08-01
Alimtuma
Neno hili linamaanisha Yakobo alimwambia Yusufu aende na Yusufu akaenda.
Mtoto aliyependwa
Hii inaweza kutafasiriwa kama "mtoto aliyempendwa zaidi kuliko watoto wengine."
Kukagua
Hii inamaanisha Yusufu alienda na kuangalia kama kila kitu kipo sawa kwa ndugu zake. Lugha nyingine zinaweza kusema "kuangalia hali ya kaka zake."
Kaka
Hawa walikua kaka zake wakubwa na Yusufu.
Kuangalia kundi la mifugo
Kwa kuwa ilikuwa safari ya siku kadhaa, unaweza kusema "waliokuwa mbali wakichunga mifugo."
08-02
Alikwenda kwa kaka zake
Njia nyingine ya kutafasiri hili ni "akafika eneo ambalo kaka zake walikuwepo."
Kutekwa
Walimchukua kinyume na matakwa yake. Haikua sahihi kwa wao kufanya hivi.
Wafanya biashara ya utumwa
Walikua watu waliofanya biashara ya kununua watu toka kwa mmiliki mmoja na kuwauza kama watumwa kwa mmiliki mwingine.
08-03
Damu ya mbuzi
Kaka zake na Yusufu walitaka Yakobo afikiri kuwa damu iliyokuwa katika nguo ni damu ya Yusufu.
08-04
Kiongozi wa serikali
Mtu huyu alikua sehemu ya serikali ya Misri. Njia nyingine ya kusema hivi ni "kiongozi katika serikali ya Misri."
08-05
Akajaribu kulala na Yusufu
Njia nyingine ya kusema hivi ni "alijaribu kumshawishi Yusufu awe naye kimwili." "Kulala na" ni njia ya kuelezea ili kuepuka kuwa neno la kuchukwaza.
Kumtenda Mungu dhambi
Ni kinyume na amri za Mungu kwa watu kulala pamoja kabla hawajaoana. Yusufu hakutaka kufanya dhambi kwa kutokutii amri za Mungu.
Kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu
Njia nyingine ya kusema haya yaweza kuwa "kuendelea kumtii Mungu."
08-06
Ilimsumbua sana
Hii inamaanisha kuwa Mfalme aliogopa na kuchanganyikiwa (kwa sababu ya alichokuwa amekiona kwenye ndoto).
Washauri wake
Walikua wanaume wenye uwezo na maarifa ya pekee wenye uwezo wa kueleza maana ya ndoto. Tafsiri nyingine zinawaelezea kama "wazee wenye hekima."
Maana ya ndoto
Watu wa Misri waliamini kuwa ndoto zilikua na ujumbe toka kwa miungu ikiwaambia kitakachotokea baadaye. Mungu alitumia ndoto za Farao kumwambia kitakachotokea.
08-07
Kutafsiri ndoto
"Kutafsiri" ni kusema maana ya kitu fulani. Hivyo Yusufu alikua na uwezo wa kuwaambia watu maana ya ndoto zao.
Yusufu aletwe kwake
Njia nyingine ya kusema hivi inaweza kuwa "aliwaamuru watumishi wake wampeleke Yusufu kwake."
Mungu atatuma
Mungu atasababisha mazao yakue vizuri kwa miaka saba na baada ya hapo atasababisha wazalishe chakula kidogo sana ili watu na wanyama wasiwe na chakula cha kutosha.
Njaa
Bustani na mashamba yatazalisha chakula kidogo sana hivyo watu na wanyama hawatakua na chakula cha kutosha.
08-08
Alishawishiwa na
Farao alishangazwa na hekima za Yusufu na akampa heshima. Alimuamini Yusufu afanye maamuzi yenye hekima ambayo yatawafaidisha watu. Ingekua sahihi kusema "alishawishiwa na hekima za Yusufu."
Mtu wa pili mwenye mamlaka makubwa
Farao alimfanya Yusufu kuwa mwenye nguvu na kiongozi wa muhimu sana katika Misri. Farao tuu ndiye aliyekua mwenye nguvu na muhimu kuliko Yusufu.
08-09
Kuhifadhi vyakula vingi.
Walichukua vyakula toka kwenye mavuno mengi na kupeleka mijini na kuvihifadhi huko. Hivyo vyakula vikawa vya Farao.
08-10
Misri lakini pia Kaanani
Kwenye lugha nyingine inaweza kueleweka vizuri au kua na uhalisia zaidi ukisema "nchi ya Misri, lakini pia nchi ya Kaanani."
Njaa ilikua kali
Njaa ilikua mbaya sana. Kulikua na chakula kidogo sana na watu wengi nje ya Misri walikua na njaa kali.
08-11
Watoto wake wakubwa
Hawa walikua kaka zake wakubwa na Yusufu waliomuuza utumwani.
Hawakumtambua Yusufu
Hawakujua kama yule mtu ni Yusufu, kwa kuwa sasa Yusufu alikua na umri mkubwa tofauti na mara ya mwisho walipomuona na alikua amevaa kama kiongozi wa Wamisri.
08-12
Aliwajaribu kaka zake
Yusufu aliwaweka kaka zake wakubwa kwenye wakati mgumu kuona kama watamlinda mdogo wao au watamtendea mabaya kama walivyomtendea Yusufu. Walipomlinda mdogo wao Yusufu akajua kuwa wamebadilika.
Kama wamebadilika
Njia nyingine ya kusema hivi ni, "kama wamekua tofauti na walivyokua." Miaka iliyopita kaka zake na Yusufu walimuuza utumwani. Yusufu alitaka kujua kama sasa wapo tayari kufanya yaliyo mema.
Msiogope
Njia nyingine ya kusema hivi ni, "Hampaswi kuogopa adhabu yoyote toka kwangu." Kaka zake Yusufu waliogopa kwa sababu walimkosea sana Yusufu na sasa kama kiongozi mkubwa ana mamlaka ya kuwaadhibu. Yusufu angekataa kuwauzia chakula, au hata kuwaweka gerezani au kuwaua.
Ubaya kwa wema
Kaka zake Yusufu wakafanya yaliyo mabaya kwa kumuuza Yusufu kama mtumwa na akapelekwa Misri. Lakini Mungu aliliruhusu hilo ili Yusufu awahudumie maelfu ya watu toka katika njaa ikiwemo familia yake yenyewe. Hili lilikuwa jambo zuri sana.
08-14
Japokuwa Yakobo alikua mzee alienda Misri
Kulikua na umbali toka Kaanani kwenda Misri na ilikua vigumu kwa mzee kutembea au kuendesha mkokoteni kwa umbali huo.
Kabla Yakobo hajafa
Yakobo alifia Misri. Hakuweza kurudi Kaanani nchi ambayo Mungu alimuahidi kumpa yeye pamoja na uzao wake.
08-15
Agano la ahadi
Muda mrefu uliopita Mungu aliweka makubaliano na Ibrahamu kuwa atampa uzao mwingi, wataimiliki ardhi ya Kaanani na kuwa taifa kubwa. Mungu pia aliahidi kua watu wote watabarikiwa kupitia uzao cha Ibrahimu.
Kurithisha kwa
Njia nyingine ya kusema hivi yaweza kuwa "kurithisha kwa" au "kumpa" au "kutumika kwa." Ahadi za Mungu kwa Ibrahimu pia zilikua kwa watoto wake na wajukuu na kwa uzao wake wote. Tazama pia maelezo katika OBS 6-4.
Makabila kumi na mbili ya Israeli
Mungu alimuahidi Ibrahimu, Isaka na Yakobo kuwa uzao wao utakua taifa kubwa. Baadae Mungu alibadili jina la Yakobo kuwa Israeli. Kuzao wa watoto 12 wa Yakobo ukawa makabila makubwa 12. Makabila haya 12 yalitengeneza taifa lililoitwa Israeli ambalo liliitwa kwa jina jipya la Yakobo.