Nahum
Nahum 1
Nahum 1:1
Maelezo ya jumla
Nahumu anaelezea uharibifu wa Ninawi katika shairi.
Maono kuhusu Ninawi.
Ujumbe kutoka kwa Mungu kuhusu mji wa Ninawi.
Mwelkoshi.
Mtu kutoka kijiji cha Mwelkoshi.
Nahum 1:2-3
Yahwe
Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale.
hatakuwa na namna ya kuacha kuwahesabia hatia adui zake
Hii inamaanisha kwamba Yahwe atawahukumu na kuwaadhibu adui zake wasipomtii yeye.
Nahum 1:4-5
Maelezo ya jumla
Nahumu anaendelea kueleza nguvu ya Yahwe juu ya dunia yote.
Milima hutetema kwenye uwepo wake, na vilima huyeyuka; dunia huanguka mbele zake
"Milima, vilima, na dunia humwogopa Yahwe"
hutetema
kama mtu ambaye ameogopa
huanguka
"hudondoka chini ya ardhi kwa woga"
Nahum 1:6
Maelezo ya jumla
Nahumu anaongea kuhusu uwezo wa Yahwe
ukali wa hasira yake
"nguvu ya hasira yake" au" kiwango (jumla au kiasi)cha hasira yake"
Ghadhabu yake imemwagwa kama moto, na miamba ameibomoa mbalimbali
kwa tafasiri nyingine ni : "humwaga hasira yake kama moto na kubomoa miamba kwa kuisambaratisha."
Nahum 1:7-8
boma
sehemu salama iliyojengwa kwa ajili ya ulinzi dhidi ya maadui
siku ya taabu
Wakati adui anapofanya shambulio. Kwa tafsiri nyingine: "Wakati mambo mabaya yanapotokea"
Nahum 1:9-11
Maelezo ya jumla
Nahumu anawaambia watu wa Ninawi jinsi ambavyo Yahwe atawashughulikia.
atakomesha
"kuacha kabisa kufanya"
taabu haitainuka mara ya pili
"Hatakushambulia kwa mara ya pili"
Watakuwa....chao
Nahumu anazungumza kwa Waisraeli kwa ufupi juu ya watu wa Ninawi.
watakuwa wamevurugika kama michongoma
"kabiliwa na matatizo mengi ambayo yatawazuia kuvamia"
wataharibiwa kabisa
Yahwe ataiharibu kabisa Ninawi yote
aliimarisha uovu
aliwahamasisha watu kufanya mambo maovu
Nahum 1:12-13
Maeleza ya jumla
Yahwe anazungumza kwa Waisraeli juu ya Ninawi.
Wananguvu ... watanyolewa... zao
watu wa Ninawi
hata hivyo watanyolewa
"Watakatwa." Yahwe anatumia picha ya kukata sufu kwenye kondoo kuonyesha njinsi atakavyo liharibu jeshi la Ninawi , hata kama wapo wengi.TN: " wataharibiwa "
nitaivunja ile nira ya watu kutoka kwako
TN: "nitakuweka huru kutoka ktika utumwa mwa watu hao"
nitaikata minyororo yako
"kata minyororo ambayo waliwafunga kama watumwa"
Nahum 1:14
Yahwe
"Yahwe" ni jina binafsi la Mungu ambalo alijifunua kwa Musa kwenye kichaka kilichowaka moto.
Nahum 1:15
juu ya milima kuna miguu ya mtu aletaye habari njema
"mtu analeta habari njema"
mtu mwovu
Nahumu anazungumza kwa watu wa Ninawi kana kwamba ni mtu mmoja.
ameondolewa kabisa
Nahumu anazungumza juu tukio la baadaye kana kwamba tayari limekwisha tokea.
Nahum 2
Nahum 2:1-2
Maelezo ya jumla:
Nahumu anaelezea uharibifu wa Ninawi katika shairi.
Yule ambaye atakuvunja vipande vipande
Ni namna ya picha ya mtu anayevunja chungu. TN: " Atakuharibu"
Yule ambaye atakuvunja
Mtu ambaye ni "Yule" hajawekwa wazi, kwa hiyo tafsiri inatumia kauli jumuishi: "mtu ambaye atakuvunja vipande vipande."
Linda kuta za mji, linda barabara, jitieni nguvu ninyi wenyewe, yakusanyeni majeshi yenu.
kujitayarisha kwa ajili vita
Linda kuta za mji
"Panga walinzi kwenye kuta kwa ajili ya kukinga"
Maana Yahwe anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli
Hii inamaana kuwa Yahwe atamfanya Yakobo na Israeli kuwa wakuu, na watu watawapenda tena.
wateka nyara
watu wanaoiba vitu kwa nguvu, mara nyingi katika vita
waliwaharibu
waliangamiza kila kitu.
kuharibu matawi ya zabibu zao
hapa taifa linaongelewa kana kwamba ni mzabibu uliolimwa. TN: " na kuling'oa taifa lenu kana kwamba ni shamba la mzabibu"
Nahum 2:3-4
mashujaa wake
askari wa mtu " ambaye takuvunja"Ninawi "vipande vipand":(2:1).
mivinje
aina ya mti ambao ubao wake unafaa kwa ajili ya silaha.
Magari ya vita yapo kasi kwenye mitaa
" madereva wa magari ya vita wanaendesha kwa fujo kwenye mitaa"
Yapo kama kurunzi
Hii inarejea kwenye mng'aro wa magari ya vita yanapoakisi mwanga kutoka kwenye jua.
Nahum 2:5-7
atakuvunja vipande vipande
rejea kwenye fasiri ya 2:1
anawaita maafisa wake
inaweza kumaanisha: 1. "anawakusanya maafisa wake" au 2. " anafikiria juu ya maafisa wake"
wana...kwao... hawa...
askari ambao wataushambulia Ninawi
katika kutembea kwao
"wanapotembea"
Nahum 2:8-10
nyara
Vitu vilivyoibiwa kwa nguvu, hasa katika vita.
hakuna mwisho wake
TN: "kuna kiasi kikubwa"
fahari ya vitu vyote vizuri vya Ninawi
inaweza kumaanisha: 1) "vitu tele vyote vizuri" au 2) "kiasi cha vitu vyote vizuri"
Moyo wa kila mtu unayeyuka
"Watu wote wamepoteza ujasiri wao"
Nahum 2:11-12
pango la simba
Ninawi inalinganishwa na pango la simba kwa sababu ni sehemu ambayo wauwaji wanaishi na sehemu ambapo wanaweka vitu walivyoiba kutoka kwa watu waliowaua.
alirarua
"kabwa" simba wameng'ata makoo ya wahanga ili kuwazuia wasipumue.
kulijaza pango lake mawindo, makao yake kwa mizoga iliyoraruliwa
Mafungu haya mawili yanasema jambo jambo moja kwa njia tofauti. Pango ni sehemu ya simba kujificha, mara nyingi huwa ni shimo.
Nahum 2:13
Tazama
"Fahamu hili"
upanga utateketeza simba wenu vijana
"askari wenu watakufa vifo si vya kawaida"
upanga
"askari mwenye upanga"
utateketeza
"kuwala wote"
simba wenu vijana
"vijana wenu wenye ubora"
Nitazuia nyara zenu kutoka kwenye nchi yenu
Neno "nyara" linarejea utajiri ambao Ninawi alipatia kutoka kwenye nchi zingine.Hii inamaanisha Yahwe ataharibu uwezo wa Ninawi wa kuiba kutoka katika mataifa mengine.
Nahum 3
Nahum 3:1-2
Maelezo ya jumla
Nahumu anaendelea kuelezea uharibifu wa Ninawi katika shairi ambalo lilianza kwenye 1:1.
mji uliojaa damu
Askari wa Ninawi waliwaua watu wengi. TN: "Mji unahusika juu vifo vya watu wengi"
Nahum 3:3-4
marundo ya maiti, mafungu makubwa ya miili; hakuna ukomo wa miili
Mwandishi anaweka mkazo wa mauaji mengi dhidi ya Ninawi ambopo jambo hili limetajwa mara tatu (3)
maiti
Miili ya watu ambao wamekufa
hakuna ukomo wa miili
"kuna idadi kubwa ya miili"
kahaba mzuri, mzoefu wa uchawi
Kama vile makahaba wanavyouza kiburudisho cha kimwili na wachawi huuza maarifa na nguvu zilizopatikana kwa miujiza, watu wa Ninawi nao huuza watu waliowachukua katika vita na kujipatia faidi kwa dhambi yao.
Nahum 3:5-7
Tazama
Neno hili linavuta usikivu kwa kile kinachokuja baadaye.
ni nani ataomboleza kwa ajili yake?' Ni wapi ninaweza kumpata mtu wa kukufariji?
TN: "hakuna mtu atayelia kwa ajili yake, na siwezi kupata mtu wa kumfariji."
Nahum 3:8-9
Maelezo ya jumla
Nahumu anaongea kwa watu wa Ninawi kana kwamba wao ndiyo mji wenyewe.
je wewe ni bora kuliko Noamoni...yenyewe?
TN: "Ninyi si bora zaidi ya Noamoni...yenyewe."
Noamoni
mji mkuu wa zamani wa Misiri, ambao Waashuru waliuteka.
ambao ulinzi wake ilikuwa bahari, ambao ukuta wake ilikuwa bahari yenyewe
Haya mafungu mawili ya maneno yana maana zenye kufanana. Maneno "bahari" yana maana ya mto Nile ambao ulitiririka karibu kwenye mji na kusababisha ugumu wa kushambuliwa.
ulinzi... ukuta
Miji ya zamani ilikuwa na "kuta" kubwa ili kuwazuia washambuliaji, na mstari wa mbele wa walinzi kuwazuia maaduai wasiufikie ukuta.
Nahum 3:10-11
Maelezo ya jumla
Nahumu anaongea kwa watu wa Ninawi kana kwamba wao ndiyo mji wenyewe
Lakini
Huu ni mwendelezo wa kulinganisha Ninawi na Noamoni tangu 3:8. Inaweza kumaanisha: "japo kuwa" au "hata kama"
Noamoni
mji kuu wa azamani wa Misiri, ambao Waashuru waliuteka
alikwenda...wake
Noamoni
walivunjwa vipande vipande
Wavamizi waliwaua watoto wa Noamoni kwa urahisi kama kwamba wanavunja chungu cha udongo.
walifungwa minyororo
weka katika utumwa. TN: "wakawa watumwa"
Nahum 3:12-13
Maelezo ya jumla
Nahumu anaongea kwa watu wa Ninawi kana kwamba wao ndiyo mji wenyewe.
Ngome
Neno hili, ambalo lingeweza kutafsiriwa kama " ngome ya jeshi" inarejea milki yote ya Ninawi na Ashuru.
Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva mapema: kama zikitikiswa, zitaangukia kwenye kimywa cha mlaji
Mji wa Ninawi utachukuliwa kwa urahisi kama tunda kutoka kwenye mti.
watu miongoni mwenu ni wanawake
"watu wako ni dhaifu na hawawezi kujilinda wao wenyewe"
bawaba zake
Mihimili mikubwa ya mbao ambayo ilishikilia mageti na haikuwezekana kufungua ukiwa nje ya mji. Kuchomwa moto kwa mihimili kulifanya isiwezekane kufunga mji tena.
Nahum 3:14-15
Maelezo ya jumla
Nahumu anaongea kwa watu wa Ninawi kana kwamba wao ndiyo mji wenyewe.
Utateketezwa kama nzige wachanga wanavyoteketeza kila kitu
uharibifu utaharibu kama nzige wanavyoteketeza kila kitu katika njia yao.
utakuteketeza
ni "moto" au "upanga"
Ninyi wenyewe mjitengeneze kuwa wengi kama nzige wachanga, na wengi kama nzinge waliopevuka
nzinge waliopevuka-"Mujizidishe wenyewe kama tunutu! Mujizidishe wenyewe kama nzige waliopevuka!" pengine haya ni maneno ya kuanza aya mpya.
Ninyi wenyewe mjitengeneze kuwa wengi kama nzige wachanga
Maana yake watakuwa mji mkubwa sana wenye watu wengi na wataharibu nchi nyingi.
Nahum 3:16-17
Maelezo ya jumla
Nahumu anaongea kwa watu wa Ninawi kana kwamba wao ndiyo mji wenyewe.
Umezidisha wafanyabiashara wako zaidi kuliko nyota mbinguni
Wafanyabiashara wa Ninawi hawawezi kuhesabika kama nyota katika anga. TN:"Unawafanyabiashara zaidi kuliko uwezo wa mtu kuhesabu."
wafanyabiashara
"wachuuzi" au "watu wanaonunua na kuuza vitu"
Wafalme
Neno linalotumiwa katika siasa "Viongozi"
wakuu wenu wa majeshi
Neno linalotumiwa katika jeshi "viongozi"au mamlaka zingine za kiserikali
Nahum 3:18-19
wachungaji
"wachungaji" hawa ni watawala wa watu wa Ashuru.
Ni nani aliyejiepusha kwa uovu wako wa daima?
TN: "Mfululizo wa matendo yenu maovu yamewaumiza watu wengi na mataifa"