Malachi
Malachi 1
Malachi 1:1-3
Agizo la neno la Bwana kwa Israel kwa Mkono wa Malaki.
"Bwana alizungumza haya maneno kwa waisrael kupitia Malaki"
Kwa mkono wa Malaki
kupitia kutenda kwa Malaki
Lakini wasema, "Umetupenda kwa namna gani?"
Hili swali linaonyesha shaka, au maswali juu ya ukweli wa neno la Mungu. Mungu anatumia swali kuwakemea watu. Tafsiri mbadala: lakini wasema, "Hujatupenda!"
Hakuwa Esau ndugu yake Yakobo?
"Nitawaambia jinsi ninavyowapenda ninyi. mnajua kwamba Esau ni ndugu yake Yakobo."
Asema Bwana
Bwana mwenye kweli amesema haya"
Nimempenda Yakobo
Bwana alichagua kuwa na mahusiano na Yakobo na kuwa Mungu ya Yakobo.
Nimemchukia Esau
Bwana alimkataa Esau
Nimeifanya Milima yake kuwa ya uharibifu na kuteketezwa
"Nimeifanya milima yake kuwa haifai kukaa ndani yake"
Na nimeufanya urithi wake kuwa sehemu ya mbweha wa mwituni
"Na nimeifanya nchi anayorithi kuwa jangwa ambapo wanyama pekee wanaweza kuishi"
Malachi 1:4-5
Kama Edom akisema
'Kama watu wa Edomu wakisema."
lakini nitawaangusha chini
"Nitaiangamiza"
na wanaume watawaita
"na wanaume wa taifa lingine watawaita"
nchi ya uovu
"nchi ya watu waovu
Macho yako yataona hiki
"Utaona hiki kikitokea'; hii ni kuwa, hawatahitaji mtu yeyote kuwaambia kilichotokea.
Malachi 1:6-7
mnadharau jina langu
"mmenifanyia kama mnayenichukia"
Lakini mwasema, 'ni kwa namna gani tumekudharau?
"ninyi makuhani mnasema, 'je tumekutendeaje kama tuna kuchukia? Tafsiri zingine zinasema: Mnanidharau lakini mwasema hapana!"
Mkate ulio najisi.
chakula ambacho hakikubaliki kwa dhabihu
Na mnasema, 'Tunakunajisi kwa namna gani?'
Tafsiri nyingine: Mnadhani mmekubalika kwangu lakini sivyo.
Malachi 1:8-9
Unapotoa wanyama vipofu kwa ajili ya kuteketezwa, huo sio uovu?
mnajua vizuri sana kuwa ni dhambi kutoa wanyama vipofu kwa ajili ya sadaka ya kutekezwa.
Na mtakapotoa vilivyo vilema na vigonjwa, hiyo siyo uovu?
Na mnajua vizuri sana kwamba ni dhambi kutoa vilivyo vilema na vigonjwa!"
Toa zawadi kwa watawala wenu; atawakubali au atawahurumia tu?
Hamwezi kutoa zawadi mbele ya watawala wenu! kama mlifanya, mnajua kabisa hawezi kukubali au kuwahurumia.
Zawadi
kutoa kama zawadi kuonyesha heshima
Na sas,... ni neema kwetu
Malaki hazungumzii kwa ajili ya Mungu. Anazunguza moja kwa moja kwa wasraeli.
Pamoja sadaka ya namna hii kwa sehemu yenu, atapokea aina yeyote?
"Unapotoa kile kisichoruhusiwa, Mungu atafurahishwa na ninyi?" hii ni kukemea. "Kama utatoa sadaka iliyokataliwa Mungu hakika Mungu hatakuwa na furaha na ninyi!"
Malachi 1:10-12
Oh, kama pekee
Hii inaelezea hisia kubwa.
ili kwamba msiwe mnawasha moto juu ya madhabahu yangu bure
"ili kwamba msitengeneze moto kuteketeza sadaka na dhambi kwa kutoa sadaka zisizo na maana"
Kutoka mikononi mwenu
"Kutoka kwenu"
jina langu
"mimi"
Kutoa mawio ya jua mpaka machweo yake
"Kila mahali," Sambamba na"Katika mataifa" na "kila sehemu"
Jina langu ni kuu katika mataifa
"Nitaheshimika katika mataifa yote"
kila sehemu uvumba utafukizwa kwa jina langu
"katika mataifa haya watu watafukiza uvumba kwa ajili yangu katika ibada"
Malachi 1:13-14
anaye koroma
kuonyesha kutoheshimu kwa kupiga kelele kupitia pua
Nitaikubali hii kutoka kwenye mikono yenu?"
nitaikubali hii kutoka kwenu? hii ni kukemea. Tafsiri zingine : "Sitakuba hakika hii kutoka kwenu!"
Alaaniwe mwenye kudanganya, mwenye mnyama dume katika kundi lake na akaapa kumtoa kwa kwangu
"Nitalaani vitu viovu kwa yeyote anayedanganya kwangu ambaye anaye mnyamna mkamilifu katika zizi lake na anaahidi kumtoa kama sadaka "
na hajatoa kwangu, Bwana, ambayo ni ujanja ujanja
"na pia dhabihu kwangu, Bwana, na mnyama ambaye hayuko imara"
Malachi 2
Malachi 2:1-2
liweke moyoni
"Fanya kuwa la Muhimu"
Malachi 2:3-4
Nitapaka mavi katika nyuso zenu
"Nitawaendesha ninyi bila heshima"
Mtachukuliwa mbali nayo
"watawatupa ninyi juu ya rundo la mavi"
Lawi
Yehova asema juu ya kabila la Lawi ingawa ni mtu mkoja
Malachi 2:5-7
Agano langu pamoja naye ilikuwa ni juu ya yhai na amani
"Kusudi la agano langu pamoja na Lawi ilikuwa ni juu ya makuhani kuishi maisha ya ushindi na amani"
Nilitoa hivi vitu kwake ili kuonyesha heshima kwa ajili yangu
Nilitoa vitu hivi kwake ili kwamba aniheshimu"
midomo
uwezo wa kuongea na kujulisha watu
ulinzi
"Kuhifadhi"
Malachi 2:8-9
"kudharauliwa na uovu mbele za watu
"Watu wamechukia na hawawaheshimu makuhani."
mmeonyesha upendeleo katika maelezo yenu.
"makuhani walionyesha tabia yakawaida kwa watu waliyoyapenda na hali ya ugumu wa tabia kwa watu ambayo hawakuipenda."
Malachi 2:10-12
Sisi sote hatuna baba mmoja? Hatuna Mungu mmumbaji mmoja?
"haya Maswali ni kuonyesha kukemea. "Sisi sote kwa hakika tunaye baba mmoja, Mungu wetu aliyetuumba sisi!"
Kwa nini tuna hila kila mmoja na ndugu yake, na kulikufuru agano la baba zetu?
hii pia ni kukemea. Hatupaswi hakika kuwatendea ndugu zetu na kutokuheshimu agano la Mungu na kutotii amri zake!"
mnafanya hila
kutomtii Mungu
Kwa ajili ya Yuda ameliharifu mahali patakatifu pa Bwana
"Wanaume wa Yuda hawakutii hekalu la Mungu"
na ameoa binti wa mungu mgeni
"na wameoa wanawake kutoka katika mataifa yanayoabudu miungu."
kila ukoo wa mtu ambaye amefanya haya
"Kila watoto na wajukuu wa mtu yeyote aliyefanya haya"
hata mmoja aliyeleta sadaka kwa Bwana wa majeshi
"hata kama mtu wa dhambi akileta sadaka kwa Mungu lakini hakutubu dhambi zake"
Malachi 2:13
akilia na kuugua
Maneno "Kilio" na "Kuugua" yanachangia maana moja yanakazia uimara wa kulia. "na kilio kikuu"
kutoka mikononi mwako
"Kutoka kwako"
Malachi 2:14-16
amefunika mavazi yake kwa vurugu
ni vurugu tu
Jilindeni ninyi kwa ninyi katika roho na kutokuwa na uaminifu.
"Kwa hiyo uamue kabisa kuwa mwaminifu kwa mke wako!"
Malachi 2:17
Mkisema
"kuwapotoisha wengine kwa kusema"
Yuko wapi Mungu wa haki?
Makuhani wanamkemea Mungu. "Mungu kwa hakika hakuonyesha haki kwa watu waovu!"
Malachi 3
Malachi 3:1-3
Nani atavumilia siku ya kuja kwake? na nani atasimama akionekana?
"Kwa hakika hakuna hata mmoja atakayekuwa na uwezo wa kumsaidia Bwana.
Kwa kuwa n yeye ni kama asafishaye kwa moto na kama sabuni ya kufulia.
Mungu analinganisha uwezo wake wa kutawala watu na kuwasafisha kutoka dhambini kwenda kwenye sabuni yenye nguvu kusafisha au nguvu ya moto unavyoyeyusha kitu. hii ni njia nyingine ya kusema kuwa Nguvu ya Mungu ya kufanya kitu haizuiliwi.
na atawasafisha wana wa Lawi
"na atawakusanyana kuwasafisha wana wa Lawi kutoka dhambini"
atawaboresha na kuwa kama dhahabuau shaba
Mungu ataondoa thambi kutoka kwa walawi na kuwafanya kuwa safi zaidi.
na wataleta sadaka ya haki kwa Bwana
"Na wataleta sadaka ya ibada iliyokubalika kwa Bwana"
Malachi 3:4-5
siku za kale, na miaka ya zamani
hizi aya mbili kimsingi zina maana mojana zinasisitiza kuwa sadaka zilipaswa kumpendeza Bwana. "kama ilivyokuwa huko nyuma."
karibia
"Sogea karibu"
Usimwonee mfanya kazi katikamshahara wake
"Usimlipe mfanyakazo mshahara kutokana na yeye alivyo"
kumweka mbali mgeni kutoka kwenye haki zake
kukataa wageni kuishi kwenye jamii ambayo ni haki kila mtu anapata.
Malachi 3:6-7
tokea siku za baba zenu mmegeuka kwingine na kuiacha amri na hamkuitunza
"Hamkutii amri zangu toka kipindi cha mababu zenu"
Tutakurudiaje?
"Hatujaenda mbali na wewe, kwa hiyo hatuwezi kurudi kwako."
Malachi 3:8-9
Mwanadamu atamwibia Mungu?
hii ni kukemea. Mwanadamu hakika hawezi kumwibiaMungu
Malachi 3:10-12
zaka kamili
"Zaka zote"
nyumba yangu
"hekalu langu"
Nijarinuni sasa katika hili...kama sitafungua kwa ajili yenu madirisha ya Mbinguni
"Kama mtanijaribu...Nitafungua madirisha ya mbinguni"
nitamkemea alaye
nitazuia wadudu na magonjwa
Malachi 3:13-15
walimjaribu Mungu na kujiepusha
walijaribu kumfanya akasirike, lakini hakuwahukumu"
Malachi 3:16
na kitabu cha kumbukumbu kilikuwa kimeandikwa mbele zake waliomwogopa Bwana
Hii inaweza kumaanisha 1) Waisrael waliandika kitabu ambacho wangekumbuka kile walichokuwa wameahidina kwa majina ya watu wenye hofu na Bwana au 2) Bwana alimfanya mtu flani huko mbinguni kuandika kitabu kikiwa na majina ya wale wanaomwogopa Bwana.
kitabu cha kumbukumbu
kitabu cha kuwasaidia watu kukumbuka mambo muhimu
heshimu jina lake
kumheshimu yeye
Malachi 3:17-18
watakuwa wangu
"Watakuwa watu wangu"
miliki yangu mwenyewe
"Hazina yangu maalumu"
Nitatenda
"Nahukumu"
kutofautisha kati ya
tazama tofauti kati ya au nitawaongoza kwa tofauti
Malachi 4
Malachi 4:1-6
tazama
"angalia" au "sikiliza" au "Uwe makini kwa kile nataka kuakuambia"
siku inakuja, ikiwaka kama tanuru
"siku ya hukumu inakuja, ni nitawahukumu watu waovu kama mkulima anavyochoma makapi na majani"
majivuno...waharifu
Tafsiri kama ulivyofanya "Kiburi" na "waharifu"
watakuwa mabua
"choma kama mimea mikavu"
Siku inayokuja itawachoma wote
"katika siku hiyo nitawachomawote"
sitaacha mzizi wala tawi
"hakuna kitakachobaki'
Jua la wenye haki litawainukia likiwa na uponyaji katika mbawa zake
Hii inaweza ikawa 1) Bwana, ambaye siku zote hutenda haki, atakuja na kuwaponya watu waokatika siku hiyo au 2) katika siku hiyo Bwana atajidhihirisha kwa watu wake wenye haki na kuwaponya.
mbawa
mbawa