Song of Solomon
Song of Solomon 1
Song of Solomon 1:1-4
Maelezo ya Jumla
Sehemu ya Kwanza ya kitabu yaanza 1:2.
Wimbo wa Nyimbo
"Wimbo ulio Bora" au Nyimbo iliyo Nzuri Sana"
ambao ni wa Sulemani
"unao muhusu Sulemani" au "ambao aliutunga"
mafuta yako ya upako
"Mafuta unayo paka mwilini mwako"
yana manukato mazuri
"yanukia vizuri"
jina lako ni kama marashi yaeleayo
Mwanamke anagundua kuwa mpenzi wake ana sifa nzuri. "jina lako ni zuri kama harufu ya mafuta mtu aliyo mimina
Nichukuwe nawe
"Ni lete pamoja nawe." Neno "wewe" la husu mpenzi
tutakimbia
Neno "tu" la husu mwanamke na mpenzi wake
kuhusu wewe
"kwasababu yako"
acha ni shereheke
"acha ni shereheke"
Ni halisi kwa wanawake wengine kukupenda
"Wote wanao kupenda wako sahihi"
Song of Solomon 1:5-6
Mimi ni mweusi lakini mzuri
"Ngozi yangu ni nyeusi, lakini bado ni mzuri"
mweusi kama hema za Kedari
Makabila ya kuhama hama ya Kedari yalitumia ngozi nyeusi ya mbuzi kujenga nyumba zao. Mwanamke analinganisha ngozi yake na hizi hema.
mzuri kama mapazia ya Sulemani
Ana fananisha ngozi yake na mapazia mazuri Sulemani aliyo tengeneza ama kwa jumba lake au kwa ajili ya Hekalu.
limeniunguza
"kuchomwa"
Wana wa mama yangu
"Kaka zangu wa kambo." Hawa kaka zake labda walikuwa na mama mmoja kama huyu mwanamke lakini sie baba mmoja.
mtunzi wa mashamba ya mizabibu
"mtu aliye tunza shamba la mizabibu"
lakini shamba langu la mizabibu sijatunza
Mwanamke ana jilinganisha na shamba la mizabibu. "lakini sijaweza kujitunza mwenyewe."
Song of Solomon 1:7
unalisha mifugo yako
"kulisha mifugo yako"
unapumzisha mifugo yako
"wanapo lala mifugo yako"
Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako?
"Niambie ili nisitange miongoni mwa mifugo ya rafiki zako ninapo kutafuta"
angaika
"anaye zunguka"
marafiki
"jamaa" au "wafanya kazi wenza"
Song of Solomon 1:8
fuata nyayo za mifugo yangu
"fuatisha nyuma ya mifugo"
nyayo
alama za kwato za mifugo kwenye ardhi
ulishe watoto wako wa mbuzi
"lisha watoto wa mbuz zako" au "acha mifugo yako ile"
Song of Solomon 1:9-11
Maelezo ya Jumla
Mpenzi wa mwanamke anaendelea kuzungumza
mpenzi wangu
"ninaye mpenda"
na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao
Mpenzi ana mlinganisha mwanamke na farasi mzuri wa kike.
magari ya farasi ya Farao
"Farasi wa Farao wanao vuta magari"
yaliochanganywa na fedha
"na madoa ya fedha"
Song of Solomon 1:12-14
amelala kitandani mwake
"amekaa mezani mwake"
yakasambaza arufu
"yakatoa harufu yake nzuri"
nardo
mafuta watu wanayo tumia kufanya ngozi yao safi na nyororo.
Mpenzi wangu ni kwangu kama
"Kwangu mimi, mpenzi wangu ni kama"
lala usiku katikati ya maziwa yangu
"analala katikati ya maziwa yangu usiku kucha." Wanawake wanaweka kiasi kidogo cha manemane ya gharama kifuani mwao kuwapa harufu nzuri.
mua ya hena
maua kutoka jangwa dogo la miti watu walio tumia kama marashi
Song of Solomon 1:15
Ona
Neno "Ona" hapa la ongeza msisitizo kwa kinacho fuata.
macho yako ni kama ya hua
Hua ni ishara ya usafi, bila hatia, upole na upendo. "macho yako ni mapole na mazuri kama ya hua.
Song of Solomon 1:16-17
Ona
Neno "Ona" hapa la ongeza msisitizo kwa kinacho fuata.
mtanashati
"muonekano mzuri" au "mzuri" au "pendeza"
Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi
Mwanamke anaeleza msitu kama ni nyumba yao. "Matawi ya mti wa mierezi ni kama nguzo za nyumba yetu.
nguzo
mbao kubwa zinazo saidia nyumba yote
na boriti zetu ni matawi ya miberoshi
"na matawi ya miberoshi ni kama boriti zetu
boriti
vipande vya mbao vinavyo shikilia dari la nyumba
Song of Solomon 2
Song of Solomon 2:1-2
Mimi ni ua katika tambarare
Mwanamke anajilinganisha na ua katika tambarare
Tambarale
Sehemu ya ardhi ambayo iko sawa, haina miti, na huota aina nyingi za majani na maua
Nyinyoro katika bande
Mwanamke anajilinganisha mwenyewe na nyinyoro katika bonde ni sawa na kujilinganisha mwenyewe na maua yaliyo katika tambarale
Nyinyoro
ua lenye harufu nzuri lililo na umbo kama tarumbeta
Bonde
Hii ina maana ya sehemu kubwa iliyo sawa katikati ya milima
kama nyinyoro ...mwananchi wangu
Mwanaume ana maanisha mwanamke huyo ni zaidi ya mzuri na wathamani kuliko wanawake wadogo wote, kama nyinyoro ni zaidi ya ua zuri na lenye thamani kuliko miiba yote ya porini iliyo lizunguka
Mpenzi wangu
Ona ilivyo tafsiriwa hii katika 1:9
Binti wa mwananchi wangu
"Wanawake wadogo wengine"
Song of Solomon 2:3-4
Kama mti wa mpera ... kijana mdogo
Kama mti wa mpera ni zaidi ya faraja na furaha zaidi ya miti yote msituni kwa hiyo mpendwa wa mwanamke ni zaidi ya faraja na furaha zaidi ya wanaume wadogo wote
Mti wa mpera
Mti unaozaa matunda madogo ya njano ambayo ni matamu sana
Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana
Mwanamke anapata furaha na faraja akiwa karibu na mpendwa wake
Na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu
Mwanamke analinganisha starehe anayo ipata kwa mpendwa wake na tunda tamu
Ukumbi wa maakuli
Ni chumba kikubwa ambapo watu hula mlo mkubwa na kufurahia kutembeleana
Na bendera yake
"bendera" ni kipande kikubwa cha nguo ambacho watu hupeperushwa juu mbele ya jeshi ili kuongoza na kuwapa ujasiri wanaume wengine
Bendera yake juu yangu ilikuwa upendo
Mwanamke angeweza kuwa na wasiwasi wa kuingia ukumbi wa maakuli, lakini mapenzi ya mpendwa wake yalimuonesha njia na kumpa ujasiri wa kuingia. "lakini upendo wake uliniongoza nakunipa ujasiri kama bendera."
Song of Solomon 2:5-6
Ni uishe
"Nirudishie uwezo wangu" au "Nipatie nguvu"
Keki za mizabibu
"kwa kunilisha mikate iliyo tengenezwa na mizabibu iliyonata pamoja kama chapati" au "'kwa kunipa keki za mizabibu"
Ni nuishe kwa mapera
"nifadhili kwa kunipa mapera" au "nisaidie kwa kunipa mapera"
Kwakuwa nimedhohofika na mapenzi
"kwasababu mapenzi yangu yana nguvu sana hadi najiskia dhaifu."
Mkono wa kushoto ... mkono wa kulia
"mkono wa kushoto ... mkono wa kulia"
Wanikumbatia
"kunishikilia"
Song of Solomon 2:7
Mabinti wa Yerusalemu
"wanawake wadogo wa Yerusalemu"
Kwa swala na paa wa porini
Wanyama hawa wa porini wana aibu na uwoga, lakini waza uzoefu wa uhuru kabisa.
Swala
Wanyama wanafanana kabisa na hayala na wapo haraka, wembamba na wana aibu
Wa porini
"ambao wanaishi upande wa nchi"
Hatuta vuruga mapenzi yetu hadi yatakapoisha yenyewe
"hatuta jivuruga tukiwa katika mapenzi hadi yatakapo isha"
vuruga
"Ghasia" au "Usumbufu"
Song of Solomon 2:8-9
Oh, huyu yuwaja
Neno "Oh" hapa linaongea msisistizo kwa kile kinachofuata.
Akiruka ruka juu ya milima,akiruka vilimani
"akiruka juu ya milima , akikimbia haraka juu ya vilima ." Mpenzi anakimbia haraka na mwenye neema kama swala, hata juu ya ardhi mbaya ya milima na vilima.
Kama swala au mtoto mdogo wa paa
Mwanamka anamlinganisha mpenzi wake na swala au paa mdogo kwasababu yupo haraka, mzuri, na mwenye neema kama wanyama hawa.
Swala
Ona jinsi ilivyotafsiriwa "swala" katika 8:2
Mtoto mdogo wa paa
"paa mdogo" au "mwana mdogo wa hayala"
Tazama, amesimama
Neno "tazama" hapa linaonesha kwamba mwanamke ameona kitu cha kuvutia.
Nyuma ya ukuta wetu
"upande mwengine wa ukata wetu." Mwanamke yupo kwenye nyumba na mpenzi wake yupo njee ya nyumba.
akishangaa kupitia dirishani
"anatazama kupitia madirisha"
akichungulia wavuni
"anashangaa kupitia wavuni"
wavu
vipande virefu vya mbao mtu alivyo viunga pamoja ili kutengeneza mfuniko wa dirisha au mwingilio tofauti
Song of Solomon 2:10-11
Amka
"Nyanyuka juu"
mpenzi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:9
Angalia, baridi imepita
Neno "Angalia" hapa laongeza mkazo kwa linalo fuata.
mvua imeisha na kwenda
Katika Israeli, kunanyesha kipindi cha mvua tu.
Song of Solomon 2:12-13
Maua yametokeza
"Waeza ona maua" au "Watu wanaeza ona maua."
juu ya nchi
"katika nchi yote hii"
wakati wa kupunguza matawi
"majira ya watu kupunguza matawi"
na kuimba kwa ndege
" na ndege kuimba"
sauti za hua zimesikika
"waeza sikia hua wakilia" au "watu waeza sikia sauti za hua"
mizabibu imestawi
"mizabibu imetoa maua" au "mizabibu ina maua"
yatoa
Neno "ya" linahusu kustawi kwa mizabibu.
marashi
"arufu nzuri"
Song of Solomon 2:14
Maelezo ya jumla:
Mpenzi wa mwanamke anaongea.
Hua wangu
Mpenzi wa mwanamke anamlinganisha mwanamke na hua kwasababu ana sura nzuri na sauti nzuri kama ya hua na kwasababu alikuwa awe naye katika sehemu ya mbali na watu kama hua anavyo ishi eneo la mbali na watu.
katika miamba ya mawe
"sehemu ya kujificha ya miamba." Miamba ni mipasuko mikubwa ya mawa ya milimani.
katika miamba ya siri ya mipasuko ya milima
"katika sehemu za siri za mporomoko wa mlima." Maneno haya yanaeleza sehemu ambayo mpenzi anataka kuona sura ya mwanamke
sura yako
"muonekano wako" au "ufumo wako" au "uonekanavyo"
Song of Solomon 2:15
mbweha
Hili ya weza kutafsiriwa kama "mbwa mwitu." Hawa wanyama wanaonekana kama mbwa wadogo na mara nyingi walitumika kwenye mashahiri ya mapenzi kuwakilisha wanaume vijana wenye shauku wanaoweza kumpumbaza binti.
yetu
Neno "yetu" la weza kumaanisha 1) mwanamke na mpenzi wake au 2) mwanamke na familia yake nzima.
mbweha wadogo
Mbweha wanazaa watoto wao majira ya masika mizabibu inapo chipua.
wanao haribu
"wanao vuruga" au "wanao angamiza." Mbweha na mbwa mitu wanaharibu mashamba ya mizabibu kwa kuchimba mashimo na kula mizabibu na mizaituni. Hii pia yaweza wakilisha wanaume vijana wanao haribu mabinti.
limestawi.
Hii yaweza wakilisha mwanawake mdogo aliye tayari kwa ndoa na kuzaa watoto. Ona jinsi ulivyo tafsiri hii 2:12
Song of Solomon 2:16-17
Mpenzi wangu ni wangu
"Mpenzi wangu ni sehemu yangu"
na mimi ni wake
"na mimi ni sehemu yake"
anakula
"ujishibisha" au "ula majani." Mwanamke anamlinganisha mpenzi wake na mnyama anaye kula mimea miongoni mwa nyinyoro, kama paa au ayala mdogo.
vivuli kutoweka
Mwanamke anaeleza vivuli kama vile vinakimbia wanga wa jua.
kama ayala au mtoto mdogo wa paa
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:8
ayala
aina ya mafano wa swala wenye pembe zilizo pinda
paa
swala wa kiume
Song of Solomon 3
Song of Solomon 3:1-2
nilikuwa na shauku ya yeye ni mpendaye; nilimtafuta
Hii imerudiwa kwa mkazo.
nilimtafuta, lakini sikumpata
"nilikuwa nataka kuwa naye" au "nilikuwa na shauku naye"
nilikuwa na shauku ya yeye ni mpendaye
Ona jinsi ulivyo tafsiri "yeye nafsi yangu impendaye" 1:7
kwenda kupitia mji
"kutembea mjini"
kupitia mitaa na sokoni
Neno "sokoni" la ashiria eneo la katikati ya mji ambapo mitaa na barabara uja pamoja. Ni sehemu ambapo watu uuza vitu, eneo la bihashara, na sehemu watu wanakuja kunzungumza pamoja.
Nilimtafuta
"kumtafuta"
Song of Solomon 3:3-4
Walinzi
watu wenye wajibu wa kulinda mji usiku kuwa weka watu salama
walipo kuwa doria katika mji
"walio kuwa wakipita kwenye mji" au "walio kuwa wanatembea mjini
kitandani
"chumba walichokuwa wanalala"
yeye aliyenichukua mimba
"yeye aliye beba mimba na mimi" au "yeye aliye ni beba tumboni mwake" Hii ina maana ya mama yake.
Song of Solomon 3:5
Ninataka muape ... yatakapo isha
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:7
Song of Solomon 3:6-7
Maelezo ya Jumla
Hapa ni mwanzo wa Sehemu ya Tatu ya kitabu
Nini hiyo inayo toka nyikani
Kundi la watu wanao safiri kutoka nyikani kwenda Yerusalemu. Kwasababu nyikani iko chini ya bonde la Yordani na Yerusalemu iko juu ya milima, watu lazima waende juu kufikia Yerusalemu.
kama nguzo za moshi
Kwasababu watu walitimua vumbi sana walipo kuwa wakisafiri, vumbi lilionekana kama moshi kwa mbali.
umefukizwa manemane na ubani
"harufu nzuri ya moshi wa manemane na uvumba umeizunguka."
pamoja na unga wote wa manukato unao uzwa na wafanya biashara
"na harafu nzuri ya moshi wote unga wafanya bihashara wanauza."
unga
udogo safi unao patikana kwa kusaga kitu kigumu
Angalia
Hili neno hapa linaonyesha kuwa mnenaji sasa amegundua jibu kwa swali la mstari wa 6.
nikitanda
Hii ya husu kitanda chenye shuka linalo weza kubwa sehemu moja kwenda nyingine.
mashujaa sitini wamekizunguka, wanajeshi elfu sitini wa Israeli
Hii mistari miwili ya husu watu hao hao sitini. Mstari wa pili wa fafanua kuwa "mashujaa" ni "wanajeshi wa Israeli."
mashujaa
wanaume wanao pigana
Song of Solomon 3:8-9
wa vita
"katika pambano"
akijizatiti na
"ilikuji linda dhidi ya" au "kuweza kupigana na"
maasi ya usiku
Hii ya husu hatari yeyote inayo weza kuja giza la usiku, kama majambazi.
kiti cha kifalme
kiti chenye miti mirefu watu wanacho tumia kubeba watu muhimu
Song of Solomon 3:10-11
Nguzo zake
Neno "zake" la husu kiti cha Mfalme Sulemani.
Nguzo
Neno "nguzo" hapa la husu vipande vya mbao vinvyo shikilia kitambaa cha hema kwenye kiti chake.
Ndani mwake
"Ndani yake kulikuwa"
kulipambwa na upendo
"kulifanywa pazuri kwa upendo" au "kulishonewa upendo." Hii ya hashiria kwamba wanawake walifanya kiti cha mfalme kizuri kwa namna ya kipekee kuonyesha upendo wao kwa Sulemani.
na mtazame mfalme Sulemani
"muone mfalme Sulemani." Neno "tazama" la husu kumuangalia mtu au kitu kwa muda mrefu, mara nyingi kwa hisia kali.
akivikwa taji
"amevaa taji"
Song of Solomon 4
Song of Solomon 4:1
O, wewe ni mzuri ... Macho yako ni ya hua
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:15
Nywele zako ... Mlima Gileadi
Mbuzi mara nyingi ni weusi kwa rangi na wanapo tembea milimani nywele zao zinaonekana kama mawimbi ya nywele za mwanamke.
Song of Solomon 4:2
Meno yako ni kama kondoo walio nyolewa
Baada ya kondoo kunyolewa, wameoshwa na ngozi yao yaonekana nyeupe sana. Haya maneno yalinganisha weupe wa meno ya mwanamke na mng'ao mweupe wa manyoya ya kondoo baada ya manyoya yao kunyolewa.
wakitoka sehemu ya kuoshwa
Hii ina maana kondoo wanatoka kwenye maji. "wakitoka kwenye maji baada ya watu kuwaosha"
Kila mmoja ana pacha
Kwa kawaida kondoo uza wana kondoo wawili kwa wakati mmoja. Hawa wana kondoo huwa wamefanana. Kila meno ya mwanamke yana jino linalo fanana upende wa pili wa mdomo wake. Hivyo ni kama kila jino lina pacha kama wana kondoo.
hamna ata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.
Hakuna meno yao yaliyo poteza jino lingine linalo fanana upande wa pili. Mwanamke hajapoteza meno yake.
aliyefiwa
Kupoteza mpendwa aliye kufa.
Song of Solomon 4:3
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumsifu mwanamke.
kama uzi mwekendu
Haya maneno yanalinganisha rangi midomo ya mwanamke na uzi mwekundu.
wapendeza
"ni mzuri"
kama majani ya komamanga
Makomamanga yanateleza, ya duara, na yana rangi nyekundu.
nyuma ya kitambaa chako
Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:1
Song of Solomon 4:4-5
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumsifu mwanamke.
Shingo yako ni kama
"shingo yako ni ndefu na nzuri kama"
wa Daudi
"mbao Daudi alijenga"
umejengwa kwa mistari ya mawe
Wanawake walikuwa na mikufu iliyo funika shingo zao kwa mistari ya mapambo. Mpenzi analinganisha hii mistari ya mapambo na mistari mistari ya mawe kwenye mnara.
na ngao elfu moja
Mpenzi analinganisha mapambo ya mkufu wa mwanamke na ngao zinazo ni'ng'nia kwenye mnara.
ngao elfu moja
"ngao 1,000."
ngao zote za wanajeshi
"ngao zote za mashujaa hodari"
kama swala wawili, mapacha wa ayala
Maziwa ya mwanamke ni mazuri, yamelingana na mepesi kama watoto wa wili wa swala aya wa ayala.
mapacha
watoto wa mama aliye zaa watoto wawili kwa wakati mmoja
ayala
Ona jinsi ulivyo tafsiri "ayala" 2:7
wakila miongoni mwa nyinyoro
"kula mimea miongoni mwa nyinyoro." Mapacha wazuri wawili na mtoto ayala ni wazuri zaidi wakati nyinyoro imewazungukaa.
Song of Solomon 4:6-7
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumsifu mwanamke.
Hadi jioni ifike na vivuli viondoke
Ona jinsi ulivyo tafsiri mstari 2:16 ambapo neno ni moja na hili.
nitaenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani
Mpenzi anaelezea matamanio yake ya kufurahia maziwa ya mwanamke kwa kulinganisha na milima au vilima anayo i penda. Maziwa yake ni duara na yametokeza kama milima au vilima. Yananukia vizuri kama manemane na uvumba.
nitaenda kwenye mlima ... vilima vya ubani
Hii mistari inarudia wazo kwa utofauti kidogo wa kukazia mvuto wa maziwa ya mpenzi.
mlima wa manemane
"mlima ulitengenezwa kwa manemane" au "mlima uliyo na manemane"
Wewe ni mzuri kwa kila namna
"Kila sehemu yako ni nzuri" au "Wewe wote ni mzuri"
mpenzi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:9
hakuna lawama ndani yako
"Hauna lawama"
Song of Solomon 4:8
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kuongea na mwanamke.
Njoo nami ... shimoni mwa simba
Mpenzi anataka bibi arusi wake aje nae kutoka sehemu ya hatari. Hii ni fumbo na wala wapenzi hawapo kwenye hii milima au shimoni.
kutoka Lebanoni
"mbali kutoka Lebanoni"
Amana
jina la mlima karibu na Damsko
Seneri
jina la mlima karibu na Amana na Herimoni. Watu baadhi wanadhani hii ya husu mlima mmoja na Hermoni.
shimoni
Sehemu simba na chuwi wanaishi, kama mapango au mashimo kwenye ardhi
Song of Solomon 4:9
Maelezo ya jumla
Mpenzi anaendelea kuongea na mwanamke.
Umeuiba moyo wangu
Anasema mapenzi yake na upendo wake ni wa mwanamke. "umenasa upendo wangu"
dada yangu
Mwanamke ana pendwa sana na mpenzi kama dada yake mwenyewe. Sio kaka na dada kihalisia.
kwa mtazamo mmoja tu wako kwangu, kwa mkufu mmoja wa shingo yako
Macho yote ya mwanamke na mikufu yake ina mvutia mpenzi kwake.
Song of Solomon 4:10-11
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumsifu na mwanamke.
Jinisi gani upendo wako ulivyo mzuri
"Upendo wako ni wa ajabu"
dada yangu, bibi arusi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:9
Jinsi gani zaidi upendo wako ulivyo bora kuliko mvinyo
Hii mistari inarudia wazo moja kwa maneno tofauti kwa kukazia.
Jinsi gani zaidi upendo wako ulivyo bora kuliko mvinyo
"Upendo wako ni bora kuliko mvinyo." Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:1
arufu ya marashi yako kuliko manukato yeyote
"harufu ya mafuta yako ni bora kuliko harufu ya manukato yeyote."
marashi ... manukato
Ona jinsi ulivyo tafsiri haya maneno 1:1
Midomo yako ... chini ya ulimi wako
Hii mistari inarudia wazo moja kwa maneno tofauti kwa kukazia.
Midomo yako, bibi arusi wangu, yatiririka asali
Mpenzi anadhani mabusu ya mwanamke ni matamu kama asali; au, kwasababu maneno anayozungumza ni matamu kama asali.
asali na maziwa vichini ya ulimi wako
Mpenzi anadhani mabusu ya mwanamke ni matamu kama asali; au, kwasababu maneno anayozungumza ni matamu kama asali.
arufu ya mavazi yako ni kama marashi ya Lebanoni
"harafu ya nguo zako ni kama harufu ya Lebanoni." Miti mingi ya mierezi yaota Lebanoni. Miti ya mierezi yanukia vizuri, hivyo Lebanoni ingenukia vizuri.
Song of Solomon 4:12-14
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumsifu mwanamke.
Dada yangu, bibi arusi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:9
ni bustani ilio fungwa
Mpenzi anamlinganisha mwanamke na bustani iliyo fungwa kwasababu yeye ni wake tu na anaweza mfurahia. Anaweza pia kusema kuwa yeye bado ni bikra ambaye bado hajamfurahia.
chemchemi iliyo fungwa kwa muhuri
Mpenzi anamlinganisha mwanamke na chemchemi iliyo fungwa kwa muhuri kwasababu zile zile alizo mlinganisha na bustani iliyo fungwa.
Matawi yako ... aina tofauti za manukato
Mpenzi anamuelezea jinsi mwanamke alivyo mzuri kwa kumfananisha kama bustani iliyo jaa vitu vizuri.
kichaka
sehemu miti mingi inapo ota pamoja
yenye matunda tofauti
"matunda mbali yaliyo bora"
hina
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:12
Nardo
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:12
Zafarani
kiungo kinacho toka kwenye sehemu iliyo kauka kutoka kwenye uzi wa chano katikati ya ua.
mchai
Hili ni jani lenye harufu nzuri ambalo watu wanatumia kutengeneza mafuta ya upako.
mdalasini
kiungo kilicho tengenezwa na ganda la mti ambalo watu utumia kupika
manemane
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:12
aloes
aina kubwa ya mmea wenye harufu nzuri sana
aina zote za uvumba
"uvumba bora"
Song of Solomon 4:15-16
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumsifu mwanamke.
Wewe ni bustani ya chemchemi
"Wewe ni chemchemi katika bustani." Mpenzi ana elezea jinsi alivyo mzuri kwa kumfananisha na maji.
maji safi
maji safi ya kunywa
mifereji inayo shuka kutoka Lebanoni
Kwasababu Lebanoni ilikuwa na milima iliyo funikwa kwa miti, mifereji kutoka Lebanoni ilikuwa misafi na ya baridi.
Amka ... manukato yake yatoe marashi
Mwanamke anazungumza na upepo wa kaskazini na wa kusini kama ni watu.
Amka
"Anza kwenda"
vuma katika bustani yangu
Mwanamke ana utaja mwili wake kwa kuuongelea kama bsutani.
ili manukato yake yatoe marashi
"itume harufu yake nzuri"
Mpenzi wangu na ... matunda ya chaguo
Mwanamke anamkaribisha mpenzi wake kumfurahia kama mkewe.
matunda ya chaguo
"matunda mazuri"
Song of Solomon 5
Song of Solomon 5:1
Nimekuja
Ni dhahiri kuwa mpenzi wa mwanamke anazungumza.
nimekuja katika bustani yangu
Mwanamme anaelezea mwanamke kama bustani. Usiku wa arusi, mwanamme anaweza kumfurahia mwanamke. Anaelezea hili kama kuja katika bustani yake.
dada yangu
Mwanamme anamuita mwanamke dada kwasababu mpenda sana kama angempenda dada yake. "yeye ni mpendaye"
Nimekusanya udi wangu ... na maziwa yangu
Mwanamme anatumia haya maumbo kutoka kwenye bustani kuhashiria kwamba ameweza kufurahia sehemu nyingi za mwanamke.
manukato
mimea yenye harufu nzuri au ladha
Song of Solomon 5:2
Maelezo ya Jumla
Hapa ni mwanzo wa Sehemu ya Nne ya kitabu
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anatumia tafsida kueleza ndoto yake ili kwamba iweze kutafsiriwa kwa njia mbili tofauti: 1) mwanamke anaeleza ndoto kuhusu usiku mpenzi wake alipo kuja kumtembelea nyumbani mwake; na 2) mwanamke anaeleza ndoto kuhusu kuanza kulala na mpenzi wake.
lakini moyo wangu ulikuwa umeamka
"lakini moyo wangu ulikuwa umeamka"
Nifungulie
Hii ya husu kufungua mlango lakini yaweza tafsiriwa kama ombi la kimapenzi. "Fungua mlango kwa ajili yangu" au "Jifungue kwangu"
dada yangu
Maneno ya mahaba. Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:9
mpenzi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:9
hua wangu
Ona Jinsi ulivyo tafsiri 2:14
usiye na doa
"mkamilifu wangu" au "mwaminifu wangu" au "usiye na hatia wangu"
unyevu
matone ya maji au ukungu unaoa kuwa wakati wa baridi ya usiku hali ya hewa inaposhuka
nywele zangu na unyevu wa usiku
hewa nyevu ya usiku ya fanya nywele za mwanamme kulowa kwasababu kasimama nje.
kichwa changu kimelowa na matone, nywele zangu na unyevu wa usiku
Hii mistari miwili ina maanisha kitu kimoja.
Song of Solomon 5:3-4
joho
nguo nyembamba watu waliyo vaa kwenye ngozi yao
lazima nilivae tena?
"sitaki kuvalishwa tena"
Nimeosha miguu yangu
Tafsiri zinazo wezekana ni 1) mwanamke aliosha miguu yake ili aweze kwenda kitandani au 2) Neno "miguu" wakati mwengine la tumika kama tafsida kueleza sehemu za siri za mwanamke. "nimejiosha"
Mpenzi wangu anaeka mkono wake kwenye kitasa
Tafsiri zinazo wezekana ni 1) mpenzi anafikia nyumbani kwa kupitia kitobo kwenye mlangao ili kufungua mlango au 2) huu ni mwanzo wa tendo la mapenzi. Katika huu muktadha, "mkono" waelezewa kama tafsida ya sehemu za siri za mwanamme.
Mpenzi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:12
kitasa
"kufuli"
Song of Solomon 5:5
Nimeamka kumfungulia mlango mpenzi wangu
Tafsiri zinazo wezekana ni 1) mwanamke aliinuka kutoka kitandani kuweza kumuingiza mpenzi wake ndani ya nyumba au 2) "Nimejianda kuweza kujifungua kimapenzi kwa mpenzi wangu."
mikono yangu ... vidole vyangu
Maneno "mikono" na "vidole" yaweza kumaanisha viungo vya siri vya mwanamke.
unyevu wa udi
"kwa udi wa maji"
Song of Solomon 5:6
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kueleza ndoto yake.
Nimemfungulia mlango mpenzi wangu
"Nimejifungua kwa mpenzi wangu."
mpenzi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:12
Moyo wangu ukadidimia; nikakosa tumaini
"Moyo wangu ukaondoka." Alipo zungumza, nilihisi kama nimekufa"
Song of Solomon 5:7
Walinz
wao wanao kesha na kulinda mji usiku
walinipata mimi
Neno "mimi" la muhusu mwanamke.
askari katika ukuta
wanaume wanao linda kuta"
nguo yangu ya juu
nguo ya nje ambayo watu wanavaa juu ya nguo yao ingine sehemu ya mabegani wanapo enda sehemu ya hadhara.
Song of Solomon 5:8
Ninataka uhaidi, mabinti wa Yerusalemu
Ona jinsi ulivyo tafsiri "Ninataka uhaidi, mabinti wa Yerusalemu," 2:7
ninaumwa sababu ya upendo wangu kwake
Upendo wake una nguvu hadi anaumwa.
Song of Solomon 5:9
wewe uliye mzuri miongoni mwa wanawake
Ona jinsi ulivyo tafsiri "mzuri miongoni mwa wanawake" 1:8
Kwanini mpenzi wako bora
"Nini ya mfanya mpenzi wako bora"
hadi utuulize tuweke nadhiri kama hii
"na ana kusababisha utufanye tu chukuwe nadhiri kama hii"
nadhiri kama hii
Ona hiyo nadhiri 5:8
Song of Solomon 5:10-11
amenawiri na ana ng'aa
Yaelezwa kuwa mwanamke ana eleza ngozi ya mpenzi wake.
amenawiri
"ana afya tele" au "ni msafi." Mpenzi ana ngozi ambayo haina shida.
kati ya wanaume elfu kumi
"bora ya 10,000" "bora kuliko yeyote" au "hakuna aliye kama yeye"
Kichwa chake ni dhahabu safi
Kichwa cha mpenzi kina thamani kwa mwanamke kama dhahabu safi.
kunguru
ndege mwenye manyoya meusi sana
Song of Solomon 5:12
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kumuelezea mpenzi wake.
Macho yake ni kama ya hua
Ona jinsi ulivyo tafsiri "macho yako ni kama ya hua" 1:15
pembezoni ya vijito vya maji
Mwanamke anaweza kuwa anatumia hili umbo kusema kwamba macho ya mpenzi wake ya unyevu kama mifereji ya maji.
yameoshwa na maziwa
"yamejiosha yenyewe katika maziwa." Hua wanawakilisha watoto wa mpenzi. Haya yamezungukwa na macho yake yote, ambayo ni meupe kama maziwa.
yameundwa kama mikufu
Macho yake ni mazuri hadi yanaonekana kama madini ambayo sonara ameyaweka pamoja.
Song of Solomon 5:13
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kumuelezea mpenzi wake.
Mashavu yake ... arufu ya marashi
Hii ya fafanua kuwa mashavu yake ni kama vitanda vya manukato kwasababu vyote vinatoa harufu nzuri.
vitanda vya manukato
bustani au sehemu ya bustani watu wanapo otesha manukato
vinavyotoa arufu ya marashi
"vinavyotoa harufu nzuri"
Midomo yake ni nyinyoro
Mwanamke inawezekana ana linganisha midomo yake na nyinyoro kwasababu ni mizuri na inanukia vizuri.
tiririka udi
"inayo tiririka na udi uliyo bora." Midomo yake ni minyevu na inanukia vizuri kama udi.
nyinyoro
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:16
Song of Solomon 5:14
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kumuelezea mpenzi wake.
Mikono yake ni ya mianzi ya dhahabu
Mwanamke anatumia hili umbo kusema kwamba mikono yake ni mizuri na ya thamani.
tumbo lake ni pembe lililo funikwa yakuti samawi
Mwanamke anatumia hili umbo kusema kwamba tumbo lake ni zuri na ya thamani.
yakuti samawi
Yakuti samawi ni ya jiwe safi na la thamani. Hili aina ya yakuti samawi lina njano au rangi ya dhahabu.
Song of Solomon 5:15
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kumuelezea mpenzi wake.
Miguu yake ni nguzo za marimari
Miguu yake ina nguvu na mizuri kama marimari ya nguzo
Marimari
jiwe lenye imara lenye rangi tofauti na watu wana lisugua kulifanya nyororo
iliyo ekwa juu ya dhahabu safi
Miguu yake ina thamani kama chini ya dhahabu safi inayo wezezesha nguzo za marimari.
muonekano wake ni kama Lebanoni
Lebanoni ili kuwa eneo zuri lenye milima mingi na miti.
mizuri kama mierezi
"yenye kutamanika kama mierezi" au "vyema kama mierezi"
Song of Solomon 5:16
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kumuelezea mpenzi wake.
Mdomo wake ni mtamu
Mwanamke anatumia hili umbo kuelezea utamu wa busu la mpenzi wake au maneno matamu anayo sema.
ni mzuri sana
"kila sehemu yake ni nzuri" au "yeye ni mzuri"
Huyu ni mpenzi wangu, na huyu ni rafiki yangu
Neno "Huyu" la muelezea mtu mwanamke aliye maliza kumuongelea. Waweza pia tafsiri haya maneno kama "Yule ni mpenzi wangu, na hivi ndivyo rafiki yangu alivyo."
mabinti wa Yerusalemu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:5
Song of Solomon 6
Song of Solomon 6:1
Kwa njia gani mpenzi wako ameenda
"mpenzi wako ameelekea wapi"
ulio mzuri miongoni mwa wanawake
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:8
ilitumtafute nawe?
"Tuambie, ilitumtafute kwa pamoja."
Song of Solomon 6:2-3
Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake
Ona ufafanuzi wa umbo hili 5:1
vitanda vya manukato
Ona jinsi ulivyo tafsiri " vitanda vya manukato" katika 5:13. Mpenzi amekuja kufurahia mvuto wa mwili wa mwanamke ambao ni mzuri kama manukato.
kula katika bustani na kukusanya nyinyoro
Mwanamke anatumia haya maumbo kuhashiria kwamba mpenzi wake ana mfurahia yeye.
kula
Ona jinsi ulivyo tafsiri "ana kula" 2:16
kukusanya nyinyoro
"kuokota nyinyoro"
nyinyoro
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:16
Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri "Mpenzi wangu ni wangu na mimi ni wake" 2:16
na kula katika nyinyoro kwa raha
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:16
Song of Solomon 6:4
Maelezo ya Jumla
Hapa ni mwanzo wa Sehemu ya Tano cha kitabu
ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu
Mpenzi ana fananisha uzuri wa mwanamke na mvuto wake kwa miji mizuri na ya kuvutia.
wapendeza
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:5
waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele
waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele** Uzuri wa mwanamke ni una nguvu hadi unamfanya mpenzi ahisi hana msaada, kama jeshi lilikuwa linamfuata.
Song of Solomon 6:5
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kumsifu mwanamke.
yana nizidi ukali
"kuniogopesha." Macho ya mwanamke ni mazuri hadi yana mfanya mpenzi kuhisi kuzidiwa na kuogopa kwasababu haweza zuia nguvu.
Nywele zako ... kutoka miteremko ya Mlima Gileadi
Ona jinsi ulivyo tafsiri "Nywele zako ... kutoka Mlima Gileadi" 4:1
Song of Solomon 6:6-7
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumsifu mwanamke.
Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso
Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:3
Song of Solomon 6:8-9
Kuna malikia sitini, masuria themanini
Kuna malikia 60, masuria 80."
wanawake wadogo bila idadi
Maneno, "bila idadi" yamaanisha hakuna anaweza kuwahesabu. "maelfu ya wanawake wadogo"
Hua wangu, asiye na doa wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri "Hua wangu, asiye na doa wangu" 5:2
ni yeye pekee
"ni wa pekee" au "ni mmoja wa wachache." Mpenzi ana mtofautisha mwanamke na wanawake wengine. Japo kuwa kuna wanawake wema wengi, mwanamke ana simamawa kipekee miongoni mwa wote.
ni binti muhimu wa mama yake
"kwa mama yake ni binti maalumu" au "yeye ni binti wa mama yake ambaye ni wa kipekee"
mwanamke aliye mzaa
"mwanamke aliye mzaa." Haya maneno ya muongelea mama yake.
na kumuita mbarikiwa
"na kukiri kuwa mambo yamemuendea vizuri" au "kusema kuwa yeye alikuwa na bahati"
Song of Solomon 6:10
Maelezo ya Jumla
Yale malikia na masuri walisema kuhusu mwanamke. Ingawa, tafsiri zingine zinaona kuwa mpenzi wa mwanamke anaongea katika huu mstari pia.
Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha
Wanatumia hili swali kusema kuwa wanadhani mwanamke ni wa ajabu.
anaye jitokeza kama kukicha
Mpenzi anatumia hili umbo kusema kuwa mwanamke ni mzuri na wa utukufu kama kunavyo pamba zuka na kung'aa.
waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele
waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele** Uzuri wa mwanamke ni una nguvu hadi unawafanya wanawake wahisi hawana msaada, kama jeshi lilikuwa linamfuata. Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:4
Song of Solomon 6:11-12
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kuongea mwenyewe.
milozi
Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:12
mimea midogo
"mimea michanga" au "matawi mapya"
imestawi
"imefungua maua yake"
Nilikuwa nina furaha nikahisi kama nimepakia gari ya farasi la mtoto wa mfalme
Mpenzi anatumia umbo hili ili kuonyesha jinsi alivyo na furaha.
Song of Solomon 6:13
Geuka nyuma, geuka nyuma
Hii imerudiwa kwa mkazo.
kukushangaa
kuangalia kitu kwa umakini kwa muda
kana kwamba nina cheza katika ya mistari miwili ya wachezaji
Ingekuwa kitu kizuri kuona mwanamke akicheza na wachezaji wengine.
Song of Solomon 7
Song of Solomon 7:1
Jinsi gani miguu yako ilivyo yaonekana mizuri kwenye viatu
Ina hashiriwa kwa muendelezo kutoka 6:13 kuwa mpenzi wa mwanamke ana muelezea akiwa anacheza. "Miguuu yako ni mizuri sana ndani ya viatu vyako."
binti wa mfalme
Japo mwanamke hakuzaliwa katika familia ya kifalme, jinsi anavyo onekana na kutenda ana sababisha kuonekana kama binti wa mfalme. "una tabia njema" au "wewe uliye mrembo"
Mapaja yako ni kama mikufu
Umbo la mapaja ya mwanamke ni kama madini ya thamani ambaye mjuzi wa kutengeneza ame ya chonga kikamilifu.
Mapaja yako
Neno "mapaja" ya lina husu sehemu ya mwili wa mwanamke uliyo juu ya magoti.
Song of Solomon 7:2
Maelezo ya Jumla
Mpenzi wa mwanamke anaendelea kumuelezea yeye anaye mpenda
Kitovu chako ni kama duara la bakuli
Kitovu cha mwanamke kina umbo zuri kama kibakuli.
Kitovu
Sehemu illiyo ingia ndani katika tumbo, ambayo ni kovu lililo baki ambalo lilimuunganisha mtoto na mama yake
kamwe kisikose mchanganyiko wa mvinyo
Watu walitumia mitungi mikubwa kuchanganya maji na mvinyo au theluji kwa ajili ya sherehe. Watu walifurahia ladha ya mvinyo kwenye sherehe.
Tumbo lako ni kama ngano iliyo umuka
Watu walidhani kuwa rangi ya ngano ni nzuri sana ya mwili na kwamba ngano iliyo umuka ya duara ni nzuri. "Tumbo lako lina rangi nzuri na liladuara kama ngano iliyo umuka."
ngano iliyo umuka
Hii ni ngano iliyo kusanywa baada ya watu kuipeta na kuisaga.
kuzungushiwa nyinyoro
Maua mazuri yanafanya ngano iliyo petwa na kukusanywa kuonekana nzuri.
nyinyoro
aina ya maua makubwa
Song of Solomon 7:3-4
Maelezo ya Jumla
Mpenzi wa mwanamke anaendelea kuelezea yeye anaye mpenda.
Maziwa yako mawili ni kama watoto wawili wa ayala, mapacha wa ayala
Ona jinsi ulivyo tafsiri: 4:4
Shingo yako ni kama mnara wa pembe
Mpenzi analinganisha shingo yake na mnara uliyo tengenezwa kwa madini ya mapembe.
macho yako ni kama maziwa ya Heshiboni
"macho yako ni meupe na yana ng'aa kama mabwawa ya maji ya Heshiboni."
Heshiboni
jina la mji wa mashariki wa mto wa Yordani
Bathi Rabimu
jina la mji
Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni
Pua yake ni ndefu na wima kama vile mnara uivyo mrefu na wima.
ambao watazama Damasko
"unao wawezesha watu kutazama kuelekea Damasko"
Song of Solomon 7:5-6
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kumuelezea yeye anaye mpenda.
Kichwa chako ni kama Karmeli
Mwanamke analinganishwa na Mlima Karmeli ambao umeinuka kuliko kitu chochote karibu yake.
zambarau nyeusi
Tafsiri zinazo wezekana ni 1) "nyeusi iliyo koa" au 2) "nyekundu iliyo koa."
Mfalme amestaajabishwa na vifundo vyake
"Nywele zinazo ni'ng'inia ni nzuri hadi mfalme anashindwa kuacha kuzitamani."
vifundo
marundo ya nywele yanayo ni'ng'inia kutoka kichwani mwa mwanamke.
Song of Solomon 7:7-8
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaelezea nini angependa kufanya kwa yeye anaye mpenda.
Urefu wako ni wa kama mti wa mtende
"Una simama kama mti wa mtende." Mwanamke ni mrefu, kasimama wima, na anavutia kama mti wa mtende.
mti wa mtende
mti mrefu wa wima unao zalisha matunda matamu ya rangi ya brauni yanayo ota kwa makundi
maziwa yako kama vifungu vya matunda
Mbegu katika mti wa mtende vinaota katika vifungu vizuri vinavyo teremka chini ya mti.
Ninataka kuupanda ... matawi yake
Mwanamme anataka kumshika mwanamke.
Maziwa yako nayawe kama vifungu vya mizabibu
Mwanamke anataka kushika maziwa yake yaliyo kaza lakini malaini kama mizabibu iliyo jawa na maji yake.
harufu ya pua yako yawe kama mapera
"harufu inayo toka kwenye pua yako inukie vizuri kama mapera."
mapera
Neno "mapera" la husu ladha ya tunda tamu, lenye rangi ya njano, aina nzuri ya tunda.
Song of Solomon 7:9
Maelezo ya Jumla
Mpenzi anaendelea kueleza nini angependa amfanyie mwanamke.
Mdomo wako na uwe kama mvinyo bora
"Ninataka kuuonja mdomo wako kama mvinyo bora."
ukishuka taratibu kwa mpenzi wangu
Mpenzi anafurahia mabusu mororo ya mwanamke.
ukiteleza kwenye midomo yetu na meno
"unao shuka kwenye midomo yetu na meno"
Song of Solomon 7:10-11
Mimi ni wa mpenzi wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:2
na ananitamani
"na ana shauku juu yangu" au "ana nitaka"
Song of Solomon 7:12
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kuzungumza na mpenzi wake.
Tuamke mapema
"inuka mapema" au "amka mapema"
imemea
"ipo katika mwanzo wa kustawi"
imechipua
maua yanapo funguka
imetoa mau
"maua kufunguka kwa mimea"
nitakupa penzi langu
"nitakuonyesha penzi langu" au "nitafanya mapenzi na wewe"
Song of Solomon 7:13
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kuzungumza na mpenzi wake.
Mitunguja
Hili ni jina la mmea unao toa harafu kali lakini nzuri. Harufu kidogo ya lewesha na kuchochea hamu ya kufanya mapenzi.
ya toa harufu yake
"ya zalisha harufu yake"
katika mlango
Ina hashiria kuwa mlango ni wa nyumba yao.
kila aina ya matunda, mpya na ya kale
"kuna kila aina ya matunda mazuri, yaliyo mapya na ya zamani"
niliyo kuhifadhia
"kubakiza kwa ajili yako" au "kulinda kwa ajili yako"
Song of Solomon 8
Song of Solomon 8:1
kama kaka yangu
Mwanamke anatamani angemuonyesha mpenzi wake mahaba hadharani kama ngefanya kwa kaka yake. Hasemi kuwa mwanamke anaruhusiwa kufanya mapenzi na kaka yake.
ningekuona nje
"wewe hadharani"
ningekubusu
Mwanamke inawezekana anambusu kaka yake kwenye shavu kumsalimia.
kunidharau
"kunifanya nijisika haya"
Song of Solomon 8:2-3
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kuzungumza na mpenzi wake.
Nitakuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu
Kama mpenzi angekuwa kaka yake, angemleta kwa nyumba ya familia. Hii ilikuwa kawaida katika huo utamaduni na bado unaendelea kwa baadhi.
na utanifundisha
Hii yaweza tafsiriwa kama "na ata nifundisha." Kwasababu mwanamke hana uzoefu wa kufanya mapenzi, ana fikiri kuwa mpenzi wake au mama yake angemfundisha jinsi ya kufanya mapenzi.
Nitakupa mvinyo ulio chachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga
Mwanamke anatumia haya maumbo kusema kuwa atajitolea kwa mpenzi wake na kufanya mapenzi naye.
mvinyo ulio chachwa
"mvinyo wenye viungo" au "mvinyo wenye viungo ndani yake" Hii ya wakilisha nguvu ya kulevya ya mapenzi.
jwisi ya komamanga
Mwanamke ana wakilisha kimiminika chake na maji ya komamanga.
Mkono wake wa kushoto...wanikumbatia
Tazama ilivyo tafsiriwa "Mkono wake wa kushoto upo chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kulia wanikumbatia" ndani ya 2:5.
Song of Solomon 8:4
Ninataka ... wanaume wa Yerusalemu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:7
kuwa ... hadi yatakapo isha
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:7
Song of Solomon 8:5
Maelezo ya Jumla
Hapa ni mwanzo wa Sehemu ya Sita ya kitabu, sehemu ya mwisho
Ni nani huyu anaye kuja
"Mwangalie huyu mwanamke wa ajabu anaye kuja." Ona jinsi ulivyo tafsiri maneno kama haya 6:10
nimekuamsha
"Nimekuamsha uamke"
mti wa mpera
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:3
pale
chini ya mpera
alijifungua wewe
alikuzaa
Song of Solomon 8:6
Maelezo ya Jumla
Mwana mke anaendelea kuzungumza na mpenzi wake.
Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako
Maana zinazo wezekana ni 1) Kwasababu mihuri ilikuwa muhimu, watu waliweka shingoni mwao au mikononi mwao. Mwanamke anataka kuwa na mwanamme wake kama muhuri. Au 2) Muhuri waonyesha nani anamiliki kitu chenye muhuri wake. Mwanamke anataka awe kama muhuri moyoni mwa mpenzi wake na mkononi ili kuonyesha mawazo yake, hisia, na matendo ni yake.
kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti
Mauti ina nguvu sana kwasababu inawashinda ata watu wenye nguvu duniani.
hayana kurudi kama kwenda kuzimu
Kuzimu hakuruhusu watu kurudia uhai baada ya kuwa wamekufa. Mapenzi yana msimamo kama kuzimu kwasababu hayabadiliki.
miale yake yalipuka ... kuliko moto wowote
Mapenzi yana nguvu kama moto.
yalipuka
"kuchomeka ghafla"
Song of Solomon 8:7
Maelezo ya Jumla
Mwanamke anaendelea kuongea na mpenzi wake.
Maji yalio zuka hayawezi kuzimisha upendo
Mpenzi yana nguvu kiasi kwamba ni kama moto mkali usio weza kuzimwa kwa bahari iliyo jawa na maji.
Maji yalio zuka
"Maji ya bahari" au "Kiasi kikubwa cha maji"
hayawezi kuzimisha
"hayawezi kutokomeza" au "hayawezi kuondoa"
wala mafuriko hayawezi kuondoa
Mapenzi kamwe hayabadiliki na ubaki hivyo daima ni kitu ambacho mafuriko yenye nguvu kiasi gani hayawezi kusogeza.
mafuriko
Katika Israeli, maji kutoka kwenye mvua utiririka mabonde marefu membamba. Hii ujenga mafuriko ya maji yenye nguvu kiasi cha kusogeza vizingiti vikubwa na miti. Ata leo mafuriko wakati mwengine uamisha madaraja imara sana.
kuondoa
"kubeba kando" au "kusafishia mbali"
Mwanaume akitoa ... ukarimu wake utadharauliwa
"Ata kama mwanaume ... ata dharauliwa sana."
mali zake zote
"vyote anavyo miliki"
kwa ajili ya upendo
"ili apate mapenzi" au "ili anunue mapenzi"
ukarimu wake utadharauliwa
"watu wata mdharau hakika" au "watu wata mdhihaki vikali"
Song of Solomon 8:8
hatakayo ahidiwa kuolewa
"mwanamme anakuja na kutaka kumuoa"
Song of Solomon 8:9
Maelezo ya Jumla
Kaka zake mwanamke wanaendelea kuongea miongoni mwao.
Kama ni ukuta ... mbao za mierezi
Kwasababu matiti yake ni madogo, ana kifua kitupu kama ukuta au mlango. Kaka zake wana amaua kumpa mapambo ili kumsaidia dada yao kuonekana mzuri zaidi.
tutampamba
"tuta mremba"
Song of Solomon 8:10
matiti yangu sasa ni kama nguzo imara
matiti ya mwanamke ni marefu kama minara.
hivyo nimekomaa machoni pake
Mpenzi wake sasa anamuona ni mwanamke aliye komaa, na hilo la mpendeza.
machoni pake
Hapa "machoni pake" ya husu mpenzi wake.
Song of Solomon 8:11-12
Baali Hamoni
Hili ni jina la mji kaskazini mwa Israeli.
wao ambao watalitunza
"watu watakao simamia"
Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake
"Kila mwanaume alipaswa kumpatia Sulemani shekeli elfu moja kama malipo ya matunda ya shamba la mizabibu.
kuleta shekeli elfu moja za fedha
"kuleta shekeli 1,000 za fedha"
Shamba langu ka mzabibu ni langu
"Mimi ndiye muhusika wa shamba langu la mizabibu." Mwanamke anajitaja kama shamba la mizabibu kama ilivyo 1:5
shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi
Mwanamke ana mpatia bure faida ya mizabibu kwa Sulemani japo kuwa ni yake anaeza kumpa yeyote anayetaka.
Song of Solomon 8:13
sauti yako
"kwa sauti yako"
Song of Solomon 8:14
uwe kama paa au mtoto wa paa
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:16
milima ya manukato
Mwanamke anatumia hili umbo kukaribisha mpenzi wake amfurahie.