Mtu tajiri atachakaa katikati ya safari zao
Kama ambavyo maua hayafi ghafla lakini yanachakaa kwa mda mfupi , pia matajiri hawatakufa ghafla lakini watachukua mda mfupi kupotea.
Katikati ya kazi yake.
Shughuli za kila siku za tajiri zinazungumzwa kama safari aliyokuwa anaifanya. Hii inaelezea namna ambavyo hakufikiri chochote juu ya kifo chake hapo baadae na hivyo kitakuja ghafla.
James 1:12-13
Sentensi unganishi.
Yakobo anawakumbusha waamini wanaosema Mungu hasababishi majaribu; anawaambia namna ya kukabiliana na majaribu.
Baraka
Bahati, vizuri.
Kuvumilia majaribu
Kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu uwapo katika magumu.
Kushinda majaribu
Amethibitishwa na Mungu.
Kupokea taji ya uzima
Uzima wa milele unazungumziwa kama taji ya maua inayowekwa kwenye kichwa cha washindi. "pokea uzima wa milele kama tuzo"
Imeahidiwa kwa wale wanaompenda Mungu.
Hii imeelezewa katika hali ya utendaji "Mungu aliahidi taji ya uzima kwa wale wampendao"
Anapojaribiwa
"Anapotamani kufanya uovu"
Nimejaribiwa na Mungu
Hii imeelezewa katika hali ya utendaji. "Mungu amesababisha nifanye maovu"
Mungu hajaribiwi na uovu
Hii imeelezewa katika hali ya utendaji. "Mungu hatamani kufanya lolote ovu"
Wala mwenyewe hamjaribu yeyote
"Na Mungu mwnyewe hamsababishi mtu kufanya uovu"
James 1:14-16
Kila mtu anajaribiwa na tamaa zake mwenyewe
Tamaa za mtu zinazungumzwa kama vile mtu mwingine ameshawishi afanye dhambi.
Zinamshawishi na kumvuta mbali
Tamaa mbaya zinaendelea kuzungumzwa kama mtu anavyoweza kumshawishi mwingine.
Kushawishi
kuvutia, kumshawishi mtu kufanya uovu.
Ndipo baada ya tamaa ya dhambi kubeba mimba, dhambi huzaliwa, na baada ya dhambi kukomaa sawasawa, huishia katika mauti.
Tamaa inaendelea kuzungumzwa kama mtu, na hapa inaelezewa wazi kama mwanamke mwenye mimba ya mtoto. mtoto anaelezewa kama dhambi. Thambi ni mtoto mwingine wa kike ambaye anakuwa na kupata mimba naanazaa kifo. Mtiririko huu ni picha inayoonyesha namna ambavyo mtu atakufa kiroho na kimwili kwa sababu ya tamaa zake mbaya na dhambi.
Msidanganyike
"Msiache mtu yeyote awadanganye" au "msijidanganye wenyewe"
James 1:17-18
Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika
Sentensi hizi mbili zina maana moja. Yakobo alizitumia kusisitiza kuwa kila kizuri alichonacho mtu kinatoka kwa Mungu.
Baba wa nuru.
Mungu, muumbaji wa nuru zote zilizopo juu angani (jua, mwezi na nyota) inajulikana kuwa ni Baba yao.
Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo
Hii inamuelezea Mungu kama mwanga usiobadilika tofauti na jua, mwezi, sayari na nyota ambazo zinapita katikati ya anga na zinabadilisha nuru yake. "Mungu habadiliki kama jua, mwezi na nyota ambazo zinatokea na kupotea"
Kutupa sisi
Neno "sisi" linamaanisha Yakobo na hadhira yake.
Katupa uzima
Mungu aliyetupa uzima wa milele anazungumziwa kana kwamba ametupa uzima.
Neno la kweli
Ujumbe wa kweli wa Mungu.
Kama uzao wa kwanza
Yakobo anatumia utamaduni wa Kiebrania wa zao la kwanza kama njia ya kuelezea thamani ya Mwamini wa Kikristo kwa Mungu. anaelezea kuwa kutakuwa na waamini wengi sana baadae.
James 1:19-21
Mnajua hili
Yaweza kumaanisha 1) "mnajua hili" kama amri, kuwa makini juu ya lile ninalotaka kuwaandikia au 2) "mnajua hili" kama sentensi kwamba ninataka kuwakumbusha juu ya jambo ambalo mnalijua.
Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea
Watu wanapaswa kusikiliza kwa makini na kuzingatia maneno haya " usiwe mwepesi kuongea" haimaanishi uongee taratibu.
si mwepesi wa hasira
"usishikwe na hasira mapema"
hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu
Mtu anapokuwa na hasira hawezi kufanya kazi ya Mungu, ambayo ni haki.
wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote
Dhambi na ubaya vimezungumzwa hapa kama vitu ambavyo vinapaswa kuwekwa mbali au kutupwa.
wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote
Hapa uchafu wa dhambi na ubaya vinamaanisha kitu kimoja. Yakobo ameyatumia kusisitiza ni kwa jinsi gani dhambi ilivyo mbaya. "Acheni kufanya aina zote za dhambi"
uchafu wa dhambi
Hapa uchafu inamaanisha dhambi na ubaya.
Kwa unyenyekevu
"Bila kujivuna" au "bila kiburi"
lipokeeni neno lililopandwa
Neno "kupanda" linamaandishwa kuweka kitu flani ndani ya kitu kingine. Hapa neno la Mungu limetumika kama mmea ambao unapaswa kukua ndani ya waamini. "Utii ujumbe wa Mungu aliousema kwako"
lipokeeni neno lililopandwa
"Neno" linamaanisha neno la Mungu linalosimama kama ujumbe wa ukombozi ndani ya Yesu Kristo ambapo Mungu anawaambia waamini. Wakiliamini, Mungu atawaokoa.
kuokoa roho zenu
"Awaokoe ninyi toka kwenye hukumu ya Mungu"
roho
Hapa neno "roho" inamaanisha mtu.
James 1:22-25
Litiini neno
Wanapaswa kutii amri zilizoamriwa na Mungu.
Mkijidanganya wenyewe
"mnajidanganya wenyewe
Kwa kuwa kama yeyote alisikiaye neno bila kulitendea kazi ni sawa na mtu ajiangaliaye uso wake halisi katika kioo.
Mtu anayesikiliza maneno ya Mungu lakini hayatii anafananishwa na mtu anayejiangalia kwenye kioo na baadae anasahau muonekano wake.
uso wake halisi
Uso wake kama ulivyo.
Hujitathmini uso wake na baada ya mda mfupi husahau
Mtu anayejiangalia uso wake na baadae akasahau muonekano wake ni sawa na mtu aliyesikia neno la Mungu na kusahau alichosikia.
mtu yule anayeiangalia kwa uangalifu sheria kamili.
Hii inaendelea kuelezea picha ya sheria kama kioo.
Sheria kamili ya uhuru
"sheria kamili inayoruhusu watu kuwa huru"
Mtu huyu atabarikiwa katika utendaji wake.
Hii inaweza kuelezewa katika hali ya kutenda "Mungu atambariki huyu mtu kama akiitii sheria"
James 1:26-27
kujiona mwenyewe kuwa mtu wa dini
"Anadhani anamuabudu Mungu kwa usahihi
Ulimi wake
Kuudhibiti ulimi wa mtu inamaanisha kudhibiti kauli zake.
udanganyifu
"mjinga" au "kupotosha"
Moyo wake
Hapa moyo inamaanisha imani yake au mtazamo wake.
Dini yake ni bure
"Anamuabudu Mungu bure"
Safi na isiyoharibiwa
Yakobo anaizungumzia dini , namna watu wanavyomuabudu Mungu kama kitu amabacho ni safi na kisichoharibiwa. Hii ni utamaduni wa Kiyahudi kuelezea namna ambavyo kitu kimekubalika na Mungu. "kukubalika kabisa"
mbele za Mungu wetu na Baba
Anaelezewa Mungu.
Yatima
Yatima
Wajane katika mateso yao
Wanawake wanaoteseka kwa sababu waume zao wamefariki.
Kujilinda na ufisadi wa dunia
Kutokubali uovu wa dunia hii ukakusababisha ukatenda dhambi
James 2
James 2:1-4
Sentensi unganishi:
Yakobo anaendelea kuwaambia waamini wa Kiyahudi waliotawanyika namna ya kuishi kwa kupendana na kuwakumbusha kutowapendelea matajiri juu ya masikini.
Ndugu zangu
Yakobo anawaandikia ndugu zake ambao ni waamini wa Kiyahudi . "waamini wenzangu" au "ndugu zangu katika Kristo"
Ishikeni imani ya Bwana Yesu Kristo
Mwamini Yesu Kristo.
Bwana wetu Yesu Kristo
Neno "wetu" linamaanisha Yakobo na waamini wenzake.
upendeleo kwa watu wengine
shauku ya kumsaidia mtu fulani zaidi ya mwingine
Kama mtu fulani
Yakobo anaanza kuelezea hali ambayo waamini wanamthamini sana tajiri kuliko masikini.
amevaa pete za dhahabu na mavazi mazuri
"amevaa kama mtu tajiri"
keti hapa mahali pazuri
"keti hapa sehemu ya heshima"
simama pale
"hamia sehemu isiyo na heshima"
Kaa chini ya miguu yangu
Hamia sehemu ya kunyenyekea
Je, hamuhukumiani ninyi wenyewe, na kuwa waamuzi wenye mawazo mabaya?
Yakobo alitumia swali kuwakemea wasomaji wake. "Mnahukumiana wenyewe kwa wenyewe na kufanya maamuzi mkiwa na mawazo mabaya"
James 2:5-7
Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa
Yakobo anawachukulia wasomaji wake kama ndugu. "kuweni makini, ndugu zangu wapendwa"
Mungu hakuwachagua ... wampendao?
Yakobo anatumia swali kuwafundisha wasomaji wake wasiwe na upendeleo. "Mungu aliwachagua ... mpende yeye"
masikini
"watu masikini."
Kuwa tajiri katika imani
Kuwa na imani kubwa ni utajiri. "kuwa na imani thabiti kwa Kristo"
Warithi
Watu ambao Mungu aliwaahidi watairithi mali na utajiri kama vile watu warithipo toka kwa ndugu wa familia.
Lakini ninyi
Yakobo anaongea na hadhira yote.
mmewadharau masikini
"Mmewadhalilisha masikini"
Je, sio matajiri wanaowatesa ninyi
Hapa Yakobo anatumia maswali kuwasahihisha wasomaji wake. "Ni matajiri wanaowatesa ninyi."
tajiri
"watu matajiri"
wanaowatesa
"wanaowatendea mabaya"
Sio wao ... mahakamani?
Hapa Yakobo anatumia maswali kuwasahihisha wasomaji wake. " matajiri ndio wao ... mahakamani."
wanaowaburuza mahakamani
"wanaowapeleka kwa nguvu mahakamani na kuwashitaki kwa hakimu"
Hawalitukani ... mnaitiwa?
Hapa Yakobo anatumia swali kurekebisha na kufundisha wasomaji wake. "Matajiri ... mnaitiwa?
Jina zuri
"jina la Kristo" hii ni njia moja wapo ya kuelezea jina la Yesu. "Kristo ambalo kwalo mnaitiwa"
mnaitiwa
"mnajulikana kwalo"
James 2:8-9
ninyi mkiitimiza
Neno "ninyi" inamaanisha waamini wa Kiyahudi.
kutimiza sheria ya kifalme
"kutii sheria za Mungu." Mungu alitupa sheria za Musa zilizorekodiwa katika agano la kale.
Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe
Yakobo ananukuu maneno toka kitabu cha mambo ya walawi.
Jirani yako
"watu wote"au "kila mtu"
mwafanya vyema
"mnafanya vyema" au "mnafanya yaliyo sahihi"
Kama mkipendelae
"kutoa huduma ya kipekee" au "kutoa heshima kwa"
kutenda dhambi
"kutenda dhambi" ni kuvunja sheria.
mtahukumiwa kwa shiria kama wavunja sheria.
"mna makosa ya kuvunja sheria"
James 2:10-11
Kwa kuwa yeyote atiiye
"Yeyoye anayetii"
bado akajikwaa ... sheria yote
Kujikwaa ni kuanguka chini wakati mtu anatembea. kutotii sheria ni sawa na kujikwaa wakati wa kutembea.
katika nukta moja
kwa sababu ya kutotii kwa sheria moja tuu
Kwa kuwa Mungu aliyesema
Hii inamuelezea Mungu aliyempa sheria Musa.
usifanye
"kufanya" ni kuchukua hatua
Kama ninyi .... lakini una ... ume
"ninyi" inamaanisha "kati yenu" Japokuwa Yakobo aliwaandikia waamini wengi wa Kiyahudi kwenye sehemu hii ametumia umoja kama vile alikuwa amzungumzia mtu mmoja.
James 2:12-13
Kwa hiyo zungumzeni na kutii
"hivyo mnatakiwa muongee na kufanya" Yakobo aliwaamuru watu kufanya hivi.
mko karibu kuhukumiwa na sheria ya uhuru.
"Mungu atawahukumu lwa sheria ya uhuru"
Kwa sheria
Mungu atawahukumu kulingana na sheria
Sheria ya uhuru
"Sheia inayotoa uhuru wa kweli"
Huruma hujitukuza juu
"Huruma ni bora kuliko" au "huruma inashinda" Hapa huruma na haki vimezungumwa kama vile ni mtu.
James 2:14-17
Sentensi unganishi
Yakobo anawatia moyo waamini waliotawanyika kuonyesha imani yao mbele za watu. Kama vile Abrahamu alivyoionesha imani yake kwa vitendo.
Kuna uzuri gani, ndugu zangu, kama mtu anasema ninayo imani, lakini hana matendo?
Yakobo anatumia swali kuifundisha hadhira yake. "Waamini wenzanhu, sio vizuri kabisa mtu akisema ana imani lakini hana matendo."
anayo imani
Yakobo anazungumzia imani, kumuamini Mungu.
haina matendo
Yakobo anazungumzia matendo kuwa ni kufanya matendo mema.
Je, imani hiyo yaweza kumwokoa?
Yakobo anazungumzia imani kuwa kumuamini Mungu kuna nguvu ya pekee katika kumuokoa mwanadamu lakini Imani haitoshi. "Imani hiyo haiwezi kumuokoa."
kumuokoa
"Kumuokoa toka kwenye hukumu ya Mungu."
mkaote moto
"kuwa na nguo za kutosha kuvaa" au "kuwa na sehemu ya kulala."
mle vizuri
"kuwa na chakula cha kutosha."
ya mwili
kula, kuvaa na kuishi vizuri.
yafaa nini?
Yakobo anatumia swali hili kuifundisha hadhira. "hivi sio vizuri."
wa kiume na wa kike
Waamini wenzangu katika Yesu, wanaume kwa wanawake
imani ... imekufa
Yakobo anaizungumzia imani kuwa ni hai mtu afanyapo matendo mema na imekufa kama mtu hatafanya matendo mema.
imani ... ina matendo
Imani inaambatana na mtu afanyaye matendo mema.
James 2:18-20
Bado mtu fulani anaweza kusema
Yakobo alikuwa anasahihisha uelewa wa hadhira yake juu ya imani na matendo.
Una imani, na mimi ninayo matendo
"Inakubalika iwapo mtu mmoja ana imani na mwingine ana matendo." Yakobo anaelezea ni kwa namna gani watu wnaweza kulumbana dhidi ya mafundisho yake.
Una imani, na mimi ninayo matendo ... nionyeshe imani yako
Yakobo anazungumzia imani na matendo kama vitu ambavyo watu wanaweza kuwa navyo na kuwaonesha wengine.
nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu
Yakobo anazungumza kuwa imani inaweza kuonekana endapo mtu atafanya matendo mema. "Nitaionesha imani yangu kwa kufanya matendo mema"
mapepo nayo yanaamini hivyo na kutetemeka.
"mapepo nayo yanaamini, lakini yanaogopa kwa hofu. Yakobo anafananisha mapepo na watu wanaosema wana imani lakini hawafanyi matendo mema. Yakobo anasema pepo wana busara maana wanamuogopa Mungu wakati watu hawamuogopi.
Je, unataka kujua, ewe mtu mpumbavu, namna ambavyo imani hiyo pasipo matendo isivyofaa?
Yakobo alitumia swali kuwakemea watu ambao hawakumsikiliza. "Ewe mpumbavu, hautaki kunisikiliza thibitisha namna isivyofaa imani bila matendo.
Je, unataka kujua ... isivyofaa?
"Nitawaonyesha ni jinsi gani ... isivyofaa."
James 2:21-24
Maelezo ya jumla
Kwa kuwa kulikuwa na waamini wa Kiyahudi walijua habari za Abrahamu ambaye waliambiwa na Mungu zamani.
Je, si baba yetu Abrahamu alihesabiwa haki
Hili ni swali linalotumika kuwakemea wapumbavu walioelezewa toka 2:18 waliokataa kuamini kuwa imani na matendo vinaenda sambamba." Abrahamu baba yenu alihesabiwa haki."
haki kwa matendo
"haki kwa kufanya matendo mema"
Baba
"baba" imetumika kama "mababu"
Mnaona
Neno "wewe" linamaanisha umoja. Yakobo anaongea na hadhira yake kama anaongea na mtu mmoja.
mnaona
kuona inaweza kumaanisha "kuelewa"
imani yake ilifanya kazi na matendo yake
Yakobo anazungumzia imani inafanya matendo mema. Imani ya Abrahamu kwa Mungu kuhusu Isaka inamfanya Abrahamu kumheshimu Mungu kwenye wakati mgumu. Kwa kumheshimu Mungu imani yake ikakuwa.
kwa matendo imani yake ilifikia kusudio lake
Kwa kumwamini Mungu Abrahamu alitimiza kusudi la Mungu. "kwa kuwa Abrahamu alimtii Mungu alimwamini Mungu kabisa"
Maandiko yalitimia
"Hii ilitimiza maandiko"
Akahesabiwa kuwa ni mwenye haki
"Mungu aliiona imani yake kuwa imemfanya kuwa mwenye haki." Imani ya Abrahamu na haki vilimpa thamani.
mnaona
Yakobo tena anazungumza na hadhira yake kwa kutumia wingi toka kwenye umoja "wewe"
kwa matendo mtu huhesabiwa haki, na si kwa imani tu .
"Matendo na imani ndio yanayomfanya mtu kuwa na haki na sio imani tuu."
James 2:25-26
Hali kadhalika, ... haki kwa matendo
Yakobo alikuwa anasema kama ilivyokuwa kweli kwa Abrahamu ndivyo ilivyokuwa kweli kwa Rahabu. wote walihesabiwa haki kwa matendo.
hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa haki kwa matendo ... barabara nyingine
Yakobo alitumia swali kuwaelekeza watu. "hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa ... barabara nyingine."
Rahabu yule kahaba
Rahabu alikuwa mwanamke aliyezungumzwa katika agano la kale na Yakobo alitegema hadhira yake inafahamu.
haki kwa matendo
Yakobo anazungumzia matendo kama kitu cha kumiliki.
wajumbe
Watu wanaoleta habari njema toka sehemu nyingine.
kuwapeleka kwa barabara nyingine
"aliwasaidia kutoroka mjini"
Kwa kuwa kama vile mwili usipokuwa na roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.
Yakobo anazungumzia imani imani isiyo na matendo kama mwili uliokufa usio na roho.
James 3
James 3:1-2
sio watu wengi
"siyo wengi wenu" Yakobo anatengeneza senyensi ya jumla.
Ndugu zangu
"wapendwa waumini wenzangu."
tutapokea hukumu kubwa sana
"Mungu atatuhukumu sisi kwa nguvu kwa sababu hatuna udhuru, wakati tufanyapo dhambi kwa sababu twajua na kufahamu Neno lake vizuri kuliko watu wengine."
Tutapokea
Yakobo anapanga makundi ya wale ambao hufundisha Maandiko kama yeye. Ingawa baadhi ya waumini ambao wangepokea barua hii, wangekuwa walimu wa Maandiko, wengi wasingeweza.
Kwa kuwa wote tunajikwaa.
Neno "wote" Yakobo amelitumia kumaanisha hadhira yake.
Kujikwaa
Dhambi imezungumzwa kama tendo la kujikwaa wakati wa kutembea. "kuanguka au kutenda dhambi"
Hawezi kujikwaa katika maneno yake.
"Hawezi kufanya dhambi kupitia maneno anayo zungumza."
Ni mtu mkamilifu.
"Amekomaa kiroho"
Kuongoza mwili wake wote.
Yakobo anazungumza juu ya moyo wake, hisia zake, na matendo yake. "kuongoza tabia yake" au "kuongoza matendo yake"
James 3:3-4
Ikiwa tunaweka rijamu kwenye midomo ya farasi.
Yakobo anazungumza kuhusu rijamu za farasi. Rijamu ni kipande kidogo cha chuma kinaachowekwa katika mdomo wa farasi ili kumuongoza kule anakoelekea.
Sasa ikiwa
"Kama" au "Endapo"
Farasi
"Farasi" ni mnyama mkubwa anayetumika kubeba vitu au watu. "endapo tunaweka rijamu katika vinywa vya farasi"
Tazama pia kwamba meli...huendeshwa kwa usukani mdogo sana.
"Meli" ni kama gari kubwa linaloelea juu ya maji. "Usukani"ni kipande kidogo cha mti au cha chuma kilicho nyuma ya meli kinachotumika kuiongoza meli kule inakoelekea. Neno "usukani" lingeweza kutafsiriwa kama "kifaa".
Maelezo ya jumla
Yakobo anajaribu kukuza mjadala juu ya vitu vidogo kutawala vitu vikubwa.
Zinasukumwa na kwa upepo mkali.
"Upepo mkali unazisukuma"
Zinaendeshwa kwa usukani mdogo sana popote nahodha atakapotaka kugeuka.
"Uwe na kifaa kidogo ambacho mtu anaweza kukitumia kuongozea meli mahali iendakako."
James 3:5-6
Vivyo hivyo.
Neno hili huashiria mlingano wa ulimi kwa rijamu za farasi na usukani wa meli katika mistari iliyotangulia.
Hujisifia mambo makuu sana
"mambo" ni ujumla wa vitu vyote ambavyo watu hawa wanajisifia.
Angalia
"fikiri kuhusu"
Jinsi msitu ulivyo mkubwa unawashwa na cheche moja!
"Ulimi mdogo wa moto unaweza kuwasha moto utakao unguza miti mingi!"
Ulimi pia ni moto.
Kama moto unavyo uunguza na kuteketeza vyote vinavyochomwa, ulimi, husimama badala ya mambo ambayo mtu huyatamka, yanaweza kuwaumiza watu vibaya. "Ulimi ni kama moto."
Ulimwengu wa uovu umewekwa katikati mwa viungo vya mwili wetu.
"Ni sehemu ndogo ya mwili wetu, lakini una uwezo wa kufanya dhambi katika aina zote za mambo."
Ambao hunajisi mwili wote.
Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Inaweza kutufanya sisi tusimpendeze Mungu kabisa" au "Inaweza ikatufanya sisi tusikubalike kwa Mungu."
Na huweka katika moto njia ya uzima.
Msemo huu "njia ya uzima" una maana ya maisha yote ya mtu. "na unaweza kuharibu maisha yote ya mtu."
Na wenyewe unachomwa katika moto katika jehanamu.
Neno "wenyewe" limesimama badala ya ulimi. Pia, hapa neno "jehanamu" limesimama badala ya nguvu za uovu au nguvu za shetani. Hii ingeweza kutafsiriwa kama kishazi kazi: "kwa sababu shetani huutumia kwaajili ya uovu."
James 3:7-8
Kila aina ya .... na mwanadamu.
Usemi huu "kila aina" humaanisha "aina nyingi." hii inaweza kutafsriwa kama fungu la maneno yanayoonesha kutenda; "Watu wamejifunza kudhibiti aina nyingi za wanyama wa mwitu, ndege, vitambaavyo, na viumbe wa baharini."
Kitambaacho.
Huyu ni mnyama ambaye hutembea juu ya ardhi kwa kujikokota.
Kiumbe wa baharini
Huyu ni mnyama ambaye anaishi majini.
Lakini kuhusu ulimi hakuna hata mmoja miongoni mwa watu awezaye kuchunga ulimi.
Hapa "ulimi" humaanisha kile ambacho mtu hutamka. Maana kamili inaweza kutajwa kwa uwazi kama hivi: "hakuna mtu hata mmoja awezaye kudhibiti ulimi wake pasipo msaada wa Mungu."
Muovu asiyedhibitiwa
Ulimi umezungumziwa kama vile ni uovu usioweza kudhibitiwa. Yakobo anafananisha na tamaa za mtu kuongea mambo maovu.
Umejaa sumu ya kufisha
Yakobo anafananisha uwezo wa mtu kuongea mabaya kama vile nyoka au mmea wenye sumu. Sumu ni maneno yaumizayo ambayo yanaweza kusemwa kwa mtu.
James 3:9-10
Kwa ulimi tuna.
"Tunatumia ndimi zetu kusema maneno ambayo."
Tunawalaani watu.
Kumuomba Mungu awaumize wengine
Ambao wameumbwa katika sura ya Mungu.
"Ambaye Mungu amemfanya katika sura yake."
Kutoka kinywa kilekile inatoka baraka na laana
Maneno yaliyobeba baraka na laana yanatoka katika kinywa cha mtu.
Ndugu zangu.
"Wakristo wenzangu"
Mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.
"Hili ni kosa."
James 3:11-12
Usemi unaounganisha.
Baada ya kuweka mkazo kwamba maneno ya waumini hayatakiwi kuwa ya baraka na laana, Yakobo anatoa mifano ya kufundisha wasomaji wake kuwa watu wanamheshimu Mungu kwa kuishi katika njia sahihi.
Je, chemchemi moja hutoa maji matamu na machungu?
Yakobo anatumia swali lisilodai jibu kuwafundisha wasomaji kuhusu sanjari ya mpangilio wa maumbile. "Chemchemi moja haitoi maji matamu na machungu."
Ndugu.
"Waumini wezangu"
Je,mti wa mtini huzaa mizeituni, au mzabibu huzaa matunda ya mtini?
Yakobo anatumia neno la picha ya umbo kuwafundisha wasomaji kuhusu sanjari ya mpangilio wamaumbile. "Mtini hauwezi kuzaa mzeituni, wala mzabibu hauzai matunda ya mtini"
James 3:13-14
Nani miongoni mwenu ana hekima na ufahamu? Haya mtu huyo.
Yakobo anatumia swali hili kufundisha wasikilizaji wake kuhusu tabia ya unyofu. Maneno " hekima" na "ufahamu" ki-msingi yana maana ileile. "Mtu ambaye ana fikiri kuwa ana hekima sharti"
Onesha maisha mema.
"Onesha tabia njema" au "Ioneshe"
Kwa matendo yake katika unyenyekevu ambao unatoka katika hekima.
"Pamoja na matendo yake mema na unyenyekevu ambao hutokana na kuwa na hekima ya kweli."
Kuwa na wivu mkali na nia ya ubinafsi katika mioyo yenu.
Neno "moyo" hapa lina maana ya jaziba au fikra. "Hutapenda kushiriki jambo na wengine na daima unajiweka mwenyewe katika nafasi ya kwanza."
Usijiinue na kuwa kinyume na ukweli.
"Usiseme uongo na kujifanya kama una hekima."
James 3:15-18
Hii siyo
"Hii" inarejea katika wivu wa kijinga na nia za ubinafsi kama zilivyoelezwa katika mistari iliyipita.
Hekima ishukayo chini kutoka juu
Ubora wa hekima inayozungumziwa ni kana kwamba ni ile ambayo Mungu aliituma chini toka mbingune
Niya kidunia.
Neno "niya kidunia" humaanisha thamani na tabia za watu ambao hawamheshimu Mungu. "Kutomheshimu Mungu."
Ni ya kishetani.
"Bali ni kutoka kwa mapepo."
Kwa sababu mahali palipo na wivu na nia ya ubinafsi.
"Kwa sababu popote palipo na watu ambao hujihudumia wao binafsi bila kujali wengine."
Kuna ghasia.
"Kuna vurugu" au "kuna mtafaruku."
Kila tabia ya uovu.
"Kila aina ya tabia ya dhambi" au "kila aina ya tendo la uovu."
Kwanza ni safi.
"Kwanza ni takatifu."
Kisha yenye amani na upendo.
Inayopenda**- "kisha ni yenye amani."
Yenye wema
Yenye moyo**- "wema" au "yenye kujali."
Na tunda jema.
Tunda hili jema linalinganishwa na matendo mema. "matendo mema"
Kamilifu
"Yenye kuaminika" au "yenye ukweli."
Na tunda la haki limepandwa katika amani kwa wote watendao mambo ya amani.
Hii inalinganisha amani na haki katika maisha yetu kama kupanda na kuvuna mazao. "wale ambao huishi katika amani wanafafanya ambacho Mungu husema ni haki."
Si ya kiroho.
"Si ya kutoka kwa Roho Mtakatifu" au "si ya kiroho."
Juu
Hapa "juu" inamaanisha Mungu
James 4
James 4:1-3
Sentensi unganishi
Yakobo anawakemea waamini waliokosa unyenyekevu. Anawaonya kuwa makini na namna wanavyozungumza na watu wengine.
Maelezo ya jumla
Maneno "ninyi, wewe" imetumika kama wingi kuwaelezea waamini walioandikiwa na Yakobo.
ugovi unatoka wapi ... migogoro
Maneno "ugonvi, migogor" yanamaanisha kitu kimoja. Yakobo anayatumia kusisitiza kuwa nazungumzia juu ya mvutano kati ya watu.
ugonvi na migogoro
Ni tabia zinazotokea katika jamii
Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita
Yakobo anatumia swali kukemea hadhira yake. "ni kwa sababu mna tamaa mbaya" "kwa sababu mnatamani vitu vibaya"
Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu?
Yakobo anazungumzia tamaa kama adui anayeleta vita kati ya waamini. kwa hali halisi ni watu ndio wenye tamaa hizi na kugombana wenyewe kwa wenyewe. "mnatamani maovu na mwishoni nmaumizana wenyewe kwa wenyewe"
Ndani ya washirika wenu
Yaweza kuwa na maana kuwa 1) kuna ugonvi kati ya waamini au 2) vita ambayo ni ugonvi upo ndani ya kila mwamini.
Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho.
"mnauwa" inaelezea ni kwa kiasi gani watu wanaweza kufanya lolote baya ili wawezea kupata wanachokitaka. "Mnafanya uovu wa kila namna ili mpate msichoweza kukipata"
Mnapigana na kugombana
"kupigana na kugombana" zinamaanisha kitu kimoja. Yakobo anatumia kusisitiza namna ambavyo watu wanagombana wenyewe kwa wenyewe.
Mnaomba vibaya
Yaweza kuwa na maana kuwa 1) mnaomba mkiwa na nia mbaya au 2) mnaomba vitu ambavyo hampaswi kuomba au mnaomba vitu vibaya.
James 4:4-5
Enyi wazinzi
Yakobo anazungumza na waamini akiwafananisha na mke aliyelala na mwanaume mwingine ambaye sio mume wake. "ninyi sio waaminifu kwa Mungu"
Hamjui kwamba ... Mungu?
Yakobo alitumia hili swali kuifundisha hadhira yake. "Mnajua ... Mungu"
urafiki na ulimwengu
Maneno haya yanaelezea uhusiano uliopo kwenye mifumo ya duniani na tabia zake.
urafiki na ulimwengu
Hapa mfumo wa ulimwenguni unaelezewa kama vile ni mtu ambaye watu wengine wanaweza kuwa na urafiki naye.
urafiki na ulimwengu ni uadui dhidi ya Mungu
Kuwa rafiki na ulimwengu inamaanisha kuwa adui wa Mungu. "urafiki na dunia" inamaanisha watu ambao ni marafiki wa dunia na "uadui dhidi ya Mungu" inamaanisha watu ambao wanampinga Mungu. "Marafiki wa ulimwengu ni maadui wa Mungu"
Au mnadhani maandiko hayana maana
Yakobo anatumia swali kueleza kuwa "Kuna maana katika maandiko"
Roho aliyoweka ndani yetu
Tafisi nyingine zinaelezea "roho" kama Roho Mtakatifu. Na tafsiri zingine zinamaanisha roho ya binadamu ambayo kila mtu ameumbwa nayo. Tunapendekeza kuwa utumie maana nyingine ambayo ipo katika tafsiri zinazotumika na wasomaji wako.
James 4:6-7
Lakini Mungu hutoa neema zaidi
"Japokuwa nafsi zetu hutamani tusivyoweza kuvipata, Mungu atatupa zaidi neema, tukijinyenyekeza wenyewe"
Hutoa neema zaidi
Neema imezungumzwa kama kitu kinachoweza kutolewa.
Kiburi
"mtu mwenye kiburi"
nyenyekea
"mtu mnyenyekevu"
Hivyo
"Kwa sababu hii"
Jitoeni kwa Mungu
"mtii Mungu"
Mpingeni ibilisi
"mpingine ibilisi" au "Msifanye mambo ambayo ibilisi anawaambia mfanye"
atakimbia
"atakimbia mbali"
ninyi
Hii inamaanisha hadhira ya Yakobo.
James 4:8-10
Taarifa ya jumla.
Neno "ninyi" linamaanisha waamini waliotawanyika ambao Yakobo anawaandikia.
Sogeeni karibu na Mungu, na yeye atakaribia karibu nanyi
Hapa anamaanisha kuwa wakweli na wazi kwa Mungu.
Safisheni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na takaseni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
Hizi ni sentensi mbili zinazoendana.
Safisheni mikono yenu
Hii ni amri kwa watu kufanya mambo ya haki na sio maovu. "Ishini namna ambavyo inampendeza Mungu"
Takaseni mioyo yenu
"mioyo" inamaanisha mawazo ya mtu na hisia zake" Mheshimu Mungu kwa mawazo yako"
nia mbili
"Nia mbili" linamaanisha mtu ambaye hawezi kufanya maamuzi juu ya jambo fulani. "Mtu ambaye hawezi kuamua amtii Mungu au la"
Huzunika, omboleza, na Lia
Maneno haya matatu yana maana moja. Yakobo anayatumia kwa pamoja kuonesha kuwa watu watahuzunika sana kwa kutokumtii Mungu" Yakobo anasema haya kama amri.
Geuzeni kicheko chenu kuwa huzuni na furaha yenu kuwa maombolezo
Hapa kicheko kimezungumzwa kuwa kitageizwa kuwa huzuni na furaha kuwa maombolezo. "Acheni kucheka na mtubu kwa Mungu"
Nyeyekeeni wenyewe mbele za Bwana
"Jinyenyekezeni mbele za Mungu"
Atawainua juu
Yakobo anazungumza namna ambavyo Mungu anamuheshimu mtu mnyenyekevu na kumnyanyua toka chini. "atakuheshimu wewe"
James 4:11-12
Maelezo ya jumla
Maneno "wewe" au "ninyi" yametumika kuwaelezea waamini walioandikiwa na Yakobo.
Kunena kinyume
"kusema vibaya kuhusu" au "kupinga"
Ndugu
Yakobo anawazungumzia waamini kama ndugu waliozaliwa pamoja. "waamini wenzangu"
bali mnaihukumu
"bali mnafanya kama mtu anayetoa sheria"
Ni mmoja tu ambaye ni mtoa sheria na hakimu
Hapa anamaanisha Mungu. "Mungu ndiye atoaye sheria na ahukumuye"
Wewe ni nani ambaye unamhukumu jirani yako?
Yakobo anatumia swali hili kuikemea hadhira yake. "Ninyi ni binadamu na hamuwezi kuwahukumu binadamu wengine"
James 4:13-14
kukaa huko mwaka
Yakobo anazungumzia kutumia mda kama pesa. "kaeni huko mwaka mzima"
Ni nani ajuaye nini kitatokea kesho
Yakobo anatumia swali hili kuisahihisha hadhira yake. "Hakuna ajuaye kitakachotokea kesho"
maisha yenu ni nini hasa?
Yakobo alitumia swali hili kufundisha waamini kuwa maisha ya kimwili sio ya muhimu sana. "fikirini juu ya maisha yenu ya kimwili"
Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea.
Yakobo anawafananisha watu na ukungu ambao hutokea na kupotea kwa haraka. "mnaishi kwa muda mfupi na kufa"
James 4:15-17
Badala yake mngesema
Badala yake, mtazamo wenu uwe?"
sisi tutaishi
Neno "sisi" halimaanishi Yakobo au hadhira yake lakini ni mfano wa namna ambavyo hadhira ya Yakobo inatakiwa iishi.
tutafanya hiki au kile.
"kufanya kile ambacho tumepanga kufanya"
kwake yeye ajuaye kutenda mema lakini hayatendi, kwake huyo ni dhambi.
Yeyote anayeshindwa kufanya jambo ambalo anapaswa kufanya anatenda dhambi.
James 5
James 5:1-3
Sentensi unganishi
Yakobo anawaonya matajiri juu ya starehe na utajiri.
enyi mlio matajiri
Yaweza kuwa na maana ya 1) Yakobo anawapa onyo kali wale wanaoamini kwenye utajiri au 2) Yakobo anazungumza kuhusu watu wasioamini ambao ni matajiri. "enyi mlio matajiri na mnaosema mnamcha Mungu"
kwa sababu ya taabu inayokuja juu yenu
Yakobo anaelezea kuwa watu hao watateseka sana baadae na taabu yao inakuja. "kwa kuwa mtateseka sana baadae"
Utajiri wenu umeharibiwa na mavazi yenu yametafunwa na wadudu waharibifu. Dhahabu zenu na fedha zenu zimekosa thamani
imetafunwa. Dhahabu zenu na fedha zimekosa thamani. Yakobo anazungumza juu ya matukio haya kama vile yameshatokea. Yakobo anazungumzia utajiri wa duniani haudumu na hauna uzima wa milele. "Utajiri wenu umeharibiwa, nguo zenu zimetafuwa na dhahabu zenu na fedha zimekosa thamani"
utajiri ... nguo ... dhahabu
Hivi vitu vimetajwa kama mifano ya vitu vya thamani kwa mwanadamu.
uharibifu wake utashuhudia dhidi yenu
"uharibifu" ni neno linaloelezea namna ambavyo chuma yaweza haribika. Yakobo anazungumzia kuhusu uharibifu kwa kuwa umesababishwa na watu waovu na matendo yao. "Na Mungu akiwahukumu kuharibiwa kwa mali zenu kutakuwa kama mtu anayewahukumu mahakamani"
Itaangamiza ... kama moto
Uharibifu unazungumzwa kama vile moto ambao utakuja kuwaangamiza watu.
Miili yenu
"mwili" inamaanisha mwili mzima.
Moto
Moto inatumika kuwakumbusha watu kwamba mara nyingi inamaanisha hukumu ya Mungu itakayokuja juu ya waovu.
Katika siku ya mwisho.
Hii inaelezea wakati muafaka wa Mungu kuja kuhukumu ulimwengu. Waovu wanadhani wanahifadhi utajiri kwa ajili ya baadae lakini wanachokifanya wanahifadhi hukumu. "wakati ambao Mungu anataka kuwahukumu"
James 5:4-6
Sentensi unganishi
Yakobo anaendelea kuwaonya matajiri juu ya starehe na utajiri.
malipo ya watendakazi-wale ambao hamjawalipa kwa kuvuna katika mashamba yenu- wanalia
Pesa ambayo ilitakiwa ilipwe imeelezewa hapa kama mtu anayelalamika juu ya dhuluma aliyofanyiwa. "kwa kuwa hamwalipi mliowaajiri kufanya kazi kwenye mashamba yenu mnafanya makosa"
kilio cha wale waliovuna mazao yenu kimeyafikia masikio ya Bwana wa Majeshi.
Kilio cha wanaovuna kimesikika mbinguni. "Bwana wa majeshi amesikia kilio cha wavunaji"
kwenye masikio ya Bwana wa Majeshi
Mungu anazungumziwa kuwa ana masikio kama mwanadamu. "Bwana wa majeshi amesikia"
Mmejinenepesha mioyo yenu kwa siku ya machinjo
Hapa watu wanaelezewa kama wanyama, wanaolishwa vizuri ili wanenepe na kuchinjwa kwa ajili ya karamu. Japokuwa hamna atakayesherehekea siku ya hukumu. "Tamaa zeni zinawaandaa kwa hukumu ya milele"
mioyo yenu
"Mioyo" imezungumziwa kama kituo cha tamaa za mwanadamu. Neno hili linasimama kumuelezea mtu kwa ujumla.
Mmemhukumu ... mwenye haki
"Mmehukumu" inaweza isiwe na maana ya kisheria ya kupitisha hukumu ya kifo. Bali inawazungumzia watu waovu na wenye nguvu wanaoamua kuwanyanyasa masikini mpaka wanakufa.
mwenye haki
"Mtu anayefanya mambo yanayofaa" Hii sentensi inaelezea watu wenye haki kwa ujumla na sio mtu mmoja.
asiyeweza kuwapinga
"Asiye kinyume na ninyi"
James 5:7-8
Sentensi unganishi
Yakobo anabadilisha mada toka kwenye kuwakemea matajiri na kuwapa mawaidha waamini.
Maelezo ya jumla
Kwa kufunga Yakobo anawakumbusha waamini kuhusu ujio wa Bwana na kuwapa mafundisho mafupi namna ya kuishi kwa ajili ya Mungu.
Kwa hiyo vumilieni
"Kwa ajili ya hili kuweni na subira na uvumilivu"
mpaka ujio wa Bwana
Sentensi hii inaelezea ujio wa Yesu, atakapoanzisha ufalme wake duniani na kuhukumu watu wote. "Mpaka Kristo atakapokuja"
Mkulima
Katika mazungumzo haya Yakobo anatumia mkulima na mwamini kuelezea namna ya kuwa mvumilivu.
Kazeni mioyo yenu
Yakobo anawataka waamini wawe na mioyo thabiti na kuwa na msimamo. "Kuweni na msimamo" au "Ifanyeni imara mioyo yenu"
kuja kwake Bwana ni karibu.
"Bwana atarudi mapema"
James 5:9-11
Nsinung'unikiane, ndugu ... ninyi
Yakobo anawaandikia waamini wa Kiyahudi waliotawanyika.
ninyi kwa ninyi,
"kila mmoja na mwenzake"
Hamtahukumiwa
Hii yaweza kuwa "Kristo hatawahukumu ninyi"
hakimu anasimama mlangoni
Yakobo anamfananisha Yesu, kama hakimu kwa mwanadamu na kuelezea ni kuwa bado mda mfupi sana Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu"
mateso na uvumilivu wa manabii
"ni kwa namna gani manabii walivumilia mateso na hukumu"
walionena katika jina la Bwana
"Waliongea kwa jina la Bwana kwa watu"
Tazama
"Tazama" inasisitiza "sikiliza kwa makini" au "kumbuka"
wale wanaovumilia
"Wale watakaoendelea kumtii Mungu hata katika hali ngumu"
James 5:12
Zaidi ya yote
"Hii ni muhimu" au "Hasa"
ndugu zangu
"waamini wenzangu"
msiape
"kuapa" ni kusema kuwa utafanya jambo au jambo fulani ni kweli na kuwa na wajibu kwa mamlaka za juu. "Msiape"
aidha kwa mbingu ama kwa nchi
Maneno "mbingu" na "nchi" linamaanisha mamlaka ya kiroho na kibinadamu zilizopo mbinguni na duniani.
"ndiyo" yenu na imaanishe "ndiyo" na "hapana" yenu na imaanishe "hapana
Fanya ulichosema utafanya bila kuapa"
msije kuangukia chini ya hukumu
Kuhukumiwa inazungumzwa kwa mtu aliyeanguka na kulemewa na kitu kizito. "Hivyo Mungu hatawahukumu"
James 5:13-15
Kuna yeyote miongoni mwenu ana mateso? Lazima aombe
"Kama kuna mtu yeyote anapata mateso yampasa kuomba"
Je, mtu yeyote ni mwenye kuchangamka? Na aimbe sifa
"Mtu yeyote akiwa na furaha, yampasa aimbe nyimbo za kusifu"
Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Na aite
"Mtu yeyote akiwa mgonjwa na aite watu"
maombi ya imani yatamponya mgonjwa, na Bwana atamwinua
Mwamini akimuombea mgonjwa, Mungu atasikia maombi yake na kumponya mtu huyo. "Mungu atasikia maombi ya mwamini aombapo kwa imbani na kumponya mgonjwa.
James 5:16-18
Maelezo ya Jumla
Kwa kuwa haw walikuwa waamini wa kiyahudi, Yakobo anawakumbusha watu kuomba kwa kukumbuka moja wa manabii na namna walivyoomba.
Kwa hiyo ungameni dhambi zenu
Hii ni kukubali makosa yako kwa waamini wengine ili uweze kusamehewa.
ninyi kwa ninyi,
"kila mmoja na mwenzake"
ili muweze kuponywa
"Ili Mungu awaponye"
Maombi ya mwenye haki huzaa matokeo makubwa
Maombi ni kitu chenye nguvu sana. "Mtu anayemcha Mungu akiomba, Mungu anafanya mambo makuu"
Juhudi
"shauku"
Tatu ... sita
"3 ... 6"
mbingu zilimwaga mvua
Mbingu inamaanisha mawingu ambayo inaelezwa kama chanzo cha mvua. "Mvua ilishuka toka mawinguni"
nchi ikatoa mavuno.
Hapa nchi inaelezwa kama chanzo cha mavuno
Matunda
"Matunda" inamaanisha mazao ya mkulima
James 5:19-20
Ndugu zangu
"Waamini wenzangu"
kama yeyote miongoni mwenu anapotoka kutoka kwenye ukweli, lakini mtu mwingine akamrejesha
Mwamini ambaye anaacha kumwamini Mungu na kumtii yeye anafananishwa na kondoo aliyeondoka kwenye kundi. Mtu anayemrejesha ili amwamini Mungu tena anafananishwa na mchungaji anayetafuta kondoo aliyepotea. "Mtu yeyote akiacha kumtii Mungu na mwingine akamsaidia kuanza kumtii Mungu tena"
yeyote amwongozaye mwenye dhambi kuondoka katika njia yake ya ukosaji... atafunika wingi wa dhambi.
Yakobo anamaanisha kuwa Mungu atatumia matendo ya huyu mtu ya kumrejesha aliyekosa ili atubu na kuokolewa. Lakini Yakobo anaongea kama vile huyu mtu mwingine ndo ameokoa nafsi ya mwenye dhambi toka kwenye kifo.
ataponya nafsi yake kutoka katika mauti na atafunika wingi wa dhambi.
Hapa "kifo" inamaanisha kufa kiroho, kutengana na Mungu. "Atamuokoa na kifo cha kiroho na Mungu atamsamehe mkosaji dhambi zake zote"
atafunika wingi wa dhambi.
Yawza kumaanisha kuwa 1) Mtu atakayemrejesha ndugu aliyetenda uovu, dhambi zake zitasamehewa. au 2) Ndugu aliyetenda uovu akirudi kwa Bwana , dhambi zake zitasamehewa. Dhambi inazungumzwa kama jambo ambalo Mungu atawasamehe watu wake.