Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

44-01

Siku moja

Hii sentensi inatoa utangulizi wa tukio amabalo limetokea wakati ulio pita, lakini halielezi muda maalumu. lugha nyingi zina usemi wa jinsi hii wakati wa kuanza kueleza simulizi ya kweli.

Mtu aliye kiwete

Hii inaweza pia kutafasiriwa kama, " kilema." Hii inamaanisha mtu ambaye hawezi kutumia miguu yake kwa ukamilifu, na hawezi kusimama au kutembea.

44-02

Katika jina la Yesu

"Jina" hii inasimama badala ya mamlaka na nguvu za mtu. Kwa hiyo usemi huu unamaanisha, " Kwa mamlaka ya Yesu."

Simama

Hii maana yake ni , "simama juu."

44-03

Ua wa hekalu

Ni makuhani pekeyao ndio ambao waliingia hekaluni, lakini wayahudi wa kawaida waliruhusiwa kuja katika eneo hili ambalo lilizunguka hekalu.

44-05

Mwanzilishi wa uzima

Hii ni kwamba, Yule aliye umba uzima" au, "yeye yule atupaye uzima" au, yeye ambaye anafanya watu waishi" hii inamaanisa Yesu.

Matendo yako

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "mambo uliyofanya." Hii inamaanisha maswali yao juu ya Pilato kumuua Yesu.

Mrudie Mungu

Hii maana yake ni kwamba, "amua kumtii Mungu."

Dhambi zako zitasafishwa

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Mungu ataosha dhambi zenu" au, Mungu ataondoa dhambi zenu ana kuwafanya muwe safi." hii inazungumzia Mungu kuwatakasa watu katika roho zao kwa kuondoa dhambi zao kabisa. Hii haimaanishi tendo halisi la kuosha.

44-06

Ujumbe wa Petro

Hii ni, " ujumbe ambao Petro alikuwa amewahubiri."

Idadi ya wanaume

Hii ilikuwa ni ongezeko la idadi ya wanawake na watoto ambao waliamini

44-08

Kuponywa

Hii maana ya keni , " kuwa salama" au, "kuwa mwenye nguvu"

Walimkataa

Hii ni, " walikataa kumpokea" au, "walikataa kumwamini Yesu" au, walikataa kuamini kuwa Yesu ni mwokozi."

Lakini hakuna njia nyingine ya kutuokoa isipokuwa kupitia uwezo wa Yesu

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Lakini njia pekee ya kuokolewa ni kupitia uwezo wa Yesu Kristo" au, " lakini Yesu pekee anaweza kutuokoa, kwa uwezo wake."

Kuokolewa

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kuokolewa kutoka dhambi zetu" au, "kwamba tunaweza kuokolewa kutoka katika dhambi zetu."

44-09

Walishangazwa

Hii ni kwamba, " walistaajabu" au, walishangaa."

Kawaida

Hii ni ile "iliyozoeleka" ya hali ya chini." Petro na Yohana walikuwa wavuvi wa kawaida.

Ambao hawakuwa na elimu

Hii ni kwamba, "ambao hawakuwa na elimu ya darasani." hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "ambao hawajaenda kwenye shule ya dini."

Kisha walikumbuka

Hii inaweza kutafsiriwa kama, " lakini kisha walifikiri juu ya ukweli kwamba."

Walikuwa pamoja na Yesu

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "walitumia muda pamoja na Yesu" au, walikuwa wamefundishwa na Yesu."

Baada ya kutishwa

Viongozi walisema wangemuadhibu Petro na Yohana kama wangeendelea kuwafundisha watu kuhusuYesu.

Waruhusu waende

Hii ni kwamba, "waliwaruhusu waondoke."