04-01
Miaka mingi baada ya gharika
Vizazi vingi vimepita baada ya gharika
tena, watu wengi
Familia ya Noah iliongezeka na kuwa na watu wengi wa kuujaza mji
lugha inayofanana
Hii inamaanisha kulikuwa na lugha mojja hivyo watu walielewana
mji
Ni vyema kutumia neno la jumla linalomaanisha mji kwakuwa kifungu hakitaji jina maalumu.
04-02
mnara mrefu kuifikia mbingu
mnara huo ulikuwa mrefu kiasi kwamba ncha yake ilifika angani.
Mbingu
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama "anga."
04-03
alibadili lugha yao
Kwa ghafla Mungu aliwapa lugha tofauti tofauti na hivyo hawakuweza kuelewana tena.
lugha nyingi mbalimbali
Badala ya kundi moja kubwa kuzungumza lugha moja, sasa waligawaanyika katika makundi mengi madogo madogo na kila kundi likawa na lugha yake.
aliwatawanya watu
Wakati Mungu alipobadilisha lugha zao, alisababisha watu hao kutawanyika na kila kundi lilienda sehemu yake.
Babeli
Hatujui kwa hakika mahali ambapo mji huu ulikuwa, zaidi ya kwamba ulikuwa mahali fulani huko Mashariki ya kati.
alichanganya
Hii inaelezea jinsi ambavyo watu walichanganywa wakati ambapo hawakuweza kuelewana baada ya Mungu kubadili lugha yao.
04-04
Mamia ya miaka baadaye
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "vizazi vingi baada ya watu kugawanyika katika lugha mbalimbali."
Ondoka katika nchi yako
Hii inaelezea eneo ambalo Abramu alizaliwa na kuishi.
na familia yako
Mungu alikuwa anamwita Abramu na famia yake tu, na kuwaacha ndugu zake wengine.
kukufanya kuwa taifa kubwa
Mungu angemfanya Abramu kuwa na watoto wengi, na wangekuwa taifa kubwa na la muhimu.
04-05
alichukua
lugha zingine zinaweza kusema "alileta"
Mungu alimuonesha
kwa namna fulani Mungu alimudokezea Abramu kuhusu mahali alipopaswa kwenda. Kifungu hiki hakielezi jinsi ambavyo Mungu alimuonesha.
nchi ya Kanaani
jina la nchi hiyo iliitwa "Kanaani."
04-06
ardhi yote utakayoiona
Kama Abramu alikuwa amesimama juu mlimani, angeweza kuona eneo kubwa.
kama urithi
Mungu aliahidi kumpa Abramu na uzao wake ardhi kama vile baba huwa watoto wake ardhi mali.
Kisha Abramu akakaa katika nchi
Abramu aliishi mahali pale pamoja na wote alioenda nao.
04-07
Melkizedeki
Melikizedeki alikuwa ni mtu mwenye mamlaka ya dini katika Kanaani ambaye alipokea sadaka na kuziwasilisha kwa Mungu.
Mungu aliye juu
Watu wa Kanaani waliabudu miungu mimgi ya uongo. Jina "Mungu aliye juu" lilimtambulisha Mungu wa kweli ambaye Melkizedeki alimwabudu.
04-08
Miaka mingi
Miaka mingi ilipita tangu Mungu alipomuahidi Abramu mtoto.
kama nyota angani
msemo huu unamaanisha kuwa uzao wa Abramu utakuwa na watu wengi kiasi kwamba hakuna atakayeweza kuwahesabu.
04-09
pande mbili
sehemu hizi mbili zinaweza kuwa, watu wawili, makundi mawili ya watu, au mtu mmoja na kundi la watu. Katika hili patano lilikuwa kati ya Mungu na Abramu.
kutokana na mwili wako
Kwa mwili wake binafsi Abramu angempa mimba mkewe, ili kwa pamoja wapate mtoto wao kwa njia ya asili. Hii ilikuwa ni ahadi ya ajabu sana maana Abramu na sara walikuwa wazee sana.
Hawakuwa na mtoto wa kiume
Abramu hakuwa na uzao ambao wangeirithi ardhi yake.