Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

09-01

Waliitwa waisraeli

Kundi la uzao wa Yakobo uliitwa "Israeli" ambalo ni jina alilopewa Yakobo na Mungu. Watu wa kundi lile waliitwa "Waisraeli."

09-02

Farao

"Farao" ni neno la kimisri linalomaanisha kuwa mfalme wao. Yawezekana Farao huyu alikua ni mtoto wa Farao aliyekufa, ambaye ni uzao wa Farao aliyefahamika na Yusufu.

Kuwafanya wana wa Israeli watumwa

Hiyo ni "kuwalazimisha waisraeli kufanya kazi ngumu kinyume na matakwa yao na kuwatumikisha kwa ukatili mbaya."

09-03

Mateso

Hii inamaanisha waliteseka sana kwa sababu ya namna walivyotumikishwa na kulazimishwa kufanya kazi. Walikatishwa tamaa.

Mungu aliwabariki

Mungu aliwajali na kuwawezesha kuvumilia mateso na pia kuwawezesha kuwa wengi kwa kuwapa watoto.

09-04

Kuona

Njia nyingine ya kusema neno hili ni "aligundua" au "alijua."

09-05

Kwa kwadri walivyoweza.

Walimficha mtoto toka kwa waisraeli mpaka ilipokua ngumu kumuweka mtoto katika hali ya usalama nyumbani kwao.

09-06

Mto Nile

Ukweli Nile ni mto uliopo kaskazini mashariki mwa Afrika

Mto Nile unapita Misri na kumwaga maji yake bahari ya Mediteranian. Mazao yalikua vizuri kwenye bonde lenye rutuba wamisri wengi waliishi karibu na Mto Nile kwa kuwa ilikua ni chanzo muhimu cha maji na mazao ya chakula.

09-07

Alimchukua kama mtoto wake

Alikuwa mtoto wa kike wa mfalme. Alipomfanya musakuwa mwanawe, Musa akawa mtoto wa kiume wa mfalme Misri.

Kumlea

Njia nyingine ya kusema hivi ni "kumyonyesha yule mtoto Musa."

09-08

Kukua

Njia nyingine ya kusema hivi ni "akawa mtu mzima"

Muisraeli mwenzake

Aya hii ina maanisha mtumwa wa kiisraeli. Neno "mwenzake" linaonyesha kuwa Musa pia alikua muisraeli. Japokuwa mtoto wa Farao wa Misri alimlea Musa lakini Musa alikumbuka kuwa yeye ni Muisraeli halisi.

09-10

Jangwani

Jangwani ni sehemu kubwa yenye mwamba na kame. Ardhi hiyo sio nzuri kwa kukuzia mazao ya chakula na watu wachache wanaishi hapo.

09-11

Jangwani

Angalia jinsi ya kutafasili hili katika 9-10.

09-12

Alikuwa akichunga kondoo zake

Hii inamaanisha alikuwa akifanya kazi ya kuchunga kwa kuwaongoza kondoo kwenye maji na majani na kuwalinda. Pia inaweza kutafasiriwa kama "kuwahudumia kondoo"

Kichaka hakikuteketea

Mungu alitengeneza kichaka chenye moto lakini moto huo haukuteketeza kichaka kile.

Sauti ya Mungu ikasema

Hii inaweza kutafasiriwa kama, "Mungu akasema kwa sauti kubwa." Musa akasikia Mungu akisema lakini hakumuona Mungu.

Vua viatu vyako

Mungu alimtaka Musa avue viatu vyake ili kuonyesha heshima kwa Mungu. Kuweka sawa sababu ya jambo hili waweza kusema "vua viatu vyako maana upo kwenye ardhi takatifu."

Ardhi takatifu

Ilikuwa takatifu kwa namna ambavyo Mungu aliitenga na ardhi nyingine ya kawaida na kuifanya kuwa ya pekee ambayo anaweza kujidhihirisha.

09-13

Mateso ya watu wangu

Hii inaweza kutafasiriwa kama, "mateso makali ambayo watu wangu wanayapitia. lugha nyingine zinaweza kutafasiri kama "namna wamisri walivyowapa maumivu makali watu wangu".

Watu wangu

Hii inawaelezea wana wa Israeli. Mungu aliweka agano pamoja na Ibrahimu na kizazi chake kuwa atawabariki na kuwafanya kuwa taifa kubwa. Kupitia agano hili wana wa Israeli wakawa watu wake Mungu.

kuwatoa..... nje ya utumwa wao Misri

Hii inaweza kuatafasiriwa kuwa "kuwaweka huru toka kwenye utumwa huko Misri" au "Kuwatoa nje ya Misri walipokuwa watumwa."

09-14

NIKO AMBAYE NIKO

Maelezo haya yanaonyesha kuwa Mungu anaweza kujielezea mwenyewe na sio kwa kitu kingine tunachokifahamu na hawezi kufananishwa na kitu kingine.

MIMI NIKO

Jina hili linasisitiza kuwa ni Mungu pekee aliyekuwepo kabla na ataendelea kuishi.

Jina langu

Jina ambalo Mungu alimwambia Musa na wana wa Israeli wote wamuite ni "Yahweh" linalofanana na "MIMI NIKO" lenye maana "YEYE YUKO".

Jina langu

Jina ambalo Mungu alimwambia Musa na wa Israeli wote kwa kutumia kwa ajili yake ni "Bwana," ambayo ni kuhusiana na "MIMI NIKO" na inaonekana kumaanisha, "NDIYE."

Watu

Tazama tafasiri katika 09:13

09-15

aliogopa na hakutaka kwenda

Musa alijua kuwa Farao alitaka kumuua na hakuamini kama ataweza kufanya mambo ambayo Mungu alitaka ayafanye.

Kaka yake na Musa

Haruni alikua kaka yake na Musa toka kwa mama na baba wa kiisraeli. Haruni alikua na miaka mingi zaidi kuliko Musa.

Msumbufu

Hii inamaanisha Farao alikataa kumtii Mungu. unaweza pia kuongeza "alikua msumbufu na hakukubali kusikiliza (au hakutii)"