26-01
Baada ya kushinda majaribu ya shetani, Yesu alirudi
Unaweza kuliweka jambo hili katika sentensi mbili na kusema, " Yesu hakufanya mambo mabaya ambayo shetani alijaribu kumshawishi kufanya na kwa hiyo alimshinda. Na baada ya hayo, Yesu alirudi." Neno "kushinda" linaweza pia kutafasiriwa kwa " Kupinga" au "Kukataa" au "Kutokubali"
Katika Nguvu ya Roho Mtakatifu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Wakati nguvu ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi ndani yake" au " Na Roho Mtakatifu alikuwa akimwongoza kwa nguvu."
Alikwenda kila mahali akifundisha
Hii ni kwamba, "Alisafiri kwenda miji tofauti na sehemu zingine na akafundisha watu pale."
Kila mmoja
Hii ni kwamba, "Kila mmoja aliye mjua au kusikia habari zake."
Alimsema vizuri
Hii ni kwamba, "Alisma mambo mema juu yake."
26-02
Mahali pa ibada
Hii ni, "Jengo ambalo wayahudi walikusanyika kumwabudu Mungu." Hii pia inaweza kutafsiriwa kama jengo la ibada."
Gombo
Gombo lilikuwa ni karatasi ndefu au ngozi ambayo ilikunjwa ambayo ilikuwa na maandishi juu yake.
Gombo la nabii Isaya
Hii ni, " Gombo ambalo lilikuwa na maneno ambayo nabii Isaya alikuwa ameandika." Isaya alikuwa ameandika juu ya gombo mamia ya miaka kabla. Hii ilikuwa ni nakala ya gombo hilo.
Alifungua gombo
Hii inaweza kutafsiliwa kama, "Alifungua gombo" au, "Alilikunjua gombo.
26-03
Tangaza habari njema kwa masikini
Hii ni, "Waambie masikini na wahitaji habari njema kwamba Mungu atawasaidia."
Uhuru wa ufungwa
Hii ni, Kuwaambia watu ambao ni wakosaji kifungoni kwamba wataachiliwa."
26-04
Maneno niliyosoma mbele yenu yanatokea sasa
Njia zingine za kutafsiri hii zingekuwa, "Maneno ambayo umeyasikia nikiyasoma yametimilika sasa" au "Leo maneno niliyoyasoma kwenu yametimi kama mlivyoyasikia."
26-05
hakuna nabii anayekubalika katika mji wa kwao
Sentensi hii inamaana, "watu hawatambuwi mamlaka ya nabii aliyekulia katikati yao."
26-06
Elisha
Elisha alikuwa nabii wa Mungu ambaye alikuja baada ya Eliya. Kama vile Eliya, Elisha aliwakabili wafalme wa waisrael ambao walifanya dhambi dhidi ya Munguna alifanya miujiza ambayo Mungu alimpa uwezo wa kuifanya.
kamanda
Huyu ni "kiongozi wa jeshi."
wakawa na hasira juu yake.
Wayahudi hawakupenda kusikia kuwa Mungu amebariki kundi la watu wowote isipokuwa waowenyewe, kwahiyo wakawa na hasira kwa kile ambacho Yesu alifanya.
26-07
mahali pa kuabudia
Hii ni, "nyumba ambayo wayahudi walikusanyika kumwabudu Mungu." hii pia inaweza kutafsiriwa kama " Nyumba ya ibada."
Lakini Yesu akaondoka Mbele yao
"Lakini" inaweza kutafsiriwa kwa neno zito la kukanusha au sentensi kam vile "Lakini badala yake" au, "Hatahivyo" kuonesha kwamba watu hawakuweza kufanya lolote walilolipanga kumfanyia Yesu.
26-08
alienda mpaka mkoa wa Galilaya
Hii ni kwamba, "Sehemu zote katika galilaya" au, kutoka mali hadi mahali pengine katika Galilaya
26-09
waliokuwa na mapepo ndani yao
Hii ni, "ambao walitawaliwa na roho za kiovu."
Yesu alipo waamuru.
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " wakati Yesu aipotoa amri kwao."
26-10
walijifunza kutoka kwake.
Hii ni kwamba, "walijifunza kutoka katika yale aliyowafundisha" au, "walijifunza katika yote aliyosema na kutenda."