37-01
Siku moja
Maneno haya yanaonesha tukio lililotukia kipindi kilichopita, lakini hayaelezi muda maalumu. Lugha nyingi zinanjia inayofanana katika kuanza kusimulia habari ya kweli.
Mariamu
Mama yake Yesu pia aliitwa Mariamu. Huyu alikuwa ni mwanamke mwingine tofauti na mama yake Yesu.
Ugonjwa huu siyo wa kifo
Hii inaweza kutafsirika kwamba, "matokeo ya ugonjwa huu siyo kifo" au, Lazaro ni mgonjwa, lakini kifo hayatakuwa matokeo kwenye ugonjwa huu." Huenda wanafunzi wa Yesu walifikiri inamaanisha kwamba Lazaro asingelikufa. Lakini Yesu alijua kwamba, ingawaje Lazaro atakufa kutokana na ugonjwa wake mwisho wake atakuwa hai.
Ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu
Hii ni, "hii itawasababisha watu kumtukuza Mungu kwa jinsi alivyo mkuu."
Lakini alisubiri mahali alipokuwa kwa siku mbili
Hii ingelitafasiriwa kuwa, "lakini alibaki mahali alipokuwa kwa siku mbili, hata kama walitaka aende na amponye Lazaro.
37-02
Uyahudi
Hii inarejea sehemu ya kusini mwa Israeli, ambako waliishi kabila la Yuda. Lugha nyingine itapendelea kusema, "mkoa wa uyahudi."
Amelala usingizi, na lazima nimwamshe
Tafasiri kipengele hiki kwa maneno ya kawaida kwenye lugha yako yaani "kulala" na "amka." Ingawa Yesu alikuwa akitumia maneno haya akiwa na maana nyingine, bado wanafunzi hawakumwelewa.
37-03
Atapata nafuu
Wanafunzi walidhani, "hakuna sababu ya sisi kwenda kwake sasa, sababu atapata nafuu."
Nafurahi
Inaweza kutafasiriwa kuwa, "mimi ninafuraha" au, "hiyo ni nzuri." haina maana alikuwa na alifurahia kifo cha Lazaro, lakini zaidi kwamba alikuwa na furaha kwamba Mungu alikuwa aoneshe jinsi alivyo mkuu.
37-04
Martha
Martha alikuwa dada wa Lazaro na Mariamu.
Alikwenda kukutana na Yesu
Hii ni kwamba, "alikwenda kumwona Yesu alipokuwa anakuja mjini."
Kaka yangu asingelikufa.
Hii ni, "ungelimponya kaka yangu na asingelikufa" au, "ungelizuia kufa kwa kaka yangu."
Lolote uombalo toka kwake atakupa
Hii ni, "atanfanya lolote unalomwomba toka kwake."
37-05
Mimi ni ufufuo na uzima
Hii, "mimi" iliyotumika hapa ni kauli mojawapo yenye nguvu sana kati ya kauli zake Yesu anazosema kuhusu uasili wake. Hapa Yesu anaashiria kwamba yeye ni "mpaji" au "chanzo" cha ufufuo na uzima. Ikiwezekana tafasiri maneno haya kwa namna ambayo inaweka wazi umhimu wa asili. Hii inaweza kutafasirika kwamba, "Mimi ndiye hufufua watu na huwapa uzima"
Ataishi hata kama akifa
Hii ni, "hata kama atakufa, ataishi milele." Neno la kiingereza "Yeye" si kwamba linarejea kwa wanaume tu pia wanawake wanaoamini wataishi milele.
Martha
Martha alikuwa dada yake Lazaro na Mariamu.
Hatakufa
Hii inaweza kutafasiriwa kwamba, "ataishi milele."
37-06
Mariamu
Huyu ni mwanamke ambaye siyo mama yake Yesu.
Alianguka miguuni pa Yesu
Hii ni, "alipiga magoti miguuni pa Yesu" ikiwa ishara ya heshima.
Kaka yangu hangelikufa
Ni kwamba, "ungelifanya kaka yangu asife" au, "ungalizuia kifo cha kaka yangu" au, "kaka yangu angelikuwa hai."
37-07
Yeye aliwaambia
Hii ni, "Aliwaambia watu pale." Huenda alikuwa hawaambii Martha na Mariamu kuliondoa jiwe.
Ondoa jiwe
Baadhi ya lugha zitapendelea kusema, "ondoa jiwe kutoka kwenye kaburi."
Martha
Martha alikuwa dada yake Lazaro na Mariamu.
Amekufa kwa siku nne
Hii pia inatafsirika kama, "Alikufa siku nne zilizopita na mwili wake umelazwa pale."
37-08
Mimi sikuwaambia ninyi?
Hili, "kumbukeni kwamba niliwaambia." Si kwamba Yesu anawauliza swali ili apate jibu, hivyo lugha zingine zitatafsiri hii kama amri.
Ona utukufu wa Mungu
Hii ni, "tazama utukufu wa Mungu uliyodhihilishwa" au "tazama Mungu anavyoonesha ukuu wake."
Liondoe jiwe
Baadhi ya lugha zitasema, "liondoeni jiwe mahali pa mlango wa kaburi."
37-09
Unanisikia
Hii ni, ""unanisikiliza." Inaweza kusaidia kuongoza, "kama niombavyo kwako" au, "nizungumzapo kwako."
Njoo nje
Baadhi ya lugha zinaweza kupendelea kusema, "toka nje kaburini"
37-10
Lazaro alikuja kutoka nje
Baadhi ya lugha zitasema, "Lazaro toka kaburini."
Sanda
Hii ni, "nguo za kuzikia" Hii inawea kutafsirika kama, "sanda" au, "vazi maalumu."
Sababu ya muujiza huu
Hii ni, "kwasababu Mungu alishafanya muujiza huu wa kushangaza" au, "kwasababu Yesu tayari alishamfufua Lazaro."
37-11
Wivu
Huo ni "wivu wa Yesu wa nguvu na mashuhuri " au "wivu ambao wayahudi walikuwa wanauamini kwa Yesu."
Kusanyika pamoja
Hiyo ni, "kutana pamoja" au, "unganisha pamoja." huu haukuwa mkutano wa kawaida, lakini ni mkutano maalumu kwa lengo la kupanga jinsi ya kumuua Yesu.