35-01
siku moja
Hii aya inatambulisha tukio ambalo lilitokea kipindi cha nyuma, lakini haisemi muda kamili. lugha nyingi zina namna moja ya kuanza kutoa habari ya kweli.
Watoza Ushuru
Watoza ushuru walidhaniwa kuwa wenye dhambi kabisa waliiba pesa kwa watuykwa kukusanya ushuru kwa hali ya juu kuliko walivyoagizwa na serikali.
35-02
habari
Yesu alitumia habari hii ili kufundisha ukweli kuhusu ufalme wa Mungu. haiko wazi kama tukio lilitokea kweli au hakuna. kama lugha yako ina habari kama hiyo ya kufikirika au kweli, unaweza kuitumia hapa.
35-03
Urithi wangu
hii ingetafsiriwa kama, "Sehemu ya mali yako ambayo itakuwa haki yangu ya halali unapokufa"
Mali
Hii ni "Mali" au, "milki." Hii mali inaweza pia kuwa ardhi, wanyama, na pesa"
35-04
Alitapanya pesa zake
hiyo ni, "kutumia pesa bila kupata chochote cha thamani kwa kubadilisha." Kwa lugha zingine inaweza kutafsiriwa kama, "Kutupa pesa" au, "Kula pesa zote."
Maisha ya dhambi
hii ni, "kutenda vitu viovu."
35-05
Njaa kali ilitokea
Hii ni, "kulikuwa na chakula kidogo." kwa lugha zingine hii inaweza kutafsiriwa kama, "Kulikuwa na njaa kali."
hakuna pesa kununua chakula
kwa sababu ya njaa, chakula kilikuwa na gharama kubwa, na tayari alishatumia pesa zake zote.
kazi
hii inalenga kazi ambayo unaweza ukafanya kwa ajili ya mtu mwingine ili akulipe pesa. kama hii haiko wazi, hii sentensi inaweza kuanza hivi, "Ili kujipatia pesa, alipata kazi."
Kulisha nguruwe
Hii ni, "kutoa chakula kwa nguruwe." hii pia inaweza kudhaniwa kuwa ni kazi ya hali ya chini katika jamii kwa kipindi hiki. kama lugha yako ina badhi ya maneno kwa kazi ya hali ya chini, tumia neno hili.
35-06
Nafanya nini?
Hii ni, "kwa nini ninaishi hivi?" au, "sipaswi kuishi hivi!" au, "haileti maana kwangu kuishi namna hii." kijana alikuwa haulizi maswali, kwa hiyo lugha zingine zinaweza kutafsiri hii kama maelezo.
35-07
akiwa mbali
hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "Ndani ya maeneo ya nyumba ya babaye, lakini bado ni mbali kidogo." kijana alipokuwa akikaribia kwenye nyumba ya baba yake, lakini alikuwa mbali na hata watu wa nyumbani hawakuweza kumwona. Hakikisha isije ikajulikana kuwa alikuwa bado katika nchi tofauti.
akuhurumia
Hii ni, "Alipenda kwa upendo wa dhati na huruma"
35-08
nimekosa mbele za Mungu na mbele zako
hii inaweza kutafsiriwa kama, "Kuasi kinyume na Mungu, na pia nimeasi mbele zako."
Sisitahili
inawezekana pia kusema, kwa hiyo sisitahili" au, "kama matokeo, sisitahili."
35-09
Ndama mzuri
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Ndama mnene." huyu alikuwa ndama aliyenenepeshwa ili kwamba akipikwa alete radha nzuri.
Mwanangu alikuwa amekufa, lakini sasa ni mzima!
hii ni, "Hii ni kama mwanangu alikuwa amekufa na sasa ni mzima!" au, "niliomboleza kana kwamba " Mwanangu alikufa, na sasa nafurahi kwa sababu ni kama amerudi kuwa hai tena! Baba alitumia maelezo haya ili kueleza furaha aliyonayo kuwa mtoto wake amerudi nyumbani.
alikuwa amepotea na sasa amepatikana
hiyo ni, " ni kama nilikuwa nimempoteza lakini sasa nimepata."
35-10
Muda mfupi
hii inaweza kutafsiriwa kama, "muda si muda" au, "Baada ya muda kitambo."
35-12
Mbuzi mmoja mdogo
Mbuzi mdogo anaweza kuliwa na watu wachache kuliko ndama aliyenona, na asingeweza kuthaminiwa sana. kaka mkubwa analalamika kuwa baba yake anamwona mtoto mwenye dhambi ni mhimu kuliko yeye.
Mtoto huyu ni wako
fafanuzi hii inaonyesha kuwa mtoto mkubwa alikuwa na hasira. inaonyesha kumkataa mdogo wake na kumkasirikia baba yake kwa kumkaribisha nyumbani tena mtoto mpotevu. lugha zingine pia zina njia ambayo si ya moja kwa moja ya mawasiliano ya vitu hivi.
kutumia pesa zako
hii ni, "aliponda pesa ulizompa" au, "alikula mali yako" kama inawezekana tumia maelezo ambayo yanaonyesha hasira za kaka mkubwa.
kuchinja ndama aliyenona
Hii ni, "Kuua ndama aliyenona kwa ajili ya kukla kwenye sikukuu."
35-13
ni haki kwetu
Hii ni, "Ni kitu sahihi kwetu kufanya" au, "Ni kitu sahihi kwetu"
Ndugu yako
baba alirejea kwa mwana wake mdogo kama, "Ndugu yako" kumkumbusha mwana mkubwa mahusiano yake kwa mdogo wake na alivyopaswa kumpenda mdogo wake.
alikuwa amekufa, lakini sasa yuko hai
Angalia jinsi unaweza kutafsili hii
alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana!
Angalia jinsi unaweza kutafsili hii