Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

03-01

baada ya muda mrefu

Simulizi hii ilitokea baada ya vizazi vingi (mamia ya miaka) baada ya uumbaji.

walikuwa waovu na katili

Ni rahisi kusema, "walikuwa waovu na walifanya mambo ya ukatili."

ikawa mbaya

Inaweza kueleweka kwa kusema "Watu walikuwa wakiishi kwa njia ya uovu na ubaya ambazo hazikumpendeza Mungu."

Mungu aliamua kuwaangamiza

Hii haimaanishi kuwa dunia itaharibiwa kabisa. ila Mungu alikusudia kuwaangamiza watu wote waliomuasi Yeye na walio sababisha maovu na ukatili. Mafuriko pia itauwa wanyama na ndege wote katika nchi.

Mafuriko makubwa

Maji mengi ambayo yengeifunika dunia, hata sehemu ambazo mara nyingi ardhi i kavu, na hata kufunika vilele vya milima mirefu.

03-02

akapata kibali

Mungu alipendezwa na Nuhu, kwasababu alimcha na kumtii Mungu. Japokuwa siyo kwamba Nuhu hakuwa na dhambi, Mungu alimhurumia na akaweka mpango wa kumuokoa yeye na familia yake kutoka kwenye mafuriko makubwa. Hakikisha haitaonekana kana kwamba Nuhu alipata bahati, au kwamba ilitokea tu akaponyoka. Bali, ni mpango na chaguo la Mungu.

Mafuriko

Maji mengi yenye kuleta maafa.

mpango wa kutuma

Mungu alipanga kuleta mafuriko yatakayo funika dunia mzima kwa kuruhusu mvua nyingi. Hii ni kwamba alipanga kusababisha mafuriko ya mvua nyingi.

03-03

safina

Safina ni aina ya mashua ambayo ni kubwa kiasi kwamba inaweza kubeba watu wanane, na wanyama wawili wawili kwa kila kundi la wanyama, pamoja na malisho yao kwa kadri ya muda wa mwaka mmoja.

03-04

Nuhu aliwaonya

Nuhu aliwaambia watu wote kuwa Mungu ataiangamiza dunia kwa sababu ya dhambi.

wamrudie Mungu

Hii ilimaanisha kuacha kufanya dhambi na kuanza kumtii Mungu.

03-06

Mungu akatuma

Muhu alikuwa hana haja ya kuwatafuat wanyama bali Mungu aliwatuma kwake.

waliotumika kwa sadaka ya kuteketezwa

Kwa lugha nyingie, inaweza kuwa rahisi kusema kuwa "wanyama wale waliokubalika na Mungu kwa sadaka ya kuteketezwa." Mungu aliamua watu wamtolee wanyama kama sadaka ya kuteketezwa, hata hivyo aliwaruhusu tu Kumtolea aina fulani ya wanyama.

Mungu mwenyewe alifunga mlango

Hii inatia mkazo kuwa ni Mungu mwenyewe ndiye aliyefunga mlango.

03-07

mvua iakaanza kunyesha, na kunyesha , na kunyesha

Hii inasisitiza kuwa kulikuwa na mvua isyokuwa ya kawaida, mvua kubwa sana. Lugha nyingine huenda zina namna ya kutia mkazo.

maji pia yalitokea ardhini

Hii iliashiria kulikuwa na maji mengi yaliyotokea ardhini.

Dunia yote ikafunikwa

Hii ilimaanisha dunia yote ilifunikwa na maji.

03-09

Mvua kukatika

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, "mvua iliacha kunyesha."

Safina ikatua

Kulikuwepo na maji mengi kutokana na mvua iliyofunika hata milima. Safina ilielea mlimani na maji yalipoanza kwenda chini, safina ilienda chini na maji na safina ikatulia kwenye mlima.

miezi mitatu baadaye

Maji yaliendelea kupungua kwa muda wa miezi mitatu baadaye.

milima ilionekana

Njia nyingine za kutafsiri hii ni "vilionekana" "vikatokeza", vilikuwa vimeonekana. "Inaweza ikawa rahisi kusema, "Baada ya miezi mitatu, maji yalishuka kiasi kwamba Nuhu na familia yake walianza kuona vilele vya milima.

03-10

kunguru

Aina ya ndege mweusi anayeruka na kula aina ya majani na wanyama, ikiwa ni pamoja na nyama zilizooza za wanyama.

03-11

njiwa

Ndege mdogo mweupe na kijivu mwenye kuruka na kula mbegu na matunda.

tawi la mzabibu

Mti wa mzabibu una mafuta ambayo watu hutumia kupikia na kujipaka. Kama lugha yako haina neno la "tawi la mzabibu" unaweza kutafsiri kama ni tawi linalotokana na mti uitwao "mzabibu" au tawi kutoka kwa "mti wenye mafuta."

maji yalianza kukauka/kwenda chini

Inaweza ikawa rahisi kwa lugha yako kusema, maji yaliendelea kuisha, au "kiwango cha maji kilipungua au kilishuka."

03-12

alisubiri wiki moja zaidi

Unaweza kusema, alisubiri suku zaidi, Neno "kusubiri" inaonyesha kuwa Nuhu alisubiri ili maji yakauke kabla ya kumtuma njiwa tena.

03-13

Miezi miwili baadaye

Hii ina maana miezi miwili baada ya Nuhu kumuachia njiwa kutoka katika safina. Huenda ni muhimu kusema hii kwa lugha rahisi kama haijaeleweka.

Muwe na watoto wengi

Hakikisha inaeleweka kuwa ni amri na shauku ya Mungu, unaweza kusema "Ni lazima kuwa na watoto wengi" au "Nataka ninyi muwe na watoto wengi."

Muijaze nchi

Kama haijaeleweka, unaweza ukasema "muijaze dunia na watu" au "ili pawepo na watu wengi waishio duniani."

03-14

aina ya wanyama waliopaswa kutolewa dhabihu

Njia nyingine ya kusema hii ni, "wanyama ambao watu hutumia kumtolea Mungu dhabihu ya kuteketezwa."

Mungu alifurahishwa

Mungu alipendezwa na Nuhu kwa kumtolea dhabihu ya kuteketezwa kwa wanyama hao.

03-15

kamwe tena

Hii inamaana "hatarudia tena" au "hatarudia tena wakati wowote" mifano: "Sitalaani tena ardhi" au sitalaani tena ardhi kwa wakati wowote au kwa hakika sitalaani tena ardhi.

kulaani ardhi

Ardhi na viumbe vingine vyote hutaabika kwa sababu ya dhambi za wanadamu.

Dunia

Hii inamaanisha ardhi na viumbe vingine vyote vinavyoishi duniani.

watu ni wenye dhambi tangu utotoni mwao

Njia nyingine ya kusema hii ni, "watu hufanya matendo maouvu kwa maisha yao yote."

03-16

upinde wa mvua

Huu ni upinde wa mwanga wenye rangi ambazo mara nyingi hutokea angani pale panapo kuwepo na mvua ya ngurumo.

ishara

Ishara ni kama kitu au tukio ambayo ina maana fulani au inayoashiria kitu ambacho ni cha kweli au kitatokea.

ishara ya ahadi yake

Kwa lugha nyingine inaweza ikawa vizuri kusema "kuonyesha kuwa ameahidi."

kila wakati

Hakikisha inafahamika ya kuwa, ni kila wakati upinde wa mvua inaponekana na kuendelea. Huenda ni Muhimu kuongeza, "Kuanzia sasa na kila wakati."

alicho ahidi

Hii inarejea, ile hali ambayo Mungu aliahidi kutoangamiza dunia tena kwa kutumia mafuriko.