2 Thessalonians
2 Thessalonians 1
2 Thessalonians 1:1-2
Maelezo ya Jumla:
Paulo ndiye mwandishi wa barua hii, lakini anawajumuisha Silwano na Timotheo kama wapelekwaji wa barua. Anaanza kwa kusalimia kanisa la Thesalonike.
Maelezo ya Jumla:
Maneno "sisi" linamaanisha Paulo, Silwano naTimotheo, au kama limetumika vinginevyo. Pia neno " ninyi" ni wingi na lina maanisha waumini wa kanisa la Wathesalonike.
Silwano
Huu ni muundo wa Kilatini "Silas." Ni mtu yule yule aliyeorodheshwa katika kitabu cha Matendo kama msafiri mwenzi wa Paulo.
Neema iwe juu yenu
Paulo kawaida anatumia salamu hii katika barua zake.
2 Thessalonians 1:3-5
Maelezo ya Jumla:
Paulo anatoa shukrani kwa ajili ya waumini katika kanisa la Thesalonike.
kupaswa kutoa shukrani kwa Mungu
Paulo anasema anapaswa kumshukuru Mungu mara kwa mara.
ndugu
Hapa "ndugu" inamaanisha Wakristo wenzetu, ikijumuisha wanaume kwa wanawake.
Hivi ndivyo ipasavyo
"kwa kuwa hiki ni kitu sahihi cha kufanya" au " ni vyema"
Upendo ambao kwa kila mmoja amefungamanishwa na mwenzake
"mnapendana nyinyi kwa nyinyi"
kila mtu na mwenzake
Kila mtu na mwenzake lina maanisha Wakristo wenzetu."
sisi wenyewe
Hapa "wenyewe" limetumika kusisitiza kujisifu kwa Paulo.
kwamba mpate kuhesabiwa kuwa mnastahili kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Hii inakwemwa katika muundo tendaji. AT: "kwamba Mungu atawahesu kuwa wa sehemu ya ufalme wa Mungu."
2 Thessalonians 1:6-8
Sentensi Unganishi:
Paulo anapoendelea, anaoongea kuhusu Mungu kuwa mwenye haki.
ni haki kwa Mungu
"Mungu yuko sahihi" au "Mungu ni wa haki"
na raha kwenu
Unaweza kuifafanua kwamba Mungu ndiye arudishae raha. AT:" na kwamba Mungu arudishe raha kwenu."
malaika wa nguvu zake
"Malaika wa Mungu wenye nguvu"
Katika mwali wa moto atalipiza kisasi kwa wale wasiomjua Mungu na wale
"Bwana Yesu atawaadhibu kwa mwali wa moto wale wasiomjua Mungu na wale" au "Kisha kwa mwali wa moto atawaadhibu wale wote wasiomjua Mungu na wote ambao hawamtii Bwana Yesu" (UDB)
2 Thessalonians 1:9-10
watateseka
Neno "wataseka" wanamaanishwa watu wasioitii injili.
atakapokuja sike ile
Hapa "siku ile" ni siku Yesu atakaporudi duniani.
ili atukuzwe na watakatifu wake
Hii inaweza kusemwa katika hali halisi. AT: "watu wake waliomwamini watamtukuza "
watastaajabishwa na wale wote walioamini
Hii inaweza kuwa katika hali tendaji. "wale wote walioamini watashangaa" au "wale wote walioamini watamshangaa yeye"
2 Thessalonians 1:11-12
Pia tunaendelea kuomba kwa ajili yenu
Paulo anasisitiza jinsi anavyoomba mara nyingi kwa ajili yao. AT: Pia mara kwa mara tunaomba kwa ajili yenu.
kuita
Neno "kuita" lina maanisha Mungu anateua au anachagua watu kuwa watoto wake, kuwa watumishi wake na wahubiri wa ujumbe wa wokovu kwa njia ya Yesu.
kutimiza kila haja ya wema
"awawezeshe kufanya mema kwa kila namna mnavyo tamani" (UDB)
ili kwamba mpate kulitukuza jina la Bwana wetu Yesu
Hili linaweza kuelelezewa katika muundo tendaji. AT: "ili kwamba mweze kulitukuza jina la Bwana wetu Yesu"
Ili mtukuzwa na yeye
Hili linaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "Yesu atawatukuza ninyi"
kwa sababu ya neema ya Mungu wetu
kwa sababu ya neema ya Mungu"
2 Thessalonians 2
2 Thessalonians 2:1-2
Maelezo ya Jumla:
Paulo anawaasa waumini wasidanganywe kuhusu siku ambayo Yesu atarudi.
Sasa
Neno "Sasa" linaonyesha kubadilika kwa mada katika maelekezo ya Paulo.
Ndugu
Neno "ndugu" linamaanisha Wakristo wenzetu, linajumuisha wote wanaume na wanawake. AT: " kaka na dada"
Kwamba msisumbuliwe au kuhangaishwa kwa urahisi
kwamba msiruhusu mambo yawasumbue kwa urahisi.
kwa ujumbe au barua ambayo inadhaniwa kutoka kwetu
"kwa maneno au barua iliyoandikwa ambayo inadhaniwa kutoka kwetu.
kwa tokeo kwmba
"kusema kwamba'
siku ya Bwana
Hii inamaanisha wakati atakaporudi duniani kwa ajili ya waumini.
2 Thessalonians 2:3-4
Maelezo ya Jumla:
Paulo anafundisha kuhusu mtu wa uasi.
haitakuja
"siku ya Bwana haitakuja"
anguko
hii inamaanisha wakati ujao ambao watu wengi watampa Mungu kisogo.
na mwana wa uasi amefuniuliwa
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: na Mungu anamfunua mtu wa uasi
mwana wa uaharibifu
Paulo anaongea uharibifu kama mtu alizaa mwana ambaye lengo lake ni kuharibu kila kitu. AT: "yeye aharibuye kila kitu anachoweza"
vyote vinavyoitwa Mungu au vivavyoabudiwa
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "kila kitu ambacho watu hukifanya kuwa Mungu au kila kitu ambacho watu huabudu"
anajiinua mwenyewe kama Mungu
"anajionyesha mwenyewe kama Mungu"
2 Thessalonians 2:5-7
Hamuyakumbuki...mambo haya?
Paulo anatumiwa swali lisilohitaji kujibiwa kuwakumbusha mafundisho ambayo aliwafundisha awali alipokuwa nao. Hii inaweza kuelezewa kama. AT: " Ninauahakika kuwa mnakumbuka... haya mambo."
mambo haya
Hii ina maanisha kurudi kwa Yesu, siku ya Bwana , na mtu wa kuasi.
atafunuliwa tu kwa wakati muafaka
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "Mungu atamfunua mtu wa uasi kwa muafaka"
siri ya kuasi
Hii ina maanisha kwa siri ambayo Mungu mwenyewe anaifahamu.
anayemzuia
kumzuia mtu ni kuwashikilia nyuma au hali kutowafanya kuendelea na kile wanachotaka kufanya.
2 Thessalonians 2:8-10
ndipo mwenye kuasi atakapofunuliwa
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: Halafu Mungu atamruhusu mwenye kuasi ili kujionyesha mwenyewe.
kwa pumzi ya kinywa chake
Hapa neno "pumzi" linamaanisha nguvu ya Mungu. AT: "kwa nguvu ya neno lake lilotamkwa"
Ufunuo wa kuja kwake utamfanya kuwa sio chochote
Wakati Yesu atakaporudi duniani na kujionyesha, atamshinda yule mwenye kuasi.
kwa nguvu zote, ishara, na maajabu ya uongo
"kwa nguvu zote, ishara, na maajabu ya uongo"
na uongo wote wenye udharimu
Mtu huyu ataumia kila aina ya ubaya kuwadanganyawatu ili wamwamini yeye badala ya Mungu.
Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea
Huyu mtu atapewa nguvu na shetani na atadanganya kila mtu ambaye hakuamini katika Yesu.
wanaopotea
Hapa "potea" lina wazo la milele au uangamivu wa milele
2 Thessalonians 2:11-12
Kwa sababu hii
" Kwa sababu watu hawapendi kweli"
Mungu anawatumia kazi yenye uongo ili waamini uongo
Paulo anaongea kuwa Mungu anaruhusu kitu kutokea kwa watu kana kwamba anawatumia. AT: "Mungu anaruhusu mtu wa kuasi awadanganye"
wote watahukumiwa
Hii inaaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT:" Mungu atawahukumu wote"
wale ambao hawakuamini kweli badala yake wakajifurahisha katika udhalimu
"wale ambao walifurahia udhalimu kwa sababu hawakuiamini kweli"
2 Thessalonians 2:13-15
Sentence Unganishi
Paulo sasa anabadilisha mada.
Maelezo ya Ujumla:
Paulo anatoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya wakristo na anawatia moyo.
Lakini
Paulo anatumia neno hili hapa kuanzisha kubadili mada.
inatupasa kumshukuru Mungu wakati wote
Hii ni hali ya kukuza tukio au jambo la kawaida na kulifanya kuwa kubwa zaidi kuliko uhalisia wake. AT: "tunapaswa kuendelea kutoa shukrani"
tunapaswa
Neno tunapaswa linamaanisha Paulo, Silwano, na Timotheo.
ndugu mpendwao na Bwana
Hili linaweza kulezwa katika muundo tendaji. AT: "kwa kuwa ndugu Bwana anawapenda"
ndugu
Hapa "ndugu" linamaanisha wakristo wenzangu, inajuisha wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike.
malimbuko kwa ajili ya wokovu
"kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuamini katika Yesu na kuokolewa.
katika utakaso wa Roho
"na kuwatenga ninyi kwa ajili ajili yake kwa njia ya Roho"
imani katika kweli
"kuamini katika kweli" au "kuwa na ujasiri katika kweli"
kwa hiyo, ndugu, simameni imara
Paulo anawaasa waumini waendelee kushikilia imani yao katika Yesu.
elewa tamaduni
hapa "tamaduni" linamanisha kwa ukweli wa Kristo ambao Paulo na mitume walifundisha. Paulo anaongea nao kana kwamba wasomaji wake wangeweza kushika neno kwa mikono yao.
uliyofundishwa
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: tuliyowafundisha"
iwe kwa neno au kwa barua yetu
unaeza kuelezea kwa timilifu zaidi habari. AT: "iwe kwa kile tulichowafundisha gerezani au kile tulichowandikieni kwa barua"
2 Thessalonians 2:16-17
Sentensi Unganishi:
Paulo anamaliza na baraka kutoka kwa Mungu.
Sasa
Paulo anatumia neno hili kuonyesha badiliko la mada.
Bwana wetu ...aliyetupenda na kutupatia
Neno hili "aliyetupenda" na "sisi" linajumisha waumini wote.
Bwana Yesu Kristo mwenyewe
Neno "yeye mwenyewe" liongeza msisitizo kwa neno "Bwana Yesu Kristo."
awafariji na kuifanya imaramioyo yenu
"mioyo" linamaanisha kwenye sehemu ya hisia. AT: "awafariji na kuwaimarisheni kwa"
2 Thessalonians 3
2 Thessalonians 3:1-3
Maelezo ya Jumla:
Paulo anawaomba waumini waombe kwa ajili yake na wenzake
Na sasa
Paulo anatumia neno "sasa" kubadilisha mada.
ndugu
hapa neno "ndugu" linamaanisha wakristo wenzetu, linajumisha wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike"
neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa
Paulo anaongea kutawanya kana kwamba Neno la Mungu linakimbia toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. AT: "kwamba watu wengi zaidi na zaidi hivi karibuni watasikia ujumbe wetu kuhusu Bwana wetu Yesu na kuuheshimu"
kwamba tuweze kuokolea
Hili linaweza kusemwa katika muundo tendaji: AT: "kwamba Mungu atuokoe" au " kwamba Mungu aweze kutuokoa sisi"
Kwa sababu sio wote wanayo imani
"kwa kuwa watu wengi hawaamini katika Yesu"
ambaye atawaimarisha ninhyi
"ambaye atawaimarisha ninyi"
yule mwovu
"Shetani"
2 Thessalonians 3:4-5
Tunao ujasiri
' Tunayo imani" au "tunaamini"
kuongoza mioyo yenu
Paulo anamwelezea Bwana kuwahamasishaWakristo wampende Mungu kana kwamba Bwana alikuwa akiwaongoza katika njia
mioyo
Hii ni sitiari kwa ajili ya hisia au takwa, ambayo inaongoza upendo na uaminifu.
kwa upendo wa Mungu na kwa uvumilivu wa Kristo
paulo anaongea upendo wa Mungu na uvumilivu wa Mungu na Kristo kana kwamba kulikuwa na mwisho katika njia. AT:Ni namna gani gani Mungu anawapenda na jinsi gani ambayo Kristo alivyovumilia kwa ajili yetu.
2 Thessalonians 3:6-9
Maelezo ya Jumla:
Paulo anawapa waumini maelekezo ya mwisho kuhusu kufanya kazi na sio kukaa bila kufanya kazi.
Sasa
Paulo anatumia neno hili kuonyesha kubadili mada.
katika jina la Bwana Yesu Kristo
"kwa mamlaka ya Yesu"
ndugu
hapa "ndugu" linamaanisha wakristo wenzetu, inajumuisha wote wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike"
Bwana wetu
Neno "wetu" linamaanisha waumini wote.
kuishi bila kufanya kazi
"ni mzembe na anazuia kufanya kazi"
kutuiga sisi
" kufanya kama Paulona wenzake" au " kutenda kama Paulo na watenda kazi wenzake'
Hatukuishi kati yenu kama wale wasio na nidhamu
Paulo anatumia maneno hasi ili kusisitiza maneno chanya. AT: "Tuiishi miongoni mwenu kama waliokuwa na nidhamu sana"
tulifanya kazi usiku na mchana
"tulifanya kazi wakati wa usiku na wakati wa mchana" au "tulifanya kazi muda wote"
katika kazi ngumu na shida
Paulo anasisitizajinsi hali yake ilivyokuwa ngumu. kazi ngumu inamaanisha kazi ambayo inahitaji juhudi kubwa. Ugumu inamaanisha walivumia maumivuna mateso.AT: "katika hali ngumu.
Tulifanya hivi sio kwa sababu hatukuwa ma mamlaka
Paulo anatumia neno hasi kusisitiza upande chanya. Hii inaweza kusemwa kama chanya. AT: "pasina shaka tulikuwa na mamlaka."
2 Thessalonians 3:10-12
baadhi wanaenenda paipo utaratibu
Hapa "enenda" linasimama kwa kumaanishatabia katika maisha. AT: "baadhi wanaishi maisha ya "kubweteka" au "wengine ni wavivu"
lakini badala yake ni watu wanaoenenda pasipo utaratibu.
Hawa nia watu wanaoingilia mambo ya wengine pasipo kuombwa kufanya hivyo.
kwa utulivu
"katika utulivu, amani utulivu." Paulo anawaasa watu wazembe waiotaka kufanya kazi waache kuchunguza mambo ya wenzao."
2 Thessalonians 3:13-15
Lakini
Paulo anatumia neno hili kutofautisha kati ya wakristo wavivu na wachapakazi.
ninyi, ndugu
Neno "niny" linamaanisha wakristo wote wa Thesalonike.
ndugu
Neno "ndugu" hapa linamaanisha wakristo wenzangu, inajumuisha wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike"
msizimie roho
"Kuzimia moyo" ni neno linalomaanisha kuchoka, au kukata tama." "msikate tamaa au "msichoke"
muwe makini naye
Mmtambue kuwa ni nani.AT: "mmtambue mbele za watu"
ili kwamba aweze kuaibika
Paulo anawaelekeza waumini kujihadhari nawaumini wavivu kama kitendo cha kuwaadibisha.
2 Thessalonians 3:16-18
Maelezo ya Jumla:
Paulo anahitimisha maoni/ ufafanuzi wake wakristo wa Thesalonike.
Bwana wa amani mwenyewe awape ninyi
Unaweza kuweka wazi kuwa haya ni maombi ya Paulo kwa Wathesalonike. AT: "Ninaomba kwamba Bwana wa amani mwenyewe awapeni..."
Bwana wa amani mwenyewe
"Mwenyewe" inaelezea kwamba Bwana mwenyewe atawapa amani wakristo.
Hii ni salamu yangu mwenyewe, Paulo, kwa mikono yangu mwenyewe
"Mimi, Paulo, naandika salamu kwa mkono wangu mwenyewe"
Hivi ndivyo niandikavyo
Paul anaweka wazi kwamba hii barua inatoka kwake na sio ya kubumba