15-01
Hatimaye ulifika wakati wa
"Hatimaye" inamaanisha "Mwishowe" au "baada ya kungoja kwa muda mrefu."
Wapelelezi wawili kwenda Yeriko mji wa Kanaani
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "watu wawili kwenda Yeriko, mji wa kanaani, kutafuta habari za mji huo."
umelindwa kwa kuta imara
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "umelindwa kwa kuta nene, imara zilizojengwa kwa mawe kuwakinga dhidi ya adui zao."
toroka
Ni sawa pia kuongeza, "toroka kutoka kwa watu ambao walitaka kuwadhuru huko Yeriko."
familia yake
Rahabu aliomba ulinzi kwa kwa ajili ya baba, mama, kaka, na dada zake. Tumia neno katika lugha yako ambalo linajumuisha watu hawa.
15-02
Makuhani waanze kwenda kwanza
kwa baadhi ya lugha inaweza kusaidia ukiongeza, "Waache Makuhani watangulie kuvuka mto kwanza kabla ya watu wengine."
mkondo wa maji ukasimama kutiririsha maji
Kwa baadhi ya lugha inaweza kusaidia ukiongeza, "na maji yaliyokuwa mbele yao yalitiririka kwenye chini."
15-03
Baada ya watu kuvuka mto Yorodani
Kwa baadhi ya lugha ni vyema kusema, "Watu walivuka mto Yorodani na kisha..."
jinsi ya kuvamia
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "uhalisia wa namna ambavyo angefanya ili kuvamia."
mara moja kila siku kwa muda wa siku saba
Hii ni kwamba, waliuzunguka mji mara moja kila siku kwa muda wa siku saba.
15-04
wakati walipotembea kuuzunguka mji kwa mara ya mwisho
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "Wakati wa mzunguko wao wa mwisho kwenye mji ule."
walipuliza tarumbeta zao
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "Walipiga tarumbeta zao" au, "walicheza tarumbeta zao."
15-05
alifanyika kuwa sehemu ya
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "ambao baadaye waliungana na jamii ya Israeli" au, "ambaye baadaye walifanyika kuwa sehemu ya taifa la Israeli."
15-06
makubaliano ya amani
Haya ni makubaliano baina ya makundi mawili ya watu kwamba wataishi kwa amani.
Lakini kundi moja la Wakanaani lililoitwa Wagibeoni
Baadhi ya lugha zinaweza kuanza na, "Lakini siku moja kundi moja la Wakanaani waitwao Wagibeoni..."
walimdanganya Yoshua wakisema
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "Walimdanganya Yoshua kwa kusema..."
ni wapi Wagibeoni wametokea
Kwamba, "Wagibeoni walikoishi" au, "yalipokuwa makao ya Wagibeoni."
15-07
wakatuma ujumbe kwa Yoshua wakiomba msaada
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "waliwatuma baadhi ya watu wao kumwambia Yoshua kuwa walihitaji Waisraeli wawasaidie kujikinga na maadui."
15-08
kuwafikia Wagibeoni
Kwamba, "kufika kwa Wagibeoni" au, "kufika mahali ambapo Wagibeoni waliishi." Wagibeoni waliishi Kanaani, lakini Kanaani ilikuwa kubwa kiasi kwamba jeshi la Israeli lilisafiri usiku kucha kufika mahali walipokuwa Wagibeoni.
wakawashitukiza majeshi ya Waamori
Waamori hawakujua kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja kuwavamia.
15-09
Mungu akaipigania Israeli
Mungu alikuwa upande wa Israeli dhidi ya adui zao
akasababisha Waamori kuchanganyikiwa
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "aliwafanya Waamori wahamaki"
mawe makubwa ya mvua
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "mapande makubwa ya barafu yalianguka chini kutoka angani."
15-10
Mungu
Katika Biblia, neno "Mungu" humaanisha nafsi ya milele aitwaye "Yahweh," ambaye aliumba ulimwengu pasipo kitu. Yahweh ana nafsi tatu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu
Israeli
Israeli ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Israeli maana yake ni, "Alipambana na Mungu." Kizazi cha Yakobo walijulikana kama watu wa Israeli, taifa la Israeli, au Waisraeli.
Waamori
Waamori walikuwa kikundi cha watu walioishi Kanaani kipindi cha Yoshua. Waamori waliishi katika miji ya karibu na mto Yorodani. Kila mji uliongozwa na mfalme. Mungu aliahidi kuwapa Israeli ardhi ya Kanaani pamoja na ardhi ya Waamori.
15-11
wakawavamia na kuwaangamiza
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "walipigana nao na kuwashinda."
15-12
Mungu alitoa...ardhi
hii inaweza kutafasiriwa kama, "Mungu aliwapa kila kabila kipande cha ardhi"
akaipa Israeli amani kwenye mipaka yake yote
hii inaweza kutafasiriwa kama, "Mungu aliwafanya Waisraeli kupata amani na makundi ya watu waliowazunguka" au, "nchi nyingine katika Israeli."
15-13
Wakati Yoshua alipokuwa mzee
Inaweza kueleweka zaidi ukisema, "Miaka mingi baadaye, wakati yoshua alikuwa mzee." Yoshua alikuwa na zaidi ya miaka 100 kwa kipindi hiki.
kubaki kuwa waaminifu kwa Mungu
kwa maneno mengine, wangekuwa watii kwa Mungu. Wangemwabudu na kumtumikia Mungu pekee; wasingeabudu au kutumikia miungu mingine.
kuzifuata sheria zake
Hii inamaanisha kwamba watu wangetii sheria ambazo Mungu aliwapa hapo kwanza kama sehemu ya agano.