Lamentations
Lamentations 1
Lamentations 1:1-2
kama mjane
Haya maneno yana fananisha Yerusalemu na mwanamke asiye kuwa na ulinzi sababu mume wake amefariki.
Alikuwa mtoto wa mfalme miongoni mwa mataifa
"Matifa mengine yali heshimu Yerusalemu kama yalivyo muheshimu binti wa mfalme"
amelazimishwa utumwani
"amefanywa kuwa mtumwa"
Analia na kuomboleza
Mwanandishi anaelezea Yerusalemu kama mwanadamu mwenye hisia. Mji pia una wakilisha wakazi wake. "Wao wanao ishi humo wanalia na kuomboleza."
lia na kuomboleza
Neno "kuomboleza" lina husu sauti mtu anayo toa anapo "lia" kwa nguvu.
Lamentations 1:3
Yuda ameenda matekani
"watu wa Yuda wamepelekwa nchi ya kigeni"
hapati pumziko lolote.
"haoni pumziko" "ana wasiwasi tu"
Wanao wakimbiza wamewapata
"Wote walio kuwa wana mkimbiza wamefanikiwa kumkamata"
katika upweke wake
"alipo kuwa ana uwitaji"
Lamentations 1:4-5
Barabara za Sayuni zinaomboleza
Mwandishi anaelezea barabara zinazo elekea Sayuni zinaomboleza kama ni mwanadamu
sherehe iliyo andaliwa
"sherehe Mungu aliyo waambia wa shereheke"
Malango yake ... Makuhani wake
Neno "yake" na "wake" yaelezea Sayuni.
katika ugumu
"ana uchungu" au "ana kosa matumaini"
Maadui wake wamekuwa bwana zake
"Maadui wa Sayuni wana mtawala"
maadui wake wana fanikiwa
"maadui wake wanakuwa matajiri"
Yahweh
Hili ni jina la Mungu alilo lidhihirisha kwa watu wake katika Agano la Kale.
Lamentations 1:6
Uzuri umemwacha binti wa Sayuni
"Kila kitu kilicho kuwa kizuri cha binti wa Sayuni kimeharibiwa"
binti wa Sayuni
Hili ni jina
kama ayala ambaye haoni malisho
Watoto wa mfalme wanaliganishwa na swala asiye kuwa na kitu cha kula.
ayala
Ayale ni mnyama wa umbo la kati, anaye kula majani ambaye mara nyingi uwindwa na wanadamu. Pia ni mnyama mzuri wa kumtazama.
bila uwezo kwa
"lakini sio imara sana kukimbia kutoka"
wanao wakimbiza
"mtu anaye wakimbiza"
Lamentations 1:7
Katika siku za mateso yake na kutokuwa na nyumba
"Wakati Yerusalemu inapo kuwa inateswa na haina makazi"
hazina
"utajiri"
awali
"wakati uliyo pita" au "kabla ili janga halija tokea"
Wakati watu wake walipo angukia mikononi mwa adui
Hapa neno "mikononi" la husu jeshi la adui.
hakuna aliye msaidia
"hakuna msaidizi aliye kuwa naye"
waliwaona na kucheka maangamizo yake
Hii ina maana kuwa walikuwa na furaha na wakadhihaki Yerusalemu ilipo haribiwa.
maangamizo yake
"kwasababu aliharibiwa"
Lamentations 1:8-9
Yerusalemu ili tenda dhambi sana
Hii yaelezea Yerusalemu kama mtu aliye tenda dhambi, pia ina wakilisha wakazi wa Yerusalemu.
uchi wake
Yersualemu inaelezea kama mwanamke ambaye sehemu zake za siri zimefunuliwa kwa kila mtu amuaibishe.
Anguko lake lilikuwa baya
"Kuanguka kwake kulishangaza" au "hao walioyo muona
Angalia mateso yangu, Yahweh
Maana zinazo wezekana 1) mwandishi wa Maombolezo anaongea moja kwa moja na Yahweh au 2) Yerusalemu inaelezewa kuongea na Yahweh kama mtu.
Angalia
"kuwa makini"
Lamentations 1:10
ameeka mkono wake kwenye
"amechukuwa sehemu ya" au "ameiba"
hazina
utajiri
uliamuru
Hii ina maana kuwa mwandishi au mji bado unaongea, baada ya kuanza 1:8
Lamentations 1:11-12
hazina
"utajiri"
kurejesha uhai wao
"kuokoa uhai wao" au "kurejesha uweza wao"
Tazama, Yahweh, ni kumbuke mimi
Hapa Yerusalemu anaanza kuongea moja kwa moja na Yahweh.
Sio kitu kwako, wote mnao pita?
Hili ni shitaka la watu wanao pita Yerusalemu na hawaijali.
Sio kitu kwako
Hapa Yerusalemu anaendelea kuongea, lakini sasa kwa watu wanaopita.
Angalia na uone kama kuna mtu mwenye uzuni kama uzuni ninao teswa nao
Hii maana hapa inaelezea kuwa hakuna mtu aliye teseka kiasi hichi.
Angalia na uone
Haya maneno yana maana moja. Pamoja yana mkaribisha msomaji kuelewa kwa kuona kwamba hakuna mtu aliye teseka sana.
uzuni ninao teswa nao
"uzuni Yahweh anayo ni tesa nayo"
siku ya hasira yake kali
"Alipo kuwa na hasira kali"
Lamentations 1:13-14
alipo tuma moto kwenye mifupa yangu na umenishinda
"ametuma adhabu kali ndani yangu, na imeniharibu" au "ametuma adhabu mbaya katikati ya Yerusalemu, na imeharibu mji"
amenikabidhi mikononi mwao
"acha maadui zangu wanishinde"
Lamentations 1:15
wanaume wangu hodari walio niokoa
Katika hichi kipengele Yerusalemu bado yaelezewa kama mwanamke anaye jielezea.
wanaume hodari
"wanajeshi wenye nguvu"
kusanyiko
Hapa adui anaye shambulia Yerusalemu anaelezewa kama ni mkutano wa watu waliyo kuja pamoja ili kushitaki na kuhukumu.
wanaume imara
wanaume katika wakati kipindi chao cha nguvu
Bwana amewakanyaga ... chombo cha kusagia mvinyo
Hapa hukumu ya Mungu yaelezewa kama Yerusalemu ni mizabibu aliyo ikanyaga ili kukamua jwisi.
binti bikra wa Yuda
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, mbapo hapa yaelezewa kama mwanamke. Neno "bikra" la hashiria kuwa mwanamke ni msafi.
Lamentations 1:16-17
ninalia
Hii bado ni Yerusalemu anaongea kama ni mwanamke, sasa ana hisia za uzuni.
Sayuni ametandaza mikono yake
Sayuni ni kama mtu anaye inua mikono yake kuomba msaada. Hapa Yerusalemu hajizungumzii yeye tena, lakini mwandishi anaelezea Yerusalemu.
hao karibu na Yakob
"watu karibu na Yakobo" au "mataifa yanayo zunguka Yakobo"
wawemaadui wake
Hapa neno "wake" la husu Yakobo.
Lamentations 1:18-19
nimeas
Hapa Yerusalemu anaanza kuzungumza tena, kama alikuwa mwanamke.
muone uzuni wangu
"ona jinsi gani nilivyo na majonzi"
Mabikra wangu na wanaume wangu hodari
"watu wangu wengi"
wanaume hodari
Ona jinsi ulivyo tafsiri 1:15
walikuwa na hila kwangu
"wali ni saliti"
kurejesha uhai wao
"kuokoa maisha yao" au "kurejesha uweza wao"
Lamentations 1:20
kwa kuwa nipo kwenye ugumu
Yerusalemu anaendelea kujizungumzia kama ni mwanamke, lakini sasa anazungumza moja kwa moja na Yahweh.
tumbo langu lina nguruma
Neno "nguruma" la maanisha kuangaika kwa nguvu, kawaida kwa mzunguko. Hii haimanishi kiuhalisia, lakini ndivyo linavyo jisikia.
moyo wangu umetibuka ndani yangu
"moyo wangu umevunjika" au "nina majonzi sana"
upanga umemliza
Upanga una husu adui, na "chukuwa" yamanisha "kuua" "adui anaua"
ndani ya nyumba kuna mauti tu
Maana inayo wezekana ni 1) katika nyumba, kila mtu ana kufa au 2) nyumba ni kama kaburi.
Lamentations 1:21-22
Wamesikia sononeko langu
Yerusalemu anaendelea kuongea kama mtu.
umenifanyia hivi
Hapa neno "wewe" la muhusu Yahweh.
Lamentations 2
Lamentations 2:1-2
Maelezo ya Jumla
Shairi lipya la anza. Mwandishi wa Maombolezo anatumia njia nyingi tofauti kuelezea kwamba watu wa Israeli wamepoteza upendeleo wa Mungu.
wingu la hasira yake
Maana inayo wezekana ni 1) Mungu anatishia kuwadhuru watu wa Yerusalemu au 2) Mungu tayari amesha wadhuru
binti wa Sayuni ... binti wa Yuda
Haya ni majina ya kishairi ya Yerusalemu, ambayo hapa yanazungumziwa kama ni mwanamke.
Ametupa utukufu wa Israeli chini kutoka mbinguni hadi duniani
"Yerusalemu amepoteza upendeleo wote na Bwana"
Hajakumba
"hajatilia maanani"
stuli yake
Hapa "stuli" ya wakilisha sehemu ambayo Mungu anaonyesha ukarimu wa kuwepo. Maana kadhaa hapa ni 1) "mji wake wa upendo Yerusalemu" au 2) "agano lake na Israeli."
siku ya hasira yake
kipindi cha wakati kwa ujumla, sio siku ya masaa 24
amemeza
"kaharibu kabisa" kama vile mnyama asivyo bakiza kitu anapo meza chakula
miji imara ya binti wa Yuda
Maana zinazo wezekana ni 1) miji yote imaraYuda nzima, au 2) kuta imara za Yerusalemu.
Lamentations 2:3-4
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anaendelea kutumia mifano kuelezea upizani wa Mungu kwa Yuda.
amekata kila pembe ya Israeli
Hapa "pembe" (ambalo ni, pembe la mnyama) lina maana ya "uweza"
Ameurudisha mkono wake
"ameacha kutulinda na maadui zetu"
amepindisha upinde wake kuelekea kwetu
Mwanajeshi alipaswa kupindisha upinde wake ili kuupiga.
hema la binti wa Sayuni
"nyumba za watu Yerusalemu"
binti wa Sayuni
Kuna jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo linazungumziwa hapa kama mwanamke.
Amemwaga gadhabu yake kama moto
"ameonyesha jinsi alivyo na hasira kwa kuwa haribu kila kitu kama mtu anavyo washa moto"
Lamentations 2:5-6
Amemeza
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:1
Ameongeza kilio na maombolezo
"Amesababisha zaidi na zaidi watu kulia na kuomboleza"
binti wa Yuda
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo hapa la zungumziwa hapa kama mwanamke.
kajumba cha bustani
jengo dogo la kuhifadhia vifaa vya au kumuhifadhia mtu anaye tunza bustani
amesababisha kukusanyika na Sabato kusahaulika Sayuni
"amesababisha watu Sayuni kusahau kukusanyika na Sabato"
Lamentations 2:7
Ametoa ... mikononi mwa adui
"Ameugeuza kwa ... kwa adui"
Wamepaza sauti nyumbani mwa Yahweh, kama siku ya sherehe
Huu ni mfano wa kushangaza katika ya furaha, kelele za sherehe za Israeli na sauti za ushindi za wa Babilonia.
Lamentations 2:8-9
binti wa Sayuni
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo la zungumziwa hapa kama mwanamke.
Amenyoosha kamba ya kipimo
"Amepima urefu wa ukuta" hivyo anajua kiasi cha kuharibu
hajauzuia mkono wake kutoharibu
"Ameharibu kwa kutumia nguvu zake zote"
hajauzuia mkono wake
"ameuweka mkono wake kwake"
Amefanya minara na ukuta kuomboleza; pamoja vilipotea
"Kwasababu ameharibu minara na kuta, inaonekana kama watu wanao omboleza na kupoteza nguvu"
Lamentations 2:10
binti wa Sayuni
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo la zungumziwa hapa kama mwanamke.
keti chini
kuonyesha walikuwa wana omboleza
Lamentations 2:11-12
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anatoka kuelezea Yerusalemu na kueleza mapito yake.
Macho yangu yamekaukiwa machozi yake
"Nimelia hadi siwezi kulia tena"
sehemu zangu za ndani zimemwagika chini
"sehemu yangu ya ndani ipo katika uzuni"
kwasababu ya uharibifu wa binti wa watu wangu
"binti wa watu wangu" ni jina la kishairi la Yerusalemu,ambalo hapa la zungumziwa kama mwanamke.
Mbegu ziko wapi na mvinyo?
Maneno "mbegu ba mvinyo" ni namna ya kusema "chakula na kinywaji."
Lamentations 2:13-14
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anaanza kwa kusema na Yerusalemu.
Nini naeza kusema ... Yerusalemu?
"Hakuna nacho weza kusema ... Yerusalemu."
binti wa Yerusalemu
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo hapa la zungumziwa kama ni mwanamke.
Naweza kufananisha na nini ... Sayuni?
"Hakuna nachoweza kukufananisha nacho ... Sayuni."
Nani anaweza kukuponya?
"Hakuna anaye weza kukuponya"
Lamentations 2:15-16
wana piga makofi
namna ambazo watu wana wa tania wengine na kuwa tusi
binti wa Yerusalemu
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo hapa la zungumziwa kama ni mwanamke.
Huu ndio mji walio uita 'Ukamilifu wa uzuri,' ''?
Hili ni swali linalo tumika kueleza kejeli." Huu mji walio uwita 'Ukamilifu wa uzuri,' 'Furaha ya Dunia Yote' sio mzuri wala wafuraha tena!"
Tumemmeza yeye
"Tumeharibu Yerusalemu kabisa" kama mnyama anavyo meza chakula
Lamentations 2:17
menyanyua pembe za maadui zako
Hapa "pembe" (kwamba ni, pembe ya mnyama) mara nyingi yaelezea uweza.
Lamentations 2:18-19
Mioyo yao ikamlilia
Maana inayo wezekana ni 1) "Watu wa Yerusalemu wamepiga kelele kutoka kwenye vilindi vyao" au 2) mwandishi anataka kuta zipaze sauti kwa Yahweh.
kuta za binti wa Sayuni ... kila mtaa
Mwandishi anaongea na kuta za Yerusalemu. Anataka watu wa Yerusalemu kufanya anacho ambia kuta zifanye.
binti wa Sayuni
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo hapa la zungumziwa kama ni mwanamke.
Fanya machozi yako kutiririka chini kama mto
"kulia machozi mengi"
usiku na mchana
"wakati wote"
Usijipatie hauweni
"Usijiruhusu upumzike"
mwanzo usiku wa manane
"mara nyingi wakati wa usiku" hiyo ni kwamba, mlinzi anapo kuja kulinda
Nyoosha juu mikono yako
Hili ni tendo linalo fanywa wakati wakuomba.
kwenye njia ya kila mtaa
"pale njia zinapo kutana" au "kwa barabarani"
Lamentations 2:20
Wanawake wale tunda la uzazi wao ... wajali?
"Wanawake wasiwale watoto wao ... wajali?
tunda la uzazi wao
"watoto walio bado wadogo"
Lamentations 2:21-22
wadogo kwa wakubwa
wadhaifu na watu wazima wenye nguvu
hofu yangu
"washambuliaji niliyo kuwa nawaogopa"
kama ungewaita watu katika siku ya maakuli
"kama wange kuwa wanakuja kwenye sherehe"
Lamentations 3
Lamentations 3:1-4
Sentesi Unganishi
Shairi lipya laanza
chini ya gongo la hasira ya Yahweh
Ngongo ni fimbo watu waliyo tumia kupiga na kuadhibu mtu.
kutembea kwenye giza kuliko kwenye nuru
Hii ina maanisha kuishi kwenye kuchanganyikiwa pamoja na giza.
amenigeuzia mkono wake dhidi yangu
"amekuwa adui wangu" au "anatumia nguvu yake kunihukumu"
Lamentations 3:5-8
Amejenga vifusi vya udogo dhidi yangu
Vifusi vya udogo vina muwezesha jeshi shambulizi kuvuka kuta na kuvamia mji.
kunizingira na uchungu na ugumu
"kanizunguka na vitu vilivyo na maumivu na vigumu kuvumilia"
anazima maombi yangu
"anakataa kusikiliza maombi yangu"
Lamentations 3:9-11
Ameziba njia yangu
"alinizuia kuto mtoroka"
mawe ya kuchonga
mawe mtu aliyo yakata katika maumbo yakulingana yanayo ingiliana na kuimarisha ukuta
mawe; amefanya njia yangu mbaya
Maana inayo wezekana ni 1) "mawe, hivyo siwezi kwenda sehemu" au 2) "mawe; kila njia ninayo ichukuwa haiende mahali"
amegeuza pembeni njia zangu
Maana inayo wezekana ni 1) "amenivuta nje ya njia" au 2) "kasababisha njia yangu kwenda kumelekeo mbaya"
Lamentations 3:12-15
Amepindisha upinde wake
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:3
maini
viungo vya tumbo linalo peleka mkojo kwenye kibofu.
kichekesho kwa watu wangu wote
Maana inayo wezekana ni 1) "mtu ambaye Israeli yote yamcheka" au 2) "mtu ambaye watu wote wa dunia wanamcheka"
Amenijaza kwa uchungu
"Ni kama kanilazimisha nile mimea michungu"
maji machungu
jwisi chungu kutoka kwenye majani na maua ya mimea
Lamentations 3:16-18
Alivunja ... amenisukuma
ni maneno mawili Mungu anayo mnyenyekesha mwandishi
Nafsi yangu imenyimwa amani
Mwandishi pitii tena furaha au starehe kwenye maisha yake.
Ustahimilivu wangu umeangamia
"Tafsiri zingine zinasema, "Utukufu wangu umeangamia," lakini hapa "utukufu" una maana ya uvumilivu au uweza.
Lamentations 3:19-21
nimeinama ndani yangu
Haya maelezo yana hashiria msongamano wa mawazo na kukosa tumaini.
Lakini ni vuta hili akilini mwangu
Mwandishi anataka kuwambia wasomaji ni anatumainia.
Lamentations 3:22-24
uaminifu wako
Mwandishi anazungumza na Yahweh.
Yahweh ni urithi wangu
"Kwasababu Yahweh yupo nami, nina kila kitu ninacho kiitaji"
Lamentations 3:25-29
wanao msubiri
Maana inayo wezekana ni 1) "wote wanao mtumainia" (UDB) au 2) "yeye anaye msubiri kwa uvumilivu kutenda."
anaye mtafuta
"mtu anaye mtafuta"
kubeba nira
"kuteseka"
imewekwa juu yake
"nira imewekwa juu yake"
aeke mdomo wake kwenye vumbi
"kuinama chini na mdomo kwenye ardhi"
Lamentations 3:30-33
Maelezo ya Jumla
Mwandishi anaongea juu ya yeye anaye msubiri Yahweh 3:25
Acha atoa shavu lake kwa yeye anaye mpiga
"Acha aruhusu watu wampige"
japo anatia
"japo Yahweh anasababisha"
watoto wa mwanadamu
"wanadamu" au "watu"
Lamentations 3:34-36
Kukanyaga chini ya mguu
"Kumtumia vibaya" au "Kumuua"
Lamentations 3:37-39
Sio kutoka mdomoni mwa Aliye Juu majanga na mazuri yanakuja?
"Mungu anapunguza mahafa au mafanikio kwa kila mtu"
Lamentations 3:40-43
Na tunyanyue mioyo yetu na mikono yetu
Ili kuwa ni utamaduni wa Waisraeli kunyoosha mikono yao wakiomba kwa Mungu.
Tumekosea na kuasi
Maneno "kosea" na "kuasi" yanashiriki maana moja. Pamoja yana hashiria kuwa makosa ni sawa na kuasi dhidi ya Yahweh.
Umejifunika na hasira
Hapa hasira inazungumziwa kama ni vazi Mungu alilo livaa. Kiebrania mara nyingi cha ongelea hisia kama vile ni nguo.
Lamentations 3:44-47
Maelezo ya Jumla
Maombi yaliyo anza 3:40 yanaendelea.
Umejifunika na wingu ili kwamba kusiwe na ombi linaloweza kupita
"Unatumia mawingu kama ngao kuzuia maombi yetu"
Umetufanya kama uchafu na taka miongoni mwa mataifa
Maneno "uchafu" na "tak" yote ya husu vitu watu walivyo vikataa na kuvitupa.
miongoni mwa mataifa
Maana inayo wezekana ni 1) mataifa mengine yana onekana kama taka taka (UDB), au 2) kwamba Yahweh ametupa kama uchafu miongoni mwa mataifa.
maafa na uharibifu
Haya maneno mawili yana shiriki maana moja na ya husu uharibifu wa Yerusalemu.
Lamentations 3:48-50
Macho yangu yanatiririka na miferiji ya machozi
"Machozi yana tiririka kutoka machoni mwangu kama maji yanavyo tiririka mtoni" kwasababu nalia
kwasababu ya watu wangu
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:11
Lamentations 3:51-54
Macho yangu yana ni sababishia uzuni
"Ninacho kiona kina ni sababisha maumivu"
mabinti wa mji wangu
Maana inayo wezekana ni 1) wanawake wa Yerusalemu au 2) wakazi wote wa Yerusalemu.
Wamenitupa kwenye shimo
"Wameniua kwa kunizamisha kwenye kisima"
wakanitupia jiwe
Maana inayo wezekana ni 1) "wametupa mawe" au 2) "wamefunika kisima kwa jiwe."
Nimekatwa mbali
"Nimeuawa" au "Nimezama"
Lamentations 3:55-57
Nililiita jna lako
"Nilikuita kwa ajili ya msaada"
kutoka kina cha shimo
Maana inayo wezekana ni 1) "kutoka kisima kirefu" au 2) "kutoka kaburini"
Ulisikia sauti yangu
"Ulisikia nilicho kisema"
Usifunge sikio lako
"Usikatae kunisikia"
Lamentations 3:58-61
ulitetea kesi yangu
Hii yatoa picha ya mahakama, ambapo mwandishi anashitakiwa. Katika hii picha, Mungu anamtetea, kama wakili anavyo mtetea mteja wake.
hukumu kesi yangu
Hapa Mungu haendelei kuonekana kwenye picha kama wakili, lakini kama mtoa hukumu.
matusi yao, mipango yao yote dhidi yangu
Hii mistari miwili ina shiriki maana moja na imewekwa pamoja kwa mkazo.
Umesikia dhihaka yao
"Umesikia wakinikejeli"
Lamentations 3:62-63
Midomo ya hao wanao inuka kinyume changu
"Maneno hao walio inuka dhidi yangu wamenena"
hao wanao inuka kinyume changu
"hao wanao nishambulia"
jinsi wanavyo keti na kuinuka
"kila wanacho fanya"
Lamentations 3:64-66
Walipize, Yahweh, kwa kadiri ya waliyo fanya
"Wamenifanya ni teseke, Yahweh, hivyo tafadhali wafanye wateseka sasa"
taacha mioyo yao bila lawama
"wasabishe wa sijisikie aibu"
nchini ya mbingu
"popote walipo duniani"
Lamentations 4
Lamentations 4:1-2
Maelezo ya Jumla
Shairi lipya la anza.
Mawe matakatifu
mawe yaliyo unda hekalu
katika kila njia ya mtaa
Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:18
Wana wa Sayuni
Maana inayo wezekana ni 1) Wanaume wadogo wa Yerusalemu au 2) watu wote wa Yerusalemu.
lakini sasa hawana thamani zaidi ya majagi ya udogo, kazi ya mikono ya mfinyazi!
"watu wali wachukulia kuwa si kitu kama vishungu vya udogo wafinyazi wanavyo tengeneza!"
Lamentations 4:3
mbwa wa mitaani wanatoa maziwa yao kuwanyonyesha watoto wao
Hii ina maana kuwa mbwa wa mitaani wa kike kwa uhuru wanaruhusu watoto wao kunyonya.
mbwa wa mitaani
mbwa wa kali, wa katili wa wanyama wa chafu
binti wa watu wangu
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo hapa la zungumziwa kama ni mwanamke. Ona jinsi ulivyo tafsiri 2:11
Lamentations 4:4-5
wao walio lelewa kwa kuvaa nguo za zambarau
Kuvaa nguo rangi ili hashiria mtu ana utajiri.
Lamentations 4:6
Hukumu
Maana inayo wezekana ni 1) "adhabu kwa dhambi" au 2) "dhambi."
binti wa watu wangu
Hili ni jina la kishairi la Yerusalemu, ambalo linazungumziwa hapa kama ni mwanamke.
ilipinduliwa kwa dakika
"Mungu alimuonyesha kwa dakika"
hakuna aliye yanyua mkono kumsaidia
"japo hakuna mtu aliyw msaidia"
Lamentations 4:7-8
Viongozi wake walikuwa wasafi kuliko theluji
Maana inayo wezekana; 1) "Viongozi wetu walikuwa wazuri kutazama awali" (UDB) kwasababu walikuwa wenye afya kimwili au 2) watu waliwapenda viongozi wao kwasababu viongozi walikuwa wasafi kimatendo jinsi theluji na maziwa yalivyo meupe.
Viongozi wake
Viongozi wa Yerusalemu
yakuti samawi
jiwe la gharama linalo tumika kwenye mikufu
Muonekano wao umekuwa mweusi kama giza
Hii ya weza maanisha 1) jua limefanya ngozi za viongozi kuwa nyeusi au 2) moshi kutoka kwenye moto ulio choma Yerusalemu umefunika nyuso zao.
hawatambuliki
"Hakuna anaye weza kuwatambua"
imekuwa kavu kama kuni
kwasababu hawana chakula cha kutosha na maji
Lamentations 4:9-10
Hao walio uawa kwa upanga
"Hao wanajeshi maadui waliyo waua
hao walio kufa kwa njaa
"hao walio umwa na njaa hadi mauti"
walio potea
"hao waliyo kuwa wembamba na wadhaifu kwasababu walikuwa wana kufa kwa njaa"
wakatobolewa kwa ukosefu wa mavuno shambani
Ukosefu wa chakula unazungumziwa hapa kama ni upanga.
Mikono ya wanawake wenye huruma
"wanawake wenye huruma"
Lamentations 4:11
Yahweh alionyesha gadhabu yake yote; alimwaga hasira yake kali
Yahweh alikuwa na hasira sana, na amefanya kila kitu alichotaka kufanya kuonyesha alikuwa na hasira.
alimwaga hasira yake kali
Hasira ya Mungu ni kama moto, maji ya moto anayo mwaga.
Aliwasha moto Sayuni
Hii inaweza maanisha 1) hasira ya Mungu ni kama moto uliyo haribu Yerusalemu, au 2) kwamba Mungu alisababisha maadui wa chome Yerusalemu kwa moto.
Lamentations 4:12-13
Wafalme wa dunia hawaku amini, wala wakazi wa dunia,
"Hakuna mtu popote aliye amini"
maadui au wapinzani
Haya maneno mawili yana maana moja na yanakazia kuwa hawa ni watu waliyo waliyo tamani kudhuru Yerusalemu.
dhambi za manabii na maasi ya makuhani
Hii mistari miwili ina maanisha kitu kimoja na kukazia kuwa hawa viongozi wa kiroho walikuwa wanahusika na kuanguka kwa Yerusalemu.
walio mwaga damu ya wenye haki
Wote makuhani na manabii walikuwa na hatia ya mauaji.
Lamentations 4:14-15
Walikuwa wamejitia unajisi kwa damu hiyo
Kwasababu wameshiriki mauaji, hawana usafi, wasio weza kumtumikia Mungu au kuwa na watu wa kawaida.
Lamentations 4:16
akawatawanyisha
akawatawanyisha makuhani na manabii
hawatazami tena
"haendelei kuwa kubali tena" au "haendelei kuwa idhinisha tena"
Lamentations 4:17-18
Macho yetu yalikwama
Maana inayo wezekana ni 1) walitafuta watu wawasaidie, lakini hakuna msaada uliyo kuja au 2) waliendelea kutafuta masaada kutoka kwa watu wasingeweza kuwa saidia.
Walifuata hatua zetu
"Maadui zetu waliwafuta kila sehemu walipo enda"
mwisho wetu
"Wakati wa sisi kufa"
Lamentations 4:19-20
Pumzi katika pua zetu
Hii ni cheo cha mfalme, anaye toa uzima kwa watu wake kama pumzi inavyo upa mwili uhai.
aliye kamatwa katika shimo
Hapa "shimo" la husu mtego wa adui, mpango wao wa kumkamata adui.
Lamentations 4:21-22
Shangilia na ufurahi
Haya maneno mawili yana maana moja na yana kazia uzito wa furaha. Mwandishi anatumia haya maneno kwa kejeli.
Binti wa Sayuni ... binti wa Edomu
Haya ni majina ya kishairi ya watu wa Yerusalemu na nchi ya Edomu, ambapo hapa yana zungumziwa kama mwanamke.
kwako pia kikombe kitapitishwa
Mvinyo watu wanao kunywa kutoka kwenye kikombe ni hishara ya hasira ya Yahweh.
ata funua dhambi zako
"kuweka wazi dhambi zako"
Lamentations 5
Lamentations 5:1-4
Maelezo ya Jumla
Shairi lipya la anzu.
Kumbuka
"Fikiria kuhusu"
uone aibu yetu
"angalia hali ya aibu tuliyo nayo"
Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni
"Umeruhusu wageni kuchukua "
nyumba zetu kwa wageni
"umeruhusu wageni wachukuwe mali za urithi wetu"
Tumekuwa yatima ... mama zetu ni kama wajane
Watu wa Yerusalemu hawana mtu wa kuwalinda kwasababu wanaume wamekufa vitani au wameenda matekani.
Lazima tulipe fedha kwa maji tunayo kunywa
"Lazima tulipe fedha kwa maadui zetu ili tunywe maji yetu"
tulipe fedha kupata mbao zetu
"maadui zetu wanatuuzia mbao zetu"
Lamentations 5:5-7
Hao wanakuja kwetu
Jeshi la wa Babilonia.
Tumejitoa kwa
"tumefanya maridhiano na" au "tumejisalimisha kwa"
tupate chakula cha kutosha
"ili tuwe na chakula cha kutosha kula"
hawapo tena
"wamekufa"
tumebeba dhambi zao
"tunabeba adhabu ya dhambi zao"
Lamentations 5:8-10
Watumwa walitutawala
Maana inayo wezekana ni 1) "Sasa watu wanao tutawala wao wenyewe ni watumwa kwa mabwana zao Babilonia" (UDB) au 2) "Watu walikuwa watumwa Babilonia wanatutawala."
kutuokoa na mikono yao
Hapa neno "mkono" la husu nguvu.
kwasababu ya upanga wa nyikani
"kwasababu kuna watu nyikani wanao ua watu kwa upanga"
Lamentations 5:11-12
Wanawake wanabakwa Sayuni ... mabikra katika mji wa Yuda
"Wanawake wote, wadogo na wakubwa, wanabakwa Yerusalemu na miji ya Yuda"
Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao
Maana inayo wezekana ni 1) "Kwa mikono yao, wamenyonga watoto wa wafalme" au 2) wamefunga mikono ya watoto wa wafalme pamoja kwa kama ili miguu yao isiguse chini.
Lamentations 5:13-14
Wazee
wanaume wasio na "nguvu" tena
lango la mji
sehemu wazee wangetoa mashauri, lakini pia sehemu watu wange kutana
miziki
sehemu ya sanaa katika lango la mji
Lamentations 5:15-16
Taji limeanguka kichwani mwetu
Maana inayo wezekana ni 1) "Sisi hatuvai tena maua kichwani mwetu kwa ajili ya sherehe" au 2) "Hatuna tena mfalme"
Lamentations 5:17-18
macho yetu yanafifia
"tuna ona kwa shida kwasababu ya machozi yetu"
mbwa wa mitaani
Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:3. Sehemu zilizo haribiwa zilikuwa zimevamiwa na mbwa hawa wa mitaani, pamoja na wengineo.
Lamentations 5:19-22
kiti chako cha enzi
"nguvu yako na mamlaka ya kutawala kama mfalme"
vizazi na vizazi
"wakati wote"
Kwanini unatusahau milele? Kwanini unatutelekeza kwa siku nyingi?
"ni kama vile utatusahau milele au usiturudie kwa kipindi kirefu"
Fanya upya siku zetu kama zilivyo kuwa hapo zamani
"Fanya maisha yetu mazuri, kama yalivyo kuwa" au "Fanya tuwe wakuu kama tulivyo kuwa"
vinginevyo labda uwe umetukataa na una hasira kwetu kupita kiasi
Maana inayo wezekana ni 1) mwandishi ana ogopa kwamba Yahweh anaweza kuwa na hasira asiwarejeshe au 2) anasema kuwa Yahweh ana hasira hadi hawezi kuwarejesha (UDB)