Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

31-01

Aliwaaga makutano.

Hii ni namna nyingine ya kusema, "aliwaruhusu waende zao"

Mlimani

Hii ni, "Upande wa Mlimani"

31-02

Wakati huo huo

Hii ni kwamba "Wakati Yesu alipokuwa akiomba juu Mlimani"

wakapiga kasia za Mtumbwi wao

Mtumbwi ulikuwa na tanga (Nguo inayofungwa kwenye mtumbwi ili upepo unapokuja ipate kuuendesha), lakini mtumbwi usingeweza kufanya kazi upepo unapobadilisha uelekeo." "upepo unapovuma kinyume chao"

ngumu sana

Hii ni "ngumu zaidi" au " ngumu zaidi"

31-04

roho

Hii ni "roho" walidhani Kuwa Yesu ni roho, maana mtu wa kawaida hawezi kutembea juu ya Maji.

Msiogope

Kwa baadhi ya Lugha inaweza kuwa kiasili zaidi kusema "acha kuendelea kuwa na uoga"

Mimi ndiye!

Kwa baadhi, inaweza ikawa zaidi ya kawaida kutafsiri kuwa " mimi ndiye, Yesu"

31-05

kama ni wewe

Hii ni "Kama kweli ni wewe, na kama siyo roho."

Njoo!

Hii ni, "Njoo hapa" au "Njoo kwangu" au "Njoo, Tembea uje kwangu"

31-06

alipoangalia kwingine

Hii inaeleza maana, "Aliangalia mbali na". inaweza pia kutafsiriwa kama "Kuacha kuangalia kwa".

31-07

Wewe mtu mwenye imani ndogo

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "Una imani ndogo sana juu yangu!" au, "Hauniamini mimi sana!"

kwa nini una mashaka?

Hii ni kwamba, "Hupaswi kuwa na mashaka juu yangu! au, "Unapaswa kuniamini mimi kabisa." Hili si swali la kweli lakini ni njia katika lugha hii ili kufanya wazo imara. Katika lugha nyingi, ina faa zaidi kufafanua hii kama maelezo au taarifa.

31-08

Wakati Yesu na Petro walipoingia kwenye mtumbwi, Upepo

Ingekuwa vizuri zaidi kusema "Petro na Yesu wakaingia kwenye mtumbwi, na baadaye upepo."

Walimwabudu Yesu

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Wakainama chini kumwabudu Yesu." Hili ni neno ni wazo ni kuinama kimwili mbele ya mtu fulani kutokana na heshima na unyenyekevu

Hakika wewe ni mwana wa Mungu.

Njia nyingine ya kusema hii ni, "Wewe kweli ni mwana wa Mungu" au "Ni hakika na ni kweli kuwa wewe ni mwana wa Mungu.