28-01
Sikumoja
Sentensi hii inatoa utangulizi wa jambao ambalo lilitokea nyakati za nyuma, lakini halielezi muda maalumu. Lugha nyingi zina namja hii ya kuanza kueleza simulizi ya kweli.
Kiongozi kijana tajiri
Huyu kijana alikuwa tayari ni tajiri na kiongozi mwanasiasa mwenye nguvu, ingawa alikuwa bado ni kijana.
Alimwendea Yesu
Hii ni kwamba alimfuata Yesu
Mwalimu Mwema
Hii inamaanisha "Mwalimu mwenye haki" Alikuwa hamaanishi kuwa Yesu alikuwa tu ni mwalimu aliye pitia mafunzo.
Kuwa na uzima wa milele
Hii ni kwamba, "Kupokea uzima wa milele" au. "Kuishi na Mungu milele na milele."
Kwa nini kuniita "mwema"
Yesu hakatai kuwa yeye ni Mungu, isipokuwa anamuomba mtawala kuelewa kuwa Yesu ni Mungu.
Kuna mmoja tu aliye mwema, na huyo ni Mungu
Njia nyingine ya kusema hili ingelikuwa, "Aliye mwema kweli kweli ni mmoja tu ambaye ni Mungu." au, "Mungu ndiy pekee aliye mwema kweli kweli."
28-02
Ni mambo gani nahitaji kutii?
Hii ni kwamba, "Ni sheria gani zitakazo tosheleza mimi kupokea uzima wa milele?"
Kama unavyo jipenda mwenyewe
Hii ni kwamba, "kadiri unavyo jipenda mwenyewe" au, "kiwango kile kile unacho jipenda mwenyewe,"
28-03
Tangu nikiwa kijana
Njia nyingine ya kusema hili ingekuwa, "kuanzia wakati nilipo kuwa mtoto hadi sasa."
Jambo gani ambalo bado napaswa kulifanya?
Hii ni kwamba, "Nini zaidiambacho nahitajika kukifanya" au, Nahitaji kufanya nini kama nyongeza ya haya niliyokwisha fanya?"
Akampenda
Yesu alimuhurumia. chagua nenolinalo maanisha upendo ambao unalingana na ule upendo ambao Mungu anao kwa watu.
28-04
Wewe
Kama lugha yako ina neno tofauti na "wewe"kutegemeana na idadi ya watu waliokusudiwa, tumia hali ya umoja.Yesu alikuwa anasema amri hii kwa mtu huyu mmoja.
Mkamilifu
Hii inamaana, "mtu wa haki kabisa."
Kila kitu unachomiliki
Hii ina maana, "kilakitu ambacho ni mali yako."
Hazina
Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "utajiri" au, utajiri mwingi"
Mbinguni
Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, " iliyo mbinguni wakati utakapofika pale," kinyume na utajiri ambao Yesu alimwambia kijana kuutoa "hapa na sasa."
28-05
Aliposikia alicho kisema Yesu
Hii ni kwamba, aliposikia Yesu akimwambia kutoa alivyo kuwa navyo."
28-06
Kuingia katika ufalme wa Mungu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kufanyika raia katika ufalme wa Mungu."
Ngamia
Ngamia ni wanyama wakubwa ambao maranyingi wanatumika kubeba mizigo mizito. ikiwa ngamia hawajulikani katika lugha ya eneo lako,sentensi kama,"Myama mkubwa sana" au, Mnyama wa mzigo" linaweza kutumika. ikiwa utachgua kutumia mnyama mkubwa badala ya ngami, hakikisha kuwa mnyama unaye mtumia anajulikana na watu kama vile watu ambao Yesu alizungumza nao walivyo mjua mnyama. kama vile , "Punda."
Tundu la sindano
Hii inarejea kwenye tundu dogo mwishoni mwa sindano ya kushonea nguo. Wazo la kitu kikubwa kama ngamia kupita katika tundu la sindano imekusudiwa kuwakilisha jambo ambalo haliwezekani.
28-07
Shikwa na mshangao
Hii ni hali ya, "kustajabisha
Nani anaweza kuokoka
Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "ikiwa watu matajiri hawezi kuokoka, nji jinsi gani mtu wingine yeyote anaweza kuokoka?" Watu wengi waliamini kuwa kuwa tajiri ni dalili ya kupata upendeleo wa Mungu.
Okoka
Hapa inarejea katika hali ya kuokoka katika hukumu ya Mungu na hukumu ya dhambi na kuruhusiwa kuwa raia katika ufalme wa Mungu.
28-08
"Kwa watu mambo haya hayawezekani
Hii ni kwamba, haiwezekani kwa watu kufanya hivi" au, watu wenyewe hawawezi kujiokoa wenyewe."
kwa Mungu mambo yote yanawezekana".
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "Mungu anaweza kufanya jambo lolote, hata kuokoa mtu tajiri" au, Mungu anaweza kufanya mambo yasiyowezekana, kwa hiyo anaweza kuokoa hata mtu tajiri."
28-09
Tumeacha kila kitu
Hii ni kwamba, kuachana na mambo yote" , au, kuachilia vitu vyote tulivyo miliki."
Je, tutapata thawabu gani?"
Njia nyingine ya kusema hivi ni, " ni zawadi gani tutapokea" au, Ni jinsigani tutazawadiwa?" inaweza pia kuwa muhimu kuongeza, kwa sababu tumefanya hivi?"
28-10
Aliye acha
Hii ni mtu "aliye acha" au, " aliye achana " au,"aliye hesabu jambo kutokuwa la muhimu kuliko Mungu.
Kwa ajili yangu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Kwa sababu yangu" au, kwa ajili yangu."
Mara 100 zaidi
Hii inamaana, "zaidi sana kuliko alivyo kuwa navyo mwanzoni."
Wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho
Hii ni, " watu ambao ni wa muhimu sasa, hawata kuwa wa muhimu baadaye."
Wengi wa mwisho watakuwa wa kwanza
Hii ni kwamba, wale wanaofikiriwa kuwa si wa muhimu duniani watafikiriwa kuwa wa muhimu mbinguni" au, "watu wengi ambao wanadhaniwa sasa kuwa na thamani ndogo hapa duniani watathaminiwa zaidi mbinguni."