Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

06-01

Alimtuma mmoja wa watumishi wake.

Hii inaweza kutafasiriwa kuwa "alimwambia mmoja wa watumishi wake kurudi nyuma." Neno "nyuma" linamaana kuwa mtumishi anatakiwa arudi sehemu ambayo Ibrahamu aliishi miaka mingi iliyopita kabla hajaenda Kaanani. Hakikisha tafsiri ya sehemu hii ina maana kamili.

Kwenye ardhi.

Ardhi hii ilikua mashariki ambapo Ibrahamu alikuwa akiishi sasa hivi.

Kumleta mke kwa ajili ya mtoto wake Isaka.

Hii iinaweza kutafasiriwa kama "kumleta mwanamke ambae hajaolewa ili mwanae Isaka amuoe."

06-02

Mjukuu wa kaka yake na Abrahamu.

Alikua binti wa mtoto wa kaka yake na Abrahamu. Babu yake alikuwa kaka yake na Abrahamu.

06-03

Rebeka alikubali

Japokuwa wazazi wa Rebeka walipanga ndoa yake, hawakumlazimisha kwenda kuolewa na Isaka.

06-04

Ahadi.... zilizorithishwa

Ahadi za agano ambalo Mungu aliweka na Abrahamu hazikuwa kwa ajili yake tu, bali kwa ajili ya kizazi chake.

Isiyohesabika

Hii inaweza kutafasiriwa kama "nyingi sana." Neno "isiyohesabika" ina maana vitakuwepo vizazi vingi ambavyo watu watashindwa kuvihesabu.

06-05

Tumboni mwa Rebeka

Hii ni, "ndani ya tumbo lake."

06-06

Toka wa wanawe wawili

Hii ni, "kutoka kwenye uzao wa watoto wawili."

Watashindana wenyewe kwa wenyewe

Watoto wote wawili na taifa ambalo litatokana na wao wataendelea kushindana.

Mtoto mkubwa

Japokua watoto walikua mapacha, mtoto anayezaliwa wa kwanza ndiye anayepewa nafasi kama mtoto wa kwanza.

Kumtumikia mdogo

Hii inaweza kutafasiriwa kama, "mwana mdogo anatakiwa kufanya yale atakayoambiwa na mkubwa ayafanye."

06-07

Watoto wa Rebeka walizaliwa.

Lugha nyingine zina njia tofauti ya kusema haya kama, "pale Rebeka alipowaona na kuwachukua" au, "pale Rebeka alipowaleta kwenye mwanga."

Mtoto mkubwa ..... mtoto mdogo

Hii inaweza kutafasiriwa kuwa, "mtoto atakayekuja kwanza ... mtoto wa pili atakayekuja." Hakikisha kuwa namna ambavyo "mkubwa" na "mdogo" inatafsiriwa iendelee kuleta maana kuwa watoto hawa ni mapacha.

Nyekundu

Hii inaweza kumaanaisha kuwa ngozi yake ilikua nyekundu sana au nywele katika mwili wake zilikua nyekundu.

Nywele

Esau alikua na nywele nyingi mwilini mwake. Waweza kusema kuwa "mtoto mkubwa alikua mwekundu na mwenye nywele nyingi."