Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

29-01

Siku moja

Sentensi hii inatoa utangulizi wa tukio lililo tokea wakati ulio pita, ingawa halielezi muda maalumu. Lugha zilizo nyingi zinanamna hii hii ya kueleza simulizi iliyo ya kweli.

Ndugu yangu

Neno hili mara nyingine lilihusisha watu amabo hawakuwa ndugu wa damu, lakini ambao walikuwa na mahusiano thabiti kama vile mahusiao ya ki dini, kabila, n.k.

Ndugu yangu akinikosea

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, ambaye amefanya jambo baya kwangu."

Si maa saba, bali sabini mara saba!

Hii inaweza kutafsiriwa kama, " hupaswi kusamehe mara saba tu, bali unapaswa kusamehe sabini mara saba." Yesu alikuwa hamaanishi idadi kamili ya matukio ya kusamehe. alimaanisha kuwa lazima kuwasamehe watu mara kwa mara wanaotukosea.

Kwa hili Yesu alimaanisha

Hii ni, "wakati Yesu aliposema hili alimaanisha."

29-02

Ufalme wa Mungu unafananishwa

Njia nyingine ya kusema hivi ingekuwa, " utawala wa Mungu kwa watu wake unafanana"au, " Jinsi Mungu anavyotawala watu inafananishwa na."

mfalme alie

Hii kutafsiriwa kama, "Ni kama ufalme wa mfalme ambaye" au, "unaweza kulinganishwa na utawala wa mfalme ambaye."

Tengeneza hesabu pamoja na mtumwa wake

Hii ni kwamba, "kusanya madeni yote ya watumwa wanayodaiwa" au, "kusanya fedha kutoka kwa watumwa ambazo waliazima.

29-03

kulipa deni,

Hii ni, "lipa pesa alizodaiwa na mfalme."

kulipa deni lake.

Hii inaweza kutafsiriwa kama, tumia pesa uliyopokea kutokana na mauzo na ulipe sehemu ya deni ninalokudai."

29-04

alianguka na kupiga magoti

Hiini kwamba, " kwa haraka alipiga magoti chini juu ya ardhi."hii ilikuwa ni njia ya kuonesha unyenyekevu na haja yake kwa mfalme kumsaidia. Hakikisha kwamba isije ikaonekana kana kwamba alianguka chini kwa bahati mbaya.

Mbele ya mfalme

Hii ina maana. " mbele ya mfalme"

Alimuonea huruma

Hii inamaana, "kuwa na huruma" Kujisikia kuumia. Mfalme alijua kuwa mtumwa pamoja na familia yake watateseka sana iwapo wangeuzwa utumwani.

akafuta deni lake lote

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "alisema kuwa mtumwa hakuhitaji kulipa pesa yoyote aliyokuwa anadaiwa na mfalme."

29-05

mtumishi mwenzake

Hii inarejea kwa mtu mwingine ambaye pia alikuwa mtumishi wa mfalme.

29-06

mtumishi mwenzake

Tafsiri sentensi hii sawa sawa na 29:5.

kupiga magoti

Sentensi hii inamaana sawa na 29: 4.

alimtupa mtumishi mwenzake ndani ya gereza

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "alitaka yule mtu atiwe gerezani." "Neno tupa" ni mfano unao maanisha ilifanyika kwa njiaya ulazima.

29-07

kilicho tokea

Hii ni kwamba, " mtumishi alikataa kufuta deni la mtumwa mwingine na akamuweka kifungoni."

walifadhaika sana

Hii ni kwamba , " walifadhaika sana."

29-08

alimwita yule mtumishi

Hii ni kwamba, " alimuamru mtumwa kuja kwake" au aliwaamuru walinzi wake kumleta mtumishi kwake."

Ulinisihi

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "alinisihi" au, kwa haraka aliniomba niwe mwenye rehema."

ungefanya vivyo hivyo

Hii ni kwamba, "ungelimsamehe yule mtu aliye kudai kama vile mimi nilivyo kusamehe wewe."

Kumtupa

Hii ni kwamba, "alimuamuru mlinzi wake kumweka."

29-09

Ndipo Yesu akasema

Lugha zingine zingeongeza, " kwa wanafunzi wake."

Hivi

"Hivi" inarejea katika namna mfalme alivyo muadhibu mtumwa asiye samehe.

Baba yangu wa mbinguni

Hii ni, " Baba yangu aliye mbinguni."Yesu anaeleza uhusiano wake wa kipekee kwa Mungu baba.

Ndugu zenu

Hii inafanana na neno lililo tumika katika 29:1

Kutoka moyoni

Hii ni kwamba, "kwa dhati" au, "kweli" au, "halisi" au, "kwa uaminifu."