36-01
Siku moja
Kipengele hiki kinatambulisha tukio ambalo lilitokea kipindi kilichopita, lakini halielezi muda maalumu. Lugha nyingi huanza kuelezea habari ya kweli kwa njia inayofanana.
Yakobo
Huyu ni Yakobo tofauti na yule aliyeandika Kitabu cha Yakobo kwenye Biblia. Kwa kuweka wazi hili, baadhi ya lugha zinaweza kuhitaji kidogo kutumia majina tofauti mawili au kutofautisha kulitamka.
36-02
Kitu cheupe
Hiki ni , "cheupe zaidi" pia kinaweza kutafsiriwa kama nuru (chanzo cha mwanga) au angavu
36-03
iliyoonekana
Vilevile inawezekana kusema, "ilionekana bila kujua ilikotokea." Ghafla walikuwa pale au, walitokea kwa ghafla.
kifo chake, ambacho kingetokea karibuni
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "jinsi atakavyo kufa karibuni" au, "jinsi ambavyo wangemuua muda si mrefu"
ndani ya Yerusalemu
Baadhi ya lungha zinaweza kupendelea kusema, "katika jiji la Yerusalemu."
36-04
vibanda
Hii vilevile inaweza kutafasiriwa kama, "kivuli" au vibanda vya bustanini" au, hema. Hii inarejea kwenye baadhi ya vibanda vidogo vya muda, kama walivyovitengeneza wayahudi kutokana na matawi wakati wa sikuuu ya kiyahudi.
hakujua ambacho alikuwa akisema
Ni kwamba "alikuwa anazungumza bila kuelewa kilichokuwa kinatokea" au, " alizungumza bila kufikiria vizuri kwa sababu alikuwa na furaha sana."
36-05
Sauti toka mawinguni ikisema
Vilevile hii inaweza kutafasiriwa kama, "sauti ilizungumza kutoka mawinguni inasema, "au, Mungu alisikika kutoka mawinguni na kusema."
Msikilizeni Yeye
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "ni Yeye pekee ambaye mnapaswa kumsikiliza."
Anguka chini
Huku ni, "kuinama chini kwa haraka" au, "kufika chini ghafla." yaani kusujudu. Hakikisha kwamba tafasiri ya "anguka" haimaanishi ajali. Huenda walifanya hili kwa unyenyekevu na hofu bila kutegemea.
36-06
Aliwagusa
Hii ni "akaweka mkono wake juu yao."Lugha zingine zinaweza kupendelea kuonesha aliwagusa wapi. Kama hivyo, hii ingetafasiriwa kama, "aliwagusa kwenye bega" au, "aliweka mkono wake kwa kila mtu begani."
Msiogope
Hii pia ingelitafasiriwa kwamba, "acha kuogopa"
Inuka
Hii inaweza kutafasiriwa kwamba, "inuka" au, "Tafadhali nakuomba inuka." Hakikisha inaleta maana kwamba Yesu alisema hili kwa upole.
Yesu pekee ndiye alibakia pale
Pia inawezekana kuongeza, Musa na Eliya tayari walishaondoka" yaani hawakuwepo pale.