Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

22-01

Watu wake

Hii ingeweza kuwa imetafsiriwa kama, "watu wake wa Israeli "au" watu wake, Wayahudi." Lakini inajumuisha maelezo ya nyongeza kama haijaeleweka watu hawa walikuwa wakina nani.

Miaka 400 iliopita

Namna nyingine ya kusema hili ingekuwa," miaka 400 ilipita," au hii ilikuwa miaka 400." Miaka 400 ilikuwa imepita tangu Malaki, nabii wa mwisho katika agano la kale.

Wakati hakuongea nao.

Hiki ni ,"kipindi ambacho Mungu hakukuwapa jumbe manabii wake kwa ajili ya watu wake."

Watu wanaomcha Mungu

Ni kwamb,a "watu waliomtii Mungu."

22-02

Malaika

Hii inamaanisha malaika aliyekuja kwa Zakaria ".

Aliyejazwa na Roho Mtakatifu

Ni kwamba," aliyeongozwa na Roho Mtakatifu "au" aliyepewa hekima na nguvu na Roho Mtakatifu."

Ninawezaje kujua hili litatokea?

Njia nyingine ya kutafsiriwa ni, "Ninawezaje kuwa na uhakika kwamba hili litatokea kweli?"

22-03

Kuwa mjamzito

Baadhi ya lugha zingine zina njia zenye adabu na kusema ,"kuwa mjamzito" Tumia maelezo ambayo hayatawadhalilisha wasomaji.

22-04

Mimba ya miezi sita

Alishakuwa tayari na ujauzito wa miezi sita au alikuwa ndani ya miezi sita ya mimba yake.

Mjamzito.

Lugha tofauti zina tamaduni tofauti za kuongea kuhusu ujauzito,kama alikuwana mtoto,"au"alikuwa na mmoja kwenye mwili wake au "alikuwa na tumbo."Baadhi ya lugha zina njia za kipekee zenye adabu ,kama anatarajia."Tumia maelezo ya kwamba ambayo hayatawadhalilisha wasomaji.

Elizabeth.

Alikuwa mke wa Zakaria.Malaika alimwambia Zakaria kwamba Elizabeth angejifungua mtoto mwanaume.

Jamaa ya Elizabeth

Tafsiri nyingi zinasema" binamu" lakini hapa hatuwezi kujua kwa uhakika namna gani hawa wanawake wawili walirandana.Neno la jumla kama" jamaa"au "binamu 'litaweza kuwa limetumika.

Alikuwa amechumbiwa .

Ni kwamba ilikuwa ahadi.

22-05

Namna gani hii inaweza kuwa.

Ni kwa kwamba "Namna gani naweza kuwa mjamzito?"Mariamu hakuwa na mashaka na ukweli wa maneno ya malaika ,lakini anauliza inawezaje kutokea.

Roho Mtakatifau atakujia na nguvu ya Mungu itakufunika

Hizi ni njia mbili zinasema kitu kimoja." Kwa nguvu ya Mungu,Roho Mtakatifu atakusababisha kwa muujiza uwe mjamzito."Akikisha tafsiri ya maneno haya hayatamkwi kama kulikuwa mawasiliano yoyote ya kimwili yaliyojumuishwa.Hii ilikuwa muujiza.

22-06

Elizabethi

Angalia maelezo kuhusu Elizabeti

Upesi Elizabeti aliposikia salamu yaMariamu

Kwa baadhi ya lugha zingine ingekuwa vizuri kusema,"Mariamu alipomsalimia Elizabeti na ghafla Elizabeti alimsikia.

Kichanga kiliruka ndani yake

Kichanga kilisogea haraka ndani ya tumbo la Elizabeti na kujibu salamu ya Mariamu .

Nini Mungu alifanya kwao

Hii inarejea kwamba wanawake wote wawili walikuwa wajawazito kupitia uwezo wa kimungu .Mariamu alibeba mimba bila mwanaume,na Elizabeti alibeba mimba na Zakaria baada ya kupitisha muda wa kuzaa mtoto.

22-07

Elizabeti

Angalia maelezo kuhusu Elizabeti

Mungu asifiwe

Ni kwamba ,"Wote tunaweza kumsifu Mungu."

Ataitwa

Hii ni njia nyingine ya kusema",ingekuwa ,"au'itajulikana kama,Kwa hakika Yohana aliweza kuwa nabii wa Mungu aliye juu.

Nabii

Ni kwamba ,"nabii muhimu sana"Yohana angekuwa nabii ambapo agano la kale manabii waliotabiriwa wangekuja kabla ya masihi.

Mungu mkuu

Njia nyingine kusema hii ingekuwa Mungu ambaye ni mkuu sana kuliko vitu vyote" au "Mungu ambaye anatawala juu ya kila kitu."