Joshua
Joshua 1
Joshua 1:1-3
Yahwe
Hili ni jina la Mungu ambalo alilidhihirisha kwa watu wake katika Agano la Kale.
Nuni
Baba yake na Yoshua
Vuka mto huu wa Yordani
''Kuvuka" ina maana ya " kwenda upande mwingine wa mto,"au kusafiri kutoka upande mmoja wa mto hadi upande wa pili."
wewe pamoja na watu hawa
Neno 'wewe' humrejelea Yoshua.
Nimewapeni ninyi
Neno "ninyi' linarejelea Yoshua na taifa la Israeli.
Nyao za miguu yenu
Ina maana ya sehemu zote ambazo Yoshua atazitembelea katika safari yake ng'ambo ya Mto Yordani.
Joshua 1:4-5
Maelezo ya jumla
Yahweh anaendelea kuzungumza na Yoshua
Nchi yenu
Neno 'yenu' linarejelea makabila ya Israeli na si Yoshua pekee yake.
kusimama kinyume chako
Katika mstari wa 5 maneno 'chako' na 'yako' yanamrejelea Yoshua.
Sitakupungukia wala kukuacha
Maneno 'sitakupungukia' na 'kukuacha' kimsingi yanamaanisha kitu kile kile. Yahwe aliyatumia kwa pamoja ili kukazia na kuonesha kwamba hatayafanya mambo haya. "Nitakuwa pamoja nawe siku zote."
Joshua 1:6-7
Maelezo ya jumla
Yahwe anampa Yoshua mfululizo wa maagizo
Uwe hodari na jasiri sana
Yahwe anamwagiza Yoshua ashinde hofu zake kwa ujasiri.
Usikengeuke upande wa kulia au wa kushoto
Maneno haya yaweza kumaanisha agizo halisi. "Ifuate sheria kwa hakika" au ''Zifuate kwa ukweli na hakika"
ili uweze kufanikiwa
"kutimiza lengo lako" au "kufikia lengo lango"
Joshua 1:8-9
Maelezo ya jumla
Yahweh anaendelea kuongea na Yoshua
Siku zote uuongee
Hii ina maana kwamba Yoshua alitakiwa kuongea juu kitabu cha sheria mara kwa mara. Neno 'mchana na usiku' huongeza mkazo na uzito.
Kisha utastawi na kufanikiwa
Kimsingi maneno haya mawili yanamaanisha kitu kile kile na pia yanatia mkazo juu ya kufanikiwa kwa hali kubwa.
Je si mimi niliyekuagiza?
Hii inamrejelea Yahweh akimwamuru Yoshua. "Ni mimi niliyekuagiza!"
Uwe hadori na jasiri!
Yahweh anamwagiza Yoshua.
Joshua 1:10-11
Nendeni katika kambi na waagizeni watu, 'andaeni... kuimilik
Nukuu ya maneno yaliyo katika funga semi yaweza kuelezwa kama "Nendeni katika kambi na uwaamuru watu waandae mahitaji kwa ajili yao. Baada ya siku tatu watavuka mto huu wa Yordani na kuingia ndani yake na kuimiliki nchi ambayo Yahweh Mungu wao anawapa ili kuimiliki.
Watu
Watu wa Israeli
katika siku tatu
Siku tatu baada ya sasa
vukeni mto huu wa Yordani
"kuvuka" ina maana ya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya mto.
Joshua 1:12-13
Maneno ya jumla
Makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manasee yalichagua kukaa mashariki mwa Mto wa Yordani.
Warubeni
Hawa ni wazawa wa Warubeni.
Wagadi
Hawa walikuwa ni wazawa wa Gadi.
Joshua 1:14-15
Maelezo kwa ujumla
Yoshua anaendelea kuongea na Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.
Watoto wenu
"watoto wenu wadogo"
ng'ambo ya Yordani
Inarejelea upande wa mashariki wa mto Yordani. baadaye Waisraeli wengli waliweza kuishi magharibi wa Yordani, hivyo wakaaita sehemu ya mashariki "ng'ambo ya Yordani' Lakini kwa wakati huu watu wote wakali katika upande wa mashariki mwa Yordani.
kuwapa ndugu zenu pumziko
Hii inarejelea waisraeli kuwashinda manabii wao wote wanaokaa katika nchi ya Kanaani ambao walipaswa kuwashinda.
uta........ na kuimiliki
Hii ina maana ya kuishi maisha yao kwa amani katika nchi
ng'ambo ya Yordani, mahali jua linapochomoza
Inarejelea upande wa mashariki mwa mto wa Yordani.
Joshua 1:16-18
Maelezo ya jumla
Waisraeli hawa walikuwa ni Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase ambao walimjibu Yoshua.
Yeyote anayeasi maagizo yako na kutotii maneno yako
Virai hivi vya manane kimsingi vina maana moja tu na pia vinatia mkazo kuwa aina yoyote ya uasi itaadhibiwa.
atauawa
Hii inaweza kuelezwa kwa kauli tendaji: ''Tutamwua''
Uwe hodari na jasiri tu
Mungu pamoja na Waisraeli walizingatia mambo yote kuwa ya muhimu kwa Yoshua kuendelea kama kiongozi wao.
Joshua 2
Joshua 2:1-3
Nuni
Huyu ni baba yake na Yoshua
Shitimu
Hili ni jina la mahali katika upande wa mashariki wa Mto wa Yordani. Ina maana ya "Miti ya Akasia."
Wapelelezi
Hawa ni watu waliotembelea nchi ili kupata taarifa juu ya jinsi ya Israeli kuitwaa.
Joshua 2:4-5
Maelezo ya jumla
Rahabu yule kahaba aliwahifadhi wale wapelezi wawili wa Israeli ili wasidhuriwe.
Lakini mwanamke alikuwa amewachukua na kuwaficha
Tukio hili lilifanyika kabla ya wajumbe wa wafalme hawajaongea naye.
Mwanamke
Neno hili linamrejelea Rahabu, kahaba.
Machweo
Huu ni muda ambao siku inaanza kubadilika na kuwa giza la usiku.
Joshua 2:6-7
Lakini alikuwa amewachukua.....darini
Haya ni maelezo ya msingi na yanaeleza jinsi alivyowaficha wanaume katika 2:4
Darini
Dari lilikuwa bapa na imara, ambalo watu waweza kutembea tembea juu yake
kitani
NI mmea ambao ulikuaukiwa na nyuzi nyuzi, ambazo zilitumika kwa kutengeneza nguo
Hivyo, watu waliwafuatilia njiani
Watu waliwafuatilia wapelelezi kwasababu ya kile ambacho Rahabu alikuwa amewaambia katika 2:4
vivuko
Hizi ni sehemu za mto ambazo hazina kina kirefu cha maji kiasi kwamba watu wanaweza kuvuka kwa kutembea kwa miguu.
Joshua 2:8-9
walikuwa hawajalala
Hii inarejelea kwenda kulala wakati wa usiku
Ninajua kwamba Yahweh amewapa ninyi nchi
Neno 'ninyi' linawarejelea watu wa Israeli
hofu juu yenu imetuingia
"hofu yaweza kuelezewa kwa hali tofauti." " Sisi tunawaogopeni ninyi."
watayeyuka mbele yenu
Watu wenye hofu wanalinganishwa na kuyeyuka kwa barafu na kutiririkia mbali. Maana zinazokubalika ni 1)watakuwa wadhaifu mbele za uwepo wa Waisraeli 2) watasambazwa.
Joshua 2:10-11
Maelezo ya jumla
Rahabu anaendelea kuongea na wapelelezi wa Kiisraeli.
Bahari ya mianzi
Hili ni jina jingine la Bahari Nyekundu
Sihoni na Ogu
Haya ni majina ya wafalme wa Waamori
mioyo yetu iliyeyuka na hapakuwa na ujasiri wowote uliosalia
Virai hivi vya maneno vina maana sawa, yameunguanishwa ili kuonesha mkazo. Maneno "mioyo yetu ikayeyuka" yanalinganisha mioyo ya watu waoga na kuyeyuka kwa barafu na kutiririka.
Joshua 2:12-13
Maelezo ya jumla
Rahabu anaendelea kuongea na wapelelezi wa kutoka Israeli
tafadhali mniapie ... Nipeni ishara ya uhakika
Maneno haya yanafanana kimaana kumhusu Rahabu akitafuta uhakika kutoka kwa wapelelezi.
Nimekuwa mwema kwenu
Neno 'kwenu' linarejelea wapelelezi wawili
kuhifadhi maisha...mtatuokoa katika kifo
Ni njia ya upole ya kusema "msituue sisi."
Joshua 2:14
Maelezo ya jumla
Wapelelezi wa Kiisraeli wanatoa ahadi ambayo Rahabu aliiomba
Maisha yetu kwa ajli ya maisha yenu
Hii ni njia nyingine ya kusema, " Kama tukifa, mtakufa. Kama tukiishi, nanyi mtaishi."
Joshua 2:15-17
Maelezo ya jumla
Wapelelezi wa Israeli wanaendelea kuongea na Rahabu.
kama hautalifanya hili
jambo hili linaelezea juu ya sharti la ahadi ambalo wapelelezi walikuwa wamelifanya kwa Rahabu. Neno 'hili' linarejelea juu ya kufunga kamba katika dirisha katika 2:18
Joshua 2:18-19
Sentensi kiunganishi
Wapelelezi wa Kiisraeli wanafafanua sharti walilolisema katika 2:15
Maelezo ya jumla
Wapelelezi wa Kiisraeli wanaendelea kuongea na Rahabu
Na yeyote aendaye mtaani nje ya milango ya nyumba yako
Maneno haya yanaelezea juu ya sharti kwa kuweka hali ambayo yaweza kutokea
damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao
Hii ina maana ya "kifo chao kitakuwa kwasababu ya makosa yao wenyewe"
juu ya vichwa vyao
Neno "vichwa" linawakilisha uwajibikaji binafsi
hawatakuwa na hatia yoyote
watakuwa waadilifu wasio na kosa
kama mkono utanyoshwa juu
"kama tutasababisha madhara
Joshua 2:20-21
Maelezo ya jumla
Wapelelezi wa Kiisraeli wanaendelea kuonge na Rahabu juu ya ahadi zao kwake
Maelezo ya jumla
Wapelelezi walimtaka Rahabu kukaa kimya juu ya safari yao la sivyo wangekuwa huru dhidi ya kiapo cha kuilinda familia yake.
Ikiwa utaongea
kiwakilishi 'u' kinamrejelea Rahabu
Yote uliyoyasema nayatimie
Rahabu alikubaliana na matakwa ya kiapo ili kuokoa familia yake
Joshua 2:22
Maelezo ya jumla
Wapelelezi wa Israeli wanaondoka Yeriko
watu waliowafuatilia walirudi
Wale watu waliowafuatilia walirudi katika mji wa Yeriko
bila kuwaona
Hili linarejelea hao watu ambao hawakuwapata wapelelezi
Joshua 2:23-24
Wale watu wawili walirudi
Watu wawili walirudi katika kambi ya Waisraeli
walirudi na kuvuka mto
Haya maelezo ya maana sawa yakirejelea kurudi kule walikokuwa katika kambi ya Waisraeli
kuvuka
"kuvuka'' ina maana ya kwenda upande wa pili wa ukingo wa mto. Kusafiri kutoka upande huu hadi upande wa pili wa Yordani"
Nuni
Hili ni jina la kiume; baba yake na Yoshua
kila kitu kilichotokea kwao
"mambo yote ambayo watu walikuwa wameyapata na kuyaona."
sisi
Neno hili 'sisi' linawarejelea Waisraeli
Wenyeji wote wa nchi wanayeyuka
Watu wa nchi mbele ya Israeli ni kama kitu kinachoyeyuka katika joto.
Joshua 3
Joshua 3:1
Aliamka
Maana ya neno "alimka'' ina maana ya ''kuinuka"
Shitimu
Ni sehemu katika nchi ya Moabu, maghariibi mwa Mto Yordani mahali ambapo Waisraeli walikuwa wamepiga kambi kabla ya kuingi katika nchi ya Kanaani.
Joshua 3:2-4
Maafisa
Hawa ni watu walioshikilia nafasi za maamlaka na kutoa maagizo
watu
Hili ni taifa la Israeli
dhiraa elfu mbili
"dhiraa 2,000" Neno ''dhiraa'' ni kipimo ambacho ni sawa na umbali kutoka kwenye kiwiko cha mkono hadi mwisho wa vidole.
Joshua 3:5-6
Jitakaseni ninyi wenyewe
Maneno haya yanarejelea maandalizi maalumu ya kuwa safi kidini au kiroho mbele za Mungu.
Yahweh atafanya maajabu
Yahweh atakuwa akifanya miujiza kwa ajili ya watu wote kuona na kushuhudia
Chukueni sanduku la agano
Haya yanawarejelea walawi ambao hulichukua Sanduku la Agano kwa kusudi la kulibeba kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Joshua 3:7-8
Maelezo ya jumla
Yahweh anamwambia Yoshua kile ambacho kuhani alipaswa kufanya
nitakufanya kuwa mtu mkubwa
Yahweh atamheshimu Yoshua mbele ya watu wote wa Israeli.
macho ya Waisraeli
Inawarejelea Waisraeli wote watakaoona tukio hili
ukingo wa maji ya Yordani,
Yoshua ataukaribia ukingo wa Mto wa Yordani
Joshua 3:9-11
Maelezo ya jumla
Yoshua anawaambia kile ambacho Yahweh alikuwa yuko karibu kufanya
atawaondosha mbele yenu
Yahweh atafukuzia mbali watu wengine walioishi katika ili watoke au wauwawe.
kuvuka
"kuvuka" ina maana ya kwenda upande mwingie wa ukingo wa mto, au '' kusafiri kutoka upande kwenda upande mwingine."
Joshua 3:12-13
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kuwaambia Waisraeli juu ya miujiza ambayo Yahweh ataifanya
Maelezo ya jumla
Kama vile baba wa Israeli walivyovuka katika Bahari nyekundu, watu hawa watashuhudia kuvuka Mto Yordani katika nchi kavu.
nyayo za miguu
ina maana ya sehemu za chini ya miguu yao
chemichemi
Neno hili linarejelea mwelekeo wa mtiririko wa maji ya mto Yordani kuelekea Israeli.
yatasimama katika chuguu moja
Maji yatatulia katika sehemu moja. Hayatatiririka kuelekea waliko makuhani.
Joshua 3:14-16
sanduku la agano
Neno ''sanduku'' hapa linarejelea sanduku ambalo lina mbao za mawe
ukingo wa maji
Inarejelea sehemu ya juu ya maji kama vile ilivyo katika ukingo wa kisima ambapo maji hutiririkia katika sehemu kavu
Yordani hujaa hadi katika kingo zake zote katika kipindi chote cha mavuno
Haya ni maelezo ya msingi na yanakazia yale ambayo Yahweh anayafanya.
Joshua 3:17
Maelezo ya jumla
Uvukaji wa kimuujiza wa Mto Yordani unaendelea
Yordani
Neno hili linarejelea sehemu ya chini udongoni ya Mto Yordani
kuvuka
Neno hili lina maana ya kwenda upande mwingine wa mto. Kusafiri kutoka upande mwingine kwenda upande wa pili.
Joshua 4
Joshua 4:1-3
Maelezo ya jumla
Ingawa Yahweh alikuwa anaongea moja kwa moja na Yoshua, matukio yote yalihusu Israeli.
kuvuka
Neno hili lina maana ya kwenda upande mwingine wa mto. Kusafiri kutoka upande mwingine kwenda upande wa pili
Yordani
Mto Yordani
Uwape agizo hili.........
Nukuu hii inaweza kuelezwa kwa kauli isiyo ya moja kwa moja. "Uwape agizo hili wachukue mawe kumi na mbili kutoka katikati ya mto Yordani mahali ambapo makuhani walisimama katika nchi kavu na kuyaleta na kuyaweka mahali mtakapolala usiku huu."
Joshua 4:4-5
Maelezo ya jumla
Yoshua anawaambia watu kumi na wawili kitu cha kufanya
katikati ya Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe moja mabegani
Kila mtu kati ya watu kumi na wawili walitakiwa kuchukua mawe makubwa kutoka sehemu ya chini ya Mto Yordani na kuyabeba mpaka sehemu nyingine ili kujenga jengo la ukumbusho.
Joshua 4:6-7
Maelezo ya jumla
Yoshua anawaambia Waisraeli maana ya fungu la mawe kumi na mawili.
Maji ya Yordani yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh
Sentesi hii inaweza kuelezwa katika kauli tendaji: "Yahweh aliyatenga maji ya Yordani mbele ya sanduku la agano lake"
Maji ya Yordani
Mto Yordani
yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh
Mto Yordani ulizuiliwa na Mungu ili usitiririke kuelekea sanduku la Agano ambalo lilikuwa limebebwa na makuhani.
maji ya Yordani yalisimamishwa
Maji yaliyotiririka katika Mto Yordani yalikoma mbele ya sanduku ili kwamba kila mtu pamoja na agano lenyewe lisafiri katika nchi kavu.
Joshua 4:8-9
Maelezo ya jumla
Yoshua na Israeli wanaendelea kufanya kama Yahweh alivyowaagiza.
walichukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani
Hii inawarejelea watu kumi na wawili waliochukua mawe kutoka udongo ulio katikati ya Mto Yordani
Kisha Yoshua akayapanga mawe kumi na mbili katikati ya Yordani
Haya yalikuwa mawe kumi na mawili ya ziada, siyo yale mawe ambayo watu kumi na wawili waliyachukua kutoka katika undongo wa mto.
Joshua 4:10-11
Yordani
linarejelea Mto Yordani
Watu
Linarejelea taifa la Israeli.
Kuvuka
Hii ina maana ya kwenda upande mkabala wa ukingo wa mto. "kusafiri kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine."
mbele za watu
Hii inarejelea kuwa mbele za watu au katika macho ya watu wote. Kila mmoja aliliona sanduku lililokuwa limebebwa na makuhani.
Joshua 4:12-14
Kabila la Rubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase walipita kama jeshi
Hawa walikuwa ni wanajeshi wa makabila matatu ambayo yalikuwa yanatimiliza wajibu wao wa kuwaongoza Waisraeli katika vita kwa ajili ya kukaa upande wa mashariki wa Mto Yordani.
kama ambavyo wa....
Neno 'wa' linarejelea watu wa Israeli
Walimheshimu Musa
Neno hili halimaanishi to kuheshimu lakini pia kutii agizo lake na kumjali kama amiri jeshi wa jeshi lao kama walivyomfuata Musa.
Joshua 4:15-16
Maelezo ya jumla
Yahweh anamwambia Yoshua ili awaambie makuhani watoke katika Mto Yordani.
Joshua 4:17-18
Maelezo ya jumla
Mwandishi alikuwa anakiweka wazi kile kilichogawanya Mto Yordani hakikuwa cha tofauti na kile kilichogawanya Bahari Nyekundu kwa ajili ya kizazi kilichotangulia.
maji ya Yordani yalirudi katika sehemu zake na kujaa hadi katika kingo zake
Mto Yordani ulikuwa ukifurika katika kingo zake na kugharikisha eneo kabla na baada ya Israeli kuvuka katika nchi kavu.
Siku nne
Siku 4
Joshua 4:19-21
kukwea kutoka Yordani
Hii inarejelea kipindi ambacho Israeli ilivuka Mto Yordani katika nchi kavu.
Katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza
Huu ni mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiebrania. Siku ya kumi iko karibu na mwisho wa mwezi wa tatu wa kalenda za Kimagharibi.
Mawe kumi na mawili ambayo yalichukuliwa katika Yordani
Kila kabila lilitakiwa kuchukua jiwe moja kutoka katika Mto wa Yordani ili Yoshua aweze kutengeneza kumbukumbu ya tukio la kuvuka mto.
Joshua 4:22-24
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kuwakumbusha watu kusudi la kurundika mawe.
waambieni watoto wenu
Ilikuwa ni kazi ya Israeli kuwafundisha watoto wao juu ya miujiza ya Mungu ili kwamba waweze kumheshimu Yahweh milele.
mkono wa Yahweh ni nguvu
Kifungu hiki kinarejelea Nguvu ya Yahweh kuwa ni wenye nguvu. "Yahweh ni Mwenye nguvu"
Joshua 5
Joshua 5:1
mioyo yao ikayeyuka, na hapakuwa na moyo wowote ndani yao
Virai hivi viwili kimsingi vinamaaanisha kitu kimoja na kutia mkazo zaidi juu ya hofu yao.
mioyo yao ikayeyuka
Hapa "mioyo" inarejelea ujasiri wao. Walikuwa wameogopa sana kana kwamba ujasiri wao uliyeyuka kama sega la asali katika moto. "Walipoteza ujasiri wao wote."
hapakuwa na moyo wowote ndani yao
Hapa neno "moyo" linarejelea juu ya utashi wao wa kupigana. "Hawana tena hamu ya kupigana"
Joshua 5:2-3
Tengenezeni visu vya mawe na mara moja mwatahiri wanaume wote
Kulikuwa na watu waume zaidi ya 600,000/, hivyo na ijulikane kuwa wakati Yoshua alikua ni kiongozi wa kazi hii, watu wengi walimsaidia. Twaweza kusema pia "Yoshua na waisraeli wenyewe walijitengenezea visu vya mawe........ waliwatahiri wanaume wote.
Gibea Haaraloti
Hili ni jina la mahali/sehemu ambalo lilikuwa ni kwa ajili ya kumbukumbu ya Waisraeli kujitoa kwao mbele kwa Yahweh. Ina maana ya "kilima cha magovi"
Joshua 5:4-5
Maelezo ya jumla
Sababu ya kuwafanya wanaume wote watahiriwe imeelezwa
watu wa vita
Hawa ni watu amba walikuwa na umri wa kutosha kuwa wanajeshi.
Joshua 5:6-7
hawakuitii sauti ya Yahweh
Hapa neno "sauti" linarejelea vitu ambavyo Yahweh aliyasema. "tii mambo yale ambayo Yahweh amewaagiza"
nchi inayotiririka maziwa na asali
Mungu alizungumzia juu ya nchi ambayo ilikuwa nzuri kwa wanyama na mimea kana kwamba yalikuwa ni maziwa na asali kutoka kwa wanyama na mimea ilikuwa ikitiririka katika nchi. Pia twaweza kusema "Nchi ambayo ilikuwa ni ni nzuri kwa kufugia mifugo na kukuzia mazao."
Joshua 5:8-9
Siku hii nimeiondoa kwenu aibu ya Misri.
Aibu yao imeongelewa kana kwamba ni jiwe kubwa lililozuia njia yao. Hapa neno "kuiondoa'' ina maana ya "kuihamisha" Au twaweza kusema, Siku hii ya leo nimeiondoa aibu yako ya Misri
Joshua 5:10-11
siku ya kumi na nne ya mwezi,
Hii ni siku ya karibu na mwisho wa mwezi Marchi katika Kalenda ya Nchi za Magharibi. "Siku ya kumi na nne ya mwezi wa Kwanza"
Joshua 5:12
Mana
Mana kilikuwa ni chakula cheupe cha nafaka ambacho Mungu aliwapatia Wana wa Israeli ili wale katika kipindi cha miaka 40 walioishi jangwaani baada ya kuwa wametoka Misri. Mana ilionekana kama vipande vyeupe vilivyoonekana juu ya nchi kila asubuhi katika umande. Ilikuwa na ladha tamu kama asali. Waisraeli walikusanya mana kila siku isipokuwa siku ya Sabato. Siku moja kabla ya Sabato Mungu aliwaambia waisraeli kukusanya mana mara mbili ili wasikusanye siku ya kupumzika. Neno 'mana' lina maana ya ''Hiki ni nini?" Katika Biblia neno 'Mana' pia hurejelewa kama "Mkate kutoka mbinguni" na "nafaka kutoka mbinguni."
Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli.
Istilahi hii "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Lina maana ya "Alishindana na Mungu." Uzao wa Yakobo ulikuja ukajulikana kama "Watu wa Israeli," "taifa la Israeli''l au Waisraeli. Mungu alifanya Agano na taifa la Israeli. Walikuwa ni watu wake wateule. *Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mawili. .
Kanaani, Wakanaani
Kanaani alikuwa ni mtoto wa Hamu, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wana wa Nuhu. Wakanaani walikuwa ni uzao wa Kanaani. Neno "Kaanani" au "nchi ya Kanaani" pia inarejelea sehemu ya nchi iliyo katikati ya Mto Yordani na Bahari Kuu (Meditraniani). Nchi hii ilikaliwa na Wakanaani, pamoja na baadhi ya makabila mengine. *Mungu alimwahidi Ibrahimu kumpa nchi ya Kanaani na uzao wake, yaani Waisraeli.
Joshua 5:13
aliinua macho
Hapa, neno kuinua macho linazungumziwa kana kwamba Yoshua aliinua macho yake dhahiri katika mikono yake. Maneno haya yana maana ya "aliaangalia juu"
tazama
Neno "tazama" linalotoa tahadhari kwetu ili tuweze kuzingatia kwa namna ya kipekee kwa maelezo mapya.
alikuwa amechomoa upanga wake na ulikuwa mkononi mwake
Kiwakilishi 'a' na kimilikishi 'wake' yanmrejelea mtu yule aliyekuwa amesimama mbele ya Yoshua.
Joshua 5:14-15
Akajibu
Kiwakilishi 'a' kinawakilisha mtu yule ambaye Yoshua alimwona
la hasha
Hili ni neno la mwanzoni la jibu la mtu kwa swali la Yoshua. "Je uko upande wetu au wa maadui zetu?"Jibu fupi hili laweza kuelezwa kama "Siko upande wenu wala upande wa adui zenu"
Yoshua akainamisha uso wake juu ya nchi akaabudu
Hili lilikuwa ni tendo la ibada/ kuabudu
Vua viatu vyako miguuni mwako
Hili lilikuwa ni tendo la heshima na unyenyekevu
Joshua 6
Joshua 6:1-2
Basi
Neno hili limetumika hapa kuonesha pumziko katika masimulizi. Hapa msimlizi anatueleza kwanini malango ya Yeriko yalikuwa yamefungwa
nimeweka Yeriko katika mkono wako, mfalme wake pamoja na wanajeshi wake waliofunzwa.
Sehemu hii maneno "katika mkono wako" yana maana kwamba Yahweh alimpa Yoshua uwezo wa kuwaangamiza. Pia twaweza kusema, "Ninakupatia nguvu za kuishinda Yeriko, mfalme wake, na wanajeshi wakeo waliofundishwa."
Joshua 6:3-4
Sentensi kiunganishi
Mungu anaendelea kuongea na Yoshua juu ya kile ambacho watu walitakiwa kukifanya.
Ni lazima mfanye hivi kwa siku sita
"Ni lazima ufanye hivi mara moja kila siku kwa siku sita"
Makuhani saba lazima wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele za sanduku
Makuhani saba wangetembea mbele ya makuhani wengine ambao walikuwa wanalibeba sanduku na kutembea kuuzunguka mji.
Joshua 6:5
Sentensi kiunganishi
Mungu aendelea kuongea na Yoshua juu ya kile watu walichopaswa kufanya
watapuliza pembe za kondoo waume kwa nguvu kuu,
Kiwakilishi 'wa' kinarejelea makuhani saba. "Pembe za kondoo" na "tarumbeta" ni tarumbeta za pembe za kondoo dume ambazo makuhani walikuwa wakizipuliza katika 6:3
ukuta wa mji
"Huu ulikuwa ni ukuta wa nje wa mji" au "ukuta uliouzingira mji."
Joshua 6:6-7
Nuni
Huyu ni baba yake na Yoshua
Lichukueni sanduku la agano
"Libebeni sanduku la agano"
Joshua 6:8-9
Makuhani saba walibeba tarumbeta saba za pembe za kondoo mbele ya Yahweh
Maana zinazoweza kukubalika juu ya "mbele za Yahweh ni 1)"katika utii kwa Yahweh" 2) sehemu ya mbele ya sanduku la Yahweh"
walipuliza tarumbeta
"Walizipiga tarumbeta zao sana" au "makuhani walipuliza tarumbeta za pembe za beberu"
Sanduku la Yahweh liliwafuata kwa nyuma yao
Inaweza kuelezwa dhahiri kuwa kulikuwa na watu waliobeba sanduku. au " Makuhani walikuwa wamelibeba sanduku la agano la Yahweh waliwafuata kwa nyuma yao.""
walipuliza tarumbeta zao
"Walizipiga tarumbeta zao sana" au "makuhani walipuliza tarumbeta za pembe za beberu"
Joshua 6:10-11
Sauti yoyote isitoke vinywani Sauti yoyote isitoke vinywani
Sauti kutoka vinywani mwao inarejelea kuongea au kupiga kelele kwao
Lakini Yoshua aliwaagiza watu
Yoshua alikuwa amewaamuru watu kabla ya kuanza kutembea kwa kuuzunguka mji.
Joshua 6:12-14
wakipuliza tarumbeta
Hii ina maana kwamba walizipuliza tarumbeta kiasi cha kuzifanya zitoe sauti kubwa kwa mara nyingi. Pia inaweza kumaanisha kuwa "Waliendelea kuzipiga tarumbeta zao kwa nguvu," au "Makuhani waliendelea kuzipuliza pembe za kondoo dume."
Walifanya hivi
Hii ina maana ya "Waisraeli walitembea kuizunguka Yeriko mara moja kwa kila siku."
Joshua 6:15-16
Watu
Neno hili linawarejelea watu wa Israeli
walipiga tarumbeta
"Waliziliza tarumbeta kwa nguvu" au "kuzipuliza tarumbeta za pembe za beberu"
amewapa ninyi
Neno"ninyi" linarejelea taifa lote la Israeli.
Joshua 6:17-19
Sentensi kiunganishi
Yoshua anaendelea kuongea na watu wa israeli.
Mji pamoja na vitu vyote ndani yake vitatengwa kwa Yahweh kwa ajili ya uharibifu.
Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa kauli tendaji: "Ni lazima kuzitenga kwa Yahweh mji na kila kitu ndani yake kwa ajili ya kuharibiwa"
iweni waangalifu juu ya kuchukua vitu
Kuwa mwangalifu kunaongelewa kana kwamba wao ni walinzi wenyewe. "Iweni waangalifu msivichukue vitu"
mtaleta matatizo katika kambi
Kufanya kitu fulani kinachofanya mambo mabayaa kutokea katika mji kunasemwa kama kuleta matatizo juu yake.
Hazina ya Yahweh
Mkusanyiko wa vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kumwabudia Yahweh.
Joshua 6:20-22
watu wakapiga kelele
"Watu wa Israeli wapiga kelele"
Ilikuwa
Neno hili limetumika hapa kuonesha tukio muhimu katika habari.
makali ya upanga
Ingawa watu wengi wa Israeli hutumia upanga, katika sehemu hiii inarejelea mashambulizi yenye vurugu au vita kwa ujumla. Au twaweza kusema "Kwa panga zao zenye makali" au "katika vita"
Joshua 6:23-24
Na wakachoma mji
kiwakilishi 'wa'kinawarejelea wanajeshi wa Kiisraeli. Hairejelei wale vijana wawili tu waliowatoa nje Rahabu na familia yake.
Joshua 6:25
anaishi Israeli
Kiwakilishi 'a'kinamrejelea Rahabu na kinawakilisha uzao wake. Yaani "Uzao wake unaishi Israeli."
mpaka leo
"sasa" au "hata leo" uzao wa Rahabu ulikuwa bado unaishi Israeli wakati mwandishi wa awali alipokuwa akiandika habari hii.
Joshua 6:26-27
Alaaniwe machoni pa Yahweh mtu yule anayeujenga mji huu
kulaaniwa mbele la Yahweh ina maana ya kulaaaniwa na Yahweh. Yaani "Yahweh na amlaani mtu yule atakayejenga.."
Ataujenga msingi kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza
Matokeo ya mtu kuweka malango mapya kwa mji wa Yeriko ilikuwa ni kwamba mwana wake wa kwanza wa kiume angekufa. Hii inaongelewa kana kwamba ilikuwa ni gharama ambayo mtu alitakiwa kuilipa. "Kama utauweka msingi, atampoteza mwana wake wa kwanza.
kwa gharama ya mzaliwa wake wa pili atapachika milango yake
Matokeo ya mtu kuweka malango mapya kwa mji wa Yeriko ilikuwa ni kwamba mtoto wake mdogo wa kiume angekufa. Hii inaongelewa kana kwamba ilikuwa ni gharama ambayo mtu alitakiwa kuilipa. "Kama utauweka msingi, atampoteza mwana wwake mdogo."
umaarufu wake ulienea
"Umaarufu wa Yoshua ulienea" Kujulikana miongoni wa watu katika nchi yote, kunasemwa kama kuenea kwa umaarufu wake. "Yoshua alijulikana na kuwa maarufu katika nchi yote.
Joshua 7
Joshua 7:1
vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu
"Vitu ambavyo Mungu alikuwa amevisema lazima vitengwe kwa ajili yake kwa kuviteketeza"
Akani...Karmi... Zabdi...
Haya ni majina ya wanaume.
Hasira ya Yahweh ikawaka
"Hasira" na "kuwaka" yanaonesha uzito, siyo kwamba moto ulikuwapo dhahiri. "Hasira ya Yahweh iliwaka kama moto"
Joshua 7:2-3
Watu wote
Inarejelea jeshi lote la Israeli.
watu ni wachache
linarejelea watu wa Ai
Joshua 7:4-5
watu wapatao elfu tatu tu kutoka katika jeshi
Hawa ni wanaume walikuwa sehemu ya jeshi. "Watu elfu tatu waliokuwa ni sehemu ya jeshi waliopanda."
watu elfu tatu.... watu thelathini na sita
wanaume sita..-"3,000 watu ... 36 wanaume"
mioyo ya watu iliogopa... ujasiri wao uliwatoka
Vifungu hivi viwili vya maneno vina maana sawa na vimeunganishwa ili kutilia mkazo kwamba watu waliogopa sana.
mioyo ya watu
Kirai hiki kinawarejelea wanajeshi wa Kiisraeli
ujasiri wao ukawatoka
"hawakuwa na ujasiri tena ndani yao"
Joshua 7:6-7
alizirarua nguo zake. Yeye pamoja na wazewe wa Israeli waliweka mavumbi juu ya vichwa vyao na wakainamisha vichwa vyao hadi katika nchi mbele ya sanduku la Yahweh
Walifanya vitu hivi ili kumwonesha Mungu jinsi walivyo na huzunisshwa na kufedheheshwa.
Kutuweka katika mikono ya Waamori ili kutuangamiza?
Yoshua alikuwa anauliza kama hii ni sababu ya Mungu kuwaleta ng'ambo ya Yordani. "Je ulifanya hivi ili kututia katika mikono ya Waamori ili kututeketeza?"
Kutuweka katika mikono ya Waamori ili kutuangamiza?
Katika mikono ya Waamori inawakilisha utawala na mamlaka. Kuwatia Waisraeli katika mikono ya Waamori ni kuwaruhusu Waamori kuwa na mamlaka juu ya Waisraeli na kuwaangamiza.
ikiwa kama tulifanya maamuzi tofauti
Neno "ikiwa kama" linaonesha kuwa haya ni matakwa ambayo bado hayajatokea. "Ninatamani tungefanya maamuzi tofauti."
Joshua 7:8-9
Maelezo ya jumla
Yoshua anamwelezea Mungu juu ya wasiwasi uliokuwepo
niseme nini, baada ya Israeli kuwatega migongo maadui zao!
Yoshua aliyasema haya kuonesha jinsi alivyokuwa amekatishwa tamaa kana kwamba alikuwa hana hata neno la kusema. "Sijui kitu cha kusema.Israeli imegeuka na kukimbia mbele za adui zao."
Israeli kuwatega migongo maadui zao
Kufanya hivyo kunamaanisha kukimbia kutoka kwa maadui zao. "Israeli imekimbia kutoka kwa maadui zao."
watatuzunguka na kuwafanya watu wa nchi kulisahau jina letu
Kuwafanya watu wasahau jina la Israeli ina maana ya kuwafanya waasahau Waisraeli. Kwa namna hii watalifanya hili kwa kuwaua Waisraeli. "Watatuzunguka na kutuua, na watu wa dunia watatusahau sisi."
Na utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?
Kifungu cha maneno "jina lako kuu" mahali hapa kina maana ya Sifa za Mungu na uweza. "Na je utafanya nini ili watu wajue kuwa wewe ni mkuu."
Na utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?
Yoshua alitumia swali hili kwa ajili ya kumtahadharisha Mungu kwamba kama Waisraeli watauwawa, ndipo watu wengine watadhani kuwa Mungu si mkuu. "Hakutakuwa na kitu utakachokifanya kwa ajili ya jina lako kuu" au "Watu hawatajua kwamba wewe ni mkuu."
Joshua 7:10-12
Maelezo ya jumla
Yahweh anamwambia Yoshua kwanini Israeli imelaaniwa.
kwanini umelala kifudifudi?
Mungu alitumia swali hili kumkemea Yoshua kwa kulala kifudifudi. "Acha kulala hapo kifudifudi katika uchafu!."
vitu vilivyokuwa vimetengwa
Hivi ni vitu "viliwekwa kwa ajili ya kuharibiwa" kutoka katika 6:17 "Vitu vilivyolaaniwa" au "Vitu vile ambavyo Mungu amevilaani"
Wameiba na kisha pia wakaficha dhambi yao
Kuficha dhambi ina maana ya kujaribu kuwafanya watu wengine wasijue kuwa wametenda dhambi. "Wameviiba vitu vile na kisha walijaribu kuwaficha watu wasijue kuwa wametenda dhambi"
hawataweza kusimama mbele za maadui zao
Kusimama mbele ya maadui zao kuna maana ya kupigana kwa mafanikio dhidi ya maadui zao. Hivyo ina maana ya "hawataweza kupigana kwa mafanikio dhidi ya maadui zao" au "hawataweza kuwashinda maadui zao."
Walitega migongo yao kwa maadui zao
Kutega migongo kuna maana ya kukimbia mbali kutoka kwa maadui zao.
Sitakuwa pamoja nanyi tena
Kuwa pamoja na Israeli kuna maana ya kuwasaidia Waisraeli. "Sitawasaidieni tena."
Joshua 7:13
Sentensi kiunganishi
Yahweh anaendelea kuongea na Yoshua na kumwambia kitu cha kuwaambia watu
Watu
Inarejelea watu wa Israeli
Hamtaweza kusimama mbele ya maadui zenu
Kusimama mbele za maadui zao kuna maana ya kupigana kwa mafanikio dhidi yao. "Hamtaweza kuwashinda maadui zenu"
Joshua 7:14-15
Sentensi kiunganishi
Yahweh anaendelea kumwambia Yoshua kile anachopaswa kuwaambia watu.
mtajisogeza wenyewe kwa makabila
Kulikuwa na makabila kumi na mawili yaliyowafanya watu wa Israeli. Kifungu cha maneno "kwa makabila" kina maana ya "kila kabila"
Kabila lile ambalo Yahweh atalichagua litasogea karibu kwa koo zake
Kabila hujengwa na makabila mengi. "Kutoka katika kabila ambalo Yahweh amelichagua, kila kabila litakaribia,"
Kabila ambalo Yahweh atalichagua
Viongozi wa Israeli watapiga kura, na kwa kufanya hivi, wangejifunza ni kabila gani Yahweh alikuwa amelichagua.
Ukoo ule ambao Yahweh atauchagua lazima usogee karibu kwa nyumba
Ukoo ulijengwa na familia/nyumba kadhaa. "Kutoka katika ukoo ambao Yahweh ameuchagua, kila nyumba itasogea karibu."
Nyumba ambayo Yahweh ataichagua lazima isogee karibu kwa mtu mmoja mmoja
Nyumba iliundwa na watu kadhaa. "Kutoka katika nyumba ambayo Yahweh ameichagua, kila mtu atasogea karibu"
Itakuwa hivi mtu yule atakayechaguliwa
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji "Yeye ambaye Yahweh anamchagua"
amelivunja agano la Yahweh
Kuvunja agana kuna maana ya kutolitii. "Ameliasia agano la Yahweh"
Joshua 7:16-18
Maelezo ya jumla
Yoshua anafuata agizo la Yahweh la kuwaleta Waisraeli mbele za Yahweh.
aliwaleta Israeli karibu
Maneno "kabila kwa kabila" lina maana ya kila kabila.
Kabila la Yuda lilichaguliwa
Maneno haya yanaweza kuelezwa kawa muundo tendaji. "Yahweh alilichagua kabila la Yuda"
Akausogeza karibu ukoo wa Zera mtu kwa mtu,
kirai "mtu kwa mtu" ina maana ya kila mtu. Watu katika sentensi hii walikuwa ni viongozi wa nyumba zao.
ukoo wa Zera
Ukoo uliitwa kawa jina la mtu aliyeitwa Zera
Zabdi...Akani...Karmi...Zera
Haya ni majina ya wanaume.
Joshua 7:19-21
ufanye ukiri wako kwake
Maneno "fanya ukiri wako" yaweza kufafanuliwa kwa kitenzi 'kiri' "Kiri kwake"
Usinifiche
Kuficha maelezo ina maana ya kujaribu kumficha mtu asijue. "usinizuie kujua kile ulichokifanya."
Shekeli mia mbili
Hii ni zaidi ya kilogramu mbili
shekeli hamsini
Hii ni zaidi ya gramu 500
Vimefichwa chini ardhini
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Nilivificha chini ardhini."
Joshua 7:22-23
Walipoangalia
"Watu wale Yoshua aliwatuma waliaangalia"
Walivimwaga
kumwaga vitu vingi chini
Joshua 7:24
bonde la Akori
Jina la maana ya "bonde la matatizo," lakini ni vizuri kulitafsiri jina Akori kama linavyosikika.
Joshua 7:25-26
"Kwanini umetusumbua?
Yoshua anatumia swali hili kumkemea Akani. "Umetutesa"
Na wakawachoma wote kwa moto, na wakawapiga mawe
Maana zinazokubalika 1) Waisraeli waliichoma familia ya Akani hadi kifo na kisha wakawafunika kwa mawe. 2) Waisraeli waliipiga kwa mawe familia ya Akani na kisha wakaichoma kwa moto miili yao.
Yahweh akaachilia mbali hasira yake
Kuachilia mbali hasira ina maana ya kuacha kuwa na hasira. Kuwaka kwa hasira ina maana ya kuwa na hasira kali.
hata leo
Ilikuwa bado linaitwa bonde la Akori katika kipindi ambacho mwandishi aliandika. "hata leo" au "hata sasa"
Joshua 8
Joshua 8:1-2
Usiogope; usivunjike moyo
Vifungu hivi viwili vya maneno kimsingi vinamaanisha kitu kimoja. Yahweh ameviunganisha pamoja kutia mkazo kwamba hakuna sababu ya kuogopa.
nimemtia mkononi mwako mfalme wa Ai... na nchi yake
Kuwatia katika mkono wa Israeli ina maana ya kuwapa waisraeli ushindi na kuwatawala. "Nimewapeni ushindi dhidi ya mfalme wa Ai na watu wake, na nimewapeni utawala juu ya mji wake na nchi yake."
Nimewapeni
Mungu anaongelea juu ya ahadi alizoahidi kufanya kana kwamba alikuwa ameshakifanya, kwasababu atalifanya kwa uhakika. "NItawapa kwa uhakika"
mfalme wake
Neno 'wake' inarejelea mji wa Ai.
Joshua 8:3-4
watu wa vita
"jeshi la Israeli"
watu elfu thelathini
wanaume 30,000
Joshua 8:5-7
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea to kuelezea mapango wa vita kwa wanajeshi wake
atawapa mkononi mwenu.
"mkono" inaashiria utawala na nguvu za watu walizo nazo juu ya maadui zao.
Joshua 8:8-9
Maelezo ya jumla
Yoshu anamalizia kueleza mpango wa vita kwa wanajeshi wake.
Yoshua akawatuma
Maneno haya yanamrejelea Yoshua akiwatuma watu thelathini walikuwa wamechaguliwa ili kuivamia Ai mahali ambapo watakaa ili kuvizia.
sehemu ya kuvizia
"mahali ambapo wangejificha mpaka wakati wa kushambulia."
Joshua 8:10-12
watu elfu tano
"Wanaume 5,000" Kundi hii linaonekana kuwa sehemu ya watu "elfu thelathini (8:8). Hili ni kundi dogo lilosalia katika hali ya kuvizia wakati watu wengine 25,000 walipouvamia mji.
Joshua 8:13-14
Maelezo ya jumla
Waisraeli wanajianda kupigana na watu wa Ai.
jeshi kubwa
kundi kubwa la watu wapiganaji, si kundi lile lililokuwa katika hali ya kusubiri
walinzi wa nyuma
wale walikuwa wamewekwa katika hali ya kuvizia upande wa magharibi mwa mji.
Joshua 8:15-17
walikubali wenyewe kushindwa mbele yenu
"waache washindwe mbele ya watu wa Ai." Maneno"mbele yao" yana maana ya kile ambacho watu wa Ai wakiona na kukifikiria.
walikubali wenyewe kushindwa mbele yenu
Neno "kushindwa" laweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "waache watu wa Ai wafikiri kwamba wameshawashinda Waisraeli."
mbele yao...waliwafuata...walivutwa mpaka mbali
Maneno "yao" na "wa" yanarejelea jeshi la Ai.
walikimbia... waliwafuata
Maneno haya yanalihusu jeshi la Israeli.
Watu wote waliokuwa kwenye mji waliitwa kwa pamoja
Maneno haya yanaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " viongozi wa mji walliwaita watu wote kwa pamoja katika mji.
Watu wote waliokuwa katika mji
Mwandishi anaongelea kwa njia ya jumala juu ya watu wote, lakini ilikuwa ni juu ya watu wote wanaoweza kupigana.
Waliuacha mji
"Waliuacha mji ukiwa hauna ulinzi kabisa" au " baada ya kutoka, kulikuwa hakuna mtu yeyote wa kuulinda mji"
Joshua 8:18-23
nitaitia Ai mikononi mwako.
Kuiweka Ai katika mkono wa Israeli ina maana ya kuipa Israeli ushinid na utawala juu ya Israeli.
Joshua 8:24-26
baada ya Israeli walipokuwa wamemaliza kuuwaua wenyeji ... baada ya wao wote... walipokuwa wamekwisha kulala kwa ncha ya upanga
Mwandishi anatumia sentens hizi, ambazo zote zina maana moja, zikiwa na maana ya Israeli walikuwa wamelitii agizo la Mungu la kumwua kila mtu huko Ai.
walikuwa wameanguka kwa makali ya upanga
Hapa maana ya kuanguka ni kufa, na makali ya upanga yanamaanisha vita au jeshi la Israeli.
elfu kumi na mbili
"12,000"
Joshua 8:27-28
mahali palipoachwa ukiwa
Ni sehemu ambapo watu walioishi hapo kwanza, lakini sasa hakuna mtu aishiye hapo.
Joshua 8:29
hata leo
"leo" au "hata sasa"
Joshua 8:30-33
Mlima Ebali
Ni mlima ulioko huko Kanaani.
Joshua 8:34-35
Halikusalia hata neno moja katika yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua ambalo halikusomwa
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa kauli kubalifu kama "Yoshua alisoma kila neno kati ya yote ambayo Musa aliyaagiza" au "Yoshua aliisoma sheria yote ya Musa."
Israeli
Neno hili linalirejelea taifa la Israeli
Joshua 9
Joshua 9:1-2
Yordani
Jina la Mto Yordani
chini ya amri moja
amri hapa inamwakilisha mtu yule aliyewaamrisha. Kuwa chini yake ina maana ya kutii amri yake. "Kutii amri ya kiongozi mmoja."
Joshua 9:3-5
mpango wa udanganyifu
mpango wa uongo ulikusudia kuwahada Yoshua na Waisraeli.
mikavu na yenye uvundo
"kavu na iliyojaa fangasi" au iliyochina na kuharibika"
Joshua 9:6-8
Watu wa Israeli
inalirejelea taifa lote la Israeli
Wahivi
Hili ni jina jingine la Wagibeoni
Huenda mnaishi karibu nasi. Twawezeje kufanya agano nanyi?
Yoshua anatia mkazo kuwa watu wa Israeli lazima wafuate amri ya yahweh juu ya vitu vyote. "kama mnaishi karibu nasi, hatuwezi kufanya agano nanyi"
Joshua 9:9-10
Yordani
Hili ni jina la Mto Yordani
Sihoni
Hili ni jina la Mfalme wa Waamori aliyeshindwa.
Heshiboni
Hili ni jina la mji wa kifalme wa taifa la Moabu.
Ogu
Hili ni jina la mfalme wa Bashani aliyeshindwa
Ashitarothi
Hili ni jina la mji uliojulikana kwa kuabudu mungu mke aliyeitwa kwa jina hilo hilo.
Joshua 9:11-13
mkononi mwako
Kifungu hiki cha maneno kina maana ya "kuchukua" Neno 'mkono' linamaanisha kumiliki vitu vya Wagibeoni.
mkutane nao na muwaambia
Neno 'nao' linawarejelea watu wa Israeli.
Joshua 9:14-15
Yoshua akafanya amani pamoja nao na kufanya agano pamoja nao ili waishi. Viongozi wa watu nao pia wakawaapia
Sentensi hizi mbili zinaongelea juu ya jambo lile lile lililotokea. Yoshua, kiongozi wa taifa aliahidi kutowaua Wagibeoni. Viongozi wa taifa la Israeli, hivyo hivyo walifanya agano. "Yoshua na viongozi wa Israeli walifanya agano la damu na watu wa Gibeoni."
watu
Neno hili hapa linawarejelea watu wa Israeli.
Joshua 9:16-17
siku tatu
inarejelea namba tatu katika mpangilio
Kefira
Huu ni mmoja kati ya miji ya Wagibeoni.
Beerothi
Hili ni jina la mahali.
Kiriathi Yearimu
Hili ni jina la mahali.
Joshua 9:18-19
watu
Neno hili hapa linamaanisha taifa la Israeli.
Joshua 9:20-21
Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji
"Wagibeoni wakawa wakata kuni na wabeba maji."
Joshua 9:22-23
nyumba ya Mungu wangu
Maneno haya hapa yana maana ya sehemu ya Yahweh ya kukaa, yaani Hema la kukutania.
Joshua 9:24-25
Chochote kilicho chema na haki
Maneno 'chema' na 'haki' yanamaanisha kimsingi kitu kile kile. "chochote kilicho sawa na haki"
Joshua 9:26-27
aliwafanyia
neno hili linawarejelea Wagibeoni.
hadi leo
Kirai "hadi leo" kina maana ya wakati ambao mwandishi alikuwa anaishi. "hata sasa"
Joshua 10
Joshua 10:1-2
Ikawa
Neno hili limetumika hapa kuonesha pumziko katika mtiririko wa masimulizi ya habari. Hapa mwandishi anaongelea mtu mpaya katika habari, Adonizedeki.
Adonizedeki
Hili ni jina la kiume la mfalme muhimu
Joshua 10:3-4
Yarmuthi
Hili ni jina la mji
Lakishi
Hili ni jina la mji
Egloni
Hili ni jina la mji
Hohamu...Piramu...Yafia... Debiri
Haya ni majina ya wafalme
Njooni kwangu
Yerusalemu ni mji ulioinuliwa sana kuliko miji mingine ya Kanaani. "Safirini mje hapa nilipo"
Joshua 10:5
Yarmuthi
Hili ni jina la mji
Lakishi
Hili ni jina la mji
Egloni
Hili ni jina la mji
Joshua 10:6-7
Walisema
Kiwakilishi 'wa' kinawarejelea Wagibeoni.
Msiuondoe
Hili ni ombi la upole lililoelezwa kwa kauli hali lakini likitegemea tendo chanya.
mikono yenu
Neno 'mkono' lina maana ya nguvu za watu wa Israeli. "Tumia nguvu zako kutulinda sisi."
Joshua 10:8
Nimewatiwa wote katika mkono wako
Hapa neno "mkono" linawakilisha nguvu za watu wa Israeli na uwezo wao wa kuwashinda maadui zao.
Joshua 10:9-10
Yoshua aliwafikilia
Jina Yoshua, kamanda wao, limetumika hapa kuonesha Jeshi lote la Israeli.
Bethi Horoni
Hili ni jina la sehemu
Azeka...Makeda
Haya ni majina ya sehemu
Joshua 10:11
alitupa mawe makubwa kutoka mbingun
"kutupa mawe makubwa ya mvua kutoka mawinguni"
Joshua 10:12
Jua lisimame katika Gibeoni, na mwezi, usimame katika bonde la Aijalon
Yoshua anaomba kwamba Yahweh angefanya mwendelezo wa muda ukome katika siku hii.
jua...mwezi
Yoshua analiagiza jua na mwezi kana kwamba walikuwa ni watu.
Bonde la Aijaloni
Hili ni jina la mahali
Joshua 10:13-14
taifa
Hili linarejelea watu wa Israeli.
Je hili halikuandikwa katika Kitabu cha Yashari
Mwandishi anatumia swali hili kama usuli kuwakumbusha msomaji kwamba tukio hilo ni vizuri kumbukumbu. Katika: 'hii imeandikwa katika Kitabu cha Yashari'
Joshua 10:15-17
Makeda
Hili ni jina la mji
Taarifa zilimfikia Yoshua
Wajumbe walikuja na kumwambia Yoshua. "Mtu fulani alimwambia Yoshua."
Joshua 10:18-19
katika mkono wenu
Maneno haya "katika mkono wenu" hapa yana maana ya "utawala wako"
Joshua 10:20-21
Makeda
Hili ni jina la mahali
Na hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema hata neno moja kinyume na watu wa Israeli.
Hapa "neno moja" linaongelea juu ya maadui wa Israeli. "Hakuna hata mmoja aliyethubutu kulaumu au kupinga kinyume"
Joshua 10:22-23
Yarmuthi...Lakishi... Eguloni
Haya ni majina ya sehemu
Joshua 10:24-25
Kila mtu wa Israeli
Kila askari jeshi wa Israeli
Joshua 10:26-27
hadi leo
mpaka mwandishi alipoandika habari hii
Joshua 10:28
Aliwateketeza wote kabisa pamoja na kila kiumbe hai kilichokuwa huko. Hakuna hata mmoja aliyesalia.
Sentensi ya pili ni fupisha sentensi na kutia mkazo kwamba Yoshua hakumwacha hai mtu au mnyama yeyote.
Joshua 10:29-30
Libna
Hili ni jina la mji
aliitia katika mkono wa Israeli
hapa neno 'mkono' una maana ya "kutawala" "Aliwapa Israeli utawala dhidi yao"
Joshua 10:31-32
Libna... Lakishi
Haya ni majina ya miji muhimu
katika mkono wa Israeli
Kauli hii ina maana ya "kuwata utawala kwa taifa la Israelil." "Bwana aliiweka Lakishi chini ya utawala wa Israeli
Joshua 10:33
Horamu
Hili ni jina la kiume la mfalme
Gezeri
HIli ni jina la mji
Joshua 10:34-35
Egloni
Hili ni jina mji
Waliupiga kwa upanga na waliteketeza kila mtu ndani yake
Sentensihizi zina maana moja. kwa pamoja vinaonesha utimilifu
Lakishi
Hili ni jina la mji
Joshua 10:36-37
Egloni
Hili ni jina la mji
aliuteka mji na kuwaua kwa upanga
upanga unawakilisha jeshi la Israeli, na kitendo cha kuwapiga na kuna maana ya kuwachinja
Waliuteka mji na kuwaua kwa upanga watu wote ndani yake pamoja na mfalme wake, kujumuisha na vijiji vyote vilivyoizunguka. Waliteketeza kabisa kila kiumbe hai ndani yake, hawakuacha hata mtu mmoja aliyesalia
Sentensi hizi mbili zinazungumzia kimsingi maana moja, na zimeunganishwa ili kutia mkazo. Kwa pamoja zinatia mkazo na kuonesha ukamilifu wa uharibifu.
Joshua 10:38-39
Debiri
Hili ni jina la mji
Waliwaua wote kwa upanga
Neno 'upanga' linawakilisha jeshi la Israeli na kuwaua ina maanya ya wazo la kuwaua na kuwaharibu.
Joshua 10:40-43
Hakuna hata mfalme moja aliyebaki hai kati ya wafalme wake wote
virai hivi viwili vina maana sawa na vinatia mkazo juu uharibifu halisi ambao watu Israeli walikuwa wameagizwa naYahweh.
Yoshua aliwaua kwa upanga
upanga unawakilisha jeshi la Israeli na kuwaua ina maanaya wazo la kuwaua na kuwaharibu.
Joshua 11
Joshua 11:1-3
Yabini...Yobabu
Haya ni majina ya wafalme
Ashafu...Kinerethi...Dori...Mlima Hermoni
Haya ni majina ya mahali
Hazori...Madoni...Shimuroni...Akshafu...Kinerethi...Dori ...Mlima Hermoni
Haya ni majina ya mahali
Joshua 11:4-5
Maelezo ya jumla
Wafalme wa Kanaani wamshambulia Yoshua na taifa la Israeli.
wanajeshi wengi sana, hesabu yao ilikuwa kama mchanga wa pwani
Maneno haya ya kutia chumvi yanatia mkazo kwamba jeshi lilikuwa kubwa lenye watu wengi sana ambalo wafalme hawa walilikusanya.
Meromu
Hili ni jina la sehemu/mahali
Joshua 11:6-7
ninawatia hao kwa Waisraeli wakiwa wafu
Yahweh anaiwezesha Israeli kulishinda jeshi la adui na kuwaua wanajeshi wote, na inaongelewa kana kwamba Yahweh ndiye aliyewaua wanajeshi na kisha akawatia kwa Waisraeli. "NItaiwezesha Israeli kuwaua wote katika vita."
Utaivunja vunja miguu ya farasi zao
"kuifanya farasi zao kuwa kilema kwa kuivunja miguu yao." Tendo hili ni la kukata misuli ya nyuma ya miguu ili farasi wasiweze kutembea.
Meromu
Hili ni jina la Mahali/sehemu
Joshua 11:8-9
Yahweh akawatia maadui katika mkono wa Israeli
Hapa neno "mkono" linawakilisha nguvu. Yahweh analiwezesha jeshi la Israeli kuwashinda maadui zao, kitendo hiki kinasemwa kana kwamba Yahweh aliwaweka jeshi la maadui katika mkono wa waisraeli.
waliwapiga kwa upanga...Waliwaua wote
Hapa neno "upanga" unawakilisha silaha zote zilizotumika kuwashambulia adui zao.
Misrefothi - Maimu
HIli ni jina la sehemu/mahali
Alivunja miguu ya farasi
Hiki ni kitendo ambacho cha kukata misuli ya nyuma ya miguu ya farasi ili farasi washindwe kukimbia.
Joshua 11:10-11
Alimwua mfalme wake kwa upanga
"Yoshua alimwua mfalme wa Hazori kwa upanga wake"
Hazori ulikuwa ni kichwa cha falme hizi zote
Mji wa Hazori ni mji muhimu, unatajwa kama kichwa cha falme zingine.
Waliwapiga kwa upanga kila kiumbe chenye uhai kilichokuwa huko, na alivitenga ili viteketezwe, hivyo hapakuwa na kiumbe hai kilichoachwa hai
Virai hivi viwili vina maana sawa na vinatilia mkazo kuwa maangamizi halisi.
alivitenga ili viteketezwe
Kiwakilishi 'a' kinamwakilisha Yoshua na kinajumuisha jeshi lote ambalo alikuwa akiliongoza. Walikiteketeza kabisa kila kitu kilicho hai katika mji. Vitu hivi vinasemwa kana kwamba viliwekwa wakfu ili viteketezwe.
Joshua 11:12-13
akawapiga wote kwa upanga
"Aliwauwa"
miji iliyojengwa juu ya vilima vya vifuasi vya udongo
"miji iliyojengwa juu vilima vidogo"
Joshua 11:14-15
kwa ajili yao wenyewe
Kirai hiki kinarejelea juu ya jeshi la Israeli.
Waliua kila mtu kwa upanga hadi pale walipokufa wote. Hakuna kiumbe hai kilichoachwa hai
Virai hivi viweili vina maana sawa na vinatilia mkazo juu ya uharibifu halisi
Yoshua hakuacha kufanya hata jambo moja
Kauli hii ya kukanusha inatilia mkazo kwamba Yoshua alifanya kili kitu ambacho Yahweh alimwagiza.
Joshua 11:16-17
Mlima Halaki...Baali Gadi
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 11:18-20
Yahweh ambaye alikuwa ameifanya kuwa migumu mioyo yao
Yahweh aliwasababisha watu wa miji kuwa wakaidi, inasemwa kana kwamba Yahweh ndiye alikuwa ameifanya mioyo yao kuwa migumu.
Joshua 11:21-22
Anakimu
Hawa walikuwa ni wazawa wa Anaki
Debiri... Ababu
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 11:23
Yoshua aliwapa Israeli kama urithi
Kitendo cha Yoshua kuwapa waisraeli nchi kunasemwa kana kwamba alikuwa amewapa Israeli urithi kama mali ya kudumu.
nchi ikapumzika bila vita
Watu walikuwa wahapigani vita tena, nchi inasemwa kana kwamba alikuwa ni mtu aliyepumzika kutoka katika vita. "Watu hawakupigana vita tena katika nchi" au "kulikuwa na amani katika nchi"
Joshua 12
Joshua 12:1-2
Basi
Neno hili limetumika hapa kuonesha pumziko katika habari kuu. Hapa mwandishi anaanza kutoa maneno ya nyuma.
hawa ni wafalme
inawarejelea orodha ya wafalme na inaendelea mpaka katika mstari wa 24
Araba... Aroeri
Haya ni majina ya mahali/sehemu
Sihoni... Heshiboni
Tafsiri maneno haya kama vile ulivyofanya katika 9:9
Joshua 12:3-5
Bahari ya Kinerethi
Hii ni sehemu. Tafsiri kama vile alivyofanya katika 11:1
Bethi Yeshimothi... Mlima PIsiga... Ashitarothi..Edrei..Saleka.
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Ogu, mfalme wa Bashani
Tafsiri maneno haya kama vile ulivyofanya katika 9:9
Refaimu... Wamakathi
haya yalikuwa majina ya makundi ya watu
Joshua 12:6
Waerubeni
Hawa walikuwa wazawa wa Rubeni
Wagadi
Hawa walikuwa wazawa wa Gadi
nusu ya kabila la Manase
Wanaitwa nusu ya kabila kwasababu nusu nyingine ya kabila walipewa urithi wao katika nchi ya Kanaani.
Joshua 12:7-8
Baali Gadi..Mlima Halaki...Araba
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 12:9-12
Enaimu...Yarmuthi...Lakishi...Eguloni..Gezeri
Haya ni majina ya miji. Tafsiri "Yarmuthi, Lakishi na Eguloni" kama ulivyofanya katika 10:3
Joshua 12:13-16
Debiri... Gederi...Horma..Aradi...Libna...Adulamu...Makeka
Haya ni majina ya miji
Joshua 12:17-20
Tapua..Heferi...Afeki...Lasharoni...Madoni...Hazori...Shimroni Meroni..Akshafu
Haya ni majina ya miji
Joshua 12:21-24
Taanaki...Megido...Kedeshi...Yokneamu...Dori...Goyimu......Tiriza
Haya ni majina ya miji
thelathini na moja kwa ujumla
"31 kwa ujumla"
Joshua 13
Joshua 13:2-3
Nchi iliyosalia ndio hii
Unaweza kuifafanua kwamba nchi ya Israeli ilikuwa bado inahitaji.
Shihori
Hili ni jina la mahali
inayofikiriwa kuwa ni mali ya Wakanaani;
Kauli hii inawezaa kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Wakanaani hufikiri kuwa ni mali yao."
Waavi
Hili ni jina la kikundi
Joshua 13:4-5
Meara...Afeki...Baali Gadi...Mlima Hermoni
Haya ni majina ya sehemu
Wagebali
Hili ni jina la kikundi cha watu walioishi huko Geba.
Joshua 13:6-7
Misrefothi Maimu
Jina la mahali
nchi ....kama urithi
Nchi ambayo Israeli wataichukua inasemwa kuwa kama ilikuwa urithi ambao wataupokea kama mali ya kudumu.
Joshua 13:8-9
Aroer...Medeba...Diboni
Haya ni majina ya mahali
bonde
sehemu ya mto iliyo ya chini sana kutoka usawa wa nchi katika kingo zake.
nyanda
nchi tambarare juu ya mto
Joshua 13:10-12
Heshiboni...Saleka... Ashitarothi...Edrei
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Maakathi...Refaimu
Haya ni majina ya makundi ya watu
Mkoa wa Wageshuri
"nchi ambayo Wageshuri waliishi"
Musa aliwapiga
Hapa "Musa" inawakilisha jeshi la Waisraeli ambalo Musa aliliongoza. "Musa na Waisraeli waliwashambulia."
Joshua 13:13
Wageshuri au Wamakathi
Haya ni majina ya makundi ya watu
Wageshuri na Wamakathi wanaishi miongoni mwa Waisraeli
"Geshuri" na "Makathi" ni majina ya waanzilishi au mababu wa Wageshuri na Wamaakathi au ni majina ya miji walioishi. "Watu wale waliishi kati ya Waisraeli.
hadi leo
hii inarejelea kipindi ambacho mwandishi alikuwa akiandika.
Joshua 13:14
halikupewa urithi na Musa
Nchi ambayo Musa aliyapa makabila ya Israeli inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao watu waliupokea kama mali ya kudumu.
Urithi wao ni sadaka za Yahweh
Mwandishi anaongelea juu ya heshima kubwa ambayo Walawi walikuwa nayo ya kumtumikia Yahweh kama makuhani na ya kwamba sadaka zingekuwa urithi wao.
sadaka za Yahweh
"sadaka ambazo watu walizileta kwa Yahweh"
zilitolewa kwa moto
kauli hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambazo makuhani walizichoma kwa moto"
Joshua 13:15-16
Aroeri...Medeba
Haya ni majina ya sehemu/mahali
bonde... nyanda
Tafsiri manen haya kama ulivyofanya katika 13:8
Joshua 13:17-19
Heshiboni...Diboni...Bamothi...Baali... Bethi Baalimeoni...Yahazi....Kedemothi....Mefathi... Kiriathaimu.......Sibuma...Zerethishahari.
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 13:20-21
Bethi Peori...Pisiga..Bethi Yeshimothi...Heshiboni
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Sihoni...Evi...Rekemu...Zuri...Huri...Reba
Haya ni majina ya watu
pamoja na viongozi wa Midiani
"kama ambavyo alikuwa amewashinda viongozi wa Midiani"
Joshua 13:22-23
huu ni mpaka wao
Mto Yordani ulikuwa mpaka upande wa magharibi wa nchi ambayo kabila la Reubeni waliipokea.
Huu ulikuwa urithi wa kabila la Rubeni
Nchi ambayo Musa aliwagawia kabila la Rubeni inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni urithi ambao kabila la Rubeni walipokea kama mali ya kudumu.
uliotolewa kwa kila ukoo,
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji: "ambao Musa aliwapa kila ukoo."
Joshua 13:24-26
Yazeri...Aroeri...Heshiboni...Ramathi Mizipe...Betonimu...Mahanaimu...Debiri
Haya ni majina ya mahali
Joshua 13:27-28
Bethi Haramu...Bethi Nimra....Zafoni....Heshiboni
Haya ni majina ya mahali/sehemu
Huu ni urithi wa kabila la Gadi
Nchi ambayo Musa aliwagawia kabila la Gadi inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni urithi ambao kabila la Gadi walipokea kama mali ya kudumu.
Joshua 13:29-31
Musa aliwapa urithi nusu ya kabila la Manase
Nchi ambayo Musa aliwapa nusu ya kabila la Manase inazungumziwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao aliwapa kama mali ya kudumu.
nusu ya kabila la Manase
Ni nusu tu ya kabila ilipokea nchi hii kwasababu nusu nyingine ilipokea nchi katika upande mwingine wa mto Yordani.
Uligawiwa
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Musa aliugawa"
Mahanaimu...Yairi...Ashitarothi...Edrei.
haya ni majina ya mahali/sehemu
Makiri
Hili ni jina la mwanaume.
hii iligawanywa
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Musa alizigawa hii miji"
Joshua 13:32-33
Huu ni urithi ambao Musa aliowagawia
Nchi ambayo Musa aliyagawia makabila ya Israeli upande wa mashariki wa mto Yordani unazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni urithi ambao Musaaliwapakama urithi.
Yahweh, Mungu wa israeli, ni urithi wao
Mwandishi anazungumzia juu ya heshima kubwa ambayo Walawi walikuwa nayo kwa kumtumikia Yahweh kama makuhani kana kwamba Yahweh kilikuwa ni kitu fulani ambacho watarithi.
Joshua 14
Joshua 14:1
Maeneo haya ya nchi ambayo watu wa Israeli waliyapokea kama urithi wao
Nchi ambayo waisraeli waliipata inazungumzwa kana kwamba ilikuwa ni urithi ambao waliupata kama mali ya kudumu.
Urith huu uligawanywa kwao na Eliazeri kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya mababu wa familia zao kati ya watu wa Israeli
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambao Eliazeri kuhani , mwana wa Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa makabila ya familia za mababu zao katika Israeli waliwapa."
Viongozi wa makabila
Hawa walikuwa viongozi wa kila kabila
Joshua 14:2-5
Urithi wao ulichaguliwa kwa kupiga kura
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. Eliazeri, Yoshua na viongozi wa makabila walipiga kura kuamua urithi wao."
kwa mkono wa Musa
Hapa neno "mkono" unamwakilisha Musa mwenyewe na ina maana ya Yahweh alimtumia Musas kama wakala ili kutoa agizo hili.
Musa alikuwa amewapa urithi makabila mawili na nusu ng'ambo ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi wowote
Makabila mawili na Nusu yalipewa urithi ng'ambo ya Yordani, lakini kwa Walawi hawakupewa urithi wowote. Nchi ambayo Musa aliyapa makabila inasemwa kana kwamba ni urithi ambao walipokea kama miliki yao ya kudumu.
Na hakuna sehemu yoyote ya urithi waliyopewa Walawi katika nchi
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Na Musa hakuwapa sehemu yoyote ya urithi kwa Walawi katika nchi."
sehemu ya nchi
Kipande cha ardhi
lakini walipewa miji ya kuishi ndani yake
Kitenzi huenda kimetolewa kwa maelezo yaliyotangullia."lakini aliwapa miji fulani ili kuishi ndani yake."
maeneo ya malisho
haya ni mashamba ya nyasi kwa ajili kulishia mifugo.
riziki zao
hivi ni vitu walivyohitaji ili waweze kuhudumia familia zao.
Joshua 14:6-7
Yefune
Hili ni jina la mwanaume
Mkenizi
Hili ni jina la kikundi cha watu
Nilimletea taarifa tena kama nilivyotakiwa kufanya katika moyo wangu.
Hapa neno "moyo" linawakilisha mawazo. Hii ni nahau inayorejelea taarifa iliyotolewa kwa uadilifu.
Joshua 14:8-9
waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa woga
Kitendo cha kuwafanya watu waogope kinaongelewa kama ilikuwa ni kuyeyusha mioyo ya watu.
Lakini mimi nilimfuata Yahweh kabisa
Kuwa mwaminifu kwa Yahweh kunaongelewa kama kumfuata Yahweh. "Nilibaki mwaminifu kwa Yahweh"
nchi ambayo miguu yako imetembea juu yake itakuwa urithi wako na kwa watoto wako milele
Nchi ambayo Kalebu na watoto wake wangepewa inaongelewa kana kwamba ni urithi ambao wangeupokea kama miliki ya kudumu.
nchi ambayo miguu yako imetembea juu yake
hapa maneno "miguu yako" inamwakilisha Kalebu.
Joshua 14:10-11
Tazama
"Sikiliza" Neno hili linaongeza mkazo kwa kile kilichosemwa baadaye.
wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani
"Wakati watu wa israeli walisafiri huko jangwani"
Nguvu zangu za sasa ni sawa na nguvu zangu za kipindi kile
"Bado nina nguvu sasa kama nilivyokuwa hapo mwanzo."
kwa kwenda na kwa kuja.
Hii ni nahau inayorejelea shughuli za kila siku. "Kwa ajili ya mambo ninayoyafanya kila siku."
Joshua 14:12
nchi ya milima
Maana zinazokubalika a) vilima vingi vikubwa au milima midogo au b)mlima mmoja.
Anakimu
Hili ni jina la kikundi cha watu
Joshua 14:13-15
alimpa Hebroni kama urithi wake
Hebroni inaongelewa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao Kalebu aliupokea kama mali ya kudumu.
hata leo
hii inarejelea kipindi ambacho mwandishi wa kitabu hiki
alimfuata kabisa Yahweh,
Kuwa mwaminifu kwa Yahweh kunatajwa kana kwamba kumfuata Yahweh kweli kweli. "Alibaki akiwa mwaminifu kwa Yahweh"
Kiriathi Arba
Hili ni jina la mahali/sehemu
Kisha nchi ikawa na raha bila vita.
Watu walikuwa hawapigani vita tena. Hali hii inaangaliwa kama nchi kupumzika kama vile mtu anavyopumzika kutoka katika vita.
Joshua 15
Joshua 15:1-2
Sini
Hili ni jina la sehemu ya jangwa
ghuba
sehemu ndogo ya ziwa ambayo imeingia katika sehemu ya nchi kavu
ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini
"kutoka katika ghuba iliyokabili upande wa kusini sehemu ya mwisho ya Bahari ya Chumvi" Virai hivi viwili vya maneno vinarejelea sehemu moja. Kirai cha pili kinafafanua sehemu unapoanzia mpaka wa kusini.
iliyokabili upande wa kusini
"ambayo imegeukia kuelekea kusini"
Joshua 15:3-4
Mpaka wao
"Mpaka wa nchi iliyo mali ya kabila la Yuda"
Akirabimu...sini....Hebroni... Addari...Karka...Azimoni
Haya ni majina ya sehemu/mahali
kijito cha Misri
huu ni mto mdogo wa maji katika ukingo wa upande wa kusini magharibi mwa nchi, karibu na Misri.
Joshua 15:5-6
katika mdomo wa Yordani
Sehemu ambayo mto humwaga maji yake baharini inazungumzwa kana kwamba ulikuwa ni mdomo wa mto.
mpaka...ulianzia
"mpaka...ulikuwa"
Bethi Hogla...Bethi Araba
haya ni majina ya sehemu/mahali
JIwe la Bohani
Hili lilikuwa ni jiwe kubwa lililowekwa na mtu fulani kama alama ya mpaka na liliitwa kwa jina la mtu aliyeitwa Hohani.
Joshua 15:7-8
Debiri...bonde la Akori...mlima wa Adumimu..En shemeshi... En Rogeli...bonde la Ben Hinnomu..Bonde la Refaimu
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 15:9-10
Nefutoa..Mlima Efroni...Baala..Kiriathi Yearimu..Mlima Seiri..Mlima Yearimu.... Kesaloni...Bethi Shemeshi...Timna.
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 15:11-12
Shikeroni...Mlima baala...Yabuneeli
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 15:13-15
Kiriathi Arba...Debiri...Kiriathi Seferi
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Arba...Anaki...Sheshai...Ahimani...Talmai
Haya ni majina ya watu
wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki
Majina haya yanawakilisha koo za watu ambao walikuwa ni uzao wa Sheshai, Ahimani, na Talmai. Maneno "wana' na "wazawa" katika muktadha huu yanamaanisha kitu hicho hicho kimoja. "Koo tatu , Sheshai, Ahimani na Talmai, waliokuwa wazawa wa Anaki."
Alipanda kutoka pale kinyume
"Alienda kutoka hapo ili kupigana dhidi"
Joshua 15:16-17
Kiriathi Seferi
Hili ni jina la sehemu/mahali
Akisa
Hili ni jina la mwanamke
othinieli ...Kenazi
Haya ni majina ya wanaume.
Joshua 15:18
Akisa alienda kwa Othinieli
Hii ni nahau ambayo inamrejelea Akisa kuwa mke wa othinieli. "Wakati Akisa alipokuwa mke wa Othinieli."
alimsihi amwombe baba yake shamba
Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli ya moja kwa moja. 'alimsihi, 'mwombe baba yangu anipe shamba"
Joshua 15:19
chemichemi ya juu na chemichemi ya chini
Maneno "juu" na "chini" yanaongelea masuala ya mwinuko wa kijiografia katika sehemu za vijito vya maji.
Joshua 15:20
Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda,
Nchi ambayo kabila la Yuda lilipokea inaongelewa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupata kama mali ya kudumu.
waliopewa kufuatana na koo zao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao"
Joshua 15:21-24
Sentensi kiunganishi
mwandishi anaorodhesha miji ya kusini ambayo Yuda waliimiliki. Orodha inaendelea mpaka 15:29
Joshua 15:25-28
Maelezo unganishi
Orodha ya miji inaendelea
Joshua 15:29-32
maelezo unganishi
Orodha ya miji inaendelea
Joshua 15:33-36
Maelezo ya jumla
Mwandishi anaorodhesha miji ya upande wa Kaskazini ambayo Yuda iliimiliki.
Joshua 15:37-39
sentensi kiunganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:40-41
Sentensi kiunganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:42-44
Sentensi kiunganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:45-47
Sentensi kiunganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
makazi
"vijiji"
Kijito cha Misri
Mto mdogo wa maji katika ukingo wa upande wa kusini wa nchi karibu na Misri.
Joshua 15:48-51
Sentensi unganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:52-54
Sentensi unganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:55-57
Sentensi unganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:58-59
Sentensi unganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:60-62
Sentensi unganishi
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo Yuda ilipewa kuimiliki
Joshua 15:63
hadi leo hii
kipindi kinachorejelewa hapa ni kipindi ambacho mwandishi aliandika kitabu hiki.
Joshua 16
Joshua 16:1-2
Kabila la Yusufu
Kabila la Yusufu liliunganisha makabila ya wana wake wawili, Manase na Efraimu. Kwakuwa nusu ya kabila la Manase lilikuwa limeweka makazi mashariki mwa Yordani, sehemu hii inarejelea kabila la Efraimu na nusu nyingine ya kabila la Manase.
Luzi ...Atarothi
Haya ni majina ya mahali
Waarkiti
hili ni jina la kikundi cha watu
Joshua 16:3-4
Wayafuleti
Hili ni jina la kikundi cha watu
Loweri Bethi Horoni ... Gezeri
haya ni majina ya sehemu
makabila ya Yusufu, Manase na Efraimu
"makabila ya Manase na Efraimu, wana wa Yusufu"
waliupokea uirithi wao
Nchi ambayo makabila ya Manase na Efraimu waliimiliki inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu.
Joshua 16:5-7
Eneo la kabila la Efraimu ambalo lilikuwa limegawanya kwa koo zao
Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Eneo ...ambalo Yoshua aliwagawia kwa kufuata koo zao."
Atarothi Addari...Bethi Horoni ya juu...Mikimethathi...Taanathi Shilo...Yanoa...Naara
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 16:8-9
Tapua...Kana
Haya ni majina ya sehemu
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Efraimu
Nchi ambayo kabila la Efraimu waliimiliki inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu
Walipewa kwa koo zao
Maelezo haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwagawia kwa koo zao"
miji yao iliyochaguliwa
Maelezo haya yaweza kuelezwa kwa kauli tendaji. Miji ambayo Yoshua alikuwa ameichagua."
iyokuwa ndani ya urithi wa kabila la Manase
Nchi ambayo kabila la Manase waliimiliki inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu
Joshua 16:10
hadi leo
kipindi hiki kinachorejelewa hapa ni kipindi ambbacho mwandishi aliandika kitabu hiki.
Joshua 17
Joshua 17:1-2
mzaliwa wa kwanza wa Manase, ambaye alikuwa
"alikuwa ni mzaliwa wa kwanza"
Makiri...Abi Ezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi, na Shemida
Haya yalikuwa ni majina ya wanaume
Watoto wa Makiri walipewa nchi ya Gileadi na Bashani
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Yoshua aliwapa nchi ya Gileadi na Bashani wazawa wa Makiri.
Nchi iliyobaki iligawiwa .... walipewa kwa koo zao
Maelezo haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Yoshua aliwapa nchi.... na aliwapa kwa kufuata koo zao."
Joshua 17:3-4
Zelofehadi...Heferi...Eliazari
Haya ni majina ya wanaume
Mahila, Noa, Hogila, Milka, na Tirsa
Haya ni majina ya wanawake.
atupatie urithi wetu
Nchi inaongelewa hapa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao watu walilpewa kama mali ya kudumu. "kutupa sisi sehemu ya nchi kama urithi"
aliwapa wanawake hao urithi
Maana zinazokubalika a)"Yoshua aliwapa wale wanawake urithi" b) Eliazeri aliwapa wanawake urithi.
Joshua 17:5-6
alipewa sehemu kumi za nchi
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Yoshua aliwapa sehemu kumi za nchi."
"sehemu kumi"
"vipande kumi"
aliupokea urithi
Nchi inaongelewa hapa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao watu walilpewa kama mali ya kudumu. "kutupa sisi sehemu ya nchi kama urithi"
Nchi ya Gileadi iligawanywa
Hii inaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. "Yoshua aliwapa nchi ya Gileadi"
Joshua 17:7-8
Upande wa Kusini
"kuelekea kusini"
Mikimethathi ...Tapua
Haya ni majina ya mahali/sehemu
Joshua 17:9-10
Mpaka
"Mpaka wa nchi ya Manase"
kijito
sehemu ndogo ya mto
Kana
Jina la kijito
Kwa upande wa kaskazini ulifika hata Asheri
Maana zinakubalika ni a) mpaka wa nchi ya Manase ulifika na kugusua nchi ya kabila la Asheri b)ambayo waweza kusafiri kutoka Kaskazini na kufika Asheri.
upande wa mashariki, Isakari
Kitenzi huenda ni kile kile ambacho kimetolewa virai vilivyotangulia.
Joshua 17:11-13
Bethi Shani...Ibleamu...Dori...Endori...Taanaki...Megido....Nafethi.
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 17:14-15
wazawa wa Yusufu
Inarejelea makabila ya Efraimu na Manase
Kwanini umetupa mgao mmoja wa nchi na sehemu moja kwa ajili ya urithi, kwa kuwa tuko wengi , na kwa muda wote Yahweh umetubaliriki?
Watu wa makabila ya Efraimu na Manase waliuliza swali hili ili kutia mkazo kwamba Yoshua alitakiwa kuwapa sehemu kubwa ya nchi. "Ulitakiwa ungekuwa umetupa sisi sehemu zaidi ya kila mtu...Yahweh ametubariki."
mgao mmoja wa nchi na sehemu moja kwa ajili ya urithi
Virai hivi viwili kwa msingi vina maana moja. Katika kirai cha pili kinahusu juu nchi inayozungumziwa kama urithi ambao watu waliupokea kama mali kudumu.
sehemu
Kipande
watu wengi
Watu wengi kwa namba
"Kama ninyi ni watu wengi katika hesabu
Kwa kuwa ninyi ni watu wengi sana katika hesabu yao.
Refaimu
Hili ni jina kikundi cha watu
Joshua 17:16-18
Bethi Shani....Yezreeli
Haya ni majina ya mahali/sehemu
Nyumba ya Yusufu
Hapa neno "nyumba" inarejelea wazawa
Mtaufyeka
"Mtausafisha msitu wa miti" au " mtaikata miti yake"
Joshua 18
Joshua 18:1-2
na waliishinda nchi
Walikuwa wamewashinda watu walioishi katika nchi kabla hawajaweka hema la kukutania.
yalikuwa bado hayajapewa urithi wao
Nchi ambayo watu watairithi inaongelewa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao wangeupokea kama mali yao ya kudumu.
Joshua 18:3-4
Je mtaacha mpaka lini katika kuingia nchi ambayo Yahweh, Mungu wa baba zenu, amewapeni ninyi?
Yoshua aliuliza swali hili ili kuwatia moyo Waisraeli kuchukua umiliki wa nchi.
nchi juu na chini
maneno "juu na chini" yana maana ya kila mwelekeo/sehemu
Wataandika maelezo pamoja na maelekezo kuhusu urithi
Hii ina maana kwamba wataeleza sehemu za nchi ambazo kila kabila lingepokea kwa ajili ya urithi.
urithi wao
Nchi ambayo watu watairithi inaongelewa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao wangeupokea kama mali yao ya kudumu
Joshua 18:5-6
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendeleza hotuba yake kwa watoto wa israeli
Wataigawanya nchi
Wataigawa nchi
Yuda itasalia
"Kabila la Yuda litabaki"
nyumba ya Yusufu
Hapa neno "nyumba" inawakilisha wazawa wa Yusufu. Kirai kinayarejelea makabila ya Efraimu na Manase.
Joshua 18:7
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendeleza hutoba yake kwa watoto wa Israeli.
hana sehemu
Hakuna sehemu ya nchi
kwa kuwa ukuhani wa Yahweh ni urithi wao
Yoshua anazungumzia juu ya heshima kubwa ambayo Walawi walikuwa nayo kwa kumtumikia Yahweh, ilikuwa kana kwamba ulikuwa ni urithi.
nusu ya kabila la Manase
"nusu ya kabila la Manase"
wameshapokea urithi wao
Nchi ambayo watu watairithi inaongelewa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao wangeupokea kama mali yao ya kudumu
Joshua 18:8-9
Maelezo ya jumla
Yoshua anaongea na watu Ishirini na moja ambao walitakiwa kwenda kuiangalia nchi.
Juu na chini katika nchi
Maneno "juu na chini" yana maana ya sehemu zote."Pande zote za nchi" au "katika nchi yote"
Joshua 18:10
kila kabila lilipewa sehemu ya nchi.
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "kwa kila kabila Yoshua aliwapa sehemu ya nchi"
Joshua 18:11-12
Katika kabila la Benyamini, ugawanaji wa nchi ulifanyika kwa kupewa kwa koo zao
Hii inaweza kuelezwa muundo tendaji. "Kila kabila la Benyamini lilipewa kwa kufuata koo zao."
ati ya wazawa wa Yuda na wazawa wa Yusufu
"kati ya nchi ambayo ni mali ya wazawa wa Yuda na nchi iliyo mali ya wana wa Yusufu."
Wazawa wa Yusufu
hii inawarejelea kabila la Efraimu na Manase.
Bethi Aveni
Hili ni jina la mahali/sehemu
Joshua 18:13-14
Luzi...Atarothi Addari...Bethi Horoni...Kiriathi Baali...Kiriath Yearimu.
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 18:15-16
Kiriathi Yearimu...Efroni...Neftoa...Beni Hinomu...Refaimu...Hinnomu...En Rogeli
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 18:17-18
Eni Shemeshi...Gelilothi...Adumimu...Bethi Araba
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Jiwe la Bohani
Hili lilikuwa ni jiwe kubwa ambalo mtu fulani aliliweka kama alama na liliitwa kwa jina la mtu aliyeitwa Bohani.
bega la Bethi Araba
Nchi ambayo ina mteremko au mgongo ulioinama inasemwa kana kwamba ni bega. "Mteremko wa Bethi Araba"
Joshua 18:19-20
Bega la kaskazini la Bethi Hogla
Nchi ambayo ina muundo wa mteremko inazungumzwa kana kwamba ni bega.
Bethi Hogla
Hili ni jina la sehemu/mahali
huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Benyamini
Nchi ambayo kabila la Benyamini iliipokea inazungumzwa kana kwamba ilikuwa ni urithi wa ambao waliupokea kama mali ya kudumu.
walipewa kwa kila ukoo wao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji: "Yoshua aliwapa nchi kwa kila koo"
Joshua 18:21-24
Maelezo ya jumla
Mwandishi anaorodhosha miji ambayo ilikuwa katika nchi na ambazo kabila la Benyamini walipewa kuimiliki kama urithi wao.
vijiji vyake
"Vijiji vilivyoizunguka"
Joshua 18:25-28
Maelezo ya jumla
Mwandishi anaendelea kuorodhoshe miji ambayo ilikuwa katika nchi na ambazo kabila ala Benyamini.
Huu ulikuwa ni urithi wa Benyamini
Nchi na miji ambayo kabila l Benyamini walipewa inaongelewa kana kwamba ilikuwa ni urithi kama mali ya kudumu.
Joshua 19
Joshua 19:1
Upigaji wa pili wa kura uliangukia kwa Simoni
"Mara ya pili Yoshua alipopiga kura, kura ilionesha kabila la Simoni"
wa pili
Namba ya pili katika orodha
waligawiwa kwa kila ukoo wao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji: " Yoshua aligawa nchi kwa kila kabila lao"
Urithi wao ulikuwa katikati ya urithi ulikuwa ni mali ya kabila la Yuda.
Nchi waliyopewa makabila haya inazungumzwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu. "Nchi waliyopokea kama urithi ilikuwa katikati ya nchi ambayo kabila la Yuda walipewa kama urithi"
Joshua 19:2-4
Maelezo ya jumla
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo ilikuwa katika nchi ambayo kabila la Simoni waliipokea kama urithi wao.
Urithi waliokuwa nao
Nchi na miji ambayo kabila la Simoni liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu.
Joshua 19:5-7
Maelezo ya jumla
Mwandishi anaorodhesha miji ambayo ilikuwa katika nchi ambayo kabila la Simoni waliipokea kama urithi wao.
Ziklagi
Tafasiri kama ulivyofanya katika 15;19
Joshua 19:8-9
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simon
Nchi na miji ambayo kabila la Simoni liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu
waliopewa kwa koo zao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao"
Hii ni kwasababu nchi waliyopewa kabila la Yuda
Sentensi hii inaweza kuelezwa wa muundo tendaji: "Sehemu ya nchi ambayo Yoshua aliigawa kwa kabila la Yuda"
sehemu yao ya katikati
"Katikati ya sehemu ya nchi ya Yuda"
Joshua 19:10-11
Upigaji wa kura ya tatu
Tafasiri kirai hiki kama vile ulivyofanya katika 19:1
ya tatu
namba ya tatu katika orodha
Saridi...Marala..Dabeshethi...Yokineamu
Haya ni majina ya sehemu/mahali
mkabala na Yokineamu
"ng'ambo ya pili kutoka Yokineamu"
Joshua 19:12-13
Saridi....Kisilothi Tabori....Daberathi...Yafia...Gathi Hefa...Ethikazini...Rimoni...Nea
Haya ni majina ya sehemu/mahali.
Joshua 19:14-16
Hannathoni...Efta Eli Katathi...Nahalali...Shimroni...Idala...Bethlehemu
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Bethlehemu
Hii siyo ile "Bethlehemu" ambayo iko kusini mwa Yerusalemu katika Yuda.
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Zabuloni,
Nchi na miji ambayo kabila la Zabuloni liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu
waliopewa kwa kufuatana na koo za
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao"
Joshua 19:17-19
Upigaji kura wa nne
Tafasiri kirai hiki kama vile ulivyofanya katika 19:1
wa nne
namba ya nne katika orodha
Kesulothi...Shunemu...Hafaraimu...Shioni...Anaharathi
Haya ni majina ya mahali/sehemu
Joshua 19:20-22
Rabithi...Kishioni...Ebezi...Remethi...Enganimu...Enihada...Bethipazezi..Shahazuma
Haya ni majina ya mahali/sehemu
Tabori
Hili ni jina la mlima
Joshua 19:23
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Isakari
Nchi na miji ambayo kabila la Zabuloni liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu
waliopewa kwa kufuatana na koo za
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Yoshua aliwapa kwa koo zao."
Joshua 19:24-26
Upigaji wa kura ya tano
Tafasiri kirai hiki kama ulivyofanya katika 19:1
wa tano
namba ya tano katika orodha
walipewa kwa koo zao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao"
Helkathi, hali, Beteni, Akshafu, Allameleki, Amadi, na Mishali..Shihori Libnathhi
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 19:27-28
Bethi Dagoni...Bonde la Iftaheli...Bethimeki..Neieli..Kabuli...Ebroni...Rehobu...Hammoni ...Kana.
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 19:29-30
Hosa...Akizibu...Umma... Afeki...Rehobu
Haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 19:31
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri
Nchi na miji ambayo kabila la Asheri liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu waliopewa kwa kufuatana na koo zao
waliopewa kwa koo zao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao"
Joshua 19:32-34
Upigaji wa kura wa mara ya sita
Tafasiri kirai hiki kama ulivyofanya katika 19:1
ya sita
namba ya sita katika orodha
walipewa kufuatana na koo zao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao
Helefu...Zaananimu...Adaminekebu...Yabuneeli...Lakumu...Zazinothi Tabori Hukkoki
Haya ni majina ya miji
Joshua 19:35-37
Ziddimu...Zeri...Hamathi..Rakathi...Kinerethi...Adama...Raa..Hazori...Edrei...Eni Hazori
Haya ni majina ya miji
Hamathi
Hii si lile eneo la "Hamathi" bali ni eneo la upande wa magharibi mwa Bahari ya Galilaya.
Joshua 19:38-39
Yironi...Migdaleli..Horemu...Bethi Anathi
Haya ni majina ya miji
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali
Nchi na miji ambayo kabila la Nafutali liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu,
walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao
Joshua 19:40-42
Upigaji wa kura ya saba
Tafasiri kirai hiki kama ulivyofanya katika 19:1
ya saba
namba ya saba katika orodha
Eneo lao la urithi
Nchi na miji ambayo kabila la Dani liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu,
Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi, 42Shaalabini, Aijaloni, na Ithila
Haya ni majina ya mahali/sehemu
Joshua 19:43-46
Eloni, Timna, Ekroni, 44Eliteke, Gibethoni, Baalathi, 45Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni, Me -Yarkoni, na Rakoni
Haya ni majina ya miji
sambamba na eneo la karibu na Yopa
"mkabala na Yopa" au "pembeni ya Yopa"
Joshua 19:47-48
Leshemu
Hili ni jina la mji
Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani,
Nchi na miji ambayo kabila la Dani liliipokea inasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu,
waliopewa kufuatana na koo zao
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ambayo Yoshua aliwapa kwa koo zao
Joshua 19:49-50
walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao
Mji ambao Yoshua alipokea unasemwa kana kwamba ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu
Timnathi Sera
Hili ni jina la mji
Joshua 19:51
Na huu ndio urith...waligawa
Nchi na miji ambayo makabila mbalimbali yaliipokea inasemwa kama ulikuwa ni urithi ambao waliupokea kama mali ya kudumu.
Joshua 20
Joshua 20:1-3
kwa mkono wa Musa
Hapa neno "mkono" linarejelea maandiko ambayo Musa aliyaandika. "kupitia mambo ambayo Musa aliyaandika"
akiua mtu bila kukusudia
Hii hutokea pale ambapo mtu humwua mtu mwingine bila kunuia kufanya hivyo.
kulipiza kisasi kwa damu ya mtu aliyeuliwa kulipiza kisasi kwa damu ya mtu aliyeuliwa
Hapa kumwaga damu ya mtu kuna maana ya kifo. Muundo tendaji unaweza kutumika."kulipiza kisasi cha kifo cha mtu"
Joshua 20:4
Atakimbilia
Hapa kiwakilishi 'a' kinamrejelea mtu yule aliyeua bila kukusudia.
na ataeleza kesi yake kwa wazee wa mji ule
"kuwashawishi wazee wa mji ule ya kwamba aliua mtu bila kukusudia.
Kisha watamwingiza
Kiwakilishi 'wa' kinawarejelea wazee na kiwakilishi "m' kinamrejelea mtu aliyeua bila kukusudia.
kuishi miongoni mwao
Hii inarejelea mji wote kwa ujumla, na si kwa wazee tu.
Joshua 20:5-6
kulipiza kisasi kwa damu ya mtu yule ambaye aliuliwa
Sentensi hii yaweza kutumia muundo tendaji. "kulipiza kifo cha mtu"
kumtoa
Neno hili lina maana ya kumweka mtu chini ya mtu mwingine mwenye mamlaka.
amesimama mbele ya kusanyiko
Hiki ni kirai kinachoeleza juu ya kutafuta haki kutoka katika mahakamaya kusanyiko la wananchi wenzake.
Joshua 20:7-8
Maelezo ya jumla
Kuna majina mengi sana katika sehemu hii
Yordani
Hili ni jina la Mto Yordani
Joshua 20:9
Mtu huyu hatakufa kwa mkono wa mtu yule
Hapa neno "mkono" lina maana kwamba mtu huyu atakuwa mhanga au mtendwa wa moja kwa moja wa mtu aliyemwua mkimbizi
kulipiza kisasi cha damu iliyomwagw
Hii inaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. "kulipiza kifo cha mtu"
Joshua 21
Joshua 21:1-2
Eliazari...Nuni
Haya ni majina ya watu
Waliwaambia
"Walawi wakawaambia"
Yahweh aliwaagizeni ninyi kwa mkono wa Musa
Kirai "kwa mkono wa" kina maana kwamba Yahweh alimtumia Musa kama chombo ili kuleta agizo lake.
Joshua 21:3
miji ifuatayo
Hii inarejelea miji ambayo itaorodheshwa kwenye mstari unaofuata.
Joshua 21:4-5
Upigaji wa kura
Hii ni njia ya kuchagua ambayo ilikuwa ya kubahatisha yaani bila mpango maalumu ili kuondoa utashi wa viongozi, mara kwa mara ilifanywa kwa wazo kuwa Mungu ataamua matokeo.
Wakohathi
Makuhani hwa katika kundi hili walikuwa ni wazao wa Mwana wa Lawi aliyeitwa Kohathi. Na sehemu yao walikuwa ni wazawa wa Haruni, ambaye ni mjukuu wa Kohathi.
miji kumi na tatu....miji kumi
Hii ni hesabu ya miji
Nusu kabila
Nusu ya kabila kwasababu nusu nyingine ilikuwa imepokea urithi wake kabla ya kuvuka Mto Yordani.
Joshua 21:6-7
Gershoni
Gershoni alikuwa ni mmoja wa wana wa Lawi
Upigaji wa kura
Hii ni njia ya kuchagua ambayo ilikuwa ya kubahatisha yaani bila mpango maalumu ili kuondoa utashi wa viongozi, mara kwa mara ilifanywa kwa wazo kuwa Mungu ataamua matokeo
Merari
Merari alikuwa ni mmoja kati ya wana wa Lawi
Joshua 21:8-10
Yahweh alivyokuwa ameagiza kwa mkono wa Musa
Kirai "kwa mkono wa" kina maana kwamba Yahweh alimtumia Musa kama chombo ili kuleta agizo lake.
koo za Wakohathi
Makuhani katika kundi hili walikuwa ni wazawa wa mwana wa Lawi aliyeitwa Kohathi. Sehemu yao nyingine walikuwa ni wazawa wa Haruni, ambaye ni mjukuu wa Kohathi.
Upigaji wa kura
Hii ni njia ya kuchagua ambayo ilikuwa ya kubahatisha yaani bila mpango maalumu ili kuondoa utashi wa viongozi, mara kwa mara ilifanywa kwa wazo kuwa Mungu ataamua matokeo
Joshua 21:11-12
Arba alikuwa ni baba wa Anaki
Haya ni maelezo ya nyuma juu ya jina la mtu aliyeuanzisha mji wa Kiriathi Arba.
Anaki
Hili ni jina la mwanaume
Nchi ya milima
Hii ni sehemu ya nchi ambayo kiuasilia imeinuka, ni ndogo kuliko mlima
Maeneo ya malishi
Hii ni sehemu iliyo na majani mengi au mimea inayofaa kwa ajili ya kulishia mifugo au wanyama
Mashamba ya mji
Maeneo ya nchi yaliyo wazi, mara nyingine huwa imepandwa mazao ambayo ni mali au yameuzunguka mji.
Vijiji
hizi ni jamii ndogo, mara nyingi ni ndogo kuliko mji
Joshua 21:13-16
Libna...Yatiri...Eshetmoa...Holoni...Debiri...Aini...Yutta
haya ni majina ya miji
miji tisa...makabila mawili
hesabu ya miji na makabila katika kifungu
Joshua 21:17-19
Kutoka katika kabila la Benyamini walipewa Gibea pamoja na maeneo yake ya malisho, na Geba
hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Kabila la Benyamini lilipewa Gibea."
Geba...Anathothi...Almoni
haya ni majina ya miji
miji kumi na tatu
"miji 13"
Joshua 21:20-22
familia ya Kohathi
Makuhani katika kundi hili walikuwa ni wazawa wa mwana wa Lawi aliyeitwa Kohathi. Sehemu yao nyingine walikuwa ni wazawa wa Haruni, ambaye ni mjukuu wa Kohathi.
walipewa miji
Hii inaweza kuelezwa muundo tendaji: "Walipokea miji"
upigaji wa kura
Hii ni njia ya kuchagua ambayo ilikuwa ya kubahatisha yaani bila mpango maalumu ili kuondoa utashi wa viongozi, mara kwa mara ilifanywa kwa wazo kuwa Mungu ataamua matokeo
Gezeri...Kibzaimu...Bethi Horoni
haya ni majina ya miji
miji minne kwa ujumla
Hii inarejelea orodha kwa hesaby yake kwa jumla.
Joshua 21:23-24
Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke
Hii inaeweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. "Kabila la Dani waliwapa ukoo wa Kohathi eneo la Elteke.
ukoo wa Kohathhi
Makuhani katika kundi hili walikuwa ni wazawa wa mwana wa Lawi aliyeitwa Kohathi. Sehemu yao nyingine walikuwa ni wazawa wa Haruni, ambaye ni mjukuu wa Kohathi.
Elteke...Gibethoni..Aijaloni...Gathrimoni
Haya ni majinia ya miji
Joshua 21:25-26
Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanak
Hii inaweza kuelezwa kwa kauli tenda. "Nusu ya kabila la Manesa waliwapa ukoo wa Kohathi mji wa Taahaki."
Taanaki ...Gathirimmoni
Haya ni majina ya miji
miji miwili...miji kumi kwa ujumla
Hesabu ya miji iliyoorodhoshwa
ukoo wa Kohathi... koo za Wakolathi
Makuhani katika kundi hili walikuwa ni wazawa wa mwana wa Lawi aliyeitwa Kohathi. Sehemu yao nyingine walikuwa ni wazawa wa Haruni, ambaye ni mjukuu wa Kohathi.
Joshua 21:27
Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golan
Maelezo haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Nusu ya kabila la Manase, koo zingine za walawi, walipokea kutoka kwa nusu ya kabila la Manase mji wa Golani."
Golani...Beeshitera
Majina ya miji
aliyeua mtu bila kukusudia
Hii na kifo kilichotokana na tendo la ambaye hakukusudia kumdhuru mtu.
miji miwili
hesabu ya miji
Joshua 21:28-31
Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Koo za Gershoni walipokea pia Kishoni"
Kishoni....Daberathi...Yarmuthi....Enganimu...Mishali...Abdoni...helkathi...Rehobu
Haya ni majina ya miji
Kutoka katika kabila la Asheri, walipewa miji minne kwa ujumla - Mishali
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tenda. "Walipokea kutoka kabila la Asheri mji wa Mishali."
miji minne kwa ujumla
Hii inarejelea hesabu ya miji iliyoorodheshwa
Joshua 21:32-33
Kutoka kwa kabila la Nafutali, nasaba za Gershoni walipewa miji mitatu kwa ujumla - Kedeshi
Muundo tendaji unaweza kutumika pia. "Koo za Gershoni zilipokea Kadeshi kutoka kwa kabila la Nafutali"
Gershoni
Hili ni jina la mtu
Hamothidori...Kartani
Haya ni majina ya miji
miji kumi na mitatu kwa ujumla
"miji 13 kwa ujumla wake"
Joshua 21:34-35
Na kwa Walawi waliosalia, koo za Merari waliokuwa wamepewa kutoka katika kabila la Zabuloni: Yokneamu
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji: "Walawi waliobaki - koo za Merari - walipokea Yokneamu kutoka katika kabila la Zabuloni
Merari
Jina la mtu
Yokneamu ..Karta..Dimna ....Nahalali
Majina ya miji
miji minne kwa ujumla
Miji inarejelewa kwa ujumla katika hesabu yake.
Joshua 21:36-38
Kwa mbari za Merari walipewa miji minne kutoka katika kabila la Rubeni: Bezeri
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Koo za Merari zilipata Bezeri kutoka katika kabila la Rubeni."
miji minne
Hii inarejelea jumla ya hesabu ya miji
Bezeri...Yahazi...Kedemothi...Mefaathi...Ramothi
majina ya miji
Kutoka katika kabila la Gadi walipewa miji ya Ramothi
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " Walipata mji wa Ramothi kutoka kwa kabila la Gadi."
Mahanaimu
Hili ni jina la mji
Joshua 21:39-40
Koo za Merari zilipewa pia Heshiboni
Maelezo haya yaweza kuelezwa kwa muundo tandaji. " Koo za Merari zilipata pia mji wa Heshiboni"
Heshiboni...Yazeri
haya ni majina ya miji
miji kumi na miwili kwa ujumla
"miji 12 jumla yake"
miji kumi na miwili walipewa wao kwa kupiga kura.
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Walipata miji kumi na miwili kwa kupiga kura."
kupiga kura
Hii ni njia ya kuchagua ambayo ilikuwa ya kubahatisha yaani bila mpango maalumu ili kuondoa utashi wa viongozi, mara kwa mara ilifanywa kwa wazo kuwa Mungu ataamua matokeo
Joshua 21:41-42
Miji waliyopewa Walawi kutoka katikati ya nchi
Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Walawi walipata miji yao katika sehemu ya katikati ya nchi"
miji Arobaini na minane
"miji 48"
Joshua 21:43-45
aliwaapia
"alitoa kiapo"
Hakuna hata adui mmoja atakayeweza kuwashinda
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Walimshinda kila mmoja miongoni mwa adui zao."
Yawhew aliwatia maadui wao wote mikononi mwao.
hapa kirai "mikononi mwao" ina maana "ndani ya mamlaka yao"
Hakuna hata kitu kimoja miongoni kwa ahadi nzuri ambazo Yahweh alizisema kwa nyumba ya Israeli ambazo hazikutimia. Ahadi zote zilitimia
sentensi imeelezwa kwa kukanusha ili kutia nguvu maelezo yake. "Kila ahadi njema ambayo Yahweh alikuwa ameisema kwa nyumba ya Israeli ilikuwa kweli."
Joshua 22
Joshua 22:1-3
Warubeni
watu wa kabila la Yuda
Wagadi
Watu wa kabila la Gadi
Mmeitii sauti yangu
mahali hapa "sauti yangu" ina maana ya vitu ambavyo Yoshua alikuwa amevisema. "mlitii kila kitu nilichosema."
Bado hamjawaacha ndugu zenu
Hii inaweza kusemwa kwa namna isiyo ya kukanusha. "Mmebakia pamoja na ndugu zetu."
Joshua 22:4-6
kutembea katika njia zake
Mtu anayemtii Yahweh anasemwa kana kwamba alikuwa anatembea katika njia au barabara za Yahweh. "kutii kila kitu anachokisema"
kwa moyo wenu wote na kwa roho zenu zote.
Maneno "moyo" na "roho" hapa yametumika kurejelea mtu mzima. "kwa vyote unavyovifikiria na kuvihisi" au "kwa utu wako mzima"
Joshua 22:7-8
Yordani
Jina la Mto Yordani
chuma
Metali ngumu, imara na ya sumaku
nyara
jeshi lililoshinda huchukua kila kitu chenye thamani kutoka kwa watu waliowashinda.
Joshua 22:9
amri za Yahweh, kwa mkono wa Musa.
Kirai "kwa mkono wa" kina maana ya kwamba Yahweh alimtumia Musa kama wakala kufikisha agizo lake. "Amri ambayo Yahweh alimwambia Musa awapeni ninyi."
Joshua 22:10-11
Yordani
Huu ni ufupisho wa Mto Yordani
mbele ya nchi ya Kanaani
Makabila ya Israeli walioishi ng'ambo ya Mto Yordani wangeingia Kanaani kwa kupitia sehemu ambayo walijenga madhabahu. Hii sehemu inasemwa kana kwamba ilikuwa mbele ya au kwenye lango la kuingia Kanaani ambapo makabila mengine yalikuwa yanaishi.
Gelilothi
Jina la mji
Joshua 22:12
vita
hali ya mapigano au ugomvi wa silaha baina ya mataifa mawili au makundi ya watu.
Joshua 22:13-14
Eliezari
Jina la mtu
Joshua 22:15-16
Kusanyiko lote la Yahweh linasema
Watu wote wa Israeli wanasemwa kwa pamoja kwa umoja kana kwamba ni mtu mmoja. "Watu wengi wote wa Israeli wanauliza"
Joshua 22:17-18
Je dhambi zetu huko Peori hazikututosha?
Swali hili hutia mkazo juu ya dhambi zao za awali. Hii inaweza kuandikwa kwa maelezo haya. "Tumeshatenda dhambi huko Peori."
Bado hata sasa hatujajitakasa wenyewe kwa dhambi hiyo
sentensi hii inaweza kuelezeka vizuri kwa kauli ya kukubali. Bado tunahangaika na hatia za dhambi ile.
Je, nanyi leo pia mwageuka na kuacha kumfuata Yahweh?
Swali hili limetumika kwa ajili ya kuwakemea watu kwa ajili ya dhambi yao. Hii pia yaweza kuandikwa kama maelezo. "Hamtakiwi kugeuka na kuacha kumfuata Yahweh leo!"
Joshua 22:19-20
Akani...Zera
majina ya wanaume
Je hakuwa Akani mwana wa Zera aliyeivunja imani kwa vitu vile ambavyo vilikuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu? Na je ghadhabu ya Mungu haikushuka kwa watu wote wa Israeli?
Maswali haya yametumika kuwakumbusha watu juu ya hukumu kwa ajli ya dhambi zilizopita. Maswali haya yanaweza yakaandikwa kama maelezo. "Akani mwana wa Zera, alitenda dhambi kwa kuchukua vitu vilivyokuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu. Na kwasababu ya hiyo Mungu aliwaadhibu watu wote wa Israeli."
Joshua 22:21-23
Kama ilikuwa ni katika uasi..... basi Yahweh na atuadhibu.
Makabila matatu yanafanya kauli mbili zenye nadharia tete zinazosisitiza kuwa haikuwa kweli. Hawakujenga madhabahu ili kumwabudu mungu mwingine.
Joshua 22:24
Maelezo ya jumla
Makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya Manase wanatoa majibu yao sasa.
watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu.....Mungu wa Israeli?
Haya ni mashitaka ya kinadharia ambayo makabila haya matatu yanadhani kuwa watoto wa makabila mengine wangeweza kufanya kwa wakati ujao.
Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?
Makabila matatu yanatumia swali lisilohitaji majibu ili kutilia mkazo juu ya hali ambayo walikuwa wakiiepuka. Swali hili laweza kuandikwa kama maelezo. "Hamna kitu cha kufanya na Yahweh, Mungu wa Israeli."
Joshua 22:25
Maelezo ya jumla
Makabila ya Rubeni, Gadi, na nusu ya Manase yanaendelea kutoa majibu yao
Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani....hamna kitu chochote naYahweh
Huu ni mwendelezo wa mashitaka ya kinadharia ambayo makabila yale matatu yanadhani kuwa watoto wa makabila mengine wangeweza kufanya kwa wakati ujao.
Yordani
Huu ni ufupisho wa Mto Yordani
watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waacha kumwabudu Yahweh.
Makabila haya matatu yalijenga madhabahu ili kuepuka hali inayodhania isije ikatokea wakati ujao.
Joshua 22:26-27
Maelezo ya jumla
Makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya Manase wanatoa majibu yao sasa.
iwe ni ushahidi kati yetu na ninyi
Madhabahu inazungumzwa kana kwamba ilikuwa ni ushahidi ambao ungeweza kushuhudia haki kwa makabila matatu.
ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, "Hamna sehemu katika Yahweh."'
Hii ni hali nadharia inayodhaniwa ambayo makabila matatu hayakutaka itokee.
ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, "Hamna sehemu katika Yahweh."'
"hakuna sehemu" au " hamna urithi"
Joshua 22:28-29
Maelezo ya jumla
Makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wanamalizia kujibu sasa
'kama hili litasemwa....ushahidi kati yetu ninyi.
Makabila matatu yanaelezea uwezekano wa jibu lao kwa shutuma ambazo zinaweza kutokea au zisitokee hapo baadaye.
Na iwe mbali nasi kwamba tunataka kugeuka kinyume na Yahweh,
Nafasi isiyowezekana ya kuasi inasemwa kana kwamba ni kitu kilicho mbali sana kutoka kwao. "Hakika tusingeasi"
kuacha kumfuata yeye
kuacha kumfuata Yahweh kunasemwa kana kwamba walikuwa wanageukia mbali na kumwacha.
Joshua 22:30-31
waliposikia maneno
Hapa "maneno"yanarejelea juu ya ujumbe ambao uliundwa kwa maneno. "walisikia ujumbe"
yalikuwa ni mazuri machoni pao
Hapa maneno "machoni pao" inamaanisha "katika mawazo yao"
hamjatenda uvunjaji wa imani kinyume naye
"kuvunja agano lako kwake"
mmewaokoa watu wa Israeli kutoka katika mkono wa Yahweh.
Mahali hapa kirai "mkono wa Yahweh" inarejelea juu ya hukumu. Kitendo cha kulinda watu kinasemwa kama ni kuwaokoa kutoka katika mkono wake.
Joshua 22:32-33
Taarifa yao ilikuwa nzuri katika macho ya watu
Mahali hapa maneno "nzuri katika macho" ina maana ya "kupokelewa" "Watu waliipokea taarifa ya viongozi"
kuiharibu nchi
"kuharibu kila kitu katika nchi."
Joshua 22:34
kwa kuwa walisema
Hii inarejelea kwa Warubeni na Wagadi
Ni ushahidi miongoni mwetu
Madhabahu inasemwa kana kwamba alikuwa ni shahidi ambaye angeshuhudia kwa ajili ya makabila matatu.
Joshua 23
Joshua 23:1-3
mzee sana
aliishi miaka mingi
Joshua 23:4-5
Yordani
Kifupisho cha Mto Yordani
Upande wa magharibi
Hii inaonesha mwelekeo wa machweo ya jua.
Joshua 23:6-8
msikengeuke upande wa kulia wala upande wa kushoto
Kitendo cha kutotiii maagizo ya sheria za Musa kinasemwa kana kwamba ni kugeuka upande wa kulia au upande wa kushoto mbali na njia sahihi.
msichanganyikane
Maana zinazokubalika 1)kuwa na urafiki wa karibu nao 2) kuoana nao
msiyataje
kuyasema
miungu yao
Hii inarejelea juu ya miungu ya mataifa yaliyosalia.
kumshika sana Yahweh
"kumshikilia Yahweh kwa nguvu" Kumwamini Yahweh kunasemwa kana kwamba ni kumshikilia kwa nguvu.
hadi leo
"mpaka muda wa sasa"
Joshua 23:9-11
kusimama mbele yenu
Mahali hapa neno "kusimama" linawakilisha kujiweka imara kwa kusimama juu ya ardhi katika vita. Neno "yenu" linalejelea taifa zima la Israeli.
mmoja
namba moja
elfu
"1,000"
Joshua 23:12-13
kushikamana na watu walioalia wa mataifa haya walioba
Kitendo cha kubali imani za mataifa haya kunasemwa kana kwamba ni kuwashikilia kwa nguvu. "kubali imani za watu walisalia za mataifa haya."
kitanzi na mtego
Maneno haya "kitanzi" na "mtego" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile. kwa pamoja yanaongelea juu ya mataifa mengine kana kwamba yalikuwa ni mitego hatari kwa waisraeli kwa kusababisha matatizo.
viboko migongoni mwenu na miiba machoni mwenu
Virai hivi vinaongelea juu ya matatizo ambayo yataletwa na mataifa haya juu ya Israeli kana kwamba vilikuwa ni viboko na miiba kwao.
Joshua 23:14-15
Na sasa ninaenda katika njia ya dunia yote
Yoshua anatumia neno la upole kurejelea juu ya kifo chake. "Ninakwenda kufa"
mnajua kwa moyo na roho zenu zote
Mahali hapa maneno "moyo" na "roho" yana maana sawa. Kwa pamoja yanatia mkazo juu ya ufahamu wa ndani wa mtu binafsi.
Hakuna hata moja lililoshindikana
Maneno haya yanatia mkazo kwamba ahadi zote za Yahweh zimetimia. Hii pia yaweza kuelezwa kawa kauli kubalifu. "kila neno lilitimia"
Joshua 23:16
Atafanya hivi
Hii inarejelea juu ya hukumu iliyotishiwa katika mstari uliotangulia.
kuiabudu miungu mingine na kuiinamia
Virai hivi viwili kimsingi vinazungumzia juu ya jambo moja lile lile. Kirai cha pili kinaelezea jinsi watu "wanavyoabudu miungu mingine"
ndipo hasira ya Yahweh itawaka kinyume nanyi
"kuwaka"ni lugha ya picha kuonesha mwanzo wa hasira ya Yahweh, kama moto, inawashwa au inaanzishwa au inaanza kuwaka kiurahisi kama kwenye majani makavu au vijiti vidogo vidogo. "Yahweh ataanza kuwa na hasira nanyi"
Joshua 24
Joshua 24:1-2
Kisha Yoshua aliyakusanya pamoja makabila yote ya Israeli
Kitendo cha Yoshua kuyaalika makabila kinazungumzwa kana kwamba ni kuyakusanya kwa pamoja katika kikapu. "Yoshua aliyaomba makabila yote ya israeli yakutane pamoja naye."
wakajihudhurisha mbele
"walikuja na kusimama mbele ya" au "kuja mbele"
miaka mingi iliyopita
miaka mingi ya nyuma
Hiki ndicho
Yoshua anaanza kwa kunukuru kile Yahweh alikuwa amekisema hapo mwanzo. Nukuu inaendelea mpaka mstari wa 13.
Tera...Nahori
Haya ni majina ya wanaume
Joshua 24:3-4
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kunukuu kile ambacho Yahweh alikisema katika kujishughulisha kwake na watu wake.
Seiri
Jina la sehemu au mahali
Walishuka kwenda
Misri ilikuwa ni sehemu ya chini katika mwinuko wa nchi ya Kanaani
Joshua 24:5-6
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kunukuu kile ambacho Yahweh alikisema katika kujishughulisha kwake na watu wake
niliwatoa ninyi...niliwatoa baba zenu nje
Yahweh anaendelea kuelezea katika virai hivi viwili ambavyo vinawarejelea waisraeli wote, kwa wakati uliopita na wa sasa.
Joshua 24:7
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kunukuu kile ambacho Yahweh alikisema katika kujishughulisha kwake na watu wake
Baba zenu...yenu
Yahweh anaendelea kuelezea katika virai hivi viwili ambavyo vinawarejelea waisraeli wote, kwa wakati uliopita na wa sasa
bahari
hapa inarejelewa bahari ya mitende
jangwaani
sehemu isiyokaliwa na watu, kame,
Joshua 24:8
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kunukuu kile ambacho Yahweh alikisema katika kujishughulisha kwake na watu wake
nanyi
Neno "nanyi" ni wingi katika hotuba hii ikirejelea taifa lote la Israeli.
Yordani
Ni ufupisho wa Mto wa Yordani
niliwatia katika mkono wenu
Hapa neno "mkono" linarejelea nguvu, uwezo au mamlaka. "kuwawezesha ninyi ili kuwashinda"
Joshua 24:9-10
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kunukuu kile ambacho Yahweh alikisema katika kujishughulisha kwake na watu wake
Balaki...Zipori
majina ya wanaume
ninyi
Neno hili "ninyi" limetumika katika wingi kurejelea taifa lote la Israeli.
niliwaokoa na mkono wake
Hapa neno "mkono" linarejelea nguvu, uwezo au mamlaka. "kuwawezesha ninyi ili kuwashinda"
Joshua 24:11-12
Maelezo ya jumla
Yoshua anaendelea kunukuu kile ambacho Yahweh alikisema katika kujishughulisha kwake na watu wake
Nanyi
Neno hili "nanyi" limetumika katika wingi kurejelea taifa lote la Israeli.
Yordani
hiki ni kifupisho cha Mto Yordani
manyigu
ni wadudu wadogo wanaopaa kwa kasi wanaoishi katika kundi kubwa la wadudu.
Joshua 24:13
Maelezo ya jumla
Yoshua anahitimisha kunukuru kile ambacho Yahweh alikuwa amekisema katika kushughulika na watu wake.
Joshua 24:14-15
Na kama inaonekana kuwa ni vibaya machoni penu
Hapa maneno "machoni penu" ni lugha mbili za picha zimetumika, inarejelea kwanza kwa macho yao, au inahusishwa na hamu/tamaa yao.
nyumba yangu
Hapa inarejelea familia iliyoishi katika nyumba yake.
Joshua 24:16-18
sisi na baba zetu ..sisi
Watu wanaongea kana kwamba walikuwa pamoja na baba zao kwa wakati huo, na kuongea maneno haya "sis" na "baba zetu"
nyumba ya utumwa
Mahali hapa neno "nyumba" ni lugha ya nahau kurejelea sehemu/mahali pa utumwa wao. "sehemu ambapo sisi tulikuwa watumwa"
mataifa yote ambayo tulipita kati kati yake
"mataifa ambayo sisi tulipita katikati yake"
Joshua 24:19-20
watu
hii inawarejelea Waisraeli
Mungu mwenye nguvu
Mungu anataka watu wake kumwabudu Yeye peke yake
Atawaangamizeni
Hasira ya Yahweh inaongelewa kana kwamba ilikuwa ni moto ambao ungewateketeza.
Joshua 24:21-23
Watu
inawarejelea Waisraeli
geuzeni moyo wenu umwelekee Yahweh,
Kuamua kumtii Yahweh ni kitendo kinachosemwa kuwa ni sawa na kugeuza moyo wao kumwelekea Yeye. Mahali hapa, neno "moyo" linawakilisha mtu mzima. Na kwa hali hii, "moyo" liko katika wingi kurejelea Waisraeli kama kundi moja.
Joshua 24:24-26
Watu
inawarejelea Waisraeli
Tutaisikiliza sauti yake
Mahali hapa neno "kuisikiliza" lina maana ya kutii. "Tutatii kila kitu atakachotwambia kufanya"
Aliziweka maagizo na sheria
Kitendo cha kuweka sheria kinasemwa kana kwamba Yoshua aliweka kitu halisi mahali fulani.
kitabu cha sheria za Mungu
Hii inaonekana kuwa ni mwendelezao wa maandishiya Musa
kulisimamisha hapo
"kuliweka hapo"
Joshua 24:27-28
watu
Inawarejelea Waisraeli
jiwe hili litakuwa ushuhuda ....limeyasikia maneno yote
Jiwe ambalo Yoshua aliliweka linasemwa kana kwamba alikuwa ni mtu ambaye alisikia kile kilichosemwa na angekuwa na uwezo wa kushuhudia juu ya kile kilichosemwa.
hamtakiwi
"kama mtafanya"
Joshua 24:29-30
miaka 110
"miaka mia moja na kumi"
Timnathi Sera...Mlima Gaashi
haya ni majina ya sehemu/mahali
Joshua 24:31
Siku zote za Maisha ya Yoshua
Lugha hii imetumika kuonesha maisha yote ya Yoshua.
walidumu pamoja na Yoshua
"waliishi muda mrefu zaidi ya Yoshua"
Joshua 24:32-33
Mifupa ya Yusufu ambayo watu wa Israeli waliileta kutoka Misri, waliizika huko shekemu
Mpangilio wa sentensi hii unaweza kubadilishwa hasa sehemu yake ya mwanzo ili kuleta msaada zaidi. "Watu wa Israeli walileta mifupa ya Yusufu kutoka Misri na kuizika huko Shekemu"
vipande mia moja
"vipande 100"
Eliazeri
Jina la mwanaume
Gibea
Hili ni jina la sehemu/mahali