2 Peter
2 Peter 1
2 Peter 1:1-2
Simon Petro
"Kutoka Kwa Simoni Petro." Lugha Yako inaweza kuwa na namna fulani ya kumtambulisha mwandishi wa barua. Mimi Simon Petro niliandika barua hii.
Mtumwa na Mtume waYesu Kristo
Petro anaongelea mtazamo wake wa kuwa mtumwa wa Yesu Kristo. Pia alipewa nafasi na mamlaka ya kuwa mtume wa Kristo
Kwa wale
Petro anaonekana kuwaandikia waumini wote watakaosoma waraka huu. Kwenu waumini.
Tumepokea
Sisi mitume tumepokea
Neema iwe kwenu
Neno "ninyi" linamaanisha waumini wote kwa ujumla
Yesu Bwana wetu
Yesu Bwana wa waumin na Mitume
Neema na iwe kwenu;amani iongezeke kupitia maarifa ya Mungu na Yesu Bwana wetu.
Upole wenu na amani uongezeka kwa sababu mnamjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
2 Peter 1:3-4
Aliyetuita
Kwanza Mungu alitufikia. "Sisi" Neno hili linamanisha Petrop pamoja na wasikilizaji wake.
Kwa ajili ya uzuri wa utukufu wake
"kwa njia ya heshima yake na uzuri wa maarifa"
Kwa njia hii alitutumainishi ahadi kuu za thamani
"Ahadi za thamani za Mungu zilikuja njia ya heshima na uzuri wa maarifa"
asili ya Mungu
"tabia ya ukamilifu wa Mungu"
kwa kadiri tunavyoendelea kuachc uovu wa dunia
kadiri unavyoendelea kuziacha tamaa mbaya za dunia."
2 Peter 1:5-7
Kwa sababu hii
Kwa sababu ya kile ambacho Mungu amefanya
maarifa
"uzuri wa maarifa"
Kwa sababu ya uzuri maarifa
kwa kutumia uzuri wa maarifa uongeze ufahamu
kupata upendo wa ndugu
kuwa wapole kwa sisi kwa sisi
2 Peter 1:8-9
mambo haya
haya mambo ni:- imani, uzuri, maarifa, kiasi, uvumilivu, utauw, upendo wa ndugu, na upendo.
"Ninyi hamtakuwa tasa au msiozaa matunda"
mtazaa matunda
yeyote asiyekuwa na mambo haya
mtu yeyote asiyekuwa na mambo haya
huyaona mabo ya karibu tu, yeye ni kipofu
usemi huu unamfananisha mtu anayefikiria mambo ya duniani tu kuwa yako vizuri mbele yake, kama mtu asiye na macho.
2 Peter 1:10-11
kwa hiyo
Neno "kwa hiyo" linaanzisha mwitikio wa waumini kwa kile kilichosemwa mapema.
kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yenu
Neno " wito" linamaanisha mwaliko wa ujula waMungu kwa watu wote. Neno "uteule" linamaanisha watu maalumu ambao Mungu amewchagua. Maneno haya mawili yana maana sawa.
hamtajikwaa
hamtashindwa kiroho na katika tabia njema
2 Peter 1:12-15
Kwa hiyo
Mwandishi anataka kutengeneza maelezo ambayo yanatokana na kile alichoandiaka mwanzoni.
Nitakuwa tayari kuwakumbusha mambo haya
Petro anaonyesha kuwa ataendelea kuwakumbusha waumini jinsi ya kumfuata Kristo
juu ya mabo haya
jinsi waumini inavyowapasa kukua katika imani
kuwaamsha
huu ni ufafanuzi unaomaanisha "kuwaandaa ili wawe tayari"
nimo katika hema hii
Haya maelezo yanaytumika badala ya "kwa sababu bado ninaishi"
Nitajitahidi kwa bidii kwa ajili yenu ili mkumbuke mambo haya
"Ntatumia juhudi zangu kuwafundish mambo haya ili muyakumbuke"
Nitaiondoa hema yangu
huu nu ufafanuzi wa "Nitakufa"
Baada yakuondoka Kwangu
Maelezo haya yanaonyesha "baada ya kufa kwangu"
2 Peter 1:16-18
Pale sauti iliposikika toka katika utukufu mkuu
Petro anamaanisha yeye mwenyewe na yule mwanafunzi mwingine, Yakobo, na Yohana waliposikia ile sauti ya Mungu.
Kwa kuwa sisi hatukufuata hadithi zilizoingizwa kwa ustadi
Kwa kuwa sisis mitume hatukufuata hadtibzilizotengenezwa kwa ustadi
Yetu
waumini wote ikijumuisha sisi mitume
Pale tulipokuwa naye kwenye ule mlima matakatifu
Petro anamaanisha wakati ule Yesu alipobadilika sura yake ikang'aa mbele ya Petro, Yakobo na John (Tazama Mathayo)
2 Peter 1:19-21
Tunalo hili neno la unabii lililothibitika
Perto anamaanisha wale Mitume. Mitume wnaujumbe kutoka kwa malaika ambao wanajua kuwa ndiyo ukweli kutoka kwa Mungu
Ambalo kwalo mwafanya vyema kulitekeleza
Petro anawaelekeza waumini kuwa na utayari kwa jumbe za kinabii
Ni kama taa ing'aayo gizani mpaka kunapokucha
Ujumbe wa kinabii umelinganishwa na taa inayotoa Mwanga gizani mpaka mwanga unapowadia asubuhi.
Na nyota za mawio zionekanapo katika mioyo yenu
Nyota ya asubuhi ni Kristo anayekuja kuishi kwenye mioyo yetu.
isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu
Roho mtakatifu aliwaongoza watu hawa, kwa hiyo waliongea ambacho Mungu alitaka waongee.
2 Peter 2
2 Peter 2:1-3
Manabi wa uongo walikuja kwa Israeil, na walimu a uongo watakuja kwenu
Kama ile manabii wa uongo walivyokuja wakiidanganya Isreli, vivyo hivyo walimu wa uongo watakuja wakidanganya uongo juu ya Kristo
Ukengeufu
Haya ni maoni yaliyo kinyume na mafunisho ya Kristo na ya Mitume
Bwana aliyewanunua
Yesu ndiye Bwana aliyelipa kwa ajili ya dhambi za watu wote kwa njia ya kifo chake, na kuzikwa kwake na ufufuo.
nja za aibu
Neno "zao" linawakilisha manabii na walimu wa uongo" jinsi matendo yao yalivyo ya zinaa iliyokidhiri.
2 Peter 2:4-6
Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka
Hii inaanzisha Mpangilio wa sentensi zinazoanza na "kama"
bali aliwatupa kuzimu ("Tartarus)
"Tartarus
ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia
Mungu atawaweka katika gereza wakisubiri hukumu ya mwisho
Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani...wakati alipoachilia gharika juu yaulimwengu ulioasi
Mungu aliuhribu ulimwengu wa zamani na watu waasi kwa gharika
Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomorra kiasi cha kuwa majivu
Mungu alitumia moto kuwaharibu watu wasi mcha Yeye katika miji ya Sodoma na Gomora
bali alimhifadhi Nuhu
Mungu alimwokoa mtu wa haki Nuhu katika gharika
ili iwe mfano kwa ajili ya watu waovu katika siku za usoni
kama vile Sodoma na Gomora ilivyoharibiwa kwa moto katika siku za usoni Mungu atawaharibu katika ziwa la moto.
2 Peter 2:7-9
alimwokoa Ltu mtu wa haki
Mungu alimwokoa Lutu aliyeishi maisha ya tabia njema
akitesa nafsi yake kwa ajili ya yale alyosikia na kuyaona
Lutu aliendelea kuteseka na kuhrasiwa na tabia za anasa za wenyeji wa Sodoma na Gomora
tabia chafu za wsiofuata sheria
"anasa na tabia inayoharibika ya watu waliovunja sheria ya Mungu"
mtu wa haki
Hii inamaanisha Lutu mtu wa haki
watu wa Mungu
"watu wanaomtii Mungu"
alikuwa akitesa roho yake
Aliusumbua utu wake wa ndani
jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajil ya hukumu skatika siku ya mwisho
Watu wasio haki hawataiepuka hukumu ya Mungu. Watakapokufa watakataliwa mpaka siku ya hukumu
2 Peter 2:10-11
kwa hakika huu ndio ukweli
Neno "huu" linamaanisha Mungu kuwalinda watu wasio haki gerezani mpaka siku ya hukumu.
wale wanaoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka
Watu wasio haki wanaoendela kuishi katika tamaa ya mwilii na kuwachukia viongozi wao au watawala wao.
mwili
Neno "mwili" linamaanisha ubinadamu katika dhambi ya asili ya mwanadamu
wana ujasiri katika dhamiri zao
Neno "dhamiri" linamaanisha wale wanaoendelea katika uharibifu wa tamaa katika dhambi zao za asili na hawaheshimu malaika na mamlaka ya kiroho
Hwaogopi kuwakufuru watukufu
Wasio haki hawaogopi kuwachokoza na kuwanenea maovu malaika
malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu
Malaika wana nguvu za mwili na wa mamalka kuliko wanadamu
Lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana
"lakini malaika hawaleti humu iumizayo dhidi ya hawa watu kwa Bwana"
2 Peter 2:12-14
hawa wanyama wasio na akili
Kama vile wanyama wasivyoweza kueleza kwa mantiki, vivyo hivyo hawa watu hawaezi kuwa na mantiki, "Hawa walimu wa uongo wako kama wanyama wasio na akili"
Hawajui wanachotukana
Huongea uovu ambao hawaujui
wataangamizwa
Mungu atwaangamiza watu hawa
Wataumizwa kwa ujira wa maovu yao
"Wanachofikiri kuwa ni kizuri kwao, kiuhalisia ni kibaya kwao"
Wamejaa uovu na uchafu
Neno "uchafu" na "uovu" vinamaanisha maana moja. Waalimu wa uongo hufedhehesha na kutahayarisha amabavyo ni sawa na uchafu na uovu ambavyo mtu hawezi kviondoa
hufurahia udanganyifu wanaposherehekea na wewe
huendele katika furaha ya kuwadanganya watu wasio hatia na katika macho yao hawaonyeshi hatia
macho yao yamefunikwa na uzinzi, hwatosheki kutenda dhambi
"wanatamani kila mwanmke wanayemuona na kamwe hawatosheki"
wana mioyo iliyofunzwa kujaa tamaa
" inawakirisha mtu kama kamili, alifunzwa katika mawazo na na mattendo ya uchoyo. wanatamani utajiri na miliki isiyo haki.
2 Peter 2:15-16
Wameiacha njia ya kweli, wamepotoka na wamefuata...
"walimu wa uongo .wameiacha...wamepotoka..wamefuata". Walimu wa uongo wamekataa kumtii Mungu kwa kukataa kilicho sahihi
aliyependa kupata malipo yasiyo haki
alipokokea malipo ya anasa na yenye matendo ya dhambi
Lakini alikemwa kwa ajili ya ukosaji wake
alionywa vikali kwa kutokutii kwake
alizuia wazimuwa nabii
Mungu alitumia punda kuzuia upumbavu wa nabii
2 Peter 2:17-19
Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji
Kama vile chemichemi zilizokauka na hazitoi maji kwa ajili ya maisha ya kawaida, vivyo hivyo mafundisho yao hayawaongozi watu katka maisha ya kiroho. Ni eneo la uongo kuwafariji waatu, kisima kikavu
Ni kama mawingu yanayotoweshwa na upepo
Mawingi mengine hubeba mvua. Mvua hii huleta maji yanayokuza au maji yagharikishayo. Hawa watu ni kama hayo mawingu yanayobeba uharibifu.
Huongea kwa majivuno matupu
Hotuba zao ni za kujivuna zisizo na maana.
Huangusha watu kwa tamaa ya mwili
Wanawavuta watu ili waingie katika dhambi ya mwili na matendo ya anasa.
Huwaahidi watu uhuru wakati waowenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi.
Huahidi uhuru wa uongo, uhuru unaowapeleka watu kutendda dhambi. huu ni utumwa wa dhambi.
Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa kile kinachmtawala
Mwanadamu hufanya kwa tamaa mabo yale anayopungukiwa kiasi
Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosji
Hujaribu kuwaangamiza watu ambao ni wapya katika imani.
2 Peter 2:20-22
Yeyote ajiepushaye na uchafu wa ulmwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo
Mtu yeyote ambaye amempokea Bwana na Mwokozi Yesu Kristo na kugeuka kutoka kwenye uchafu na maisha yasyo matakatifu.
Hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo
Ni wabaya zaidi kwa sababu wana maarif ya maisha matakatifu na wamechagua kurudi kwenye maisha ya dhambi
kama wasingeifahamu njia ya haki
Maisha ya yanayompendza Mungu.
amri takatifu walizopewa
Sheria za Mungu na amri za Mungu ambazo wamepewa wangejua namna ya kuishi kwa ajili ya Mungu
Mithali hii...mbwa huyarudia matapishi yake, Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope."
Ni usemi wa busara unaowalinganisha wale wanaoijua kweli lakini wanrudia maisha ya uasi. "Mbwa huyarudia matapishi yake" imenukuliwa toka Mithali 26:11. Katika namna yeyote maana yake inabaki kuwa "mnyama hawezi kufundishika ili asijnajisi mwenyewe"
2 Peter 3
2 Peter 3:1-2
Maelezo ya ujumla
Petro anaanza kuzungumza kuhusu siku za mwisho
kukuamsha katika akili
Petro anasema kwa kusababisha wasomaji wake kufikiri kuhusu mambo haya kama alikuwa anawaamsha kutoka kwenye usingizi. "kuwasababisha kufikiri kwa mawazo safi"
maneno yaliyosemwa kabla na manabii watakatifu
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "maneno ambayo manabii watakatifu walisema wakati uliopita"
amri ya Bwana wetu na mwokozi kwa kutumia mitume
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "amri ya Bwana wetu na Mwokozi, ambayo mitume wenu waliwapa"
2 Peter 3:3-4
Ujue ili kwanza
"Ujue hili kama jambo la muhimu sana."
wakienenda saswasa na matakwa yao
Hapa neno "matakwa" urejea kwa tamaa mbaya ambazo ziko kinyume na mapenzi ya Mungu. "kuishi sawasawa na tamaa zao mbaya"
kuendelea
kitendo, tenda
Iko wapi ahadi ya kurudi kwake?
Wabishi wanauuliza swali la utupu kusisitiza kuwa hawaamini kuwa Yesu atarudi. Neno "ahadi" urejea kwa kutimizwa kwa ahadi kuwa Yesu atarudi. "Ahadi ya kuwa Yesu atarudi sio kweli! Hatarudi!
Baba zetu walikufa
Hapa "Baba" urejea kwa mababu walioishi zamani. "Walikufa" ni lugha ikimaanisha walikufa.
vitu vyote vilikuwa hivyo tangu mwanzo wa uumbaji.
Wabishi wanajadili kwamba hakuna chochote katika ulimwengu kimeweza kubadilika, haiwezi kuwa kweli kwa Yesu kurudi.
tangu mwanzo wa uumbaji.
Hii inaweza kutofasiriwa kama kikundi cha maneno ya kitenzi. "Kwani Mungu aliumba ulimwengu"
2 Peter 3:5-7
mbingu na nchi vilianza... zamani, kwa amri ya Mungu
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu alianzisha mbingu na nchi... zamani kwa neno lake"
vilianza kutokana na maji na kupitia maji
Hii inamaanisha kuwa Mungu alisababisha ardhi kutoka kwenye maji, kukusanya maji kwa pamoja kufanya ardhi ionekane.
kupitia neno lake
Hapa "neno lake" urejea kwa neno la Mungu na maji
ulimwengu kwa kipindi hicho, ikiwa imejaa maji, iliharibiwa
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu aliujaza ulimwengu na maji kwa kipindi hicho na kuuharibu"
mbingu na dunia zimetunzwa kwa neno hilo hilo kwa ajili ya moto.
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu kwa neno lile lile, ametunza mbingu na nchi kwa ajili ya moto."
kwa neno hilo hilo
Hapa "neno" usimama kwa Mungu, atakaye toa neno.
Vimehifadhiwa kwa ajili ya siku ya hukumu
Hii kusemwa katika kauli tendaji na kuanza sentensi mpya. "Anawatunza kwa ajili ya siku ya hukumu"
kwa ajili ya siku ya hukumu na maangamizi ya watu wasio wa Mungu
Hii inaweza kusemwa pamoja na maneno ya kitenzi. "kwa siku wakati anapohukumu na kuharibu watu wasio wa Mungu"
2 Peter 3:8-9
Hii haiwezi kuchenga ujumbe wako
"Hauwezi kushindwa kuelewa hili" au "Usipuuze hii"
kwamba siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu moja
"kwamba kutoka kwa mtazamo wa Bwana, siku moja nia kama miaka elfu moja"
Si kwamba Bwana anafanya pole pole kutimiza ahadi
"Bwana si kwamba anafanya pole pole kutimiza ahadi zake"
kama inavyofikiriwa kuwa
Baadhi ya watu wanafikiri kuwa Bwana si kwamba anafanya pole pole kutimiza ahadi zake kwa sababu mtazamo kuhusu wakati ni tofauti na Mungu.
2 Peter 3:10
hata hivyo
Ijapokuwa Bwana ni mvumilivu na anataka watu watubu, hakika atarudi na kuleta hukumu.
siku ya Bwana itakuja kama mwizi
Petro anazungumza juu ya siku ambayo Mungu atamhukumu kila mmoja kama mwizi anayekuja pasipo kutegemewa na kuwashtusha watu.
Mbingu itapita kwa kupaza kelele
"Mbingu zitapita"
Vitu vitateketezwa kwa moto
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu atateketeza kwa moto"
Vitu
Maana zinazowekana ni 1) vitu vya mbinguni kama vile jua, mwezi, na nyota au 2) vinavyofanya mbingu na nch, kama vile mchanga, hewa, moto na maji.
nchi na matendo yatafunuliwa
Mungu ataiona dunia yote na matendo yote ya kila mmoja, na atahukumu kila kitu. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu ataiweka wazi nchi na kila kitu watu walichofanya."
2 Peter 3:11-13
Sentensi unganishi
Petro anaanza kwa kuwaambia wakristo namna watakavyo ishi wakati wanasubiri siku ya Bwana.
Kwa kuwa vitu vyote vitateketezwa kwa njii hii.
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Tangu Mungu atahukumu mambo haya yote katika njia hii"
je utakuwa mtu wa aina gani?
Petro anatumia swali la kejeli kusisitiza kile atakachosema badae, kwamba "wanapaswa kuishi maisha ya utakatifu na utaua" "unajua ni aina gani ya watu wanapaswa kuwa"
mbingu itateketezwa kwa moto, na vitu vitayeyushwa katika joto kali
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu ataangamiza mbingu kwa moto, na ataviyeyusha
sehemu ambayo watakatifu wataishi
Petro anazungumza juu ya "utakatifu" kama ilivyokuwa kwa mtu. HIki ni kirai cha watu anaishi au sehemu ya watu watakao ishi kwa utakatifu.
2 Peter 3:14-16
jitahidi kuwa makini na kutolaumika na kuwa na amani pamoja naye
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "jitahidi kuishi katika njia ili kwamba Mungu asikute doa na kulaumiwa na kuwa na amani na yeye na kila mmoja"
doa na kutolaumiwa
Maneno "doa" na "kutolaumiwa" kimsingi umaanisha kitu kile kile na kusisitiza maadili ya usafi."usafi kamili"
doa
Hii usimama kwa ajili ya "kosa"
zingatia uvumilivu wa Bwana wetu katika wokovu
Kwa sababu Bwana ni mvumilivu, siku ya hukumu bado haijatokea. Hii uwapa watu fursa ya kutubu na kuokolewa, kama alivyo elezea katika 3:8. "Pia, nafikiri kuhusu uvumilivu wa Bwana wetu kama kukupa fursa ya kutubu na kuokolewa"
kutokana na hekima ambayo alipewa.
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "kutokana na hekina ambayo Mungu alimpa"
Paulo anaongelea hayo yote katika barua zake,
"Paulo anaongelea katika barua zake uvumilivu wa Mungu kuwaongoza katika wokovu"
kuna vitu ambavyo ni vigumu kuvielewa.
Kuna vitu katika barua za Paulo ambavyo ni vigumu kuvielewa.
Watu wasio na adabu na uimara wameviharibu vitu hivyo
watu wajinga na wasio na uimara hutofasiri vibaya vitu katika barua za Paulo kwamba ni ngumu kuelewa.
Wajinga na uimara
"Wasio wa kawaida na legarega" Hawa watu hawajafundishwa namba ya kutofasiri maandiko na hawajafanywa imara katika ukweli wa injili.
Kuelekea maangamizi yao.
"matokea yake ni maangamizi yao"
2 Peter 3:17-18
Sentensi unganishi
Petro anamalizia kuwaelekeza wakristo na kumalizia barua yake.
Hivyo, wapendwa kwa kuwa mnayafahamu hayo.
"Hayo" urejea kwa ukweli kuhusu uvumilivu wa Mungu na mafundisho ya walimu wa uongo.
jilindeni wenyewe
"jilindeni wenyewe"
ili kwamba msipotoshwe na udanganyifu wa walaghai
Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "ili kwamba walaghai wasiwapotoshe kwa maneno yao ya udaganyifu
msipotoshwe...udanganyifu
Kushawishiwa kuto mtii Mungu kunaongelewa kama kuondolewa katika njia sahihi ya kufuata. Udanganyifu na mafundisho ya uongo yanaongelewa kama watu wanaoweza kumoongoza mtu nje ya njia sahihi.
kupoteza uaminifu wako
Uaminifu unaongelewa kama kitu cha kumiliki ambacho wakristo wanaweza kukipoteza. "wewe acha kuwa mwaminifu"
mkue katika neema na ufahamu
"kuongozeka katika neema na ufahamu"
neema na ufahamu wa Bwana na mwokozi Yesu Kristo
Unaweza kutofasiri "neema" na 'ufahamu" kutumia maneno kitenzi. Ona utakavyo tofasiri maneno hayo hayo katika 1:1 na 1:8 na 2:20. "kuwa na uzoefu zaid na zaid na Bwana na Mwokozi Yesu Kristo kukutenda wema wewe, na kwamba unapata kumjua yeye vizuri na vizuri"