Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

49-02

kutoa mapepo

Hii inamaanisha kwamba, "alitoa mapepo kwa watu."

Aliwafufua wafu

Hii inaweza kutafsiriwa kwamba, "alisababisha watu waliokufa kuwa hai tena."

49-03

mwalimu mkuu

Hii ni sawa na kusema: "mwalimu muhimu" au "mwalimu bora."

Kwa njia hiyo hiyo

Hii ni sawa na, "kama ilivyo" au, "kwa sawa kiasi kama kile" au, "kwa kiwango kama kile."

49-04

mali zako

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "fedha yako" au "milki yako."

49-05

kuokolewa kutoka katika dhambi zenu

Hii ni sawa kusema kwamba, "kuokolewa kutoka kwenye hali ya kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zenu" au "kwamba Mungu ataweza kuwasamehe dhambi zenu" au, "kupokea wokovu ili mtoke katika dhambi zenu."

49-06

wengine hawata

Hii ni kusema kwamba, "watu wengine hawatampokea na kwa hiyo hawataokolewa."

mbegu ya neno la Mungu

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, "mbegu, ambayo inaweza kulinganishwa na neno la Mungu." Kipengele hiki kinaleta mlinganisho kati ya mbegu na neno la Mungu.

49-08

ametengwa na Mungu

Hii inaweza pia kutafsiriwa kuwa, " hawezi kuishi na Mungu" au "hawezi kuwa karibu na Mungu" au "hawezi kuwa na uhusiano na Mungu."

49-09

alimtoa Mwanawe wa pekee

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, "alitoa Mwanawe wa pekee kwa ulimwengu kama dhabihu kwa dhambi" au, "alitupatia Mwanawe pekee awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu."

kila aaminiye

Hii pia inaweza kutafsiriwa kuwa, "yeyote aaminiye."

kila aaminiye katika Yesu hatahukumiwa kwa dhambi zake bali ataishi na Mungu milele

Hii pia inaweza kutafsiriwa kwamba, "Wakati yeyote akimwamini Yesu, Mungu hatamhukumu mtu huyo kwa ajili ya dhambi zake, lakini atamruhusu kuishi na Mungu milele."

49-10

Kwa sababu ya dhambi zenu

Inaweza kutafsiriwa kwamba, "Kwa sababu mmetenda dhambi." Kuiweka vizuri hii ni kwamba anaongea kuhusu watu wote, kwa baadhi ya lugha inaweza kuwa sawa kama hii itatafsiriwa kwamba, "Kwa sababu watu wote wametenda dhambi, wana hatia, kwa hiyo wanastahili kifo."

Mungu anapaswa kuwa na hasira

Hii yaweza kutafsiriwa kwamba, "Itakuwa sawa kwa Mungu kuwa na hasira."

Alimwaga hasira yake kwa

Hii ni kusema kwamba, "alielekeza hasira yake kwa" au, "aliweka hasira yake yote juu" au "alimkasirikia tu."

alipokea hukumu yenu

Hii inaweza kutafsiriwa kwamba, "alihukumiwa badala yenu" au, "alihukumiwa kwa ajili ya dhambi yako." Kuiweka sawa ni kwamba hii hutumika kwa kila mtu, inaweza pia kutafsiriwa pia kwamba, "alihukumiwa kwa dhambi ya kila mtu."

49-11

chukua

Hii ni sawa na kusema, "ondoa adhabu ya" au, ondoa hukumu kwa." Dhabihu ya Yesu husababisha Mungu kutazama dhambi zetu kama kwamba hazijwahi kuwepo.

49-12

Matendo mema hayawezi kuwaokoa

Hii inamaanisha kuwa, "Kufanya mambo mazuri hakuwezi kuwaokoa ninyi kutoka katika dhambi zetu" au "Hamuwezi kufanua kitu chochote chema cha kutosha ninyi wenyewe kuwaokoa kutoka katika hukumu yennu ya dhambi zenu."

Mungu huosha dhambi zenu

Sawa na, " huondoa dhambi zenu kikamilifu" au, "huchukua dhambi zenu na kuwafanya ninyi safi." Hii inazungumzia kuhusu Mungu kutakasa roho za watu kwa kuondoa kikamilifu dhambi zao. Haimaanishi kuoshwa kimwili.

badala yenu

Hii ni kusema kwamba, "kwa niaba yenu."

alimrudisha katika uhai tena

Hii inaweza pia kutafsiriwa kwamba, "alimfanya kuwa hai tena."

49-13

anaweza kuwa na uhusiano wa karibu na ninyi

Hii inaweza kutafsiriwa hivi, "ili kwamba uweze kuwa mtoto wake" au, "ili kwamba uweze kuwa rafiki yake" au, "ili uweze kumilikiwa naye."

49-14

amini katika yeye

Hii inaweza kutafsiriwa kwamba, "amini katika yeye" au, au amini katika yeye ili akuokoe" au, "weka tumaini la maisha yako yote kwake."

mmebatizwa

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, "muwe na mtu fulani wabatize" au, "muwaache wawabatize ninyi."

amini kwamba

Hii inaweza kutafsiriwa kwamba, "kiri kwamba" au, "kubali kwamba."

chukua

Hii ni sawa na kusema, "ondoa adhabu ya" au, ondoa hukumu kwa." Dhabihu ya Yesu husababisha Mungu kutazama dhambi zetu kama kwamba hazijwahi kuwepo.

49-15

ufalme wa giza wa Shetani

"Giza" imetumika hapa kurejea kwenye dhambi na kila kitu ambacho ni kiovu. Hii inaweza kutafsiriwa hivi. "Uovu wa Shetani, ambao ni kama giza hutawala juu ya watu."

Ufalme wa Mwanga wa Mungu

"Mwanga" hapa unarejea kwa utakatifu na uzuri wa Mungu. Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Haki ya Mungu, ambayo ni kama mwanga hutawala juu ya watu." Biblia mara kwa mara hulinganisha uovu na giza, na wema na mwanga.

49-16

anakuchukulia kama

Hii ni sawa na, "hukufikiri wewe kama umekuwa" au, "akuangalia wewe kama" au "akuita kama."

49-17

jaribiwa kutenda dhambi

Hii ni kusema, "kujaribiwa kutenda dhambi ingawa unajua dhambi ni mbaya."

ni mwaminifu

Katika muktadha huu ina maana kwamba Mungu, "hutunza ahadi zake."

ungama dhambi zenu

Hii inaweza kutafsiriwa hivi, "kiri kwa Mungu kile ulichokosa."

Atawapa nguvu ya kupambana dhidi ya dhambi

Maana yake ni, " Atawapa nguvu ya kiroho ya kukataa kufanya dhambi."

49-18

kuwa na uhusiano wa kina zaidi naye

Hii pia inaweza kutafsiriwa kuwa, "kumpenda yeye zaidi" au, "kumjua yeye zaidi" au, "kuwa mwaminifu zaidi kwake."