Romans
Romans 1
Romans 1:1-3
Paulo
Lugha yako inaweza kuwa na namna ya kumtambulisha mwandishi wa barua. "Mimi Paulo naandika barua hii." Unaweza pia kusema ni kwa nani barua iliandikwa.
kuitwa kuwa mtume, na kutengwa kwa ajili ya injili ya Mungu
"Mungu alinita mimi kuwa mtume na alinichagua kuwaambia watukuhusu injili"
Kuitwa
Hapa inamaana kuwa Mungu aliteua au kuchagua watu kuwa watoto wake, kuwa watumishi wake na watangazaji wa ujumbe wake wa wokovu kupitia kwa Yesu.
Hii ni injili ambayo aliiahidi kabla kwa mitume wake kwenye maandiko matakatifu
Mungu aliwaahidi watu wakekwamba atawaandalia ufalme. Aliwaambia mitume waandike ahadi hizi kwenye maandiko.
Ni kuhusu mwana wake
Hii inamaanisha "Injili ya Mungu," habari njema ambayo Mungu aliwaahidi kuwapa mwanawe ulimwenguni.
Mwana
Hiki ni cheo cha muhimu sana kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
Aliyezaliwa toka kwa uzao wa Daudi kutokana na mwili
Hapa neno "mwili" linamaanisha mwili unaoonekana. "Ambaye ni uzao wa Daudi kutokana na asili ya mwili" au "aliyezaliwa kwenye familia ya Daudi."
Romans 1:4-6
Maelezo yanayounganisha:
Paulo anazungumza kuhusu majukumu yake katika kuhubiri.
Alithibitishwa kuwa mwana wa Mungu.
Neno "yeye" linamaanisha Yesu. "Mungu alimthibitisha yeye kuwa mwana wa Mungu"
Mwana wa Mungu
Ufufuo wa Yesu unathibitisha kuwa alikuwa na ndiye "mwana wa Mungu." Hiki ni cheo cha muhimu sana cha Yesu.
Roho ya utakatifu
Hii inmaanisha roho mtakatifu.
kwa ufufuo wa wafu
"kwa kuleta tena kwenye uhai baada ya kufa"
Tumepokea neema na utume
"Alinichagua mimikuwa mtume" au "Mungu alinipa zawadi ya neema ya kuwa mtume." "Mungu kwa neema yake alinipa zawadi"
Sisi
Hapa neno "sisi" linamaanisha Paulo na mitume 12 waliomfuata Yesu lakini ukiwatoa waamini katika kanisa la Roma.
kwa kutii imani kati ya mataifa yote, kwa ajili ya jina lake.
Paulo anatumia neno "jina" akiwa anamzungumzia Yesu. "kwa ajili yakuwafundisha mataifa yote kutii kwa sababu ya imani yao kwake"
Romans 1:7
Barua hii ni kwa ajili ya wpote waliopo Roma, wapendwa wa Mungu, walioitwa kuwa watu watakatifu
"Naandika barua hii kwenu nyote mliopo Roma ambao mnapendwa na Mungu na mmechaguliwa kuwa watu wake"
Neema iwe kwenu, na amani
"Neema na amani iwe kwenu"
Romans 1:8-10
Ulimwengu wote
Hii inamaanisha ulimwengu walioufahamu, ambao ni ngome wa Roma.
Kwa kuwa Mungu ni shahidi yangu
Paulo anasisitiza kwamba ameomba kwa bidii kwa ajili yao na kwamba Mungu alimuona akiwa anaomba.
Kwa roho yangu
Hapa inamaanisha roho ya mtu ni sehemu yake ambayo inamtambua Mungu na kumwamini.
Injili ya mwanawe
Habari njema (injili) ya Biblia ni kwamba mwana wa Mungu alijitoa mwenyewe kama mkombozi wa dunia.
Mwana
Hiki ni cheo cha muhimu sana kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
Nakutaja wewe
"Niliongea na Mungu kuhusu wewe"
Kila mara kwenye maombi yangu nimekuwa nikiomba kuwa.. Hatimaye nifanikiwe... kuja kwako
Kila mara naomba, na kumwambia Mungu kwamba... Nifanikiwe... kuja kukutembelea wewe"
Kwa njia yoyote
"Kwa njia yoyote ambayo Mungu ataruhusu"
Hatimaye
"mwisho"
Kwa mapenzi ya Mungu
"kwa sababu Mungu ametamani hivyo"
Romans 1:11-12
Sentensi unganishi:
Paulo anaendelea kuweka wazi maelezo yake kwa watu wa Rumi kwa kuelezea shauku yake ya kuwaona mmoja mmoja.
Kwa kuwa natamani kuwaona
"kwa kuwa nataka kuwaona"
Kwa kuwa
"kwa sababu"
baadhi ya zawadi za roho, ili kuwatia nguvu
"baadhi ya zawadi toka kwa Roho Mtakatifu, ambayo itawasaidia na kuwatia nguvu"
Ambayo ni, mfarijiane kati yenu, kupitia imani ya kila mtu, yenu na yangu
"Namaanisha kwamba nataka tutiane moyo kwa kutumia uzoefu wa imani yetu kwa Yesu"
Romans 1:13-15
Sitaki msifahamu
Paulo anasisitiza kwamba alitaka wawe na taarifa hii. "Nilitaka ninyi mfahamu haya"
Ndugu
Hapa anamaanisha Wakristo wenzake, ukijumuisha wote wanaume na wanawake.
Lakini nilikuwa nimezuiwa
"kuna kitu kilikuwa kinanizuia"
Muwe na tunda
"Tunda" linawakilisha watu wa Roma amabao Paulo alitaka kuwaongoza waamini injili.
Kama ilivyo kati ya Mataifa
"Kama ambavyo watu walikuja kuamini injili kwemye taifa lingine la Mataifa"
Nina deni kwa wote
"Lazima nipeleke injili kwa"
Romans 1:16-17
Siionei haya injili
"Nina ujasiri ninapoongea kuhusu injili, japokuwa watu wengi wanakataa"
Kwa kuwa siionei haya
Paulo anaelezea kwa nini anataka kuhubiri injili Roma.
Kwa kuwa ndani yake
Hii inaelezea injili. Paulo anaelezea kwa nini anahubiri injili kwa ujasiri.
Ni nguvu ya Mungu ya wokovu kwa kila mtu anayeamini
"Ni kupitia injili nguvu ya Mungu inawaokoa wanaomwamini Kristo"
Kwa Wayahudi kwanza na kwa Wagiriki
"kwa watu wa Kiyahudi na watu wa Kigiriki"
Kwanza
Hii inaweza kuwa na maana kuwa 1) "ya kwanza kwa sababu ya mda" au 2) "ya muhumu sana"
Haki ya Mungu inadhihirishwa toka imani mpaka imani
"Mungu amedhihirisha kuwa ni kwa imani toka mwanzo mpaka mwisho watu wanakuwa na haki" "Mungu amedhihirisha haki yake kwa wale walio na imani, na matokeo yake wanaimani zaidi" au "kwa sababu Mungu ni mwaminifu, amedhihirisha haki yake, na matokeo yake watu wamekuwa na imani zaidi"
Mwenye haki ataishi kwa imani
"Ni watu wanaomwamini Mungu ndio anaowaona wenye haki, na wataishi milele"
Romans 1:18-19
Sentensi unganishi:
Paulo anadhihirisha hasira kuu ya Mungu dhidi ya wanaotenda dhambi.
Kwa kuwa ghadhabu yake
Paulo anaelezea kwa nini watu wanatakiwa kuisikia injili.
Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa
"Mungu amedhihirisha hasira yake"
Dhidi
"juu ya"
uasi wote na udhalimu wa watu
"uasi wote na mambo ya udhalimu ambayo watu wanayatenda"
kuuficha ukweli
"walificha taarifa za kweli kuhusu Mungu"
ambayo inajulikana kuhusu Mungu inaonekana kwao
"wanaweza kujua kuhusu Mungu kwa sababu ya wanayoyaona"
Kwa kuwa Mungu
Paulo anawaonyesha kwa nini watu wanajua mambo kuhusu Mungu.
Mungu amewaangazia
"Mungu ameyaonyesha hayo kwao"
Romans 1:20-21
Kwa kuwa
Paulo anaelezea namna ambavyo Mungu alijidhihirisha mwenyewe kwa wanabamu
Mambo yake yasiyoonekana yameonekana wazi
"mambo yasiyoonekana" ni mambo yasiyoonekana kwa macho. Yamekuwa "yameonekana wazi" kwa sababu watu wameelewa kuwa wako pale japokuwa hawawezi kuona kwa macho yao.
Ulimwengu
Hii inamaanisha mbingu na dunia, pamoja na vyote vilivyomo.
Asili ya Mungu
"Ubora na tabia za Mungu" au "mambo ya Mungu yanayomfanya awe Mungu"
Wanaelewe kupitia vitu vilivyoumbwa
"watu wanaweza kuelewa kuhusu Mungu kwa kuangalia vitu alivyovifanya"
Watu hawa hawatakuwa na udhuru
"Watu hawa hawatasema kuwa hawakujua"
Wakawa wajinga kwenye mawazo yao
"wakaanza kuwaza mambo ya kijinga"
Mioyo yao isiyo na hisia ilikuwa na giza
Maelezo haya yanaonyesha moyo uliokuwa na giza ikimaanisha wamekosa uelewa. "mioyo yao haiwezi tena kuelewa"
Romans 1:22-23
Wanadai kuwa na hekima, lakini wakawa wajinga.
"Walipokuwa wanadai kuwa wana hekima, wakawa wajinga"
Wao...wao
Watu
Wakabadilisha utukufu usioharibika
"wakauza ukweli kuwa Mungu ni mtukufu na hatakufa" au "wakaacha kuamini kuwa Mungu ni mtukufu na hatakufa"
kwa kufananisha na sura ya
"na badala yake walichagua kuabudu sanamu waliotengenezwa kufanana na"
mtu anayeharibika
"mtu ambaye atakufa"
Romans 1:24-25
Kwa hiyo
"kwa sababu hii"
Mungu aliwapa ili
"Mungu aliwaruhusu wajiingize" au Mungu aliruhusu"
Wao...yao...wenyewe...wale
"binadamu"
Tamaa za mioyo yao kwa uchafu
"Vitu vya maadili machafu walivyotamani kuwa navyo"
kwa miili yao kufedheheshwa kati yao wenyewe
Walifanya matendo ya mwili yasiyofaa na udhalilishaji.
badala ya
Inaweza kuwa na maana 1) "badala ya" au 2) "pamoja na"
Romans 1:26-27
Hii
"uzinzi na dhambi ya uasherati"
Mungu aliwapa ili
"Mungu aliruhusu wajiingize"
Tamaa ya kufedhehesha
"tamaa za aibu za kimwili"
Kwa kuwa wanawake wao
"kwa sababu wanawake wao"
Wanawake wao
wanawake wa "mwanadamu"
Wakageuza matumizi ya asili kinyume na asili
"Wakaanza kujamiiana kwa njia ambayo Mungu hakuitengeneza"
Wakaungua kwa tamaa zao
"wakapata tamaa kali za mwili"
Isivyofaa
"kudhalilisha" au "chafu" au "dhambi"
Waliopokea adhabu kwa sababu ya upotoshaji wao
"Waliopokea adhabu inayostahili toka kwa Mungu kwa sababu ya upotoshaji wao"
kupotosha
Tabia ambayo ni mbaya na isiyofaa.
Romans 1:28
Kwa sababu hawakuthibitisha kuwa na Mungu katika ufahamu wao
"Hawakufikiri kuwa kulikuwa na umuhimu wa kumjua Mungu"
Wao...yao...wale
Maneno haya yanamaanisha "binadamu"
Aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa
Mungu aliruhusu akili zao zijazwe na uasherati na uwatawale"
sio sahihi
"kudhalilisha" au "isiyo na heshima" au "dhambi"
Romans 1:29-31
Walijazwa na
"Ndani yao walikuwa wanatamani" au "walikuwa na matamanio makubwa ya kufanya matendo ya"
Romans 1:32
Wanaelewa taratibu za Mungu
Wanajua kuwa Mungu anataka waishi kwenye njia zake za haki.
kufanya mambo hayo
"kufanya matendo maovu"
Kustahili kifo
"wanastahili kufa"
Romans 2
Romans 2:1-2
Sentensi unganishi:
Paulo amesema kuwa wato wote ni wenye dhambi na anaendelea kuwakumbusha kuwa watu wote ni waovu.
Kwa hiyo umekosa sababu ya kujitetea
Neno "kwa hiyo" linaonyesha sehemu mpya ya barua. Inaonyesha suluhisho la sentensi ikionyesha yaliyosemwa "tangu Mungualipowaadhibu watu wanaoendelea kutenda dhambi, na hataonea huruma kwa sababu ya dhambi zao"
Wewe ni
Paulo haongei na mtu. Anajifanya kama Myahudi anayelumbana naye. Paulo anafanya haya kuwafundisha wasikilizaji wake kuwa Mungu atamhukumu kila mtu anayeendelea kutenda dhambi, awe Myahudi au wa Mataifa.
Wewe
Hapa neno "wewe" ni umoja.
Wewe mtu, wewe unayehukumu
Hapa neno "mtu" ilitumika kumdhihaki mtu aliyefikiri anaweza kufanya kama Mungu na kuwahukumu wengine. "Wewe ni binadamu tuu, lakini unawahukumu wengine na kusema kuwa wanastahili hukumu ya Mungu"
kwa unavyohukumu kwa wengine unahukumu kwako mwenyewe.
"Lakini unajihukumu mwenyewe kwa sababu unafanya mambo maovu kama wanavyofanya wengine"
Lakini twajua
Hii inajumuisha Wakristo walioamini na Wayahudi ambao sio Wakristo.
Hukumu ya Mungu ni kutokana na kweli ikiwaangukia wao
"Mungu atawahukumu watu kwa kweli na haki"
Wale wanaofanya mambo hayo
"watu wanaofanya mambo maovu"
Romans 2:3-4
Lakini
"kwa hiyo"
Fikiria hili.
"fikiria kuhusu hili ninalokwenda kukwambia"
Mtu
Tumia neno la jumla kwa binadamu.
Wewe unayewahukumu wanaofanya mambo hayo japokuwa na wewe unafanya vivyo hivyo.
"Wewe unayesema mtu anastahili adhabu ya Mungu wakati unafanya mambo maovu"
Je utaepuka hukumu ya Mungu?
"hautaepuka hukumu ya Mungu!"
Au unadharau utajiri wa wema wake, na hukumu yake iliyochelewa, na uvumilivu... tubu?
"Unajifanya kama hujali kwamba Mungu nimwema na ni mvumilivu akisubiria muda mrefu kabla ya kuwahukumu watu, kwa hiyo wema wake utasababisha watu watubu."
Unadharau utajiri wake... uvumilivu
"fikiria utajiri... uvumilivu sio muhimu" au "fikiria... sio vizuri"
HaUjui kuwa wema wake una maana ya kukusababisha utubu?
"Unatakiwa ufahamu kuwa Mungu anakuonyesha kuwa ni mwema hivyo utubu."
Romans 2:5-7
Sentensi unganishi:
Paulo anaendelea kuwakumbusha watu kwamba watu wote ni waovu.
Lakini ni kwa kadri ya ugumu wako na moyo wako usiotubu
Paulo anamfananisha mtu aliyekataa kusikia na kumtii Mungu na kitu kigumu, kama jiwe. Moyo unamaanisha mtu mzima. "Ni kwa sababu umekataa kusikiliza na kutubu"
Ugumu na moyo usiotubu
Mstari "moyo usiotubu" inaelezea neno "ugumu"
Unajiwekea mwenyewe akiba ya ghadhabu
Neno "kujiwekea" inamaanisha mtu aliyekusanya mali zake na kuziweka sehemu salama. Paulo anasema badala ya mali mtu anakusanya adhabu ya Mungu. Kadri unavyoendelea bila kutubu, ndivyo adhabu inavyozidi kuwa kubwa. "unaifanya adhabu yako inakuwa mbaya zaidi"
siku ya ghadhabu... siku ambayo Mungu atadhihirisha hukumu yake ya haki
Hii inamaanisha siku hiyo hiyo. "Ambayo Mungu atawaonyesha watu kuwa ana hasira na anahukumu watu wote kwa haki."
Kulipa
"Kutoa tuzo ya haki au adhabu"
kwa kila mtu kipimo sawa kwa matendo yake
"kutokana na kila mtu alivyofanya"
Wametafuta
Hii inamaanisha kwamba walienenda kwa njia ambazo ziliwapa matokeo hasi toka kwa Mungu siku ya hukumu.
Sifa, heshima na kutokuharibika.
Walitaka Mungu awasifu na kuwaheshimu, na walitaka wasife kabisa.
Kutoharibika
Hii inamaanisha, kimwili, sio ya maadili, kuoza.
Romans 2:8-9
Sentensi unganishi:
Japokuwa sehemu hii inazungumzia watu waovu wasio na dini, Paulo anajumuisha kuwa wote wasio Wayahudi na Wayahudi ni waovu mbele za Mungu.
Ubinafsi
Kujitafutia, "choyo" au "mtu anayejali kujipa furaha yeye mwenyewe"
Kutokutii ukweli lakini kutii wasio na haki
Mistari hii miwili ina maana sawa. Ya pili inaelezea ya kwanza.
Ghadhabu na hasira kali itakuja
yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza hasira ya Mungu. "Mungu ataonyesha hasira yake kuu"
Dhiki na shida juu ya
Maneno "dhiki" na "shida" yana maana sawa na hapa yansisitiza namna mbavyo adhabu ya Mungu itakavyokuwa mbaya. "Adhabu mbaya ya Mungu itatokea"
Kwa kila nafsi ya mwanadamu
Hapa Paulo ametumia neno "nafsi" kuonyesha kuwa anamaanisha mtu kwa ujumla. "kwa kila mtu"
Amefanya uovu
"ameendelea kufanya mambo maovu"
Kwa Wayahudi kwanza , na pia kwa Wayunani
"Mungu atawahukumu Wayahudi kwanza, na baada ya hapo atawahukumu ambao sio Wayahudi"
Kwanza
Inaweza kuwa na maana 1) "ya kwanza kwa utaratimu na wakati" au 2) "hakika" au "ya muhimu sana"
Romans 2:10-12
Lakini sifa, heshima na amani vitakuja.
"Lakini Mungu atatoa sifa, heshima na amani"
Tenda mema
"endeleeni kufanya yaliyo mema"
Kwa Wayahudi kwanza , na pia kwa Wagiriki
"Mungu atawapa tuzo Wayahudi kwanza, na baada ya hapo ambao sio Wayahudi"
Kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu
"Kwa kuwa Mungu hapendelei baadhi ya watu juu ya wengine" au "kwa kuwa Mungu anausawa kwa watu wote"
Kwa wingi wao kama walivyotenda dhambi
"Kwa wale walotenda dhambi"
Bila sheria pia wataangamia bila sheria
Paulo anarudia "bila sheria" ili kusisitiza kuwa haijalishi kama hawajui sheria ya Musa. Kama wakitenda dhambi Mungu atawahukumu. "Bila kujua sheria za Musa bado watakufa kiroho"
na wingi wao kama walivyotenda dhambi
"Na wote waliotenda dhambi"
Kwa kutii sheria watahukumiwa kwa sheria
"Na kujua sheria za Musa, Mungu atawahukumu kutokana na sheria ya Musa.
Romans 2:13-14
Sentensi unganishi:
Paulo anaendelea kuwafanya wasomaji wajue kwamba kutii sheria za Mungu inatakiwa hata kwa wale ambao hawana sheria za Mungu.
Kwa
Kama lugha yako ina njia nyingine aya kuelezea kuwa mstari wa 14 na 15 unaingilia mawazo makuu ya Paulo na kumpa msomaji taarifa za ziada. Unaweza ukaiweka 2:14-15 kabla ya 2:13 au baada ya 2:16. "kwa sababu"
Sio wasikilizaji wa sheria
"Sio tuu kwa wale wasikilizaji wa sheria ya Musa"
Walio na haki mbele za Mungu
"wale wanaompendeza Mungu"
lakini ni kwa watendaji wa sheria
"lakini ni kwa wale wanaoitii sheria ya Musa"
Kina nani watakuwa waadilifu.
"ambao Mungu atawapokea"
Walio na sheria kwao wenyewe
"Walio na sheria za Mungu ndani mwao"
Romans 2:15-16
Kwa hili walionyesha
"Kwa kutii sheria walionyesha"
Matendo yaliyotakiwa na sheria yaliyoandikwa kwenye mioyo yao
"Mungu ameandika kwenye mioyo yao mambo ambayo sheria inawataka wafanye" au "Walifahamu ni nini sheria iliwataka wao wafanye"
Yaliyotakiwa na sheria
"Sheria inataka" au "Ambayo Mungu ameamuru kupitia sheria"
kuwashuhudia wao, na mawazo yao wenyewe ama kuwashitaki au kuwalinda kwa ajili yao wenyewe
"waambie kama hawatii au wanatii amri za Mungu"
Siku ambayo Mungu atahukumu
Hii inaelezea mwisho wa mawazo ya Paulo "hii itatokea siku ambayo Mungu atahukumu"
Romans 2:17-20
Ikiwa wewe unajiita Myahudi
Hapa neno "kama" haimaanishi Paulo ana mashaka au hana uhakika. Anasisitiza kuwa sentensi hii ni ya kweli. "Sasa mnajiona wenyewe kama watu watu wa Kiyahudi."
Kutegemea torati, kujisifu kwa furaha katika Mungu
"na ninyi mnategemea sheria ya Musa na kujisifu kwa furaha kwa sababu ya Mungu"
Kujua mapenzi yake
"Na nyie kujua mapenzi ya Mungu"
kama mlivyoelekezwa na sheria
"kwa kuwa mmeelewa ni nini sheria ya Musa inafundisha"
Ikiwa una ujasiri... na ukweli
Kama lugha yako ina namna ya kutafsiri maelezo ya Paulo kwenye sura ya 2:19-20. unaweza kuweka 2:19-20 kabla ya 2:17.
Kwamba ninyi wenyewe ni viongozi wa vipofu, mwanga kwa walio gizani.
Sentensi hizi zina maana inayofanana. Paulo anafananisha Myahudi anayemfundisha mtu kuhusu sheria kumsaidia mtu ambaye haoni. "kwamba ninyi wenyewe ni kama viongozi kwa mtu aliye kipofu, na ni mwanga kwa mtu aliyepotea gizani"
Mkufunzi wa wajinga
"Unawarekebisha wale wanaofanya makosa"
Mwalimu wa watoto
Hapa Paulo anawafananisha wale wasiojua chochote kuhusu sheria kama watoto. "na uwafundishe wale wasiojua sheria"
na mlichonacho kwenye sheria maarifa na kweli
"kwa sababu mna hakika kuwa mnaelewa ukweli ulioandikwa kwenye sheria"
Romans 2:21-22
Wewe, pia, unayefundisha watu, haujifunzi mwenyewe?
Paulo alitumia swali kuwakemea wasikilizaji wake. "Lakini haujifunzi wenyewe wakati unawafundisha wengine!"
Wewe unayehubiri mtu asiibe, je unaiba?
Paulo alitumia swali kuwakemea wasikilizaji wake. "Unawaambia watu wasiibe, lakini wewe unaiba!"
Wewe unayehubiri mtu asizini, je unazini?
Paulo alitumia swali kuwakemea wasikilizaji wake. "Unawaambia watu wasizi, lakini wewe unazini!"
Nyie mnaochukia sanamu, je mnaiba mahekalu?
Paulo anatumia swali kuwakemea wasikilizaji wake. Mnasema mnachukia sanamu, lakini mnaiba mahekalu!"
Mnaiba mahekalu
Inaweza kuwa na maana 1) "kuiba vitu toka kwenye mahekalu ya wapagani kuviuza na kupata faida" au 2) "msipeleke kwenye hekalu la Yerusalemu pesa zote ambazo ni za Mungu" au 3) "kufanya mzaha kuhusu miungu."
Romans 2:23-24
Ninyi mnaojisifu kwa furaha kwenye sheria, je hamumtii Mungu kupitia uvunjaji wenu wa sheria?
Paulo anatumia swali kuwakemea wasikilizaji wake. "Ni uovu mnavyojifanya mnajivunia kwa sheria, wakati huo huo hamuitii na kuleta aibu kwa Mungu."
Jina la Mungu haliheshimiwi kati ya Mataifa
"Matendo yenu maovu yanaleta aibu kwa Mungu kwenye fikra za Mataifa"
Jina la Mungu
Neno "Jina" linamaanisha umilele wa Mungu, sio tuu jina lake.
Romans 2:25-27
Maelezo yanayounganisha:
Paulo anaendelea kuonyesha kwamba Mungu, kwa sheria zake, anawaadhibu hata Wayahudi ambao wana sheria za Mungu.
Kwa kuwa tohana imekupa faida wewe
"Nasema haya yote kwa sababu kutahiriwa kumekupa faida"
Kama ukiwa mkiukaji wa sheria
"Kama usipotii amri zilizopo katika sheria"
Kutahiriwa kwako kutakuwa kutokutahiriwa
Hii inamfananisha Myahudi asiyetii sheria na mtu ambaye ametahiriwa lakini anaonekana kama hajatahiriwa : anaweza kuwa Myahudi lakini akaishi kama mtu wa Mataifa. "Ni kama vile haujatahiriwa"
Mtu asiyetahiriwa
"Mtu ambaye hajatahiriwa"
Kuyashika maagizo ya sheria
"kutii kilichoamriwa kwenye sheria"
kutokutahiriwa kwake hakuwezi kuchukuliwa kama kutahiriwa? Na ambaye hajatahiriwa kwa asili hawezi kukuhukumu... sheria?
Paulo aliuliza maswali mawili kusisitiza kuwa kutahiriwa sio jambo la kumfanya mtu kuwa na haki mbele za Mungu. "Mungu atamchukulia kama mtu aliyetahiriwa.... na mtu ambaye hajatahiriwa ... atakuhukumu... sheria."
Romans 2:28-29
Kwa nje
Hii inamaanisha mambo ya nje ya Kiyahudi ambayo watu wanayaona.
Siyo ya nje tuu katika mwili
Hii inamaanisha mabadiliko ya nje katika mwili wa binadamu.
Ni Myahudi kwa ndani, na tohara ni ile ya moyoni
Mistari hii miwili ina maana inayofanana. Mstari unaosema, "Ni Myahudi kwa ndani," inaelezea kuwa, "tohara ni ile ya moyoni."
Ndani
Hii inaonyesha thamani na motisha ya mtu ambaye Mungu amembadilisha.
Kwa Roho, sio kwenye barua
"Barua" ni sehemu ndogo ya maandishi katika lugha. Hapa inamaanisha maandiko. "kupitia kazi ya roho mtakatifu, sio kwa sababu unajua maandiko."
Kwa Roho
Hii inaweza kuwa na maana ya ndani, sehemu yakiroho ya mtu, tofauti na nje "barua" ya sheria. Pia inamaana ya Roho Mtakatifu.
Romans 3
Romans 3:1-2
Sentensi unganishi:
Paulo anatangaza faida walionazo Wayahudi kwa sababu Mungu aliwapa sheria zake.
Kisha ni faida gani aliyonayo Myahudi? Na ni manufaa gani ya tohara?
"Kisha Wayahudi hawana kufaidika na ahadi ya Mungu, ingawa Mungu aliahidi wangeweza!"
Ni kubwa
"Kuna faida nyingi"
Kwanza kabisa
Hii ina maana kwamba ama 1) "Kwanza katika utaratibu wa wakati" au 2) "Amina" (UDB) au 3) "Muhimu zaidi."
Romans 3:3-4
Lakini itakuwaje iwapo baadhi ya Wayahudi hawakuwa waaminifu? Je, kutoamini kwao hufanya uaminifu wa Mungu ni batili?
Paulo anatumia maswali haya na kufanya watu kufikiri. Baadhi ya Wayahudi hawakuwa waaminifu kwa Mungu, hivyo baadhi ya kuhitimisha kwamba Mungu hakutaka kutimiza ahadi yake.
Haiwezekani kamwe kuwa
Msemo huu mzito kuhusu kwamba hii inaweza kutokea. Unaweza kuwa na maelezo kama hayo katika lugha yako kwamba unaweza kutumia hapa. AT 'Hiyo haiwezekani' au 'Hakika siyo.'
Badala
"Tunapaswa kusema hili badala"
Kama ilivyokua imeandikwa
"Maandiko ya Kiyahudi wenyewe kukubaliana na ninachosema"
Romans 3:5-6
Lakini ikiwa uovu wetu unaonyesha haki ya Mungu, tuseme nini?
Paul ni kuweka maneno haya katika kinywa cha mtu imaginary Wayahudi anazungumza. 'Kwa sababu uovu wetu unaonyesha kuwa Mungu ni mwenye haki, nina swali'
Mungu si mwema wakati anapotoa ghadhabu yake, ni nani?
"Je, Mungu, aletaye ghadhabu juu ya watu, wasio waadilifu?" au "Hatuwezi kusema kwamba Mungu, aletaye ghadhabu, si mwema." au "Ni lazima kusema kwamba Mungu, aletaye ghadhabu, ni mwema."
Naongea kwa mujibu wa mantiki ya kibinadamu
"Ninasema hapa nini watu kwa kawaida kusema"
jinsi gani Mungu atauhukumu ulimwengu?
Paulo anatumia swali hili kuonyesha kuwa hoja dhidi ya Injili ya Kikristo ni ujinga, tangu Wayahudi wote wanaamini kwamba Mungu anaweza na kuwahukumu watu wote. AT "Na sisi wote tunajua kwamba Mungu kwa kweli kuhukumu ulimwengu!"
Romans 3:7-8
Lakini ikiwa kweli ya Mungu ya uongo wangu hutoa sifa tele kwa ajili yake, kwa nini ningali bado kuhukumiwa kuwa mwenye dhambi!
Hapa Paulo anafikiria mtu kuendelea kukataa Injili ya Kikristo. adui kwamba anasema, kwa sababu dhambi yake inaonyesha haki ya Mungu, basi Mungu hapaswi kutangaza kwamba yeye ni mwenye dhambi juu ya siku ya hukumu kama, kwa mfano, anamwambia uongo.
kwanini si kusema ... kufika?
Hapa Paulo anazusha swali lake mwenyewe, ili kuonyesha jinsi ujinga ni hoja za adui yake imaginary adversary. "Mimi ili kama kusema ... kuja!"
kama sisi ni waongo huripotiwa kwa kusema
"Baadhi uongo kuwaambia wengine kwamba hiki ni nini tunasema"
hukumu juu yao ni
Itakuwa sawa tu wakati Mungu analaani maadui hawa wa Paulo, kwa kusema uongo kuhusu kile Paulo amekuwa akifundisha.
Romans 3:9-10
Kuunganisha maelezo
Paulo anajumuisha kwamba wote wana hatia ya dhambi, hakuna walio wema, na hakuna wa kumtafuta Mungu.
Nini basi? Je, sisi kuwatetea wenyewe?
Maana inawezekana ni 1) 'Sisi Wayahudi hawapaswi kujaribu kufikiria kwenda kuepuka hukumu ya Mungu, kwa sababu tu sisi ni Wayahudi!" (UDB) au 2) "Sisi Wakristo hatujaribu kuficha mambo maovu kwamba tunafanya!'
Hapana kabisa
Maneno haya ni yenye nguvu zaidi kuliko rahisi 'hapana,' lakini si lenye nguvu "hakika si!"
Romans 3:11-12
Hakuna mtu ambaye anaelewa
"Hakuna mtu kweli anatambua ukweli wa Mungu"
Hakuna mtu ambaye anamtafuta Mungu
'Hakuna mtu wa dhati anaejaribu kuwa na uhusiano mwema na Mungu'
akageuka mbali
Hapa hii ina maana kuacha kufanya kitu fulani. AT "kukataliwa Mungu na mapenzi ya haki yake kwa ajili yao"
kuwa haina maana
"zimeharibika mbali kama mapenzi ya Mungu kwa ajili yao ni wasiwasi"
Romans 3:13-14
Wao... wao
neno 'wao' hapa linahusu "Wayahudi na Wagiriki'"ya
Makoo yao ni kama kaburi wazi
Paulo anatumia neno picha maana kwamba kila kitu watu wasemacho ni watu wabaya na machukizo
Ndimi zao zimedanganya
"Watu kusema uongo"
Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu
"kamili" hapa ni kukua na neno "vinywa" hapa inawakilisha mawazo ya watu. AT 'Mengi ya yale watu wanasema ni hatari na maana ya kuumiza watu wengine.
Romans 3:15-18
Wao...wao... Watu hawa.... wao
Hii inahusisha Wayahudi na Wayunani
Miguu yao ina mbio kumwaga damu
"Wapo katika haraka ya kudhuru na kuua watu"
Uharibifu na mateso ni katika njia zao
'Kila mtu anaishi katika njia hiyo kwamba wao kwa makusudi kujaribu kuharibu wengine na kusababisha wao kuteseka'
Njia ya amani
"Njia" ni "barabara" au "njia" AT: "Jinsi ya kuishi kwa amani na wengine"
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao
"Kila mtu anakataa kumpa Mungu heshima anayostahili"
Romans 3:19-20
chochote Sheria inasema, anaongea na
'Kila kitu ambacho sheria inasema watu lazima kufanya ni kwa' au 'amri yote ambayo Musa aliandika katika sheria ni kwa ajili ya'
ili kwamba kila kinywa inaweza kuwa kimefungwa
'Hivyo kwamba hakuna mtu anauwezo wa kusema chochote halali kujitetea mwenyewe'
mwili
Hapa ina maana kwa njia ya mfano kumaanisha binadamu wote au viumbe hai wote.
kwa
Maana inawezakua ni 1) Kwa sababu hiyo" au 2) "Hii ni kwa sababu" au 3) "Badala."
kupitia sheria inakuja kutambua dhambi
"Wakati mtu anajua sheria ya Mungu, anatambua kwamba yeye si mwema bali mwenye dhambi mbele za Mungu"
Romans 3:21-22
Sentensi unganishi
neno "lakini" hapa linaonyesha Paulo amekamilisha utangulizi wake na sasa anaanza kufanya hatua yake kuu.
sasa
Neno 'sasa' linahusu wakati tangu Yesu alipokuja duniani.
pasipo sheria haki ya Mungu ilipatikana kujulikana
"Mungu amefanya kujulisha njia ya kuwa mwema bila kutii sheria"
Ilikuwa kushuhudiwa kwa sheria na manabii
Maneno "sheria na manabii" rejea sehemu ya andiko kwamba Musa na manabii waliandika na kusimama kwa maandiko ya Wayahudi, ambayo yameelezewa hapa kama watu ambao hutoa ushahidi mahakamani. AT "na yale ambayo Musa na manabii waliandika kuthibitisha hili."
yaani, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo
"Ninamaanisha kwa haki ambayo Mungu anatupa wakati tunaamini katika Yesu Kristo"
Kwa maana hakuna tofauti
"Kwa kuwa Mungu huwaona Wayahudi kwa njia hiyo hiyo huwaona Mataifa"
Romans 3:23-24
Wako huru kuthibitishwa kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu
"Mungu anawathibitisha kwa njia ya neema yake kwa sababu Kristo Yesu amewakomboa"
Romans 3:25-26
kupuuza
Maana inawezeakua ni 1) kupuuza au 2) kusamehe.
Haya yote yaliyotokea kwa maandamano ya haki yake wakati huu wa sasa. Hii ilikuwa ili aweze kuthibitisha mwenyewe tu, na kuonyesha kwamba yeye anahalalisha mtu yeyote kwa sababu ya imani yake kwa Yesu
'"Alifanya hiya ili kuonyesha haki yake wakati huu wa sasa. Alionyesha kwamba yeye ni mwenye haki na mtu ambaye inahalalisha kila mtu aliye na imani katika Yesu
Romans 3:27-28
Kwa misingi gani? ya matendo? Hapana, lakini kwa misingi ya imani
Majibu ya Paulo ya maswali kejeli kusisitiza kwamba kila hatua yeye anayopanga ni maamuzi ya kweli. AT: "Kwa misingi gani tunaweza kujivunia kutengwa? Je, tunatengwa kwa misingi ya matendo? Hakuna, badala, ni tunatengwa kwa misingi ya imani. "
Kwa msingi gani?
"Kwa sababu gani?"
Kwa matendo?
"Tunaweza kujivunia kutengwa kwa sababu sisi tunatii sheria?"
Kwa msingi wa imani
Kwa sababu tunaamini katika Yesu
bila
"mbali na"
Romans 3:29-30
Au ni Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu?
"Kama Mungu angeweza tu kuhalalisha watu ambao wanatii sheria, bila yeye kuwa ni Mungu wa Wayahudi tu?'
Romans 3:31
Sentensi unganishi
Paulo amehakikisha sheria kwa imani
Je, Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo?
"Je, sisi kupuuza sheria kwa sababu tuna imani?"
Hata kidogo
"Bila shaka hiyo si kweli!" au "Hakika si!" (UDB). Msemo huu kutoa nguvu iwezekanavyo jibu hasi kwa uliotangulia kejeli. Unaweza kutaka kuwa na kujieleza kama hiyo katika lugha yako kwamba unaweza kutumia hapa.
sisi kutekeleza sheria
"sisi kutii sheria"
Sisi
Kiwakilishi Hii inahusu Paulo, waumini wengine, na wasomaji.
Romans 4
Romans 4:1-3
Sentensi unganishi
Paul anathibitisha kwamba hata katika zamani waumini walikuwa haki kwa imani na si kwa sheria.
Tutapata nini basi kusema kwamba Abrahamu baba yetu kwa jinsi ya mwili, kupatikana?
Paulo anatumia swali kupata mawazo ya msomaji na kuanza kuzungumza juu ya kitu kipya. AT 'Hivi ndivyo Ibrahimu baba yetu kimwili kupatikana.
Kwa nini andiko husema
"Kwa maana tunaweza kusoma katika maandiko"
na ikahesabiwa kwake kuwa haki
"na Mungu alimtambua Abrahamu kuwa mtu mwenye haki"
Romans 4:4-5
Sasa kwa ajili yake ambaye anafanya kazi, malipo ni hayahesabiwi kuwa ni neema, bali kama vile zinadaiwa
Hii ni kuelezea hali ambapo mtu ambaye anafanya kazi anatarajia kuwa atalipwa kwa kazi. Mtu huyo hakubali malipo kama zawadi ya bure au "neema."
malipo
"Mshahara" au "kulipa" au "kile chuma kwa kufanya kazi"
kile zinadaiwa
"Nini mwajiri wake anadaiwa naye"
yule ambaye amehalalishwa
"Katika Mungu, ambaye amehalalisha"
imani yake inahesabiwa kuwa haki
"Mungu anaona imani ya mtu huyo kuwa ni haki" au "Mungu anaona kuwa mtu mwenye haki kwa sababu ya imani yake"
Romans 4:6-8
David pia anatoa baraka juu ya mtu ambaye Mungu amemhesabia haki bila matendo
"Vile vile, Daudi aliandika kuhusu jinsi Mungu huwambariki mtu ambaye Mungu humfanya kuwa haki bila matendo"
maovu ambao ni kusamehewa ... ambao dhambi zao zimefunikwa ... yule ambaye Bwana si kuhesabu dhambi
Dhana hiyo imeelezwa kwa njia tatu tofauti. AT "ambao uovu Bwana alivyowasamehe ... ambao dhambi Bwana amezifunika ... ambao dhambi Bwana hatazihesabu."
Romans 4:9-10
Kisha ni baraka hii alitamka tu juu ya wote waliotahiriwa, au pia juu ya wale wasiotahiriwa?
'Je, Mungu awabariki tu wale waliotahiriwa, au pia wale wale ambao si waliotahiriwa?'
tunasema
Paulo akihutubia waumini wote Wayahudi na wa Mataifa.
Imani ilihesabiwa kwa Abraham kwa haki
"Mungu alichukuliwa imani ya Ibrahimu kuwa ni haki"
Romans 4:11-12
muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa tayari mwendawazimu wakati yeye alikuwa katika kutotahiriwa
'Ishara inayoonekana kwamba Mungu kuchukuliwa kwake mwenye haki kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu kabla ya kutahiriwa'
Hii ina maana kwamba haki itakuwa imehesabiwa kwao
"Ili kwamba Mungu anaweza kufikiria kuwa haki"
Romans 4:13-15
kwamba ahadi ilitolewa kwa Ibrahimu na wazawa wake, ahadi hii kwamba wangekuwa warithi wa Dunia
Kwamba Mungu aliahidi Ibrahimu na kizazi chake kwamba wangeweza kurithi dunia
Badala yake, ilikuwa kupitia haki wa imani
Maneno "Mungu hutoa ahadi" wanaachwa nje ya msemo huu lakini wao wanaelewa. AT "lakini Mungu alimpa ahadi kwa imani ambayo yeye aliiona kuwa ni haki."
kama wote wafuatao sheria ndio warithi
'Ikiwa ni wale ambao wanatii sheria ambayo kwamba watarithi nchi'
imani ilifanywa tupu, na ahadi ilifutwa
"Imani haina thamani na ahadi ni maana'
lakini ambapo hakuna sheria, haiwezekani kuivunja
"Lakini ambapo hakuna sheria, hakuna kitu chochote cha kuasi" au "kwa sababu kuna kitu kwa watu huasi tu ambapo kuna sheria"
Romans 4:16-17
Kwa sababu hii hii hutokea kwa imani, hivyo kwamba inaweza kuwa kwa neema
Hapa ni sababu sisi kupokea ahadi tunapomwamini Mungu ni hivyo kwamba inaweza kuwa hadiya
Matokeo yake, ahadi ni hakika kwa wazao wote
'Ili wazao wote wa Abrahamu waweze hakika kupokea ahadi'
wale wanaojua sheria
Hii ina maana ya Wayahudi ambao hufuata sheria ya Musa.
wale ambao ni kutoka imani ya Abrahamu
Hii ina maana ya wale ambao wana imani kubwa kama Abrahamu kabla ya kutahiriwa.
baba yetu sisi sote
Hapa neno "sisi" linawahusu Paul na ni pamoja na waumini wote Wayahudi na wasio Wayahudi katika Kristo. Ibrahimu ni babu wa kimwili wa Wayahudi, lakini yeye ni baba wa kiroho wa wale walio na imani.
kama ilivyoandikwa
Ambapo imeandikwa zinaweza kufanywa wazi. "kama ilivyoandikwa katika maandiko"
Nimekufanya wewe
neno "wewe" ni umoja na inahusu Abraham
Abrahamu alikuwa katika uwepo wa yule anaemuamini, yaani, Mungu, ambaye huwapa wafu uzima
'Ibrahimu alikuwa katika uwepo wa Mungu ambaye kuaminiwa, ambaye huwapa uzima wale waliokufa'
Romans 4:18-19
Licha ya hali zote za nje
maana kamili ya 'hali za nje' zinaweza kufanywa wazi. AT 'Hata ingawa ilionekana vigumu kwa yeye na watoto wake.'
Basi akawa baba wa mataifa mengi
'Na matokeo ya imani ya Ibrahimu ilikuwa ni kwamba akawa baba wa mataifa mengi.'
kulingana na kile alikuwa amesema
'Kama Mungu akamwambia Ibrahimu'
Hivyo itakuwa kizazi chako
ahadi full Mungu alimpa Ibrahimu zinaweza kufanywa wazi AT 'Utakuwa na wazawa zaidi unaweza kuhesabu.'
Yeye hakuwa dhaifu katika imani
'Aliendelea kuwa imara katika imani yake'
Abrahamu alikubali kuwa mwili wake mwenyewe alikwisha kufa-akiwa na umri wa karibu miaka mia moja. Pia alikiri hali ya kufa ya tumbo la Sara
Hapa umri wa Ibrahimu zamani na kukosa uwezo wa Sara kuwa na watoto ni ikilinganishwa na kitu ambacho ni wafu. Hii inasisitiza kuwa ilionekana vigumu kwa wao kuwa na watoto. AT 'Abraham alitambua yeye alikuwa mzee sana na Sara mkewe hakuweza kuwa na watoto.'
Romans 4:20-22
hakusita katika kutoamini
"Hakuwa na mashaka." AT 'agizo juu ya kutenda kwa imani.'
alikuwa imara katika imani
"Akawa na nguvu katika imani yake"
Alikuwa akijua hakika
"'Ibrahimu alikuwa na uhakika kabisa"
yeye pia alikuwa na uwezo wa kukamilisha
"Mungu alikuwa na uwezo wa kufanya"
Kwa hiyo hii ilikuwa pia kuhesabiwa kwake kama haki
"Mungu kuhesabiwa imani ya Ibrahimu kuwa ni uadilifu" au "Mungu kuchukuliwa Ibrahimu haki kwa sababu Ibrahimu aliamini yeye"
Romans 4:23-25
Sasa ilikuwa ni
'Sasa' limetumika hapa kuungana kuwa Ibrahimu alifanya haki kwa imani kuwasilisha siku kuhesabiwa haki muumini kwa imani katika kifo cha Kristo na ufufuo.
tu kwa faida yake
kwa Ibrahimu tu'
kwamba ikahesabiwa kwake
'Kwamba Mungu kuhesabiwa haki kwake' au 'Mungu kuchukuliwa kwake mwenye haki'
kwa ajili yetu
Neno 'sisi' inahusu Paul na ni pamoja na waumini wote katika Kristo.
Hiyo ilikuwa imeandikwa pia kwa ajili yetu, waliowekewa kuhesabiwa, sisi ambao wanaamini
"Ilikuwa pia kwa faida yetu, kwa sababu Mungu alizingatia haki yetu pia kama tunaamini"
Yeye aliyemfufua
'Mungu aliyemfufua'
Hii ni moja ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu
'Hii ni yule ambaye Mungu kukabidhiwa kwa wale waliokuwa wanamuua'
na kufufuka ili tupate kuhesabiwa haki
'Na ambaye Mungu alimrudishia uhai hivyo sisi tutafanywa sahihi na Mungu"
Romans 5
Romans 5:1-2
Kuunganishi Sentensi
Paulo anaanza kusema mambo mengi tofauti yanayotokea pindi Mungu anawathibitisha wakristo
Tangu
"Kwa sababu"
sisi...vyetu
Yote yanayotokea kwa "sisi" na "vyetu" urejea kwa wakristo wote na inapaswa kuhusisha.
kupitia Bwana wetu Yesu Kristo
"kwa sababu ya Bwana wetu Yesu Kristo"
Bwana
Hapa "Bwana" ina maanisha kwamba Yesu ni Mungu
Kupitia yeye sisi pia tuna upenyo kwa imani kufikia neema ambayo tunasimama
Paulo analinganisha wakristo kupokea neema kwa mtu aliyesimama mbele ya mfalme. "Kwa sababu ni ndani ya Yesu tuna amini, Mungu utupa neema kusimama mbele ya Mungu."
Romans 5:3-5
Si hivi tu
Neno "hivi" urejea kwa mawazo yaliyoelezwa ndani
Sisi...vyetu...sisi
Yote yanayotokea kwa "sisi" "vyetu" na "sisi" urejea kwa wakristo wote na inapaswa kuhusishwa
kukubalika
Neno hili "kukubalika" urejea kwa usemi wa Mungu kwamba hii ni nzuri
ujasiri kwa wakati ujao
Hii ni hakika kwamba Mungu atatimiza ahadi zake zote kwa wale wanao mwamini Kristo.
Romans 5:6-7
sisi
Neno "sisi" hapa urejea kwa wakristo wote na inapaswa kuhusishwa.
Romans 5:8-9
thibitisha
"huonyesha"
sisi...sisi
Yote yanayotokea kwa "sisi" na "sisi" urejea kwa wakristo wote na inapaswa kuhusishwa.
Zaidi ya yote, basi, sasa tumethibitishwa kwa damu yake
"Je si zaidi yeye atafanya kwetu kwa ajili yetu sasa kwamba tumelithibitishwa kwa damu yake"
kuokolewa
Hapa inamaanisha kwamba kupitia kifo cha Yesu pale msalabani, Mungu amekwisha kumsaheme na kumuokoa kwa adhabu ya jehanamu kwa ajili ya dhambi zake.
Romans 5:10-11
sisi...sisi
Yote yatokeayo kwa "sisi" urejea kwa wakristo wote na inapaswa kuhusishwa.
Mwana wake...maisha yake
"Mwana wa Mungu...maisha ya mwana wa Mungu"
tulikuwa tumepatanishwa kwa Mungu kupitia kifo cha mwana wake
Kifo cha mwana wa Mungu kimetupa msamaha wa milele na kutufanya sisi marafiki pamoja na Mungu, kwa wote wanaoamini katika Yesu.
Mwana
Hili ni jina muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu
baada ya kuwa tumepatanishwa
"sasa basi Mungu hutuona sisi marafiki wake tena"
Romans 5:12-13
Sentensi unganishi:
Paulo aeleza kwa nini kifo kilitokea hata kabla ya sheria ya Mungu haijaandikwa.
kupitia mtu mmoja dhambi iliingia...kifo kiliingia kupitia dhambi
Paulo aelezea "dhambi" kama jambo hatari ambalo liliweza kuja katika ulimwengu kupitia uwazi ulio sababishwa na matendo ya "mtu mmoja" Adamu. Hii "dhambi" basi ilifanyika uwazi ambako "kifo", jambo jingine la hatari, pia lilikuja ulimwenguni.
Romans 5:14-15
Bila shaka
"Bado" au "Hapakuwa na kuandikwa kwa sheria kutokea wakati wa Adamu mpaka wakati wa Musa, lakini"
kifo kilitawala kutokea Adamu mpaka Musa
Paulo analinganisha kifo na mfalme. "watu waliendelea kufa kutokea wakati wa Adamu mpaka wakati wa Musa kama matokeo ya dhambi zao."
hata kwa wale hawakutenda dhambi kama kutotii kwa Adamu
"hata watu ambao dhambi zao zilikuwa tofauti na za Adamu waliendelea kufa"
yeye ni mfano wa yeye aliyepaswa kuja
Adamu alikuwa mfano wa Kristo, ambaye alijitokeza badae. Alikuwa na vitu vya kufanana naye.
Kwa kuwa kama...wengi walikufa...zaidi sana neema ya Mungu na zawadi...kuongezeka
Ni muhimu kwamba "wengi walikufa," lakini ni ya umuhimu zaidi kwamba "neema ya Mungu na zawadi" ziliongezeka
zaidi ilivyofanya neema...na zawadi...kuongezeka
"Neema... na zawadi" zilikuwa kubwa na imara kuliko makosa
Romans 5:16-17
Kwa kuwa zawadi si tokeo la yule aliyefanya dhambi
"zawadi si tokeo la dhambi ya Adamu"
kwa upande mmoja
"Kwa sababu ya upande mmoja"
kwa upande mmoja, hukumu ya kukataliwa ilikuja kwa sababu ya kosa la mtu mmoja. Lakini kwa upande mwingine
Kikundi cha maneno "kwa upande mmoja" na 'lakini kwa upande mwingine" utanguliza njia mbili tofauti za kufikiri kuhusu kitu fulani. "hukumu ya kukataliwa ilikuja kwa sababu ya makosa ya mtu mmoja, lakini"
baada ya makosa mengi
"baada ya dhambi za wengi"
Kosa la mmoja
Kosa la Adamu
kifo kilitawala
"kila mmoja alikufa"
maisha ya yule mmoja
maisha ya Yesu Kristo
Romans 5:18-19
kupitia kosa moja
"kupitia dhambi moja iliyofanywa na Adamu" au kwa sababu ya dhambi ya Adamu"
tendo moja
dhabihu ya Yesu Kristo
kutotii kwa mtu mmoja
kutotii kwa Adamu
utiifu wa mtu mmoja
utiifu wa Yesu
Romans 5:20-21
sheria ilikuja na
"Sheria ilikuja kwa siri"
kosa liweze kuongezeka
Hii ina maanisha vyote kwamba "watu wapate kuelewa kwa kiasi gani wamefanya dhambi" na "watu wapate kufanya dhambi zaidi."
kuongezeka
"kuongezeka"
kama dhambi utawala katika kifo
"kama dhambi ilivyosababisha kifo"
hata neema iweze kutawala kupitia haki kwa maisha ya milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu
"neema iliwapa watu maisha ya milele kupitia haki ya Yesu Kristo Bwana wetu"
Bwana wetu
Paulo anawajumuisha wasomaji wake na wakristo wote.
Romans 6
Romans 6:1-3
Sentensi unganishi:
Chini ya neema, Paulo anawambia wale wanaomwaminiu Yesu kuishi maisha mapya kama wafu katika dhambi na hai kwa Mungu.
Tutasema nini? Tuendelee katika dhamb ili kwamba neema iwe tele?
Paulo anategemea swali mtu mwingine atauliza kuhusiana na kile alichokiandika kuhusiana na neema
sisi...sisi
Kiwakilishi nomino "sisi" urejea kwa Paulo, wasomaji wake, na watu wengine.
tele
"kuongezeka sana"
Romans 6:4-5
Tulikuwa tumezikwa, basi, pamoja naye kupitia ubatizo katika kifo
Hii inalinganisha ubatizo wa mkristo katika maji pamoja na kifo cha Yesu na kuzikwa katika kaburi. Hii inasisitiza kwamba mkristo katika Kristo anagawana faida katika kifo chake, ikimaanisha dhambi haina nguvu tena juu ya mkristo.
kama vile Kristo alikuwa ameinuliwa toka mauti kupitia utukufu wa Baba, ili kwamba tuweze kutembea katika upya wa maisha.
Hii umlinganisha mkristo anakuja kwa maisha ya kiroho kwa Yesu na kurudi katika maisha ya kimwili. Maisha mapya ya kiroho humwezesha mtu kumtii Mungu. Tofasiri mbandala, "kama vile Baba alivyomleta Yesu katika uhai baada ya kufa, tuwe na maisha ya kiroho mapya na kumtii Mungu"
kuunganika pamoja naye katika kufanana kwa kifo chake...muunganike katika ufufuo wake.
"muungane pamoja naye katika kifo chake...muungane pamoja naye katika uhai baada ya kifo." "kufa pamoja naye...kurejee kwa uhai pamoja naye."
Romans 6:6-7
utu wa zamani ulisulubishwa pamoja naye
Hapa, Paulo arejea kwa mkristo kama mtu mmoja kabla hawajamwamini Yesu na mtu tofauti baada ya kumwamini Yesu. "Utu wa zamani" urejea kwa mtu kabla hajamwamini Yesu. Mtu huu ni mfu kiroho na dhambi umtawala. Paulo aelezea utu wetu wa zamani wa dhambi kama kufa pale msalabani pamoja na Yesu pindi tunapo mwamini Yesu. "utu wetu wa dhambi ulikuwa pale msalabani pamoja na Yesu."
utu wa zamani
Hii ina maanisha hapo awali mtu alikuwa lakina kwa sasa si hivyo. "mtu wa nyuma".
mwili wa dhambi
mwanadamu kamili wa dhambi
ili kuharibiwa
"ili afe"
hatutakuwa tena watumwa wa dhambi
Paulo analinganisha nguvu ya dhambi kuwa juu ya mtu kumiliki uongozi wa mtumwa: mtu asiye na Roho Mtakatifu mara nyingi huchagua kile kiovu. Hayuko huru kufanya yale yanayompendeza Mungu. "tusiwe watumwa tena wa dhambi" au "tusichague kufanya kile kilicho dhambi."
Yeye aliyekwisha kufa ametangazwa kuwa ana haki kulingana na dhambi
"Mungu atamtangaza haki yeyote yule aliyekufa kwa nguvu ya dhambi"
Romans 6:8-9
tumekwish kufa pamoja na Kristo
Ijapokuwa Kristo alikufa kimwili, hapa "kufa" urejea kwa wakristo kufa kiroho kwa nguvu ya dhambi. "tumekufa kiroho pamoja na Kristo."
Tunajua ya kuwa Kristo amekwisha inuliwa toka mauti
"Mungu alimleta Kristo katika uhai baada ya kufa"
Kifo hakimtawali tena
Hapa "kifo" kimeelezwa kama mfalme au kiongozi ambaye ana nguvu juu ya watu. "Hawezi kufa tena."
Romans 6:10-11
Kwa kuzingati kifo kwamba alikufa kwa dhambi, alikufa mara moja kwa yote.
Kifungu cha maneno "mara moja kwa yote" ina maanisha kumaliza kitu kabisa. Maana nzima ya hii inaweza kufanywa wazi. "Kwa maana alipokufa aliivunja nguvu ya dhambi kabisa.
Kwa njia hiyo, ninyi pia mnapaswa kufikiri
"Kwa sababu hii fikirini"
jihesabuni wenyewe
"fikirini wenyewe kama" au "kujiona wenywe kama"
kufa kwa dhambi
Hapa "dhambi" urejea kwa nguvu inayoishi ndani yetu na kutufanya sisi kutenda dhambi. "kufa kwa nguvu ya dhambi"
kufa kwa dhambi kwa upande mmoja, lakini kwa upande mwingine, kuwa hai kwa Mungu
Kikundi cha maneno "kwa upande mmoja" na "kwa upande mwingine" utanguliza njia mbili tofauti za kufikiri kuhusiana na kitu. "kufa kwa kifo lakini pia kuwa hai kwa Mungu."
kuwa hai kwa Mungu katika Kristo Yesu
"kuishi kwa kumtii Mungu kwa nguvu ya Kristo Yesu anayokupa"
Romans 6:12-14
Sentensi unganishi:
Paulo anatukumbusha sisi kwamba neema uongoza juu yetu, wala si sheria, sisi si watumwa wa dhambi, lakini watumwa wa Mungu.
msiache dhambi iwaongoze... Msiruhusu dhambi kuwaongoza
"Dhambi" inaelezwa kama mfalme wa mtu au bwana.
mwili wako wa kufa
Kikundi hiki cha maneno urejea kwa sehemu ya mwili wa mtu, ambayo utakufa. "wewe"
ili kusudi kwamba muweze kutii tamaa zake
Bwana. "dhambi" huitaji mwenye dhambi kutii amri za bwana kwa kufanya maovu.
Msitoe sehemu ya mwili wenu kwa dhambi kama vyombo vya udhalimu.
Hii picha ni ya mwenye dhambi anayetoa sehemu ya mwili wake kwa bwana wake au mfalme. "Msijitoe ninyi kwa dhambi ili kwamba msitende yasio faa."
lakini jitoeni kwa Mungu, kama walio hai kutoka kwenye mauti
"lakini jitoeeni ninyi kwa Mungu, kwa sababu amekwisha kuwapa ninyi maisha mapya ya kiroho"
sehemu ya miili yenu kama vyombo vya haki kwa Mungu
"acha Mungu akutumie kwa kile kimfurahisha cho yeye"
Msiruhusu dhambi kuwaongoza ninyi
"Msiache tamaa za dhambi kukuongoza kwa kile unachofanya" au "Usiruhusu wewe mwenyewe kufanya maovu unayotaka kufanya"
Kwa kuwa hamko chini ya sheria
Maana kamili inaweza kufanywa wazi. "kwa kuwa hamjafungamana na Sheria ya Musa, ambayo isingeweza kuwapa nguvu ya kuacha kufanya dhambi."
lakini chini ya neema
Maana kamili inaweza kufanywa wazi. "lakini mmefungamana na neema ya Mungu, ambayo inawapa nguvu ya kuacha kufanya dhambi."
Romans 6:15-16
Basi sasa? Tufanye dhambi kwa sababu hatuko chini ya sheria, lakini chini ya neema? La hasha
Paulo anatumia swali kusisitiza kwamba kuishi chini ya neema siyo sababu ya kutenda dhambi. "Hata hivyo, kwa sababu tumefungamana na neema badala ya Sheria ya Musa hakika haimaanishi tunarusiwa kufanya dhambi."
La hasha
"Hatutapenda kuona hicho kufanyika!" au "Mungu na anisaidie nisifanye hivyo!" Usemi huu uonyesha hamu mno ya nguvu kwamba hii haifanyiki. Unaweza kuhitaji kuwa na usemi kama huo katika lugha yako kwamba ungetumia hapa.
Hamjui kuwa kwake yeye mnaojitoa kama watumwa kwamba ni kwa yeye mnakuwa watumwa, ni yeye mnapaswa kumtii.
Paulo anatumia swali kumkaripia yeyote atakaye fikiri neema ya Mungu ni sababu ya kuendelea kutenda dhambi. "Mnapaswa kujua kwamba nyie ni watumwa kwa bwana mliyemchagua kumtii."
Hii ni kweli hata kama ni watumwa kwa dhambi ambayo hupelekea mauti, au watumwa wa utiifu ambayo hupelekea haki
Hapa "dhambi" na "utiifu' yameelezwa kama mabwana ambapo mtumwa atatumikia. Hii inaweza kutofasiriwa kama sentensi mpya. "Nyie sio watumwa wa dhambi, ambayo huleteleza kifo cha kiroho, au watumwa wa utiifu, ambayo husababisha Mungu awatangaze wanyofu.
Romans 6:17-18
Lakini ashukuriwe Mungu!
"Lakini namshukuru Mungu!"
Kwa kuwa mlikuwa watumwa wa dhambi
Hapa "dhambi" imeelezwa kama bwana ambapo mtumwa ataitumikia. Pia, "dhambi" urejea kwa nguvu inayoishi ndani yetu ambayo hutafanya sisi kuchagua kufanya kile kiovu. "Kwa kuwa mlikuwa watumwa wa nguvu ya dhambi."
lakini mmekwisha kutii toka moyoni
Hapa neno "moyo" urejea kuwa na hisia za kweli kwa kufanya kitu. "lakini hakika mlitii".
sampuli ya mafundisho yale mlipewa
Hapa "sampuli' urejea kwa njia ya kuishi ambayo hupelekea kwa unyoofu. Wakristo hubadilisha njia zao za kuishi za zamani kufanana na njia hii mpya ya kuishi ambayo viongozi wakristo huwafundisha. "mafundisho ambayo viongozi wa kikristo waliwapa ninyi."
Mme kwisha fanywa huru toka dhambi
"Kristo amewaweka huru toka kwenye nguvu ya dhambi"
watumishi wa unyoofu
"kwa sasa umtumishi wa kufanya kilicho sahihi"
Romans 6:19-21
Naongea kama mwanadamu
Paulo anaeleza "dhambi" na "utiifu" kama "utumwa". "Ninazungumza kuhusu utumwa kuelezea dhambi na utiifu."
kwa sababu ya udhaifu wa mwili wako
Mara nyingi Paulo utumia neno "mwili" kama kinyume cha "roho". "kwa sababu hamuelewi kwa kina mambo ya kiroho."
ilitolewa sehemu ya mwili wenu kama watumwa kwa uchafu na uovu
Hapa, "sehemu ya mwili" urejea kwa mtu kamili. "kujitoa kwenu kama watumwa kwa kila kiovu na kuto mpendeza Mungu"
toeni sehemu ya mwili wenu kama watumwa wa haki kwa ajili ya utakaso
"jitoeni kama watumwa kwa kile kilicho sahihi mbele zake Mungu ili kwamba awatenge na awape nguvu kumtumkia yeye"
Kwa wakati huo, ni tunda lipi ulipata kwa mambo ambayo sasa unayaonea aibu?
Paulo anatumia swali kusisitiza kwamba kutenda dhambi hakuleti kitu chochote kizuri. "Hakupata chochote kwa kufanya mambo hayo ambayo kwa sasa yanatia aibu."
Romans 6:22-23
Lakini kwa sasa umekwisha fanywa huru toka dhambi na kufanywa watumwa kwa Mungu
"Lakini sasa Kristo amekwisha waweka huru toka kwenye dhambi na amewafungamana na Mungu"
Tokeo ni uzima wa milele
"na tokeo la haya yote ni kwamba mtaishi milele pamoja na Mungu"
Kwa mshahara wa dhambi ni kifo
"Neno "mshahara" urejea kwa malipo yatolewayo kwa yeyote kwa ajili ya kazi zao. "Basi kama unatumikia dhambi, utapokea kifo cha kiroho kama malipo" au "kwa kuwa kama unaendelea kutenda dhambi, Mungu atakuhukumu na kifo cha kiroho."
lakini zawadi huru ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
'lakini Mungu kwa uhuru hutoa uzima wa milele kwa wale walio wa Kristo Yesu Bwana wetu"
Romans 7
Romans 7:1
Taarifa unganishi:
Paulo anaelezea jinsi sheria inavyowatawala wale wote wanaotaka kuishi chini ya sheria.
sheria humtawala mtu muda wote anaoishi
Paulo anatoa mfano wa hili
Romans 7:2-3
anaitwa mzinzi
Yule ambaye "ameita" hayupo wazi, hivyo sema kwa ujumla kadiri iwezekanavyo. Mf. "Mungu atamhesabu yeye kuwa mzinzi" au "watu watamuita yeye mzinzi."
Romans 7:4-5
Kwa hiyo
Hii inarejea maneno haya "Kwa sababu ya jinsi sheria hufanya kazi"
tuweze kuzaa matunda kwa ajili ya Mungu
"tuweze kufanya mambo yanayompendeza Mungu"
kuzaa matunda
Hapa inamaanisha kubadilika hali ya ndani ya kiroho.
Romans 7:6
Taarifa unganishi:
Paulo anatukumbusha kwamba Mungu hatufanyi sisi kuwa watakatifu kwa njia ya sheria.
sisi
kiwakilishi hiki cha jina humaanisha Paulo na wale walioamini.
barua
"sheria ya Musa"
Romans 7:7-8
Tutasema nini basi?
Paulo anatambulisha mada mpya.
Isiwe hivyo kamwe
"Ndiyo hiyo si kweli!" Msemo huu unatoa kwa nguvu jibu hasi kwa swali la mtego lililotangulia. Unaweza kuwa na msemo unaofanana na huu katika lugha yako ambao unaweza kuutumia hapa.
Mimi nisingeijua dhambi kamwe, isingelikuwa ni kwa njia ya sheria...Lakini dhambi ilichukua nafasi...ikaleta kila aina ya tamaa
Paulo anaifananisha dhambi sawa na mtu ambaye anaweza kutenda.
dhambi ilichukua nafasi kupitia amri na kuleta kila aina ya tamaa ndani yangu
Wakati sheria ya Mungu inatuambi tusifanye jambo, ni kwa sababu tumeambiwa tusifanye ndio maana tunataka tufanye zaidi. "dhambi ilinikumbusha amri kutokutamani vitu viovu, na hivyo nilitamani vitu hivyo viovu zaidi kuliko mwanzo" au "kwa sababu nilitaka kutenda dhambi, wakati niliposikia ile amri ya kutotamani vitu viovu, nilivitamani"
dhambi
"hamu yangu ya kufanya dhambi"
tamaa
Neno hili linajumuisha kwa pamoja hamu ya kumiliki vitu vya wengine na tamaa mbaya ya zinaa.
pasipo sheria, dhambi imekufa
"kama kusingelikuwa na sheria, kusingelikuwa na uvunjifu wa sheria, hivyo kusingelikuwa na dhambi"
Romans 7:9-10
dhambi iliutawala uhai
Hii inaweza kumaanisha 1) " Nilitambua kuwa nilikuwa natenda dhambi" (UDB) 2) "Nilitamani sana kutenda dhambi."
Ile amri ambayo ingelileta uzima iligeuka kuwa mauti kwangu.
Paulo hakufa kabisa kimwili. "Mungu alinipa mimi amri ili nipate kuishi, lakini badala yake iliniua mimi."
Romans 7:11-12
Kwa maana dhambi ilichukua nafasi kwa ile amri na kunidanganya mimi. Kupitia ile amri, iliniua mimi.
Paulo anaielezea dhambi kama mtu anayeweza kufanya mambo 3: kuchukua nafasi, kudanganya, na kuua.
dhambi
"hamu yangu ya kutenda dhambi"
kuchukua nafasi kupitia amri
tazama ulivyotafasiri hapo awali
Romans 7:13-14
Taarifa unganishi:
Paul anazungumzia kuhusu vita iliyopo katika utu wake wa ndani kati ya dhambi katika utu wake wa ndani na sheria ya Mungu - kati ya dhambi na wema.
Hivyo
Paulo anatambulisha mada mpya.
kilicho kizuri
Hii inamaanisha sheria ya Mungu.
fanyika kifo kwangu
"ilisababisha mimi nife"
Isiwe hivyo kamwe
"Kwa hakika hiyo si kweli!" Msemo huu unatoa jibu hasi kwa nguvu kufuatia swali la mtego la awali. Unaweza kuwa na msemo unaofanana na huu katika lugha ambao unaweza kuutumia.
dhambi...ilileta mauti ndani yangu
Paulo anaiona dhambi kana kwamba ni mtu anayeweza kutenda.
ilileta mauti ndani yangu
"ilinitenga mimi na Mungu"
kwa njia ya amri
"kwasababu mimi sikuitii amri"
Romans 7:15-16
Taarifa unganishi:
Paulo anaongea kuhusu vita iliyopo kwenye utu wake wa ndani kati ya mwili wake na sheria ya Mungu - kati ya dhambi na wema.
Kwa maana nilifanyalo, kwa hakika silielewai
"Mimi sina uhakika kwanini nafanya mambo niyafanyayo"
Kwa
"Mimi sielewi kwanini nafanya niyafanyayo kwa sababu"
nisilolipenda, natenda
"Mambo ambayo najua si mema ndiyo niyafanyayo"
Lakini
"Hata hivyo"
Mimi nakubaliana na sheria
"Mimi najua kuwa sheria ya Mungu ni njema"
Romans 7:17-18
dhambi iishiyo ndani yangu
Paulo anaielezea dhambi kama kiumbe hai kilicho na nguvu ya kumhimiza yeye
mwili wangu
"asili ya ubinadamu wangu"
Romans 7:19-21
njema
"matendo mema" au "utendaji mwema"
uovu
"matendo maovu"
Romans 7:22-23
utu wa ndani
Sehemu ya mtu inayobaki baada ya mtu kufa
Lakini naona kanuni ya tofauti ndani ya viungo vya mwili wangu. Inapigana dhidi ya kanuni mpya kwenye akili yangu. Inanichukua mimi mateka
"Mimi naweza tu kufanya kile ambacho utu wangu wa kale unachoniambia kufanya, sio kuishi kwa njia mpya ambayo Roho ananionesha mimi"
kanuni mpya
Hii ni asili mpya ya kiroho iliyo hai.
kanuni ya tofauti katika viungo vya mwili wangu
Hii ni asili ya kale, jinsi watu walivyo wanapozaliwa.
kanuni ya dhambi iliyo ndani ya viungo vya mwili wangu
"asili yangu ya dhambi"
Romans 7:24-25
Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
"Nataka mtu mmoja aniweke mimi huru from utawala wa kile ambacho mwili wangu hutamani" (UDB).
shukrani na ziwe kwa Mungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu
Hili ni jibu la swali katika 7:24
Hivyo basi, kwa upande mwingine mimi mwenyewe natumikia sheria ya Mungu kwa akili zangu. Hata hivyo, kwa upande mwingine, kwa mwili mimi natumikia kanuni ya dhambi
Akili na mwili vimetumika hapa kuonesha jinsi vinavyoshabihiana aidha kwa kutumikia sheria ya Mungu au kanuni ya dhambi. Kwa akili na ufahamu mtu anaweza kuchagua kumpendeza na kumtii Mungu na kwa mwili au asili ya mwili kuitumikia dhambi. "Akili yangu inachagua kumpendeza Mungu, lakini mwili wangu huchagua kuitii dhambi."
Romans 8
Romans 8:1-2
Sentensi unganishi:
Paulo anatoa majibu kwa mapambano aliyonayo dhidi ya dhambi na wema.
kwahiyo
"kwa sababu hii" au "kwasababu ambacho nimekwisha kuwaambieni ninyi ni kweli"
kanuni...kanuni
Neno "kanuni" hapa linaelezea jinsi mambo yanavyofanya kazi kwa asili. Hii haina uhusiano wowote na taratibu zilizowekwa na watu.
Romans 8:3-5
Kwa maana kile ambacho sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili, Mungu alifanya
Hapa sheria inaelezwa kama mtu ambayo hakuweza kuvunja nguvu ya dhambi. "Maana sheria haikuwa na nguvu ya kutuzuia sisi kutenda dhambi, kwasababu dhambi iliyokuwa ndani yetu ilikuwa na nguvu sana. Lakini Mungu aliweza kutuzuia sisi kutenda dhambi."
katika mwili
"Kwasababu ya asili ya dhambi ya watu"
Yeye...alimtuma Mwana wake pekee kwa mfano wa mwili wa dhambi...sadaka ya dhambi...aliihukumu dhambi
Mwana wa Mungu aliiridhisha hasira takatifu ya Mungu dhidi ya dhambi kwa kuutoa mwili wake na uhai wa kibinadamu kama sadaka ya kudumu ya dhambi.
Mwana
Hili ni jina la muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
kwa mfano wa mwili wa dhambi
"aliyeonekana kama mwanadamu mwenye dhambi mwingine yeyote"
kuwa sadaka ya dhambi
"ili kwamba afe kama sadaka kwajili ya dhambi zetu"
na alihukumu dhambi katika mwili
"na Mungu alivunja nguvu ya dhambi kupitia mwili wa Mwana wake"
mahitaji ya sheria yaweze kutimizwa kwetu
"tuweze kutimiza mahitaji ya sheria"
sisi ambao tusioenenda kwa jinsi ya mwili
"sisi ambao hatuzitii tamaa zetu za dhambi"
bali kulingana na yule Roho
"lakini wale ambao wanamtii Roho Mtakatifu"
Romans 8:6-8
Sentensi unganishi:
Paulo anaendelea kulinganisha miili yetu sisi kama waumini na Roho tuliye naye.
nia ya mwili...ile nia ya Roho
"jinsi ambavyo wenye dhambi hufikiri...jinsi ambavyo wale wanaomsikiliza Roho Mtakatifu hufikiri"
kifo
Hapa hii inamaanisha kutengwa kwa mtu na Mungu
Romans 8:9-10
katika mwili...katika Roho
Angalia maneno haya yalivyotafsiriwa hapo awali.
Roho...Roho wa Mungu...Roho wa Kristo
Haya yote yanamuelezea Roho Mtakatifu
kama ni kweli kwamba
Maneno haya hayamaanishi kwamba Paulo ana mashaka kwamba baadhi ya watu hawana Roho wa Mungu. Paulo anataka wote watambue kwamba wanaye Roho wa Mungu.
Kama Kristo yumo ndani yenu
Jinsi Kristo anavyoishi ndani ya mtu inaweza kuwekwa wazi. "Kama Kristo anaishi ndani yako kupitia Roho Mtakatifu"
kwa upande mwingine, mwili umekufa kwa mambo ya dhambi, lakini kwa upande mwingine
Kipande cha sentensi "kwa upande mwingine" na "lakini kwa upande mwingine" huonesha njia mbili za namna ya kufikiri kuhusu jambo fulani. "mwili umekufa katika mambo ya dhambi, lakini"
mwili umekufa kwa mambo ya dhambi
Uwezekano wa maana hizi mwili 1) mtu amekufa kiroho katika nguvu ya dhambi au 2) bado mwili wa nyama utakufa kwasababu ya dhambi.
roho ipo hai kwa mambo ya haki
maana yake yaweza kuwa 1) mtu yupo hai kiroho, Mungu amempa nguvu kufanya yaliyo sahihi au 2) Mungu atamrejesha mtu uzimani baada ya kufa kwasababu Mungu ni mwenye haki na huwapa walioamini uzima wa milele.
Romans 8:11
kama roho...anaishi ndani yenu
Paulo anaamini kuwa Roho Mtakatifu anaishi ndani ya wasomaji wake. "Kwa kuwa Roho...anaishi ndani yenu"
ya yule aliyemfufua
"ya Mungu, aliyemfufua"
fufuliwa
Hapa hii imaanisha kumfanya mtu alikufa kuwa hai tena.
mwili wa kibinadamu
"mwili wa nyama" au "miili, ambayo siku moja itakufa"
Romans 8:12-13
Hivyo basi
"Kwasababu yale niliyokwisha kuwaambia ni kweli"
ndugu
"waumini wenzangu"
sisi tu wadeni
Paulo analinganisha utii kama kulipa deni. "tunahitaji kutii"
lakini sio kwa mwili kuishi kulingana na mwili
"lakini sisi si wadeni wa mwili, na sisi hatupaswi kuzitii tamaa zetu za dhambi"
Kwa maana mkiishi kwa jinsi ya mwili
"Kwasababu mkiishi tu kwa kupendeza tamaa zenu za dhambi"
mko karibu kufa
"hakika mtatengwa na Mungu"
lakini ikiwa kwa Roho mnayafisha matendo ya mwili
"Lakini ikiwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu mnaacha kuzitii tamaa zenu za dhambi"
Romans 8:14-15
Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu
"Kwa watu wote ambao Roho wa Mungu anawaongoza"
wana wa Mungu
Hapa hii inamaanisha walioamini wote katika Yesu na mara nyingi hutafsiriwa kama "watoto wa Mungu."
Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa tena hata muogope
"Kwa kuwa Mungu hakuwapa ninyi roho inayowanya ninyi kuwa watumwa tena wa nguvu ya dhambi na hofu ya hukumu ya Mungu"
ambayo kwayo tunalia
"inayotufanya sisi tulie"
Abba, Baba
"Abba" ni "Baba" kwa lugha ya Kiaramaiki.
Romans 8:16-17
warithi wa Mungu kwa upande mmoja. Na warithi pamoja na Kristo kwa upande mwingine
Vipande vya sentensi "kwa upande mmoja" na "kwa upande mwingine" hutambulisha njia mbili tofauti za kufikiri kuhusu jambo fulani. "warithi wa Mungu na pia warithi pamoja na Kristo"
kwamba pia tuweze kupewa utukufu pamoja naye
"kwamba atatutukuza sisi pamoja naye"
Romans 8:18-19
Sentensi unganishi:
Paulo anatukumbusha kuwa miili yetu itabadilishwa katika ukombozi wa miili
Kwa
Hii inasisitiza "Mimi nafikiri." Haimaanishi "kwasababu"
Mimi nafikiri kwamba...haistahili kulinganishwa na
"Mimi sifikiri kwamba...yanastahili kulinganishwa na"
itafunuliwa
"Mungu atayafunua" au "Mungu atafanya yajulikane"
viumbe vinatazamia kwa shauku
Kila kitu ambacho Mungu ameumba kimeelezwa kama mtu anayengoja kitu kwa shauku.
kwa kufunuliwa kwa wana wa Mungu
"kwa wakati ambao Mungu atawafunua watoto wake"
wana wa Mungu
Hapa hii imaanisha walioamini wote katika Yesu na mara nyingi imetafsiriwa kama "watoto wa Mungu"
Romans 8:20-22
Kwa maana uumbaji ulitiishwa chini ya ubatili
"Kwa maana Mungu alisababisha kile alichokiumba kisiweze kufikia lengo ambalo alilolikusudia"
sio kwa mapenzi yake, bali yake yeye aliyevitiisha
Hapa "uumbaji" umeelezwa kama mtu ambaye anaweza kutamani. "sio kwa sababu kwamba hiki ndicho vitu vilivyoumbwa vilihitaji, bali kwasababu ndicho ambacho Mungu alihitaji"
ni katika tumaini kwamba uumbaji wenyewe utawekwa huru
"Kwasababu Mungu alijua kwamba atauokoa uumbaji."
kutoka utumwa hadi uharibifu
Paulo anavilinganisha vitu vyote katika uumbaji na watumwa na "uharibifu" wao. "kutoka kuoza na kufa"
kwenye uhuru wa utukufu wa wana wa Mungu
"na atawaweka huru atakapowapa heshima watoto wake"
Kwa maana twajua ya kuwa uumbaji nao pia unaugua na kuteseka kwa uchungu pamoja hata sasa
Uumbaji unalinganisha na mwanamke anavyougua wakati wa kuzaa mtoto. "Kwa maana twajua ya kuwa kila kitu ambacho Mungu amekiumba kinataka kuwa huru na huugua kama mwanamke anayezaa"
Romans 8:23-25
tulio na malimbuko ya Roho
Paulo analinganisha jinsi walioamini wanavyopokea Roho Mtakatifu sawa na malimbuko na mboga za masika zinavyokua. Hii inasisitiza kwamba Roho Mtakatifu ni mwanzo tu wa mambo ambayo Mungu atawapa walioamini.
kusubiri kufanywa wana, ukombozi wa miili yetu
"kusubiri wakati tutakapokuwa washiriki halisi wa familia ya Mungu na atakapookoa miili yetu kutoka katika kuharibika na mauti"
Kwa maana ni kwa taraja hili tuliokolewa
"Kwa maana Mungu alituokowa kwasababu tulikuwa na imani naye"
Lakini tunachotarajia kitatokea bado hakijaonekana, kwa maana ni nani atarajiaye kile akionacho tayari?
Paulo anatumia swali kuwasaidia wasikiliaji wake kuelewa maana ya "kujiamini."
Romans 8:26-27
Sentensi unganishi:
Ingawa Paulo amekuwa akisisitiza kwamba kuna mapambano ndani ya walioamini kati ya mwili na Roho, anathibitisha kuwa Roho anatusaidia sisi.
kuugua kusikoweza kutamkwa
"kuugua ambako hakuwezi kuelezewa kwa maneno"
Romans 8:28-30
Sentensi unganishi
Paulo anawakumbusha walioamini kwamba hakuna kinachoweza kuwatenganisha na upendo wa Mungu.
kwa wale wote walioitwa
"kwa wale wote ambao Mungu aliwachagua"
wote aliowajua tangu asili
"wote ambao aliwajua hata kabla ya kuwaumba"
Yeye pia aliwachagua tangu asili
"yeye pia aliufanya mwisho wake" au "yeye pia aliupanga tangu awali"
wafananishwe na sura ya Mwana wake
Mungu alipanga kabla ya kuanza kwa uumbaji kuwakuza wale wamwaminio Yesu, Mwana wa Mungu, kuwa watu wafananao na Yesu. "kwamba angewabadilisha wawe kama Mwana wake."
Mwana
Hili ni jina la muhimu la Yesu, Mwana wa Mungu.
kwamba awe mzaliwa wa kwanza
"ilikwamba Mwana wake awe mzaliwa wa kwanza"
kati ya ndugu wengi
"miongoni mwa akina kaka na dada wengi ambao ni wa familia ya Mungu"
Wale ambao aliwachagua tangu asili
"Wale ambao Mungu aliwapangia kabla"
hao pia akawatukuza
Neno "kutukuzwa" ni nyakati zilizopita kuonesha msisitizo kwamba hili litatokea hakika.
Romans 8:31-32
Tuseme nini basi juu ya mambo haya? Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
Paulo anatumia swali kusisitiza wazo kuu kwa yale aliyoyasema hapo awali. "Hiki ndicho tunachopaswa kujua kutoka haya yote: kwa Mungu anatusaidia sisi, hakuna awezaye kutushinda sisi"
Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe
Mungu Baba alimtuma Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, msalabani kama sadaka takatifu isiyo na mwisho ya muhimu kumridhisha asili ya milele ya Mungu dhidi ya dhambi ya wanadamu.
bali alimtoa
"lakini alimkabidhi kwa adui"
atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
Paulo anatumia swali kwa ajili ya msisitizo. "Yeye kwa hakika na kwa uhuru atatupatia vitu vyote"
Romans 8:33-34
Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki
Paulo anatumia swali kusisitiza. "Hakuna mtu anayeweza kutuhukumu sisi kwa Mungu kwasababu ndiye atupatanishaye naye."
Ni nani atakayewahukumia adhabu?
Paulo anatumia swali kusisitiza. Hatarajii jibu kutoka kwao. "Hakuna atakayetuhukumu"
na zaidi ya hayo, yeye pia alifufuliwa
"ambaye muhimu sana Mungu alimfufua kutoka wafu" au "ambaye kwa muhimu zaidi aliurudia uzima"
Romans 8:35-36
Ni nani atakayetutenga sisi na upendo wa Kristo?
Swali hili linaonekana kuuliza kuhusu mtu, lakini jibu lifuatalo linazuia matukio, sio watu. Hivyo Paulo labda anaongea kuhusu matukio kama vile na watu
Dhiki, au shida, au mateso, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
"Haiwezekani hata kama mtu yeyote atatusababishia shida, atatuumiza, atachukua mavazi yetu au chakula, au hata kutuua."
Dhiki, au shida
Maneno haya yote yana maana moja.
Kwa faida yako
Hapa "yako" ipo katika umoja na inamaanisha Mungu.
tunauawa mchana kutwa
Hapa "sisi" inarejea kwa yule aliyeandika kifungu hiki cha Maandiko na inajumuisha wale wote wanaomtii Mungu. Maneno "mchana kutwa" ni maneno yaliyoongezwa kusisitiza kiwango cha hatari waliyomo. Paulo anatumia sehemu hii ya Maandiko kuonesha kwamba wote walio wa Mungu watarajie nyakati ngumu. "adui zetu wanaendelea kututafuta watuue"
Sisi tulihesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa
Hii inalinganisha kati ya watu wanaouawa kwasababu ya utii wao kwa Mungu na wanyama. "Maisha yetu hayakuwa na thamani kwao kuliko kondoo wanaowaua"
Romans 8:37-39
sisi ni zaidi ya washindi
"tunao ushindi kamili"
katika yeye aliyetupenda
Aina ya upendo ambao Yesu alituonesha unaweza kuwekwa wazi. "kwasababu ya Yesu, aliyetupenda sana alikuwa tayari kufa kwa ajili yetu."
Mimi nimekwisha shawishika
"Nimeshawishiwa" au "Nina ujasiri"
mamlaka
Maana inaweza kuwa 1) mapepo (UDB) au 2) wafalme na watawala wa kibinadamu.
wala nguvu
Maana inaweza kuwa 1) viumbe vya kiroho vyenye nguvu au 2) wanadamu wenye nguvu.
Romans 9
Romans 9:1-2
Sentensi unganishi:
Paul anaeleza kuhusiana na shauku yake kwamba watu wa taifa la Israeli wangeokolewa, kisha anasisitiza njia tofauti ambazo Mungu ameandaa kwa kuamini.
na dhamiri yangu hushuhudia ndani yangu katika Roho Mtakatifu.
Njia mbadala ya utofasiri: "Roho Mtakatifu huongoza dhamiri yangu na kuhakiki nisemacho"
kwa kuwa kwangu mimi kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu.
Kama nafsi ya Paul ambayo inahuzunika inahitajika kusemwa, tumia tofasiri nyingine: " Ninakuambia kwamba ninahuzunika kwa wingi na kwa undani."
huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma
Hii misemo miwili inamaanisha haswa maana ile ile. Paulo anatumia kwa pamoja kwa kusisitiza ni kwa namna gani hisia zake zilivyo.
Romans 9:3-5
Kwamba ningetamani mimi mwenyewe kulaaniwa na kutengwa mbali na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, wale wa jamii yangu katika mwili.
Mimi binafsi ningekuwa tayari kumwacha Mungu anilaani mimi na, kuniweka mimi mbali na Kristo milele kama hiyo ingewasaidia ndugu zangu waisraeli, watu wa kundi langu, kumwamini Kristo."
Wao ni waisraeli
"Wao, kama mimi, ni waisraeli. Mungu aliwachagua wao kuwa uzao wa Yakobo"
Wao ni watangulizi ambako Kristo amekuja kwa heshima ya mwili.
Kristo amekuja kwa mwili kama mzao kutoka kwa watungulizi wao.
Romans 9:6-7
Sentensi unganishi:
Paulo anasisitiza kwamba wale waliozaliwa katika familia ya Israeli wanaweza kwa kweli kuwa sehemu ya Israeli kupitia imani.
Lakini si kwamba ahadi za Mungu zimeshindwa kutimia
"Lakini Mungu hajashindwa kutimiza ahadi zake"
Kwa kuwa si kila mtu aliye Israeli ni mwiisraeli halisi.
Mungu hakuzifanya ahadi zake kwa uzao wote kimwili wa israeli (au Yakobo), lakini kwa uzao wake wa kiroho, kwamba, wale walio na imani katika Yesu.
Si wote ni uzao wa Ibrahihim ni watoto wake hilisi.
"Wala si kwamba ni wana wa Mungu kwa sababu ni wazao wa Ibrahimu"
Romans 9:8-9
watoto wa mwili
Hii inarejesha kwa watu ambao ni uzao wa Ibrahimu kwa mwili.
Watoto wa Mungu
Hii inarejesha kwa watu ambao ni uzao wa kiroho walio na imani ndani ya Yesu.
watoto wa ahadi
Hii inarejesha kwa watu watakaoridhi ahadi ya Mungu.
Sara atapewa mtoto
"Nitampa Sara mwana"
Romans 9:10-13
baba yetu Isaka...sasa hivi
Katika utamaduni unaweza kuhitaji kuweka 9:11 baada ya 9:12. Tofasiri mbadala: "baba yetu Isaka, ilisemwa kwake, ' Mkubwa atamtumikia mdogo.' Sasa watoto walikuwa bado hawajazaliwa...kwa sababu ya yeye aitae. Ni sasa"
baba yetu
Isaka alikuwa mtangulizi wa Paulo na wakristo wayahudi katika Rumi.
kubeba mimba
"alibeba ujauzito"
kwa kuwa walikuwa bado hawajazaliwa na hakuwa amefanya lolote zuri au baya
"kabla watoto hawajazaliwa na hakuwa amefanya lolote zuri au baya"
ili kwamba kusudi la Mungu kulingana na uchaguzi lisamame
"ili kwamba Mungu anachotaka kifanyike kulingana na uchaguzi wake kifanyike"
kwa kuwa watoto walikuwa bado hawajazaliwa
"kabla watoto hawajazaliwa"
na hakuwa amefanya lolote zuri au baya
"si kwa sababu ya lolote walikuwa wamefanya"
kwa sababu yake
kwa sababu ya Mungu
ilikuwa imesemwa kwake, "Mkubwa atamtumikia mdogo".
Mungu alisema kwa Rebeka, 'Mwana mkubwa atamtumikia mwana mdogo"
Nilimpenda Yakobo, lakini nilimchukia Esau
Mungu alimchukia Esau pekee katika ulinganisho wa kiasi gani alivyompenda Yakobo.
Romans 9:14-16
Basi tena tutasema nini?
Paulo anatumia swali kusahihisha hitimisho kwamba Mungu si dhalimu.
La hasha
"Hilo haliwezekani!" au bila shaka!" Usemi hii kwa nguvu hukanusha kwamba hii ingewezekana kufanyika. Unaweza kuwa na usemi wa kufanana katika lugha yako kwamba ungeweza kutumia hapa.
Kwa kuwa anasema kwa Musa
"Kwa kuwa Mungu anasema kwa Musa"
Si kwa sababu yeye anataka, wala kwa sababu ya yeye akimbiae
"Si kwa sababu ya wale watu hupenda au kwa sababu wanajaribu kwa nguvu"
wala si kwa sababu ya yeye akimbiae
Paul anamlinganisha mtu anayekimbia mbio kwa mtu ambaye anajitahidi kwa nguvu kufikia lengo.
Romans 9:17-18
Kwa kuwa maandiko husema
Hapa andiko limefanyika nafsi hai kama Mungu anazungumza na Farao. "Maandiko hutunza kumbukumbu kwa Mungu kusema"
Mimi...changu
Mungu anarejesha kwake mwenyewe.
wewe
umoja
na ili kwamba jina langu litangazwe katika inchi yote.
"na kwamba watu waweze kulitangaza jina langu katika inchi yote"
na yeye ambaye apendaye, humfanya kuwa mgumu wa moyo.
Mungu humfanya mgumu wa moyo yule apandaye kumfanya.
Romans 9:19-21
Kisha utasema kwangu
Paulo anazugumza hukumu ya mafundisho yake kama vile alikuwa anaongea na mtu mmoja. Unaweza kuhitajia kutumia wingi hapa.
yeye...yake
Maneno 'yeye' na 'yake' hapa yanarejesha kwa Mungu
hivi kilichofinyangwa cha weza sema... matumizi ya kila siku?
Paulo anatumia haki ya mfinyazi kutengeneza aina yoyote ya chombo anachotaka kutokana na udongo kama mfano wa haki ya muumbaji kufanya chochote anachotaka na umbaji wake.
kwanini ulinifanya hivi mimi
Neno "wewe" hapa urejea kwa Mungu.
Romans 9:22-24
yeye...yake
Maneno "yeye" na "yake" urejea kwa Mungu.
vyombo vya gadhabu...vyombo vya rehema
"watu wanaostahili gadhabu...watu wanaostahil rehema"
wingi wa utukufu wake
"utukufu wake, ambao ni dhamani kubwa"
ambao alikwisha kuandaa kwa ajili ya utukufu.
"ambao alikwisha kuaanda mbele ya wakati kutoa utukufu"
pia kwa ajili yetu
Neno "yetu" hapa urejea kwa Paulo na wakristo wenzake.
kuitwa
Hapa hii ina maanisha Mungu amewateua au kuchagua watu kuwa watoto wake, kuwa watumishi wake nd watangazaji wa ujumbe wake wa wokovu kupitia Yesu.
Romans 9:25-26
Sentensi unganishi:
Kaitka sehemu hii Paul anaeleza namna kuto amini kwa waisraeli kama taifa kulisemwa mbele ya wakati na nabii Hosea.
Kama asemavyo katika Hosea
"Kama Mungu asemavyo pia katika kitabu cha Hosea aliandika"
Hosea
Hosea alikuwa nabii
Nitawaita watu wangu ambao hawakuwa watu wangu
" Nitawachagua watu ambao hawakuwa watu wangu kuwa watu wangu"
mpendwa wake ambaye hakuwa amependwa
"Nitamchagua yeye ambaye siku mpenda kuwa mmoja wa yule ninaye mpenda"
wana wa Mungu aliye hai
Neno "hai" linaweza kurejea kwa kigezo kwamba Mungu ni pekee wa "kweli", na siyo kama sanamu za uongo. Tofasiri mbadala: "watoto wa Mungu wa kweli"
Romans 9:27-29
hulia
"huita"
kama mchanga wa bahari
"ni zaidi kuhesabu"
wataokolewa
Kuokolewa imetumika katika maana ya kiroho. Kama mtu "ameokolewa", ina maanisha kwamba kupitia kuamini kifo cha Yesu pale msalabani, Mungu amekwisha msahehe na kumkomboa yeye kutoka katika kuhukumiwa kwa dhambi yake.
neno
Hii inarejea kwa kila kitu Mungu alichosema au kuamuru.
yetu...sisi
Hapa maneno "yetu" na "sisi" urejea kwa Isaya na kuwajumuisha waisraeli
tungekuwa kama Sodoma, na tumefanywa kama Gomora
Unaweza kufanya kwa uwazi namna waisraeli wangekuwa kama Sodoma na Gomora. Tofasiri mbadala: "tungekuwa wote tumeteketezwa, kama miji ya Sodoma na Gomora ilivyoteketezwa.
Romans 9:30-31
Tutasema nini basi?
Tofasiri mbadala: "Hivi ndivyo tunapaswa kusema"
Kwamba mataifa
Tofasiri mbadala: "Tutasema kwamba wa mataifa"
ambao hawakuitafuta haki
"ambao hawakujaribu kumfurahisha Mungu"
hawakuweza kuifikia
"hawakuweza kuipata haki kwa kuifata sheria"
Romans 9:32-33
Kwani si hivyo?
"Kwanini hawakuweza kuifikia haki?"
kwa matendo
"kwa kujaribu kufanya mambo ambayo yangemfurahisha Mungu" au "kwa kuifata sheria"
jiwe la kujikwaa
"jiwe ambalo watu wanajikwaa"
kama ilivyo kwisha andikwa
"kama Isaya nabii aliandika"
amini ndani yake
Kwa sababu jiwe husimama kwa ajili ya mtu, unaweza kuhitaji kutofasiri "amini katika yeye"
Romans 10
Romans 10:1-3
Sentensi unganishi:
Paulo anaendelea na wazo lake kwa waisraeli kuamini lakini akisisitiza kwamba wale walio wayahudi na yoyote yule anaweza kuokolewa kwa imani katika Yesu.
Ndugu
Hapa ina maanisha wakristo wenzetu, ikijumuisha wote wanuame na wanawake.
shauku ya moyo wangu
"shauku yangu kuu"
ni kwa ajili yao, kwa ajili ya wokovu wao
"ni Mungu atakaye waokoa wayahudi"
Romans 10:4-5
Kwa kuwa Kristo ni hitimisho la sheria
"Kwa kuwa Kristo kwa ukamilifu alitimiliza sheria"
kwa kuwa haki ipo kwa yoyote ambaye huamini.
"ili kwamba aweze kumfanya kila moja aaminie katika yeye kuwa sawa mbele yake Mungu"
uamini
Hapa ina maanisha kuamini kitu ni kukubali au kusadiki kuwa ni kweli.
haki inayo kuja kutokana na sheria
"namna gani sheria humfanya kuwa sawa mbele zake Mungu"
Mtu ambaye hufanya haki ya sheria ataishi kwa haki hii
"Mtu ambaye kwa ukamilifu utii sheria ataishi kwa sababu sheria itamfanya yeye kuwa sawa mbele ya Mungu"
ataishi
Hii inaweza kurejea kwa 1) uzima wa milele au 2)maisha ya dunia katika ushirika pamoja na Mungu.
Romans 10:6-7
Lakini haki inayotokana na imani husema hivi
Hapa "haki" imeelezwa kama mtu ambaye anaweza kuongea. "Lakini Musa anaandika hivi kuhusiana na namba imani humfanya mtu sawa mbele za Mungu"
Usiseme ndani ya moyo wako
Musa alikuwa anaongea na watu kama vile walikuwa ni mtu mmoja. "Usiseme kwako mwenyewe"
Nani atakayepaa kwenda mbinguni?
Musa anatumia swali kufundisha wasikiizaji wake. Maelekezo yake ya awali, "Usiseme" huitaji jibu hasi kwa swali hili. "Hakuna mmoja asijaribu kwenda juu mbinguni"
hii ni kwamba, kumleta Kristo chini
"ili kusudi kwamba wamlete Kristo chini ya inchi"
Nani atakaye shuka katika shimo kubwa
Musa anatumia swali kuwafundisha wasikilizaji wake. Maelekezo yake ya awali, "Usiseme" huitaji jibu hasi kwa swali hili. "hakuna mmoja ajaribu kwenda chini na kuingia eneo ambao roho za watu waliokufa wapo"
hii ni, kumleta Kristo juu kutoka kwa wafu
" ili kusudi kwamba waweze kumleta Kristo kutoka kwa wafu."
kufa
Hapa ina maanisha pale mwili wa mtu huacha kuishi.
Romans 10:8-10
Lakini inasema nini?
Neno "ina" urejea kwa "haki"
Neno liko karibu nawe
"Ujumbe uko wapi"
katika mdomo wako
Neno "mdomo" urejea kwa kile mtu husema. Tofasiri mbadala: "kiko katika kile usemacho"
na katika moyo wako
Neno "moyo" urejea kwa akili ya mty au kile ufikiria. Tofasiri mbandala: "na kiko katika kile unachofikiri"
kama kwa mdomo wako unatambua Yesu kuwa Bwana
'kama unakiri kwamba Yesu ni Bwana"
amini katika moyo wako
"kubali kuwa ni kweli"
alimfufua yeye kutoka kwenye mauti
Hapa ina maanisha kwamba Mungu alimsababisha Yesu kuwa hai tena
utaokolewa
"Mungu atakuokoa"
Kwa kuwa kwa moyo mtu huamini kwa haki, na kwa kinywa hukiri wokovu
"Ni kwa akili kwamba mtu husadiki na kuwa mbele za Mungu, na ni kwa kinywa mtu hukiri na Mungu umuokoa"
Romans 10:11-13
Yeyote ambaye anamwamini yeye hatatahayarika
"Yeyote asiye amini atatayarika." Hasi hapo imetumiwa kwa usisitizo. "Mungu atamheshimu ambaye anamwamini."
hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani
"Kwa njia hii, Mungu huwaona Wayahudi na wasio wayahudi sawa"
na yeye ni tajiri kwa wale wote wamwitao
"na uwabariki kwa wingi wote wamwaminio"
Kwa kila aliitae jina la Bwana ataokolewa
Neno "jina" urejea kwa Yesu. " Bwana atamuokoa kila amtegemeae."
Romans 10:14-15
Basi watawezaje kumwita yeye wasiye mwamini?
Paulo anatumia swali kusisitiza umuhimu wa kupeleka habari njema za Kristo kwa wale ambao hawajasikia. Neno "wale" urejea kwa wale ambao si wa Mungu. "Wale ambao hawamwamini Mungu hawawezi kumwita yeye"
Na watawezaje kuamini katika yeye ambapo hawajamsikia?
Paulo utumia swali jingine kwa sababu ile ile. "Na hawawezi kuamini katika kama hawajasikia ujumbe wake" au "Na hawawezi kuamini katika yeye kama hawajasikia ujumbe kuhusiana na yeye."
kuamini katika
Hapa ina maanisha kukiri kwamba kile mtu alichosema ni kweli.
Na watawezaje kusikia pasipo mhubiri?
Paulo anatumia swali jingine kwa sababu ile ile. "Na hawawezi ujumbe kama hakuna mtu wa kuwambia"
Na watawezaje kuhubiri, mpaka watumwe?
Paulo anatumia swali jingine kwa sababu ile ile. Neno "wale" urejea kwa wale wa Mungu. "Na hawawezi kuwaambia watu wengine ujumbe mpaka mtu awatume"
Ni mzuri miguu ya wale wanaotangaza habari njema za mambo mazuri
Paulo anatumia "miguu" kuwakilisha wale wanaosafiri na kuleta ujumbe kwa wale amba hawajasikia. "Inafurahisha pindi waleta ujumbe huja na kutuambia habari njema."
Romans 10:16-17
Lakini wote hawakusikiliza
"Lakini si Wayahudi wote walisikiliza'
Bwana, nani ambaye ameamini ujumbe wetu?
Paulo anatumia swali hili kusisitia kwamba Isaya alitabiri katika Maandiko kwamba Wayahudi wengi hawataamini katika Yesu. "Bwana, wengi wao hawaamini ujumbe wetu"
ujumbe wetu
hapa, "wetu" urejea kwa Mungu na Isaya.
amini
kubali au amini kwamba ni kweli
Romans 10:18
Lakini nasema, "Hawakusika?" Ndiyo, bila shaka
Paulo anatumia swali kwa msisitizo. "Lakini, nasema bila shaka Wayahudi wamesikia ujumbe kuhusiana na Kristo
Sauti yao imeenda katika inchi yote, na maneno yao mwisho mwa ulimwengu
Maelezo haya yote kwa msingi humaanisha kitu kile kile na yanatumiwa kwa msisitizo. Neno "yao" inarejea jua, mwezi, na nyota. Hapa wameelezwa kama wapeleka ujumbe kwa kuwaambia watu kuhusiana na Mungu. Hii inarejea kwa namna kuishi kwao uhushuhudia nguvu na utukufu wa Mungu. Inaweza kufanywa wazi kwamba Paulo ananukuu Maandiko hapa. "Kama ilivyoandikwa katika Maandiko, 'Jua, mwezi na nyota ni udhibitisho wa nguvu na utukufu wa Mungu, na kila aliye katika ulimwengu huyaona na ujua ukweli kuhusiana na Mungu"
Romans 10:19
Zaidi, nasema, "Waisraeli hawakujua"
Paulo anatumia swali kwa msisitizo. Neno "Israeli" urejea kwa watu walio ishi katika taifa la Israeli. "Tena nakwambia watu wa Israeli hawakujua ujumbe.
Kwanza Musa anasema, "Nitakukasirisha... Nitakuchochea
Hii ina maanisha kwamba Musa aliandika chini kile Mungu alisema. "Mimi" urejea kwa Mungu, na "wewe" urejea kwa Waisraeli. "Kwanza Musa anasema kwamba Mungu atakukasirisha...kukuchoea
kwa kipi siyo taifa
"kwa wale hautazamii kuwa ni taifa halisi" au "kwa watu wasio na taifa lolote"
Kwa maan ya taifa lisilo na uelewa
"kwa taifa lenye watu wale wasionijua mimi au amri zangu"
Nitakuchochea wewe kwa hasira
"Nitakufanya wewe kukasirika"
wewe
Hii inarejea kwa taifa la Israeli
Romans 10:20-21
Taarifa ya ujumla:
Hapa maneno "mimi" na "yangu" urejea kwa Mungu
Na Isaya ana ujasiri wa kutosha kusema
Hii ina maanisha nabii Isaya aliandika kile Mungu alikwisha sema.
Nilipatikana na wale ambao hawakunitafuta mimi
Pia, manabii mara nyingi huongelea mambo yajao kama vile yamekwisha tokea. Hii inasisitiza kwamba unabii bila shaka utatimia. "Ijapokuwa watu wa Mataifa hawatanitafuta, watanipata"
Nilionekana
"Nilifanya mwenyewe kuonekana"
anasema
"Yeye" ni Mungu, anaongea kupitia Isaya
Kwa siku yote
Kifungu cha maneno haya kinatumika kusisitiza mwendelezo wa juhudi za Mungu. "mwendelezo"
Nilinyosha mikono yangu watu wasio na utiifu na wabishi
"Nilijaribu kukukaribisha na kukusaidia, lakini ulikataa msaada wangu na kuendelea kutotii"
Romans 11
Romans 11:1-3
Maelezo yanayounganisha:
Japokuawa Israeli kama taifa lilikataliwa na Mungu, Mungu alitaka waelewe kuwa wokovu unakuja kwa neema bila kazi.
Basi naseema
"Mimi, Paulo, nikasema"
Je Mungu amewakataa watu wake?
Paulo alijiuliza hili swali ili awajibu maswali ya Wayahudi wengine waliokuwa wamekasirika kwamba Mataifa wamewekwa kuwa watu wa Mungu, wakati mioyo ya Wayahudi ikiwa imefanywa kuwa migumu.
Hata kidogo
"Hiyo haiwezekani" au "la hasha!" Ufafanuzi huu unakataa kwa nguvu kwamba hii haiwezi kutokea. Unaweza kuwa na ufafanuzi mwingine kwa lugha yako ambayo unaweza kutumia hapa.
Kabila la Benjamini
Hii inaelezea kabila ambalo ni kizazi cha Benjamini, moja kati ya makabila 12 ambayo Mungu aliwagawanya wana wa Israeli kwayo.
Aliowatambua
"Aliowafahamu tangu mwanzo"
Je, hamjui andiko linasema nini kuhusu Eliya, jinsi alivyomsihi Mungu juu ya Israeli?
"Hakika mnajua nini kimeandikwa kwenye maandiko. Mnakumbuka Eliya alivyomsihi Mungu juu ya Israeli."
Andiko linasema nini
Paulo anaelezea ni nini kimeandikwa kwenye maandiko.
Wao wamewauwa
"Wao" ni watu wa Israeli.
Nami nimesalia peke yangu
Neno "mimi" linamaanisha Eliya
Romans 11:4-5
Lakini ni nini Mungu alijibu akiwaambia?
Paulo anatumia swali hili kuwaleta wasomaji kwenye wazo linalofuata.
Ni nini jibu la Mungu akiwaambia
"Mungu aliwajibu vipi"
Yeye
Neno "yeye" linamaanisha Eliya
Watu elfu saba
"watu 7000"
Mabaki
Hapa inamaanisha sehemu ndogo ya watu waliochaguliwa na Mungu kupokea neema yake.
Romans 11:6-8
Lakini ikiwa ni kwa neema
Paulo anaendelea kuelezea namna neema ya Mungu inavyofanya kazi. "kwa kuwa neema ya Mungu inafanya kazi kwa rehema"
Ni nini basi?
"Tuhitimishe vipi?" "hivi ndivyo ambavyo tunapaswa kukumbuka."
Mungu amewapa roho ya ubutu, macho ili wasione, na masikio ili wasisikie
Huu ni ufafanuzi kuhusu ukweli kwamba niwabutu kiroho. Hawana uwezo wa kuona na kusikia ukweli wa kiroho.
Roho ya
Hapa inamaanisha "kuwa na tabia za" mfano "roho ya hekima."
Macho ili wasione
Kuona kwa jicho moja ilichukuliwa kuwa sawa na kupata uelewa.
Masikio ili wasisikie
Kusikia kwa masikio ilichukuliwa kuwa sawa na utii.
Romans 11:9-10
Acha meza zao ziwe na wavu
"Meza" inawakilisha sherehe, na "neti" au "mtego" inawakilisha adhabu. Nakusihi Mungu wakamate na uwatege katika sherehe zao"
Makwazo
"kitu kinachowafanya watende dhambi"
na kulipiza kisasi dhidi yao
"kitu kinachokuruhusu kulipa kisasi kwao"
Ukawainamishe migongo yao daima
Daudi alimuomba Mungu awafanye adui zake kuwa watumwa wanaobeba mizigo mizito kwenye migongo yao daima.
Romans 11:11-12
Maelezo yanayounganisha
Pamoja na kuwa Israeli kama taifa lililokataliwa na Mungu, Paulo anawaonya Mataifa kuwa makini na wasifanye kosa lile lile.
Wameona mashaka hata kuanguka?
"Je Mungu amewakataa daima kwa sababu wametenda dhambi?"
Hata kidogo
"Hiyo haiwezekani" au "la hasha!" Ufafanuzi huu unakataa kwa nguvu kwamba hii haiwezi kutokea. Unaweza kuwa na ufafanuzi mwingine kwa lugha yako ambayo unaweza kutumia hapa.
Dunia
Hapa inamaanisha watu wa duniani.
Romans 11:13-14
kuwatia wivu
Tafsiri kifungu hiki njia sawa kama alivyofanya katika (Rom:10:19)
walio mwili mmoja na mimi
Hii inamaanisha "Wayahudi wenzangu"
Romans 11:15-16
Kwao
Hii inawaelezea Wayahudi wasioamini
Dunia
Hii inamaanisha watu wa duniani.
kupokelewa kwao kutakuwaje ila uhai toka kwa wafu?
"Hivyo basi, Mungu atawapokea vipi wakimwamini Kristo? Itakuwa kama wamekuja tena kwenye uhai toka kwenye kifo"
Kama matunda ya kwanza ni takatifu, hivyo ni bonge la unga.
Paulo anamfananisha Ibrahimu, Isaka na Yakobo, mababu wa Israeli na ngano ya kwanza kuvunwa, na Waisraeli ambao ni uzao wa wanaume hao ni unga unaotokana na ngano itakayovunwa baadae.
Kama mizizi ni takatifu, vivyo hivyo na matawi
Paulo anamfananisha Ibrahimu, Isaka na Yakobo, mababu wa Israeli na mizizi ya mti, na Waisraeli ambao ni uzao wa wanaume hao kama matawi ya miti.
Takatifu
Mazao ya kwanza kuvunwa daima yanakuwaga "matakatifu" hii ni, yameachwa kwa ajili ya Mungu. Hapa "mazao ya kwanza" yanasimama kwa watu wa kwanza kumuamini Kristo.
Romans 11:17-18
Kama wewe, tawi pori la mizeituni
Neno "wewe" na "tawi pori la mizeituni" linaelezea Watu wa Mataifa walikubali wokovu kupitia Yesu.
Ulipandikizwa kati yao
"Walipachikwa kwenye mti kati ya matawi yaliyobaki"
Mizizi ya utajiri wa mizeituni
Hii inamaanisha ahadi za Mungu.
Usijisifu juu ya matawi
"Usisieme kuwa wewe ni bora zaidi ya Wayahudi waliokataliwa na Mungu"
si wewe ambaye unasaidia mizizi, bali mizizi inakusaidia wewe
Waamini wa Mataifa waliamini kuwa walikombolewa tuu kwa sababu ya agano la ahadi la Mungu lililofanywa kwa Wayahudi
Romans 11:19-21
Matawi yalikatwa
"Mungu aliyakata matawi"
Matawi
Neno hili limetumika kuwaelezea Wayahudi walikataliwa na Mungu.
Naweza kupandikizwa
maneno haya yametumika kuwaelezea waamini wa Mataifa waliokubaliwa na Mungu. "anaweza kunipachika"
"walikatwa"
"aliwakata"
wao... wale
Maneno "wao" au "wale" inamaanisha Wayahudi ambao hawakuamini.
Lakini wewe simama kwa imani yako
"Lakini ubaki kwa sababu ya imani yako"
Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, je, unadhani atakuhurumia wewe
"Kwa maana ikiwa Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, je, unadhani atakuhurumia wewe"
Matawi ya asili
Hii inamaanisha Wayahudi
Romans 11:22
matendo mema na ukali wa Mungu
Paulo anawakumbusha waamini wa Mataifa kwamba japokuwa Mungu amekuwa mwema sana kwao, hatasita kuwahukumu na kuwaadhibu.
Vinginevyo wewe pia utakatiliwa mbali
"Vinginevyo Mungu atakukatilia mbali"
Romans 11:23-24
kama hawataendelea katika kutoamini kwao
"Kama Wayahudi wanaanza kumiamini Kristo"
Watapandikizwa tena
"Mungu atawapandikiza tena"
Kupandikiza
Hii ni hatua ya kawaida ambapo tawi lililo hai la mti mmoja linapachikwa kwenye mti mwingine ili liweze kukua kwenye ule mti mpya.
Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa nje kwa asili ya mzeituni mwitu, na kinyume cha asili walipandikizwa katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana hawa Wayahudi, ambao ni kama matawi ya asili kuweza kupandikizwa tena ndani ya mzeituni wao wenyewe?
"Ikiwa Mungu atakukata nje kwa asili ya mzeituni mwitu, na kinyume cha asili walipandikizwa katika mzeituni mzuri, si zaidi sana hawa Wayahudi, ambao ni matawi ya asili, kwenye mzeituni wao wenyewe?"
Matawi
Paulo anawafananisha wanachama wa watu wa Mungu na matawi ya mti.
Wao..... Wale
Ilipojitokeza "wao" au "wale" inamaanisha Wayahudi.
Romans 11:25
Sitaki ninyi msijue
"Natamani sana mtambue"
Mimi
Neno "mimi" linamaanisha paulo.
wewe...wewe... ninyi
Maneno haya "wewe" na "ninyi" yanamaanisha Mataifa walioamini.
ili kwamba msiwe na hekima katika kufikiri kwenu wenyewe.
Waamini wa mataifa wanaweza kuamini kwamba wana hekima zaidi kuliko Wayahudi wasioamini. "Ili msifikiri kwamba mna hekima zaidi ya mlivyo"
ubaguzi mgumu umetokea katika Israeli
Baadhi ya Wayahudi walikataa kukubali wokovu kupitia kwa Yesu.
hadi kukamilika kwa mataifa kutakapokuja
Neno "mpaka" linaelezea kuwa Wayahudi wengi wataamini baada ya Mungu kumaliza kuwaleta Mataifa kanisani.
Romans 11:26-27
Maelezo yanayounganisha
Paulo anasema mkombozi atakuja toka Israeli kwa utukufu wa Mungu.
Hivyo Israeli wote wataokoka
"Hivyo Mungu atawaokoa Waisraeli wote"
Waisraeli wote wataokoka
Hii imeongezwa chunvi. Wayahudi wengi wataokolewa.
Romans 11:28-29
Kwa upande mmoja... kwa upande mwingine
Hizi ni sentensi zinazotumika kufananisha vitu viwili tofauti kuhusu kitu. Paulo alitumia kuelezea kwamba Mungu aliwakataa Wayahudi, lakini pia bado anawapenda.
Wanachukiwa kwa sababu yenu
Upendo wa Mungu kwa Mataifa ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba ukilinganisha upendo kwa Wayahudi ukaonekana kama chuki.
Kwa kuwa walichukiwa
"Mungu aliwachukia Wayahudi"
Kwa ajili ya zawadi na wito wa Mungu usiobadilika
"Kwa sababu zawadi ya Mungu na wito wake hauwezi kubadilika"
Romans 11:30-32
Mlikuwa mmemuasi
"Hamkumtii hapo zamani"
Ninyi
Hii inamaanisha waamini wa Mataifa, na ni wingi.
Mungu amewafunga watu wote katika uasi
Hii pia inaweza kumaanisha Mungu anawafanya wasiweze kuacha kumuasi, kama wafungwa walioshindwa kutoroka gerezani. "Mungu amamfanya kila mtu kuwa mfungwa kwa kuasi"
Romans 11:33-34
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu!
"Jinsi zinavyoshangaza faida za hekima ya Mungu na maarifa"
Hazichunguziki hukumu zake, na njia zake ni zaidi ya kugundua
Hatuwezi kabisa kuelewa mambo ambayo anayaamua na kujua njia anazotumia juu yetu.
Romans 11:35-36
Hivyo atalipwa tena
"Hivyo Mungu atamlipa tena"
Kumlipa yeye
Neno "yeye" linamaanisha mtu aliyempa Mungu
yeye
Sehemu nyingine "neno" yeye linamaanisha MUngu
Romans 12
Romans 12:1-2
Maelezo yanayounganisha:
Paulo anatuambia namna ambavyo maisha ya mwamini yanatakiwa yawe na namna waamini wanavyotakiwa kutumika.
Nawasihi Basi, ndugu, kwa huruma zake Mungu
"Waamini wenzangu, kwa sababu ya neemakuu ambayo Mungu ametupa nawasihi sana"
itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai
Hapa Paulo ametumia neno "miili" akimaanisha mtu. Paulo anamfananisha mwamini wa Kristo anayemtii Mungu na wanyama ambao Wayahudi waliwaua na kutoa sadaka kwa Mungu. "Mjitoe kabisa kwa Mungu mkiwa hai kama sadaka iliyokufa kwenye madhabahu hekaluni"
Takatifu, iliyokubalika na Mungu
Maana nyingine yaweza kuwa 1) "sadaka ambayo unampa Mungu pekee na itakayomtukuza" au 2) "Inayokubalika na Mungu kwa kuwa ni safi"
Hii ni huduma yenu ya kiroho
Inaweza kumaanisha 1) "Hii ni njia sahihi ya kumwabudu Mungu" au 2) "hii ndo namna ya kumwabudu Mungu kwenye roho zenu"
msiifuatishe namna ya dunia hii
Inamaanisha kwamba 1) "Msiishi kama dunia inavyoishi" au 2) Msifikirie kama dunia inavyofikiri."
Msiifuatishe
Hii inaweza kumaanisha 1) " Msiache dunia kuwaambia ni nini cha kufanya" au Msiache... nini cha kufikiria" au 2) "Msiruhusu kufanya kama dunia wanavyofanya"
Dunia hii
Hii inamaanisha watu wasioamini, wanaoishi katika dunia hii.
bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu.
"lakini muacheni Mungu awabadilishe namna mnavyofikiri" au "lakini mwacheni Mungu awabadilishe namna mnavyoenenda kwa kuwabadilisha kwanza namna mnavyofikiri"
Romans 12:3
kwa sababu ya neema niliyopewa,
Hapa "neema" inaelezea Mungu alivyomchagua Pulo kuwa Mtume na kiongozi wa kanisa. "Kwa kuwa Mungu alinichagua kuwa Mtume"
Kwamba kila mtu ambaye yupo miongoni mwenu hapaswi kufikiri zaidi juu yenu wenyewe kuliko mnavyopaswa kufikiri
"Kwamba mtu asifikiri kwamba ni bora zaidi ya watu wengine"
Badala yake, mnapaswa kufikiri kwa njia ya hekima
"Lakini mnapaswa kuwa na hekimakwa namna mnavyofikiri kuhusu ninyi wenyewe"
kama ambavyo Mungu amewapa kila mmoja kiasi fulani cha imani.
Ikiwa Mungu amewapa kila mmoja kiasi tofauti cha imani kwamba mnapaswa kufikiri kwa makini"
Romans 12:4-5
Kwa kuwa
Paulo anaelezea kwa nini Wakristo hawapaswi kufikiria kuwa wao ni wa maana zaidi ya wengine.
Tuna viungo vingi katika mwili mmoja
Paulo anawafananisha Waamini wote katika Krosto kama sehemu tofauti zamwili. Amefanya hivi kuonyesha japokuwa waamini wanamtumikia Kristo kwa njia tofauti, kila mtu ni mali ya Kristo na anamtumikia kwa njia ya muhimu.
Kiungo
Hivi ni vitu kama macho, tumbo, na mikono.
Mmoja mmoja kwa kila mmoja
"Kila mwamini ni sehemu ya mwili wa mwamini mwingine" "na kila muumini ameunganishwa pamoja na waamini wengine"
Romans 12:6-8
Tuna zawadi mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa
"Mungu ammempa kila mmoja wetu uwezo wa kufanya vitu tofauti kwa ajili yake"
Itendeke kwa kadiri ya imani yake
Inaweza kuwa na maana kuwa 1) "atoe unabii ambao hautazidi kiwango cha imani amabyo Mungu ametupa" au 2) "Aseme unabii unaokubaliana na mafundisho ya imani yetu."
Kama zawadi ya mtu ni kutoa
Maana inaweza kuwekwa wazi. "Ikiwa matu ana zawadi ya kutoa pesa au kitu chochote kwa wahitaji"
Romans 12:9-10
Pendo lisiwe na unafiki
"Acha upendo uwe wa wazi" au "Acha upendo uwe wa kweli"
Upendo
Hili ni neno lingine linalomaanisha upendo wa ndugu au upendo kwa rafiki au kwa wanafamilia. huu ni upendo wa asili wa binadamukati ya marafiki au ndugu.
Kuhusu upendo wa ndugu, mpendane
Paulo ameanza kuonyesha idadi ya vitu tisa, kila kimoja kikionyesha "Kuhusu....." "kuwaambia waamini wanapaswa kuwa watu wa aina gani.
Kuhusu upendo wa ndugu
"Kwa namna ambavyo unaweza kumpenda mwamini mwenzako"
Mpendane
"Muwe na uaminifu" kama wanafamilia.
Kuhusu heshima, mheshimiane.
"Waheshimu na watii wengine" au, tumia sentensi mpya, "Kama unavyowaheshimu waamuni wenzako, watii"
Romans 12:11-13
Kuhusu bidii, msiwe na wasiwasi. Kuhusu roho, myatamani. Yanayohusu Bwana, mtumikieni.
"Msiwe wavivu kwenye zamu zenu, bali mtamani kumfuata roho na kumtumikia Bwana"
Furahini kwa ujasiri mlionao kuhusu siku zijazo.
"Kuweni na furaha maana ujasiri wenu upo katika Mungu"
Mvumilie katika matatizo yenu
"Muwe wavumilivu wakati mgumu unapokuja"
Endeleeni kuomba
"Na mkumbuke kuomba kila mara"
Mshiriki katika mahitaji ya waumini.
Hili ni jambo la mwisho kwenye orodha inayoanza "Kuhusu mahitaji ya waamini, mshiriki pamoja nao" au "Ikiwa" au "Wakristo wenzako wakiwa na tatizo, musaidie kile wanachohitaji"
Mtafute njia nyingi za kuonesha ukarimu.
"Muwakaribishe nyumbani kwenu ikiwa wanahitaji mahali pa kukaa"
Romans 12:14-16
Muwe na nia moja ninyi kwa ninyi
"Mkubaliane ninyi kwa ninyi" au "muishi kwa umoja ninyi kwa ninyi"
Msifikiri kwa njia ya kujivuna
"Msifikiri kuwa ninyi ni bora sana kuliko wengine"
Muwakubali watu wa hali ya chini
"Wakaribisheni watu mnaoona hawana umuhimu"
Msiwe na hekima juu ya mawazo yenu wenyewe
"Msifikiri kuwa ninyi mna hekima nyingi kuliko mtu yeyote yule"
Romans 12:17-18
Msilipe ovu kwa ovu
"Msifanye yaliyo maovu kwa mtu aliyewafanyia maovu"
Fanyeni mambo mema machoni pa watu wote
"Fanyeni mambo ambayo kila mtu ataona ni mazuri"
Kama ilivyowekwa kwenu, kuweni na amani na watu wote
"Fanyeni lolote mnaloweza kuwa na amani na kila mtu"
Kama ilivyowekwa kwenu
"Kama mnavyoweza kudhibit na ni wajibu kwa"
Romans 12:19-21
Kisasi ni changu; nitalipa
Mistari hii miwili inamaanisha kitu kimoja kwa kusisitiza kwamba Mungu atawalipiza watu wale. "Nitawalipiza ninyi"
Adui yako .... mlishe..... mnyweshe... ukifanya hivi, utakusanya ... Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya
Aina zote za "wewe" au "yako" inamuelezea mtu mmoja.
Lakini adui yako akiwa na njaa.... kichwa chake
Paulo ananukuu sehemu nyingine ya maandiko. "Lakini pia imeandikwa, 'ikiwa adui yako ana njaa... kichwa chake"'
Mlishe
"Mpe chakula"
Kusanya makaa ya moto juu ya kichwa chake
Paulo anafananisha adhabu watakayoipata maadui na kaa la moto linalowekwa kwenye vichwa vyao. maana nyingine zaweza kuwa 1)"kumfanya mtu aliyekuumiza kujisikia vibaya kwa namna alivyokutendea" au 2) "Kumpa Mungu sababu ya kuwahukumu adui zako vibaya zaidi"
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema
Paulo anauelezea "ubaya" kama kitu kinachoishi. "Msiwaache waliowaovu wawashinde, ila muwashinde kwa kufanya yaliyo mema."
Romans 13
Romans 13:1-2
Sentensi unganishi
Paulo anawaambia waamini jinsi ya kuishi chini ya watawala wao.
Na kila nafsi iwe tiifu
"Kila mkristo anapaswa kutii"
Mamlaka iliyo juu
"Watawala wa srikali."
Kwa ajili ya
"Kwa sababu"
Hakuna mamlaka isipokuwa inatoka kwa Mungu
"Mamlaka yote yatoka kwa Mungu"
Mamlaka iliyopo imewekwa na Mungu
"Watu walio katika mamlaka wapo kwa sababu Mungu amewaweka pale"
Mamlaka hiyo
"Hiyo mamlaka ya kiserikali"
Wale waipingao
" Wale wanaopinga mamlaka ya kiserikali"
Romans 13:3-5
Kwa kuwa
Paulo anaeleza nini kitatokea ikiwa serikali itamtia hatiani mtu.
Watawala si watu wa kuogofya
Watawala hawafanyi watu waogope.
Kwa mema... kwa maovu
Watu hutambulika kwa " matendo yao mema" au " matendo yao mabaya"
Je unatamani kuwa mwenye kuogopa mamlaka
"Ngoja nikueleze jinsi ya kuogopa mamlaka"
Utasifiwa kutokana na hiyo
Serikali itasema mambo mazuri juu ya wale watendao mema.
Habebi upanga bila sababu
"Anabeba upanga kwa sababu iliyo njema" au " anauwezo wa kuwaadhibu watu, na atawaadhibu watu."
Mlipakisasi kwa gadhabu
" Mtu anaye adhibu watu kama maelezo ya hasira ya serokali dhidi ya maasi"
Si tu kwa sababu ya gadhabu, lakini pia kwa sababu ya dhamiri.
"Siyo tu kwamba serikali haitawaadhibu, bali pia utakuwa na dhamiri safi mbele za Mungu"
Romans 13:6-7
Kwa sababuya hili
"Kwa sababu serikali huwaadhibu watenda maovu"
Wewe ... lipa kwa kila mtu
Paulo hapa anawambia waamini.
Kwa
" Hii ni sababu kwa nini unapaswa kulipa kodi"
Hudumia
"Toa huduma" au "fanya kazi"
Ushuru
Hii inamaanisha fedha unayolipa kw aajili ya ushuru.
Romans 13:8-10
Senensi unganishi
Paulo anawaambia waamini jinsi ya kufanya kwa majirani.
Usidaiwe na mtu kitu chochote
"Lipa unachodaiwa na serikali na kila mtu yeyote"
Usidaiwe
Tendo hili liko katika hali ya u wingi na linawahusu waamini wote wa Rumi.
Upendo
Hii ina maanisha upendo ambao unatoka kwa Mungu ambao unaelekeza mazuri kwa wengine, hata kama haimfaidii mtu mwenyewe.
Isipokuwa
Sentensi mpya: " Kuwapenda wakristo wengine ni deni moja ambalo unaweza kuendelea kudaiwa"
Uta
Mahali popote palipo na neno "uta" katika 13:9 ni katika hali ya umoja, ingawa mwandishi alikuwa akiwaambia kundi la watu kana kwamba alikuwa mtu mmoja, kwa hiyo unaweza kutumia neno lenye kuonesha u wingi hapa.
Tamani
Kutamani kuwa au kumiliki kitu fulani ambacho mtu hana na asingeweza kuwa nacho au kumiliki.
Upendo haudhuru
Sentensi hii inaonesha upendo kama mtu aliye mwema kwa watu wengine. " Watu wanao penda wenzao hawawezi kuwadhuru."
Kwahiyo
"Kwa sababu upendo haudhuru jirani wa mtu"
Romans 13:11-12
Usiku umeendelea sana
" Wakati uliopo wa dhambi umekaribia kumalizika"
Siku imekaribia
"Kristo atarudi upesi"
Matendo ya giza
Haya ni matendo maovu ambayo watu wanpendelea kuyafanya usiku, wakati hakuna mtu anaye weza kuwaona.
Tuvae silaha za nuru
" Inatupasa kumruhusu Mungu kutulinda kwa kufanya tu yale ambayo tunataka watu waone tunayafanya"
Romans 13:13-14
Nasi tu...
Paulo anajumlisha wasomaji wake na waamini wengine pamoja na yeye mwenyewe.
Kama katika siku
"Katika hali ya kuonekana" au tukijua kuwa kila mtu anaweza kutuona"
Ugomvi
Hii inamaanisha njama dhidi ya na mabishano na watu wengine.
Wivu
Hii inamaanisha hisia hasi ya mtu dhidi ya mafanikio ya mtu mwingine au faida juu ya mtu mwingine
Mvae Bwana Yesu Kristo
Hii inamaanisha kukubali asili mema ya Kristo kana kwamba ni vazi letu la juu ambalo watu wanaweza kuona.
Vaa
Kama lugha yako ina usemi wa wingi wa maagizo, unaweza kutumia hapa.
Usitoe mwanya kwa mwili
"Usiupe nafasi yoyote moyo wako wa zamani kufanya mambo mabaya"
Mwili
Hapa inamaanisha asili ya dhambi ya mtu.
Romans 14
Romans 14:1-2
Sentensi unganishi
Paulo anawatia moyo waamini kukumbuka kuwa wana wajibika kwa mungu.
Wadhaifu katika imani
Hii inamaanisha wale ambao waliona hatia juu ya kula na kunywa vitu kadha wa kadha.
Bila kutoa hukumu kwa maswali hayo
"Na msiwalaumu kutokana na maoni yao"
Kwa upande mmoja, mtu mmoja anaimani kula chochote, bali kwa upande mwingine
Sentensi "Kwa upande mmoja" na "kwa upande mwingine" inatambulisha njia mbili tofauti za kuwaza juu ya kitu fulani. " Mtu mmoja ana imani kula kitu chochote lakini"
Romans 14:3-4
Wewe ni nani, wewe unaye hukumu mtumishi ambaye ni mali ya mtu mwingine?
Paulo anatumia swali kukemea wale wanao hukumu wengine. " wewe si Mungu, na hunaruhusa ya kuhukumu mojawapo wa watumishi wake"
Wewe, wewe
U-moja
Ni mbele ya bwana wake kuwa anasimama au kuanguka
"Ni bwana wake tu anaweza kuamua ikiwa atamkubali mtumishi au atamkataa"
Lakini atamfanya asimame, kwa kuwa Bwana ana uwezo wa kumsimamisha.
"Lakini Bwana atamkubali kwa sababu anauwezo wa kumfanya mtumishi akubalike"
Romans 14:5-6
Kwa upande mmoja, mtu huthamini siku moja kuliko nyingine. kwa upande mwingine, mtu huthamini sikuzote sawasawa.
Sentensi "kwa upande mmoja na kwa upande mwingine" vinatambulisha njia mbili za kufikiri juu ya kitu. " Mtu mmoja anafikiri siku moja ni ya muhimu kuliko zingine zote, lakini mtu mwingine anafikiri kwamba siku zote ni sawa"
Acha kila mtu ashawishike ndani ya fikra zake
Maana halisi inaweza kuelezwa. "ila mtu awe na uhaika wa kuwa anachofanya anamheshimu Mungu"
Yule ashikaye siku, anashika kwa ajili ya Bwana
"Mtu anaye abudu katika siku fulani hufanya kwa kumtii Bwana"
Na yule alaye, anakula kwa ajili ya Bwana
"Kila mtu anaye kula aina zote za chakula hufanya hivyo kwa ajili ya kumtii Bwana"
Yeye asiye kula, hujizuia kutokula kwa ajili ya Bwana
" Mtu asiye kula baadhi ya vyakula anafanya hivyo kwa ajili ya Bwana"
Romans 14:7-9
Sisi
Paulo anajumlisha wasomaji wake.
Wafu na wanaoishi
"Wale waliokufa na wale ambao wanaishi
Romans 14:10-11
Kwa nini unamuhukumu ndugu yako? Na wewe kwa nini unamdharau ndugu yako?
Paulo anaeleza jinsi ambavyo anaweza kuwakemea miongoni mwa wale wasomaji wake. "Ni vibaya kwako kumhukumu ndugu yako, na ni vibaya kwako kumdharau ndugu yako!" au " Usimuhukumu na kumdharau ndugu yako!"
Kwa sababu sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu
"Kiti cha hukumu"kinaashiria mamlaka ya Mungu ya kuhukumu. kwa kuwa Mungu atatuhukumu sisi sote"
Kama niishivyo
Sentensi hii inatumika kuanzisha kiapo au kiapo makini. "Unaweza kuwa na uhakika kuwa hii ni kweli"
Kwangu mimi kila goti litapigwa, na kila ulimi utatoa sifa kwa Mungu
Paulo anatumia maneno "Goti" na "ulimi" kumaanisha mtu. Pia,Bwana anatumia neno "Mungu" kumaanisha yeyemwenyewe. " Kila mtu atainama na kutoa sifa kwangu"
Romans 14:12-13
Atatoa hesabu yake kwa Mungu
"atatoa maelezo ya matendo yetu kwa Mungu
Lkini badala yake amua hivi, kwamba hakuna mtu atakaye weka kitu cha kujikwaa au mtego kwa ndugu yake
Hapa "kitu cha kujikwaa" na "mtego" inamaanisha kitu kilekile. " Lakini fanya kuwa lengo lako kutofanya au kusema neno lolote ambalo linaweza kumfanya mwamini mwenzako kufanya dhambi"
Ndugu
Hapa hii inamaanisha mwamini mwenzako, ikijumuisha wanawake na wanaume.
Romans 14:14-15
Najua na ninashawishika katika Bwana Yesu
Hapa maneno "jua" na " Ninashawishika" yanamaanisha kitu kilekile; Paulo anayatumia kusisitiza uhakika wake. "Nina uhakika kwa sababu ya mahusiano yangu na Bwana Yesu"
Hakuna kilicho safi kwa ajili yake chenyewe
"Kila kitu chenyewe ni safi"
Kwa ajili yake mwenyewe adhaniye kuwa ni safi, kwake yeye si safi
Lakini kama mtu akidhani kuwa kitu fulani si safi, hivyo kwake yeye si safi na anapaswa kuwa mbali nacho"
Ikiwa ni kwa sababu ya chakula ndugu yako anaumia
"Ikiwa utaumiza imani ya mwamini mwenzako kwa mabo ya chakula." hapa neno "yako" linamaanisha imani thabiti na " ndugu" linamaanisha aliye dhaifu katika imani.
Hautembei tena katika upendo
"Hauoneshi tena upendo"
Romans 14:16-17
Usifanye matendo yako mema yakasababisha watu kuwadhihaki
"Usifanye mambo, hatakama unadhani mambo hayo kuwa ni mazuri, ikiwa kama watu watasema ni mabaya"
Matendo yako mema
Hii inamaanisha matendo ya watu ambao ni imara katika imani.
Watu
Maana zaweza kuwa 1. waamini wengine, au 2. wasio amini.
Kwa kuwa ufalme wa Mungu siyo juu ya chakula na vinywaji, bali kwaajili ya haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu
"Kwa kuwa Mungu hakuandaa ufalme wake ili aweze kutawala kile tunacho weza kula na kunywa. aliandaa ufalme wake ili kwamba tuweze kuwa na mahusiano na yeye na Roho Mtakatifu aweze kutupatia amani na furaha"
Romans 14:18-19
Amethibitishwa na watu
"Watu wata mthibitisha" au " watu watamuheshimu"
Tutafute mambo ya amani na mambo ambayo yatawajenga kila mtu na wenzake.
"Tutafute kuishi kwa amani na kusaidia mmoja na mwingine kukua katika imani"
Romans 14:20-21
Si jambo jema kula nyama, wala kunywa divai, wala chochote ambacho ndugu yako anaona ni vibaya
"Ni afadhali usile nyama au kunywa divai au chochote ambacho kinawaza kumsababisha mwenzako afanye dhambi"
Yako
Hii inamaanisha imani thabiti na "Ndugu" inamaanisha ndugu aliye dhaifu.
Romans 14:22-23
Hizi imani ambazo mlizo nazo
Hii inamaanisha imani juu ya vyakula na vinywaji
Wewe mwenyewe
U- moja kwa sababu Paulo anawambia waamini, unaweza kutumia tafsiri ya u-wingi.
wamebarikiwa wale jihukumu katika jambo ambalo anathibitika
"Wamebalikiwa watu ambao hawawezi kuhisi hatia kwa yale wanayo kusudia kufanya"
Ambaye anamashaka amehukumiwa ikiwa atakula
"Mungu atasema kwamba mtu hufanya vibaya ikiwa hana uhakika kama ni sawa kula chakula fulani, lakini hatahivyo anakula" au "Mtu ambaye hana uhakika kama ni sawa kula chakula fulani na anakula atakuwa na shida katika dhamiri"
Kwa sababu haitokani na imani
"Mungu atasema kuwa ni vibaya kwa sababu anakula kitu amabacho anaamini Mungu hataki ale"
Jambo lolote lisilotokana na imani ni dhambi
Unafanya dhambi ikiwa unafanya jambo ambalo huamini kuwa Mungu anataka ulifanye"
Romans 15
Romans 15:1-2
Kauli unganishi
Paulo ana hitimisha hii sehemu kuhusu maisha ya muumini kwa ajili ya wengine kwa kuwakumbusha jinsi Kristo alivyoishi.
Sasa
Tafasri hili kwa kutumia maneno katika lugha yako linalotumika kutambulusha wazo jipya katika mdahalo.
sisi tulio na nguvu
"sisi tulio na nguvu katika imani
Sisi
Kkiwakilishi hiki cha jina kinamwelezea Paulo, wasomaji wake na waumini wengine
dhaifu
"wale ambao ni dhaifu katika imani"
kumwimarisha
Kuimarisha imani yake
Romans 15:3-4
Matusi ya wale waliokutukana yamenipata mimi
"Matusi ya wale waliomtukana Mungu yamempata Kristo pia"
Kwa chochote kilichotangulia kuandikwa, kiliandikwa kwa kutuelekeza
"Kila kitu kilichoandikwa katika maandiko wakati uliopita kiliandikwa kutujulisha sisi"
yetu...sisi
Paulo anawaunganisha wasomaji wake na waumini wengine.
Romans 15:5-7
Kauli Unganishi
Paulo anawatia moyo waumini kukumbuka kwamba wote waumini mataifa na wayahudi ambao wameamini wamefanywa mmoja katika Kristo.
na...Mungu...akupatie
"Omba kwamba...Mungu atakupa.
"kuwa na nia sawa kwa kila mmoja
"kuwa kwenye makubaliano na kila mmoja" au " kuwa na muunganiko"
Kumsifu kwa kinywa kimoja
"kusifu kwa pamoja kama vile ni kinywa kimoja kilikuwa kinaongea"
Romans 15:8-9
Kwakuwa nasema
Neno "Mimi linafafanua juu ya Paulo.
"Kristo amefanywa mtumishi wa tohara
Yesu Kristo alikuja kuwasaidia Wayahudi"
ili kwamba aweze kuthibitisha ahadi walizopewa mababa
"kwamba Mungu aweze kuzithibitisha ahadi alizowapa mababa wa Wayahudi"
kama ilivyoandikwa
"kama ilivyoandikwa kwenye maandiko"
na kwa mataifa
"na Kristo amefanywa mtumishi wa mataifa"
Romans 15:10-11
Tena inasema
"Tena andiko linasema" au Tena Musa anasema"
pamoja na watu wake
"pamoja na watu wa Mungu"
Kumsifu yeye
"Kumsifu Mungu"
Romans 15:12
shina la Yese
Yese alikuwa baba wa kimwili wa Mfalme Daudi. "uzao wa Yese"
Watu wa Mataifa watakuwa na ujasiri ndani yake
"Yeye/yake" hapa inamaanisha uzao wa Yese, ambaye ni Masihi.
Romans 15:13
Mungu wa tumaini
"Mungu, ndani yake tunatumaini"
awajaze na furaha yote na amani
"awajaze na furaha kuu na amani"
muweze kuzidi katika tumaini
"muweze kuwa na tumaini kamilifu"
Romans 15:14
Sentensi unganishi:
Paulo anawakumbusha waumini wa Rumi kwamba Mungu alimchagua ili kuwafikia mataifa kwa injili.
kujazwa na maarifa yote
"kujazwa na elimu ya kutosha katika kumfuata Mungu"
pia kuonyana kila mmoja na mwenzake
"pia kuweza kumfundisha kila mmoja"
Romans 15:15-16
kipawa nilichopewa na Mungu
Kipawa hiki ni kile alichochaguliwa kuwa mtume bila kujali mateso aliyowatendea waumini kipindi cha kuamini kwake. "kipawa ambacho Mungu alinipa"
kujitoa kwa mataifa uweze kukubaliwa
"Mungu anaweza kupendezwa na mataifa iwapo wanamtii yeye"
Romans 15:17-19
Hivyo furaha yangu iko katika Kristo Yesu na katika mambo ya Mungu.
"Kwahiyo nina sababu ya kufurahi katika Kristo Yesu na katika kazi ya Mungu aliyonipa kuitenda"
Haya mambo yametimizwa kwa neno na kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu, na kwa nguvu za Roho mtakatifu
"Kwa ajili ya utii wa mataifa, pekee nitanena kile Kristo ametimiza kupitia kwangu katika maneno na matendo yangu kwa nguvu za ishara na ajabu kupitia nguvu za Roho Mtakatifu."
ishara na maajabu
maneno haya mawili hakika yana maana moja ya miujiza ya namna tofauti tofauti.
ili kwamba kutoka Yerusalemu, na kuzungukia mbali kama Iliriko
Hii ni kutoka mji wa Yerusalemu na umbali kwenda jimbo la Iliriko, mkoa ulio karibu na Italia.
Romans 15:20-21
Kwa njia hii, tamaa yangu imekuwa kuitangaza injili, lakini si mahali Kristo anajulikana kwa jina
"Kwasababu hii, Ninataka huihubiri habari njema katika sehemu ambazo kamwe hazijasikia habari za Kristo"
Ambao kwa yeye hawana habari zake aliyekuja
"Wale ambao hakuna hata mmoja alishawaambia habari zake"
Romans 15:22-23
Sentensi unganishi:
Paulo anawaambia waumini wa Rumi kuhusu mipango yake ya kwenda Yerusalemu na anawaomba waumini kuombea.
Nilikuwa pia nimezuiliwa
Haina umuhimu kumtambua aliyekua amemzuia Paulo. "Walinizuia" au "watu walinizuia"
sina tena sehemu yoyote katika mikoa hii
Paulo anamaanisha kuwa hakuna sehemu katika maeneo haya wanamuishi watu ambapo Injili haijahubiriwa
Romans 15:24-25
katika kupita
"kama na kwenda kupitia Rumi" au "wakati niko safarini"
kufurahia ushirika wenu
"kufurahi kutumia kiasi cha muda pamoja nanyi" au "Kufurahi kuwatembelea"
Hispania
Hili ni jimbo magharibi mwa mji wa Rumi ambapo Paulo alitamani kupatembelea
Romans 15:26-27
Ndiyo, ilikuwa kwa upendo wao
"Waumini wa Makedonia na Akaya walipendezwa kutenda" au "walifurahia kutenda"
hakika wamekuwa wadeni wao
"hakika watu wa Makedonia na Akaya ni wadeni kwa waumini wa Yerusalemu"
ikiwa mataifa wameshiriki katika mambo yao ya kiroho, wanadaiwa na wao pia kuwahudumia
"tangu mataifa wameshiriki mambo ya rohoni na waumini wa Yerusalem, Mataifa wanadai huduma kwa waumini wa Yerusalemu"
Romans 15:28-29
utoshelevu
"Kutimizwa katika usalama"
tunda
Neno hili linazungumzia fedha.
Nitakuja katika utimilifu wa baraka za Kristo.
"Nitakuja na baraka kamilifu za Kristo"
Romans 15:30-32
Sasa
Kama lugha yako ina namna ya kuonyesha Paulo ameacha kuongelea kuhusu mambo mazuri ana tumaini. Na sasa anaanza kuzungumzia juu ya hatari anayokutana nayo, itumie hapa.
Ninawasihi
"Ninawatia moyo"
ndugu
"Hapa ina maana ya kujumuisha waumini wote wa kiume na wa kike.
shiriki
"tenda kwa bidii" au "hangaika"
kuokolewa
"Kuokolewa toka hatari" au "kulindwa"
Romans 15:33
na Mungu wa amani
"Mungu wa amani" inamaanisha Mungu anayewafanya walioamini wawe na amani thabiti.
Romans 16
Romans 16:1-2
Kauli unganishi
Kisha Paulo anasalimia waumini walio wengi huko Rumi kwa kutaja majina
Namkabidhi kwenu Fibi
"Nawaomba mumheshimu Fibi"
Fibi
Hili ni jina la mwanamke
dada yetu
Neno hili linamwelezea Paulo na waumin9 wote. "Dada yetu katika Kristo"
Kenkrea
Hii ilikuwa ni bandari ya mji wa Giriki.
Mpokee katika Bwana
"Mkaribisheni kwasababu sisi sote tumemilikiwa na Bwana"
Katika kicho cha thamani cha waumini
" katika njia ambayo waumini wangeweza kukaribisha waumini wengine"
simama pamoja naye
"Mmusaidie"
amekuwa mhudumu wa wengi na wangu mwenywe pia
"amewahudumia watu wengu, na amenisaidia mimi pia"
Romans 16:3-5
Prisila na Akila
Priska anajulikana kama Prisila, alikuwa mke wa Akila
watenda kazi nami katika Kristo Yesu
"Ambaye anatenda kazi na mimi kuwaambia watu habari za Yesu Kristo"
lisalimie kanisa lililo katika nyumba yao
"Wasalimie waumini ambao hukutana nyumbani mwa nyumba ya Mungu.
Epanieto
Hili ni jina la mwanaume
mzaliwa wa kwanza katika Asia kwa Kristo
kivumishi hiki kinamaanisha kuwa Epanieto alikuwa mtu wa kwanza katika Asia kumwamini Yesu.
Romans 16:6-8
Mariamu
Hili ni jina la Mwanamke.
Yunia
Hili linaweza kuwa 1) Yunia ni jima la mwanamke, au siyo vile, 2) Yunia ni jina la mwanaume.
Anroniko...Ampliato
Haya ni majina ya wanaume.
mpendwa wangu katika Bwana
"rafiki yangu mpendwa na muumini mwenzangu"
ni maarufu miongoni mwa mitume
Hii inaweza kutafasiriwa kama "Mitume wanawafahamu vyema"
Romans 16:9-11
Urbano...Stakisi...Apele...Aristobulo...Herodioni... waliokubaliwa katika Kristo
Haya ni majina wa wanaume.
kukubaliwa katika Kristo
neno "kukubaliwa" linamaanisha kwamba mtu amejaribiwa na kuthibitishwa kuwa mkweli.
walio katika Bwana
hii inamaanisha wale wote walioweka tumaini katika Yesu.
Romans 16:12-14
Turufena...Trifosa...Pesisi
Haya ni majina ya wanawake
Rufio...Asikrito...Flegoni...Heme...Patroba...Hema
Haya ni majina ya wanaume.
aliyechaguliwa katika Bwana
"ambaye Mungu amemchagua" kwasababu ya sifa maalumu.
mama yake na wangu
"mama yake, ambaye namfikiria kama mama yangu"
Romans 16:15-16
Filogo...Neria...Olipa
Haya ni majina ya wanaume.
Yulia
Jina la mwanamke ambaye pengine alikuwa ameolewa na Filologo.
busu takatifu
jinsi ya kuonesha hisia za upendo kwa wumini wenzako
Romans 16:17-18
Kauli unganishi
Paulo anatoa onyo la mwisho kwa waumini kuhusu umoja na kuishi kwa ajili ya Mungu
tafakari juu ya
"kuwa waangalifu kwa"
ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi
"ambao wanasababisha waumini kubishana kila mmoja kwa mwingine na kuacha kuwa na imani kwa Mungu"
Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza
'Wanafundisha mafundisho ambayo hayakubaliani na ukweli mliokwisha jifunza tayari"
Geukeni mtoke kwao
"jitengeni mbali na wao"
bali kwa matumbo yao wenyewe
Hapa "tumbo" linafafanua tamaa za kimwili. "Lakini wanataka kufurahisha tamaa zao mbaya"
Kwa maneno yao laini na pongezi za uongo
Maneno "laini" na "pongezi za uongo" kimsingi yana maana moja. Paulo anafafanua jinzi gani hawa watu wanavyowadanganya waumini. "kwa kusema mambo ambayo yanaonyesha ni mema na ya kweli"
kutokuwa na hatia
"ambao hawana hatia wanawatumainia wao" au "ambao hawawajui hawa waalimu wanaowatia upumbavu"
Romans 16:19-20
Kwa mfano wa utii wenu mwamfikia kila mmoja
"Wakati mnapomtii Yesu kila mmoja husikia hivyo"
Mungu wa amani hatakawia kumwangamiza Shetani chini ya nyayo zenu
Kivumishi "kumwangamiza chini ya nyayo" kinafafanua ushindi kamili juu ya adui. "Mungu hatakawia kukupa amani ya ushindi kamili dhidi ya Shetani"
bila hatia mbele ya uovu
"Bila kuchanganywa katika uovu"
Romans 16:21-22
Kauli unganishi
Paulo anatoa salamu kutoka kwa waumini ambao wako pamoja naye.
Lukio...Yasoni...na Sospeter...Tertio
Haya ni majina ya wanaume.
Tertio
Tertio ndiye mwanaume aliyeandika yale Paulo aliyoyafundisha.
Nawasalimu katika Bwana
"Nawasalimu ndugu waumini katika Bwana"
Romans 16:23-24
Gayo...Erasto...Kato
Haya ni majina ya wanaume
mwenyeji
Inamaanisha waumini waliokutana katika nyumba yake na kuabudu.
mtunza hazina
Huyu mtu ndiye aliyekuwa akitunza fedha ya kikundi.
Romans 16:25-26
Kauli unganishi
Paulo anahitimisha kwa maombi ya baraka
sasa
Neno hili "sasa" linaonyesha kufikia mwisho wa barua.
kufanya msimame
"kufanya imani yenu kuimarika"
kulingana na injili na mafundisho ya Yesu Kristo"
Habari njema ambayo nimeihubiri kuhusu Yesu Kristo
kulingana na ufunuo wa siri iliyofichwa kwa muda mrefu
"Kwa kuwa Mungu ameifunua siri kwetu waumini ambayo alikuwa ameitunza muda mrefu"
Lakini sasa imekwisha funuliwa na kufanywa kujulikana na maandiko ya unabii kulingana na amri ya Mungu wa milele
"Lakini sasa Mungu wa milele ameifanya ijulikane kupitia maandiko"
kwa utii wa imani miongoni mwa mataifa yote
"ili kwamba mataifa yote yatamtii Mungu kwasababu ya imani yao kwake"
Romans 16:27
kwa Mungu pekee mwenye hekima...kuwe na utukufu milele. Amina
Hapa "kupitia Yesu Kristo" kunaeleza kile ambacho Yesu alifanya. Kumpa utukufu kunamaanisha kumpa Mungu sifa.