Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

46-01

Alitunza nguo za wanaume waliomuua Stefano

Angalia maelezo kutoka hadithi sehemu 45-6.

Kutoka nyumba hadi nyumba

Hiyo ina maana ya kwamba "kwenye nyumba nyingi."

Dameski

Dameski sasa ni makao makuu ya nchi ya Syria. Nyakati zile za Sauli, lilikuwa jiji lililokuwa linamilikiwa na Dola la Kirumi. Watu wengi huko hawakuwa Wayahudi, lakini kulikuwa na baadhi ya Wayahudi na pia baadhi ya Wakristo waliokuwa wakiishi huko.

46-02

Alipokuwa akienda

Hiyo ina maana "akiwa katika safari yake"

46-04

Lakini Anania akasema

Kama haiko wazi sana kwanini neno "Lakini" linatumika hapa, hili neno linaweza kutafsiriwa kama " Lakini Anania aliogopa, na hivyo akasema"

Mungu akamjibu

Hii inaweza kutafsiriwa kama "Ili kumhakikishia Anania, Mungu alisema" ili kuweka wazi kwa nini Mungu alisema hili.

Alitangaze jina langu

Hii ni " kufundisha kuhusu mimi" au "kunifanya mimi nijulikane"

Kwa ajili ya jina langu

Hii ni "kwa ajili yangu" au "kwa sababu yangu" au "kwa sababu ananitumikia mimi" au "kwa sababu anawafundisha watu wengine kuhusu mimi"

46-05

hapa

Hiyo ina maana "Dameski"

upate kuona tena

Hii ingeweza kutafsiriwa pia kama "kuweza kuona tena"

nguvu zake zikamrudia

Hii ingeweza kutafsiriwa pia kama "akawa mwenye nguvu tena" au "akajisikia vizuri"

46-06

Mara hiyo

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama"Maramoja" au "Kisha"

alijadiliana na Wayahudi

Hii pia ingeweza kutafsiriwa kama "aliwapa Wayahudi sababu njema za kuamini katika Yesu" au , "aliongea kwa ushawishi pamoja na Wayahudi"

46-07

malango ya miji

Malango yalikuwa ndiyo njia pekee ya kawaida ya kuingia au kutoka kwenye miji iliyokuwa imezungushiwa ukuta.

walimteremsha akiwa ndani ya kikapu ukutani

Njia nyingine ya kusema hiki ingekuwa "walimsaidia kuingia ndani ya kikapu kikubwa na kukishusha hicho kikapu na yeye akiwa ndani yake juu ya ukuta wa mji"

46-08

wamkubali Sauli

Hii ina maana "waliamini kwamba Sauli pia alikuwa muumini katika Yesu"

46-09

mji wa Antiokia

Huu ulikuwa mji wa zamani ambao unapatikana mahali ambapo hivi sasa ni sehemu ya kusini kabisa wa nchi ambayo sasa inajulikana kama Uturuki, karibu na mpaka wa Syria na karibu na Bahari ya Mediterania. Ni kama umbali wa maili 450 kaskazini magharibi mwa Yerusalemu.

kulikomaza kanisa

Hii ingeweza pia kutafsiriwa kama, "kulisaidia kanisa kukua imara kiroho" au "kuwasaidia waumini katika Yesu kukuwa imara katika imani yao" au, "kuwasaidia watu kuamini kwa uthabiti ndani ya Yesu"

46-10

siku moja

Hii sentensi inatambulisha tukio ambalo limetokea huko nyumba, lakini haisemi ni wakati gani hasa. Lugha nyingi zinanamna kama hiyo ya kuanza kuhadithia hadithi.

nitengeeni

Sentensi hii inaweza kutafsiriwa kama, "Kuwateuwa Paulo na Barnaba kufanya kazi maalumu ambayo nimewachagua kufanya."

kanisa

Hii ingeweza pia kutafsiriwa kama, "waumini" au, "wakristo."

wakawawekea mikono juu yao

Hii ingeweza pia kutafsiriwa kama, "waliwabarikia kwa nguvu na mamlaka ya Roho Mtakatifu kwa kuwawekea mikono juu yao" au, "waliweka mikono juu yao kama alama ya umoja wao katika Roho," Baadhi ya Lugha zingelazimika kusema ni wapi walipoweka mikono yao. Kama ni hivyo ungelisema waliweka mikono juu ya vichwa vyao, mabega au mgongo yao.

wakawatuma waende

Hiyo ni ina maana ya kwamba, "wakawatuma waende huko" au, "wakawatuma waende katika sayari yao.