Zechariah
Zechariah 1
Zechariah 1:1-3
Katika mwezi wa nane
Huu ni mwezi wa nane katika kalenda ya Kiyahudi. Katika kalenda ya sasa ni mwishoni mwa Octoba na mwanzoni mwa Novemba.
mwaka wa pili wa kumiliki kwake Dario
"mwaka wa pili tangu Dario alipokuwa mfalme"
Neno la Yahwe lilikuja
"Yahwe alinena neno lake"
Berekia...Ido
Haya ni majina ya wanaume.
Yahwe alikuwa na hasira sana juu ya baba zenu
"Kuwakasirikia sana babu zenu"
Nirudieni
Neno "rudi" inamaanisha mabadiliko. Yahwe anawaambia watu wa Israeli kubadilika kutoka kutokumtii na kumtii.
asema Yahwe wa majeshi
Kifungu hiki mara kwa mara kitafasiriwa kama "asema Yahwe" katika UDB. Na kirai hiki kimetumika sana katika kitatu cha Zakaria.
Nitawarudia ninyi
Kwa kusema atawarudia watu wa Israeli, Yahwe anasema watakuwa na mambo mema yakitokea kwa sababu atakuwa akiwasaidia.
Zechariah 1:4-6
walilia
"kupiga kelele"
Kugeuka kutoka
"kubadilika"
Lakini hawakuweza kusikia wala kunijari
Vifungu hivi vyote vinamaanisha watu wa Israeli wasingeweza kutii maagizo ya Yahwe.
asema Yahwe
Kifungu hiki mara kwa mara kitafasiriwa kama "asema Yahwe" katika UDB. Na kirai hiki kimetumika sana katika kitabu cha Zakaria.
Wako wapi baba zenu? Na manabii, je wapo hapa daima?
Maswali haya yote yameulizwa kuonesha kwamba kwa kweli watu wanakufa.
Lakini maneno yangu na maagizo niliyowaamru watumishi wangu manabii, je hayakuwapata baba zenu?
Maswali haya yametumika kuonesha watu wa Israeli kwamba kila jambo ambalo Bwana alikuwa amewaambia manabii wake kuwaonya babu zao, yalikuwa yametimia.
Maneno yangu na amri zangu
Hii yote inaonesha Mungu aliyokuwa ameyasema kwa manabii.
kuwapata baba zenu
Yahwe anazungumzia unabii wake kama vile unawakimbilia babu zao ili uwapite. Neno "kupata" lamaanisha kuwapita
matendo na njia zetu
"mwenendo na matendo yetu"
Zechariah 1:7-9
Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, ndiyo mwezi wa Shebati,
siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, ndiyo mwezi wa Shebati** - "Shebat" ni mwezi wa kumi na moja katika kalenda ya Kiebrania. Siku ya ishirini na nne ni sawa na karibu katikati ya mwezi wa pili katika kalenda ya sasa.
Neno la Yahwe lilikuja
Yahwe alisema neno lake
Berekia... Ido
Haya ni majina ya wanaume.
miti ya mihadasi
ni aina ya miti midogo yenye maua yenye rangi.
Zechariah 1:10-11
Hawa ni wale... Walijibu
Maneno "hawa" na "wale" inamaanisha farasi kati ya miti ya mihadasi
kuzunguka duniani
Maana yaweza kuwa: 1) "kuiangalia dunia yote" au 2) "kutembea duniani mwote"
kati ya miti ya mihadasi
ni aina ya miti midogo yenye maua yenye rangi
dunia yote imetulia na kustarehe
"watu wote duniani walikuwa na amani"
imekaa na kuwa na amani
Vifungu vyote vinamaanisha kuweza kutulia pasipo na cha kuogopa.
Zechariah 1:12-13
imeteswa na kudhurumiwa
Maana pendekezwa 1) "umekuwa na hasira juu(UDB) au 2) "imekuwa ikitendewa bila heshima"
nena nami, kwa maneno mazuru, maneno ya faraja
Vifungu hivi vinazungumzia maneno ambayo ni mema na ya faraja.
Zechariah 1:14-15
Nami nina hasira juu ya mataifa yaliyo na utulivu
Nimekarishwa sana na mataifa yanayofurahia amani na usalama"
Nilikasirika kidogo tu
"Nilikuwa na hasira kidogo tu na watu wa Yuda"
Zechariah 1:16-17
Nimeirudia Yerusalemu kwa rehema nyingi
Kurudi Yerusalemu inamaanisha kuchukua tena jukumu la kuwaudumia watu wa Israeli kama mfalme kurudi kuwaongoza watu kutoka katika shida.
Nyumba yangu itajengwa ndani yake
"Hii inamaanisha kujengwa tena kwa hekalu katika Yerusalem"
hili ni tamko la Yahwe wa majeshi
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe." Na kifungu hiki kimetumika mara kwa mara katika kitabu hiki.
Kipimo kitanyoshwa juu ya Yerusalemu
"Yerusalemu itakaguliwa kabla ya kujengwa"
Miji yangu kwa mara nyingine itajawa na uzuri
Yahwe anamaanisha mambo mema atakayoyafanya kwa ajili ya watu wake Israeli kama ambavyo kimiminika kinavyoweza kujaa katika miji na kufurika.
Yahwe ataifariji tena Sayuni
"Yahwe atawatia moyo watu wa Israeli"
Zechariah 1:18-19
Maelezo ya Jumla:
Zakaria anaendelea kuelezea ono lake
Niliinua macho yangu
Kifungu hiki kinamaanisha kuelekeza kichwa chako katika kutazama
pembe ziliyoitawanya Yuda
Hii inawakilisha majeshi yaliyowashambulia watu wa Israeli.
Zechariah 1:20-21
Maelezo ya Jumla:
Yahwe anaendelea kuelezea maono ya Zakaria kwa ajili yake.
Wafua chuma
Watu wanaofanya kazi ya kutengeneza vitu kutokana na chuma. Wanatumika kumaanisha upanga wa jeshi.
Pembe zilizomsambaratisha Yuda
Hawa ni majeshi yaliyoishambulia Yuda
Hakuna mtu angeinua kichwa chake
Hii inamaanisha mtu anayeogopa kutazama kitu kinachomwogopesha.
Kuwaondoa
"kuondoa hayo mataifa"
kuzitupa pembe chini
"kuwashinda maadui"
kuinua pembe yoyote
hii inamaana ya kupuliza pembe ili kuliamuru jeshi.
Zechariah 2
Zechariah 2:1-2
Maelezo ya Jumla:
Zakaria anaendelea kuelezea maono yake.
Niliinua macho yangu
"Nilitazama juu"
kipimo cha kupimia
kamba yenye urefu fulani inayotumika kwa kupima vitu vikubwa.
Hivyo aliniambia
"Hivyo mtu mwenye kamba ya kupimia aliniambia"
Zechariah 2:3-5
malaika mwingine akaenda kukutana naye
Huyu ni malaika mwingine ambaye hajawai kutokea hapo mwanzo, na hivyo anatambulishwa kama mshiriki mwingine.
Malaika wa pili akamwambia, "Nenda uongee na mtu yule
Malaika mwingine alimwambia malaika aliyekuwa ameongea na Zakaria, "Nenda haraka uongee na mtu mwenye kipimo"
Yerusalemu inakaa katika nchi wazi
Kifungu hiki kinamaanisha kwamba Yerusalemu haitazungukwa na kuta.
kuwa kwake ukuta wa moto kumzunguka
Yahwe anasema atailinda Yerusalemu na kulinganisha ulinzi wake na ukuta wa moto.
Hili ni tamko la Yahwe
Kifungu hiki wakati mwingine kinatafasiriwa kama asema Yahwe.
Zechariah 2:6-7
Kimbieni! kimbieni!
Maneno haya yamerudiwa na yanaonesha umuhimu kwa ujumbe unaofata. Umetumika mara mbili kwa sababu ujumbe ni mhimu sana.
nchi ya kaskazini
Inamaanisha Babeli
nimewatawanya kama pepo nne za anga
Hii inamaanisha watu wa Israeli wako mbali mmoja kwa mwingine. Pepo nne zinamaanisha sehemu mbalimbali za dunia.
binti Babeli
Hii inamaanisha mji mkuu wa Babeli.
Zechariah 2:8-9
Maelezo ya Jumla:
Zakaria anasema jinsi Yahwe anavyomtuma kuwahukumu mataifa walioiteka Yerusalemu.
Kuwateka ninyi
"kuiba vitu kutoka Yerusalemu baada ya kuwa imeshambuliwa"
maana kila akugusaye
"Kugusa" inamaanisha kudhuru
mboni ya jicho la Mungu
mboni ya jicho inamaanisha sehemu nyeusi katika jicho inayomwezesha mtu kuona. Hii ni sehemu muhimu sana katika mwili wa mtu. Hii inaonesha kwamba Yerusalemu ni ya muhimu sana kwa Mungu na ni kitu ambacho Mungu atakilinda.
tikisa mkono wangu juu yao
hii ni ishara inayotumika kuonesha Mungu amechagua Kuharibu jambo fulani.
na watakuwa mateka
Miji yao imeharibiwa tiyari na imeachwa wazi kwa watu kuiba chochote watakacho.
Zechariah 2:10-11
binti Sayuni
Hili ni jina lingine kwa Yerusalemu linalorejerea kwa mji kama binti wa mji wa Sayuni ya mbinguni.
kupiga kambi
kuweka mahema na kuyatumia
Hili ni tamko la Yahwe
Kifungu hiki wakati mwingine kinatafasiriwa kama asema Yahwe
mataifa watajikusanya kwa Yahwe
"mataifa yatamtii Yahwe"
katika siku hiyo
"kwa wakati ule"
Zechariah 2:12-13
Yahwe atamiliki... katika nchi takatifu
"Yahwe ataifanya Yuda mali yake ya nchi takatifu"
miili yote
Yahwe anarejerea kwa viumbe hai wote kwa kuwaita miili. Mwili ni kitu walichonacho viumbe wote.
maana ameinuka kutoka mahali patakatifu pake
Hii inamaanisha Yahwe kusababishwa kuchukua hatua juu ya nchi.
Zechariah 3
Zechariah 3:1-3
Maelezo ya Jumla:
Yahwe anamwonesha ono Zakaria
Je! hiki si kinga kilichotolewa motoni?
"Yoshua ni kama ukuni uliotolewa motoni"
kinga kilichotolewa motoni
Kinga ni kipande cha ukuni uwakao kinachotolewa motoni kabla hakijaisha. Hii inamrejerea Yoshua, aliyeokolewa kutoka mateka ya Babeli na kurudi Yerusalemu.
mavazi machafu
katika ono hili mavazi yanatumika kama alama ya kuonesha dhambi.
Zechariah 3:4-5
kukuvalisha vazi safi
Hapa vazi safi linatoa alama ya utakatifu.
kilemba
kipande cha nguo kinachozungushwa kichwani
Zechariah 3:6-7
alimwagiza Yoshua kwa dhati
"alimwagiza Yoshua katika hali ya kuzingatia kwa dhati"
takwenda katika njia zangu
Inamaanisha kutembea katika mapenzi yake.
kama mtatunza maagizo yangu
"ikiwa mtakumbuka na kutii maagizo yangu"
linda nyua zangu
"kuwajibika kwa maeneo yake maalumu"
Zechariah 3:8-9
Maelezo ya Jumla:
Malaika wa Yahwe anaendelea kuengea na Yoshua.
wenzako wanaoishi nawe
"makuhani wengine wanaoishi nawe"
mtumishi wangu tawi
Jina "tawi" linapaswa kutafisiriwa vilevile kama tawi la mti. Inamaana kuwa mtumishi wa Yahwe atakuja kutoka kwa Yahwe kama tawi litokavyo katika mti.
macho saba
Hizi ni pande saba.
chonga
"chora"
andishi
maneno yaliyoandikwa juu ya kitu fulani au kukatwa katika kitu fulani
hili ni tamko la Yahwe wa majeshi
Kifungu hiki mara nyingi hufasiriwa kama "asema Yahwe"
Zechariah 3:10
katika siku hiyo
"katika wakati huo"
hili ni tamko la Yahwe wa majeshi
Kifungu hiki mara nyingi hufasiriwa kama "asema Yahwe"
Zechariah 4
Zechariah 4:1-3
kuniamsha kama mtu aamshwavyo usingizini
"kunifanya kuwa na hadhari kama mtu aliyeamshwa usingizini"
vinara vya taa
sehemu za taa vinavyowashwa moto
upande wa kushoto
"upande wa kushoto wa bakuri"
Zechariah 4:4-5
malaika, malaika mkuu
Malaika ni kiumbe wa kiroho aliyeumbwa na Mungu. Malaika wanaishi kwa kumtumikia Mungu kwa kufanya chochote anachowaambia kufanya. Jina "malaika mkuu" linamhusu malaika anayetawala au kuwaongoza malaika wote. . Neno "malaika" kwa kawaida linamaanisha "mjumbe". . Neno "Malaika mkuu" linamaanisha "mjumbe mkuu." Malaika pekee aliyetajwa kama "malaika mkuu" katika Biblia ni Mikaeli. .Katika Biblia, malaika watoa ujumbe kutoka kwa Mungu. Jumbe hizi zinahusisha maelekezo jinsi Mungu alivyotaka watu wafanye.
Pia malaika waliwaambia watu juu ya matukio yaliyokuwa yatendeke au yametendeka. Malaika wanamamlaka ya Mungu kama wawakilishi wake na wakati mwingine walizungumza katika Biblia kama vile Mungu mwenyewe alikuwa akiongea. Njia nyingine malaika wanatumika kwa kuwalinda na kuwatia nguvu watu Kirai maalumu, "malaika wa Yahwe" kina maana zaidi ya Moja: 1) Malaika anayemwakilisha "malaika anayemwakilisha Yahwe" au "mjumbe anayemtumikia Yahwe" 2)Yaweza kumhusu Mungu mwenyewe, anayeonekana kama mwanadamu alipoongea na mtu. Pengine moja kati ya maana hizi yaweza kuelezea matumizi ya "mimi" na malaika kama vile Mungu Mwenyewe alikua akiongea.
bwana(lord), bwana(master), bwana(sir)
Neno "bwana" linamaanisha mtu mwenye umiliki au mamlaka juu ya watu.
Neno hili wakati mwingine linatafasiriwa kama "bwana"(master) linapomweleza Yesu au linapomtaja mtu anayemiliki watumwa. Baadhi ya matoleo ya Kiingereza yanalitafasiri kama bwana(sir) katika mazingira ambapo mtu kwa heshima anamtaja mtu mwenye cheo cha juu.
Jua, maarifa, kutambulisha
"Kujua" inamaanisha kufahamu kitu au kuwa na habari juu ya ukweli. "kujulisha" inamaanisha kusema habari.
Neno "maarifa" lahusu habari anayoijua mtu. Yaweza kujua jambo katika ulimwengu wa roho au mwili. "kujua kuhusu" Mungu yamaanisha kufahamu ukweli kumhusu yeye kwa sababu ya yaliyofunuliwa. "Kujua" Mungu inamaanisha kuwa na uhusiano naye. Hii pia inahusu kuwafahamu watu wengine. Kujua mapenzi ya Mungu yamanisha kufahamu alichokiagiza, au kufahamu anachotaka mtu afanye. "Kujua sheria" kujua alichokiagiza Mungu au kufahamu alichokielekeza Mungu katika sheria ya Musa. Wakati mwingine "maarifa" inatumika kama mbadala wa "hekima," inayohusisha kuishi katika hali inayompendeza Mungu. "Maarifa ya Mungu" wakati mwingine inatumika kama mbadala wa "hofu ya Yahwe."
Zechariah 4:6-7
Taarifa ya Kuunganisha:
Malaika alinayeongea na Zakaria anaendelea kuelezea ono.
Zerubabeli
Hili ni jina la mwanamme
Siyo kwa nguvu au uwezo
Maana pendekezwa 1) neno "uwezo" na "nguvu" kimsingi lamaanisha jambo lilelile na linasisitiza nguvu ya Zerubabeli, au 2) kwamba neno "uwezo" linamaanisha nguvu za kijeshi na neno "nguvu" linaonesha uwezo wa kimwili wa Zerubabeli.
U nani wewe, mlima mkubwa?
Yahwe anauliza swali hili kwa mlima kuonesha kwamba Roho wa Yahwe, wala siyo mlima ananguvu zaidi ya kumshinda Zerubabeli.
atalishusha jiwe la juu
jiwe la juu ni jiwe la mwisho linalowekwa kitu kinapojengwa.
Zechariah 4:8-11
Taarifa ya Kuunganisha:
Malaika alinayeongea na Zakaria anaendelea kuelezea ono
Neno la Yahwe lilikuja
"Yahwe alisema neno lake"
Mikono ya Zerubabeli... mikono yake itaimaliza
Zerubabeli anasimamia ujenzi wa hekalu. Kujenga kunatajwa kama "mikono yake" japokuwa yawezekana mikono yake isiweke mawe.
kuweka msingi
Msingi ni chanzo cha jengo na sehemu ya kwanza ya mradi wa ujenzi.
Ni nani aliyezarau... mambo madogo?
Swali hili haliitaji jibu ila linawaambia wasizarau "siku ya mambo madogo."
siku ya mambo madogo
Kifungu hiki ni jina kwa ajili ya wakati ambapo kila siku kazi rahisi zilifanywa. Muda wote wa ujenzi wa jengo unatajwa kama siku moja japokuwa ilichukua miaka kadhaa kukamilika.
Jiwe la kupimia
Jiwe linalounganishwa na kamba. Linatumika kuamua kama kuta za jengo zimenyooka au hapana.
taa saba ni macho ya Yahwe
Hizi taa saba ni alama za macho ya Yahwe.
macho ya Yahwe
Neno "macho" linamtaja Mungu akiona kwa sababu macho hutumika kwa kuona.
Zechariah 4:12-13
mirija miwili ya dhahabu
"imetengenezwa kwa dhahabu"
Je! wafahamu hivi ni nini?
"Unapaswa kujua hivi ni nini, lakini haujui."
Zechariah 4:14
Hawa ni wana wa mafuta mabichi ya mizeituni
Hii ni njia ya kishairi ya kusema, "watu waliotiwa mafuta"
simama mbele
Taarifa hii inawakilisha wazo la kutumikia.
Zechariah 5
Zechariah 5:1-2
Kisha niligeuka
Neno "Mimi" linamtaja Zakaria.
kuinua macho yangu
Hii inamaanisha kuangalia juu ya kitu fulani. Anasema "Niliinua macho" kwa sababu hii ni sehemu ya mwili mtu anayotumia kuona.
Tazama
Neno "tazama" linaonesha kwamba Zakaria alishangazwa na alichokiona.
dhiraa
Dhiraha ni sawa na sentimita 46.
Zechariah 5:3-4
Maelezo ya Jumla:
Malaika anaendelea kuongea na Zakaria.
anakwenda juu ya uso wa
Kifungu hiki kinahusu laana kama wingu linalosambaa kufunika uso wa nchi. Neno "uso" inahusu uso wa nchi kama uso wa mtu juu ya nyuso za kichwa chao.
kutegemea inachosema upande mmoja
"kutegemea na kile ambacho gombo limeandika upande mmoja"
kwa kadili ya maneno yao
Kifungu "maneno yao" kinamaanisha kile kilichosema katika nadhiri zao.
Nitaipeleka
Neno "hiyo" inahusu laana.
hili ni tamko la Yahwe wa majeshi
Kifungu mara nyingi kimefasiriwa kama "asema Yahwe. Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
nyumba
Hii inamaanisha familia ya mtu na kila anachokimiliki.
wa yule aapaye
"wa yule aapaye"
mbao
mti unaotumika kwa ujenzi.
Zechariah 5:5-7
Inua macho yako
Kifungu hiki kinamwamru mtu kutazama juu kwa kurejerea macho yake.
Kifuniko cha risasi
Hii inahusu kifuniko kizito. Risasi ni madini mazito.
kulikuwa na mwanamke chini yake amekaa ndani yake
Mwanamke asingeweza kutosha halisi ndani ya kikapu wa umbo hili.Japokuwa ono la Zakaria alitosha ndani ya kikapu. Mara nyingi maono ya maumbo ya vitu yanatiwa chumvi. Wote mwanamke na kikapu wanawakilisha mambo mengine.
Zechariah 5:8-9
Huu ni uovu
mwanamke anawakilisha uovu.
na upepo ulikuwa chini ya mbawa zao.
Kifungu hiki kinaeleza jinsi wanawake walivyotumia mbawa zao kuchukuliwa na upepo na kuruka.
walikuwa na mabawa kama mabawa ya korongo
Wanawake walikuwa na mbawa zilizoonekana kama za korongo. Huyu ni ndege mkubwa mwenye mabawa ya mita 2 hadi 4.
kati ya nchi na mbingu
Kikapu kiliinuliwa juu angani. Inasema "kati ya nchi na mbingu" kuvuta usikivu wao na kuonesha kikapu kilipokuwa kwa kwa kuwahusisha.
Zechariah 5:10-11
Wanapeleka wapi kikapu?
Wanawake wanapeleka wapi kikapu?
Ili kwamba hekalu litakapokuwa tiyari... katika msingi wake ulioandaliwa
"na wakati hekalu litakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa mahali palipoandaliwa"
Zechariah 6
Zechariah 6:1-4
inua macho yangu
Hii inamaanisha kutazama katika jambo fulani.
milima miwili iliyokuwa imetengenezwa kwa shaba
"milima miwili ilikuwa ya shaba"
kibandawazi cha kwanza ... kibandawazi cha pili.
"kibandawazi cha 1... kibandawazi cha 2"
Zechariah 6:5-6
Hizi ni pepo nne za mbinguni
Malaika anaeleza kwamba vibandawazi pamoja na farasi vinawakilisha pepo nne za mbinguni.
pepo nne
Neno "pepo" linamaanisha pande nne: kaskazini, mashariki, kusini, na magharibi. Walakini, baadhi ya matoleo mapya yanafasiri maneno haya ya Kiebrania kumaanisha "roho nne."
farasi weupe wanakwenda nchi ya magharibi
baadhi ya matoleo mapya yanafasiri maneno haya ya Kiebrania kumaanisha "farasi weupe wanatoka baada yao."
Zechariah 6:7-8
Wakawatamama
"Kutazama farasi weusi"
Zechariah 6:9-11
neno la Yahwe lilikuja
"Yahwe alinena neno lake."
Heldai, Tobiya, na Yediya... Yehosadaki
Haya ni majina ya wanaume.
Kisha uchukue fedha na dhahabu, ufanye taji
"Kisha tumia fedha na dhahabu kufanya taji.
Yoshua mwana wa Yehosadaki
Huyu siyo yule aliyekuwa msaidizi wa Musa; huyu ni kuhani mkuu ambaye ametajwa katika kitabu cha Hagai.
Zechariah 6:12-13
Kuongea naye na kusema
"Yahwe alimwambia malaika ili aongee na Zakaria na kusema"
jina lake ni tawi
Malaika wa Yahwe anampa jina hili Yoshua mfalme mpya.
atakuwa
Kifungu "kukua" ni neno la picha la tawi kuanza kuchipua.
kuinua utukufu wake
Maana pendekezwa: 1) "kuongeza utukufu wa hekalu" au 2)"inua na kuvaa utukufu wa hekalu yeye mwenyewe kama mtu angeweza kuvaa nguo"
ufahamu wa amani utakuwa kati ya vyote viwili
"wajibu wake wa mfalme na kuhani utaunganishwa."
Zechariah 6:14-15
Taji itawekwa katika hekalu la Yahwe
"Nitaweka taji yangu katika hekalu langu"
Taji
Neno "taji" inamtaja mfalme kama ambavyo mfalme angevaa taji.
iliwekwa katika hekalu la Yahwe
Hii inahusu mfalme pia akiwa kuhani, kama kuhani anatumika hekaluni.
Heldai, Tobiya, na Yedaya
Haya ni majina ya wanaume
kama kumbukumbu ya ukarimu wa mwana wa Zefania
Baadhi ya matoleo ya kisasa yanafasiri kifungu hiki "kama kumbukumbu kwa Heni, mwana wa Zefania" au "kama kumbukumbu kwa mwenye neema, mwana wa Zefania." Pia, baadhi ya matoleo ya kisasa yanafasiri neno "Heni" kumaanisha jina "Yosia."
walioko mbali
Hii inawahusu Waisraeli waliokuwa wamesalia Babeli.
hivyo utajua
Neno "wewe" inamaanisha watu wa Israeli.
sikilizeni kweli
"sikilizeni kwa uaminifu"
Zechariah 7
Zechariah 7:1-3
Mfalme Dario alipokuwa mfalme kwa miaka nne.
"katika mwaka wa nne tangu Dario awe mfalme"
siku ya nne ya mwezi wa Kisleu(ndio mwezi wa tisa)
"Kisileu" ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiebrania. Siku ya nne ni sawa na mwishoni mwa Novemba katika kalenda ya sasa.
neno la Yahwe lilikuja
"Yahwe alinena neno lake"
Shareza na Regemu Meleki
Haya ni majina ya wanaume.
walisema, "je! niomboleze... miaka?
Neno "wale" linamrejerea Shareza na Regemu Meleki.
katika mwezi wa tano
Wayaudu walifunga wakati wa sehemu ya mwezi wa tano wa kalenda ya Kiebrania kwa sababu huu ndio wakati Wababeli walipoliaribu hekalu la Yerusalemu. Mwezi wa tano ni wakati wa sehemu ya mwisho wa Julai na mwanzoni mwa Agosti katika kalenda ya sasa.
Zechariah 7:4-7
katika wa tano
"mwezi wa tano"
katika mwezi wa saba
Wayaudi waliomboleza wakati wa sehemu ya mwezi wa saba wa kalenda ya Kiebrania kwa sababu katika mwezi huu Wayaudi waliokuwa wamebaki Yerusalemu walikimbilia Misri baada ya kuuawa kwake Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua kuwa gavana juu ya Yuda. Mwezi wa saba ni wakati wa mwishoni mwa Septemba na mwanzoni mwa Oktoba katika kalenda ya sasa.
kwa miaka hii sabini
Watu wa Israeli walikuwa wamekuwa watumwa kwa miaka 70 huko Babeli.
mlipokula na kunywa
Kifungu hiki kinamaanisha walipokula na kunywa katika sherehe kuheshimu jinsi Yahwe alivyokuwa ameandaa kwa ajili yao.
Je ni kweli mlifunga kwa ajili yangu?
Swali linatumika kuwalaumu Waisraeli kwa kutomweshimu Yahwe walipofunga.
Je! hamkula na kunywa kwa ajili yenu wenywewe?
Swali linatumika kuwalaumu Waisraeli waliosherehekea sherehe kwa kutomweshimu Yahwe kwa sherehe zao.
Yahwe alisema kwa kinywa cha manabii wa zamani
Zakaria anarejerea manabii wa zamani kwa kurejerea sehemu ya mwili wao uliosema neno la Yahwe.
Haya hayakuwa maneno yaleyale... upande wa magharibi?
Swali hili laweza kuandikwa kama taarifa: "Haya yalikuwa maneno halisi yaleyale... upande wa magharibi."
Ilikaliwa
"waliishi ndani yake"
chini ya vilima
Hivi ni vilima kabla haujafika kwenye milima.
Zechariah 7:8-10
neno la Yahwe lilikuja
"Yahwe alinena neno lake."
Kila mtu na afanye hivi
Neno "hivi" inamaanisha jinsi mtu anavyopaswa kuhukumu.
mjane
mwanamke aliyefiwa mme
yatima
mtoto ambaye wazazi wake wamefariki
mgeni
Mtu aliyekatika nchi ya ugeni
kusiwa na mtu miongoni mwenu anayepanga madhara yoyote kinyume cha mwingine mioyoni mwenu.
"msifanye mipango ya kutenda uovu"
Zechariah 7:11-12
wakashupaza mabega yao
"walikuwa kama ng'ombe wanaokataa kuwekewa nira" au "walikuwa kama ng'ombe aliyekataa kutii"
waliziba masikio yao
"walikataa kusikia"
waliifanya migumu mioyo yao kama mwamba
"Walikataa kutii ujumbe wa Yahwe"
kwa kinywa cha manabii
"kupitia maneno ya manabii"
Zechariah 7:13-14
nitawatawanya kwa upepo wa kisurisuri
"nitawakusanya kamba kisurisuri kinavyosambaza majani"
kisurisuri
upepo wenye nguvu unaojisokota unaposafiri, ukisambaza vitu mbalimbali mahali pote.
Zechariah 8
Zechariah 8:1-3
Neno la Yahwe wa majeshi lilinijia kusema
Yahwe wa majeshi aliniambia
Nina huruma kwa ajili yake kwa hasira kubwa
"Nimejaa na hasira kwa ajili ya Sayuni"
mlima wa Yahwe wa majeshi
Hii inarejerea Mlima Sayuni.
Mlima mtakatifu
Hapa "Mtakatifu" yamaanisha "ni mali ya Yahwe."
Zechariah 8:4-5
iwe katika mitaa ya Yerusalemu
"kuwa inaishi Yerusalemu"
katika mikono yake kwa sababu amezeeka
Wasaa wa kuzeeka ni alama ya amani na mafanikio.
Na mitaa ya mji itajaa
Maeneo ya wazi ya mji yatakuwa yamejaa watu katika shughuli zao za kawaida.
Zechariah 8:6-8
Kama jambo haliwezekani katika mcho ya
"Ikiwa jambo fulani halionekani kuwezekana"
masalia ya watu hawa
"watu wa Yuda waliosalia"
Je! lisiwezekane pia machoni pangu?
Mungu anauliza swali hili ili kuwashawishi watu wake kuamini ahadi zake.
Hili ni tamko la Yahwe
Kifungu hiki kwa kawaida kimetafsiriwa kama "asema Yahwe. Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
Ninaelekea kuwakomboa watu wangu
"Niko karibu kuwakomboa watu wangu walikwenda uamishoni"
Zechariah 8:9-10
Msingi wa nyumba yangu ulipowekwa
"Msingi wa nyumba yangu ulipowekwa mahali pake" kwa "mlipokuwa mkijenga msingi wa nyumba yangu"
Itieni nguvu mikono yenu
"fanyeni kazi kwa bidii"
Maana kabla ya siku hizo
"Kabla hamjaanza kulijenga hekalu"
Hakuna mazao yaliyokusanywa ndani
"hakukuwa na mazao ya kuvuna"
Hakukuwa na faida kwa mtu wala mnyama
Haikuwa na faida kwa mwanadamu na wanyama wao kuilima nchi, kwa sababu hawakupata chakula kutoka ndani yake.
Zechariah 8:11-12
kama siku za kale
"kama katika wakati uliopita"
Nitakuwa pamoja na masalia ya watu hawa
"Sasa nitawabariki watu hawa" au "Sasa nitawatendea watu hawa kwa upole"
mbegu ya amani itapandwa
"Nitawafanya kuwa katika amani"
Hili ni tamko la Yahwe
Kifungu hiki kwa kawaida kimetafsiriwa kama "asema Yahwe. Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
nchi itatoa mazao yake
"kutakuwa na kuvuna kwema katika mashamba"
mbingu zitatoa umande wake
Umande kwa kawaida ilikuwa ni ishara ya mafanikio. Yaani "kuwatuwa na mvua nyingi"
kuyarithi yote haya
"kuwa na haya yote wakati wote"
Zechariah 8:13-15
Mlikuwa mfano wa laana kwa mataifa mengine
"Nilipowaadhibu, mataifa mengine yalijifunza"
Nyumba ya Yuda na nyumba ya Israeli
"Watu wa Yuda na Israeli"
Mikono yenu itiwe nguvu
"fanyeni kazi kwa bidii"
siwazuru
"kuwaadhibu"
kuchokoza hasira yangu
"kunikasirisha"
hakujuta
"hakuamua kuwaadhibu kidogo"
Zechariah 8:16-17
mnalopaswa kufanya
"Ninyi" inawarejerea watu wa Yuda.
Ongeeni kweli, kila mtu na jirani yake
"semeni kweli kwa kila mtu"
Hukumuni kwa kweli, haki, na amani malangoni penu
"Hukumuni kwa haki katika mahakama zenu ili watu waishi kwa amani.
wala msivutwe na nadhiri za uongo
Msikubaliane na watu wasemao uongo katika mashitaka mahakamani"
Hili ni tamko la Yahwe
Kifungu hiki kwa kawaida kimetafsiriwa kama "asema Yahwe. Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
Zechariah 8:18-19
Kisha neno la Yahwe wa majeshi likanijia mimi
"Mimi" inamrejerea Zakaria.
Mfungo wa mwezi wa nne
Wayaudi waliomboleza katika kipindi cha sehemu ya mwezi wa nne wa kalenda ya Kiebrania kwa sababu huu ulikuwa wakati Wababeli walipovunja ukuta wa Yerusalemu. Mwezi wa nne ni wakati wa mwishoni mwa Juni na mwanzoni mwa Julai katika kalenda ya sasa.
mwezi wa tano
Wayaudu walifunga wakati wa sehemu ya mwezi wa tano wa kalenda ya Kiebrania kwa sababu huu ndio wakati Wababeli walipoliaribu hekalu la Yerusalemu. Mwezi wa tano ni wakati wa sehemu ya mwisho wa Julai na mwanzoni mwa Agosti katika kalenda ya sasa.
mwezi wa saba
Wayaudi waliomboleza wakati wa sehemu ya mwezi wa saba wa kalenda ya Kiebrania kwa sababu katika mwezi huu Wayaudi waliokuwa wamebaki Yerusalemu walikimbilia Misri baada ya kuuawa kwake Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua kuwa gavana juu ya Yuda. Mwezi wa saba ni wakati wa mwishoni mwa Septemba na mwanzoni mwa Oktoba katika kalenda ya sasa.
mwezi wa kumi
Wayaudi waliomboleza wakati wa sehemu ya mwezi wa kumi katika kalenda ya Kiebrania kwa sababu huu ni wakati Wababeli walipoanza kuuhsusu Yerusalemu. Mwezi wa kumi ni mwishoni mwa Desemba na mwanzoni mwa Januari katika kalenda ya Magharibi.
Zechariah 8:20-22
Watu watakuja tena
"Watu watakuja tena Yerusalemu"
Watu wengi na mataifa yenye nguvu yatakuja
"Watu wengi watakuja, wakiwemo kutoka mataifa makubwa"
Zechariah 8:23
watashika pindo la vazi lenu
"watashika mavazi yenu kuvuta makini yenu"
Na twende nanyi
"Tafadhari tusafiri pamoja nanyi kwenda Yerusalemu"
Mungu yu pamoja nanyi
"Mungu yu pamoja nanyi watu"
Zechariah 9
Zechariah 9:1-2
Hili ni tamko la neno la Yahwe kuhusu
"Huu ni ujumbe wa Yahwe kuhusu"
Nchi ya Hadraki na Dameski
"Watu wa nchi ya Hadraki na mji wa Dameski
Kwa maana jicho la Yahwe lipo juu ya watu wote
"Maana Yahwe anamwangalia kila mtu" Lakini, matoleo mengi ya kisasa yanafasiri kifungu hiki kama "macho ya watu" na ya wale wa makabila yote ya Israeli yanamwangalia Yahwe."
Hamathi
"Watu wa nchi ya Hamathi"
Tiro na Sidoni
"Watu wa Tiro na Sidoni"
japokuwa ni wenye hekima sana
Pengine Zakaria hakumaanisha hakika kwamba watu wa Hamathi walikuwa wenye hekima.
Zechariah 9:3-4
amejijengea ngome
Hapa mji wa Tiro umepewa picha kama ya mwanamke.
kurundika fedha kama mavumbi na dhahabu safi kama matope mitaani
"kukusanywa kwa dhahabu na fedha nyingi mitaana kama mchanga "
Tazama! Bwana atamnyang'anya
"Iweni tayari! Bwana atachukua miliki za Tiro"
na kuharibu nguvu zake juu ya bahari
"na kuharibu meli za Tiro ambazo watu wanazitumia kupigana juu ya bahani"
hivyo ataharibiwa na moto
"na kuuteketeza mji hata mavumbini"
Zechariah 9:5-7
taona
"ataona Tiro ikiharibiwa"
Wageni watafanya makazi yao katika Ashidodi
"Wageni wataichukua Ashidodi na kufanya makao yao pale"
nami nitakiondoa kiburi cha Wafilisiti
"Nitawafanya Wafilisita wasijivune tena"
Nitaondoa damu yao katika vinywa vyao na machukizo yao kutoka kati ya meno yao
Hii inamaanisha nyama pamoja na ndamu ndani, na nyama iliyotolewa kwa vinyago. Yaani "Sitawaruhusu tena kula nyama pamoja damu ndani yake, na nitawazui kula chakula kilichotolewa kwa sanamu"
Zechariah 9:8
Nitaweka kambi karibu na nchi yangu
Mungu anaongea juu yake kama alikuwa jeshi.
Zechariah 9:9-10
Piga kelele kwa furaha, ewe binti Sayuni! Piga kelele kwa shangwe, ewe binti Yerusalem!
Mistari hii miwili inamaanisha jambo moja na inazidisha agizo la kufurahi.
binti Sayuni... binti Yerusalem
"Sayuni" ndiyo "Yerusalemu." Nabii anauzungumzia mji kanakwamba ni binti.
juu ya punda, juu ya mwanapunda
Vifungu hivi viwili kimsingi vinamaanisa jambo moja na vinamrejerea mnyama mmoja. Mstari wa pili unaweka wazi kwamba huyu ni mwanapunda.
kukatilia mbali kibandawazi kutoka Efraimu
"Kuharibu vibandawazi vitumikavyo kwa vita katika Israeli"
farasi kutoka Yerusalemu
"farasi wa vita katika Yerusalemu"
upinda utakatiliwa mbali kutoka katika vita
Hapa upinde unawakilisha silaha zote zitumikazo kwa vita. "Silaha zote za vita zitateketezwa"
Maana atanena amani kwa mataifa
Hapa tendeo la kutangaza amani linawakilisha tendo la kufanya amani.
utawala wake utakuwa kutoka bahari hata bahari, na kutoka katika mto hadi miisho ya dunia
"ufalme wake utakuwa juu ya dunia yote!"
Zechariah 9:11-13
Lakini kwenu
Hapa "ninyi" inamaanisha watu wa Israeli.
shimo ambalo halina maji
Shimo hapa linawakilisha uhamisho.
Rudini ngomeni
"Rudini katika nchi yenu mahali mtakapokuwa salama"
wafungwa wa tumani
Hii inamaanisha Waisraeli waliokuwa kifungoni waliokuwa bado wanamatumaini kwamba Mungu atawakomboa.
pinda Yuda kama upinde wangu
Watu wa Yuda wanatajwa kama walikuwa upinde uliobebwa na Mungu kwa vita.
kulijaza podo langu kwa Efraimu
Watu wa Israeli, ufalme wa kaskazini, wanatajwa kama walikuwa mishale ambayo Mungu angewapigia adui zake. Podo ni mfuko unaotunza mishale ya askari.
Nimewainua wana wenu, Sayuni, kinyume cha wana wenu, Ugiriki,
Mungu anazungumza na watu wa mataifa mawili tofauti kwa wakati mmoja.
Zechariah 9:14-15
Maelezo ya Jumla:
Sehemu hii ya unabii inaendelea na maneno ya Hosea, badala ya maneno ya Yahwe yaliyonenwa kupitia kwake.
Ataonekana kwao
Neno "wao" linamaanisha watu wa Mungu. Yaweza pia kuwa "taonekana angani kwa watu wake" au "atakuja kwa watu wake"
tapiga kelele kama radi
Wakati mwingine Waisraeli walidhani miale ya radi kama mishale aliyopiga Mungu.
piga tarumbeta
Tarumbeta ilikuwa ni pembe ya kondoo. Watu waliipuliza kama ishara ya vita au matukio mengine.
ataendelea na dhuruba kutoka Temani
Wakati mwingine Waisraeli walifikiri kwamba Mungu alikuwa akisafiri kwa upepo wa tufani utokao kusini.
atararua
"kushinda kabisa"
kuyashinda mawe ya kombeo
Waisraeli watawashinda askari wanaopigana kwa kutumia kombeo. Askari hawa wanawakilisha adui wote wa Israeli, haijarishi silaha walizonazo.
Ndipo watakapo kunywa na kupiga kelele kama mtu aliyelewa kwa mvunyo
"Watapiga kelele na kusherehekea ushindi wao kwa kelele kama walikuwa wamelewa."
watajazwa kwa mvinyo kama mabakuli
Pengine inamaanisha mabakuli makuhani waliyotumia kubeba damu ya mnyama katika madhabahu.
kama pembe za madhabahu
Madhabahu zilikuwa na pembe damu zilipokusanywa.
Zechariah 9:16-17
Maelezo ya Jumla:
Zakaria anaendelea kuongea na watu.
Ndipo watakapo kunywa na kupiga kelele kama mtu aliyelewa kwa mvunyo
"katika nchi yetu watakuwa kama mawe mazuri katika taji"
vijana watastawi juu ya nafaka
Vijana wataishi kwa chakula wanachopata kutoka katika mavuno.
na bikra juu ya divai tamu
Mabinti watafurahia mvinyo mpya. Hizi ni rejea kwa vijana wa kiume na kike wakiwakilisha hesabu ya watu wote wa Israeli
Zechariah 10
Zechariah 10:1-2
Maelezo ya Jumla:
Zakaria anaenelea kuongea na watu.
hufanya mvua ya miunguromo na dhoruba
"hufanya mawingu ya dhoruba"
sanamu uongea kwa uongo
"sanamu zinatoa ujumbe wa uongo"
waganga hunena uongo
"waganga wanaona maono ya uongo"
wanasema ndoto za udanganyifu
"waganga wanasema uongo kuhusu ndoto zao ili kuwadanganya watu"
wanapotea kama kondoo
"watu hawajui njia ya kufuata"
Zechariah 10:3
Gadhabu yangu inawaka dhidi ya wachungaji
"Wachungaji" wanawakilisha viongozi wa watu wa Mungu.
ni mabeberu - viongozi - nitakao waadhibu
"Mabeberu" wanawakilisha viongozi wasiofaa
Yahwe wa majeshi atalihudumia pia kundi la kondoo wake, nyumba ya Yuda
"Nitaiangalia nyumba ya Yuda"
kuwafanya kama farasi wake wa vita!
"Tawapa uwezo wangu wa nguvu isiyoogopesha"
Zechariah 10:4-5
Kutoka kwao litatoka jiwe kuu la pembeni
"Jiwe la pembeni litatoka kwao." Kiongozi mhimu anazungumzwa kama vile jiwe kuu la msingi wa jengo.
kutoka kwao kitatoka kigingi cha hema
"kigingi cha hema kitatoka kwao." Viongozi wakuu wanazungumzwa kama vile vigingi vikubwa vinavyolishikilia hema mahali pake.
kutoka kwao utatoka upinde wa vita
"upinde wa vita utatoka kwao." Viongozi wa kijeshi wanasemwa kama walikuwa upinde uliotumiwa vitani.
Watakuwa kama mashujaa
"Watakuwa wenye nguvu vitani"
wawakanyagao adui zao katika matope ya mitaani vitani
"wawashindao adui zao kwa ukamilifu"
nao watawaabisha wapanda farasi
"nao watawashinda adui zao wapiganao nao katika farasi"
Zechariah 10:6-7
Nitaitia nguvu nyumba ya Yuda
"Nitawaimarisha watu wa Yuda"
nyumba ya Yusufu
Hii inamaanisha watu wa ufalme wa Israeli kaskazini.
nilikuwa sijawaondoa
"Nilikuwa sijawakataa"
Efraimu atakapokuwa kama shujaa
"Efraimu" inarejerea ufalme wa Israeli ya kaskazini.
mioyo yao itafurahi kama kwa mvinyo
"nao watakuwa kweli na furaha sana
wana wao wataona na kufurahi. Mioyo yao itanifurahia!
"Wana wao wataona yaliyotokea na watafurahi kwa sababu ya yale Yahwe aliyowafanyia!
Zechariah 10:8-10
Nitawanong'oneza
kunong'oneza ni kutoa sauti ya juu, nyembamba kupitia midomo iliyominywa. Kwa kawaida hutolea kuwapa wengine ishara,
mpaka kutakapokuwa hakuna nafasi tena kwa ajili yao
Watu wataendelea kwenda Yuda na itajazwa watu hata kusiwe na nafasi ya watu kuishi pale tena.
Zechariah 10:11-12
Nitapita katika bahari ya mateso yao
Maandiko mara nyingi urejerea bahari kama picha ya shida na magumu mengi.
na nitavikausha vilindi vyote vya Nile
"Nitaufanya Mto Nile kukauka"
Utukufu wa Ashuru utashushwa chini
Hapa "utukufu wa Ashuru" pengine unamaanisha jeshi la Ashuru.
na fimbo ya Misri itakwenda mbali kutoka kwa Wamisri
"na nguvu ya Misri kutawala mataifa mengine itakwisha."
hili ni tamko la Yahwe wa majeshi
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
Zechariah 11
Zechariah 11:1-3
Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mielezi yako
Nabii anaongeza na nchi ya Lebaboni kama vile alikuwa ni mtu.
Omboleza, enyi miti ya misonobari, kwani mierezi imeanguka
"Ikiwa miti ilikuwa watu, ingelia kwa huzuni. Misonobari imebaki pekee kwa sababu mierezi imechomwa na kuanguka."
Ombolezeni, enyi mialoni ya Bashani, kwani msitu wenye nguvu umeshushwa.
"Ikiwa miti ya mialoni iliyoko Bashani ingekuwa watu, wangeomboleza, kwani msitu mzito umeangushwa."
Wachungaji wanapiga yowe
"Wachungaji wanalia kwa sauti"
kwa kuwa utukufu wao umeharibiwa
"Utukufu wao" pengine inawakilisha nyasi nyingi ambapo wachungaji walipeleka kondoo wao.
kwa kuwa kiburi cha Mto Yordani
"kwa sababu miti walipokaa kando ya Mto Yordani imeharibiwa."
Zechariah 11:4-6
Maelezo ya Jumla:
Hapa Yahwe anaanza kutoa maelekezo kwa Zakaria katika muundo wa mfano kuhusu wachungaji na kondoo.
wenyeji wa nchi
"watu wa nchi"
hivi ndivyo asemavyo Yahwe
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
kumwelekeza kila mtu katika mkono wa jirani yake
"kumfanya kila mtu kutawaliwa na mtu mwingine"
katika mkono wa mfalme wake
"katika utawala usio wa haki wa mfalme wake"
wataiharibu nchi
"hawatakuwa na huruma juu ya watu wa nchi"
hakuna hata mmoja wao nitakayemwokoa kutoka katika mkono wao
"lakini sitawaokoa watu wa Yuda kutoka katika nguvu zao"
Zechariah 11:7-9
Maelezo ya Jumla:
mfana kuhusu wachungaji na kondoo unaendelea.
kondoo walioamriwa kuchinjwa
"kundi la kondoo waliokuwa wamekusudiwa kuchinjwa"
gongo
gongo ni miti inayotumika kwa makusudi mbalimbali, ikiwemo kuwaongoza watu. Yaweza kuwa na aina mbalimbali za ncha.
upendeleo
Matoleo mbalimbali yanafasiri neno la Kiebrania katika mazingira haya kama "neema" na "uzuri"
Umoja
Hili ni wazo la udugu kati ya sehemu mbili za Israeli, ufalme wa kaskazini na ufalme wa kusini.
sikuwavumilia tena
"Sikuweza kuwavumilia tena wenye kondooo waliokuwa wamewaajiri"
Zechariah 11:10-12
Maelezo ya Jumla:
Mfano wa wachungaji na kondoo unaendelea
nikaivunja kuvunja agano nililokuwa nimelifanya na kabila zangu zote
Hapa nabii anaongea na kutenda kama Yahwe.
amesema
"alikuwa amesema kwao ujumbe"
vipande thelathini vya fedha
gramu 330 za fedha. Shekeli ilikuwa na uzito wa gramu kumi na moja.
Zechariah 11:13-14
Maelezo ya Jumla:
Mfano kuhusu wachungaji na kondoo unaendelea
hazina
vyumba vya kuhifadhi vitu katika hekalu la Yahwe
thamani nzuri zaidi
Hii inamaanisha kwamba thamani hii ilikuwa ndogo sana kwa mchungaji aliyekuwa akaifanya kazi ya Yahwe.
vipande thelathini vya fedha
gramu 330 za fedha. Shekeli ilikuwa na uzito wa gramu kumi na moja.
Zechariah 11:15-16
Maelezo ya Jumla:
Mfano wa wachungaji na kondoo unaendelea.
kondoo walionona
Kondoo mwenyew afya, aliyekua vizuri.
atapasua kwato zao
pengine kama tendo la ukatili
Zechariah 11:17
Maelezo ya Jumla:
Mfano wa wachungaji na kondoo unaendelea.
Ole kwa wachungaji wasiofaa
"Huzuni ya namna gani inamsubiri mchungaji huyu asiyefaa"
uje dhidi ya mkono wake na jicho lake la kulia
"jereha mkono wa kulia na kuchomwa jicho la kulia"
Upanga na uje dhidi ya
"upanga" hapa unawakilisha adui watakao mshambulia mchungaji
mkono wake
nguvu ya kupigana
jicho lake la kulia
uwezo wa kuona wakati akipigana.
Zechariah 12
Zechariah 12:1-3
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaanza sehemu inayozungumzia shambulio lijalo dhidi ya Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa mji.
tamko la neno la Yahwe
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
azitandaye mbingu
"aliyeumba anga"
kuweka msingi wa dunia
"kuiweka dunia yote mahali pake"
aiumbaye roho ya mtu ndani yake
"aliumba roho ya mtu"
kikombe
"kikombe cha kitu cha kunywa"
kiwafadhaishacho watu wote wamzungukao
Hii ni, kinywaji ni pombe itakayowafanya majeshi wanaoishambulia Yerusalemu kulewa na kushindwa kupigana.
yeye
Huo ni, mji wa Yerusalemu. Ilikuwa kawaida kwa kiebrania kuzungumzia mji au nchi kama ni mwanamke.
jiwe zito kwa watu wa jamaa zot
"kisichowezekana kuondolewa"
Zechariah 12:4-5
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaendelea na sehemu inayozungumzia shambulio lijalo dhidi ya Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa mji.
siku hiyo
Siku majeshi yatakapoishambulia Yerusalemu.
Hili ni tamko la Yahwe
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
Nitaiangalia kwa upendeleo
"Nitailinda"
nyumba ya Yuda
"watu wa Yuda"
wasema mioyoni mwao
Inamaanisha kwamba watafikiri na kujisemea wenyewe.
kwa sababu wa Yahwe wa majeshi
"kwa sababu wanamwabudu Yahwe wa majeshi"
Zechariah 12:6
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaendelea na sehemu inayozungumzia shambulio lijalo dhidi ya Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa mji.
siku hiyo
Hii inamaanisha wakati Yerusalemu itakaposhambuliwa na Mungu uwashinda adui zake.
kama mitungi ya moto katika miti... nafaka iliyosimama
kama mitungi ya moto kati ya mabua ya nafaka yasiyovunwa shambani"
vyungu vya moto
Kitu ambacho watu wa kale walitumia kubebea makaa ya moto.
miale ya moto
Ukuni unaowaka upande mmoja unaotoa nuru mtu anapotembea au kuchukua moto mahali fulani.
utateketeza watu wote walio karibu
"nitawaharibu watu wawazungukao"
Yerusalemu atakaa mahali pake tena
Watu wa Yerusalemu wataishi tena katika mji wao.
Zechariah 12:7-9
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaendelea na sehemu inayozungumzia shambulio lijalo dhidi ya Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa mji.
hema za Yuda
Hapa "hema" uwakilisha nyumbani, na nyumba zinawawakilisha watu wanaoishi ndani yake.
nyumba ya Daudi
Maana pendekezwa 1) wazao wa Daudi au 2) daraja la watawala.
malaika wa Yahwe
Huyu ni malaika wa Yahwe aliyetumwa kuwalinda watu.
Zechariah 12:10-11
nitamwaga roho ya huruma na kuiombea
"Nitawapa watu roho ya rehema kwa wengine na kuniombwa rehema"
waliyemchoma
"waliyemwua kwa mchoma"
maombolezo huko Yerusalemu yatakuwa kama maombolezo ya Hadadi Rimoni
Hadadi Rimoni yaweza kuwa ni sehemu ambapo Mfalme mwema Yosia alikufa vitani baada ya kujeruhiwa katika Vita ya Megido. Inaonekana kwamba baadaya yalitokea mapokeo ya kuomboleza kwa ajili ya kifo chake pale. Baadhi ya watu, lakini wanafikiri kwamba Hadadi Rimoni ililikuwa jina la mungu wa uongo aliyeaminiwa kufa kila mwaka, tukio ambalo wafuasi wake wangekwenda kumwombolezea.
Megido
Hili ni jina la tambarare katika Israeli.
Zechariah 12:12-14
Nchi
Hii inawahusu watu wote waliokuwa wanaishi katika nchi ya Yuda.
Nyumba ya Daudi... ya Nathani... ya Lawi
Wazao wa Daudi... wa Nathani ... wa Lawi.
Zechariah 13
Zechariah 13:1-2
kijito
Mahali ambapo kwa asili maji yanatiririka kutoka ardhini.
kwa ajili ya dhambi zao na uchafu
"Kutakasa dhambi na uchafu wao"
hili ni tamko la Yahwe wa majeshi
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
kuondoa majina ya sanamu katika nchi
kufuta ibada ya sanamu katika nchi yote"
Nitawaondoa pia katika nchi manabii wa uongo na roho wao mchafu
"Pia nitaondoa manabii wa uongo na roho wao wachavu katika nchi."
Zechariah 13:3
baba yake na mama yake waliomzaa
Kifungu "waliomzaa" kinaelezea "baba yake na mama yake" ili kuonesha mshangao kwamba wazazi wangemtendea hivi mwanao.
Hautaishi
Lazima ufe"
watamchoma
Kumchoma ili kumwua."
Zechariah 13:4-6
kwamba kila nabii
Inawahusu manabii wa uongo siyo manabii wa Yahwe.
hawatavaa tena vazi la singa
"vazi" linalotajwa hapa ni lile zito la nje. Lililotengenezwa kwa manyoya ya wanyama lililovaliwa na manabii.
kuilima ardhi
Hili ni "shamba"
ardhi ndiyo kazi yangu tangu ujana wangu
Baadhi ya matoleo ya kisasa yanafasiri sehemu hii kama "mtu alinipata tangu ujana wangu," yaani, kumpata kama mtumishi.
Majeraha haya katika mikono yako ni nini?
"Ulipataje majeraha hayo katika kifua chako? hii inamaanisha kwa desturi ya kawaida kwa manabii wa uongo kujidhuru wenyewe katika sherehe zao.
atajibu
Hii ni , atajibu kwa uongo.
Zechariah 13:7
Upanga! inuka mwenyewe
"wewe, upanga! Unapaswa kuamka." Hii ni amri kutoka kwa Yahwe kwa mchungaji wake kupigwa na kuawa.
dhidi ya mchungaji wangu
Hii inamaanisha mfalme fulani au mtumishi fulani wa Yahwe.
hivi ndivyo asemavyo Yahwe wa majeshi
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
kondoo
"Kondoo" ni watu wa Israeli.
wadogo
Pengine inarejerea kwa Waisraeli wote walio dhaifu na bila ulinzi.
Zechariah 13:8-9
hili ni tamko la Yahwe
Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria.
Nitaipitisha theluthi katika moto
Madini yanapitishwa motono ili kusafishwa au kuboreshwa. Hii inaonesha watu wakipata mateso ili kwamba wawe waaminifu zaidi kwa Mungu.
kuwasafisha kama fedha isafishwavyo; nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo
Kusafisha inamaanisha kufanya madini ya thamani kama vile fedha safi zaidi. Madini kama vile fedha na dhahabu yanajaribiwa ili kuona jinsi yalivyosafi au na nguvu. Haya yote yanatumika kuwafanya watu kuwa waaminifu zaidi kwa Mungu.
Zechariah 14
Zechariah 14:1-2
Maelezo ya Jumla:
Sura hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa.
mateka wenu watakapogawanywa katikati yenu
Inamaanisha "Adui zenu watachukua mali yenu yote na kuigawana mbele yenu"
nitayakusanya mataifa yote kinyume cha Yerusalemu kwa vita
"Nitayafanya mataifa kuishambulia Yerusalemu"
kumbukumbu ya watu haitaondolewa mjini
"Adui zenu wataacha masalia kukaa katika mji"
Zechariah 14:3-4
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa
kama apigavyo vita katika siku ya vita
"Kama alivyopiga vita zamani"
miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeitun
"Miguu yake" inamtaja Yahwe mwenyewe.
Zechariah 14:5
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa
Azali
Hili ni jina la mji au kijiji mashariki ya Yerusalemu.
watakatifu
Pengine hii inataja malaika wa Mungu.
Zechariah 14:6-8
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa.
maji yaliyohai
Kwa kawaida hii inamaanisha maji yatiririkayo, tofauti na maji yaliyotuama.
bahari ya mashariki
Hii inamaanisha Bahari ya chumvi, iliyomashariki mwa Yerusalemu.
bahari ya magharibi
Hii inamaanisha bahari ya Mediterania.
Zechariah 14:9-11
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa.
kutakuwa na Yahwe, Mungu mmoja, na jina lake pekee
"kutakuwa na Mungu mmoja pekee, Yahwe, atakayeabudiwa"
Araba... Geba... Rimoni
Haya ni majina ya maeneo
Yerusalemu itaendelea kuwa juu
Hii inamaanisha mwinuko wa mji wa Yerusalemu, kama mita 760 juu ya usawa wa bahari.
Yeye
Yerusalemu na miji mingine imetajwa kwa kiwakilishi cha jina la kike(she)
ataishi mahali pake mwenyewe
"ataishi mahali amekuwa akiishi daima"
lango la Benjamini... lango la kwanza... Lango la pembeni
Haya ni majina mbalimbali ya malango katika ukuta wa Yerusalemu.
Mnara wa Hananeli
Hii inamaanisha sehemu yenye nguvu katika ulinzi wa mji ukutani. Pengine ulijengwa na mtu aliyeitwa Hananeli.
shinikizo la mfalme
Pengine inamaanisha mahali mvinyo wa familia ya kifalme ulipotengenezewa.
Zechariah 14:12-13
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa
wamesimama katika miguu yao
"kutembea tembea"
na mkono wa mwingine utainuliwa kinyume cha mkono wa mwenzake
Kila mtu atamshambulia mwenzake.
Zechariah 14:14-15
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa.
Yuda atapigana pia na Yerusalemu.
Baadhi ya matoleo yanasomeka, "Yuda pia atapigana kwa ajili ya Yerusalemu." Nakala ya Kiebrania haiko wazi.
Watakusanya utajiri
"Watateka mali"
kwa wingi
"kwa kiwango kungi"
Zechariah 14:16-18
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa
akaenda kinyume cha Yerusalemu
"Iliyoishambulia Yerusalemu"
itashambulia mataifa
"itaadhibu mataifa kwa ukali"
Zechariah 14:19
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa
Zechariah 14:20-21
Maelezo ya Jumla:
Mistari hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa
yatakuwa kama mabakuri mbele ya madhabahu
"Itakuwa takatifu kama mabakuri yaliyotumika madhabahuni"
kila chungu katika Yerusalemu na Yuda kitatengwa kwa ajili ya Yahwe wa majeshi
Aina mbalimbali ya vyungu na vifaa vingine vilifanywa maalumu ili kutumika hekaluni kwa ajili ya kumwabudu Yahwe na kwa sadaka. Vilikuwa maalumu, havikutumika kwa jambo lingine lolote.
Hakutakuwa na wafanyabiashara tena katika nyumba ya Yahwe wa majeshi
Ilikuwa ni desturi kwa wafanyabiashara kuwauzia watu vitu walivyoviitaji kwa ajili ya ibada ya Yahwe hekaluni. Baadhi ya tafasiri zina "Wakanaani" badala, kwa maana nakala ya Kiebrania yaweza kuwa na maana mbili: "wafanyabiashara" na "Wakanaani."