Proverbs
Proverbs 1
Proverbs 1:1-3
Maelezo ya Jumla
Mstari wa 2-23 ni mashairi
kwa kufunza hekima na mafundisho
"kwa kukufunza jinsi ya kuwa na busara na kukuelekeza namna ya maisha kuishi kwa uadilifu.
kwa kufunza maneno ya ujuzi
"kwa kukusaidia kufahamu mafundisho ya busara"
ili kupokea
"ili tuweze kupokea"
ili kupokea mafundisho kwa ajili ya kuishi
" mpate kufunzwa namna ya kuishi"
Proverbs 1:4-6
pia ni kuwapa hekima wajinga
' pia kuwafunza wale ambao ni wajinga namna ya kuwa na busara"
wajinga
"bila uzoefu, isiyo kamavu/uchanga"
kuwapa maarifa na busara vijana
"na kuwafunza vijana wanachohitaji kufahamu na jinsi ya kutambua jambo zuri la kufanya"
busara
kufahamu kinachopaswa kufanyika katika mazingira husika.
Watu wenye busara wasikie na kuongeza elimu yao
"Wale wenye busara wazingatie na kujifunza zaidi"
watu wenye ufahamu wapate mwongozo
"watu wenye ufahamu wajifunze kwa methali hizi jinsi ya kufanya maamuzi mazuri"
vitendawili
misemo ambayo mtu anaweza kuifahamu baada tu ya kutafakari juu yake.
Proverbs 1:7-9
Maelezo ya Jumla
baba anamfundisha mtoto wake.
hofu ya Yahwe ni mwanzo wa maarifa
"Lazima umwogope Yahwe kwanza ili uanze kujua busara" au "lazima kumheshimu na kuwa na staha kwa Yahwe kwanza ili kujifunza busara"
Yahwe
Hili ni jina lake Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale.
wapumbavu hudharau hekima na mafundisho
"wale wasiothamini busara na maelekezo ni wapumbavu"
wala usijiweke kando
Hii ni nahau kumaanisha " usipuuzie" au " usikatae"
vitakuwa kilemba cha neema kwa ajili ya kichwa chako na mikufu yenye kuning'inia shingoni mwako
"yatakufanya uwe na busara kama kuvaa kilemba kwenye kichwa chako au mikufu kuzunguka shingo yako inavyokupendeza"
kilemba
duara iliyofumwa kwa majani au maua
mikufu
mapambo yanayovaliwa shingoni
Proverbs 1:10-11
wakijaribu kukushawisha kwenye dhambi zao
" jaribu kukuvuta kwenye dhambi wanazotenda"
kataa kuwafuata
usiwasikilize
kama watasema
mfano wa ushawishi wa wenye dhambi
tuvizie
kujificha na kusubiri muda muafaka
Proverbs 1:12-14
Maelezo ya Jumla
Mstari 12-14 ni mwisho wa kauli ya kihisia ya waovu ambao wanajaribu kuwashawishi wengine kufanya dhambi.
Tuwameze wangali hai, kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya
wenye dhambi wanaongea juu ya kuwaua watu wasio na hatia kama kuzimu ambavyo hupeleka chini kwa wafu watu wenye afya.
Tuwameze..., kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya
kaburi linafananishwa kama mtu ambaye huwameza wanadamu na kuwapeleka chini katika sehemu ya wafu.
kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya
waovu wanatarajia kuwaangamiza mateka wao kwa jinsi ile ile ambayo kuzimu(sehemu ya wafu) inavyowachukua hata watu wenye afya.
tuwafanye kama wale ambao huanguka kwenye shimo
"shimo" ni neno jingine lenye maana ya kuzimu au sehemu ambayo wafu huishi.
Tupa kura yako pamoja nasi
Hii ni nahau "jiunge nasi"
Sisi kwa pamoja tutakuwa na mkoba mmoja
"Mkoba" hapa unawakilisha kila kitu wanachoiba. "Sisi tutagawana kwa usawa kila kitu ambacho tumeiba"
mkoba
begi kwa ajili ya kubebea fadha
Proverbs 1:15-17
usiende katika njia ile pamoja nao; usiruhusu mguu wako kugusa ambapo wao hupita
kuepuka kuwa kwenye njia ya wenye dhambi" usiende pamoja na wenye dhambi au kutende matendo yao"
miguu yao hukimbilia maovu
"wapo tayari kutenda mambo maovu"
miguu yao hukimbilia
"miguu" inawakilisha mtu mwenyewe.
kumwaga damu
"damu" ni uzima wa mtu. Kumwaga damu ni kumuua mtu.
Kwa maana haifai kutandaza ... akiona
Hekima ya ndege ambao hujinasua na mitego wanayoiona inalinganishwa upumbavu wa wenye dhambi ambao hunaswa kwenye mitego ambayo hujitengenezea wenyewe.
Proverbs 1:18-19
Watu hawa huvizia ili kujiangamiza wenyewe- huweka mtego kwa ajili yao wenyewe
watu hujiangamiza wenyewe kwa mambo ya dhambi... ni kama hutega mtego kwa kujiangamiza wenyewe.
Hivyo ndivyo zilivyo njia za kila mmoja
"hivi ndivyo inavyotokea kwa kila mmoja"
mapato ya udhalimu huondoa maisha ya wale ambao huyashikilia
"mapato ya udhalimu yatawaharibu wale ambao hushushikamana nayo"
Proverbs 1:20-22
Maelezo ya Jumla
Katika 1:20-1:33 Hekima inaongelewa mithili ya mwanamke anayeongea na watu.
Hekima analia kwa sauti
"Hekima ni kama mwanamke ambaye hulia kwa sauti kuu"
hupaza sauti yake
Hii ni nahau "Huongea kwa sauti kuu"
katika viwanja
sehemu ambapo huweza kuwa na watu wengi. "kwenye soko" au "katika viunga vya mji"
kwenye kelele kuu za mitaa
sehemu ambapo mitaa yenye shughuli nyingi imeunganika au juu ya ukuta ambapo watu walioko kwenye kelele za mitaa wanaweza kuona na kusikia hekima ikiongea.
Hata lini, ninyi watu wajinga, mtapenda kuwa wajinga?
Hekima anatumia swali hili kuwakemea wasio na hekima. "Ninyi ambao ni wajinga lazima mkome kupenda kuwa wajinga"
wajinga
"bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga"
Hata lini, ninyi wenye dhihaka, mtapenda dhihaka, na hata lini, ninyi wapumbavu, mtachukia maarifa?
Hekima anatumia swali hili kuwakema wenye dhihaka na wapumbavu. " Ninyi ambao hudhihaki lazima muache kupenda dhihaki, na ninyi wapumbavu lazima muache kuchukia maarifa"
Proverbs 1:23-25
Maelezo ya Jumla
Hekima anaendelea kuongea.
Sikiliza
"kusikiliza kwa umakini"
Mimi nitamimina mawazo yangu kwenu
Hekima anawaambia watu kila kitu anachofikiri juu yao, mawazo yake yanaongelewa mithili ya kimiminika ambacho anaweza kuwamiminia.
Mimi nitafanya maneno yangu yajulikane kwenu
" Nitawaambia yale ninayoyafikiria"
Mimi nimeunyosha mkono wangu
Hii ni nahau maana yake " Nimewaalikeni kuja kwangu"
Proverbs 1:26-27
Maelezo ya Jumla
Hekima anaendelea kuongea, akieleza ambacho hutokea kwa wale ambao humdharau.
Mimi nitacheka
kwa hiyo hekima ya mwanamke inawacheka kwa sababu wameipuuza.
katika msiba wenu
" mambo mabaya yanapotokea kwenu"
wakati hofu itakapo kuja
"wakati mtakapoogopa"
wakati hofu ya kuogopesha itakapokuja kama dhoruba... kama kisulisuli ... kuja juu yenu
mambo ya kutisha yatakayotekea kwa watu yanalinganishwa kama dhoruba itayowakumba na kusababisha hofu na maumivu.
kisulisuli
dhoruba ya upepo mkali ambao husababisha uharibifu
Proverbs 1:28-30
Sentensi Unganishi
Hekima anaendelea kuongea
Kisha wataniita
" Kisha wale ambao hunipuuza watanililia kwa msaada"
Kwa sababu wamechukia maarifa
Maarifa ni kujifunza."Kwa sababu wamekataa kujifunza ili wawe na busara"
hawakuchagua hofu ya Yahwe
" hawakumwogopa Yahwe" au "hawakumheshimu na kumtukuza Yahwe"
Hawakufuata maagizo yangu
"hawakuweza kukubali maagizo yangu" au " walikataa ushauri wangu"
Proverbs 1:31-33
Maelezo ya Jumla
mstari wa 33 unahitimisha kauli ya hekima ambayo ilianzia katika 1:20.
watakila matunda ya njia zao
"watapata madhara yanayotokana na matendo yao"
kwa matunda ya njama zao watashibishwa
"watateseka kwa mipango yao miovu"
wajinga
"bila uzoefu, isiyo kamavu/uchanga"
hufa wakati wanaporudi nyuma
"hufa kwa kuwa wanakataa kujifunza"
kutojali kwa wapumbavu kutawaangamiza
" wapumavu watakufa kwa sababu hawajali wanachopaswa kufanya"
kutojali
kukosa hamu juu ya jambo fulani
Proverbs 2
Proverbs 2:1-2
Maelezo ya Jumla
Baba anamfundisha mtoto wake kwa kutumia shairi.
kama utapokea maneno yangu
Hapa "maneno" yanawakilisha mafundisho " kama utasikiliza ambacho ninakufundisha"
kama utapokea
Huu ni mfululizo wa kauli zenye mashariti zinazofika tamati katika 2:5
zihifadhi amri zangu ndani yako
" zihesabu amri zangu kuwa za thamani kama hazina"
masikio yako yawe na usikivu kwa ajili ya hekima na kuelekeza moyo wako kwenye ufahamu
"kama masikio yako yatakuwa masikivu kwa ajili ya hekima na kuelekeza moy wako kwenye ufahamu"
masikio yako yawe na usikivu
"Jilazimishe kusikiliza kwa umakini wewe mwenyewe"
Hekima
"sikiliza mabo ya busara ambayo ninakufundisha"
elekeza moyo wako kwenye ufahamu
"jitahidi sana kufahamu maana ya busara"
Proverbs 2:3-5
Kama utalia kwa ajili ya ufahamu na kupaza sauti yako kwa ajili yake
'Kama utaweka umuhimu kumwomba Mungu na kumsihi kwa ajili ya ufahamu"
Kama utalia ... kama ukitafuta
Hizi ni kauli zenye amri, zingatia 2:1 na 1:1-2
paza sauti yako
Hii ni nahau, maana yake kuongea kwa sauti kuu au kupiga kelele.
kama utautafuta kama ambavyo ungetafuta fedha na kutafuta ufahamu kama ambayo ungetafuta hazini iliyositirika
kufanya bidii ili kujua maana ya busara.
kama utautafuata... kutafuta ufahamu
Kuwa na jitihada kuijua busara ni kama vile mtu ambavyo hutafuta vitu amabavyo ni vya lazima kwake.
utapata maarifa ya Mungu
kufanikiwa kumjua Mungu kunapewa picha ya kitu ambacho mtu hupata baada ya kutafuata.
Proverbs 2:6-8
kutoka katika kinywa huja maarifa na ufahamu
Hapa "kinywa" kinawakilisha Yahwe mwenyewe au Jambo ambalo anasema."Kutoka kwa Yahwe huja maarifa na ufahamu" au "Yahwe anatuambia sisi kile tunapaswa kukijua na kukifahamu"
Huhifadhi sauti ya hekima kwa ajili ya wale ambao humpendeza
Yahwe hufundisha kweli kwa wale ambao humpendeza.
kamili
yenye kutegemewa
yeye ni ngao kwa wale
Kwa kuwa Yahwe anauwezo wa kuwalinda watu wake anatajwa kama ngao.
ambao hutembea katika uadilifu
wanaoishi kama wanavyopaswa
huzilinda njia za mwenye haki
Mungu huwalinda wale ambao hutenda haki
atailinda njia yao
huwalinda wale ambao...
Proverbs 2:9-10
haki
adili
kila njia njema
kuishi katika njia ambao humpendeza Mungu.
hekima itaigia kwenye moyo wako
Hapa "moyo" unamaanisha utu wa ndani wa mwanadamu. "utajifunza namna ya kuwa na busara ya kweli"
yatakupendeza nafsi yako
"yatakupa furaha"
Proverbs 2:11-13
Busara Itakulinda, ufahamu utakuongoza
"kwa sababu unafikiri kwa kutafakari na kuifahamu kweli na ubaya utakuwa salama"
Busara
hali ya kuwa makini katika matendo na maongezi
atakulinda
kuongoza, kukinga au kumjali mtu au kitu
Vitakuokoa kutoka katika njia ya uovu
utajua kuishi mbali na yale maovu
kutoka katika njia ya uovu
uovu unaongelewa kama kwamba ni njia ya kupita mtu
ambao huziacha njia za haki na kutembea katika njia za giza
mtu anapoacha kutenda haki lakini huamua kutenda uovu ni kama mtu anayeacha kutembea kwenye njia sahihi na kuchagua kutembea kwenye njia ya giza.
ambao huacha
Hapa neno "ambao" linahusu watu wenye kuongea mambo ya kupotosha.
Proverbs 2:14-15
Hufurahia
hawa ni watu waliotajwa katika 2:11
hufurahia katika upotevu wa uovu
wanafurahi kutenda mambo ambayo wanajua ni maovu
Hufuata njia za udanganyifu
huwadanganya watu wengine
na hutumia udanganyifu huficha mapito yao
na hudanganga ili mtu yeyote isifahamu jambo walilofanya
Proverbs 2:16-17
Maelezo ya Jumla
Baba anaendelea kumfundisha mtoto wake jinsi ambavyo hekima itamlinda.
Hekima na busara vitakuokoa
"kama utakuwa na hekima na busara, utajiokoa wewe mwenyewe"
mwenza wa ujana wake
mume wake, ambaye aliyemwoa tangu ujanani
agano la Mungu wake
agano la ndoa ambalo amelifanya na mume wake katika uwepo wa Mungu.
Proverbs 2:18-19
nyumba yake inaelekea mauti
kwenda kwenye nyumba yake husanabisha mauti au njia ya kwenda nyumbani kwake ni njia ya kuelekea katika mauti.
mapito yake yatakuongoza
njia za kwenda kwenye nyumba yake zitakuongoza au namna ya anavyoishi itakuongoza.
kwa wale waliopo kwenye kaburi
roho za watu wafu, ni picha ya sehemu ya wafu
huingia kwake
kwenda kwenye nyumba yake na kulala pamoja naye, kama ambayo mtu anavyo lala na malaya.
hatazifikia njia za uzima
hawataishi maisha ya furaha tena au hawataweza kurudi katika nchi ya watu wenye uhai
Proverbs 2:20-22
kwa hiyo
mwandishi anasema faida za kupata ufahamu na busara
utatembea katika njia... fuata njia
utaishi katika njia... kufuata mfano
waovu wataondolewa kutoka katika nchi
"Yahwe atawaondoa waovu kutoka katika nchi"
waovu... wasioamini
"wale ambao ni waovu ... wale wasiokuwa na imani" au "watu waovu ... watu wasioamini"
wasioamini wataondolewa katika nchi
ambao hawaamini atawaondoa katika nchi
Proverbs 3
Proverbs 3:1-2
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anaongea kama baba akimfundisha mtoto wake kwa kutumia shairi.
usizisahau amri zangu
"usiyasahau niyokuagiza"
yatunze mafundisho yangu ndani ya moyo wako
"Nilichokufundisha ukikumbuke daima"
wingi wa siku na miaka ya uzima
utaishi maisha marefu
Proverbs 3:3-4
usiruhu agano la uadilifu na uaminifu viondoke kwako
Hakikisha unatekeleza agano la uadilifu na uaminifu daima.
uyafunge pamoja kwenye shingo yako
uoneshe kwa furaha kama mtu ambovyo huvaa mikufu shingoni
yaandika kwenye kibao cha moyo wako
daima uyakumbuke kana kwamba umeyaandika kwenye kibao cha kudumu
katika upeo wa Mungu na wanadamu
katika hukumu ya Mungu na wanadamu
Proverbs 3:5-6
kwa moyo wako wote
" mambo yako yote"
usitegemee ufahamu wako mwenyewe
usiweke tumaini katika ufahamu wako wenyewe
katika njia zako zote
"katika kila jambo ulifanyalo"
yeye atazinyosha njia zako
atakupa mafanikia
Proverbs 3:7-8
usiw wenye busara katika macho yako mwenyewe
"usiwe wenye busara katika mawazo yako mwenyewe"
geuka mbali kutoka katika uovu
"usitende uovu"
itakuwa uponyaji katika mwilini mwako
"kama utafanya hivi, itakuwa uponyaji kwa ajili ya mwili wako"
Proverbs 3:9-10
ulivyozalisha
"kuvuna"
ghala zako zitajazwa
"ghala zako zitajaa"
ghala
majengo au chumba ambapo chakila huhifadhiwa
mashikizo yako yatapasuka
vifaa vyako vya kutunzia vitajaa kupita kawaida, kama vinakaribia kupasuka.
Proverbs 3:11-12
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anaandika kama baba akimfundisha mwanawe.
mwana ambaye humpendeza
baba huonesha upendo kwa mwanae
Proverbs 3:13-14
mtu ambaye hujipatia hekima
mtu anayepata hekima
mbadala ambao fedha itakupa
faida ya biashara au uwekezaji
Proverbs 3:15-16
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anaongea juu y hekima kama vile anaongea na mwanamke.
thamani
"a gharama" au "ghari"
ni mwenye wingi wa siku katika mkono wake wa kulia; katika mkono wake wa kushoto ni utajiri na heshima
hekima humpa mtu siku nyingi na utajiri na heshima
wingi wa siku
Hii nahau maana yake"maisha marefu"
Proverbs 3:17-18
Njia zake ni njia za upole na mapito yake yote ni amani
Hekima inatakutendea kwa upole na kukupa amani daima
Yeye ni mti wa uzima kwao ambao humshikilia
Hekima ni kama mti ambao huhifadhi uzima kwao ambao hula matunda yake
mti wa uzima
mti unaota uzima au mti ambao matunda yake hudumisha uzima
kwao ambao humshikilia
wao ambao hushikilia kwenye matunda yake
Proverbs 3:19-20
Yahwe aliumba dunia... aliziimarisha mbingu
Yahwe aliumba dunia.. aliziunda mbingu
vina hufunguka wazi
alisababisha mito kutiririka au alisababisha kuwepo kwa bahari
umande
maji ambayo hutokea ardhini wakati wa usiku
Proverbs 3:21-22
usiyapoteze kwenye upeo
usiyasahau
Yatakuwa uzima nafsini mwako
yatakuwa uzima kwa ajili yako
urembo wa kuvutia wa kuvaa shingoni mwako
kuonekana unavutia kama mtu ambavyo hujiremba mwenyewe kwa mikufu ya shingoni
urembo wa kuvutia
urembo ambao huonyesha kibali cha Yahwe
Proverbs 3:23-24
utatembea kwenye njia yako kwa usalama
maisha yako utaishi kwa usalama
mguu wako hautajikwaa
hutafanya mambo yenye makosa
wakati wa kulala
wakati unaposhuka kulala
usingizi wako utakuwa mtamu
usingizi wako utakuwa mzuri au utalala kwa amani
Proverbs 3:25-26
uharibidu wa waovu, wakati unapokuja
"Wakati waovu wanaposababisha uharibifu"
Yahwe atakuwa upande wako
Yahwe atakusaidia na kukutetea
ataulinda mguu wako usinaswe katika mtego
atakulinda na wale ambao wanataka kukudhuru
Proverbs 3:27-28
usizuie mazuri
"usizuie vitu vizuri" au "usizuie matendo mema"
wakati yapo katika uwezo wako kuyatenda
" wakati unao uwezo wa kusaidia"
unapokuwa na pesa
mtu anapokuwa na uwezo wa kusaidia leo, bali akamwambia jirani yake rudi tena keshao. "unapokuwa na pesa kwa wakati huu"
Proverbs 3:29-30
jirani
kwa kawaida ni mtu anayeishi jirani, au ambaye anayeishi katika jumuiya au kundi la watu wenye kufahamiana.
anayekuamini, mwaminifu
mtu mkweli na kutumainiwa
Proverbs 3:31-32
... wala usicahague moja ya njia zake
"usichague kuiga njia yake yoyote"
mtu mjanja ni chukizo kwa Yahwe
"Yahwe humchukia mtu mjanja"
mtu mjanja
mtu wenye dharau au mdanganyifu
mtu mwaminifu humpeleka katika ujasiri
"Yahwe ni rafiki wa karibu kwa waaminifu"
Proverbs 3:33-34
Laan ya Yahwe ipo juu ya mtu mwovu
"Yahwe ameilaani familia ya mtu mwovu"
Huibariki maskani ya watu wema
"huzibariki familia za watu wema"
huwapa fadhila watu wanyenyekevu
"huonyesha fadhila kwa watu wanyenyekevu" au "ni mkarimu kwa watu wanyenyekevu"
Proverbs 3:35
watu wenye busara hurithi heshima
"Watu wenye busara watapata heshima ya sifa njema"
wapumbavu watainuliwa kwa aibu yao
"Yahwe atamfanya kila mtu aone aibu ya wapumbavu"
Proverbs 4
Proverbs 4:1-2
Maelezo ya Jumla
Mwandishi ananena kama baba anayewafundisha watoto wake.
Sikiliza
"kusikiliza kwa umakini"
utajua maana ya ufahamu
"utajua jinsi ya kufahamu" au "utapata ufahamu"
Mimi ninakupa maagizo mazuri
"Ninachokufundisha mimi ni kizuri"
Proverbs 4:3-4
Mimi nilipokuwa mwana kwa baba yangu
"Mimi nilipokuwa bado mvulana nikijifunza kwa baba yangu"
mpole na mtoto pekee
"mtoto mpole wa pekee"
moyo wako uyazingatie maneno yangu
"Ukumbuke daima yale ambayo ninakufundisha"
Proverbs 4:5-6
Maelezo ya Jumla
Baba anaendelea kuwafundisha watoto wake mambo ambayo yeye alifundishwa na baba yake
Jipatie hekima
"fanya bidii kupata hekima kwa ajili yako mwenyewe" au "pata hekima"
usiyasahau
"yakumbuke"
usiyakatae
"kubali"
maneno ya kinwa changu
"yale ninayonena"
usimwache hekima na naye atakulinda; mpende na yeye atakuweka salama
Mwandishi ananena juu ya hekima kama mwanamke ambaye humlinda mtu ambaye ni mwaminifu.
usimwache hekima
" ishikilie kwa nguvu kabisa hekima"au " uwe mwaminifu kwa hekima"
mpende
" mpende hekima"
Proverbs 4:7-9
Maelezo ya Jumla
Baba anamalizia kuwafundisha watoto wake yale ambayo alifunzwa na baba yake.
tumia mapata yako yote kujipatia ufahamu
"thamini ufahamu zaidi kuliko yote unayoyamiliki"
mtunze hekima na yeye atakutukuza
"kama utamlea hekima, atakupa heshima kubwa"
mtunze
kujihisi au kuonyesha upendo mkuu kwamtu au kitu
atakuheshimu endapo utamkumbatia
"kama utapenda sana hekima, hekima itasababisha watu wakuheshimu"
ataweka kilemba cha heshima juu ya kichwa chako
"Hekima itakuwa kama kilemba juu ya kichwa chako ambacho huonesha heshima kuu"
Kilemba
duara iliyofumwa kwa majani au maua
atakupatia taji zuri
" hekima ni kama taji zuri juu ya kichwa chako"
Proverbs 4:10-12
na uyasikilize maneno yangu
"sikiliza kwa kuzingatia ninachokufundisha"
utakuwa na miaka mingi ya maisha yako
"utaishi miaka mingi"
Nianakulekeza katika njia ya hekima; Mimi ninakuongoza kwenye njia nyoofu
"niakufundisha jinsi ya kuishi kwa busara; ninafafanua njia njema ya kuishi"
unapotembea, hapana mtu atakayesimama katika njia yako na kama ukikimbia, hutajikwaa
"unapopanga kitu, utafanikiwa kukitekeleza"
Proverbs 4:13-15
shika maagizo, usiyaache yaondoke
"endelea kutii yale niyokufundisha na usiyasahau"
maana ni uzima wako
"maana yatautunza uzima wako"
usiifuate njia ya waovu na usienende kwenye njia ya wale watendao maovu
"usifanye yale wanayofanya watu waovu na usijiunge katika matendo ya watu watendao ubaya"
Jiepushe nayo
"iepuke njia ya waovu"
Proverbs 4:16-17
hawezi kulala hadi watende ubaya
watu waovu hutamani kutenda matendo mabaya
wameporwa usingizi wao
"hawawezi kulala"
hadi wamwangushe mtu
"mpaka wadhuru mtu"
wanakula mkate wa uovu na kunywa mvinyo wa vurugu
"wanakula mkate ambao wanaupata kwa kutenda mambo maovu na kunywa mvinyo ambao wanaupata kwa njia ya vurugu"
Proverbs 4:18-19
njia ya watu wenye haki ... njia ya waovu
"mwenendo wa watu wenye haki ...mwenendo wa waovu"
njia ya watu wenye haki ni kama nuru ya awali ambayo huzidi kung'ara
"watu wenye haki hutembea kwenye njia yao kwa salama kwa kuwa jua la asubuhi huangaza juu yake na wanga hung'aa zaidi
nuru ya awali
Hii ni mapambazuko au mawio
hadi mchana mkamilifu
"mpaka jua ling'are kwa wangavu zaidi" au "hadi mchana haswa"
njia ya waovu ni kama giza
"watu waovu hutembea kwenye hatari maana njia yao haina mwanga kuwawezesha kuona"
hawajua ambapo hujikwaa
"hawajua kwa nini hukumbwa na madhara na bahati mbaya"
Proverbs 4:20-21
sikiliza
"kusikiliza kwa umakini"
tega sikio lako kwenye kauli zangu
"sikiliza kwa usikivu kwa mambo amabyo ninakuambia"
usiache ziondoke kutoka machoni pako
"usiache kuzitafakari "
uzihifadhi moyoni mwako
"uzikumbuke daima"
Proverbs 4:22-23
maneno yangu ni uzima
"maneno yangu yanaleta uzima"
kwa wale wanaozipata
"kwa wale wanaozifahamu na kuzitenda"
afya katika mwili wao wote
"maneno yangu yataleta afya katika mwili wote kwa wale wanaoyapata"
utunze moyo wako salama na kuulinda
"tunza akili yako salama na kuyalinda mawazo yako"
kwa bidii yote
"kwa uthabiti na nguvu"
kutoka kwenye moyo wako hububujika chemchemi za uzima
"kila kitu unachosema huja kutoka katika mawazo yako" au "mawazo yako hubainisha mwenendo wa maisha yako"
Proverbs 4:24-25
weka mbali nawe maongezi ya ukaidi na weka mbali mazungumzo ya ufisadi
"usiongope na kusema kwa udanyanyifu"
macho yako yatazame mbele na ukaza mtazamo mbele sawasawa
"utazame mbele daima na ukaze mtazamo wako mbele moja kwa moja"
Proverbs 4:26-27
sawazisha njia kwa ajili ya mguu wako
"Tayarisha vizuri yale unayotaka kuyafanya"
sawazisha njia
"njia laini au "njia tulivu"
kisha njia zako zote zitakuwa salama
"kisha kila kitu unachofanya kitakuwa sawa"
usigeuke upande wa kulia au wa kushoto
"tembea wima kwenda mbele wala usiiache njia iliyo sawa"
ondoa mguu wako kwenye maovu
"kaa mbali na maovu" au "ondoka kwenye maovu"
Proverbs 5
Proverbs 5:1-2
Maelezo ya Jumla
Mwandishi ananena kama baba anayewafundisha watoto wake.
tega masikio yako
"sikiliza kwa makini"
busara
angalia 1:4
midomo yako iyalinde maarifa
"utaongea ambacho ni ukweli tu"
Proverbs 5:3-4
midomo ya malaya hutona asali
"maneno ya malaya ni matamu, kana kwamba hutona asali" au "busu la malaya ni tamu, kana kwamba midomo yake hutona asali"
kinywa chake ni laini kuliko mafuta
"kauli yake inashawishi na laini kuliko mafuta ya mizeituni" au "busu lake ni laini kuliko mafuta ya mizeituni"
lakini mwisho ni mchungu kuliko pakanga
"lakini mwishoni ni mchungu kama radha ya pakanga na atasababisha madhara"
pakanga
mmea ambao unaradha ya uchungu
hukata kama upanga wenye makali
"humjeruhi mtu, kama unavyojeruhi upanga mkali"
Proverbs 5:5-6
miguu yake huelekea chini kwenye mauti
"miguu yake" hapa anaongelewa mtu malaya. "Anatembea katika njia ambayo inaeleke kwenye mauti" au "mwenendo wake huelekea kwenye mauti"
hatua zake huelekea kwenye njia ya kuzimu
"hutembea katika njia ya kuzimu"au " tabia yake humpeleka kwenye njia ya kuzimu"
yeye haifikirii njia ya uzima
"hajali kuhusu mwenendo wa kumwongoza katika uzima"
hatua za mguu wake hutanga tanga
"hutembea katika njia ovu" au "hutanga tanga kana kwamba amepotea"
Proverbs 5:7-8
Sasa
Hapa walimu anaondoka katika hali na kuonya juu ya umalaya na kuanza kutoa ushauri.
nisikilize... usiache kusikiliza
sikiliza
usiache kusikiliza
"usikome kusikiliza"
maneno ya kinywa changu
"maneno yangu"
njia yako iweke mbali naye
"kaa mbali naye"
usiukaribie mlango wa nyumba yake
"usiende karibu na mlango wa nyumba yake" au " hata usisogee karibu na nyumba yake"
Proverbs 5:9-10
katika njia hiyo
inahusu njia aliyoizungumzia hapo mwanzo
hutatoa heshima yako kwa wengine
"isipoteze heshima yako nzuri miongoni mwa watu wengine" au "usipoteze utajiri wako kuwapa watu wengine"
au miaka ya uzima wako kwa mtu mkatili
"au kumpati mtu makatili uzima wako" au "kusababisha mtu mkatili akuue ungali bado kijana"
mtu mkatili
pengine huyu ni mume wa mke malaya, ambayo atamshughulikia kwa ukatili mtu anayelala na mke wake
wageni hawatasherekea kwa utajiri wako
"wageni wasikuchukulie utajiri wako wote"
kazi yako uliyofanya isiende katika nyumba ya wageni
"vitu ulivyopata visimalizike kwa kuishia kwenye famila za wageni"
Proverbs 5:11-12
nyama yako na mwili wako vikateketea
"mwili wako ukapotelea mbali" au "ukapotea"
vikateketea
"kuchoka kimwili" au "kuwa dhaifu na afya mbaya"
Mimi nilichukia mafundisho ... moyo wangu ulidharau kusahihishwa
huyu mtu alichukia alichoambiwa na walimu wake
jinsi gani nilichukia mafundisho
"nilichukia sana wakati mtu aliponielekeza"
moyo wangu ulidharau masahihisho
"Niliwadharau watu waliponionya"
Proverbs 5:13-14
kutega masikio yangu kwa walimu wangu
'"kuwasikiliza wale walionielekeza"
katikati ya kusanyiko, miongoni mwa watu waliokusanyika
jumuiya ilikusanyika ama kumwabudu Mungu au kuhukumu dhidi ya makosa yake.
Proverbs 5:15-17
maji kutoka katika birika lako mwenyewe ... maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe
Mwandishi anazunguza juu ya mume kulala na mke wake pekee kana kwamba ni kunywa maji kutoka kwenye kisima au birika lake mwenyewe.
maji yanayotiririka
"maji mapya" au "maji ya kutiririka"
yapasa chemchemi zako ... miferji yako ya maji itiririke katika njia kuu?
"Chemchemi yako haipaswi ...mifereji yako ya majiji haipaswi kutiririka katika njia kuu"
njia kuu
maeneo ya wazi katika jiji au mjini ambapo miji miwili au zaidi inapokutana. Sehemu ya kawaida watu kukutana na kuongea.
Yawe
hii nahusu chemchemi na mifereji ya maji
wala si kwa ajili ya wageni pamoja nawe
"usichangie na wageni"
Proverbs 5:18-19
Chemchemi yako na ibarikiwe
"uweze kufurahia daima pamoja na mke wako"
mke wa ujana wako
"mwanamke ambaye ulimwoa wakati ukiwa kijana" au "mke wako kijana"
Ni ayala apendaye na kulungu mwenye madaha
"Ni mwanamke mzuri na mwenye kependeza kama ayala au kulungu"
mwenye madaha
"mzuri wakati apotembea"
maziwa yake yakutosheleze
"maziwa yake yakujaze furaha kama maziwa ya mama yanavyowatosheleza watoto wake kwa chakula"
daima akuleweshe kwa upendo wake
'upendo wake na ukutawale kama pombe inavyomtawala mlevi"
kwa upendo wake
kwa upendo wake kwako
Proverbs 5:20-21
Mwanangu, kwa nini wewe, uwe mateka wa malaya; kwa nini kuyakumbatia maziwa ya mwanamke asiye mwadilifu?
"Mwanangu, usitekwe na malaya!Usikumbatie maziwa mwanamke asiye mwadilifu!"
uwe mateka wa malaya
"kuruhusu malaya kukuteka wewe"
huona kila jambo... huzitazama njia zote
Mungu anafahamu kila jambo analolifanya kila mtu
njia zote anazochukia
"kila sehemu anapokwenda" au "kila kitu anachofanya"
Proverbs 5:22-23
mtu mwovu atatekwa kwa makosa yake mwenyewe
"mtu mwovu hataweza kuepuka madhara ya makosa yake"
nyuzi za dhambi yake zitamshika kwa nguvu
"kwa sababu ya dhambi zake, atakuwa kama mnyama aliyenaswa katika mtego"
upumabavu wake mkuu utampoteza
"upumbavu wake mkuu utamwongoza upotevuni"
upumabavu wake
"kwa sababu ya upumabavu wake"
Proverbs 6
Proverbs 6:1-2
weka pesa zako
tunza sehemu ya pesa zako
mdhamana kwa ajili ya mkopo wa jirani yako
maana: jirani yako anaweza kuja kwako kwa ajili ya kukopa au jirani yako anataka mkopo kwa mtu mwingine, lakini unaahidi kumlipa mkopesahaji kama jirani yako hataweza.
jirani
maana nyingine ni "rafiki"
umeweka mtego kwa ajili yako mwenyewe
"umetengeneza mtego ambao utakunasa wewe mwenyewe"
maneno ya kinwa chako
"ulichosema" au "ulichoahidi kufanya"
Proverbs 6:3
jiokoe mwenyewe
jilinde mwenyewe" au "jisaidie mwenye kutoka katika matatizo haya"
umeangukia kwenye mkono wa jirani yako
"jirani yako anaweza kuleta madhara kwako kama akitaka" au "jirani yako ananguvu juu yako"
jirani
"rafiki"
Proverbs 6:4-5
Macho yako usiyape usingizi na kope kope za macho yako kusinzia
"kaa macho, na kufanya unachoweza"
macho yako... kope zako
" mwenyewe"
jiokowe mwenyewe kama swala kutoka kwenye mkono wa mwindaji
"Epa kutoka kwa jirani yako kama swala ambaye hukimbia kutoka kwa mwindaji"
swali
Huyu ni mnyama ambaye hula majani na mara nyingi watu humwinda kwa ajili ya nyama. Mnyama huyu ni maarufu kwa kwa kukimbia mbbali upesi
kutoka kwenye mkono wa mwindaji
"kutoka kwenye udhibiti wa mwindaji"
kama ndege kutoka kwenye mkono wa mwindaji wa ndege
"epa kama ndege ambaye huruka kwenda mbali kutoka kwa mwindaji wa ndege"
Proverbs 6:6-8
Mtazame...zitafakari
"jifunze ...fikiri juu yake" au "cunguza kwa umakini... tafakari"
chungu
ni mdudu mdogo ambaye huishi ardhini au kichuguu anachojenga mwenyewe. Huishi katika makundi ya maelfu, na wanaweza kunyanyua viti vikubwa kuliko wenyewe.
zitafakari njia zake
"tafakari jinsi chungu anavyotenda"
kamanda, ofisa, au mtawala
Haya ni maneno yenye maana moja kusisitiza kuwa hakuna mtu mwenye mamlaka rasmi juu ya chungu .
huandaa chakula chake wakati wa jua... wakati wa mavuno huhifadhi chkula chake
Hapa inaonesha ni jinsi gani chungu huwajibika
wakati wa jua
ni majira ambapo baadhi ya miti huzaa matunda
Proverbs 6:9-11
Je utalala hata lini ... lini utainuka kutoka kwenye usingizi?
"Amka, wewe mtu mzembe! Inuka kwenye kitanda chako"
Usingizi kidogo ... mikono kujipumzisha
Haya ni aina ya mambo amabayo watu wazembe husema
Lala kidogo, sinzia kidogo
"nitaendelea kulala zaidi"
kukunja mikono kwa kujipumzisha
"nitakunja mikono yangu kwa utaulivu na kupumzika kidogo"
na umasikini wako utakuja
"ukiendelea kuwa mzembe, umasikini wako utakuja" au " Wakati umelala, umasikini utakuja"
umasikini wako utakuja kama mnyang'anyi
ghafula utakuwa masikini, kana kwamba mnyang'anyi amekuja na kukuibia kila kitu ulichonacho"
na uhitaji wako kama askari mwenye silaha
"na utakuwa mhitaji kana kwamba askari mwenye silaha amekuibia vitu vyako vyote"
askari mwenye silaha
"askari ambaye ameshikilia silaha" au "mtu mwenye silaha"
Proverbs 6:12-13
Mtu asyefaa...mtu mwovu
inasisitiza juu ya ubaya wa huyu mtu "mtu asiyekuwa na thamani-mtu mwovu"
huishi kwa udanganyifu wa kauli zake
"husema uongo daima"
hukonyeza macho yake, akifanya viashiria kwa miguu yake na kusonta kwa vidole vyake
Hii ni vile mtu mwovu huwasiliana kwa siri ili kudanganya watu wengine.
hukonyeza macho yake
mtu akikonyeza hufumba jicho moja kwa muda mfupi kama kiashiria cha siri kwa mtu mwingine.
Proverbs 6:14-15
Hutunga uovu
"huandaa ubaya" au "Hujitayarisha kufanya matendo mabaya"
kuchochea mafarakano daima
"Siku zote husababisha kutoelewana" au " hutafuta mafarakano daima na kuyaendeleza"
Kwa hiyo
"kwa sababu hiyo"
msiba wake utamkuta kwa ghafula
"msiba wake utamkamata"
msiba wake
hii inahusu msiba utakaotokea ambao mhusika ameusababisha.
ghafla; kwa muda mchache
kwa haraka sana au "bila kutazamia"
Proverbs 6:16
vitu sita ambavyo Yahwe huchukia, saba ambavyo
Maana yake: Yahwe huchukia vitu vingi na wala si mara moja.
ambavyo vinamchukiza
"amabavyo husababisha ajisikie karaha"
Proverbs 6:17-19
Sentensi Unganishi
Hii ni orodha ya vitu ambayo Yahwe huchukia kama vilivyotajwa katika 6:16
macho...ulimi... mikono... moyo...miguu
Sehemu zote hizi za mwili zinamwelezea mwandamu kamili "watu"
humwaga damu ya
"kuua" au "uuaji wa mtu kwa kusudi"
njama mbaya
"mipango miovu"
anong'onaye uongo
"kusema uongo siku zote"
mafarakano
agalia 6:14
mtu apandaye mafarakano
"mtu amabaye huondoa maelewano"
Proverbs 6:20-21
tii amri ya baba yako... usiyaache mafundisho ya mama yako
Maana yake baba na mama wote wanahusika katika kufundiha na mchakato wa kufunza
usiayache mafundisho ya mama yako
"tii mafundisho ya mama yako"
yafunge katika moyo wako; yakaze kwenye shingo yako
Hizi ni amri na maelekezo kama zimeandikwa unaweza kuziweka katika mwili wako au kuvaa mwilini mwako ili kujikumbusha mwenyewe.
Proverbs 6:22-23
Wakati unapotembea... unapolala... unapoamka
Hii inasisitiza kuwa masomo yanathamani muda wote
yatakuongoza... yatakulinda...yatakufundisha
mwandishi anarudia rudia kuonesha kuwa masomo haya yanathamani kwa vitu vya namna yoyote.
taa..mwanga...njia ya uzima
masomo yanafanya maisha kuwa mazuri na rahisi." yana faida kama taa...yanasidia kama mwanga katika giza..ni muhimu kuyafuta kama njia ya kuishi"
njia ya uzima
"njia inayoenda kwenye uzima" au "njia ya kuishi ambayo Mungu ameiruhusu"
Proverbs 6:24-25
itakutunza dhidi ya
"inakuokoa kutoka" au "inakulinda kutoka"
mwanamke mwovu...mwanamke mwovu
"malaya" pia angali 5:3
mwovu
"mbaya kimaadili"
uzuri wake
"kile kilicho kizuri kwake"
akunase
"kuwa na hali ya kudhibiti"
kope za macho yake
"macho yake mazuri"
Proverbs 6:26-27
bei ya kipande cha mkate
Hapa inaongelea gharama ya vitu siyo gharama ya kiroho au gharama ya maadili "kidogo"
atagharimu uhai wako
"mke wa mtu mwingine ataangamiza maisha yako kwa sababu kila wakati anahitaji zaidi" au "mume wa mke atakuwinda na atakuua"
Mtu anaweza kubeba moto kwenye kifua chake bila kuunguza nguo zake?
Jibu ni hapana "Kila mume ambaye hubeba moto kwenye kifua chake ataunguza nguo zake."
bila kuunguza
"bila kuteketeza" au "bila kuharibu"
nguo zake
nguo zinawakilisha mtu mwenyewe.
Proverbs 6:28-29
Mtu anaweza kutembea juu ya makaa ya moto bila kuungua miguu yake"
jibu ni hapana. "kila mtu anayetembea juu ya makaa ya moto miguu yake itaungua"
kutembea juu ya makaa ya moto
Hii inamaanisha kufanya uzinzi
kutembea
ni kwenda mwendo wa polepole kwa umbali mrefu ukitembea
kuungua
chomeka
Proverbs 6:30-31
kumdharau mwizi
" hawamtazami mwizi kwa dharau" au " hawafikiri mwizi ni mwovu"
kama atakamatwa
"mtu akimkamata"
katika nyumba yake
"ambayo anamiliki"
Proverbs 6:32-33
Mtu
"mwanaume"
ambacho anasitahili
'adhabu sitahiki kwa kile alichafanya"
aibu yake
" atakuwa na kumbukumbu za tendo lake la aibu"
Proverbs 6:34-35
hasira
"udhika sana"
hataonesha huruma
mtu ambaye mke wake amezini na mwanaume wingine " atakuumiza kadri anavyoweza"
wakati wa kulipiza kisasi
"kipindi analipza kisasi"
kulipiza kisasi
ni mtu kusababisha maumivu kwa mtu mwingine ambaye alitangulia kumwumiza hapo mwazo
fidia
"malipo"
hataweza kununuliwa
"hutaweza kumlipa pesa za kutosha kuibadili akili yake"
ingawa
"hata kama"
utampa
"kutoa kitu" au "kuadidi kutoa"
Proverbs 7
Proverbs 7:1-3
Tunza maneno yangu
"Tii maneno yangu"
uzihifadhi amri zangu ndani yako mwenyewe
"zikariri amri zangu"
tunza maagizo yangu
"tii maagizo yangu"
kama mboni ya jicho lako
Mboni ya jicho ipo ndani ya jicho ambayo watu huilinda sana wakati kitu kinaporukia usoni. "Mboni" inawakilisha kitu ambacho mtu hukithamini na kukilinda zaidi. "kama mali yako yenye thamani zaidi"
uzifunge katika vidole vyako
1) mwandishi alitaka mwanae achore baadhi ya amri za Mungu kwenye pete na kuivaa au 1) mwandishi alitaka mwanae akumbuke daima amri za Mungu, kana kwamba ni petefulani ambayo aliivaa daima
ziandike kwenye kibao cha moyo wako
"zikumbuke vizuri amri zangu kana kwamba umeziandika kwenye jiwe"
Proverbs 7:4-5
Mwabie hekima, "Wewe ni dada yangu"
"Thamini hekima kama ambavyo ungempenda dada yako"
mwite ufahamu jamaa yako
"ufahamu uchukulie kama ambavyo ungemtendea jamaa yako"
jamaa
"ndugu" au "mmoja wa wanafamilia"
mwanamke malaya
Maana yake ni mwanamke yeyote ambaye mwanaume hajamwoa. " Mwanamke ambaye hupaswi kufanya naye chochote"
Mwanamke mwovu
Hii inamaanisha ni kwa mwanamke yoyote ambaye hajulikani kwa mwanaume
kwa maneno yake laini
"ambaye huongea vitu vya kufurahisha, lakini anataka kukudanyanya"
Proverbs 7:6-7
shubaka
ni wavu wa dirishani
Wajinga
"bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga"
Proverbs 7:8-9
kona yake
"kona ambapo mwanamke mgeni alikuwa amesimama"
Kona
sehemu ambayo barabara mbili zinakutana
wakati wa jioni
muda ambapo giza linaanza kuingi na karibu kuwa giza
Proverbs 7:10-12
mwenye moyo wa uongo
Hapa "moyo" unamaanisha makusudi au mipango " mwanamke anakusudia kumdanganya mtu"
Alikuwa mwenye kelele na ukaidi
"aliongea kwa sauti sana na kutenda kwa namna aliyopenda"
miguu yake haikutulia nyumbani
"hakukaa nyumbani"
alisubiri kuvizia
"alisubiri kumnasa mtu"au "alisubiri ili ampate mtu ambaye ataweza kumshawishi kutenda dhambi"
Proverbs 7:13-15
yeye
Yeye inawakilisha mwanamke ambaye alitajwa katika 7:10
akamshika
"alimshikilia kwa nguvu"
kwa uso na haya
"kwa uso usiokuwa na hisia za aibu"
Mimi nimelipa nadhiri zangu
"nimetimiza dhabihu zangu nilizoahidi kwa Mungu"
kuutafuta uso wako
"kukutafuta" au "kukutafuta mahali ulipo"
Proverbs 7:16-18
nimekinyunyiza kitanda changu kwa
"nimetandaza juu ya kitanda changu"
udi
aina ya magamba kutoka kwenye mti ambayo hunukia vizuri
mdalasini
hiki ni kiungo kinachotengenezwa kutokana na magamba ya mti ambayo hunukia vizuri na radha nzuri
tushibe kwa upendo
"tufanye mambo ya upendo kwa kila mmoja kadri tunavyotaka"
Proverbs 7:19-21
hayupo nyumbani kwake
"hayupo nyumbani"
Mwezi mpevu
nyakati ambapo mwezi utoa mwanga sana
akamgeuza
"mwanamke akamshawishi mwanaume"
yeye...yake
mwanake aliyeolewa anayetaka kulala na mwanaume kijana
midomo laini
"kufurahisha kwa maneno ya kudanganya"
alimpotosha
"alimshawishi kufanya jambo baya" au alimshawishi kufanya dhambi pamoja naye"
Proverbs 7:22-23
ghafla akamfuata
"kwa haraka aliamua kwenda pamoja naye"
kama maksai akienda...kwenye mtego
ujinga na pasipo kutarajia kijana namfuata malaya ni kama vile wanyama ambavyo huwa hawajui hatari ambayo huwa inawakabili.
machinjo
sehemu ya kuulia mnyama ili kula nyama yake
ayala
angalia 5:18
Hadi mshale umtoboe hadi kwenye ini lake
"mpaka mwindaji ampige kwenye sehemu zake nyeti zaidi"
ini
kiungo hiki kinawakilisha sehemu muhimu sana ya mwili wa ayala
ingekuwa gharama ya uhai wake
" angeweza kufa haraka"
Proverbs 7:24-25
Sasa
Hii ni kuleta usikivu kwa wana wa msemaji anapohitimisha funzo hili
Moyo wako usizigeukie njia zake
"moyo wako ukae mbali kutoka kwenye njia za mwanamke malaya" au " Usiruhusu moyo wako ufanye mambo ambayo mwanamke malaya hufanya"
moyo wako
Hapa moyo unawakilisha matamanio ya mtu
usipotee katika njia zake
"usiiache njia sahihi ili kuzifuata njia zake"
Proverbs 7:26-27
amesababisha watu wengi kuanguka hali wamejeruhika
"amesababisha watu wengi kufa"
nyumba yake ipo kwenye njia za kwenda kuzimu ... hutelemka chini
Hapa "njia" inawakilisha aina ya tabia ambayo hufuatwa na watu wapumbavu. Kuzimu ilikuwa jina la ulimwengu wa wafu
kwenye njia za kwenda kuzimu...chini kwenye vyumba vyenye giza la mauti
maana yake wahanga wa mwanamke wataangamia
vyumba vyenye giza la mauti
Hapa inaonesha picha ambapo wafu wamelala katika vyumba mbalimbali huko kuzimu
Proverbs 8
Proverbs 8:1-3
Maelezo ya Jumla
Hekima ananena kwa watu katika mistari 4-36
Maelezo ya Jumla
Mistari mingi katika sura ya 8 ni mlinganisho au usambamba
Je Hekima haiti?
Hekima anaita
Je Hekima haiti?
Maana yake 1)Je hekima siyo kama mwanamke ambaye huita? 2) Je mwanamke aitwaye Hekima haiiti?
Je Ufahamu hapazi sauti yake?
Hapa neno "Ufahamu" ni sawa na neno "Hekima"
malango kwenye njia ya kuingia mjini
Nyakati za kale, miji mara nyingi ilikuwa na kuta za nje pamoja malango.
anaita
Hekima imevikwa sifa ya utu kama mwanamke(angalia Tashhisi)
Proverbs 8:4-5
Maelezo ya Jumla
Hekima ananena kwa watu katika mistari 4-36
sauti yangu ni kwa ajili ya wana wa wanadamu
Hapa "sauti" inawakilisha maneno yote yaliyoongewa "maneno yangu ni kwa ajili ya wana wa wanadamu"
wana wa wanadamu
"watu wote"
wajinga
"bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga"
kujifunza hekima
"kujifunza namna watu wenye busara hutenda" au "kujifunza maana ya kuwa mwenye busara"
lazima mpate akili ya ufahamu
"lazima muanze kufahamu vitu kwa akili zenu"
Proverbs 8:6-7
wakati midomo yangu inapofunguka
Midomo inamaanisha kinywa cha mtu anayeongea " wakati nipofumbua mdomo wangu kuongea"
adili
"sawa" au "haki"
kinywa changu hunena
" mimi ninasema"
kilicho cha kweli
"kile ambacho watu wanapaswa kuamini"
uovu ni chukizo katika midomo yangu
"uovu ni chukizo kwangu" au "kusema vitu viovu ingekuwa ni chukizo kwangu"
uovu
inamaanisha maneno maovu
Proverbs 8:8-9
maneno ya kinywa changu
"mambo ninayofundisha"
lililogeuzwa
"uongo"
yamenyooka
"kweli na safi "
maneno yangu yapo wima kwa wenye kujipatia maarifa
"wale wanaojua maana ya haki na uovu hufahamu kuwa ninachafundisha ni sahihi"
wima
"kweli"
Proverbs 8:10-11
jipatie mafundisho yangu kuliko fedha
"fanya juhudi zaidi kufahamu mafundisho yangu kuliko kujipatia fedha"
Maana Hekima ni bora zaidi kuliko malijani; hakuna hazina inayolingana naye.
"Maana mimi Hekima ni bora kuliko malijani, hakuna hazina inayolingana na mimi"
Proverbs 8:12-13
Mimi, Hekima, huishi kwa Busara
Busara imeongelewa hapa kama mtu
Busara
"kuamua vema"
Mimi humiliki maarifa na busara
"Mimi ni mwenye maarifa na busara" au " Ninajua vitu vingi, na mimi ni mwangalifu"
busara
kuwa mwangalifu kuhusu kile unachosema na kufanya; kuwa na tahadhari usisababishe maumivu au uharibifu kwa wengine
kauli za udanganyifu
"maongezi mabaya"
udanganyifu
iliyogeuka kutoka kwenye haki
Proverbs 8:14-16
ushauri mzuri
mapendekezo ya busara
ushauri
mausia ambayo hutolew ili kumsaidia mtu
sahihi
nzuri, ya kutegemewa
Mimi ni utambuzi
"Mimi ni utambuzi"
wakuu
moja ya wanachama wa familia muhimu katika taifa
Proverbs 8:17-18
nawapenda
Huu ni upendo wa asili kati ya marafiki au ndugu
bidii
kuedelea kwa nguvu na uangalifu
Kwangu kuna utajiri na heshima
"Mimi ninautajiri na heshima"
utajiri unaodumu na haki
"kwa hiyo, nitatoa utajiri wa kudumu na haki kwa wale wanaonitafuta"
haki
"uwezo wa kuishi aktika njia iliyo safi"
Proverbs 8:19-21
Matunda yangu
ambacho hekima huzalisha au husababisha
faida yangu
manufaa au faida ambayo hekima husababisha
Natembea katika njia ya haki
"Ninaishi kwa haki" au " Ninatenda ambacho ni haki"
katikati ya njia za uadilifu
"Ninafanya mambo makalifu" au "Ninatenda ambacho ni haki"
hazina
ghala kwa ajili ya vitu vya thamani
Proverbs 8:22-23
kwanza katika matendo yake
"nilikuwa wa kwanza miongoni mwa vitu alivyoviumba"
nyakati za kale
"muda mrefu uliopita"
nyakati
muda mrefu
Niliumbwa
"Mungu aliniumba"
toka mwazo wa dunia
"tokea wakati ambapo Mungu aliiumba dunia"
Proverbs 8:24-25
Maelezo ya Jumla
Hekima anaendelea kuongea
Kabla milima kuwepo
"Kabla Mungu hajaifanya misingi ya milima na kuiweka mahali pake"
Proverbs 8:26-27
Nilizaliwa ...nilikuwepo
Hekima anaongea kuhusu yeye mwenyewe
nilizaliwa
"nilikuwa hai"
thibitisha
" umbwa" au "fanywa"
alipochora duara juu ya sura ya kina
"wakati alipoweka alama juu uso wa bahari umbali ambao mtu anaweza kuona katika bahari kwa kila upande"
kina
"bahari"
Proverbs 8:28-29
Maelezo ya Jumla
Hekima anaendela kunena
imarisha
kuweka katika maisha ya kudumu
wakati chemchemi katika kina zilipoimarishwa
"wakati Mungu alipoimarisha chemchemi katika kina"
chemchemi katika kina
Waebrani wa zamani waliamini bahari ilipata maji yake kutoka katika chemchemi kwenye kitako cha bahari
alipoumba mpaka kwa ajili ya bahari
"alipoumba ufukwe kwa ajili ya bahari"
pale alipoweka mpaka kwa ajili ya misingi ya nchi kavu
Neno la kiebrania "dunia" pia linamaanisha "nchi"
"pale alipoweka mpaka kwa ajili ya misingi ya nchi kavu"
"wakati Mungu alipoweka mpaka kwa ajili ya misingi ya dunia"
Proverbs 8:30-31
Nilikuwa ubavuni wake
Hekima anasema alikuwa karibu na Yahwe, kumaanisha kuwa alikuwa msaidizi wake katika kuumba dunia.
fundistadi mjuzi
Huyu ni mtu amabye aliyefundishwa kwa miaka kutengeneza vitu vizuri kwa matumizi kama samani au nyumba
furaha
chanzo cha raha au sababu ya kufurahi
siku kwa siku
"muda wote"
dunia yake yote
"ulimwengu wote alioumba" au " aliumba kila kitu"
wana wa wanadamu
"watu aliowaleta kuishi ulimwenguni"
Proverbs 8:32-34
Sasa
Hii ni kuleta usikivu kwa wana wa msemaji anapohitimisha funzo hili
Nisikilizeni
Hekima anaendelea kuongea juu yake mwenyewe
wale wanaozifuta njia zangu
"wale wanaofanya kile ninachofundisha"
usiziache
"hakikisha unazifuata"
ataangalia kila siku kwenye milango yangu, akisubiri pembeni ya nguzo za milango yangu
"mtu mwenye busara husubira nje ya nyumba ya hekima wakati wa asubuhi ili ampe huduma" au "mtu mwenye busara husubira nje ya nyumba ya hekima ili hekima aje na kumfundisha"
Proverbs 8:35-36
Anionaye mimi....Anionaye mimi... hunichukia
Hekima anaongea juu yake yeye mwenyewe
yeye anayeshindwa
" yeye anayekosa kuniona mimi"
maisha yake mwenyewe
"maisha"yanawakilisha mtu mwenyewe
Proverbs 9
Proverbs 9:1-2
Maelezo ya Jumla
Mistari hii inatoa mfano ambayo hekima inafikiriwa kuwa mwanamke anayetoa ushauri mzuri kwa watu.
Hekima ameijenga nyumba yake
Mwandishi anazungumza kuhusu hekima kana kwamba ni mwanamke ambaye ameijenga nyumba yake mwenyewe.
Amechinja wanyama wake
"amechinja wanyama kwa ajili ya nyama kwa chakula chajioni"
amechanganya mvinyo wake
katika Israeli ya kale watu walichanganya mvinyo kwa maji "ameandaa mvinyo wake kwa kuuchanganya kwa maji"
Ameandaa meza yake
"ametayarisha meza yake"
Proverbs 9:3-4
Maelezo ya Jumla
Mistari hii inaanza kutoa ujumbe wa Hekima, ambayo imepewa sifa ya mtu mwanamke.
amewatuma wafanya kazi wake
Hawa wafanyakazi walikwenda na kuwakaribisha watu kuja kwenye sherehe ambayo Hekima ametayarisha.
wafanya kazi wake
Vijana wa kike au wasichana ambao wapo kwenye huduma ya heshima, mwanamke mzima, kama vile Hekima.
anaita
" anatangaza" au " anawaalika". "kwa sauti kuu anarudia kuwakaribisha"
sehemu ya juu kabisa ya mji
Mwaliko unatangazwa kwenye sehemu ya juu kabisa ili watu wote wausikie vizuri
nani ambaye ni mjinga?...mtu alinayepungukiwa na akili njema
" mtu yeyote ambaye ni mjinga,...yeyote anayepungukiwa na akili njema"
ni mjinga
"bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga"
ageukie hapa
" aiache njia yake na aje kwenye nyumba yangu"
Proverbs 9:5-6
Maelezo ya Jumla
Mistari hii inaendeleza ujumbe wa Hekima
njoo...kula...kunywa...ondoka ..ishi ...tembea
Mri hizi zote zipo kwenye wingi; Hekima anahutubia watu wengi kwa wakati mmoja.
mvinyo niliouchanganya
katika Israeli ya kale watu walichanganya mvinyo kwa maji "ameandaa mvinyo wake kwa kuuchanganya kwa maji"
acheni matendo ya ujinga
"acheni tabia yenu ya ujinga"
matendo ya ujinga
"bila uzoefu, isiye na ukomavu au mwenye hali ya uchanga"
njia ya ufahamu
"namna ya kuishi ambayo mtu mwenye busara huishi"
Proverbs 9:7-9
Maelezo ya Jumla
Mistari hii inaendeleza ujumbe wa Hekima
Mwenye kumwadibisha... wenye kumkemea
Tungo zote mbili zina maana sawa.
mwenye dhihaka
"mtu anayetukana watu wengine" au " mtu ambaye anapenda kuwafanya watu wengine waonekane wabaya"
hupokea matusi
"hupokea matendo ya kikatili"
mwenye kumkemea
"mtu yeyote anayemwelekeza"
usimkosoe
"usimwelekeze"
mkosoe mtu mwenye busara, na yeye...mfundishe mtu menye haki na yeye
'Kama utamwelimisha mtu mwenye busara, yeye...kama utamfundisha mtu mwenye haki , yeye"
mkosoe mtu mwenye busara...mfundishe mtu menye haki
Hivi virai viwili kimsingi vinasema jambo moja.
Proverbs 9:10-12
Maelezo ya Jumla
Mistari hii inahitimisha ujumbe wa Hekima
Hofu ya Yahwe
angalia katika 1:7
kwa njia yangu siku zako zitazidishwa
"Nitazidisha siku zako" au " Nitasababisha uishi siku nyingi"
kwa njia yangu
Hekima, imepewa utu kama wanamke, anaendelea kuongea hapa.
siku zako zitazisishwa, na utaongezewa miaka ya uzima
...hekima inafaida kubwa
utaongezewa miaka ya uzima
Nitaongeza miaka ya maisha yako" au "Nitaongeza miaka katika maisha yako" au "Nitakuwezesha kuishi muda mrefu"
Kama ni mwenye... na kama ni mwenye dharau
watu wenye busara hufaidika wenyewe kwa sababu ya hekima yao, na wenye dharau huteseka kwa sababu ya tabia zao.
utaichukua
Tabia mbaya wa mtu ni kama mzigo mzito ambao mtu huyo hupaswa kuubeba mgongoni mwake.
Proverbs 9:13-15
Maelezo ya Jumla
Mistari hii inaanza kuelezea upumbavu ambao umepewa sifa ya binadamu kama mwanamke
mwanamke mpumbavu
" upumbavu wa mwanamke"
hajafundishwa na hafahau kitu
Maana yake mwanamke mpumbavu asiyefaa " Hajui kitu chochote kabisa"
hajafundishwa
"Hajajifunza kutokana na auzoefu" au " Ni kijana na mjinga"
hutembea kwa unyofu katika njia yao
Hii ni nahau "Hufikira mambo yao mwenyewe tu" au " hujali shughuli zao wenyewe"
Proverbs 9:16-18
ni mjinga
"bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga"
njoo hapa
'Acha njia yake na uje hapa"
humwabia
Huyu mwanamke mpumbavu ambaye ametambulishwa katika 9:13
wale ambao hawana akili
"ambao hawana hekima" au "wale wasio na busara"
Maji ya wizi ni matamu, na mkate wa siri hufurahisha sana
Mwanamke mpumbavu anaongea raha ya maji ya wizi na mkate unaoliwa kwa siri kuwaambia wanaume kuwa kama watalala naye watapata raha. Anasema "Unaweza kufurahia kwangu kama unavyofurahia maji ambayo umeyaiba au mkate ambao ni wa siri"
kwamba wafu wapo pale
"kwamba wanaume walikwenda kwake sasa wamefariki"
chini kuzimu
"kuzimu" humaanisha ulimwengu wa wafu.
Proverbs 10
Proverbs 10:1-3
Maelezo ya Jumla
Mistari mingi katika sura ya 10 niulingafu sambamba
mithali za Sulemani
Baada ya utangulizi katika Sura 1-9, Sura ya 10 inaanza mafundisho ya mithali; misemo mifupi inayofundisha hekima.
kusanywa
jipatia kitu kwa kipindi
Yahwe hataiacha nafsi ya mtu mwenye haki kwenda njaa
"Yahwe huhakikisha kwamba wale watendao haki wanapata chakula"
Proverbs 10:4-5
mkono mvivu
"Mkono" unawakilisha nguvu na uwezo wa mtu. KTN: "mtu asiyetaka kufanya kazi"
mkono wenye bidii
"Mkono" unawakilisha nguvu na uwezo wa mtu. "Mtu anayefanya kazi kwa nguvu"
Proverbs 10:6-7
juu ya kichwa
"kichwa" kinawakilisha mtu mwenyewe. " vimetolewa kwa"
kinywa cha waovu
"maneno wanayoongea waovu"
hufunika
hificha ukweli
jina
"kumbukumbu"
Proverbs 10:8-9
angamia
"kuharibiwa" au "kutofaa kwa matumizi"
udanganyifu
sio kweli, ongo, fedheha
Proverbs 10:10-11
yeye ambaye hukonyeza jicho
"ambaye hufanya alama kwa ashiria"
atashushwa chini
"wengine watamwangamiza"
kinywa cha mwenye haki
"maneno ya mtu mwenye haki"
ni maji ya chemchemi ya uzima
kauli ya mtu huyu mwenye haki ni kama chemchemi ya maji ilivyo kwenye nchi kavu, huhifadhi maisha ya wanyama na watu.
kinywa cha mwovu
"maneno ya mtu mwovu"
kinywa cha mwovu hufunuka vurugu
Mtu mwovu huonekana kusema mambo ambayo hayana madhara lakini mipango yake ni kuvuruga mambo dhidi ya wengine.
Proverbs 10:12-13
upendo hufunika
upendo hutenda kazi sawa na mtu huondoa shida kati ya watu badala ya kuichochea.
kwenye midomo ya mtu mwenye ufahamu
"ambayo mtu mwenye akili husema"
fimbo ni kwa ajili ya mgongo
"mtu asiye na akili anahitaji adhabu kali"
Proverbs 10:14-15
kinywa cha mpumbavu
"maneno ya mtu mpumbavu"
mji wake wenye ngome
"usalama wale"
Proverbs 10:16-17
mshahara..faida
Haya ni matokea ya kuteda mema au uovu
Kuna njia ya kwenda kwenye uzima kwa yule ambaye hufuata maonyo
"Mtu ambaye hutii mafundisho ya busara atakuwa mwenye furaha na maisha marefu"
lakini yule ambaye hukataa kurudiwa huelekea kupotea
"lakini yule ambaye hatii mafundisho ya busara hatakuwa na maisha mazuri"
Proverbs 10:18-19
ana midomo ya uongo
"husema uongo"
maovu hayakosi
"kuna dhambi nyingi"
Proverbs 10:20-21
ulimi wa mtu mwenye haki
"Chochote anachosema mtu mwenye haki"
fedha safi
fedha inawakilisha misemo ya thamani "... thamani mno"
hulisha
sababisha kuendelea au kuwa imara
Proverbs 10:22-23
Ubaya ni mchezo ambao mpumabavu hucheza
"Wapumbavu hufurahi katika ubaya"
Proverbs 10:24-25
kitamkuta kwa ghafla
shinda...
waovu ni kama dhoruba
kama ambavyo dhoruba huja na kuondoa kila kitu hivyo watu waovu hawataonekana
msingi unaodumu daima
"ni mwanzo kwa ajili ya jambo ambalo hudumu daima"
Proverbs 10:26-27
Kama siki kwenye meno na moshi kwenye macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale ambao wamemtuma
"siki" na "moshi" vinawakilisha mambo ambayo huumiza macho na meno ya mtu. " Kumtuma mtu mvivu kwenda kukamilisha kazi haifai na inaleta uchungu"
siki
kimiminika kichungu hutumiwa kwa radha au kutunza chakula.
miaka ya waovu
" muda wa kuishi mtu mwovu"
Proverbs 10:28-30
miaka ya waovu
"muda wa kuishi mtu mwovu"
hataondolewa
"atakuwa salama"
Proverbs 10:31-32
kwenye kinywa cha mtu mwenye haki
"Kwa maneno ya mtu mwenye haki"
ulimi wa udanganyifu utakatwa
"Mungu atafunga vinywa vya watu amabo husema uongo"
midomo ya mwenye haki huyajua yanayokubalika
"mtu mwenye haki hujua kuongoa kwa namna ya kukubalika"
kinywa cha waovu
"maneno ya waovu"
Proverbs 11
Proverbs 11:1-2
Maelezo ya Jumla
Mistari mingi katika sura ya 11 ni ulingafu sambamba.
Yahwe huchukia vipimo ambavyo si sahihi
"Mungu huchukia vipimo vya uongo" au " Mungu huchukia watu wanapodanganya"
lakini hufurahia katika kipimo sahihi
"lakini hufurahia njia za uadilifu" au lakini hufurahi watu wanapokuwa waadilifu"
Proverbs 11:3-4
waongo
"watu waongo" au "wale ambao ni waongo"
Utajiri ni ubatili kwenye siku ya ghadhabu
siku ya ghadhabu ni "siku ya hukumu" au "siku za mwisho". "utajiri wa mtu hatamsaidi wakati Mungu atakapokuja kuhukumu"
Proverbs 11:5-6
huinyosha njia yake
"anamwelekea safi"
waovu... waongo
" wale ambao ni waovu ... wale ambao ni waongo"
waongo hunaswa kwa ujanja wao
"Wale ambao hufanya ubaya hukamatwa kwa matamanio yao"
waongo
tayari kusaliti uaminifu; wasaliti, wadanganyifu
Proverbs 11:7-8
tumaini lilokuwa kwenye nguvu zake
"ujasiri aliokuwa nao kwa nguvu zake mwenyewe"
hupotea
"hutokomea"
Mtu mwenye haki hulindwa katika taabu
"Mungu humlida katika taabu mtu ambaye hutenda haki"
taabu huja
"taabu humpata"
Proverbs 11:9-11
Kwa kinywa chake mwovu
"maneno ya mwovu"
mji hukua
"makundi ya watu hufanikiwa" au "jumuiya hufanikiwa"
kwa kinywa cha wabaya
"maneno ya watu wabaya"
Proverbs 11:12-13
hulitunza jambo
"hujizuia kuongea juu ya jambo"
Proverbs 11:14
washauri
wale ambao hutoa mapendekezo ya kutendeka jambo; wanaoshauri
Proverbs 11:15-16
ambaye huchukia kutoa
"ambaye hukataa kutoa"
watu wasiokuwa na huruma
watu wakatili, bila huruma, korofi
hushika utajiri
"wanatamaa ya utajiri"
Proverbs 11:17-18
yule ambaye
"mtu ambaye"
hupanda ambacho ni haki
" hutawanya ambacho ni haki"
huvuna mshahara wa kweli
"hakika atapewa thawabu"
Proverbs 11:19-20
yule ambaye
"mtu ambaye"
hufuta mabaya
"hukimbilia uovu" au "hutafuta uovu"
ambao mioyo yao hufuata
"wenye mawazo maovu"
Proverbs 11:21-22
haikosi kupatiwa adhabu
"wataadhibiwa"
Kama pete ya dhahabu... bila ufahamu
mwanamke bila ufahamu hafai kama pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe
bila ufahamu
"bila akili ya kawaida" au "ambaye ni mpumabavu"
Proverbs 11:23-24
yule ambaye hupanda mbegu
"mtu ambaye hujiandaa kwa wakati ujao"
nitakusanya hata zaidi
"nitajipatia hata zaidi"
asiyepanda
" asiye jiandaa"
Proverbs 11:25-26
atafanikiwa
"atapata zaidi"
yule ambaye
"mtu ambaye ni mkarimu" au" mtu yeyote"
mtu ambaye hukataa kuuza
mtu ambaye hubania utajiri wake badala ya kuwasaidia ambao ni wahitaji
yeye auzaye zawadi jema hukifunika kichwa chake
zawadi njema hutolewa kama taji ya heshima kwa yule ambaye huuza" au " mtu ambaye huiuza anaheshimiwa kwa baraka nyingi"
Proverbs 11:27-28
yule ambaye hutafuta kwa bidii
yule ambaye hutafuta kwa uangalifu na bidii
ataanguka
"ataangamizwa"
kama jani, watu wenye haki watasitawi
"watu wenye haki watafanikiwa kwa namna ile ile ambayo jani lenye afya hustawi"
watu wenye haki watasitawi
watu wenye haki watafanikiwa
Proverbs 11:29
ataurithi upepo
"hatarithi kitu chochote"
Proverbs 11:30-31
mwenye haki atakuwa kama mti wa uzima
"Wale watendao haki wataleta uzima kwao wenyewe na kwa wengine"
mti wa uzima
angalia 3:17
ni zaidi kiasi gani
"ni zaidi"
Proverbs 12
Proverbs 12:1-2
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anatumia ulinganifu katika sura hii yote
Maelezo ya Jumla
katika mistari ya 1-15 analinganisha hekima na upumbavu
yeyoye
"mtu yeyote ambaye"
yule achukiaye sahihisho
"mtu ambaye hataki kuambiwa jambo la kufanya"
ni mpumbavu
"asiye na busara"
Proverbs 12:3-4
Mtu hawezi kuimarishwa kwa ubaya
"hakuna mtu anayeweza kuwa thabiti na salama kwa kufanya ubaya"
hataweza kung'olewa
"kung'olewa" kunawakilisha kuchomolewa kutoka ardhini kama mmea au mti. Hivyo hili haliwezi kutokea kwa watu watendao haki.
mke mwema ni taji ya mume wake
"mke mwema ni alama ya heshima kuu kwa mume wake"
yeye aletaye aibu ni kama ugonjwa ambao huozesha mifupa yake
"matendo ya aibu ya mwanake huharibu ushawishi wa mume wake na furaha"
Proverbs 12:5-6
maneno ya watu wabaya ni uviziaji kwa ajili ya kuua
"mabo ya udanganyifu ambayo watu waovu huyasema ni kama mtu anayevizia kuua mtu kwa kushitukiza"
maneno ya waadilifu huwahifadhi salama
"ushauri kutoka kwa mtu mwadilifu huwahifadhi watu salama"
waadilifu
wenye haki, waaminifu
Proverbs 12:7-8
watu waovu wametupwa
"Watu watawatupa watu waovu" au "watu watawaondoa watu wabaya kutoka kwenye mamlaka"
nyumba
"familia" au "uzao"
mtu husifiwa kwa namna ya wingi wa hekima yake
"watu watawasifu ambao wanahekima"
yule anayefanya uchaguzi wa udanganyifu huchukiwa
"watu watamchukia yule ambaye kila wakati huwaza mambo mabaya" au " watu watamchukia yule ambaye huchukua mambo mazuri na kuyabadilisha kuwa mabaya"
Proverbs 12:9-10
bora kupata cheo ambacho siyo muhimu
"Ni bora kuwa mtu wa kawaida"
ni mkatili
"husababisha mateso"
Proverbs 12:11-12
miradi
"mipango" au "shughuli"
matunda
matendo na wawazo hudhihirisha tabia ya mtu kama mti unavyodhilidhwa kwa matunda yake.
Proverbs 12:13-14
mtu mwovu hunaswa maongezi yake mabaya
"Mambo mabaya ambayo husemwa na mtu mwovu yatamnasa"
kama kazi ya mikono yake inavyompa thawabu
kama ilivyo kazi njema anayoifanya inampa thawabu"
Proverbs 12:15-16
macho pake mwenyewe
"katika maoni yake mwenyewe"
ushauri
mapendekezo ya busara
ni mwerevu
" ni mwenye busara" au "mwenye akili njema"
Proverbs 12:17-18
Maneno ya mtu ambaye hunena kwa haraka ni kama makali ya upanga
"anachonena mtu bila kufikiri kinaweza kuumiza sana kama kama vile amechoma kwa upanga"
ulimi wa mwenye busara
"amabyo watu wenye busara husema"
huleta uponyaji
"faraja na uponyaji"
Proverbs 12:19-20
midomo yenye uaminifu hudumu daima
"mtu mwaminifu udumu daima"
ulimi wenye kudanganya ni kwa kitambo tu
" yeye ambaye hudanganya hudumu kwa kitambo tu"
washauri
watu ambao hutoa mwongozo wa mapendekezo ili kufanyika jambo;
Proverbs 12:21-22
Hakuna mabaya yanayokuja
"mambo mema huja"
Yahwe anachukia midomo inayodanganya
"Yahwe huwachukia wale ambao husema uongo"
Proverbs 12:23-24
husitiri maarifa yake
"Huwa haongei kila kitu ambacho anakijua"
mkono wenye bidii
"watu wenye bidii"
afanyishwa kazi kwa nguvu
"atakuwa mtumwa"
Proverbs 12:25-26
Mashaka
hisia za woga au hofu, wasiwasi
zitamwelemea
"...tasababisha kuwa na huzuni au sikitishwa"
lakini neno zuri humfanya afurahi
" lakini wengine wapomsemesha kwa upole, hufurahia tena"
Proverbs 12:27-28
hawawezi kuoka mawindo yao wenyewe
"mawindo" maana yake ni wanyama waliokamatwa au kuuliwa wakati wa kuwinda. "kuoka" ni namna ya kupika chakula
utajiri wa thamani
"hazina yenye thamani"
Proverbs 13
Proverbs 13:1-2
Mwana mwenye busara husikia
"Mwana mwenye busara hutii"
hatasikiliza karipio
"hatajifunza kutokana na kukaripiwa" au "hataweza kutii japo atakaripiwa"
kutoka kwenye matunda ya kinywa chake
"kutoka kwenye maneno ya kinywa chake " au "kutokana na usemi wake"
hamu
shauku au kupendelea kitu
waongo
wale ambao wapo tayari kusaliti au kuwadanganya wengine
Proverbs 13:3-4
kinywa chake
" Ambacho ananena"
apanuaye midomo yake
"kuongea sana" au "kuzungumza mno"
hamu...hamu
Angalia 13:1
tamani sana lakini hapati kitu
"hamu ya kubwa sana lakini hapati kitu"
hamu ya watu wenye bidii itamalika kabisa
|"watu wenye bidii watapata maisha ya kutoshelezwa" au "kuwa na bidii kutawafanya watu watosheke kabisa"
watu wenye bidii
watu ambao hufanya kazi kwa uangalifu na nguvu endelevu
Proverbs 13:5-6
chukizo
sababisha hisia kali za kuchukia
haki huwalinda wale
"Njia ya kuishi iliyothibitishwa na Yahwe hulinda"
ambao hawana kasoro katika njia yao
"amabo hawana makosa katika njia yao ya kuishi" au "ambao huishi maisha ya uadilifu"
ubaya huwageuzia mabali wale ambao hutenda dhambi
"ubaya huwageza wenye dhambi kutoka katika njia ya mafanikio"
Proverbs 13:7-8
amabye hujitarisha mwenyewe
"ambaye hujifanyia utajiri yeye mwenyewe"
hasikii kitisho
1) hakuna mtu atakaye mtisha kumwibia maana hana kitu cha kuibiwa au 2) hatasikiliza sahihisho la watu kwa sababu hana kitu cha kupoteza kama watamwadhibu " hasikilizi karipio"
Proverbs 13:9-10
Nuru ya watu wenye haki hufurahia
"ushawishi wa watu wenye haki huleta furaha"
taa ya watu waovu itazimishwa
"watu waovu watapoteza ushawishi wao"
Majivuno huzaa ugomvi
" Mara nyingi majivuno husababisha ugomvi"
sikiliza
"fuata" au "jali"
ushauri mzuri
maoni ambayo husaidia na kufaidisha
Proverbs 13:11-12
utajiri hudhoofika
"utajiri hupungua" au "utajiri hupotea taratibu "
kufanya kazi kwa mkono wake
"kufanya kazi kwa nguvu za mwili"
hufanya fedha yake istawi
"hufanya pesa yake iongezeke"
wakati tumaini linapositishwa
"wakati mtu anapotumaini kwa ajili ya jambo lakini hapokei hadi muda mrefu"
huvunja moyo
"husababisha huzuni kali"
shauku ikitimizwa ni mti wa uzima
mtu akipokea ambacho alitumaini na kufurahi ni kama mti unaotoa uzima. "shauku iliyotimizwa ni kama mti wa uzima"
mti wa uzima
"mti ambao unatoa uzima" au "mti ambao mtunda yake hutoa idhini ya uzima"
Proverbs 13:13-14
mwenye kuheshimu amri atapata thawabu
"watampa tuzo yeye ambaye anaheshimu amri"
chemchemi ya uzima
"chanzo kizuri cha uzima"
tanzi ya mauti
"mitego ambayo huekea kwenye mauti"
Proverbs 13:15-16
lakini njia ya mwongo haina mwisho
"lakini tabia ya waongo itasababisha uharibifu wao wenyewe"
mwongo
"mtu mwongo"
mpumbavu huonesha upumbavu wake
"mpumbavu huonesha upumavu wake kwa kila"
Proverbs 13:17-18
huanguka kwenye taabu
"hufanya kitu kibaya"
mjumbe
"tarishi" au "mtu wa mahusiano"
hujifunza katika sahihisho
"hujifunza ambapo mtu humsahihisha"
Proverbs 13:19-20
ni tamu
"yenye kuleta furaha" au "inafurahisha"
hamu
shauku au kupendelea kitu
ataumia
"ataangamia"
Proverbs 13:21-22
msiba huwakimbilia watenda dhambi
"mwenye dhambi hupata taabu popote wanapokwenda"
watu wenye haki hupewa thawabu ya mema
"Mungu huwapa thawabu watu wenye haki kwa mema"
wajukuu wake
"wana wa wana wake"au "watoto wa watoto wake" au "wazao wake"
utajiri wa mwenye dhambi umehifadhiwa kwa ajili ya mtu mwenye haki
" yeye atendaye haki atapokea utajiri ambao umahifadhiwa na mwenye dhambi"
Proverbs 13:23-24
shamba lisilolimwa
"shamba ambalo halijaandaliwa kwa kuzalisha chakula" au " shamba ambalo ni tupu tayari kwa kupanda"
lakini huondolwa kwa udhalimu
"lakini udhalimu hukichukua chakula" au " watu wadhalimu hukichukua chakula"
huzingatia kumwelekeza
" nakikisha namwelekeza"
Proverbs 13:25
hutimiza hamu yake
"hujiridhisha mwenyewe"au " hutimiza hamu yake"
tumbo la mwovu huona njaa daima
"mtu mwovu huwa na njaa daima kwa ajili ya kupata zaidi"
Proverbs 14
Proverbs 14:1-2
huijenga nyumba yake
"huifanya nyumba yake kuwa bora"
numba
1) nyumba halisi, ambalo ni jengo anamoishi 2) inaweza kumaanisha familia yake
kwa mikono yake
"mikono" inawakilisha matendo anayofanya. "yeye mwenyewe" au "kwa namna ambavyo anajiheshimu"
yeye ambaye ... yeye ambaye
"mtu ambaye ... mtu ambaye"
huenenda kwa uadilifu
"huenenda katika njia ya haki na uaminifu katika maisha yake"
humdharau
"kukosa adabu" au " kuonesha kuchukia"
katika njia zake humdharau yeye
"zake" huyu ni mtu asiye mwamnifu na "yeye" ni kiwakilishi kumwakilisha Yahwe
Proverbs 14:3-4
kinywa cha ... midomo ya
Kinywa na midomo vyote vinahusiana na kile ambacho mtu hunena
kipukizi la kiburi chake
chipukizi ni kitu amabacho huota kutoka kwenye kitu kingine. " ambacho huzalishwa na kiburi chake"
busara
"watu wenye busara"
ataihifadhi
"atawalinda kutoka ktatika madhara" au " atawatunza salama"
hori la kulia
hori ni kontana ambapo huwekwa chakula kwa ajili ya wanyama
mazao mengi
"mavuno mazuri"
kwa nguvu ya maksai
"nguvu" inawakilisha kazi imara anayoweza kufanya maksai "kwa sababu ya kazi anayofanya maksai"
Proverbs 14:5-6
hupumua uongo
"hudanganya daima"
na hakuna kitu
"na hekima haipo pale" au "lakini hatapata hekima"
huja upesi kwa
"hupatikan kwa urahisi" au "hupata bila ugumu"
mtu mwenye ufahamu
"mtu mwenye hekima" au "mtu mwenye ufahamu"
Proverbs 14:7-8
kwenye midomo yake
"kwa kauli zake" au "kwa ushauri wake"
busara
mtu mwenye maamuzi mazuri au akili
njia yake mwenyewe
"mwenendo wake" au "namna ya maisha yake"
upumavu wa wapumbavu ni udanganyifu
upumbavu wa wapumbavu ni kufikiri kuwa wanabusara, wakati hawana.
Proverbs 14:9-10
wakati dhabihu ya hatia inapotolewa
...wapumbavu hawaombi msamaha kwa Mungu au watu kwa ajili ya mambo mabaya wanayofanya.
lakini miongoni waadilifu hushiriki fadhila
"lakini waadilifu hufurahia wema pamoja" au "Wema wa Mungu huonekana miongoni mwa waadilifu"
uchungu
"huzuni" au "simanzi"
hakuna mgeni
"wale wasiomfahamu"
Proverbs 14:11-12
hema
"kaya"
sitawi
"kufanikiwa sana"
kuna njia ambayo huonekana sawa kwa mtu
"watu hufikiri kwamba namna wanavyoishi ni njia sahihi"
Proverbs 14:13-14
moyo huweza kucheka
"Hisia za mtu zinaweza zinaweza kuonesha furaha"
kuwa katika maumivu
"kukabiliwa na maumivu" au "umia"
yeye ambaye
mtu ambaye
stahiki ya njia zake
"anachostahili, hulingana na namna anavyoishi"
alivyo
" ambacho anakimiliki" au " ambacho anahaki ya kukifanya"
Proverbs 14:15-16
mjinga
"bila uzoefu, asiye mkomavu, bado na hali ya uchanga"
hatua zake
"matendo yake"
hugeukia mbali na uovu
"huepuka matendo maovu"
huacha kwa ujasiri
"hupuuza kabisa"
Proverbs 14:17-18
ni mwepesi kukasirika
"kuwa na hasira kwa haraka"
mjinga
"bila uzoefu, asiye mkomavu, bado na hali ya uchanga"
hurithi upumabavu
"rithi" maana yake kumiliki kitu kwa kudumu
upumabavu
mawazo na matendo ya kipumbavu
watu wenye busara
"watu werevu"
huvikwa taji ya maarifa
"vaa maarifa kama vile kilemba"
Proverbs 14:19-20
huinama chini
kuinama kwa unyenyekevu kuonesha adabu na heshima kwa mtu
kwenye malango ya mwenye haki
"kuonana na mtu mwenye haki"
mtu maskini huchukiwa hata na rafiki zake mwenyewe
"kila mmoja humchukia mtu maskini hata jirani zake"
Proverbs 14:21-22
yule...yule
"mtu ..mtu"
maskini
"watu fukara"
Je wale ambao hupanga mabaya hawapotei?
"wale ambao hupanga mabaya watapotea"
ambao hupanga mabaya
"amabo hufanya mipango ya uovu" au " amabo hufanya mipango ya mambo mabaya"
Proverbs 14:23-24
lakini kukiwa na maongezi tu
"lakini kama utaongea tu" au "lakini watu wote hufanya maongezi"
taji ya watu wenye busara
"thawabu ya watu wenye busara"
upumbavu wa wapumbavu
Angalia 14:7
Proverbs 14:25
hupumua uongo
"hudanganya daima"
Proverbs 14:26-27
chemchemi ya uzima
"chanzo cha maisha"
kutoka kwenye tanzi za mauti
"kutoka kwenye mitego ambayo italeta kifo"
Proverbs 14:28-29
idadi kubwa ya watu wake
"idadi ya watu anaowatawala"
ni uharibifu wa mfalme
"mfalme hana kitu na ufalme wake utaanguka"
mwepesi wa hasira
"mtu ambaye hukasirka haraka"
Proverbs 14:30-31
moyo mtulivu
" mtazamo wa amani" au "mwenendo ambao ni wa amani"
huozesha mifupa
"husababisha mtu kukosa afya mwilini na rohoni"
yule ambaye... yule ambaye
"mtu ambaye ... mtu ambaye"
laana
maana yake kutamani mambo mabaya yaweze kutokea kwa mtu.
maskini ...mhitaji
"mtu maskini...mtu mhitaji"
huonesha fadhila kwa
"ni mkarimu kwa" au " husaidia"
Proverbs 14:32-33
hushushwa chini kwa matendo yake mabaya
"matendo mabaya humsukuma" au " matendo mabaya huharibu"
Hekima hukaa katika moyo
"hekima ipo katika namna ya kufikiri na kutenda"
ufahamu
"mtu mwenye ufahamu"
hujidhihirisha yeye mwenyewe
" huhakikisha kuwa watu wanamjua"
yeye
neno "yeye" linawakilisha hekima
Proverbs 14:34-35
aibu
"kuleta fedheha "
kwa busara
"kwa werevu"
yule ambaye
"mtumishi ambaye"
Proverbs 15
Proverbs 15:1-2
jibu la upole huodoa ghadhabu
"kumjibu mtu kwa upole kutatuliza ghadhabu ya huyo mtu"
lakini neno la ukatili huchochea hasira
"lakini kuongea kwa ukali husababisha yule mtu kuwa na hasira zaidi"
ulimi wa watu wenye busara hutamka maarifa
"watu werevu hutamka maarifa wanapoongea"
hutamka maarifa
"huyafanya maarifa yavutie" au " hutumia maarifa kwa usahihi"
kinywa cha wapumbavu humwaga upumbavu
"wapumbavu huongea upumbavu siku zote"
Proverbs 15:3-4
macho ya Yahwe yapo kila mahali
"Yahwe huona kila kitu"
mema na maovu
"watu wema na watu waovu"
ulimi uponyao ni mti wa uzima
" maneno ya upole ni kama mti ambao hutoa uzima"
ulimi wenye kudanganya huvunja moyo
"kauli ya uongo husababisha mtu kuvunjika moyo"
Proverbs 15:5-6
yeye ambaye hujifunza kutokana na sahihisho
"yeye ambaye hujifunza wakati wa kusahihishwa na mtu mwingine"
busara
"werevu"
mapato ya mtu mwovu humpa
"utajiri ambao mtu mwovu hujipatia humpa"
Proverbs 15:7-8
midomo ya watu wenye busara husambaza maarifa
"kauli ya watu wenye busara hutawanya maarifa"
siyo mioyo ya wapumbavu
" wapumbavu hawasambazi maarifa" au " wapumbavu hawana maarifa katika mioyo yao" au "wapumbavu hawafahamu maarifa"
watu waadilifu
"watu wanaoishi kwa haki"
ni furaha yake
"humfurahisha"
Proverbs 15:9-10
Yahwe huchukia njia ya watu waovu
"Yahwe huchukia namna ambavyo watu waovu huishi"
yule ambaye huandama haki
"mtu ambaye hujitahidi kuishi kwa haki"
yeyote ambaye huiacha njia
"yeyote ambaye huacha kuishi kwa haki"
yeye ambaye huchukia sahihisho
"mtu ambaye huchukia wakati watu wengine wanapomwelekeza"
Proverbs 15:11-12
kuzimu na uharibifu vipo wazi mbele ya Yahwe
"Yahwe anajua kila kitu kuhusu sehemu walipo wafu"
Je ni zaidi mara ngapi kwa mioyo ya wana wa wanadamu?
hii ni nahau kumaanisha "mawazo ya wanadamu"
mioyo ya wana wa wanadamu
"mawazo ya wanadamu"
mwenye dharau huchukia sahihisho
"mwenye dharau huchukia wakati wa kurudiwa"
hatakwenda kwa wenye busara
"hatakwenda kwa wenye busara kutafuta ushauri wao"
Proverbs 15:13-14
moyo wenye furaha huufanya uso kuwa mchangamfu
"mtu anapokuwa na furaha, uso wake ni mchangamfu"
huvunja moyo
" humfanya mtu akate tamaa"
moyo wa mwenye ufahamu
"mtu mwenye ufahamu"
kinywa cha wapumbavu hula upumbavu
"watu wapumbavu hutamani upumbavu kana kwamba ni chakula ambacho wangekula"
Proverbs 15:15-16
siku zote za watu walidhulumiwa ni taabu
"watu waliokandamizwa wanataabu katika siku zao zote"
moyo mchangamfu unasikukuu bila kikomo
"mtu mchangamfu hufurahia maisha, kana kwamba anasherehekea sherehe isiyokuwa na mwisho"
unasikukuu bila kikomo
"sikukuu za daima"
mafadhaiko
"wasiwasi"
Proverbs 15:17-18
mlo wenye mboga
"mlo kidogo" au "chakula kidogo"
ambapo kuna upendo
" ambapo watu wanapendana kila mmoja"
huduma ya ndama aliyenona pamoja na chuki
"kutengewa ndama aliyenona kwa chuki"
ndama aliyenona
"mlo wa gharama' au "sherehe"
kwa chuki
"ambapo watu huchukiana"
huchochea mabishano
"husababisha watu kubishana zaidi"
Proverbs 15:19-20
njia ya mvivu ...njia ya mwadilifu
"maisha ya mvivu...maisha ya mwadilifu"
njia ya mvivu ni kama sehemu yenye uwa wa miiba
"maisha ya mvivu ni kama mtu anayejaribu kutembea kwenye uwa wa miiba"
njia ya mwadili ni njia panda iyojengwa
watu wenye uadilifu hupata baraka katika maisha yao kana kwamba wanatembea juu ya barabara nzuri
njia panda iyojengwa
Hii ni njia pana, tambarare na isiyo na vikwazo
Proverbs 15:21-22
mtu mwenye ufahamu hutembea katika njia iliyonyooka
"mtu mwenye ufahamu hutenda yaliyo sawa"
mipango hubatilika
"mipango hushindikana"
ambapo hapana ushauri
"wakati hakuna mtu wa kutoa ushauri"
washauri
watu ambao hutoa mwongozo wa mapendekezo kwa ajili ya shughuli
hufanikiwa
"mipango hufanikiwa"
Proverbs 15:23-24
jibu la kufaa
"jibu la kutosheleza" au " jibu linalofaa"
jinsi gani ni zuri neno kwa wakati wake
"neno ambalo mtu huongea kwa wakati sahihi ni zuri"
njia ya uzima huelekea juu....kutoka chini kuzimu
Mwandishi anaongelea namna ya kuishi ambayo matokeo yake ni uzima kama njia iendayo juu na namna ya kuishi ambayo matokea yake ni kifo ni kama njia iendayo chini kwenye sehemu ya wafu.
Proverbs 15:25-26
urithi
"nyumba" maana yake ni kaya, mali au utajiri.
maneno yenye upole ni safi
"maneno ya upole ni safi" au "maneno mazuri ni safi"
Proverbs 15:27-28
moyo wa mwenye haki hutafakari kabla ya kujibu
"mtu atendaye mema hutafakari cha kusema kabla ya kujibu"
kinywa cha watu waovu humimina mabaya yake yote
"watu waovu wanasema mambo mabaya daima"
kinywa cha watu waovu humimina mabaya yake yote
"moyo wa mtu mwovu humimina mabaya yake yote" au " vinywa vya watu waovu humwaga maovu yake yote"
Proverbs 15:29-30
Yahwe yupo mbali kutoka kwa watu waovu
"Yahwe awasikilizi watu waovu" au " Yahwe hawajibu watu waovu"
nuru ya macho
"kuonesha hisia za uchangamfu"
huleta furaha kwenye moyo
"mtu mwenye hisia za kuchangamka kwa sababu ya furaha" au "watu hupata furaha wanapomwona mtu mwenye hisia za uchangamfu"
habari njema ni afya kwenye mwili
"kupokea habari njema husababisha mtu ajisikie vizuri"
Proverbs 15:31-32
utabaki miongoni mwa watu wenye busara
1) watu wataendelea kukufikiria kuwa mtu mwenye busara au 2) utaendelea kufurahia ushirika wa watu wenye busara.
Proverbs 15:33
hofu ya Yahwe hufundisha hekima
"mtu anapokuwa na hofu ya Yahwe, hujifunza kuwa na busara"
hofu ya Yahwe
angalia 1:7
unyenyekevu huja kabla ya heshima
mtu lazima kwanza ajifunze unyenyekevu kabla Yahwe hajamheshimu.
Proverbs 16
Proverbs 16:1-2
Mipango ya moyo huwa ni ya mtu
"mtu hufanya mipango katika akili zake"
kwa Yahwe huja jibu kutoka katika ulimi wake
1) Yahwe hunena jibu lake katika mipango ya mtu -maana yake Yahwe hutambua matokeo ya mipango ya mtu au 2) Yahwe huwezesha mtu kunena juu ya mipango aliyoiandaa.
jibu kutoka katika ulimi wake
"jibu ambalo hunena"
Njia zote za mtu ni safi machono pake mwenyewe
mtu hudhani kwamba kila kitu anachofanya ni safi"
Yahwe huipima mioyo
"Yahwe hufanya uamuzi kwenye mawazo ya mtu"
Proverbs 16:3-4
hata waovu kwa ajili ya siku ya taabu
" hata waovu aliwaumba kwa ajili ya siku ya taabu"
Proverbs 16:5-6
kila mmoja mwenye moyo wa kiburi
"kila mtu mwenye kiburi"
hawatakosa kuadhibiwa
"Yahwe atawaadhibu"
kwa agano la uaminifu na mdhamana kosa hulipiwa
"Yahwe hulipa kwa ajili ya uovu kwa agano la uaminifu na mdhamana"
watu hugeuka kutoka katika uovu
"watu huacha kufanya mambo maovu"
Proverbs 16:7-8
huwafanya
"Yahwe hufanya"
pato kubwa
"kujipatia pesa nyingi"
udhalimu
tendo lisilo la haki
Proverbs 16:9-10
kwenye moyo wake mtu hupanga njia yake
"mtu hupanga katika akili jambo atakalofanya"
Yahwe huziongoza hatua zake
Yahwe huamua matokeo ya mipango ya mtu
ushauri upo kwenye midomo ya mfalme
"kila anachosema mfalme ni ushauri"
ushauri
uamuzi kutoka kwa Mungu, hukumu takatifu
katika hukumu kinywa chake hakisemi uongo
"anapotamka hukumu, huwa hasemi uongo"
kinywa chake hakisemi uongo
"husema kweli"
Proverbs 16:11-12
Vipimo vya kweli hutoka kwa Yahwe
Yahwe anataka haki na fadhila wakati wa kufanya biashara. Watu ambao si waadilifu hutumia vipimo vizito au vyepesi katika vipimo vyao ili kupata zaidi wanaponunua au kuuza.
vipimo vyote katika begi ni vya kwake
1) Yahwe tayari amebainisha namna kila kipimo kitakavyo pima 2) Yahwe anahusika kwa kila kipimo abacho mfanyabiashara hutumia.
hicho ni kitu cha kudharauliwa
"hicho ni kitu ambacho watu hukidharau" au "hilo ni jambo ambalo Yahwe hulichukia"
maana kiti cha enzi huthibitishwa kwa kutenda haki
"maana mfalme huthibitisha utawala wake kwa kutenda haki"
Proverbs 16:13-14
midomo ambayo husema haki
"mtu ambaye husema kweli"
ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa kifo
"mfalme mwenye hasira anaweza kuua watu"
Proverbs 16:15-16
Maelezo ya Jumla
mstari wa 15 unapinga na ule wa 14
katika nuru ya uso wa mfalme kuna uzima
"mfalme anapofurahi, watu huishi"
fadhila zake ni kama wingu ambalo huleta mvua ya masika
mfalme anapoonyesha fadhila kwa mtu ni kama wingu ambalo huleta mvua kukuza mazao
Ni bora kiasi gani kujipatia hekima badala ya dhahabu
"Ni bora sana kupata hekima kuliko kupata dhahabu"
yapasa zaidi kuchagua kupata ufahamu kuliko fedha
"Mtu anapaswa kuchagua kupata ufahamu zaidi kuliko kupata fedha"
Proverbs 16:17-18
Njia kuu ya watu waadilifu
"njia ya haki ambayo watu waadilifu huishi "
kuacha uovu
"kuwalinda kutoka katika kutenda mabaya"
moyo wa kiburi
"tabia ya majivuno"
anguko
"maangamizi" au " kushindwa"
Proverbs 16:19-20
nyara
vitu vilivyochukuliwa katika mapigano
walichofundishwa
"walichojifunza"
Proverbs 16:21-22
yule mwenye busara katika moyo wake anaitwa ufahamu
" watu watamwita ufahamu yule mwenye busara katika moyo" au " yule mwenye busara katika moyo atapata heshima ya kuwa mtu mwenye ufahamu"
utamu wa kauli
"kauli ya upole" au "kaui ya kufurahisha"
ufahamu ni chemchemi ya uzima
" ufahamu ni kama chemchemi itiririkayo maji yanayotoa uzima"
Proverbs 16:23-24
moyo wa mtu mwenye busara hutoa
"mawazo ya mtu mwenye busara hutoa"
hutoa utambuzi kwenye kinywa chake
"hufanya kauli yake kuwa ya busara"
kwenye midomo yake
"yale anayosema"
maneno yakupendeza ni sega la asali
"maneno ya kupendeza ni kama sega la asali"
matamu kwenye nafsi
1) inawakilisha hamu na shauku ndani ya mtu "tamu kiasi kiasi cha kutosha kumfanya mtu afurahi" au 2) "tamu kwa radha"
uponyaji kwenye mifupa
"uponyaji katika mwili"
Proverbs 16:25-26
kuna njia ambayo huonekana swa kwa mtu
"mtu hufikiria kwamba namna anavyoishi ni sawa"
lakini mwisho wake ni njia kuelekea kwenye mauti
ni njia kuelekea kwenye kifo
shauku ya mfanyakazi hufanyakazia kwa ajili yake
"mfanyakazi hushughulika kutimiza hamu yake"
njaa yake humhimiza
"huendelea kufanyakazi kwa sababu ya njaa yake"
Proverbs 16:27-28
mtu asiyefaa huchimba madhara
"mtu asiyefaa hutafuta madhara kana kwamba anachimba kitu chini ya ardhi"
asiyefaa
"mwovu"
madhara
"ubaya" au "taabu"
kauli yake ni kama moto unaounguza
"huumiza watu kwa maneno yake, kama moto unaounguza vitu"
mmbeya
mtu ambaye husema uzushi au husambaza uvumi
Proverbs 16:29-30
mtu mwenye jeuri hulala kwa jirani yake
"mtu mwenye jeuri humshawishi jirani yake"
mtu mwenye jeuri
"mtu jeuri" au "mtu ambaye hutenda vurugu"
humwogoza katika njia isiyo nzuri
"humsababisha kufanya mambo yasiyo mazuri"
njia isiyo nzuri
"njia mbaya sana"
yule ambaye hukonyeza jicho lake...wale ambao hudhibiti midomo
angalia 10:10
wataleta maovu
"atafanya mambo mabaya"
Proverbs 16:31-32
mvi ni taji ya utukufu
"mtu aliyeishi muda mrefu wa kutosha kupta mvi ni kama yule anayevaa taji kichwani pake"
ni faida
"mtu hupata faida"
anayetawala roho yake
"yule anayetawala hasira yake"
Proverbs 16:33
kura hurushwa kwenye mikunjo
"mtu hurusha kura kwenye mkunjo wake"
uamuzi hutoka kwa Yahwe
Yahwe huamua namna kuanguka kura au si kura lakini Yahwe ambaye huamua nini kitokee.
Proverbs 17
Proverbs 17:1-2
kuwa na utulivu
Hapa "utulivu" unawakilisha "amani" "kuwa na amani"
kuliko nyumba iliyojaa sherehe pamoja na ugomvi
"kuliko kuwa katika nyumba iliyojaa sherehe ambayo inaugomvi"
Proverbs 17:3-4
Kalibuni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu
"karibuni hutumika kusafisha fedha na tanuru hutumika kusafisha dhahabu"
Yahwe husafisha mioyo
Yahwe huwajaribu watu ili kuwasaidia kuacha ubaya na upumbavu...hivyo Yahwe husafisha kuondoa kila kitu ambacho si safi. "Yahwe huijaribu mioyo ya watu"
mioyo
...mawazo na hamu za watu
midomo miovu
"mtu mwovu" au "maongezi mabaya"
hutega sikio
"husikiliza"
ulimi wa uharibifu
"mtu mharibifu" au "maongezi ya uharibifu"
Proverbs 17:5-6
maskini
"wale ambao ni maskini"
Muumba wake
" yule ambaye alimuumba"
kwa bahati mbaya
"kwa taabu za watu wengine"
ni taji ya
"huleta heshima na taadhima kwa"
wazee
" wale ambao ni vikongwe" au "watu wenye umri mkubwa"
Proverbs 17:7-8
kauli ya kushawishi
"kauli nzuri"au "kauli nzuri"
midomo ya uongo haifai kabisa kwa mkuu
"Haifai kabisa kwa mkuu kudanganya"
hongo ni kama jiwe la miujiza kwa yule atoaye
"hongo hufanyakazi kama jiwe la miujiza kwa yule anayeitoa" au "hongo hufanya kazi kama jiwe la miujiza kwa yule anayetoa rushwa"
kila anapogeuka
" kwa kila anachofanya" au "kila anachojaribu kufanya kwa kutoa hongo"
Proverbs 17:9-10
kosa
jambo ambalo huumiza au humkasirisha mtu
ambaye hurudia jambo
"ambaye hurudia kosa la nyuma"
huondoa
"hutenganisha"
karipio huenda ndani ya mtu ...kuliko mapigo yaendayo ndani ya mpumbavu
"karipio utendaji mwingi kwa mtu... kuliko mapigo mia kwa mpumbavu"
mtu mwenye ufahamu
"mtu anayefahamu"
mapigo mia kwenda
"mamia ya mapigo kwenda"
Proverbs 17:11-12
hutafuta uasi
hutafuta kuasi
mjumbe katili atatumwa dhidi yake
"mjume katili atakuja dhidi yake"
atatumwa dhidi yake
"atatumwa kwenda kumdhuru"
dubu aliyeibiwa watoto wake
"dubu ambaye aliyepoteza watoto wake"
katika upumbavu wake
"ambaye hufanya upumbavu"
Proverbs 17:13-14
ubaya hautaondoka katika nyumba yake
"mambo mabaya hayatakoma kutokea kwake na familia yake"
mwanzo wa faraka ni kama mtu ambaye humwaga maji kila mahali
"kuanzisha ugomvi ni kama kusukuma maji na na kuruhusu yaende kila mahali"
kupasuka
"kuanza"
Proverbs 17:15-16
Yule ambaye humwacha huru mtu mwovu na mtu ambaye humlaumu mtu mwenye haki
" Yule ambaye huwaacha huru watu waovu na yule ambaye huwalaumu mwenye haki"
humwacha huru
halalisha, tangaza mtu kuwa hana hatia
kwa nini mpumbavu yapasa alipe pesa kujifunza juu ya hekima, wakati hana uwezo wa kujifunza juu yake?
"mpumbavu hapaswi kulipa pesa kujifunza juu ya hekima kwa sababu hana uwezo kujifunza juu yake"
Proverbs 17:17-18
ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa taabu
"ndugu yupo kwa ajili ya wakati wa taabu"
akili
"maamuzi ambayo si mazuri"
ahadi za lazima
ahadi ambazo ni lazima zitimizwe na mara nyingi ni mzigo kwa yule anayefanya ahadi hii
Proverbs 17:19-20
husababisha mifupa kuvunjika
"husababisha mtu kusafiri na kujiumiza mwenyewe"
mwenye moyo mdanganyifu
"ambaye ni mdanganyifu" au "asiye mwaminifu"
mwenye ulimi wa ukaidi
" hunena kwa ukaidi" au "hunena uovu"
huanguka katika msiba
"atapatwa na msiba"
Proverbs 17:21-22
moyo mchangamfu ni dawa njema
"moyo mchangamfu ni kama dawa ambayo hukufanya ujisikie vizuri zaidi"
hukausha mifupa
"humfanya mtu awe dhaifu na kukosa afya"
Proverbs 17:23-24
kwa kupotosha njia za haki
"kwa kuzuia kufanyika kwa haki" au "kwa kuzuia haki"
huelekeza uso wake kwenye hekima
"hutenda kwa busara"
macho ya mpumbavu ni
"mpumbavu ni"
mwisho wa dunia
" hutaza mambo yasiyowezekana"
Proverbs 17:25-26
mwana mpumbavu ni huzuni kwa baba yake
"mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake"
mwana mpumbavu ...na uchungu kwa mwanamke
mwana mpumbavu...huleta uchungu kwa mwanamke
aliyemzaa
"mzazi wake"
uchungu
hisia za maumivu, huzunu
si vema ..wala si vizuri
"siku zote ni vibaya... na ni uovu"
mtu mwenye haki
"mtu asiyekuwa na hatia,"
kuwachapa
charaza vikali
wenye uadilifu
"ambao ni waaminifu"
Proverbs 17:27-28
hutumia maneno machache
"husema maneno machache"
hata mpumbavu hufikiriwa kuwa mwenye busara
"watu hudhani hata mpumbavu ni mwenye busara"
hufunga kinywa chake
"haongei"
hudhaniwa kuwa ni mwenye akili
"watu humdhania kuwa ni mwenye akili"
Proverbs 18
Proverbs 18:1-2
ajitengaye
"kaa mbali na watu wengine"
hupingana na maamuzi yote yaliyosahihi
" huyakataa maamuzi yote yaliyosahihi"
maamuzi sahihi
"maamuzi mema" au "uchaguzi sahihi"
mpumbavu hapati raha katika ufahamu,
mpumbavu huchukui ufahamu na ufurahia katika"
lakini kwa kufunua kilichopo katika moyo wake mwenyewe tu
"lakini kwa kuwaambia wengine kile kilichopo katika moyo wake mwenyewe"
Proverbs 18:3-4
Dharau huja pamoja naye-sambamba na aibu na shutuma
"huonyesha dharau kwa watu wengine na husabbisha wajisikie aibu na kushutumiwa"
aibu na shutuma
aibu ambayo ama huwakumba watu wengine au mtu mwovu"
maneno ya kinywa cha mtu ni maji yenye kina;... chemchemi ya hekima ni mkondo utiririkao
"maneno yakinywa cha mwenye hekima ni maji yenye kina...chemchemi ya hekima mkondo utiririkao"
maneno ya kinywa cha mtu ni maji yenye kina
"maneno ya kinywa cha mtu ni ya maana sana kama maji yenye kina"
maneno ya kinywa
maneno ya mtu
chemchemi ya hekima ni mkondo utiririkao
"chanzo cha hekima ni tele kama maji ya chemchemi ibubujikayo"
Proverbs 18:5-6
si vema kwa...kwa mtu mwenye haki
"Ni vema kumtendea mtu mwovu kama anavyositahili, na kutenda haki kwa mtu mwenye haki"
midomo ya mpumbavu huleta
"anasema mtu mpumbavu huleata"
huleta
"husababisha"
kinywa chake hukaribisha mapigo
"kinywa chake husababisha watu kutaka kupiga"
kinywa chake
"maneno yake anayosema"
Proverbs 18:7-8
kinywa cha mpumbavu ...kwa midomo yake
"ambacho mpumbavu hunena... kwa kile asemacho"
ni uharibifu wake
"ataangamizwa"
hujitega mwenyewe
"atasababisha matatizo kwa ajili yake mwenye"
maneno ya umbeya ni kama chembe mtamu
maneno ya udaku yanafurahisha kusikiliza"
maneno ya umbeya
"maneno ambayo mtu mbeya huongea"
chembe
"vipande vidogo vya chakula"
huzama katika sehemu za ndani ya mwili
"huingia katika akili ya mtu na kuathiri mawazo yake"
Proverbs 18:9-10
mvivu katika kazi yake ni ndugu yake aliye mharibifu
" anafanana na"
mvivu
"mzembe"
aliye mharibifu zaidi
" mwenye kuharibu kila kitu" au "mwenye uharibifu daima"
jina la Yahwe ni mnara imara
"Yahwe hulinda kama mnara imara" au "Yahwe huwalinda watu wake kama mnara ambao ni imara"
jina la Yahwe
"Yahwe"
wenye haki
"wale ambao hutenda mema" au "watu waadilifu"
huikimbilia na kuwa salama
"hukimbilia kwake na wapo salama" au "wanamtafuta na wapo salama"
Proverbs 18:11-12
mali ya tajiri ni mji wake wenye ulinzi
"mtu tajiri hutegemea mali yake kama mji unavyotegema ukuta wake"
tajiri
"mtu tajiri"
mji wake wenye ulinzi
mji wenye ulinzi imara kama ukuta na mnara
katika mawazo yake ni kama ukuta mrefu
"hudhani utampatia ulinzi kama ukuta mrefu"
kabla ya anguko lake moyo wa mtu hujivuna
"kwanza moyo wa mtu hujivuna, lakini baadaye huja anguko lake"
anguko
hushuka kwa heshima ya mtu au afya
moyo wa mtu
mawazo na hisia za mtu
unyenyekevu huja kabla ya heshima
"mtu lazima awe mnyenyekevu kabla ya kuweza kuheshimiwa"
Proverbs 18:13-14
ni upumbavu wake na aibu
"ni upumbavu wake na anapaswa kupata aibu"
roho ya mtu itapona ugonjwa
"mtu mwenye matumaini atapona ujonjwa" au "kama mtu amejaa matumaini ndani yake, ataondokana na ugonjwa"
lakini moyo ulivunjika ni nani anaweza kuusitahimili?
"lakini ni vigumu kusitahimili moyo uliovunjiaka"
moyo uliovunjiaka
kuhuzunika, kuwa na mahuzuniko
Proverbs 18:15-16
moyo wa mwenye busara hupata
"mwenye busara hutamani kupata"
mwenye busara
"wale wenye busara" au "watu wenye busara"
hupata
"ongeza" au "jipatia"
kusikia kwa mwenye busara hutafua
"mwenye busara huitafuta kujifunza juu ya"
mwenye busara
"watu wenye busara"
huitafuta
hutafuta kujifunza juu ya "maarifa"
huweza kufungua njia
"kutengeneza fursa kwa ajili yake"
humleta mbele
"humwezesha kutambulishwa kwa"
Proverbs 18:17-18
kwanza
"mtu wa kwanza"
kupiga kura
kuchagua
na kutenganisha washindani imara
"na husababisha washindani kuacha kupigana juu ya ugomvi wao"
Proverbs 18:19-20
ndungu aliyekosewa ni mugumu kushindwa kuliko mji imara
"kama utamkosea ndugu yako, kutafuta namna ya kupatana naye tena inaweza kuwa vigumu kuliko kupigana kuuteka mji"
ugomvi ni kama makomeo ya ngome
kusulihisha ugomvi ni vigumu kama kuvunja makomeo ya ngome"
ngome
kasri lililozungushiwa uigo/ukuta
tumbo la mtu hujazwa kutokana na matunda ya kinywa chake; kwa mavuno ya midomo yake huridhishwa
" mtu hutoshelezwa kwa matokeo ya mazuri ya mambo anayonena"
matunda ya kinywa chake
"maneno yake mazuri"
tumbo la mtu hujazwa
"mtu hutoshelezwa"
kwa mavuno ya midomo yake
"maneno yake mazuri"
huridhishwa
"hufurahishwa"
Proverbs 18:21-22
mauti na uzima hutawaliwa kwa ulimi
"ulimi unaweza kuongoza kwenda kwenye uzima au mauti" au "maneno ya watu wanayonena yanaweza kuwaongoza kwenda kwenye uzima au mauti"
kwa ulimi... kupenda ulimi
"kwa maneno ambayo watu huongea ...kupenda kuongea"
watakula matunda yake
"atapokea madhara yake"
Proverbs 18:23-24
marafiki wengi humleta kwenye uharibifu
"marafiki wengi watamharibu"
huja karibu sana kuliko
"mwaminifu kuliko" au "huwa mwema zaidi"
Proverbs 19
Proverbs 19:1-2
bora mtu maskini
"ni bora kuwa mtu maskini"
ambaye hutembea katika uadilifu wake
"ambaye huishi katika uadiifu" au "ambaye huishi kwa uaminifu"
ni mpotofu katika kauli
"huongea kwa kupotosha" au "huongea kwa namna mbaya"
kuwa na hamasa bila maarifa
"kufanya kazi kwa bidii bila kujua unachokifanya"
ambaye hukimbia haraka sana hukosea njia
"ambaye hutenda kwa haraka hufanya makosa" au " ambaye hufanya haraka hufanya maamuzi dhaifu"
Proverbs 19:3-4
moyo wake hukasirika
moyo unawakilisha hisia zake " hughadhabika"
utajiri huongeza marafiki wengi
"wale wenye ukwasi hupata marafiki wengi kwa urahisi"
mtu maskini hutengwa na marafiki zake
"umaskini husababisha mtu kupoteza marafiki zake"
Proverbs 19:5-6
shahidi wa uongo hatakosa kuadhibiwa
"hakika watamwadhibu shahidi wa uongo"
yeye ambaye hunong'ona uongo hataokoka
"watamkamata mtu yule ambaye hunong'ona uongo"
mtu mkarimi
mtu ambaye mara nyingi hutoa vitu
kila mtu ni rafiki
"huonekana kwamba kila mtu ni rafiki" au "karibia kila mtu ni rafiki"
Proverbs 19:7-8
jinsi gani rafiki zake huzidi kwenda mbali naye!
"kwa hiyo marafiki zake watamchukia na kujitenga naye"
huyapenda maisha yake mwenyewe
"hujipenda mwenyewe"
ahikaye ufahamu
"mwenye ufahamu"
Proverbs 19:9-10
shahidi wa uongo hatakosa kuadhibiwa
"hakika watamwadhibu shahidi wa uongo"
hunong'ona uongo
"hudanyanya daima"
haifai
"siyo sawa"
anasa
hali ya ukwasi na furaha
sembuse kwa mtumwa
"haifai zaidi kwa mtumwa" au "ni vibaya zaidi kwa mtumwa"
Proverbs 19:11-12
Busara humfanya mtu awe mpole
" mtu mwenye busara ni si mwepesi wa hasira"
Busara
angalia 1:4
ni utukufu wake kusamehe
"itakuwa utukufu kwake kusamehe" au "wengine dhani kuwa ni heshima kama atasamehe"
kusamehe
kusahau jambo kwa lengo
ghadhabu ya mfalme ni kama ngurmo ya simba kijana
" ghadhabu ya mfalme ni hatari kama shambulizi la simba kijana"
lakini fadhila yake ni kama umande juu ya majani
"lakini fadhila yake inaburudisha kama umande juu ya majani" au "fadhila yake inaburudisha kama umande juu ya ardhi wakati wa asubuhi"
Proverbs 19:13-14
ni uharibifu kwa baba yake
"atafanya uharibifu kwa baba yake"
mke mgomvi ni maji ya kutona tona daima
"mke mgomvi anakera na kufadhaisha kama maji yenye kuvuja daima"
mke mgomvi
"mke mbishi" au " mke asiye na makubaliano"
Nyumba na ukwasi ni urithi kutoka kwa wazazi
"watoto hurithi nyumba na mali kutoka kwa wazazi"
busara
angalia 12:23
mke mwenye busara anatoka kwa Yahwe
"Yahwe hutoa mke mwenye busara"
Proverbs 19:15-16
uvivu humtupa mtu kwenye usingizi mzito
""uvivu humfanya mtu alale sana" au " mtu mvivu hulala sana"
kwenda njaa
"kuwa na njaa"
amri
"amri ambayo alifundishwa"
hulinda maisha yake
"huyatunza maisha yake"
njia zake
"namna anavyoishi "
Proverbs 19:17-18
yeye ambaye ni mkarimu kwa maskini humkopesha Yahwe
"mtu ambaye hutoa kwa maskini hutoa kwa Yahwe"
maskini
"watu fukara au watu maskini"
wakati kuna matumaini
"wakati bado ni mdogo" au "wakati bado anaweza kufundishwa"
na wala usitamani kumwua
""lakini usimwadhibu sana atakufa" au " kama hutamwadhibu utamwangamiza"
usitamani
"kusudia kumweka"
Proverbs 19:19-20
mtu mwenye hasira
"mtu ambaye hupata hasira upesi"
lazima alipe malipo ya kosa
" lazima apate madhara ya hasira yake" au "lazima abebe matokeo ya matendo yake wakati wa hasira"
kama utamwokoa
" kama utamaidia baada ya kupata hasira yake ya ghafla"
mara ya pili
"mara mbili" au "tena"
sikiliza ushauri na ukubali maelekezo
haya ni maneno ya kusisitiza umuhimu.
sikiliza
"zingatia ushauri"
Proverbs 19:21-22
katika moyo wa mtu
"katika akili ya mtu" au "hamasa ya mtu"
kusudi la Yahwe
"mipango ya Yahwe" au "kusudi la Yahwe"
hilo litasimama
Hii ni nahau maanya yake " hilo litatokea"
Proverbs 19:23-24
Kumheshimu Yahwe huleta uzima kwa watu; kila mmoja wenye nayo atatosheka
"ambao wanamheshimu Yahwe wataishi muda mrefu; mwenye kumheshimu Yahwe atatoshelezwa"
kila mmoja mwenye
"kila anayemheshimu Yahwe"
ametosheka na hana madhara
"atatosheka; atakuwa salama"
mvivu
angalia 10:26
huzika mkono wake katika sinia
"huzamisha mkono wake kwenye sinia" au "huweka mkono wake kwenye sahani". katika utamaduni wa Biblia watu walitumia mikono kula kama watu wengine wanavyofanya hata leo
hataurudisha tena juu kwenye kinywa chake
" lakini ni mvivu kuuleta mkono kwenye kinywa ili kula mwenyewe"
Proverbs 19:25
mpige mwenye dhihaka, na mtu mjinga
"ukimpiga mwenye dhihaka, mtu mjinga"
mpige
"wadhibu"
mtu mjinga
mtu asiye na uzoefu, au "mtu ambaye bado mchanga"
busara
agalia 12:23
mwadibishe mwenye ufahamu, na
"kama utamwadibisha yule mwenye ufahmu"
atapata maarifa
"atajua zaidi"
Proverbs 19:26-27
huleta aibu na fedheha
"huleta aibu na fedheha kwake mwenyewe" au "huleta kwenye familia yake mwenyewe"
kama utaacha kusikiliza maelekezo
"kama utaacha kuzingatia maelekezo" au "kama utaacha kutii maelekezo"
utapotea
"utaacha" au " au utageuka nyuma"
maneno ya maarifa
"maarifa"
Proverbs 19:28-29
kinywa cha waovu humeza makosa
"waovu hufurahia kutenda uovu kama wanavyofurahia kula chakula"
kinywa cha waovu humeza makosa
watu waovu wanawakilishwa na "kinywa"
waovu
"watu waovu"
hukumu ipo tayari kwa ajili ya wenye dhuhaka na mapigo kwa ajili
"Yahwe yupo tayari kuwahukumu wenye dhihaka na kuwapiga"
mapigo kwa ajili ya migongo
"mapigo yapo tayari kwa ajili ya migongo"au " yupo tayari kuipiga migongo yao"
mapigo
kuchapa kwa kutumia fimbo au mjeredi
Proverbs 20
Proverbs 20:1-2
mvinyo ni dhihaka na kileo ni mgomvi
Hapa inaeleza juu ya hatari ya kunywa pombe nyingi
mvinyo ni dhihaka
"mtu ambaye hulewa kwa mvinyo hudhihaki"
kileo ni mgomvi
"mtu ambaye hulewa kwa kileo huanzisha mapinga"
mgomvi
mtu ambaye hupigan kwa makelele, hasa katika sehemu za watu wengi
yeyote ambaye hupotea kwa kunywa hana busara
"anayekunywa hadi kushindwa kufikiri vizuri "
kwa kunywa
"kunywa" hapa inamaanisha kunywa pombe
hana busara
"ni mpumbavu"
kumwogopa mfalme ni kama kumwogopa simba kijana anayeunguruma
ghadhabu ya mfalme hufanya watu waogope kama vile wanakabiliana na simba kijana mwenye kuunguruma"
mwenye kumkasirisha
"kumfanya mfalme akasirike"
hufidia uhai wake
"atakufa"
Proverbs 20:3-4
ni heshima
"maana yake mtu huyu ataheshimiwa"
kila mpumbavu hurukia kwenye mabishano
"kila mpumbavu huingia kwenye mabishano kwa haraka" au " kila mpumbavu ni mwepesi kujiunga kwenye mabishano"
kulima
kuandaa shamba kwa ajili ya kupanda
wakati wa kupanda
majira ya kupanda
lakini hatapata kitu
"hatapata kitu cha kuvuna"
Proverbs 20:5-6
kusudio la moyo wa mwanadamu ni kama maji yenye kina
"Ni vigumu kufahamu kusudi katika moyo wa mwanadamu ni kama kufika kwenye kilindi cha kisima" au " kusudi la moyo wa mwanadamu ni vigumu kulifahamu"
mtu mwenye ufahamu
"mtu yule mwenye ufahamu"
atayateka
"atasababisha kusudi kujulikana" au "atalichungu za"
mwaminifu
"mwenye kuaminika"
lakini ni nani anaweza kumpata mtu ambaye ni mwaminifu?
" lakini watu wachache wanaweza mtu ambaye ni mwaminifu" au "lakini ni vigumu kupata mtu ambaye ni mwaminifu kweli "
Proverbs 20:7-8
hutembea katika uadilifu
"huishi kwa uadilifu wake" au " huishi kwa uamninifu"
mwana wake watafuata baada yake
"mwana wake baada yake"
hupepeta kwa macho yake mabaya yote ambayo yapo mbele yake
"huona na kuchambua maovu ya namna mbalimbali ambayo huletwa mbele yake"
Proverbs 20:9-10
nani anaweza kusema, " moyo wangu nimeuweka safi; nipo huru kutokana na dhambi zangu"?
"hakuna mtu anaweza kusema kwamba moyo wake ni safi na yupo huru kutoka dhambini"
moyo wangu
"mimi mwenyewe"
safi
mtu ambaye Mungu humtafakari kuwa anakubalika kiroho.
nipo huru kutokana na dhambi zangu
"sina dhambi" au "sijatenda dhambi"
Proverbs 20:11-12
hata kijana anajulikana kwa matendo yake
"watu wanamjua kijana kwa matendo yake"
mwenendo wake
"matendo yake" au "kwa yale anayotenda"
safi na adili
maneno haya yana maana moja, yanahimiza jinsi kijana alivyo mwema "safi"
masikio ambayo husikia na macho ambayo huona
maana yake ni kwamba Yahwe aliumba milango yetu yote ya fahamu.
Proverbs 20:13-14
huwa maskini
"anakuwa maskini"
fumbua macho yako
"uwe tayari" au "uwe macho"
"Mbaya! Mbaya!" anasema mnunuzi, lakini akiondoka hujisifu
"Mbaya! Mbaya!" anasema mnunuzi kumkosoa muuzaji, lakini baada ya kununua anakwenda zake akijisifu kuhusu bei ndogo aliyolipa"
Proverbs 20:15-16
midomo ya maarifa ni marijani ya thamani
"midomo yenye maarifa inathamani kama marijani ya gharama sana"
midomo ya maarifa
"maneno yenye busara" au "maneno ya maarifa"
chukua vazi lake yeye ambaye ameliweka dhamana kwa ajili ya mgeni
"chukua vazi kama dhamana kutoka kwa mdhamini wa mgeni ambaye ameahidi kulipa kwa kitu achoazima mgeni"
ameliweka dhamana
"dhamini kuwa kilichoazimwa kitarudishwa" au "ahidi kulipa deni"
shikilia rehani
" shikilia koti lake kama dhamana ya malipo"
Proverbs 20:17-18
mkate uliopatikana kwa udanganyifu
"mkate ambao mtu ameupta kwa kudanganya"
kwa udanganyifu
"kwa kuwadanganya wengine"
mkate
"chakula"
ladha yake tamu
" ladha yake ni nzuri"
lakini baadaye kinywa chake kitajaa kokoto
"lakini baadaye ladha yake itakuwa kama kokoto katika kinywa chake" au " lakini punde ladha yake ni kama mchanga katika kinywa chake"
kokoto
vipande vidogo vya jiwe
mipango himarishwa kwa ushauri
"watu huimarisha mipango kwa namna ya ushauri"
Proverbs 20:19-20
mbeya
maana yake mtu ambaye husengenya sana.
usishirikiane pamoja na
" hupaswi kuwa na urafiki na"
kama mtu atamlaani
"Maana yake kama mtu ataonyesha shaukua ya mambo mabaya yatokee kwa mtu mwingine"
taa yake itazimwa katikati ya giza
"maisha yake tatakoma ghafla kama mwanga ambao umepulizwa katika giza" au "atakufa ghafla"
taa yake itazimwa
"taa yake itazimika"
taa yake
" mwanga wa taa yake"
zimwa
kusababisha mwanga uondoke
Proverbs 20:21-22
hapo mwanzo
"kabla ya muda"
nitalipiza
"nitakuadhibu"
kumsubiri Yahwe
"kuwa na imani kwa Yahwe" au " kumtumaini Yahwe"
Proverbs 20:23-24
Yahwe huchukia kipimo visivyo sawa na vipimo vya udhalimu si vizuri
tungo zote mbili zinahusika na jambo moja la kuonyesha "ubaya"
hatua za mtu huogozwa na Yahwe
"Yahwe huongoza hatua za mtu"
hatua za mtu
matendo ya mtu
je kwahiyo anaweza kuifahamu njia yake?
"kwa hiyo mtu hawezi kuifahamu njia yake"
kuifahamu njia yake
"kuifahamu kwa nini mambo kadhaa hutokea katika maisha yake"
Proverbs 20:25-26
ni mtego
"ni hatari"
kusema kwa haraka
kusema jambo kwa haraka na bila kufikiri kwa umakini maana yake
kuweka nadhiri
"kuweka wakifu kwa Yahwe" au "kutamka kuwa ni takatifu"
kuwapepeta waovu
"kuwatenga waovu"
waovu
"wale ambao ni waovu" au "watu waovu"
na kuwazungushia gurudumu la kupuria juu yao
"na huwaadhibu vikali"
gurudumu la kupuria
"mkokoteni wa kupuria"
Proverbs 20:27-28
roho ya mtu ni taa ya Yahwe, ikichunguza sehemu zake zote za ndani
"Yahwe anetupatia roho ya kujitambua kwa undani, kama taa inavyokufanya uone katika giza"
agano la uaminifu na dhamana humlinda mfalme
"mfalme hujilinda yeye mwenyewe kwa agano lake la uaminifu na mdhamana"
humlinda mfalme
humweka salama mfalme kutoka katika madhara
kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa upendo
kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa upendo wake
kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa upendo
"mfalme huhakikisha kuwa atatawala kwa muda mrefu kwa kuonyesha upendo kwa wengine"
Proverbs 20:29-30
mapigo ambayo hujeruhi husafisha mabaya na mapigo husafisha sehemu za ndani
"kumpiga aliyefanya kosa kutamsahihisha na kumfanya kuwa mtu mzuri"
Proverbs 21
Proverbs 21:1-2
moyo wa mfalme ni mkondo wa maji katika mkono wa Yahwe
"yahwe hutawala moyo wa mfalme kama mtu anavyoyaongoza maji kwa ajili ya umwagiliaji"
moyo wa mfalme
"mawazo ya mfalme na matendo" au" jinsi mfalme anavyofikiri na ambacho anataka kufanya"
kila njia ya mtu ni sawa katika macho yake mwenyewe
"kila mtu hufikiria kwamba anafanya mema"
ni nani huipima mioyo
"ni nani atayahukumu mawazo"
Proverbs 21:3-4
kutenda haki
"kufanya kila ambacho Yahwe anafikiri kuwa ni haki"
kutenda ...haki
"kuwatendea watu namna Yahwe anavyotaka watu kuwatendea watu wengine"
haki inakubalika zaidi mbele ya Yahwe
"Yahwe anataka zaidi-haki
macho yenye kiburi na moyo wa majivuno
"watu wanaotaka wengine kufikiri kuwa ni bora kuliko watu wengine"
macho yenye kiburi
mtu ambaye anataka watu wengine wafahamu kwamba anafikiri yeye ni bora kuliko wao.
moy wa majivuno
mtu ambaye hufikiri yeye ni bora kuliko wengine
taa ya waovu
"mambo ambayo huwasaidia watu waovu kama taa inavyosaidia kuon kwenye giza"
Proverbs 21:5-6
bidii
"mtu mwenye bidii" au "mtu ambaye hufanya kazi kwa bidii"
huja katika umaskini
"huwa maskini"
kujipatia utajiri
"kupata utajiri "
mvuke upitao upesi
"umende unaotoweka"
na mtego ambao huua
ambao huvutia wanyama kwenye mtego
Proverbs 21:7-8
vurugu ya waovu itawasukimia mbali;
Mungu atawaadhibu watu waovu ambao huwaumiza majirani zao wasio kwa sababu ya matendo ya vurugu wanayofanya
vurugu ya waovu
"matendo ambayo waovu hutenda kwa ajili ya kuwaumiza majirani zao wasiokuwa na hatia"
huwasukumia mbali
"kuwakamata na kuwalazimasha kuonekana mbele za Mungu ili aweze kuwahukumu"
njia ya mtu mwenye hatia ni udanganyifu
"mtu mwenye hatia huishi katika njia ya udanganyifu"
danganyifu
"mbaya"
Proverbs 21:9-10
pembe ya darini
Waisraeli wa kale walitumia muda wao mwingi kwenye dari zao, ambapo ilikuwa baridi zaidi kuliko ndani ya nyumba, na wakati mwingine watu walijenga sehemu ya kutosha kulala katika pembe ya dari
mgomvi
mtu ambaye mara nyingi hubisha au hulalamika
hamu ya waovu ni kutamani ubaya
kutamani
kutamani
"kuwa na hamu kubwa mno"
hakuna huruma machoni pake
"hana huruma" au "ni mchoyo sana"
Proverbs 21:11-12
mwenye dhihaka anapoadhibiwa
" mtu anapomwadhibu mwenye dhihaka"
mjinga
"bila uzoefu, asiye mkomavu, bado na hali ya uchanga"
mwenye dhihaka
"mtu anayewadhihaki wengine"
mwenye busara anapofundishwa
"mtu anapomfundisha mwenye busara"
hushika maarifa
maarifa yanaongelewa kama ni kifaa ambacho mtu kukisha na kuhifadhi kwa ajili yake.
mwenye haki
"mtu wa haki yeyote" au "Yahwe ambaye ni mwenye haki"
huangalia
" tafakari kwa makini"
watu waovu huleta kwenye maangamizi
"huwaangamiza"
Proverbs 21:13-14
azibaye masikio yake kwenye kilio cha maskini
Hii ni nahau "ambaye hatasikiliza wakati watu maskini wanapoomba msaada"
hatajibiwa
"hakuna atakayefanya jambo lolote kwa ajili ya kumsaidia"
hutuliza hasira
"kumfanya mtu mwenye hasira ajisikie vizuri na asiendelee kuwa na hasira tena"
Proverbs 21:15-16
haki inapotendeka
"watawala wanapotenda haki"
huzurura kutoka kwenye njia ya ufahamu
Hii ni nahau "kuacha kuishi kwa busara"
atapumzika katika kusanyiko la wafu
"atabaki katika kusanyiko la roho za wafu"
Proverbs 21:17-18
ni fidia kwa
"fidia"mtu kuchukua nafasi ya mtu mwingine
mdanganyifu
mtu ambaye huwaumiza wale ambao wanamwami kwa kudanganya na kutenda kwa uongo
watu waadilifu
"watu wenye haki" au " watu waaminifu' au "watu watendao haki"
Proverbs 21:19-20
busara
"mtu wa busara"
huyaharibu
"huyatumia yote"
Proverbs 21:21-22
huupima mji
"hupanda juu ya ukuta unaouzunguk mji"
mji wa wenye nguvu
"mji ambao mashujaa wanaishi" au "mji wa mashujaa wenye nguvu"
huuangusha
"huuharibu"
ngome ambayo huitumaini
"kuta na minara kuuzunguka mji ambavyo vilidhaniwa kwamba hakuna mtu angeweza kuvuka kuingia kwenye mji, hivyo walijiona kuwa wapo salama"
Proverbs 21:23-24
yeye mwenye kulinda kinywa chake na ulimi
"yeye ambaye ni mwangalifu katika maneno anayoyasema"
mtu mwenye kiburi na majivuno...hutenda mambo kwa maringo na ufahari
"watu mwenye kiburi na majivuno hutenda mambo kwa marigo na ufahari"
mwenye kiburi na majivuno
maneno haya yana maana moja kumaanisha jinsi mtu alivyo na kiburi
dhihaka ndilo jina lake
"mwenye dhihaka anapaswa kuitwa "dhihaka"
Proverbs 21:25-26
uchu wa mvivu humfisha
"mtu mvivu hutaka kukaa bila kazi, na kwa sababu hiyo atakufa" au mtu mvivu atakufa kwa sababu hataki kufanya kazi"
mkono wake hugoma
"yeye hugoma"
hutamani
"taka kitu kwa hamumno" au "kuwa na uchu sana"
hutoa na wala hazuii
"hutoa kila kitu ambacho anapaswa" au "hutoa kwa ukarimu"
Proverbs 21:27-28
dhabihu ya mwovu ni chukizo
Yahwe huichukia dhabihu ya mwovu.
mwovu
"mtu mwovu" au "watu waovu"
hata ni chukizo zaidi
"Yahwe huichukia zaidi dhabihu"
atasema kwa wakati wote
hii ni kwa sababu watu hawatasahau ambacho amesema
Proverbs 21:29
huufanya uso wake kuwa mgumu
"hujifanya kuwa na ujasiri" au "hatasikiliza kurudiwaiwa"
ni mnyofu katika njia zake
" anauhakika kwamba yale atendayo ni haki kwa sababu huhakikisha ni hakika kabla ya kutenda"
Proverbs 21:30-31
hakuna hekima, hakuna ufahamu, na hakuna ushauri ambao
"Yahwe ni mkuu kuliko kuliko kitu chochote ambacho mtu anakifahamu, anakifikiri au anachosema. "hakuna mwenye busara, ufahamu wa kitu chochote, au mwenye kuwaagiza wengine kufanya jambo furani"
kusimama dhidi ya Yahwe
"kumshinda yahwe" au " kufanya kazi dhidi ya mapenzi ya Yahwe" au " kuonesha kwamba anahaki na Yahwe amekosea"
farasi hutayarishwa kwa ajili ya siku ya mapigano
"wanajeshi huandaa farasi kwa ajili ya siku ya mapigano"
siku ya mapigano
"wakati kuna mapigano"
Proverbs 22
Proverbs 22:1-2
jina jema huchaguliwa dhidi ya utajiri mwingi
"mtu anapaswa kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi"
jina jema
"wetu wengine waone ya kuwa ni mtu mwema"
hufanana kwa hili
"wanafanana kwa namna moja" au "wanafanana kwa hili"
Proverbs 22:3-4
mtu mwenye busara
"mtu ambaye ni mwenye busara" au "mtu mwenye akili njema" angali 12:15
mjinga
"bila uzoefu, asiye mkomavu, bado na hali ya uchanga"
Proverbs 22:5-6
miiba na mitego huwa katika njia ya mkaidi
wakaidi watapata taabu kwa sababu ya "miiba" ya asili na "mitego" ya kutengenezwa na wanadamu.
mitego
mitambo ya kunasa wanyama
mkaidi
"watu wakaidi"
mwenye kuyalinda maisha yake
"watu ambao wanataka kuishi kwa muda mrefu"
njia anayopaswa kuifuata
"namna ya kuishi"
Proverbs 22:7-8
kopa ...kopesha
"kopa pesa ...kopesha pesa"
yeye anayepanda udhalimu atavuma taabu
"kama mtu atawatendea kwa udhalimu watu ambao wanauwezo mdogo kuliko yeye, baadaye watamsababishia taabu".
fimbo ya ghadhabu yake itanyauka
1) mtawala dhalimu atapoteza mamlaka yake ambayo aliyatumia kwa kutenda udhalimu kwa watu. 2)watu watajibu dhidi ya udhalimu wake aliotumia kuwaumiza, na hatakuwa na nguvu ya kuwazuia. "hatakuwa na mamlaka aliyoyatumia kuwaumiza watu"
itanyauka
...miti inapokauka
Proverbs 22:9-10
mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa
"Mungu atambariki mwenye jicho la ukarimu"
mwenye jicho la ukarimu
"mtu mkarimu" au "mtu ambaye yupo tayari kutoa vitu kwa ajili ya watu wengine"
mkate
Mkate ulikuwa chakula kikuu kwa watu wengi nyakati za Biblia, mara nyingi ulitumika kuwakilisha chakila kwa ujumla.
mabishano na matukano vitaondoka
"watu hawatabishana tena au kusema vitu vya kuumizana"
Proverbs 22:11-12
apendaye usafi wa moyo
" kupenda kuwa na moyo safi" au "kutaka kuwa safi"
huruma
"mpole"
macho ya Yahwe hutazama
"Yahwe huyalinda maarifa"
hutazama maarifa
"huyalinda maarifa"
huyapindua
"huyaharibu"
udanganyifu
"mtu mdanganyifu"
Proverbs 22:13-14
mtu mvivu husema
"hutoa visingizio ili asifanye kazi"
kinywa cha malaya ni shimo refu
"maneno yasemwayo na malaya yatakuvuta, na utakuwa kama umeangukia kwenye refu na hatari"
malaya
Angalia 5:3
hasira ya Yahwe huchochewa
"Yahwe hukasirika"
hudumbukia ndani yake
"hufanya dhambi kwa sababu ya malaya"
Proverbs 22:15-16
upumbavu umefungwa katika moyo wa mtoto
"moyo wa mtoto umejaa mambo ya kipumbavu"
fimbo ya adabu
mzazi kutumia namna yoyote ili kuadibisha kama vile kumchapa mtoto kwa fimbo.
huondoa
"itamfanya mtoto kuwa na busara"
kuongeza utajiri wake
"kuwa tajiri" au " kupata pesa zaidi"
kuwapa watu matajiri
"kuwapa pesa watu matajiri"
atakuwa maskini
Nahau "atakuwa maskini"
Proverbs 22:17-19
Maelezo ya Jumla
Mstari wa 17 unaanza utangulizi wa sehemu mpya ya kitabu cha Mithali
tega sikio lako na usikilize
"sikiliza kwa umakini"
maneno ya busara
"ambayo watu wenye hekima husema"
tumia moyo wako kwa
"fanya bidii kufahamu na kukumbuka"
maarifa yangu
"maarifa niliyonayo, ambayo ninakupatia"
yote yapo tayari kwenye midomo yako
"unaweza kuyaongea muda wowote"
wewe leo
msemaji anasisitiza kuwa maneno haya nanamhusu msikilizaji wala si mtu mwingine
Proverbs 22:20-21
Maelezo ya Jumla
Mistari hii inaendelea na kukamilisha utangulizi ulianza katika mstari wa 22:17
je sikuandika kwa ajili yako ...wewe?
"unapaswa kufahamu kuwa nimeandika kwa ajili ...yako"
misemo thelathini
katika tafasiri zingine inasomeka "misemo yenye ubora"
kwa wale waliokutuma
maana yake msikilizaji ni mtu ambaye ametumwa na watu kupata habari ya mafundisho na kuwarudishia majibu.
Proverbs 22:22-23
Maelezo ya Jumla
mistari hii inaanza kueleza juu ya "misemo themathini " 22:20
usimwibie ...kumponda
nyanganya ...dhulumu
maskini
"mtu yeyote ambaye ni maskini" au "watu maskini"
kumponda
saga kuwa unga, maana yake kufanyia dhuluma
mhitaji
'mtu ambaye hana mahitaji kwa ajili ya kuishi"
kwenye lango
sehemu ambapo watu walileta vitu na kuuza na kuamuliwa mambo mbalimbali.
Yahwe atatetea shitaka lao
"Yahwe atawatetea wahitaji kutoka kwa wale wanaowaonea" au ""Yahwea atahakikisha kuwa wahitaji wanapokea haki"
atapokonya uhai wao wale ambao waliwaibia
"atawaangamiza wale ambao wakandamiza watu maskini"
Proverbs 22:24-25
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
mtu ambaye hutawaliwa na hasira
"mtu asiyeweza kutawala hasira yake"
ghadhabu
kuonesha nguvu nyingi kwa hasira
utakuwa chambo kwa ajili ya nafsi yako
"utakuwa kama mnyama alaye chambo na mtego hujifunga na hujindwa kujiokoa"
chambo kwa ajili ya nafsi yako
"chambo ni kitu ambacho mtu amekiweka ili aweze kukuangamiza"
Proverbs 22:26-27
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
wapigao mikono
ni kitendo cha kushikana mikono na kuweka agano la makubaliano. Wandishi anaonya juu ya kuweka ahadi ya kulipa deni la mtu.
katika kufanya reheni
"kukubali kulipa kitu ambacho mtu mwingine anadaiwa"
Proverbs 22:28-29
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
kale
ya zamani sana
jiwe la mpaka
jiwe kubwa ambalo linaonesha ardhi ya mtu mwingine inapokomea na mwanzo wa ardhi ya mtu
baba
wahenga
je unamwona mtu mwenye ujuzi katika kazi yake?
"fikiri juu ya mtu unayemfahamu mwenye ujuzi katika kazi yake"
simama mbele
huwa ni mtumishi wa wafalme na watu wengine wenye vyeo watamtazama kuwa wenye hadhi ya juu na kuhitaji uduma yake.
Proverbs 23
Proverbs 23:1-3
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
weka kisu kooni mwako
1) "uwe mwangalifu usile sana" au 2) "usile kitu chochote kabisa"
usitamani
"usishikwe na hamu sana kupitiliza" angalia 21:9
vyakula vizuri
"chakula maalumu na vya gharama"
ni vyakula vya hila
Hii ni nahau "anakupa chakula ili aweze kukudanganya"
Proverbs 23:4-5
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
usifanye kazi kwa nguvu sana
"usifanye kazi sana kiasi kwamba uwe na uchovu kila siku"
yatamulika juu yake
....kuutamaza utajiri kwa kipindi kifupi
hakika utajiri utajitwalia mabawa kama tai na kuruka juu
"utajiri utapotea kwa haraka kama vile tai anavyoweza kuruka"
mabawa kama tai
mabawa kama mabawa ya tai
Proverbs 23:6-8
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
mwenye jicho ovu
1) asiyependa kutoa vitu kwa watu wengine au 2) mtu mwovu
usitamani
"usishikwe na hamu sana kupitiliza" angalia 21:9
vyakula vizuri
"chakula maalumu na vya gharama" angalia 23:1
moyo wake haupo pamoja nawe
Hii ni nahau " Kwa uhalisia hataki ufurahie huo mlo"
utatapiki kile chakula kidogo ulichokula
"utatamani kwamba usingekula kitu chochote"
utakuwa umeharibu sifa zako
"hataweza kufurahi hata kama utasema maneno mazuri juu yake na chakula"
Proverbs 23:9-11
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
katika masikio ya mpumbavu
"ambapo mpumbavu anaweza kukusikia"
Kale
ya zamani sana
jiwe la mpaka
jiwe kubwa ambalo linaonesha ardhi ya mtu mwingine inapokomea na mwanzo wa ardhi ya mtu mwingine. angalia 22:28
nyang'anya
Maana yake kuanza kutumia ardhi ( au kitu) ambacho ni cha mtu mwingine
yatima
watoto ambao wamefiwa na wazazi
mkombozi wao
Yahwe
atatetea shitaka lao dhidi yako
"atawalinda yatima dhidi yako" au "atahakikisha kuwa yatima wanapokea haki na wewe anakuadhibu"
Proverbs 23:12
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
tumia moyo wako kwa
Hii ni nahau "fanya bidii kufahamu na kukumbuka" pia angalia 22:17
mafundisho
1) "mambo ambayo watu wanakuambia ni mema na yale mabaya" au 2) "vile watu wanakuambia wanapokusahihisha"
na masikio yako
"tumia masikio yako" au "sikiliza kwa makini"
kwenye maneno ya maarifa
"mimi ninapokuambia ambacho nakijua"
Proverbs 23:13-14
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
usimnyime mtoto mafundisho
"usipuuze kumfundisha mtoto" au "usikatae kumfundisha mtoto"
usimnyime
kataa kutoa kitu ambacho unajua mtu mwingine anakihitajia
fimbo
"kipande cha mti"
ni wewe unayepaswa kumchapa ... na kuokoa nafsi yake
"wewe ndiye unayepaswa kumchapa...na kuokoa nafsi yake." hakuna mtu mwingine wa kufanya hivyo.
na kuokoa nafsi yake kutoka kuzimu
"na utamlinda na ulimwengu wa wafu" au " utamlinda dhidi ya kifo"
Proverbs 23:15-16
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
midomo yako inenapo
"wakati usemapo jambo"
Proverbs 23:17-18
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
isiruhusu moyo wako kuwahusudu wenye dhambi
" usijiruhusu mwenyewe kuwahusudu wenye dhambi" au "hakikisha huwahusudu wenye dhambi"
tumaini lako hataondolewa
"Mungu hataruhusu mtu yeyote kuondoa tumaini lako" au " Mungu atalinda ahadi yake aliyoifanya kwako"
Proverbs 23:19-21
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
Sikia-wewe! mwanangu
"mwanangu sikiliza kwa makini."
uelekeze moyo wako katika njia
"hakikisha unatenda kwa busara"
walaji wa nyama walafi
1) watu wanaokula nyama zaidi ya mahitaji yao" au 2) "watu wanaokula chakula kingi zaidi ya hitaji lao."
usingizi utawavika matambara
"kwa sababu wanatumia muda mwingi kwa kula na kunywa,wala hawafanyi kazi kwa hiyo watakuwa maskini"
Proverbs 23:22-23
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
usimdharau
"onesha adabu kwa"
Inunue kweli, wala usiiuze; nunua hekima, mafundisho, na ufahamu
" Fanya namna yoyote ili uweze kufahamu kweli, uwe na busara, uweze kujifunza namna ya kutenda, ili ufahamu jema na baya; wala usifikirie kitu kingine kuwa ni muhimu zaidi ya haya"
Proverbs 23:24-25
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
baba wa mtu mwenye haki atafurahi sana, na mwenye kumzaa mtoto mwenye busara atamfurahia
"baba wa mtu mwenye haki, mzazi wa mtoto mwenye busara, atashangilia sana na atamfurahia"
atamfurahia
"atafurahia kwa ajili ya mtoto wake"
Proverbs 23:26-28
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
nipe moyo wako
"nisikmalaya ilize kwa makini" au "nitumaini kabisa"
macho yako yatazame
" zingatia sana"
malaya...mwanamke mwasherati
Kuna aina mbili za wanawake washerati. "malaya" ni mwanamke ambaye hajaolewa, au "mke wa mume mwingine aliyeolewa. kwa pamoja wanaunda namna ya mwanamke mwasherati.
malaya ni shimo refu
"kulala na malaya ni kama kudumbukia kwenye shimo refu "
malaya
Huyu ni mwanamke ambaye hajaolewa anayefanya mambo ya ngono, wala si wale tu ambao hufanya ngono kwa ajili ya pesa.
shimo refu...kisima chembamba
Sehemu hizi mbili ni rahisi kutumbukia na vigumu kutoka "shimo" kwa sababu ni "refu" na "kisima" kwa kuwa ni "chembamba"
mwanamke mwasherati ni kisima chembamba
"kulala na mke wa mume mwingine ni kama kuangukia ktika kisima chembamba"
kisima
shimo katika ardhi ambalo watu huchimba kwa ajili ya kupata maji
huvizia
kukaa kwa kujificha na kuwa tayari kushambulia mhanga napofika
mdanganyifu
"watu wadanganyifu" au "wale ambao huwadhuru wengine kwa kwa kuwadanganya"
Proverbs 23:29-30
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye mapigano? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani mwenye majeraha bila sababu? Ni nani mwenye macho mekundu?
"Sikilizeni nataka kuwaambia mtu wa ole, huzuni, mapigano, malalamiko, mjeraha bila sababu, na macho mekundu."
macho mekundu
"macho kuwa na rangi nyekundu kama ya damu"
Wale ambao hukawia sana kwenye mvinyo, wale ambao hujaribu kuchanganya mvinyo
Hili ni jibu la maswali ya mstari wa 29. Kuelezea watu ambao hunywa sana mvinyo.
hukawia sana kwenye mvinyo
hutumia muda mwingi kunywa mvinyo na hunywa mvinyo mwingi
kuchanganya mvinyo
1) kuchanganya aina mbalimbali za mvinyo au 2) vileo vingine ambavyo ni vikali kuliko mvinyo
Proverbs 23:31-33
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
Mwishoni
"baada ya kunywa"
huuma kama nyoka ...choma kama kifutu
" hukufanya ujisikie vibaya kama umeumwa nyoka au kama kifutu amekuchoma"
kifutu
aina ya nyoka mwenye sumu
moyo wako utasema vitu vya kupotosha
"utafikiri na kuamua vitu vya kupotosha"
vitu vya kupotosha
vitu ambayo Mungu amevitaja kuwa vibaya na viovu ; vitu ambavyo havifai
Proverbs 23:34-35
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
anayelala juu ya mlingoti
"anayelala juu kwenye ndoo karibu namlingoti"
mlingoti
ufito wa mbao mrefu ambao huwekwe kwenye meli wakati wa safari ya majini
walimpiga ...lakini hakuumia. walinipiga, wala siku hisi kitu
Kwa sababu mtu mlevi hafikirii vizuri, anadhani kuwa watu wanampiga, lakini hasikii maumivu na wala hakumbuki chochote.
nitaamka lini?
mtu mlevi anashangaa ni wakati gani atakuwa na busara tena, wakati madhara ya pombe yatakapoisha.
Proverbs 24
Proverbs 24:1-2
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
mioyo yao
"wao"
midomo yao
"wao"
huongea juu ya madhara
"huongea jinsi ya kutengeneza(kusababisha ) matatizo"
Proverbs 24:3-4
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
kwa hekima nyumba hujengwa
"watu wanahitaji kuwa busara kama wanajenga nyumba nzuri"
kwa ufahamu huimarishwa
"watu wanahitaji kufahamu wema na ubaya kama wanataka kuimarisha nyumba"
kuimarisha
"nyumba" inawakilisha familia... familia ambayo huishi kwa amani
Kwa maarifa vyumba hujazwa
"watu wanahitaji kufahamu vitu vya thamani na vizuri kama wanataka kujaza vyumba vyao"
Proverbs 24:5-6
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
shujaa wa hekima
"shujaa mwenye busara"
mtu mwenye maarifa huongeza nguvu zake
"mtu anayejua mambo mengi ni imara kwa sababu anavijua vitu hivi"
kwa uongozi wa busara
"kama unawatu wenye busara wakikuelekeza jambo la kufanya"
kupigana
"pambana"
washauri
wale ambao huwaambia maafisa wa serikali mambo ya kufanya
Proverbs 24:7
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
juu sana kwa ajili ya mpumbavu
Hii ni nahau " ni vigumu sana kwa mpumbavu kufahamu"
hufumbua kinywa chake
"huongea"
Proverbs 24:8-9
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
bwana wa njama
" mtu mfitinishaji" au "mchochezi"
Proverbs 24:10
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
nguvu zako ni chache
"unazo nguvu chache sana" au " ni dhaifu kabisa"
Proverbs 24:11-12
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
wale ambao wanachukuliwa
"wanao wachukua"
wanachukuliwa
"kokotwa kupelekwa mbali"
pepesuka
kutemea upande na karibia na kuanguka. Neno hili linaeleza jinsi mtu anavyotembea anavyokokotwa kupelekwa sehemu.
mchinjaji
"sehemu ambayo watu watauwawa, watawaua kama vile wanavyoua wanyama"
kama unasema,"Tazama...hili",
Mwandishi anajibu jambo ambalo msomaji anaweza kufikiria.
Tazama, sisi
"Tusikilizeni sisi ! hatujafanya chochote kibaya , kwa sababu sisi"
je yeye aupimaye moyo hafahamu usemayo?
"yeye aupimaye moyoanafamu ambacho unasema"
yeye ambaye
" ni Yahwe" au "Yahwe ambaye"
aupimaye moyo
"anajua namna watu wanavyofikiri vyema na hamu zao"
yeye mwenye kuongoza maisha yako, je yeye hajui?
"yeye ambaye huyaongoza maisha yako anayajua"
Je Mungu hatampa kila mmoja kile anachostahili?
"Mungu atampa kila mtu kile anachostahili"
Proverbs 24:13-14
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
tumaini lako halitakoma
"tumaini lako litaendelea"
Proverbs 24:15-16
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
usivizie
"kujificha na kusubiri muda utimie"
nyumba yake
nyumba ya mtu mwenye haki
huinuka
"kusimama tena"
watu waovu huangushwa kwa maafa
"Mungu atatumia maafa kuwaangusha watu waovu"
huangushwa
kuangushwa
maafa
wakati ambapo mambo mabaya hutokea kwa watu na mali zao
Proverbs 24:17-18
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
adui yako huanguka
" jambo baya hutokea kwa adui yako"
moyo wako usifurahi
"usifurahi" " au "jizuie usije ukafuraha"
geuza ghadhabu yake kutoka kwake
"kuacha kuwa na hasira juu yake na kukukasirikia wewe badala yake"
Proverbs 24:19-20
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
taa ya watu waovu itazimwa
Maisha ya watu waovu itakoma kama taa inavyozimika
Proverbs 24:21-22
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ni mwendelezo wa "misemo thelathini"(22:20)
Hofu
heshima ya kina na utiisho kwa ajili ya mtu mwenye mamlaka
ni nani ajuaye ukubwa wa uharibifu ambao utakuja kwao wote?
"hapana ajuaye ukubwa wa uharibifu ambao utakuja kwao wote?
kwao wote
Maneno haya yanamwakilisha Yahwe na mfalme
Proverbs 24:23
Hii pia ni misemo ya wenye busara
Sentensi hii inaanza mkusanyiko mpya wa mithali
shitaka kwenye sheria
mazingira ya kwenda mbele ya hakimu ambapo kuna mtu anayeshutumiwa kwa kuvunja sheria
Proverbs 24:24-25
Yeyote asemaye kwa mtu mwovu ...atalaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa
"watu watamlaani yeyote anayemwambia mtu mwovu ...,na watu wa mataifa mengine watamchukia"
mtu mwovu ...mtu mwenye haki
1)watu hawatamwita mtu yeyote mwovu kuwa ni mwenye haki au 2) hakuna mtu atakayesema mtu mwenye hatia ya kosa ni mwenye haki
watapata furaha
"watafurahi sana"
zawadi za wema zitawajia
"watu watawapa zawadi nzuri"
zawadi za wema
"baraka" au "vitu vizuri"
Proverbs 24:26-27
hubusu midomo
"kuonyesha urafiki wa kweli"
Proverbs 24:28-29
kwa midomo yako
"kwa yale asemayo"
Nitamlipa
"kufanya kisasi dhidi yake"
Proverbs 24:30-31
miiba
mimea ambayo haina manufaa yenye miiba miakali
upupu
mimea ambaya imejaa majani yenye kuwasha
ulikuwa umeangushwa
"ulikuwa umeanguka"
Proverbs 24:32-34
nikapokea mafundisho
"nilijifunza somo"
usingizi kidogo ....kwa kupumzika -na umaskini huja
"unaweza kujisemea mwenyewe, usingizi kidogo ...kwa kupumzika-lakini unasikini utakuja"
umaskini huja juu yako
"umaskini huja juu yako kama mwivi"
mahitaji yako kama askari mwenye silaha
"mahitaji yako yatakuja kwako kama askari mwenye silaha"
Proverbs 25
Proverbs 25:1-3
kuficha jambo
"kuyahifadhi baadhi ya mambo ya siri"
lakini utukufu
"lakini ni utukufu"
kuchunguza
"hulichunguza jambo" au "hufanya uchunguzi kwa mambo ambayo Mungu ameyaficha"
Kama mbingu ni kwa ajili ya kimo na dunia ni kwa ajili ya kina, ndivyo moyo wa wafalme usivyochunguzika
"Hakuna mtu wenye kuweza kupima kimo cha mbingu au kina cha dunia, hata hakuna mtu anawezakuufahamu moyo wa wafalme"
mbingu
Hii ni jula ya vitu vyote tunavyoviona angani pamoja na jua, mwezi, na nyota.
Proverbs 25:4-5
takataka
malighafi kwenye chuma ambayo watu ambayo watu huwa hawahitaji na huiondoa kwa kukichoma chuma.
kiti chake cha enzi kitathibitishwa kwa kutenda
"mfalme atathibitisha kiti chake cha enzi kwakutenda" au "atakuwa na mamlaka ya kutawala kwasababu anatenda"
Proverbs 25:6
jitukuze
kumpa mtu heshima.
mfalme
mtu ambaye ni mtawala mkuu wa mji, jimbo au nchi.
Proverbs 25:7-8
ni bora yeye akuambie, "Njoo huku juu"
maana yake kupelekwa sehemu ya meza ambayo ni karibu na mfalme. "ni bora mtu akukaribishe kukaa karibu na mfalme"
mbele ya mkuu
"mbele ya mtu mkuu"
Maana utafany nini mwishoni wakati jirani yako atakapokuaibisha?
" Maana hutajua ufanye nini mwisho wakati jirani yako atakapukuaibisha" au "Maana kama jirani yako anamaelezo, atakuaibisha, na hutakuwa na kitu cha kusema ili kujitetea mwenyewe."
Proverbs 25:9-10
hoja yako
"mabishano yako"
usiifunue siri ya mtu mwingine
" usiwashirikishe watu wengine siri ya jirani yako"
na habari mbaya juu yako ambayo haiwezi kunyamazishwa
"wala hutaweza kumzuia kuwaambia wengine mambo mabaya juu yako" au " na atawaambia wengine watu mambo mabaya juu yako na hutakuwa na sifa njema tena"
Proverbs 25:11-12
Neno linalosemwa katika hali ya kufaani ni tufaha za dhahabu kwenye vyano vya fedha
"Neno linalosemwa kwa wakati sahihi ni zuri kama tufaha za dhahabu kwenye vyano vya fedha"
ufaha za dhahabu kwenye vyano vya fedha
"matunda yaliyopakwa rangi ya dhahabu yaliyowekwa kwenye bakuli la fedha "
Neno linalosemwa
"ujumbe ambao mtu huusema"
pete ya dhahabu au pambo lilitotengenezwa kwa dhahabu safi ndivo alilivyo karipio la busara kwenye sikio lenye kusikiliza
"karipio la busara kwenye sikio lenye kusikiliza ni zuri na la thamani kama pete ya dhahabu au pambo la dhahabu"
sikio lenye kusikiliza
"mtu aliye tayari kusikiliza"
Proverbs 25:13-14
kama baridi ya theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu
mjumbe mwaminifu anafananishwa na baridi ya theluji kwa sababu vyote hivi ni vizuri.
baridi ya theluji
Hii ni lugha ya picha kuonesha uzuri wa jambo.
theluji
barufu ambayo hudodoka kutoka angani kama mvua
hurejesha uhai wa bwana zake
huwafanya bwana zake walidhoofika na kuchoka kuwa imara na kubrudika tena.
mawingu na upepo bila mvua ndivyo alivyo mwenye kujisifu ...hakutoa
"Mwenye kujisifu ...bila kutoa ni kama mawingu na upepo bila mvua
Proverbs 25:15
Kwa uvumilivu mtawala anaweza kushawishiwa
"Mtu mwenye uvumilivu anaweza kumshawishi mtawala" au "mtu mwenye uvumilivu anaweza kuongea kwa mtawala na kuyabadilisha mawazo yake"
ulimi laini unaweza kuvunja mfupa
"kauli ya upole inaweza kushinda upinza imara"
Proverbs 25:16-17
Maelezo ya Jumla
mstari wa 16 unaeleza kanuni ya ujumla, na mstari wa 17 hautoi mfano mahususi. Ni sitiari kuonesha kufanya jambo zuri kupita kiasi na kujuta baadaye.
Proverbs 25:18-19
Mtu ashuhudiaye uongo dhidi ya jirani yake ni kama rungu litumikalo kwenye vita, au upanga, au mshale wenye makali
shahidi wa uongo analinganishwa na silaha ambazo zinaweza kujeruhi au kuangamiza watu
mtu asiyemwaminifu unayemtumaini wakati wa taabu ni kama jino bovu au mguu wenye kuteleza
"Kumtumaini mtu asiye mwaminifu wakati wa taabu kutaleta maumivu kwako kama jino bovu au mguu wenye kuteleza"
Proverbs 25:20
magadi ya soda
haya ni madini ambayo hutoa povu na sauti yanapogusana na asidi kama siki.
huimba nyimbo
"kuimba nyimbo za furaha"
roho nzito
"mtu mwenye huzuni"
Proverbs 25:21-22
makaa ya moto juu ya kichwa chake
"kusababisha ajisikie hatia kwenye dhamiri na aibu kwa tendo alilofanya"
Proverbs 25:23-24
upepo wa kaskazini
Katika Israeli upepo kutoka kaskazini maranyi ulileta mvua.
mtu ambaye hunena siri
"mtu mwenye hasira"
hukasirisha nyuso
huwafanya watu wengine wakasirike
pembe ya dari
angalia
mke mgomvi
mke ambaye mara nyingi hubishana na kulalamika
Proverbs 25:25-26
kama maji ya baridi kwa mwenye kiu, ndivyo ilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali
maji ya baridi yanafananishwa na habari njema maana vyote huburudisha na kufurahisha
kama chemchemi iliyochafuka au bomba lililoharibiwa ndivyo alivyo mtu mwenye haki apepesukapo mbele ya watu waovu
mtu anatarajia kupata maji safi kwenye chemchemi au bomba, ndivyo mwenye haki anapaswa kusimama kwa kile anachokiamini. Hivyo chemchemi au bomba lililoharibika ni kama mwenye haki anayeanguka.
apepesukapo mbele ya watu waovu
1) kukataa kupambana na watu waovu 2)kujiunga na uovu wao
apepesukapo
"kushindwa kusimama"
mbele ya waovu
"watu waovu wanapomshambulia" au "watu waovu wanapomshawishi kutenda maovu"
Proverbs 25:27-28
siyo vema kula asali nyingi mno; hivyo ni kama kutafuta heshima baada ya heshima
kupata heshima na kula asali ni vizuri, lakini unaweza kula asali nyingi sana na unaweza kutumia nguvu nyingi ili watu wakuheshimu.
siyo vema
"ni jambo baya"
hivyo ni kama kutafuta heshima baada ya heshima
"ni kufikiria kila wakati jinsi watu wengine wanapaswa kukuheshimu" au "hivyo ni kuongea sifa nyingi sana kwa watu"
mtu asiyejitawala ni kama mji uliobomolewa na usiokuwa na ukuta
Mtu asiyejitawala na mji bila ukuta wote ni dhaifu na wapo katika hatari.
uliobomolewa na usiokuwa na ukuta
"ambao ukuta wake umeangushwa na jeshi na kuharibiwa"
Proverbs 26
Proverbs 26:1-2
Kama theluji wakati wa joto au mvua kwenye mavuno
"kama ambavyo ingekuwa ni ajabu kuwa na theluji wakati wa joto na mvua kipindi cha mavuno "
hivyo laana isiyositahili haishuki
laana ambayo haimdhuru mtu imeongelewa kana kwamba ni ndege ambaye hatui."laana isiyositahili haitui mahali pake"
laana isiyositahili
"laana kwa mtu ambaye haimstahili"
shuka
tuajuu ya mtu au kitu
Proverbs 26:3-4
mjeledi ni kwa ajili ya farasi, lijamu kwa ajili ya punda na fimbo ni kwa ajili mgongo wa wapumbavu
mjeledi, lijnamu na fimbo ni vitu ambavyo watu hutumia ilikuwafanya farasi, punda, na wapumbavu wanataka nini.
lijamu kwa ajili ya punda
lijamu imetengenezwa kwa nyuzinyuzi. Watu huweka kwenye vichwa cha punda na kushikilia yuzi moja ili kumfanya punda atembee kama wanavyotaka.
fimbo ni kwa ajili mgongo wa wapumbavu
Nyakati za Biblia watu waliweza kuwacha watoto wao au watumwa wao kwa fimbo ya mti ili kuwatia adabu.
Proverbs 26:5-6
mjibu mpumbavu na ujiunge katika upumbavu wake
mjibu mpumbavu kulingana na aupumbavu wake " au "mjibu mpumbavu kipumbavu"
hivyo hatakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe
"hivyo hawezi kuwa mwenye busara kwa mtazamo wake" au "hivyo hafikirii wenyewe kuwa ni mwenye busara"
yeye apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu
"yeye anayemtuma mpumbavu kupeleka ujumbe"
hukata miguu yake mwenyewe na kunywa vurugu
"hujiumiza mwenyewe kama mtu anayejikata miguu yake na kunywa vurugu"
kunywa vurugu
vurugu inaonelewa kama kimiminika ambach o mtu anaweza kunywa.
Proverbs 26:7-8
kama miguu...mithali katika kinywa cha wapumbavu
"mithali katika kinywa cha wapumbavu ni kama miguu ya mtu aliyepooza ambayo kuning'inia"
aliyepooza
mtu ambaye hawezi kutembea au kuhisi chochote katika mwili wake wote.
katika kinywa cha wapumbavu
" katika maongezi ya wapumbavu" au " wapumbavu husema"
kujaribisha jiwe kwenye teo
"jaribishia jiwe kwenye teo ili lisiweze kurushwa"
kutoa heshima kwa mpumbavu
"kumheshimu mpumbavu"
Proverbs 26:9-10
kama mwiba ...ni methali katika kinywa cha wapumbavu
"mithali katika kinywa cha wapumbavu ni hatari kama mwiba kama unaochoma kwenye mkono wa mlevi"
mwiba ambao unaenda kwenye mkono wa mlevi
kama mtu mlevi anashikilia kichaka chenye miiba, mwiba utamchoma mkononi mwake
katika kinywa cha wapumbavu
"katika kauli ya wapumbavu" au "amba hunena wapumbavu"
amwajiriye mpumbavu
"kumpa kazi mpumbavu"
Proverbs 26:11-12
kama mbwa kuyarudia matapishi yake
"kama mbwa anavyokula matapishi yake"
Je unamwona mtu ambaye ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe?
" mfikirie mtu ambaye hudhani kwambani mwenye busara lakini hana"
Kuna tumaini zaidi kwa kwa mpumbavu kuliko kwake
"mpumbavu anaweza kuwa na busara zaidi kuliko yeye "
Proverbs 26:13-14
Mtu mvivu husema , "kuna simba ....katikati ya njia kuu!"
Mtu mvivu hulala na husema kwamb hawezi kwenda nje na kufanya kazi kwa sababu kuna simba njiani au katikati ya njia kuu.
kuna simba njiani
angalia 22:13
bawaba
vipande vya chuma ambavyo huubana mlango kwenye ubao au kitu kingine ili kuweza kufunguka na kufanga
Kama mlango unavyorudi kwenye bawaba zake, ndivy o alivyo mtu mvivu juu ya kitanda chake
Mlango na mtu mvivu huzunguka lakini hawaendi popote.
Proverbs 26:15-16
huweka mkono wake kwenye sinia
"huweka mkono wake kwenye sinia kula chakula"
hana nguvu kuunyanyua juu kwenye kunywa chake
Hii ni kuonesha uzembe wake. Huuacha mkono wake karibu na chakula lakini hawezi kula chakula.
Mtu mvivu ni mwenye busara zaidi machono pake mwenyewe kuliko watu saba wenye ufahamu
"Mtu mvivu hufikiri ni mwenye busara zaidi kuliko watu saba ambao wanaweza kujibu kwa akili"
Proverbs 26:17
Kama mtu ashikaye masikio ya mbwa, ndivyo alivyo mpitaji ambaye hupata hasira kwenye ugomvi ambao si wake
"mpitaji ambaye hupata hasira kwenye ugomvi wa watu wengine ni kama mtu ambaye hushikilia masikio ya mbwa"
Kama mtu ashikaye masikio ya mbwa
"kama mtu ayemkasirikia mbwa na kumshika masikia yake"
mpitaji ambaye hupata hasira kwenye ugomvi ambao si wake
mpitaji ataanza kubishana na watu waliokuwa wakipigana atawakasirisha na watamuumiza
Proverbs 26:18-19
kama kichaa ...yule adanganyaye...nakuambia utani?
kichaa na mwogo wote huumiza watu lakini huacha kuwajibika kwa hayo.
nilikuwa nakuambia utani?
"nilikuwa natania tu" au "usinilaumu. Nilikuwa natania tu"
Proverbs 26:20-21
mbeya
mtu ambaye hupiga sogansana
Mkaa ni kwa ajili ya kuchoma makaa na kuni kwa ajili ya moto
"Kama mkaa unavyosaidia kuchoma makaa na kama kuni zinavyosaidia moto kuwaka"
kuchochea ugomvi
"kusababisha watu wapigane" au "kusababisha watu wabishabe"
Proverbs 26:22-23
maneno ya umbeya ni kama chembe tamu
"maneno ya umbeya hutamanisha kusikiliza"
hushuka chini katika sehemu za ndani ya mwili
"na huingia katika akili ya mtu na kuyaathiri mawazo yake"
kama rangi ya kioo iliyofunikwa kwenye chombo cha udogo ndivyo vilivyo midomo iwashayo na moyo wa uovu
"Watu wenye midomo ya kuwasha na mioyo ya uovu wapo kamachombo cha udongo kilichofunikwa kwa rangi ya kung'aa"
rangi ya kioo iliyofunikwa kwenye chombo cha udogo
"kioo chenye kungara ambacho hufunika chungu cha udongo"
midomo iwashaya
"kauli yenye hisia" au "kusema vitu vizuri"
moyo wa uovu
"mawazo mabaya" au "tamaa mbaya"
Proverbs 26:24-26
huficha hisia zake kwa midomo yake
"huficha hisia zake kwa namna anavyoongea" au " huongea kwa jinsi ambayo watu hawawezi kufahamu hisia zake za kweli"
huweka uongo ndani yake mwenyewe
"kwa hila hupanga kuumiza watu"
lakini hamwamini
"lakini haamini kile anachosema"
maana kuna machukizo saba katika moyo wake
"moyo wake umejaa mambo ya chuki" au "maana moyo wake umejaa chuki"
Ingawa chuki yake imefichwa kwa uongo
"ingawa uongo wake umefunikwa kwa chuki" au "Ingawa hufunika chuki yake kwa uongo"
Ingawa chuki yake imefichwa kwa uongo
"Ingawa hudanganya kuhifadhi chuki yake ili watu wasijue" au "Ingawa hudanganya ili watu wasijue ya kuwa anawachukia"
kusanyiko
"jamii ya waisraeli"
Proverbs 26:27-28
achmbaye shimo atatumbukia ndani yake
"Achimbaye shimo kumtega mtu mwingine atatumbukia mwenyewe"
jiwe litaviringika kurudi kwake yeye anayelisukuma
"mtu akisukuma jiwe ili liviringike chini ya kilima na kumgonga mtu, badala yake jiwe litamrudia yeye"
ulimi udanganyao huwachukia watu unaowajeruhi
"mwogo huwachukia wale ambao huwaumiza kwa uongo wake"
Kinywa chenye kusifia huleta uharibigu
mtu ambaye huwasifu wengine huleta taabu au mtu ambaye huwasifu wengine huababisha uharibifu juu yao
kusifia
tukuza mtu kwa namna isiyofa, kumsifu mtu kwa mambo ambayo si ya kweli
Proverbs 27
Proverbs 27:1-2
usijifufu kwa ajili ya kesho
"usijisifu kwa ajili ya mipango yako ya kesho"
siku italeta nini
"nini kitatokea katika siku" au "nini kitatatokea kesho"
kinywa chako mwenyewe... midomo yako
"wewe mwenyewe"
mgeni na siyo midomo yako
"mgeni na akusifu na wala siyo midomo yako mwenyewe"
Proverbs 27:3-4
uchochezi wa mpumbavu ni mzito kuliko vyote
"uchochezi wa mpumbavu ni vigumu kuuvumilia kuliko vyote"
uchochezi wa mpumbavu
"taabu inayosababishwa na mpumbavu" "uchochezi" maana yake maneno ua mtendo yanayosababisha hasira au uchungu
kuna ukatili wenye ghadhabu na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anaweza kusimama mbele ya wivu?
"mtu mwenye ghadhabu ni mkatili na mtu mwenye hasira anaogopesha, lakini ni nani anaweza kusimama mbele ya mtu mwenye wivu?
ukatili
ukali"
mafuriko ya hasira
"uharibifu wa hasira"
lakini ni nani anaweza kusimama mbele ya mtu mwenye wivu?
"lakini hakuna awezaye kusimama mbele yake mwenye wivi"
kusimama mbele ya mtu mwenye wivu
"kumzuia mtu mwenye wivu" au "kubakia imara wakati mtu mwenye wivu anapomshambulia"
Proverbs 27:5-6
bora karipo la wazi
"bora kukemewa katika hali ya wazi"
kuliko upendo wa siri
"kuliko upendo ambao haupo wazi" au "kuliko kupendwa kwa siri"
Mwaminifu ni majeraha yaliyosababishwa na rafiki
"majeraha ambayo husababishwa na rafiki ni mdhamana " maana yake maumivu au huzuni ambayo mtu hupata wakati rafiki yake anapomkemea au kusahihisha.
Mwaminifu ni majeraha yaliyosababishwa na rafiki
"Ingawa huleta huzuni, karipio la rafiki ni la kutegemewa"
lakini adui anaweza kukubusu kwa wingi sana
"busu nyingi za adui ni siyo za kutegemewa" au "adui anaweza kujaribu kudanganya kwa busu maridhawa"
wingi sana
"maridhawa" au "kwa wingi"
Proverbs 27:7-8
mtu aliyekula na kushiba
"mtu aliyetosheka" au "mtu aliyekula kiasi cha kushiba"
hukataa hata sega la asali
Sega la asali lingetamanisha, lakini si kwa mtu ambaye tayari amekwisha kula na kushiba.
kila kitu kichungu ni kitamu
"kila kitu chenye ladha ya uchungu ni kitamu kwa kuonja"
kama ndege ambaye hutanga tanga kutoka kwenye kiote chake ndiyo alivyo mtu ambaye hupotea ambapo anaishi
"kutanga tanga" na "kupotea" maana yake ni moja kwenye mstari huu
Proverbs 27:9-10
Marashi
mafuta ya kutamanisha au malihamu
huufanya moyo ufurahi
"humfanya mtu kujisikia furaha"
utamu wa rafiki hutoka katika ukweli wa shauri lake
"tunamthamini rafiki kwa ushauri wake"
nyumba ya ndugu yako
ndugu hapa ni mmoja kutoka katika kabila moja, ukoo, au kundi la watu.
msiba
taabu kubwa au bahari mbaya
Proverbs 27:11-12
huufanya moyo wangu ufurahi
"hunifanya kujisikia furaha"
kisha nitatoa jibu kwa yule mwenye kunidhihaki
"kisha nitajibu kwa yule anayenidhihaki mimi kwa kumwambia habari yako"
mtu mwenye busara huiona taabu na kujificha mwenyewe, lakini watu wajinga huendela na kuteseka kwa ajili yake
Angalia 22:3
mtu mwenye busara
mtu mwerevu" au "mtu mwenye akili njema"
watu wajinga
"watu ambao hawana uzoefu na hawaja pevuka kifikira"
Proverbs 27:13-14
chukua vazi la yule ambaye ameweka dhamana kwa ajili ya mgeni
angalia 20:15
ameweka dhamana
angalia 20:15
shikilia rehani
Angalia 20:15
yeye ampaye jirani yake baraka
"kama mtu atampa jirani yake baraka"
hiyo baraka itadhaniwa kuwa ni laana
"jirani atadhania hiyo baraka kuwa ni laana"
Proverbs 27:15-16
mgomvi
maana yake kuwafanya watu wachukiane kula mmoja au kusababisha mabishano makubwa kati ya watu.
kutona tona daima
"kutona tona kwa mvua daima"
siku ya mvua
siku yenye mvua mfululizo"
kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kujaribu kuyashika mafuta katika mkono wako wa kulia
ni vigumu au haina maana kujribu kumzuia ni kama kujaribu kuuzuia upepo au kushika mfuta katika mkono wako
kumzuia
"kumweka chini ya utawala" au "kumzuia katika ugomvi"
kuuzuia upepo
"kuushikilia upepo" au "au kuudhibiti upepo"
Proverbs 27:17-18
chuma hunoa chuma; katika njia hiyo hiyo, mtu humnoa rafiki yake
" Kama chuma kinaweza kunoa kipande kingine cha chuma, hivyo tabia ya mtu huendelezwa kwa uongozi wa rafiki yake"
atunzaye
"hudumia, jali"
yeye amlindaye bwana wake ataheshimiwa
"bwana atamheshimu yeye ambaye humlinda"
Proverbs 27:19-20
moyo wa mtu
" namna mtu anavyofikiri"
mharabu
" mwenye kuharibu"
havishibi
" jaa, tosheka"
macho ya mtu
" matamanio ya mtu"
Proverbs 27:21-22
kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu
"kalibu inatumika kusafisha fedha na tanuru hutumika kusafisha dhahabu "
kalibu
Ni kontena linalotumika kupasha joto vitu kwa joto kali
tanuru
jiko ambalo linaweza kuwa moto sana
mtu hujaribiwa wakati wa kusifiwa
"wakati watu wanapomsifu mtu, pia huwa wanampima"
Kama utamtwang mpumbavu ...bado upumbavu wake hautaondoka kwake
Maana yake mpumbavu hata kama atateseka na kuumia atabaki mpumbavu.
mchi
kifaa kigumu chenye ncha ya duara, hutumika kwa ajili ya kutwanga vitu kwenye kinu au bakuli
Proverbs 27:23-25
hakikisha unafahamu hali ya makundi yako ya kondoo na yajali makundi yako
maneno haya yanaweka msisitizo juu ya kujali
makundi yako ya kondoo
makundi ya kondoo
makundi
makundi ya mbuzi
je taji hudumu kwa vizazi vyote?
"taji haidumu kwa vizazi vyote"
taji
hapa inamaanisha utawala wa kifalme
majani mapya huonekana
"majani mapya huanza kukua"
Proverbs 27:26-27
Sentensi Unganishi
mistari 26 na 27inakwenda pamoja na mistari 23 hadi 25 kama mithali moja
kondoo watakupa mavazi yako
"sufu za kondoo zitakupa vazi"
mbuzi watakupa thamani ya shamba kwa ajili ya nyumba yako
"ukiuza mbuzi wako watakupa thamani ya shamba"
kwa ajili ya nyumba yako
"kwa ajili ya familia yako yote"
na chakula kwa ajili ya watumishi wsichana
"na kutakuwa na maziwa ya mbuzi kwa chakula cha watumishi wako wasichana"
chakula
chakula
Proverbs 28
Proverbs 28:1-2
kwa sababu ya uhalifu katika nchi
"kwa sababu ya namna nchi navyokosea"
uhalifu katika nchi
"uhalifu wa watu katika nchi"
kwa mtu mwenye ufahamu na maarifa
" kwa mtu anayefahamu na kujua jinsi ya kutawala"
Proverbs 28:3-4
dhulumu
"tendea vibaya"
kama mvua inayoshesha ambayo haiachi chakula
mtu maskini wenye kudhulumu watu wengine maskini ni kama mvua ambayo hunyesha kwa nguvu wala haiachi mazao ya kuvuna.
mvua inayonyesha
mvua ya uharibifu
kuiacha sheria
"kuacha sheria ya Mungu"
waishikao sheria
"wale wanaotii sheria ya Mungu"
hupigana dhidi yao
hupingana nao au huwazuia
Proverbs 28:5-6
watu waovu
"watu watendao mambo mabaya"
hawafahamu haki
"hawafahamu maana ya haki"
wale wamtafutao Yahwe
wale wanaotaka kumjua Yahwe
hufahamu kila kitu
"hufahamu maana ya haki"
bora mtu maskini ...kuliko mtu tajiri
"ni bora kuwa maskini ...kuliko kuwa mtu tajiri"
aendaye kaika uaminifu wake
"huishi kwa uaminifu"
ambaye ni mdanaganyifu katika njia zake
"ambaye si mwaminifu katika yale ayatendayo"
Proverbs 28:7-8
yeye ashikaye sheria
"yeye ambaye anatii sheria ya Mungu"
mwana mwenye ufahamu
"mwana anayefahamu"
warafi
"watu wanaokula sana"
humwaibisha baba yake
"humtia aibu baba yake"
hufanikiwa
"huongeza utajiri wake"
lipisha riba kubwa
"lipisha pesa ya ziada kwa kukopa"
riba
pesa inayolipwa na mkopaji kwa kutumia pesa ya mtu mwingine
hukusanya utajiri wake
"huleta mali zake pamoja"
kwa mwingine
"mtu mwingine"
huruma
"kumsikitikia mtu mwingine"
Proverbs 28:9-10
Kama yeye
"kama mtu"
atageuzia mbali sikio lake kuisikia sheria
"atageuzia mbali sikio lake kusikia na kutii sheria"
hata maombi yake ni chukizo
"Mungu anachukia hata maombi yake"
chukizo
angalia 3:31
Yeyote mwenye kumpotosha mwenye haki katika njia mbaya
"Yeyote anayesababisha mwenye haki kwenda katika mwelekeo mbaya"
Yeyote mwenye kumpotosha...njia mbaya ataanguka
"kama mtu yeyote atampotosha...njia mbaya ataanguka"
mwenye haki
"watu wanyoofu"
ataanguka kwenye shimo lake mwenyewe
"ataanguka kwenye mtego ambao ameuchimba"
wakamilifu
"watu wakamilifu"
watapata urithi mzuri
"watarithi kitu kizuri"
Proverbs 28:11-12
kuwa mwenye busara machoni pake mwenyewe
"kuwa mwenye busara katika mawazo yake mwenyewe" au "kijifikira ni mwenye busara"
mwenye ufahamu
"anayefahamu"
atamchunguza
"ataona asili yake ya kweli"
kunapokuwa na ushindi kwa watu wenye haki
"watu wenye haki wanapofanikiwa"
wainukapo waovu
"wakati waovu wanapopata mamlaka"
waovu
"watu waovu"
watu hujificha wenyewe
"watu huende kujificha"
Proverbs 28:13-14
huficha dhambi zake
"hufunika dhambi zake "
fanikiwa
"nufaika" au "endelea"
yeye ambaye huziungama na kuziacha atapata rehema
"Mungu ataonesha rehema kwa yule ungama na kuziacha"
yeye ambaye huishi kwa kicho daima amebarikiwa
"Mungu atambariki yule ambaye huishi kwa kicho daima"
huishi kwa kicho
huishi maisha ya kicho
kicho
kumheshimu sana Yahwe na kuonesha kwamba unamtii
mwenye kuufanya mgumu moyo wake
"mtu ambaye huufanya mgumu moyo wake"
kuufanya mgumu moyo wake
"kukataa kumtii Mungu"
ataangukia katika taabu
"ataishia kwenye taabu"
Proverbs 28:15-16
Kama simba aungurumaye au dubu mwenye hasira ndivyo alivyo mtawala mwovu juu ya watu maskini
watu maskini ambao hawana msaidizi dhidi ya mtawala mwovu ni kama watu ambao simba anawaungurumia na dubu anawashambulia
dubu mweye hasira
dubu ni mnyama mkubwa mwenye manyoya mengi na ni hatari sana, ana makucha na meno makali
mtawala aliyepungukiwa ufahamu
"mtawala ambaye hana ufahamu"
mnyonyaji
mtu ambaye huwatendea watu kwa ukatili na kuyafanya maisha yao kuwa magumu
yeye achukiaye udhalimu
"yeye achukiaye kuwa dhalimu"
huongeza siku zake
huishi maisha marefu
Proverbs 28:17-18
aliyemwaga damu ya mtu
"aliyeua mtu"
mkimbizi
mtu anyekimbilia mbali kuogopa kuogopa kukamatwa
hadi kifo
"maisha yake yote"
yeye anayekwenda katika uaminifu atakuwa salama
"Mungu atamweka salama mtu ambaye huenenda katika uaminifu"
yeye
mtu yeyote ambaye
anayekwenda katika uaminifu
"huishi kwa uaminifu"
yeye mwenye njia ya udanganyifu
"mtu ambaye haishi kwa uaminifu"
ataanguka ghafula
"ataharibikiwa ghafula" au "ataangamia ghafula"
Proverbs 28:19-20
hufanya kazi kwenye ardhi yake
maana yake kulima , kupanda na kutunza mazao
yeyote
mtu yeyote
afuataye mambo yasiyofaa
mtu anayeshughulika na mambo ambayo hayazalishi chochote.
atapata umaskini mwingi
"atakuwa maskini sana"
yeye apataye utajiri kwa haraka hatakosa adhabu
"Mungu atamwadhibu yule ambaye hupata utajiri kwa haraka"
yeye apataye utajiri kwa haraka
"yeye anayejaribu kupata utajira kwa haraka"
Proverbs 28:21-22
kwa kipande cha mkate mtu atafanya ubaya
"mtu atafanya dhambi kwa ajili ya kupata faida kidogo"
fanya ubaya
tenda dhambi
mtu bahili
"mtu mchoyo" Huyu ni mtu ambaye hapendi kutumia mali au pesa yake kwa ushirika na wengine
hufanya haraka kutajirika
mtu bahili huwinda utajiri " ni mroho kwa ajili ya utajiri"
umaskini utakuja juu yake
"ghafula atakuwa maskini"
Proverbs 28:23-24
yeye amwadibishaye mtu, baadaye atapata kibali kutoka kwake kuliko yule ambaye humsifu kwa ulimi wake
"mtu atakuwa mwenye fadhila kwe aliyemwadibisha kuliko mtu mwenye kumsifu kwa ulimi wake"
yeye amwadibishaye
"kama mtu anaadibisha"
humsifu kwa ulimi wake
"humsifu kwa maneno"
humsifu
kumtukuza mtu kwa namna ambayeo si ya kweli. au kumsifu mtu kwa mambo ambayo si ya kweli
yeye aibaye
"mtu anayeiba"
na husema, "Hiyo si dhambi,"
"na kusema hiyo siyo dhambi"
rafiki wa
"ni mtu wa aina ya "
Proverbs 28:25-26
mtu mroho
mtu mchoyo anayetaka vitu zaidi, pesa au chakula kuliko mahitaji yake
huchochea mgogoro
"husababisha mgogoro "
yeye nayeutumaini moyo wake
"mtu anyejiamini mwenyewe"
yeyote
"mtu yeyote ambaye"
huenda kwa hekima
"hufuta mafundisho ya busara"
Proverbs 28:27-28
Mwenye
mtu
maskini
"watu maskini"
hatapungukiwa kitu
" hupata kila kitu anachohitaji"
yeye afumbaye macho yake kwao atapokea laana nyingi
1) watapokea laana nyingi toka kwa maskini "maskini watatoa laana nyingi kwa yeyote afumbaye macho kwao"au 2"watu watatoa laana nyingi kwa yeyote afumbaye macho yake kwa maskini"
yeye
mtu yeyote
afumbaye macho yake
"asiyejali" au "anayeacha kusaidia"
watu waovu wanapoinuka
"watu waovu wanaposhika mamlaka au utawa katika mamla
huangamia
" huondoka " au "huanguka kutoka kwenye mamlaka" au "huharibiwa"
huongezeka
"huzidi" au "huinuka katika mamlaka"
Proverbs 29
Proverbs 29:1-2
shupaza shingo yake
"kataa maonyo "
atavunjika katika muda mfupi
"Mungu atamvunja ghafla"
pasipo kupona
"na hakuna mtu ataweza kumsaidia"
watu hushusha pumzi
"watu watakuwa na hofu na huzuni"
Proverbs 29:3-4
kwa haki
"kwa kutenda haki"
Proverbs 29:5-6
humsifu jirani yake
humwambia jirani yake mambo ya uongo ili afanye makosa
hutandaza mtego katika miguu yake
"hutega mtego kumnasa mtu huyo"
katika dhambi ya mtu mwovu kuna mtego
Hutamani kufanya mabaya kwa watu wengine, lakini Mungu atayatumia matendo yake hayo kumwadhibu.
Proverbs 29:7-8
huwasha moto kwenye mji
"huwashawishi watu wa mji kufanya ghasia"
hugeuza ghadhabu
huwafanya watu wenye hasira kuwa na amani
Proverbs 29:9-10
akibisha na
"kwenda mahakamani dhidi ya "
hughadhabika na kucheka
mpumbavu hukasirika na kumzuia mwenye busaa asiongee
ghadhabika
chukia sana
haptatakuwa na utulivu
"hawataweza kumaliza tatizo"
hutafuta maisha yake
Nahau ambaya maana yake "kutaka kuua"
Proverbs 29:11-12
huzingatia
"sikiliza" angalia 17:3
maafisa wake wote watakuwa waovu
"ni kana kwamba mtawala anawafundisha maafisa wake kuwa waovu"
Proverbs 29:13-14
mdhalimu
mtu ambaye huwatendea watu ukatili na kuyafanya maisha yao kuwa magumu
Yahwe huyatia nuru macho yao wote
Hii ni nahau "Yahwe huwapa uzima watu "
kiti chake cha enzi
"ufalme wake"
Proverbs 29:15-16
fimbo na maonyo hutoa hekima
"kama mzazi atatumia fimbo kwa mtoto wake na kumuonya, mtoto atakuwa na busara"
fimbo
Wazazi walitumia viboko katika Israeli kama vifaa vya kuleta nidhamu kwa kuwachapa watoto wao.
maonyo
kumwambia mtu kuwa jambo analofanya halifai
makosa huongezeka
"watu wengi watafanya makosa na dhambi za zitakuwa mbaya zaidi"
anguko la wale watu waovu
"wale watu waovu huanguka" au "wale watu waovu hupoteza utawala wao"
Proverbs 29:17-18
yeye ambaye huitunza sheria amebarikiwa
"Mungu atambari mtu yule itunzaye sheria"
Proverbs 29:19-20
mtumwa hatarekebishwa kwa maneno
"hutaweza kumrekebisha mtumwa kwa kuongea naye"
mtu mwenye haraka katika maneno yake umemtazama?
"unapaswa kutambua kitu ambacho hutoke kwa mtu mwenye haraka katika maneno yake"
Proverbs 29:21-22
ambaye humdekeza mtumwa wake
"ambaye huruhusu mtumwa wake kuacha kazi na hutendea vema mtumwa wake kuliko watumwa wengine"
mwisho wake
"mtumwa anapokua"
kutakuwa na taabu
mtumwa atakuwa mtu dhaifu
huchochea ugomvi
"husababisha mabishano zaidi kwa watu" Angalia 15:17
bwana wa ghadhabu
"mtu ambaye hupata hasira upesi"
Proverbs 29:23-24
mwenye roho ya unyenyekevu atapewa heshima
"Yahwe atasababisha watu kumheshimu mwenye roho ya unyenyekevu"
huyachukia maisha yake mwenyewe
"huwa na uadui kwake mwenyewe"
husikia laana na hasemi kitu
"hasemi neno hata baada ya watu kutoa laana juu yake"
Proverbs 29:25-26
kumwogopa mtu hufanya mtego
"mtu yeyote anayeogopa atakachotendewa na watu ni huwa kama mtego"
mtego
kitanzi ambacho hukamata wanyam kwa kamba
yeye ambaye anamtumaini Yahwe atalindwa
"Yahwe atamlinda yule ambaye anamtumaini"
wengi ambao huutafuta uso wa mtawala
"watu wengi wanataka mtawala wao awajali"
kutoka kwa Yahwe ni haki kwa mtu
Ni Yahwe anayetaka kuona kuwa watu wanatendewa kwa haki
Proverbs 29:27
chukizo
mtu anayepaswa kuchukiwa
Proverbs 30
Proverbs 30:1-3
Aguri...Yake...Ithiel...ukali
Haya ni majina ya watu
Aguri mwana wa Yake
Aguri ni mtoto halisi wa Yake, wala si mjukuu
kwa Ithiel, kwa Ithiel na ukali
"Hii ni kwa Ithiel, kwa Ithiel na ukali '
Hakika
"kweli" au "Hakuna shaka kwamba"
Mimi sina ufahamu wa wanadamu wala sima maarifa ya Mtakatifu
"Mimi sifahamu chochote ambacho wanadamu wanapaswa kuvifahamu
Proverbs 30:4
Ni nani ...chini?Ni nani...mikono?...Ni nani...kanzu? Ni nani....dunia?
"Hakuna mtu..."
mbinguni
ambako Mungu anaishi
kusanya upepo kwenye uwazi wa mikono yake
"kamata upepo katika mikono yake"
uwazi wa mkono yake
"mkono yake"
kusanya
rundika pamoja vitu vidogo vilivyotawanyika
imarisha miisho ya dunia yote
"ameweka mipaka ya ukomo wa dunia"
Jina lake ni nani, na jina la mwanae ni nani?
"niambie jina lake na jina la mwanae kama unawajua"
Hakika unajua!
"Sidhani kama unamjua mtu anayeweza kufanya mambo hayo"
Proverbs 30:5-6
limejaribiwa
"ni kama chuma cha thamani ambacho kimetolewa uchafu wote"
yeye ni ngao kwa wale wanaokimbilia kwake
"anawalinda wale wanaokuja kwake na kumwomba awalinde "
kuongeza katika maneno yake
kusema maneno mengine zaidi ya yale aliyosema
utathibitishwa kuwa
"atathibitisha kuwa ume.."
Proverbs 30:7-9
weka upuuzi na uongo mbali nami
"usiruhusu watu waongee upuuzi na uongo kwangu" au "usiniruhusu kuongea upuuzi na uongo"
upuuzi
uongo, maneno ambyo hana maana
usinipe umaskini wala utajiri
"usiruhusu niwe maskini sana wala tajiri sana"
kama nitapata vingi sana, nitakukataa wewe na kusema
Ni hali ya nadharia, msemaji si tajiri lakini inawezekana kuwa tajiri
kama nitakuwa maskini, nitaiba na kukufuru
Hii inaelezea hali ya nadharia ambayo haijatokea lakini inawezekana mwandishi akawa maskini
nitaiba na kukufuru jina la Mungu
"nitawafanya watu wanaojua kuwa nimeiba vitu wafikiri kuwa hakuna Mungu" au " Nitaharibu heshima ya Mungu kwa kuiba"
Proverbs 30:10
uzushi
kusema uongo juu ya mtu mwingine kwa kusudi la kumuumiza
atakulaani
mtumwa atakulaani
utakuwa na hatia
"watu wataona ni mwenye hatia"
Proverbs 30:11-12
kizazi ambacho kinalaani ...na hakibariki .....kizazi ambacho ni
"kizazi cha watu wenye kulaani ...na hawabariki ...kizazi cha watu ambao ni "
kizazi
aina au aina au kundi
ni safi machoni pao wenyewe
" huamini kuwa wapo safi"
hawajaoshwa uchafu wao
"Mungu hajawasamehe dhambi zao"
uchafu
takataka , siofaa
Proverbs 30:13-14
macho yao yameinuka...kope zao zimeinuka juu
watu ambao hudhani kuwa wao ni bora kuliko watu wengine.
kuna kizazi ambacho meno yao ni upanga, na taya zao ni visu, hivyo wanaweza kuwararua maskini ...na wahitaji
Watu wa kizazi ambao huongea vitu vibaya sana ,wanaongelewa mithili ya wanyama mwitu...wanawala maskini na wahitaji
taya
mifupa ya usoni ambapo meno huota
Proverbs 30:15-17
Mruba anao binti wawili
Huu ni mfano wa kuonesha uroho, kutaka vitu zadi kila mara "Uroho anao binti wawili"
mruba
ni aina ya mnyoo amba huganda kwenye ngozi na kunyonya damu
Wanalia "Nipe na nipe "
" kwa pamoja wote wanaitwa nipe mimi"
kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisemi "Yatosha"
"Kuna vitu vinne ambavyo havitosheki, ambavyo havisemi, "Yatosha"
ambavyo havitosheki
"daima vinataka zaidi"
ardhi ambayo haitosheki kwa maji
ardhi ambayo haizalishi tena chakula kwa sababu hakuna mvua imeongelewa kana kwamba mtu ambaye hana maji ya kutosha kwa kunywa
beza utiifu kwa mama
"humfikiria mama yake kuwa hana maana na hawezi hata kumtii"
macho yake ...tai
Mwandishi anatoa taswira mbili kwa namna inavyotokea kwa watu wanaofariki wakiwa mbali na makazi ya watu
macho yake yatadonolewa na kunguru wa bondeni
" kunguru wa bondeni watayadonoa macho yake"
kunguru
ndege weusi ambao hula mimea na mizoga ya wanyama
ataliwa na tai
"tai watamla"
tai
moja ya ndege wakubwa ambao hula mizoga ya wanyama
Proverbs 30:18-19
kuna vitu vitatu ambavyo ni ...vinne ambavyo sivifahamu
"kuna baadhi ya vitu vya kushangaza kwangu ambavyo sivifahamu -vinne ni ":
katika moyo wa bahari
"katikati ya bahari"
Proverbs 30:20
hula na kuufuta mdomo wake
...kufanya uzinzi na kisha kuoga.
Proverbs 30:21-23
chini ya vitu vitatu dunia hutetemeka, na chini ya vinne haiwezi kuvivumilia
"kuna baadhi ya vitu huifanya dunia kutetemeka, ambavyo haiwezi kuvivumilia, vinne katika hivyo ni:"
mpumbavu anaposhiba chakula
"Mpumbavu mwenye chakula cha kutosha"
mwanamke aliyechukiwa anapoolewa
"mwanamke ambaye watu wanamchukia anapoolewa" au "mwanamke aliyetengwa anapoolewa"
anapochukua nafasi ya bibi yake
anapotawala nyumba(kaya au familia)
Proverbs 30:24-26
wibari
wanyama wasio na mkia, wana masikio ya duara na miguu mifupi
Proverbs 30:27-28
mjusi
Reptilia mdogo mwenye miguu minne, mwili mrefu na mkia
Proverbs 30:29-31
Kuna vitu vitatu ambavyo ni ...vinne ambavyo fahari kwa namna ya kutembea kwake
"kuna baadhi ya vitu ambavyo hutembea kwa fahari. Vinne ya hivi ni :"
fahari
tukufu kama mfalme
jogoo aendaye kwa mikogo
kuku dume ambaye hutembea kwa kujidai
Proverbs 30:32-33
kusuka
chekecha kwa nguvu
siagi
maziwa ya wanyama ambayo yamesukuwa na kuwa mazito
Proverbs 31
Proverbs 31:1-3
Mfalme Lemueli
hili ni jina la mfalme
Mwanangu, ni nini? Mwana wa tumbo langu, ni kitu gani? Unataka nini, mwana wa nadhiri zangu?
1) "unafanya nini"? au " hupaswi kufanya hivyo unavyofanya sasa" 2) "sikiliza ninachokuambia" 3) "usifanye mambo ambayo nitakuonya dhidi yake."
mwanangu...mwana wa tumbo langu... mwana wa nadhiri zangu
msemaji anataka msikiaji atambue na kuheshimu msema anayezungumza.
mwana wa tumbo langu
tumbo linawakilisha mtu
mwana wa nadhiri zangu
1) nadhiri za ndoa ya mama 2) nadhiri baada ya ndoa yakuwa kama Mungu angeruhusu kupata mtoto angeli mweka wakifu kwa Mungu
usiwape wanamke nguvu zako
"usifanye juhudi sana ili kufanya ngono na wanawake" ama nje ya ndoa au kwa vimada
au njia zako kwa wale ambao huwaharibu wafalme
"au kuruhusu wale ambao huwaharibu wafalme kukushauri"
njia zako
"namna unavyoishi" au "kazi unayofanya"
wale ambao huwaharibu wafalme
labda ni mwanamke malaya
Proverbs 31:4-5
Lemueli
Hili ni jina la mtu
ambacho kimeamriwa
"ambacho Mungu ameamru" au "ambacho wafalme wameamru wenyewe"
### potosha\
"badilisha" au " pindisha" au "kana"
Proverbs 31:6-7
na mvinyo
" na mpe mvinyo"
katika uchungu wa dhiki
"ambao nafsi zao zinauchungu" au "ambao wapo katika mateso"
umaskini wake
"jinsi alivyo maskini"
taabu yake
"mambo mabaya ambayo yanatokea kwake"
Proverbs 31:8-9
ongea kwa ajili ya wale ambao hawawezi kuongea
"watetee wale ambao hawawezi kujitetea wenyewe"
kwa ajili ya madai ya wote ambao wanaangamia
"hivyo watu watende haki kwa wale wote wanaoangamia"
kwa ajili ya madai
"ongea kwa ajili ya madai" au "ongea kwa niaba ya"
watu maskini na wahitaji
"watu ambao ni mskini hawawezi kupata vitu ambavyo wanahitaji"
Proverbs 31:10-12
Ni nani anaweza kumpata mwanamke mwema?
"si wanaume wengi wanaoweza kumpata mwanamke mwema"
thamani yake ni kuu kuliko marijani
"anathamani kuliko marijani"
hatakuwa maskini
"daima atapata kile anachohitaji"
Proverbs 31:13-15
sufu
manyoya ya kondoo ambayo hutumika kutengeneza nguo
kitani
mmea ambao nyuzi zake hutumika kutengeneza nguo ya kitani
kwa furaha ya mikono yake
"hujisikia furaha kufanya kazi kwa mikono yake "
mfanya biashara
mtu anayenunu na kuuza
hugawa kazi kwa ajili ya mtumishi wake wa kike
"huwaambia watumishi wake wa kike kazi ambazo kila mmoja wao anapaswa kufanya kwa siku"
Proverbs 31:16-17
matunda ya mikono yake
"pesa alizopata"
yeye mwenyewe hujivika nguvu
"hujiandaa yeye mwenyewe kwa kazi nzito"
na huifanya mikono yake kuwa imara
"na huitia nguvu mikono yake kwa kufanya kazi yake"
Proverbs 31:18-19
huona
"huangalia kwa uangalifu"
usiku wote taa yake haizimika
"huwasha taa usiku kucha anapokuwa akifanya kazi"
kisokotea
fimbo nyembamba yenye ncha ambayo hutumika katika kutengeneza nyuzi
Proverbs 31:20-21
kwa mkono wake huwafikia maskini
"huwasaidia maskini"
kwa mkono wake huwafikia
angalia 31:18.
huvikwa nguo nyekundu
"nyekundu" haimaanishi rangi ya nguo lakini ni vazi la gharama na lenye joto. "kuwa na mavazi ya gharama na yenye joto "
nyekundu
rangi nyekundu, lakini yenye michirizi ya chungwa.
Proverbs 31:22-23
kitani
vazi ambalo limetengzwa kwa kitani
mume wake anajulikana
"mume wake anaheshiwa na watu"
anapoketi pamoja na wazee wa nchi
kutengeneza sheria na kusuruhisha kesi
Proverbs 31:24-25
kitani
vazi lililotengenezwa kwa kitani
mishipi
vipande virefu vya nguo huvaliwa kiunoni au kwenye bega moja
huvikwa nguvu na heshima
"kila mtu anaweza kumwona yupo imara na kwa hiyo wanamheshimu"
huucheka wakati ujao
"haogopi yatakayotekea wakati ujao"
Proverbs 31:26-27
hufumbua kinywa chake kwa ahekima
"hunena kwa busara"
sheria ya ukarimu ipo kwenye ulimi wake
"huwafundisha watu kuwa na ukarimu"
huangalia njia za nyumba yake
"huhakikisha kuwa familia yake yote inaishi katika njia ambayo inampendeza Mungu"
hawezi kula mkate wa uvivu
"siyo mvivu "
uvivu
kutofanya kazi yoyote na kuwa mzembe
Proverbs 31:28-29
huinuka na
husimama au hufanyakazi kwa juhudi
humwita aliyebrikiwa
"humpongeza"
umewapita
"umefanya vizuri zaidi kuliko"
Proverbs 31:30-31
madaha ni udanganyifu
"mwanamke mwenye huruma anaweza kuwadanganya watu" au "mwanamke mwenye tabia njema anaweza kuwa mwovu"
uzuri ni ubatili
"mwanamke ambaye ni mzuri sasa hawezi kuwa mzuri daima"
atasifiwa
"watu watamsifu"
matunda ya mikono yake
"pesa anazopata" angalia 31:13 na 31:16
kazi zake na zimsifu katika malango
"watu wakuu wa mji na wamsifu kwa kazi zake nzuri alizofanya"