Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

42-02

Hawakumtambua

Hii ni, " hawakujua kuwa alikuwa ndiye Yesu."

Mambo ambayo yalikuwa yametokea

Hii inamaanisha mafundisho na miujiza ya Yesu, kifo chake, na taarifa za kufufuka kwake.

42-03

Siku ya Tatu

Baadhi ya lugha zingeweza kusema, " siku ya tatu baada ya kifo chake."

Ilikuwa imekaribia jioni

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "siku ilikuwa inaishiria" au, jua lilikuwa linazama" au, "ilikuwa inaanza kuwa usiku."

42-04

Alitoweka mbele ya macho yao

Hii inawza kutafsiriwa pia kama, "alikuwa ameondoka" au, "alikuwa hayupo hapo."

42-05

Mioyo yetu ilikuwa inaungua

Hii maana yake ni kwamba, "tulikuwa na shauku na shangwe ndani ya mioyo yetu" au, "tulikuwa tunaanza kupata tumaini" au, "tuliona furaha." Lugha zingine zina njia tofauti ya kueleza hali hii kama vile, "Mioyo yetu ilichochewa" au, " mioyo yetu ilipashwa moto." Kama utatumia maneno yanayo eleza hali ya moyo kuungua, hakikisha isije ikamaanisha kuwa walikuwa wamekasirika.

42-06

Amani iwe kwenu

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, " na muwe na amani" au, " amani iwe nayi."

Mzimu

Hii inamaanisha roho ya mtu aliye kufa.

Mashaka

Hii ni kwamba, "mashaka ya kuwa niko hai na niko hapa nanyi."

Kuhakikisha

Hii inamaana, kuthibitisha."

42-07

Lazima itimie

Hii inawza kutafsiriwa kama, lazima itokee."

Fungua akili zao ili kwamba waweze kuelewa.

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "kuwawezesha kuelewa" au, "kuwafanya waweze kuelewa."

Siku ya tatu

Hii ni kwamba, "baada ya siku tatu" au, siku tatu baadaye."

42-08

Tangaza

Hii maana yake ni kwamba, julisha" au, "hubiri."

Watafanya hivi wakianzia Yerusalem

Hii ni kwamba watafanya hivi wakianzia Yerusalem" au, wataanza kutangaza mambo haya katika Yerusalem."

Ninyi ni mashahidi wa mambo haya

Hii ni kwamba, mmeona mambo haya yakitokea" au, "mtawaeleza watu wengine mambo ambayo mmeyaona yakitokea."

42-10

Mamlaka yote ya mbinguni na duniani yamekabidhiwa kwangu

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "Mungu amenipatia mamlaka yote ya mbinguni na duniani" au, "Mungu amenipatia mamlaka kamili juu ya kila mtu aliye mbinguni na duniani" au, " ninamamlaka yote mbinguni na duniani."

Fanya watu kuwa wanafunzi katika makundi yote ya watu

Hii ni, saidia watu kutoka kila kundi la watu wawe wanafunzi wangu."

Katika jina la

Sentensi hii inamaanisha mambo yote mawili, "kwa mamlaka ya" na , "chini ya mamlaka ya ." ikiwa kwa hali halisi ikieleweka kwa jinsi hii katika lugha yako. Hii sentensi inaweza kurudiwa kama, kwa jina la Baba, kwa jina la mwana, na kwa jina la Roho mtakatifu."

42-11

atawajilieni

Hii in, " atawashukia chini" au, "atakuja kwenu."

Wingu lilimfunika wasimuone

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "alipotelea kwenye wingu."

Mkono wa kuume wa Mungu

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " upande wa kulia wa Mungu."

Juu ya mambo yote

Hii ni, "juu ya kila kitu."