Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

23-01

Alijua hakuwa mtoto wake

Ni kwamba,"alijua kwamba si ye mmoja ambaye alisababisha yeye kuwa mjamzito."

Kumuabisha Mariamu

Ni kwamba ,"kusababisha Mariamu kufedheheka au," kumdhalilisha Mariamu katika jamii ,"Yusufu alikuwa mtiifu kwa Mariamu hata hivyo ingeonekana kama alikuwa kwenye uzinzi.

Alipanga kwa siri kumuacha

Hii inaweza ikatafsiriwa kuwa alipanga kumuacha bila kuwambia wengine kwa nini" ,au alipanga kumuacha yeye bila kuwaambia wengine kuhusu ujauzito wake ."Kwa sababu Yosefu alikuwa mwenye haki, alitaka kutatua hali hiyo kwa njia nzuri inayowezekana, ambayo ndani ya tamaduni inaweza kumpa talaka kwa siri.

Kumuacha

Kwa baadhi ya lugha zingine ingekuwa vizuri kusema,"kuvunja uchumba"au Yusufu na Mariamu walichumbiana au,"waliahidiana kuoana," Lakini utamaduni wa Kiyahudi kuchana ilikuwa inatakiwa ili kuvunja uchumba.

Kwenye ndoto

Ni kwamba,wakati alikuwa amelala na ndotoni"

23-02

Usogope kumchukua Mariamu kama mkeo

Hii pia iliweza kuwa imetafsiriwa hivi,Acha kufikiri hutaweza kumuoa Mariamu"au,"Usisite kuwa na Mariamu kama mke wako."

Ni kutokana na Roho Mtakatifu

Ni kwamba,"alibeba mimba kwa muujiza wa Roho Mtakatifu."

23-03

Hakulala naye

Ni kwamba ,"hakushiriki tendo la ndoa naye."Alitunza ubikira wake mpaka kuzaliwa kwa mtoto.

23-04

Wakati muda ulipofika wa Mariamu kuzaa

Ni kwamba,"Wakati ulipokaribia mwisho wa ujauzito wa Mariamu."

Serikali ya Kirumi

Rumi ilikuwa imeteka na kutawala juu ya Israeli kwa wakati huu.

Kwa ajili ya Sensa

Ni kwamba Kuwa wamehesabiwa kwa ajili ya kunakili."au,"Kwamba serikali iweze kuandika majina yao kwenye orodha "au wawe wamehesabiwa na serikali."Sensa hii ilikuwa haswa inafanywa kwakusudi la kuwatoza watu kodi.

23-05

Hakuna nafasi ya kukaa

Ni kwamba ",hakuna nafasi ya kawaida ya kukaa".Kwa sababu Bethlehemu ilijaa watu wengi kwa wakati ule.vyumba vya kawaida kwa wageni tayari vilishajaa.

Eneo ambalo wanyama waliishi.

Hili lilikuwa ni eneo la kulaza wanyama,siyo eneo waliloishi watu.Tafsiri hili kwa neno kwamba lilikuwa kwa kawaida eneo la kulishia wanyama.

Hori la kulishia

Ni kwamba ,"boksi la kulisha wanyama"au,la mbao,au boksi la jiwe kwa ajili ya kulishia wanyama."Boksi lilokuwa limejazwa na nyasi kavu kupatia nyasi laini usoni kwa mtoto kulazwa chini.

23-06

Wakichunga mifugo yao

"Mifugo" ni kundi la kondoo wachungaji walikuwa wakilinda kondoo ,na kuwalindaa kutoka wezi.

Mng'ao wa malaika

Hii ingeweza pia kuwa imetafsiriwa hivi,"malaika alizungukwa na mwanga mkali."Mng'ao wa mwanga ulionekana kama mwanga unaoshabihiana na giza la usiku.

Waliogopa

Kutokea kwa malaika mwenye nguvu ya ki

Msiogope.

Hii mara zote humaanisha ,"acha kuwa na mashaka."Wachungaji walikuwa na mashakawakati walipomuona malaika alikuwa akiwaambia hamhitaji kuwa na wasiwasi.

23-07

Hori la kulisha

Ni kwamba,"Boksi la kulishia wanyama."Pia angalia namna hii ilivyotafsiriwa

Alifungwa kwenye vipande vya nguo.

tamaduni za wakati huo zilikuwa kuwabana watoto wanaozaliwa ndani nguo ndefu .Ingeweza kuwa muhimu kusema,alifungwa kwenye nguo ndefu zinazotawala ndani ya njia za kitamaduni."

Walijazwa na malaika

Hii inaamaanisha kwamba pale palikuwa na malaika walioona kujaa kwa mawingu

Utukufu kwa Mungu

Hii inaweza kuwa imetafsiriwa ,"Acha tumpe Mungu utukufu!"au"Mungu anastahiliheshima yote na utukufu!"au,Wote tumpe utukufu Mungu!"

Amani duniani

Njia nyingine kusema hii ingeweza kuwa," amani iwepo duniani ,"

Watu aliowaridhia

Hii iwe imetafsiriwa hivi,'watu ambao Mungu huwaangalia juu kwa kuwaridhia furaha ,au kuwapa matumaini mema."

23-08

Yote waliyosikia na kuona

Ni kwamba ," kwa kila kitu walichosikia na kuona."Hii inajumuisha Malaika wa utukufu na ujumbe wa ajabu pamoja kuona

23-09

Baadaye

Haikuwa sahihi ni muda gani ulikuwa baada ya kuzaliwa mtoto kabla wenye busara alipoiona nyota, lakini inaweza kuchukua muda wa miaka miwili kwa wao kujianda kwa safari na kusafiri kwenda Bethlehemu.

Wenye busara

"Wenye busara" walikuwa waganga ambao wamesoma nyota , Pia walikuwa na uwezo wa kuwa manabii katika agano la kale waliandika na kutabiri kuzaliwa kwa masihi

Nyota isiyo ya kawada

Nyota waliyotaarifiwa haikuwa nyota ya kawada.Ilikuwa ni kitu ambacho kilitokea muda aliozaliwa Yesu .

Waligundua

Baadhi ya lugha zinaongeza kutoka katika masomo yao,hawa wanafunzi waligundua."

Nyumba

Hawakukaa tena kwenye eneo la wanyama ambapo alizaliwa.

23-10

Wenye busara

Wenye busara

Wakainama

Ni kwamba,'"wakainama chini kwenye ardhi,"wakati huo hii ilikuwa desturi ya kuonyesha heshima kubwa au kuheshimu

Ya ghali

Ni kwamba,"yenye dhamani sana."