Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

16-01

Na hawakuwaondoa.

Hii inaelezea jinsi ambavyo hawakumtii Mungu, hivyo katika baadhi ya lugha ingekuwa vyema kuianza hii kama sentensi mpya," Hawakufanya"

Kuwaondoa Wakanaani waliobakia

Hii inaweza kutafasiriwa, " kupigana na wakanaani waliobakia na kuwalazimisha waondoke kwenye nchi.

Au kutii sheria za Mungu.

hii ina manisha ya kuwa pia watu hawakuzitii sheria ambazo Mungu aliwapa waisrael katika Mlima Sinai.

Mungu wa kweli

Ni kwamba, "Mungu halisi" Yehova ndiye pekee ambaye watu wanapaswa kumwabudu.

Jinsi walivyofikiri ya kuwa ingekuwa sahihi kwa ajili yao

Hii inamanisha ya kuwa wote walifanya yale waliyotaka kufanya, ikiwa ni pamoja na uovu mwingi.

16-02

Walimuomba Mungu awaepushe.

Hii ni kwamba, walimwomba Mungu awasaidie na kuwaweka huru kutoka kwa maadui zao.

16-03

Mungu alituma

Hii inaweza kutafasiriwa kama, "Mungu alichagua" au "Mungu alimteuwa" au " Mungu alimwinua."

Alileta Amani

Hii inaweza kutafasiriwa kama, "alirurhusu watu waishi bila kuwa na hofu" au "alimaliza mapigano" au "aliwazuia maadui zao kuwateka".

Nchi.

Hiyo inaelezea Kanaani, nchi ya ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahim.

Watu walimsahau Mungu.

Inamanisha ya kuwa," Watu waliacha kufikiri kuhusu Mungu na kupuuzia alichokuwa amewaamuru."

16-04

Mazao

Hii inaelezea Mimea ambayo waisrael waliyokuwa wakilima katika bustani zao au mashamba yao, kwa ajili ya chakula.

Waliogopa sana, wakajificha.

Hii inaweza kutafasiriwa kama, " Wali waogopa sana Wamidiani, hivyo wakajificha."

Wakamlilia

Hii inaweza kutafasiriwa kama," waliita kwa sauti" or " Waliomba kwa uchungu sana."

Awaokoe

Hii inaweza kutafasiriwa kama, "kuwaweka huru" au "kuwanusuru na maadui hawa."

16-05

Siku Moja.

Aya hii inatambulisha tukio lililo tokea kipindi cha nyuma, lakini haikutaja muda maalumu. Lugha mbalimbali zina namna sawa za kuelezea simulizi ya kweli.

Kupura nafaka

Nafaka ilikuwa ni ngano, yenye vipande vidogo vya nafaka, au mbegu juu ya maganda yake. "Kupura" ni kuachanisha mbegu za mimea kutoka kwenye maganda kwa kupepeta vipande vya nafaka. Mbegu ni chakula lakini maganda sio chakula.

Sirini.

hapa ni pale Gideoni alikuwa akipura nafaka katika sehemu iliyofichika, kwa hiyo Wamidiani hawakuweza kumuona.

Mungu yupo pamoja nanyi

hii humanisha " Mungu yupo pamoja na wewe kwa namna yaki pekee" or "Mungu anayo malengo ya kukutumia kwa namna ya kipekee."

16-06

Kuvunja

Hii inamanisha kuwa," kuileta chini hasa," au "kuiharibu au kuiteketeza kabisa."

Aliogopa watu.

Gidioni aliogopa ya kuwa wenzake wa israel waliokuwa wakiabudu sanamu ile ile wangemkasirikia.

Walisubiri mpka wakati wa usiku.

Namna nyingine ya kusema maneno haya ni, "walisubiri mpka giza lilipoingia". Gidioni aliivunja madhabahu usiku wake ambapo kila mtu alikuwa amelala ili asiwepo wa kumuona.

16-07

Kwa nini mnajaribu kumsaidia mungu wenu?

Hili sio swali sahihi la kuulizia taarifa. Namna nyingine ya kusema inaweza kuwa ni, "hamtakiwi kumsaidia mungu wenu" au " hampaswi kumsaidia mungu wenu."

Na kama ni mungu, ajilinde mwenyewe

Hii inamaana ya kuwa, "kama angelikuwa ni mungu wa kweli, angekuwa na uwezo wa kujitetea mwenyewe."

16-08

Walikuja tena kuwaibia waisrael.

Hii ingetafasiriwa kama "walikuja tena kwenye nchi ya waisrael kuwaibia vitu."

hawakuweza kuhesabika.

Hii ingetafasiriwa kama, " idadi ya Wamediani ilikuwa ni kubwa kiasi cha kutohesabika" au " ilikuwa ni ngumu kuwahesabu Wamediani wote."

kwa ishara mbili

Hii ingetafasiriwa kama, "kutenda miujuiza mara mbili" au " kufanya mambo mawili yasiyowezekana yawezekane."

Kwamba Mungu angemtumia.

Hii ingetafasiriwa kama, "Mungu angemwezesha" au "Mungu angelimsaidia" au " Mungu alikuwa akimuita."

Kuiokoa israel.

Hii ingetafasiriwa kama, " Kuinusuru Israel kutoka kwa Wamidiani."

16-09

Ishara

Hii ingetafasiriwa kama, " Miujiza" au " Mambo yasiyowezekana"

Ngozi ya Kondoo

Hii ni ngozi ya kondoo yenye manyoya juu yake, Manyoya ni kama sufu ambayo hukamata maji mengi(hushikilia maji mengi),kwa tafasiri hii inatoa udhibitisho kuwa ngozi hii imefunikwa na nywele laini na nyembamba

Na kuwe na umande asubuhi.

Hii inaweza kutafasirirwa kama, " umande utokee asubuhi" au " umande ushuke asubuhi." "Umande" haya ni matone ya maji ambayo huonekana kwenye aridhi wakati wa asubuhi". kiuhalisia umande hufunika kila kitu kwa pamoja."

Mungu alifanya hivyo.

Hii ingetafasiriwa kama, "Mungu alitenda kile ambacho Gidioni alichomuomba atende."

16-10

Askari 32,000 walikuja kwa Gidioni.

Baadhi ya lugha zingeweza kuiweka sentensi ifuatayo mwanzoni mwa simulizi; Gididoni aliwaita waisrael ili waje wapigane na Wamidiani.

Wengi sana.

Ni kwamba, walikuwa askari wengi sana tofauti na jinsi Mungu alivyokuwa akihitaji kwa ajili ya mapigano. Kama askari wengi wangepigana na kushinda, wangefikiri ya kuwa wameshinda vita kwa nguvu zao wenyewe na wasingetambua ya kuwa Mungu ndiye ametenda.

Isipokuwa Askari 300.

Sentensi hii ingemanisha ya kuwa, "Hivyo Gidioni akaruhusu Askari 300 tu kubaki, na wengine walielekea nyumbani."

16-11

Kushuka chini.

Askari wa Midiani waliweka kambi kule bondeni na walikuwa chini zaidi ya askari wa israel.

Hamtakuwa na hofu kamwe.

Hii inamanisha kuwa," hamtaogopa tena"

Alichokuwa amekiota

Hii ni kwamba,"kitu ambacho alikuwa amekiona kwenye ndoto" au " ndoto aliyokuwa nayo."

16-12

Pembe

Hii ingetafasiriwa kama, " tarumbeta" au "Pembe ya tarumbeta." Pembe hizi zilitoka kwenye kondoo dume na zilitumika kuwaita wanaume kwa ajili ya vita(mapigano).

Kurunzi

kuna uwezekano kuwa ilikuwa ni kipande cha kuni kilichofunikwa na nguo na iliyosokotwa kwenye mafuta ilikusudi iweze kuwaka vizuri. (hii haikuwa kurunzi ya kisasa iwakayo kwa betri)

16-13

Wakapaza sauti.

Hii ingetafasiriwa kama, "alitoa sauti kubwa" au " kusema kwa sauti kubwa"

Upanga

Upanga ni siraha yenye kisu kirefu, chnye makali na mkono wa kushikia. Watu hushika sehemu ya mkono na kumpiga au kumchoma adui na kupitia sehem yenye makali. Kama watu wako wasipokuwa na siraha kama namna hii, ungetafasiri kama, "kisu kirefu" au"panga" "kisu cha porini"

Upanga kwaYehova kwa Gidioni.

Inamanisha ya kuwa, " tutapigana wa Yehova na kwa Gidioni."

16-14

Mungu aliwachanganya Wamidiani.

Mungu alisababisha Wamidiani wachanganyikiwe. Walitaka kuwashambulia Waisrael, lakini badala yake walijishimbuliana wao kwa wao.

Waisrael waliobaki

Hii ingetafasiriwa kama, " Waisrael wengi wa kiume". inaelezea baada ya Askari kurudi nyumbani.

Waliitwa.

Ni kwamba, " waliitwa nje" au " waliombwa kuja" sentensi hii ingetafasiriwa kama, " Gidioni alituma watu kuwaita wanaume wa israel kutoka kwenye nyumba zao"

16-15

Hakuwarusu wafanye haya

Gidioni alijua ya kuwa ilikuwa ni vyema Waisrael wamfanye Mungu kama Mfalme wao.

Lakini aliwauliza

Aya hii inaanza na " lakini" kwa sababu alichokifanya badaye hakikuwa na hekima.

16-16

Gidioni alitumia dhahabu kutengeneza vazi maalumu.

Hii ingetafasiriwa kama, "Gidioni aliiyeyusha dhahabu ambayo watu walimpatia na akatengeneza vazi la maalumu kutoka kwenye dhahabu.

Walimuacha Mungu.

Hii ingetafasiriwa kama, "hawakumtii Mungu" au " waliacha kumwabudu Mungu."

16-17

Hali hii ilijirudia mara kwa mara

Hii ingetafasiriwa kama," Mambo haya yaliendelea kujirudia mara kwa mara" au" Mambo haya yalitokea mara nyingi"

16-18

Hatimaye

Hii ingetafasiriwa kama, " Baada ya aduu zao kuwashambulia mara nyingi" au " Baada ya miaka mingi ya kushambuliwa na mataifa mengi tofauti."

Wakamuomba Mungu awape Mfalme

Hii ingetafasiriwa kama, "walimtaka Mungu awape Mfalme" au "waliendelea kumuomba Mungu kwa ajili ya Mfalme."

Kama mataifa mengine

Mataifa mengine yalikuwa na Mfalme. Waisrael walitaka wawe kama wao na wapate Mfalme.

Mungu hakulitaka Ombi hili

Hii ingetafasiriwa kama, " Mungu hakukubaliana na walichomuomba," Mungu alijua yakuwa walikuwa wakimkataa kama Mtawala wao na badala yake walichagua kuwafuata viongozi wao.