2 Samuel
2 Samuel 1
2 Samuel 1:1-2
Siku ya tatu
"Baada ya siku tatu"
Nguo zake zikiwazimeraruliwa na akiwa na vumbi juu ya kichwa chake
Katika utamaduni huu, mtu kurarua mavazi yake na kuweka vumbi kichwani pa mtu lilikuwa tendo la kuombolezo.
Aliinamisha uso wake chini na kujifanya yeye mwenyewe kuwa si kitu
Hili lilikuwa ni tendo la kuonesha utii kwa Daudi, ambaye kwa wakati huo alikuwa mfalme wa Israeli.
2 Samuel 1:3-5
Wengi wameanguka na wengi wameuawa
Maana yake yaweza kuwa 1) "Wengi walikuwa wamejeruhiwa na wengine walikuwa wameuawa" au 2) "Wengi walikuwa wamejeruhiwa na kuuawa."
2 Samuel 1:6-7
Kwa bahati nilikuwa
Taarifa hii inasisitiza kwamba mtu yule hakuwa amepanga kukutana na Sauli
Sauli alikuwa ameegemea mkuki wake
Maana yake yaweza kuwa 1) Sauli alikuwa amedhoofika na alitumia mkuki kumsaidia au 2) Sauli alikuwa akijaribu kujiuwa kwa kuuangukia mkuki wake.
2 Samuel 1:8-10
Akaniuliza, 'Wewe ni nani?' Nikamjibu, 'Mimi ni Mwamaleki.'
Nukuu hii ingeweza kutaarifiwa kama kauli tendwa. Mfano "Aliniuliza mimi nilikuwa nani, nami nikamwambia kuwa nilikuwa Mwamaleki"
Mimi ni Mwamaleki
Hawa ni watu walewale Daudi aliokuwa ametoka kuwashambulia katika 1:1.
shida kubwa imenipata
Shida ya Sauli inasemwa kama kitu cha kutisha ambachokimemshikilia. Maana nyingine yaweza kuwa "nimeteswa vibaya sana"
uhai ungalimo ndani yangu
Nahau hii inamaanisha kwamba yu ngali hai au "ningali hai"
asingeweza kuishi baada ya kuwa ameanguka
"Hata hivyo angekufa tu"
2 Samuel 1:11-13
Daudi akararua mavazi yake... watu waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile
Daudi na watu wake walirarua mavazi yao kama ishara ya kuomboleza kwa ajili ya Mfalme Sauli.
alikuwa ameanguka
Hii inamaanisha "alikuwa ameuawa."
Kwa upanga
Hapa upanga unahusianishwa na vita, yaweza kumaanisha "katika magwanda ya kijeshi"
Unatoka wapi?
Yule mtu alikuwa amekwisha eleza kuwa yeye ni Mwamaleki katika 1:8. Bila shaka Daudi anamwuliza yule mtu kuthibitisha kwa sababu ya hukumu kali aliyokuwa anaelekea kuitamka juu ya mtu yule.
2 Samuel 1:14-16
Kwa nini hakuogopa kumwua mtiwa mafuta wa Yahwe... mkono?
Mbalaga ni swali linalotumika kumkemea mtu. inaweza kutafsiriwa kama taarifa. Ulipaswa kumwogopa Yahwe na usingemwua mtiwa mafuta wake... mkono!"
Mfalme aliyetiwa mafuta na Yahwe
Usemi huu unasimama badala ya Sauli, ambaye alikuwa amechaguliwa na Mungu.
mkono wako
Kirai hiki kinaonesha kufanya jambo fulani wewe mwenyewe, wewe "mwenyewe" au "binafsi"
Mpige chini
Nahau hii inamaanisha "alimwua."
Damu yako i juu ya kichwa chako
Hapa "damu" inaonesha "kumwaga damu" na inahusishwa na kifo. Hapa "kichwa chako" inamwonesha yule mtu na inamaanisha kwamba anawajibika. Yaani "unahusika kwa kifo chako mwenyewe" au "Umesababisha kifo chako mwenyewe"
kinywa chako kimeshuhudia dhidi yako
Hapa "kinywa chako mwenyewe" inamwone yule mtu mwenyewe. "Umejishuhudia mwenyewe"
2 Samuel 1:17-20
Maelezo kwa Ujumla
Daudi anaimba wimbo wa maombolezo kwa Sauli na Yonathani
Wimbo wa Upinde
Hili lilikuwa jina la wimbo
Kitabu cha Yashari
Neno "Yashari" humaanisha "Unyofu."
iliyoandikwa katika Kitabu cha Yashari
Hii ni taarifa ya mwanzo iliyoongezwa kumweleza msomaji yaliyotendeka katika wimbo
Utukufu wako, Israeli, umekufa
"Utukufu wako" inamwonesha Sauli.
Wenye uwezo
Kifungu "wenye uwezo" inamhusu Sauli na Yonathani. Kisifa nomino hiki kipo katika wingi, na kinaweza kutaarifiwa kama "wenye uwezo"
wameanguka
Neno "wameanguka" linamaanisha "kufa"
Msisema katika Gathi...msiitangaze katika mitaa ya Ashkeloni
Vifungu hivi viwili vinamaanisha jambo moja na vimerudiwa kama sehemu ya ushairi wa wimbo
Gath...Ashkeloni
Gathi na Ashkeloni ni miwili kati ya miji mikubwa ya Wafilisiti. Wafilisiti walimwua Sauli na Yonathani
ili binti za Wafilisiti wasifurahi...ili binti za wasiotahiriwa wasisherehekehee.
Vifungu hivi viwili vinamaanisha jambo moja na vimerudiwa kama sehemu ya ushairi wa wimbo.
binti za wasiotahiriwa
kifungu hiki kinawahusu watu wasiomfuata Yahwe, kama vile Wafilisiti.
2 Samuel 1:21-22
Milima ya Gilboa
Daudi anaongea moja kwa moja kwa "Milima ya Gilboa" kama kwamba ilikuwa ikisikiliza wimbo wake
Haya na kusiwe na umande juu yenu
Daudi analaani ardhi alipofia Mfalme Sauli vitani. Hii ilikuwa siyo heshima kwa Sauli, aliyekuwa mfalme mtiwa mafuta wa Mungu.
ngao ya mwenye uwezo imechafuliwa
"Mwenye uwezo" hapa inaonesha kwa Sauli. Ngao ilichafuliwa kwa sababu ilianguka juu ya ardhi, na kwa sababu damu ya mfalme ilimwagwa juu yake.
Ngao ya Sauli haijatiwa mafuta tena
Ngao ya Sauli ilikuwa imetengenezwa kwa ngozi. Ili kuitunza, ilipakwa mafuta. Inaweza pia kutafsiriwa kuwa "hakuna mtu atayeijali ngao ya Sauli tena"
Kutoka katika damu yao waliouawa, kutoka miili ya wenye nguvu, upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, na upanga wa Sauli haukurudi patupu
Sauli na Yonathani wanaoneshwa hapa kuwa wapiganaji hatari na mashujaa.
upanga wa Sauli haukurudi patupu
Upanga wa Sauli unazungumziwa kama kitu hai kwamba ungeweza kurudi wenyewe. Badala ya kurudi patupu, ulikuwa ukiwa na damu ya adui wa Sauli uliowauwa.
2 Samuel 1:23-24
hawakutenganishwa wakati wa kufa kwao
Kirai "hawakutenganishwa"kinasisitiza kuwa walikuwa pamoja wakati wote. Inaweza pia kuwa kwamba "hata wakati wa kufa kwao walikuwa pamoja"
Walikuwa wepesi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.
Sauli na Yonathani wanaongelewa kana kwamba walikuwa na kasi kuliko tai na nguvu kuliko simba.
aliyewavika mavazi ya thamani pamoja na vito vya thamani, na aliyetia mapambo ya dhahabu katika mavazi yenu.
"Aliyewapa mavazi mazuri na mapambo." Virai viwili hivi vinamaana moja inayolenga juu kuwaandalia wanawake mavazi ya thamani na ya kuvutia.
2 Samuel 1:25-27
Jinsi wenye uwezo walivyoanguka
Kifungu hiki kinajirudia katika mstari wa 25 na 27 kusistiza kwamba mashujaa hodari wa Israeli wamekufa. Inaweza pia kuwa "Watu wenye uwezo wamekufa vitani.
wenye nguvu
"nguvu" hapa ina wingi na inaweza kumhusu Sauli na Yonathani pekee, au askari wote wa Israeli. Inaweza pia kuwa mashujaa wenye nguvu.
wameanguka
hii ni njia laini ya kusema "wamekufa vitani."
Yonathani amekufa
Hii inaweza kutaarifiwa katika kauli tendaji. Yaani "Yonathani amekufa vitani" au adui amemwua Yonathani"
Juu ya mahali pako pa juu
Daudi anaendelea kuielekeza sehemu hii ya wimbo katika milima ya Gilboa kama alivyoanza katika 1:21.
Yonathani ndugu yangu
"ndugu" hapa imetumika katika hali ya urafiki wa karibu sana.
Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, kupita upendo wa wanawake.
Hapa "upendo" umetumika katika hali ya urafiki na uaminifu. Uaminifu wa Yonathani kwa Daudi ulikuwa mkuu kuliko uaminifu alionao mwanamke kwa mmewew na watoto.
silaha za vita zimeangamizwa
"silaha zao zimeharibiwa"
2 Samuel 2
2 Samuel 2:1-3
baada ya haya
Baada ya Daudi kuomboleza kifo vya Sauli na Yonathani vitani.
panda katika mojawapo ya miji ya Yuda
Siklagi ulikuwa chini katika mwinuko kuliko Yuda. Inaweza pia kuwa "uendee mmojawapo ya miji ya Yuda"
Daudi akaenda pamoja na wakezi wawili.
Siklagi ulikuwa chini kuliko Hebroni. Inaweza kuwa pia kwamba "Daudi alisafiri kwenda Hebrani pamoja na wake wake wawili"
2 Samuel 2:4-5
Daudi alitiwa mafuta kuwa mfalme
Katika tendo hili la fumbo, walitia mafuta juu ya kichwa cha Daudi kuonesha kwamba amechaguliwa kuwa mfalme.
nyumba ya Yuda
Hapa "nyumba" imetumika kuonesha kabila. Yaani kabila la Yuda.
Yabeshi Gileadi
Hili ni jina la mji katika eneo la Gibea.
2 Samuel 2:6-7
Maelezo kwa Jumla
Daudi anaongea na watu wa Yabeshi Gileadi
Jambo hili
Walimzika Sauli
mikono yenu itiwe nguvu
Hapa "mikono" inawaonesha watu wa Yabeshi Gileadi. Yaani "mwe imara"
wamenitia mafuta kuwa mfalme
Katika tendo hili, walimimina mafuta juu ya kichwa cha Daudi kuonesha kwamba alikuwa amechaguliwa kuwa mfalme.
2 Samuel 2:8-9
Ner...Ishboshethi
Haya ni majina ya wanaume
Mahanaim...Gileadi...Yezreeli
Haya ni majini ya sehemu
2 Samuel 2:10-11
nyumba ya Yuda
Hapa ''nyumba" imetumika kumaanisha "kabila"
nyumba ya Yuda ilimfuata Daudi
Kutii utawala wa Daudi kunaoneshwa kama kumfuata. Yaani "kabila la Yuda walimtii Daudi kama mfalme wao"
2 Samuel 2:12-13
Abneri...Neri...Ishboshethi...Sauli...Seruya
Haya ni majina ya wanaume
2 Samuel 2:14-15
Abneri
Abneri alikuwa ni binamu wa Mfalme Sauli katika Agano la Kale *Abneri alikuwa Jemedari mkuu wa jeshi la Sauli, na alimtambulisha kijana Daudi kwa Sauli baada ya Daudi kumwua Goliathi
-inuka,inuka,inuka,inuka, inuka
-inuka, inuka juu - kwa ujumla, neno "inuka" linamaanisha"inuka juu" au "weka juu."
Benjamini
Alikuwa mtoto mdogo kuliko wote aliyezaliwa kwa Yakobo na mke wake Raheli. Jina linamaanisha, "mwana wa mkono wangu wa kuume"
2 Samuel 2:16-17
walianguka chini pamoja
Hii ni njia nyepesi ya kusema walikufa. Yaani "walikufa wote wawili"
Helkathi Hazzurimu
Hili ni jina lilitotolewa kuwakumbusha watu kilichotokea pale.
Vita ilikuwa kali sana siku ile
Inaweza kusaidia kueleza kwa ufupi kwamba hii ilikuwa vita kubwa iliyotokea baada ya mashindano ya vijana. Yaani "Wengine pia walianza kupigana pia. Ilikuwa vita kali sana siku hiyo"
2 Samuel 2:18-19
Seruya...Yoabu...Abishai...Asaheli...Abneri
Haya ni majina ya wanaume
Asaheli alikuwa mwepesi miguuni kama swala.
Hapa Asaheli analinganishwa na swala, mnyama akimbiaye kwa kasi sana.
swala pori
Mnyama huyu mdogo mwenye miguu minne, na pembe mbili ndefu kichwani, hukimbia haraka sana.
Akimfuatia bila kugeuka upande mwingine
Hapa "bila kugeuka" imeelezwa kwa muundo hasi kusistiza ukaribu alioifuata njia ya Abneri.
2 Samuel 2:20-21
Asaheli
Hili ni jina la mwanaume
Kugeuka...geuka upande
"usinifuate...acha kumfuata Abneri"
kamata mmojawapo ya vijana na uchukue silaha yake
Abneri alikuwa akimwambia Asaheli kuua na kumteka askari kijana ambaye siyo hatari kama Abneri. Hakutaka kumwua Asaheli.
2 Samuel 2:22-23
Kwa nini nikupige hata chini
Swali hili lisiloitaji jibu linatumika kumwonya Asaheli hatari iliyomkabili. "Kupiga hadi chini" ni njia laini ya kusema "kuuwa." Yaani "sitamani kukuuwa."
Jinsi gani basi ningeweza kumtazama usoni Yoabu, nduguyo?
Swali hili lisilohitaji jibu linasisitiza kwamba Abneri hapendi kupigana na kumwua Asaheli kwa sababu ingeharibu uhusiano wake na Yoabu. Hapa "kuinua uso wangu kwa Yoabu" inamaanisha angekuwa na aibu sana kumtazama Yoabu.
geuka upande
Hii inamaanisha "kuacha kumfuatia"
sehemu ya mwisho ya mkiki wake
Hii inaonesha mpini, ambayo siyo kali au kuweza kuchoma kitu. Inaweza kuwa kwamba Abneri alikuwa akijaribu kumzuia Asaheli asimfuatie, na hakukusudia kumwua.
2 Samuel 2:24-25
Abishai
Hili ni jina la mwanamme
kilima cha Ama...Gia
Haya ni majina ya sehemu
2 Samuel 2:26-27
Kuita
"piga kelele"
Ni lazima upanga urarue daima?
Swali hili linasisitiza kwamba vita ilikuwa imeendelea muda mrefu. Hapa "upanga" inaonesha mapigano. Mauaji katika vita yanaoneshwa kama mnyama wa mwituni anakula askari. Inamaanisha pia "Hatuitaji kutumia kupigana na kuuana."
Je haujui kwamba itakuwa uchungu mwishowe?
Swali linatumika kumlazimisha Yoabu kukubari kwamba kuendelea kupigana kungeishia maafa makubwa. Hapa "uchungu" ni neno lililotumika kuonesha matesa makali ambayo yangetukia.
Je hata lini utawazuia watu wako wasiwafuatie ndugu zao.
Swali hili linakusudiwa kumshawishi Yoabu kuacha kupigana na Waisraeli wenzake. Hapa "ndugu" inawakilisha watu wa taifa la Israeli. Yaani "Acha sasa jambo hili ili Waisraeli wasiendelee kuuana.
kama Mungu aishivyo
Hiki ni kiapo kikubwa sana. Inamaana ya "pamoja na Mungu kama shahidi wangu" au "Mungu anathibitisha kuwa namaanisha ninachosema."
kama usingesema hivyo...kuwafuatia ndugu zao hata asubuhi
Taarifa hii ya kukisia inaongelea ambacho kingetokea kama Abneri asingemwambia Yoabu kwa hekima.
2 Samuel 2:28-29
piga tarumbeta
tarumbeta zilitumika kuashiria agizo kulingana na umbali.
kuwafuatia Israeli tena
Hapa "Israeli"inaonesha watu waliokuwa wanapigana upande wa Israeli.
Araba...Mahanaimu
Haya ni majina ya sehemu
2 Samuel 2:30-32
Asaheli
Hili ni jina la mwanamme
watu 360 wa Benjamini pamoja na Abneri
"watu 360 kutoka Benjamini waliomfuata Abneri." Abneri hakufa.
wa Benjamini
Kifungu kinamaanisha "kutoka kabila la Benjamini."
Kumwinua Asaheli
"waliochukua mwili wa Asaheli"
Siku ikawia asubuhi huko Hebroni
"walifika Hebrono alfajiri asubuhi iliyofuata."
2 Samuel 3
2 Samuel 3:1
Sasa
Neno limetumika hapa kuonesha mkato katika habari kuu. Samweli hapa anatoa habari kuhusu vita kati ya Daudi na wafuasi wa Sauli.
nyumba
hapa "nyumba" inamaanisha "wafuasi."
kuwa imara zaidi na zaidi
kifungu hiki kinamaana ya idadi ya watu waliomsaidia Daudi kuongezeka
kudhoofika zaidi na zaidi
kifungu hiki kinamaanisha kupungua kwa idadi ya walioisaidia nyumba ya Sauli
2 Samuel 3:2-3
wana walizaliwa kwa Daudi
Hii inaweza kutaafiwa katika muundo tendaji. Yaani wake wa Daudi walizaa wana sita
mzaliwa wa kwanza...mwana wa pili...tatu
Hii ni hesabu kwa mpangilio wa wana wa Daudi
Ahinoamu...Abigaili...Maaka
Haya ni majina ya wanawake. Ni wake wa Daudi.
Kileabu...Nabali...Talmai
Haya ni majina ya wanaume.
2 Samuel 3:4-5
mwana wa nne...mwana wa tano...wa sita
Hii ni hesabu ya mpangilio wa wana wa Daudi
Shefatia...Ithreamu
Haya ni majina ya wana wa Daudi
Haggithi...Abitali...Egla
Haya ni majina ya wakeze Daudi.
2 Samuel 3:6-7
Ikawa
Inatambulisha tukio jipya katika habari ya mzozo kati ya wafuasi wa Daudi na familia ya Sauli.
Nyumba ya Sauli
Inaonesha familia ya Sauli na wafuasi waliochukuo umiliki wa maeneo yake alipokufa.
nyumba ya Daudi
Inaonesha wafuasi wa Daudi.
Abneri akajipa nguvu katika nyumba ya Sauli
Kuongezeka kwa nguvu ya Abneri juu ya familia ya Sauli kunasemwa kama alikuwa na nguvu za mwili. Yaani "Abneri akawa na nguvu zaidi juu ya familia na wafuasi wa Sauli"
Rizpa...Aiya
Haya ni majina ya wanawake.
Ishboshethi
Hili ni jina la kiume, mwana wa Sauli.
Kwa nini ulilala na suria wa baba yangu?
Isboshethi anauliza swali hili kumkemea Abneri akifanya kama mfalme. Yaani "Haukuwa na haki ya kulala na suria wa baba yangu!"
kulala na
Hili ni linalopunguza ukali wa neno likimaanisha kukutana kimwili.
2 Samuel 3:8
Je mimi ni kichwa cha mbwa aliye wa Yuda?
Swali hili limetumiwa na Abnera kama hasira ya kukataa lawama ya Isboshethi. Hinaweza kufasriwa kama taarifa. Yaani "mimi siyo msaliti nikimtumikia Daudi!"
mkonono mwa Daudi
Hapa "mkono"inawakilisha nguvu ya kushinda.
Na bado leo unaniraumu kwa ajili ya huyu mwanamke?
Abneri anauliza swali hili kwa ajili ya kumkemea Ishboshethi. Haiko wazi kama kweli Abneri alilala na Rispa, au kama aliraumiwa kwa uongo. Maana yake inaweza kuwa 1) Abneri alikuwa na hatia. Yaani "haupaswi kujisikia vibaya kwamba nililala na mwanamke huyu!" au 2) Abneri hakuwa na hatia. Yaani "haupaswi kudhani kwamba nimelala na mwanamke huyu!"
2 Samuel 3:9-11
Mungu na anitendee hivyo ...na zaidi pia, ikiwa sifanyi
Huu ni muundo wa nadhiri ya dhati katika siku hizo. Abneri anamwomba Mungu amhukumu kw a ukali asipoitunza nadhiri yake. Lugh yako mara nyingi ina njia ya kuonesha kiapo. Yaani "namwomba Mungu kuniadhibu nisipotenda.
nyumba ya Sauli
Hapa "nyumba" inaonesha familia na wafuasi wa liosalimiki katika kifo cha Sauli.
kiti cha enzi cha Daudi
Kifungu hiki kinaonesha mamalaka ya Daudi kama mfalme.
2 Samuel 3:12-13
kwa Daudi
Baadhi ya matoleo yanaongeza "alipokuwa huko Hebroni" na mengine yameondoa hiyo. Unaweza kuongeza kifungu ikiwa kimo katika toleo la taifa.
Nchi hii ni ya nani?
Nakala la halisi ya swali hili haiko wazi. Maana pendekezwa ni 1) Abneri alikuwa na nguvu ya kumpa Daudi nchi. Yaani "Nchi hii ni yangu au 2) Daudi amechanguliwa na Mungu kuitawala nchi: Yaani nchi hii ni haki yako.
mkono wangu uko pamoja nawe
Hapa "mkono" unawakilisha msaada waa Abneri anaoutoa kwa Daudi. Yaani:"Nitakusaidia"
hautauona uso wangu mpaka umlete kwanza Mikali
Daudi anaeleza masharti ya kukutana na Abneri. Hapa "uso" inamhusu Daudi mwenyewe. Yaani: "Hautaniona mpaka umlete Mikali kwanza.
Mikali
Hili ni jina la binti Sauli. Alikuwa mke wa kwanza wa Daudi.
2 Samuel 3:14-16
magovi mia moja ya Wafilisiti
Hii inawakilisha namba ya watu aliowaua Daudi ili Sauli amruhusu kumwoa Mikali. Govi ni sehemu iliyojikunja inayofunika kiungo cha uzazi cha mwanamme.
kumtoa kwa mme wake
Paltieli alikuwa mme wa pili wa Mikali. Sauli alimpa baada ya Daudi kumkimbia Sauli.
Paltieli... Laishi
Haya ni majina ya wanaume
Bahurimu
Hili ni jina la kijiji.
2 Samuel 3:17-18
Basi fanya hivyo
"Hivyo sasa mfanyeni Daudi kuwa mfalme wenu"
Kwa mkono wa mtumishi wangu Daudi
Hapa "mkono" unataja nguvu ya Daudi kuwashinda Wafilisiti. Yaani nitamtia nguvu mtumishi wangu Daudi"
mkono wa Wafilisiti
Hapa "mkono" unaonesha nguvu juu ya Israeli. Yaani:"nguvu ya Wafilisiti"
mkono wa adui zao wote
Hapa "mkono" unaonesha nguvu juu ya Israeli. Yaani: "nguvu ya adui zao wote"
2 Samuel 3:19-20
ishirini kati ya watu wake
Idadi ya watu waliokuja na Abneri
watu wa Benjamini...nyumba yote ya Benjamini
taarifa zote mbili zinahusu wazao wa Benjamini, waliokuwa mojawapo ya makabila ya Israeli
2 Samuel 3:21
Israeli wote
Kifungu himi kinamaanisha "wote katika taifa la Israeli."
Hivyo Daudi akamruhusu Abneri kuondoka
Waliachana kama marafiki. Daudi hakuwa amemkasirikia Abneri.
2 Samuel 3:22-23
mateka
Hivi ni vitu vinavyochukuliwa kutoka kwa adui.
Abneri hakuwa na Daudi huko Hebroni
Tiyari Abneri alikuwa ameondoka kurudi nyumbani.
wakamwambia Yoabu
"mtu fulani alimwambia Yoabu"
Neri
Hili ni jina la mwanamme. Yeye ni babu wa Sauli.
2 Samuel 3:24-26
Umefanya nini?
Hili ni swali lililoulizwa na Yoabu ili kumkemea Daudi kwa kumwacha Abneri kuondoka kwa amani. "Usingefanya hivi!"
Kwa nini umemwacha aondoke?
Yoabu anauliza swali hili kwa kumkemea Daudi kwa kumwacha Abneri kutoroka. Inaweta kufasiriwa kama taarifa. Yaani "Abneri alikuwa hapa nawe umemwacha aondoke!"
Je haujui...kila ukifanyacho?
Yoabu anauliza swali hili kumshawishi Daudi kuamini kwamba Abneri anapanga njama dhiki ya Daudi. Yaani: "Hakika unajua... kila ukifanyacho."
Kisima cha Sira
"Sara" ni jina la mahali kisima kilipokuwa.
2 Samuel 3:27
katikati ya lango
Hii inahusu mojawapo ya malango katika ukuta wa mji huko Hebroni. Kama UDB inavyoonesha, malango ya mji yalijengwa kama sehehu ya majengo yaliyowekwa ukutani. Ndani ya njia kulikuwa na milango kuelekea vyumba vya ndani, mahali wageni wangepokelewa na biashara na shughuli za kimahakama zingefanyika. Yawezekana ilikuwa ndani ya mojawapo ya vyumba hivi Yoabu alimwua Abneri
damu ya Asaheli
Hapa "damu"inahusishwa na kifo cha Asaheli. Yaani: "kifo cha Asaheli"
Asaheli
Hili ni jina la mwanamme.
2 Samuel 3:28-30
Neri...Abishai...Asaheli
Haya ni majina ya wanaume.
damu ya Abneri
"Damu" hapa inahusu kifo cha Abneri.
iwe juu ya kichwa cha Yoabu
Kifungu kinamaanisha tokeo la hatia litakuwa juu ya Yoabu na familia yake kama kitu kizito kilichoanguka juu yao. Yaani kusababisha "matatizo kwa Yoabu siku zote"
nyumba yote ya baba yake
"Nyumba" hapa inahusu vizazi. Kifungu "nyumba yote ya baba yake" kinarejea kwa uzao wote wa baba wa Yoabu.
Kusikosekane kuwa
Huu ukanushi wa kujirudia unasisitiza kuwa kutakuwa na mtu daima mwenye matatiza yaliyoainishwa.
ameuawa kwa upanga
"Upanga" hapa unarejesha kwa kifo kibaya. "Yaani alikufa vibaya"
anayekwenda bila chakula
"mwenye njaa"
2 Samuel 3:31-32
Rarua mavazi yako, vaa gunia
Haya yalikuwa matendo ya kuonesha uzuni.
Mfalme alilia kwa sauti
Maneno "alilia" na "alilia kwa sauti" kwa kawaida yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza jinsi gani Daudi alimwombolezea Abneri.
2 Samuel 3:33-34
Je ilimpasa Abneri kufa kama afavyo mpumbavu?
Hili swali lisiloitaji jibu hutumika kuonesha kwamba kifo chake hakikuwa cha haki.
Mikono yako haikuwa imefungwa. Miguu yako haikuwa imefungwa minyororo.
Sentensi mbili hizi zinaonesha wazo moja. Yanaweza kuunganishwa katika sentense moja. Yaani "Haukuwa mwalifu gerezani" au "ulikuwa mwenye haki kwa kutofanya kosa"
Mikono yako haikuwa imefungwa
Hii inaweza kuelezwa katika kauli tendaji. Yaani "Hakuna aliyekuwa amekufunga mikono"
Miguu yako haikuwa imefungwa
Hii inaweza kuelezwa katika kauli tendaji. Yaani "Hakuna mtu aliyekuwa amekufunga minyororo miguu.
wana wa uovu
Hii inarejea kwa watu wasio haki au waovu.
2 Samuel 3:35-36
watu wote wakaja
Huku kutia chumvi kwa kukusudia kunatumika kuonesha kuwa taifa la Israeli kumjari Daudi katika uzuni yake. Yaani:"Watu wengi walikuja"
Mungu na anifanyie hivyo, na zaidi, ikiwa
Huu ni muundo wa nadhiri ya dhati wakati huo. Daudi anamwomba Mungu kumhukumu kwa ukali ikiwa atakula chochote kabla ya jua kuchwa. Yaani "Ninamwomba Mungu anaifanyie hivyo ikiwa"
2 Samuel 3:37-39
Je hamjui kwamba mtu mkuu ameanguka leo hii katika Israeli?
Swali hili lisilodai jibu limetumika kuonesha jinsi Daudi alivyomweshimu Abneri. Hapa "kuanguka"ni neno linalomaanisha "kifo". Inaweza kutafsiriwa kama taarifa. Yaani: Ni wazi kwamba mtu mkuu amekufa leo katika Israeli!"
mwana mfalme na mtu mkuu
Vifungu hivi viwili vyote vinamrejerea Abneri.
Neri...Seruya
Haya ni majina ya wanaume.
ukatili
"bila huruma"
2 Samuel 4
2 Samuel 4:1-3
Ishbosheth...Baana...Rekabu...Rimoni
Haya ni majina ya wanaume.
Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili...muda huu
Hii inawatambulisha Baana na Rekabu katika habari.
mikono yake ikadhoofika
Katika kifungu hiki "mikono yake" inamwakilisha Ishboshethi. Yaani: "Ishboshethi akadhoofika au kupoteza nguvu"
maana Beerothi pia ilihesabiwa kuwa sehemu ya Benjamini, na Wabeerothi walikimbilia Tittaim na wamekuwa wakiishi pale mpaka sasa
Hapa mwandishi anatoa mazingira ya Beerothi kwa msomaji. Beerothi ilikuwa sehemu ya nchi ya Benjamini.
Beeroth...Gittaim
Haya ni majina ya sehemu.
2 Samuel 4:4
Maelezo kwa Jumla
Mstari huu unaacha habari kuu na kutoa maelezo ya mazingira kuhusu Mefiboshethi, uzao wa Sauli kupitia Yonathani badala ya Ishboshethi. Baadaye Mefibosheshi atakuwa mhusika mhimu katika kitabu.
Umri wa miaka mitano
Huu ulikuwa ni umri wa mwana wa Yonathani wakati wa kifo cha baba yake.
Kilema cha miguu
Kifungu kinamaanisha "kutokuweza kutembea."
habari kuhusu Sauli na Yonathani
Hii inarejea kwa taarifa kuhusu vifo vyao.
Mlezi
Huyu ni mwanamke au msichana aliyeajiriwa kulea watoto wadogo
akawa kilema
Hii inaeleza jinsi Mefiboshethi alivyojeruhiwa hivyo kutokuweza kutembea.
Mefiboshethi
Hili ni jina la mwana wa Yonathani, mjukuu wa Sauli.
2 Samuel 4:5-7
Maelezo kwa Jumla
Habari inarudi kwa tendo la Baana na Rehabu waliokuwa wemetambulishwa katika 4:1
Joto la mchana
Mchana, sehemu ya siku ambapo joto ni kali zaidi
kupepeta ngano
"kuondoa makapi kutoka katika ngano.
2 Samuel 4:8-10
anatafuta maisha yako
usemi unamaanisha "anataka kukuua."
Kama aishivyo Yahwe
Hii ni kati ya nadhiri zenye nguvu Daudi alizoziapa, kama ambavyo Yahwe ni shahidi. Yaani: "Naapa kwa uhai wa Yahwe"
aliyeniuokoa uhai wangu
"Uhai" hapa unarejea kwa Daudi mwenyewe. Yaani "aliyeniokoa"
2 Samuel 4:11-12
Ni kiasi gani zaidi...nisiutake uhai wake kutoka mkononi mwako, na kukuondoa kutoka duniani?
Swali hili linaonesha kwamba watu walikuwa wametenda kosa kubwa sana. Inaweza kutafsiriwa kama taarifa. Yaani: "hata unahatia kubwa zaidi! Ni wajibu wangu kutaka damu yake kutoka mkononi mwako na kukuondoa duniani."
kutaka damu yake mkononi mwako
Kifungu "damu yake" kinawakilisha uhai wa Ishboshethi. Hapa "kutoka mkononi mwako"inawakilisha Rehab na Baana, wana wa Rimon Mbeerothi kutoka 4:5. Yaani: "tazama unawajibika kwa kifo cha Ishboshethi"
kata mikono na miguu yao na kuwatundika
Hii yalikuwa matendo ya kuonesha ukali kwa hao watu.
wakakichukua kichwa cha Ishboshethi na kukizika kaburini
hili lilikuwa ni tendo la kuonesha heshima kwa Ishboshethi. Hii ingeweza kuelezwa kwa ufupi. Yaani "walimweshimu Ishboshethi kwa kuzika kichwa chake kaburini."
2 Samuel 5
2 Samuel 5:1-2
tu nyama na mfupa wako
Kifungu kinamaanisha "undugu." Yaani "sisi tunauhusiano nawe" au sisi tu wa familia moja."
wakati mfupi uliopita
Hii ni habari ya kihistoria. Sauli alikuwa mfalme wao kabla ya Daudi.
Utawachunga watu wangu Israeli, nawe utakuwa mtawala juu ya Israeli
Vishazi viwili hivi vinamaanisha kimsingi jambo moja na linasistiza kwamba Yahwe alikuwa amemchagua Daudi kuwa mfalme.
Utawachunga watu wngu Israeli
Hapa kuwatawala watu kunazungumzwa kana kwamba ni kuwachunga. Yaani: "utawaangalia watu wangu Israeli" au "Utatawala juu ya Israeli watu wangu"
2 Samuel 5:3-5
Wakamtia mafuta Daudi kuwa mfalme juu ya Israeli
"Kutiwa mafuta" ni tendo la alama ya kuonesha kwamba wanatambua kwamba Mungu alikuwa amemchagua Daudi kama mfalme.
2 Samuel 5:6-7
Maelezo kwa Jumla
Daudi na jeshi la Israeli wanaishambulia Yerusalemu
Hautaingia humu isipokuwa utazuiwa na vilema na vipofu
Hii inaweza kuelezwa katika muundo chanya. Yaani: "ikiwa utakuja hapa, hata vipofu na vilema wataweza kukuondoa."
vipofu na vilema
Watu wasioweza kuona wala kutembea
2 Samuel 5:8-10
Daudi akasema, "Watakaowapiga Wayebusi
Daudi alikuwa akiongea na askari wake. Yaani: Daudi aliwambia askari wake, "Wanaotaka kuwa ondoa Wayebus" (UDB)
'Vipofu na vilema'
Maana pendekezwa ni 1) hii inarejerea kwa watu ambao ni vilema na vipofu kweli au 2) hii ni maana inayoonesha Wayebusi ndani ya Yerusalemu kama wote walikuwa dhaifu na wasio na uwezo.
2 Samuel 5:11-12
Hiram
Hili ni jina la mwanamme
mafundi selemala
wanaoshughulika na mbao
Wajenzi
wanaojenga
2 Samuel 5:13-16
Shamua...Shobabu...Nathani...Sulemani...Ibari...Elisha...Nefegi...Eliada...Elifeleti
Haya ni Majin ya wana wa Daudi
wana na binti walizaliwa kwake
hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. Yaani: "alikuwa na wana zaidi na mabinti" au "walimzalia wana zaidi na mabinti"
waliozaliwa kwake
Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. Yaani "kwamba wakeze walimzalia" au "alikuwa"
2 Samuel 5:17-18
Daudi alikuwa ametiwa mafuta kama mfalme juu ya Israeli
Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. Yaani: "Israeli walikuwa wamemtia mafuta Daudi kama mfalme"
wakatoka wate wakimtafuta
Kifungu hiki kinarejea kwa baadhi ya Wafilisiti wakimtafuta Daudi.. Kina tia chumvi kuonesha ni kiasi gani Wafilisiti walivyotaka kumpata Daudi.
Bonde la Mrefai
Hili ni jina la mahali
2 Samuel 5:19-21
Baali Perazimu
Hili ni jina la sehemu.
Yahwe amewafurikia adui zangu mbele zangu kama mafuriko ya maji
Daudi anazungumzia ushindi aliompa Yahwe kama yalikuwa mafuriko yaliyopitiliza kingo zake na kuifunika nchi, yakisababisha uharibifu. Yaani: "Yahwe amewashinda adui zangu kama mafuriko yanavyoishinda nchi"
2 Samuel 5:22-23
Wafilisiti wakaja tena
"Walikuja" kwa sababu Wafilisiti waliishi upande wa chini kuliko ngome ya Daudi.
Bonde la Mrefai
Hili ni jina la sehemu.
miti ya miforosadi
"Miforosadi" ni aina ya miti, na "miti" inaelezea miti ya miforosadi iliyopamoja.
2 Samuel 5:24-25
Mtakaposikia...Yahwe atakuwa amekwenda mbele yenu kulipiga jeshi la Wafilisiti
Hii ni mwendelezo wa maelekezo ya Yahwe kwa Daudi yaliyoanza katika 5:22. Yahwe hapa anajisema katika nafsi ya tatu.
Mtakaposikia sauti ya kwenda katika upepo ukivuma kupitia juu ya miti ya miforsadi
"Wakati upepo unavuma kupitia juu ya miti ya miforsadi kama watu wanaotembea"
Geba...Gezeri
Haya ni majina ya mahali.
2 Samuel 6
2 Samuel 6:1-2
Basi
Neno hili linaonesha sehemu mpya ya taarifa.
watu wote wateule wa Israeli
Aina hii ya maana inawakilisha jeshi la taifa la Israeli.
Elfu thelathini
"30,000"
kutoka Baala katika Yuda kulileta sanduku kutoka pale
Inaonesha kuwa wanalichukua sanduku kutoka Yerusalemu. Yaani: "kutoka Baala uliopo Yuda kulipeleka Sanduku la Mungu huko Yerusalemu"
kulileta sanduku la Mungu kutoka pale
Yerusalemu ilikuwa juu kuliko pengine sehemu nyingine yoyote katika Israeli, hivyo ilikuwa kawaida kwa Waisraeli kusema kukwea au kushuka kutoka Yerusalemu.
kulipandisha
Neno "leta" laweza kutafsiriwa kama "chukua."
Baala
Hili ni jina la mahali
ambalo linaitwa kwa jina langu Yahwe wa majeshi
Jina la Yahwe lilikuwa limeandikwa juu ya sanduku.
akaaye juu ya makerubi
"akaaye katika sehemu ya mamlaka kati ya makerubi"
kukaa katika kiti cha enzi
kukaa juu ya kiti cha enzi au mahali pa mamlaka
2 Samuel 6:3-5
Maelezo kwa Jumla
Daudi na jeshi la taifa la Israeli wanaliondoa sanduku la agano.
Abinadabu...Uza...Ahio
Haya ni majina ya wanaume.
nyumba yote ya Israeli
Aina hii ya maana inawakilisha watu wa Israeli. Yaani: "Waisraeli wengine wote pamoja nao"
Matari
Hiki ni chombo cha kimziki kama kichwa cha ngoma pamoja na vipande vya chuma kuzunguka sehemu inayosikika kifaa kinapotikiswa au kupigwa.
kayamba
chombo cha mziki chenye vitu vingi vidogo vigumu ndani yake, ikifa sauti ya kimziki kinapotikiswa
Matowazi
Sahani mbili nyembamba za chuma zinazogongwa pamoja kufanya sauti ya juu.
2 Samuel 6:6-7
Nikoni
Hili ni jina la mwanaume.
hasira ya Yahwe ikawaka
Hapa "hasira ya Yahwe" inaongelewa kama ilikuwa ni moto.
kwa dhambi zake
Ilikuwa ni dhambi ya Uza kulishika sanduku kwa sababu Yahwe alikuwa ameamru kwamba kusiwepo mtu atakayeligusa sanduku.
2 Samuel 6:8-9
Peresi Uza
Hili ni jina la mahali. Mtu anayetafasiri anaweza kuongeza maelezo ya chini kusema, "Jina Peresi Uza linamaanisha 'adhabu ya Uza."'
hadi siku hiyo
Hii inamaanisha hadi wakati habari hii ilipokuwa inaandikwa, siyo sasa katika karne ya ishirini na moja.
Jinsi gani sanduku la Yahwe lije kwangu?
Daudi anatumia swali hili kusisitiza kwamba anaogopa kulipeleka sanduku Yerusalem. Yaani: "Ninaogopa sana kulileta sanduku la Yahwe Yerusalemu."
2 Samuel 6:10-11
Obedi Edomu Mgiti
Hili ni jina la mwanamme.
alimbariki
"Yey" hapa inarejerea kwa Obedi Edomu Mgiti.
2 Samuel 6:12-13
Basi
Neno hili linaanza kama sehemu mpya ya habari.
Daudi aliambiwa
Hii inaweza kutaarifiwa katika muundo tendaji. Yaani: "watu walimwambia mfalme Daudi"
Nyumba ya Obedi Edomu
"Nyumba" hapa inawakilisha familia. Yaani: "Obedi Edomu na familia yake"
wakalileta sanduku la Mungu
Yerusalemu ilikuwa juu kuliko karibu eneo lolote katika Israeli, hivyo ilikuwa kawaida kwa Waisraeli kuzungumzia kupanda kwenda au kushuka kutoka Yerusalemu. Yaani: "kuondoa sanduku la Mungu"
kupandisha
Neno "kuleta" laweza kufasiriwa kuwa "chukua."
2 Samuel 6:14-15
Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote
Kucheza hapa ni aina ya kumwabudu Yahwe kwa furaha.
kitani
nguo iliyotengenezwa kutokana na nyuzi za mti wa kitani.
nyumba yote ya Israeli
Hapa "nyumba" inawakilisha watu wa Israeli. Yaani: "Waisraeli wengine wote pamoja naye"
kulipandisha sanduku la Yahwe
Yerusalemu ilikuwa juu pengine kuliko eneo lolote katika Israeli, hivyo ilikuwa kawaida kwa Waisreali kusema juu ya kupanda kwenda au kushuka kutoka Yerusalemu.
kupandisha
kifungu hiki"kupandisha" chaweza kufasiriwa kama "chukua."
2 Samuel 6:16-17
Basi...moyoni mwake
Neno "basi" linaonesha kukatishwa kwa habari. Hapa msimuliaji anatoa taarifa juu ya Mikali.
Mikali
Alikuwa ni binti wa Mfalme Sauli na pia mke wa kwanza wa Daudi.
alimdharau moyoni mwake
Hapa "moyo" unawakilisha mawazo na hisia. Yaani: "alimwangalia kwa dharau"
mbele za Yahwe
"kwa Yahwe"
2 Samuel 6:18-19
aliwabariki watu kwa jina la Yahwe wa majeshi
Kubariki "katika jina la Yahwe wa majeshi" inamaanisha kubariki kwa nguvu na mamalaka ya Yahwe, au kama mwakilishi wake.
keki ya zabibu kavu
mkate mtamu uliookwa kutokana na zabibu kavu
2 Samuel 6:20
Mikali
Ni jina la mke wa kwanza wa Daudi.
ondoka
Hapa "alikuja" laweza kufasiriwa kama "kwenda."
Jinsi gani mfalme wa Israeli alivyokuwa mtukufu leo.
Hii ni aina ya usemi. Mikali anamaanisha kinyume cha kile alichosema, na haamini Daudi alitenda kwa heshima. Mikali anazungumzia kucheza kwa Mfalme Daudi na mwenendo wake bila heshima.
mbele ya wacho ya wajakazi
Hapa "macho ya wajakazi" inawakilisha wajakazi. Yaani: "mbele ya wajakazi"
mpumbavu
Daudi analinganishwa na mtu asiye na adabu na mpumbavu.
2 Samuel 6:21-23
aliyenichagua juu ya baba yako
Hapa "yako" inarejerea kwa Mikali.
juu ya watu wa Yahwe, Israeli
Hapa "juu ya watu wa Yahwe" na "Israeli" inamaanisha kitu kimoja.
nitakuwa hata zaidi nisiyefaa kuliko hivi
Daudi anatumia usemi wa kumaanisha kinyume chake. Haamini kwamba alichokifanya hakikuwa na heshima au kwamba matendo yake yatakuwa hayaheshimiwi.
Nitajishusha mbele ya macho yangu mwenyewe
Hapa "katika macho yangu mwenyewe" inawakilisha anachofikiri mtu au kufikiri juu ya kitu fulani. Yaani: "nitajihesabu mimi mwenyewe si kitu"
Lakini kwa hawa wajakazi uliowasema, nitaheshimiwa.
Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. Yaani: "Lakini wajakazi uliowasema wataniheshimu"
hakuwa na watoto hata siku ya kufa kwake
"hakuwa na uwezo wakuzaa watoto hata siku ya kufa kwake"
2 Samuel 7
2 Samuel 7:1-2
Ikawa
Kifungu kinaonesha mwanzo wa habari nyingine.
alipewa kupumzika kutokana na adui wote waliomzunguka
"kupewa usalama kutokana na adui wote waliomzunguka." Hapa "pumziko" ni jina dhahania. Yaani: "kusababisha makundi ya maadui kuacha kushambulia Israeli"
Ninaishi katika nyumba ya mwerezi
Mwerezi ni aina ya mti unaojulikana kwa uimara. Ni sawa na mninga katika utamaduni wetu. Inaaweza kuwa: "Ninaishi katika nyumba nzuri na ya kudumu"
sanduku la Mungu linakaa katikati ya hema
Hema ni makazi ya muda. Yaani: sanduku la Mungu lakaa katika eneo la muda"
2 Samuel 7:3-5
fanya lililomo moyoni mwako
Hapa "moyo" unawakilisha akili. Yaani: "fanya unalofikiri linapaswa kufanyika"
maana Yahwe yupo nawe
Hapa "pamoja nawe" linamaanisha Mungu anamsaidia na kumbariki Daudi.
neno la Yahwe lilikuja
Hii ni aina ya usemi kumaanisha kwamba Yahwe alisema. "Yahwe alisema ujumbe"
neno la Yahwe
Hapa "neno" linawakilisha ujumbe wa Yahwe
na akasema, "Nenda na umwambie Daudi mtumishi wangu, 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Je wewe utanijengea nyumba ya kuishi?
Hii ina nukuu ndani ya nukuu. Yaani: "na kusema, "Nenda na umuulize Daudi kama anadhani atakuwa ndiye wa kunijengea nyumba nitakayoishi."
Je wewe utanijengea nyumba ya kuishi?
Yahwe anatumia nukuu kusisitiza kwamba Daudi hatajenga nyumba kwa ajili ya Yahwe. Nukuu hii inaweza kufasiriwa kama taarifa. Yaani: "Hautanijengea nyumba ya kuishi"
kunijengea nyumba
Hapa nyumba inamaanisha hekalu. Katika 7:11 Yahwe atasema kwamba atamjengea Daudi nyumba. Pale "nyumba" inamaanisha familia.
2 Samuel 7:6-7
Je niliwai kusema jambo lolote kwa kiongozi yeyote wa Israeli niliyemchagua kuwachunga watu wangu Israeli, kusema, "Kwa nini hamjanijengea nyumba ya mwerezi?
Hii ina nukuu ndani ya nukuu nyingine. Nukuu ya moja kwa moja inaweza kuelezwa kama nukuu isiyo ya moja kwa moja. Yaani: "Sijawai kumwambia mmojawapo wa viongozi, niliowachagua, kunijengea hekalu la mbao za mwerezi."
Je niliwai kusema jambo lolote kwa kiongozi yeyote wa Israeli
Yahwe anatumia nukuu kusisitiza kwamba hakuwai kuwambia viongozi wa Israeli kumjengea nyumba.
Kwa nini hamkuwai kunijengea nyumba ya mwerezi?
Ikiwa Yahwe alikuwa amewauliza viongozi swali hili, angekuwa ametumia swali kuwalaumu kwa kutomjengea nyumba ya mwerezi. Lakini, Yahwe alisema hapo mwanzo kwamba hakuwa amewauliza swali hili. Yaani: "Mlipaswa kuwa mmenijengea nyumba ya mwerezi."
niliowateua kuwachunga watu wangu Israeli
Viongozi wanasemwa kama wachungaji na watu kama kondoo.
2 Samuel 7:8-9
Maelezo kwa Jumla
Yahwe anafafanua ahadi zake kwa Mfalme Daudi kupitia nabii Nathani.
Basi
Hii haimaanishi "sasa," lakini imetumika kuonesha utayari kwa jambo mhimu lifuatalo.
mwambie mtumishi wangu Daudi, "Hivi ndivyo asemavyo Yahwe wa majeshi: 'nilikutoa...jina kuu kwa ajili yako, kama jina la wakuu waliopo juu ya nchi.
Hii inanukuu ndani ya nukuu. Yaweza kufasiriwa: "mwambie Daudi mtumishi wangu kwamba nilimtoa... jina kuu kwa ajili yake, kama jina la mojawapo wa watu wakuu waliopo duniani"
mwambie Daudi mtumishi wangu
Yahwe bado anamwambia nabii Nathani anachopaswa kumwambia Daudi.
nimekuwa pamoja nawe
Hapa "pamoja nawe" inamaanisha kwamba Yahwe amemsaidia na kumbariki Daudi.
na nimewaondoa adui zako wote
Yahwe aliwaaribu adui wa Daudi inazungumzwa kana kwamba Yahwe aliowaondolea mbali, kama ambavyo mtu angekata vipande vya nguo au tawi kutoka katika mti.
kufanya jina kuu kwa ajili yako
Hapa "jina" inawakilisha heshima ya mtu.
kama jina la wakuu waliopo duniani
Kifungu "wakuu" inamaanisha watu mashuhuri.
2 Samuel 7:10-11
Maelezo ya Jumla
Yahwe anaendelea kueleza ahadi zake kwa Mfalme Daudi kupitia nabii Nathani.
Nitateua mahali
"Nitachagua sehemu"
nitawapanda pale
Yahwe anawafanya watu waishi katika nchi daima na kwa usalama inazungumzwa kama kama angewapanda katika nchi.
na hawatasumbuliwa tena
Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji: Yaani: "na hakuna atakayewasumbua tena"
kutoka siku
Hapa "siku" inawakilisha kipindi kirefu.
Niliwaamru waamzi
Baada ya Waisraeli kuingia katika nchi ya Kanaani na kabla ya kuwa na wafalme wa kuwatawala, Mungu aliteua viongozi walioitwa "waamzi" kuwaongoza katika nyakati za shida.
Nami nitakupa pumziko kutoka kwa adui zako wote...anakwambia kwamba atakutengenezea nyumba
Yaweza kufasiriwa: "Nami nitampa pumziko kutoka kwa adui zake wote... anamwambia kwamba atamtengenezea nyumba"
Nikupumzisha kutoka kwa adui zako wote
"Nitakupa usalama kutoka kwa adui zako wote." Hapa "pumziko" ni nomino dhahania. Yaweza kuwa: "Nitawafanya adui zako wote waache kukushambulia"
Nitakutengenezea nyumba
Maana hii hapa ya "nyumba" inarejea kwa wazao wa Daudi kuendelea kumiliki katika Israeli. Katika 7:3 Yahwe alimuuliza Daudi ikiwa angemjengea nyumba. Pale "nyumba" inawakilisha hekalu.
2 Samuel 7:12-14
Maelezo ya Jumla
Yahwe anaendelea kueleza ahadi zake kwa Mfalme Daudi kupitia nabii Nathani.
Siku zako zitakapokamilika na ukalala na baba zako
Vifungu hivi viwili vina maana sawa na vimeunganishwa kwa msisitizo. Vyote ni njia ya nyepesi ya kuonesha kifo na kufa.
Nitainua mzao baada yako
Yahwe aliteua mzao wa Daudi inaoneshwa kama Yahwe angeinua juu.
atakaye toka katika mwili wako
Usemi huu unamaanisha kwamba mtu huyo atakuwa mzao wa Daudi.
Nitauimarisha ufalme wake
Hapa "ufalme wake" inawakilisha nguvu ya kumiliki.
nyumba kwa jina langu
Hapa "jina" renarejea kwa Yahwe. Yaani: "makazi yangu ya kudumu"
Nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake daima.
Hapa "kiti cha enzi" inawakilisha nguvu ya mtu kumilki kama mfalme.
Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwanangu
Unabii katika 7:12-14 unarejea kwa Sulemani, mwana wa Daudi. Lakini, mambo ya unabii yatatimizwa na Yesu.
2 Samuel 7:15-17
Maelezo ya Jumla
Yahwe alimaliza kueleza ahadi zake kwa Mfalme Daudi kupitia nabii Nathani.
Lakini umaminifu wangu wa kiagano hautamwacha, kama nilivyomwondolea Sauli
Neno "uaminifu" ni jina dhahania linaloweza kuelezwa kama "aminifu." Lakini pia taarifa hii yaweza kufasiriwa katika muundo chanya. Yaani: "Lakini nitabaki mwaminifu kwake, tofauti na nilivyokuwa kwa Sauli"
kutoka mbele yako. Nyumba yako... mbele yako. Kiti chako cha enzi
Hapa "wewe" inarejea kwa "Daudi". "kutoka mbele ya Daudi. Nyumba ya Daudi... mbele yake. Kiti chake cha enzi"
Nyumba yako na ufalme wako utathibitishwa daima mbele yako. Kiti chako cha enzi kitasimamishwa daima.
Sentensi hizi mbili zinamaana sawa na zinasisitiza nasaba ya Daudi kutawala daima.
Nyumba yako na ufalme wako utaimalika daima mbele yako
Hapa neno "nyumba" inawakilisha uzao wa Daudi, watakao tawala kama wafalme. Hapa "ufalme" humaanisha jambo lilelile kama "nyumba." Utaona nikiimalisha familia yako na utawala wao juu ya watu wa Israeli daima"
Kiti chako cha enzi kitakuwa imara daima
Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha nguvu ya kutawala kama mfalme.
maneno haya yote
Hapa "maneno" yanawakilisha kile alichokisema Yahwe.
Alimwambia kuhusu ono lote
"Alimwambia kuhusu kila kiti Yahwe aliyomwonesha"
2 Samuel 7:18-20
Mimi ni nani, Yahwe Mungu, na familia yangu ni nini hata umenileta katika kiwango hiki?
Daudi anauliza swali hili kuonesha hisia za ndani alizozihisi baada ya kusikia tamko ya Yahwe. Swali hili lisiloitaji jibu laweza kufasiriwa: "mimi na familia yangu hatusitahili heshima hii, Yahwe Mungu."
Hili lilikuwa jamba dogo mbele yako
Hapa "mbele yako" inawakilisha alichokikusudia Yahwe kiwe.
familia ya mtumishi wako
Hapa Daudi anajirejerea kama "mtumishi wako."
Kwa kitambo kijacho
Hii inaongelea wakati kama kitu fulani kisafiricho na kuwasili mahali fulani.
Nini zaidi, Mimi Daudi naweza kukwambia?
Daudi anatumia swali hili kusisitiza kwamba hana kilichaobaki cha kumwambia Yahwe.
mtumishi wako
Hapa Daudi anajirejerea kama "mtumishi wako." Hii yaweza kuelezwa katika nafsi ya kwanza
2 Samuel 7:21-23
Kwa ajili ya neno lako
Hapa "neno" linawakilisha alikiahidi Mungu.
kutimiza kusudi lako mwenyewe
"kukamilisha ulichopanga kufanya"
kwa mtumishi wako
Daudi anajirejerea kama "mtumishi wako."
Kama tulivyosikia kwa masikio yetu
Kifungu "kwa macho yetu wenyewe" inatumika kwa msisitizo.
Kama tulivyosikia
Hapa "sisi" inamwonesha Daudi na taifa la Israeli.
Na ni taifa gani lililo kama watu wako Israeli, taifa pekee juu ya dunia ambalo wewe, Mungu, ukikwenda na kukikomboa kwa ajili yako mwenyewe?
Daudi anatumia msisitizo wa swali kwamba hakuna taifa lingine kama Israeli. Yaani: "Hakuna taifa lililo kama watu wako Israeli, taifa moja juu ya nchi ambalo wewe, Mungu, ulikwenda na kulikomboa kwa ajili yako."
Kijifanyia jina wewe mwenyewe
Hapa "jina" inawakilisha heshima ya Yahwe.
kwa nchi yako
Hapa "nchi" inawakilisha watu.
Uliyaondoa mataifa
Hapa "mataifa" inawakilisha makundi ya watu waliokuwa wakiishi Kanaani.
2 Samuel 7:24-26
Maelezo ya Jumla
Daudi aliendelea kuongea na Yahwe.
Hivyo basi
Hapa "basi" haimaanishi "sasa," lakini inatumika kuleta usikivu kwa jambo muhimu kama ifuatavyo.
Na ahadi uliyoifanya kuhusu mtumishi wako na familia yake iwe imara daima
Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. Yaani: "Na ufanye ulichoniahidi na familia yangu, na ahadi yako isibadilike"
mtumishi wako na familia yake
Daudi anajisema katika nafsi ya tatu. Yaweza kuwa: "mimi na familia yangu"
Jina lako na liwe kuu daima
Hapa "jina" inawakilisha heshima ya Yahwe.
Nyumba yangu, Daudi, mtumishi wako
Hapa "nyumba" inawakilisha familia.
Umethibitishwa mbele yako
Hii yaweza kuwa "ni salama kwa sababu wewe" au "unaendelea kwa sababu yako"
2 Samuel 7:27-29
kwa mtumishi wako kwamba utamjengea nyumba
Daudi anajirejerea kama "mtumishi wako"
kwamba utamjengea nyumba
Hapa aina hii ya usemi "nyumba" inarejea kwa uzao wa Daudi kuendelea kuwa watawala wa Israeli. Katika 7:3 Yahwe alimwambia Daudi kama angekuwa mjenzi wa nyumba ya Yahwe. Hapa "nyumba" inawakilisha hekalu.
Basi
Hii haimaanishi "sasa," lakini inatumika kutoa angalizo kwa jambo mhimu lifuatalo.
maneno yako ni ya kuaminika
Hapa "maneno" yanawakilisha anachosema Yahwe. Yaani: "Ninaamini ukisemacho"
na kwa baraka yako nyumba ya mtumishi wako itabarikiwa daima
Hii inaweza kutaarifiwa kwa muundo tendaji. Yaani: "na utaendelea kuibariki familia yangu daima.
nyumba ya mtumishi wako
Hapa Daudi anajirejerea mwenyewe kama "mtumishi wako." Yaani: "nyumba yangu" au "familia yangu"
nyumba
Hapa "nyumba" inawakilisha familia ya Daudi.
2 Samuel 8
2 Samuel 8:1
Daudi akashambulia
Hapa Daudi anawakilisha askari wake.
2 Samuel 8:2
Kisha akashinda
Hapa "yeye" inarejea kwa Daudi anayewakilisha askari wake.
akawapima watu wakekwa mstari... akapima mistari miwili ya kuuwa, na mstari mmoja kamili wa kuacha hai.
Hapa "mstari" ni "kamba." Daudi aliwafanya askari walale chini ili wapimwe na kuwekwa katika makundi matatu. Waliokuwa katika makundi mawili waliuawa, na katika la tatu, waliachwa hai.
2 Samuel 8:3-4
Kisha Daudi akamshinda Hadadezeri
Hapa wote "Daudi" na "Hadadezeri" wanawakilisha majeshi yao. "Daudi na jeshi lake walimshinda Hadadezeri na jeshi lake"
Hadadezeri... Rehobu
Haya ni majina ya wanaume.
Soba
Hili ni jina la jimbo katika Shamu.
Kuurudisha ufalme wake
"Kurudisha utawala juu ya mkoa" au "kulishika tena mkoa"
askari wa miguu ishirini elfu
"20,000 watu wa miguu"
Daudi akawakata miguu
Hili ni tenda ambapo sehemu ya nyuma ya miguu inakatwa ili farasi wasiweze kukimbia.
kutunza ya kutosha
"kutenga ya kutosha" au kutunza ya kutosha"
vibandawazi mia moja
"vibanda wazi 100"
2 Samuel 8:5-6
Daudi akaua
Hapa Daudi anawakilisha askari wake.
Washami elfu ishirini
washami 22,000
Akaweka ngome huko Shamu
"aliagiza kundi kubwa la askari wake kubaki Shamu"
2 Samuel 8:7-8
Daudi akachukua... Mfalme Daudi akachukua
Hapa Daudi anawakilisha askari wake.
Beta na Berothai
Haya ni majina ya mahali.
2 Samuel 8:9-10
Tou...Hadoramu
Haya ni majina ya wanaume.
Hamathi
Hili ni jina la mahali.
Daudi alishinda
Hapa "Daudi" inawakilisha jeshi lake.
2 Samuel 8:11-12
na Amaleki
"na Waamaleki"
Vitu vilivyotekwa
Hivi ni vitu vya thamani askari wanavyoviteka kutoka kwa walioshindwa.
Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba
Hili ni jina la mfalme wa Soba
2 Samuel 8:13-14
Jina la Daudi likajulikana sana
Hapa "jina" linarejea kwa heshima ya Daudi. Yaani "Daudi alikuwa maarufu sana"
Bonde la chumvi
Hili ni jina la mahali. Mahali pake kabisa hapafahamiki.
Watu elfu themanini.
"watu 18,000"
Akaweka ngome katika Edomu yote.
"Aliagiza makundi ya askari wake kubaki katika maeneo yote ya Edomu"
2 Samuel 8:15-18
Yoabu mwana wa Seruya
Hili ni jina la mwanaume
Ahiludi... Ahitubu... Ahimeleki... Seraya... Yehoiada
Haya ni majina ya wanaume.
Ahiludi alikuwa mwenye kuandika taarifa.
Mwandishi alikuwa mtu aliyekuwa akiongea na watu na kuwambia matangazo ya mfalme.
Wakerethi... Wapelethi
Haya ni majina ya makundi ya watu. Hawa walikuwa walinzi wa Daudi.
2 Samuel 9
2 Samuel 9:1-2
Kwa ajili ya Yonathani
"kwa sababu ya upendo wangu kwa Yonathani"
Kwa ajili ya Yonathani
Yonathani alikuwa mwana wa Sauli na rafiki wa karibu sana wa Daudi.
Siba
Hili ni jina la mwanaume.
Mimi ni mtumishi wako
Siba anajiita "mtumishi wako" kuonesha heshima kubwa kwa Daudi.
2 Samuel 9:3-4
Ninaweza kuonesha ukarimu wa Mungu
Yaweza kufasiriwa kuwa "naweza kuwa mkarimu kama niliyomwaidi Mungu"
mlemavu katika miguu yake
"Ambaye miguu yake imearibika." Neno "miguu" hapa linaonesha uwezo wa kutembea.
Makiri... Amieli
Haya ni majina ya wanaume.
Lo Debari
Hili ni jina la sehemu.
2 Samuel 9:5-6
Mfalme Daudi akatuma
Inafahamika kwamba Daudi alituma wajumbe.
Mefiboshethi
Hili ni jina la mwanaume
alikuja kwa Daudi
Neno "alikuja" laweza fasiriwa kuwa "alikwenda."
Mimi ni mtumishi wako
Mefiboshethi anajirejerea kama "mtumishi wako" kuonesha heshima kubwa kwa mfalme.
2 Samuel 9:7-8
Kwa ajili ya Yonathani baba yako
"Kwa sababu nilimpenda baba yako, Yonathani"
Utakula daima katika meza yangu.
Hapa "meza" inawakilisha kuwa pamoja na Daudi katika uwepo. Kula na mfalme mezani ilikuwa ni heshima kubwa.
Mtumishi wako ni nini, hata umwangalie kwa upndeleo mbwa mfu kama mimi?
Swali hili lisiloitaji jibu laonesha kuwa Mefiboshethi anafahamu kuwa hana umuhimu wowote wa mfalme kumjari.
mbwa mfu huyo
Hapa Mefiboshethi anawakilisha uzao wa Sauli, na anajilinganisha na "mbwa mfu." Mbwa walikuwa wanyama wasioheshimiwa, mbwa mfu alikuwa hana umuhimu kabisa.
2 Samuel 9:9-10
Ni lazima ale Daima katika meza yangu
Hapa "meza yangu" inawakilisha kuwa pamoja na Daudi.
Basi Siba... watumishi
Hapa "basi" inaonesha mkato wa habari. Msimuliaji anatoa taarifa kuhusu Siba.
wana kumi na watano na watumishi ishirini
"wana 15 na watumishi 20"
2 Samuel 9:11-13
Mtumishi wako atafanya yote ambayo bwana wangu mfalme amemwagiza mtumishi wake
Siba anajitaja kama "mtumishi wako" na kumtaja Daudi kama "bwana wangu". Mtumishi wako atafanya yote ambayo wewe bwana wangu mfalme umeagiza.
Mika
Hili ni jina la mwana wa Mefiboshethi.
wate walioishi katika nyumba ya Siba
Hapa "nyumba" inawakilisha familia ya Siba.
Anakula katika meza ya mfalme daima
Hapa "meza" inawakilisha kuwa pamoja na Daudi au katika uwepo wake.
Japokuwa alikuwa kilema katika miguu yote miwili.
Hakuweza kutembea.
2 Samuel 10
2 Samuel 10:1-3
Hanuni...Nahashi
Haya ni majina ya wanaume
Je unadhani...wewe?
Viongozi wanatumia swali kushauri kwamba mfalme asimwamini Daudi.
Kupeleleza
Kutafuta habari kuhusu mtu fulani kwa siri.
Je Daudi haja...uteka?
Viongozi wanatumia swali kushauri kwamba mfalme asimwamini Daudi.
Ili kuupindua
Hapa "huo" inarejea kwa mji ambao unawakilisha watu walioishi pale.
mji
Hapa "mji" inahusu Raba, mji mkuu wa Waamoni.
2 Samuel 10:4-5
kunyoa ndevu nusu ya zao
Inamaanisha tusi la kuwadharirisha watu.
walikuwa wameaibika sana
Hapa "kwa kina" ni usemi unaomaanisha "sana"
Kisha mrudi
Inamaanisha kwamba watapaswa kurudi Yerusalemu
2 Samuel 10:6-8
wakawa harufu mbaya kwa Daudi
Kifungu "kuwa harufu mbaya" inamaanisha kuwa chukizo
Beth Rehobu... Soba... Maaka... Tobu
Haya ni majina ya mahali.
Elfu ishirini... elfu... elfu kumi na mbili
"20,000... 1,000...12,000"
kwa langu la mji wao
Hapa "mji" inarejea kwa Raba, mji mkuu wa Waamoni
2 Samuel 10:9-10
Maelezo ya Jumla
Vita na ya Washami na Amoni inaendelea.
Na kwa sehemu ya jeshi iliyosalia, akaiweka chini ya mamlaka ya Abishai nduguye.
"Akamweka Abishai nduguye mkuu wa jeshe lililosalia"
2 Samuel 10:11-12
Maelezo ya Jumla
Yoabu analiweka tayari jeshi kwa vita.
Kwangu, kisha wewe, Abishai, lazima uniokoe
Hapa "mimi" inarejea kwa Yoabu anayewakilisha askari wake. Pia, Abishai anawakilisha jeshi lake.
2 Samuel 10:13-14
Kutoka kwa Abishai
Hapa Abishai anawakilisha askari wake.
Ndani ya mji
Hapa "Mji" unahusu Raba, makao makuu ya Waamaoni.
Na kurudi Yerusalemu
"na kurudi Yerusalemu
2 Samuel 10:15-16
Washami walipoona kwamba wameshindwa na Israeli
Hii yaweza kufasiriwa kama: "Washami walipotambua kuwa Waisraeli walikuwa wanawashinda"
Hadadezeri... Shobaki
Haya ni majina ya wanaume.
kutoka ng'ambo ya Mto Frati
Hii inamaanisha upande wa mashariki wa Mto Frati.
Walikuja kwa Helamu
Hapa "walikuja kwa" yaweza kufasiriwa kuwa "walikwenda kwa" au "walikutanika kwa"
Helamu
Hili ni jina la sehemu.
katika kichwa chao
Kifungu hiki kinaoneshwa nafasi ya mamlaka.
2 Samuel 10:17-19
Daudi alivyoambiwa hiki
Inamaanisha "Daudi aliposikia kuhusu hili"
Kusanya Isreali wote pamoja
Hapa "Israeli" inawakilisha jeshi la Israeli.
Helamu
Jina la mahali
Kinyume na Daudi na kupigana naye
Hapa Daud anawakilisha askari wake.
Daudi aliua
Hapa Daudi anawakilisha askari wake.
Mia saba... elfu arobaini
"700... 40,000"
Shobaki jemedari wa jeshi lao alijeruhiwa na kufa pale
Hii yaweza kufasiriwa: "Waisraeli walimjeruhi Shobaki jemedari wa jeshi wa Washami, na akafa pale"
Shobaki... Hadareza
Haya ni majina ya wanaume.
waliona kwamba walikuwa wameshindwa na Israeli
Yaweza kufasiriwa kuwa " walitambua kuwa Waisraeli walikuwa wamewashinda"
2 Samuel 11
2 Samuel 11:1
Ikawa wakati wa majira ya kipupwe
"Ilitokea wakati wa majira ya kipupwe." Hii inatambulisha tukio jingine katika habari.
katika wakati
"wakati wa mwaka"
Daudi akampeleka Yoabu, watumishi wake, na jeshi lote la Israeli
Daudi aliwapeleka waende vitani.
Jeshi la Amoni
"Jeshi la Waamoni"
Raba
Hili ni jina la mji.
2 Samuel 11:2-3
Hivyo ikawa
"Hivyo ikatokea" au "Hivyo ikatendeka". Mwandishi anatumia kifungu hiki kutambulisha tukio jipya katika habari.
Hivyo Daudi akatuma
Hapa neno "tuma" linamaanisha Daudi alipeleka mjumbe.
Akawauliza watu ambao wangeweza kujua kuhusu mwanamke
Daudi alikuwa anajaribu kutafuta mwanamke yule alikuwa nani. Neno "yeye" inarejea kwa Daudi, lakini inamaanisha mjumbe aliyetumwa na Daudi. Alipaswa kuuliza habari kuhusu mwanamke.
Je siye Bethsheba... naye ni mke wa Uria Mhiti.
Swali hili linatoa taarifa na laweza kuandikwa kwa maelezo. Huyu ni Bathsheba... naye ni mke wa Uria Mhiti."
2 Samuel 11:4-5
Hezi
Kipindi cha mwanamke cha mwezi
na kumchukua
"na kumchukua." Daudi alimchukua mwanamke, lakini alikuwa mjumbe aliyekuwa ametumwa aliyemchukuwa na kumleta kwa Daudi.
Akaja kwake ndani, naye akalala naye
Kifungu "alikuja kwake ndani" inaonesha hali ya Daudi kufanya tendo la ndoa na mwanamke.
Alituma na kumwambia Daudi; akasema, "Niko mjamzito"
Hapa neno "alipeleka" linamaanisha kwamba alipeleka mjumbe kumwambia Daudi kwamba alikuwa mjamzito.
2 Samuel 11:6-8
Kisha Daudi akatuma
Hapa neno "kutuma" inamaanisha kwamba Daudi alituma mjumbe.
Yoabu anaendeleaje, jeshi linaendeleaje, na vita inaendeleaje
Daudi alikuwa akiuliza ikiwa Yoabu na jeshi walikuwa wanaendelea vema na kuhusu maendeleo ya vita.
Shuka nyumbani kwako
Maana pendekezwa kwa kifungu "shuka chini" ni 1) Nyumba ya Uria ilikuwa chini kuliko kasiri la Daudi au 2) Nyumba ya Uria ilikuwa na umuhimu mdogo kulinganisha na kasiri la mfalme.
Nawa miguu yako
Kifungu hiki kinamaanisha kurudi nyumbani kupumzika wakati wa usiku baada ya kufanya kazi mchana kutwa.
Mfalme alituma zawadi kwa Uria
Daudi alituma mtu kupeleka zawadi kwa Uria.
2 Samuel 11:9-11
Bwana wake
Neno "yake" inarejerea kwa Uria na neno "bwana" inarejerea kwa Daudi.
Je haujatoka safarini? Kwa nini haukwenda nyumbani kwako?
Hili swali linaonesha ushangao wa Uria kwa nini hakumtembelea mke wake.
Israeli na Yuda
Hii inarejea kwa majeshi yao yaani "majeshi ya Israeli na Yuda"
Jinsi gani basi mimi naweza kwenda kwangu... pamoja na mke wangu?
Swali hili linasisitiza hali ya Uria kukataa kumtembelea mke wake.
Kwa hakika kama uishivyo, sitafanya hivyo.
Uria anaapa kwa ahadi yenye nguvu kwamba hatakwenda nyumbani kwa mke wake kwa vile askari wengine wapo vitani.
2 Samuel 11:12-13
alikula na kunywa mbele yake
Uria alikula na kunywa na Daudi
chini katika nyumba yake
Maana pendekezwa hapa kwa neno "chini" 1) nyumba ya Uria ilikuwa chini ya ile ya Daudi. 2) nyumba ya Uria ilikuwa na umuhimu mdogo kuliko ile ya Daudi
2 Samuel 11:14-15
akaituma kwa mkono wa Uria
Kifungu "mkono wa Uria" inamrejea Uria mwenyewe.
Mbele kabisa ya vita vikali zaidi
"mbele zaidi ya vita mahali ambapo vita ni vikali sana"
Kumwacha
"Amru askari kurudi nyuma na kumwacha"
awe amepigwa na kuuawa
"Awe amejeruhiwa na kuuawa"
2 Samuel 11:16-17
Kuhusuru mji
Neno "kuhusuru" linaweza kuelezwa kwa kitendo "kuzingira" na "kushambulia". Yaani "jeshi lake lilizunguka na kuushambulia mki"
baadi ya askari wa Daudi walianguka
Neno "anguka" ni usemi laini wa kuonesha askari waliouawa. Yaani "baadhi ya askari wa Daudi waliuawa.
Na Uria Mhiti aliuawa pale
Inamaanisha "Uria Mhiti naye alikuwa miongoni mwao.
2 Samuel 11:18-20
Yoabu alituma neno kwa Daudi
"Kutuma neno" kunamaanisha kuwa alituma mjumbe kutoa taarifa kwa Daudi
Kwa nini mlikaribia hivyo... kutoka katika ukuta?
Yoabu anasema kwamba Daudi anaweza kumkemea kwa kuuliza swali hili. Yaweza kuwa "Hamkupaswa kuwa mmeukaribia mji hivyo ili kupigana nao. Kwani wangeweza kurusha mishale kutokea ukutani"
Piga kutoka ukutani
Inaonesha watu wa mji wakirusha mishale kwa adui wao kutokea ukutani.
2 Samuel 11:21
Ni nani aliyemwua Abimeleki mwana wa Yerubeshethi?
Yoabu anasema Daudi anaweza kumkemea kwa kuuliza swali hili. Yafaa kuwa "Kumbuka jinsi Abimeleki mwana wa Yerubeshethi alivyouawa!"
Abimeleki mwana wa Yerubeshethi
Hili ni jina la mwanaume. Babaye anajulikana pia kwa jina la Gideoni.
Je mwanamke hakurusha jiwe la juu la kusagia juu yake kutoka ukutani hivyo kwamba alikufa katika Thebezi?
Yoabu anasema Daudi aweza kumkemea kwa kuuliza swali. Yafaa kuwa "Kumbuka alikufa huko Thebezi mwanamke aliporusha jiwe la juu la kusagia juu yake kutokea ukutani"
kutokea ukutani
"kutokea juu ya ukuta wa mji"
Jiwe la kusagia nafaka
Jiwe zito ambalo lingeweza kuzunguka, lililotumika kwa kusaga nafaka ili kutengeneza mkate
Thebezi
Hili ni jina la mji.
Kwa nini mliukaribia ukuta kiasi hicho?
"Hamkupaswa kuwa mmeukaribia ukuta kiasi hicho!"
2 Samuel 11:22-23
lango
"lango la mji"
2 Samuel 11:24-25
Warusha mishale wao warusha
"Walirusha mishale"
Baadhi ya watumishi wa mfalme waliuawa
"Waliwauwa baadhi ya watumishi wa mfalme"
Mtumishi wako Uria Mhiti ameuawa
"Walimwua mtumishi wako Uria pia"
Watumishi wa mfalme
Hapa "watumishi" inarejerea askari, siyo watumwa, kwa sababu askari walikuwa watumishi wa mfalme.
Maana upanga hula huyu kama ulavyo mwingine.
Hapa "upanga" inarejerea kwa mtu anayemwua mwingine kwa upanga. Kumwua mtu kwa upanga unazungumzwa kama vile ni "kula" watu.
Ongezeni mashambulizi
"Piganeni kwa nguvu zaidi"
2 Samuel 11:26-27
Aliomboleza kwa kina
Hapa mwandishi anazungumza maombolezo yake kama yalikuwa ndani yake zaidi.
Huzuni
Hisia kali ya huzuni iliyosababisha maumivu, kukata tamaa au matatizo
Daudi alituma na kumchukua nyumbani
Hapa neno "tuma" linamaanisha alituma mjumbe kumchukua na kumleta kwake.
Kutopendezwa
"aliyehuzunishwa" au "kasirishwa"
2 Samuel 12
2 Samuel 12:1-3
kondoo jike
kondoo jike
alikuwa kama binti kwake
Hii inaonesha ukaribu wa mtu huyu na kondoo wake mdogo.
2 Samuel 12:4-6
Mtamba wa kondoo
Kondoo jike
Hasira ya Daudi ikawaka kinyume cha
Hapa mwandishi anaeleza jinsi Daudi alikuwa na hasira sana kama vile mwili wake ulikuwa umechemka kwa sababu ya hasira.
Mgeni wake
Ilikuwa ni kwa ajili ya chakula cha mgeni wake
Akamwambia Nathani kwa hasira
Hii inamaanisha kwamba Daudi aliongea na Nathani kwa hasira.
Kama Yahwe aishivyo
Hii inaeleza kwamba Daudi alikuwa akiapa kiapo au ahadi ya kuaminika.
Kumwua
Hii inamaanisha kumwua. Yaani kufa
Anapaswa kulipa kondoo mara nne
Kiasi tajiri alichopaswa kulipa kilikuwa mara nne ya thamani ya kondoo.
Huruma
Kujisikia huzuni na upendo kwa anayeumia au kutopendwa
2 Samuel 12:7-8
Kutoka mkononi mwa Sauli
Hapa neno "mkono" linaonesha utawala. Yaani "kutoka katika utawala wa Sauli"
wake za bwana wako katika mikono yako
Hapa Yahwe anaeleza Daudi akiwa na wake za bwana wake kama wake wake mwenyewe, kwa kusema kwamba wako "mikononi mwako."
Pia nilikupa nyumba ya Israeli na Yuda
Hapa Yahwe anaongelea jinsi alivyompa Daudi mamlaka yake kama mfalme juu ya Israeli na Yuda kama vile alimpa nyumba ya Israeli na Yuda. Kifungu "nyumba ya" kinamaanisha "watu wa."
Ikiwa hayo yangekuwa machache kwako
"Ikiwa nisingekupa vya kutosha"
2 Samuel 12:9-10
Hivyo kwa nini umedharau... Yahwe, hata kufanya maovu mbele zake?
Swali hili linatumika kumkemea Daudi. Yaani "haukupaswa kumdharau ... Yahwe na kufanya yaliyomaovu mbele zake!"
Hata kufanya yaliyomaovu mbele zake
"Mbele" ya Yahwe inarejea kwa kile anachofikiri. Hii inazungumzia anachohesabu kuwa uovu halisi.
Umemwua Uria Mhiti kwa upanga
Daudi hakumwua Uria kwa mkono wake, bali alipanga Uria alivyouawa. Kifungu "kwa upanga" kinaonesha jinsi alivyokufa vitani.
Ulimwua kwa upanga wa jeshi la Amoni
Inaonesha kwamba Daudi hakumwua kwa mkono wake bali alipanga jinsi ya kuuawa kwa Uria mkononi mwa Waamoni.
Upanga hautaondoka nyumbani mwako
Hapa neno "upanga" linaonesha watu wanaokufa vitani. "Nyumba" ya Daudi inarejerea wazawa wake.
2 Samuel 12:11-13
Katika nyumba yako mwenyewe
Hapa "nyumba" ya Daudi inarejerea kwa familia yake.
Mbele za macho yako
Hapa Daudi anarejerewa kwa kutajwa macho yake kusisitiza ambacho angeona.
mbele ya Israeli yote
Hapa inaonesha watu wote wa Israeli kujua juu ya kilichotendeka kwa wake zake kama vile wote walishuhudia tukio.
Wakati wa mchana
Wazo la kufanya jambo "hadharani" au katika njia ambayo watu wanafahamu kinachotendeka kama kinafanyika mchana.
Kutenda dhambi yako
"alitenda dhambi"
Kupita
Yahwe amesamehe dhambi ya Daudi. Hii inazungumzwa kama Yahwe anaipitisha dhambi kama kilikuwa kitu alichokipita na kutokukijari.
Hautakufa
Hatakufa kwa sababu ya kutenda dhambi hii na mwanamke.
2 Samuel 12:14-15
Kudharau
Kutokupenda au kumchukia mtu au kitu
Yahwe alimpiga mtoto... na akawa mgonjwa sana.
Yahwe anaonekana kusababisha ugonjwa wa mtoto kama vili amempiga.
mtoto aliyezaliwa kwako
Kifungu "kuzaliwa kwako" inamaanisha kwamba huyu ni mtoto wa Daudi
Mtoto ambaye mke wa Uria alimzalia Daudi
Hii inamaana kwamba alizaa mtoto ambaye Daudi ndo alikuwa baba yake.
2 Samuel 12:16-18
Kusihi
Kuombeleza au kuomba kwa hamu kubwa
kwenda ndani
Daudi alikwenda ndani ya chumba chake alipokuwa peke yake.
Kumwinua kutoka sakafuni
" na kumsihi kuinuka kutoka chini"
Ikawa
"Ilitokea"
Hakuisikiliza sauti yetu
Hapa "sauti" inasisitiza kwamba walikuwa wakiongea.
Siku ya saba
Hii ni siku ya saba tangu mtoto azaliwe
Tazama
Usemi unatumika kuwafanya watu wawe "makini"
Je atajitendeaje ikiwa tutamwambia kwmba mtoto amekufa?!
Watumishi wanauliza swali hili kuonesha hofu yao. Yaani "tunaogopa kwamba anaweza kujidhuru ikiwa tutamwambia kwamba mtoto amekufa!"
2 Samuel 12:19-20
Kunong'oneza
"kuongea polepole sana"
Kutambua
"Kuelewa"
Inuka
"simama juu"
2 Samuel 12:21-23
Maelezo ya Jumla
Mistari hii ina maswali yasiyoitaji majibu msisitizo ambao Daudi anatambua kwamba Yahwe ameruhusu hili kutendeka.
Nani ajuaye kuwa Yahwe atanirehemu, ili mtoto aishi?
Daudi anauliza swali hili kusisitiza kwamba hakuna ajuaye kama Yahwe angemwacha mtoto aishi. Hii inaweza kuandikwa kama taarifa. Hakuna ajuaye kwamba Yahwe atanirehemu ili mtoto aishi.
Lakini sasa amekufa, hivyo kwa nini nifunge?
Daudi anatumia swali hili kutoa msisitizo kwamba hana haja ya kufunga tena.
Je naweza kumrudisha tena?
Daudi anatumia swali hili kutoa msisitizo kwamba mtoto hawezi kurudi kuwa hai.
Nitakwenda kwake
Daudi anaonesha kwamba atakapokufa atakwenda kwa mtoto.
2 Samuel 12:24-25
Akaingia kwake, na kulala naye
Kifungu "kuingia kwake" ni tamathali ya kuonesha kwamba Daudi alifanya tendo la ndoa na mkewe. Vifungu hivi viwili vinamaana moja na vinatumika kusisitiza kwamba walilala pamoja.
Alituma neno kupitia nabii Nathani
Hapa "neno" inarejerea kwa Yahwe aliyemwambia Nathani kumwambia Daudi.
Yedidia
Hili ni jina lingine la Sulemani mwana wa Daudi, Yahwe alilolichagua kwa ajili yake.
2 Samuel 12:26-28
Yoabu akapigana... akaukamata
Hapa mwandishi anasema "Yoabu" lakini anarejerea kwa Yoabu na askari waliopigana pamoja naye.
Raba
Kupigana dhidi ya mji hu, halisia inamaanisha kupigana dhidi ya watu wa Raba.
Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema
"Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi kumwambia"
Wamechukua sehemu ya kusambaza maji mjini
"Kukamata" eneo inamaanisha kuchukua umilki.
Kupiga kambi kinyume
Hii inamaanisha kuzunguka na kushambulia.
Nimepigana... nimekamata... ikiwa nitachukua
Hapa Yoabu anajisemea mwenyewe wakati halisia anarejerea kwake na askari wake.
Uchukue... chukua mji
"Kuchukua" eneo inamaanisha kuchukua umilki.
Utaitwa
Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. Yaani "watu watauita"
2 Samuel 12:29-30
Alipigana
Hapa mwandishi anazungumzia Daudi wakati kwa uhalisia anarejerea kwa Daudi na askari wake.
Talanta
Kwa vipimo vya sasa ni sawa na "kilo 34"
Jiwe la thamani
Jiwe la nadra kupatikana kama vile almasi, rubi, na mengine
Taji iliwekwa katika kichwa cha Daudi mwenyewe
Waliweka taji katika kichwa cha Daudi.
Akaondoa
Hapa mwandishi anazungumzia Daudi wakati ki halisia anarejerea kwa askari wa Daudi.
Mateka
Vitu vya thamani vinavyochukuliwa kutoka kwa adui aliyeshindwa.
Kwa wingi
"kiwango" au "idadi"
2 Samuel 12:31
Akawaleta watu nje
Daudi hakuwaleta nje watu mwenyewe; aliwaagiza askari wake kuwaleta nje.
misumeno, sululu, na shoka
Hivi ni vifaa vya kukata miti au kuvuja ardhi.
Sehemu ya kutengenezea matofali
Sehemu ambapo matofali yanakausha na kufanywa magumu
Miji yote ya watu wa Amoni
Hii inarejerea kwa watu katika mji.
2 Samuel 13
2 Samuel 13:1-2
Ikawa baada ya haya
"Ilitukia baada ya haya." Kifungu hiki inatambulisha tukio jipya katika habari.
Dada wa kambo
Amnoni na Tamari walikuwa watoto wa baba mmoja lakini mama tofauti
Dada
Absalomu na Tamari walikuwa watoto wa baba na mama mmoja.
Amnoni alichanganyikiwa kiasi cha kuwa mgojwa kwa kwa sababu ya Tamari dada yake
Hii ni kwa sababu Amnoni alimtamani ili alale nae.
2 Samuel 13:3-4
Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi
Haya ni majina ya wanaume. Shama alikuwa kaka wa Daudi.
Mwelevu
mwenye akili au mdanganyifu
Kuwa na mawazo
Ni hali ya kihisia au huzuni ya hali ya juu
Je hautaniambia?
Swali hili ni ombi la Yehonadabu ili aambiwe kwa nini Amnoni ana hali hiyo.
2 Samuel 13:5-6
Yehonadabu
Hili ni jina la mwanaume
Kujifanya kuugua
Kuwa na mwonekano wa kuwa mgonjwa
na kula kutoka mkononi mwake... niweze kula mkononi mwake
Hili ni ombi lake ili ahudumiwe chakula peke yake.
kwa ugonjwa wangu mbele yangu
Chakula si kwa ajili ya ugonjwa wake, bali ni kwa ajili yake kwa sababu ni mgonjwa. Kifungu "mbele yangu" ni ombi kwa kuandaa chakula mbele yake.
2 Samuel 13:7-9
Daudi akatuma neno
Hii inamaanisha kwamba alituma mjumbe kuongea na Tamari
Donge
Mchanganyiko wa unga na maji unaotumika kwa kuokea.
Kuukanda
Kutumia mikono kulichanganya donge
mbele yake
Hii inamaanisha kwamba Tamari alitengeneza mkate mbele ya Amnoni.
Hivyo kila mtu akatoka
"Kutoka nje kwa mtu" inamaanisha kuwaacha.
2 Samuel 13:10-12
Ili nile mkononi mwako
Hili ni ombi kwa Tamari kumhudumia chakula binafsi
Usinilazimishe
Hii inamaanisha kwamba "usinilazimishe kulala nawe"
Jambo lisilofaa
La kuaibisha sana
2 Samuel 13:13-14
Maelezo ya Jumla
Tamari anaendelea kuongea na Amnoni
Ningeenda wapi kujiepusha na aibu ambayo ingewekwa juu yangu maishani?
Tamari anauliza swali hili kusisitiza kiasi gani angeona aibu kama atalala naye.
Kujiepusha na aibu hii.
Tamari anazungumzia kuondoa aibu yake kama vile ingekuwa adui au mtesaji aliyetaka kumkwepa.
2 Samuel 13:15-17
Maana uovu huu wa kunifanya niondoke ni mkuu zaidi
Jina la dhahania "uovu huu mkuu" linaweza kuoneshwa kwa kitenzi.
Funga mlango nyumba yake
Hii inamaanisha kufunga mlango ili asiingie tena.
2 Samuel 13:18-19
Akafunga mlango nyuma yake
Hii inamaanisha kufunga mlango ili kwamba asiweze kuingia tena.
akaweka majivu kichwani pake na kuchana vazi lake. Akaweka mikono yake kichwani pake
Haya ni matendo ya kuomboleza au kuhuzunika katika utamaduni wa Kiisraeli. Hii ilionesha kwamba alikuwa na huzuni sana.
2 Samuel 13:20-22
Je amekuwa nawe Amnoni nduguyo?
Hii ni njia laini ya kuuliza je Amnoni amekuwa na uhusiano wa tendo la ndoa nawe.
Nyamaza
Hii inamaanisha kutomwambia mtu juu ya jambo fulani.
Usiliweke jambo hili moyoni
Kifungu "kuweka jambo moyoni" inamaanisha "kuhofu juu yake."
Hivyo Tamari akabaki peke yake
Hii inamaanisha kwamba hakuolewa.
hakusema lolote
"alinyamaza"
2 Samuel 13:23-24
Ikawa baada ya miaka miwili mizima
Hii inamaanisha kuwa miaka miwili imepita na inatambulisha tukio linalofuata katika habari. Kifungu "mikaa kamili" inamaanisha miaka miwili kamili.
Wakata manyoya
Hawa ni watu wanaokata manyoya ya kondoo
Baal Hazori
Hili ni jina la mahali.
Basi tazama
Hiki ni kifungu inachotumika kuonesha umakini kwa ajili ya kile kinachofuata.
mtumishi wako
Absalomu anajiita "mtumishi wako" kuonesha heshima.
Anawakatao kondoo manyoya
Ilikuwa desturi kwa watu katika Israeli kufanya sherehe baada ya kukata kondoo wao manyoya.
mfalme aweza
Japokuwa na aongea na mfalme baba yake, anamwita "mfalme" badala ya "wewe" kuonesha heshima yake.
2 Samuel 13:25-26
Tafadhari mwache ndugu yangu Amnoni aende nasi
Mwana mkuu alimwakilisha baba yake katika utamaduni wa Kiisraeli. Amnoni alikuwa mwana mkuu wa Daudi.
Kwa nini Amnoni aende nanyi?
Daudi alifahamu kwamba Absalomu na Amnoni hawakuwa marafiki.
2 Samuel 13:27-29
Absalomu alimsihi Daudi
Hapa mwandishi anamzungumzia Absalomu akimsihi Daudi kumwacha Amnoni kuja kama vile kuweka msukumu wa kimwili juu yake.
Msiogope
Hii inamaanishi hawaitaji kuogopa matokeo ya kumwua Amnoni.
Je siyo mimi niliyewaagiza?
Absalomu anauliza swali hili kusistiza kwamba atalaumiwa yeye kwa kuagiza wafanye hivyo.
si kuwaagiza
Kile alichokiagiza Absalomu kinaweza kuelezwa kwa swali kama je sikuwaagiza kumwua?
wana wote wa mfalme
Hii haiwahusishi Absalomu na Amnoni aliyekufa. Inawahusu wana wa mfalme aliowaruhusu kwenda kwenye sherehe.
kila mtu
Hii inahusisha wana wa mfalme walioondoka shereheni.
2 Samuel 13:30-31
Hivyo ikawa
"Ikatukia." Kifungu hiki kimetumika kutambulisha tukio linalofuata katika habari.
Njiani
"kusafiri njiani"
Habari ikamfikia Daudi kusema
Hapa inasema kwamba habari ilikuja,mtu alikuja na kumwambia Daudi ile habari.
Ndipo mfalme alipoinuka
"Kisha mfalme akainuka"
akachana nguo zake, na kulala juu ya sakafu
Alifanya hivi kuonesha kwamba alikuwa na huzuni sana.
pamoja na nguo zao zimechanwa
Walifanya hivi kuonesha huzuni yao na kuomboleza pamoja na mfalme.
2 Samuel 13:32-33
Yehonadabu... Shama
Huyu ni mwana wa nduguye Daudi
Bwana wau asiamini
"Bwana wangu, usiamini"
bwana wangu
Yehonadabu anamwita Daudi "bwana wangu" kuonesha heshima.
Amnoni alimwaribu dada yake
Hii ni njia rahisi ya kusema Amnoni alimbaka dada yake.
bwana wangu mfalme asi
"bwana wangu mfalme, usi"
kuweka taarifa hii moyoni
Kifungu "kuweka jambo moyoni" inamaanisha "kuhofu juu ya jambo fulani."
2 Samuel 13:34-36
Kuangalia
Hii inamaanisha mtumishi alikuwa akiangalia kwa mbali wakati akilinda katika ukuta wa mji.
Kuinua macho yake
Hapa mtumishi anaangalia juu ya kitu kinachozungumziwa kama aliinua macho yake.
Hivyo ikawa
Kifungu hiki inatambulisha jambo linalofuata katika habari.
Wakainua sauti zao
Hapa wana kulia kwa sauti kunasemwa kama vile sauti zao zilikuwa kitu kilichoinuliwa angani.
2 Samuel 13:37-39
Talmai... Amihudi
Haya ni majina ya wanaume.
kwa ajili ya mwanawe
"mwanawe Amnoni"
Alipokuwa kwa miaka mitatu
"Alipokaa kwa muda wa miaka mitatu"
Akili wa Mfalme Daudi ulitamani
Hapa Daudi anarejerewa kwa moyo wake kusisitiza mawazo yake.
Maana alikuwa amefarijika kuhusu Amnoni na kifo chake.
"Hii ni kwa sababu hakuwa na huzuni tena juu ya Amnoni kufa.
2 Samuel 14
2 Samuel 14:1-3
Basi
Neno hili linatumika hapa kuonesha kikomo katika habari kuu. Hapa mwandishi anazungumzia mtu mwingine katika habari.
Seruya
Hili ni jina la mwanamme
Kufahamu
Hii inamaana kuwa Yoabu alitambua alichokuwa anafikiri Daudi.
akapeleka neno Tekoa na kutaka mwanamke mwerevu aletwe.
Hii inamaanisha kuwa alituma mtu akiwa na ujumbe huko Tekoa na kumletea mwanamke.
Tekoa
Hili ni jina la eneo
Uwe kama mwanamke aliyeomboleza
Yoabu anatoa mlinganisho, akieleza kwa mwanamke jinsi alivyomtaka aonekane.
aliyekufa
Hii inarejea kwa mtu aliyekufa, siyo wafu wote kwa jumla.
2 Samuel 14:4-6
akainamisha uso wake juu ya ardhi
Alifanya hivyo kuonesha heshima yake na utii kwa mfalme.
mmoja alimpiga mwingine
"mmoja wa wanangu alimpiga mwenzake kwa kitu.
2 Samuel 14:7
ukoo wote
"familia yangu yote"
Mtumishi wako
Mwanamke anatumia jina hili kuonesha heshima yake kwa mfalme
Kumwua
Hii inamaanisha kuua
Wangemwaribu na mrithi pia
Ikiwa wangemwua na ndugu mkosaji kusingekuwa na mwana aliyesalia kurithi mali ya familia.
Hivyo wangelizima hata kaa liwakalo lililosalia
Hapa mwanamke anarejerea kwa mwana pekee aliyesalia kama kaa liwakalo. Anazungumzia mtu kumwua mwanawe kama kulizima kaa liwakalo.
Hawatamwachia mme wangu siyo jina wala mzao
Hii inaweza kuelezwa katika muundo chanya.
Siyo jina wala mzao
Hii inahusu mwna kubeba jina la familia kwa kizazi kijacho.
juu ya uso wa nchi
"juu ya nchi." Kifungu hiki kinasisitiza familia isingeendelea kuwepo baada ya mme kufariki. "juu ya nchi" inamaanisha juu ya ardhi ambapo watu wanatembea.
2 Samuel 14:8-9
Nitaagiza jambo utakalofanyiwa
Inamaanisha nitalishugulikia jambo hili
Tekoa
Ni jina la sehemu
Hatia iwe juu yangu na juu ya familia ya babangu
Hii inamaanisha kwamba ikiwa watu watasema kwamba mfalme amekosea kusaidia familia ya mwanamke yeye hatakuwa na hatia.
mfalme na kiti chake cha enzi
Hapa neno "kiti cha enzi" linarejerea yeyote angekuja kuwa mfalme mahala pa Daudi.
Hawana hatia
"Ni msafi." Hapa mwanamke anaongelea mfalme kuwa safi kwa kuisaidia familia yake ikiwa angekuwa ameisaidia tayari.
2 Samuel 14:10-11
Kusema chochote kwako
Hapa vitisho vya maneno vinazungumzwa kwa ujumla.
Hatakugusa tena
Hapa Daudi anazungumzia mtu kutomgusa au kumtisha, kwa kusema kwamba mtu hata kugusa. Inaonesha kwamba Daudi hataruhusu mtu kumtisha ili kumsumbua.
kwamba wasimwaribu mwanangu
"Kwamba hawatamwua mwanangu" au "kwamba hawatamnyonga mwanangu"
Tafadhari, mfalme na amkumbuke Yahwe Mungu wake
Maana kisiwa 1) Kifungu "kukumbuka" ni usemi unaomaanisha kuomba. Yaani "Tafadhari mwombe Yahwe Mungu wako au 2) Hapa "kumbuka" inamaanisha kukumbuka na inaonesha kwamba baada ya kumkumbuka Yahwe atatoa ahadi kwa jina lake.
Mlipa kisasi cha damu
Hii inarejerea kwa mtu anayetaka kulipiza kisasi cha kifo cha ndugu yake.
Kumwangamiza mwingine zaidi
"kusababisha mwingine zaidi afe." Hii ni nyongeza kwa mwingine aliyeuawa.
Hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utakaoanguka chini.
Hii inamaana kwamba mwanawe hatapata madhara, ambayo inatia chumvi kwamba hatapoteza hata unywele mmoja.
Kama Yahwe aishivyo
Mara kwa mara watu waliahidi na kulinganisha kwa uhakika jinsi ambavyo wangeakikisha ahadi zao kwa jinsi Yahwe anavyoishi.
2 Samuel 14:12-14
sema neno zaidi
"kusema nawe neno zaidi." Mwanamke anaomba kusema na mfalme jambo lingine.
Mtumishi wako
Kuonesha heshima kwa mfalme
Kuongea zaidi
Mfalme alimpa ruhusu kuongea zaidi.
Kwa nini basi umetenda jambo la namna hiyo kwa watu wa Mungu?
Mwanamke anauliza swali hili kumkemea Daudi kwa jinsi alivyomtendea Absalomu.
Mfalme ni kama mwenye hatia
Mwanamke anamlinganisha mfalme na mtu mwingine aliye na hatia bila kusema moja kwa moja.
Mwanawe aliyefukuzwa
Hii inaweza kuelezwa kama "mwanawe aliyetengwa.
Maana wote ni lazima tufe, nasi ni kama maji tukimwagika juu ya ardhi... juu tena.
Hapa mwanamke anazungumzia mtu anayekufa kama maji yamwagikayo juu ya nchi.
Mungu... hutafuta njia kwa wale waliofukuzwa kurudishwa tena.
Mwanamke anaonesha kwamba Daudi anapaswa kumrudisha mwanawe.
2 Samuel 14:15-17
kwa sababu watu wamenitisha.
Maneno yanayokosekana yanaweza kuongezwa katika kifungu hiki. Yaani "kwa sababu watu wameniogopesha hata nimekuja"
Mtumishi wako
Hii ni kuonesha heshima kwa mfalme hivyo anajiita "mtumishi wako"
Kumtoa mtumishi wake
Hapa kifungu "kumtoa" inamaanisha kumkabizi katika mikono ya mtu mwingine.
Kutoka katika mkono wa mtu
Hapa "mkono" unarejerea katika mamlka ya mtu.
Kutoka katika urithi wa Mungu
Hii inamaanisha kwamba wasingekuwa na mzao yeyote wa kuishi katika nchi ambayo ingelithiwa na wazao wao.
Neno la bwana wangu mfalme
Kirai jina "neno" kinaweza kuelezwa na kitenzi "husema"
Maana kama malaika wa Mungu, ndivyo alivyo bwana wangu... kutoka uovu
Hapa Daudi, mfalme, analinganishwa na "malaika wa Mungu." Hii ni kwa sababu wote wanajua jinsi ya kutofautisha mema kutoka mabaya.
2 Samuel 14:18-20
Tafadhari usinifiche neno lolote nikuulizalo
Muundo wa kinyume umetumika hapa ili kusisitiza na unaweza kuelelezwa kwa muundo chanya. Yaani "tafadhari niambie ukweli kuhusu lolote ninalokuuliza"
Je si mkono wa Yoabu uliopamoja nawe katika hili
Hapa neno "mkono" linaonesha ushawishi wa Yoabu.
Kama uishivyo
"Hakika kama uishivyo." Hapa mwanamke analinganisha uhakika wa alichokisema Daudi amesema kwa hakika kwamba anaishi, ili kusisitiza jinsi taarifa ilivyo ya kweli
Hakuna awezaye kuelekea mkono wa kulia... mfalme alivyosema
Hapa mwanamke anaeleza ugumu wa kuongea na mfalme na kumficha asigundue ukweli kwa kulinganisha na mtu asivyoweza kuelekea upande wowote.
Mkono wa kulia au wa kushoto
Taarifa inatoa milengo miwili na inamaanisha "popote."
Bwana wangu ni mwelevu
Bwana wangu mfalme ni mwenye hekima"
Ni mwenye hekima, kama hekima ya malaika wa Mungu
Mwanamke analinganisha hekima ya Daudi na ya malaika kusisitiza jinsi alivyo mwenye hekima.
2 Samuel 14:21-22
Hivyo mfalme akamwambia Yoabu
Hii inamaana kwamba mfalme alitaka Yoabu aletwe mbele yake ili kwamba aongee naye.
Basi tazama
Kifungu kimetumika kuonesha usikivu wa mtu kwa kusikiliza kwa makini kinachosemwa baada ya hapo.
Jambo hili
Hii inarejea kwa anachotaka Yoabu mfalme akifanye.
Yoabu akainamisha uso wake chini
Yoabu alifanya hivi kwa kumweshimu mfalme na kuonesha shukurani yake.
mtumishi wako
Hii ni kuonesha heshima kwa mfalme
Nimepata kibari mbele zako
Kifungu "kuona kibari" kinamaanisha kuthibitishwa na mtu fulani. Kifungu "mbele yako" kinarejea kwa anachokifikiri mfalme.
Katika hilo mfalme
"kwa sababu mfalme"
Mfalme ametimiza haja
"Umefanya nilichokuomba kufanya"
2 Samuel 14:23-24
lakini hataweza kuuona uso wangu... uso wa mfalme
Hapa neno "uso" linamrejerea mfalme.
2 Samuel 14:25-27
Basi
"Basi" inaonesha badiliko katika habari kuu. Hapa Samweli anatoa sehemu nyingine ya habari.
Hakukuwa na mtu katika Israeli aliyesifiwa kwa uzuri kama Absalomu
Watu walimsifu Absalomu kwa uzuri wake wa sura kuliko walivyomsifu mwingine yeyote.
Kutoka katika wayo wa mguu wake hadi katika utosi wake hakuwa na waa lolote
Hii inamaanisha kwamba hakuwa na kasoro.
shekeli mia mbili
Katika vipimo vya sasa ni sawa na "kilo mbili na nusu"
Kwa kiwango cha kipimo cha mfalme
Mfalme alikuwa na kipimo kilichoamua kiwango cha uzito wa shekeli, uzito mwingine na vipimo vingine.
Walizaliwa kwa Absalomu wana watatu na binti mmoja
Inamaanisha Absalomu alikuwa na watoto watatu wa kiume na binti mmoja.
2 Samuel 14:28-29
Uso wa mfalme
Hii inamaansisha mfalme.
Absalomu akatuma neno kwa Yoabu
Hii inamaanisha kwamba alittuma mjumbe kwa Yoabu akiwa na ombi.
Kumpeleka kwa mfalme
Inaoneshwa kwamba Absalomu alimtaka Yoabu kuja kwake ili amwone na kuingilia kati ili aweze kumwona mfalme.
Hivyo Absalomu akatuma neno mara ya pili
Hii inamaanisha kwamba alituma tena mjumbe kwa Yoabu akiwa na ombi lilelile.
2 Samuel 14:30-31
Tazama
Hapa neno hili linatumima kama usemi kuwakumbusha watu juu ya jambo fulani.
2 Samuel 14:32-33
Tazama
Neno hili limetumika hapa kama usemi kusisitiza, na kuthibitisha kinachosemwa baada ya hapa.
Nilituma neno
Hii inamaana alituma mjumbe.
Kwa mfalme kusema
Ujumbe kwa mfalme hapa umeandikwa kama Absalomu ndiye alikuwa mzungumzaji. Absalomu alikuwa akimwomba Yoabu kusema ujumbe kwa niaba yake.
Uso wa mfalme
Hii inamrejerea mfalme.
Aliinama chini mbele ya mfalme hadi kwenye ardhi
Absalomu anaonesha heshima kwa mfalme.
Mfalme akambusu Absalomu
Hii inamaanisha kwamba mfalme alisamehe na kumrudisha Absalomu.
2 Samuel 15
2 Samuel 15:1-2
Ikawa
Kifungu hiki kinatambulisha tukio jingine katika habari
Na watu hamsini kwenda mbele yake
Watu hawa wangekwenda mbele ya kibandawazi kwa kumweshimu Absalomu.
Mtumishi wako
Mtu alipomjibu Absalomu alimrejerea kwa kusema "mtumishi wako" kuonesha heshima yake kwa Absalomu.
2 Samuel 15:3-4
Hivyo Absalomu angemwambia
Inaonesha kwamba mtu alimwambia Absalomu shitaka lake. Yaani Absalomu angemwuliza tatizo lake lilikuwa ni nini, ndipo mtu alipomweleza Absalomu kwa nini alitafuta haki.
Vema na haki
Maneno yana maana moja na yanatumika pamoja kusisitiza kwamba shitaka lake lilikuwa jema.
kusikiliza kesi yako
"Kusikiliza" shitaka inamaanisha kuisikiliza na kufanya maamuzi.
2 Samuel 15:5-6
yeye hunyosha mkono na kumshika na kumbusu
Hili ni tendo la salamu ya kiurafiki.
kwa hukumu
Hii inamaanisha kwamba walimjia mfalme ili kuamua migogoro yao
Hivyo Absalomu akaiba mioyo ya watu wa Israeli
Hii inamaanisha kwamba Absalomu aliwashawishi watu kumtii yeya zaidi ya Daudi. Hapa mwandishi anaongelea jinsi watu walivyomtii Absalomu kwa kusema aliiba mioyo ya watu.
2 Samuel 15:7-8
Ikawa
Kifungu hiki kinatumika kutambulisha tukio linalofuata katika habari.
hata mwisho wa miaka minne Absalomu
Hii inarejerea miaka minne baada ya kurudi Yerusalemu.
na kutimiza nadhiri niliyoiweka kwa Yahwe nilipokuwepo Hebroni
"kwenda Hebroni na pale nitatimiza nadhiri niliyomfanyia Yahwe"
Kwa miaka minne
Hapa Absalomu anajirejerea katika namna ya kumweshimu mfalme.
2 Samuel 15:9-10
Hivyo Absalomu akainuka
"Hivyo Absalomu anaondoka"
Katika makabila yote ya Israeli
Hapa sehemu walipoishi makabila ya Israeli zinatajwa kama makabila yenyewe.
Sauti ya tarumbeta
"tarumbeta ikipigwa"
2 Samuel 15:11-12
Waliokuwa wamearikwa
Inamaanisha "watu waliokuwa wamepewa taarifa"
Wakaenda katika ujinga wao
Hawakuwa wanatambua kwa undani kilichokuwa kinakwenda kutendeka
Akamwita Ahithofeli
Hii inamaanisha kwamba alituma wajumbe kumwita Ahithofeli na kumleta kwake.
Ahithofeli
Hili ni jina la mwanamme.
Gilo
Hili ni jina la sehemu.
2 Samuel 15:13-15
Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana
Hapa watu wanarejerewa kwa "mioyo" kusisitiza utiifu wao kwa Absalomu.
kujiepusha na Absalomu... kwa haraka... na ataleta
Hapa Daudi anaongelea Absalomu na watu aliokuwa nao kama "Absalomu" yeye mwenyewe kwa sababu watu walikuwa wanafuata mamlaka ya Absalomu.
kuushambulia mji kwa ukali wa upanga
"Mji" unatajwa kuonesha watu wa mji. "Ncha ya upanga" inarejerea kwa panga za waisraeli kusisitiza kwamba waliwaua watu vitani.
kusababisha madhara
Hii inamaanisha kusababisha madhara kutokea.
2 Samuel 15:16-18
kulitunza kasiri
Hapa neno "kutunza" linamaanisha kutunza.
katika nyumba ya mwisho
Hii inarejerea nyumba ya mwisho ambayo wangefikia wakati wanaondoka mjini.
Wakerethi... Wapelethi
Hawa walikuwa watumishi wa Daudi
Wagiti
Hili ni kundi la watu waliokuwa katika nchi ya Palesitina
Watu mia sita
"watu 600"
2 Samuel 15:19-20
Itai
Hili ni jina la mwanamme.
Mgiti
Hii ni aina ya kabila fulani
Kwa nini ulikwenda nasi pia?
Swali hili linaonesha kwamba mfalme hakuwa amewaomba kwenda naye.
Kwa nini mimi niwafanye mtangetange pamoja nasi?
Swali hili linasisitiza kwamba Daudi hakutaka Itai aende.
Kwa vile uliondoka jana tu
Kutia chumvi huku kunatumika kusisitiza. Itai Mgiti alikuwa amekaa pale kwa miaka kazaa.
Utiifu na uaminifu na uambatane nanyi.
Hii ni baraka ambayo Daudi anampa.
2 Samuel 15:21-23
Kama Yahwe aishivyo, na kama bwana wangu mfalme aishivyo
Hapa mwandisha anafanya ahadi ya dhadi. Analinganisha uhakika wa kutimiza ahadi kwa uhakika wa kuishi kwa mfalme na Yahwe.
mtumishi wako
Itai anajitaja kwa heshima ya mfalme.
kwamba ni maisha au kifo
"hata kama nitauawa nikikusaidia"
Nchi yote ikalia kwa sauti kuu
Wengi wa watu wa Israeli walilia kwa sauti walipomwona mfalme akiondoka. Huku ni kutia chumvi kwamba nchi yote ililia.
kwa sauti kuu
Hapa watu wengi waliokuwa wakilia wanatajwa kama walishirikiana sauti kuu.
Bonde la Kidroni
Hili ni jina la eneo karibu na Yerusalemu
2 Samuel 15:24-26
Nikiona kibari machoni pa Yahwe
Hapa "macho ya Yahwe" inaonesha mawazo na maoni ya Yahwe. Ikiwa "nitaona kibari" inamaanisha kama atapendezwa nawe.
Mahali aishipo
"Mahali uwepo wake ulipo." Sanduku la agano linaashiria uwepo wa Yahwe. Hii inarejerea mahali sanduku lilipo.
2 Samuel 15:27-29
Ahimaasi
Hili ni jina la mwanamme.
Abiathari
Hili ni jina la mwanamme
Je wewe si mwonaji?
Swali hili linatumika kumkemea Sadoki.
Tazama
Hii inamtaka msikilizaji kuwa msikivu kwa kinachofuata.
Hata neno litakapotoka kwenu
Hii inaonesha yeye akipeleka mjumbe kwa mfalme.
Kunitaarifu
Hapa mfalme anaonesha kwamba atapokea ujumbe kumtaarifu kinachofanyika Yerusalemu.
2 Samuel 15:30-31
mikuu mitupu
bila kuvaa viatu au kandambili
kichwa chake kimefunikwa
Hii ni ishara ya kuomboleza na aibi
Ahithofeli
Hili ni jina la mwanamme
waaini
Watu wanaoungana kinyume cha mwingine
Tafadhari ligeuze shauri la Ahithofeli katika upumbavu
Daudi anamwomba Yahwe alifanye shauri la Aithofeli katika upumbavu na kutokufaa.
2 Samuel 15:32-34
Ikawa
"Ilitukia." Kifungu hiki kinaonesha tukio linalofuata katika habari.
juu njiani
Neno "juu" limetumika hapa kwa sababu Daudi alipanda juu katika mwinuko na yupo juu ya kilima.
Mahali Mungu alipokuwa akiabudiwa
Hii inaweza kuelezwa kuwa "mahali ambapo watu walikuwa wakimwabudu Mungu"
Hushai
Hili ni jina la mwanamme.
Mwarki
Hili ni jina la kundi la watu.
Vazi lake likiwa limechanwa na udongo kichwani
Hili ni tendo la kuonesha aibu au toba. Hapa neno "udongo" linamaanisha uchafu.
Utalibadili shauri la Aithofeli kwa ajili yangu
Maoni ya Daudi kwa Hushai kwamba apinge kile Aithofeli anachoshauri.
2 Samuel 15:35-37
Je haunao pamoja nawe Sadoki na Abiathari makuhani?
Daudi anauliza swali hili ili kumwambia Hushai kwamba hayupo peke yake. Yaani kuonesha kwamba "Sadoki na Abiathari makuhani watakuwepo kukusaidia."
chochote unachosikia... lolote usikialo
Hii ni kuzidisha maana; haimaanishi kila neno asikialo. Inamaanisha mambo muhimu ayasikiayo.
Ahimaasi... Yonathani
Haya ni majina ya watu.
Kwa mikono yao
Kifungu "mikono yao" kinarejerea kwa wana na kinamaanisha kwamba wangehudumu kama wajumbe.
2 Samuel 16
2 Samuel 16:1-2
Siba
Hili ni jina la mwanamme
Mefiboshethi
Hili ni jina la kijana wa Yonathani mwana wa Sauli.
Mikate mia mbili... vichala mia moja... vishada mia moja
"mikate 200 ... vichala 100... vishada 100"
Vipande vya mikate
visehemu vya mikate
vishada mia moja vya mizeituni... vishada vya tini
Kifungu hiki kinamaanisha vishada vya mizeituni vilivyosindikwa pamoja
Mizeituni
vichala vilivyo kaushwa
Kiriba vya mvinyo
"Kiriba cha ngozi kilichojaa mvinyo"
Kuzimia
"Kuchoka sana sana"
2 Samuel 16:3-4
Mjukuu wa bwana wako
"Mefiboshethi, mjukuu wa bwana wako"
mjukuu
mwana wa mtoto wa mtu.
Tazama
Hapa neno hili linatumika kuvuta makini ya mtu kwa kinachofuata.
Nyumba ya Israeli
Hii inahusu watu wa Israeli
Nitaurudisha ufalme wa baba yangu kwangu
Mjukuu wa Sauli kuruhusiwa kutawala kunazungumzwa kana kwamba ni kuurudisha ufalme katika familia yao.
Mefiboshethi
Hili ni jina la mwanamme, aliyekuwa kijana wa Yonathani mwana wa mfalme Sauli.
Nainama kwa unyenyekevu kwako
Siba hainami kiuhalisia mbele za mfalme anapoongea. Hii inamaanisha kwamba atamtumikia mfalme kwa kiwango kilekile cha unyenyekevu kama ambavyo angefanya kama angeinama kiuhalisia mbele zake.
kupata kibari mbele zako
Kifungu "kuona kibari" kinamaanisha kukubaliwa na mtu. Kingungu "mbele zako" inaonesha anachofikiri mfalme.
2 Samuel 16:5-6
Bahurimu
Jina la mahali
Shimei... Gera
Haya ni majina ya wanaume
Badala ya
"Hata hivyo kulikuwa na"
Walinzi
Hawa ni watu wanaomlinda mtu mhimu.
2 Samuel 16:7-8
mwovu
Mtu mwovu, mkosaji au mvunja sheria.
mtu wa damu
Hapa "damu" inaonesha watu wote aliokuwa amewaua vitani.
Yahwe amekulipa
Yahwe anawalipa kwa kuwaadhibu.
Kwa damu ya familia ya Sauli
Hapa "damu" inaonesha watu waliokuwa wameuawa kutoka katika familia ya Sauli. Mfalme alikuwa anawajibika kwa kufa kwao.
ambaye umemiliki badala yake
Daudi alitawala kama mfalme juu ya watu ambao Sauli alikuwa amewamilki.
katika mkono wa Absalomu
Hapa "mkono" unaonesha mamlaka.
2 Samuel 16:9-10
Abishai
Hili ni jina la mwanamme
Seruya
Hili ni jina la mwanamme
Kwa nini mbwa mfu huyu amlaani bwana wangu mfalme
Abishai aliuliza swali hili kuonesha hasira yake juu ya mtu yule.
Umbwa mfu huyu
Hapa mtu anaelezwa kwamba hafai kwa kulinganishwa na mbwa mfu.
Nifanye nini nanyi, wana wa Seruya
Swali hili liliulizwa ili kuwakosoa wana wa Seruya.
Pengine ananilaani kwa sababu
"Anaweza kuwa ananilaani kwa sababu"
Mlaani Daudi.' Nani sasa awezaye kumwambia, 'Kwa nini unamlaani mfalme
Hii inasemwa kama swali kusisitiza kwamba jibu ni kwamba "hakuna."
2 Samuel 16:11-12
Mwanangu, aliyetoka katika mwili wangu
Daudi anamweleza mwanawe katika njia hii kusisitiza ukaribu uliopo kati ya baba na mwana.
anataka kuchukua uhai wangu
Hii ni njia laini ya kuonesha hali ya kumwua mtu.
Si zaidi sana mbenjamini huyu akatamani anguko langu
Daudi anatumia swali hili kuonesha kwamba hashangazwi kwamba mtu yule anataka kumwua.
anatamani anguko langu
Hapa Daudi anaelezea tamaa ya mtu ya kumwua kama vile Daudi alikuwa kitu ambacho mtu alitaka kukiangamiza.
Mwache peke yake alaani
Hapa kifungu "mwache peke yake" kinamaanisha kuacha kumzuia kufanya anachokifanya.
ataangalia
Hapa "kutazama" kunamaanisha "kujari"
maangaiko niliyofungiwa
Hapa Daudi anazungumzia maangaiko kama vile yalikuwa ni mnyama mkari ambaye Mbenjamini amemfungia.
2 Samuel 16:13-14
Shimei alikwenda kando yake juu ya upande wa kilima
Shimei alikuwa akitembea sambaba na Daudi na watu wake, japokuwa Shimei alikuwa juu upande wa kilima.
2 Samuel 16:15-16
Ahithofeli
Hili ni jina la mwanamme
Hushai
Hili ni jina la mwanamme
Ikawa kwamba
"Ikawa kwamba." Kifungu hiki kinatumika kutambulisha tukio linalofuata katika habari
Mwarki
Hili ni jina la mwanamme
2 Samuel 16:17-18
Utiifu
Hisia nzito ya kusaidia na upendo
Je huu ndiyo utiifu wako kwa rafiki yako? Kwa nini haukwenda pamoja naye?
Maswali haya yanaulizwa kumkosoa Hushai.
Yule ambaye Yahwe
Hushai anamrejerea Absalomu
Yule ambaye... huyo ndiye mtu... pamoja naye
Hapa Hushai anamrejerea Absalomu katika nafsi ya tatu kuchukua msisitizo kutoka kwake na kuelekeza kwa Yahwe na watu aliowachagua. Hii inaweza kuandikwa katika nafsi ya pili.
2 Samuel 16:19
Kwani ni nani ninayepaswa kumtumikia? Je sipaswi kutumika mbele za mwana?
Hushai anauliza swali hili kusisitiza kwamba anataka kumtumikia Absalomu.
2 Samuel 16:20-21
Ahithofeli
Hili ni jina la mwanamme
kulitunza kasiri
Kifungu "kutunza" kinamaanisha kuangalia.
kuwa kitu kinachonuka mbele ya baba yako
Ahithofeli anazungumia Absalomu kumchukiza baba yake kama vile kingekuwa kitu ambacho kina harufu ya kuchukiza.
Kisha mikono ya wote walio pamoja nawe itatiwa nguvu
Hapa watu waliomfuata Absalomu wanarejerea kwa kutaja mikono yao. Habari hii itaitia nguvu utiifu wa watu kwa Absalomu na kuwapa hamasa.
2 Samuel 16:22-23
Kutanda
"Kuweka"
juu ya kasri na Absalomu akalala... masuria wa baba yake mbele za Israeli wote.
Hii inamaanisha kwamba watu walikuwa wanaweza kuliona hema na Absalomu akiingia na kutoka ndani ya hema pamoja na wanawake. Kifungu hiki "Israeli wote" kinatia chumvi, maana ni wale tu walikuwa karibu na kasiri wangeweza kuiona.
Basi ushauri wa Ahithofeli... ilikuwa kama vile mtu alisikia
Hapa mwandishi analinganisha ni kwa kiasi gani watu waliamini ushauri wa Ahithofeli kama vile ambavyo wangeamini ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu.
kama mtu anavyosikia kutoka katika kinywa cha Mungu mwenyewe
Hapa kinywa cha Mungu kinamwakilisha na kinasisitiza hotuba yake.
2 Samuel 17
2 Samuel 17:1-4
Ahithofeli
Hili ni jina la mwanamke
Watu kumi na mbili elfu
"watu 12,000"
inuka na
"kuanza ku"
njoo
"Kuja kwa"
amechoka na dhaifu
Kimsingi maneno haya yanamaanisha kitu kimoja na yanatumika kwa pamoja kusisitiza jinsi Daudi alivyokuwa dhaifu.
tutamshangaza kwa hofu
Hapa neno "hofu" laweza kuelezwa kwa kisifa "kuogopa."
Nitamshambulia mfalme peke yake
Inaonesha kwamba alikusudia kumwua mfalme.
kuwarudisha watu wote
Hii inamaanisha watu wote waliokuwa pamoja na Daudi.
kama bibi harusi akija kwa mmewe
Hapa Ahithofeli anazunguza furaha ya watu kwa kulinganisha na furaha ya bibi harusi.
Kuwa katika amani
Hii inamaanisha kuwa na amani au kuishi kwa amani.
chini yako
Hii inahusu kuwa chini ya mamlaka ya mfalme.
2 Samuel 17:5-7
Hushai Mwarki
Huyu alikuwa rafiki wa Daudi
Ahithofeli
Hili ni jina la mwanaume.
2 Samuel 17:8-10
Wako kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake
Hasira ya askari hapa inalinganiswa na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake.
dubu
mnyama mkubwa na mkali anayetembea kwa miguu minne na ana makucha na meno makali
Mtu wa vita
Hii inamaanisha amepigana vita nyingi na anajua kwa kina njia ya vita.
Tazama
Neno hili limetumika kuvuta makini ya mtu kwa kile kinachofuata
shimo
tundu refu katika ardhi
au katika sehemu ningine
Hili ni eneo lingine analoweza kuwa amejificha.
baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa
Inamaanisha watu wa Daudi watakapokuwa wamewauwa baadhi ya watu wa Absalomu
mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu
Nomino "machinjo" inamaanisha tukio ambapo watu wengi wameuawa kwa ukatili.
ambao mioyo yao ni kama mioyo ya simba
Hapa askari wanatajwa kwa "mioyo" yao. Pia, ujasiri wao mkuu unalinganishwa na ule wa simba.
2 Samuel 17:11-12
kwamba Israeli wote wakusanywe pamoja kwako
Askari wote wanatajwa hapa kama "Israeli wote"
kutoka Dani hadi Beersheba
Kifungu hiki kinamaanisha kutoka mpaka wa kaskazini hadi mpaka wa kusini wa Israeli
wengi kama mchanga ulioko ufuweni mwa bahari
Hii ni kuzidisha maana pale chembe zote za mchanga zinalinganishwa na idadi ya askari wa Israeli.
kwamba wewe mwenyewe unakwenda vitani
Kifungu hiki "binafsi" kinamaanisha kwenda wewe mwenyewe na wala siyo kutuma mtu mwingine.
kuja juu yake
Hii inamaana ya kwenda kwake kwa kusudi la kumshambulia.
tutamfunika kama umande unavyofunika ardhi
Jeshi la Absalomu linaelezwa kulifunika jeshi la Daudi kama umande unavyoifunika ardhi wakati wa asubuhi.
umande
mvuke unaoanguka juu ya ardhi kama maji na kuifunika ardhi wakati wa usiku na kuacha ardhi imeloa.
Hatutaacha hata mmojawao ... akiwa hai
Sentensi hii imetumika kusisitiza kwamba watamwua kila mtu.
Yeye mwenyewe
Maneno haya yote yanamtaja Daudi.
2 Samuel 17:13-14
Ndipo Israeli wote
Hii inawahusu askari wa Israeli na siyo Waisraeli wote.
tutaleta kamba juu ya mji huo na kuukokotea mtoni, hata kusionekane hata jiwe moja dogo lililosalia
Hii inamaanisha kwamba askari wangeuangusha mji chini na kukokota vipande vyake katika mto
hata kusionekane hata jiwe moja dogo lililosalia.
Hii ni kutia chumvi kwa kueleza ni jinsi gani watakavyouangamiza mji. Hii siyo katika hali halisia.
Hushai Mwarki
Huyu ni rafiki wa mfalme Daudi. Arki ni jina la kundi la watu katika Israeli
Ahithofeli
hili ni jina la mshauri wa Daudi
Kukataliwa kwa shauri jema la Ahithofeli
Neno "kukataliwa" linaweza kuelezwa na kitenzi "kataa"
kulete angamizo juu ya Absalomu
"Kuleta" kitu fulani juu ya mtu inamaanisha kusababisha jambo kufanyika kwake.
2 Samuel 17:15-16
Sadoki ... Abiathari
Haya ni majina ya wanaume
vile na kwa njia hiyo
Kifungu kinamaanisha "kama hivi" kuhusu kile Ahithofeli alichokuwa amekisema mwanzo
vivuko vya Araba
Hii ni sehemu ya mto isiyo na kina kirefu ambayo watu wanaweza kuvuka kwa kutembea. Araba ni nchi kandokando ya sehemu zote mbili za mto Yordani
Kwa jinsi yoyote
Hii inamaanisha kuhakikisha unafanya jambo kwa namna yoyote.
Mfalme atamwezwa
Hapa mfalme na watu wake kuuawa wanaelezwa kama vile walikuwa "wamemezwa" na adui.
2 Samuel 17:17-18
Yonathani... Ahimaasi
Haya ni majina ya wanaume
Ujumbe ulipokuja
Hapa "ujumbe" unaelezwa kama unakuja kwao, wakati uhalisia ni mwanamke aliyeleta taarifa kwo.
wakati huu
wakati mmoja
Hivyo Yonathani na Ahimaasi wakaondoka
Inaoneshwa kwamba walikuta kwamba kijana amemwambia Absalomu kuwepo kwao pale.
chemichemi za En Rogeli... Bahurimu
Haya ni majina ya sehemu, karibu na Yerusalemu. Bahurimu ni mji mdogo.
Wakashuka
"Waliteremka wenyewe kisimani na kujificha"
2 Samuel 17:19-20
Mama wa nyumba ile
"mke wa mtu yule"
Ahimaasi... Yonathani
Haya ni majina ya wanaume.
2 Samuel 17:21-22
Ikawa
"Ikatukia." Kifungu hiki kinaonesha tukio jingine katika habari
vuka juu ya maji haraka
Hapa "maji" yanarejerea Mto Yordani.
Ahithofeli ametoa mashauri haya na haya
usemi "haya na haya" umetumika mahali pa habari ambayo tiyari msomaji anaifahamu. Hapa inahusu ushauri alioutoa Aithofeli kwa Absalomu katika 17:1.
Hata ilipofika alfajiri hakuna hata mmoja aliyesalia kwa kutouvuka Yordani
Sentence hii imetumika kusisitiza kwamba wote walivuka mto.
2 Samuel 17:23
Ona
"jua" au "tambua"
ushauri wake haukufuatwa
Hii inaweza kuelezwa kwamb "Absalomu hakuwa ameufuata ushauri wake"
kupanda juu ya punda
Kuweka nguo au ngozi ya kukalia juu ya punda au farasi kwa aliyempanda kukaa juu yake.
Kuweka mambo yake katika utaratibu
Alijiandaa kwa kifo chake kwa kuwaambia familia yake cha kufanya baada kufa kwake.
Kwa njia hii
"Hivi ndivyo ilivyo"
alizikwa
Hii yaweza kuelezwa "kuwa walimzika"
2 Samuel 17:24-26
Mahanaimu... Gileadi
Hii ni baadhi ya miji katika Israeli
Amasa... Yoabu... Yetheri... Nahashi
Haya ni majina ya wanaume
Mwishimaeli
Huyu ni uzao wa Ishmaeli. Baadhi ya nakala zinaonesha kuwa "Mwisraeli"
Abigaili... Seruya
Haya ni majina ya wanawake.
2 Samuel 17:27-29
Ikawa
Kifungu kinatambulisha tukio linalofuata katika habari
Mahanaimu... Raba... Lo Debari... Rogelimu
Haya ni majina ya miji au sehemu.
Shobi... Nahashi... Makiri... Amieli... Barzilai
Haya ni majina ya wanaume.
Mwamoni... Mgileadi
Haya ni majina ya makundi ya watu
magodoro na mabulangeti
godoro ni kitu laini cha kulalia, na blangeti ni nguo ya kujifunika ili kupata joto.
Unga
Unga ni nafaka iliyopondwa kuwa laini na unatumika kutengeneza mkate au ugali.
Iliyookwa
"Iliyopikwa"
Maharage
mbegu zipikwazo kwa kuliwa
dengu
Ni aina ya mbegu zinazopikwa na kuliwa
siagi
maziwa yaliyoganda na kuwa magumu
Kiu
Hitaji la maji ya kunywa au kimiminika kingine.
2 Samuel 18
2 Samuel 18:1-2
Daudi akawahesabu askari waliokuwa pamoja naye na akaweka
Daudi hakuhesabu watu wote mwenyewe, lakini ni watu wake waliowahesabu.
Makapteni
Kapteni ni mtu mwenye mamlaka juu ya kundi la askari.
moja ya tatu... tatu nyingine
tatu... tatu nyingine** - "moja ya tatu ya jeshi... therusi nyingine ya jeshi." Therusi ni sehemu moja kati ya sehemu tatu ya kitu kimoja kizima.
Abishai... Seruya
Haya ni majina ya wanaume
Itai
Hili ni jina la mwanamme.
Mgiti
Huyu ni mtu kutoka Gathi, mji wa Wafilisiti.
Mimi mwenyewe nitakwenda pamoja nanyi pia bila shaka
Hii ni kwenda pamoja na jeshi vitani.
2 Samuel 18:3-4
Nusu yetu
Neno "nusu" linarejea kwa kitu kimoja kati ya viwili vinavyolingana.
Wewe ni zaidi ya watu elfu kumi kati yetu
Hii inamaanisha kwamba jeshi la adui linahesabu kumwua Daudi kuna thamani ya kuua watu 10,000. Idadi ya watu 10,000 ni hesabu iliyotiwa chumvi ili kusisitiza idadi kubwa zaidi ya watu.
elfu kumi
"10,000"
Kwa hiyo ni afadhari zaidi ukitusaidia ukiwa mjini
Daudi angeweza kuwasaidia akiwa mjini kwa kuwashauri na kupeleka watu kuwasaidia.
2 Samuel 18:5
Abishai
Hili ni jina la mwanamme
Itai
Hili ni jina la mwanamme
Mmtendee kwa upole kwa ajili yangu
"Kwa ajili yangu, msimdhuru." Kifungu "mmtendee kwa upole" inamaanisha kuwa mpole kwa mtu bila kumdhuru.
Kwa ajili yangu
"faida yangu" au "kwa ajili yangu"
kijana, pamoja na Absalom
"Kijana Absalomu"
2 Samuel 18:6-8
jeshi likaenda nyikani dhidi ya Israel
Hii inamaanisha kwamba walikwenda na kupigana nao vitani.
eshi la Israeli likashindwa mbele ya askari wa Daudi
Inaweza kuelezwa katika muundo tendaji yaani "Askari wa Daudi walilishinda jeshi la Israeli"
Machinjo makuu
Tukio ambapo watu wengi waliuawa kwa ukatili.
Watu elfu ishirini
"20,000"
watu wengi wakaangamizwa na msitu kuliko upanga
Hapa "msitu" unaelezwa kama ulikuwa hai kuweza kufanya kitendo. "Upanga" inahusu jeshi la Daudi lililoweza kupigana kwa upanga.
2 Samuel 18:9-11
Ikatukia kwamba Absalomu akakutana na askari wa Daudi
Hili ni tukio lilotokea wakati wa vita.
na kichwa chake kikanaswa katika matawi ya mti
Absalomu alikuwa na nywele ndefu zilizonasa kwenye matawi ya mti.
Tazama
Neno hili linavuta makini ya mtu kwa ajili ya kinachofuata.
Ning'inia
Kuelea juu bila kukanyaga juu ya nchi au kitu.
kati ya nchi na anga
"Hewani"
Kwa nini haukumpiga hata chini
Swali hili linamaanisha alipaswa kuwa amemuua.
shekeli kumi za fedha na mkanda
Katika viwango vya sasa ni sawa na gramu 110 za fedha.
mkanda
Huu ni mkanda maalumu unaoonesha kwamba mtu fulani ni askari mwenye cheo ili apewe heshima.
2 Samuel 18:12-13
shekeli elfu za fedha
"shekeli 1,000 za fedha." Katika vipimo vya sasa ni sawa na salafu 1,000" au "kilo 11 za sarafu"
nisingeinua mkono wangu juu ya mwana wa mfalme
Kifungu "kuinua mkono" kinamaana ya kushambulia.
Mtu asimguse
Hapa "kugusa" inamaanisha "kudhuru"
Uongo
Neno "uongo" laweza kuelezwa kwa kirai kitenzi. Lakini pia inahusu kutotii agizo la mfalme.
Hakuna cha kufichika kwa mfalme
Hii inamaana jinsi mfalme anavyojua karibu kila kitu kitendekacho kama vile kila kitu kilikuwa na umbo kujua kilipo.
2 Samuel 18:14-15
Sitakusubiri
Yoabu anamaanisha kwamba hawezi kusubiri kwa kuongea na yule mtu.
Moyo wa Absalomu
Hapa moyo wa Absalomu unatajwa kama kifua au sehemu ya juu ya mwili.
Silaha
Hii inarejerea vyote viwili silaha za kuvaliwa kwa kujilinda na silaha za kumshambulia adui.
2 Samuel 18:16-17
likarudi kutoka kuwafuatia Israeli
Hapa "Israeli" inarejerea kwa jeshi la Waisraeli.
Kisha Yoabu akapiga tarumbeta na jeshi likarudi kutoka kuwafuatia Israeli, hivyo Yoabu akalirudisha jeshi
Hii inaelezea alichokiagiza Yoabu kwa kupinga tarumbeta. Yaweza pia kutafsiriwa kuwa "kisha Yoabu akapiga tarumbeta kuwarudisha wanajeshi na jeshi likarudi kutoka katika kuwafuata Israeli"
Walimchukua Absalomu na kumtupa
"Walichukua mwili wa Absalomu na kuurusha shimoni"
wakaufukia mwili wake chini ya rundo kubwa la mawe
Baada ya kuuweka mwili wake shimoni waliufunika kwa rundo la mawe.
Wakati Israeli wote
Hapa "Israeli wote" inarejerea kwa askari wa Kiisraeli. Neno "kimbia" lamaanisha kuondoka.
2 Samuel 18:18
Bonde la Mfalme
Hili ni jina la eneo.
Sina mwana wa kuchukua kumbukumbu ya jina langu
Absalomu anatumia kifungu "jina langu" kujitaja mwenyewe na familia yake.
hivyo inaitwa Mnara wa Absalomu hata leo
Hii yaweza kuelezwa kuwa hivyo watu wakaiita nguzo ya Absalomu tangu siku hiyo.
Hata leo hii
Hii inamaanisha wakati kitabu kinaandikwa.
2 Samuel 18:19-20
Sadoki
Hili ni jina la mwanamme.
Ahimaasi
Hili ni jina la mwanamme
niende kwa mfalme na habari njema
Hapa Ahimaasi anazungumzia kukimbia na kwenda kumwambia mfalme habari njema kama vile habari njema ilikuwa ni kitu alichokibeba.
mkono wa adui zake
Hapa "mkono" unamaanisha kutawala. Yaani "kuwatawala adui"
mchukua habari
"Anaye toa taarifa"
Hautachukua taarifa
Hii inamaanisha kutokupeleka taarifa kwa mfalme.
2 Samuel 18:21-23
mwambie mfalme ulichokiona
Yoabu anamwambia kwenda na kumwambia mfalme kuhusu habari ya vita.
2 Samuel 18:24-25
Basi
Neno hili limetumika hapa kuonesha mwisho wa habari na kuana kwa sehemu nyingine katika habari.
na kuinua macho yake
Hapa mlinzi kuona jambo inazungumzwa kana kwamba aliinua macho yake.
Anahabari kinywani
Hapa mfalme anaongelea mtu mwenye taarifa kama vile taarifa ilikuwa ni kitu kilichokaa kinywani mwake.
2 Samuel 18:26-27
Nadhani kukimbia kwake mtu aliye mbele ni kama kukimbia kwake Ahimaasi mwana wa Sadoki
Mlinzi analinganisha jinsi mtu anavyokimbia kama jinsi Aimaasi anavyokimbia kudhani kwamba anaweza kuwa yeye.
Ahimaasi... Sadoki
Haya ni majina ya wanaume
2 Samuel 18:28-30
akainama yeye mwenyewe uso wake chini mbele ya mfalme
Alifanya hivi ili kumweshimu Mfalme.
Atukuzwe Yahwe
"Atukuzwe Yahwe." Hapa "kubarika inamaanisha kutukuza.
watu walioinua mkono wao kinyume cha bwana wangu mfalme
Hapa Ahimaasi anazungumzia watu wanaompinga mfalme kama vile walikuwa wakiinua mikono yao juu yake.
fujo kubwa
Hii inamaanisha kuwa watu walikuwa wakifanya mambo kama hayakuwa sawa
Geuka kando
"Toka njiani" au "simama kando"
2 Samuel 18:31-33
Inuka kinyume
Inamaanisha kupinga.
Adui wa bwana wangu mfalme,... wawe kama huyo kijana
Mkushi anatumia kulinganisha kama njia laini ya kumwambia mfalme juu ya kifo cha Absalomu.
kuhuzunika
kuchanganyikiwa
2 Samuel 19
2 Samuel 19:1-2
Yoabu aliambiwa
Yaweza kuelezwa kuwa kuna mtu alimwambia Yoabu.
Tazama
Hii inavuta makini ya mtu kwa ajili ya kifuatacho.
Hivyo siku ile ushindi uligeuzwa kuwa maombolezo kwa jeshi lote
Hii inamaanisha kwamba jeshi lote liliomboleza badala ya kusherehekea.
2 Samuel 19:3-4
kama watu waonao haya baada ya kukimbia vitani
Mwandishi analinganisha jinsi askari alivyokuwa akiingia mji kama ambavyo askari wanavyokwenda baada ya kukimbia vita. Hii inamaanisha kwamba walijisikia kuaibika.
Nyemelea
Kwenda bila kutakawengine wakuone
Mfalme alifunika uso wake
Hii ni njia ya kuonesha huzuni na maombolezo.
2 Samuel 19:5-6
Leo umeziaibisha nyuso za askari wako
Hapa askari wanatajwa kwa nyuso zao kusisitiza jinsi ambavyo wangeficha nyuso zao kwa sababu ya aibu.
Siyo kitu kwako
Kifungu hiki kimetiwa chumvi, lakini kinaonesha uthamani mdogo alionao Daudi kwa jeshi lake.
kame Absalomu angesalia na sisi sote tungekufa hilo lingekufurahisha
mwandishi anaonesha hali ya kuhisi.
2 Samuel 19:7-8
Naapa kwa Yahwe
Yoabu anafanya nadhiri madhubuti.
Usipokwenda, hakuna mtu hata mmoja atakayebaki
Hii inamaanisha kwamba askari wangebaki iwapo tu Daudi angekwenda.
Hakuna atakayesalia
Hii inaonesha wao kubaki watiifu kwake.
Wote wakaambiwa
Hii inaweza kuelezwa kuwa wengi wao.
Tazama
Hii imetumika kuvuta makini ya mtu kwa ajili ya habari inayofuata.
Watu wote
Hapa "watu" inahusu waliomfuata Daudi.
Israeli walikimbia kila mtu nyumbani kwake
Hapa "Israeli" inahusu askari wa Waisraeli waliomfuata Absalomu.
2 Samuel 19:9-10
kutoka katika mkono wa adui zetu
Hapa "mkono" unamaanisha umiliki.
kutoka katika mkono wa Wafilisiti
Hapa "mkono" unamaanisha umiliki. Yaani kutoka chini ya miliki ya Wafilisiti.
kuikimbia nchi mbele ya Absalomu
Hii inamaanisha aliikimbia nchi mbele ya Absalomu.
Amekufa vitani
"alikufa vitani"
kwa nini hatuongei juu ya kumrudisha mfalme tena
Hii inamaanisha wanapaswa kuangalia uwezekano wa kumrudisha Daudi kwa kuwa Absalomu alikuwa amekufa.
mfalme
Inamrejerea Daudi
2 Samuel 19:11-12
akapeleka kwa Sadoki na Abiathari
Hii inamaanisha kwamba Daudi alipeleka mjumbe kwa Sadoki na Abiathari.
Kwa nini ninyi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme kwenye kasri lake?
Swali hili linaulizwa kuwakemea wazee wa Yuda. Yaweza kuwa "mngekuwa wa kwanza kumrudisha mfalme, siyo watu wa Israeli."
kwa vile usemi wa Israeli wote unamtaka mfalme arudi
Neno "ongea" ni nomino dhahania linaloweza kuelezwa kwa kitenzi "ongea" au "sema"
Kumrudisha mfalme katika kasiri lake
Hapa kurejesha mamlaka ya mfalme yanazungumzwa kama vile kumrudisha katika makao yake.
Ninyi ni ndugu zangu, nyama na mfupa wangu
Hapa mfalme anaeleza jinsi wanavyohusiana kwa kusema kwamba wana mwili na mfupa mmoja. Lakini pia maneno "ninyi ni" yaweza kuongezwa katika kirai cha pili.
Kwa nini basi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme?
Hili ni swali la pili na pia ni karipia kwa wazee wa Yuda.
2 Samuel 19:13-15
Amasa
Hili ni jina la mwanamme
Je wewe si mwili na mfupa wangu?
Daudi anatumia swali kusisitiza uhusiano wao.
mwili wangu na mfupa wangu
Hapa Daudi anawazungumzia kuhusiana kwao kwa kusema kwamba wana mwili na mfupa mmoja.
Mungu anifanyie hivyo
Huu ni usema unaomaanisha Mungu kumwua
Akaishawishi mioyo
Hapa utiifu wa watu unazungumzwa kama "mioyo".
Kama mtu mmoja
Hii inazungumzia watu kuungana katika utiifu wao kwa mfalme kama vile walikuwa walikuwa na nia moja.
walipeleka kwa mfalme
Hii inamaanisha kwamba walipeleka ujumbe kwa mfalme.
2 Samuel 19:16-18
Gera... Siba
Haya ni majina ya wanaume.
Bahurimu
Hili ni jina la sehemu
watu elfu moja... wana kumi na watano... watumishi ishirini
"watu 1,000... wana 15... watumishi 20"
mbele ya mfalme
Hii inamaanisha kwamba mfalme alikuwepo na alikuwa anafahamu kilichokuwa kinaendelea.
2 Samuel 19:19-20
Kukumbuka
Ni kukumbuka jambo
mtumishi wako
Hapa Shimei anajitaja kwa njia hii kuonesha heshima kwa mfalme.
2 Samuel 19:21-23
Abishai
Hili ni jina la mwanamme
Seruya
Hili ni jina la mwanamme.
Je Shimei asife kwa hili kwa vile alivyomlaani mtiwa mafuta wa Yahweh?
Seruya alimkasirikia Shimei kwa kumlaani Daudi na anasema anapaswa kufa.
Mtiwa mafuta wa Yahwe
Hii inamrejerea Daudi. Inamaana kwamba Daudi alikuwa mfalme aliyetiwa mafuta na Yahwe
Nifanye nini nanyi... hata leo mkawa adui zangu?
Daudi anatumia swali hili kumkemea Abishai. Hii inamaanisha kwamba hawakuwa na sababu ya kuwa adui.
Je mtu yeyote atauawa leo katika Israeli? Kwani sijui kama leo mimi ni mfalme juu ya Israeli?
Daudi anatumia swali kuendelea kumkemea Abishai. Kumaanisha "Hakuna mtu atakayeuawa leo katika taifa la Israeli.
Je kuna mtu atakayeuawa
Kifungu "kuuawa" inamaanisha kunyongwa au kuuawa.
Kwani sijui kama leo mimi ni mfalme juu ya Israeli?
Maana yake yaweza kuwa 1) "Ninajua kwamba mimi bado ni mfalme wa Israeli." 2) "Leo mimi ni mfalme juu ya Israeli!"
2 Samuel 19:24-25
Mefiboshethi
Hili ni jina la mwanaume
Hakuwa ameivalisha miguu yake
"Hakuwa ameitunza miguu yake." Miguu ya Mefiboshethi ilikuwa na ulemavu. Kifungu kinaonesha hakuwa ameitunza miguu yake vizuri.
Kwa nini haukwenda nami, Mefiboshethi?
Daudi anazungumzia kwa nini hakwenda naye pale yeye na watu waliomfuata walipoondoka Yerusalme.
2 Samuel 19:26-28
Siba
Hili ni jina la mwanamme
Bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu
Hapa hekima ya Daudi inalinganishwa na hekima ya malaika.
Fanya lililojema machoni pako
Hii inamaanisha kufanya unalodhani kuwa sawa.
Kwa maana nyumba yote ya baba yangu walikuwa maiti mbele ya bwana wangu mfalme
Mefiboshethi anazungumza jinsi ndugu zake walivyostahili kuuawa kama vile tiyari walikuwa wameuawa na walikuwa wafu.
nyumba ya bwana wangu
Hii inawahusu ndugu wa baba yake.
hiyo nililiye haki gani zaidi kwa mfalme?
Mefiboshethi anatumia swali kusisitiza kwamba hana haki ya kuomba chochote kwa mfalme.
2 Samuel 19:29-30
Kwa nini kueleza yote zaidi?
Daudi anatumia swali kumwambia haitajiki kuendelea kuongelea mgogoro wake na Siba.
2 Samuel 19:31-33
Berzilai
Hili ni jina la mwanaume
Rogelimu... Mahanaimu
Haya ni majina ya maeneo
Mgileadi
Hili ni jina la ukoo katika Israeli.
Yordani
Mto Yordani
Miaka themanini
"Umri wa miaka 80"
Kuhudumia
"kuandaa"
2 Samuel 19:34-36
Kwani kuna siku ngapi zilizosalia maishani mwangu, hata niende na mfalme huko Yerusalemu?
Hapa Berzillai anamaanisha kwamba yeye ni mzee na kwamba hakuna haja ya yeye kumsindikiza Daudi. Yaweza kumaanisha kuwa sitaweza kuishi muda mrefu. Kwa hiyo hakuna haja ya kwenda na mfalme huko Yerusalem.
Miaka themanini
"umri wa miaka 80"
Kwa nini basi mtumishi wako awe mzigo kwa bwana wangu mfalme?
Hapa Berzilai anamaanisha kwamba hapendi kuwa mzigo kwa mfalme.
Je naweza kutofautisha kati ya mema na mabaya?
Berzilai anatumia maswali kusisitiza kwa nini hapendi kwenda Yerusalemu. "Mema" na "mabaya" yanamaanisha kinachotamaniwa na kisichotamaniwa.
Je mtumishi wako aweza kuonja anachokula na kunywa?
Barizilai anatumia maswali ya kusisitiza kwa nini haitaji kwenda Yerusalemu.
Je naweza kuisia zaidi sauti za wanaume na wanawake waimbao?
Berizilai anatumia maswali ya msisitizo kwa nini hapendi kwenda Yerusalemu.
Kwa nini basi mtumishi wako awe mzigo kwa bwana wangu mfalme?
Berizilai anatumia swali kusisitiza kwamba hafikirii kwama anapaswa kwenda na mfalme huko Yerusalemu.
Kwa nini mfalme anilipe kwa thawabu hiyo?
Berizilai anatumia swali kusisitiza kwamba hajui ni lini mfalme angemlipa kwa njia hii.
2 Samuel 19:37
Maelezo ya Jumla
Berzilai anaomba kwamba Kimhamu aachwe kuchukua nafasi yake.
Kimhamu
Hili ni jina la mwanaume
katika kaburi la baba na mama yangu
Hii haimaanishi kwamba anataka kufa mara tu baada ya makaburi yao, lakini anamaanisha kwamba anataka afe katika mji walipozikwa.
Yeye avuke
Hii inamaanisha kuvuka Mto Yordani.
2 Samuel 19:38-39
Kimhamu atavuka nami.
Hii inarejerea kuvuka Mto Yordani.
2 Samuel 19:40-41
akavuka kuelekea Gilgali
Walivuka Mto Yordani kuelekea Gilgali.
Kimhamu
Hili ni jina la mwanamme
kumleta mfalme
"kumsindikiza mfalme." Walivuka Mto Yordani.
Jeshi la Yuda lote na nusu ya jeshi la Israeli likamleta mfalme.
"Jeshi la Yuda lote na nusu jeshi ya Israeli likamleta mfalme"
Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda... na watu wote wa Daudi pamoja naye?
Watu wa Israeli wanatumia swali hili kuonesha kwama wajisikia kwamba wamesalitiwa na ndugu zao wa Yuda.
Kukutolosha
Waisraeli wanazungumza jinsi watu wa Yuda walivyomsindikiza mfalme kuvuka mto kama vile mfalme alikuwa kitu kilichoibwa kisicho chao.
Yordani
Mto Yordani
2 Samuel 19:42-43
Kwa nini basi mkasirike juu ya hili?
Watu wa Israeli wanauliza swali hili kuwakemea watu wa Israeli.
Je sisi tumekula chochote ambacho mfalme amekitoa? Je ametupa zawadi yoyote?
Watu wa Yuda kama swali linavyoonesha wanaonesha kwamba hawajachukua chochote kwa mfalme.
Hata hivyo tuna haki zaidi kwa mfalme kuliko ninyi
"Tuna madai makubwa kwa Daudi kuliko ninyi." Yaani "tuna haki zaidi ya kumhudumia mfalme na kuwa naye kuliko ninyi"
Kwa nini basi kutudharau?
Waisraeli wanauliza swali hili kuonesha hasira yao. Yaweza kuwa "hamkupaswa kutudharau hivyo!"
Je hatukuwa wa kwanza kupendekeza kumrudisha mfalme wetu?
Watu wa Israeli wanauliza swali hili kuwakumbusha na kuwakemea watu wa Yuda.
Lakini maneno ya watu wa Yuda hata yakawa makali kuliko maneno ya watu wa Israeli.
Hapa "maneno" yarejerea mazungumzo ya watu wa Yuda.
2 Samuel 20
2 Samuel 20:1-2
kuwa mahali pamoja
Hii inarejerea mji wa Gilgali.
Sheba... Bikri
Haya ni majina ya wanaume.
Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese
Maelezo haya yote yanamaanisha kitu kimoja. Shiba anasisitiza kwamba yeye na makabila ya Israeli hawana uhusiano na Daudi. Yaani urithi wa Daudi na familia ya baba yake hawana uhusiano na Israeli.
2 Samuel 20:3
kulitunza kasiri
Hapa kifungu "kutunza" inamaanisha kuangalia.
nyumbani chini ya ulinzi
Ikiwa nyumba iko "chini ya ulinzi" inamaanisha kuna mlinzi aliyepo katika nyumba.
walikuwa imefungwa
Inamaana hawakuruhusiwa kutoka ndani
wajane
Hawa ni wanawake ambao waume zao wamefariki.
2 Samuel 20:4-5
Amasa
Huyu ni jemedari wa jeshi la Daudi.
2 Samuel 20:6-7
Abishai
Huyu ni jemedari mwingine wa jeshi la Daudi.
Hasitudhuru zaidi
"hasituumize zaidi"
watumishi wa bwana wako, askari wangu
Kifungu "askari wangu" inafafanua "watumishi" wapi. Daudi anajitaja mwenyewe kama "bwana wako" kama njia rasmi ya kuongeza na mtu mwenye cheo cha chini.
kumfuatia
"kufukuza mtu"
mbali na upeo wa macho yetu
Hapa Daudi anataja jeshi lake kwa uoni wao kusisitiza kwamba Shiba na watu wake wangejificha hata wasiwakamate.
ataona miji yenye ngome
Hii inamaana kwamba Shiba na watu wake wangeingia katika miji hii na kujificha kutoka jeshi la Daudi. Neno "yeye" linasimama badala ya Shiba lakini linawarejerea wote Shiba na watu wake.
Wakelethi... Wapelethi
Haya ni majina ya makundi ya watu waliokuwa wakimlinda Mfalme Daudi.
2 Samuel 20:8
Walipokuwa
"Walipokuwa Yoabu na watu wa Yuda"
mkanda
mshipi wa ngozi au kitu kingine kilichotengenezwa kufunga vazi au silaha.
upanga ukadondoka
upanga ukaanguka
upanga ukadondoka
Yoabu aliuacha upanga uanguka ili kumpumbaza Amasa kwa kufikiri kwamba Yoabu hakuwa na silaha, hata amruhusu Yoabu kumkaribia.
2 Samuel 20:9-10
binamu yangu
Amasa alikuwa mwana wa dada wa mama wa Yoabu.
kwa utaratibu
"kwa upole"
akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu
Hii ilikuwa njia ya kawaida a watu kusalimiana.
jambia
upanga mfupi ambao ni rahisi kuuficha ulikuwa mapigano ya karibu na mauaji.
matumbo kumwagika
utumbo ulitoka nje.
2 Samuel 20:11-13
aliye kwa ajili ya Daudi
Kuwa "kwa ajili" ya mtu inamaanisha kumuunga mkono.
Amasa akalala akigaagaa katika damu yake
Amasa alikuwa akaijivingirisha katika damu yake, lakini kwa wakati huu yawezekana alikwisha kufa. Inaelezwa hivi kuonesha mwili wake ulivyoonekana.
watu wote wakasimama... kumkaribia wakasimama
Inaanisha waliacha kutembea na kushangaa maiti ya Amasa.
Alimbeba Amasa
"aliubeba mwili wa Amasa"
Baada ya Amasa kuondolewa njiani
Hii yaweza kuelezawa kuwa baada ya mtu kuuondoa mwili wa Amasa njiani.
katika kumfuatia
Nomino dhahania yaweza kuelezwa kama kitenzi.
2 Samuel 20:14-16
Sheba akapita
Hapa "Sheba" inarejerea kwa wote Sheba na jeshi lake.
Abeli wa Bethi Maaka
"Abeli wa Bethi Maaka." Majina yote yanahusu sehemu moja na yaweza kuunganishwa. Ni mji karibu na kabila ya Yuda.
Wa Waberite
Hili ni jina la kundi la watu.
na pia kumfuata Sheba
"Walimfuata Sheba pia"
kujenga buruji
Hii inamaanisha walitumia silaha ya kubomolea kuungonga ukuta. Chombo hiki kilikuwa ni mti mrefu wenye ncha or kuwekewa ncha ya chuma. Kilishikiliwa na watu kadhaa ambao gonga ncha kwenye ukuta.
Walimpata
"Yoabu na askari walimpata"
dhidi ya ukuta kinyume cha mji
"dhidi ya ukuta wa mji"
Sikilizeni, sikilizeni tafadhari
Kurudia kwa neno "sikilizeni" kunasisitiza ombi la mwanamke.
2 Samuel 20:17-19
Sikiliza maneno ya mtumishi wako
Mwanamke anajitaja kama "mtumishi wako." Hii in njia laini ya mtu kuongea na mtu mwenye mamlaka.
na ushauri huo ungemaliza jambo
"na ushauri huo ungetatua tatizo"
wenye amani na uaminifu zaidi katika Israeli
Maneno yanayokosekana waweza kuongeza kuwa wa amani na mji mwaminifu zaidi katika Israeli"
Mji mama katika Israeli
Hii inamaanisha umuhimu wa mji katika nchi ya Israeli kama vile ulikuwa mji wenye heshima kama mama mwenye heshima.
Kwa nini unataka kuumeza urithi wa Yahwe?
Hapa mwanamke anatumia swali kupendekeza kwa Yoabu cha kuacha kufanya.
Kuumeza
Mwanamke anazungumzia adui kuuaribu mji kama ulikuwa chakula cha kumezwa.
urithi wa Yahwe
Mji unaoneshwa kama urithi wa Yahwe kusisitiza kwamba unamilikiwa na Yahwe.
2 Samuel 20:20-22
Iwe mbali, iwe mbali nami, hata
Hapa anarudia kifungu hiki kusisitiza kwamba asingefanya vile.
hata nikameze au kuharibu
Hii inamaanisha kuharibu mji.
kumeza au kuharibu
Katika vifungu vyote maana yake ni kuharibu. Katika kifungu cha kwanza "kuharibu" inasemwa kama ndiko "kumeza." Hii yaweza kuunganishwa.
ameinua mkono wake dhidi ya
Hii inamaanisha kuasi na kupigana na mtu fulani.
Mtoeni peke yake
Yoabu anawambia watu wa mji kumtoa Sheba peke yake.
Nitauacha mji
Hapa "mimi" inawataja wote Yoabu na askari.
Kichwa chake kitarushwa
Yaweza kuwa tutakurushia kichwa chake.
Kisha mwanamke akawaendea watu wa mji katika hekima yake
Inamaanisha mwanamke alitenda kwa busara na kuongea na watu wake walichopaswa kufanya.
kila mtu nyumbani kwake
"Kila mtu alirudi nyumbani kwake"
2 Samuel 20:23-26
Basi
Inaonesha mkato katika habari. Sehemu inayofuata inatoa mazingira ya watu waliomtumikia Mfalme Daudi
Yoabu alikuwa juu... Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu... Adoramu alikuwa juu
Kifungu "alikuwa juu" kinaonesha kuwa na mamlaka juu ya kundi la watu.
Yehoyada... Yehoshafati... Ahiludi
Haya ni majina ya wanamme.
Wakerethi... Wapelethi
Hawa walikuwa walinzi binafsi wa Daudi
Watu waliofanya kazi ya shuruti
"watumwa"
Adoramu... Sheva... Ira
Haya ni majina ya wanaume
Muyairi
Hili ni jina la kundi la watu.
2 Samuel 21
2 Samuel 21:1
alitafuta uso wa Yahwe
"Uso" inamaanisha uwepo wa Yahwe. Inamana Daudi aliomba kwa Yahwe kwa ajili ya njaa.
kwa sababu ya Sauli na familia yake ya mauaji
Sauli alikuwa ameuwauwa Wagibioni wengi, na wazao wake wana hatia kwa sababu ya dhambi hii.
2 Samuel 21:2-3
Basi
Inaonesha kuisha kwa habari na kutoa mazingira ya habari inayofuata kuhusu Wagibeoni.
Niwatendee nini? Nifanyeje upatanisho... ahadi?
Mistari hii miwili ina maana inayofanana. Yaani "Nifanyeje kuondoa dhambi hii, ili mwabariki watu wa Yahwe, waumilikio wema wake na ahadi zake?
2 Samuel 21:4
Si jambo la fedha wala dhahabu
"Pesa hazitaweza kutatua tatizo"
2 Samuel 21:5-6
aliyepanga kinyume chetu
"aliyefanya mipango dhidi yetu"
haya na tupewe watu saba kutoka katika uzao wake
Yamaanisha "waruhusu watu wako kutopa wazao wake saba"
Tutawatundika
"tutawanyonga kwa kuwatundika"
Katika Gibea ya Sauli
Sauli alikuwa anatoka katika mji wa Gibea.
Aliyeteuliwa na Yahwe
Yaweza kuwa "atakayechaguliwa na Yahwe"
2 Samuel 21:7-9
Mefiboshethi
Alikuwa mwana wa Yonathani.
Rispa... Aiya
Rispa alikuwa mwanamke na babaye aliitwa Aiya.
Amoni na Mefiboshethi... Adrieli... Barzilai
Haya ni majina ya wanaume. Huyu siyo Mefiboshethi mwana wa Yonathani.
Mikali
Hili ni jina la binti wa mfalme Sauli na alikuwa mke wa kwanza wa Daudi.
Mmeolathi
Hili ni jina la kundi la watu.
Akawakabidhi katika mikono ya Wagibeoni.
"mikono ya wagibeoni" inamaanisha Wagibeoni.
Wakauawa
Wagibeoni waliwauwa.
2 Samuel 21:10-11
Rispa... Aiya
Rispa alikuwa mwanamke na babaye aliitwa Aiya
Daudi aliambiwa
Mtu fulani alimwambia Daudi
2 Samuel 21:12-13
Yabeshi Gileadi
Huu ulikuwa ni mji katika eneo la Gibea.
Eneo la wazi
Hili ni eneo karibu na lango la mji ambapo watu walifanya kazi mbalimbali.
Bethi Shani
Hili ni jina la eneo
Gilboa
Hili ni jina la mlima
Waliokuwa wametundikwa
"Ambao Wagibeoni waliwanyonga kwa kuwatundika"
2 Samuel 21:14
Zela
Hili ni jina la mji huko Benjamini
Kishi
Hili ni jina la mwanamme.
Babaye
"baba yake Sauli"
2 Samuel 21:15-17
Ishibibenobu
Hili ni jina la mwanamme.
shekeli mia tatu
"shekeli 300"
Abishai mwana wa Seruya
Abishai na Seruya ni majina ya wanaume
usije ukaizima taa ya Israel
"Taa ya Israeli" ni usemi unaomaanisha uongozi wa Daudi na kama angekufa watu wangekosa mwelekeo sahihi.
2 Samuel 21:18-19
Ikawa baada ya haya
Kifungu kinaonesha mwanzo wa sehemu inayofuata
Gobu
Hili ni jina la mji.
Sibekai... Safu... Elhanani mwana wa Jari... Goliathi
Haya ni majina ya wanaume.
Muhushathi... Mrefai... Mbethlehemu... Mgiti
Haya ni majina ya wakundi ya watu.
Mrefai
Kundi hili la watu walijulikana kwa ushujaa wao mkubwa.
ambaye mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji
Mtu alipokuwa anafuma nguo alipitisha nyuzi katika ndoano zilizounganishwa katika mti ulioitwa "mti wa mfumaji." Hii inamaana kwamba mkuki wa Goliathi ulikuwa siyo mkuki wa kawaida.
2 Samuel 21:20-22
Numba ishirini na nne
Numba ina ** - "vidole 24 vya mikono na miguu kwa pamoja"
Mrefai
Kundi hili la watu walijulikana kwa ushujaa wao mkubwa.
Yonathani mwana wa Shama
Huyu alikuwa nduguye Daudi.
waliuawa kwa mkono wa Daudi na kwa mkono wa askari wake
"kwa mkono wa" humaanisha "kupitia" au "kwa". Maana yake ni Daudi na watu wake waliwaua.
2 Samuel 22
2 Samuel 22:1-2
Maelizo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaanza. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
katika mkono wa adui zake wote na katika mkono wa Sauli
Huu ni mwendelezo kutoka maadui na kwenda kwa adui maalumu wa Daudi, Mfalme Sauli.
kutoka mkono wa
"Inamaanisha kutoka katika nguvu ya"
Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu
Usemi huu unamaanisha mwendelezo katika sehemu, "mwamba" kwa ujumla "ngome." Ngome inajengwa kwa mawe mengi makubwa. Hii inamaanisha kwamba Yahwe ananguvu za kulinda watu wake katika madhara.
2 Samuel 22:3-4
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaanza. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
Mungu ni mwamba wangu... Yeye ni ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.
Semi hizi zote ni alama za nguvu na uwezo wa Mungu. Zinasisitiza uwezo wa Mungu wa kulinda na kuokoa watu wake
Astahiliye kusifiwa
Yaani "anayestahili kupokea sifa"
Nitaokolewa na adui zangu
"Ataniokoa na adui zangu"
2 Samuel 22:5-6
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaanza. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho.
Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maji ya uharibifu yakanishinda
Daudi anawalinganisha waovu waliotaka kumwua kama mafuriko ya maji yatakayo kumzamisha. Mistari hii miwili ina maana moja na imetumika kwa msisitizo.
Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka
Hii ni picha ya maji yaendayo kasi na kuharibu kila kitu yapitapo.
Vifungo vya kuzimu vilinizunguka; kamba za mauti zikaninasa
Daudi anazungumzia mauti na kuzimu kama watu watakao kumnasa kama mwindaji anasavyo mnyama. Vifung viwili hivi vina maana moja na imetumika kwa msisitizo.
2 Samuel 22:7
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
Katika shida yangu
"katika taabu zangu kubwa"
akaisikia sauti yangu katika hekalu lake,
Daudi anamaanisha hekalu la mbinguni anapoishi Yahwe. Hekalu la duniani lilikuwa bado kujengwa.
kilio changu cha msaada kikafika masikioni mwake
Usemi wa "masikio yake" inaonesha Yahwe akisikiliza kilio cha Daudi kwa msaada.
2 Samuel 22:8-9
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
Kisha nchi ilitikisika... ikawashwa kwayo
Hili ni jibu la Yahwe kwa kilio cha Daudi msaada kutoka kwa adui zake. Daudi anatumia taswira ya dunia kutikisika na moto kutoka kwa Yahwe kusisitiza hasira kari ya Yahwe.
Dunia ilitikisika... mbingu zikatetemeka
Daudi anazungumzia mitizamo hii miwili kuhusisha kila kitu katika uumbaji.
na ilitikiswa , kwa sababu Mungu alikuwa na hasira.
Hii yaweza kumaanisha "kwa sababu hasira ya Mungu ilizitikisa."
mianzi ya pua yake... kinywa chake
Daudi anamzungumzia Yahwe kama vile alikuwa na sehemu hizi za wanadamu.
Makaa yaliwasha kwayo
Hapa hasira ya Yahwe inalinganishwa na moto, uliosababisha makaa kuwashwa.
2 Samuel 22:10-12
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
Alizifungua mbingu... akamwaga mawingu angani
Daudi anazungumzia njia za Yahwe kwa kumwokoa Daudi kutoka kwa adui zake kama mawingu ya dhoruba yakusanyikayo juu ya sehemu. Hii inasisitiza nguvu za Mungu na hasira yake.
chini ya miguu yake
Daudi anamzungumzia Mungu kama ana miguu ya watu.
Alionekana katika mawingu ya upepo
Yaweza kuwa "alionekana juu ya mawingu ya upepo"
mawingu ya upepo
Hii inaonesha upepo kama ulikuwa ni ndege
Na akafanya giza hema kumzunguka
Giza alilolifanya Yahwe linalinganishwa na hema limfichalo kabisa.
2 Samuel 22:13-15
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
Kutoka katika radi mbele zake... miale ya radi na kuwasambaratisha
Daudi anaendelea kumweleza Yahwe, anayemlinganisha na kimbunga, akija kumwokoa kutoka kwa adui. Hii inasisitiza nguvu ya Mungu na hasira yake kwa adui wa Daudi.
Makaa ya moto yalidondoka mbele zake kutoka katika radi
Maana yake yaweza kuwa 1) "kutoka katika mwanga mwangavu alituma makaa yawakayo" au 2) "kutoka katika mwangaza wake alituma radi"
Aliyejuu sana alipiga kelele. Akapiga mishale.
Daudi anamweleza Yahwe akifanya matendo anayoweza kufanya mtu.
Alipiga mishale... miale ya radi
Daudi analinganisha radi kutoka kwa tufani ya Yahwe na mishale wangetumia askari.
2 Samuel 22:16
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
Ndipo njia za maji zilipoonekana... pumzi ya pua zake
Yahwe alipopiga kelele katika shambulio lake kwa adui za Daudi, inalinganishwa na nguvu zake za kufanya mambo katika vilindi vya bahari na nchi. Hii inaonesha uwezo wake mkuu na hasira yake kali.
misingi... ilifunuliwa
Daudi analinganisha hasira ya Yahwe na miondoka ya ardhi.
2 Samuel 22:17-18
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
kutoka katika vilindi vya maji
Daudi analinganisha adui zake na mafuriko yanayotishia kumzamisha.
Aliokoa kuatoka kwa adui yangu mwenye nguvu.
Adui wa Daudi walikuwa na nguvu. Alimsifu Mungu kwa kumkomboa kutoka kwa adui zake wote.
2 Samuel 22:19-21
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho
Walikuja kinyume changu siku ya shida yangu
"Adui zangu walipigana nami nilipokuwa katika shida kubwa"
siku ya shida yangu
Neno "siku" linawakilisha muda Daudi alipokuwa katika shida.
Lakini Yahwe alikuwa msaada wangu
"lakini Yahwe alinisaidia"
mahali palipo na nafasi
Hapa ni mahali pasipo na hatari na adui wasingemnasa.
kipimo cha usafi wa mikono yangu
Hapa "usafi wa mikono yangu" inamaanisha kitu kimoja "haki"
2 Samuel 22:22-23
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
Nimezitii njia za Yahwe
"Njia za Yahwe" inamaanisha jinsi Yahwe anavyotaka watu wake kuenenda. Hii inamaanisha Daudi alifanya kile Yahwe alichotaka afanye.
mekuwa mbele yangu
Hii inamaanisha Daudi mara kwa mara husoma na kutafakari maagizo ya Mungu
2 Samuel 22:24-25
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
Nimejiepusha na dhambi
Hii ni kuchagua kutomtenda dhambi Yahwe
kwa kadiri ya usafi wangu mbele zake
"Usafi wangu" inamaanisha kilekile "utakatifu wangu"
2 Samuel 22:26-27
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
lakini kwa wakaidi unajionesha kuwa mkaidi
"kaidi" inamaanisha kuwa mkaidi, na "mpotevu" inamaanisha kutoka katika mema na haki. Inamaanisha Mungu huwashughulikia watu kwa hekima.
2 Samuel 22:28-29
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
macho yako ni kinyume cha wenye kiburi
"macho yako" inamaanisha anachoona Yahwe. Inamaanisha Mungu humwona mwenye kiburi.
Unawashusha chini
"unaharibu kiburi chao"
wewe ni taa yangu, Yahwe. Yahwe humlika katika giza langu.
Usemi huu unamlinganisha Yahwe na taa, inamaana Humpa Daudi nuru na msaada wa kuona mambo yanapoaribika.
2 Samuel 22:30-31
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
Naweza kupita vipingamizi
"Vipingamizi" vyamaanisha kundi la askari au ukuta wa mawe. Yote yamaanisha Mungu humwezesha Daudi kuwashinda adui zake.
Naweza kuruka ukuta
Daudi ametia chumvi ili kusisitiza msaada wa Yahwe.
Neno la Yahwe ni safi
"Kila anachosema Yahwe ni kweli"
Yeye ni ngao
"Ngao" yasisitiza uwezo wa Mungu kuwalinda watu wake.
2 Samuel 22:32-33
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea.
Maana ni nani aliye Mungu isipokuwa Yahwe? Na ni nani aliyemwamba isipokuwa Mungu?
Daudi anatumia maswali kusisitiza kwamba hakuna Mungu zaidi ya Yahwe.
aliyemwamba
Daudi anamlinganisha Yahwe na mwamba kusisitiza nguvu zake na uwezo wa kuwalinda watu wake.
humwongoza asiye na hatia katika njia yake
Yahwe humlinda asiye na hatia katika usalama na kuondoa kila kinachoweza kumdhuru.
2 Samuel 22:34-35
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea.
Huifanya myepesi miguu yangu kama kurungu na kuniweka katika vilima virefu.
Miguu ya Daudi inafananishwa na ya kurungu kwa kutiwa chumvi. Yahwe anampa Daudi nguvu za kuondoka kwa kasi na kumwandalia mahali salama kwa ulinzi na pumziko.
Mikono yangu... na vitanga vyangu
Vyote vinamrejerea Daudi.
Kupinda upinde wa shaba
Ni mtu mwenye nguvu pekee awezaye kutumia upinde ulitengenezwa kwa madini.
2 Samuel 22:36-37
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
hii ngao ya wokovu wako
Daudi anailinganisha nguvu ya Yahwe ya kuokoa sawa na ngao inayomkinga askari na adui yake.
Matakwa yako
Mungu alijibu maombi ya Daudi na kumpa baraka na mafanikio juu ya adui zake
7Umeitengenezea miguu yangu nafasi chini yangu
Yahwe amemweka Daudi mahala salama ambapo adui zake hawawezi kumnasa. "Miguu" inamaanisha uwezo wa Daudi wa kusimama salama.
2 Samuel 22:38-39
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
fuatia adui zangu
"kufukuza adui zangu"
Niliwararua na kuwasambaratisha
Daudi anajilinganisha na hayawani wakali.
chini ya miguu yangu
"Miguu" hapa inamaanisha nguvu na kumiliki ushindi juu ya adui zake.
2 Samuel 22:40-41
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
Unanivika nguvu kama mkanda kwa vita
Hapa nguvu atoazo Yahwe zafananishwa na mkanda unaomwezesha Daudi kufanya mambo yenye nguvu.
unawaweka chini yangu wanaoinuka kinyume changu
"ulinisaidia kuwashinda walioshindana nami"
migongo ya shingo za adui zangu
Maana yake yaweza kuwa 1) Daudi kuona migogo ya adui zake walipokimbia au 2) Daudi kuwaka mguu wake nyuma ya shingo ya adui zake baada ya kuwashinda.
niliwaangamiza kabisa
"Niliwaangazi kabisa"
2 Samuel 22:42-43
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
Walilia
"adui zangu walilia"
walimlilia Yahwe, lakini hakuwajibu
Muda wa hukumu ya Yahwe juu yao ilikuwa juu yao.
kama vumbi juu ya ardhi... kama matope mitaani
Inamaanisha Daudi aliwaangamiza adui zake kabisa. Vifungu hivi viwili "kama vumbi juu ya ardhi" na "kama tope mitaani" vina maana moja na vimetumika kwa msisitizo.
2 Samuel 22:44-46
Maelezo ya Jumla:
Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea
kutoka katika mashutumu ya watu wangu
Hii inarejerea miongoni mwa Waisraeli walioasi dhidi ya Mfalme Daudi.
Umeniweka kama kichwa cha mataifa.
"Uliniweka kama mtawala juu ya mataifa." Hapa "mataifa" yamaanisha nchi nyingine tofauti na Israeli.
Watu ambao sikuwajua
"Wageni"
kutoka katika mashutumu ya watu wangu
Yaweza kuwa "wageni walinipigia magoti"
2 Samuel 22:47-49
Mwamba wangu atukuzwe. Mungu na ainuliwe
Mistari hii ina maana inayofanana na imetumika kwa msisitizo.
mwamba wangu... mwamba
Daudi anamlinganisha Yahwe na mwamba kusisitiza uwezo wake wa kuwalinda watu wake.
awawekaye watu chini yangu.
Yeye awawekaye watu chini ya utawala wangu.
Uniweka huru mbali na adui zangu
"Uliniokoa na adui zangu na kunipa heshima"
kutoka kwa watu wenye ghasia
"kutoka kwao watakao kunidhuru"
2 Samuel 22:50-51
Maelezo ya Ujumla
Daudi anahitimisha wimbo wake kwa Yahwe
kwa jina lako
Hapa neno "jina" inaonesha heshima ya Yahwe.
na uonesha uaminifu wake wa kiagano kwa mtiwa mafuta wake
Daudi anaweza kuwa anarejerea ahadi alizosifanya Yahwe katika 7:8
2 Samuel 23
2 Samuel 23:1-2
Basi
Hii inaonesha mwanzo wa sehemu nyingine ya kitabu
haya ni maneno ya mwisho
Hii inaonesha atakachokisema Daudi katika 23:1.
mtu aliyeheshimiwa sana, aliyetiwa mafuta na Mungu wa Yakobo
Hii yaweza kumaanisha: "Mtu ambaye Mungu wa Yakobo alimweshimu na kumtia mafuta"
aliyetiwa mafuta na Mungu wa Yakobo
Kutiwa mafuta kulifanywa kwa kumimina mafuta juu ya kichwa cha mtu katia kuchagua ambaye angemtumikia Mungu kama mfalme au kuhani.
Mzaburi
Huyu ni mtu aandikaye zaburi au nyimbo.
kwangu
kwa Daudi
na neno lake lilikuwa katika ulimi wangu
"juu ya ulimi wangu" ni usemi unaomaanisha Daudi.
2 Samuel 23:3-4
Maelezo ya Ujumla
Hii inaendeleza maneno ya mwisho ya Daudi.
Mungu wa Israeli alinena, Mwamba wa Israeli... nami
Hapa "Mungu wa Israeli" na "Mwamba wa Israeli" ni yuleyule. Vingungu vyote viwili vinazungumzia jambo moja la msingi. Daudi anamlinganisha Mungu na mwamba kusisitiza uwezo wake wa kulinda watu.
Atawalaye kwa haki juu yangu, atawalaye katika hofu ya Mungu
Mistari miwili hii inasema kwamba mfalme atamweshimu Mungu na kufanya Mungu anachotaka.
kwa hofu ya Mungu
"kumweshimu Mungu"
Atakuwa kama mwanga wa asubuhi...nuru ya jua baada ya mvua
Hapa Mungu anamlinganisha mfalme na nuru ya asubuhi na nuru ya jua baada ya mvua. Zote ni njia za kusema mfalme huyu angekuwa wa kupendwa na Mungu na baraka kwa watu. Vifungu hivi viwili vina maana inayofanana na vimetumika kwa msisitizo.
2 Samuel 23:5
Maelezo ya Ujumla
Hii inaendeleza maneno ya mwisho ya Daudi
Hakika, je familia yangu haiko hivi mbele za Mungu?
Hapa Daudi anakubaliana ya Mungu.
Je yeye hajafanya... njia?
Daudi anakubari kwamba Mungu amefanya agano naye.
taratibu na hakika
Hii inamaanisha agano la Mungu limeratibiwa vizuri na halitabadilika hivyo familia ya Daudi inaweza kuliamini.
Je yeye haongezi wokovu wangu... tamaa?
Daudi anaaamini kwamba Mungu atamsaidia daima na kumfanya afanikiwe.
2 Samuel 23:6-7
Maelezo ya Ujumla
Hii inahitimisha maneno ya mwisho ya Daudi.
Lakini yasiyofaa yote yatakuwa kama miiba na kutupwa mbali
Hapa waovu wanalinganishwa na miba isiyofaa.
kwa maana haiwezekani kukusanywa kwa mikono
"Kwa maana hakuna awezaye kuichukua kwa mikono yake bila kumwumiza"
Ni lazima yachomwe mahali yalipo
"Yalipo" ndipo yanapochomewa." Hii inamaanisha kwamba Mungu atawaharibu waovu.
2 Samuel 23:8
Yeshbaali
Hili ni jina la mwanamme. Matoleo mengine yanasomeka Yoshebu Bashebethi, Jashobeamu, Ishbaali, au Ishboshethi kwa hiyo nakala mbalimbali za kale zina tofauti hizi.
Mhakimoni
Hili ni jina la kundi la watu.
Mia nane
"800"
2 Samuel 23:9-10
Maelezo ya Ujumla
Hii inaendeleza orodha ya mashujaa wa Daudi.
Jeshi likarudi baada ya Eleaza
Hii inamaana jeshi lilirudi baada ya Eleaza kurudi kutoka vitani. Yaweza pia kuwa "Jeshi la Israeli lilirudi kwenye uwanja wa vita baada ya Eleaza kuwa ameshinda vita"
kwa ajili tu ya kuteka nyara miili
"Kuchua pekee walivyotaka katika maiti za maadui"
2 Samuel 23:11-12
Maelezo ya Ujumla
Hii inaendeleza orodha ya mashujaa wa Daudi
shamba la dengu
"katika shamba ambalo mtu alikuwa amepanda zao la dengu"
dengu
mbegu ya bapa, inaliwa kama maharage
jeshi lilikimbia
"jeshi la Waisraeli lilikimbia"
2 Samuel 23:13-14
Watatu kati ya thelathini
Hawa siyo askari waliotajwa katika 23:8
thelathini
"30" au "Askari thelathini wa Israeli waliokuwa mashujaa zaidi"
Pango la Adulamu
"Pango lililopo karibu na mji wa Adulamu." "Adulamu ipo karibu na Bethlehemu.
Bondel la Mrefai
Mrefai ni mtu aliyekuwa mmiliki wa bonde.
katika ngome yake
"katika eneo lake la ulinzi"
Wafilisiti wlikuwa wamejieneza katika Bethlehemu
"Baadhi ya askari wa Wafilisiti walikuwa wakimiliki kijiji cha Bethlehemu"
2 Samuel 23:15-17
kupita kati ya jeshi
"walipigania njia yao kupitia jeshi la adui"
Je ninywe damu ya watu waliohatilisha maisha yao?
Daudi analinganisha maji na damu kwa sababu wale watu walihatarisha maisha yao ili kuyalete kwake. Anatumia swali kusisitiza hili.
2 Samuel 23:18-19
Abishai ... Seruya.
Haya ni majina ya wanaume
kapteni juu ya watatu
Inamaana Abishai alikuwa kiongozi wa wale watatu walikwenda kumchukulia Daudi maji.
watu mia tatu
"watu 300"
alitajwa pamoja na wale askari watatu.
"Watu walimtaja walipozungumzia wale mashujaa zaidi watatu"
hakuwa maarufu zaidi ya wale watatu?
Swali linasisitiza jinsi alivyokuwa maarufu.
wale mashujaa watatu
Hii inarejerea kwa Yoshebu Bashebethi, Eleaza na Shama. Abishai hakuwa maarufu kama hawa askari hawa.
2 Samuel 23:20-21
Kabseeli
Hili ni jina la mji.
Yehoiyada
Hili ni jina la mwanamme.
Arieli
Hili ni jina la mwanamme.
2 Samuel 23:22-23
alifanya matendo haya
"alifanya matendo haya makuu"
naye alitajwa kati ya mashujaa watatu
"watu walimsifu kama wale mashujaa watatu"
Alikuwa na heshima kuliko mashujaa thelathini kwa ujumla wao, lakini hakuwa na heshima kama wale mashujaa watatu
"Alikuwa maarufu zaidi ya askari wale 30 isopokuwa wale watatu bora zaidi"
wale mashujaa zaidi watatu
Hii inamaanisha Yoshebu Bashebethi, Eleaza, na Shama.
mlinzi wake
Kundi la askari waliowajibika kumlinda Daudi
2 Samuel 23:24-28
Maelezo ya Ujumla
Hii ni orodha ya mashujaa wa Daudi
Thelathini
"Askari 30 maarufu zaidi"
2 Samuel 23:29-32
Maelezo ya Ujumla
Hii inaendeleza orodha ya mashujaa wa Daudi
2 Samuel 23:33-36
Maelezo ya Ujumla
Hii inaendeleza orodha ya mashujaa wa Daudi
2 Samuel 23:37-39
Maelezo ya Ujumla
Hii inahitimisha orodha ya mashujaa wa Daudi
Jumla yao thelathini na saba
jumla yao saba** - "kulikuwa na 37 jumla yao"
2 Samuel 24
2 Samuel 24:1-2
Hasira ya Yahwe iliwaka juu ya Israeli
Neno "kuwaka" linamaanisha kuwasha moto. Hasira ya Yahwe inalinganishwa hapa na kule kuwasha moto
alimchochea Daudi kinyume chao
"alimfanya Daudi kuwapinga"
Nenda, wahesabu Israeli na Yuda
Katika sheria ya Musa, Mungu alizuia wafalme wa Israeli kuhesabu wapiganaji.
Dani hadi Beersheba
Kifungu kinatumia majina mawili, Dani kaskazini ya mbali na Bersheba, kusini ya mbali, kuwakilisha nchi nzima.
Hesabu watu wote... wanaofaa kwa vita
Hii inamaanisha wanaume wote isipokuwa walio watoto, wazee, au wasioweza kupigana kwa sababu ya udahifu wa miili yaoo.
2 Samuel 24:3-4
wazidishe... mara mia zaidi
Inamaanisha "kuzalisha watu mia moja kwa kila mtu aliyekuwepo wakati huo."
neno la mfalme lilikuwa la mwisho dhidi ya Yoabu
Yoabu na majemedari wengine wa Mfalme Daudi hawakufanikiwa kumshawishi Daudi kutochukua sensa.
neno la mfalme
Kifungu kinawakilisha agizo la mfalme juu yao.
2 Samuel 24:5-7
Walivuka
"Yoabu na majemedari wengine wa jeshi walivuka"
Aroeri
Huu ulikuwa mji katika ukingo wa Mto Arnoni.
Yazeri
Huu ni mji huko Gadi.
Tahitimu Hodshi
Huu waweza kuwa mji wa Kadehsi katika nchi ya Wahiti.
2 Samuel 24:8-9
walikuwa wameondoka
"Yoabu na majemedari walikuwa wameondoka"
miezi minane na siku ishirini
"miezi 9 na siku 20"
Ndipo Yoabu alipotoa taarifa ya hesabu kamili kwa mfalme kuhusu watu wawezao kupigana vita
Ndipo Yoabu alipomwambia mfalme jumla ya watu waliotayari kwa vita"
Katika Israeli
Hii inahusu makabila ya kaskazini mwa Israeli.
800,000... 500,000
"mia nane elfu... mia tano elfu"
wafutao upanga
Hii inamaanisha watu waliokuwa tiyari kwa vita jeshini.
wa Yuda
Hii inamaanisha kabila ya Yuda.
2 Samuel 24:10
moyo wa Daudi ukamchoma
"moyo" hapa unamaanisha hisia na dhamira ya Daudi.
Sasa, Yahwe, iondoe hatia ya mtumishi wako
Daudi anajitaja kama "mtumishi wako." Hii ni njia ya upole ya kuongea na mwenye mamlaka.
2 Samuel 24:11-12
neno la Yahwe likaja
Inamaanisha Yahwe aliongea. "Yahwe aliongea ujumbe wake."
neno la Yahwe
Hapa "neno" linawakilisha ujumbe wa Yahwe.
mwonaji wa Daudi
Hii inamaanisha Gadi alikuwa nabii wa ikulu.
2 Samuel 24:13-14
nipo katika shida kubwa
"nipo katika shida ya kutisha"
Haya na tuanguke katika mikono ya Yahwe kuliko kuanguka katika mikono ya mwanadamu
Hapa "mikono" inamaanisha mamlaka au umilki.
2 Samuel 24:15-16
muda uliopangwa
Huu ni muda Mungu aliokuwa amepanga kusitisha tauni.
elfu sabini
"70,000"
kutoka Dani hadi Beersheba
Hii inamaanisha taifa lote
6Malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili kuuharibu
"mkono" unawakilisha nguvu ya malaika.
Yahwe akabadilisha nia yake kuhusu madhara
Inamaanisha Yahwe alisitisha baya alilokuwa amemruhusu malaika kufanya.
Basi rudisha mkono wako
"mkono" unamaanisha nguvu ya malaika.
Arauna
Hili ni jina la mwanamme
sakafu ya kupulia
Hii ilikuwa ni sehemu ngumu, iliyo na ubapa mahali nafaka zilikuwa zinapulwa.
2 Samuel 24:17
Nimetenda dhambi, na nimetenda kwa ukaidi
Hivi vifungu vinamaanisha kitu kimoja na vimetumika kwa msisitizo.
Lakini kondoo hawa, wamefanya nini?
Daudi anatumia swali na analinganisha watu na kondoo kusisitiza kwamba hawajakosa.
Tafadhari mkono wako uniadhibu mimi
Hapa "mkono" unamaanisha nguvu.
2 Samuel 24:18-20
kumsujudia mfalme uso wake mpaka juu ya ardhi
Alikuwa akionesha heshima kubwa kwa mfalme.
2 Samuel 24:21-23
ili tauni iondolewe miongoni mwa watu
"Ili kwamba Yahwe aiondoe tauni kutoka kwa watu"
Ulifanyie lolote lolote lililojema machoni pako
Kifungu "machoni pako" kinawakilisha wazo au oni la Daudi.
miganda ya kupuria
fito zilizotumika kupuria ngano.
2 Samuel 24:24-25
sitatoa chochote... nisichokigharimia
"Nitatoa tu kile nilichokilipia"
shekeli hamsini
"shekeli 50." Shekeli ni sawa na gramu 11.
badala ya nchi
Neno "nchi" linawakilisha watu wa Israeli.