2 John
2 John 1
2 John 1:1-3
Sentensi Unganishi
Baada ya salamu, Yohana anawaonyesha waumini kuwa upendo na kweli vinakwenda sambamba
Maelezo ya Jumla
Kihistoria mtume Yohana amekubalika kuwa ndiye mwandishi wa barua hii. Anasema "pendaneni" hii pengine barua hii liliandikiwa kanisa.
Maelezo ya Jumla
"ninyi" na "yenu" katika barua hii yanaonyesha wingi
Maelezo ya Jumla
katika barua hii Yohana anatumia maneno "sisi" na 'yetu" ikimaanisha Yohana mwenyewe pamoja na wasomaji wake
Kutoka kwa mzee kwenda kwa mwanamke mteule na watoto wake
Barua za wakati huo zilianza na jina la mwandishi, kwa kushupisha inaweza kusomeka:- " mimi, Yohana mzee, ninaandika barua hii kwa mwanamke mteule na watoto wake"
Mzee
Ni rejea kwa Yohana, mtume na mwanafunzi wa Yesu. Anajiita mzee labda kwa sababu ya umri wake mkubwa au kwa sababu ni kiongozi kanisani.
kwa mwanamke mteule na watoto wake
Pengine hii ina maana ya kundi au kusanyiko na waumini .
ambaye nampenda katika kweli.
" Ninyi watu ninaowapenda katika kweli"
wanao ifahamu kweli
"ambao wanao fahamu ukweli kuhusu Mungu na Yesu"
Baba...Mwana
Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu
katika kweli na upendo.
Neno "kweli" linaelezea "upendo." Pengine inamaanisha "katika upendo wa kweli"
2 John 1:4-6
...wewe, mwanamke, nakuandikia
Ni maneno ambayo yametumiwa katika hali ya umoja.
kama vile tu tulivyoipokea amri hii kutoka kwa Baba
"Kama vile Mungu Baba alivyo tuagiaza"
siyo kwamba nakuandikia amri mpya
" siyo kwamba nakuagiza kufanya jambo jipya"
bali ile tuliyokuwa nayo tokea mwanzo
Hapa neno "mwanzo" inamaanisha " tulipoamini kwa mara ya kwanza" kwa maneno mengine:- " lakini nawaandikia kama tulivyoagizwa na Kristo kufanya tulipoamini mara ya kwanza."
tunapaswa kupendana sisi kwa sisi.
Hii inaweza kutafisiriwa kama sentensi mpya: "Na alitupa amri kwamba tunapaswa kupendana."
Hii ndiyo ile amri, kama mlivyoisikia tokea mwanzo, kwamba mnapaswa kuenenda katika hiyo.
" Mungu amewaagiza tangu mwanzo mlipoamini mpendane"
2 John 1:7-8
Sentensi Unganishi
Yohana anawaonya kuhusu wazushi, na kuwakumbusha kubaki katika mafundisho ya Kristo na kujiepusha na waasi
Kwa kuwa wadanganyifu wengi wamesambaa katika ulimwengu.
"Walimu wengi wa uongo wamekwisha liacha kusanyiko" au " wadanganyifu wengi wapo ulimwenguni"
wadanganyifu wengi.
"walimu wengi wa uongo" au "wazushi"
katika ulimwengu
Hapa inaelezea kila mtu aliyeko hai katika ulimwengu huu.
Yesu Kristo alikuja katika mwili.
"Yesu alikuja katika hali ya mwili wa kibinadamu."
Huyu ndiye mdanganyifu na mpinga Kristo
" Ni wale wanaowadanganya wengine na kumpinga Kristo mwenyewe"
mpinga Kristo.
" kinyume na Kristo"
Jiangalieni wenyewe.
"Iweni macho" au " iweni waangalifu."
hampotezi mambo
"kutopoteza tuzo zenu za wakati ujao kule mbinguni."
tuzo kamili
"tuzokamili kule mbinguni"
2 John 1:9-11
Yeyote aendeleae mbele
Hii inaonyesha mtu anaye dai kufahamu zaidi juu ya Mungu na ukweli kuliko mtu yeyote "Yeyote anayesema kuwa anafahamu zaidi kuhusu Mungu." au " Yeyote anayeikana kweli"
hana Mungu
" si mali ya Mungu"
Yeye adumuye katika fundisho anaye Baba na Mwana
"Wale wanaofuata mafundish ya Kristo ni mali ya Baba na Mwana"
Baba na Mwana
Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu
msimkaribishe katika nyumba zenu
Hapa ina maanisha kumkaribisha na kumtendea heshima ili kujenga uhusiano na naye.
hushiriki katika matendo yake maovu
" Hushiriki naye katika matendo yake ya uovu" au" humsaidia katika matendo yake maovu."
2 John 1:12-13
Sentensi Unganishi
Yohana anamalizia barua yake kwa kuonyesha shauku ya kuwatembelea na anatoa salamu kutoka kanisa jingine
Maelezo ya Jumla
Maneno "kwako" yanaonyesha umoja katika mstari wa 12. Neno "yenu" linaonyesha wingi mstari wa 13
sikutaka kuyaandika kwa karatasi na wino
Yohana hakutaka kuyaandika mambo mengi lakini alitaka kuja kuongea nao ana kwa ana.
Watoto wa dada yenu mteule
Yohana anazungumza habari ya kanisa jingine kana kwamba ni dada kwa kanisa analowaandikia na waumini wa kanisa hilo anawafananisha na watoto. Hapa inasisistiza kwamba waumini wote ni familia ya kiroho.