Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

01-01

Mwanzo

Huu ni, "mwanzo wa vitu vyote" kabla ya kuwepo kitu chochote isipokuwa Mungu.

Aliumba

Hapa inatumika kumaanisha kutengeneza kitu pasipokutumia kitu.

Ulimwengu

Hii inajumuisha kila kitu ambacho Mungu aliumba duniani na mbinguni, vyote vinavyo onekana na visivyo onekana.

Dunia

Neno "Dunia" linamaanisha ulimwengu wote ambao watu wanaishi.

Giza

Giza maana yake kutokuwepo na mwanga kabisa, kwasababu Mungu alikuwa bado hajaumba mwanga.

Utupu

Mungu bado hajaumba kitu chochote isipokuwa Dunia iliyofunikwa na maji.

Hakuna kilichokuwa kimeumbwa

Hapakuwepo na uumbaji wa vitu isipokuwa maji iliyofunika dunia.

Roho wa Mungu

Roho wa Mungu, wakati mwingine huitwa Roho Mtakatifu, alikuwepo toka mwanzoni, alitembea juu ya dunia ili aumbe vyote alivyo kusudia.

01-02

Mungu akasema

Mungu aliumba mwanga kwa kutamka neno.

Na iwe

Hii ni amri iliyotokea mara moja kwasababu ilinenwa na Mungu. Inaweza kutafsiriwa kwa njia ya kawaida kuwa ni neno lenye uhakika wa kutokea. Kwa mfano, unaweza kutafsiri kama, "Mungu akasema, 'Pawepo na Mwanga.'"

Mwanga

Huu ni mwanga maalum ambao Mungu aliumba-jua halikuumbwa hadi baadaye.

Ikawa nzuri

Maneno haya yalitumika mara kwa mara katika historia ya uumbaji, na kusisitiza kuwa kila hatua ya uumbaji ilikuwa ikimpendeza Mugu na kutimiza mipango na kusudi lake.

Uumbaji

Neno hili limetumika hapa kumaanisha siku sita ambazo Mungu alivifanya vitu vyote vilivyoko.

01-03

Siku ya pili

Kazi za Mungu za uumbaji ulifuata utaratibu, makusudi na mpangilio. Vitu alivyoumba kwa kila siku zilijenga na kutegemea vitu vya siku iliyotangulia.

Mungu akasema

Mungu aliumba anga kwa kusema neno.

Kuumba

Mungu aliumba anga pasipokuwepo na kitu.

Anga

Neno hili linamaanisha sehemu yote ya juu ya Dunia, hii ikiwa ni pamoja na hewa tunayovuta na mbingu.

01-04

Siku ya tatu

Ni siku iliyofuata kwenye mtiririko ambapo Mungu aliandaa Dunia kwa Maisha.

Mungu akasema

Mungu aliumba nchi kavu kwa kuamuru.

dunia

neno hili limetumika kumaanisha sehemu vumbi au udongo, ambayo ardhi iliyo kavu imetegenezwa.

Kuumba

Neno hili linatumika kumaanisha, kutengeneza kitu pasipo kutumia kitu chochote.

01-05

Mungu akasema

Mungu aliumba mimea yote kwa kuamuru.

Nchi na izae

Hii ni amri iliyotokea mara moja kwa sababu Mungu alinena.

Aina zote

Hii ni aina mbali mbali ya mimea na miti.

Kuumba

Neno hili linatumika kumaanisha, kutengeneza kitu pasipo kutumia kitu chochote.

Kilikuwa chema

Neno hili limetumika mara nyingi katika historia ya uumbaji, hii ikisisitiza ya kuwa kila hatua ya uumbaji ilimpendeza Mungu na kutimiza lengo na kusudi yake.

01-06

siku ya nne

Ni siku ilyofuata kwa mpangilio wa uumbaji wa siku ambayo Mungu aliumba.

Mungu akasema

Mungu aliumba jua, mwezi, na nyota kwa kuamuru.

mwanga

Ni kitu ambacho kinang'aa angani na kutoa mwanga kwa dunia.

usiku na mchana, nyakati na miaka

Mungu aliumba mianga tofauti tofauti ili kutofautisha sehemu ya muda kuanzia ndogo hadi kubwa, na kuziweka zijirudia kwa wakati wote hadi mwisho wa wakati.

Kuumba

neno hili linatumika kumaanisha, kutegeneza kitu pasipo kutumia kitu chochote.

01-07

siku ya tano

Mungu aliendelea na mpangilio wake wa uumbaji ambayo alianza siku nne zilizopita.

Mungu akasema

Mungu aliziumba ndege na vitu viishivyo majini kwa kuamuru.

Kila kiumbe kinacho ishi na kwenda majini

Mungu hakuumba tu samaki, bali kila aina ya viumbe vyenye kuishi na kwenda ndani ya maji. Kila mmoja anaishi kwa sababu Mungu alichagua kuumba.

ndege wote

Mungu hakuumba tu aina moja ya ndege, lakini aliumba aina mbalimbali za ndege wazuri ajabu wenye kutofautiana maumbo, ukubwa na rangi.

ni vyema

Neno hili limetumika mara nyingi katika histora ya uumbaji, hii ikisisitiza kuwa kila hatua ya uumbaji ilikwenda kama ilivyokusudiwa kutokana na mpango wa hekima ya Mungu na kusudi lake.

aliwabariki

Mungu aliongea nia yake kuwa wangebarikiwa na kwamba mambo yao yote yaengekwenda vema katika dunia aliowaweka.

01-08

siku ya sita

Jambo lililofuata, mpangilio katika mfuatano wa siku za matendo ya uumbaji.

Mungu akasema

Neno alilo liongea Mungu ndiyo njia ambayo wanyama waliumbwa.

aina mbambali

Hii inamaanisha vitu vingi tofauti tofauti, lakini vyenye mpangilio.

wanyama wa nchi

Ni aina mbalimbali ya wanyama walioishi juu ya aridhi, mbali na ndege, au wanyama walioishi majini.

wanyama wa shambani

Ni aina ya wanyama wanaishi kwa amani na watu juu ya ardhi, kwa jina lingine ni wale wanyama wa kufugwa.

wanaotambaa juu ya nchi

Hii inajumisha jamii ya wanyama wote watambaao kama reptilia na wadudu.

porini

Ni aina ya wanyama ambao mara nyingi hawaishi kwa amani na watu, hii ni kwa sababu wanaogopa watu, au ni hatari kwao.

ni vyema

Neno hili limetumika mara nyingi katika histora ya uumbaji, hii ikisisitiza kuwa kila hatua ya uumbaji ilikwenda kama ilivyokusudiwa kutokana na mpango wa hekima ya Mungu na kusudi lake.

01-09

Na tumfanye

Hii inaonyesha makusudi ya Mungu, kufanya maamuzi ya kumtengeneza mtu kwa namna ya aina yake na kwa makusudi fulani. Inawezekana kutafsiriwakama, "Tutafanya."

Sisi...yetu...sisi

Biblia inafundisha kuwa kuna Mungu mmoja, lakini kwa maneno ya Agano la Kale "Mungu" iko katika neno la wingi. Na Mungu hutumia maneno ya wingi pale anapoongelea juu yake. Wengine wanafahamu hii kama njia maalumu ya kuelezea ukuu wa Mungu, na wengine hufahamu hii kama Mungu Baba akiongea kwa Mwanaye na Roho Mtakatifu, ambao wote ni Mungu.

kwa mfano wetu

Mfano, ni taswira inayowakilisha sura ya kitu halisi au mtu. Watu walifanywa kwa namna ambayo wanaweza kuonyesha na kuwakilisha baadhi ya tabia na sifa za Mungu.

kama sisi

Watu wanazishriki baadhi ya tabia za Mungu ila siyo tabia zote. Maneno haya yanaweza kutafsiriwa kuwa mwanadamu anafanana na Mungu, ila hayuko sawa na Mungu na au jinsi alivyo.

mamlaka

Mungu aliwapa watu uhuru na nguvu ya kutawala, kuongoza na kuamua namna dunia na wanyama watakavyotumika.

01-10

alichukua vumbi

Mungu alimfanya mwanadamu kwa kutumia mavumbi kutoka ardhini. Neno hili pengine linaweza kuwa tofauti na neno lililotumika mara kwa mara la neno dunia.

alimfanya

Neno hili linaonyesha kuwa Mungu mwenyewe alimtengeneza mwanadamu. Hii ni sawa na mwanadamu anavyo tengeneza kitu kwa mikono waye mwenyewe. Hakikisha neno lingine tofauti na "uumbaji" linatumika, hii ni tofauti na alivyo umba vitu vingine vyote ambavyo alifanya hivyo kwa kuamuru kwa kutamka tu.

mtu

Kwa wakati huu aliyetengenezwa ni mwanaume tu, mwanamke alitengenezwa baadaye kwa njia nyingine.

akampulizia uhai

Neno hili inaonyesha Nafsi ya Mungu, tendo la ukaribu la kuhamisha uhai wake kwenda kwenye mwili wa Adamu, linganisha na namna mtu anavyotoa hewa.

uhai

Katika tendo hili, Mungu alimpulizia mwanadamu uhai wa mwili na roho ndani ya mtu.

adamu

Jina la adamu ni sawa na neno katika agano la kale lenye maana ya "mtu" na ni sawa na neno la udongo/mavumbi ambao alifanywa kwayo.

bustani

Ni eneo la ardhi lililopandwa miti na mimea kwa kusudi-mara nyingi kuzalisha chakula au kufanya sehemu kuwa nzuri.

aitunze

Kuendeleza bustani kwa kulimia, kupalilia, kunyeeshea, kuvuna, kupanda n.k.

01-11

katikati

Sehemu ya katikati hutia mkazo na umuhimu wa miti hizo miwili.

bustani

Ni eneo la ardhi lililopandwa miti n amimea kwa kusudi -mara nyingi kuzalisha chakula au kufanya sehemu kuwa nzuri.

Mti wa uzima

Mtu alaye matunda katika mti huu hatakufa kamwe.

mti wa ujuzi wa mema na mabaya

Matunda ya mti huu humuwezesha mtu kutambua mema na mabaya.

ujuzi

Kuelewa au kufahamu kwa kuwa na uzoefu nao.

mema na mabaya

Mabaya ni kinyume cha mazuri. Kama ambavyo mazuri humaanisha yale mazuri yanayompendeza Mungu, mabaya humaanisha kitu chochote ambacho hakimpendezi Mungu.

kufa

Katika hali hii, atakufa kimwili na kiroho.

01-12

siyo vema

Hii ni mara ya kwanza katika uumbaji kwa kitu kutokuwa kizuri. Ina maanisha "bado haijawa nzuri" kwa sababu Mungu hajamaliza kazi ya kumuumba mwanadamu.

peke yake

Adamu alikuwa mwanadamu mwenyewe, pasipo kuwapo na nafasi ya kuwa na uhusiano na mwanadamu mwingine. Na hakuweza kuwazaa watoto na kuongezeka.

Msaidizi wa Adamu

Hapakuwepo yeyote aliyefanana kiasi cha Adamu kuweza kuungana naye kukamilisha shughuli alizopewa na Mungu. Hakuna mnyama awezaye kufanya havyo.

01-13

usingizi mzito

Huu ulikuwa usingizi usio wa kawaida.

akatoa ubavu mmoja na kutengeneza

Maneno haya, yanaonyesha kitendo cha Mungu kutoa ubavu wa Adamu na kutengeneza mwanamke.

mwanamke

Alikuwa mwanamke wa kwanza, mwanadamu mwenye jinsia ya kike ambaye alikuwa hajatengenezwa hadi wakati ule.

akamleta kwake

Ni Mungu mwenyewe ndiye aliyewatambulisha. Alimleta Mwanamke kwa Adamu, kama kutoa zawadi nzuri kwake.

01-14

Hatimaye!

Adamu alisema hivyo kuonyesha kuwa alikuwa akisubiri kitu kama mwanamke.

Kama mimi

Mwanamke alikuwa ni mwanadamu kama Adamu, pamoja na kwamba kulikuwepo na tofauti za umuhimu kati yao.

Mwanamke

Neno hili linamanisha muundo wa kike ambayo siyo mwanaume.

kutengenezwa kutokana na mwanaume

Mwanamke alitengenezwa kutokana na mwili wa Adamu.

mwanaume atamuacha

Hii ilitamkwa kwa wakati uliopo ili kuonyesha mwenendo utakao kuwepo katika siku za baadaye. Adamu alikuwa hana mama wala baba, lakini wanaume wengine wote watakuwa nao.

watakuwa mmoja

Mme na mke watashirikiana katika mahusiano ya karibu na kipekee, katika umoja na kujitoa kwa kila mmoja wao kwa mahusiano yanayozidi mahusiano na watu wengine wote.

01-15

Mungu alimtengeneza

Mungu alimtengeneza mwanaume na mwanamke kwa namna ya kipekee.

kwa sura yake

Taswira au sura ni kiwakilishi halisi cha kitu au mtu. Mungu aliwatengeneza watu ili kuonyena na kuwakilisha baadhi ya tabia na sifa za Mungu, lakini siyo kuwa sawa na yeye.

chema sana

Hii inaonyesha zaidi ya maneno yaliyotumika hapo nyuma ya kama ni chema, vyema. Chema sana inamaanisha kwa uumbaji wote na siyo to kwa mwanaume na mwanamke. Kila kitu ilikuwa sawasawa na kama Mungu alivyokitaka kiwe.

Uumbaji

Siku sita ambazo Mungu alitumia kuumba kila kitu.

01-16

siku ya saba

Ni siku iliyofuata baada ya siku ya sita kuisha.

amemaliza kazi yake

Mungu alimaliza kazi ya uumbaji ila bado anafanya kazi zingine.

Mungu akapumzika

Mungu "alipumzika" kwa sababu kazi ya uumbaji ulikamilika. Mungu hakuchoka, au si kwamba ameshindwa kuendelea.

Aliibariki siku ya saba

Mungu alikuwa na mpango nzuri maalum kwa siku ya saba, na kwa kila siku ya saba baadaye.

akaifanya takatifu

Hii ina maana, "Mungu alitenga" siku hii kama siku maalum. Haitatumika kama siku nyingine za wiki.

ulimwengu

Hii inajumuisha kila kitu alihoumba Mungu hapa duniani na mbinguni, yale yanayo onekana na yasiyo onekana.