17-01
Mfalme wa kwanza wa Israel
Hii ingetafasiriwa kama, " Mfalme wa kwanza kutawala Israel."
Siku moja
Hii ingetafasiriwa kama, "Wakati mwingine badaye" au " Miaka badaye."
Angekuwa Mfalme katika nafasi yake.
Namna nyingine ya kusema ni, " kuchukua nafasi yake kama Mfalme wa Israel" au " Kutawala kama Mfalme badala yake."
17-02
Kuchunga
Inamanisha, " kutunza kwa ajili ya" au " kulinda" au "kujali kwa ajili ya."
17-03
Jitu kubwa liitwalo Goliathi.
"Jitu kubwa" hii inaelezea Mtu mkubwa asiye wa kawaida na mwenye nguvu. Goliathi alikuwa ni Askari mkubwa kwenye jeshi lililokuwa likipigana na israel
17-04
Siku moja.
Aya hii inatambulisha tukio lililotokea kipindi cha nyuma lakini hakuna muda maalumu uliotajwa wa tukio kutokea. Lungha nyingi zinamfanano katika kusimulia simuliz hizi za kweli.
Kuthibitisha kwa Sauli.
hii ni kwamba, " kumshawishi Sauli" au " Kumhakikishia Sauli."
Kuwa Mfalme.
Daudi hakutaka kumkosea Mungu kwa kumuuwa Mtu ambaye Mungu alimuweka kama Mfalme wa Israel.
17-05
Alimfanikisha
Hii ni kwamba, "alimsaidia kukamilisha mambo mazuri aliyotaka kuyafanya."
Mji mkuu wake
Huu ni, "Mji mkuu katiaka ufalme wake." Daudi aliishii Yerusalemu na akatawala huko.
Kipindi cha utawala wa Daudi
Hii ni, " katika kipindi ambacho Daudi alikuwa Mfalme wa israel." au "Daudi alitawala kama Mfalme wa israel."
17-06
Jenga Hekalu
Daudi alitaka kujenga jengo la kudumu kwa ajili ya kumwabudu Mungu ambalo lingekaa badala ya hema la kukutania.
17-07
Nabii Nadhani
inaweza ikawa halisi zaidi katika lugha zingine kusema, "Nabii alietwa Nadhani."
Mtu wa vita
Inamanisha kuwa " Mtu ambaye anapigana vita" Daudi aliuwa watu wengi sana katika vita dhidi ya maadui wa israel. Mungu hakuwa anamuadhibu Daudi lakini Mungu alihitaji mtu wa amani wa kujenga Hekalu ambapo watu wangemwabudu yeye.
Hekalu hili
Inamaana ya kuwa, "Jengo hili la kuabudia" au " Sehemu hii ya kuabu."
Kutoka dhambini
Inamaana ya kuwa, "Mabaya yaliyowapata kutokana na matokeo ya dhambi zao."
17-08
Maneno haya
Inamanisha ya kuwa, "Maneno ambayo Nabii aliyasema." hiii inarejea kwenye ahadi.
Ni heshima kubwa
Watu walioishi kabla, walimuheshimu Daudi kwa sababu baadhi ya uzao wake walikuwa wafalme wa israel na mmoja wao angelikuwa Masihi.
17-09
Daudi alitawala kwa haki na uaminifu kwa miaka mingi.
inaweza kutafasirirwa kama, " Daudi alipowatawala watu kwa miaka mingi alitenda yale yaliyokuwa sahihi na sawa, na alikuwa mwaminifu kwa Mungu."
Kuelekea mwisho wa maisha yake
Inaweza tafasiriwa kama, "Daudi alipokuwa Mzee" au " badaye katika maisha ya Daudi."
Kutenda dhambi hasa
Ni sawa na kusema, "'kutenda dhambi kwa kuasi." Dhambi ya Daudi ilikuwa ya Uasi.
17-10
Siku moja.
Aya hii inatambulisha tukio lililo tokea kipindi cha nyuma, lakini haijaonesha mda sahihi wa tukio kutokea. Lugha nyingi zinamfanano kwa kaunza kuelezea simulizi za kweli.
Akaona
Betisheba aliekuwa akioga nje ya nyumba yake, lakini sehemu ya Daudi ilikuwa juu na alikuwa na uwezo wa kuona juu ya ukuta uliokuwa chini
Kuoga
Hii inaweza kutafasiriwa kama, " alikuwa akioga" au " alikuwa akijiosha."
17-11
Badala ya kutazama pembeni
Inamanisha ya kuwa, Daudi hakutazama upande kipindi mwanamke alikuwa anaoga, kama alivyotakiwa kufanya.
Alilala naye
Hii ni sawa na kussema ya kuwa Daudi alifanya tendo la ndoa na Betisheba.
17-12
Kuwa na mke wake
inamaanisha kuwa, " aende nyumbani akakae mkewe." Daudi aliwataka watu hasa Uria, ili waamini ya kuwa Betisheba alikuwa na mimba yenye mtoto wa Uria.
Pale ambapo adui alikuwa na nguvu
Inamaanisha kuwa, sehemu fulani kwenye vita ambapo mapigano yalikuwa yakiendelea.
17-13
Alichokuwa amekifanya Daudi
Hii inarejea kuzini kwa Daudi na Betisheba pamoja na mauwaji ya mmewe, Uria.
17-14
Mapigano katika Nyumba ya Daudi
"Mapigano" haya yalikuwa makali. katika mambo haya, mmoja wa watoto wake alimuuwa mtoto wake na kuchukua nafasi ya Daudi kama Mfalme wakati ambao Daudi alikuwa akitawala. Ikiwezekana tumia neno ambalo litapunguza ukali wa ugomvi ndani ya familia.
Nguvu ya Daudi ilidhoofika sana.
inaweza kutafasiriwa kama, " Daudi akawa hana nguvu tena" au " Daudi akapoteza Mamlaka yake .