48-01
Mungu aliumba ulimwengu
Hiyo ina maana kwamba, "Mungu aliufanya ulimwengu kutoka katika utupu au katika hali ya kutokuwa na kitu."
Pasipo dosari yoyote
Hiyo ina maana kwamba, "sahihi kabisa kama inavyotakiwa kuwa" kukamilisha yote yale ambayo Mungu alikusudia kwayo.
Hapakuwa na dhambi
Kwa baadhi ya lugha siyo rahisi kuelezea "dhambi" kama kitu, badala yake dhambi inaelezewa kama kitendo. Katika mazingira hayo hii ingeweza kutafsiriwa kama, "Hakuna ambaye aliwa kutenda dhambi" au, "Watu hawakutenda dhambi" au, "Hakuna jambo ovu lililotokea."
Hapakuwa na magonjwa wala kifo
Hiyo ina maana kwamba, "Hakuna aliyeugua na hakuna aliyekufa" au, "Hawakuugua wala hawakufa."
48-02
Bustani
Hii inaelezea juu ya bustani iliyotengenezwa na Mungu mahali alipowaweka watu wa kwanza mtu mume na mtu mke.
Alimdanganya Eva
Hiyo ina maana kwamba, "alimdanganya Eva." Shetani alimdanganya kwa kumuongoza Eva kutilia mashaka kile ambacho Mungu alikisema. Kwa kufanya hivi, alimlaghai Eva kwa kumuweka katika hali ya kutomtii Mungu.
48-03
la hatari zaidi
Hiyo ina maana kwamba, "mbaya zaidi" au, "bado mbaya"
48-04
atakiponda kichwa cha shetani
Hii ingeweza kutafsiriwa pia kama, "kukanyaga kwenye kichwa cha shetani na kukiharibu kabisa" au, "Kukivunja kichwa cha Shetani kwa kukikanyaga juu yake." Hii ni namna ya sura ya mtu anayekanyaga juu ya kichwa cha nyoka. Kichwa kinakuwa kimepondwa kabisa na nyoka anakuwa amekufa na kwa hiyo hawezi kudhuru.
atakigonga kisigino
Hii ni namna ya sura ya nyoka ardhini akiuuma mguu wa mtu. Katika habari hii, Shetani angesababisha Masihi kuteseka, lakini asingemharibu.
atamfufua tena
Hiyo ina maana kwamba, "kumfanya awe hai tena."
48-05
kuangamizwa kwa sababu ya dhambi zao
Hii ingeweza kutafsiriwa pia kama, "kila mmoja anapaswa kuadhibiwa milele na Mungu kwa sababu wametenda dhambi."
48-06
alijitoa mwenyewe
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, " Yesu aliruhusu yeye mwenyewe auwawe."
alibeba adhabu
Hiyo ina maana kwamba, "alipokea adhabu katika mwili wake mwenyewe."
48-07
watu wote wa duniani
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, "watu kutoka pande mbalimbali zote za dunia."
uzao wa Ibrahimu kwa jinsi ya kiroho
Hiyo ina maana kwamba, "kiroho anahusiana na Ibrahim, na mmoja wa watu wa Mungu."
48-08
badala ya mwanawe Isaka
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, "mahali pa mwanawe Isaka" au, "Katika mahali pa mwanawe Isaka" au, "ili kwamba asimtoe sadaka mwanawe Isaka kuwa sadaka ya kuteketezwa."
kustahili kufa
Hiyo ina maana kwamba, "ilitupasa kufa."
kufa badala yetu
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "kufa mahali pa kila mmoja wetu" au, "ili kwamba asituuwe sisi."
48-09
alituma pigo la mwisho juu ya Misri
Hiyo ina maana kwamba, "alisababisha maafa ya mwisho kuja juu ya Misri." Hili lilikuwa pigo la kumi pale Mungu aliposababisha mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Wamisri kufa.
kondoo asiye na kasoro
Hiyo ina maana kwamba, "kondoo bila kuwa na kasoro yoyote"
damu yake
Hiyo ina maana kwamba, "damu ya mwana wa kondoo."
miimo ya mlango
Kama miimo ya milango haijulikani, hii inaweza kutafsiriwa kama, "milango."
aliziruka
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, "kupita." Unaweza kutaka kulioanisha neno hili linavyotafsiriwa na jinsi neno "pasaka" linavyotafsiriwa.
48-10
Mwanakondoo wetu wa Pasaka
Hiyo ina maana kwamba, "Mwanakondoo wa pasaka aliyeuwawa kwa ajili yetu" au, "mwanakondoo aliyeuwawa ili Mungu apite juu yetu" au, "mwanakondoo aliyeuwawa ili kwamba Mungu asituuwe."
hakuwa na kosa wala dhambi yoyote
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "hakuwahi kutenda dhambi."
damu yake Yesu
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, "Sadaka ambayo Yesu alijitoa mwenyewe alipokufa kwa ajili ya wenye dhambi." Neno "damu" hapa linamaanisha pia "kifo."
adhabu ya Mungu humruka mtu huyo
Kauli hii inamaanisha, "Mungu hamuadhibu mtu." Itafsiri kutumia maneno yanayoonyesha uhusiano wake na neno "Pasaka" na "Mwanakondoo wa Pasaka." Kama neno "alituhifadhi" limetumika katika neno Pasaka, hii inaweza kutafsiriwa kama, "Mungu alimuacha huyo mtu bila kumuadhibu."
48-11
Israel ambao ni wateule wake
Hiyo ina maana kwamba, "Wanaisrael, watu aliowachagua" au, "watu wake aliowachagua, Wanaisrael."
48-12
nabii mkubwa
Hiyo ina maana kwamba, "nabii muhimu sana."
nabii mkuu zaidi
Hiyo ina maana kwamba, "nabii muhimu sana sana."
Yeye ni Neno la Mungu
Hiyo ina maana kwamba, "Anaitwa Neno la Mungu" kwa sababu anafunua tabia ya Mungu. Manabii wengine walihubiri ujumbe ambao Mungu aliwapa, lakini Yesu alimfunua Mungu katika mahubiri yake na matendo yake.
48-14
Mfalme wa ulimwengu wote
Hiyo ina maana kwamba, "Mfalme juu ya kila mmoja na kila kitu kila mahali."