21-01
Tangu mwanzo
Hiki ni kipindi dunia ilipoumbwa kwa mara ya kwanza.
Kumponda nyoka kichwa .
Pasipo kichwa cha nyoka kupondwa, nyoka anaweza kumjeruhi mtu.Tumia neno "kuponda" likiwasilisha kwamba kichwa chake kimeharibiwa .
Nyoka alikuwa shetani
Shetani aliongea na Eva katika umbo la nyoka. Hii haimaanishi kwamba shetani ni nyoka kwa sasa. "Nyoka alikuwa... ni muonekano wa shetani".
aliyemdanganya Eva
Hii ni kwamba, "aliyemdanganya Eva." Nyoka alimdanganya Eva kwa kumfanya kutia shaka kile Mungu alichokisema ,na kumrubuni asimtii Mungu.
21-02
Kwa yeye
Hii ni kwamba," sababu ya mmoja wa wazao wake."
21-03
Kuinua nabii mwingine kama Musa.
Hii ni," kuteua nabii mwingine kama Musa "au," kusababisha nabii mwingine aje atakaye kuwa kama Musa."
Nabii kama Musa
kuwa kama Musa, nabii ajaye atakuwa na mamlaka kuu kutoka kwa Mungu ya kuongoza na kuokoa watu wake.
21-04
Uzao wake Daudi
Namna nyingine ya kusema hili, ni "atakuwa mzawa moja kwa moja wa Daudi mwenyewe"
21-05
Kupitia nabii Yeremia Mungu aliahidi
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, "Kupitia jumbe ambazo Mungu alimpa Yeremia, Mungu aliahidi, "au, "Nabii Yeremia aliwaambia watu ahadi za Mungu".
Lakini si kama
Agano jipya litakuwa kweli na enye matunda. watu watamjua Mungu kweli, wataishi kweli kama watu wake, na atawasamehe dhambi zao kabisa, kutokana na dhabihu ya Masihi mwenyewe kujitoa mara moja kwa wote wamwaminio.
Andika sheria yake kwenye mioyo ya watu
Huu ni mfano wa maana, "saidia watu wake kufahamu sheria zake na kutamani kuzitii kwa uaminifu.Ikiwa inawezekana,tunza picha ya maandiko kwenye mioyo yao,tangu hii tofauti ya njia ya Mungu aliaandika sheria zake kwenye vibao vya mawe kwa ajili ya Waesraeli.Ikiwa haiwezekaniunaweza kutafsiri maana.
Kuwa watu wake
Hii itaweza kuwa imetafsiriwa hivi, "kuwa watu wake wa dhamani,"kuwa watu wake wa kipekee."
Kuanza agano jipya
Hii kwamba,"Kuwa mmoja wa kusababisha agano kuleta matokeo,"au,"kuleta agano jipya kwa watu wake."
21-06
Nabii mkamilifu
Masihi atakuwa ni nabii ambaye ni mkamilifu katika kumtii Mungu, na kuwapa watu kila neno lililonenwa na Mungu, na atamwakilisha Mungu vizuri na kuwasaidia kumjua na kumfahamu Mungu.
21-07
Kwa niaba ya
Hii inaweza kutafsiriwa hivi,"kwa manufaa ya ,"au," kwa sehemu ya ,"
Kama mbadala wa kuadhibiwa dhambi zao.
Mungu aliwaruhusu watu kuleta wanyama ili kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zao kama kukumbushwa adhabu ya makosa ya wategemezi wao waliyofanya kwa Mungu na kuondoa dhambi zao. Mungu alizikubali hizo dhabihu kama njia ya kufunika dhambi kwa muda mfupi na hakuwaadhibu watu kwa ajili ya hilo.
Kuhani mkuu mkamilifu
Tofauti na makuhani wakuu wengine, Masihi hatafanya dhambi, na ataondoa kabisa dhambi za watu.
Kujitoa peke yake.
Hii ni, " aliruhusu kuuwawa."
Dhabihu kamilifu
Hii ni ,"dhabihu ambayo haina kosa, au mawaa".
21-08
kukaa enzini mwa baba zake Daudi
Kwa desturi, Enzi ni kiti cha mfalme au malkia ambacho kina wakilisha mamlaka yao.Maelezo haya yanaweza kutafsiriwa hivi,"Kuwa na mamlaka ya kutawala kama baba yake Mfalme Daudi alivyofanya",au,"kuwa uzao wa mfalme Daudi na kuendeleza utawala wake juu ya watu wa Mungu."
Dunia yote
Hii ingeweza kutafsiriwa hivi,"Kila mtu kila mahali,"
21-09
Malaki
Malaki alikuwa nabii wa mwisho katika agano la kale
Kunenwa kabla
Hii inaweza kuwa imetafsiriwa hivi,"aliyetabiriwa "au,"aliyetolewa unabii."Ina maana kusema kwamba kitu kitatokea baadaye.Malaki aliongea ujumbe wa Mungu kwa watu miaka 400 kabla ya Masihi kuja.
Aliyetabiriwa
Kwa muktadha huu ,"aliyetolewa unabii"ina maana sawa na" aliyetabiriwa"na "anayetazamiwa," inamaanisha nabii alisema kitu ambacho itatokea kwa muda mrefu wa baadaye.
Masihi atazaliwa na bikira
Njia nyingine ya kusema hii itaweza kuwa," bikira anatajifungua Masihi."
Mika
Mika alikuwa nabii wa Mungu katika Agano la kale ambaye, kama Isaya, aliongea ujumbe kutoka kwa Mungu takriban miaka 800 kabla ya Masihi kuja
21-10
Watu waliovunjika moyo
Hii inaeleza na kurejea watu waopitia katika huzuni iliyokithiri
Kuwatangazia uhuru mateka
Hii ni kwamba ,"kuwambia wafungwa wanaweza kuwa huru."Hii pia iaweza kumaanisha kuweka huru watu kutoka kwenye utumwa wa dhambi.
kuwatoa magerezani
Ni kwamba," atawaweka huru wote waliokuwa na dhuluma waliokuwa ndani ya kifungo".Hii inaweza pia kurejea kuwaweka watu hurukutoka kwenye mzigo wa dhambi
Wasiweze kusikia,kuona,kuongea,au kutembea.
Inaweza kuwa vizuri kusema,"wasiosikia ,wasioona,wasioongea,au wasiotembea,Baadhi ya lugha zingine zina maneno ya kipekee katika hali hizi,"kiziwi"kipofu".
21-11
Kuchukiwa bila sababu na kukataliwa.
Hii inaweza kuwa imetafsiriwa hivi,"kuchukiwa na kukataliwa,hata hivyo hakufanya chochote cha tofauti,"au"hata hivyo hakuwa na hatia.'
Kunenwa kabla
Hii inamaanisha kwamba aliyenena kuhusu vitu vinaweza kutoka kwa baadaye.Maneno mengine yenye maana sawa ni "aliyetabiriwa"aliyetolewa unabii"
Kugawa nguo zake
Hii ni ,"kucheza mchezo wa kamari na kutambua ambaye anaweza kushinda nguo zake."
Zakaria
Zakaria alikuwa nabii katika agano la kale ambaye aliongea na watu wa Mungu baada ya kurudi katika nchi waliyoahidiwa kutoka utumwani Babeli.Hii ilikuwakati miaka 500 kabla ya masihi kuja .
Sarafu thelathini za fedha .
Kwa wakati huo kila sarafu ilikuwa na thamani ya kiasi cha fedha ya mtu kuweza kuingiza kwa siku nne.
21-12
Kuchomwa
Hii ni,"kumchoma,"kitu chenye ncha kali kitakachoweza kupenyeza mwilini mwake kama sehemu ya kuadhibiwa kwa dhambi za watu.
21-13
Hakuwa na dhambi
Hii inaweza kuwa imetafsiriwa "Hakuwahi kutenda dhambi,"
Anapokea adhabu kwa ajili ya dhambi za watu wengine
Hii ni kusema,"Kuchukua pekee yake adhabu ambazo wengine walitenda,"au"kuadhibiwa katika sehemu ya watu wengine."
Ilikuwa Utayari wa Mungu
Hii ni ,"kujazwa kusudi la Mungu."kipengele hiki kinaamanisha kwamba kifo cha Masihi kilikuwa tayari kimepangwa na Mungu kutokea ili kwamba dhabihu itaweza kulipia dhambi za watu.
kuharibu
Ni kwamba ,"kutupa kabisa,"kuua,"au,kumaliza kuharibu,"
21-14
Kumfufua yeye katika wafu
Ni kwamba" kumsababisha yeye kuwa hai tena ,"
Kupitia kifo cha Masihi na ufufuo ,Mungu ataweza.
Hii inaweza ikawa imetafsiriwa hivi,"Mungu ataweza kutumia kifo cha masihi na ufufuo "au" kifo cha Masihi na ufufuo kinaweza kuwa njia ambayo Mungu ataweza.
Kuanza agano jipya
Ni kwamba 'kuweka agano jipya ndani ya matokeo."
21-15
Ndani ya ulimwengu
Hii ingeweza kutafsiri kama, "Kwa watu wa ulimwengu." Masihi atatumwa si tu kwa wayahudi, bali kwa watu wote.