40-01
walimpeleka
Hii ni, " walimlazimisha kwenda naye." Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "walimchukua."
Kumsulibisha
Hii ni, "Kumuua juu ya msalaba."
40-02
Fuvu
Mlima uliokaribu na Yerusalemambao una mawe meupe juu yaliyo mithili ya sehemu ya juu ya fuvu.
Wasamehe, kwa sababu hawajui watendalo
Hii ni, "Hawajui maana ya jambo ambalo wanalifanya, kwa hiyo tafadhali wasamehe." Maaskari walidhani kuwa Yesu alikuwa mharifu aliyestahili kufa. Hawakuelewa kuwa alikuwa mwana wa Mungu.
40-03
Wlipigia kura mavazi ya Yesu
Hii inamaana, "walifanya mchezo wa bahati ya kushinda nafasi ya kuchukua mavazi ya Yesu." Hatujui jinsi gani walifanya haya, lakini katika baadhi ya tamaduni indeweza kutafsiriwa kama, "kutupa mawe kwenye ardhi kwa ajili ya kujishindia mavazi ya Yesu" au, "Kuchagua vijiti ili kuamua nani angeweza kushinda kuchukua mavazi ya Yesu."
Walitimiliza unabii amabao ulisema
Hii ni, "Walifanya kile ambacho maandiko yalitabiri muda mrefu uliopita kuhusu jambo ambalo lingetokea kwa Masihi." au, "Walifanya jambo ambalo nabii aliandika muda mrefu uliopita."
40-04
Wanyang'anyi wawili
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "majambazi wawili" hawa ni watu ambao ni wahalifu ambao walitumia nguvu kuiba vitu.
Je huna hofu ya Mungu?
Mwizi hategemei jibu la swali hili, ni njia ambayo baadhi ya lugha hutumia kuweka sentensi yenye mkazo. kama lugha yako haitumii maswali kama ilivyo hapa, hivyo tafsiri jambo hili kama, "Lazima uwe na hofu ya Mugu!"
Sisi tunahatia lakini mtu huyu hana hatia
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "wewe na mimi tumefanya mambo maovu na tunastahili kufa, lakinimtu huyu, Yesu, hajafanya kitu chochote kibaya na hastahii kufa," "sisi" neno hili linajumuisha wezi, lakini halijumuishi Yesu.
Mtu huyu
Sentesi hii inamaanisha Yesu.
Tafadhali unikumbuke
Hii inamaana, "Tafadhari nipokee" au, Tafadhali nikaribishe" au, "niruhusu niwe pamoja na wewe." "Kumbuka" mahali hapa halimaanishi kukumbuka jambo baada ya kulisahau. Tafsiri jambo hili katika njia ambayo itawasilisha ombi la kumsihi mtu.
Katika ufalme wako
Hii ni, Wakati utakapo simamisha ufalme wako" au, "wakati unatawala kama mfalme."
Paradiso
Hili ni jina lingine la "Mbinguni"
40-05
Tutakuamini
Hii ni, "Tutakuamini" au, " Tutaamini kuwa wewe ni Masihi."
40-07
Imekwisha
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "imekwisha" au, imemalizika" au, "Nimeimaliza" au, "nimemaliza kazi." Hii inamaana kazi ya Yesu ya wokovu ilikuwa imemalizika.
Mikonono mwako
Hii inamaana, "chini ya uangalizi wako"
Akainamisha kichwa
Hii inamaana aliinama kichwa chake."
Akaitoa roho yake
Hii ni, " aliitoa roho yake kwa Mungu" au, "aliikabidhi roho yake kwa Mungu na akafa."
Pazia kubwa
Hii ilikuwa nguo ya kitambaa kubwa, imara imening'inizwa hekaluni. Ilikuwa kama ukuta uliotenganisha chumba kimoja na kingine. Inaweza pia kutafsiriwa kama, pazia nene" au, "nguo ya kitambaa iliyo ning'inizwa" au, " chandarua , ngao."
40-08
Kupitia kifo chake
Hii ni, "Kwa njia ya kifo chake" au, "kwa kufa kwake."
Alifungua njia
Hii ni, " alifanya iwezekane."
Kuja kwa Mungu
Hii ni, " kuja karibu na Mungu" au, " nenda karibu na Mungu" au, "karibia Mungu" au, "kumjua Mungu ki- binafsi." Kuchanika kwa pazia kulionesha kwamba kizuizi kati ya Mungu na watu kimeondolewa.
40-09
Yusufu
Huyu hakuwa ni mume wa Mariam. Alikuwa ni mtu mwingine aliye itwa Yusufu.
Alimuomba Pilato auchukuwe mwili wa Yesu
Hii ni kwamba, "alimuomba Pilato awaruhusu kuuchukua mwili wa Yesu kutoka msalabani."