Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

45-01

Kanisa la kwanza

Hili ni, "Kanisa wakati lilipo anza."

Alikuwa na tabia nzuri

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "aliye kuwa anatazamwe vizuri na watu." Lugha zingine zinaweza kutafsiri hii kama, "alikuwa na jina zuri."

Alikuwa amejaa roho mtakatifu na hekima

Hii ninaweza pia kutafsiriwa kama, "alikuwa na nguvu na uwezo kutoka kwa Roho Mtakatifu na alikuwa na hekima nyingi" au, "alijaa Roho Mtakatifu na alikuwa mwerevu."

Toa hoja kwa ushawishi

Hii ni, "kutoa sababu zenye kushawishi kwa nini."

45-02

Siku moja

Hii sentensi inatoa utangulizi wa tukio ambalo limetokea wakati ulio pita, ingawa halielezi muda maalumu. Lugha nyingi zina njia kama hii ya kueleza simulizi ya kweli.

45-03

Je mambo haya ni kweli?

Hii maana yake ni kwamba, "je mashitaka haya juu yako ni ya kweli?" au, "je mambo haya wanayosema watu hawa juu yako ni ya kweli? " au, "je ni kweli kuwa ulisema mambo maovu kuhusu Musa na Mungu?"

Kila mara mnamkataa Roho Mtakatifu

Hii ni kwamba, "hamkumtii Roho Mtakatifu" au, "kila mara mlikataa kumsikiliza Roho Mtakatifu."

Baba zenu

Hii inaweza kutafsiriwa kama, " baba zenu, waisraeli."

45-04

wakaziba masikio yao

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "waliweka mikono yao kwenye masikio yao." Hii ilikuwa kuonesha kuwa walikuwa hawataki kusikia kile alichokisema Stefano.

kupaza sauti kubwa.

Walipaza sauti kwa hasira. Tafsiri jambo hili kwa njia ambayo itaonesha kuwa walikuwa wamekasirika sana.

45-05

Wakati Stefano akifariki

Hii maana yake ni kwamba, "wakati Stefano akikata roho."

Alilia kwa sauti

Hii maana yake ni kwamba , "alilia kwa sauti kuu" au, "alisema kwa sauti ya juu."

Usiwahesabie dhambi hii."

Hii maana yake ni kwamba, "usiwaone kama watu wenye hatia kwa dhambi hii ya kuniua mimi."

45-06

Akalinda nguo zake

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "aliyalinda makoti yake." inawezekana alikuwa anahakikisha kuwa hayaibiwi au kuharibiwa.

Lakini licha ya hii

Viongozi wa Wayahudi walidhani kuwa wangesimamisha kuenea kwa mafundisho ya Yesu kwa kuwatesa wafuasi wake. badala yake jambo hili liliwafanya watawanyike na kueneza ujumbe kwa upana zaidi.

45-07

Siku moja

Hii sentensi inatoa utangulizi wa tukio ambalo limetokea wakati ulio pita, laki haisemi muda maalum. Lugha nyingi zina namna hii ya kueleza simulizi ambayo ni ya kweli.

Ethiopia

Ethiopia ni nhi katika Afrika ya Mashariki.

45-08

Muethiopia

Huyu ni, "mtu wa nchi ya Ethiopia.

Alikaribia gari la farasi

Hii maana yake ni kwamba "alikaribia gari" au, "alisogelea gari."

Kama mwanakondoo akaapo kimya

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "kama mwanakondoo anapokuwa kimya hata kama anakaribia kuuwawa

45-09

Alikuwa ni Isaya anaandika kuhusu

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " Isaya alikuwa anamlenga nani."

45-11

Maji

Tumia neno ambalo linamaanisha maji mengi kama vile bwawa, ziwa, au kijito.

Naweza kubatizwa?

Hii inaweza kutafsiriwa kama, " je kuna sababu yoyote ya kunizuia nisibatizwe?"

45-12

Alimpeleka Filipo pengine

Hii ni kwamba, "alimchukua Filipo" au, "alimnyakua zake Filipo."