Ephesians
Ephesians 1
Ephesians 1:1-2
Sentensi Unganishi
Majina ya Paulo peke yake kama mwandishi wa hii barua kwa waamini wa kanisa la Efeso
Maelezo ya Jumla
Bila kutajwa vinginevyo, pote palipo na " kwenu" na "Yako" ya husu waamini wa Efeso pamoja na waamini wote na kwa hiyo ni wingi.
Paulo, Mtume ... Kwa watakatifu wa Mungu Efeso
Lugha yako yaweza kuwa na namna ya kumtambulisha mwandishi wa barua na waliokusudiwa. " Mimi, Paulo, Mtume na waandikia hii barua kwenu, watu watakatifu wa Mungu Efeso.
Walio waaminifu katika Kristo
"Katika Kristo Yesu" na misemo kama hiyo ni mifano inayo jitokeza kwenye barua za agano jipya. Zinaeleza mahusiano madhubuti sana kati ya Kristo na ao wanao mwamini.
Neema kwenu na amani.
Hii ni salamu zoefu na baraka ambayo Paulo utumia kwenye barua zake.
Ephesians 1:3-4
Sentensi unganishi
Paulo anafungua barua kwa kuongea kuhusu nafasi ya waamini na usalama wao mbele za Mungu.
Maelezo ya Jumla
Katika hiki kitabu, vinginevyo kuelezwa, maneno "sisi" na "wote" ya husu Paulo, waamini wa Efeso, na waamini wote.
Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa.
'Hii pia yaweza ekwa hali tendaji. " Acha tumsifu Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Aliyetubariki
"kwa kuwa Mungu ameyubariki sisi"
Kila baraka za rohoni
"Kila baraka zinakuja kutoka katika Roho wa Mungu"
Katika maeneo ya bingu
"katika ulimwengu wa roho". Neno "bingu" la husu mahali Mungu alipo.
Ndani ya Yesu
"Ndani ya Yesu " sawa na maelezo ambayo ni mafumbo kila mara hutokea kwenye barua za Agano jipya. Zinaeleza aina ya mahusiano mazito yanayowezekana kati Kristo na wote wanaomwamini.
Tuwe watakatifu na tusiwe na lawama
Paulo anatumia maneno mawili yenye kufanana akisisitiza uadilifu.
Ephesians 1:5-6
Maelezo ya Jumla
Maneno "wake", "Yeye", na "yeye" yamuhusu Mungu.
Mungu ametutangazia sisi kuwa warithi wake
Neno' sisi' linamhusu Paulo, Kanisa la Efeso, na waamini wote ndani ya Kristo."Mungu alipanga muda mrefu kuturithi."
Kuwa urithi
Hapa " warithi" inahusu kuwekwa ndani ya familia ya Mungu.
Kupitia Yesu Kristo
Mungu aliwaleta waamini kwenye familia yake kupitia kazi ya Yesu Kristo.
Mpendwa wake wa kipekee
"Mpendwa wake pekee, Yesu Kristo" au "Mwanae, anaye mpenda"
Ephesians 1:7-8
Kwa mwana wake wa kipekee
"kwa mwana wa Mungu wa kipekee, Yesu Kristo"
Utajiri wa neema yake
Paulo anazungumzia neema ya Mungu kana kwamba ilikuwa ni vitu vya thamani: "ukuu wa neema ya Mungu" au "kushikamana na neema ya Mungu"
Ametumwagia hii neema kwa sana
"Ametupa sisi hiki kiasi kikubwa cha neema" au " Amekuwa mkarimu sana kwetu"
katika hekima na ufahamu
Yamkini tafsiri zilizopo ni 1) "sababu anayo hekima zote na ufahamu" 2) "ilituwe na hekima kubwa na ufahamu"
Ephesians 1:9-10
kwa kadiri ya alivyo pendezwa
Yamkini tafsiri zilizopo ni 1) "sababu alitaka kutufahamisha" au 2) " ndivyo alivyo taka"
na aliyo ionyesha katika Kristo
"na alionyesha kusudi hili ndani ya Kristo
katika Kristo
"kwa njia ya Kristo"
kwa lengo la kuwa na mpango
Sentensi mpya ya weza anza hapa. " Alifanya hivi kwa lengo la kuwa na mpango" au "Alifanya hivi, akifikiria kuhusu mpango.
kwa wakati timilifu
"Kwa kuwa wakati ukiwa mwafaka" au "kwa wakati aliyo uteuwa"
Ephesians 1:11-12
Tulichaguliwa kuwa warithi
Hii yaweza nenwa kama kauli tendaji. "Mungu ametuchagua sisi kuwa warithi"
Tumechaguliwa... ni sisi ambao ni wa kwanza
"Mungu alituchagua hapo awali"
Ili kwamba tuwe wa kwanza
Hapa neno "sisi" la husu wa Yahudi waamini walio sikia habari njema, sio waamini wa Efeso.
Ili kwamba tuwe sifa za utukufu wake
"ili kwamba tuishi kumsifu kwa utukufu wake.
Ephesians 1:13-14
Tumetiwa mhuri na ahadi ya Roho Mtakatifu
Nta ilikuwa ya wekwa kwenye barua na kuchapwa na alama inayowakilisha nani katuma barua. Paulo anatumia huu utamaduni kutuonyesha picha jinsi gani Mungu amemtumia Roho Mtakatifu kutu hakikishia kwa sisi ni wake. "Mungu aliweka mhuri wokovu wetu na Roho Mtakatifu akionyesha umiliki wake."
Dhamana ya urithi wetu
Kupokea ahadi ya Mungu ya zungumziwa hapa kama vile mtu anavyo rithi mali au utajiri kutoka katika familia. "ahadi ya kuwa tutapokea kile ambacho Mungu ametuahidi"
Ephesians 1:15-16
Sentensi unganishi
Paulo anaomba kwa ajili ya waamini wa Efeso na anamsifu Mungu kwa ajili ya nguvu waliyo nayo kupitia Kristo.
Sijaacha kumsifu Mungu
Paulo anatumia "sijaacha" kusisitiza kuwa anaendelea kumsifu Mungu. "Naendelea kumshukuru Mungu"
Ephesians 1:17-18
roho ya hekima na mafunuo ya ufahamu wake
":hekima ya kiroho ya kufahamu mafunuo yake"
macho yenu ya moyoni yatiwe nuru
"kipengele macho ya rohoni "inaelezea uwezo wa mtu kupata ufahamu.'kwamba upate ufahamu na kutiwa nuru."
macho yenu ya moyoni yatiwe nuru
Hii yawezwa tajwa kama njeo tendaji. Ili Mungu awatie nuru mioyo yenu" au "kwamba Mungu awatie nuru ufahamu wenu"
kutiwa nuru
"kufanywa kuona"
urithi
Kupokea kile ambacho Mungu amewaahidi waamini, ya elezewa kana kwamba mtu anarithi mali na utajiri kutoka kwa nduguye wa familia.
watakatifu wote wa Mungu
Hii yawezwa tajwa kama njeo tendaji. "Wote wale ambao amewatenga kwa ajili yake" au "wote wale ambao ni wake kabisa"
Ephesians 1:19-21
ukuu uzidio wa nguvu yake
Nguve za Mungu za pita sana nguvu zingine.
ndani yetu
"kwa faida yetu" au "kwa uhusiano nasi"
kufanya kazi katika nguvu zake
"nguvu yake kubwa ambayo ya fanya kazi ndani yetu"
alimfufua kutoka kwa wafu
"alimfufua kutoka kwa wafu" au "alimfanya kuishi tena"
kumketisha katika mkono wake wa kuume
"Kristo aliye keti mkono wa kuume wa Mungu" au "kristo aliye keti sehemu ya adhama"
mahali pa mbingu
"katika ulimwengu wa roho". Neno "mbingu" la husu sehemu Mungu alipo. Ona jinsi illivyo tafsiriwa katika 1:3
juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi
Hii ni misemo tofauti ya matabaka ya viumbe wa rohoni, kwa malaika na mapepo. " mbali zaidi ya aina tofauti za viumbe wa rohoni"
kila jina litajwalo
Hii ya weza tajwa katika kauli tendaji. Tafsiri zilizopo ni 1) "Kila jina mwanadamu atoalo" au 2) "Kila jina Mungu atoalo"
Jina
Tafsiri zilizopo ni 1) Cheo au 2)nafasi ya mamlaka.
wakati huu
"Katika wakati huu"
wakati ujao
"hapo baadae"
Ephesians 1:22-23
Mungu amevitiisha
Mungu ameweka" au "Mungu ameweka"
vitu vyote chini ya miguu ya Kristo
Hapa miguu inawakisha ubwana wa Kristo,mamlaka,na nguvu:"vitu vyote chini ya nguvu ya Kristo"
alifanya yeye kichwa ...ambacho ni mwili wake
kama mwili wake ,kichwa hutawala vitu vyote vinavyohusu mwili wake hivyo ni Kristo kichwa cha mwili wa kanisa.
Kichwa cha vitu vyote katika kanisa
Hapa "kichwa" kinahusu kiongozi au mmoja ambaye yupo kwenye madaraka "mtawala juu ya vitu vyote ndani ya kanisa."
ambacho ni mwili wake
Kanisa kila mara hurejea mwili wa Kristo.
"ukamilifu wake ambao hujaza vitu vyote katika njia zote"
"Kristo hujaza kanisa na kwa mwili wake na nguvu ambazo hutupatia na kuzuilia maisha na vitu vyote"
Ephesians 2
Ephesians 2:1-3
Sentensi Unganishi:
Paulo anawakumbusha waamini walivyokuwa hapa mwanzo na sasa namna walivyo mbele za Mungu.
Na ninyi mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu
Hii inaonyesha ni kwa namna gani watu wana dhambi kiasi cha kushindwa kumtii Mungu kwa namna ile ile wafu wasivyoweza kujishughulisha kimwili tena.
makosa na dhambi zenu
Maneno "makosa" na "dhambi" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile. Paulo anayatumia yote pamoja kuweka mkazo wa ukubwa wa dhambi ya watu.
hapo mwanzo mlienenda
Hii inaelezea tabia ya namna watu walivyoishi
kwa kumfuata mtawala wa mamlaka ya anga
Mtume Paulo anatumia neno "anga" kumaanisha tabia za ubinafsi na ufisadi wa watu waaishio humu duniani.
mtawala wa mamlaka ya anga
Hii inamaanisha ibilisi au shetani
roho yake yule
Sentensi "roho yake yule" inamaanisha ibilisi au shetani.
Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu, tulikuwa tukifanya mapenzi mwili na ya akili.
Maneno "mwili" na "nia" yanawakilisha mwili wote.
wana wa ghadhabu
Watu ambao Mungu amewakasirikia
Ephesians 2:4-7
Mungu ni mwingi wa rehema
"Mungu amejaa rehema" au "Mungu ni mwema sana kwetu"
kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi
"kwa sababu ya pendo lake kubwa kwetu" au "kwa sababu anatupenda sana"
wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya
Hii inaonyesha ni jinsi gani mtu mwenye dhambi hawezi kumtii Mungu mpaka pale anapopewa maisha mapya ya kiroho kama tu vile mtu mfu asivyoweza kujishughulisha na maisha ya mwili huu isipokuwa amefufuliwa kutoka katika wafu.
alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo
"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweze kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.
alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo Yesu.
Kama alivyokwisha kumfufua Kristo, atatufufua na sisi na tutakuwa na Kristo mbinguni.
ndani ya Kristo Yesu
"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweza kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.
katika nyakati zijazo
"huko baadaye"
Ephesians 2:8-10
Kwa maana ni kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani
Wema wake Mungu kwetu ni sababu iliyotuwezesha sisi kuokolewa kutoka katika hukumu kama tu tutamwamini Yesu.
Haitokani na
Neno "haitokani" linahusu au linarejea kwamba "kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani"
...kutoka kwetu
Neno "kwetu" linaelezewa kumaanisha Paulo na waamini wote katika Efeso.
sisi tu kazi ya Mungu
Neno "sisi" linaelezewa kumaanisha Paulo na waamini wote katika Efeso
katika Yesu Kristo
"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweza kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.
Ephesians 2:11-12
Maelezo au Sentensi unganishi:
Paulo anawakumbusha hawa waamini kwamba Mungu aliwafanya watu wamataifa na Wayahudi kuwa mwili mmoja kupitia Kristo na msalaba wake.
wamataifa kwa jinsi ya mwili
Hii inaongelea juu watu ambao hawakuzaliwa Wayahudi.
msiyotairiwa
Watu ambao si Wayahudi hawakutairiwa walipokuwa watoto na hivyo Wayahudi waliwaona hao kama watu wasiomfuata Mungu.
tohara
Hili lilikuwa neno lingine linaloelezea juu ya Wayahudi kwa sababu watoto wote wachanga wa kiume walitairiwa walipokuwa na umri wa siku nane.
tohara ya mwili
Kutahiriwa kulifanywa juu ya miili ya watoto wadogo wa kiume.
watu wa Israel
"jamii ya watu wa Israel"
wageni kwa agano la ahadi
Tafsiri mbadala: "hamkujua ahadi za agano la Mungu"
Ephesians 2:13-16
Sasa katika Kristo Yesu
Paulo anawatofautisha Waefeso kabla ya kumwamini Kirsto na baada ya kumwamini Kristo
ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu, mmeletwa karibu na Mungu
Kwa sababu ya dhambi za waamini, walikuwa wametengwa na Mungu. Hata hivyo, sasa Yesu amewaleta karibu na Mungu kwa damu yake.
yeye ndiye amani yetu
Tafsiri mbadala: "Yesu hutupa amani yake"
Kwa mwili wake
Tafsiri mbadala: "Kwa kifo chake juu ya msalaba"
ukuta wa utenganisho
Tafsiri mbadala: "ukuta wa chuki" au "nia mbaya"
umetutenganisha
Herufi za kwanza "ume" zinaelezea kwamba huo ukuta uliwatenganisha wote Paulo na Waefeso, ambao uliwatenga waumini wa Kiyahudi kutoka kwa waumini wasiokuwa Wakiyahudi (wamataifa)
aliiondoa sheria ya amri na kanuni
Damu ya Yesu ilileta utoshelevu wa sheria ya Musa ili kwamba wote Wayahudi na watu wa mataifa wanaweza kuishi kwa amani ndani ya Mungu.
mtu mmoja mpya
Mtu mmoja mpya, mtu wa jamii ya watu waliokombolewa.
ndani yake
Ni muunganiko na Yesu ambao unafanya upatanisho uwezekane kati ya Wayahudi na watu wa mataifa.
kuwapatanisha watu wote
Tafsiri mbadala: "kuwaleta pamoja wote wawili yaani Wayahudi na watu wa Mataifa (wamataifa)"
kupitia msalaba...kwa njia ya msalaba
Hii ni kwamba, kwa njia ya Kifo cha Kristo juu ya msalaba.
aliufisha (aliuua) uadui kwa msalaba
Yesu aliondoa kabisa sababu ambayo iliwafanya Wayahudi na watu wa mataifa kuwa maadui. Hawakuhitajika tena kuishi kulingana na sheria ya Musa.
Ephesians 2:17-18
Maelezo au Sentensi Unganishi.
Paulo anawaambia waamini wakiefeso kwamba watu wa mataifa walioamini wamefanyika wamoja na mitume na manabii, na ni hekalu kwa Mungu katika Roho Mtakatifu.
amani iliyotangazwa
Tasfiri mbadala: "injili ya amani iliyotangazwa" au "injili ya amani iliyotangazwa kwa uwazi"
ninyi mliokuwa mbali
Hii inazungumzia juu ya watu wa mataifa au wale wasio Wayahudi.
wale waliokuwa karibu
Hii inazungumzia juu ya Wayahudi.
Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi sote wawili tuna nafasi.
Hapa "sisi sote wawili" inazungumzia juu ya Paulo, waamini wa Kiyahudi na waamini wasio Wayahudi.
kwa yule Roho Mtakatifu
Waamini wote, yaani Wayahudi na watu wa mataifa, wamepewa haki ya kuingia mbele za uwepo wa Mungu Baba kwa Roho Mtakatifu yule yule.
Ephesians 2:19-22
ninyi watu wa mataifa si wageni na wasafiri tena. bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe wa nyumbani mwa Mungu.
Hii inaelezea hali ya kiroho ya watu wa mataifa kabla na baada ya kuwa waamini kwa namna ile ile ambayo watu wasiokuwa raia wanavyoweza kuwa raia wa taifa fulani.
si wageni tena
" si watu wa nje tena"
na wasafiri
"na watu wasio raia"
mmejengwa juu ya msingi
Paulo analinganisha Familia ya Mungu na jengo. Yesu akiwa jiwe kuu la pembeni, na mitume wakiwa ndiyo msingi na waamini wakiwa boma (jengo lenyewe)
jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukuwa kama hekalu.
Paulo anaendelea kulinganisha Familia ya Kristo na jengo. Kwa namna ile ile ambayo mjenzi anaungamanisha mawe pamoja wakati akijenga, vivyo hivyo Kristo anatuungamanisha pamoja.
ndani yake...ndani ya Bwana
Haya ni maelezo ya mfano juu ya "ndani ya Kristo Yesu". Haya yanatokea mara nyingi katika nyaraka (barua) za Agano Jipya. Yanaelezea uhusiano wa nguvu sana unaoweza kuwepo baina ya Kristo na wale wanaomwamini yeye.
ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho
Hii inaeleza namna waamini wanawekwa pamoja kuwa mahali ambapo Mungu ataishi siku zote kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu
Ephesians 3
Ephesians 3:1-2
kauli unganishi
Kufanya wazi ukweli siri kuhusu kanisa kwa waumini, Paulo anataja nyuma umoja wa Wayahudi na Mataifa na hekalu la ambayo waumini sasa ni sehemu.
Kwasababu ya hii
"Kwasababu ya neema ya Mungu kwako"
mfungwa wa Kristo Yesu
"moja ambaye Kristo Yesu amemuweka katika gereza"
usimamizi wa zawadi ya Mungu kwamba yeye alinipa kwa ajili yenu
"Wajibu Mungu alinipa kusimamia neema yake juu yenu"
Ephesians 3:3-5
kutokana na jinsi ufunuo ulivyo funuliwa kwangu
Hii inaweza alisema katika fomu ya kazi. AT: "nini Mungu alinifunulia"
nililivyoyokuandikia kwa kifupi kwenye barua nyingine.
Paulo anataja barua nyingine ameandika kwa watu hawa.
Kwa vizazi vingine ukweli huu haukufanywa utambulike kwa watoto wao
"Ambayo Mungu hakufanya anajulikana kwa watu katika siku za nyuma"
Ila kwa sasa umewekwa wazi kwa Roho
"Sasa Roho umebaini" au "sasa Roho imefanya ni maalumu"
mitume wake na manabii wenye kuwekwa wakfu
"mitume na manabii ambao Mungu amewatenga kwa utumishi"
Ephesians 3:6-7
Watu wa mataifa ni warithi wenzake ... kwa njia ya Injili
Huu ni ukweli ulio fichika Paulo anaanza kuelezea katika mstari uliopita. Watu wa mataifa waliompokea Kristo pia watapokea urithi kama kama waumini wa Kiyahudi.
wanachama wenzake wa mwili
Kanisa ni mara nyingi hujulikana kama mwili wa Kristo.
katika Kristo Yesu
"Katika Kristo Yesu" na maneno kama ni mafumbo ambayo mara nyingi yametokea katika Agano Jipya. Yanaelezeamahusiano ya nguvu inawezekana kati ya Kristo na walio amini katika Yeye.
Kupitia Injili
Maana inawezekana ni 1) kwa sababu ya Injili watu wa mataifa ni washiriki wengine wa ahadi au 2) kwa sababu ya Injili watu wa mataifa ni warithi na viungo vya mwili na washirika wenzake katika ahadi.
Ephesians 3:8-9
Mungu amenipa zawadi hii japo kuwa mimi ni mtu mdogo kati ya wale wanaopata nafasi kwa Mungu
"Ingawa mimi ni mdogo anastahili watu wote wa Mungu, Mungu amenipa zawadi hii ya neema"
kuleta kila mtu katika mwanga na kuwaambia kuhusu mpango wa siri za Mungu
"kuwafanya watu wote kufahamu mpango wa Mungu"
kuwaambia kuhusu mpango wa siri wa Mungu kwamba Mungu (aliyeviumba vitu vyote) alikuwa amejificha kwa miaka katika siku za nyuma
"kitu ambacho Mungu alikificha kwa mda mrefu uliopita. Alipo umba kila kitu"
wale waliotengwa kwa Mungu
Hii inaweza semwa katika: "wale ambao Mungu amewatenga kwa ajili yake mwenyewe "
usiopimika
haiwezekani kujulikana kabisa
utajiri wa Kristo
Paulo anazungumzia ukweli kuhusu Kristo na baraka yeye huleta kana kwamba vilikuwa utajiri wa mali.
kuwaelimisha watu wote kuhusu mpango wa siri wa Mungu ni nini.
"angaza mwanga kwenye mpango wa Mungu ili watu wote wajue ni nini" au "kuwaambia watu wote ni nini mpango wa siri ya Mungu"
uliofichwa kwa miaka mingi kuanzia mwanzo Mungu alivyoumba kila kitu.
Hii inaweza semwa kama: "Kwamba Mungu, aliyeviumba vitu vyote, alikuwa ameficha kwa umri mrefu katika siku za nyuma"
Ephesians 3:10-11
viongozi na mamlaka yaliyopo mbinguni zitakuja kujulikana pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu
ilikuwa upande asili ya hekima ya Mungu ** - "Mungu atafanya hekima yake kubwa ijulikane kwa viongozi na mamlaka katika ulimwengu wa roho kupitia Kanisa "
pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu
ilikuwa upande asili ya hekima ya Mungu ** - hekima ya Mungu tata
watawala na mamlaka
Maneno haya yanashiriki maana sawa. Paulo anatumia yote pamoja na kusisitiza kwamba kila kiumbe cha kiroho watajua hekima ya Mungu.
kulingana na mpango wa milele
"katika kutunza mpango wa milele" au "sambamba na mpango wa milele"
katika Kristo Yesu Bwana wetu
Kwa njia ya Kristo
katika ulimwengu wa roho
Kuona jinsi ya kutafsiriwa hii angalia 1:3
Ephesians 3:12-13
kauli unganishi
Paul anamsifu Mungu katika mateso yake na anaomba kwa ajili ya waumini hawa wa Efeso.
upatikanaji kwa kujiamini
"upatikanaji katika uwepo wa Mungu kwa kujiamini" au "uhuru wa kuingia katika uwepo wa Mungu kwa ujasiri"
kwa sababu ya imani yetu kwake
"kwa sababu ya imani yetu katika Kristo"
tuna ujasiri
"sisi bila hofu" au "tuna ujasiri"
kujiamini
"hakika" au "uhakika"
Huu ni utukufu wako
Hapa "utukufu wako" kujisikia katika ufalme ujao. Wakristo wa Efeso wanapaswa kujivunia mateso ya Paulo gerezani. "Hii ni kwa manufaa yako" au "unapaswa ujivunie hii"
Ephesians 3:14-16
Kwa sababu hiyo
"Kwa sababu Mungu amefanya yote haya kwa ajili yenu"
Napiga magoti kwa Baba
"Nina inama chini kwa maombi kwa Baba" au "Mimi kwa unyenyekevu kumwomba Baba"
kwa kupitia kwake kila familia hapa duniani na minguni imetajwa
kitendo cha kumtaja hapa pengine pia inawakilisha kitendo cha kujenga: "aliyeumba na kutaja jina kila familia mbinguni na duniani"
Namwomba Mungu wewe
"kuwa angeweza kukupa"
kwamba akubariki, kutokana na utajiri wa baraka zake, akufanye imara kwa nguvu
"Mungu, kwa sababu yeye ni kubwa sana na myenye nguvu, anaweza kuruhusu wewe kuwa na nguvu kwa uwezo wake"
Awajalieni
"angetoa"
Ephesians 3:17-19
kauli unganishi
Paulo anaendelea maombi aliyoyaanza
kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani. Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake
Hili ni ombi la pili Paulo anaomba kwamba Mungu "awapatie" Waefeso "kulingana na utajiri wa utukufu wake "; kwanza ni kwamba wangeweza "kuimarishwa"
mioyo kwa njia ya imani
hapa "moyo" inawakilisha utu wa ndani, na "kupitia" inaonyesha njia ambayo Kristo anaishi ndani ya muumini. Kristo anaishi katika mioyo ya waumini kwa sababu neema ya Mungu inaruhusu wao kuwa na imani.
imani. Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Uwe katika pendo lake ili uweze kuelewa
maana inawezekana ni 1) "Imani. Naomba kwamba utakuwa na mzizi na msingi katika upendo wake ili uweze kuelewa" au 2) "Imani hivyo utakuwa na mzizi na msingi katika upendo wake. Nina omba pia uweze kuelewa "
kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake
Paulo analinganisha imani yao kwa mti wenye mizizi au nyumba iliyojengwa juu ya msingi imara. "kwamba utakuwa kama mti wenye shina zuri na nyumba yenye msingi wa jiwe."
Ili uweze kuelewa
Hili ni ombi la pili ambalo Paulo anapiga magoti yake na kuomba: la kwanza ni, Mungu awape kuimarishwa na kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yao kupitia Imani. na "uelewa" ni kitu cha kwanza kabisa Paulo aliomba kwamba Wafilipi wenyewe waweze kufanya.
waaminio wote
"waaminio ndani ya Kristo" au "watakatifu woote"
upana, urefu, kimo, na kina cha upendo wa Kristo
Paulo anatumia maneno hayo kuelezea kwa namba gani ambayo Kristo anatupenda.
ili upate kujua ukuu wa upendo wa Kristo
Hili ni jambo la pili kwamba Paulo anaomba kwamba Waefeso wataweza kufanya; kwanza ni kwamba wao "waelewa." "kwamba uweze kujua ukuu wa upendo wa Kristo"
ili mpate kujazwa na ukamilifu wote wa Mungu
Hili ni ombi la tatu ambalo Paulo anapiga magoti yake na kuomba: la kwanza ni,mpate "kuimarishwa" na la pili ni kwamba "muweze kuelewa"
Ephesians 3:20-21
kauli unganishi
Paulo anamalizia sala yake kwa baraka.
Maelezo ya ujumla:
maneno "sisi" na "sisi" katika kitabu hiki yanaendelea kuwahusisha Paul na waaminio wote.
Sasa kwake
"Sasa kwa Mungu, ambaye"
kila kitu mbali, mbali juu
Mungu anaweza kufanya zaidi kuliko tunayoweza milele kuomba au kufikiria.
Ephesians 4
Ephesians 4:1-3
kauli unganishi
Kwasababu ya kile Paulo amekuwa akiwaandikia Waefeso, anawatia moyo namna gani kuishi maisha yao kama waamini na tena anasisitiza umoja wa waamini.
Kama mfungwa kwa ajili ya Bwana
"kama mtu ambaye yuko gerezani kwa sababu ya uchaguzi wake wa kumtumikia Bwana"
Nawasihi ninyi kuishi maisha yanayoendana na wito
Neno "ninyi" linamaanisha Waefeso waamini. AT: "Nawatia moyo ninyi kujitunza wenyewe kwa namna nzuri ya wito."
Kwa unyenyekevu mkubwa na upole na uvumilivu, mkichukuliana kila mmoja katika upendo
"jifunzeni kuwa wanyenyekevu, wapole, waumilivu na kuchukuliana kila mmoja katika upendo"
Tunzeni umoja wa Roho katika kifungo cha amani
"tafuteni kuishi pamoja kwa amani kuuhifadhi umoja wa Roho"
Ephesians 4:4-6
Mwili mmoja
Kanisa mara nyingi linatafasiriwa kama mwili wa Kristo.
Roho moja
"Roho Mtakatifu mmoja tu" (UDB)
Pia mliitwa katika ujasiri wa taraja moja
"Mungu aliwachagua ninyi katika tumaini moja la uhakika"
Baba wa wote ... juu ya wote ... na katika yote ...na ndani ya wote
"Baba wa kila kitu...juu ya kila kitu...kupitia kila kitu...katika kila kitu"
Ephesians 4:7-8
kauli unganishi
Paulo anawakumbusha waamini juu ya karama ambazo Kristo huwapa waamini kutumia katika kanisa ambalo ni mwili wote wa waamini.
maelezo ya jumla
Nukuu hii imetoka katika wimbo mfalme Daudi aliimba.
Kwa kila mmoja wetu amepewa karama
Hii yaeza elezwa kwa kutumia kauli tendaji. "Mungu ametoa karama kwa kila mmoja wetu" au "Mungu alitoa karama kwa kila muumini"
Alipopaa juu sana
"wakati Kristo alipokwenda juu mbinguni"
Ephesians 4:9-10
Alipaa
"Kristo alikwenda juu"
Pia alishuka
"Kristo alishuka pia"
Pande za chini za dunia
Yaweza kumaanisha kwamba 1) "katika maeneo ya chini, ya dunia" au 2) "katika sehemu za chini, za dunia."
Aweze kuvijaza vitu vyote
"iliaweze kuwa kila mahali kwa nguvu zake"
jaza
"kamilisha" au "kuridhisha"
Ephesians 4:11-13
Kristo alitoa karama kama hizi
"Kristo alitoa karama kwa kanisa kama hizi"
kuwawezesha waamini
"kuwaanda waamini" au "kuwapatia waamini"
Kazi ya huduma
"kuwahudumia wengine"
Kwa ajili ya ujenzi wa mwili wa Kristo
Hii inalinganishwa ukuaji wa kiroho kwa kufanya mazoezi kuongeza nguvu ya mwili wa binadamu."
kuujenga
"uboreshaji"
mwili wa Kristo
"mwili wa Kristo" wa husu waumini mmoja mmoja wa mwili wa Kristo.
Kuufikia umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu
Maarifa ya Yesu Kristo kama mwana wa Mungu ni ya mhimu katika kuufikia umoja wa imani na ukomavu kama waamini.
Kufikia umoja wa imani
"kuwa na usawa wa nguvu katika imani"
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo mhimu cha Yesu.
Kuwa wakomavu
AT: "Kuwa waamini waliokomaa"
mkomavu
"mtu mzima," "amekuwa," au "mkamilifu"
Ephesians 4:14-16
Kuwa kama watoto
Hii ni kulinganisha waamini ambao hawajakuwa kiroho na mtoto ambaye amekuwa na udhoefu mdogo sana katika maisha."
Kurushwarushwa na kuchukuliwa huku na huku na kila upepo wa fundisho
Hii inamlinganisha muumini ambaye hajakomaa na husikia fundisho potofu na boti ambayo inarushwa na upepo katika mwelekeo usio sahihi juu ya maji.
Kwa hila ya watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka
"kwa watu wajanja ambao hupotosha waamini kwa uongo wa kiujanja"
Katika yeye aliye kichwa...mwili wote hukua na kujengeka wenyewe juu
Paulo anatumia mwili wa binadamu kuelezea namna gani Kristo husababisha waamini kfanya kazi pamoja katika umoja kama kichwa cha mwili husababisha sehemu za mwili kufanya kazi pamoja ili kukuwa kiafya.
pamoja na kila kiungo
"kiungo" ni ukanda madhubuti unao unganisha mifupa katika mwili.
Ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe juu katika upendo
"Hivyo, waamini wanaweza kusaidiana kila mmoja na mwenzake kukua katika upendo"
Ephesians 4:17-19
Sentensi unganishi:
Paulo anawaambia wao kile ambacho hawapaswi kufanya sasa tu kwasababu wao kama waamini wamewekewa mhuri na Roho Mtakatifu wa Mungu.
Hivi nasema kwahiyo, na ninawasihi ninyi katika Bwana
"Kwahiyo, ninawatia moyo kwa nguvu katika Bwana"
Msitembee tena kama wamataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao
"Acheni kuishi kama wamataifa na fikra zao zisizonamaana"
Kutiwa giza katika fikra
Hawawezi kufikiri au kuhoji kwa usahihi.
kufukuzwa kutoka katika maisha ya Mungu kwa ujinga uliomo ndani yao na kwa ugumu wa mioyo yao
"Hawawezi kuhisi maisha ya Mungu kwa sababu akili zao zimepofushwa na ni wagumu"
Kufukuzwa
"kukatiliwa mbali" au "kutengwanisha"
ujinga
"ukosefu wa maarifa" au "ukosefu wa taarifa"
sababu ya ugumu wa mioyo yao
Wamekataa kumsikiliza Mungu na kufuata mafundisho yake.
wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu
Paulo anawaongelea awa watu kama wao ni vitu wanaojikabidhi wao wenyewe kwa watu, na anaongelea jinsi wanavyo taka kuridhisha tamaa zao za mwili kana kwamba ndio mtu wanao jikabidhi kwake. "Wanacho taka tu nikuridhisha tamaa zao za mwili"
jikabidhi
"kujitoa kabisa"
Ephesians 4:20-22
Lakini hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo
"Lakini hamkujifunza kumfuata Kristo kwa namna hii"
Kama mmesikia kuhusu yeye na mmefundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli iliyo ndani ya Yesu
"Kwavile mmesikia kuhusu Yesu na mmejifunza ukweli kuhusu yeye"
Ninyi lazima mvue utu wa kale- ule ambao unakubaliana na tabia zenu za kale, ambao umeharibika sawasawa na tamaa za udanganyifu
AT: "Ninyi lazima mziondoe tabia ambazo zilikuwa za kawaida kwa njia za maisha yenu ya kale, ambazo zilikuwa mbaya kama tamaa zenu mbaya zilivyowadanganya ninyi"
Lazima muuvue utu wa kale
Lazima mwachane na tabia zote za dhambi kama tu kuvua nguo na kuzitupa mbali. AT: "Lazima mbadili tabia zenu."
Zile zinazoendana na mwenendo wenu wa kale
AT: "tabia ambazo zinakubaliana na asili yenu ya kale" au "tabia ambazo zinakubaliana na ukale wenu"
Ambayo imeharibiwa kulingana na tamaa danganyifu
AT: "ambayo inaendelea kukua vibaya kwasababu ya tamaa za mwili zidanganyazo"
Ephesians 4:23-24
vueni utu wenu wa zamani
Paulo anazungumzia tabia njema kana kwamba ni vipande vya nguo. "Lazima ubadili tabia" au Lazima uweke mbali mtu wa kale"
mfanywe upya katika roho ya akili zenu
Hii ya weza badilishwa katika njeo tendaji. "Mungu anaweza kukusaidia ukuwe karibu na yeye na kufikiri kwa namna mpya"
Ili kwamba mweze kuvaa utu mpya
Mtu asiye mwamini anakuwa mtu mpya anapokuwa muumini katika Kristo kama ilivyo kwa mtu anavyovaa nguo mpya na kuonekana tofauti kabisa.
unaoendana na Mungu
" inayo akisi tabia ya Mungu" au "yenye kuonyesha jinsi Mungu alivyo"
Ephesians 4:25-27
Wekeni mbali uongo
"Lazima mwache kusema uongo"
Mnene ukweli, kila mmoja na jirani yake
"Waamini lazima wanene ukweli kwa majirani zao"
Sisi ni wajumbe kila mmoja kwa mwingine
"Sisi sote ni wajumbe wa familia ya Mungu"
Mwe na hasira, lakini msitende dhambi
"mnaweza kukasirika, lakini msitende dhambi"
Msiliruhusu jua kuzama mkiwa na hasira zenu
"Lazima mwache kuwa na hasira kabla usiku haujaingia" au "muiondoe hasira yenu kabla ya siku haijaisha"
msimpe ibilisi nafasi
"Msimpe ibilisi fursa ya kukupeleka dhambini"
Ephesians 4:28-30
Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu
"msiruhusu lugha mbaya itoke kinywani mwenu" au "msiruhusu mazungumzo maovu yatoke kinywani mwenu"
Badala yake maneno ambayo ni msaada kwa kuwajenga wengine
"badala yake neneni maneno ambayo ni msaada katika kutoa afya kwa waamini wengien"
Kuwapa neema wao ambao wanasikiliza
"kwa njia hii mtatoa neema kwa wale ambao wanasikiliza"
faida
"saidia" au "msaada"
Msimhuzunishe
"msitese" au "msiudhi"
Kwa yeye ambaye mmewekewa mhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi
Paulo anasema Roho Mtakatifu amewaakikishia waamini kuwa Mungu atawapatia ahadi aliyo waahidi. Roho ni kama alama ambayo Mungu amewaekea watu wake kuonyesha kuwa anawamiliki. "Ni Roho ambaye Mungu amekupa kuonyesha kuwa anakumiliki na ata kukomboa kwa wakati muafaka"
Ephesians 4:31-32
sentensi unganishi
Paulo anamaliza maelekezo ya kuhusu yapi waamini wasifanye na anamaliza na yapi wafanye.
lazima muweke mbali
tafsiri zilizopo ni 1) lazima ufanye mwenyewe au 2) "lazima umuruhusu Mungu aondoe"
weka mbali uchungu wote
"acha kuwa na hasira ya mambo mabaya watu walio kufanyia"
ghadhabu
wakati wa hasira nzito
hasira
neno lililo zoeleka la hasira
mwe na huruma
" badala yake, lazima uwe na huruma
msameheane
"upole" au "huruma sana"
Ephesians 5
Ephesians 5:1-2
Kauli unganishi
Paulo anaendelea kuwaambia waumini jinsi wanavyotakiwa na wasivyotakiwa kuishi kama watoto wa Mungu.
Kwa hiyo mwe wa kumuiga Mungu
"Hivyo ninyi mfanye mambo ambayo Mungu hufanya"
kama watoto wake wapendwa
Mungu anatamani sisi tumuige yeye maadam sisi ni watoto wake.
tembea katika upendo
"ishi maisha ya upendo"
sadaka na dhabihu, harufu nzuri inayompendeza Mungu
"sadaka inayonukia vizuri na dhabihu kwa Mungu"
Ephesians 5:3-4
uovu wa kujamiiana au uchafu au tamaa ya anasa lazima usidokezwe kati yenu, kama ilivyo sahihi kwa waumini
"siruhusu hata mawazo ya uovu wa kujamiina au uchafu au urafi kupatikana kati ya watu wa Mungu"
uchafu wowote
"maadili yoyote yasiyosafi"
kupenda anasa kwa ulafi
NI: "kutamaa kwaajili ya walivynavyo wengine"
kama ilivyosawa kwaajili ya waumini
NI: "tabia zenu daima ziwe zinazofaa kama watu watakatifu wa Mungu"
lazima usidokezwe kati yenu
"lazima usitajwe kati yenu" au "lazima usigundulike kati yenu"
Ephesians 5:5-7
urithi
Kupokea kile Mungu alicho ahidi waamini ni mfano wa mtu kurithi mahali au utajiri kwa familia.
matupu
"Msiruhusu mtu yeyote awadanganye kwa hoja za uongo" au "Msiruhusu mtu yeyote awakoseshe ninyi kwa maneno yasiyokuwa na maana"
Ephesians 5:8-12
Hapo kale ulikuwa giza
Kama tu mmoja hawezi kuona gizani, ndivyo watu wanaoishi katika dhambi wanapungukiwa ufahamu wa kiroho.
Lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana
Kama tu mmoja anaweza kuona katika nuru, ndivyo watu ambao wanaishi katika haki wanaufahamu wa kiroho.
kwa sababu tunda la haki ni uzuri wote, haki, na kweli
kazi zinazotoka kwenye maisha ya muumini (uzuri, haki, na kweli) zinafanana na tunda zuri linalozalishwa na mti wenye afya.
hazina ushirikiano pamoja na kazi zisizozaa za giza
"Usijihusishe na kazi za dhambi au wasioamini"
kazi zisizozaa za giza
kazi za mtu fulani anayeishi katika giza la kiroho zinafanana na matendo maovu ya watu wanaofanya kazi za uovu wamefichwa na giza usiku.
lakini afadhali uwafichue
"lakini heri uwaweke wazi kuwa wanamakosa"
Ephesians 5:13-14
sentensi unganishi
Haijulikani kama nukuu hii ni zile za Nabii Isaya au ni nukuu ya nyimbo zilizoo imbwa na waamini.
Kila kitu kimefunuliwa na nuru
Kama vile nuru hufunua vitu ambavyo vilikuwa vimefichwa katika ulimwengu unaoonekana, hivyo nuru ya Kristo inafunua uovu wa matendo ya kiroho ya wasioamini katika ulimwengu wa kiroho.
Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka kwa wafu
Wasioamini wanahitaji kuamka kutoka katika kifo cha kiroho kama vile mtu ambaye amekufa lazima afufuke tena ili kusudi aitikie.
wewe ulalaye ... atang'aa juu yako
"wewe" ya husu "aliyelala"
Kristo ataangaza juu yako
Kristo atamwezesha asiyeaamini kufahamu kiasi cha msamaha kilichotolewa na maisha mapya kama vile nuru inavyoonesha dhahiri kilichoko pale ambacho kilikuwa kimefichwa na giza.
Ephesians 5:15-17
Hivyo basi uwe makini jinsi mnavyoishi, siyo kama watu wasio na hekima bali kama wenye hekima
Wasio na hekima hawajilindi wenyewe kinyume na dhambi. Kwa hali yoyote watu wenye hekima wanaweza kutofautisha dhambi na kuikimbia. NI: "Hivyo basi ni lazima muwe makini muishi sawa na watu wenye hekima zaidi kuliko mtu mpumbavu" au "Hivyo basi lazima mwe makini kuishi sawasawa na mtu mwenye hekima."
Komboa wakati
Tunalo chaguo la kuishi katika dhambi ambalo ni sawa kama kutumia wakati wetu bila hekima. Au tunaweza kuishi tukifanya ambacho Bwana anataka sisi tufanye na kuutumia muda wetu kwa hekima. KWAMBA: "Tumia muda wako kwa hekima."
kwasababu siku ni mbaya
Neno "siku" linamaanisha ni katika muda unaoishi
Ephesians 5:18-21
sentensi unganishi
Paulo anamaliza maelekezo yake kwa jinsi gani waamini wapswa kuishi.
Na usilewe kwa mvinyo
"Na usilewe kutokana na kunywa mvinyo"
badala yake uwe umejaa na Roho Mtakatifu
"badala yake uwe uliyejaa na Roho Mtakatifu"
katika zaburi na sifa na nyimbo za kiroho
"pamoja na aina zote za nyimbo za kumsifu Mungu"
daima mkitoa shukrani
"Mtoe shukrani daima"
mkijitoa wenyewe
"Kwa unyenyekevu jitoeni wenyewe"
Ephesians 5:22-24
sentensi Unganishi:
Paulo anatoa maelekezo kwa mume na wake juu ya jinsi wanavyopaswa kutendeana.
yeye ni mwokozi wa mwili
NI: "Kristo ni Mwokozi wa mwili wa waumini" au "Kristo ni Mwokozi wa waumini wote"
Hivyo pia wake wawe kwa waume zao katika kila kitu
NI: "hivyo wake lazima pia wawe watiifu kwa waume zao katika kila jambo"
Ephesians 5:25-27
wapendeni wake zenu
Hapa "pendo" linarejea pasipo ubinafsi, kutumika, au kutoa upendo.
kujitoa mwenyewe kwaajili yake, kwamba unaweza kumfanya yeye mtakatifu kwasababu yeye alitusafisha sisi
Maneno "mwenyewe" na "yeye" yanarejea kwa Kristo. Maneno "yeye" na "sisi" yanarejea kwa Kanisa.
kajitoa mwenyewe kwaajili yake
NI: "Kristo alitoa kila kitu kwaajili yake"
yeye alitusafisha sisi kwa kutuosha kwa maji kupitia neno
Maana zinazowezekana ni 1) Paulo anarejea kuwa umekuwa ukisafishwa kwa neno la Mungu na kupitia ubatizo wa maji katika Kristo au 2) Paulo anasema Mungu alitufanya sisi wasafi kiroho kutoka katika dhambi zetu kwa neno la Mungu kama tunavyoifanya miili yetu safi kwa kuiosha kwa maji.
kwamba yeye aweza kujiwasilishia mwenyewe kanisa
"kwamba anaweza kuwasilisha kwake mwenyewe kanisa"
bila waa au kunyanzi
Paulo anasema kuhusu Kanisa kama vazi ambalo ni safi na liko katika hali nzuri. Anatumia wazo lile lile katika namna mbili kusisitiza utakatifu wa Kanisa.
takatifu na bila makosa
Kauli "bila makosa" kimsingi inamaanisha kitu kile kile "mtakatifu." Paulo anatumia viwili pamoja kusisitiza utakatifu wa kanisa.
Ephesians 5:28-30
kama miili yao wenyewe
NI: "kama wapendavyo miili yao wenyewe"
badala yake anaurutubisha
"badala yake anautunza" au "yeye anaulinda"
sisi tu viungo vya mwili wake
Inawezekana ikamaanisha 1) "sisi ni jumuiya ya mwili wake" au 2) waumini wanashikamana kuutengeneza mwili wa Kristo kama vile viungo vya mwili wa mwanadamu vinavyoshikamana kuunda mtu.
Ephesians 5:31-33
kwa kisababishi hiki
"kwa sababu hii"
lazima kumpenda mke wake kama yeye mwenyewe
Maneno haya "yeye" na "mwenyewe" yanarejea kwa mwanaume muumini ambaye kaoa.
mke lazima amheshimu mume wake
"mke lazima amtii mume wake"
Ephesians 6
Ephesians 6:1-3
sentensi unganishi
Paulo anatoa maelekezo kwa watoto, wababa, wafanya kazi, na mabwana.
Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana
Paulo anarejea kwa watoto kuwatii wazazi wao wa kimwili.
Ephesians 6:4
Na ninyi akina baba msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira
"Ninyi wababa msifanye mambo ambayo yatawafanya watoto wenu wakasirike" au "Ninyi akina baba msiwasababishie wattoto wenu kuwa na hasira"
muwalee katika maonyo na maagizo ya Bwana
"wasaidieni kukua katika mafunzo na mafundisho ya Bwana"
Ephesians 6:5-8
watumwa, iweni watiifu kwa
"Ninyi watumwa mnapaswa kutii"
kwa heshima kubwa na kutetemeka
Hizi ni njia mbili zinazofanana kuonyesha heshima kuhusu mabwana zao.
kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. Tiini kama vile mnavyomtii kristo
"Nyeyekeeni kwa hofu, kama kumtii kristo"
usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama
"siku zote fanya kazi kama ulivyokuwa ukifanya kazi kwa ajili ya kristo mwenyewe, hata kama mabwana zenu hawawatazami"
kama watumwa wa Kristo
watumikieni mabwana zenu ingawa bwana wenu duniani ni Kristo.
Watumikieni kwa mioyo yenu yote. Kana kwamba kumtumikia Bwana na wala si wanadamu
"fanya kwa furaha maana unafanya kwa ajili ya Bwana na si kuwafurahisha wanadamu."
Ephesians 6:9
fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu, na msiwatishie
Msiwatishie watumwa wenu, lakini muwafundishe kama Kristo angeweza kuwafundisha"
mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni
"kwa sababu mnajua kuwa Krisato ni Bwana wa wote watumwa na Mabwana zao"
Mkijua kuwa hakuna upendeleo kwake
"Na hana upendeleo"
Ephesians 6:10-11
sentensi unganishi
Paulo anatoa maelekezo kuwafanya waumini kuwa na nguvu katika hii vita tunaishi kwa ajili ya Bwana.
iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake
"Hii inategemea kikamilifu katika Bwana kuwapa nguvu ya ya Kiroho"
Vaeni silaha zote za Mungu zilizo kamili, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani
Wakristo wanapaswa kutumia raslimali zote ambazo Mungu amewapa ili kusimama kinyume na shetani kama vile maaskari wa wanavyoweka siraha za kujikinga mwenyewe kutoka kwa uvamizi wa maadui.
Ephesians 6:12-13
damu na nyama
Hii fafanuzi inahusiana na watu, siyo roho ambazo hazina mwili wa Binadamu.
kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu
wakristo wanapaswa kutumia raslimali za kukinga ambazo Mungu amewapa katika kupigana na shetani kwa njia ile askari hubeba silaha ili kujilinda dhidi ya maadui.
Ephesians 6:14-16
hatimaye simameni imara
maneno "simameni imara" ni lugha yenye maana ya "kuzuia vikali"
mkanda wa kweli
kweli inashika kila kitu pamoja kwa ajili ya muumini kama mkanda unavyoshika nguo zote za askari pamoja.
haki kifuani
Zawadi ya haki inafunika mioyo ya waumini kama kitu cha kulinda kifuaniani kwenye kifua cha Askari.
mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu ili kutangaza injili ya ya Amani
Ni askari pekee anavaa ili kumpa maalifa ya kutembea, muumini anapaswa kuwa na maarifa imara ya injili ya amani ili kuwa tayari kuitangaza.
kila hali mkichukua ngao ya Imani
Imani ambayo Mungu amempa muumini ni lazima itumike kwa ajili ya ulinzi wakati shetani anapovamia kama vile ngao ambayo askari anaitumia kujikinga kutoka katika uvamizi wa maadui.
kuizima mishale ya mwovu Ibilisi
Uvamizi wa shetani katika kumvamia muumini ni kama mishale ya moto inayorushwa kwa askari na adui.
Ephesians 6:17-18
Na mvae kofia ya wokovu
Wokovu uliopewa na Mungu unalinda mawazo ya muumini kama vile kofia inavyolinda kichwa cha askari.
na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu
Neno la Mungu, limevuviwa na Roho Mtakatifu, ili litumike kwa kupigana kinyume na kuwalinda waumini kutoka kwa mwovu kama vile askari anavyotumia upanga kupigana na kujilinda dhidi ya adui anayevamia.
pamoja na kusali na kuomba, ombeni kwa Roho
"Ombeni wajati wote katika Roho kama unavyoomba na ufanye maombezi maalumu"
kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waumini wote
"Mara kwa mara tuwe macho kwa kuomba kwa ajili ya waumini wote"
Ephesians 6:19-20
sentensi unganishi
Paulo anawaomba kuomba kwa ajili ya ujasiri wake katika kusema injili wakati akiwa gerezani na akasema anamtuma Tikiko ili kuwafariji. Kisha alitoa baraka za amani na neema kwa waumini wote wanaompenda Yesu.
ili niweze kupewa ujumbe
"Kwamba Mungu anipe neno" au "Mungu atanipa ujumbe"
ninapofungua mdomo wangu ili kuufanya ujulikane kwa ujasiri
"Ninapoongea kufafanua kwa ujasiri"
kwa sababu hii mimi ni balozi niliyefungwa minyororo
Niko gerezani sasa kwa sababu ya kuwa mwakilishi wa Injili"
kwamba katika kifungo changu niseme kwa ujasiri kama ninavyowiwa kusema
"Kwamba niseme ujumbe wa Mungu kwa ujasiri wakati nikiwa humu gerezani"
Ephesians 6:21-22
mambo yangu
"Yaliyonipata" au "Hali yangu"
Tikiko
Tikiko alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakitumika na Paulo.
atawajulisha kila kitu
"Atawaambia kila kitu"
Ephesians 6:23-24
Sentensi unganishi
Paulo anafunga barua yake kwa wa Efeso na baraka ya amani na neema kwa wote waamini wanao mpenda Kristo.